Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli Alitaka Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Liongeze Kasi ya Uzalishaji wa Mazao ya Chakula

$
0
0
Shirika la uzalishajimali lililo chini ya Jeshi la Kujenga Taifa (Suma – JKT) litaanza kutekeleza mpango wa kufuga samaki kwa kutumia vizimba (Cages) katika bahari ya Hindi baada ya mpango huo kuonesha mafanikio makubwa katika mito na maziwa mbalimbali hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa JKT Meja Jenerali Michael Isamuhyo muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Meja Jenerali Isamuhyo amesema ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba umepata mafanikio makubwa katika maeneo mbalimbali nchini hususani katika ziwa Viktoria na kwamba ili kupanua ufugaji huo Suma-JKT inajielekeza kufuga samaki katika bahari ya Hindi.

Ameongeza kuwa pamoja na ufugaji wa Samaki, Rais Magufuli ameliagiza Jeshi la Kujenga Taifa kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na shughuli zilizotajwa katika misingi ya uanzishaji wa jeshi hilo ili Serikali isipate gharama za kununua chakula kwa ajili ya vijana wanaokwenda kupata mafunzo ya JKT na pia kupata chakula cha ziada ambacho kitatumika kutatua tatizo la uhaba wa chakula katika maeneo yatakayokumbwa na uhaba.

Meja Jenerali Isamuhyo ameongeza kuwa Rais Magufuli ameitaka JKT kujenga mabwawa kwa ajili ya kuanzisha kilimo cha umwagiliaji katika maeneo yanayofaa kwa kilimo hicho.

Aidha, Mkuu huyo wa JKT amebainisha kuwa JKT itahakikisha inasimamia utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais na kuongeza kuwa kazi hii itakwenda sambamba na utekelezaji wa majukumu mengine ya JKT yaliyoainishwa katika uanzishwaji wake mwaka 1963 ikiwemo ujenzi kwa gharama nafuu.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

08 Novemba, 2016

Kangi Lugola Adai Mkataba wa EPA Utatuletea USHOGA.....Asisitiza serikali isiusaini ili Kuwalinda Wanaume

$
0
0

Mbunge  wa Mwibara Kangi Lugola, ameupinga  kwa  nguvu  zake zote  mkataba  wa EPA kwa madai kwamba hauna manufaa yoyote kwa taifa letu na kwamba ndani ya mkataba huo kuna vishiria vya USHOGA

Lugola aimeitaka serikali isiusaini mkataba huo ili kulinda maumbile ya wanaume yanayotaka kuharibiwa kupitia mkataba huo.

Msikilize hapo chini alipokuwa akitoa mchango wake bungeni

TANZIA:Aliyewahi kuwa Waziri wa elimu awamu ya tatu, Joseph Mungai afariki dunia

$
0
0


Aliyewahi kuwa waziri wa Elimu Tanzania Joseph Mungai amefariki Dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu

Geofrey Mungai mtoto wa Marehemu amesema marehemu alipelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuanza kutapika mfululizo na kudhaniwa kwamba alikuwa amekula kitu kibaya.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Novemba 9

Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi Kufuatia Kifo c ha Joseph Mungai

Waziri Mkuu aomba Serikali ya Uingereza ihamasishe wawekezaji zaidi kutoka nchini humo kuja kuwekeza katika sekta ya Viwanda

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiomba Serikali ya Uingereza ihamasishe wawekezaji zaidi kutoka nchini humo ili waje kuwekeza kwenye sekta ya viwanda.

Ametoa kauli hiyo jana (Jumanne, Novemba 8, 2016) wakati akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Bibi Sarah Cooke alipokutana naye ofisini kwake Bungeni, mjini Dodoma.

“Mheshimiwa Balozi utusaidie kualika wawekezaji wengi zaidi kwenye maeneo ya kilimo, viwanda vya usindikaji mazao ya wakulima, wavuvi na wafugaji, sekta ya mafuta na gesi, nishati na ujenzi wa makazi hasa kwa mkoa wa Dodoma ambako hivi sasa ni Makao Makuu ya Serikali,” alisema.

Alimweleza Balozi huyo kwamba Tanzania imedhamiria kuwa nchi ya uchumi wa kati na hivyo imejipanga kuwa na viwanda vya kutosha ili iweze kusindika mazao yake hapa nchini na itoe ajira kwa wananchi wake.

Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo pia kuishukuru Serikali ya Uingereza kwa msaada wake mkubwa wa ujenzi wa nyumba za walimu na shule mkoani Kagera zilizoathiriwa na tetemeko la ardhi lilitokea Septemba 10, mwaka huu.

Kwa upande wake, Balozi Cooke ambaye alifika kujitambulisha rasmi, amesema ameguswa na juhudi zinazofanywa na Serikali katika kukabiliana na masuala ya ufisadi na rushwa. “Kaulimbiu yenu kwamba rushwa haikubaliki (zero tolerance on corruption) inaonyesha jinsi mlivyodhamiria kupambana na baa hili,” alisema.

