Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Video: Magari Yasiyotii Sheria Yatolewe Matairi-JPM

$
0
0
Leo  Rais Magufuli amefungua rasmi awamu ya kwanza ya miundombinu na utoaji wa huduma ya usafiri wa haraka wa mabasi (BRT) katika Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza kabla ya kufungua rasmi awamu ya kwanza ya mradi huo Rais Magufuli ameiomba Benki ya Dunia kuharakisha mchakato wa kutoa fedha za mkopo utakaowezesha kuanza kwa ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya barabara ya Ubungo (Ubungo Interchange) ili kuongeza ufanisi wa mradi. 

Pia ametoa onyo kali kwa magari ya kawaida, bajaji na pikipiki kuingia katika barabara za mabasi ya mwendo kasi huku akisisitiza msimamo wake wa kutaka yatolewe matairi pindi yanapokamatwa

==> Isikilize hotuba yake hapo chini

Habari Zilizopo Katika Magazeti hya Leo Alhamisi ya January 26

Askari wa SUMA JKT Watiwa mbaroni kwa kuua Wafugaji Wanne na kujeruhi Watano

$
0
0
Jeshi la polisi mkoa wa Arusha, linawashikilia Askari wanne wa SUMA JKT kwa tuhuma za kuhusika kuwaua wafugaji wanne kwa kuwapiga risasi na kuwajeruhi wengine watano kwenye vurugu zilizotokea eneo la Oldobnyo Sambu wilayani Arumeru.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, alisema chanzo cha mauaji hayo ni wafugaji wa kimaasai kuwavamia askari hao ambao walikuwa wamekamata ng’ombe ambao waliingizwa ndani ya msitu wa hifadhi ambao ni wa serikali, kwa ajili ya malisho, kutokana na ukosefu wa malisho.

Kamanda, Mkumbo,amesema Askari hao ambao wanalinda msitu huo maarufu , shamba la miti la Meru USA Plant ,ambalo ni la serikali, walianza oparesheni zao majira ya saa 2.30 asubuhi za kuondoa mifugo iliyoingizwa ndani ya msitu huo.

Askari hao wa SUMA JKT, awali walikamata ng’ombe 45 , mbuzi na kondoo 65 na kuwapeleka kwenye zizi maalumu lililopo kituo cha polisi Oldonyo Sambu.

Askari hao waliendelea na oparesheni hiyo na ilipofika majira ya saa 8 mchana walipata taarifa ya kuwepo kwa kundi jingine  katika msitu huo na kufanikiwa kukamata ng’ombe 80, mbuzi na kondoo 70 kwa lengo la kuwapeleka kwenye zizi hilo la serikali.

Amesema wakati wanawaswaga mifugo hao ndipo kundi la wananchi wakiwa na silaha za jadi walipojitokeza mbele yao wakitaka kuwakomboa mifugo hao kwa nguvu.

Hatua hiyo iliwalazimu askari nao kuanza kuwafyatulia risasi na kusababisha vifo vya vijana wanne na watano kujeruhiwa.

Amewataja wananchi waliouawa kuwa ni Mbayan Melau (27), Julius Kilusu (45), Lalasehe Meibuko (25), na Seuri Malita (32) na hakuna askari aliyejeruhiwa.

Diwani wa kata ya Oldonyo Sambu, Raymond Lairumbe amesema hatazika miili hiyo, mpaka viongozi wa serikali watakapofika eneo hilo kuzungumza nao na huku majeruhi wanne waliolazwa hospitali ya Mount Meru Arusha, wakiomba msaada wa kutolewa risasi katika miili yao.

Mkuu wa Wilaya ajiuzulu, amwandikia barua Rais Dkt Magufuli

$
0
0
Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Uyui Bw.Gabriel Mnyele akizungumza na Mwandishi wa habari wa Azam tv Juma Kapipi wakati akiwa ofisi za CCM Wilaya ya Uyui ikielezwa kuwa alikuwa ameitwa na Uongozi wa chama hicho kufuatia kuwepo kwa taarifa kwamba ameamua kuachia ngazi nafasi ya Ukuu wa wilaya hiyo ya Uyui jambo ambalo alilithibitisha kwa Katibu wa CCM wilaya ya Uyui kwamba ni kweli amemwandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli. 

 *****
Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Gabriel Simon Mnyele amejiuzulu nafasi hiyo leo Alhamisi Januari 26, 2017 na kuwaaga madiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano alioufanya wilayani humo.

Akieleza sababu ya kufanya uamuzi huo, Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa alimwandikia Rais Dkt Magufuli barua ya kujiuzulu nafasi hiyo akielezea kusongwa na majukumu binafsi.

