Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli ateua Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,  tarehe 17 Januari, 2017 amemteua Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania.

Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Juma anachukua nafasi ya Mhe. Jaji Mohamed Chande Othman ambaye amestaafu.

Kabla ya kuteuliwa kushika nafasi ya Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Juma alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania.

Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Juma atakaimu nafasi ya Jaji Mkuu wa Tanzania mpaka hapo Mhe. Rais Magufuli atakapofanya uteuzi wa Jaji Mkuu wa Tanzania.

Uteuzi wa Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Juma unaanza mara moja.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

17 Januari, 2017

Taarifa ya makusanyo ya kodi kwa nusu ya mwaka wa fedha 2016/17

$
0
0
Katika kipindi cha miezi sita ya mwaka wa Fedha 2016/17 yaani kuanzia Julai hadi Disemba 2016, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya kodi jumla ya shilingi trilioni 7.27 ikilinganishwa na shilingi trilioni 6.44 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho mwaka wa fedha  2015/16.
 
Ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2016/17 umeongezeka kwa asilimia 12.74.
 
Mlinganisho wa makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2015/16 na 2016/17 ni kama ifuatavyo:
MWEZIMWAKA 2015/16MWAKA 2016/17Ongezeko
JULAI925,384.71,069,458.515.57
AGOSTI923,316.91,154.222.525.01
SEPTEMBA1,132,310.31,378,048.921.70
OKTOBA1,037,179.81,131,094.99.05
NOVEMBA1,027, 939.61,123,509.79.30
DISEMBA1,403, 189.81,414,921.80.84
JUMLA6,449,321.17,271,256.2612.74

Jitihada mbalimbali zinafanywa ili kuhakikisha TRA inaongeza makusanyo kwa kuongeza ufanisi katika ukusanyaji, kuhimiza maadili mema kwa watumishi, kuboresha mifumo ya ukusanyaji, kushirikiana na vyombo vingine vya dola na wananchi katika kuziba mianya ya upotevu wa mapato pamoja na kufuatili, kuhimiza matumizi ya mashine za kielektronik na kuhimiza ulipaji wa kodi ya majengo.
 
TRA inaendelea kuhimiza wafanyabiashara wote waliosajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kuwasilisha ritani za VAT kabla ya tarehe 20 ya kila mwezi kama ilivyobadilishwa katika Sheria ya Fedha ya 2016.
 
Pamoja na hayo tunawakumbusha na kuwahimiza wananchi wa Dar es Salaam ambao hawajafanya uhakiki wa taarifa za Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kuhakiki taarifa zao kabla ya tarehe 31 Januari 2017 ili zoezi hilo liweze kuanzishwa katika mikoa mingine.
 
TRA inatoa wito kwa wafanyabiashara kulipa kodi stahiki kwa hiari na wakati ili serikali ipate mapato yake ambayo yataiwezesha kuwahudumia wananchi wake kikamilifu.
 
Kwa wafanyabiashara wenye madeni ya nyuma wanashauriwa kujitokeza kuonana na Mameneja wa Mikoa na Wilaya kujadiliana jinsi watakavyolipa madeni yao bila kuathiri biashara zao.
 
Wamiliki wa majengo wanaaswa kutoa ushirikiano kwa kulipia ankara zao za kodi ya majengo kwa hiari .

Pamoja Tunajenga Taifa Letu’
Richard M. Kayombo
MKURUGENZI WA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI

Picha 4: Nabii awanywesha waumini kemikali ya kusafishia injini ili kuondoa Mapepo

$
0
0
Mtu mmoja anayejiita Nabii nchini Afrika Kusini amezua taharuki baada ya picha kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha akiwanywesha waumini wake kemikali ya kusafishia injini na kusema kuwa ina ladha kama asali.

Nabii Theo Bongani Maseko wa kanisa la Breath of Christ Ministries lililopo mjini Johannesburg amesema kuwa kemikali hiyo inashambulia virusi ndani ya mwili wa binadamu na kutambua mapepo.

Maseko alisema kuwa unywaji wa kemikali hiyo hauna madhara yoyote kiafya kwani yeye mwenyewe amewahi kunywa.

“Ina ladha kama asali, nimewahi kunywa mara mbili” alisema Maseko.

Aidha, alisema kuwa waumini wake wote ambao tayari wameshatumia dawa hiyo hakuna hata mmoja aliyepata matatizo ya kiafya na kwamba wote wamekuja na ushuhuda wa kuponywa matatizo yao. Alisema kuwa Mungu alimpa wito huo kabla hata hajazaliwa.

Nabii huyu si yeye pekee aliyefanya vitu vya kushangaza kwani kuna mwingine alikuwa akiwapulizia waumini dawa ya kuuwa wadudu na mwingine akiwanywesha petroli.

Vijana wawili wafariki dunia wakati wakipiga ‘selfie’

$
0
0
Vijana wawili wamefariki walipokuwa wanajipiga picha katika barabara ya reli katika mji mkuu wa India Delhi.

Kundi la vijana lilikwenda katika kituo cha reli kupiga selfie mbele ya treni zilizokuwa zinawadia.

Lakini wawili walichelewa kuondoka katika reli hiyo na treni ikawakanyaga, polisi imesema.

Utafiti mwaka uliopita umeonyesha kuwa kumeshuhudiwa vifo vingi vinavyohusisha watu kupiga Selfi India kuliko nchi nyingine yoyote.

Wasomi kutoka chuo kikuu cha Carnegie Mellon na taasisi ya mawasiliano ya Indraprastha mjini Delhi wanasema kuwa kati ya vifo 127 vinavyotokana na watu kupiga Selfie kati ya mwaka 2014 – 2015, visa 76 vimeripotiwa India.

Tukio la hivi karibuni limejulikana baada ya vyombo vya habari katika eneo hilo kutoa taarifa Jumanne.

“Wakati wa kupiga picha, waliiona treni ikija wakasongea kando. Lakini treni nyingine ilitokezea upande wa pili na walikwama katikati. Waligongwa na mojawapo ya treni hizo,” Indian Express ilimnukuu afisa wa polisi.

Afisa mmoja wa polisi wa reli ameongeza kuwa vijana hao walimkodisha mpigaji picha mtaalamu kwa kazi hiyo.