Alisema Uingereza inaongoza miongoni mwa nchi zenye wawekezaji wengi hapa nchini na kwamba inaendeleza mpango wake wa uwekezaji ambao unalenga maeneo makuu manne ambayo ni gesi na mafuta; kilimo; nishati jadidifu na uimarishwaji wa mazingira ya kufanya biashara.

Balozi Cooke alitumia fursa hiyo kutoa pole kwa Serikali kutokana na msiba wa Spika Mstaafu wa Bunge la Tisa na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Urambo, Tabora, Mheshimiwa Samwel Sitta kilichotokea usiku wa kuamkia Novemba 7, mwaka huu katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Mkuu Wa Mkoa Wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana Akutana Na Balozi Wa Uingereza Nchini Mhe. Sarah Cooke

Mfumuko Wa Bei Wa Taifa Kwa Mwezi Oktoba 2016, Umebaki Kuwa Asilimia 4.5

$
0
0
Na Dotto Mwaibale
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2016 umebaki kuwa ni asilimia 4.5 kama ilivyo mwezi Septemba 2016.
 
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ruth Minja wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana.
 
"Hii inaamanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2016 imekuwa sawa na kasi ya upandaji wa bei ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2016" alisema Minja.
 
Minja alisema fahirisi za bei zimeongeza hadi 103.17 mwezi Oktoba, 2016 kutoka 98.72 mwezi Oktoba 2015 ambapo mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Oktoba 2016 umebaki kuwa asilimia 6.0 kama ilivyokuwa mwezi Septemba 2016.
 
Alisema mfumuko wa bei wa mwezi Oktoba umechangiwa na kuongezeka kwa kasi ya bei za bidhaa za vyakula na zisizi za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Oktoba 2016 zikilinganishwa na bei za mwezi Oktoba 2015.
 
Akizungumzia uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 96 na senti 92 mwezi Oktoba 2016 ikilinganishwa na shilingi 97 na senti 04 ilivyokuwa mwezi Septemba 2015.
 
Aidha akizungumzia hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki alisema nchini Kenya mfumuko wa bei wa mwezi Oktoba 2016 umeongezeka kidogo hadi asilimia 6.47 kutoka asilimia 6.34 mwezi Septemba 2016.
 
Alisema nchini Uganda mfumuko wa bei wa mwezi Oktoba 2016 umepungua hadi asilimia 4.1 kutoka asilimia 4.2 mwezi Septemba 2016.

TANESCO Yatoa Taarifa Kufafanua Kuhusu Bei ya Umeme

$
0
0
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyotolewa katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu ombi la kurekebisha bei za umeme kwa mwaka 2017.

Ombi la mabadiliko ya bei za umeme liliwasilishwa EWURA kulingana na agizo la kubadilisha bei za umeme la mwaka 2016 lililoanza kutumika tarehe 1 April 2016. Ifahamike kuwa bei za umeme (Electricity Tariffs) zinazotumika zilitolewa zitumike mpaka tarehe 31/12/2016, hivyo itakapofika Januari 2017, inatakiwa bei mpya za umeme (NewElectricity tariff) kutolewa kwa mujibu washeria.

Hivyo TANESCO ilitakiwa kufanya tathmini ya gharama za uzalishaji , usafirishaji na usambazaji umeme na kupeleka mapendekezo hayo kwenye Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji, (EWURA), ili kupitiwa na kufanyiwa taftishi, (kupata maoni ya wadau), ikiwa ni pamoja na Baraza la Ushauri la Serikali . Hivyo basi ikiwa bei za umeme   zitapanda au kutopanda, hiyo itategemea na mapitio ya tathmini ya gharama za kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme tulizowasilisha EWURA.

TANESCO haiwezi kuamua yenyewe kupandisha au kutopandisha bei za umeme. Kwamujibu wa sheria, EWURA inapaswa ifanye mapitio ya bei za umeme kwa kila robo mwaka (Periodic Tariff Adjustment).

Tunapenda Umma ufahamu kuwa kupanda au kushuka kwa gharama za umeme ni suala la kisheria na nijambo la kawaida kwani bei ya umeme imeshawahi kushuka katika vipindi tofauti kwa mfano Mwaka 2015 (roboya kwanza yamwaka) bei ilishuka kwa asilimia 2.5. Vivyo hivyo Mwezi Aprili mwaka 2016 pia gharama za umeme zilishuka kwa asilimia 1.6

IMETOLEWA NA:  
Mhandisi FELCHESMI MRAMBA
Mkurugenzi Mtendaji
Shirika La Umeme Tanzania, (TANESCO)

Undani wa Kifo cha Mzee Joseph Mungai

$
0
0
Mwanasiasa mkongwe na waziri wa zamani wa Serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne, Joseph Mungai, amefariki dunia.

Mungai aliyezaliwa Oktoba 24,1943 alifariki dunia   Dar es Saalam  jana baada ya kuugua kwa muda mfupi.
 
Akisimulia mazingira ya kifo cha baba yake, mtoto wa marehemu, William Mungai, jana alisema baba yake alifariki dunia wakati akipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.

