Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

TFS Yanasa Lori Likisafirisha Mbao Kinyume cha Sheria

$
0
0

______________Na Hamza Temba - WMU________________

Kikosi cha Kufuatilia na Kuzuia Uharibifu wa Misitu cha Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kwa kushirikiana na Kikosi Dhidi ya Ujangili kanda ya Dar es Salaam kimefanikiwa kukamata lori lenye namba za usajili T 676 ANQ lililokuwa likisafirisha mbao kinyume cha sheria huku zikiwa zimefichwa kwa kufunikwa na bidhaa mbalimbali ikiwemo sabuni ili zisionekane kiurahisi kwenye vituo vya ukaguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Afisa Habari wa Wakala huyo, Nurdin Chamuya alisema tukio hilo limetokea tarehe 14 Oktoba, 2016 majira ya saa kumi usiku maeneo ya Amana, Ilala Jijini Dar es Salaam baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema juu ya uwepo lori hilo katika maeneo hayo.

Chamuya alisema baada ya kupata taarifa hizo vikosi hivyo vilifika eneo la tukio na kufanya mahojiano na baadhi ya wananchi waliokuwa karibu na lori hilo ambapo mmoja kati ya wahudumu wa lori hilo alieleza kuwa lori hilo lilitokea Mkoani Kigoma na kwamba lilikuwa limepakia mzigo wa sabuni na chupa za maji zilizotumika. Dereva wa lori hilo hakuweza kupatikana.

“Wahudumu hao walipotakiwa kufungua mlango wa lori hilo kwa ajili ya upekuzi zaidi walisita kwa madai kuwa hawakuwa na funguo za lori hilo, Hatimaye   waliwasiliana na mmlikiwa wa eneo ambaye alikuwa amekabidhiwa funguo kwa ajili ya ulinzi” alisema Chamuya.

Alieleza kuwa mmiliki huyo alipofika alisema, anamfahamu mwenye gari ambaye ndiye mpangaji wa eneo lilipokutwa gari na kwamba anazo taarifa za  gari hilo,  na ameombwa apokee mzigo na kuutunza hadi atakaporudi kutoka safari ya  Mwanza kwa tatizo la msiba wa Baba yake.

Baada ya mmiliki wa eneo hilo kufanya mawasiliano na mwenye gari kuhusu mzigo uliokuwa kwenye gari hilo, mwenye gari alieleza kuwa kwa taarifa za dereva wake na ajenti aliyepakia mzigo Kigoma, gari lake lilikuwa na chupa chakavu na sabuni kutoka Kigoma na hakuna aina nyingine ya mzigo kwa ufahamu wake na akaruhusu gari hilo kufunguliwa mbele ya mwenye eneo.

“Baada ya gari hilo kufunguliwa, kilichoonekana kwa urahisi ni sabuni na mifuko michache inayosomeka kwa nje kuwa ni dawa ya kuku. Baada ya upekuzi ndipo zilionekana mbao zilizokuwa zimefichwa chini ya katoni za sabuni. Tumeshikilia Lori hilo kwa hatua zaidi za kisheria.

“Kufuatia tukio hili, Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania tunatoa onyo kali kwa wale wote wanaojihusisha na vitendo vya uvunaji na usafirishaji wa mazao ya misitu kinyume cha sheria ya misitu namba 14 ya mwaka 2002 pamoja na kanuni zake za mwaka 2004 na kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria za nchi” alisema Chamuya.

Akizungumzia athari mbalimbali za vitendo hivyo vya uvunaji holela wa mazao ya misitu bila ya kufuata taratibu za kisheria za uvunaji endelevu alisema vitendo hivyo vinatishia nchi kuwa jangwa ambapo takwimu zinaonyesha jumla ya hekta 372,000 za misitu nchini hupotea kila mwaka kutokana na matumizi makubwa ya rasilimali hizo ambayo yanazidi uzalishaji wake kwa ujazo wa mita 19.5 milioni kwa mwaka.