Mkuu wa Wilaya, Gabriel Simon Mnyele alikuwa miongoni mwa Wakuu wa Wilaya 139 walioteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 26 Juni, 2016.
Bw.Gabriel Mnyele hakuwa tayari kuelezea maamuzi aliyochukua na kuwataka Waandishi waliokuwa wakihoji hatua ya maamuzi yake wasubiri tamko kutoka juu."Mimi sina la kusema kuhusu hilo nimeamua mwenyewe,kwani mmesikia kuwa nimetumbuliwa?Aliwahoji waandishi.

Rais Magufuli kuwa mgeni rasmi Siku ya Sheria Nchini

$
0
0
Rais John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Sheria nchini zitakazofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao katika viwanja vya Mahakama jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Kaimu Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma amesema mahakama itawaelimisha wananchi jitihada mbalimbali ilizochukua zenye lengo la kuboresha huduma zake kupitia mpango mkakati wa miaka mitano inaoutekeleza katika kutoa haki kwa wakati na kuwezesha ukuaji wa uchumi.

Amesema kabla ya kilele cha maadhimisho hayo, mahakama itafanya matembezi maalum yatakayoongozwa na Rais Mstaafu Mh. Ali Hassan Mwinyi  na yataanzia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuishia katika viwanja vya Mnazi mmoja.

Katika matembezi hayo Mhe. Rais Mstaafu Mwinyi atazindua rasmi maadhimisho ya wiki ya elimu ya sheria ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuelekea maadhimisho ya kilele cha siku ya sheria nchini.
 
Aidha ametoa rai kwa wananchi kutembelea sehemu zote zilizoandaliwa kwa ajili ya utoaji elimu ya sheria nchini kwa ajili ya kujifunza na kupata huduma mbalimbali za Kisheria.

Alizitaja huduma hizo ni pamoja na taratibu za ufunguaji mashauri katika ngazi mbalimbali za mahakama, taratibu za kesi za mirathi, taratibu za kesi za dhamana, taratibu za rufaa, ndoa na talaka, taratibu za kupokea na kushughulikia malalamiko na Msaada wa Kisheria

Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini hufanyika kila mwaka mwanzoni mwa mwezi wa pili na mwaka huu yamebeba ujumbe wa Umuhimu wa Utoaji Haki kwa Wakati Kuwezesha Ukuaji wa Uchumi.

Taarifa Kutoka Ofisi Ya Rais,menejiment Ya Utumishi Wa Umma Na Utawala Bora

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania, Dkt John Pombe Magufuli amemteua Nyakimura Muhoji kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma kuanzia tarehe 17 Januari 2017. 

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Muhoji alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Utumishi wa Umma Ofisi ya Rais Menejimenti na Utumishi wa Umma.

Aidhha, Rais Dkt Magufuli amemteua Prof. Saida Yahya Othman kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa kuanzia tarehe 17 Januari 2017.

Florence Temba

MKURUGENZI WA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI,

OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA,

26 JANUARI 2017.

Mmiliki Mwenza Wa Jamii Forum Apandishwa Kizimbani

$
0
0
Mmiliki mwenza wa kampuni ya Jamii Media, Mike Mushi amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu na kuunganishwa katika mashtaka yaleyale yanayomkabili mkurugenzi wa kampuni hiyo, Maxence Melo.

Washtakiwa wote wawili walisomewa mashtaka mbele ya hakimu mkazi mkuu, Thomas Simba na Hakimu mkazi mkuu, Godfrey Mwambapa.

Wakili wa serikali, Mohamed Salum alisema kuwa washtakiwa hao wakiwa eneo la mikocheni kwa nafasi zao wakijua jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa mawasiliano kwa njia ya mtandao kufuatia chapisho lililochapishwa katika tovuti yao  waliamua kushindwa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la polisi kwa kuwanyima data walizonazo.

Hata hivyo upelelezi wa kesi hizo mbili umekamilika na washtakiwa wote hawa watasomewa mashataka yao kuanzia Februari 9 na Februari 20.
 
Mpaka sasa washtakiwa wote wawili wapo nje kwa dhamana kwa masharti ya bondi ya Milioni 10 kwa kila kosa na masharti ya kutosafiri nje ya nchi.
Maxence Melo akimweleza jambo mmiliki mwenza wa Jamii Forum Mike mushi ndani ya chumba cha Mahakama
 Maxence Melo na Mike Mushi wakimsikiliza wakili wao

Kiasi cha fedha serikali ilichopata tangu kuanza mradi wa mabasi ya mwendokasi

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amesema kuwa kwa kipindi cha kati ya mwezi Mei hadi mwezi Disemba mwaka jana, serikali ilifanikiwa kukusanya kiasi cha fedha TZS bilioni 19 katika mradi wa mabasi yaendayo haraka.

