Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Donald Trump kawafuta kazi Mabalozi wote wa Marekani duniani

$
0
0
Kwa mujibu wa  The Independent na ParsToday wanasema kuwa Rais Donald Trump wa Marekani amewafuta kazi mabalozi wote wa nchi hiyo kote duniani na wanaohudumu katika mashirika ya kimataifa ambapo uamuzi huo umefanyika katika siku yake ya kwanza kazini.
 
Trump ambaye aliapishwa Ijumaa January 20, 2017 kuwa Rais wa 45 wa Marekani, amewataka mabalozi wote walioteuliwa na mtangulizi wake, Barack Obama kuondoka kazini mara moja bila hata kuwapa muda wa kujitayarisha kuondoka kama ilivyo kawaida.
 
Inaelezwa kuwa zaidi ya mabalozi 80 wa Marekani katika nchi mbalimbali duniani walifutwa kazi Ijumaa tarehe 20 Disemba saa sita mchana ikiwa ni mara baada ya Trump kuapishwa.
 
Hatua hiyo ya Trump inatazamiwa kuvuruga uhusiano na washirika muhimu kama vile Ujerumani, Uingereza na Canada ambapo ripoti zinasema nchi hizo zinaweza kukaa bila mabalozi kwa miezi kadhaa kwani baada ya Trump kuteua mabalozi wapya watalazimika kuidhinishwa na Bunge la Congress kabla ya kuanza kazi zao.
 
Donald Trump anakosolewa kwa kuacha nafasi nyingi wazi na hivyo kuvuruga shughuli za kawaida za serikali ya Marekani na hii haya yanajiri huku maandamano yakiripotiwa kuendelea sehemu mbalimbali kupinga utawala wa kiongozi huyo. 
 
Nchini Marekani katika siku ya pili ya utawala wa Trump kumeripotiwa maandamano ya watu milioni tatu na imeripotiwa kumefanyika maandamano 637 katika maeneo mbalimbali ya Ulaya, Asia na Afrika kumpinga rais mpya wa Marekani.

Dar: Mabadiliko ya njia za daladala kutokana na uzinduzi wa mabasi ya mwendokasi

Mzee Majuto azungumzia taarifa za kifo chake zilizosambazwa

$
0
0
Kenye kipindi cha  XXL ya Clouds FM leo Januuary 24 2017 Soudy Brown amezungumza na mchekeshaji King Majuto kuhusu taarifa zinazosambazwa ambazo sio sahihi kuwa amepata ajali na amefariki.

"Na mwaka huu mnataka kunia tena, mimi ni mzima, mara kwa mara wanatangaza mimi nimekufa…. mbaya sana", amesema Mzee Majuto

==> Msikilize hapo chini

Marekani yakubali kuiuzia Kenya ndege za kivita

$
0
0
Marekani imekubali kuiuzia serikali ya Kenya ndege za kivita na vifaa vingine vya kijeshi, kwa kima cha Dola Milioni 418 sawa na Shilingi za Kenya Bilioni 43.5.

Tayari bunge la Congress limepitisha kufanyika kwa manunuzi hayo na kutoa leseni ya kuidhinisha hilo.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema Kenya itapokea ndege hizo aina za AT-802L na AT-504 na vifaa vingine vya kivita.

Marekani inasema ni muhimu sana kwa Kenya kupata vifaa hivyo kwa sababu ni mshirika muhimu na wa karibu sana katika vita dhidi ya kupambana na ugaidi hasa kundi la Al Shabab kutoka nchini Somalia.

Kenya inatarajiwa kutumia silaha hizi kuendelea kupambana na kundi la Al Shabab nchini Somalia ambalo limeendelea kutishia kuishambulia nchi hiyo kwa kujiunga na wanajeshi wa Umoja wa Afrika AMISOM mwaka 2011.

Wiki iliyopita, rais mpya wa Marekani Donald Trump alihoji umuhimu wa nchi yake kuendelea kuunga mkono vita dhidi ya Al Shabab nchini Somalia, baada ya kutofanikiwa kwa miaka 10 sasa.

Credit: RFI

UINGEREZA: Mahakama yaamuru Bunge kuhusishwa kuamua kama Serikali inaweza kuanza mchakato wa kujitoa katika Umoja wa Ulaya(EU).

$
0
0
Mahakama ya Juu nchini Uingereza imeamua kuwa ni lazima wabunge nchini humo wajadili na kupigia kura mchakato wa nchi yao  kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Uamuzi huu wa Mahakama unamaanisha kuwa Waziri Mkuu Theresa May hawezi kuanza mazungumzo ya kujiondoa kwenye umoja huo kabla ya suala hili kujadiliwa na kupigiwa kura na wabunge.

Uingereza imepewa hadi mwisho wa mwezi Machi kuanza mchakato wa kujiondoa kwenye Umoja huo baada ya raia wa nchi hiyo mwaka uliopita, kujiondoa kuwa wanachama baada ya kufanyika kwa kura ya maoni.

