Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mchungaji kizimbani kwa tuhuma za kubaka mwanaye

0
0
Mchungaji wa kanisa la  Free Pentekoste Church Tanzania (FPCT) Tawi la Gezaulole wilayani Hai, Emanueli Mwikizu (42) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Hai kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake  mwenye umri wa miaka 7.

Akisoma hati ya mashtaka mahakamani hapo mbele ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Anold Kirekiano mwendesha mashtaka wa polisi, Elisha Moleli amesema mtuhumiwa huyo alitenda kosa la kuzini akijua kufanya hivyo ni kosa la jinai.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Januari 17 mwaka huu  nyumbani kwake mtaa wa Gezaulo majira ya saa 3:30 asubuhi kwa kumwingilia kwa nguvu na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.

Mtuhumiwa huyo alikana shtaka hilo ambapo hakimu anayesikiliza kesi hiyo aliharisha hadi Februari 9 mwaka huu itakapotajwa tena na mtuhumiwa yupo rumande baada ya kushindwa masharti ya dhamana.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya January 29

Polisi Kanda Maalumu Ya Dar es Salaam yaua majambaz Wawili na Kukamata Wauza Shisha

0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewaua watu wawili wanaodaiwa kuwa ni majambazi na kukamata silaha pamoja na watuhumiwa kadhaa wa matukio ya kihalifu wakiwemo 7 wanaotuhumiwa kutengeneza kadi 7 za bandia za chanjo ya homa ya manjano

Akizungumza na vyombo vya habari, jana Jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro alisema, mnamo tarehe 23 mwezi wa kwanza mwaka 2017 majambazi hao walitekeleza tukio la mauaji na kupora kiasi cha shilingi milioni 1 na laki 3 huko Boko Basihaya na polisi iliwasaka na kuwakamata na wakakiri kutenda mauaji hayo na kwamba walipojaribu kutoroka ndipo walipouawa.

Akielezea kukamatwa kwa watu 7 wanaodaiwa kutengeneza kadi bandia za homa ya manjano ambazo mtu hupaswa kuchomwa chanjo hiyo kabla ya kusafiri nje ya nchi, Kamisha Sirro alisema, watu hao wamekuwa wakitoa kadi hizo na kudai fedha nyingi kinyume cha sheria.
Kamanda Sirro akionesha mkasi unaotumiwa na wahalifu kuvunja vitu mbalimbali

Jeshi hilo pia limewakamata watuhumiwa 92 wa makosa mbalimbali, ikiwemo wizi wa magari na pikipiki, watengenezaji wa gongo, shisha na uuzaji wa bangi.

Pia limekusanya zaidi ya Shilingi milioni 918, kwa ukamataji wa makosa ya usalama barabarani katika kipindi cha siku 10.
Kamanda Sirro akionesha magari yaliyokuwa yameibiwa katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam

Rais Magufuli amjibu Mkuu wa Wilaya aliyeomba kujiuzulu

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemjibu Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora aliyeomba kujiuzulu wadhifa huo.

Katika majibu yake Rais Magufuli ameridhia uamuzi huo na kwamba uteuzi wa mtu mwingine atakayejaza nafasi hiyo utafanyika baadaye.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Gerson Msigwa imesema

"Ombi la Bw. Gabriel Simon Mnyele aliyeomba kujiuzulu wadhifa wake wa Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora limekubaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora itajazwa baadaye."

Taarifa za kujiuzulu kwa mkuu huyo wa wilaya zilianza kusambaa jana zikidai kuwa aliaga katika Kamati ya Madiwani wa CCM na kamati ya siasa ya wilaya, pamoja na kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Halmashauri kuwa ameamua kuachia ngazi, bila kueleza sababu za uamuzi huo.
.

Wanajeshi Waua Kondakta Kwa Kipigo Tanga

0
0
Kondakta wa daladala linalofanya safari zake kati ya Nguvumali hadi Raskozone, Salim Kassim amefariki dunia baada ya kudaiwa kushambuliwa ndani ya kambi ya jeshi jijini Tanga.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba, kondakta huyo alikufa wakati akipelekwa katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo na chanzo cha kifo bado kinachunguzwa.

Imeelezwa kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku, ambapo mashuhuda walidai kuona kondakta huyo akichukuliwa na wanajeshi na kuingizwa kambini na baadaye alitolewa akiwa hajitambui

Akizungumzia tukio hilo, Khalid Juma mkazi wa Nguvumali jijini hapa alisema askari hao wamekuwa na desturi ya kuwapiga wananchi bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria.

“Tumekuwa tukipata vipigo kila wakati, licha ya viongozi kupata taarifa za matukio hayo wamekaa kimya na hili tukio ni la tatu kutokea hapa,” alidai Khalid.

Diwani wa Kata ya Nguvumali ambaye pia ni Meya wa Jiji la Tanga, Alhaji Mustapha Selebosi alisema sababu za kipigo hicho ni mwanafunzi wa shule moja jijini Tanga ambaye ni mtoto wa ofisa wa JWTZ kuzozana na kondakta.