Hayo yamesemwa na Waziri Simbachawene leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni siku moja tangu Rais Dkt Magufuli alipomtaka waziri huyo kwa kushirikiana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa kueleza umma nikiasi gani wamekusanya ili ifahamike kama mradi huo unaingiza faida au ni hasara.

Waziri Simbachawene pia ameagiza vikosi vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinawaondoa wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga wanaofanya biashara zao ndani ya eneo la barabara hiyo kitu ambacho ni kinyume na sheria.

Aidha, wakati huo huo Waziri Simbachawene amewaagiza Wakuu wa Mikoa yote nchini kuhakikisha wanawachukulia hatua za kisheria wazazi wote wanaotekeleza watoto wao au kuwatuma kwenda kuwa ombaomba jambo linalopelekea ongezeko la watoto wa mitaani.

Alichokisema Waziri Mkuu Majalia Kuhusu miradi ya makaa ya mawe ya Mchuchuma na chuma cha Liganga.

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali lazima ijiridhishe ni kwa namna gani itafaidika na uwekezaji katika miradi ya makaa ya mawe na chuma kabla haijaanza.

Amesema Serikali iko katika hatua za mwisho za mazungumzo na muwekezaji kabla ya kuanza uzalishaji kwenye miradi ya makaa ya mawe ya Mchuchuma na chuma cha Liganga.

Miradi hiyo inatekelezwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) na kampuni ya Sichuan Hongda (Group) Ltd (SHG) ya China. Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Januari 26, 2017) wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mundindi baada ya kukagua eneo la mradi wa chuma cha Liganga.

“Madini haya yana viwango vya juu vya ubora, hivyo ni lazima tuwe makini kabla ya kuanza kwa uzalishaji wake. Kwani chuma chetu ni bora na tutachimba kwa zaidi ya miaka 50,”. “Hivyo maeneo haya ni nyeti na lazima Serikali ijipange vizuri na kujiridhisha kama vipengele vyote vya mkataba vimetengamaa ndipo mradi huo uanze,” amesema.

Hata hivyo amesema mradi huo hautachukua muda mrefu utaanza hivyo wananchi wawe na subira. “Hatutaki kusikia tena suala la mikataba mibovu tunataka mikataba itakayoleta tija. Akizungumzia suala la fidia kwa wananchi wanaopisha mradi, amesema kabla haujaanza lazima walipwe fidia zao na tayari fedha zipo muwekezaji anasubiri ruhusa ya Serikali.

Amesema kuna baadhi ya watu wamejipenyeza na kutaka kuiibia Serikali kupitia suala la ulipaji wa fidia. Serikali haiko tayari kuona wananchi hao wakitumika kama madaraja ya wizi. Waziri Mkuu amesema watu hao ambao hawahusiki na eneo hilo wamesababisha gharama za fidia kuwa kubwa, hivyo wataalam wanatathmini ili kubaini wahusika kabla ya kulipa.

“Tunataka wananchi wenyewe waliokuwa hapa ndiyo tuwalipe fidia yao kwa mujibu wa tathmini husika. Fidia yenu mtalipwa baada ya kuwaondoa wezi wote waliojipenyeza. “Kuna watu wanataka kuiibia Serikali kwa mgongo wenu, hili hatutakubaliana nalo. Tupo makini vumilieni inalifanyia kazi suala letu. Hakuna haki ya mtu itakayopotea,” amesema.

Naye Naibu Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Tanzania China International Mineral Resources Ltd (TCIMRL) Bw. Eric Mwingira amesema miradi ya Liganga na Mchuchuma inatekelezwa kwa mfumo unganishi ambayo ina vipengele vitano kikiwemo cha mgodi wa chuma cha Liganga.

Amesema mgodi huo wa chuma una uwezo wa kuzalisha tani milioni 2.9 kwa mwaka huku kiwanda cha kuzalisha bidhaa za chuma Liganga kitazalisha tani milioni 1.1 kwa mwaka. Bw. Mwingira amesema kipengele kingine ni mgodi wa makaa ya mawe Mchuchuma wenye uwezo wa kuzalisha tani milioni tatu kwa mwaka.

“Kipengele cha nne ni kituo cha kufua umeme cha megawati 600 huko Mchuchuma. Kati ya hizo megawati 250 zitatumika Liganga katika kuchenjua na kuzalisha chuma cha pua na megawati nyingine 350 zitaingizwa kwenye msongo wa Taifa ili kuiuzia TANESCO,” amesema.


Pia kutakuwa na njia ya msongo wa umeme wa kilowati 220 kati ya Mchuchuma na Liganga na barabara ya mkato kutoka Mchuchuma hadi Liganga.