Hata hivyo, Mahakama hiyo imeamua kuwa Mabunge ya Scotland, Wells na Ireland Kaskazini hayana umuhimu wa kujadili na kulipigia kura suala hili.

Baadhi ya wanasiasa nchini Uingereza wamekuwa wakisema serikali kuanza mchakato huo bila ya kuihusisha bunge, ni kinyume cha miiko ya kidemokrasia nchini humo.

Serikali ya Uingereza ilikwenda katika Mahakama ya Juu kutaka Majaji watoe uamuzi kuwa ina mamlaka ya kuendelea na mchakato huo lakini hata kabla ya uamuzi huu, ilisema itaheshimu uamuzi wa Mahakama.

Majaji nane waliamua kuwa mchakato huo uanzie Bungeni huku watatu wakipinga.

CCM Yaijibu CUF kuhusu Ushindi Dimani.....Yatoa siri mbili za ushindi wa kata 19 kati ya 20

$
0
0
Baada ya Chama cha Wananchi (CUF) kudai kuwa uchaguzi wa marudio uliofanyika Januari 22, 2017 ulikiuka sheria na taratibu za uchaguzi katika baadhi ya vituo hasa vya jimbo la Dimani, na kwamba ndio sababu ya mgombea wake Abdulrazak Khatib Ramadhan kushindwa katika uchaguzi huo.

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka na kujibu tuhuma hizo za CUF huku ikiilaumu kwa kushiriki kuuvuruga uchaguzi wa awali wa mwaka 2015.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Katibu wa Uenezi na Itikadi CCM, Humphrey Polepole ameishauri CUF kutafuta chanzo cha kushindwa kwake, kwani CCM haijashiriki kwa namna yoyote ile kupora ushindi huo.

“Matokeo ya Dimani yamedhihirisha CUF ilikua tatizo tangu uchaguzi uliopita, 2015 CCM ilipata kura 4400, CUF 2300, 2017 CCM imepata kura 4860 sawa na 78% CUF wamepata 1200 anguko la zaidi ya 50%,” amesema na kuongeza.

“CUF wanamtafuta wa kumuwekea lawama, sisi tunasema kushindwa kwao na kura zao kupungua lazima kuna mchawi ndani yao wenyewe hasa Zanzibar, wamtafute huyo mchawi sisi tumewapa ushauri ili wajiweke sawa.”

Aidha, Polepole ameeleza siri mbili za ushindi wa kishindo wa kata 19 kati ya 20 katika uchaguzi mdogo wa marudio nchi nzima, ambapo amesema kuwa utendaji wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli pamoja utekelezaji wa ahadi alizoahidi katika kipindi cha kampeni za uchaguzi Mkuu wa 2015 ndio sababu ya wananchi kuchagua wagombea wa CCM kwa kishindo.

“Rushwa, Ufisadi, ni adui wakubwa wa serikali ya awamu ya tano, pia inatekeleza ahadi zake zinazogusa wananchi moja kwa moja ikiwemo elimu bure kuanzia Darasa la kwanza hadi kidato cha nne,uboreshwaji wa huduma za kijamii, utilewaji mikopo kwa kina mama na vijana, ujenzi wa viwanda ambapo hutoa fursa za ajira kwa wananchi wanyonge,” amesema.

Ameongeza kua “Hizo ni siri mbili kubwa zilizotufanya tushinde kata 19 na jimbo la Dimani kwa kishindo.”

“Baadhi ya wanasiasa wanatutisha kwamba 2020 tutakutana tutaachia madaraka, kama wanatutabiria giza, kwetu CCM tuna mwanga mkubwa unaotupa hamasa ya kufanya kazi zaidi ili kuwaletea watanzania mabadiliko ya haraka,” amesema.

Amesema mwelekeo wa CCM kwa sasa ni ujenzi wa chama hicho ikiwa pamoja na kufanya uchaguzi wa viongozi ili kupata viongozi bora, wazalendo, wanaochukia rushwa na ufisadi, ubadhirifu pamoja na watakao kuwa tayari kusikiliza wananchi na kuwatumikia.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya January 25

UVCCM Yatabiri Anguko la Vyama vya Upinzani

$
0
0
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umesema kutokana na kushamili kwa ubabe, udikteta na ung’ang’anizi  wa madaraka ipo siku viongozi wa upinzani wataondolewa kwa nguvu na aibu.

Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka, jijini Dar es salaam baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokutana kutathmini ushindi wa uchaguzi.

Shaka amesema kuwa watanzania wataendelea kuiamini CCM kwa mambo mengi, ikiwemo kuleta uhuru na mapinduzi, sera, uongozi na utawala, kujali na kutazama maslahi mapana kwa manufaa ya umma na pia tabia ya utii wa sheria na kuheshimu katiba bila shuruti.

“Viongozi ving’ang’anizi wa madaraka ya kisiasa ni hatari kukabidhiwa dhamana ya madaraka na dola, ikitokea bahati mbaya siku moja wakapewa dhamana hiyo, hawatapisha wengine na huo utakuwa ni mwanzo wa kutikisika misingi ya utaifa, mshikamano na amani ya nchi,”amesema Shaka.

