Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

TRA Yakusanya Shilingi Trilioni 1.15 Mwezi Oktoba

$
0
0
Na Ally Daud-MAELEZO.
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikia kukusanya shilingi trilioni 1.15 kwa mwezi Oktoba ikiwa ni kukamilisha malengo waliyojiwekea katika ukusanyaji wa mapato.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi Bw. Richard Kayombo wakati wa mkutano  na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu  hali ya makusanyo na zoezi la uhakiki wa namba za utambulisho wa mlipa kodi (TIN)linaloendelea hivi sasa.

“Tumefanikiwa kukusanya shilingi Trilioni 1.15 kwa mwezi Oktoba mwaka huu ikiwa ni kufanikisha malengo ya ukusanyaji kodi nchini ili kukuza uchumi wa nchi pamoja kusaidia Serikali kuendeleza huduma za jamii nchini” alisema Bw. Kayombo.

Aidha Bw. Kayombo amesema kuwa mapato hayo yametokana na mikakati thabiti iliyowekwa na mamlaka hiyo katika ukusanyaji kodi hapa nchini ili kuweza kusaidia ongezeko la pato la Taifa .

Katika hatua nyingine TRA imefanikiwa kushinda kesi 9 kati ya 10 zilizokuwa zikiendelea katika mahakama mbalimbali nchini dhidi ya walipa kodi wake na kufanikiwa kupata kiasi cha takribani Bilioni 16.9 .

“Tumefanikiwa kushinda kesi 9 kati ya 10 ambazo zilifikishwa mahakamani dhidi ya walipa kodi na kupata kiasi cha shilingi bilioni 16.9 hivyo kufanya juhudi zetu za kukusanya mapato mengi zaidi” aliongeza Bw. Kayombo.

Mbali na hayo Bw. Kayombo amesema kuwa zoezi la uhakiki wa namba za utambulisho wa mlipa kodi ambalo limeanza hivi karibuni linaendelea na litafikia tamati Novemba 30 mwaka huu kwa mkoa Dar es salaam hivyo wananchi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya uhakiki huo.

Aidha Bw. Kayombo ameongeza kuwa  kila mwenye namba ya utambulisho wa mlipa kodi anatakiwa akahakiki kwa ajili ya kupata taarifa sahihi za mlipa kodi ili kuepuka kufutwa kwa  namba yake ya utambulisho baada ya zoezi hilo kumalizika kwa mkoa husika.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi ya Novemba 10

Wanafunzi hewa 65,198 wabainika shule za msingi, sekondari nchini

$
0
0
Jumla  ya wanafunzi hewa 65,198 wamegundulika kuwepo katika shule za msingi na sekondari nchini, ambako idadi ya wanafunzi hao isingebainika kiasi cha Sh milioni 931.3 zingepelekwa shuleni kuhudumia wanafunzi hewa kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Katika mkutano na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene alisema kati ya wanafunzi hao wa shule za msingi ni 52,783 na sekondari ni 12,415.

Simbachawene alisema kazi ya uhakiki wa wanafunzi katika shule za msingi na sekondari ilifanyika mikoa yote nchini kutokana na agizo la Ofisi ya Rais, Tamisemi kwa makatibu tawala wa mikoa yote ya Tanzania Bara.

Alisema waliagizwa kuhakiki idadi ya wanafunzi katika shule zote za msingi na sekondari kwa kulinganisha taarifa ilivyokuwa Machi mwaka huu wakati wa ujazaji wa madodoso ya takwimu za shule za awali, takwimu za shule za msingi, sekondari na nyaraka za mahudhurio ya wanafunzi.

Alieleza kuwa taarifa za idadi ya wanafunzi kabla ya kuhakiki Machi 2016, zilionesha kulikuwa na wanafunzi 9,746,534 wa shule za msingi na wanafunzi 1,483,872 wa shule za sekondari.

“Baada ya uhakiki tuliofanya Septemba mwaka huu, inaonesha kuwepo wanafunzi 9,690,038 wa shule za msingi na wanafunzi 1,429,314 wa shule za sekondari,” alieleza na kuongeza kuwa uchambuzi umeonesha kuwa wanafunzi 52,783 wa shule za msingi na wanafunzi 12,415 wa sekondari hawakutolewa maelezo ya uwepo wao shuleni.

