Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ataja sababu vyakula kupanda bei sokoni........Asisitiza Tanzania Haijakumbwa na Baa la Njaa

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema nchi haijakumbwa na baa la njaa na amewataka Watanzania kutosikiliza kampeni za upotoshwaji zinazofanywa na baadhi ya wafanyabiasha kuhusu hali ya chakula kwani si za kweli bali ni za uzushi zenye lengo la  kupandisha bei za vyakula.

Amesema Serikali ndio yenye jukumu la kutoa taarifa za kuwepo kwa njaa ama kutokuwepo na kwamba taarifa zinazosambazwa za kuwepo kwa baa la njaa nchini hazina ukweli wowote na Serikali inawahakikishia wananchi kuwepo kwa usalama wa chakula.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Januari 16, 2017) wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa Dodoma baada ya kuzindua safari za ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, ambapo amesisitiza kwamba hali ya upatikanaji chakula nchini ni tofauti na inavyoelezwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo baada ya kutolewa kwa taarifa katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu kuwepo kwa baa la njaa nchini jambo ambalo si la kweli. Amewataka wananchi kuwa watulivu na jambo hilo likitokea Serikali itatoa taarifa.

“Mwaka jana nchi ilikuwa na akiba ya chakula cha zaidi ya tani milioni tatu hali iliyopelekea baadhi ya Wabunge na wafanyabiashara kuomba kibali cha kuuza nafaka nje ya nchi, ambapo Serikali ilitoa kibali hicho baada ya kujiridhisha kuwepo kwa akiba ya kutosha ya chakula,” amesema.

Amesema baada ya kutolewa kwa kibali hicho tani milioni 1.5 ziliuzwa nje ya nchi na Kiasi cha tani milioni 1.5 zilizobaki zilihifadhiwa kama akiba ambapo tayari wameruhusu ziuzwe hapa nchini ili kupunguza kupanda kwa bei za vyakula nchini.

“Naomba wananchi msiwe na wasiwasi juu ya hali ya chakula nchini. Msisikilize kelele zinazopigwa na watu mbalimbali pamoja kwenye baadhi ya vyombo vya habari yakiwemo magazeti kwani taarifa hizo si za kweli. Chakula kipo cha kutosha licha ya mvua kusuasua katika baadhi ya maeneo nchini,” amesema.

Hata hivyo Waziri Mkuu amesema kuwa kwa sasa mvua zimeanza kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo amewaomba wananchi kuzitumia kwa kulima mazao ya muda mfupi yanayostahimili ukame.

Waziri Mkuu amesema kwamba endapo kutatokea uhaba wa chakula nchini, Serikali itatoa utaratibu wa namna ya upatikanaji wa chakula kwa wananchi wake.

Kuhusu kupanda wa bei ya vyakula katika baadhi ya masoko amesema inatokana na kuwepo kwa uhaba wa chakula katika nchi jirani.

Aidha, Waziri Mkuu amesema kwamba Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, itatoa taarifa kuhusiana na hali halisi ya chakula nchini kwa sasa na pia itatoa taarifa kuhusu hali ya mvua ili Watanzania waweze kupata ukweli wa hali ilivyo.

 IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Waziri Tizeba atoa tamko kuhusu hali ya chakula na uwepo wa njaa nchini.

$
0
0
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba amelazimika kutoa ufafanuzi kuhusu hali ya chakula nchini huku akisisitiza kuwa Tanzania ina chakula cha kutosha na haina njaa kabisa.

Dkt. Tizeba ametoa ufafanuzi huo leo wakati akiongea na waandishi wa habari, na kusema kuwa watu wanaoneza taarifa za kuwepo kwa njaa Tanzania wana lengo la kuingiza mahindi yao yasiyo na ubora ili wafanye biashara, jambo ambalo serikali imelikataa.

Akizungumzia uhalisia wa hali, amesema kilichotokea ni kupanda kwa bei ya mahindi, hali iliyosababishwa na uamuzi wa serikali kuuza nafaka hiyo katika mataifa jirani yaliyokuwa na uhitaji mkubwa, ingawa kiwango kilichouzwa kilikuwa ni sehemu ya mahindi ya ziada.

"Mwaka jana gunia la mahindi kwa bei ya wastani wa kitaifa ilikuwa 65,000 lakini sasa ni 85,000 na wala haijafikia mara mbili mara tatu kama inavyosemwa ingawa kuna maeneo kama rorya imefikia hadi 150,000 kutokana na wao kutegemea misimu miwili wakajikuta wanatumia akiba yao lakini hali ya hewa ikawa tofauti kwahiyo kuna wafanyabishara wakaamua kutumia hiyo fursa kupandisha bei zaidi" Amesema.

Ameendelea kusema ..... "Mavuno ya nafaka yalikuwa tani milioni 16 wakati mahitaji yakiwa tani milioni 13 kwahiyo ziada ilikuwa tani milioni 3, kwahiyo katika hiyo ziada milioni 1.5 ikasafirishwa nje, wenzetu walikuwa wananunua kwa gharama yoyote kwa kuwa walikuwa na shida, hiyo ndiyo maana bei ya nafaka imepanda sana hasa mahindi, kwa sasa bei imefika hadi mia 8 mia 9 na wauzaji ni walewale, kwahiyo hawezi kuuza ndani kwa bei ya chini lakini kupanda huko kulitarajiwa"

Amesema kupanda bei kwa mahindi kulitarajiwa na ni kwa kawaida na wala hakuwezi kumaanisha kuwa Tanzania kuna njaa wakati nafaka zote zinapatikana kila kona ya Tanzania

"Hakuna soko halina mahindi, hakuna soko halina mchele, hakuna soko halina maharage, masoko ya mijini yamejaa viazi..... nchi ina ziada tani milioni 3 kwanini mnataka tukanunue tena tani milioni 1 za nini?"

Kuhusu ukame, amesema ni kweli kuna hali ya upungufu wa mvua, na hiyo inafahamika maana ilishatabiriwa na kuwataka wananchi watunze akiba yao ya chakula na wasidanganyike kukiuza, kwa sababu hali ya hewa haitakuwa nzuri katika baadhi ya maeneo.

Amewasihi wananchi waache tamaduni ya kung'ang'ania chakula cha aina moja na kuwataka kutumia mchele na viazi kama wanaona mahindi yamepanda bei.. "Nafaka siyo mahindi tu, tunao mchele na mpunga wa kutosha, na viazi vipo kutoka Tunduma, watumie hivyo"

Waziri huyo amepiga marufuku mtu yoyote kutoa taarifa za njaa kwa kuwa serikali ndiyo inayojua hali ya chakula kupitia vyanzo vyake.