==>Zaidi, Tazama  Video Hii

Furahia Vifurushi vya tiGo .......Jiunge na Megamix kwa kupiga *148*00# , kisha chagua Vifurushi Bomba vya Internet

0
0
Jua zaidi, tatua zaidi! Jiunge na Megamix kwa kupiga *148*00# , kisha chagua Vifurushi vya Internet

Kasi ya uokoaji watu 14 waliofukiwa mgodini yazidi kupamba moto

0
0
Bado kazi ya uokoaji wa watu 14 waliofukiwa na kifusi katika Mgodi wa Dhahabu wa Kampuni ya RZ Union Mining Ltd uliopo Kata ya Nyarugusu mkoani Geita inaendelea, na hadi jana waokoaji hawajafanikiwa kuokoa mtu yoyote.

Pamoja na juhudi hizo za uokoaji, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga amesema kuwa ana imani watu hao wataokolewa wakiwa hai.

Amesema kuwa jana imefanyika kazi kubwa ya kuchimba kifusi ili kutafuta njia ya kuwafikia waathirika huku mipira zaidi ya Oxygen ikiingizwa chini ya mgodi waliko watu hao ili kuwaongezea hewa.

Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Latson Mponjoli amesema juhudi za uokoaji zinaendelea kwa ushirikiano wa vikosi vya uokoaji vya Kampuni ya Geita Gold Mine (GCM), Jeshi la Zimamoto na Polisi pamoja na kikosi cha ukoaji cha Sekta ya Madini.

Amesema hali ni shwari katika eneo hilo na wana matumaini ya kuwafikia watu hao wakiwa hai.

Pia, Kampuni inayoendesha mgodi huo imesema kutokana na kitabu cha orodha ya watu wanaojiandikisha kuingia mgodini, kuna majina ya Watanzania 12 na Mchina mmoja waliofukiwa kifusini. Ilielezwa kuwa watu pia waliomshuhudia Mtanzania mmoja akingia mgodini humo bila kujiandikisha na hivyo kufanya waliofukiwa kufikia 14.

Watanzania 13 na raia mmoja wa China walifukiwa na kifusi juzi usiku baada ya udongo kuziba mlango waliokuwa wakitumia kuingia na kutoka.

Mwanafunzi Chuo cha Ardhi kizimbani kwa Kuchapisha ujumbe wa Uongo WhatsApp Kuhusu Godbless Lema

0
0
Mwanafunzi  wa Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es Salaam (ARU) amefikishwa katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kupandishwa kizimbani akikabiliwa na kosa la kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa What’sApp.

Akimsomea hati ya mashtaka, mshtakiwa huyo, Wakili wa Serikali, Adolf Mkini mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa alidai kuwa mshtakiwa huyo  ambaye pia anadaiwa kuwa ni kada wa Chadema Januari 3, 2017
alichapisha taarifa za uongo.

Alidai kuwa mshtakiwa huyo kupitia mtandao wa WhatsApp kwenye kundi linalotumia jina la Lowassa Foundation and Bunge Live alichapisha taarifa za uongo kuwa; Nimepata rehema ya mipango michafu sana iliyokuwa inapangwa na bado inapangwa dhidi ya uhai wa (Mb), Godbless Lema…’

Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikana kuhusika na kosa hilo.

Upande wa mashtaka umedai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na hana pingamizi na dhamana.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mwambapa alimpa masharti ya dhamana mshtakiwa huyo ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh 2 milioni  kwa kila mmoja pamoja na barua.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo aliepuka kwenda lumande baada ya kutimiza masharti hayo ya dhamana.

Mume na mmiliki wa Famasi Watiwa mbaroni Kwa Kusababisha Kifo cha mjamzito

0
0
Watu  wawili, akiwemo mmiliki wa duka la dawa muhimu za binadamu katika kijiji cha Itagata wilayani Manyoni, wanashikiliwa na Polisi mkoani Singida kwa tuhuma za uzembe wa kusababisha kifo cha mjamzito, Heleni Maduhu (29).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni mume wa marehemu, Bahame Kamuda (32) na Joseph Hengwe (50) ambaye ni mmliki wa duka la dawa katika kitongoji cha Kilulumo, kijiji cha Itagata Tarafa ya Itigi wilayani Manyoni.

Alisema tukio lilitokea kitongoji cha Lulanga kijijini hapo Januari 25, mwaka huu saa 9.30 alasiri wakati mjamzito huyo akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Misheni ya Itigi kwa matibabu zaidi kutokana na kuvuja damu nyingi baada ya kujifungulia kwenye duka la Dawa la Hengwe.

Alisema kuwa siku moja kabla, mume wa mjamzito huyo alimpeleka mkewe kwenye Zahanati ya kijiji Itagata ili kufanyiwa uchunguzi ambapo inadaiwa muuguzi wa Zahanati hiyo, Grace Simon iliwaambia njia ya uzazi ilikuwa haijafunguka; hivyo akawashauri warudi nyumbani.

Alisema kuwa aliporejea nyumbani hali ya mjamzito huyo ikawa mbaya hivyo kumlazimu mumewe kumpeleka Zahanati ya jirani ya Misheni katika Kijiji cha Mitundu kwa matibabu zaidi.

