MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
. Akiwa gorofa ya kwanza kwenda gorofa ya pili, akakutana na askari wawili wakishiuka chini, akaishusha kofia yake chini kidogo, akapisha na askari hao wakimtazama.
“Ngoja kwanza”
Askari mmoja alizungumza baada ya kushuka ngazi sita kwenda chini, akatoa picha iliyopo mfukoni mwake.
“Ndio huyu tunaye mtafuta”
Askari mmoja alizungumza na kuanza kupandisha kwenda ngazi za juu huku akikimbia, kwa bahati nzuri akafanikiwa kumuona mzee Godwin akitembea kwenye moja ya kordo.
“Simama polisii”
Askari huyo alizungumza huku bunduki yake akiwa amemnyooshea mzee Godwin kwa nyuma.
ENDELEA
“Nyoosha mikono yako juu”
Watu walio karibu na eneo alipo simama Mzee Godwin pamoja na askari hao walipo nyuma yake mita chache kutoka sehemu alipo, wakabaki wakishangaa tukio hilo kwani hawakujua ni kwanini askari hao wamemshikia mtutu mtu huyo. Taratibu Mzee Godwin akanyoosha mikono yake juu, huku akiwa bado hajageuka kuwatazama askari hao. Askari mmoja akamkonyeza mwenzake amfwate mzee Godwin, kwenda kumfunga piungu.
Kwa umakini mkubwa askari huyo akaanza kutembea kwa kunyata huku bunduki yake aina ya SMG akiwa ameishika vizuri mikononi mwake. Kitendo cha kumfikia Mzee Godwin, ikawa ni moja ya kosa kubwa sana, mzee Godwin akageuka na teke la mguu wa kustoto, lililo mchota askari huyo miguu yake na kujikuta akianguka kama mzingo na bunduki yake akiitupia pembeni, kwa uharaka wa hali ya juu, mzee Godwin, akaichomoa bastola yake iliyo ichomeka kiunoni mwake kwa nyuma.
Hakuhitaji hata kuwa na huruma na askari aliye mshikia bunduki, akibabaika. Akapimga risasi moja ya paja askari huyo, akaanguka huku akilia kwa uchungu na maumivu makali sana.
Mlio wa bastola yake ukawafanya watu kutawanyika, si madaktari wala wagonjwa walio jiweza, kila mmoja akaikoa roho yake, hata kushangaa kwao kukaingia doa. Askari wengine walio kuwa kwenye maeneo tofauti ya hospitali, baada ya kusikia mlio huo wakakimbilia katika jengo hilo la maabara.
Askari aliye anguka chini, baada ya kuona mwenzie ametandikwa risasi ya paja na anaendelea kuhangaika hangaika chini, huku akilia, akajaribu kurusha teke la chini, ambalo lilimuangusha mzee Godwin. Askari huyo akanyenyuka, huku akikunja ngumi, mzee Godwin akasimama huku akitabasamu, kwani akimuangalia askari huyo, umri wake wapata miaka ishirini na tatu hadi tano.
Askari akaanza kurusha ngumi zake, zilizo mkosa Mzee Godwin, kwani aliweza kuzikwepa zote huku akiendelea kumuonea huruma kijana huyo. Mzee Godwin akakimbia kwa kasi, askari huyo akanzanza kumfukuza, mzee Godwin akafika hadi karibu ya ukuta, kwa uwezo mkubwa alio kuwa nao akakanyaga ukutani, na kujigeuza kwa kasi, askari huyo akakutana na teke zito la kichwa lililo muangusha chini, na kupoteza fahamu hapo hapo.
“Nice job, kijana”
Mzee Godwin alizungumza huku akijiweka sawa koti lake. Akiwa katika kordo hiyo, askari mmoja akajitokeza akiwa na bunduki. Askari akaanza kufyatua risasi kwa mawenge yaliyo muingia baada ya kumuona wezake wakiwa wamelala chini, mmoja akiwa ametulia kimya na mwengine akiendelea kulia huku damu nyingi zikiwa zimesambaa kwenye sakafu.
Mzee Godwin, akauvamila mlango ulipo mbele yake, na kuingia ndani ya chumba hicho, alicho wakuta madaktari wawili wakiwa wamelala chini ya meza kwa woga. Mzee Godwin akaufunga mlango kwa ndani kisha akaichomoa bastola yake.
“Simameni”
Aliwaamrisha askari hao, wakatoka chini ya meza huku kila mmoja akionekana kuwa ni muoga kupindukia, kwani haja ndogo ilianza kuitotesha suruali yake.
“Vueni nguo haraka”
Kila walicho ambiwa ndicho ambacho madaktari hao waliweza kukifanya, Mzee Godwin naye akaanza kuvua nguo zake na kubakiwa na nguo za ndani.
“Wewe kikojozi vaa hizi”
Akamrushia daktari nguo zake, kisha yeye akachukua nguo za daktari mwengine. Alipo maliza kuvaa mavazi hayo ya kidaktari pamoja na miwani, akamuamrisha daktari huyo kuvaa, kofia yake aliyo kuwa ameivaa.