Nogesha Upendo Ya Vodacom Yaja Na Tsh Bilioni 32 Za M-pesa

$
0
0
Wakati wateja na wananchi mbalimbali wakiendelea kunufaika na promosheni ya Nogesha Upendo ya Vodacom katika kujishindia mamilioni ya fedha kila siku pindi wanunuapo vifurushi kwenye simu zao, sasa malipo ya faida ya kutumia M-Pesa ambayo yameanza wiki hii yanaufanya mwanzo wa mwaka mpya kuwa mzuri zaidi kwa mamilioni ya wateja na mawakala wa M-Pesa.

Awamu hii ya malipo ya faida ya utumiaji wa M-Pesa inafikia jumla ya Tsh Bilioni 32/- na itawawezesha watumiaji wa M-Pesa kuuanza mwaka vizuri ambapo kila mtumiaji atapata sehemu ya gawio kulingana na matumizi ya akaunti yake ya M-Pesa. Malipo haya yanafanyika kwa awamu na yatawanufaisha wateja na mawakala wa M-Pesa waliopo kila kona ya Tanzania. Ikiwa ni mwendelezo wa mtandao huo kuwarudishia faida ya gawio hilo kampuni hiyo  imekwishagawa zaidi ya Tsh Bilioni 39 katika awamu zilizopita. Hii inamaanisha kwamba awamu hii itakapokamilika, ni zaidi ya Tsh Bilioni 70 zitakuwa zimewekwa moja kwa moja kwenye mifuko ya wateja wetu.

“Ugawaji huu wa faida ya kutumia M-Pesa kwa wateja na mawakala wetu ni muendelezo wa dhana kuu ya promosheni yetu ya”Nogesha Upendo”. Kila mtumiaji wa M-Pesa atapata pesa ya ziada kwenye akaunti yake, ambayo atakuwa na uhuru wa kuitumia vyovyote anavyopenda kama kununua vifurushi, kulipia huduma na bidhaa au kuwatumia ndugu na jamaa zake. Mteja mwenye matumizi makubwa kwenye M-Pesa, anapata gawio kubwa “zaidi la faida” Alisema Ian Ferrao, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania.
Kuona kiasi cha gawio lako, tuma SMS yenye neno KIASI kwenda 15300. Utapokea SMS inayoonesha kiasi cha pesa kitakachotumwa kwenye akaunti yako. Vifurushi vya Cheka, Intaneti na YaKwakoTu vinaweza kununuliwa kwa kutumia gawio hili la faida. Kununua vifurushi kwa kutumia pesa uliyopokea, Piga *150*00# chagua NUNUA MUDA WA MAONGEZI/VIFURUSHI kisha chagua kifurushi unachohitaji.

Promosheni ya Nogesha Upendo ipo kwenye wiki ya 7 sasa ambapo zaidi ya wateja 200 washajishindia Tsh Milioni 1 pesa taslimu na 600 wengine wameshashinda Tsh 100,000/- za kila siku. Kuendelea kuongeza nafasi za kushinda zawadi za siku na wiki za hadi Tsh Milioni 1/- mteja anatakiwa kununua kifurushi chochote cha Vodacom ambapo ataingia kwenye droo moja kwa moja.

Waziri Nape Kawajibu Waliobeza Diamond Platnumz Kukabidhiwa Bendera Ya Taifa.......Ridhiwan Kikwete Hajataka Kukaa Kimya, Kamjibu Tena Nape

$
0
0
Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Tanzania Nape Nnauye sio kwamba hakuona maoni ya Watanzania kwenye mitandao ya kijamii baada ya yeye kumkabidhi bendera mwimbaji wa bongofleva Diamond Platnumz kwenda Gabon kwenye michuano ya Afrika.

Waziri Nape ameziona comments za Watanzania na yeye amewajibu baada ya Diamond kuhudhuria kwenda kutumbuiza kwenye mashindano hayo ya soka Afrika yanayofanyika Gabon ambapo Nape baada ya kuona imekua gumzo mitandaoni yeye kumpa Diamond bendera.

Kupitia Twitter  yake Waziri Nape alichukua picha ya Diamond akiwa na wengine wa Afrika walioziwakilisha nchi zao kwenye mashindano yao wakiwa na bendera na kuandika "Ulizeni tena kwanini nilimkabidhi bendera Diamond"
 
==>Kwa sababu mjadala umekua mrefu sana kupitia twitter,baada ya post ya Waziri Nape kwenye watu walioandika tena ni Mbunge Ridhiwani Kikwete ambaye ameandika: Nafikiri Waziri amepanik kutokana na mashambulizi lkn ukweli ni kuwa tunahitaji kushiriki afcon 2019

Rais Magufuli Afanya Uteuzi Wa Wabunge Wawili Na Balozi Mmoja.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 16 Januari, 2017 amefanya uteuzi wa Wabunge wawili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Balozi mmoja.

Wabunge walioteuliwa ni Alhaji Abdallah Majula Bulembo na Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi.

Wabunge wateule hawa wataapishwa kwa taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Abdallah Bulembo ndiye mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), na pia alikuwa ni mujumbe wa Bunge Maalum la Katiba, kabla ya majukumu ya kuendesha kampeni za urais mwaka 2015 zilizomuingiza Rais Magufuli madarakani.

Kwa upande wake Prof Kabudi, ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Sheria, lakini kilichong'arisha zaidi ni pale alipoteuliwa na Rais Kikwete kuwa mmoja kati ya wajumbe wa Tume ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya Katiba, iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Jaji Mst. Joseph Sinde Warioba.

Prof. Kabudi amekuwa mahiri katika mihadhara mbalimbali kitaifa, hasa wakati ule wa mchakato wa Katiba Mpya.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Benedicto Martin Mashiba kuwa Balozi.

Kituo cha kazi na tarehe ya kuapishwa kwa Balozi Mteule Benedicto Martin Mashiba itatangazwa

Breaking News: Lowassa Akamatwa na Jeshi la Polisi Geita

$
0
0
Waziri Mkuu mstaafu na aliyekuwa mgombea urais kwa CHADEMA Mh. Edward Lowassa na mbunge wa Geita (M) Viti maalum Upendo Peneza wamekamatwa  na jeshi la Polisi Geita mjini.

Taarifa zinaarifu kuwa  Lowassa amefika Geita leo akitokea Kagera  ambapo alipofika stendi ya zamani Geita wananchi walimsimamisha. Aliposhuka kwenye gari kuwasalimu wanageita, polisi wakamkamata na kumpeleka kituo cha Polisi Geita. 

Lowassa alikuwa anaenda kwenye kampeni za uchaguzi Kata ya Nkome

Lowassa Kaachiwa Huru....Mashuhuda Waeleza Jinsi Alivyokamatwa

$
0
0
Waziri mkuu Mstaafu na Mgombea wa Urais 2015 kupitia CHADEMA, Edward Lowassa leo alikamatwa na jeshi la Polisi  wakati akiwa anaenda kwenye kampeni za uchaguzi Kata ya Nkome na baadaye aliachiwa  huru ambapo taarifa za polisi zinadai kuwa walimzuia kwa sababu za kiusalama.