Hata hivyo, Kamanda Magiligimba alidai kuwa wakiwa njiani, mumewe aliona hali ya mkewe inazidi kuwa mbaya zaidi, aliamua kumpeleka kwenye duka la dawa muhimu linalomilikiwa na Hengwe lililopo jirani ambapo alijifungua mtoto wa kiume.

“Kutokana na mjamzito huyo kuvuja damu nyingi baada ya kujifungua, mumewe aliamua kumkimbiza katika Hospitali ya Misheni ya Itigi kwa pikipiki lakini kwa bahati mbaya hawakuweza kufika mbali kabla ya mama huyo kufariki dunia,” alisema Magiligimba.

Waziri Mkuu amtwisha mzigo Ole Sendeka Kuhusu mapato na matumizi ya Mamlaka ya Maji ya Mji wa Njombe

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka leo awapeleke wakaguzi wa heshabu kwenda kukagua mapato na matumizi ya  Mamlaka ya Maji ya Mji wa Njombe (NJUWASA).

Ametoa agizo hilo jana (Ijumaa, Januari 27, 2017) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Mpechi, Halmashauri ya Mji wa Njombe.

Waziri Mkuu alisema wakaguzi hao mbali na kukagua mapato na matumizi ya mamlaka hiyo pia waangalie kama wananchi walihusishwa katika ukokotoaji wa gharama za malipo ya bili za maji.

Alitoa agizo hilo baada ya wananchi kuilalamikia mamlaka hiyo kupitia mabango kwamba wanatozwa bili kubwa ya maji licha ya huduma hiyo kupatikana kwa kusuasua katika mji huo.

Kufuatia malalamiko hayo Waziri Mkuu alimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa NJUWASA, Bw. Daudi Majani kutoa ufafanuzi juu ya jambo hilo ambapo alisema kwa mwezi wanakusanya sh. milioni 75 zinazotumika kuendeshea na uboreshaji wa huduma.

“Maji hakuna unasema unaboresha unaboresha huduma gani? Wananchi wanalalamika maji hakuna na mnawatoza gharama kubwa, Mkuu wa Mkoa kesho peleka wakaguzi wakakague kwa mwezi anakusanya kiasi gani na anafanyia nini,”

Wakati huo huo, Waziri Mkuu aliwataka watumishi wa umma kujiwekea utaratibu wa kwenda kwa wananchi na kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuzitafutia ufumbuzi badala ya kujifungia maofisini.

“Uwepo wa mabango mengi kwenye mikutano ya hadhara ya viongozi ni ishara tosha kwamba watendaji hamuendi kwa wananchi kuwasikiliza kero zao. Mabango mengi hapa si ya Waziri Mkuu ni hapahapa,” alisema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Rais Magufuli Aelekea Addis Ababa, Ethiopia, Kwenye Mkutano Wa 28 Wa Wakuu Wa Nchi Za Umoja Wa Afrika

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,  tarehe 28 Januari, 2017 ameondoka nchini na kuelekea Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia ambako atahudhuria mkutano kilele wa 28 wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika (AU) unaoendelea nchini humo.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli ameagwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Bw. Paul Makonda.

Pamoja na kuhudhuria Mkutano huo, akiwa Addis Ababa Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Bara la Afrika wanaohudhuria Mkutano huo.

Hii ni ziara ya kwanza ya Mhe. Rais Magufuli nje ya Afrika Mashariki tangu aingie madaraka kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 05 Novemba, 2015

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
28 Januari, 2017

Wachimbaji Waliofukiwa na Kifusi Wasema Wako Hai.....Watuma Majina Yao

0
0
Wakati  imeelezwa kuwa waokoaji katika mgodi wa dhahabu wa RZ Union ulioko Geita , wamebakiza mita tatu kuwafikia waliofukiwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Medard Kalemani akizungumza na ndugu wa watu waliofukiwa amesema kwamba wanafanya mpango wa kuwapelekea chakula wachimbaji hao.

Amesema kwamba jana wamefanikiwa kufanya mawasiliano na wachimbaji hao na kwamba wapo kumi na watano na kuwa wanachohitaji kwa sasa ni chakula.

Alisema waokoaji walifanikiwa kuwafikishia kamba na kalamu watu hao ambao waliandika majina  na  mahitaji yao na kusema kwamba wote wapo salama.

Watu hao akiwemo raia wa China mmoja walifukiwa na kifusi juzi usiku baada ya udongo kukatika na kuziba mlango waliokuwa wakitumia kuingia na kutoka na uokoaji unaendelea kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya uokoaji.

Watu wengi wapo katika eneo hilo wakiwemo ndugu wa waliofukiwa lakini kwa juhudi wanazoziona za uokoaji wametulia na kufuata maelekezo wanayopewa ikiwemo kukaa mita 500 toka eneo la tukio.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya January 29

SORRY MADAM -Sehemu ya 23 & 24 (Destination of my enemies)

0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
“LUKASSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSS…………………………………………..!!!!”
Askari huyo alipiga ukelele wa maumivu na uchungu baada ya kumshudia mwenzake huyo akikata roho, yeye akiwa gorofani, kelele hizo zikawafanya askari wangine walio kuwa wakiwa huduma ya kwanza wezo kukimbilia alipo mwenzao. Agnes akatabasamu kwa dharau kisha akamnyooshea kidole cha kati askari huyo anaye lia kwa uchungu kisha akaondoka zake kwa kujiamini sana.