Aidha, Shaka amesema kuwa inashangaza kuwaona viongozi wa kisiasa ,akiwemo Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif wakijenga himaya ndani ya vyama vyao huku wakidaiwa kufanya ubabe katika uongozi wao.

Hata hivyo amesema kuwa ukandamizaji au kukosekana  kwa uhuru wa mawazo naDemokrasia ndani ya upinzani,ni kielelezo tosha kuwa viongozi wake huimba kinadharia dhana ya demokrasia huku wakishindwa kuonyesha kwa vitendo.

Mbunge wa Kigamboni Alalamika KERO za Wananchi Kupuuzwa Daraja la Nyerere

$
0
0
Mbunge wa Kigamboni Faustine Ndugulile (CCM) amekua akipokea kero mbalimbali za wakazi wa Kigamboni ikiwemo kiwango kikubwa cha pesa kinachotozwa pale tu wanapopita na magari kwenye daraja hilo, kazifanyia kazi kwa kuzifikisha kunakotakiwa na maelezo yake ndio haya hapa chini.

"Kwa muda mrefu nimekuwa nikipokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na huduma isiyoridhisha kwenye Daraja la Nyerere linalounganisha Kigamboni na Kurasini.

Malalamiko ya wananchi yako kwenye maeneo makuu matatu:

1. Kutumika kwa madirisha machache ya kukatia tiketi. Daraja la Nyerere lina madirisha 14 ( Saba wakati wa kuingia na Saba wakati wa kutokea). Madirisha yanayotumika ni machache na hivyo kusababisha foleni isiyo na msingi.

2. Tozo za Daraja la Nyerere zipo juu sana hususan kwa magari ya abiria hali hii imepelekea Kigamboni kukosa ruti ndefu za kuelekea maeneo mengine ya Jiji la Dar Es Salaam, gari la abiria linatozwa kati ya Tsh 5000-7000 kwa kila safari ambayo ni gharama kubwa sana kwa kutwa.

3. Kutokamilika kwa kipande kilichobaki toka Darajani hadi kwa Msomali.

Kama Mbunge wa Kigamboni nimekuwa nikifuatilia suala hili kwa karibu sana bila ya mafanikio, tukumbuke kuwa Daraja la Nyerere lilizinduliwa tarehe 19.04.2016 na sasa ni zaidi ya miezi 9 hamna kinachoendelea na wahusika hawatoi majibu yanayotosheleza.

HATUA NILIZOCHUKUA HADI HIVI SASA
1. Mnamo tarehe 15.06.2016 nilimwandikia barua Waziri wa Ujenzi Mhe. Makame Mbarawa (Mb) kuhusiana na hoja hizi pamoja na kufatilia zaidi ya mara kumi kwa simu, maongezi ya ana kwa ana na meseji, barua yangu haijajibiwa hadi hivi sasa (Angalia kiambatanisho).

2. Vilevile nilikutana na Mkurugenzi wa NSSF Prog Godius Kahyarara tarehe 3.10.2016 kuhusu hoja tajwa hapo juu, aliahidi kuchukua hatua za haraka lakini hadi hivi sasa hakuna kilichofanyika.

3. Kwa kuwa usimamizi wa Daraja la Nyerere upo chini ya NSSF na kipande kilichobaki kitajengwa na NSSF, niliomba kukutana na Waziri anayesimamia taasisi hii, nilikutana na Waziri Jenista Mhagama (Mb) tarehe 3.12.2016 ofisini kwake.

"Pamoja na maelezo ya mdomo, nilimkabidhi barua ya malalamiko (Angalia kiambatanisho), Waziri aliahidi kuchukua hatua za haraka.
"Tarehe 13.12.2016 nilipata nakala ya barua aliyoandika Mhe. Waziri Mhagama kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF ili kupata maelezo na ufumbuzi wa hoja nilizotoa, pamoja na kukumbushia Mhe. Waziri Mhagama hajanipatia majibu ya hoja zangu.

"Aidha, maelezo niliyopata toka kwa Mkurugenzi wa NSSF wakati Waziri Mkuu anatembelea Kigamboni tarehe 04.01.2017 ni kwamba fedha zinazohitajika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kipande kilichobaki ni Tsh 24 Bilioni na alinihakikishia kuwa FEDHA HIZO ZIPO.

"Michoro (design) ya barabara hiyo IMESHAKAMILIKA, Mkandarasi kwa ajili ya kazi hiyo YUPO

"Pamoja na NSSF kuwa na fedha ya ujenzi wa barabara hiyo, mkandarasi aliye tayari na michoro iliyokamilika, kumekuwa na kigugumizi ya lini kazi hii itaanza inasikitisha pia kuona Mawaziri hawajibu barua pamoja na kukumbushwa mara kwa mara.

"Kinachoendelea sasa hakuna lugha nyingine ya kuielezea zaidi ya UZEMBE na KUTOWAJIBIKA, naleta taarifa hii kwenu wakazi wa Kigamboni ili nanyi mjue kinachoendelea, ninakusudia kuyapeleka malalamiko yenu kwa mamlaka ya juu zaidi baada ya mamlaka tajwa hapo juu kushindwa kupata ufumbuzi."