Amesema gharama za uwekezaji katika mradi huo unganishi ni Dola bilioni tatu, ambapo dola milioni 600 ni mtaji wa muwekezaji na mkopo utakuwa dola bilioni 2.4. Awali Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mheshimiwa Deo Ngalawa alimuomba Waziri Mkuu kuwaeleza wananchi hao ni lini watalipwa fidia za kupisha mradi wa chuma Liganga na mradi huo utaanza lini.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, ALHAMISI, 
JANUARI 26, 2017.

TAHADHARI: DECI mpya zaibukia Mwanza.....Hii Ni Kauli ya Jeshi la Polisi Jijini Mwanza

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza, linamshikilia Mkurugenzi wa kampuni binafsi iitwayo AQ Computer  Co.Ltd na wenzake 7 kwa tuhuma za kukusanya fedha zaidi ya shilingi 100,000,000/= kutoka kwa wananchi kwa njia za udanganyifu.



Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza DCP Ahmad Msangi amesema mkurugenzi huyo anayefahamika kwa jina la Happy Aloyce Mbuya miaka 35 mkazi mtaa wa Ilemela, kwa kushirikiana na wenzake 7 kupitia taasisi ya AQ Power Club wamekuwa wakiendesha moja ya vikundi vinavyojihusisha na biashara ya upatu jijini Mwanza, inayotambulika kwa jina lisilo rasmi la kupanda mbegu na kuvuna.
 
Amesema upelelezi umebaini kuwa watuhumiwa hao wamekuwa wakiwashawishi wananchi kwa kuwadanganyana kuwarubuni wajiunge na biashara ya upatu ambapo wananchi hao hushawishiwa kuwekeza fedha kidogo kwa muda mfupi katika vikundi hivyo na baada ya hapo wanaahidiwa kulipwa fedha nyingi zaidi ya zile walizowekeza bila kufanya kazi yeyote.
 
Aidha Kamanda huyo wa Polisi mkoa wa Mwanza anatahadharisha wananchi kuhusu shughuli zinazofanywa na kikundi/ kampuni nyingine binafsi ya Bega kwa Bega Microfinance Company Ltd, kutokana na watu wengi kuripoti polisi juu ya kutapeliwa fedha zao na kampuni hiyo.
 
Taasisi nyingine aliyoitaja kufanya biashara hiyo ya upatu ni 'Amka Mwanamke' (AMWA) na kwamba uchunguzi unafanywa ili kuweza kubaini ukweli wa taarifa hizo.
 
Amesema tayari jeshi hilo limewatia mbaroni wakurugenzi na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo na majalada ya kesi hizo yapo kwa mwanasheria wa serikali kwa hatua zaidi za  kisheria.
 
Endapo tuhuma hizi zitathibitik, taasisi hizo ambazo ni AQ Power Club, Bega kwa Began a AMWA zitakuwa ni sawa na taasisi ya aina hiyo iliyojulikana kwa jina la DECI ya Jijini Dar es Salaam ambayo ilibainika kufanya utapeli wa njia hiyo mwaka 2008 na kuchukuliwa hatua za kisheria

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya January 27

Watu 14 akiwamo Mchina wafukiwa mgodini Geita

$
0
0
Watu 14 akiwemo Mchina, wanahofiwa kufa baada ya kufukiwa katika mgodi wa dhahabu wa Kampuni ya RZ Union Mining Ltd uliopo Kata ya Nyarugusu mkoani Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga jana alisema watu hao wamefukiwa chini ya mgodi baada ya mlango wa kuingilia kwenye shimo la mgodi kumeguka udongo na kujiziba.

“Usiku wa kuamkia leo (jana) saa tisa kwenye mgodi huo unaoendeshwa na Wachina, mlango wa kuingilia mgodini mmoja ulimeguka na kujifunga watu 14 wakiwa ndani,” alisema Kyunga.

Kyunga alisema kwa mujibu wa kitabu cha orodha ya watu wanaojiandikisha kuingia mgodini, kuna majina ya Watanzania 12 na Mchina.

Aidha, alisema mbali na watu hao 13, pia kuna Mtanzania mmoja ambaye aliingia bila kujiandikisha na hiyo ni kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo hivyo kufanya idadi ya watu waliofukiwa kuwa 14. 

Kyunga alisema tangu jana asubuhi jitihada mbalimbali za kuondoa udongo kuwaokoa watu hao zinaendelea wakitumia mitambo na wataalamu.

“Kwa kusaidiana na Kampuni ya Geita Gold Mine (GGM) na wataalamu wengine, jitihada zinaendelea ili kuhakikisha tunawaokoa watu hao,” alisema Kyunga. 