ENDELEA
Agnes akaanza kushuka chini kwa kutumia ngazi katioka gorofa aliyo ingia huku mara kwa mara akifanya mawasiliano na Jaquline ambaye aliamua kusitisha zoaezi la kumteka raisi, akatoka nje, gari aliyo kuja nayo ikamchukua na moja kwa moja akaelekea sehemu ambayo Agnes alimuelekeza
                                                                                                      ***
     Hadi kuna pambazuka Eddy, hakuweza kupata hata lepe la usingizi, akanyanyuka kwenye kiti alicho kuwa amekaa usiku kucha, akatoka nje na moja kwa moja akaelekea kwenye makaburi ya familia yeka. Akasimama kwa dakika kadhaa akiyatazama makaburi hayo, hakuamini kwamba ni kweli familia yake imeweza kupotea gafla na kubaki akiwa peke yake, kila alipo mfikiria mzee Godwin machozi ya hasira na uchungu ndivyo yalivyo zidi kumwagika. Akastukia akishikwa mkono wake wa kushoto taratibu akaigeuza shingo yake na kumkuta Shamsa akiwa amesimama pembeni yake huku naye akionekana kuwa na huzuni nyingi sana usoni mwake.

“Madam Mery ameondoka”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya unyonge huku macho yake akiwa ameyaelekezea kwenye makaburi hayo matatu
“Amekwenda wapi?”
“Hakuniambia ni wapi alipo kwenda”
“Achana naye”
“Ila baba, kuna mambo mengi muhimu amaniambia nikuambia”
“Mambo gani?”
Eddy alizungumza huku akimtazama Shamsa usoni aliye onekena kusita kwa kile ambacho anahitaji kwenda kukizungumza mbele ya Eddy anaye mchukulia kama baba yake mlezi.
“Mbona umekaa kimya huwezi kuzungumza?”
“Ni ni kuhusiana na baba yako?”
“Baba yangu……!!”
“Ndio mzee Godwin”

Eddy akatazama kila kona, akamshika mkono Shamsa, wakatafuta sehemu iliyo tulia kwenye moja ya bustani zilizopo ndani ya njumba lake la kifahari.
“Alikuambia kuhusiana na nini?”
“Jana usikua alinieleza kila kitu kuhusiana na kikundi cha D.F.E. Hicho ni kikundi ambacho kimeanzishwa na mzee Godwin mwenyewe, kazi yake kubwa ni kuhakikisha kwamba wanalipiza visasi kwa wale wote ambao waliweza kuwatemndea ubaya katika maisha yao.”

“Aliniambia kwamba hicho ni kikundi kikubwa sana na kina wafuasi wengi ambao wengine wamo ndani ya serikali yetu ya Tanzania, na anashirikiana nao”
“Amekutajia majina?”
“Hapana hajanitajia majina. Ila anadai wafuasi hao ni watu wakubwa sana serikalini, si Tanzania pekee bali nchi nyingi za Afrika pamoja na nchi za Amerika, ikiwemo Marekani”
Shamsa akanyamaza kimya kidogo kisha akaendelea kuzungumza kwa umakini kile alicho ambiwa kukizungumza kutoka kwa madam Mery ambaye alihofia kufanya hilo.

“Watu hao wana chata ndogo kwenye sehemu za miili yao, yenye maandishia meusi D.F.E. Ameneniambia kwamba msaidizi wa mambo yote ya kikundi hicho ni mtu ambaye anakujua vizuri kuanzia A hadi Z, ukimuachilia kiongozoi wao mzee Godwin”
“Ni nani huyo?”
“Alinitajia kwa jina moja tu……..JONH”
Eddy akatumbua macho yake huku akimtzama Shamsa, akiwa haamini kitui alicho kizungumza kwani kumbukumbu ya mwisho anakumbuka jinsi alivyo vikata viungo vya John kwa kulipiza kisasi cha mambo yote aliyo mfanyia.

“JOHN…..JOHN…….!!!”
“Ndio huyo huyo John, pia ameniambia mtu wa kwanza kuweza kulengwa katika mikakati yao ni wewe, wanataka kukuangusha chini, ten echini kabisa ya aridhi”
Eddy akajikuta akishusha pumzi nyingi, woga wa gafla ukamuingia moyoni mwake, kajasho kembamba kakaanza kumwagika kwani hakujua ni jinsi gani ambavyo wanaweza kumuangusha.