Alisema kabla ya kifo hicho baba yake alianza kulalamika kuumwa na tumbo na kutapika ambako alipelekwa katika hospitali moja ambayo hakutaka kuitaja.

Alisema baada ya kufikishwa hospitalini hapo, hali yake ilizidi kubadilika na kuwa mbaya zaidi na hivyo wakaamua kumkimbiza Muhimbili kwa matibabu zaidi.

“Ni kweli baba amefariki dunia saa 10 jioni leo (jana) wakati tukimpeleka Muhimbili baada ya kulalamika kuumwa na tumbo. Hivi tunavyoongea, ndiyo tunatoka Muhimbili ila taarifa zaidi tutawapatia baada ya kikao cha ndugu,” alisema William kwa kifupi.

Ingawa William hakutaka kuzungumzia kifo hicho kwa undani, taarifa zilizopatikana na ambazo hazijathibitishwa, zinasema kiongozi huyo alikunywa kinywaji katika hoteli moja maarufu ya  Dar es Salaam.

Watu walio karibu na familia ya Mungai mameeleza  kuwa, jana mchana Mungai alikuwa katika hoteli hiyo iliyopo Msasani akipata kinywaji kwa kuwa alikuwa na mazoea ya kufika mahali hapo.

“Mzee jana alikuwa katika hoteli hiyo akiendelea na kinywaji akipendacho cha whisky. Inasemekana baada ya kutoka hotelini hapo na kurudi nyumbani kwake, alianza kutapika huku akilalamika kusikia maumivu makali ya tumbo.

“Vijana wake walimpeleka hospitali ya karibu, lakini hali ilizidi kuwa mbaya ndipo familia iliamua kumkimbiza Muhimbili ambako aliaga dunia,” alisema mtoa taarifa huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake.

Mungai  aliwahi kuwa Mbunge wa Mufindi kupitia CCM kwa miaka 35.

Pia amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini enzi za utawala wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na pia katika awamu za pili, tatu na nne.

Baadhi ya nyadhifa alizowahi kushika kwa nyakati tofauti ni uwaziri wa iliyokuwa Wizara ya Elimu na Utamaduni, Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mtoto aliyepandikizwa betri moyoni afariki dunia

$
0
0
Mtoto Happiness Josephat (6) aliyefanyiwa upasuaji wa kupandikiza betri moyoni katika Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), amefariki dunia.

Mama mzazi wa Happiness, Elitruda Malley amesema Happiness alifariki dunia ghafla juzi mchana.

Alisema   Jumapili, mtoto huyo alikuwa mzima na walikwenda kanisani kutoa sadaka ya shukrani kama ishara ya kumshukuru Mungu kwa mambo aliyowatendea na wakarudi nyumbani salama.

“Jana tumeamka vizuri lakini ghafla hali yake ilibadilika akaanza kulalamika kuwa anajisikia vibaya, tukamkimbizia Hospitali ya Selian hapa Arusha lakini tukiwa njiani alifariki dunia,” alisema.

Elitruda alisema kifo cha mwanawe kimemhuzunisha mno na  daima atamkumbuka.

“Alikuwa tayari amesharudi shuleni, alikuwa akiniambia kuwa atasoma kwa bidii ili ndoto yake ya kuwa daktari bingwa itimie aweze kusaidia watu wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali,” alisema.

Hata hivyo, alisema maziko ya Happiness yanatarajiwa kufanyika leo huko Mbulu mkoani Manyara.

Mkurugenzi wa JKCI, ambako Happiness alifanyiwa upasuaji, Profesa Mohamed Janabi amesema taarifa hiyo imemshtua ikizingatiwa mtoto huyo alikuwa anaendelea vizuri.

“Sikuwa na taarifa, nitawasiliana na mama yake   tujue hasa shida gani ilitokea, maana zipo sababu nyingi labda alipita jirani na mitambo ya umeme au simu, hizo ni sehemu hatarishi kwa mtu aliyewekewa betri kwenye moyo,” alisema.

Happiness alifanyiwa upasuaji huo wa historia nchini Julai 15, mwaka huu katika Taasisi ya JKCI wa kuwekewa betri maalumu kwenye moyo ambayo kitaalamu inaitwa ‘pacemaker’.

Kwa mujibu wa madaktari waliokuwa wakimtibia mtoto huyo, wakati alipopekekwa hospitalini hapo, mapigo yake ya moyo yalikuwa 20.

Walisema  hali hiyo kwa mtoto si ya kawaida kwa vile  anapaswa kuwa na wastani wa mapigo 60 hadi 100 kwa umri wake.

Mtoto Happiness alizaliwa na tatizo hilo ambalo mara nyingi hali hiyo huwakumba watu wazima.

Moja ya ndoto za mtoto huyo ambayo alinukuliwa akiisema ni kuwa daktari bingwa wa kutibu magonjwa mbalimbali.