“Tumeipata kamera kutoka kwa vijana iliotumika. Mlikuwa na picha na video, Video inakaguliwa, wakati picha hizo zinathibitisha kuwa walikuwa wanaruka kutoka reli moja hadi nyengine,” Naibu kamishna wa polisi Parwaiz Ahmed ameiambia Hindustan Times.

Mwaka jana wanafunzi wawili walizama walipokuwa wanapiga selfi katika mto uliofurika katika eneo la jimbo la kaskazini la Uttar Pradesh.

Na polisi mjini Mumbai imetaja maeneo 15 ambapo ‘ni hatari’ kupiga Selfie baada ya msichana wa miaka 18 kuzama baharini wakati akijipiga selfie.

Waziri Mkuu Majaliwa Afungua Duka La Dawa La MSD Katika Hospitali Ya Mpanda

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefungua duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda lililogharimu sh. milioni 55 litakalohudumia mikoa mitatu ya Kigoma, Katavi na Tabora.

Pia duka hilo itatoa huduma kwa vituo vya kutolea huduma za afya 580 ikiwa ni pamoja na hospitali za rufaa za mikoa miwili ya Kigoma na Tabora, Hospitali za wilaya sita za Nzega, Igunga, Urambo, Kobondo, Kasulu na Mpanda Mji.

Waziri Mkuu amefungua duka hilo la dawa la MSD, lililoko  katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi jana (Jumanne, Januari 17, 2017) ikiwa ni utekelezaji wa agizo alilolitoa kwa MSD Agosti 20, 2016 alipokuwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Katavi. Aliuagiuza  uongozi MSD kujenga duka hilo ili kurahisisha upatikanaji wa dawa katika mkoa huo pamoja na mikoa jirani.

Aidha, Waziri Mkuu amesema baada ya kufunguliwa kwa duka hilo Serikali haitarajii kusikia tena katika vituo vya afya na Zahanati zilizoko mkoani Katavi na mikoa jirani  zinakosa dawa. Amewaagiza Wakurugenzi kusimamia suala hilo na kuhakikisha vituo vyote vya afya vinakuwa na dawa za kutosha.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kukutana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili kutafuta namna bora ya kutumia fedha za huduma za afya zinazipatikana katika halmashauri nchini.
 
Aidha, Waziri Mkuu amesema Serikali imetoa sh. bilioni 1.5 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali ya mkoa wa Katavi ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda.

Amesema lengo la Serikali ni kuwa na Hospitali ya Rufaa kwa kila mkoa, hivyo, Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa mipya itakayojengwa Hospitali ya Mkoa ili kusogeza huduma za afya karibu na wananchi
 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bw. Laurean Bwanakunu alisema ujenzi waduka hilo la Mpanda hadi kukamilika umegharimu sh. milioni 55, huku benki ya CRDB ikitoa sh. milioni 50 na MSD imeweka dawa na vifaa tiba vya sh. milioni 104.45 na vifaa vya TEHAMA vya sh. milioni tano.

Alisema kuanzishwa kwa duka hilo kutaongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa hasa dawa ambazo hazimo katika orodha zilizoidhinishwa na Serikali kutumika katika vituo vyake vya kutolea huduma za afya ila zimeidhinishwa kutumika nchini na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Alisema dawa na vifaa tiba vilivyomo katika orodha ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) zinapatikana katika duka hilo kwa bei nafuu, hivyo kuondoa usumbufu kwa wagonjwa kwenda kuzitafuta katika maduka ya mbali na kwa bei ghali.

“Nitoe mfano mdogo wa tofauti ya dawa katika ya maduka ya MSD na maduka ya mitaani, hapa dawa ya sindano ya kutibu fungus aina ya Fluconazole inauzwa sh. 2,300 na mitaani sh. 4,500 na dawa ya sindano kwa ajili ya kushusha kisukari (Insulin) chupa moja MSD ni sh. 8,500 na mitaani sh. 20,000,” alisema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Agizo la waziri mkuu baada ya Mtwara kufanya vibaya Matokeo Kidato Cha Pili

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa Wazara wa Elimu Sayansi na Telnolojia pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenda mkoani Mtwara kufanya uchunguzi ili kubaini sababu zilizosababisha shule tisa za mwisho katika matokeo ya kidato cha pili kutoka mkoani humo.
                                                                      
Pia ameziagiza halmashauri nchini kushirikiana na Idara ya Ukaguzi ili kuhakikisha wanawasimamia vizuri walimu jambo litakalowezesha kuboresha ufundishaji na hatimaye kupata matokeo mazuri.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana (Jumanne, Januari 17, 2017) wakati akizungumza na watumishi na wananchi wa mkoa wa Katavi alipowasili Ikulu ndogo ya Mpanda kwa ajili ya kufungua duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda.

Kwa mujibu wa matokeo hayo kati ya shule 10 za sekondari zilizofanya vibaya kwenye mtihani huo, tisa zinatoka katika Mkoa wa Mtwara na moja Tanga. Shule za Mtwara zilizofanya vibaya ni Chingungwe, Malocho, Naputa, Chanikanguo, Mtiniko, Michiga, Msimbati, Salama na Lukodoka  huku ya Tanga ikiwa ni Nywelo.

“Viongozi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) waende Mtwara wakafuatilie kwa kina wajue kuna nini hadi shule tisa kati ya 10 zilizofanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kidato cha pili mwaka jana zitoke huko,” alisisitiza.

Mbali na kuuagiza huongozi wa wizara hizo kwenda mkoani Mtwara pia Waziri Mkuu amewataka wasimamie vizuri mikoa ambayo awali ilikuwa na matokeo mabaya na sasa inafanya vizuri na wahakikishe shule za mikoa hiyo hazishuki na badala yake ziendelee kupata matokeo mazuri zaidi.

Awali, akisoma taarifa ya mkoa huo, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Muhuga alisema katika matokeo ya mtihani kidato cha pili ya mwaka jana mkoa wake ulishika nafasi ya pili kitaifa ukiongozwa na mkoa wa Geita.

Alisema kwa sasa wanajipanga kuhakikisha katika mitihani ya mwaka huu wanashika nafasi ya kwanza kitaifa, hivyo alitoa wito kwa watendaji wa Idara ya Elimu, wakuu wa shule, wazazi na walezi kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha malengo hayo yanafanikiwa.