“Ahaa….aaaa aahaame ame kwenda wapi Madam Mery?”
“Hakuaniambia ni wapi anapo elekea kwa sasa, ila kitu kingine cha mwisho alicho niambia nikuambia ni kwamba, ujiudhuru nafasi yako hiyo ya uongozi kwani ni rahisi kwa wao kuweza kukupata, pili kati ya watu ambao unafanya nao kazi serikalini wana kisasi na wewe, ikiwemo wale ambao uliwaharibia biashara zao kipindi ambapo iliingia madarakani, wana uchungu na kisasi kikubwa juu yako”

Eddy akahisi kichwa chake kinapasuka kwa maumivu makali ambayo anayapata kwa taarifa hiyo ambayo si nzuri kwa upande wake. Taratibu akanyanyuka kwenye kiti alicho kaa na moja kwa moja akaelekea ndani kwake. Akafungua kabati lake lenye baadhi ya vitu muhimu, akatoa kikopo kidogo chenye dawa za kutuliza mawazo, akatoa vidogo kadhaa na kuvimeza, pasipo kutumia maji, kisha akajitupa kitandani.

“Kwa nini kila kitu kinanitokea mimi tuuuuuuuuuuuuu”
Eddy alizungumza kwa sauti ya ukali iliyo jaaa jasira na uchungu ndani yake, akiwa katika kuhangaika hangaika kitandani kujaribu kuutafuta japo usingizi, mlango wake ukagongwa mara mbili.
“Nani?”
Mlango ukafunguliwa pasipo mtu huyo kujibu, Eddy akamkuta Rahab akiwa amesimama mlangoni peke yake, Rahab akapiga hatua moja mbela na kuufunga mlango kwa ndani.
“Umefwata nini huku ndani?”
Eddy alizungumza huku akishuka kitandani

“Nimekuja nahitaji kuzungumza na wewe?”
Rahab alizungumza huku akipiga hatua kadhaa kumfwata Eddy kitandani
“Twende tukazungumzie nje ila si ndani ya chumba ninacho lala na mke wangu”
Eddy alizungumza kwa ukali kidogo, hakujali Rahab ni mke wa raisi au laa, kabla Eddy hajafika mlangoni Rahab akamuita na kumfanya Eddy kugeuka na kutazama ni kitu gani ambacho Rahab anamuitia.
“Eddy ninakupenda?”
“Upo sawa wewe?”
“Ndio nipo sawa, na ninacho kizungumza ni kitu kitokacho moyoni mwangu”

Rahaba akapiga hatua kadhaa hadi alipo simama, wakatazama kwa muda, kitendo ambacho kikaanza kumfan ya Rahab kumwagikwa na machozi.
“Eddy nipo tayari kuacha kila kitu kwenye maisha yangu, ili niwe na wewe. Wewe ni mwanaume wa kwanza katika haya maisha yangu kukupenda, ni mwauaume abaye umeweza kuziteka hisia zangu tangu siku ya kwanza nilipo kuona picha yake nyumbani kwa mama yako”
“Eddy nimekuwa mtumwa kuanzia siku hiyo nimekuwa ni mtu wa kuishi na majuto ya kwanini niliamua kuolewa na Praygod, ambaye si chagua la moyo wangu”
                                                                                                      ***
Wasiwasi mwingi ukaanza kumtawala Raisi Praygod, kila alipo jaribu kuipiga simu ya mke wake, inaita hadi kukata, akamuita mlinzi wake mmoja anaye muamini sana.
“Mama yupo wapi?”
“Ametoka kama dakika kumi zilizo pita hivi”
“Ameenda wapi?”
“Hakuniambia, ila ngoja kwanza nimpigie dereva wake”
Kijana huyo akatoa simu yake mfukoni na kumpigia dereva wa madam Rahab, simu ikaita baada ya muda ikapokelewa
“Upo wapi?”
“Nipo nyumbani kwa muheshimiwa Eddy”
“Upo na madam?”
“Ndio, ameingia ndani?”
“Mlinzi wake yupo wapi?”
“Yupo nje ya gari, kwani vipi?”
“Ahahaa hakuna kitu”

Kijana huyo akakata simu, na kumtazama raisi Praygod anaye onekena kujawa na wasiwasi kwani si kawaidia ya mke wake kuto kupoke simu kwa kipindi kirefu.
“Yupo kwa waziri wa ulinzi bwana Eddy Godwin”
‘Eddy Eddy’
Wivu wa mapenzi ukaanza kuusumbua moyo wa raisi Praygod, kila alipo jaribu kuvuta baadhi ya kumbukumbu, siku jinsi alivyo wakuta Eddy na mke wake kwenye chumba cha waziri huyo kijana mdogo, alihisi kitu kilicho kuwa kikiendelea ila hakuweza kukiweka kichwani mwake akiamini kwamba ni jambo la kawaida.

‘Kwanini leo tena aende kama walisha maliza kuzungumza jana?’
Raisi Pryagod alijiuliza tena kichwani mwake swali ambali jibu lake likajaa wasiwasi mwingi, akakumbuka kitu kimoja kilicho mstua, wakati Rahab anamueleza anakwenda kuonana na Eddy kwenye chumba chake, rangi ya mdomoni mwake, ilikuwa imekolea vizuri tu. Ila alipo ingia na kuwakuta rangi hiyo ya mdomoni haikuwa kama vile alivyo ingia nayo.
‘Au alimkiss mke wangu kilazima?’
Hapo ndipo raisi Praygod akahisi kuna kitu ambacho kinaendelea kwa watu wawili hao, asira na uchungu mkali ukampanda moyoni mwake.