Wabunge Waigomea Serikali.......Wakataa Kupangiwa Mishahara, Posho na Marupurupu

$
0
0
Wabunge  wamegomea hatua ya Serikali kutaka kusimamia posho na marupurupu yao, huku wakitaka suala hilo waendelee kujipangia wenyewe.

Msimamo huo uliotolewa na Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, umetolewa  baada ya Serikali kuwasilishwa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali namba tatu ya mwaka 2016.

Awali Serikali ilitaka suala la stahiki hizo kwa watumishi wa umma liamuliwe na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora.

Akisoma maoni ya Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohammed Mchengerwa, alisema wametoa pendekezo hilo katika  Sheria ya Utumishi wa Umma sura 298    kulinda dhana  ya mgawanyo wa madaraka.

“Tume ya Utumishi wa Bunge na Tume ya Utumishi wa Mahakama zipewe uhuru  kusimamia upangaji wa mishahara, posho na marupurupu mengine,” alisema.

Akizungumzia mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, alisema kifungu cha 18 cha Muswada huo kuhusu muda wa mnufaika   kurejesha mkopo, Mchengerwa alisema kamati inashauri mkopo uwe mwaka mmoja baada ya kumaliza masomo.

Alisema hali hiyo itasaidia kutoa fursa kwa mnufaika kuanza kulipa mkopo wake,   utaratibu ambao hutumika katika nchi nyingine kama Kenya na Zambia.

“Kuhusu wanufaika waliojiajiri kamati inapendekeza kiwango cha kurejesha mkopo kisipungue Sh 100,000 badala ya Sh 120,000 kama Serikali ilivyopendekeza,” alisema Mchengerwa.

Awali, akiwasilisha hotuba ya mabadiliko ya sheria hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju, alisema   kifungu cha 8 cha Sheria hiyo kinaanisha mamlaka ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais (Utumishi) kuwa ni pamoja na kufanya uchunguzi kwa ajili ya kuendeleza ufanisi wa utumishi wa umma.

Alisema Ibara 24 ya Muswada huo inapendekeza kuongeza kifungu kipya cha 9A cha Sheria kinachoweka masharti kuwa Taasisi, Wakala au Tume za Serikali hazitakuwa na mamlaka ya kuidhinisha mishahara na marupurupu kwa watumishi wa taasisi hizo na badala yake kibali kwa ajili hiyo kitatolewa na Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais (Utumishi).

“Marekebisho hayo yanalenga kuwa na mamlaka moja inayoratibu mishahara, posho na marupurupu na watumishi katika taasisi za Serikali na pia kuwianisha mishahara posho na marupurupu mengine kwa watumishi wa taasisi hizo.

“Masharti yaliyopendekezwa hayatatumika. Ibara hiyo imefutwa na kuandikwa upya masharti yanayopendekezwa hayatatumika kwa mishahara, marupurupu na masilahi mengine kwa Bunge,Mahakama, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),Polisi,Magereza,JKT, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Idara ya Usalama wa Taifa ili utaratibu huo kuendelea kama ilivyo sasa katika sheria zinazosimamia taasisi hizo.

“Kifungu cha 20 (1) (c) cha Sheria ya Utumishi wa umma kinaipa Tume ya Utumishi wa Umma mamlaka ya kutunga kanuni kuhusu usaili wa watumishi wa umma unaofanywa na tume hiyo,” alisema Masaju

Awali kifungu cha 8 kilikuwa kinapendekeza kufanyiwa  marekebisho  kumpa mamlaka Katibu Mkuu (Utumishi) kurekebisha na kuwianisha  mishahara, posho na marupurupu mengine kwa watumishi wa umma wakiwamo   wabunge na idara ya mahakama.

Huku ikipendekeza kuongeza kifungu kipya cha 9A kinachozizuia taasisi za umma, wakala, bodi na tume zisirekebishe au kuwianisha mishahara, posho na marupurupu mengine  kwa watumishi.

Sehemu ya tano inapendekeza marekebisho katika Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298 kwa lengo la kutoa tafsiri ya neno “recruitment secretariat”, maneno hayo yametumika katika Sheria lakini hayakuwa yamepewa tafsiri.

Kiama kwa waajiri
Alisema Ibara ya 19 ya Muswada huo, inapendekeza kufuta kifungu cha 20 na 21,ambacho kilikuwa kinaeleza kwa kuwa si rahisi mwajiri kufahamu kama mtumishi anayeajiriwa ni mnufaika wa mkopo.

Kutokana na hali hiyo,alisema Muswada unaainisha kuwa mwajiri atatakiwa kuifahamisha Bodi ya Mikopo ndani ya siku 28,baada ya mwajiriwa huyo mwenye Shahada au Astashahada ili bodi  iangalie kama mwajiriwa huyo ni mnufaika wa mikopo.

“Mwajiri ambaye atashindwa kutekeleza masharti ya kifungu hicho atakuwa anatenda kosa la jinai ambalo adhabu yake ni Sh milioni moja au kifungo cha miezi sita gerezani. Pia inapendekezwa baada ya mnufaika wa mkopo mwajiri atatakiwa kukata asilimia 15 ya mshahara wa mwajiriwa.