Kupitia kituo cha Television cha Azam wameripoti habari ya kukamtwa kwa Lowassa ambapo baadhi wa wananchi wameeleza ilivyokuwa.

"Tulikuwa kwenye msafara ya kumpokea Lowassa lakini tulipofika hapa stendi wananchi walitaka kuongea na Lowassa, kabla hata hajashuka kwenye gari askari walituvamia wakasema tuondoke moja kwa moja twende kituoni"- shuhuda

==>Sikiliza mkasa mzima hapo chini

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya January 17


Jipatie Dawa za Asili za Kupunguza Maziwa, Kutoa Michirizi, Kuondoa Chunusi, Kuongeza Maumbilie na Nguvu za Kiume

$
0
0
NATURAL BEAUTY COSMETICS ni kampuni inayoongoza kwa kutoa bidhaa original za asili zenye matokeo mazuri bila kemiko wala madhara yoyote pia tunatoa punguzo la bei la %10 kwa ajili ya Xmas and new year pata bidhaa kwetu uweze kufurahia matokeo mazuri kwa bidhaa original.

     Tunazo za:👇👇👇👇
1. Kutengeneza shepu hipsi na makalio kwa:- (a) Dawa ya kunywa au Botcho yakupaka @ 150,000/= (b)Vidonge maalum @ 150,000/=
 
2. Kupunguza au kuongeza maziwa @ 90,000
3. Kushepu miguu kuwa (Chupa ya bia) @ 100,000
( Kuludisha bikra (@) 100,000/=
 
4. Kuondoa mipasuko au michirizi @90,000/=
5.Kuwa softi na mweupe mwili mzima kwa mafuta @10,000/= vidonge maalum @150,000
 
6.Kuongeza unene wa mwili mzima @130,000/=
7.kupunguza tumbo na manyama uzembe kwa:-
(a)Dawa ya kunywa au kupaka @ 130,000/=
(b) Mkanda original wa MICRO COMPUTER @200,000/=
 
8.Kuondoa chunusi na madoa sugu (@) 100,000/=
9.Kuondoa mvi milele na zisiludi tena @ 120,000
 
10.Kuongeza maumbile kwa:- (a)Gel ya kupaka @120,000/= Mashine original ya HANDSOME UP @170,000/=
11.Kuondoa vinyweleo @90,000/=
 
12.kuotesha nywele kwenye kipara @120,000/=
13.Kuongeza nguvu za kiume na hamu ya tendo @100,000/=
14.Kuondoa makovu sehemu yoyote @90,000/=

     WASILIANA NASI KWA NAMBA :-
          065 9618585 au
             0759029968.
 
Popote ulipo utapata huduma zetu. BIDHAA  zetu zote ni GARANTII  na risiti unapewa ili kuhakikisha mafanikio yako
           Follow us 
   👇👇👇👇👇👇
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
      👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻

Kampeni zaingia dosari, mmoja achomwa mkuki Morogoro

$
0
0

Kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani zimeanza kuingia dosari baada ya mfuasi wa Chadema, Martha Maenda (33) mkazi wa Kichangani, Manispaa ya Morogoro kuchomwa mkuki mkono wa kulia tukio linalohusishwa na masuala ya kisiasa.

Maenda aliyelazwa wodi namba tatu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, alichomwa mkuki juzi saa 10:00 alfajiri, tukio linalohusishwa na uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kiwanja cha Ndege mkoani hapa.

Akizungumza akiwa hospitali, Maenda alisema akiwa pamoja na wenzake wakiandaa chai kwenye kambi ya Chadema iliyopo Mtaa wa Kimunyu, walivamiwa na watu wenye silaha za jadi ambao anadai ni wafuasi wa CCM. 

Hata hivyo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro, Fikiri Juma alikana chama hicho kuhusika akitaka Chadema waseme ukweli wa kilichotokea.

“Nikiwa na wenzangu tukiandaa chai, lilipita gari dogo lililosimama usawa wa nyumba tuliyoweka kambi; waliteremka wanaume wasiopungua wanne waliokuwa na mapanga, rungu, sime, fimbo, mkuki na kutuvamia,” alidai Maenda.

Alidai wenzake walikimbia, yeye alipojaribu alikamatwa na mmoja wa vijana hao aliyemchoma mkuki mkono wa kulia akiwa chini baada ya kuanguka.

Baadaye watu hao walitoweka kwa kutumia gari. Mganga msaidizi wa wodi aliyolazwa Maenda, Dk John Muneja alithibitisha kumpokea majeruhi huyo saa 11:00 alfajiri.
Msemaji wa Chadema wilayani Morogoro, Shaaban Dimoso alisema tukio hilo linalenga kudhoofisha kampeni za chama hicho na kwamba, siyo la kwanza kwani Januari 13, saa mbili usiku kuna mtu alivamia kambi hiyo akiwa na panga lakini alidhibitiwa na taarifa ilitolewa polisi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonce Ferdinand alithibitisha kupokea taarifa za mtu mmoja kujeruhiwa na mkuki na uchunguzi unaendelea. 

Wakati hayo yakitokea Morogoro, wananchi wa Kata ya Ngarenanyuki wilayani Arumeru mkoani Arusha, wamepinga kitendo cha baadhi ya wanasiasa kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la Naftari Ndekirwa, aliyekuwa diwani wa kata hiyo aliyefariki kwa ajali ya kuangukiwa na mti.

Mkazi wa Kijiji cha Olkung’wado, Anael Naftari alisema kitendo cha kwenda kumsalimia mjane na kuweka mashada ya maua baada ya msiba kumalizika muda mrefu linamzidishia uchungu.

Mkazi mwingine, Ndekirwa Urasa alisema hayo yanafanyika yakiwa ni mtaji wa kisiasa ili kupata kura. Katika uchaguzi huo, Chadema kimemsimamisha Aminiel Mungure kuwania udiwani, huku mgombea wa CCM ni Zacharia Nko.

Katika maeneo mengine ya kampeni, Mbunge wa Mufindi Kusini, Mendrad Kigola aliwataka wakazi wa Kata ya Igombavanu kumchagua diwani wa CCM ili kurahisisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Kigola alitoa kauli hiyo juzi akimnadi mgombea udiwani wa kata hiyo, Rashid Mkuvasa ambaye yeye alijinadi kwamba anao uzoefu na kazi hiyo kwa kuwa amekuwa diwani kwa kipindi cha miaka 10.

Silaha Mbalimbali zakamatwa pori la vikindu

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, limekamata silaha tano na risasi 12, katika pori la vikindu, zikiwa zimetelekezwa kufuatia operesheni maalumu ya siku saba.

Operesheni hiyo ililenga kukamata magari ya wizi, majambazi, wauzaji wa dawa za kulevya, wauza gongo na makosa ya usalama barabarani.