Trump Kuzuia wahamiaji kutoka nchi za Kiislamu Afrika na Mashariki ya Kati........Pia Ataweka Sheria Kali ya Kupata Visa

$
0
0
Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kutia saini sheria  kuweka masharti kuhusu wahamiaji wanaoingia nchini humo.

Taarifa kutoka Marekani zinasema ataanza kwa hatua ya kuimarisha usalama katika mpaka wa nchi hiyo na Mexico atakapozuru makao makuu ya wizara ya usalama wa ndani leo  Jumatano.

Aidha, anatarajiwa pia kutoa tangazo la kuidhinisha sheria kali zaidi za kupata visa kwa wageni kutoka eneo la Mashariki ya Kati na Afrika ambayo yana Waislamu wengi

Bw Trump ameandika kwenye Twitter kwamba leo itakuwa siku muhimu sana kwa usalama wa taifa la Marekani.

Wakati wa kampeni yake ya urais, Donald Trump aliahidi kufanyia mageuzi suala la uhamiaji Marekani.

Aligusia ujenzi wa ukuta kati ya Mexico na Marekani kuzuia wahamiaji haramu na kuwapiga marufuku Waislamu kuingia katika taifa hilo kama sehemu ya vita dhidi ya ugaidi. 

Baadaye alibadili msimamo kidogo na kufafanua kwamba watakachofanyiwa Waislamu ni kufanyiwa ukaguzi mkali kabla ya kuruhusiwa kuingia Marekani.

Anatarajiwa kufika katika wizara ya usalama wa ndani baadaye leo na anatarajiwa kusaini maagizo hayo ya kuimarisha usalama katika mpaka wa Mexico na taifa lake na baadaye wiki hiii taarifa zinaashiria atawajibikia ahadi yake ya kupunguza idadi ya wakimbizi wanaoingia Marekani.

Na hiyo ni hadi pale ukaguzi mkali utakapoanzishwa na kuzuia raia wa mataifa saba ya Afrika na kutoka eneo la Mashariki ya Kati yote yalio na idadi kubwa ya waumini wa Kiislamu.

Ubaguzi wa kidini unapigwa marufuku kwa mujibu wa katiba ya Marekani lakini inadhaniwa utawala wa Trump utaidhinisha marufuku hiyo kwa misingi kwamba ni hatua za dharura kukabiliana na tishio lililopo la ugaidi.

Awali, Bw Trump aliandika kwenye Twitter kueleza kusikitishwa kwake na kiwango cha juu cha ghasia na mauaji katika jiji la Chicago.

Vyombo vya habari wiki hii viliripoti kwamba tayari watu 228 wamepigwa risasi na wengine zaidi ya 40 kuuawa mwaka huu.

Bw Trump ameandika kwamba iwapo watawala wa Chicago hawatatua tatizo hilo la mauaji, basi atawatuma 'Feds' akimaanisha maafisa wa FBI.

Chanzo: BBC

Serikali Yasitisha Kupokea wakimbizi wa Nchi za Maziwa Makuu

$
0
0
Serikali imetangaza kusimamisha kupokea wakimbizi kutoka nchi za Maziwa Makuu kwa makundi, kutokana na kutokuwepo kwa sababu za kiusalama, zinazowafanya wakimbizi hao kukimbia nchi zao na kuomba hifadhi ya ukimbizi nchini.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametoa kauli hiyo ya serikali mjini Kigoma wakati wa uteketezaji wa silaha haramu, lililofanyika kikanda mkoani Kigoma, na kueleza kuwa kwa sasa hakuna tena wakimbizi watakaoingia kwa makundi watakaoruhusiwa kuingia nchini.

Mwigulu alisema serikali itawapokea wakimbizi mmoja mmoja na kila atakayeingia atahojiwa na mamlaka zinazohusika na mamlaka zikijiridhisha kuwa anastahili hadhi ya ukimbizi, atapokewa na kupelekwa kwenye kambi za wakimbizi zilizopo, kwani hakuna tena kambi ya wakimbizi itakayofunguliwa kwa sasa.

Alisema serikali kwa kutumia vyombo vyake, imejiridhisha kwamba hakuna hali mbaya ya usalama, inayowakimbiza raia hao kutoka kwenye nchi zao na kwamba zaidi imegundulika kuwa wengi wao wanakimbia kwa sababu za kiuchumi, kuja kutafuta namna ya kuishi ili kukidhi hali zao za maisha.

Alisema uwepo na uingiaji wa wakimbizi nchini, umekuwa na mchango mkubwa katika uzagaaji wa silaha haramu sanjari na kuongezeka kwa matukio ya utumiaji wa silaha na kuathiri uchumi na maisha ya watu mbalimbali.

Katika hatua nyingine, waziri huyo amesema serikali imefuta utaratibu wa kutoa uraia kwa makundi, kama ilivyofanya kwa wakimbizi wa Burundi waliopo nchini. Alisema kwamba kwa sasa uraia utatolewa kwa mtu kulingana na maombi yake.