Alisema kwa tafsiri rahisi hao ni wanafunzi hewa kwa shule za msingi na sekondari nchini, ambao idadi hiyo ya wanafunzi hewa kama isingebainika kwenye uhakiki huo na kupelekwa fedha, Sh milioni 931.3 zingepelekwa shuleni kuhudumia wanafunzi hewa katika mwaka wa fedha 2016/2017.

Alisema kati ya fedha hizo Sh milioni 527.8 ni kwa shule za msingi na Sh milioni 403.4 ni kwa shule za sekondari.

Aliitaja mikoa inayoongoza kuwa na wanafunzi hewa ni Tabora (12,112), Ruvuma (7,743), Mwanza (7,349), Dar es Salaam (4,096), Kagera (4,763), Rukwa (4,054), Singida (3,239), Kilimanjaro (2,594), Kigoma (2,323), Njombe (2,307), Simiyu (2,081) na Arusha (1,923).

Mikoa mingine ni Mara (1,855), Tanga (1,378), Geita (1,281), Morogoro (1,172), Mtwara (882), Mbeya (786), Shinyanga (695), Songwe (512), Manyara (330), Dodoma (284), Lindi (281), Pwani (187), Iringa (161) na Katavi (0).

Waziri huyo alisema wanafunzi hewa walianza wakati serikali ilipoanza kupeleka fedha shuleni kama ruzuku.

Alisema Sh bilioni 27 zimekuwa zikipelekwa kila mwezi kama ruzuku ya uendeshaji shule za msingi na sekondari na posho ya madaraka kwa ajili ya wakuu wa shule na walimu wakuu, lakini baadhi ya walimu waliamua kuongeza idadi ya wanafunzi ili wapate fedha zaidi.

“Huu ujinga unaweza kufanywa hata katika ngazi ya wizara ni jambo la uchunguzi, zile fedha hazipiti Tamisemi zinakwenda moja kwa moja shuleni,” alieleza na kuongeza kuwa hatua za kinidhamu zinaendelea kuchukuliwa kwa wale wote waliosababisha uwepo wa wanafunzi hewa na Tamisemi inaendelea kuhakiki takwimu zilizowasilishwa.

“Serikali haitegemei tena kuwepo suala la wanafunzi hewa. Naagiza makatibu tawala wa mikoa, wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa na wakuu wa shule kuhakikisha suala la wanafunzi hewa halijitokezi tena katika shule zote za msingi na sekondari,” alibainisha Simbachawene.

Joseph Mungai Kuwagwa Leo Dar..........Mwili wa Samwel Sitta Kuwasili Leo

$
0
0
Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Elimu, Joseph Mungai unatarajiwa kuagwa   Dar es Salaam leo katika viwanja vya Karimjee.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, mtoto wa marehemu, William Mungai alisema ibada ya kuuaga mwili huo itafanyika katika viwanja hivyo saa 5.00 asubuhi.

Hata hivyo mtoto huyo wa marehemu hakutaka kuingia kwa undani kuhusu chanzo cha kifo cha baba yake, badala yake alisema familia iachwe iendelee kushauriana na daktari.

Alisema pamoja na hayo, kifo hicho kimewashtua kwa vile  kimetokea ghafla na kwamba baada ya kuisha kwa ibada ya kuaga mwili huo, utasafirishwa hadi Mafinga, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa kwa mazishi.

“Hadi sasa familia tunajua kwamba marehemu aliugua tumbo la kawaida na tulimpeleka hospitalini ambako alifariki dunia, tunaomba familia iachwe, kwa sababu  bado tunashauriana na daktari wake.

“Tumekubaliana mwili wake uagwe kesho (leo) saa tano Viwanja vya Karimjee ambako pia historia yake yote na familia itasomwa,” alisema William.

Kifo cha Mungai kilitokea juzi jioni katika kile kilichoelezwa kuwa   alianza kujisikia vibaya baada ya kunywa kiywaji katika   hoteli moja iliyopo Msasani, ambayo aliizoea.

Mmoja wa waombelezaji waliofika nyumbani kwa marehemu jana ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)- Zanzibar, Salum Mwalimu ambaye alimwelezea Mungai kuwa aliunga mkono  mabadiliko ya siasa.