Mbali na hilo, operesheni hiyo imefanikiwa kukusanya sh. 215,090,000,kutokana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani kuanzia januari 13 mpaka 15, mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Simon Sirro.Amesema kuwa wamefanya operesheni hiyo katika pori la vikindu, Mkoani Pwani kufuatia ongezeko la matukio ya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Dar es salaam.

Aidha, Sirro amesema kuwa watuhumiwa 362, walikamatwa na makosa mbalimbali na kuongeza kuwa wamekamata silaha aina ya SMG moja, shortgun mbili na bastola mbili.

Hata hivyo, Sirro amesema kuwa katika operesheni hiyo imebainisha maeneo yaliyokithiri kwa matukio ya uhalifu ni Kigogo Freshi na Yombo Vituka.

Sababu Za Edward Lowassa Kukamatwa na Polisi Jana

$
0
0
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana alikamatwa na polisi mkoani Geita akituhumiwa kufanya mkutano bila kibali. 

Lowassa, ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alikuwa njiani akitokea mkoani Kagera, ikiwa ni mwendelezo wa ziara za viongozi wa chama hicho katika kanda zake kutekeleza Operesheni Kata Funua inayohusisha mikutano ya ndani. Hata hivyo, aliachiwa jana jioni. 

Akiwa ameongozana na viongozi na makada wa Chadema, Lowassa aliingia Geita saa 9:30 alasiri na kupokewa na umati wa wananchi waliojitokeza eneo la Nyankumbu, tayari kwa safari ya kwenda kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Nkome. 

Viongozi wengine waliokuwamo kwenye msafara huo ni Profesa Mwesiga Baregu, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Hamis Mgeja, ambaye ni kada wa chama hicho. 

Msafara huo uliokuwa wa magari matano, ukisindikizwa na pikipiki na wafuasi kadhaa wa chama hicho, ulipitia makutano ya barabara mjini Geita na kukutana na magari ya polisi yaliyosheheni askari wakiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Wilaya (OCD), Ally Kitumbo. 

Bila kuingilia msafara huo, magari ya polisi yaliufuatilia kwa nyuma ulipokuwa ukielekea Kata ya Nkome. 

Hali ya hewa ilichafuka baada ya msafara kufika eneo la Soko Kuu wakati wananchi walipouzuia wakitaka kumsalimia Lowassa, ambaye aligombea urais katika uchaguzi mkuu uliopita. 

Kiongozi huyo alilazimika kujitokeza juu ya gari lake kuwapungia na baada ya kelele za ‘njaa, njaa, njaa’ kusikika eneo hilo, Lowassa alitumia kipaza sauti kuwaomba wananchi wawe watulivu na wawaruhusu waendelee na safari yao kuwahi mkutano wa kampeni. 

“Ndugu zangu wana-Geita, natamani kuzungumza nanyi lakini sheria inanibana. Naomba muwe watulivu na mturuhusu tuendelee na msafara kuwahi mkutano wa kampeni Nkome,” alisema Lowassa. 

Askari hao wakiongozwa na OCD, walimfuata Lowassa na kumuamuru yeye na msafara wake kwenda Kituo Kikuu cha Polisi kwa mahojiano. Wakati wa kuelekea kituoni, gari lake lilitanguliwa mbele na la polisi na nyuma kulikuwa na jingine la jeshi hilo. 

Kitendo hicho kiliwafanya wananchi waliokuwa na hamu ya kumsikiliza kiongozi huyo kuongozana kwenda kituoni, jambo lililoibua taharuki na polisi kuwatawanya kwa kufyatua mabomu ya machozi.

Waandishi wapigwa
Pamoja na kuwatawanya wananchi kwa mabomu, askari hao pia waliwapiga kwa mikanda na fimbo waandishi wa habari waliokuwa wakifanya kazi yao eneo hilo. 

Hali ilivyokuwa kituoni 
Baada ya kuwasili kituoni huku polisi wakiendelea kuwazuia wananchi, Lowassa alisalia ndani ya gari lake hadi hali ilipotulia na kutakiwa kuingia kituoni. 

Ni magari mawili pekee; la Lowassa na la Profesa Baregu, yaliyoruhusiwa kuingia eneo la polisi huku viongozi wengine kama Singo Benson ambaye ni Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa Chadema, na Upendo Peneza (Mbunge wa Viti Maalumu), wakitakiwa kusubiri nje. 

Kitendo cha wananchi kuzidi kufurika kituoni hapo, kiliwafanya polisi kuimarisha ulinzi, wakizuia mtu yeyote kukatiza wala kusogelea eneo hilo. Licha ya kuzingira kituo cha polisi, askari walitanda barabara inayoelekea ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambako pia wananchi walizuiwa kukatiza. 

Lowassa apitishwa uani
Baada ya kuona wananchi wanazidi kujaa kituoni, polisi waliamua kumtoa Lowassa kupitia mlango wa nyuma na kumhamishia ofisini kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Mponjoli Mwabulambo.

 Kama ilivyokuwa Kituo cha Kikuu cha Polisi, ulinzi pia uliimarishwa eneo lote la ofisi ya RPC baada ya Lowassa kuhamishiwa huko na wananchi kupata taarifa. 

Kiongozi huyo aliyehamia Chadema akitokea CCM mwaka 2015 aliachiwa jana jioni. Kamanda Mwabulambo alisema hawakumkamata bali walizuia msafara huo kwa ajili ya usalama wake. 

Akizungumzia suala hilo, Peneza alisema huo ni muendelezo wa ukandamizaji dhidi ya viongozi wa Chadema unaofanywa na polisi mkoani Geita, akitoa mfano kitendo cha yeye kuhojiwa kwa saa kadhaa mwishoni mwa wiki iliyopita kwa madai ya uchochezi alipohutubia mkutano wa hadhara na kusema nchi inakabiliwa na njaa. 

Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Baada Ya Mkoa Huo Kushika Mkia Kwenye Matokeo ya Kidato Cha Pili

$
0
0
Siku moja  baada ya Mkoa wa Mtwara kutangazwa kushika mkia katika matokeo ya upimaji wa kitaifa wa wanafunzi wa kidato cha pili, Mkuu wa Mkoa huo, Halima Dendego amesema hayajatokea kwa bahati mbaya.

Mkuu huyo alisema licha ya kutofurahishwa na matokeo hayo, alitarajia hali ingekuwa hivyo kutokana na suala la elimu kutopewa kipaumbele mkoani Mtwara. 

Alisema tangu ateuliwe kuongoza mkoa huo, amegundua kuwa mambo mengi hayaendi sawa katika elimu, hali iliyomlazimu kujiwekea mikakati ya kujipanga upya. 

“Nimekuja Mtwara nimegundua mambo hayako sawa, nikajaribu kutafuta kiini, ndiyo nikabaini hakuna mwamko wa elimu, walimu siyo wabunifu. 