Sakata la Baa la Njaa: Zitto Kabwe Atishia Kujiuzulu Ubunge Serikali Ikiwa na Tani Milioni 1.5 za Mahindi

$
0
0
Baada ya kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kupaza sauti kuhusu hali ya chakula nchini huku akisema kuwa serikali haina chakula cha kutosha, viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Rais, Waziri Mkuu na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wameibuka na kusema kuwa si kweli kwamba nchi imekumbwa na njaa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi na Waziri wa Kilimo, Dkt Charles Tizeba ni kuwa serikali ina akiba ya chakula cha kutosheleza. Pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza juzi  mjini Dodoma aligiza Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula kusambaza chakula nchini ili kudhibiti kupanda kwa bei ya vyakula maeneo mbalimbali.

Jana kupitia ukurasa wake wa Facebook, Mbunge Zitto Kabwe aliandika maneno haya;

"Serikali ya CCM ikinionyesha tani 1.5m za chakula kutoka Hifadhi ya Taifa ya Chakula ambazo inataka kusambaza najiuzulu Ubunge mara moja.
 
Narudia, mpaka Oktoba 2016 kulikuwa na nafaka tani 90,400 tu Hivi kwenye maghala yote ya NFRA.

Tunashukuru kuwa Hivi sasa ajenda ya tishio la njaa inapata majawabu na matamko. Ndio wajibu wa vyama vya siasa. Kuibua masuala muhimu kwa nchi yetu.

Nimesikia Mwenezi wa CCM ameongea na waandishi Leo. Natarajia ndugu Ado Shaibu atamkaribisha mwenzake ulingoni"- Zitto Kabwe

CCM Yamvaa LOWASSA Sakata la Uhaba wa Chakula Nchini

$
0
0
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuna mwanasiasa mmoja ambaye hana nyenzo yoyote za kupata taarifa za uhakika ambaye amekuwa akiwaeleza na kuwaaminisha wananchi kuwa kuna tatizo la njaa ili kuzua taharuki. 

Polepole alisema baadhi ya wanasiasa wanaotangaza baa la njaa wana lengo la kuichonganisha Serikali na wananchi. 

Pamoja na kutomtaja jina, hivi karibuni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiwa katika kampeni za udiwani mjini Bukoba alikaririwa akisema, “Serikali imesema haitoi chakula, mimi nimejadiliana na chama changu tumeona tufanye mpango wa kuwatafutia chakula Watanzania. Hata kama ni kutoka nje ya nchi ninaamini dunia itatusikia.” 

Jana, akizungumza na waandishi wa habari juu ya mwenendo wa Serikali ya CCM katika kipindi cha mwaka mmoja, Polepole aliwataka wananchi kuwapuuza wanasiasa wanaoleta maneno yasiyo sahihi na yaliyojaa upotoshaji kwa Serikali. 

“Sipendi kujadili watu hapa, lakini sielewi huyu malengo yake ni nini? Tunacho chakula na imani ya CCM ni kujitegemea, ndiyo mwelekeo wa chama hiki,” alisema.

 Alieleza kuwa duniani kote kuna utaratibu unaofahamika bayana na kuwa baa la njaa siyo kitu kidogo, ni jambo kubwa na nchi inapokumbwa, mkuu wa nchi ndiye mwenye dhamana ya mwisho kutangaza. 

Polepole alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha Watanzania wanajitegemea na siyo kuwa ombaomba..., “Lakini anatokea kiongozi mmoja anawaahidi kuwa ataenda kuwaombea chakula cha bure. 

"Imeandikwa asiyefanya kazi na asile. Watanzania hawa wametutuma tuwawekee mazingira mazuri ili wafanye kilimo na biashara.

“Kiongozi anayesema nitaleta chakula cha bure na watu wasifanye kazi ni bahati mbaya sana. Imani yetu ni kubwa, Watanzania hawa wanaona mambo haya.” 

Aliwataka Watanzania kuwapuuza viongozi wa aina hiyo aliosema wanafahamu utaratibu lakini wameamua kuleta upotoshaji wa kutoa taarifa zisizo sahihi. 

Polepole aliishukuru Serikali kwa kufafanua vyema sakata hilo akisema kuna tani milioni 1.5 za chakula zitakazosambazwa sehemu mbalimbali zilizokumbukwa na ukame. 

 Alisema Awamu ya Tano, itaendelea kuishi katika misingi yake kwa kusema ukweli daima na fitina kwake mwiko. 

“Nilitarajia viongozi wote bila kujali itikadi, tungeendelea kuhamasisha wananchi kutunza nafaka na kufanya kazi kwa bidii. Hili siyo jukumu la Serikali,” alisema. 

Pia aliwataka wanasiasa wa upinzani kuacha kutumia matatizo yanayowapata wananchi kama mtaji wa kisiasa ikiwamo tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

Mbali na hilo la njaa, Polepole alizungumzia mwaka mmoja wa Rais John Magufuli na kusema amefanikiwa kutatua kero mbalimbali zilizokuwa zikilalamikiwa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2015. 

Alisema miongoni mwa kero hizo ni kuimarisha ukusanyaji wa mapato, kutimiza imani ya CCM inayosema binadamu wote ni sawa hasa katika huduma za kijamii kwenye elimu kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne. 

Alisema katika mwaka wa masomo unaoendelea sasa, vijana na watoto 20,000 wanakwenda kusoma elimu ya juu na watapata uwezeshaji wa Serikali wa kuendelea na masomo yao. 

“Huu ni mwaka wa kwanza, ambao kidesturi ni wa kujipanga lakini Serikali ya Rais Magufuli imeamua kutekeleza maendeleo kwa Watanzania huku ikiendelea kujipanga na kunyoosha nchi,” alisema Polepole.


Polisi FEKI Watatu Wakamatwa Kilimanjaro

$
0
0
Polisi mkoani Kilimanjaro kwa kushirikiana na raia wema imewatia mbaroni watu watatu wanaodaiwa kujifanya ni askari wa jeshi hilo na kuwaibia wananchi fedha na mali. 

Habari zilizopatikana jana zilisema kuwa katika upekuzi uliofanywa kwenye moja ya nyumba anayoishi mmoja wa watuhumiwa hao, kulikutwa kitambulisho cha mwalimu aliyewahi kuibiwa mamilioni ya fedha akitokea benki. 

Kwa mujibu wa habari hizo, kundi la watu hao limekuwa likiendesha vitendo vyake katika maeneo ya kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi na mitaa mbalimbali, hususan karibu na duka la Nakumatt. 