Chamuya ametoa wito kwa wananchi wote nchini kushirikiana na Serikali katika uhifadhi na ulinzi wa rasilimali za misitu na kuacha fikra potofu kuwa kazi hiyo ni ya Serikali pekee na taasisi zake kwakuwa faida zake hunufaisha jamii yote na vivyo hivyo kama athari zitajitokeza basi zitaikumba jamii yote bila kubagua.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya Octoba 28

Mafanikio Ya Kiuchumi Kutokana Na Jitihada Mbali Mbali Zilizofanywa Na Serikali Ya Awamu Ya Tano Katika Kipindi Cha Mwaka Mmoja - Benki Kuu Ya Tanzania

$
0
0
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,
alipoingia madarakani mwezi Novemba 2015 aliendeleza jitihada za kukuza uchumi wa nchi yetu kwa kuweka mkazo na kutoa maagizo kwenye maeneo kadhaa yakiwemo; kuongeza nguvu kwenye ukusanyaji wa kodi, kupiga vita rushwa, kuweka msisitizo mkubwa wa nidhamu ya matumizi ya fedha za umma, kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza matumizi katika sekta za vipaumbele vya maendeleo. Aidha, kuzitaka Wizara, Wakala na Taasisi za Umma kuweka fedha zao Benki Kuu na kuhimiza kila mtu afanye kazi na kula kwa jasho lake ili kutekeleza falsafa ya ‘Hapa kazi tu’. 