“Hakuwa na kadi ya Chadema lakini alipenda mabadiliko, mwanaye William aligombea ubunge wa Mafinga kupitia  Chadema na baba yake alimuunga mkono,” alisema.

Mbunge wa zamani wa Kwela, Chrisant Mzindakaya alisema amesikitishwa na kifo hicho ikizingatiwa wiki iliyopita walikuwa pamoja na walizungumza mambo mengi ya siasa.

“Hakuwa na kesho katika maisha yake, alilokuwa na uwezo wa kulifanya alilifanya siku hiyo hiyo, alikuwa na msimamo, hakukubali kuyumbishwa,” alisema Mzindakaya.

Wakati huohuo, mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta unatarajiwa kuwasili leo ukitokea  Ujerumani ambako alikuwa akitibiwa hadi mauti yalipomfika.

Taarifa zilizotolewa na msemaji wa familia ya marehemu, Gerald Mongella, zinasema  mwili huo utawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 9.00 mchana na kupelekwa nyumbani kwake Msasani, Dar es Salaam.

“Ijumaa(kesho) saa tatu asubuhi ibada ya kuuaga mwili huo itafanyika katika viwanja vya Karimjee ambako ndugu na wakazi wa   Dar es Salaam watapata fursa ya kuaga,” alisema Mongella.

Mwili wa Sitta utasafirishwa hadi Dodoma ambako utaagwa na wabunge na baadaye utasafirishwa kwenda Urambo kwa mazishi   Jumamosi.

Sitta alifariki Novemba 07 mwaka huu katika Hospitali ya Technal University alipokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya saratani ya tezi dume.

Ushindi wa Trump Waacha Kilio Bungeni Dodoma

$
0
0

Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amesema wabunge wanawake wamesikitishwa na kushindwa kwa mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya Chama cha Democrat, Hillary Clinton.

Dk. Tulia alitoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma jana, baada ya kutambulisha wageni mbalimbali.

Alisema walitarajia mambo yangekuwa mazuri upande wao  akiwa mama (wanawake), lakini haikuwezekana.

“Safari hii haikuwezekana, asikate tamaa maana baada ya miaka minne mambo yanaweza kuwa mazuri zaidi kuliko ilivyokuwa sasa. Nampa pole mama Clinton kwa kuwa safari hii haikuwezakana,” alisema Dk Tulia huku akishangiliwa na wabunge wanawake na kuongeza:

“Nasikia kuna watu hapa wanasema tungempeleka mheshimiwa fulani… katika maeneo yale mama Clinton angeshinda,” alisema.

Kutokana na kile kilichoonekana kupigwa butwaa na uchaguzi huo, kabla ya kuuliza swali la nyongeza jana asubuhi, Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo (Chadema), alisema ana masikitiko makubwa kwa sababu Hillary Clinton ameshindwa uchaguzi.

“Kwa niaba ya wanawake wenzangu, nampa pole mama Clinton kwa kushindwa uchaguzi, tumeumia sana na tumerudi nyuma,” alisema.

Kauli hiyo ilimfanya Dk. Tulia kumtaka aeleze amepata wapi taarifa wakati bado wabunge wanawake wana faraja  Hillary angeweza kushinda.

Hata hivyo, akijibu swali la Suzan, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Khamis Kigwangala,  alimpa pole Hillary kwa kushindwa kwenye uchaguzi huo.

Waziri Mkuu wa India aiga wazo la Rais Magufuli na kulitekeleza

$
0
0
Wakati Rais John Magufuli alitishia kubadili fedha za Tanzania katika juhudi za kuwadhibiti watu wanaodaiwa kuficha fedha, Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ametangaza kuziondoa kwenye mzunguko noti za Rupia 500 na 1,000.

Akizungumza katika mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi uliofanyika Septemba Mosi katika Ukumbi wa Mlimani City, Rais Magufuli alisema kwa mamlaka aliyonayo anaweza kuamua kubadili fedha ili zile zinazofichwa, watu hao wakose mahali pa kuzipeleka.

Alisisitiza kwa kusema kauli hiyo ni mahsusi kwa watu walioficha fedha katika majumba yao na kuwataka kuacha tabia hiyo mara moja ili fedha hizo ziingie katika mzunguko.