“Bodi au mawakala wake wawe na mamlaka ya kukagua kumbukumbuku za waajiriwa kwa lengo la kufuta taarifa zinazohusiana na wanufaika wa mkopo pamoja na kumbukumbu za  waajiriwa kwa lengo la kutafuta taarifa zinazohusiana na wanufaika wa mkopo kwa hatua zao muhimu kuhusu makusanyo wa mikopo,” alisema

AG Masaju alisema kifungu cha 57 cha sheria hiyo, kinaweka masharti kuhusu zuio kwa shughuli za binadamu zinzoathiri ulinzi wa bahari, mito, mabwawa zisifanyike ndani ya mita 60 kutoka kingo za bahari, mito au mabwawa.

Alisema hatua hiyo imekusudiwa kuimarisha ulinzi na usalama wa mazingira ya maeneo husika ya bahari, maziwa na mito na mabwawa.

“Ibara ya 11 ya Muswada inapendekeza kifungu hicho kirekebishwe katika kifungu kidogo cha pili   kuweka mwongozo wa namna ya kupima mita 60 ambako shughuli za  binadamu zimezuiliwa kufanyika.

“Kifungu cha 184 kinaeleza athari na uthamini wa mazingira. Ibara ya 12 inapendekeza kuwa kitendo cha mtu yeyote kushindwa au kukataa kufanya tathimini ya athari za Mazingira kwa mradi unaohitaji tathmini hiyo kufanyika ni kosa la jinai ambalo adhabu yake ni faini isiyopungua Sh milioni tano na isiyozidi Sh bilioni moja au kifungo kisichopungua miaka miwili,” alisema.

Serikali: Ukosefu wa ajira kwa vijana umepungua

$
0
0

Serikali ya Tanzania imesema kwamba kulingana na takwimu inaonesha kuwa  ukosefu wa ajira kwa vijana nchini Tanzania umepungua kwa asilimia mbili, kutoka asilimia 13.7 mwaka 2012 mpaka asilimia 11.7 mwaka huu.

Akizungumza jana bungeni, mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Anthony Mavunde,  alisema licha ya kupungua huko kwa ukosefu wa ajira, serikali imeweka mipango ya kuwawezesha vijana kuwa na wigo mpana wa ajira nchini.

Mhe. Mavunde alisema kuwa kwa takwimu hizo Tanzania ni nchi inayoongoza kwa kutoa ajira kwa vijana wengi zaidi kushinda baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya na Uganda.

Ratiba ya Mazishi ya Spika Mstaafu, Samwel John Sitta

$
0
0
Mwili wa aliyekuwa spika wa bunge,  Samuel Sitta unatarajia kuwasili nchini siku ya Alhamis ukitokea nchini Ujerumani ambapo alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa hiyo imetolewa na Gerald Mongela ambaye ni msemaji wa familia.  

Amesema mara baada ya mwili huo kuwasili nchini utapelekwa nyumbani kwa marehemu Masaki jijini Dar es Salaam na siku ya Ijumaa shughuli za kuaga zitafanyika katika viwanja vya Karimjee kisha kupelekwa bungeni mjini Dodoma.

“Mwili wa mpendwa wetu mheshimiwa Samuel Sitta utawasili na ndege ya Emirates siku ya Alhamis saa tisa na nusu alasiri na baada ya hapo mwili tutauleta hapa nyumbani kwaajili ya kukaa nao na kupumzika kusubiri ratiba ya Ijumaa,”alisema Mongela.

Mazishi ya Marehemu Samwel John Sitta yatafanyika siku ya Jumamosi Urambo mkoani Tabora.

Kisukari Kilisababisha Mke Wangu Wa Ndoa Kunikimbia Na Kuhamia Kwa Jirani Yangu

$
0
0
Kisukari ni  tatizo  linalo wasumbua  watu  wengi  duniani. Ama  kwa  upande  wa  wanaume, tatizo  la  kisukari  huja  na  madhara  mengi. Moja  kati  ya  madhara  yanayo  letwa  na  tatizo  la  kisukari  ni  pamoja  na  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.

Kwa  wanaume  tatizo  la  kisukari  na  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  huenda  sambamba.  Mara  nyingi, ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume  huweza  kuchukuliwa  kama dalili  ya kuwa  na  tatizo  la  kisukari.

Tatizo  hili  huweza  kuja  na  athari nyingine  za  kijamii  na kifamilia. Mfano  wa  athari  hizo  inaweza  kuwa  kukimbiwa  na  mke, mchumba, mpenzi  nakadhalika.

Tunacho  kisa kimoja  cha  kusikitisha  kinacho  muhusu  mwanaume  aliye  kimbiwa  na  mke  wake, na  kisha  mke  huyo  kuhamia  kwa  jirani  yake  kwa  sababu ya  ugonjwa  wa  kisukari.

Kisa  hiki  kinasimuliwa  na  Mchungaji & Mwinjilisti  Daniel  Kulola, alipokuwa  akihubiri  huko  Chamwino, mkoani  Dodoma.