Vyanzo mbalimbali vimedokeza watuhumiwa hao huwakamata watu na kuwapekua kisha kuwatuhumu kuwa fedha walizonazo au simu vimeibwa sehemu na wao ni washukiwa wanaotafutwa. 

Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa jana alithibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao juzi saa nane mchana katika eneo la Njoro Relini

Godbless Lema na Mkewe Kizimbani tena Leo

$
0
0
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, Augustino Rwezile, leo, anatarajia kuwasomea hoja za awali Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na mkewe, Neema katika kesi inayowakabili ya kumtukana Mkuu wa mkoa huo, Mrisho Gambo. 

Hoja hizo ilikuwa wasomewe Novemba 15, 2016 lakini zilikwama kusomwa kutokana na Lema kuugua ghafla na Wakili wa Serikali, Elizabeth Swai kumuomba hakimu kutumia busara ya Mahakama kuisogeza mbele kesi hiyo kutokana na hali ya mbunge huyo. 

Lema bado anasota rumande kwa siku 76 tangu Novemba 2, mwaka jana baada ya kukosa dhamana katika kesi inayomkabili ya tuhuma za kutumia lugha ya uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli. 

Kutokana na sababu hiyo, Hakimu Rwezile pia aliahirisha kesi ya kuhamasisha maandamano ya Ukuta inayomkabili mbunge huyo na ile ya kumtumia ujumbe mfupi wa maneno Gambo unaodaiwa kuwa na matusi hadi leo. 

Katika kesi ya kuhamasisha maandamano inayomkabili Lema peke yake, shahidi ambaye ni Mkuu wa Makosa ya Jinai Mkoa (RCO) wa Arusha, George Katabazi ataanza kutoa ushahidi wake ambao ilikuwa atoe Novemba 15.

Awali, upande wa Jamhuri ulidai utakuwa na mashahidi watano katika kesi ya kuhamaisha maandamano na upelelezi umekamilika. 

Mashahidi wengine ni ASP Damas Masawe ambaye ni (OCCID), Inspekta Adam Nyamiti, WP 6826 DC Esta Yohana na Ezekiel Denis Kwayu kutoka kitengo cha Upelelezi Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam. 

Kwa upande wa kesi ya Lema na mkewe ya kumtumia ujumbe wa matusi Gambo, itaanza kusomwa maelezo ya awali ambayo nayo itakuwa tayari kwa kuanza kusikiliza baada ya upelelezi kukamilika.

AUDIO: Mbowe Alaani Kitendo cha Polisi Kumshikilia LOWASSA Kwa Masaa Matatu

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amelaani kitendo cha polisi wa Mkoa wa Geita kumshikilia kwa zaidi ya saa tatu Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alipokuwa njiani kwenda kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo Kata ya Nkome wilayani Geita juzi.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi limesema halikumkamata mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Chadema, badala yake lilimwita kituoni kwa ajili ya kuhakikisha usalama wake na wa wananchi waliokuwa wamemzunguka.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza jana, Mbowe alisema huo ni mwendelezo wa ghiliba, hila na unyanyasaji unaofanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya viongozi wa vyama vya upinzani kwa lengo la kuinufaisha CCM.

Akifungua kikao cha dharura cha Kamati Kuu ya Chadema, Mbowe alipinga maelezo ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Mponjoli  Mwabulambo kuwa walimshikilia Lowassa kwa usalama wake, akihoji sababu za kuchukua maelezo yake.

“Tumesikia maelezo yaliyotolewa na kamanda wa Polisi kuwa Lowassa alishikiliwa kwa usalama wake. Unayemlinda usalama wake unamwandikisha maelezo?” alihoji Mbowe.

 Alisema lengo la polisi, lilikuwa ni kuhakikisha kuwa Lowassa hafiki na kuhutubia mkutano wa kampeni.

Akizungumzia kuzuiwa kwa shughuli za kisiasa nchini, kiongozi huyo alilitaka jeshi la polisi kuacha umma uonyeshe mapenzi yao kwa viongozi wanaowapenda.

“Nchi hii inastahili kuongozwa katika misingi ya sheria badala ya chuki, ghiliba na ukandamizaji kama tunavyoshuhudia hivi sasa,” alisema.

Alisema ukimya na upole wa vyama vya siasa kunyamazia ukandamizwaji, usichukuliwe kuwa ni udhaifu bali ni busara inayolenga kuepusha jamii na mgawanyiko kiitikadi.

Lowassa aliyegombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa tiketi ya Chadema baada ya kujiengua kutoka CCM, alishikiliwa mjini Geita kuanzia saa 9:30 alasiri hadi saa 12:52 jioni baada ya kusimama na kuwasalimia wananchi waliojitokeza alipokuwa eneo la soko kuu. 

==> Msikilize Hapo Chini Akizungumza

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya January 18

SORRY MADAM -Sehemu ya 19 & 20 (Destination of my enemies)

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
 Eddy akajikuta akitetemeka kwa hasira na uchungu mwingi. Machozi yakazifi kumwagika, huku akiwa ameyang’ata meno yake kwa hasira kali. Taratibu damu za pua zikaanza kumwagika, kizunguzungu kikali kikamkata, akayumba mara ya kwanza ya pili walinzi wake wakamdaka asianguka chini.

Tukio hilo likamuogopesha sana Shamsa, aliye simama nyuma yake, kwa mara nyingine nguvu zikamuishia Shamsa na kujikuta akikaa chini mwenyewe bila hata kupenda. Roho ya Rahab, ikazidi kumuuma kwani uwezo wa kutenda msaada kwa familia ya Eddy, anao ila akifanya msaada wa kuwafufua, watu wote watamkimbia, na kuamini kwamba yeye si mwanadamu na itakuwa ni miongoni mwa kasfa chafu kwa raisi Praygod, kwamba ameoa jinni.
  
ENDELEA
Madaktari waliopo katika eneo hilo wakaanza kumpatia Eddy huduma ya kwanza pamoja na Shamsa, ikawalazimu kuweza kusimamisha hudmua za mazishi kwa muda, kusubiria wahusika wakuu kkukaa katika hali nzuri. Baada ya lisaa, Eddy na Shamsa wakarejea katika viwanja vya hapo kwenye jumba lake kuendelea na mazishi ya familia yake. Rahab hakuwa na jinsi zaidi ya kuacha mazishi hayo kuweza kufanyika, huku moyoni mwake akizidi kuumia, akimuhurumia kijana mdogo Junio, kwani umri unampasa sana kuweza kuendelea kuishi katika dunia hii.