"Wanashindwa kuangalia mazingira yaliyopo na kufundisha kulingana nayo. Utoro pia umekithiri,” alisema. 

Aliitaja changamoto nyingine aliyoigundua kuwa ni udanganyifu kwenye mitihani hasa ya kuhitimu elimu ya msingi ambayo watoto wengi hufaulu kwenda sekondari.

 “Hao watoto waliofanya mtihani wa kidato cha pili mwaka jana walifaulu vizuri mtihani wa darasa la saba iweje leo washindwe, hapo ndipo utagundua kuna mazingira ya udanganyifu. 

“Watoto wengi wameingia sekondari kwa udanganyifu kwa hiyo matokeo haya tuliyajua, jambo hili nimedhamiria kulikomesha lengo langu ni kuuweka mkoa wetu katika hali nzuri,” alisema Dendego 

Alisema Januari 14, aliitisha mkutano wa wadau wa elimu; viongozi wa dini, wa halmashauri na mitaa kujadiliana namna ya kuinua kiwango cha elimu mkoani humo. 

“Tumeshapeana majukumu kila mtu katika eneo lake kuhamasisha kuhusu umuhimu wa elimu, hasa viongozi wa dini kwa waumini wao. 

“Walimu nao wanatakiwa  kufundisha kulingana na mazingira. Ubunifu ukiongezeka katika ufundishaji, taratibu tunaweza kubadilisha upepo. Naamini tukishirikiana suala hili litafanikiwa,” alisema. 

Ofisa Elimu wa mkoa huo, Fatuma Kilimia alisema amedhamiria kuimarisha usimamizi ili kumaliza tatizo la udanganyifu. 

“Tatizo hili linaonekana lilikuwapo. Hawa watoto walioanguka mtihani huu mwaka 2014 walishika nafasi ya nane kitaifa kwenye mtihani wa darasa la saba. Matokeo ni mabaya na hakuna namna ya kufanya zaidi ya kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji kwa walimu. Watoto hawawezi kufanya vizuri bila kufundishwa,” alisema. 

Katika orodha ya shule zenye matokeo mabaya ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2015, Mkoa wa Mtwara uliingiza shule 33. 

Shule hizo zilikuwa kwenye mstari mwekundu ikimaanisha kuwa wanafunzi wake walifanya vibaya kupita kiasi kwenye mtihani huo. 

Chingungwe, Naputa, Msimbati na Salama ni miongoni mwa shule za sekondari zilizokuwa kwenye mstari mwekundu katika matokeo ya kidato cha nne mwaka jana, Msimbati ikishika namba sita na Naputa namba 10. 

Akizungumzia matokeo hayo, Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiel Oluoch alisema mazingira magumu ya kazi mkoani Mtwara yamechangia kwa kiasi kikubwa matokeo hayo. 

Alisema shule nyingi zimekosa walimu kutokana na mazingira magumu na Serikali imeshindwa kulifanyia kazi suala hilo ili kupata ufumbuzi. 

“Tukubali kuwa Mtwara ni eneo lenye mazingira magumu ya kazi. Shule hazina walimu na kwa bahati mbaya Serikali imekataa kutekeleza pendekezo la CWT la kutoa posho kwa walimu walio katika mazingira magumu,” alisema. 

Oluoch alisema changamoto nyingine inayodumaza kiwango cha elimu Mtwara ni kukithiri kwa mila na desturi, hivyo kuwazuia watoto kupata haki ya elimu. 

“Wenzetu kule unyago umepewa kipaumbele. Mzazi yuko radhi amzuie mtoto kwenda shule akacheze, hapo ndipo tatizo linapotokea,” alisema Oluoch.

Kilichompata Mchungaji aliyetabiri kifo cha Rais Robert Mugabe

$
0
0
Mwishoni mwa mwaka 2016, raia na wafuasi wa vyama vya upinzani nchini Zimbabwe waliandamana kupinga utawala wa Rais Robert Mugabe ambaye amekuwa madarakani tangu 1980.

Habari zilizoripotiwa na vyombo vya habari vya kimataifa zimedai kuwa maafisa wa polisi nchini Zimbabwe wamemkamata  mhubiri aliyetabiri kwamba Rais Robert Mugabe atafariki mwezi Oktoba mwaka huu.

Pastor Patrick Mugadza alikamatwa akiwa mahakamani mjini Harare Jumatatu ambapo alikuwa ameenda kwa kesi nyingine dhidi yake. Wakili wake Gift Mtisi amewambia waandishi wa habari kuwa alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kuvalia bendera ya taifa

Wakili wake ameimbia AFP kuwa; "Alikuwa amefika mahakamani kwa kesi hiyo polisi walipomkamata wakati wa mapumziko na kumfungulia mashtaka kwa sababu ya unabii huo"

Awali alishtakiwa kwa kukosea heshima mamlaka ya Rais lakini shtaka hilo likabadilishwa baadaye na kuwa amewatusi watu wa asili fulani au dini fulani.

Pastor Mugadza wiki iliyopita aliandaa kikao na wanahabari ambapo alitabiri kwamba Mugabe atafariki Oktober 17 mwaka huu.

Mbeya: Maiti iliyozikwa yakutwa chumbani kwenye godoro.

$
0
0
Wakazi wa Isanga Jijini Mbeya wamekumbwa na taharuki baada ya tukio lisilo la kawaida ambapo maiti iliyokwenda kuzikwa katika makaburi ya zamani ya Isanga ilikutwa ikiwa kwenye godoro ndani ya nyumba alimofia.

Taarifa yaJeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya inasema kuwa tukio lilitokea mnamo tarehe 16.01.2017 majira ya saa 4:30 asubuhi katika mtaa wa Igoma “A”, Kata ya Isanga, Jijini Mbeya.

Kufuatia taarifa hiyo Polisi walifuatilia na kubaini kuwa tarehe 16.01.2017 majira ya saa 1:00 asubuhi mtu mmoja aitwaye JAILO KYANDO na mke wake aitwaye ANNA ELIEZA wote wakazi wa mtaa wa Igoma “A” waliamka asubuhi na kukuta mtoto wao wa kwanza aitwaye HARUN JAILO KYANDO amefariki dunia akiwa amelala.

Taarifa za awali zinadai kuwa marehemu tangu utoto wake alikuwa na matatizo ya ugonjwa wa kifafa hali iliyopelekea kuishi nyumbani pasipo kusoma.

Kufuatia kifo hicho msiba uliendeshwa na taratibu za mazishi zilifanyika. Majira ya saa 6:00 mchana jeneza lililetwa msibani na kuwekwa sebuleni kando ya mwili wa marehemu ambao ulikuwa umeviringishwa na blanketi na kulazwa chini kwenye godoro, baada ya maombi yaliyoongozwa na walokole waitwao BONDE LA BARAKA vijana walibeba jeneza hadi makaburi ya zamani ya Isanga na kisha jeneza kuzikwa.