Alisema ukarimu huo wa Watanzania, umekuwa na athari kubwa katika ulinzi na usalama nchini, hasa mikoa ambayo imewahifadhi watu hao kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya mauaji, ujambazi wa kutumia bunduki, lakini kupanda mbegu mbaya ya kuuana kwa kulipiza visasi ambavyo vimekuwa vikifanywa na raia hao waliopewa uraia.

“Kwa mamlaka niliyopewa, natoa amri ya kusimamisha kutoa uraia kwa makundi kama ambavyo imetoa Tanzania na haijawahi kutokea nchi nyingine, tumeona athari kubwa ya watu hao na sasa sehemu kubwa ya Mkoa wa Tabora imekuwa na hali mbaya kiusalama na tabia ya kulipizana visasi,” alieleza Mwigulu.

Akitoa taarifa kwa waziri, Kamishna wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi, Marijani Nsato alisema silaha haramu 5,608 zikiwemo bunduki za kivita, zilitarajia kuteketezwa. Nsato alisema katika silaha hizo, kulikuwa na bastola 21, Shortgun 606, SMG 166, Riffle 300, bastola bandia 21, FN Riffle 3, G3 moja, SAR 3 na magobore 4487.

Sanjali na bunduki hizo, aliitaja mikoa ambayo imeshiriki katika kuchangia bunduki haramu zilizoteketezwa kuwa ni Kagera 100, Rukwa 189, Katavi 81, Simiyu 16, Mwanza 88, Geita 82, Mara 80 na Kigoma ukiwa na jumla ya bunduki 424 ambazo zimeteketezwa katika kazi ya jana.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Emmanuel Maganga alisema mkoa huo kuwa mpakani na kupokea idadi kubwa ya wakimbizi kutoka nchi za Maziwa Makuu, kumechangia mkoa huo kuathirika kwa kiasi kikubwa na uzagaaji silaha haramu na matukio ya ujambazi kwa kutumia silaha.

Alisema mkoa utaendelea kuweka mkakati wa kudhibiti silaha haramu na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha.

Rais Magufuli Kuzindua Mradi wa Mabasi ya Mendo Kasi Leo Jijini Dar

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Joseph  Magufuli, kesho tarehe 25 /01/2017 anatarajiwa kuzindua Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji wa Huduma ya Mabasi Yaendayo Haraka (Bus Rapid Transit - BRT) katika Kituo Kikuu cha Mabasi kilichopo Kariakoo eneo la Gerezani jijini Dar es salam.

Uzunduzi huo utahudhuriwa na Rais wa Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia wa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird. 
 
Awamu ya Kwanza ya mradi wa ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) yenye urefu wa kilometa 20.9 unaojumuisha barabara ya Kimara – Kivukoni, Magomeni  - Morocco na Fire – Kariakoo ulikamilika Desemba 2015. 
 
Aidha, utoaji wa huduma ya Mabasi Yaendayo Haraka ulianza tarehe 10 Mei, 2016. Kwa sasa huduma ya mabasi katika kipindi cha mpito inatolewa katika njia nane, vituo vikuu vitano, vituo vidogo 28 na karakana moja kwa kutumia mabasi 140 yanayojumuisha mabasi makubwa 39 yenye uwezo wa kubeba abiria 160 kila moja na mabasi madogo 101 yenye uwezo wa kubeba abiria 60 kila moja. 
 
Mradi wa ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) umepangwa kutekelezwa kwa awamu sita kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari  katika Jiji la Dar es Salaam.

Imetolewa na:

Eng. Joseph M. Nyamhanga
 KATIBU MKUU (UJENZI)

Makala: Jinsi ya Kukinga Kvuli Chako Kisionekane na Wachawi

$
0
0
IMESIMULIWA  NA  DOKTA. MUNGWA  KABILI….0744  000  473.
Wachawi  wana  uwezo  wa  kumtia  mtu  nuksi na mikosi mbalimbali.

Nuksi  na  mikosi  hiyo  inaweza  kuja  katika  sura  ya  magonjwa  na maradhi sugu  yasiyopona kama  vile kisukari, ukimwi, ugumba,  mimba kuchoropoka, kifafa  nakadhalika.
 Kufukuzwa  kazi, matatizo  katika ndoa,  ajali, umasikini, vifo  na  misiba  mfululizo, kuchukiwa  na  watu  nakadhalika.

