Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Agizo la Serikali kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha sita mwezi Mei mwaka huu Ambao Hawakujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)

$
0
0
Serikali amewaagiza wote waliohitimu kidato cha sita Mei mwaka huu na ambao hawajajiunga na vyuo vya elimu ya juu, wakaripoti katika kambi za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Desemba Mosi, mwaka huu.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi ametoa agizo hilo mjini Dodoma alipozungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Habari wa Bunge.

Dk Mwinyi alisema Mei na Juni mwaka huu, JKT iliwafanyia usaili vijana wa kujiunga na JKT kwa kujitolea. Alisema usaili huo ulifanyika kwa kushirikiana na kamati za ulinzi za wilaya na mikoa.

“Wizara ya Ulinzi na JKT inapenda kuwatangazia vijana wote waliosailiwa Juni mwaka huu, kujiunga na JKT kwa kujitolea, waripoti kwenye kambi walizopangiwa ifikapo Desemba Mosi mwaka huu kwa nauli zao,” amesema Dk Mwinyi.

Dk Mwinyi amesema mafunzo hayo ni ya miezi mitatu kwa mafunzo yenye utaratibu wa kawaida na miaka miwili kwa wa kujitolea.

Ili kufanikisha hilo, Wizara ilimuagiza Mkuu wa JKT kufufua kambi ya Makuyuni JKT iwe miongoni mwa kambi kuanzia Desemba mwaka huu.

Aliagiza kambi za Luwa na Milundikwa za mkoani Rukwa, zirejeshwe kwa shughuli za JKT za kilimo na ufugaji.

Dk Mwinyi alimuagiza Mkuu huyo wa JKT pia kambi ya Mpwapwa irejeshwe kwa ajili ya kuendesha mafunzo ya kilimo na ufugaji ndani ya JKT.

Mshindi Wa Milioni Mia Moja Za Vodacom M-pawa Akabidhiwa Kitita Chache

$
0
0
Pichani ni Bi Paulina Kulwa (Kulia) akikabidhiwa hundi ya mfano wa Tsh Milioni 100 baada ya kuibuka mshindi katika promosheni ya Jiongeze na M-Pawa
Hapa kazi tu ni kaulimbiu inayohamasisha watu kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia fursa mbalimbali zilizopo, usemi huu umetimia kwa Mama Paulina Kulwa mkazi wa Mwanza baada ya kukabidhiwa kitita cha shilingi milioni mia moja kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya CBA.

Paulina alikabidhiwa hundi hiyo katika ofisi za Vodacom jijini mwanza na Meneja Masoko na huduma za Kifedha Vodacom Tanzania, Noel Mazoya na kusema lengo la kuanzisha huduma hii ni kuwasaidia Watanzania kuwa na utamaduni wa kuweka akiba.
 
Aidha, Bi Kulwa baada ya kukabidhiwa hundi alisema “Namshukuru Mungu na Vodacom kuanzisha huduma hii maana tayari imenifanya kuwa milionea na kuanzisha ajira kwa Watanzania wengine, lakini pia watoto wangu wanaenda shule na nina nyumba”

Naye Mkuu wa kitengo cha masoko Benki ya CBA, Solomon Kawishe alishukuru ushirikiano kati ya Benki yake na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania kwa kuleta neema kwa Watanzania. 
Bi Paulina Kulwa (Kulia) akiwa na pacha wake katika duka la Vodacom City Mall jijini Mwanza katika hafla ya kumpongeza na kumkabidhi hundi baada ya kuibuka mshindi katika promosheni ya Jiongeze na M-Pawa
Mshindi wa Jiongeze na Mpawa akiwa na maafisa toka Vodacom na CBA katika hafla fupi ya kumkabidhi mfano wa hundi na kumpongeza. Toka kushoto ni Ayubu Kalufya Mkuu wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Meneja Masoko wa huduma za Kifedha wa Vodacom Noel Mazoya, mshindi wa milioni 100 Bi Paulina Kulwa, Solomoni Kawiche Mkuu wa masoko - CBA na Eric Luyangi Mkuu wa MPawa - CBA

Dili Lingine Kutoka Tecno...Nunua Simu Ya Phantom 6 Au 6+ Ushinde Vocha Za Chakula

$
0
0
Tecno hawaishi kukuletea dili bomba kila kunapokucha ambapo safari hii kwa kushirikiana na Jumia wamepania kuhakikisha huduma kwa wateja wao zinakuwa bora zaidi na wanafurahia kuwa wateja wa bidhaa za kampuni hizi mbili kwa muda mrefu. 

Uboreshwaji huu wa huduma unalenga katika ubora na urahisishaji wa kutumia huduma na bidhaa za kampuni hizi hasa kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka wenye sikukuu ya Christmas na mwaka mpya.

Wateja watafaidika kwa njia mbaimbali kupitia ushiriano huu kuanzia kwenye huduma mpaka zawadi mbalimbali zitakazotolewa. 

Wateja watakaonunua simu mpya za PHANTOM 6 na PHANTOM 6 Plus watapata kuponi zitakazowawezesha kuagiza chakula popote ambapo kampuni ya Jumia inafanya kazi .Utaratibu huu umeanza rasmi 1/11/2016 ambapo pia wateja wa Jumia watakapoagiza chakula kupitia programu (Application) inayopatikana katika mfumo wa android watapata nafasi ya kushinda simu ya PHANTOM 6 na zawadi zingine kemkem zitakazo tolewa na kampuni ya JUMIA kwa hisani ya TECNO MOBILE LIMITED
Katika mwezi Novemba na Desemba kuna nafasi kubwa kwa wateja wa kampunia hizi mbili kufurahia ofa kabambe, nunua simu za TECNO PHANTOM 6 katika maduka yote yaliyopo nchini kote upate kujishindia zawadi kutoka JUMIA na TECNO MOBILE LIMITED. Usikose Fursa Hii!
 
Tembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya Tecno kufahamu zaidi kuhusiana na Tecno Phantom 6 na Phantom 6 Plus.
 
 
 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Aongoza Wabunge Kuaga Mwili Wa Mbunge Wa Dimani- Hafid Hally Tahir

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza wabunge kuuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Dimani, Zanzibar Mheshimiwa Hafidh Ally Tahir.

Bw. Tahir amefariki saa 9 alfajiri ya kuamkia leo katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na mwili wake kuagwa katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kabla ya kusafirishwa kwenda Zanzibar kwa mazishi.

Akizungumza katika tukio hilo, Waziri Mkuu ametoa pole kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, familia ya marehemu na wabunge wote.“Tumepokea taarifa za msiba huu kwa mshtuko mkubwa. Leo tupo katika wakati mgumu sana. Tumeondokewa na viongozi wengi,” amesema.

Amesema wafiwa wanatakiwa kuishi kwa upendo. “Tumuombee marehemu, tuiombee familia iwe na moyo wa utulivu katika kipindi kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.”

Bw. Hafidh alizaliwa Oktoba 30, 1953 na aliwahi kuwa Mkuu wa Sauti ya Tanzania Zanzibar (1970-1978) na amekuwa mbunge tangu 2005 hadi mauti yanamkuta.Enzi ya uhai wake, alishiriki kikamilifu katika masuala ya michezo; alikuwa mwamuzi wa soka mwenye beji ya FIFA na kocha msaidiizi wa timu ya soka ya Bunge.

Hadi jana, Bw. Hafidh alishiriki katika shughuli mbalimbali ikiwemo uchaguzi wa kupata viongozi wa Tawi la Umoja wa Wabunge WanaYanga mjini Dodoma ambapo yeye alichaguliwa kuwa Katibu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA, NOVEMBA 11, 2016.

Mke Wa Rais Mama Janeth Magufuli Aruhusiwa Kutoka Hospitali ......Awashukuru Madaktari

$
0
0
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli aliyekuwa amelazwa katika wodi ya Sewahaji ya Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam ameruhusiwa na kurejea nyumbani leo tarehe 11 Novemba, 2016 baada ya afya yake kuimarika.

Kabla ya kuondoka katika wodi ya Sewahaji alikokuwa amelazwa Mama Janeth Magufuli amewashukuru Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu mazuri aliyoyapata na pia amewashukuru Watanzania wote kwa kumuombea afya njema.

"Namshukuru sana Mungu kwamba afya yangu imeimarika, pia napenda kuwashukuru Madaktari na Wauguzi, nimepata huduma nzuri sana maana siku nilipoletwa hapa nilikuwa sina fahamu na hali yangu ilikuwa mbaya lakini mmenipigania na leo narudi nyumbani nikiwa na afya imara.

"Naomba pia niwashukuru Watanzania wote kwa kuniombea, nawahakikishie kuwa sasa nipo vizuri na madaktari wameniruhusu nirudi nyumbani ambako nitamalizia matibabu yangu" amesema Mama Janeth Magufuli.

Mama Janeth Magufuli alilazwa hospitalini hapo tangu Juzi tarehe 09 Novemba, 2016 baada ya kuugua ghafla na kupoteza fahamu.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
11 Novemba, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya Novemba 12

Tazama Video Mpya ya Wimbo wa Rosa Ree Kutoka The Industry iliyoko Chini ya Nahreel

$
0
0
Rapper Mkali wa Kike kutoka Tanzania Rosa Ree Aliyoko chini ya lebo ya Mziki ya The Industry jana ameachia Rasmi wimbo wake wa Kwanza unaoitwa One Time, Nimekuwekea Link ya Kudownload Wimbo Huo Hapa chini na Video:

DOWNLOAD AUDIO HERE
 

Godbless Lema Arudishwa Rumande Baada ya Kunyimwa Dhamana Kwa Mara ya Pili

$
0
0
Ujanja wa kisheria uliosababisha mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kukaa mahakamani kwa saa 10, umemfanya kada huyo wa Chadema kukosa tena dhamana. 

Jana, Mahakama ya Hakimu Mkazi ilishatupilia mbali hoja za Serikali za kupinga dhamana ya mbunge huyo, lakini mawakili walitumia silaha nyingine ya kukata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa kumpa dhamana Lema.

Mawakili wa Serikali walifanya hivyo muda mfupi baada ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Desderi Kamugisha kutupa hoja za kuzuia dhamana ya Lema na hivyo kumzuia hakimu kuendelea na utaratibu wa kumwachia mbunge huyo kusubiri uamuzi wa rufaa hiyo, hali iliyoibua vilio mahakamani.

Kutokana na maamuzi hayo, hatma ya Lema kupata dhamana inasubiri Mahakama Kuu kupanga jaji wa kusikiliza shauri hilo.

Lema, ambaye alifikishwa mahakamani saa 2:00 asubuhi, alirudishwa mahabusu akiwa kwenye basi la magereza lililokuwa na ulinzi mkali saa 11:00 jioni.

Katika uamuzi wake uliotupilia hoja za awali za Serikali kupinga dhamana, Hakimu Kamugisha alisoma maamuzi kwa saa 2:35 na kutoa dhamana kwa Lema.

Hakimu Kamugisha alisema upande wa mashtaka uliwasilisha hoja tatu za kupinga dhamana ya Lema katika kesi za uchochezi namba 440 na 441/2016 na hati ya kiapo ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha(RCO).