Waombolezaji waliporudi nyumbani walitaharuki kuona mwili wa marehemu mtoto HARUN JAILO KYANDO ukiwa chumbani umelazwa eneo ulipokuwa awali. 

Kutokana na hali hiyo taarifa zilifikishwa Polisi mara moja, askari Polisi walifika na kurejesha hali ya amani kwa kuuchukua mwili wa marehemu ambao kwa sasa umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.

Taratibu nyingine za mazishi zitafanyika leo tarehe 17.01.2017. Mpaka sasa bado haijafahamika ni uzembe /bahati mbaya wafiwa kusahau kuweka mwili wa marehemu kwenye jeneza au kulikuwa na hujuma zozote.

Upelelezi unaendelea kuhusiana na tukio hili.

Serikali Yamalizana Na Wenyeviti Wa Serikali Za Mitaa.......Yawaruhusu Kutumia Mihuri Yao

$
0
0
Baada ya mvutano wa muda mrefu baina ya Serikali na Wenyeviti wa Serikali za mitaa,Serikali imesitisha muongozo wake wa kuzuia kutumia mihuri kwa wenyekiti wa serikali za mitaa.

Akizungumza leo hii Jijini Dar es salaam na wawakilishi kutoka serikali za mitaa, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba Chawene amesema amesitisha muongozo uliotolewa juu ya utumiaji wa mihuri kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa mpaka hapo baadae itakapojadiliwa tena.

''Hakukuwa na dhamira yeyote ya kupunguza mamlaka ya heshima yenu Wenyeviti, lakini kama mihuri inaweza kupunguza heshima yenu nimeona kufuta muongozo huu Mpaka pale tutakapo jadili tene upya swala hili" amesema

Sanjari na hayo Waziri Simbachawene amefafanua kuwa kulikuwa na sababu za msingi za kutoa muongozo huo wa kutokutumia mihuri kutokana na matumizi mabaya ya mihuri kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa na kupelekea kuigawa ardhi bila utaratibu maalumu.

Hata hivyo Katibu wa Wenyeviti Mkoa wa Dar es salaam Mariam Machicha ameishukuru Serikali kwa kuona tatizo hilo na kuahidi kulifanyioa kazi.

Timiza Malengo Na Ndoto Zako Kupitia ‘bonus Account’ Ya NMB

$
0
0
Unafahamu kwamba ni rahisi kufikia malengo yako ya kujiwekea akiba ukiwa na “NMB Bonus Account au Business Savings Account” ambayo inakupa faida hadi 13%*? Mfano, ukiwa na lengo la kujiwekea akiba ya shilingi 500,000 kwa mwaka 2017 inabidi uweke kiasi cha shilingi 42,000 tu kwa mwezi na ukiwa na nidhamu ya kuhakikisha kwamba kiwango hakipungui kiasi ulichojiwekea basi utakuwa umechagua njia sahihi kuelekea kutimiza ndoto zako. 

Jambo la msingi ni kuhakikisha unakuwa na akaunti ambayo haiingiliani na matumizi yako ya kila siku, hii ni hatua muhimu katika kutimiza malengo binafsi uliyojiwekea ama ya kibiashara. 

NMB inatambua umuhimu wa kujijengea nidhamu ya kuweka akiba na kuwaletea wateja wake bidhaa zitakazowasaidia kuweka akiba na pia kuhakikisha wanakuza na kupata maendeleo binafsi na ya kibiashara. 

‘Bonus Account’ na ‘Business Savings Account’ ni akaunti maalum kwa ajili ya wateja wanaotaka kutimiza malengo yao binafsi au ya kibiashara. 

Labda ungependa kuweka akiba kwa ajili ya kulipia ada ya mwanao mwakani, kununua nyumba miaka minne ijayo au kuanzisha biashara miaka siku za usoni, ukiwa na akaunti hizi utakuwa umepata njia sahihi ya kufikia malengo yako. 
 
Wasiliana na NMB leo kupitia namba 0800 002 002 utimize matarajio yako kupitia NMB Bonus Account na NMB Business Savings Account.


Makamu Wa Rais Akutana Na Ujumbe Kutoka Kingdom Leadership Networks

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameuhimiza uongozi wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania kuharakisha mchakato wa kuanzisha Chuo cha Joseph Business School hapa nchini chuo ambacho kitatoa mafunzo mbalimbali ya biashara, maadili ya uongozi na ugunduzi wa mawazo ya biashara ili kusaidia mamia ya Watanzania kuimarisha shughuli zao za kiuchumi.

Makamu wa Rais ametoa kauli ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam leo alipokutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa  Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania ambao walimtembelea Makamu wa Rais kumweleza hatua ambazo wamefikia katika uanzishaji wa Chuo hicho.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema wazo la uanzishaji wa Chuo hicho ulitolewa na Dkt Bill Winston ambaye ni Mwanzilishi wa Winston Ministries mwaka jana katika Maombezi ya Taifa ambaye yeye alikuwa mgeni rasmi katika maombi hayo, anasema aliupokea kwa furaha mpango huo kwa sababu chuo hicho kitasaidia watanzania wengi kupata elimu na ujuzi wa kuimarisha biashara zao wakati taifa likielekea kwenye uchumi wa Viwanda.

Amesema hatua za uanzishwaji wa Chuo hicho hapa nchini ni fursa pekee na nzuri kwa Watanzania kujifunza ubunifu na ugunduzi katika biashara, maadili ya uongozi katika biashara ili kuongeza ufanisi katika biashara zao kwa ajili ya manufaa yao na taifa kwa ujumla hasa katika ulipaji wa kodi.
 
Kwa Upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania Ibrahimu Kaduma na Meneja Mradi Dkt Charles Sokile wamemhakikishia Makamu wa Rais kuwa hatua ambazo wamefikia kwa sasa katika uanzishaji wa Chuo hicho ni nzuri ambapo mpaka sasa wamepata majengo kwa ajili ya ofisi na maeneo ya kufundishia na hatua za usajili wa chuo hicho zipo katika hatua za mwisho.

Wamesisitiza kuwa wanataka kushirikiana ipasavyo na Serikali katika uanzishaji wa chuo hicho ambacho kitatoa elimu ya biashara hasa ugunduzi wa mawazo ya biashara nchini kama hatua ya kutekeleza kwa vitendo dhana ya kuelekea kwenye uchumi wa viwanda nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania Ibrahimu Kaduma aliyemtembelea Makamu wa Rais na kumuelezea mikakati ya kuanzisha Chuo cha Joseph Business School kushoto ni Meneja Mradi Dkt Charles Sokile.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania uliomtembelea ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Kama Una Tatizo Hili Usifikirie Kabisa Kuhusu Kufunga Ndoa ! ......Vinginevyo Uwe Tayari Kwa Jambo Lifuatalo

$
0
0
Imesimuliwa na  Dokta. MUNGWA  KABILI….+255  744  000  473.