Zipo  njia  mbalimbali  wanazo  tumia  wachawi  katika  kuwatia  watu  nuksi na mikosi, Katika  makala  ya  leo, nitaelezea  njia  moja  wapo  kama  ifuatavyo:
Katika  njia  hii, wachawi  wakitaka  kumtia  mtu  mikosi, hufanya  mambo  yafuatayo :

i.  Wanachukua  hela  ambayo  haitumiki
ii. Wanachukua   mavi ya  mbwa  mweusi ambayo  ameyanya  usiku wa manane
iii.Wanachukua  mkaa ulio kwisha  tumika, ambao  umetumika  mahali  ambapo  watu  hawalali  kama vile  kilioni  au  kwenye  baa  na migawaha  inayo  kesha lakini  mara  nyingi, huchukua  mkaa  wa  kilioni.
iv.Wanachukua  mavi   ya  ndege  anaitwa   Mumbi. Huyu ndege  aitwae  Mumbi  anapatikana  porini. Anafanana  sana  na  bata  na  ana  puyanga  la rangi  nyekundu.
v. Wanachukua  shahidi   la  kaburini  pamoja  na  ndumba  zingine  za  kichawi
vi. Wanachukua  kitu   chochote  cha  mtu  aliye  kusudiwa  kutiwa mikosi  kama  vile  jina  lake, picha  yake, mchanga  alipokanyagia, mate, kucha, au chochote  kile.
Baada  ya  hapo, mchawi  huyo  atakwenda  kaburini  usiku  wa  manane  na  kuvizika  vitu  vyote  nilivyo  vieleza  hapo  juu, huku  akisema  maneno  ya  kichawi. Basi  mtu  aliye  kusudiwa  na  uchawi  huu, kama  hana  kinga, ata andamwa  na  mikosi mikubwa  na  mizito  katika  maisha  yake  yote.

JINSI  YA  KUJIKINGA  DHIDI  YA  UCHAWI  HUU
Kujikinga  na  uchawi  huu  inabidi ufanyiwe  zindiko ama  upate  kinga maalumu  ya  kuficha  kivuli  chako. Hii  itawafanya  wachawi  washindwe  kukuona  katika  rada  zao  za  kichawi, na  wachawi  huwa  hawawezi  kumloga  mtu  ambae  haonekani  katika  rada  zao, kwa  sababu  wanawakuwa  hawajui  nguvu  zake  ziko  wapi wala  silaha  zao  haziwezi  kumshambulia mtu  ambae  haonekani  kwenye rada zao. 

Ukiwa  na  kinga  hii, hakuna  uchawi  wa  aina  yoyote  ile  unao weza  kufanyika  juu  yako, iwe  ni uchawi  wa  kukusababishia  madhara, au  uchawi  wa  mahaba  kukufunga  kimapenzi.

JINSI  YA  KUFICHA  KIVULI  CHAKO  KISIONEKANE  NA  WACHAWI
Kuficha  kivuli  chako  kisonekane  na  wachawi, fanya  kama  ifuatavyo

i.  Chukua  nywele  za  saluni
ii.  Chukua  mzizi  wa  mti  ulio  katisha  njia
iii. Chukua  tawi  la  mti  unaitwa  Ututukanga. Huu  mti  wa  Ututukanga  unapatikana  porini na baharini  na  huwa  linaonekana  shina  lake  na  matawi  yake  tu, lakini  mzizi  wake  huwa  hauonekani.
iv. Unachukua  mti   unaitwa  Msonihya
v.  Unasaga  pamoja  na  mti  unaitwa  mwavi.
vi. Baada  ya  hapo  unachukua  kuku  mweusi, unamfunga  kwenye kitambaa  cheusi  bila  kumchinja, unachukua  chungu  cheusi, unamuunguza  mpaka  anakuwa  mkaa, halafu  unamsaga  pamoja  na  miti  iliyo  tajwa  hapo  juu, unachanganya  na  mafuta  ya  simba.
vii. Unachukua  buja ama  dulya  la  ugali  wa  kilioni
viii.Unachukua kamba  ya  kitanda  alicho  lalia  maiti, au kama  maiti  ipo  kwenye  nyumba  ya  nyasi, unachomoa  nyasi  wakati  maiti  imo  ndani.
ix. Unachimba  mzizi  wa  mti  unaitwa  mputika  bila  kivuli chako  kugusa mti..
x.  Unaunguza  vyote  kwa  pamoja  ukiwa  na  kaniki  nyeusi  bila  kuvaa  nguo  yoyote  usiku wa  manane
xi. Unaipika  njia  panda pamoja na  mafuta  ya usiku.
Baada  ya  hapo, mtu  atachanjiwa  au kujichanja mwenyewe na kuoga au  kuogeshwa dawa hiyo.
Basi wachawi  watakuwa  wakijaribu  kutaka  kukutupia  uchawi, wanakuwa  hawakauoni  kwenye  rada  zao za  kichawi.

IMESIMULIWA  NA  DOKTA. MUNGWA  KABILI….0744  000  473.

PICHA: Rais Magufuli Afungua Rasmi Awamu Ya Kwanza Ya Miundombinu Na Utoaji Huduma Ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) Jijini Dar

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop pamoja na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wa kwanza kulia wavivuta kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene pamoja na  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka kadi ya Kieletroniki katika Mashine ya UDART ilikuweza kupita kama ishara ya Ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam. Pembeni yake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene akimuelekeza jambo katika mashine hizo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia mara baada ya kuendesha gari la Mwendo Kasi katika kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Haraka (BRT) mara baada ya kufungua rasmi Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mkono pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop mara baada ya kutoka kukagua moja ya basi linalotumika katika utoaji huduma ya Usafiri wa Haraka (BRT)

Taaria MUHIMU Toka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais IKULU

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 25 Januari, 2017 amefungua rasmi awamu ya kwanza ya miundombinu na utoaji wa huduma ya usafiri wa haraka wa mabasi (BRT) katika Jiji la Dar es Salaam uliotekelezwa kwa lengo la kukabiliana na msongamano wa magari ndani ya Jiji na athari zake katika shughuli za uzalishaji mali na ustawi wa jamii.