“Andaa ndege nahitaji Eddy na mwanae aliye baki wapelekwe mbali na Tanzania”
“Sawa muheshima na tuwapeleke wapi?”
“Popote ila mbali na Tanzania, na hii taarifa umpelekee baada ya kila kitu kuwa sawa”
“Sawa muheshimiwa”
“Ila Lube, hakikisha kwamba hili jambo umuelezi mke wangu,  iwe siri yako mimi na wewe”
“Sawa muheshimiwa”
“Pia hakikisha unawafwatilia hatua moja hadi nyingine, na kila kinacho endelea hakikisha kwamba unaniambia”
Raisi Praygod akajikuta akiachia tusi zito, lililo jaa hasira, akihisi hali ya mahusiano kati ya Eddy na Rahab
“Nitakuuaa wewe mshezi Eddy”
                                                                                                           ***
Madam Mery akiwa ndani ya basi la Ngorika liendalo mkoani Arusha, mawazo mengi yakamtawala moyoni mwake, kila alipo jaribu kufikiria mambo aliyo mfanyia Eddy, roho yake ilizidi kumuuma sana hadi wakati wingine akatamani kufa kwani hastahili kabisa kuwa binadamu anaye paswa kusamehewa.

Akaanza kukumbuka jinsi mahusiano mazuri yaliyo kuwepo kati yake na Mzee Godwin, kipindi alipo mleta Eddy shuleni kwake kumuanzisha kidato cha tano. Ni siku ambayo mzee Godwin aliweza kumkabidhi Eddy kwake awe anamtzama kwa kila kitu na hata baadhi ya pesa ya matumizi ya Eddy aliweza kumuachia endapo Eddy ataishiwa na pesa iwe rahisi kumsaidia.

Uchshi, ukaribu na uzuri wa Eddy, ndivyo vitu ambavyo vilimkosesha ujasiri na ustahimilivu wa kuzuia hisia zake za mapenzi juu ya Eddy. Kitu kilicho muumiza akili ni jinsi gani ambavyo angeweza kumuanza Eddy katika swala zima la mahusiano isitoshe yeye alikuwa ni mwalimu wake.

Siku ambayo aliweza kumkuta Eddy chumbani kwake akiwa ameshika mdoli wake ulio kaa kama jinsia ya mwaume, alio kuwa akiutumia katika kujichua pale hamu, zinapo mzidi, ndipo ikawa nafasi yake ya kuweza kufanya kila kitu kwa ajili ya kumpata kijana huyo aliye tokea kuutesa moyo wake.

Rais Magufuli Ahudhuria Kikao Cha Umoja Wa Afrika (AU) Mjini Addis Ababa Ethiopia

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 29 Januari, 2017 ameanza kuhudhuria mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) unaoendelea Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Asubuhi hii Mhe. Dkt. Magufuli amehudhuria mkutano ulioitishwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe. Idriss Deby Itno ambapo wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika wanakutana na Katibu Mkuu Mpya wa Umoja wa Mataifa (UN) Mhe. Antonio Guterres.

Madhumuni ya mkutano huo ni kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uhusisano kati ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, hususani katika kuimarisha masuala ya amani na usalama.

Mkutano huo utafuatiwa na mkutano maalum wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika utakaoongozwa na Mwenyekiti wa Umoja huo Mhe. Idriss Deby Itno.

Mhe. Rais Magufuli pia atahudhuria chakula cha mchana kilichoandaliwa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika (AUC) Mhe. Dkt. Nkosazana Dlamini Zuma kwa lengo la kutangaza rasmi jina la kituo kipya cha amani na usalama ambacho kimepewa jina la Mwalimu Julius Nyerere ikiwa ni kutambua mchango wake katika kupigania amani na usalama wa Afrika.

Kituo hicho kipo ndani ya majengo ya makao makuu ya Umoja wa Afrika Mjini Addis Ababa na Mhe. Rais Magufuli atatoa hotuba fupi mara baada ya kukitangaza rasmi.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Addis Ababa

29 Januari, 2017

Balozi Ombeni Sefue ateuliwa katika Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora

0
0
Mwanadiplomasia mahiri wa Tanzania aliyepata pia kuwa Katibu Kiongozi-Ikulu, Balozi Ombeni Sefue ameteuliwa kuwa Mtanzania wa kwanza kuingia katika Jopo la Watu Mashuhuri katika Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM).

Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa APRM tawi la Tanzania, Rehema Twalib anayehudhuria mikutano ya Umoja wa Afrika na APRM mjini Addis Ababa, Ethiopia, Balozi Sefue ameidhinishwa kwenye kikao cha juu ya Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika ambao ni wanachama wa APRM kilichofanyika juzi Jumamosi mchana.

“Haikuwa kazi rahisi kupata nafasi hii. Nchi nyingi za Afrika zilileta majina ya watu wao mashuhuri ili kuingia katika jopo hili muhimu. Balozi Sefue licha ya kuwa na utumishi uliotukuka kama mwanadiplomasia mkongwe pia aliungwa mkono kwa nguvu zote na Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania,” alisema Katibu Mtendaji huyo.