Viongozi wakubwa wakaanza kuondoka katika jumba la Eddy, kila mmoja akiamini kwamba kazi ya Mungu haina makosa na wengine wakiingiwa na hofu pamoja na mashaka makubwa ya kutaka kujua ni lini Mzee Godwin anaweza kukamatwa mikononi mwao.

“Eddy jikaze kaka yangu, tutazidi kuwa pamoja”
Rahab alizungumza maneno ya kumfariji Eddy huku akiwa amemkumbatia
“Sawa dada Rahab”
“Ina bidi upae mapumziko ya kwenda mbali na hapa, ili akili yako ikatulie”
“Hapana Rahab, hapa ni nyumbani kwamngu na ndipo walipo lala wapenzi wangu, siwezi kwenda popote nitakaa hapa hapa”
“Hapana Eddy, inabidi ukatafute sehemu ya kwenda kutuliza akili wewe pamoja na Shamsa, tambua ya kwamba unavyo endelea kukaa na kutazama hayo makaburi huo weza kusahau kamwe”

“Ni kweli siwezi kusahau, ila……”
Eddy akastukia akipigwa busu zito la mdomo na Rahab, jambo lililo mstua sana.
“Madam samahani unafanya nini?”
Eddy alizungumza huku akijitoa mikononi mwa Rahab
“Unaogopa nini Eddy, tambua hapa tupo chumbani peke yetu”
“Namuheshimu muheshimiwa”
“Hayupo”
Rahab alizungumza huku akianza kuvua kitenge alicho jifunga kiunoni mwake na kubakiwa na skintait, pamoja na tisheti nyeusi alivyo vaa, iliyo bandikwa picha ya Junio, Phidaya pamoja na mama Eddy.
                                                                                                ***
Mapigo ya moyo ya Mzee Godwin yakaanza kumuenda mbio, akajaribu kumtingisha Manka aweze kuamka, ila Manka hakuweza kujibu kitu chochote zaidi ya kuendelea kukaa kimya. Mzee Godwin gafla akasikia minong’ono ya watu nyuma yake, akageuka na kukuta vijana wawili wakiwa wamesimama huku wakichukua tukio la kuwaka moto la gari hiyo ndogo.
Walipo muona mzee Godwin wakastuka, kwani nao ni miongoni mwa watu walio weza kuiona picha yam zee Godwin kwenye mitandano ya kijamii akitafutwa kama Rubin na jeshi la polisi la Tanzania.
“Huyu si ndio yule gaidi”

Mmoja aliropoka huku akiigeuzia simu yake upande aliopo mzee Godwin ili kumchukua video. Kama mbogo aliye uliwa mwanaye, mzee Godwin akanyanyuka kwa kasi ya ajabu na kuwarukia vijana hao masharo baro. Akaanza kuwatandika ngumi za kutosha huku akiwatukana matusi ya uchungu sana. Vijana hao walilia kama watoto wadogo, wakajutia ni kwanini walisimamisha gari na kuja kushuhudia ajali hiyo. Mzee Godwin akachomoa mkanda wa suruali yake na kuandelea kuwachapa vijana hao kwa hasira kali, hadi wakapoteza fahamu.
Mzee Godwin akamgeukia Manka, kwa bahati nzuri akamkuta akitingisha tingisha mkono mmoja, kwa haraka akamuweka begani na kuanza kukimbia naye kuelekea alipo simamisha gari la polisi, akamuingiza Manka ndani na kuondoka naye katika eneo hilo,

Kila alipo mtazama binti yake huyo, waliye potezana naye miaka mingi ya nyuma roho yake ikaingiwa na furaa kubwa sana, moyoni mwake akaanza kumuomba Mungu ampe binti yake nafasi nyingine ya kuweza kuishi.
Majira ya saa mbili usiku akafika katika     handaki alilo muacha Tom, kwa haraka akafungua mfuniko wa kuingilia kwenye handaki hilo kisha akamshusha Manka ambaye bado fahamu hazijamrejea.

“Tom fungua mlango wa chumba cha kwanza”
Mzee Godwin alimuamrisha Tom huku akiwa anahema sana kutokana na kuchoka sana pmoja na wasiwasi mwingi unao mtawala. Akamlaza Manka juu ya kitanda.
“Babu huyu naye ni nani?”
“Utamjua hembu tumpe nafasi ya kuweza kupumzika?”
“Amefanyaje?”
“Heiii Tom sihitaji maswali Mengi”
Mzee Godwin alizungumza kwa hasira na kutoka nje ya chuma hicho, Toma akamtazama kidogogo Manka usoni kisha na yeye akatoka.
                                                                                                 ***
Wasamaria wema walo kuwa wakikatika katika barabara kuu, yakutokea mikoa ya Tanga na Arusha, wakasimama kwenye sehemu walipo ona moshi mwingi ukiendelea kuonekana katika upande wa pili wa barabara. Abiria waliomo katika basi la Ngorika, wakashuka kwenda kujaribu kuangalia gari hilo linalo teketea kwa moto.

Wakakuta vijana wawili wakiwa wamelala pembeni huku wakionekana kupoteza fahamu na miili yao ikiwa imajaa makovu ambayo, hakuna ambaye aliweza kuyatilia mashaka kwani waliamini kwamba ajali hiyo ya gari ndogo ndio imeweza kusababisha majeraha hayo.
“Niwazima hawa?”
Jamaa mmoja alizungumza huku akiwatazama. Kijana mwengine mrefu na mweusi kiasi, akawatazama vijana hao jinsi walivyo lala chini, baadhi ya watu wakataka kuwanyanyua.

“Hembu musiwanyanyue mara moja, sogeeni pembeni”
Alizungumza na kuwafanya watu wengine kumshangaa, kwani majeruhi hao wanahitaji msaada wao na si kuwaacha katika eneo hilo.
“Wewe kijana mjinga kweli, hao wangekuwa ni wadogo zako ungewaacha waendelee kulala hapo chini?”
Mzee mmoja wa kichaga alimjia juu kijana huyo anaye onekena ni mstaarabu na mtulivu sana, mwenye sura ya kipole.
“Mzee wangu nimewaomba na sijataka kutimia nguvu, hivi munavyo ona hawa wamepata ajali kweli?”

