MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
Televishen pamoja na Tv zote nchini Tanzania, zipo hewani, kuweza kuyanyakua mazungumzo ya moja kwa moja ya Raisi Praygod Makuya, kwenye uteuzi wa mawaziri wapya, hii ni kutokana na waziri mkuu kuweza kujiudhulu, kwa kusumbuliwa na matatizo ya kiafya yaliyo mchukua kipindi kirefu kukaa nje ya ofisi pasipo uwepo wake. Kama kanuni na taratibu za nchi ya Tanzania, inamlazimu raisi kuweza kufanya hivyo punde tu waziri mkuu anapokuwa ameachia kiti hicho kinacho tamaniwa na kila kiongozi aliyopo serikalini.
Raisi akaanza kutaja majina ya mawaziri wapya watakao chukua nafasi za mawaziri walio punguzwa kwenye wizara mbalimbali. Masikio ya wananchi wengi wa Tanzania, ni kwenye wizara ya ulinzi, ambayo katika siku za hivi karibuni imetokea kuyumba, hadi wananchi kuanza kupoteza imani na serikali yao pamoja na jeshi zima la polisi. Majina kadhalika ya mawaziri wapya na wazamani walio badilishwa wizara ya kaendelea kutajwa, ikafikia kwenye wizara ya ulinzi ulinzi, hapa raisi akanyamaza kidogo na kumeza fumba la mate huku akizikodolea kamera zilizopo mita chache kutoka katika sehemu aliyo simama.
“Katika wizara ya ulinzi, nimeweza kufanya mabadiliko makubwa sana, ambayo ninaamini yatakwenda kufurahiwa na wananchi walio wengi. Kwa maana katika kipindi changu cha utawala nimeweza kupokea malalamiko mengi sana kuhusiana na uhalifu katika jamii inayo tuzunguka.”
“Wizara hii nimeweza kuweka watu hodari, wanao weza kuhakikisha wanafuta hofu yote iliyo jengeka katika mioyo mingi ya wananchi”
“Basi hapa waziri wa wizara hii, anaitwa Eddy Godwin, makamu wake atakuwa Bernad Ngoswe”
Wananchi wengi wakabaki wakiwa wameshangazwa na jina hilo kwani, hawajawahi kulisikia kwenye serikali tangu raisi Praygod kuingia madarakani.
“Hivi huyo Eddy Godwin ni nani?”
Mchaga mmoja alisikika akiwauliza wezake walio kusanyika katika duka lake la kuuza tv, redio na vitu vingine vya majumbani, lililopo maeneo ya Kariakoo.
“Hata mimi simfahamu”
“Hawa watakuwa wanagawiana, kwanini wasimpe yule….yule nani….”
“Chande?”
“Hapana yule, ambaye wamekwenda kumtupia kwenye kilimo”
“Ahaaaa Masele”
“Ehee huyo huyo, yule jamaa anaonekana yupo fiti sana”
“Yaani wee acha. Ila baadaye si wanaapishwa, tutakuja kumcheki huyo jamaa mwenyewe”
“Etieee”
“Naye asije akatuletea ufala kama huyu mwenzie aliye pita Haki ya Mungu, naye tutamuombea mabaya”
“Hahaaa maswawe punguza munkari bwana”
“Sio munkarti chalii yangu, yaani waziri akiwa ovyo hata hawa watendaji wake huku chini wote wanakuwa mambumbu, hembu nenda pale sentral kaseme unatatizo uone kama hawata taka rushwa”
Nazungumzo ya watu mbalimbali katika mitaa tofauti ndani na nje ya jiji la Dar es Salaam, yalikuwa ni kuhusiana na huyo waziri mpya waliye msikia jina lake likitajwa. Wengi wao hawakuonyesha imani yoyote kwa waziri huyo, wanaamini naye atafanya madudu kama aliyo yafanya waziri aliye pita, kwa kuweza kuwapa polisi, uhuru ulio ptiliza, hadi inafikia hatua kwamba wananchi wa maisha ya chini wananyimwa haki zao za msingi, na wenye pesa ndio waliweza kupata haki zao na kuwakandamiza wale wasio kuwa nacho.
***
“Mume wangu utaweza, au ndio majukumu mazito uliyo kabidhiwa?”
Phidaya alimuulimuuliza mumewe, huku akimfunga tai vizuri kwenda kwenye sherehe ya wao kuapishwa inayo fanyikia kwenye viwanja vya ikulu muda wa jioni ya siku hii,waliyo tangazwa kama mawaziri wapya.
“Mungu ni mwema nitaweza tu”
“Eddy mume wangu usije ukaenda ukaboronga huko ikawa ni mamatizo, mengine. Napenda tuishi kwa amani”
“Baby wewe ndio mtu wa kunipa mimi moyo, ila si mtu wa kunikatisha tamaa”
“Sio kama nakukatisha tamaa mume wangu, kumbuka kwamba tumepitia shida nyingi sana, hadi leo tumepata hii amani, ninaona kwamba tutaipoteza amani hii”
“Never, nitahakikisha amani ya familia yangu kwanza, haiyumbi kisha nitahakikisha imani ya wananchi wangu, pia inapatikana”
“Sawa mume wangu mimi ninakuombea kila laheri, ila usisahau kwamba ninakupenda sana Eddy wangu, kupota maelezo”
“Nakupenda pia mke wangu”
Taratibu Phidaya akambusu mume wake mdomoni, akamuweka vizuri koti la suti aliyo ivaa. Wakatoka nje ya chumba chao na kuanza kushusha ngazi za gorofani hadi wakafika sebleni, walipo wakuta Shamsa na Junio wakitazama tv.
“Badilisheni chaneli muda si mrefu mutaniona nikiwa nimetokelezea kwenye kideo, nitaringaje”
Eddy alizungumza huku akizunguka zunguka na kuwafanya watoto wake wote kucheka.
“Mungu wangu…!! Hapa hawajapata waziri”
Phidaya alizungumza huku akicheka kicheko, kilicho mfanya hadi machozi ya furaha kumwagika.
“Weee, waziri wameupata, yaani varangati nitakalo kwenda kulianzisha ni kama shehe aliye lishwa nguruwe pasipo kujua, sasa akagundua, hiyo movie yake nitawaadisia nikirudi”
“Hembu nenda huko muda ujue unakwenda, ngoja uvuliwe huo uwaziri wako uone kama utazunguka zunguka tena”
“Nani anivue, subutuu nitampiga ngumii moja tuu, hadi aimbe haleluya”
“Dady usisahaku kuniletea zawadi?”
“Mwanangu, huko ikulu kuna zawadi gani”
“Eddy nenda bwana unachelewa, weee jizungushe zungushe kama tiara”
Eddy akambusu mke wake, akafungua mlango na kutoka nje na kumkuta dereva wa gari la serikali akiwa anamsubiria kwa ajili ya kumpeleka ikulu kwenye sherehe hiyo.
“Shikamoo muheshimiwa?”
Eddy hakuitikia salamu hiyo zaidi ya kuingia ndani ya gari na dereva huyo naye akaingia ndani ya gari, akawasha gari taratibu wakatoka kwenye geti kubwa la jumbu hili la Eddy alilo linunua siku chache baada ya kutoka katika mapumziko ya harusi yao yeye na mke wake Phidaya.