Rais Magufuli alisema katika utawala wake fedha za bure hazitakuwapo kwa sababu zilizokuwapo awali zilitokana na fedha za wizi kutoka serikalini ambazo kwa sasa zimedhibitiwa.

Alisema kwa mwendo anaokwenda nao sasa ni ngumu kwa mwananchi kupata fedha bila kufanya kazi.

Habari kutoka India zinasema Waziri Mkuu Modi alitangaza hatua hiyo ya kushangaza kwenye runinga Jumanne usiku kuwa ni mojawapo ya harakati za kukabiliana na ufisadi na ukopeshaji wa fedha haramu.

Modi alisema noti zote za Rupia 500 na 1,000 “hazitakuwa fedha halali kuanzia usiku wa manane leo” na kwamba “zitabaki kuwa makaratasi yasiyo na maana.” 

Hata hivyo, alisema noti nyingine za Rupia 100, Rupia 50, Rupia 20, Rupia 10, Rupia 5, Rupia 2 na sarafu zote zitaendelea kuwa na thamani.

“Ulanguzi wa fedha na ufisadi ndiyo vikwazo vikuu katika kukabiliana na umasikini,” alisema Modi na kuongeza: “Watu wataweza kubadilisha noti zao za zamani na mpya katika benki kuanzia Novemba 10 hadi Desemba 30 na kwamba fedha hizo hazitatumika tena.”

Benki zilifungwa jana huku huduma za mashine za kutoa pesa za ATM zikisitishwa. Badala yake noti mpya za Rupia 500 na 2,000 zitawekwa katika mfumo wa fedha kuchukua nafasi ya zilizoondolewa.

Tangazo hilo lilisababisha mtafaruku kwenye vituo vya mafuta na maeneo mengine ya biashara kwani wauzaji wa rejareja walikuwa wakikataa kupokea noti hizo huku mashine za kutolea fedha zikifungwa. Katika viwango vya ubadilishaji fedha noti ya Rupia 500 ni sawa na Sh16,000 na Rupia 1,000 ni sawa na Sh32,000.

Wateja watakuwa na uwezo wa kubadili noti hizo ili wapewe mpya au kuziweka kwenye akaunti, lakini watatakiwa kujieleza mamlaka ya mapato walivyozipata.

Maelfu waandamana Marekani kupinga ushindi wa Trump

$
0
0
Kufuatia kutangazwa kwa Donald Trump kuwa Rais mteule wa Marekani, wananchi wa Marekani wameandamana katika miji saba kupinga ushindi huo wa Trump.

Waandamanaji hao wamekusanyika nje ya mnara maarufu wa Trump ‘ Trump Tower’  mjini New York wakipaza sauti za kumpinga Trump. Wengine walionekana nje ya Ikulu ya Marekani wakipaza sauti kuwa “Not my president” (Si Rais wangu), pamoja na mabango mengine.

Wengi wa waandamanaji walioongea na CNN wameelezea kuwa wana wasiwasi sana kuhusu Trump kwavile kuongoza Marekani sio kama kuiongoza nchi yoyote duniani.

“Kwa matokeo haya tumeiangusha Dunia. Trump hakustahili kuwa Rais. Nahisi watu walipiga kura kwa hasira lakini Trump ni hatari kwa dunia,” alisema mmoja wa waandamanaji aliyejitambulisha kwa jina la James Betwell kutoka Califonia.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya Novemba 11


Wizara Ya Mambo Ya Ndani Ya Nchi Yakamilisha Rasmi Taratibu Za Ajira Za Uhamiaji Kwa Ngazi Ya Askari Na Maafisa

Picha: Rais Magufuli Alipomtembelea na Kumjulia Hali Mke wake na Wagonjwa wengine Waliolazwa Muhimbili

$
0
0
Mke wa Rais wa Tanzania John Magufuli, Janeth, amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili. Jana  Ikulu imetoa picha ya Rais Magufuli akimjulia hali katika wodi ya Sewa Haji.