“Wewe unaonaje?”
Mzee huyo aliendelea kumropokea kijana huyo, aliye achia tabasamua pana kisha akaendelea kutazama sehemu walipo lala vijana hao. Kila alipo zidi kuchunguza kwa umakini eneo hilo, ndipo alipo gundua kwamba kuna mtu ambaye aliweza kuwadhuru vijana hao kwa kuweza kuwapiga sana.

Kitu kilicho zidi kumshangaza kwa vijana hao, shawakuweza kuporwa kitu cha aina yoyote, simu zao zipo katika eneo la tukio. Akachukua simu za vijana hao wawili, kwa bhati nzuri moja ya simu bado ilikuwa inaendelea kurekodi tukio katika eneo hilo. Akaisave video hiyo kisha akaanza kuitazama, sauti za vijana hao zikasikika kwenye video hiyo huku picha ya gari hilo linalo malizikia kuteketea kwa moto.

Video hiyo ikamuonyesha mzee Godwin, akiwa amemshikila binti mmoja, ila gafla mshika kamera ya simu hiyo, akastukia akiangushwa chini na kuanza kulia kwa uchungu mkali ikiashiria kwamba mzee huyo aliweza kuwapiga vikali.
“Haya munaweza kuwachukua vijana hao”
Kijana huyo alizungumza huku akizichukua simu hizo, kisha akaituma video hiyo kwenye simu yake kisha akaituma makao makuu alipo kuwa ameitwa kwa ajili ya kazi maalumu
                                                                                                            ***
     Agnes na Jaquline baada ya kufanya tukio la kuituma video ya vitisho kwa bwana Rusev, wakaagana na mzee ambaye aliweza kuwafundisha mbinu nyingi za kupambana kutumia miili yao pasipo kutumia silaha za moto.

Agnes aliweza kufuzu kwa asilimia mia, katika kujua mbinu hizo za kupambana. Moja kwa moja wakafunga safari hadi mjini Mosscow, huku wakiwa wameziweka nywele zao katika mfumo ambao si rahisi sana kwa watu kuweza kumstukia Agnes kwamba ni muuaji aliye weza kuhusika na kifo cha waziri wa mambo ya nje wa Marekani bwana Paul Henry Jr, mwaka mmoja ulio pita.

Tiba Asilia Ya Tatizo La Kutoa Mbegu Dhaifu Za Kiume

$
0
0
IMESIMULIWA   NA   DOKTA  MUNGWA  KABILI……0744  000  473.

Mwanaume   mwenye  kutoa  mbegu dhaifu  za  kiume, hawezi  kumpa  ujauzito  mwanamke. Ili  mwanaume  awe na  uwezo  wa  kumpa  mimba  mwanamke  ni  lazima  mwanaume  huyo  awe  na  uwezo  wa  kutoa  mbegu  imara  za  kiume.

NINI   TIBA   ASILIA  YA  TATIZO  LA  KUTOA  MBEGU DHAIFU  ZA  KIUME

Zipo  tiba  asilia  za  aina  tofauti  tofauti , ambazo  zinatibu na  kuponyesha  tatizo  la  kutoa  mbegu  dhaifu  za  kiume.  Tiba  hizo  humpa  mhusika, uwezo  wa  kumjaza  mimba  mwanamke.

Katika  makala  haya  ya  leo, tuta  angazia aina  mojawapo  kati  ya  tiba  hizo.

MAHITAJI   MUHIMU
1.     Korosho  robo  kilo
2.    Maziwa  ya  mtindi robo  lita
3.    Mchele  nusu  kilo
4.    Maji  ya  uvuguvugu  lita  moja  na  nusu
5.    Bata  dume  mmoja.

JINSI   YA  KUFANYA
1.     Saa mbili kamili  asubuhi :  Chukua  mchele  robo  kilo, ulio pepetwa  na  kulowekwa  kwenye  maji  usiku  kucha. Kula  mchele  huo  pamoja  na  maji ya  uvuguvugu  lita  moja  na  nusu.  UTAFANYA  HIVYO KWA  MUDA  WA  SIKU  AROBAINI  ( 40 )  MFULULIZO.

2.    Saa  tatu  kamili  usiku :  Chukua  robo  kilo  ya  korosho, kisha  kula  pamoja  na  robo  lita  ya  maziwa  mtindi.  UTAFANYA  HIVYO  KWA  MUDA  WA  SIKU  AROBAINI  MFULULIZO.

3.    BAADA  YA  SIKU  AROBAINI :

Baada  ya  kufanya  zoezi  hilo  hapo  juu  kwa  muda  wa  siku  arobaini, panga  siku  ya  kukutana  kimwili  na  mke wako.

SIKU  YA  KUKUTANA  KIMWILI  NA  MKEO
Siku  utakayo  kutana  kimwili  na  mkeo, kabla  ya  kukutana  nae, fanya  kama  ifuatavyo:

ACHUKULIWE  BATA DUME  MMOJA ALIYE  KOMAA, KISHA  ACHINJWE  HALAFU  ACHEMSHWE  BILA  KUUNGWA  NA  CHUMVI  WALA  KIUNGO  CHOCHOTE  KILE.  UTAKULA  NYAMA  YA  BATA  HUYO  PAMOJA  NA  SUPU  YAKE  KISHA  BAADA  YA  HAPO, NENDA  KAMUINGILIE  MKEO. HAKIKA   MKE  WAKO  ATABEBA  UJAUZITO  SIKU  HIYO.

Jaribu  kutumia  tiba  hiyo  hapo  juu  uone  ufanisi  wake.

Na.  DOKTA   MUNGWA  KABILI  …..  0744 000  473.

Nataka Kujifunza Utabibu Wa Asili!

$
0
0
Kwa muda  mrefu  sasa, nimekuwa  nikipokea  simu, ujumbe  mfupi wa  maneno (sms) pamoja  na  barua  pepe  kutoka   kwa  watu  mbalimbali, kutoka  hapa  nchini  na  nchi  jirani, wakiomba  kujifunza  UTABIBU  WA  ASILI.

Katika  miaka  ya  hivi  karibuni, watu  wengi  wamekuwa  na  muamko  mkubwa sana kuhusu  tiba  za  asili.