Maagizo haya yamekuwa kichocheo cha ukuaji mzuri wa uchumi. Kupitia maagizo haya Benki Kuu tunaweza kuelezea mafanikio kadhaa yaliyopatikana katika kipindi hiki kama ifuatavyo;
1.      Kuimarisha ukusanyaji wa mapato, kuziba mianya ya ukwepaji kodi na kuelekeza matumizi katika sekta za vipaumbele vya maendeleo
·         Tangu Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani mnamo Novemba mwaka 2015, makusanyo ya mapato yameendelea kuongezeka. Kwa mfano, kati ya Januari hadi Septemba 2016, makusanyo ya mapato ya ndani yalikuwa shilingi bilioni 11,174 ikiwa ni wastani wa shilingi bilioni 1,241.55 kwa mwezi, ikilinganishwa na wastani wa shilingi bilioni 950.22 katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2015. Makusanyo ya mapato ya ndani katika 2016 yalitosheleza matumizi yote ya kawaida (recurrent) na kubakiza ziada kwa ajili ya ulipaji wa madeni ya nje (amortization) na sehemu kubwa ya matumizi kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Ukuaji wa Pato la Taifa (Real GDP)
·         Uchumi umeendelea kukua kwa kiwango kikubwa kutokana na sera nzuri za uchumi mpana (macroeconomic policies). Kasi ya ukuaji wa pato la Taifa katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016, yaani Januari-Juni 2016, imeongezeka na kufikia asilimia 6.7 ikilinganishwa na asilimia 5.7 kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2015.Ukuaji huu umechangiwa na kukamilika kwa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam na kuanza kutumia gesi katika kuzalisha umeme, usafirishaji, ukiwemo usafiri wa abiria kutumia reli na mabasi ya mwendo kasi (UDART); kuongezeka kwa matumizi ya simu za mkononi, uzalishaji wa gesi, vyuma na bidhaa zisizo za vyuma pamoja na kuimarika na kupanuka kwa huduma za kifedha. Sekta za uchumi zilizoongoza katika kasi ya ukuaji ni usafirishaji (asilimia 17.4), madini (mining and quarrying) (13.7), fedha na bima (asilimia 8.7), uzalishaji viwandani (manufacturing) (asilimia 8.3) na elimu (asilimia 8.0) kutokana na sera ya utoaji wa elimu ya msingi bila malipo iliyoanza Januari 2016. 
Mfumuko wa bei
·         Mfumuko wa bei ulibakia katika kiwango cha tarakimu moja (single digit) kutokana na sera nzuri ya fedha na ile ya bajeti pamoja na kupungua kwa bei za bidhaa duniani kote. Katika mwaka ulioishia Septemba 2016, mfumuko wa bei ulikua kwa asilimia 4.5 ikilinganishwa na asilimia 6.1 kaitka kipindi kama hicho mwaka 2015 na lengo la muda wa kati la asilimia 5.0. Kutokana na sera za uchumi mpana, pamoja na kuimarika kwa shilingi dhidi ya dola ya Marekani na bei ndogo za mafuta katika soko la dunia, mfumuko wa bei unatarajiwa kubakia karibu na lengo la kiwango cha muda wa kati cha asilimia 5.0. 
Shughuli za Serikali
·         Serikali ya awamu ya tano ilianza katika kipindi ambacho upatikanaji wa misaada ya kibajeti (GBS) ulikuwa siyo mzuri kutokana na kubadilika kwa sera za maendeleo za kimataifa (foreign development policies) katIka nchi wahisani ambapo mwelekeo ulikuwa ni kupeleka fedha za miradi moja kwa moja. Pamoja na nchi nyingi wahisani kujitoa katika kusaidia katika bajeti (GBS), Serikali ya awamu ya tano imeweza kushirikiana na wadau wa maendeleo (DPs) katika kutafuta njia mbadala za kuziba pengo hilo.
2.      Uimarishaji Wa Ukusanyaji Wa Mapato Uliendana Na Uimarishaji Wa Mazingira Mazuri ya Kibiashara
·         Sera nzuri za uchumi (macroeconomic policies) za awamu ya tano zimeendelea kukwamua na kuimarisha mazingira ya biashara.  Hii imejidhihirisha katika kuimarika kwa nakisi katika urari wa biashara (current account deficit) katika miezi tisa ya mwazo ya 2016. Nakisi ya urari wa biashara imepungua sana, kufikia dola za Marekani millioni 1,621.8 katika mwezi tisa ya 2016 kutoka nakisi ya dola milioni 3,715.5 katika kipindi kama hicho mwaka 2015. Hii ni kutokana na kuongezeka kwa mauzo ya nje ya bidhaa na huduma (utalii, dhahabu, bidhaa za viwandani), pamoja na kupungua kwa kiwango kikuwa kwa uagizaji wa bidhaa na huduma (mitaji, mafuta, chakula na bidhaa za chakula).