Taarifa ya ikulu ilisema , alipokuwa anamjulia hali mkewe, pamoja na  balozi na waziri mstaafu wa Tanzania Omar Ramadhan Mapuri, wagonjwa waliolazwa katika wodi ya Sewa Haji walimshukuru kwa hatua zilizochukuliwa na serikali kuboresha hospitali ya taifa ya Muhimbili

Pia walisema kuwa licha ya kuboreshwa kwa mazingira ya hospitali, wanapata huduma nzuri kutoka kwa madaktari na wauguzi.
Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na mkewe Mama Janeth Magufuli ambaye amelazwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu jana Novemba 10, 2016. Kulia ni Dkt Edward Ngwale akiwa na wauguzi katika wodi hiyo.
Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimjulia hali Waziri wa Zamani Balozi Omar Ramadhani Mapuri ambaye amelazwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu jana Novemba 10, 2016.
Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwashukuru na kuwapongeza kwa kazi nzuri baadhi ya madaktari na wauguzi kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alipotembelea wagonjwa pamoja na mkewe ambaye anapatiwa matibabu jana Novemba 10, 2016.
Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwafariji baadhi ya wagonjwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alipotembelea kuona wagonjwa pamoja na mkewe ambaye anapatiwa matibabu hapo jana Novemba 10, 2016.

Picha: Rais Magufuli Alivyoongoza wananchi wa Dar kuaga mwili wa Marehemu Joseph Mungai

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, jana tarehe 10 Novemba, 2016 aliwaongoza viongozi na wananchi wa Dar es Salaam kuuaga mwili wa Waziri na mbunge Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Joseph James Mungai katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na Rais Magufuli Viongozi wengine waliofika kuuaga mwili wa Marehemu Mungai ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa, Makamu wa Rais Mstaafu,  Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Waziri Mkuu Mstaafu. Frederick Tluway Sumaye, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Viongozi wengine mbalimbali wa Serikali na Siasa.

Joseph James Mungai alifariki dunia tarehe 08 Novemba, 2016 katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua ghafla na mwili wake utasafirishwa leo Ijumaa kwenda Mafinga Mkoani Iringa kwa Mazishi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na waombolezaji waliofika kuaga mwili wa Marehemu Joseph Muungai katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam Novemba 10,2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Rais Mstaafu awamu ya tatu Benjamin Mkapa pamoja na waombolezaji  wengine walipofika kuaga mwili wa Marehemu Joseph Muungai katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam Novemba 10,2016

Reli ya Standard Gauge kutoka Dar-Mwanza kuanza kujengwa Disemba, 6 mwaka huu

$
0
0
Hatua ya kwanza ya maandalizi ya ujenzi wa reli ya Standard Gauge imeshaanza ambapo awamu ya kwanza ya ujenzi huo kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza itaanza rasmi Disemba 6, 2016.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (RAHCO) Masanja Kadogosa amesema serikali imetenga trilioni 1 kwa ajili ya ujenzi huo.

“Ujenzi wa reli ya standard gauge umeshaanza lakini hatua iliyokuwepo haionekani, tenda zimeshaanza kutangazwa,” alisema  Kadogosa  wakati akiongea  na  waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.

Alisema ujenzi huo utaanza kwa awamu na kwamba awamu ya kwanza inatarajiwa kuanzwa Disemba 6, 2016 wakati ya pili itaanza Februari 15, 2016.

“Ujenzi huo utachukua miaka mitatu kukamlika, ambapo utaleta manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho. Pia utarahisisha usafirishaji wa mizigo kutokana na kwamba litakuwa na mabehewa yenye kilomita 2 ambayo sawa na ukubwa wa maroli 300,” alisema.

Alisema wamiliki wa majengo yatakayo athiriwa na ujenzi huo watalipwa fidia.

“Hifadhi ya reli ina maana kwamba kila upande inaachwa mita 30, hivyo kama kuna nyumba zitakazokuwa nje ya mita hizo zitatakiwa kubolewa wamiliki watalipwa fidia,” alisema.

Aidha, Kadogosa alisema kuna miradi mingine midogo ya ujenzi na ukarabati itafanyika ikiwemo ya ujenzi wa reli mpya ya Dar es Salaam ambayo itatumiwa kwa ajili ya usafiri kwa wakazi wa jiji hilo.