Alisema hoja ni kuwa mshtakiwa ametenda makosa hayo, wakati akiwa nje kwa dhamana kwa kesi namba 351 na 352 za mwaka 2016, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Hakimu Kamugisha alisema hoja nyingine ni kutaka Lema anyimwe dhamana kwa ajili ya kulinda usalama wake, hasa kwa kuwa kauli zake za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli zimewaudhi wananchi.

Hoja ya tatu kujali maslahi ya Taifa. Hoja hizo ziliandamana na hati hiyo ya kiapo cha RCO.

Hata hivyo, hakimu alisema mawakili wa utetezi waliokuwa wanaongozwa na John Mallya walipinga hoja hizo, wakisema dhamana ni haki ya mshitakiwa na kuwa nje kwa dhamana katika mashauri mengine ambayo hayajamtia hatiani mtuhumiwa, hayawezi kuwa sababu ya kumnyima dhamana.

Alisema mawakili hao, pia walipinga hoja za kutokutolewa dhamana kutokana na usalama wake na maslahi ya Jamhuri na pia wakakosoa hati ya kiapo kuwa ina mapungufu, hasa ya kutokuwa na uthibitisho wa mambo yaliyoelezwa.

Hakimu Kamugisha alisema msingi wa haki ya dhamana ni wa Katiba ibara ya 15(1) na (2) ambayo inaelezea uhuru wa mtu.

Alisema pia ibara ya 17 ya Katiba inatoa haki ya mtu kutembea popote na kuongeza ibara ya 16(6) B inaeleza mahakama inamchukulia mtuhumiwa yeyote kuwa hajafanya kosa hadi anakapotiwa hatiani.

Alisema washitakiwa hupelekwa mahabusu ili iwe lazima mtuhumiwa kufika mahakamani.

Hakimu Kamugisha alisema, siku zote dhamana haitolewi ikiwa tu kuna mazingira ya kisheria ambayo yameelezwa na kuwekewa masharti na utaratibu wake.

Alitolea mfano kesi ya Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP) dhidi ya Daudi Beda ambapo ilielezwa haki za mshtakiwa na sababu ambazo zinaweza kuzuia dhamana.

Alisema katika kesi hiyo, mahakama iliamua kuwa ili kunyimwa dhamana lazima kuwepo mazingira yaliyoanishwa kisheria na utaratibu ulioanishwa kisheria.

“Nimeshindwa kupata kifungu chochote cha sheria ambacho kinazuia kutoa dhamana kwa mtuhumiwa aliye nje kwa dhamana ambaye ametenda makosa mengine ambayo hayahusiani na masharti ya dhamana ya awali,”alisema.

Alisema hata maelezo kuwa watu waliohudhuria mkutano hawakuridhishwa na kauli za Lema na kwenda kulalamika kwa RCO, hayana panapoonyesha usalama wa mtuhumiwa upo mashakani.

Alisema ili hoja ya dhamana izuiwe kwa maslahi ya Jamhuri, inakuwa na hati ya maombi hayo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP) na si RCO hivyo haoni msingi wa kutotoa dhamana hiyo “Hivyo kwa uchambuzi huu wa kisheria natoa dhamana kwa mshitakiwa,” alisema.

Hata hivyo, wakati anajiandaa kuandika masharti ya dhamana, ndipo wakili mwandamizi wa Serikali, Paul Kadoshi aliwasilisha notisi za kupinga uamuzi wa dhamana hiyo.

Alisema anawasilisha notisi hiyo chini ya kifungu cha 379 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 20 ya mwaka 2002.

Alisema nia ya kuwasilisha notisi hiyo inatokana na mabadiliko ya Sheria za Makosa ya Jinai namba 27 ya mwaka 2008.

Alisema kifungu cha 31 aya G katika sheria hiyo kifungu 379(1 ) (a) kwa kuongeza maneno kuwa notisi ya kukata rufaa inaweza kujulikana kama ni rufaa.

Alisema mabadiliko ya sheria hiyo yalimpa hadhi DPP anapoeleza notisi ya rufani kuwa tayari ni rufani kamili na hivyo notisi hiyo ikitolewa mwenendo wa kesi nzima unapaswa kusimama.

Kadoshi alisema maamuzi hayo, yamefikiwa katika kesi ya Jamhuri dhidi ya Harry Kitillya na wenzake wawili, pale DPP alipowasilisha notisi na rufani na kesi kusimama.

Hata hivyo, licha ya mawakili wa utetezi, Sheki Mfinanga na Richard Shediel kupinga hoja hiyo, Haklimu Kamugisha, ambaye aliomba dakika 10 kutafakari suala hilo, alikubaliana na hoja za upande wa Serikali za kumkatalia Lema dhamana.

Kutokana na maamuzi hayo Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu amesema chama hicho kimewataka wanasheria wake, Tundu Lissu na Peter Kibatala kwenda Arusha kuongeza nguvu katika kudai haki ya Lema kuwa huru.

Mke wa Lema, Neema Lema aliwataka wakazi wa Arusha kuwa watulivu, akisema mbunge huyo anapigania uhuru wa wananchi.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya Novemba 13

Hotuba ya Waziri Mkuu ya kuahirisha mkutano wa tano wa Bunge la 11 Novemba 11

$
0
0
1. Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naomba kutumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutulinda na kutufikisha salama siku ya leo tunapohitimisha Mkutano wa Tano wa Bunge lako Tukufu tuliouanza tarehe 1 Novemba, 2016.
2. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii pia kukupa pole, kwa msiba mzito uliotokea tarehe 7 Novemba, 2016 ambao Bunge lako tukufu, Serikali na Taifa tumepata kwa kumpoteza Mheshimiwa Samwel Sitta, mmoja wa Viongozi mahiri wa Bunge hili katika historia ya nchi yetu. Msiba uliotupata wa aliyekuwa Spika Mstaafu wa Bunge la Tisa (2005-2010) na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Urambo Mkoani Tabora ni pigo kwa Taifa letu. Nasi Wabunge kwa kuwawakilisha Watanzania leo hii muda mfupi ujao tutaaga mwili wa kipenzi chetu Mheshimiwa Samuel Sitta. Tunamwomba Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema Peponi. Amina.

3. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kutoa pole kwa mjane wa marehemu, Mheshimiwa Margareth Simwanza Sitta, Mbunge mwenzetu, watoto wake na wanafamilia wote na marafiki wote kwa ujumla kutokana na msiba mzito uliowapata. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape subira katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na siku zote wamtangulize Mwenyezi Mungu katika kuwaongoza wanafamilia waliobakia.

Sina budi kukiri kuwa Taifa limempoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika uongozi na maendeleo. Enzi za uhai wake, Marehemu Mheshimiwa Sitta, alibahatika kufanya kazi na Marais wa awamu zote nne zilizopita tangu ya kwanza ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, akiwa Mbunge kwa miaka 30. Alikuwa ni Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nyadhifa nyingine alizowahi kushika ni pamoja na Mkuu wa Mikoa ya Iringa na Kilimanjaro, Waziri wa Ujenzi, Waziri aliyesimamia Ustawishaji Makao Makuu, Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa Afrika Mashariki, Waziri wa Uchukuzi na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba.

4. Mheshimiwa Spika, tarehe 8 Novemba, 2016 tumeondokewa tena na Kiongozi wa muda mrefu Serikalini Ndugu Joseph Mungai. Kiongozi huyu ameshika nafasi mbalimbali katika utumishi wa umma ikiwemo Ubunge na Uwaziri.

5. Mheshimiwa Spika, tangu tulipokutana mara ya mwisho, pametokea majanga mbalimbali yakiwemo maradhi, ajali, na matukio mengine ambayo yamesababisha vifo na majeruhi kwa Watanzania wenzetu. Sote tunakumbuka tukio la kusikitisha la watumishi wa Serikali waliopoteza maisha wakiwa kazini walipovamiwa na wanakijiji wa Makang’wa wilayani Chamwino mkoani Dodoma. Nalaani mauaji hayo na kuvitaka vyombo vya usalama kuwachukulia hatua wote waliohusika. Vilevile, katika miezi ya Oktoba na Novemba, kumetokea ajali za barabarani katika Mikoa ya Mbeya, Pwani, Singida, Lindi, Iringa, na ile iliyopoteza ndugu zetu 19 mkoani Shinyanga na kwingineko ambako ndugu zetu walipoteza maisha. Ninatoa pole kwa wafiwa wote na wale wote waliopatwa na majanga kutokana na matukio hayo. Tunawaombea afya njema wale waliopata majeraha na waliopo hospitali. Pia niendelee kuwataka Askari wa usalama barabarani kuhakikisha wanasimamia madereva na watumiaji wa Barabara kuzingatia Sheria za usalama wa barabarani.

6. Mheshimiwa Spika, leo tunahitimisha Mkutano huu wa Tano tukiwa tumekamilisha shughuli zote zilizopangwa. Naomba nitumie fursa hii kukupongeza wewe Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wenyeviti wa Bunge na Waheshimiwa Wabunge wote kwa kukamilisha kazi zote kwa ufanisi mkubwa. Nawapongeza sana!

SHUGHULI ZA BUNGE

7. Mheshimiwa Spika, katika mkutano huu tumepata fursa ya kujadili, kupokea na kushauri kuhusu mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na muongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/2018. Aidha, katika kipindi hiki, tumejadili Hoja mbalimbali za Serikali ikiwemo Miswada, Taarifa za Kamati, Mkataba wa EPA, Maazimio na Kauli mbalimbali za Mawaziri. Vilevile, Wabunge walipata majibu ya maswali mbalimbali ya msingi na ya nyongeza yaliyoulizwa na Waheshimiwa Wabunge na maswali ya Papo kwa Papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu.

8. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kumshukuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali, pamoja na Wataalam wake, kwa kazi kubwa ya kuandaa miswada mbalimbali iliyowasilishwa katika Bunge lako Tukufu. Aidha, napenda kutumia fursa hii kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa michango yao mizuri. Serikali itazingatia ushauri na maoni yenu wakati wa utekelezaji.

MAAZIMIO
9. Mheshimiwa Spika, katika mkutano huu, Waheshimiwa Wabunge wamepata fursa ya kupokea na kujadili Mkataba wa Ubia wa Uchumi baina ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya yaani East Africa Community – European Union Economic Partnership Agreement. Napenda kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa michango yenu mizuri tuliyoipata wakati wa mjadala wa Mkataba huo. Serikali itafanyia kazi maoni, ushauri na uamuzi wenu kuhusu Mkataba huo.

JUHUDI ZA SERIKALI ZA KUWAHUDUMIA WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA

10. Mheshimiwa Spika, mtakumbuka kuwa mnamo tarehe 10 Septemba, 2016 lilitokea tetemeko la ardhi katika eneo la Kanda ya Ziwa na hususan Mkoa wa Kagera. Tetemeko hilo lilisababisha athari mbalimbali zikiwemo vifo, majeruhi, uharibifu wa makazi na miundombinu ya umma na watu binafsi. Jumla ya Watu 117,721 wameathirika kwa kupoteza makazi yao, mali na athari za kisaikolojia katika Wilaya za Bukoba, Missenyi, Muleba, Karagwe na Kyerwa. Aidha, jumla ya watu 17 walipoteza maisha na 560 walijeruhiwa. Vilevile, nyumba 2,072 za makazi zilianguka kabisa na nyumba 14,595 za makazi zilibomoka, baadhi zina kuta au kupata nyufa kubwa na hivyo kuzifanya kuwa hatarishi kwa makazi ya binadamu. Vilevile, maafa haya yalisababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara na majengo ya Serikali 1,718 yaliyoharibika kwa viwango tofauti.