Thamani ya Shilingi
·         Kutokana na sera nzuri za Serikali ya Awamu ya Tano, thamani ya shilingi imebaki kuwa imara (wastani wa shilingi 2,178.6 kwa dola ya Marekani) ikilinganishwa na dola ya Kimarekani na sarafu zingine za nchi jirani na nchi washirika wa kibiashara. Kutokuyumba kwa shilingi kumechangiwa na kuimarika kwa uchumi; kuhamishwa kwa fedha za mashirika ya umma kutoka mabenki ya biashara kwenda Benki Kuu; kupunguzwa kwa matumizi yasiyo ya lazima ya Serikali na kutoterereka kwa Akiba ya Fedha za Kigeni.
Akiba ya Fedha za Kigeni
·         Akiba ya fedha za kigeni imebaki kuwa imara, ikiwa ni dola za Marekani milioni 4,096.0 kufikia mwisho wa mwezi Septemba 2016, ambao ni uwezo wa kutosheleza uagizaji nje wa bidhaa na hudumu kwa kipindi cha miezi 4. Kuongezeka (kutotetereka) kwa Akiba ya Fedha za Kigeni kunatokana na manunuzi yanayofanywa na Benki Kuu kutoka kwenye soko la ndani la fedha za kigeni na mashirika ya umma. 
3.      Kuhamisha Fedha za Mashirika ya Umma kutoka katika Mabenki Binafsi kwenda Benki Kuu ya Tanzania
Serikali ya Awamu ya Tano iliagiza utekelezaji wa Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006, hasa Sura ya 32 inayohusu utunzaji wa amana za mashirika ya umma na taasisi za serikali. Imechukua miaka tisa kuanza kutekeleza masharti ya hiyo kuhusu akaunti za Mashirika ya Umma, Idara za Serikali na Serikali za Mitaa. Kuchelewa huku, kulizifanya benki nyingi za biashara zitumie fedha hizo za umma kununua Dhamana za Serikali na Hati Fungani na hivyo kuifanya Serikali kuuziwa fedha zake yenyewe. Biashara hiyo sasa imekoma kutokana na hatua madhubuti za kuitekeleza sheria hiyo.
Hatua hizo zimewezesha kupatikana na kwa mafanikio yafuatayo:
(a)    Kufungua akaunti za amana za Mashirika ya Umma na Idara za Serikali: Kati ya Novemba 2015 hadi Oktoba 26, 2016, jumla ya akaunti 267 zenye jumla ya amana za Shilingi 206,913,915,522.06 zimefunguliwa. Aidha, baadhi ya taasisi hizo zimefungua akaunti za fedha za kigeni 131 zenye Dola 163,480,125.75, sawa na shilingi 357,694,000,000.00. Hivyo jumla ya amana zote za shilingi na fedha za kigeni za mashirika na taasisi za umma zinazotunzwa Benki Kuu ni shilingi 564,608,460,663.00
(b)   Amana za akaunti za Serikali za Mitaa: Serikali imeamua kufungua akaunti maalum kwa ajili ya kutunza amana za Serikali za Mitaa. Mradi huu umeanza kutekelezwa kuanzia mwezi Aprili 2016 na mpaka sasa jumla ya mikoa mitano imeunganishwa. Mikoa hiyo ni Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya na Mwanza. Mpaka tarehe 26 Oktoba 2016, amana za halmashauri za mikoa hiyo mitano ambazo zipo Benki Kuu ya Tanzania zinafikia kiasi cha shilingi 108,387,942,351.15. Bila kukamilisha sehemu ya mradi huu, fedha hizi zingekuwa kwenye benki za biashara.
Matokeo:
·         Kwa upande Serikali;
·Kumeleta uwazi kuhusu mapato na matumizi ya mashirika hayo
·Kupungua kwa gharama za usimamizi wa ujazi wa fedha (liquidity management) kwenye mzunguko.
·         Kwa mabenki;
·kumeleta usawa katika ushindani kati ya mabenki badala ya wachache kunufaika kwa kupata amana za mashirika ya umma.
·kumeleta ubunifu kwa mabenki katika kubuni bidhaa (bank products) mbali mbali mpya ili kujiongezea amana.
·Kutokana na Sera ya Fedha ambayo ni rafiki, malengo mapana ya Serikali, ukuaji wa uchumi na ukuaji wa fedha ukuwa ndani ya malengo.
·Katika kipindi cha miezi tisa ya 2016, amana katika mabenki ya biashara zimeongeza kutoka asilimi 9.84 katika miezi tisa ya mwanzo wa mwaka 2015 na kufikia asilimia 11.59 kaitka miezi tisa yam waka 2016. Vile vile, riba za mikopo kwa mwaka mmoja zilipungua kutoka wastani wa asilimia 15.49 na kufikia asilimia 13.87
·Mwenendo huu wa riba ulipelekea kupungua kwa tofauti kati ya riba za mkopo na zile za amana kutoka wastani wa asilimia 5.92 ilivyokuwa katika miezi tisa ya mwanzo ya 2015 na kufikia wastani wa asilimia 2.28 katika miezi tisa ya 2016, ikimaanisha kupugua kwa gharama za mikopo.
 