“Kuna Mradi wa kujenga reli mpya katika jiji la Dar es Salaam na viunga vyake kwa ajili ya treni za abiria ili kupunguza msongamano wa abiria na magari. Mradi huu uko katika hatua ya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali chini ya kampuni ya ushauri ya GIBB Engineering ya Afrika Kusini na kwamba inatarajiwa kukamilika Disemba 2016,” alisema.

Picha 5: Mwili wa Spika Mstaafu Samwel Sitta Uliyopokelewa Airport Jijini Dar es Salaam

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan jana aliongoza viongozi na wananchi katika mapokezi ya Mwili wa Spika Mstaafu Samuel Sitta katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ukitokea nchini Ujerumani alipofariki wakati anapatiwa matibabu.

Akizungumzia jinsi anavyomfahamu Samuel Sitta katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alisema Taifa limeondokewa kiongozi mwadilifu,mzalendo, mchapakazi na mtetezi wa wanyonge hivyo taifa litaendelea kuumuenzi utendaji wake.

Viongozi mbalimbali waliojumuika na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika mapokezi ya mwili wa Spika Mstaafu Samweli Sitta kweye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere ni pamoja na Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Seif Ali Iddi, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika, Kikanda na Kimataifa Dkt Augustine Mahiga na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Baada ya Mwili wa Spika Mstaafu Samuel Sitta kuwasili nchini jana mchana alipelekwa nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam ambapo leo  asubuhi viongozi na wananchi watatoa heshima zao ya mwisho za kuuaga mwili wa marehemu katika viwanja wa Karimjee jijini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akimpokea mjane wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta, Mama Margaret Sitta (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaongoza viongozi mbali mbali wakati wa mapokezi ya mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta

TANZIA: Mbunge Hafidh Ali Tahir Afariki Dunia Alfajiri ya Leo Akiwa Mjini Dodoma

$
0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia, Job Ndugai (Mb) anasikitika kuwatangazia kuwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar, Hafidh Ali Tahir amefariki dunia leo saa 9 alfajiri katika Hospitali ya General mkoani Dodoma.

 Spika anaungana na Wabunge wote katika kuomboleza msiba huu.

Awali Marehemu pia alikuwa mwalimu wa soka kwenye timu ya Bunge Sports Club na mpaka usiku wa Novemba 10 alikuwa pamoja na Wabunge katika vikao  mpaka saa 2.45 usiku.

BOT Yasitisha Kuweka Dhahabu Kama Hazina Ya Rasilimali Za Kigeni

$
0
0

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imesitisha kuweka dhahabu kama hazina ya rasilimali za kigeni kwa sababu ya kuyumba kwa bei ya madini hayo katika soko la dunia na kusababisha uwezekano wa kupunguza thamani ya hazina ya rasilimali ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Igunga Mhe. Dalaly Kafumu aliyehitaji kufahamu sababu za Serikali kukataa kutunza dhahabu safi katika Benki Kuu wakati Tanzania ni nchi mojawapo inayozalisha dhahabu safi.

Mhe. Kijaji alisema kuwa jukumu la msingi la Benki Kuu ni kuandaa na kutekeleza Sera ya Fedha inayolenga kuwa na utulivu wa bei kwa ajili ya ukuaji endelevu wa uchumi wa Taifa hivyo ili kufanikisha azma hiyo Benki Kuu inadhibiti ongezeko la ujazi wa fedha kwa kutumia nyenzo mbalimbali zikiwemo za kuuza dhamana na hati fungani za Serikali pamoja na kushiriki katika soko la jumla la fedha za kigeni kati ya mabenki.

“Katika kutekeleza jukumu lake la msingi, Benki Kuu hutunza hazina ya rasilimali za kigeni zinazotosha kuagiza bidhaa nje kwa kipindi kisichopungua miezi minne lakini kwa muda mrefu sasa Benki Kuu ya Tanzania haiweki dhahabu kama sehemu ya rasilimali hizo kutokana na kuyumba kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia”, alisema Mhe. Kijaji.

Naibu Waziri huyo alitoa mfano wa kushuka kwa bei ya dhahabu katika soko la Dunia ambapo dhahabu ilishuka kutoka dola 1,745 za kimarekani katika mwezi Septemba 2012 hadi dola za kimarekani 1,068 kufikia mwezi Desemba 2015.