11. Mheshimiwa Spika, kufuatia hali hiyo, Serikali ilianzisha Kituo cha Operesheni na Kuratibu Maafa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera kwa lengo la kuharakisha huduma. Aidha, Serikali ilitoa matibabu bure kwa majeruhi wote, kuandaa na kugharamia mazishi ya watu 17 waliofariki ambapo mimi binafsi nilihudhuria na pia kutoa mkono wa pole wa Shilingi Milioni 17 kwa wafiwa. Vilevile, Serikali kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali iliwahudumia wananchi walioathirika na tetemeko kwa kuwapatia misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, madawa, nguo, makazi ya muda, vifaa vya ujenzi, vifaa tiba, vifaa vya shule na huduma ya ushauri wa kisaikolojia. Aidha, Serikali kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa na wadau mbalimbali walifanya Tathmini ya pamoja ya mahitaji ya haraka katika kukabiliana na Athari za Tetemeko hilo. Ambapo utekelezaji wa masuala muhimu yaliyoainishwa katika tathmini hiyo unaendelea.

12. Mheshimiwa Spika, ili kuwezesha wadau, taasisi na wananchi mbalimbali kuchangia maafa hayo, Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Kamati ya Maafa ya Mkoa wa Kagera ilifungua Akaunti pekee Namba 0152225617300 katika Benki ya CRDB Bukoba yenye jina la “KAMATI MAAFA KAGERA”. Hadi kufikia tarehe 10 Novemba, 2016 kiasi cha Shilingi 5,427,671,677.32 kilikuwa kimeingizwa kwenye Akaunti hiyo. Hadi kufikia tarehe 10 Novemba 2016 Salio katika Benki ni Shilingi 4,296,038,711.79 na matumizi hadi tarehe tajwa yalikuwa ni Shilingi 1,130,428,347.53. Aidha, Kamati pia ilisajili namba za simu za mkononi za kupokea michango katika Kampuni za Vodacom (M-Pesa) 0768 196 669, Tigo (Tigopesa) 0718 069 616 na Airtel (Airtel Money) 0682 950 009 kwa jina la “KAMATI MAAFA KAGERA”. Hadi kufikia tarehe 10 Novemba, 2016, kiasi cha Shilingi 16,638,747 kilichangwa kupitia mitandao hiyo ya simu. Hivyo kufanya jumla ya fedha zilizopokelewa kupitia Benki na Mitandao ya Simu kuwa Shilingi 5,444,310,424.32. Aidha, Serikali imechangia Shilingi Billioni Moja katika kukabili janga hilo.

13. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kupokea misaada kutoka kwa Washirika wetu wa Maendeleo, Balozi na hata Nchi marafiki. Mathalan, tumepokea kutoka Serikali ya Uganda Dola za Kimarekani 200,000 sawa na Shilingi Milioni 419.2, Serikali ya India Shilingi Milioni 547, Serikali ya Kuwait Shilingi Milioni 51 na Serikali ya Uingereza iliahidi kutoa Shilingi Bilioni Sita zitakazoelekezwa kwenye ujenzi wa shule.

14. Mheshimiwa Spika, tumepokea vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 357 yakiwemo maturubai, magodoro, ndoo, mashuka, vifaa tiba, dawa na chakula kutoka Serikali za Japan, China, Kenya, Pakistan, Burundi na Rwanda.

15. Mheshimiwa Spika, taarifa ya Kikosi Kazi cha Wataalam imeainisha kuwa takribani Shilingi Bilioni 63.2 zitahitajika kurejesha hali ya kawaida katika Mkoa wa Kagera kufuatia maafa hayo. Gharama hii inajumuisha ukarabati wa shule za msingi, sekondari, vituo vya afya na taasisi nyingine katika wilaya zote sita za Mkoa huo, ujenzi mpya wa shule za Ihungo na Nyakato (tayari wafadhili wamejitolea kujenga shule hizi). Aidha, hadi kufikia tarehe 10 Novemba, 2016 kiasi cha Shilingi 966,898,826 zilitumika katika kufanya ukarabati mkubwa na mdogo wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na Zahanati katika Halmashauri za Mkoa wa Kagera. Serikali inaendelea na ujenzi wa Zahanati mpya (Ishozi) inayojumuisha chumba cha Upasuaji na wodi ya kinamama na watoto na usimamizi wa ujenzi wa shule za Ihungo na Nyakato. Aidha, katika kuongeza nguvu ya urejeshaji hali jumla ya Askari 96 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwemo Wahandisi, Mafundi, Wapishi, na Madereva waliwasili Mkoani Kagera tarehe 19 Oktoba, 2016 kushiriki katika zoezi la kurejesha hali ya majengo na miundombinu.

16. Mheshimiwa Spika, Serikali inapenda kulihakikishia Bunge lako Tukufu na wananchi kwa jumla kuwa Serikali ipo pamoja na waathirika hawa katika suala hili na ina mikakati madhubuti ya kuhakikisha tunarejesha hali bora kwa kuendelea kurudisha miundombinu, kutoa huduma za kibinadamu na matibabu kwa waathirika. Aidha, napenda kuwashukuru wale wote waliochangia katika kusaidia wenzetu wa Kagera, kwani katika kipindi hiki, tumeonesha umoja wetu, upendo wa dhati, hali ya kuthaminiana na kujaliana. Mungu awabariki sana na kuwaongezea pale walipotoa. Kipekee, niwashukuru Nchi marafiki, Balozi, Wadau wa Maendeleo wa ndani na nje ya Nchi, Taasisi za Kiserikali na zisizo za Kiserikali, Taasisi za Fedha, Kampuni, Vikundi mbalimbali, pamoja na Wananchi wote wakiwemo wale waishio nje ya Nchi.

MAPENDEKEZO YA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA WA MWAKA 2017/2018

17. Mheshimiwa Spika, katika Mkutano huu wa tano wa Bunge, Serikali imewasilisha mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/2018. Napenda kutumia fursa hii kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa michango yao mizuri iliyotolewa wakati wa kujadili Hoja hiyo. Maoni na ushauri uliotolewa utazingatiwa wakati wa maandalizi ya Mpango na Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2017/2018.

TAARIFA ZA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE ZA PAC NA LAAC KUHUSU HESABU ZILIZOKAGULIWA KWA MWAKA 2013/2014 NA 2014/2015

18. Mheshimiwa Spika, katika Mkutano huu, Waheshimiwa Wabunge wamepata fursa ya kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Taarifa za Kamati za Kudumu za Bunge za PAC na LAAC kuhusu Hesabu za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Serikali za Mitaa zilizokaguliwa kwa mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2014 na tarehe 30 Juni, 2015. Serikali imepokea michango na Hoja za Waheshimiwa Wabunge na itazifanyia kazi.

19. Mheshimiwa Spika, napenda kuwakumbusha Waheshimiwa Wabunge kwamba kwa mujibu wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 hadi 2016, Serikali imetakiwa kuchukua hatua kali na za haraka kwa wale wote watakaobainika kujihusisha na ubadhirifu
na wizi wa mali ya umma, ukiukaji wa maadili ya Utumishi wa Umma na wale wanaoendeleza vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya fedha za Umma. Kutokana na maelekezo hayo, Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kuimarisha udhibiti wa matumizi ya Serikali na kuchukua hatua kwa Watumishi wa Umma wasiozingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za matumizi ya Fedha za Umma. Maafisa Masuuli wote wanakumbushwa kuzingatia kikamilifu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Kanuni zake. Aidha, Maafisa Masuuli wote wanatakiwa kuchukua hatua stahiki za kinidhamu na kisheria kwa Wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi za Serikali wanaofanya malipo yenye mashaka wakati wa kufanya manunuzi ya Umma au kuingia Mikataba na Zabuni tata za utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Hatua hizo zitapunguza na kuondoa Hoja za ukaguzi na kuimarisha usimamizi wa fedha za walipa kodi.

SEKTA YA KILIMO
Mwenendo wa Uzalishaji wa Mazao Katika Msimu wa Mvua za Vuli
20. Mheshimiwa Spika, naomba nitoe taarifa kutoka Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa kuwa, kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2016 imeonesha kuwa katika maeneo mengi ya nchi, mvua zinatarajiwa kuwa chache, kuchelewa kuanza na mahali pengine kunyesha kwa mtawanyiko usioridhisha. Aidha, kwa maeneo yanayopata mvua za vuli zikiwemo Wilaya za Kyerwa, Missenyi na Karagwe, mvua zilipoanza kunyesha zilikuwa chini ya wastani na kusababisha baadhi ya mazao yaliyopandwa kuathirika. Vile vile, taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA zinaeleza kuwa katika maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua zinazoanza mwezi Novemba hadi Aprili, mvua zitachelewa na kunyesha chini ya wastani hadi wastani katika maeneo mengi isipokuwa katika baadhi ya maeneo ya Mtwara Lindi na Ruvuma. Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kuwataka wataalam wa kilimo kuhakikisha wananchi katika maeneo yatakayopata mvua kidogo wanawezeshwa kupata mbegu za mazao yanayostahimili ukame na zinazokomaa haraka.

Aidha, niwashauri wakulima kuandaa mashamba yao mapema na kutumia mbegu hizo zinazokomaa mapema na kustahimili ukame. Niwasihi wananchi na wakulima kuendelea kutumia kwa uangalifu na kuhifadhi akiba ya chakula walichovuna au kununua kwa matumizi katika kaya zao. Nitoe wito kwa Sekta binafsi kuendelea kushiriki katika kutoa masoko ya kununua na kuuza mazao katika maeneo yenye ziada na kuyauza katika maeneo yenye uhaba.

Usambazaji wa Pembejeo za Zao laTumbaku
21. Mheshimiwa Spika, ili kuondoa kero ya upatikanaji wa pembejeo kwa zao la tumbaku kwa msimu wa 2016/2017, Serikali imebadili utaratibu kutoka ule uliohusisha zabuni kwa wauzaji wa kati (middlemen) na kuweka utaratibu mpya unaohusisha wazalishaji wa pembejeo kuzisafirisha pembejeo hizo hadi katika Vyama vya Msingi vya Ushirika moja kwa moja kwa bei ya Dola za Kimarekani 40.45 kwa mfuko wa NPK (ikilinganishwa na Dola za Kimarekani 52.7 za msimu uliopita), na Dola za Kimarekani 21 pungufu kwa mbolea aina ya Urea na CAN kwa tani moja ukilinganisha uliopita. Hadi sasa wazalishaji wawili wa mbolea za tumbaku (Kampuni ya Yara Tanzania na Rosier) wamechukua jukumu hilo. Napenda kuchukua fursa hii kuvitaka Vyama vya Ushirika kusimamia kikamilifu mpango huu ili wakulima wazalishe kitaalamu na kuongeza tija katika uzalishaji.