Alisema wakati huo huo wamefanikiwa kutoboa eneo jingine na kupitisha mabomba ya hewa ya oksijeni ili kuwafanya watu hao wasikose hewa.

Tanzania na Malawi Kukutana Kujadili Sakata la Watanzania 8 Waliokamatwa

$
0
0
Tume  ya Ushirikiano wa Pamoja ya Kudumu (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi, inatarajia kukutana nchini humo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali, ikiwemo la Watanzania nane kukamatwa nchini humo kwa tuhuma za kuingia eneo la migodini bila kuwa na kibali.

Mbali na kujadili suala la Watanzania hao, lakini pia tume hiyo itajidili mgogoro wa mpaka uliopo baina ya nchi hizo mbili katika Ziwa Nyasa.

Mkutano huo unatarajiwa kuanza Februari 3 hadi 5 mwaka huu nchini Malawi.

Akizungumza Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga alisema tume hiyo ilikuwa haijakutana kwa muda mrefu, jambo ambalo limesababisha watu kuwa na sintofahamu kati ya ushirikiano wa nchi hizo mbili.

Kasiga alisema mkutano wa tume hiyo, mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2003 jijini Dar es Salaam, hivyo kuwa kimya kwa muda mrefu kuna baadhi ya watu walidhani kuwa ushirikiano wa nchi hizo mbili si mzuri.

“Kikao kama hiki kilikaa miaka mingi kidogo… kuna masuala yaliyochelewa kutekelezwa kutokana na kukaa kwa kikao hiki, lakini kwa sasa yatatekelezwa kupitia vikao hivyo,” alisema Kasiga.

Aliongeza kuwa kwa mara ya kwanza, vikao hivyo vitashirikisha wafanyabiashara kutoka mikoa ya Njombe na Ruvuma, pia wavuvi kutoka katika mikoa hiyo ambao wataeleza namna wanavyofanya shughuli zao kwa kushirikiana na wenzao wa Malawi bila kuingilia.

Mindi alisema katika kikao hicho, ujumbe wa Tanzania utaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk Augustine Mahiga; na mbali na kujadili mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa na Watanzania waliokamatwa, pia utajadili masuala mbalimbali katika sekta za biashara, elimu, kilimo pamoja na sekta zingine.

Kasiga pia alikabidhi tuzo za Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) walizoshinda kutoka Umoja wa Afrika (AU). SSRA ambayo imekuwa wa kwanza katika Tuzo za Ubunifu Katika Sekta za Umma Afrika (AAPSIA), ilikabidhiwa kikombe pamoja na cheti cha ushindi.

Ushindi huo wameupata kupitia mradi wao wa Mradi wa Kanzidata ya Taifa ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
Bi Mindi akimkabidhi Bi. Sarah kombe la ushindi kwa niaba ya Wizara. Bi. Kibonde aliipokea zawadi hiyo kwa niaba ya Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Meneja wa Mradi wa Mfumo wa Forodha wa TANCIS kutoka TRA akipokea zawadi ya cheti cha ushindi kutoka kwa Bi. Mindi Kasiga.

Video: Rais Barrow alivyowasili Gambia

$
0
0
Maelfu ya wananchi wa Gambia wamefurika katika barabara za mji mkuu wa nchi hiyo, Banjul kumlaki Rais wao, Adama Barrow wakati akiwasili nchini mwake kuiongoza nchi hiyo baada ya kuondoka madarakani kwa rais wa mda mrefu Yahya Jammeh.

Barrow aliapishwa wiki iliyopita nchini Senegal wakati viongozi walipokuwa wakimshawishi Jammeh kuondoka madarakani baada ya kushindwa katika uchaguzi uliompa ushindi Barrow.

Barrow ameamua kurudi nchini humo mapema baada ya Wanadiplomasia kumtaka arudi mara moja nyumbani kuepuka pengo la uongozi.

Kutokana na taarifa zinazoeleza kuwa wafuasi waovu wa Jammeh wamo miongoni mwa vikosi vya usalama nchini, maelfu kadhaa ya wanajeshi wa mataifa ya Afrika magharibi wanasalia Gambia ili kuimarisha ulinzi kwa Rais Barrow.

Barrow atakaa katika makazi yake wakati ukaguzi ukifanywa katika Ikulu kutambua hatari yoyote kufuatia kuondoka kwa Yahya Jammeh kwenda uhamishoni Guinea ya Ikweta.

Majaliwa awabana watumishi Ludewa.....Ni kuhusu upotevu wa sh. milioni 700

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka kuwachukulia hatua watumishi Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa waliohusika na upotevu wa fedha za maendeleo zaidi ya sh. milioni 700 zilizopelekwa katika halmashauri hiyo kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo zikiwemo sh. milioni 300 za ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri hiyo.