APRM ni Mpango wa Afrika uliobuniwa na Wakuu wa Umoja wa Afrika kwa lengo la kuwa na chombo kitakachosaidia kuhimiza nchi wanachama kuenzi utawala bora na utoaji wa huduma bora za kiuchumi, biashara na za kujamii kwa wananchi wao kupitia mfumo wa kujitathmini zenyewe na kukosoana.

Kwa mujibu wa tovuti ya APRM, Jopo la Watu Mashuhuri ni chombo cha juu cha kuwashauri Wakuu wa Nchi Wanachama wa APRM katika uendeshaji wa Mpango huo na husimamia mchakato mzima wa kujitathmini.

Wajumbe wa jopo hilo ambao hudumu hadi miaka minne hupendekezwa na nchi zao na baada ya mchakato mrefu wenye ushindani majina ya waliokidhi vigezo huwasilishwa na kuidhinishwa na na kikao cha juu katika APRM-Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali.

Tanzania ni miongoni mwa wanachama 35 kati ya nchi 54 wa Nchi za AU zilizojiunga na APRM na ilijiunga rasmi na Mpango huo tangu mwaka 2004.Tayari Tanzania ilishafanyiwa tathmini ya kwanza ya utawala bora na inaendelea kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa.

Katika mkutano huo Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za APRM Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aliwapongeza wajumbe wa jopo hilo na kuwata kushiriki vyema katika kuihuisha APRM na kuwa chombo chenye thamani kubwa kwa Afrika kama walivyotarajia waasisi wake akina Thabo Mbeki, Olusegun Obasanjo, Benjamin Mkapa na wengine.

Balozi Sefue ataungana na wajumbe wengine wapya ambao ni pamoja na Prof. Ibrahim Agboola Gambari (Nigeria), Balozi Mona Omar Attia (Misri) Bi. Fatma Zohra Karadia (Algeria), Askofu Don Dinis Salomão Sengulane (Msumbiji) na Prof. Augustin Loada (Burkina Faso). Wajumbe wa zamani wanaoendelea ni pamoja na  Prof. Youssouf Khayal (Chad) ambaye kwa sasa atakuwa Mwenyekiti wa Jopo hilo na Brigitte Mabandla (Afrika Kusini) ambaye atakuwa Makamu Mwenyekiti.

Mkutano huo pia ulijadili Ripoti za tathmini za nchi katika maeneo anuai ya utawala bora kwa nchi za Kenya (ikiwa ni ripoti ya pili kuwasilishwa), Sudan, Chad, Senegal, Djibouti pamoja na ripoti ya utekelezaji ya Zambia.

Picha: Wachimbaji 15 waliofukiwa mgodini Geita waokolewa wakiwa hai

0
0
Wachimbaji 15 waliokuwa wamefukiwa na kifusi katika mgodi wa RZ Nyarugusu mkoani Geita wameokolewa wote wakiwa hai.

Wachimbaji hao wameokolewa leo asubuhi baada ya jitihada za uokoaji kufanyika kwa muda mrefu. Matumaini ya kuwapata watu hao yaliongeza jana usiku ambapo walituma ujumbe kwenye karatasi kuwa wapo 15 na kuorodhesha mahitaji yao

Taarifa za kufukiwa kwao zilizeleza kuwa miongoni mwa waliofukiwa ni pamoja na raia mmoja wa China.Mgodi huo unamilikiwa na mwekezaji kutoka nchini China.

Picha za zoezi la uokoaji lilivyofanyika

TAARIFA: Kukanusha Taarifa Iliyoandikwa Na Gazeti La Raia Mwema Kuhusu Kuongezwa Muda Wa Leseni Za Vitalu Vya Uwindaji Bila Kufuata Taratibu

0
0

Wizara ya Maliasili na Utalii inakanusha taarifa iliyoandikwa na gazeti la Raia Mwema Toleo Na. 494 (ISSN 1821-6250) la Jumatano tarehe 25-31 Januari, 2017 ikiwa na kichwa cha habari “Waziri Maghembe Matatani”. Habari hiyo imeeleza kuwa, Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe anadaiwa kuongeza muda wa leseni za vitalu vya uwindaji kwa kampuni za uwindaji wa kitalii kinyume na taratibu.

Aidha, habari hiyo imeeleza kuwa waziri hakufuata utaratibu uliowekwa katika kifungu cha 38 (6) cha Sheria ya Uhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 ambayo inaweka utaratibu wa kufuatwa kabla waziri hajatoa leseni upya. Pa, habari hiyo imeeleza kuwa sheria hiyo inataka itangazwe kwenye magazeti utaratibu wa kuomba vitalu kwa waombaji pamoja na kufanyiwa tathmini.

Vilevile, habari hiyo imeeleza kuwa waziri anatakiwa kushauriwa na chombo ambacho ndicho hufanyia tathmini kampuni hizo. Taarifa hiyo imeripoti kuwa hapo awali kulikuwa na kamati ya kumshauri waziri ambayo ilivunjwa mwaka 2012 na aliyekuwa waziri wa Wizara hiyo, Khamis Kagasheki na hivyo kuhoji uhalali wa kufanya maamuzi bila kushauriwa na chombo hicho.