SEKTA YA VIWANDA NA UWEKEZAJI
22. Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 17 Oktoba, 2016, Mheshimiwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji alizindua rasmi matokeo ya Sensa ya Uzalishaji Viwandani ya mwaka 2013 iliyofanyika kwa ushirikiano wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS). Zoezi la sensa hii lilitumia taarifa za uzalishaji za viwanda za mwaka, 2013, yaani viwanda vilivyokuwepo mwaka 2013 na vilivyokuwa vinazalisha. Zoezi la ukusanyaji wa taarifa za uzalishaji, za viwanda lilifanyika mwaka 2014 na mwaka 2015 ilikuwa ni kufanya uchambuzi wa kitalaamu na kuandika ripoti.

23. Mheshimiwa Spika, matokeo ya Sensa hiyo yanaonesha kuwa, kufikia mwaka 2013 Tanzania ilikuwa na jumla ya viwanda 49,243 ambapo viwanda vidogo vinavyoajiri mtu 1 – 4 vilikuwa ni Asilimia 85.13, viwanda vidogo vyenye watu 5 – 49 ni Asilimia 14.02, viwanda vya kati vyenye watu 50 – 99 ni Asilimia 0.35 na viwanda vikubwa vyenye watu kuanzia 100 na kuendelea ni Asilimia 0.5. Hivyo, Asilimia 99.15 ya viwanda vyote nchini ni viwanda vidogo.

24. Mheshimiwa Spika, katika utafiti wa mwaka jana ilionekana kuwa mpaka mwezi Oktoba, 2015 kulikuwa na viwanda 52,579. Aidha, kwa kipindi cha mwaka mmoja tu, yaani kuanzia Novemba, 2015 mpaka Oktoba, 2016 jumla ya viwanda vipya 1,843 vimeanzishwa na kufanya jumla ya viwanda vyote nchini kufikia 54,422. Ni matumaini ya Serikali kuwa kutokana na juhudi za uhamasishaji zinazofanyika, kasi ya uanzishwaji viwanda na hasa viwanda vidogo na vya kati na vikubwa itaongezeka sana.

25. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara mbalimbali za Kisekta tayari imebainisha maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kuchochea uwekezaji kama vile kuendeleza eneo la Mji wa Kigamboni na kutenga maeneo maalum ya Uwekezaji katika Mikoa mbalimbali Nchini. Hatua nyingine ni kuboresha miundombinu kama vile barabara na reli. Mfano mzuri ni ujenzi wa reli yenye urefu wa kilomita 4 katika kiwanda kipya cha KILUA GROUP cha kutengeneza nondo kilichopo Mlandizi, Pwani. Pia, Serikali inaendelea kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika. Kwa viwanda ambavyo vipo karibu na bomba la gesi watasaidiwa kuunganishwa na gesi. Vilevile, Serikali, imechukua hatua madhubuti za kuharakisha upatikanaji wa ardhi ambacho ni kivutio muhimu katika kuhamasisha uwekezaji.

Uongezaji Kasi ya Uwekezaji kwenye Sekta ya Viwanda Nchini
26. Mheshimiwa Spika, Serikali imeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha kasi ya uwekezaji kwenye sekta ya viwanda inaongezeka ili ichangie Asilimia 15 ya Pato la Taifa ifikapo mwaka 2020 Ili kutekeleza adhima hiyo hatua zifuatazo zinaendelea kuchukuliwa:-

Kwanza: Kutambua sekta za kipaumbele kwa kuzingatia viwanda vinavyotumia malighafi za ndani, na hususan kwenye sekta za kilimo na maliasili ili kuchochea uzalishaji vijiini na kuongeza ajira; viwanda vinavyotumia malighafi za ndani ambazo si za kilimo kama vile madini na kemikali; na kuweka msukumo kwenye kuanzisha viwanda visivyotumia malighafi za ndani kama vile uunganishaji wa magari na uzalishaji wa vifungashio.
Pili: Kuandaa Mpango mahsusi wa uwekezaji kwenye viwanda kupitia Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Mpaka sasa, Mifuko ya LAPF, PPF, PSPF, NSSF na GEPF tayari wameainisha miradi ya uzalishaji watakayoanza nayo.
Tatu: Kuhamasisha Sekta Binafsi, ya ndani na nje ya Nchi, kuwekeza kwenye viwanda. Kupitia makongamano ya biashara na uwekezaji nchi mbali mbali zimehamasishwa kuwekeza nchini. Baadhi ya nchi hizo ni China, Oman, Vietnman, Urusi, Morocco n.k.
Nne: Kuingia makubaliano ya ushirikiano na Nchi zingine ili kuongeza uwekezaji. Mpaka sasa Nchi ya China imechagua jimbo la Jiangsu kuleta viwanda nchini na pia kupitia Jukwaa la Ushirkiano la China na Afrika itawezesha ujenzi wa miundombinu ikiwemo Bandari ya Bagamoyo. Aidha, kwa utaratibu huu Serikali tayari imeanza utekelezaji wa mradi wa kuunganisha matrekta 2400 pale TAMCO Kibaha kufuatia ushirikiano na Serikali ya Poland, uunganishaji wa magari wa Kampuni ya Kitanzania ya SIMBA MOTOR kwa ushirikiano na Jeshi (NYUMBU) na Kampuni ya China. Vile vile, India kupitia mradi wake wa kuimarisha uwekezaji Afrika (SITA) inasaidia utekelezaji wa mikakati minne ya kukuza na kuendeleza alizeti, pamba, ngozi na mazao ya jamii ya kunde.
Tano: Kutoa elimu na mwongozo kwa Serikali ngazi ya Mikoa na Wilaya kuendelea kuhamasisha uwekezaji katika maeneo yao. Serikali imegawa Mikoa katika makundi manane ambayo Watendaji Waandamizi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji watakwenda kuzungumza na wadau ili kuhakikisha viwanda vinasambaa Nchi nzima.

27. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza jukumu hili mambo muhimu ambayo Mikoa inatakiwa kuzingatia ni pamoja na Mikoa kuweza kubaini fursa walizonazo na kuandaa taswira ya mkoa kutegemeana na fursa walizonazo. Aidha, Mikoa inahimizwa kuhamasisha wananchi juu ya uwekezaji. Vilevile, Viongozi wa Mkoa wanashauriwa kuongeza kasi ya kuhamasisha Mamlaka za Serikali za Mitaa kutenga maeneo na kuhakikisha kuwa wanazingatia katika mipango ya Halmashauri za wilaya ujenzi wa miundombinu wezeshi kwenye maeneo watakayotenga kwa ajili ya uwekezaji.

SEKTA YA ELIMU

Matokeo ya Mitihani ya Darasa la Saba 2016
28. Mheshimiwa Spika, mwezi Oktoba, 2016 Baraza la Mitihani la Taifa lilitangaza matokeo ya Mitihani wa Darasa la Saba kwa mwaka 2016. Taarifa hiyo ilibainisha kuwa katika mtihani huo, kati ya wanafunzi 789,479 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 555,291 walifaulu sawa na Asilimia 70.36. Kati yao wasichana ni 283,751 na wavulana ni 271,540. Nitumie fursa hii kuwapongeza wanafunzi wote waliofaulu na Shule zote zilizofanya vizuri na hasa wale kumi bora. Napenda kuwaagiza Viongozi wa Mikoa na Halmashauri kuendelea kukamilisha miundombinu ya vyumba vya madarasa na miundo-mbinu mingine ili kuandaa mazingira ya kuwapokea wanafunzi wanaotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwezi Januari, 2017. Kila Mkoa uweke lengo la kuhakikisha Wanafunzi wote watakaochaguliwa wanajiunga na Sekondari. Serikali kwa upande wake itahakikisha inatoa ruzuku kwa ajili ya mahitaji ya Wanafunzi watakaojiunga na Sekondari.

Mwenendo wa utoaji wa mikopo
29. Mheshimiwa Spika, tangu mwaka 1994 Serikali ilipoanza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu, jumla ya kiasi cha Shilingi Trilioni 2.44 kimekwishatolewa. Jumla ya wanafunzi 324,994 wamenufaika na fedha hizo.

30. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/2017 jumla ya wanafunzi 64,441 wamedahiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu na orodha yao kuwasilishwa Bodi ya Mikopo ya Elimu Juu. Kama alivyoeleza Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia tarehe 3 Novemba, 2016, wakati akitoa kauli ya Serikali Bungeni kuhusu upangaji na utoaji wa Mikopo ya Elimu ya Juu, ni kwamba hadi kufikia tarehe 2 Novemba, 2016 jumla ya wanafunzi 25,228 wa mwaka wa kwanza walikuwa wamekwishapewa fedha za mikopo. Kati ya wanafunzi hao, 4,787 ni Yatima, 127 wenye Ulemavu na 94 ni waliosoma Sekondari kwa Ufadhili wa Taasisi mbalimbali.

31. Mheshimiwa Spika, napenda kusisitiza kuwa wanafunzi wote wanaoendelea na masomo, ambao ni wanufaika wa mikopo na vyuo vyao vimewasilisha Bodi ya Mikopo taarifa za matokeo wameendelea kupatiwa mikopo kama ilivyokuwa katika mwaka uliopita wa masomo.

Changamoto Zilizopo za Mkopo na Utatuzi Wake
32. Mheshimiwa Spika, ili kutatua changamoto zinazojitokeza katika uratibu wa mikopo ya wanafunzi, Serikali inafanya mapitio ya mfumo wa udahili wa wanafunzi vyuoni, utaratibu mzima wa utoaji na urejeshwaji mikopo kwa lengo la kuwa na mfumo bora zaidi na kuondoa adha inayowapata wanafunzi wanapofungua vyuo kutokana na mfumo uliopo sasa. Nimeagiza kazi hii ikamilike mapema ili mapendekezo ya mfumo utakaokuwa na tija zaidi yaweze kuzingatiwa wakati wa maandalizi ya Bajeti ya 2017/2018.

SEKTA YA ARDHI

Hali ya Migogoro baina ya Watumiaji wa Ardhi Nchini:
33. Mheshimiwa Spika, nchi yetu imeendelea kukumbwa na migogoro mbalimbali ya ardhi baina ya watumiaji wa ardhi ikiwemo migogoro mikubwa baina ya wakulima na wafugaji; migororo baina ya wananchi na wawekezaji; wafugaji na hifadhi za Taifa na baina ya wakulima na baadhi ya maeneo ya hifadhi za Wilaya mbalimbali.

Juhudi na Mikakati ya Serikali ya Kuondoa Migogoro Mikubwa ya Wakulima na Wafugaji
34. Mheshimiwa Spika, migogoro ya matumizi ya ardhi baina ya Wakulima na Wafugaji imeendelea kuongezeka kutokana na ongezeko la watu na mifugo, na vijiji kutokuwa na Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi inayoainisha maeneo mahsusi kwa ajili ya Kilimo na Ufugaji. Aidha, uwepo wa mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha ukame na ukosefu wa malisho na maji katika maeneo ya wafugaji kumesababisha uhusiano hafifu baina ya jamii za wafugaji na wakulima kutokana na mifugo kuingizwa katika mashamba ya wakulima kwa mabavu.