 Hii  ni  kutokana na  ukweli  kwamba, tiba za  asili  zimethibitika kuwa  na  uwezo  mkubwa  sana  wa  kutibu  na  kuponyesha  magonjwa  na  matatizo  mbalimbali  ya  kiafya  yanayo  mkabili  mwanadamu.

Kutokana  na uwepo wa idadi  kubwa  ya  watu  wenye  uhitaji  mkubwa  na endelevu  wa  tiba  za  asili, watu  wengi  kutoka sehemu  mbalimbali  wamekuwa wakitafuta  namna  ya  kujifunza  kuhusu  utabibu  wa  asili, ili  wapate  maarifa  yatakayo wasaidia kuanzisha  huduma   ya tiba  asilia, ambayo  mbali  na  kuwasaidia  katika  kuendesha  maisha  yao  ya  kila  siku, lakini  pia  itawapa  uwezo  wa  kuwasaidia  watu mbalimbali  wenye kusumbuliwa  na  magonjwa  na  matatizo  mbalimbali  ya  kiafya.

MAHALI   UNAPOWEZA   KUJIFUNZA   UTABIBU  WA  ASILI
Kwa  mujibu  wa  SHERIA  YA  TIBA  MBADALA  YA  TANZANIA,  mtu  anaweza kuwa  tabibu  wa asili  eidha  kwa  kujifunza  au  kwa  kurithishwa.

i.                   Anaweza  kurithishwa  na  baba, babu, bibi  nakadhalika.

ii.                Anaweza  kujifunza  kwenye  chuo  rasmi. Tanzania mafunzo  rasmi  ya  tiba  mbadala  hutolewa  pale Muhimbili  kwenye  kitengo  au  Taasisi  ya  Tiba  za  Asili  iliyopo pale  Muhimbili.

Mafunzo  yanatolewa  kuanzia  ngazi  ya  cheti  na  kuendelea, na  hutolewa  kwa  wanafunzi  walio  timiza  vigezo  kama  vile  kufaulu  vizuri somo  la  Baiolojia  kwenye  mtihani wa  kidato  cha  nne  au cha  sita.

iii.              Tatu; Anaweza   kujifunza  kwa  MGANGA  AU  TABIBU  WA  ASILI.

Baraza  la  Tiba  Asilia  na  Tiba  Mbadala  litamtambua  na  kumsajili, tabibu  ambae  amepata  mafunzo yake  katika  moja  wapo  kati  ya  sehemu  nilizo zitaja  hapo  juu.
 
Toka  enzi  za mabibi  na  mababu, matabibu  wengi  wamekuwa  wakijifunza  kuhusu  UTABIBU  kupitia  kwa  matabibu  wengine.
 Hapa  kijana  anae  taka  kuwa  tabibu, huenda  nyumbani  kwa  tabibu  na  kuomba  kufundishwa  kuhusu  utabibu.
Tabibu  atamchukua  kijana  huyo na  kuanza  kumfunza  utabibu  kwa  nadharia  na  vitendo  mpaka  pale  atakapo  jiridhisha  kuwa  kijana  huyo  ameiva  kwenye  utabibu ndipo  atakapo  mtawaza  utabibu . 
 
Mara  nyingi  wazazi  wa  kijana  ndio  walio mpeleka  kijana  wao  kujifunza  utabibu kwa  faida  yake  na  ya  familia  na  ukoo  kwa  ujumla. 
Ilikuwa  ni  jambo la  heshima  na  fahari  kuu  kutoka  katika  familia  yenye  Tabibu  wa  asili, ambae  aliwasaidia  watu wenye  kusumbuliwa  na  magonjwa  mbalimbali.
Maarifa  haya  yalisambazwa  kizazi   hata  kizazi.

DOKTA.MUNGWA  KABILI  NA  MAFUNZO  YA  UTABIBU!
Watu  wengi wenye kuvutiwa  na  kazi  ya  utabibu  wamekuwa  wakinipigia  simu  kuniuliza  kama  nami pia  hutoa  mafunzo  ya  utabibu. Jibu  langu  ni  NDIO.
Toka  mwaka  1987, nimekuwa  nikitoa  mafunzo  haya  kwa  watu  mbalimbali  wenye  kuvutiwa  na  kazi  ya  utabibu.
 
 Mamia  ya  matabibu  wa  asili, wamepitia  kwenye  mikono  yangu.  Wengine  wamejifunza  utabibu kilingeni  kwangu, wengine  wamejifunza  kwa  njia  ya  masafa  marefu.
Kila  mwaka  huwa  ninatoa  mafunzo  ya  utabibu  kwa  idadi  kadhaa  ya  vijana  wa  kike  kwa  kiume, ambao  wanavutiwa  na  kazi  ya  utabibu . 
 
Mafunzo  ninayo  yatoa ni  yale  ya  JINSI  YA  KUTIBU  NA  KUPONYESHA  MAGONJWA  NA  MATATIZO  MBALIMBALI  YA  KIAFYA  KWA  KUTUMIA  DAWA  ZA  ASILI.  
 
Vijana  hawa  hujifunza  kuhusu  maelfu  ya  aina  mbalimbali  za  dawa  za  asili, kutoka  sehemu  mbalimbali  za  Tanzania  na  Afrika kwa ujumla, bila  kusahau  dawa  za  asili  kutoka  uarabuni  na  India.
 
Sifa  za  kupata  nafasi  ya  kufundishwa  nami  kuhusu  utabibu wa  asili, ni   kwanza  uwe  na  wito  wa  kufanya  kazi  ya  utabibu, pili uwe  na  akili  timamu, tatu uwe  unajua  kusoma  kuandika  na  nne  uwe  raia  mwema, tano  uwe  na  nidhamu.

Kama  una  wito na  kazi ya  utabibu  na unataka  kujifunza  kuhusu  utabibu, basi  wasiliana  nami  kwa  simu  namba  0744  000  473.
Vile  vile wapo  wazazi  na  walezi ambao  wamekuwa  wakinipigia  simu, wanasema  watoto  wao wapo  tu  mtaani, hawana  kazi  za  kufanya, je  wanaweza  kuwaleta  kwangu  wajifunze  utabibu?