Mwaka 2003, mwanamke   mmoja ambae  kimuonekano  alionekana  msomi mwenye  kazi yake  nzuri,   alinifuata   kilingeni   kwangu  akiomba  nimsaidie  kuhusu   jambo  moja.

Alisema 

“  NIPO KWENYE  NDOA  KWA  MUDA  WA  MIAKA  MINANE. MIMI NA   MUME  WANGU TUMEBAHATIKA  KUPATA  WATOTO  WATATU.

 ILA  KUNA MKAKA  MMOJA, NAE  NI  MUME  WA  MTU, ANAISHI  MTAA  WA  TATU  TOKA  TUNAPOISHI.  NAMPENDA   SANA  HUYO  MKAKA, NAOMBA  UNISAIDIE MIMI  NA  HUYO  MKAKA  TUOANE!”

Akaendelea kueleza

 “   YEYE  NDO  ALINITONGOZA. MWANZONI  NILIKUWA  NAMKATALIA  LAKINI  BAADAE  NIKAMKUBALIA, ILA  TOKA NIONJE  PENZI  LAKE  NIMECHANGANYIKIWA  KABISA! NATAKA   AWE  WANGU  PEKE  YANGU !  NAJISIKIA   WIVU   SANA   NIKIMUONA  YUPO  NA  MKE  WAKE ! NATAKA   UNIFANYIE   DAWA, MWANAUME  HUYO  AACHANE  NA  MKE  WAKE! ANIOE   MIMI   NA  AWE  NA  MIMI  TU!

NATAKA   PIA   UNIFANYIE  DAWA  NIACHANE  NA  MUME  WANGU  KWA  AMANI!  YEYE  AWE  NA  MAISHA  YAKE  NA  MIMI  NIWE  NA  MAISHA  YANGU!

MUME  WANGU ANA  PESA  NYINGI  TU  NA  MAISHA  MAZURI, LAKINI MIMI  NIMETOKEA  TU  KUMPENDA  KWA  DHATI  HUYU MKAKA.

YEYE  PIA  ANA  KAZI  YAKE NZURI, ILA  SIMPENDI KWA AJILI  YA  KAZI  YAKE AU  MALI  ZAKE. NAMPENDA  YEYE  KAMA  YEYE NA  NIPO  TAYARI  KUFANYA  LOLOTE  KWA  AJILI  YAKE!

Kwa ufupi   mwanamke  huyu  alimpenda  jamaa  huyo  kwa  sababu  ya  uwezo  wake  kitandani.

Nilimuonea  huruma  sana  mume  wa  mwanamke  huyo  pamoja  na  watoto  wake, bila  kusahau  mke  wa  jamaa  anaependwa  pamoja na  watoto  wake.

Mwanamke huyu  alikuwa  tayari  kufanya  jambo  lolote kwa ajili  ya  mwanaume  mwingine, huku  sababu  ikiwa  moja  tu. TENDO  LA  NDOA!

Piga  picha  wewe  ungekuwa  ndio mume  wa  huyo  mwanamke, halafu ukajua  mke  wako  wa  ndoa, anakwenda  kwa  mganga  wa  jadi, kupewa  dawa  ya  kumpata  mwanaume  mwingine  ambae  pia  ni  mume  wa  mtu kwa  sababu tu  ya  udhaifu  wako  katika tendo  la  ndoa!   Bila   shaka  ungeumia  sana! Lakini  huo  ndio  ukweli wenyewe na  wanawake wengi  ndivyo  walivyo!

Kwa uzoefu  wangu  wa  miongo  kadhaa  katika  kazi  ya  utabibu, nimekutana  na  kesi  kama  hizi  nyingi  sana.

Kesi nyingine  ilikuwa  ya  mwanaume, kaja  kumfunga  mke  wake. Alimfumania  mke  wake akiwa  amepiga  magoti  mbele  ya  kijana  mdogo  wa  bodaboda  akimuomba  msamaha, mara  baada  ya  kijana  huyo  kutishia  kumuacha!  Ni  jambo  lenye  kuvunja  moyo  na  kutia  uchungu  sana.

NIRUDI   KWENYE  MADA  YANGU : KAMA  UNAJIJUA  AU  UNAJIHISI, UNA  TATIZO  LA  NGUVU  ZA  KIUME,BASI USIFIKIRIE  KABISA  KUHUSU  KUFUNGA  NDOA!  VINGINEVYO  UWE  TAYARI KWA  JAMBO  NITAKALO LIELEZA  HAPA CHINI…..

Kama  unajijua  una  tatizo  la  NGUVU  ZA  KIUME, basi usifikirie  kabisa  kuhusu  kufunga  ndoa.

 Kwa  sababu, kwanza  NDOA  NI  TENDO  LA  NDOA ! Sasa  kama  wewe  uwezo  wa  kufanya  tendo  la  ndoa  hauna, unafunga  ndoa  ya  kazi  gani ?

Mwanamke anapo ondoka  kwao, na  kuja  kuishi  na  wewe, anafuata  kwanza  tendo  la  NDOA. 

Hayo mambo  mengine  kama  pesa, nakadhalika  ni  mambo  ya  ziada  tu.

Uzoefu  wangu  umeniwezesha  kugundua  kuwa, mwanamke  anampompenda  mwanaume  kwa  sababu  ya  TENDO  LA  NDOA, basi  humpenda kikwelikweli  na  huwa  tayari  kufanya  jambo  lolote  kwa  ajili  ya  mwanaume  huyo… (  UZOEFU  WANGU UNAONYESHA  KUWA  NDOA  ZA  NAMNA  HII  HUWA  ZINADUMU  SANA )

Namaanisha  ndoa  ambazo  msingi  wake  ni UIMARA KATIKA TENDO LA NDOA  kwa  upande  wa  mwanaume.

Mwanamke MchaMungu  anapo pata  bahati  ya  kuolewa  na  mwanaume  aliye  IMARA  katika  tendo  la  NDOA, hushukuru  sana  Mungu  kwa  sababu, ana  kuwa  na  uhakika  kuwa hawezi  kumuudhi Muumba  wake, kwa  kuvunja  AMRI  YA SITA  YA MUUMBA!

Miaka  ya  2000  mwanzoni, kuna  Mjumbe  wa  mtaa  mmoja, uliopo  jijini  Dar  Es  Salaam, kila  alipokuwa  akienda  kusuluhisha  mgogoro  wa  ndoa, alikuwa  anapita  kwenye  maskani  ya  vijana  wa mtaani  na  kuwaambia  kwa  utani “  NAENDA  KUJUA  MWANAMKE  GANI  HAKAZWI  VIZURI  NA  MUME  WAKE  ILI NIMSAIDIE  MUME  HUYO “.