Mradi huu wa kwanza kutekelezwa Afrika Mashariki na wa tatu Barani Afrika, umehusisha ujenzi wa Kilometa 20.9 za barabara za Kimara – Kivukoni, Fire – Kariakoo na Magomeni – Morocco, vituo vya mabasi 27, madaraja ya waenda kwa miguu 3 na vituo vikuu 3.

Awamu hii ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa miundombinu na utoaji huduma ya usafiri wa haraka wa mabasi imegharimu Shilingi Bilioni 403.5 ambapo kati yake Shilingi Bilioni 86.5 zimetolewa na Serikali ya Tanzania na Shilingi Bilioni 317 ni mkopo kutoka Benki ya Dunia.

Utekelezaji wa mradi huu umepangwa kufanywa kwa awamu 6, na awamu ya pili ambayo ipo katika maandalizi ya kumpata mkandarasi baada ya kupata fedha za mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), itahusisha ujenzi wa barabara ya kutoka katikati ya Jiji – Mbagala, Magomeni – Chang’ombe na Chang’ombe – Jitegemee. Ujenzi huu utahusisha jumla ya Kilometa 19.3 za barabara na barabara za juu 2 (Flyovers) katika eneo la Chang’ombe na Uhasibu.

Akizungumza kabla ya kufungua rasmi awamu ya kwanza ya mradi huu, Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuanzisha mradi huo katika kipindi chake cha uongozi, na amewapongeza wadau wote waliohusika katika utekelezaji ikiwemo Wizara ya Ujenzi na Benki ya Dunia iliyotoa mkopo huo.

Mhe. Rais Magufuli ameiomba Benki ya Dunia kuharakisha mchakato wa kutoa fedha za mkopo utakaowezesha kuanza kwa ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya barabara ya Ubungo (Ubungo Interchange) ili kuongeza ufanisi wa mradi.

Mhe. Dkt. Magufuli amesema nia ya Serikali yake ni kuifanya Dar es Salaam kuwa Jiji la kisasa kwa kuhakikisha inakomesha tatizo la msongamano wa magari ambapo pamoja na kutekeleza mradi huo pia itajenga reli ya kisasa (Standard Gauge) kati ya Dar es Salaam na Morogoro na kujenga barabara za haraka (Express Road) kati ya Dar es Salaam na Chalinze hivi karibuni.

“Tunataka Dar es Salaam liwe Jiji la kisasa, ndugu zangu wa Dar es Salaam nataka mniamini hivyo, hivi karibuni tunapitia tenda na tutapata Mkandarasi wa kuanza kujenga reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ambapo kuna jumla ya kilometa 200 na treni zitakazopita zitatumia mafuta na umeme”

“Lakini pia mchakato wa kujenga barabara ya haraka (Express Road) kutoka Dar es Salaam hadi Chalinze yenye njia 6 na hatua zote zimekamilika na kilichobaki ni mazungumzo na wakandarasi kabla ya kuanza kujenga” amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amezitaka mamlaka zinazohusika, kuhakikisha mradi huo unaendeshwa kwa faida, miundombinu yake inatunzwa vizuri, wananchi wananufaika kama ilivyokusudiwa na pia ametoa siku 5 kwa Jiji la Dar es Salaam kufanya uamuzi juu ya matumizi ya fedha kiasi cha shilingi Bilioni 5.8 zilizotolewa na mbia anayemiliki asilimia 51 ya hisa za kampuni ya UDA-RT.

Pamoja na Mawaziri, Mabalozi wa nchi mbalimbali na Viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa na sherehe hizo zimehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop ambaye ameipongeza Tanzania kwa kutekeleza mradi huu muhimu kwa maendeleo na ustawi wa jamii na ameahidi kuwa Benki hiyo ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara zitakazosaidia kuondoa msongamano wa malori yanayokwenda bandarini kupeleka na kuchukua mizigo.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

25 Januari, 2017

Trump Kaanza Kuwatimua Watu Marekani.......Tayari Wasomali 90 na Wakenya 2 wameondolewa Marekani

$
0
0
Raia takriban 90 wa Somalia na wawili wa Kenya wametimuliwa kutoka Marekani saa chache baada ya taarifa kuibuka kwamba Rais Donald Trump atakabiliana na watu wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.

Wote wamewasili katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

Msemaji wa serikali ya Kenya Eric Kiraithe ameambia BBC kwamba raia hao wa Somalia watasafirishwa moja kwa moja hadi Mogadishu.