Mchungaji   Daniel  Kulola  anasema

“   Wakati  nakuja  kwenye  basi, mtu  mmoja  akanipigia  simu. Aliokoka  mwaka  97  wakati nahubiri  Shinyanga. Yule  ni  mwalimu  wa  sekondari, sasa  hivi  ni  amepandishwa  cheo, amekuwa  Mratibu wa  Elimu.

 Anasema  ‘ KILA  NIKIFUMBA  MACHO, NAONA  KIFO!  PRESHA  YANGU  IPO  JUU  KULIKO  KAWAIDA, NA  NIMEPIMWA  NIMEKUTWA  NINA  KISUKARI.

KISUKARI  KIMENIFANYA  MKE  WANGU  ANIKIMBIE. AMEENDA  KUOLEWA  NA  JIRANI  YANGU. KWA  HIYO  MKE  WANGU  ANAPITA  MBELE  ZA  MLANGO  WA  NYUMA  YANGU. NA  MWANAUME   MWNGINE  AMBAE  ANA  GARI. MIMI  SINA  GARI

Fikiria maumivu  hayo. Mke  wako  wa  ndoa!, halafu  anapita  mbele  ya  nyumba  yako,kwa  sababu  wewe  ni  masikini, tena  unaumwa ! Umepata  kisukari, na  presha  ni kubwa! Yule  mtu  anasema  am ready  YANI  NINAONA  KIFO  KIPO  MBELE  YANGU…..

Kusikiliza  clip hii, bofya  kwenye  link hii : https://www.youtube.com/watch?v=P5M2WyDR-FE

UHUSIANO  ULIOPO  KATI  YA  KISUKARI  NA  TATIZO  LA  UKOSEFU  NA  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kuna uhusiano  mkubwa  sana  kati  ya  ugonjwa  wa  kisukari  na  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume .  Kufahamu  namna  ugonjwa  wa  kisukari  unavyo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, tembelea : http://www.neemaherbalist.com/2015/07/uhusiano-kati-ya-damu-na-tatizo-la.html


NINI  TIBA  YA  TATIZO  LA  NGUVU  ZA  KIUME  KWA  MWANAUME  MWENYE  KISUKARI.

Kufahamu  kuhusu  tiba  ya  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, kwa  mwanaume  mwenye  tatizo  la  kisukari, tembelea : http://www.neemaherbalist.com/2015/07/uhusiano-kati-ya-ugonjwa-wa-kisukari-na.html

HABARI  HII  IMELETWA KWENU  NA  NEEMA  HERBALIST  BLOG, KWA  UDHAMINI  MKUBWA  WA   NEEMA  HERBALIST &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC, WAUZAJI  WA  DAWA MBALIMBALI  ZA  ASILI  KAMA  VILE :

1. Dawa  asilia ya  kuunganisha  mifupa, pingili  na kukomaza mifupa.

2.Dawa  asilia ya kuondoa  maumivu ya  misuli, kurekebisha  mishipa  na  misuli

3.Dawa  asilia  kwa  wagonjwa wa  kiharusi (Kupooza)

4.Dawa  asilia ya  kutibu  majeraha

5.Dawa  asilia  ya  kutibu  vidonda ndugu

6.Dawa asilia  ya  kuondoa  uchovu na  kuwashwa

7.Dawa  asilia  ya  kuondoa mafuta  kwenye damu ( kolestrol /lehemu)

8.Dawa  asilia  ya  kutibu tatizo  la  nyongo

9.Dawa  asilia  ya  kutibu  gauti

10.Dawa  asilia  ya  uzazi  wa  mpango

11.Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  Goita

12.Dawa asilia ya  kutibu  tatizo  la  change  la watoto wachanga.

13.Dawa  asilia  ya kutibu  vidonda  vya  tumbo

14.Dawa  asilia  ya  kutibu mzio     ( Allergy)

15.Dawa asilia  ya  kutibu  tatizo  la  degedege  kwa watoto  wenye  umri  wa  kati  ya  miezi  6  hadi  tisa.

16.Dawa asilia  ya  kurutubisha  mayai  ya  uzazi  na  kuzibua  mirija  ya  uzazi  kwa  wanawake.

17.Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  utasa  kwa  wanaume.

18. Dawa  asilia  ya  kusaidia  kugeuza  mtoto  aliye  kaa  vibaya  tumboni ( Mfano: Katanguliza mikono, makalio n.k )

19.Dawa  asilia  ya kupunguza  kitambi, uzito  na  unene  uliozidi.

20.Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  vinyama  vya  puani.

21.Dawa asilia  ya  kutibu  tatizo  la  bawaziri.

22.Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  uchungu  wa  pili  baada  ya  kujifungua.

23.Dawa  asilia  ya  kutibu  majeraha ya moto  pamoja na  makovu yatokanayo  na  moyo.