Mhe. Kijaji alifafanua kuwa hazina ya rasilimali za kigeni zinaweza kuwa dhahabu – fedha (monetary gold) au fedha za kigeni ambapo uamuzi kuhusu hazina itunzwe vipi unazingatia vigezo mbalimbali vikiwemo vile vya kudumisha thamani, wepesi wa kubadilisha pamoja na faida inayopatikana kwa kuwekeza hazina hiyo.

Aidha, Mhe. Kijazi alisema kuwa ununuzi na uuzaji wa madini ya dhahabu unahitaji ujuzi maalum ambapo kwa kuzingatia jukumu la msingi la Benki Kuu inaonyesha dhahiri kuwa Benki hiyo haijajijengea uwezo katika eneo la biashara ya madini hayo.

LIVE: Fuatilia Hapa Zoezi la Kuuaga Mwili wa Samwel Sitta ambalo Linaongozwa na Rais Magufuli

$
0
0
Leo kuna shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Spika wa Bunge Maalum la Katiba(BMK), Marehemu Samwel Sitta.

Rais Magufuli ataongoza waombolezaji kuuaga mwili wa Marehemu Sitta katika Viwanja vya Karimjee.


==Fuatilia  zoezi hili hapo chini

Misiba Yasitisha Mkutano wa Bunge Mjini Dodoma Leo

$
0
0
Mkutano wa Tano  wa Bunge umeahirishwa kwa namna yake baada ya muhimili huo wa dola kupata misiba mikubwa miwili.

Misiba hiyo ni wa Spika Mstaafu, Samuel Sitta aliyefariki nchini Ujerumani na Mbunge wa Dimani(CCM) Hafidh Ally ambaye alifariki dunia usiku wa kuamkia leo (Ijumaa) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Dodoma.

Mara baada ya kutangaza  kifo cha Hafidh Spika wa Bunge,  Job Ndugai alimtaka Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge, Ajira, Kazi, Vijana Jenista kutengua kanuni ili  kuwezesha mambo vote kufanyika.

Spika alimtaka Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria  Ndogo Ndogo, Andrew Chenge kuhitimisha hoja yake ya taarifa ya Kamati iliyowasilishwa juzi bila kujadiliwa na wabunge ili  Serikali yaweze kufanyia kazi.

Baada ya kufanya hiyo, Spika ameahirisha bunge hadi saa  8.30 mchana kwa ajili ya kikao maalum cha Bunge.

Amesema mara  baada kikao maalum cha bunge kumuaga Sitta basi  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atatoa hoja yake kuahirisha Bunge kwa  kifupi sana  tofauti na wakati mwingine.

Mahakama Yampa Siku 7 Profesa Lipumba na Msajili wa Vyama Kujibu Hoja za CUF

$
0
0
Mahakama Kuu imewapa siku saba Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na wenzake kujibu madai ya chama hicho.

Msajili, Lipumba na wenzake walipewa muda huo jana na Jaji Sekieti Kihiyo kutokana na kesi ya madai iliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa CUF mahakamani hapo.

Katika kesi hiyo namba 23 ya mwaka 2016, bodi ya wadhamini CUF inaiomba mahakama itoe amri ya kubatilisha barua ya Msajili inayomtambua Profesa Lipumba kuwa ndiye mwenyekiti wa chama hicho.

Pia, wanaiomba mahakama itoe amri ya kumzuia Msajili kufanya kazi nje ya mipaka yake ya kisheria katika utekelezaji wa majukumu yake na pia itoe amri ya kumzuia Msajili kuingilia masuala ya kiutawala ndani ya chama hicho.

Mbali na Msajili na Profesa Lipumba, wadaiwa wengine katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na wanachama wengine tisa waliosimamishwa uanachama wa chama hicho, akiwamo Naibu Katibu Mkuu Bara ambaye pia ni Mbunge wa Kaliua (Tabora), Magdalena Sakaya.

Kesi hiyo ilitajwa jana mahakamani hapo kwa mara ya kwanza tangu ilipofunguliwa Oktoba 19, mwaka huu na mahakama ikataka wadaiwa kuwasilisha majibu ya madai hayo ya CUF, Novemba 17, mwaka huu.