Bw Trump alisema Jumatano itakuwa siku muhimu kwa usalama wa Marekani.

Anatarajiwa kuweka masharti makali kwa raia wa mataifa saba ya Mashariki ya Kati na Afrika yenye idadi kubwa ya Waislamu wanaotafuta viza za kwenda Marekani.

Nchi hizo ni Syria, Iraq, Iran, Libya, Somalia, Sudan na Yemen 

Video: Rais Magufuli akiendesha basi la mwendokasi baada ya kuyazindua

$
0
0
Rais Dkt John Pombe Magufuli leo amezindia awamu ya kwanza ya miuondombinu ya mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART) hafla iliyofanyika katika kituo cha mabasi hayo kilichopo Kariakoo eneo la Gerezani.

Katika uzinduzi huo alihudhuria pia Makamu wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika na Mwakilishi wa Benki ya Dunia wa Tanzania na nchi za Afrika Mashariki kutokana na mradi huo kujengwa kwa ushirikiano wa Tanzania na Benki ya Dunia.

Serikali imeeleza mpango wake wa kujenga miundombinu ya mabasi ya mwendokasi ambapo mpango huo umegawanyika katika sehemu sita katika jiji la Dar es Salaam ikiwa ni njia ya kupungaza msongamano wa magari unaosababishara hasara kubwa kwa serikali na wakazi wa jiji hili.

Baada ya kuzindua mradi huo, Rais Dkt Magufuli aliendesha kidogo basi la mwendokasi akiashiri kuyazindua rasmi.

Mradi huo wa kipekee nchini Tanzania ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza foleni na watu kuweza kuwahi maeneno yao ya kazi na nyumbani ulianza kutumika mwezi Mei mwaka jana.

VIDEO: Waziri Mkuu Majaliwa Atembelea Kiwanda Cha Chai Cha Lupembe......Hapa Kuna Video ya Mambo Yote Aliyosema Kuhusu Viwanda Nchini

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo ametembelea  kiwanda cha chai cha Lupembe ili kukikagua ambapo amezungumza na wafanyakazi kuhusu azma ya serkali katika kufufua na kujenga viwanda hapa nchini.  Waziri mkuu  yupo ziarani   mkoa wa Njombe.

==> Tazama video hapo chini kujua alichokiongea

Rais mpya wa Gambia kurejea nyumbani siku ya Alhamisi

$
0
0
Rais mpya wa Gambia Adama Barrow anatarajiwa kurejea nyumbani siku ya Alhamisi, baada ya kiongozi wa zamani Yahya Jammeh kuondoka nchini humo kwenda kuishi nchini Equitorial Guinea.

Mai Fatty msemaji wa rais Barrow ambaye amekuwa akiishi nchi jirani ya Senegal alikoapishwa, ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP kuwa rais huyo mpya atarejea nyumbani ili kuanza rasmi majukumu ya kuliongoza nchi hiyo.

Aidha, Fatty amesema rais Barrow anatarajiwa kuwasili jijini Banjul Alhamisi mchana akitokea jijini Dakar.

“Ndio, kesho mchana atawasili,” Fatty ameliambia Shirika la AFP.

Barrow aliyeshinda Uchaguzi wa mwezi Desemba mwaka uliopita, alisema hawezi kurejea nyumbani hadi pale atakapopewa idhini na jeshi la Umoja wa nchi za Afrika Magharibi ECOWAS ambalo kwa sasa lipo jijini Bajul kuhakikisha kuwa kuna usalama hasa katika Ikulu na makaazi ya rais.

Maelfu ya raia wa Gambia ambao walikimbilia katika nchi jirani ya Senegal, wameanza kurejea nyumbani baada ya Jammeh kuondoka wiki iliyopita.

Jammeh alilazimika kuondoka nchini humo baada ya kutishiwa kuondolewa kwa nguvu na jeshi la ECOWAS lakini pia baada ya marais wa Mauritania na Guinea, kuingilia kati mzozo huo na kumshawishi kuondoka nchini humo na kukabidhi madaraka.

Papa amtimua kiongozi wa dini kwa kusambaza kondomu

$
0
0
Kiongozi wa kanisa katoliki anayewasaidia raia wa Malta amejiuzulu kufuatia mgogoro na Vatican kuhusu mpango wa kusambaza mipira ya kondomu kulingana na kanisa hilo.
 
Mathew Festing mwenye umri wa miaka 67 alijiuzulu baada ya papa Francis kumtaka kufanya hivyo katika mkutano siku ya Alhamisi. 

Hatua hiyo inafuatia ufichuzi kwamba tawi la hisani la kanisa hilo huko Malta lilisambaza maelfu ya mipira ya kondomu katika taifa la Myanmar.
 
Kanisa katoliki linakataza utumizi wa mipira ya kondomu. Papa Francis alimtaka ajiuzulu na alikubali. Tawi hilo la Malta lina uwezo mwingi kama ule wa taifa zima. Hutoa pasipoti, stampu na leseni na pia lina uhusiano wa kidiplomasia na mataifa 106 ,ikiwemo Vatican.

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images