35. Mheshimiwa Spika, migogoro hii imesababisha kuwepo kwa vitendo vingi vya uvunjifu wa amani, upotevu wa maisha ya wananchi, baadhi ya wananchi kupata vilema vya maisha, uharibifu wa mali, uharibifu wa mazingira, athari za kijamii kama watoto kushindwa kwenda shule na wananchi kushindwa kushiriki katika shughuli za maendeleo kutokana na hofu jambo linaloweza kusababisha njaa na umaskini miongoni mwa jamii na Taifa.

Hatua za kutatua migogoro mikubwa ya wakulima na wafugaji
36. Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na migogoro na kuwawezesha wakulima na wafugaji kuendelea na shughuli zao bila migogoro, Serikali inaendelea kutekeleza mikakati ya kuainisha, kupima, kutenga na kumilikisha ardhi kwa ajili ya wafugaji na wakulima; na kanda za malisho kwa wafugaji wakubwa na wadogo itakayohusisha vijiji, Wilaya na Mikoa. Maeneo haya yatakayotengwa yatalindwa kwa kuyatangaza kwenye Gazeti la Serikali, na matumizi yake yatasimamiwa ili kuhakikisha wanafuga kwa kuzingatia uwiano wa malisho na mifugo.

37. Mheshimiwa Spika, mikakati hiyo ni pamoja na kuzigawanya Ranchi zilizopo katika vitalu ili wafugaji wenye ng’ombe zaidi ya 200 wahamie huko, kila kitalu kimoja kulingana na uwezo wa kitaalamu wa kulisha idadi maalum ya ng’ombe. Wafugaji wenye mifugo chini ya 200 watagawiwa maeneo katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili yao katika vijiji na watakuwa wanauza mifugo yao katika minada ambapo wafugaji kutoka Ili katika ranchi watafika kununua mifugo hapo. Kwa mikoa ambayo haina Ranchi za Taifa, watatenga maeneo yaliyo wazi kwa ajili ya wafugaji wakubwa.

38. Mheshimiwa Spika, ili kuzuia wafugaji kuhamahama kutafuta maji na huduma nyingine, Serikali kwa kushirikiana na wafugaji itaweka miundombinu ya majosho, mabwawa ya kunyweshea maji, huduma za ugani zikiwemo matibabu, elimu ya kulima malisho, unenepeshaji, uwekaji sahihi wa chapa za ng’ombe n.k.

39. Mheshimiwa Spika, pamoja na hatua hizo, jawabu la kudumu la migogoro hii ni kuhakikisha kuwa tunawawezesha wafugaji kuvuna na kupunguza mifugo bila kupata hasara, kupitia uwekezaji wa Viwanda vya Kuchakata Nyama na Usindikaji Maziwa ili kuongeza thamani. Wizara husika zikae pamoja na kubuni Mikakati na Mipango ya kuvutia wawekezaji katika eneo hili katika miaka mitatu ijayo kuwe na tofauti.

40. Mheshimiwa Spika, aidha napenda kuzikumbusha Halmashauri za Wilaya kote nchini kuendelea kuweka na kutekeleza mipango madhubuti ya matumizi bora ya ardhi, na wale wenye Benki ya Ardhi wagawe kwa busara kwa wafugaji, wazuie wafugaji wengine wasiendelee kuingiza mifugo katika maeneo ya kilimo na watumie sheria ndogo zilizopo na kama hazipo ziandaliwe na kutumiwa; na ikibidi wahalifu wapelekwe mahakamani. Aidha, niwakumbushe wafugaji wote kufuata sheria na kwamba Serikali haitasita kuwachukulia hatua wafugaji watakaoingiza mifugo yao katika mashamba ya wakulima kwa makusudi.

SEKTA YA NISHATI
Mradi Kabambe wa Kupeleka Umeme Vijijini Awamu ya Pili
41. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia umuhimu wa nishati ya umeme, Serikali imeendelea kutoa mkazo katika kutekeleza na miradi mikubwa ya uzalishaji na usafirishaji umeme pamoja na miradi ya kusambaza umeme vijijini. Ili kuhakikisha huduma ya umeme inawafikia wananchi wengi, hususan waishio vijijini, Serikali kupitia REA imeendelea kutekeleza Mradi Kabambe wa Kupeleka Umeme Vijijini Awamu ya Pili tangu mwaka 2014. Mradi huu unatekelezwa katika wilaya zote za Tanzania Bara. Hadi kufikia Oktoba, 2016 ujenzi wa kilometa za njia ya msongo wa Kilovolti (kV) 33 umefikia Asilimia 95.6; ujenzi wa kilometa za njia ya Msongo wa Volti 400 umefikia Asilimia 89.3; na ufungaji wa transfoma umefikia Asilimia 87.2. Aidha, jumla ya wateja 146,311 wa awali sawa na Asilimia 59 ya lengo la wateja 255,000 wameunganishiwa umeme kupitia mradi huo.

Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu

42. Mheshimiwa Spika, Mradi huu utatekelezwa kwa kipindi cha miaka 5 katika vijiji 7,873 vya wilaya zote za Tanzania Bara. Takriban vijiji 7,697 vitapelekewa umeme wa gridi ya Taifa na vijiji 176 umeme wa nje ya gridi (Off-grid). Mpango huu utaongeza wigo wa usambazaji umeme katika maeneo ambayo hayakufikiwa na miradi ya REA Turnkey Phase I na II. Ili kutekeleza miradi hiyo kwa kasi zaidi, Serikali ya Awamu ya Tano katika bajeti yake ya mwaka 2016/17 iliongeza fedha za kupeleka umeme Vijijini kutoka Shilingi Bilioni 357.117 zilizotengwa mwaka 2015/16 hadi Shilingi Bilioni 587.61 mwaka 2016/17. Hadi kufikia mwezi Oktoba, Serikali imetoa jumla ya Shilingi Bilioni 109.8 kwa ajili ya Mfuko wa Nishati Vijijini kutoka kwenye vyanzo vya fedha za ndani. Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 100.4 ni tozo ya mafuta na Shilingi Bilioni 9.4 ni tozo ya umeme.

43. Mheshimiwa Spika, zabuni za kupata wakandarasi wa kutekeleza mradi huu zilitangazwa tarehe 1 Agosti, 2016. Kwa sasa REA inaendelea na uchambuzi wa zabuni hizo. Taratibu zote za mradi huo zimepangwa kukamilika mwezi Januari, 2017. Natoa rai kwa viongozi mbalimbali wa Serikali wakimemo Waheshimiwa Wabunge kuwahamisha wananchi katika maeneo yao kutumia fursa ya kuunganishiwa umeme wakati wakandarasi wakiwa kwenye maeneo ya miradi. Katika kipindi hicho bei ya kuunganisha umeme ni Shilingi 27,000 tu kama ilivyotaarifiwa awali katika Bunge hili.

44. Mheshimiwa Spika, Serikali pia imeanzisha Mradi wa Kupanua Wigo wa Upatikanaji wa Umeme Vijijini (Tanzania Rural Electricity Expansion Project). Mradi huo utagharamiwa kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia wa Dola za Kimarekani milioni 209. Mradi ulizinduliwa tarehe 26 Agosti 2016, katika kijiji cha Kwedikwazu wilayani Handeni Mkoani Tanga na utawezesha kaya takriban 500,000 kupata huduma ya umeme nchini.

SEKTA YA MADINI

Migodi Mikubwa Kuendelea Kulipa Mrabaha
45. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kati ya Oktoba, 2015 na Oktoba, 2016 Serikali ilifanya ukaguzi na kuwezesha migodi mikubwa kulipa mrabaha ambapo: Migodi Mikubwa ya Dhahabu ya Biharamulo, Bulyanhulu, Buzwagi, Geita, New Luika na North Mara imelipa kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 69.4 ikiwa ni Mrabaha, sawa na Shilingi Bilioni 151.4. Vilevile, Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka umelipa kiasi cha Dola za Kimarekani 309,836 na Shilingi Milioni 676 ikiwa ni mrabaha. Aidha, Mgodi wa TanzaniteOne umelipa mrabaha wa Dola za Kimarekani 189,731 sawa na Shilingi Milioni 414.

Kuhamasisha Masoko ya Madini ya Vito Nchini
46. Mheshimiwa Spika, Serikali iliandaa mnada wa madini ya vito, hususan tanzanite uliofanyika kuanzia tarehe 9 hadi 12 Agosti, 2016 Jijini Arusha. Katika mnada huo madini yenye thamani ya Dola za Kimarekani 3,448,050, sawa na Shilingi Bilioni 7.56, yaliuzwa na kuwezesha Serikali kukusanya Dola za Kimarekani 150,491.06, sawa na Shilingi Milioni 331 ikiwa ni mrabaha kutokana na madini yaliyouzwa.

47. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kusimamia Sekta za Nishati na Madini ili ziweze kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu.

TAARIFA YA MAKUSANYO YA FEDHA KWENYE HALMASHAURI KWA MWAKA 2016/2017

48. Mheshimiwa Spika, katika Bajeti ya mwaka 2016/2017 Halmashauri ziliidhinishiwa kukusanya mapato ya Shilingi Bilioni 665.4. Hadi kufikia Septemba, 2016 Halmashauri zimekusanya Shilingi Bilioni 114.46, sawa na Asilimia 17.2 ya makisio. Kiwango hiki cha ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri bado hakiridhishi. Hivyo, naomba nitumie fursa hii kuhimiza Halmashauri zote nchini kuongeza jitihada katika kukusanya mapato ya vyanzo vya ndani. Nazihimiza Halmashauri kutumia mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji mapato na pia katika maeneo ya kutolea huduma za afya ili kudhibiti upotevu wa mapato. Aidha, naelekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa waimarishe mifumo ya udhibiti wa ndani na kuhakikisha thamani ya fedha inapatikana katika kila huduma au bidhaa inayonunuliwa na Halmashauri. Halmashauri hazina budi kuepuka matumizi ya fedha yasiyo na tija katika shughuli za uendeshaji wa Mamlaka hizo.

49. Mheshimiwa Spika, Halmashauri zote zinaagizwa zifuatilie kwa karibu mapato na matumizi ya fedha zinazopelekwa kwenye shule na kwenye vituo vinavyotoa huduma za afya ikiwemo Hospitali, vituo vya afya na zahanati. Ili kufikia azma hiyo, uwekwe utaratibu madhubuti wa ukaguzi wa mapato na matumizi ya fedha hizo kwa kushirikisha Wakaguzi wa ndani wa Halmashauri.

MAONI NA MAPENDEKEZO KUHUSU TAARIFA YA KAMATI YA BUNGE YA LAAC

50. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia ushauri mzuri na mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya LAAC kuhusu ukaguzi uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2013/2014 na 2014/2015, Serikali imeshatoa maelekezo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa zinatekeleza kwa ukamilifu maelekezo yote ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa na Kamati nyingine ili kuondoa hoja zilizojitokeza katika taarifa ya CAG. Aidha, Halmashauri zinaelekezwa kuimarisha mifumo ya uthibiti wa ndani na kutumia vizuri ushauri unaotolewa na Kamati za Ukaguzi ili kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma.