Pia, Mahakama ilielekeza upande wa Maalim Seif kuwasilisha majibu ya hoja za wadaiwa Novemba 23 na ikapanga kesi hiyo itajwe tena Novemba 24, kwa ajili ya kuendelea na hatua nyingine.

Wadai katika kesi hiyo wanawakilishwa na mawakili Juma Nassoro na Halfani Daim wakati Msajili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wanawakilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu (PSA), Obadia Kameya na Lipumba na wenzake wakiwakilishwa na Mashaka Ngole.

Katika hati ya Kiapo kinachounga mkono maombi hayo, Maalim Seif anadai kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya kuingilia utendaji wa ndani wa Vyama vya Siasa.

Anadai kuwa Sheria ya Vyama vya Siasa na Katiba ya nchi haimpi mamlaka Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa chombo cha rufaa wala kurejea mambo ya utawala ndani ya chama cha siasa.

Badala yake anadai mamlaka hayo yako kwa vyombo vya juu vya chama na Mahakama na kwamba jukumu la Msajili ni kusajili vyama na kuweka kumbukumbu za vyama hivyo.

CUF kimekuwa na mgogoro wa kiuongozi baada ya Profesa Lipumba kuandika barua ya kutengua uamuzi wake wa awali wa kujiuzulu ambao Msajili alikubaliana naye na alikiandikia barua chama kuendelea kumtambua mwenyekiti huyo. Hata hivyo, CUF ilimfukuza uanachama Lipumba.

Haya Ndio Maujanja Ya Kutumia Camera Mbili Kwenye Tecno Phantom 6.

$
0
0
Habari ndio hii…kama ulikuwa hujasikia, Phantom 6 inakuja na kamera mbili za ukweli na wengi bado hawajafahamu jinsi ya kuzitumia. 

Fuatilia video hii kujua jinsi ya kutumia na kama una Phantom 6 unaweza kujaribu kisha weka mtandaoni ukitumia hashtag #UnleashThePhantom na kama hujanunua Phantom 6 tembelea maduka ya Tecno. Usikubali kupitwa.
 

Unaweza kutembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya Tecno kufahamu zaidi kuhusiana na Tecno Phantom 6 na Phantom 6 Plus.
 

Rais Magufuli aongoza mamia ya Watanzania kuaga mwili wa Samuel Sitta .....Atuma rambirambi kifo cha Mbunge Hafidh Ali Tahir

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 11 Novemba, 2016 amewaongoza viongozi na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samuel John Sitta aliyefariki dunia tarehe 07 Novemba, 2016 katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani.

Mwili wa Marehemu Samuel John Sitta umeagwa katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam ambapo Viongozi wengine waliojumuika kuuaga mwili huo ni pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Mawaziri wakuu wastaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Frederick Tluway Sumaye, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Katipwa Wambali na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Baada ya kuagwa katika viwanja vya Karimjee, mwili wa Marehemu Samuel John Sitta umesafirishwa kwenda Dodoma ambako Wabunge, Viongozi wa Mkoa na wananchi watapata fursa ya kuuaga katika Viwanja vya Bunge na baadaye jioni utasafirishwa kwenda Tabora ambako maziko yatafanyika kesho Jumamosi huko Urambo.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo la Dimani Zanzibar Mhe. Hafidh Ali Tahir kilichotokea majira ya saa 9 usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.Mhe. Hafidh Ali Tahir amefariki dunia muda mfupi alipofikishwa hospitali baada ya kuugua ghafla.

"Nimeshtushwa sana na kifo cha Mhe. Hafidh Ali Tahir na ninakuomba Mhe. Spika Job Ndugai unifikishie salamu za pole kwa Familia ya Marehemu, Wabunge, Wananchi wa Jimbo la Dimani, Ndugu, Jamaa na Marafiki wote walioguswa na msiba huu.

"Tutamkumbuka Mhe. Hafidh Ali Tahir kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika utumishi wa umma, katika michezo na akiwa mwakilishi wa wananchi, kwa hakika tumepoteza mtu muhimu sana" amesema Rais Magufuli na kumuombea Marehemu apumzishwe mahali pema peponi. Amina.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
11 Novemba, 2016
.


Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images