24.Dawa  asilia  ya  kutiu  tatizo  la  kwikwi

25.Dawa asilia  ya  kutibu  tatizo  la  kutokwa  na  harufu  mbaya  kinywani

26.Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  kutoa harufu  mbaya mwilini

27.Dawa  asilia  ya  kusaidia  kunenepesha  mtu  aliye  dhoofu  mwili

28.Dawa  asilia ya kutibu  tatizo  la  uvimbe  wa  tumboni  ( FIBROID )

29.Dawa  asilia  ya  kisukari

30.Dawa  asilia  kwa  watu  wenye  tatizo  la  moyo, presha  ya  kupanda, presha ya  kushuka, moyo  kupanuka  na  matundu  kwenye moyo.

31.Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  U.T.I, kaswende, kisonono sugu  na  Taifodi.

32.Dawa  asilia  ya  kutibu  magonjwa  mbalimbali ya  ngozi

33.Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo la  kubanwa mkojo na  maumivu  kwenye  njia  ya  mkojo

34.Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  kujikojolea

35.Dawa  asilia  ya  kusafisha  figo  na  kibofu  cha  mkojo

36.Dawa  asilia  ya  kuondoa  sumu  mwilini

37.Dawa asilia  ya  kuondoa  maumivu  ya  hedhi

38.Dawa  asilia  za  kuondoa  sumu  ya  nyoka, na  nge.

39.Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  pumu

40.Dawa  asilia  ya  kuyeyusha uvimbe  kwenye  lango  la  uzazi.

41.Dawa asilia ya kutibu  malaria  sugu

42.Dawa  asilia  ya kutibu  tatizo  la  upara 

43.Dawa  asilia ya  kutibu  tatizo la  kikohozi sugu  na  kimeo.

44. Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  ngiri

45. Mawe  kwenye  figo

46.Kukosa  choo

47.Kukosa  hamu  ya  kula

48.Chango  la  kike

49.Kutanua  nyonga ( Kuzaa  bila  kupasuliwa )

50.Nguvu za  kiume

51.Hamu  ya tendo  la  ndoa  kwa  wanawake.

52.Mtoto kuchelewa  kutembea

DAWA   ZOTE  HIZI  NI  ZA  ASILIA KABISA  NA  HAZINA   KEMIKALI ZA  VIWANDANI.

Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR ES  SALAAM, jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING, nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO PLAZA.

Kwa  wateja  waliopo  Dar  Es  Salaam, ambao  hawana  nafasi  ya  kufika  ofisini  kwetu, watapelekewa  dawa  mahali  popote  walipo.

Kwa  wateja  waliopo  mikoani, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  mabasi.

Kwa wateja  waliopo  Zanzibar, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  boti.

Kwa wateja  waliopo Mombasa, watatumiwa  dawa  kupitia  basi  la  TAHMEED.

Kwa  wateja waliopo  jijini  Nairobi, watatumiwa  dawa  kupitia  basi  la  DAR  EXRESS.

Na kwa  wateja  waliopo  ughaibuni, watatumiwa  dawa  kwa  njia ya  POSTA  au  DHL.

WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA:

0766 – 53 83  84.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu huduma zetu, tutembelee  kila  siku, kupitia :


Rais Magufuli Ampongeza Donald Trump Kwa Kushinda Kiti cha Urais Wa Marekani

$
0
0

Leo November 9, 2016 Marekani imeweka historia nyingine baada Donald Trump wa chama cha Republican kutangazwa mshindi wa kiti cha Urais, na tayari ameanza kupokea pongezi kutoka kwa viongozi wa nchi mbalimbali ikiwemo Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Rais Magufuli ametoa pongezi zake kwa Rais Donald Trump kupitia ukurasa wake Twitter

Breaking News: Donald Trump Ndo Mshindi wa Kiti cha Urais wa Marekani

$
0
0
Mgombea wa Chama cha Republican, Donald Trump ameshinda uchaguzi mkuu wa Marekani baada ya kufikisha kura 276 huku Hillary Clinton akiwa na kura 218.

Hillary Clinton amempigia simu Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump na kumpongeza kufuatia ushindia huo alioupata.

Akizungumza na wafuasi wake baada ya kutangazwa mshindi, Trump amewataka raia wote wa Marekani, waliomchagua na ambao hawakumchagua kuungana na kuanza kuijenga nchi yao kwani muda wa kampeni na siasa za kugawanyika umekwisha.



    Msajili wa vyama vya siasa Tanzania, avifutia usajili Vyama Vitatu

    $
    0
    0
    Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania Jaji Francis Mutungi ametangaza kuvifutia usajili vyama vitatu baada ya kubainika kukiuka sheria ya usajili wa vyama.

    Vyama hivyo ni pamoja na CHAUSTA kilichopata usajili wa kudumu tarehe 5 Novemba 2001, The African Progressive Party of Tanzania ( APPT-Maendeleo) kilichopata usajili wa kudumu terehe 4 Machi 2003 na Chama cha Jahazi Asilia kilichopata usajili wa kudumu tarehe 17 Novemba 2004.

    Jaji Mutungi amesema kuwa mchakato wa kufuta usajili wa vyama hivyo umetokana na zoezi la uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa mengine ya sheria ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu lililofanyika kuanzia tarehe 26 Juni hadi 26 Julai 2016.