Majaliwa ametoa kauli hiyo Januari 26, 2017 wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Halmashauri alipokuwa katika ziara yake katika Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe.

“Mkuu wa Mkoa watu wote waliohusika na upotevu huu watafutwe popote walipo na kuchukuliwa hatua na kisha nipewe taarifa ya hatua ulizochukua. Hatuwezi kuwavumilia watu hao ambao wanachora ramani kwa sh milioni 200  na sh. milioni 100 zingine hazijulkikani zilipo,“ – Majaliwa.

Aidha, Majaliwa amemuagiza Mkuu huyo wa Mkoa kufuatilia kiasi kingine cha sh milioni 400 zilizopelekwa wilayani hapo kwa ajili ya maendeleo ambazo nazo hazijulikani zilipo.

“Tafuta waliohusika popote walipo hata kama ni nje ya Njombe waje kutueleza ziliko fedha zetu,” amesema

Majaliwa pia ameuagiza uongozi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) kuhakikisha inashirikiana nayo inafanya uchunguzi ili kubaini watu waliohusika na upotevu huo.

Mbali na hayo, Majaliwa asema Serikali haitowavumilia watumishi wote wanaojihusisha na vitendo vya ubadhilifu wa fedha za umma, hivyo amewataka watumishi wafanye kazi kwa kuzingatia sheria na maadili.

Amewataka watumishi wa umma nchini kuacha tabia ya kudokoa fedha za maendeleo zinazopelekwa katika Halmashauri zao kwa sababu Serikali iko macho na itawashughulikia wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.

Pia, Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wametakiwa kusimamia vizuri fedha za maendeleo zinazopelekwa kwenye maeneo yao na kuhakikisha zinatumika kama ilivyokusudiwa.

Kabla, Waziri Mkuu alipokuwa njiani kuelekea Ludewa Mjini akitokea katika kata ya Mundindi Waziri Mkuu alisimamishwa na wananchi wa kijiji cha Mlangali ambao waliiomba Serikali iwasaidie kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ya maji.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Michael Lameck alisema alimueleza Waziri Mkuu kwamba awali walikuwa wanapata maji ila kwa sasa hayatoki kutokana na uchakavu wa miundombinu hali iliyowafanya kuchangishana na kupata sh. milioni 95 kati ya 200 zinazohitajika.

Mara baada ya maelezo hayo, Majaliwa amemuagiza Mhandisi wa Maji wa Wilaya hiyo, Nasib Mlenge kwenda kijijini hapo leo  Januari 27 kukutana na Bw. Lameck ili kushirikiana naye na kuangalia alipofikia na kuendeleza uboreshaji wa miundombinu hiyo ili wananchi hao wapate maji.

“Mwenyekiti amechangisha sh. milioni 95 na kununua baadhi ya vifaa nyinyi mnashindwa nini. Lazima muwe makini na matatizo ya wananchi na Serikali haitaki masuala ya urasimu. Watu wana shida ya maji na mnajua tatizo mmekaa tu,” alisema.

Waziri Mkuu: Wanaojichomeka Eneo La Mgodi Ili Wapate Fidia Hawatalipwa

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuna baadhi ya watu wamejipenyeza na kutaka kuiibia Serikali kupitia suala la ulipaji wa fidia kwa wananchi wanaopisha miradi ya makaa ya mawe ya Mchuchuma na chuma cha Liganga.

Amesema kuwa Serikali haiko tayari kuona wananchi hao wakitumika kama madaraja ya wizi kwani kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu wanaojipenyeza ili kuiibia Serikali kwa njia hiyo.

Majaliwa amesema hayo leo Januari 26, 2017 katika ziara ya kikazi mkoani Njombe, ambapo amesema kuwa watu hao ambao hawahusiki na eneo hilo la mradi wamesababisha gharama za fidia kuwa kubwa, hivyo wataalam wanatathmini ili kubaini wahusika kabla ya kulipa.

“Tunataka wananchi wenyewe waliokuwa hapa ndiyo tuwalipe fidia yao kwa mujibu wa tathmini husika. Fidia yenu mtalipwa baada ya kuwaondoa wezi wote waliojipenyeza.

“Kuna watu wanataka kuiibia Serikali kwa mgongo wenu, hili hatutakubaliana nalo. Tupo makini vumilieni inalifanyia kazi suala letu. Hakuna haki ya mtu itakayopotea,” amesema.