Jibu  langu  ni, kazi  ya  utabibu  ni  kazi  inayo  hitaji  wito ndani  yake. Sio  kazi  ya  kufanya  kwa  sababu  hauna  kitu  kingine  cha  kufanya. Ni  kazi  ambayo inatakiwa  kufanywa  na  mtu  anae  ipenda  kutoka  moyoni.  Usikimbilie  kuifanya  kazi  hii  kwa  sababu  unajua  ina  maslahi  makubwa  ndani yake. Kwanza  uwe  na  wito  ndani  yako.
 
IMESIMULIWA   NA   DOKTA   MUNGWA   KABILI  0744 000 473.

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

Taarifa Toka IKULU kuhusu kuapishwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania aliyeteuliwa jana

Rais Wa Gambia Aliyegoma Kuachia Madaraka Atangaza Hali Ya Hatari Nchini Humo

$
0
0
Bunge la Gambia limerefusha utawala wa Rais Yahya Jammeh kwa miezi mitatu baada ya kiongozi huyo kutangaza hali ya hatari katika taifa hilo na ikiwa imebaki siku moja tu kabla ya muhula wake kumalizika rasmi .

Tangazo la bunge kurefusha madaraka ya rais Jammeh kwa miezi mitatu yanafuatia amri iliyotangazwa na kiongozi huyo kutokana na kile alichokiita ni kuingiliwa kwa kiasi kikubwa na mataifa ya kigeni katika uchaguzi wa Desemba mosi na mambo ya ndani ya Gambia.

Kwa tangazo hilo wananchi wa Gambia "wamepigigwa marufuku kufanya matendo yoyote ya kutoheshimu sheria, kuchochea ghasia na kuvuruga amani".

Hali ya hatari
Kupitia Televisheni ya taifa, Rais Jammeh amesema kuwa, "Mimi Sheikh Profesa Alhaji Dr Yahya A.J.J. Jammeh rais wa Jamhuri ya kiislamu ya Gambia na Amiri Jeshi mkuu, natangaza hali ya hatari kwa nchi nzima ya Gambia kama hali ilivyo na ikiwa itaendelea inaweza kusababisha hali ya hatari kwa umma", amesema Jammeh. 
 
Chini ya katiba ya Gambia hali hiyo ya hatari itadumu kwa kipindi cha siku 90 ambapo bunge la nchi hiyo tayari limepitisha azimio la kuithibitisha na hiyo inamaanisha rais Jammeh atasalia madarakani kwa kipindi cha miezi mitatu.

Marekani imemtaka rais Jammeh ambaye ameitawala Gambia kwa miaka 22 kuachia madaraka na kumkabidhi rais mteule Adama Barrow ambaye yupo nchini Senegal anakopanga kubakia hadi hapo kesho siku ya kuapishwa kwake.

Jumuiya ya kiuchumi ya mataifa 15 ya magharibi mwa Afrika ECOWAS nayo imetoa wito kwa kiongozi huyo kuheshimu matokeo ya uchaguzi na kuondoka mamlakani, wito unaoungwa mkono na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na Umoja wa Afrika na wengine.

Jammeh amekataa ujumbe wa viongozi wawili wa ngazi ya juu wa Afrika Magharibi ambao walimtolea wito wa kuondoka.

Raia wa nje waondolewa
Kutokana na tangazo hilo, mataifa ya kigeni yamesema yatawaondoa raia wake, wizara ya mambo ya kigeni ya Uingereza imeandika katika tovuti yake kuwa "uwezekano wa kuingilia kijeshi na usumbufu wa kiraia ni mkubwa", tahadhari ambayo imeungwa mkono na Uholanzi kupitia mitandao ya kijamii ikiwataka raia wake kuepuka kusafiri labda ikiwa ni kwa umuhimu.

Wakala wa utalii wa Uingereza Thomas Cook kupitia taarifa yake imesema inapanga kuwaondoa wateja wake watalii wapatao 3500 kupitia uwanja wa ndege wa Banjul katika masaa 48 yajayo.

Tayari mawaziri wanne katika serikali ya rais Jammeh wamejiuzulu wiki hii ambao ni waziri wa fedha, waziri wa biashara, waziri wa utalii, na waziri wa mambo ya nje, na kuungana na waziri wa mawasiliano ambaye aliachia wadhifa wake wiki iliyopita na sasa yuko Senegal.

Raia nchini humo wameendelea kukimbia kutoka Gambia wakielekea nchi jirani za Senegal, Guinea-Bissau na Guinea.

Taarifa kutoka Nigeria zinasema maandalizi ya kuwapeleka wanajeshi kadhaa mjini Dakar Senegal yamekamilika hali inayohusishwa na kile kinachojiri nchini Gambia.

Chanzo: DW

LIVE : Tazama Matangazo ya Moja Kwa Moja Toka IKULU .....Rais Magufuli Anamuapisha Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania

$
0
0
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma anaapishwa leo Januari 18, 2017 jioni hii  Ikulu jijini Dar es Salaam.
==> Tazama Video hii Kushuhudia Live zoezi hilo.

Kilichompata Mchungaji aliyetabiri kifo cha Rais Robert Mugabe

$
0
0
Mwishoni mwa mwaka 2016, raia na wafuasi wa vyama vya upinzani nchini Zimbabwe waliandamana kupinga utawala wa Rais Robert Mugabe ambaye amekuwa madarakani tangu 1980.

Habari zilizoripotiwa na vyombo vya habari vya kimataifa zimedai kuwa maafisa wa polisi nchini Zimbabwe wamemkamata  mhubiri aliyetabiri kwamba Rais Robert Mugabe atafariki mwezi Oktoba mwaka huu.

Pastor Patrick Mugadza alikamatwa akiwa mahakamani mjini Harare Jumatatu ambapo alikuwa ameenda kwa kesi nyingine dhidi yake. Wakili wake Gift Mtisi amewambia waandishi wa habari kuwa alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kuvalia bendera ya taifa

Wakili wake ameimbia AFP kuwa; "Alikuwa amefika mahakamani kwa kesi hiyo polisi walipomkamata wakati wa mapumziko na kumfungulia mashtaka kwa sababu ya unabii huo"

Awali alishtakiwa kwa kukosea heshima mamlaka ya Rais lakini shtaka hilo likabadilishwa baadaye na kuwa amewatusi watu wa asili fulani au dini fulani.

Pastor Mugadza wiki iliyopita aliandaa kikao na wanahabari ambapo alitabiri kwamba Mugabe atafariki Oktober 17 mwaka huu.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images