51. Mheshimiwa Spika, napenda kusisitiza kwamba Halmashauri zote ni lazima zitekeleze vipaumbele vilivyoidhinishwa katika mpango na bajeti kwa mwaka 2016/17 kwa kupanga vema utekelezaji kwa kuzingatia upatikanaji wa fedha. Halmashauri ziendelee kuimarisha usimamizi wa mikataba ili thamani ya fedha za Serikali iweze kupatikana katika miradi na Kandarasi nyingine zilizoingia Mikataba na Halmashauri.

HITIMISHO

52. Mheshimiwa Spika, wakati tunahitimisha mkutano huu leo, napenda nitumie nafasi hii kukushukuru wewe binafsi, Mheshimiwa Naibu Spika na Wenyeviti wote wa Bunge kwa kusimamia vizuri na kwa weledi mkubwa vikao vyote vya mkutano huu. Niwashukuru tena Waheshimiwa Wabunge wote kwa michango yenu. Ninashukuru pia Watendaji wa Serikali kwa kuwasaidia Mawaziri na Naibu Mawaziri katika kujibu maswali na hoja mbalimbali za Wabunge. Niwashukuru wanausalama wote kwa kazi yao nzuri. Niwashukuru madereva wote kwa kuwaendesha Mawaziri, Wabunge na Watendaji wote kwa usalama kabisa. Niwashukuru pia wanahabari wote kwa kuihabarisha jamii juu ya mkutano wetu. Kipekee, nimshukuru Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah na timu yake kwa kutuwezesha kukamilisha shughuli zote za mkutano huu kwa mafanikio makubwa.

53. Mheshimiwa Spika, mwisho, lakini si kwa umuhimu, nitumie muda huu kumwomba Mwenyezi Mungu awalinde na awaongoze Waheshimiwa Wabunge wote katika safari ya kurejea majumbani kwenu. Aidha, nawatakia kila la kheri na fanaka katika sikukuu zijazo za mwisho wa mwaka na kuwatakia mwaka mpya wa 2017.

54. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, napenda kutoa hoja kuwa Bunge lako tukufu sasa liahirishwe hadi tarehe 31 Januari, 2017, siku ya Jumanne, saa 3:00 asubuhi litakapokutana katika ukumbi huu hapa Dodoma.

55. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 86 & 87 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
"Hiyo ni picha ya ukurasa wa mbele katika gazeti hili la Jambo leo, ikibebwa na kichwa chà habari kisemacho, MTOTO WA WAZIRI MKUU NA MKEWE WATEKWA NA WATU WASIO JULIKANA, NA RISASI ZARINDIMA ENEO ZIMA LA KANISA"
Mtangazaji alizungumzà, huku akifunua kurasa ya ndani, akidai kwenda kuisoma taarifa hiyo kwa

ENDELEA
Manka akazima tv, na kuiweka rimoti mezani, akionekana kupatwa na mawazo ya gafla.
"Mbona umezima"
Nilimuuliza kwa sauti ya upole sana
"Eddy, hichi ni nini ulicho kifanya kwa Fredy wangu?"
"Nisikili......"

"Eddy hapa hakuna cha kusikiliza, umemsababishia mwenzako matatizo makubwa sana"
"Ndio nalitambua hilo, ila natambua kwamba hajauliwa, lazima atakua hai"
"Una uhakika gani, hata kama Fredy hajiwezi kitandani, lakini nimempenda hivyo hivyo."
Manka alizungumza huku akiwa amekasirika sana, machozi yakaanza kulowanisha uso wake.

"Oya mboma mimi siwaelewi?"
Amina alituuliza baada ya tukio lililo tokea, kushindwa kulielewa. Nilamuelezea kwa ufupi, akanielewa vizuri
"Sasa wewe, Manka huo ni unafki sasa. Tangu lini ukamlilia mwanaume?"
"Amina hujui tu maumivu, niliyo kua nayo nampenda Fredy tena sana"
"Hembu sikia, ishu hapa ipo hivi. Tunakwenda kwa hao mafala walio teka mke wa bro, tukimaliza tunakwenda kwa hao mafala wengine walio teka Fredy"
Amina alizungumza huku akiwasha sigara yake kwa kiberiti cha kutumia gesi.
"Yaani hapa nguvu zote zimeniishia"
"Zimekuishia kisa mwanaume. Mbona umekua fala sana mtu wangu?"

"Manka niliye kua namjua mimi ni yule wakazi, sasa Manka wewe wa kulia lia kisa mwanaume sijui umetokea dunia gani. Hembu nyanyuka tukafanye kazi"
"Siendi popote"
”Nini wewe, sasa maana ya kuja hapa ni nini?"
"Siendi"
Mgomo wa Manka ukaañza kunipa wasiwasi mkubwa, dalili mbaya ya mpango nilio upanga mbele yangu nikaanza kuuona ukianza kuharibika.
"Manka nini unafanya, nini uliniahidi kulifanya juu ya familia yangu?"
"Sawa Eddy ila elewa siendi popote"
"Sikia Eddy asikuchanganye, mziki wako nauelewa vizuri. Twende tukapige job"

Manka akanyanyuka na kuingia ndani, kwa Amina. Amina akamfwata kwa nyuma kwenda kuzungumza naye. Nikawasha Tv, ila nikaikuta tarifa hiyo ikiwa imekwisha, nikajaribu kuitafuta kwenye chanel tofauti, pia sikuipata.
"Oya mtu wako amekataa bwana, tujiandae twende tukapachunguze, kisha usiku twende"
"Poa"
Tukajiandaa, nikavaa miwanani pamoja na kofia, tukaingia kwenye gari la Amina na kuondoka.
"Hilo begi lina nini?"
Nilimuuliza Amina, àliye beba begi la mgongoni, alilo liweka siti ya nyuma.
"Lifungue"
Nikalichukua, nikalifungua. Nikakuta kamera moja aina ya Canoon, bastola tatu, magazine kumi na mbili, na mabomu manne yakurusha kwa mkono.

"Mmmmmm"
"Mbona umeguna?"
"Kazi leo ipo"
"Ahaaa ulizani nimchezo, hii ni Somalia bwana, kuingia nirahisi ila kutoka ni ngumu"
Amima alizumgumza huku akiongeza mwendo kasi wa gari lake. Chakumshukuru Mungu, htukukutana na polisi barabarani. Mwendo wa dakika arobaini na tano, tukafika kwenye majengo ya magorofa machakavu, yaliyopo nje kidogo ya mji wa Mogadishu. Amina ajasimamisha gari pembeni na kuitoa simu yake, akaniomba namba ya simu ya jamaa aliye nipigia, akaipiga, baada ya muda ikapokelewa, akaanza kuzungumza na jamaa kisomali, ambacho sikielewi kabisa.
"Amesemaje?"
Nilimuuliza Aminà baada ya kumaliza kuzungumza na jamaa huyo.

"Anasema yupo hapa"
"Ulimuambia kwamba wewe ni nani?"
"Hapana nimemuambia nahitaji kufanya nao biashara ya mafuta"
"Kwahiyo watakuja hapa tulipo?"
"Hapana nilitaka kufahamu kwamba wapo hapa"
Tukakaa ndani ya gari zaidi ya nusu saa, sikuwa ninaelewa nini maana ya Amina.
"Tunasubiri nni hapa?"
"Usiwe na hataka utaona"

Tukaendelea kusubiri zaidi ya masaa mawili, magari makubwa aina ya Scania yakatoka yakiwa na matela nyuma. Yakaingia barabara ya lami, na kuondoka kwa mwendo wa taratibu. Amina akawasha gari, taratibu tukaanxa kuyafwata.
"Tunaelekea wapi?"
"Tunayafwatilia hayo magari moja wapo ndipo alipo mke wako?"
"Umejuaje?"
"Hawa jamaa huwa wanafanya biashara ya kuuza wañawake wanao wateka katika nchi za ulaya, ambapo huku wanakwenda kuuzwa kwenye makasino na mabaa makubwa kwa ajili ya ngono"
"Sasa hapa wanawapeleka wapi?"
"Hii moja kwa moja wanakwenda baharinia àmbàpo wanawasafirisha kutumia meli"

"Mmmmmmmm"
"Usigune hii ndio dunia bwana"
Amina alizungumza huku akiongeza mwendo kasi wa gari"
Nikaanza kuzitoa bastola moja moja, na kuanza kuzikagua kama zina ubora kwa maana nimatambua chochote kitatolea muda wowote tuliwa kwenye hio safari ambayo hadi sada hivi sitambui kama kuma udhibitisho wowote wa Phidaya kuwa ñdani ya magari haya yenye makontena makubwa.
Kadri tulivyo zidi kwenda ndivyo jinsi mahari hayo yalivyo zidi kuyoyoma, Amina hakukata tamaa, kila magari yalipo kunja naye akakunja pasipo kuhofia kama wahusika wameugundua, uwepo wetu wa kuwafwatilia kwa nyuma.
"Usiyafwate kwa ukaribu zaidi watatustulia"

"Usiogope"
"Kivipi"
"Hakuna kitakacho jitokeza"
"Mmmm"
Kitu ninaçho kiamini maishani mwangu, ni kuto kumuamini mtu yoyote, mbaya zaidi wale nilio waamini wote walinifamyia unyama wa hali ya juu, nikajikuta nilihangaika na kuteseka vibaya mno. Akili yangu ikaanza kumfikiria Amina, sikuhitaji kumpa uaminifu wa aina yoyote. Magari tuliyo yafwata, tukayashuhudia yakikunja kushoto mwa barabara na kuiacha barabata ya la lami na kuingia barabara ya vumbi. Amina akasimamisha gari
"Mbona umesimamisha gari?"
"Huku walipo ingia ni hatari sana"
"Kwahiyo itakuaje?"
"Itatulazimu kwenda kwa miguu, kutokana sio mbali saña na hapa"

Tukashuka kwenye gari, tukachukua silaha zetu, kila mmoja akachukua silaha yake, tukaanza kuchanja mbuga kwa kutumia miguu. Kigiza kwa mbali kilisha anza kujitokeza, huku saa yangu ya mkononi ikinionyesha ni saa kumi na mbilo na robo. Tukatembea zaidi ya dakika kumi. Tukafika kwenye moja ya fensi , iliyo zunguka majengo machakavu, ambayo yapo pembezoni mwa bahari. Tukapenya kwenye fensi hii, iloyo na uwazi mkubwa kidogo.

Kwa mwendo wa haràka, wenye umakini, tukafanikiwa kufika kwenye moja ya nyumba. Tukashuhudia jinsi watoto wengi wa kike wakishushwa kwenye magari hayo. Amina akachukua kamera yake, na kuanza kurekodi matukio yote yanayo endelea, huku akizivuta karibu sura za wasichana hao, weñgine walipaswa kuwa mashuleni, ila ndio hivyo wametekwa.

Nikamuona Phidaya akisukumwa, kitoka kwenye gari alilo kuwepo, kuanguka kwake chini, kukanifanya nitake kujitoa muhanga, ila Amiña akaniwahi
"Umataka kufanya nini?"
"Mke wangu yule"
"Kwahiyo? Hembu tumia akili, wewe huoni walivyo wengi. Unadhani utapona?"
Amina alizumgumza huku akiwa amenikandamiza ukutani kwa nguvu zake zote.
Nikamshuhudia askari mmoja akimpiga Phidaya mgongoni kwa kutumia kitako cha bunduki mgongoni, baada ya Phidaya kukataa kunyanyuka, chini.