Huyu Ndio Mshindi Wa Tecno #kamambele…kampeni Ya Kipekee Iliyofunga Mwaka 2016

$
0
0
Kampuni inayoongoza kwa kutengeneza na kuuza simu bora barani Afrika, Tecno Mobile imemtangaza mshindi wa kampeni ya #KAMAMBELE kuwa ni Bw. Goodluck Massawe mwanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Ardhi baada ya kupata kura zaidi ya 6,000 zilizopigwa na mashabiki ambapo mshindi alitakiwa kueleza sababu kwanini anaipenda simu yake ya Tecno. 

Kampeni ya hiyo iliyozinduliwa mwaka jana mwishoni kwa lengo la kuwapatia wateja wake nafasi ya kuzuru nchini Uingereza na kushuhudia mabingwa mara 4 wa Ligi Kuu ya Uingereza klabu ya Manchester City wakicheza dhidi ya mahasimu wao Manchester United. 

Tecno Mobile hivi karibuni ilitiliana sahihi makubaliano ya kufanya kazi na klabu ya Manchester City kama “Official Mobile Partner”

Kampeni hiyo iliwashirikisha Idris Sultan, mshindi wa Big Brother Africa - Hotshots mwaka 2014 na Hamisa Mobetto mwanamitindo maarufu ambao walikuwa kwenye usukani wa #KamaMbele ambapo Idris aliibuka kinara kupitia kura za Watanzania hivyo ataongozana na mshindi Bwana Goodluck Massawe.
 
Katika ubunifu wa aina yake Tecno Mobile ilifanya mahojiano mubashara kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo Idris na Hamisa walipata kupiga stori na mashabiki wao. Mahojiano hayo yaliendeshwa na DJ Lil Ommy ambaye ni mtangazaji katika Radio ya Times FM na kufana kwa kiasi kikubwa.
 
Mshindi wa #KamaMbele alipatikana mwezi Januari 2017 baada ya kupita mchujo wa washiriki zaidi ya 5,000 na kubaki washiriki wanne tu. Baada ya mchujo huo washiriki hao walitakiwa kuomba kura kutoka kwa Watanzania kupitia video zilizotumwa kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ya Tecno Mobile na hatimaye Bw Goodluck Massawe kuibuka mshindi. 

Safari ya Idris na mshindi Goodluck Massawe inatarajiwa kufanyika katikati ya mwezi Februari na kufikia kilele chake tarehe 25 mwezi huo huo ambapo watapata nafasi ya kwenda kuangalia mtanange baina ya Manchester City na mahasimu wao Manchester United mubashara jijini Manchester, Uingereza.
 
Huu ni mwanzo tu wa zawadi kutokana na ushirikiano huu baina ya Tecno Mobile na Manchester City, unaweza kujiunga na kutembelea kurasa za kijamii za Tecno Mobile ili kupata habari njema kila zinapotokea. 
 


Chapa Kazi Kwenye Kifaa Chochote Na Mahali Popote Ukiwa Na Microsoft Office 365

$
0
0
Ulishawahi kukosa dili la hela kwasababu umepata dharura na ukashindwa kukamilisha kazi kwa wakati? Microsoft wanakwambia tumia kifaa chako mahali popote ulipo kupitia program ya Office365 kukamilisha mipango yako ya kibiashara au kiofisi, usikubali kupitwa na chochote.  

Uwe mtandaoni au la, uwe ofisini au nje ya ofisi, ukitumia kompyuta au simu yako ya mkononi yenye program endeshi ya Android, iOS au windows unapata unachohitaji muda wowote na mahali popote.
 
Kupitia vifurushi vingi ya Office365, utaweza kuweka program zilizotoka hivi karibuni za Microsoft Office kwenye vifaa vyako vya kazi hivyo kukuwezesha kufanya kazi ukiwa mtandaoni au usipokuwa mtandaoni. 
 
Programu za Office365 huboreshwa mara kwa mara na ni rahisi kuzitumia na zinakuwezesha kufikia malengo yako ya kazi.
Kuna vifurushi tofauti kulingana na mahitaji yako. Tuangalie kimoja baada ya kingine.
 
1.    ESSENTIAL – Barua pepe, program za Office mtandaoni na usalama wa kutunza taarifa zako mtandaoni
Kifurushi hiki kinakupatia;-
-    Barua pepe yenye domain yako mfano blogger@jinalakampuni.co.tz
-    GB50 kwa ajili ya kuhifadhi barua pepe
-    Unapata kuwekewa programu za Microsoft Office kwenye Kompyuta mpakato au simu yako
-    1TB kuhifadhi mafaili mtandaoni

2.    PRODUCTIVITY – Kuwekewa full package ya programu za Office kwa ajili ya biashara yako na kuhifadhi taarifa zako mtandaoni
Kifurushi hiki kinakupatia;-
-    Programu za Office 2016 kuingizwa hadi kwenye Kompyuta 5
-    Kupata program za Office mtandaoni
-    Kupata program za Office kwenye simu za mkononi
-    1TB kuhifadhi mafaili mtandaoni

3.    PREMIUM – Unapata barua pepe, program za Office mtandaoni na usalama wa kuhifadhi mafaili
Kifurushi hiki kinakupatia vyote ambavyo unakipata katika vifurushi viwili vilivyoangalia hapo awali isipokuwa ukiwa na kifurushi kipi unapata vingine vingi vya ziada. 
 