Habari hiyo siyo ya kweli, kwani Waziri hakutoa leseni za umiliki wa vitalu vipya bali ameongeza muda wa umiliki wa vitalu kwa mujibu wa kifungu cha 38 (8) cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 sambamba na kanuni ya 16 ya Kanuni za Uwindaji wa Kitalii za mwaka 2015. Sheria na Kanuni hiyo inaelezea utaratibu wa kuongeza muda wa umiliki wa vitalu kwa wale walioomba kuendelea na umiliki wa vitalu vya awali (renewal of hunting block).

Waziri kabla ya kuongeza muda wa umiliki wa vitalu (renewal) alikaribisha maombi kwa wale wanaotaka kuongezewa muda wa umiliki wa vitalu wanavyovimiliki kwa mujibu wa Sheria tajwa hapo juu kwa barua yenye Kumb. Na. CHA.79/519/47 ya terehe 22 Aprili, 2016. Aidha maombi hayo yalipitiwa na Kamati ya Ushauri ya Ugawaji wa Vitalu vya Uwindaji ambayo ipo kisheria na iliteuliwa Septemba 2013, kinyume na madai ya mwandishi kuwa Kamati hiyo haipo. Baada ya tathmini ya maombi hayo, Kamati hiyo ilimshauri Waziri kwa mujibu wa sheria.

Kwa kufuata utaratibu ulioanishwa katika Kifungu cha 38 (8) na (9) cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori, kifungu hiki kinampa Mamlaka Waziri kuongeza muda wa umiliki wa vitalu (Renew of hunting blocks). Kanuni ya 16 kanuni ndogo ya (1), (2), (3), (4), (5), (7), (8), (9) na (10) ya Kanuni za Uwindaji wa Kitalii  zinatoa utaratibu wa kufuatwa wakati wa kuongeza muda wa umiliki wa vitalu kwa muhula mwingine wa uwindaji na utaratibu huo umefuatwa.

Kwa kuzingatia utaratibu huo, wamiliki wa sasa wa vitalu kama Kanuni zinavyoelekeza, waliwasilisha maombi yao Wizarani. Idara ya Wanyamapori ilipitia maombi hayo na kuwasilisha kwenye Kamati ya Ushauri ya Ugawaji wa Vitalu vya Uwindaji. Kamati hiyo ilipitia maombi hayo tarehe 26 hadi 27 Julai 2016 na tarehe 13 Januari 2017. Hivyo, baada ya Kamati kukamilisha taratibu zote na kujiridhisha iliwasilisha ushauri wake kwa Mhe. Waziri.

Kifungu cha 38 (6) cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori alichokitaja mwandishi wa gazeti hilo, kinaeleza utaratibu wa ugawaji wa vitalu kwa waombaji wapya na siyo kwa wale wanaoomba kuendelea na umiliki wa vitalu kwa msimu mwingine (renewal).
 
Uongezaji wa muda wa umiliki wa vitalu vya uwindaji ulifuata Sheria, Kanuni na Taratibu, Hivyo tunawoamba wananchi wapuuze habari hiyo kwani mwandishi alikusudia kuupotosha umma kwa kunukuu na kutafsiri vifungu vya Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori isivyo sahihi.

Imetolewa na,
KATIBU MKUU
29 Januari, 2017

Mahakama Yapiga marufuku amri ya Rais Trump kuzuia Watu Kuingia Marekani

0
0
Mahakama moja ya New York Marekani imeridhia ombi la wanaharakati waliokwenda Mahakamani kupinga amri ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo, kupiga marufuku Wakimbizi wa Syria na raia wengine wa nchi sita za kiislamu kama Iran, Iraq, Somalia, Sudan, Libya na Yemen wasiingie Marekani.

Mahakama hiyo imeamuru wote waliozuiliwa kupitia amri hizo waachiwe ikiwa ni agizo la lililotolewa saa kadhaa baada ya kuwepo Ripoti kutoka uwanja wa ndege wa John F Kennedy New York kwamba watu kadhaa wamezuiwa kuingia Marekani wakiwemo wale ambao walikuwa wamepewa ruhusa kwenda kuishi Marekani kupitia mpango maarufu wa Green Card.

Tayari pia Raia wawili wa Iraq wameishitaki Mahakamani serikali ya Marekani baada ya kushikiliwa kwenye uwanja wa ndege wa John F. Kennedy New York na kuzuiwa kuingia Marekani ambapo inaripotiwa wakati huo kuna raia wengine 10 walikua wamezuiwa kuingia Marekani muda mfupi tu baada ya ndege kutua.

Picha: Treni ya abiria yapata ajali ikitokea Kigoma kwenda Dar

0
0
Treni ya abiria ya EXPRESS ikitokea Kigoma kuelekea Dar es salaam leo January 29 2017 imepata ajali maeneo ya Ruvu ndani ya mkoa wa Pwani ikiwa ni kilometa kadhaa kabla ya kufika kwenye jiji la Dar es salaam.
Shuhuda ambaye alikua ndani ya Treni hiyo amesema Behewa zaidi ya 10 zimepinduka na watu wanaendelea kuokolewa kwa kupitia Madirishani.

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images