Picha: Mazishi ya Spika Mstaafu Samwel Sitta

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakitoa heshima za mwisho kwa Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta kabla ya mazishi yake yaliyofanyika jana Urambo mkoani Tabora

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Y. Ndugai akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta wakati wa mazishi wa Spika huyo Mstaafu.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta wakati wa mazishi wa Spika huyo Mstaafu. Anayefuatia ni Mkuu wa Kambi ya upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yakanusha taarifa kuwa Balozi Omar Ramadhan Mapuri amefariki dunia

$
0
0
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inapenda kukanusha taarifa kutoka Kwenye baadhi ya Mitandao ya Kijamii ikidai kwamba, Mhe. Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Balozi Omar Ramadhan Mapuri (pichani) amefariki dunia.

Taarifa Rasmi ya Serikali ni kwamba taarifa hizo ni za uongo na hazina hata Chembe ya ukweli. Mhe. Kamishna Balozi Mapuri yupo hai na afya yake iko vizuri. 
 
Mheshimiwa Balozi Omar Ramadhan Mapuri ambae kwa sasa ni Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipata matibabu na baada ya kupata huduma kutoka kwa madaktari, Mheshimiwa Balozi Mapuri aliruhusiwa kurejea nyumbani siku ya Jumamosi Novemba 12 baada ya afya yake kuimarika.

Serikali imesikitishwa na taarifa za uvumi na uzushi uliosambazwa jana na leo kwenye mitandao  ya kijamii, taarifa hizi sio za kweli na tunawaomba wananchi wazipuuze.
 
Aidha, Serikali inapenda kuvionya vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa za uongo kuhusu viongozi wa Serikali.

Imetolewa na :
Dk. Juma Mohammed Salum
Kny Mkurugenzi
Idara ya Habari MAELEZO

Zanzibar

Hoja sita Zilizojadiliwa katika mkutano wa tano wa Bunge la 11

$
0
0
Licha ya Mkutano wa Tano wa Bunge uliomalizika juzi kuwa mahsusi kwa ajili ya kamati za kudumu kuwasilisha taarifa za hesabu ambazo aghalabu hufuatiwa na mijadala mizito hasa ya ufisadi, safari hii haikuwa hivyo, badala yake hoja sita tofauti na hizo ndizo zilizotikisa vikao vyake.

Mkutano huo uliofanyika kwa siku 10 na kumalizika juzi, pamoja na mambo mengine ulikuwa mahsusi kwa ajili ya kamati hizo kuwasilisha taarifa zao kuhusu hesabu zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha wa 2013/14 na 2014/15 ambazo safari hii zilipewa umuhimu mdogo ikilinganishwa na mikutano iliyopita.

Kamati zilizowasilisha taarifa zao ni ya Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (Laac) ambazo licha ya kuibua kashfa kama ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika Mradi wa Kigamboni na ukopeshaji wa vikundi vya kuweka na kukopa (Saccos), mradi wa vifaa vya utambuzi wa vidole uliokuwa ukifanywa na Kampuni ya Lugumi kwa Jeshi la Polisi na utata wa mizigo kwenye Mamlaka la Bandari Tanzania (TPA), hayakuonekana kupewa umuhimu mkubwa katika mijadala bungeni.

Mambo mengine ambayo hayakupewa umuhimu katika mkutano huo wakati wa majadiliano ni kashfa ya mradi wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) na mradi wa machinjio wa jiji la Dar es Salaam. Lakini kuna mambo ambayo yalipewa kipaumbele.

Ukata bungeni
Wabunge wengi wakiwamo wa CCM na wale wa upinzani katika michango yao walijikita zaidi katika hali ya uchumi inayowakabili wananchi pamoja na Bunge lenyewe wakisema hali hiyo imewafanya washindwe kufanya shughuli za ukaguzi wa miradi na taasisi za umma.

Mbunge wa Mpwapwa (CCM), George Lubeleje alisema ni aibu kwa wabunge kukaa kwenye kamati na kusubiri kuletewa taarifa za miradi na maofisa wa Serikali badala ya wao kwenda kuikagua ili kujiridhisha na kile walichoambiwa “Hivi ni nani aliyeua mfuko wa Bunge? Hiki tunachokifanya hapa ni kuisimamia Serikali au kupitisha tulicholetewa na maofisa wa Serikali? Hii si sawa hata kidogo ni lazima tuikatae hali hii,” alisema.

Hoja hiyo, iliungwa mkono na Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche akisema hata kamati zinazokaa hadi usiku zimekuwa zikikosa huduma ya maji ya kunywa.

Mikopo
Wabunge pia walivutana na Serikali kuhusu muda wa urejeshwaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi walionufaika katika Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 3 wa mwaka 2016. Katika muswada huo, Serikali iliwataka wanafunzi hao kuanza kulipa, mwaka mmoja baada ya kumaliza au kukatika masomo yao.

Katika mvutano huo ambao wabunge wa pande zote mbili yaani wa CCM na wa upinzani walizungumza lugha moja na Serikali ililazimika kuongeza hadi miaka miwili kwa mnufaikaji wa mikopo hiyo kuanza kufanya marejesho.

Mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara ndiye aliyepeleka mapendekezo akitaka Serikali kuongeza muda wa wanufaika hao kuanza kulipa mkopo.

Alisema kinyume chake, wanufaika kutoka familia maskini watashindwa kulipa mikopo hiyo kwa muda huo uliowekwa.

Hoja ya Waitara iliungwa mkono na Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT - Wazalendo), Kabwe Zitto, Ridhiwani Kikwete (Chalinze - CCM), Ester Matiko (Tarime Mjini - Chadema), Elibariki Kingu (Manyoni Magharibi - CCM) na Fratei Massay (Mbulu Vijijini - CCM).

Uzoefu wa ma-DED
Wabunge pia waliibua mjadala wa uteuzi wa wakurugenzi watendaji wa halmashauri (DED) na watumishi wengine katika Awamu ya Tano wasiokuwa na uwezo wa kuongoza maeneo waliyochaguliwa.

Baadhi ya wabunge walisema wakurugenzi hao walichaguliwa kutoka maeneo tofauti bila kuzingatia Sheria ya Utumishi wa Umma na uzoefu walionao katika utumishi huo hivyo kushindwa kuelewa majukumu yao na kujikuta wakivuka mipaka yao ya kazi na wakati mwingine kutokuwa na ushirikiano na watumishi.

Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini alisema wengi wao hawana uwezo wala uelewa wa shughuli za Serikali kwa kuwa hawakuwahi kufanya kazi huko na walipochaguliwa hawakupewa semina yoyote.

Hoja yake iliungwa mkono na Mwenyekiti wa Laac, Vedasto Ngombale aliyesema kamati yake imebaini maofisa wa idara na vitengo kwa baadhi ya halmashauri kutokuwa na uwezo wa kutosha kutekeleza majukumu yao.

“Kamati imeshuhudia wakuu wengi wa idara na vitengo wakishindwa kutoa majibu sahihi na kamilifu mbele ya kamati na kushindwa kuelewa shughuli zinazofanyika ndani ya idara zao,” alisema.

Tuhuma ya Sh10 milioni
Madai ya wabunge wa CCM kupewa Sh10 milioni kila mmoja ili wapitishe Muswada wa Huduma za Habari wa mwaka 2016 na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo kwa mwaka wa Fedha 2017/18, ni moja ya mambo yaliyotikisa Bunge.

Tuhuma hizo ziliibuliwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe wakati akimuuliza swali Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Madai hayo yalisababisha Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa Mwaka 2016, tofauti na miswada mingine ya sheria inayokuja bungeni kutawaliwa na vijembe baina ya wabunge wa upinzani na chama tawala.

Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma ya Jamii, Peter Serukamba alisema hakuna mbunge aliyechangia vifungu vya muswada huo ambaye alilenga katika kupinga vifungu vya muswada huo na badala yake walijikita katika vijembe tu.

“Mkitaka kujua muswada huu ni mzuri sikilizeni, hakuna mtu alipinga vifungu kama yupo mtu asimame wote mliamua kucheza katika siasa tu. Lakini kwa maana ya sheria yenyewe hakuna mtu aliyeweka neno kwa sababu kila kitu kimefanywa,” alisema Serukamba.

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Juliana Shonza alirushiana maneno na Halima Mdee (Kawe – Chadema) aliyemtamkia maneno ‘milioni 10 hizo’ baada ya kuelezea kukerwa kwake na watu wanaoingilia utendaji wa vyombo vya habari.

Kauli moja ya Epa
Kuhusu Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Jumuiya ya Ulaya na Afrika Mashariki (Epa), wabunge wote waliungana kuipinga Serikali wakisema hauna na masilahi kwa Taifa.

Mbunge wa Sikonge (CCM), Joseph Kakunda alisema mkataba huo una kila dalili ya kuirudisha nchi katika ukoloni kwa sababu vifungu vyake kwa zaidi ya asilimia 80 ni vya ukandamizaji.

Spika, Job Ndugai alipigilia msumari wa mwisho aliposema kwamba haufai.

CAG
Pia, wabunge wengi walizungumzia suala la CAG kutengewa kiasi kidogo cha fedha katika mwaka wa bajeti wa 2016/17 jambo ambalo litamfanya akague taasisi chache na hivyo kuwapa ugumu wabunge kuisimamia Serikali.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Novemba 14


ACT-Wazalendo walaani kauli ya Serikali kutowajengea wananchi......Wadai kauli hiyo ni fedheha kwa waathirika na Wadau.

$
0
0
Watanzania wanakumbuka kuwa mnamo tarehe 10 Septemba, 2016 lilitokea tetemeko la ardhi katika eneo la Kanda ya Ziwa na hususan Mkoa wa Kagera.

Tetemeko hilo lilisababisha athari mbalimbali zikiwemo vifo, majeruhi, uharibifu wa makazi na miundombinu ya umma na watu binafsi. Jumla ya Watu 117,721 wameathirika kwa kupoteza makazi yao, mali na athari za kisaikolojia katika Wilaya za Bukoba, Missenyi, Muleba, Karagwe na Kyerwa.

Aidha, jumla ya watu 17 walipoteza maisha na 560 walijeruhiwa. Vilevile, nyumba 2,072 za makazi zilianguka kabisa na nyumba 14,595 za makazi zilibomoka, baadhi zina kuta au kupata nyufa kubwa na hivyo kuzifanya kuwa hatarishi kwa makazi ya binadamu. Vilevile, maafa haya yalisababisha uharibifu mbalimbali wa miundombinu ya barabara na majengo ya watu na taasisi mbalimbali, ikiwemo shule na Hospitali.

Kufuatia maafa hayo, wananchi na taasisi mbalimbali, pamoja na nchi marafiki, waliitikia wito wa kuwasaidia wahanga wa maafa na kukarabati miundo mbinu iliyoharibika. Hadi kufikia mwezi Oktoba, Fedha, Vyakula na Vifaa mbalimbali vya Ujenzi vilikuwa vimepatikana kwa njia ya michango mbalimbali.