Kwa ufupi mwenyekiti  huyo  ali amini, migogoro  mingi  katika  ndoa, husababishwa  na UDHAIFU  KATIKA  TENDO  LA  NDOA kwa  upande  wa  wanaume.

Tendo la  ndoa  ni tendo lenye raha  sana  kwa  upande  wa  wanawake. Furaha  wanayo  ipata  wanawake wanapo fikia  katika  kilele  cha  tendo la  ndoa, HAIMITHILIKI.

Thamani  yake  ni  kubwa  mara  bilioni  kuliko  pesa  unazo muhonga  au mali  ulizo  nazo. Hivyo  kama  mwanamke  ana  uhakika  wa  kufurahia tendo  la  ndoa, basi  anaweza  kuishi  na  mwanaume  wa  aina  yoyote  ile, mahali  popote  kwa  hali  yoyote.

Kama unajijua  una  tatizo  la  NGUVU  ZA  KIUME, basi usifikirie  kabisa  kuhusu  kuoa.

VINGINEVYO  UWE  TAYARI  KUSAMEHE  DHAMBI  YA  UZINZI  na pia  uwe  tayari  kulea watoto  ambao  sio  damu  yako, na  kibaya  zaidi  uwe  tayari  kuletewa  magonjwa  ya zinaa, ikiwamo  ukimwi.

Kwa  sababu  kwa  vyovyote  vile  mke  wako  lazima  atatoka  tu nje  ya  ndoa !  Na    heshima   ya   ndoa   haitakuwepo.

Bora ubakie  kuwa  na  rafiki  wa  kike  tu, kwa  sababu  utakuwa  unakutana  nae  labda  kila  Jumamosi.

Lakini  sio kwa  mkeo. Mkeo  kila  siku  unalala  nae  kitanda  kimoja.  Na  tendo  la  ndoa  ni  haki  yake. Akikushtukia  uwezo  wako  mdogo, basi  atatafuta  tiba  mbadala, na  akiangukia  mikononi  mwa  kidume anae  ijua  kazi  yake  vizuri, basi inakuwa  bahati  mbaya  kwako.

SULUHISHO   LA   TATIZO:
Kama unasumbuliwa   na   tatizo   la   nguvu  za  kiume. Tumia   tiba  yetu ya asilia  iitwayo  KISHINDO. Tiba  hii asilia, imekuwa  ikitumika  tangu  enzi  za  mabibi na  mababu  wa  mababu.

Itakutibu  na  kukuponyesha  tatizo  lako  la  nguvu  za  kiume na  hivyo  kukupa uwezo  wa  kufurahia tendo  la  ndoa  pamoja  na  kumfurahisha  mkeo.

Pili : MPE  MKEO  TIBA  YA  KUPUNGUZA  HAMU  YA  TENDO  LA  NDOA:

Unaweza  ukawa  na  nguvu  nyingi  lakini  ukawa  na  maumbile  madogo sana ambayo  hayaendani  na  kasi  ya  mkeo. (  DAWA  ASILIA  IITWAYO  “ MKONO  WA  MTOTO” AMBAYO  HUONGEZA  UREFU  NA  UNENE  WA  UUME, IMEISHA . TIBA  HII  HUPATIKANA  KWA  UCHACHE  NA  KWA  MSIMU. HUPATIKANA MARA  MOJA  KWA  MWAKA, HUSUSANI MWEZI  WA KUMI  NA  MBILI  AU JANUARY.KWA  SASA  HAIPATIKANI  HADI  MWEZI DISEMBA )

Kwa hiyo  pamoja  na  kuwa  na nguvu  za  kiume  za  kutosha, bado  mkeo  anaweza  kutaka  kutoka  nje  ya  ndoa, kukutana  na  wanaume walio jaaliwa.

Suluhisho, mlishe  mkeo, dawa  maalumu  ya asili  ambayo  humfanya  mwanamke  kukosa  au  kuishiwa  kabisa  na  hamu  ya  tendo la  ndoa.

Tiba  hii  imekuwa  ikitumiwa  na mababu  zetu  tangu enzi na  enzi. Kwa mfano, mababu zetu  walio  jihusisha  na  uvuvi. Anaweza  kwenda n’gambo  au  kisiwa  cha  pili, na  akakaa  huko  hata  kwa  miezi  sita  na  akirudi  anakuta  mke  wake  hajaguswa  na  mtu  yoyote, kwa  sababu mke  anakuwa  hajisikii kufanya  tendo  la  ndoa.

Unaweza  hata  ukaenda  kusoma  ulaya  miaka  miwili  na  ukamkuta hajaguswa.  Kama  unaishi  nae, unaweza  kuwa  unakutana  nae  hata  mara moja  kwa  mwezi  au  kwa  wiki. 

Tiba  hii  itakupa  uhakika  kuhusu  uaminifu wa  mkeo  kwako. Kama  atatoka  nje, basi  labda  kwa  sababu  ya  fedha au nyinginezo  lakini si  kwa  sababu  ya  tendo  la  ndoa.

3. MFUNGE  MKE  WAKO ASITOKE  NJE : Kwa kutumia  tambiko maalumu  la  jadi, unaweza  kumfunga  mke  wako  na  kumfanya  asitoke  nje  ya ndoa,  hadi  siku  anaingia  kaburini.  Tambiko hili  litakuwa uhakika  na  usalama  wa  ndoa  yako.

IMESIMULIWA     NA DOKTA. MUNGWA   KABILI, ANAEPATIKANA   KWA  SIMU  NAMBA  + 255  744  000  473

Mwanamke Ajinyonga Kwa Mtandio Jijini Mwanza

$
0
0
Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Anastazia Francis miaka 48 amekutwa akiwa amejinyonga hadi kufa katika mtaa wa Nyasaka wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.

Taarifa ya jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza imesema kuwa mnamo tarehe 16.01.2016 majira ya saa 11:00 asubuhi, mwanamke huyo alikutwa akiwa amejinyonga hadi kufa ndani ya chumba chake kwa kutumia mtandio ambao alikuwa ameuning’iniza kwenye dirisha juu.

Inadaiwa kuwa mwanamke huyo baada ya mumewe kuondoka alimtuma mwanae mkubwa aliyemaliza kidato cha nne aende dukani na mwingine mdogo mwenye umri wa miaka 06 aende kufagia na ndipo alipopata mwanya wa kwenda kujinyonga hadi kufa.

Tukio hilo lilijulikana baada ya mtoto wake mdogo kurudi ndani chumbani kuchukua shati na kumkuta mama yake akiwa amejining’inizi ndipo aliita watu ili waje kumsaidia.

Taarifa hiyo ya jeshi la polisi imesema kuwa upelelezi unaendelea ili kufahamu chanzo cha tukio hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amewaasa wananchi pindi wanapopata matatizo waombe ushauri kwa watu wengine ili kuweza kuepusha maamuzi ambayo ni hatari katika maisha yao
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>