    Amesema katika zoezi hilo uhakiki ulibaini kuwa vyama hivyo vimepoteza sifa za usajili wa kudumu kwa kukiuka masharti ya sheria ya vyama vya siasa, na kwamba kila chama kilipewa ya nia ya msajili kufuta usajili wake, lakini vikashindwa kutoa utetezi wa kuridhisha ili visifutiwe usajili.

    Kufuatia uamuzi huo, Msajili amewataka waliokuwa wanachama wote wa vyama hivyo kutojiuhusisha na shughuli yoyote kwa majina ya vyama hivyo, na kwamba kufanya hivyo ni kuvunja sheria, huku akiviasa vyama vingine kuendesha shughuli zao kwa kuzingatia sheria.

    Rais Barack Obama ampongeza Rais Mteule, Donald Trump na kumualika Ikulu kujadiliana juu makabidhiano ya ofisi.

    $
    0
    0
    Rais Barack Obama wa Marekani  amempongeza Rais Mteule wa taifa hilo, Donald Trump na kumualika Ikulu kujadiliana juu makabidhiano ya ofisi.

    Treni Yanusurika Kuchomwa Moto na Wananchi....Vioo 30 vya Mabehewa Vyapasuliwa, 17 Watiwa Mbaroni

    $
    0
    0
    TRENI ya abiria  inayofanya safari zake kati ya Kituo Kikuu  cha Reli na maeneo ya Pugu  Dar es Salaam maarufu kama ‘Treni ya Mwakyembe’ nusura ichomwe moto juzi, baada ya wananchi   kudai kuchoshwa na usumbufu wa shirika hilo.

    Wananchi hao walitaka warudishiwe nauli zao  kwa kile walichodai Shirika   la Reli Tanzania (TRL)  limeshindwa kuwa na ratiba inayoeleweka.

    Tukio hilo lilitokea juzi  saa 3:00 usiku eneo la Majumbasita, baada ya treni hiyo kukaa kituoni hapo kwa muda mrefu bila kuambiwa kuambiwa chochote.

    Hali hiyo iliwafanya abiria  kuvamia kituo kidogo cha mawasiliano kilichopo eneo hilo wakitaka warejeshewe  nauli zao vinginevyo wangekichoma moto pamoja na mabehewa ya treni hiyo.

    Mwandishi aliwashuhudia abiria   wakitaka kuingia ndani ya kituo hicho huku wakiwalazimisha wafanyakazi waliokuwapo wawarudishie fedha zao za nauli.

    Purukushani hiyo iliyodumu kwa takribani saa  mbili  ilimalizika kwa abiria hao kuvunja vioo vya mabahewa ya treni vipatavyo 30.

    Wafanyakazi kuona hivyo walijifungia ndani ya kituo hicho  huku  polisi  waliokuwa wakisindikiza treni hiyo  wakitimua mbio   kunusuru  maisha yao.

    Baadhi ya abiria walisema   tangu Ijumaa   iliyopita wamekuwa wakipata usumbufu kwa kukatishiwa tiketi huku treni  ikichelewa na wakati mwingine kutoonekana  kabisa.

    Walisema  jambo hilo  limekuwa likiwasababishia hasara na kuwalazimu  kutafuta usafiri mwingine na   kuchelewa kufika  kwenye  majukumu yao.

    Kufuatia kukithiri vitendo vya uharibifu wa miundombinu ya reli na treni vinavyofanywa na baadhi ya wananchi, Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kupitia  kwa Mkurugenzi Mtendaji , Masanja Kadogosa imetoa onyo kwa wananchi kutofanya vitendo hivyo.

    “Tukio hili si mara ya kwanza kujitokeza, lilijitokeza tarehe 24, 26 na 28 mwezi wa 10 na Novemba 7 Katika matukio hayo kulitokea uharibifu wa miundombonu na kujeruhi baadhi ya wafanyakazi wa TRL akiwemo Mustapha Omary ambaye ameshonwa nyuzi 8 katika hospitali ya mnazi mmoja,” amesema.

    Amesema kutokana na uharibifu huo, watuhumiwa 17 wanashikiliwa na jeshi la polisi na kwamba upepelezi ukikamilika watachukuliwa hatua za kisheria.

    Kadogosa amedai kuwa, wahusika wa fujo na uharibifu huo ni makondakta wa dalala kwa lengo la kutisha wananchi kutoutumia usafiri wa treni.

    “Kuna watu wa daladala wanafikiri wataendelea kufanya fujo ili wananchi waone kuwa usafiri wa treni si salama wapande magari yao, sisi hatulazimishi wananchi kuutumia usafiri wetu ila kutokana na ubora wa huduma zetu wanakuja wenyewe. Pia hatusitishi kutoa huduma kwa sababu ya fujo zao sababu tutawatesa abiria wetu zaidi ya 21,000,”


    Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Reli, Simon Chillery amesema jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini wengine waliohusika.
     
    Viewing all 45270 articles
    Browse latest View live




    Latest Images