Mafanikio mengine

4.      Mwenendo wa Sekta ya Kibenki

Katika kipindi cha kuanzia Septemba 2015 hadi September 2016, sekta ya kibenki imeendelea kukua ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa taasisi mpya za kifedha ikiwemo Benki ya Waalimu Tanzania (Mwalimu Commercial Bank Plc) na Canara Bank (Tanzania) Limited. Takwimu zinaonesha kuwa mabenki yetu ni imara na salama, yakiwa na mitaji na ukwasi wa kutosha. Kufikia mwezi Septemba 2016, kulikuwa na jumla ya benki na taasisi za fedha zinazosimamiwa na Benki Kuu zipatazo 66 zenye matawi 750 nchini kote, ikilinganishwa na taasisi 62 zilizokuwa na matawi 715 mwezi Septemba 2015.

 Katika kipindi hicho, benki mbili - Guaranty Trust Bank Tanzania Ltd na Yetu Microfinance Bank Plc na taasisi ya fedha moja ya M Mortgages Tanzania Ltd zilipata leseni za muda.
Kiwango cha mitaji kikilinganishwa na mali iliyowekezwa (total capital to total risk weighted assets and off-balance sheet exposures) kilikuwa asilimia 19.24 kikilinganishwa na kiwango cha chini kinachotakiwa kisheria cha asilimia 12. Hali ya ukwasi, ambayo hupimwa kwa kuangalia uwiano kati ya mali inayoweza kubadilishwa kuwa fedha taslimu na amana zinazoweza kuhitajika katika muda mfupi (liquid assets to demand liabilities), ulikuwa asilimia 34.18 ukilinganishwa na uwiano wa chini unaohitajika kisheria wa asilimia 20. 
Mpaka kufikia Septemba 2016, mikopo chechefu ilikuwa wastani wa asilimia 9.06 ikilinganisha na wastani wa asilimia 6.61 ya Septemba 2015. Mikopo chechefu imeendelea kuwa ni changamoto katika sekta ya kibenki kutokana na ufanisi mdogo wa urejeshaji mikopo katika sekta ya kilimo na biashara.
Amana za wateja katika mabenki zilipungua kutoka shilingi trilioni 20.19 mwezi Oktoba 2015 hadi kufikia shilingi trilioni 20.01 mwezi Septemba 2016. Miongoni mwa sababu zilizochangia kupungua kwa amana kwenye mabenki ni pamoja na uamuzi wa Serikali kuhamisha sehemu ya fedha za taasisi na mashirika ya umma kutoka mabenki ya biashara kwenda Benki Kuu ya Tanzania. Aidha, mikopo (loans and overdafts) iliongezeka kutoka shilingi za Kitanzania trilioni 14.48 mwezi Oktoba 2015 hadi kufikia shilingi trilioni 15.74 mwezi Septemba 2016.
Jumla ya rasilimali (Total assets) za mabenki na taasisi za fedha ziliongezeka kwa asilimia 4.71 kutoka shilingi trilioni 26.57 mnamo Septemba 2015 mpaka shilingi trilioni 27.82 mwisho wa Septemba 2016. Kwa kipindi cha miezi tisa kufikia Septemba 2016, jumla ya faida baada ya kodi katika sekta ya kibenki iliongezeka kufikia shilingi trilioni 352.37 ikilinganishwa na shilingi trilioni 344.87 katika kipindi kilichoishia Septemba 2015.
Upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi umeendelea kuongezeka kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya teknolojia katika utoaji wa huduma za malipo ya rejareja kupitia simu za mkononi, pamoja na huduma za kibenki kupitia mawakala (agent banking services). 
Mabenki yameendelea kutumika katika kutunza fedha na mitaji ya wateja na kurahisisha miamala au malipo kwa wateja wake. Ili kulinda maslahi ya wateja na amana zao, Benki Kuu ya Tanzania imeendelea kutunga sheria, kanuni na miongozo inayotumiwa na mabenki na kusimamia utekelezaji wake.
Katika kipindi husika, Benki Kuu ya Tanzania imeendelea na jukumu  lake la kusimamia na kudhibiti mabenki na taasisi za fedha kwa niaba ya Serikali ya Tanzania.  Benki Kuu, imeendelea kuhakikisha kuwa mabenki na taasisi za fedha zina mikakati inayokidhi vigezo muhimu (minimum standards) kwa kupitia ukaguzi wa mabenki unaofanyika mara kwa mara. 
Maduka ya Kuuza Fedha za Kigeni
Idadi ya Maduka ya Kuuza Fedha za Kigeni (bureaux de change) imefikia 290 ikilinganishwa na maduka 266 yaliyokuwepo Septemba 2015. Mpaka kufikia Septemba 2016, maduka yapatayo 260 yalikuwa yanafanya biashara Tanzania Bara na 30 Tanzania Visiwani, ikilinganishwa na maduka 239 Tanzania Bara na 27 Tanzania Visiwani yaliyokuwa yanafanya biashara kufikia Septemba 2015.
Benki Kuu inasimamia  usalama, utulivu na uthabiti wa sekta ya benki Tanzania. Inalinda wateja wanaoweka amana zao kwenye mabenki na taasisi za fedha.  Mabenki yanaendelea kutoa mchango mkubwa kwenye kukuza uchumi wa nchi; kuongeza ushindani kwenye sekta ya kibenki na kuzuia matumizi mabaya ya sekta ya kifedha. Benki Kuu imeendelea kupima ustahimilivu wa mabenki wakati inapojitokeza hali ambayo inaweza kuathiri mapato na mitaji ya mabenki hayo (Stess testing). Pia, husaidia katika kutoa mwelekeo wa Sera ya kifedha nchini.
Sekta ya kibenki imeendelea kushuhudia mabadiliko makubwa katika aina za huduma zitolewazo na katika njia zinazotumika kutoa huduma hizo. Mabadiliko hayo ni pamoja na; Huduma za kibenki kwa kufuata misingi ya Shariah; Huduma za kibenki kupitia wakala; Huduma za kifedha kupitia simu za mikononi na
Benki Kuu imeendelea kusimamia benki mbili za maendeleo (TIB na TADB) ili ziweze kutoa mikopo katika sekta mbalimbali na kuweza kuharakisha maendeleo hapa Tanzania.
Mfumo wa Upashanaji wa Taarifa za Wakopaji
Mfumo wa upashanaji taarifa za wakopaji umeendelea kuleta mafanikio makubwa katika kuboresha upatikanaji wa mikopo kutoka kwenye mabenki na taasisi za fedha zinazosimamiwa na Benki Kuu, pamoja na taasisi nyingine zinazotoa mikopo(SACCOS, MFIs, Utility Companies, Car Dealers na HESLB). 