Chama chetu kimeshtushwa na kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera kwamba Wananchi walioathirika wajitegemee wenyewe na kwamba misaada yote iliyotolewa Ni ya Serikali na Taasisi zake tu. Kauli hii ya Mkuu wa Mkoa haikubaliki kwani inadhalilisha waathirika na watu wote waliojitoa kuwasaidia waathirika hao.

Tunachukulia kauli hii kama tangazo la wizi wa uaminifu wa wananchi waliochanga. Ni busara ya kawaida kuwa hatua ya kwanza katika kushughulikia maafa ni kurudisha hali ya maisha ya watu katika hali ya kawaida sambamba na ukarabati wa miundombinu. Aidha, suala la ujenzi wa miundo mbinu ya taasisi za umma ni jukumu la msingi la serikali. Kwa sababu hii:

• ACT Wazalendo tunaitaka serikali kuu kujitenga na kufuta kauli ya mkuu wa mkoa wa Kagera kwa sababu inaigombanisha serikali na wananchi inaowaongoza.

• ACT Wazalendo tunaitaka serikali kuelekeza ni misaada iliyopatikana kwa michango ya wananchi, taasisi na nchi rafiki katika kusaidia wananchi walioathirika kurudi katika maisha ya kawaida, ikiwemo ukarabati na ujenzi wa nyumba za kuishi.

• ACT Wazalendo tunatoa wito kwa taasisi za kiraia nchini kuchukua nafasi yake katika kuendelea kuikumbusha serikali wajibu wake wa msingi wa kuboresha maisha ya watu.

Janeth Rithe
Katibu wa Taifa ACT Wazalendo, Kamati ya Maendeleo ya Jamii
13/11/2016, Dar Es salaam.

Hatima ya Dhamana kesi ya Godbless Lema Kujulikana Leo

$
0
0
Wakati Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema (40) akitarajia kujua hatima ya dhamana yake katika Mahakama Kuu leo, kesho yeye na mkewe Neema Lema (33) watapanda kizimbani kwa kesi ya uchochezi dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Ijumaa iliyopita Lema alipelekwa Gereza la Kisongo, Arusha baada ya kunyimwa dhamana katika kesi nyingine ya kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli, hatua ambayo imepingwa na chama chake na mawakili wake.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Calist Lazaro alisema hawakuridhishwa na pingamizi la dhamana lililowekwa na mawakili wa Serikali kwani tayari Lema alikuwa amepewa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi.

 “Tayari tumefanya mazungumzo kuongeza nguvu za mawakili wa chama ambao wataungana na mawakili wa Arusha kudai dhamana leo,” alisema.

Mmoja wa mawakili hao, Shaki Mfinanga alisema leo wanatarajia kuwasilisha maombi ya dhamana ya Lema wakiwa na mawakili wa Chadema.

Kesi ya mkewe
Wakati hayo yakiendelea, kesho Lema na mkewe watakuwa mahakamani mbele ya kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa Arusha, Desdery Kamugisha.

Katika kesi hiyo, Hakimu Kamugisha amewapa dhamana washtakiwa hao katika kesi ya kusambaza ujumbe kumkashifu mkuu wa Mkoa Arusha.

Lema anadaiwa kuwa Agosti 20, 2016 akitumia simu namba 076415**47 ambayo imesajiliwa kwa jina la mkewe, alituma ujumbe kwenye namba ya Gambo 0766 75**75 wenye maneno ya uchochezi.

Maneno hayo; “Karibu Tutakudhibiti kama Uarabuni walivyodhibiti Mashoga” yanadaiwa ya uchochezi kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni za Adhabu, Kifungu cha 118 (a) na Kifungu cha tatu katika sheria iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010.

Katika shtaka jingine, Lema anashtakiwa peke yake, akituhumiwa kivunja Sheria ya Makosa ya Jinai namba 390 kifungu cha 35 kwa kuhamasisha maandamano kinyume cha sheria wakati wa mkakati ulioitwa Ukuta na chama hicho.

Lema alidaiwa kutenda kosa hilo kati ya Agosti Mosi hadi 26 kwa kusambaza ujumbe kupitia mtandao wa WhatsApp wakati akijua kufanya ni kosa kisheria. Katika kesi hiyo, Lema na mkewe wanatetewa mawakili wanne, John Mallya, James Lyatuu, Reygod Nkya na Mfinanga.

Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS ) amtaka Rais Shein asisaini muswada wa mafuta na gesi

$
0
0
Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS ), Omar Said Shaaban amemshauri Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein asiusaini Muswada wa sheria ya mafuta na gesi uliopitishwa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi hivi karibuni kwa madai kuwa unavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Omari ameeleza msimamo huo katika barua yake ya maneno 1,293 aliyomwandikia Dk Shein akifafanua jinsi gani muswada huo unavunja sheria na Rais huyo anavyoingizwa kwenye mtego wa kuvunja Katiba.

Katika barua hiyo, mwanasheria hiyo anasema, “Mheshimiwa Rais, zipo taarifa kuwa unajiandaa kuweka saini kwenye muswada huo uliopitishwa na Baraza la Wawakilishi ili hatimaye iwe sheria. Naomba nikunasihi uachane na mpango huo ili kujiepusha na mtego wa jaribio la kuvunja Katiba.”

Anasisitiza,“Kwa heshima naomba nikueleze kuwa jaribio la Serikali yako na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na hatua yako ya kuweka saini muswada huo ili uwe sheria, ni uvunjaji mkubwa wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo wewe umeapa kuilinda, lakini pia ni kinyume na maelekezo ya sheria inayorejewa kama ndiyo chanzo cha mamlaka ya Zanzibar kutunga sheria yake.”

Mwanasheria huyo anabainisha kuwa kama kweli nia ya dhati ipo ya kuondoa mafuta na gesi kwenye Muungano, hatua pekee na salama kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kusukuma kumalizika kwa mchakato wa Katiba Mpya au kupelekwa mabadiliko ya Katiba Bungeni kuliondoa jambo hilo kwenye Nyongeza ya Kwanza ya Katiba.

Omari alisema akiwa mwanasheria tena kiongozi kwenye kada hiyo, ana wajibu wa kikatiba, kimamlaka na kitaaluma kusimamia ulindwaji na usimamizi wa Katiba na sheria za nchi na akiwa mwenye uchungu na Zanzibar, anapenda kuona ikisimamia rasilimali zake yenyewe bila ya kukiuka masharti ya Katiba.

Alibainisha kuwa katika Katiba ya Muungano kwenye nyongeza ya kwanza, suala la mafuta na gesi ni jambo la Muungano hivyo usimamizi wake na utungiwaji sheria kwa mujibu wa Katiba zote mbili upo chini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 “Hakuna mahali duniani kote ambapo suala lenye misingi yake kikatiba linaondolewa kwa “makubaliano ya viongozi wa wakuu wa Serikali,” anasema.

Donald Trump Akataa Kulipwa Mshahara wa Urais

$
0
0
Rais mteule wa Marekani, bilionea Donald Trump amesema hatakubali kupokea mshahara wa urais pindi atakapokuwa madarakani.

Trump ameweka msimamo huo jana katika mahojiano maalum na mtangazaji maarufu, Lesley Stahl katika kipindi cha 60 Minutes, aliyetaka kufahamu kuhusu uamuzi wake juu ya mshahara wake akiwa ni mfanyabiashara mkubwa.

“Sijawahi kuzungumzia hili, lakini jibu langu ni hapana,” alisema. “Nafikiri inanibidi kupokea kwa mujibu wa sheria $1, kwahiyo ntachukua $1 (Sawa na shilingi 2,200 za Tanzania) kwa mwaka. Lakini hata sijui ni nini,” aliongeza.

Ingawa mtangazaji huyo alimkumbusha Trump kuwa anaiacha $400,000 kwa mwaka, rais huyo mteule alisisitiza, “sitachukua mshahara. Sitapokea.”

Wakati wa kampeni, Trump aliahidi kuwa atajiweka kando na biashara zake endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Marekani, na kwamba atajikita zaidi katika kutimiza ahadi zake kwa Wamarekani. Alisema kuwa biashara zake ataziacha mikononi mwa watoto wake.

Vyoo 100 kujengwa barabara ya Mwanza Kwenda Dar Es Salaam

$
0
0
Taasisi  ya The Desk & Chair Foundation (TD& CF), inatarajia kujenga vyoo 100 katika Barabara Kuu ya Mwanza-Shinyanga-Dar es Salaam unaokadiriwa kutumia Sh. milioni 500.

Mwenyekiti wa TD & CF, Alhaji Sibtain Meghjee alisema hivi karibuni mjini Mwanza kwamba mradi huo ni sehemu ya miradi mitatu mikubwa ambayo taasisi yake inatekeleza nchini.

Alisema baada ya kukamilisha mradi mkubwa wa  jengo la kupumzikia wananchi wanaokwenda kutibiwa na kuwajulia hali wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure wanatarajia kujenga vyoo 100 kwenye barabara ya kutoka Mwanza hadi  Dar es Salaam kwa basi.

Meghjee alieleza kuwa maandalizi ya awali ya mradi huo yameshaanza na kwamba watashirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ili kupata taarifa sahihi kabla ya mradi kuanza.

“Penye nia pana njia, baada ya kukamilisha ndoto yetu, leo ya mradi huu mkubwa wa ujenzi wa jengo la kupumzikia hapa Sekou Toure, tunatarajiwa kutekeleza miradi mitatu mikubwa ukiwemo wa vyoo  kwa ajili ya abiria wanaosafiri kati ya Mwanza na Dar es Salaam:

“Tunataka msamiati wa kuchimba dawa wakati wa safari ubaki kuwa historia kwa hiyo tunatarajia kufanya jaribio moja la kujenga matundu 100 ya vyoo katika njia na barabara kuu ya Mwanza hadi Dar es salaam ambavyo vitagharimu shilingi milioni 500.Tutashirikiana na mamlaka husika, ofisi yako na idara ya afya,”alisema Meghjee.

Meghjee alieleza kuwa taasisi hiyo pia ina mpango wa kutekeleza mradi wa kutengeneza viungo bandia kwa kushirikiana na kitengo cha Jairpur Foot/Knee and Limb Project cha India ambao unahitaji Dola 200,000 za Marekani (sh. milioni 44), zitakazowezesha kuanzisha huduma ya viungo hivyo bandia vya miguu, mikono, fimbo na baiskeli.

Alisema wanaendelea kuwasiliana na wafadhili watakaoshirikiana nao kwenye mradi huo na kuwahakikishia walengwa kuwa viungo hivyo vitapatikana kwa gharama nafuu mara utakapokamilika mradi huo.

Meghjee aliongeza kuwa wakati wakiendesha ujenzi wa jengo la mapumziko katika Hospitali ya Sekou Toure,walipata wazo la kujenga mabanda yatakayotumiwa na madereva wa pikipiki (boda boda) kuegesha vyombo vyao kivulini na kupata huduma ya vyoo na mabafu.

Mwenyekiti huyo wa TD & CF aliongeza zaidi kuwa endapo Halmashauri ya Jiji itaridhia na kuwapa eneo maalumu na mahususi la ujenzi wa huduma hiyo watafanya jaribio hilo moja ili kuweza kuona matunda yake.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images