-    Kukufanyia masuala yote ya kiufundi, vile vile wataisaidia timu yako ya kazi kuunganisha Kompyuta zao. Yote haya yanafanyika ndani ya muda mfupi sana. 
 
-    Una data nyingi kuzidi kipimo? Zungumza na Microsoft BURE na watakupatia gharama zote za kuhamisha data na kuzihifahdi kwa usalama mtandaoni – hivyo kukuwezesha kufanya kazi popote na kifaa chochote
 
-    Msaada wa Bure: Wanapatikana kwa njia ya simu muda wa kazi ambao ni Jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 11 jioni kila siku kupitia mfumo maalum wa tiketi ili kukusaidia.

Kwa Maelezo na taarifa zaidi tafadhali tembelea http://bit.ly/barua_pepeyabiashara au piga simu namba 0784 987363 / 0715 247365 / 022-2127641 au tuma barua pepe kwenda sales@extremewebtechnologies.com


Al-Shabab Washambulia kambi ya Wanajeshi wa KENYA Nchini Somali na Kuwaua 57

$
0
0
Kundi la al-Shabab nchini Somalia limesema wapiganaji wake wameshambulia kambi ya wanajeshi wa Kenya wanaohudumu chini ya kikosi cha Umoja wa Afrika (Amisom)nchini Somalia.

Wapiganaji hao wanadai kuwaua wanajeshi wengi kwenye shambulio hilo katika kambi ya Kulbiyow kusini mwa Somalia karibu na mpaka wa nchi hiyo na Kenya.

"Mujahideen (wapiganaji) wawili walivurumisha magari yaliyokuwa na mabomu na kuyalipua kwenye lango la kambi hiyo ya mji wa Kulbiyow kabla ya wapiganaji wengine kuingia. Baada ya makabiliano makali, tumefanikiwa kuiteka kambi," mmoja wa wasemaji wa al-Shabab Sheikh Abdiasis Abu Musab ameambia shirika la habari la Reuters.

Msemaji huyo amedai kundi hilo limewaua wanajeshi zaidi ya 57 na kutwaa magari na silaha za wanajeshi hao, taarifa ambazo msemaji wa majeshi ya Kenya amekanusha.

Kanali Paul Njuguna ameambia Reuters: "Ni uongo. Operesheni ya kijeshi inaendelea. Tunaendelea kupokea taarifa."

Al-Shabab wamekuwa wakipigana dhidi ya serikali  inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi na jamii ya kimataifa.

Wanajeshi wa Kenya pamoja na wanajeshi kutoka Djibouti, Uganda na Ethiopia, chini ya Amisom, wamekuwa wakisaidia serikali hiyo yenye makao yake Mogadishu.

Januari mwaka uliopita, wapiganaji wa al-Shabab walishambulia kambi ya majeshi ya Kenya el-Adde na kuua wanajeshi wengi.

Al-Shabab walisema waliua zaidi ya wanajeshi 100. Jeshi la Kenya halijatangaza idadi kamili ya wanajeshi waliouawa hadi wa leo.

Chanzo: BBC

Mbowe atembelea shamba lake lililopigwa marufuku na Serikali

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa  Hai, Freeman Mbowe ametembelea shamba lake la kilimo cha kisasa cha mboga mboga ( Green House) yaliyopo Hain na kuwajulia hali wafanyakazi pamoja na wataalam wake leo Ijumaa.

Pia, Mbowe amepata wasaa ya kuzungumza na baadhi ya wafanyakazi ambao walimweleza hofu kubwa waliyoingiwa  nayo ya kupoteza ajira zao wanazozitegemea katika kuendesha maisha yao ya kila siku.

Hali hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasiu Byakanwa kupiga marufuku shughuli za kilimo zinazoendeshwa na shamba la Kilimanjaro Veggies linalomilikiwa na Mbowe.

Byakanwa alitoa amri hiyo baada ya kutembea shamba hilo lenye ukubwa wa hekari mbili akisema kilimo hicho ni kinyume cha sheria kwani shamba hilo lipo ndani ya mita 60 kutoka mto Weruweru.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images