Gari za polisi wa vikosi vya kutuliza ghasia F.F.U, zikazidi kuongezeka katika hospitali ya muhimbili, hii ni baada ya kupata habari kwamba, gaidi Mzee Godwin ameweza kuonekana katika hospitali hiyo na kuwashambulia askari wawili. Wananchi walipo katika eneo la hospitali wakawekwa chini ya ulinzi mkali, hapakuwa na aliye ruhusiwa kuingia ndani ya hospitali, wala aliye ndani ya hospitali hakuruhusiwa kuweza kutoka nje. Hii yote ni kuhakikisha gaidi wao hajichanganyi na wananchi na kuweza kutoweka katika eneo la hospitali.
***
Nguvu na umahiri wa kikosi cha bwana Rusev kikazidi kuongezeka siku hadi siku, akazidi kuchukua vijana mbali mbali katika mataifa ya kiafrika, akawaingiza katika kikosi chake ili kuhakikisha mipango yake anayo ipanga inakwenda vizuri sana.
“Muheshimiwa mipango yako ni nini?”
Mshauri wake wa karibu alimuuliza bwana Rusev mara baada ya vijana zaidi ya ishirini kutoka nchi ya Afrika kuweza kuingizwa kwenye kambi yake, iliyopo chini ya bahari.
“Nahitaji kuifanya dunia nzima kuwa na kiongozi mmoja tu, ambaye ni mimi”
“Ila muheshimiwa itawezekana kweli, kutokana mataifa mengi yana nguvu sana”
“Kwa ukimya ambao tumeufanya tangu kifo cha Pual Hennry Jr, sasa ninakwenda kuitingisha dunia. Nahitaji ndoto za Adolf Hitler niweze kuzitimiza mimi”
Bwana Rusev alizungumza huku akitabasamu. Akiendelea kuwaangalia vijana hao, wakinza kupatiwa mafunzo maalumu katika ngome yake, ambayo ni ngumu sana kwa mtu kuweza kuifahamu.
Simu ya mshauri wake, ikaingia ujumbe wa video ulio mstua sana, ikabidi amuonyeshe bosi wake bwana Rusev.
“RUSEV, RUSEV RUSEV, Umenimiss eheee”
Sauti na sura ya Jaquline, vinaoenekana kwenye simu hiyo. Bwana Rusev akajikuta akiitumbulia macho video hiyo aliyo tumwa na muda mchache ulio pita.
“Huyu Malaya yupo hai?”
Bwana Rusev alizungumza kwa hasira huku akiendelea kuitazama video hiyo.
“Najua utashangaa, kuniona nipo hai. Hahahaaaaaa, ngoja niende kwenye point muhimu. Niliapa kwamba nilazima nitakuua, na hii ni moja ya ahadi nitakayo ifanya siku na muda wowote.”
“Ila kabla ya kufanya hivyo kutana na mgeni rafiki yako mpendwa”
Video hiyo ikasogezwa pembeni, ambapo bwana Rusev akaiona sura ya Agnes akitabasamu.
“Umewaacha wezangu wamekwenda jela kwa ajili yako, sasa tambua kazi ni moja tu. Tutakupeleka kuzimu mw………”
Bwana Rusev kwa hasira akaizima video hiyo ya vitisho kutoka kwa mabinti ambao anawatambua vizuri sana.
“Muheshimiwa ut…..”
Bwana Rusev akamtandika ngumi nzito mshauri wake huyo, kisha akaondoka kwa hasira na kuwafanya baadhiya askari wake kushangaa tukio hilo.
***
Mzee Godwin kuchungulia dirishani, akaona askari wengi wakiwa wamemiminika katika eneo la hospitalini, wakiwa na silaha nzito pamoja na mbwa wakali.
“Shitii”
Mzee Godwin alizungumza huku akijikuna kichwa chake
“Shika meza huko”
Aliwaamuru madkatari hao kuisukumia meza hiyo kubwa kwenye mlango, kwani alihisi muda wowote mlango unaweza kuvunjwa na askari walipo nje.
“Laleni chini”
Mzee Godwin aliendelea kuwaamrisha madaktari hao walio tii, kwani pasipo kuweza kufanya hivyo wanaweza kupoteza maisha yao. Katika kukichunguza chumba, kwa bahati nzuri akaona sehemu ya juu kuna sehemu inaweza kufunguka.
“Mukinyanya kichwa tu, ninawapasua ubongo”
Mzee Godwin alizungumza huku akipanda juu ya meza hiyo, akiendelea kutafuta ni jinsi gani anaweza kuifungua sehemu hiyo yenye mfuniko mgumu kiasi. Kwa bahati nzuri akafanikiwa kufungua mfuniko huo, akachungulia juu ya dari, akakuta uwazi mkubwa ambao unaweza kumruhusu yeye kuweza kupita pasipo wasiwasi.
“Hivi ni kwanini tusivunje mlango?”
Askari mmoja alishauri, wezake kwani ni muda umekatika wamekaa nje ya mlango huo wakishikilizia kitu kinacho endela ndani.
“Humo ndani kuna madaktari tukifanya hivyo tunaweza kuwapelekea wakauliwa
“Ila mkuu tutaendela kukaa hapa hadi saa ngapi?”
Hapakuwa na jibu lolote alilo litoa mkuu wao huyo, anaye hofia maisha ya madaktari hao.