Mfumo huo unajumuisha utaratibu wa kuweka taarifa za wakopaji kupitia Benki Kuu (Credit reference databank), na makampuni binafsi yaliyoruhusiwa kubadilishana taarifa za wakopaji na mabenki na taasisi nyingine zinazotoa mikopo. Kufikia Septemba 2016 jumla ya wakopaji waliokuwa katika mfumo huo walikuwa zaidi ya 1,600,000 ikilinganishwa na zaidi ya 900,000 ya Septemba 2015.  

Jumla ya mikopo mpaka kufikia Septemba 2016 ilikuwa ni zaidi ya 3,000,000 ukilinganisha na zaidi ya 1,690,000 ya Septemba 2015. Katika taarifa ya mazingira ya biashara (World Bank Doing Business Report, 2017), Tanzania imefanya vizuri kutoka nafasi ya 152 hadi 44 kati ya nchi  190 zilizofanyiwa utafiti huo.
Mifumo ya Malipo Nchini
Benki Kuu imeendelea na kazi yake ya kisheria ya kusimamia mifumo ya malipo nchini ambapo Sheria ya Mifumo ya Malipo Nchini 2015 imeanza kufanya kazi. Chini ya sheria hii zimeanzishwa kanuni mbili za uendeshaji wa mifumo. Kanuni hizo ni pamoja na Kanuni ya Leseni na Vibali kwa Watoa Huduma za Mifumo ya Malipo 2015 pamoja na Kanuni za Kutoa Fedha za Kielektroniki 2015.  Uwepo wa Sheria umeimarisha usalama katika mifumo ya malipo nchini na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa mifumo ya malipo ya taifa.
Kwa kipindi hiki, huduma za fedha jumuishi (financial inclusion) imeongezeka kwa kiasi kikubwa ikichangiwa na usalama uliopo kwenye mifumo ya malipo. Aidha, idadi ya watumiaji wa huduma za fedha kwa njia ya mtandao imeendelea kuongezeka kwa kasi kubwa. 

Kutokana na maendeleo haya, wananchi wamefaidika kwa kupata huduma mbali mbali za kifedha kama vile, kutuma na kupokea, kutunza fedha, huduma za bima, huduma za mikopo midogo midogo. Kadhalika, huduma za malipo ya ada mbali mbali kama vile ada za shule, kodi ndogo ndogo, faini ya makosa ya barabarani na malipo ya huduma kama za maji, umeme na televisheni. Benki kuu inaendelea kushirikiana na wadau wengine wa serikali ili kuahakikisha kuwa mifumo hii ya malipo pia inatumiwa katika kukusanya mapato ya serikali. 
Aidha, kuanzia Februari 2016, Tanzania imekuwa nchi ya kwanza duniani kuweza kufanikisha malipo ya moja kwa moja kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine (wallet to wallet interoperability). Mafanikio haya yatawezesha wananchi kupata huduma za kifedha kwa mtandao kwa urahisi na unafuu zaidi.
Uboreshwaji wa huduma za malipo ya serikali kwa njia ya kieletroniki kama mbadala wa malipo kwa njia ya cheki za serikali, baada ya kuanzisha mfumo maalumu wa malipo ya serikali ambayo unasaidia sasa serikali kulipa mishahara, pensheni pamoja na mirathi bila kutumia cheki. Mfumo huu umesaidia kuleta uharaka na usalama katika malipo ya serikali na kupunguza mianya ya wizi uliokuwa unafanywa na wahalifu kutokana na mapungufu ya mfumo wa utoaji wa cheki za serikali. Aidha ili kusaidia malipo ya mishahara, Benki kuu pia iliongeza kiwango cha ukomo wa malipo kwa njia ya kutumiana kwenye akaunti za kibenki (Electronic Fund Transfer (EFT)) kutoka Milioni Kumi (10,000,000) ya awali hadi Milioni Ishirini (20,000,000/=) ili kuiwezesha serikali kulipa malipo mengi zaidi kwa njia hii.
 
Ili kuongeza matumizi ya malipo kwa njia ya kieletroniki katika halimashauri, Benki kuu iliamua kuunganisha halmashauri kwenye mfumo wa Malipo wa TISS (Tanzania Interbank Settlement System (TISS). Hadi sasa halmashauri zote katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza (isipokuwa Ilemela and Buchosa), Arusha, Mbeya (isipokuwa Busekelo), Dodoma (isipokuwa Kondoa and Chemba) na Songwe (isipokuwa Songwe and Tunduma) zimekwishaunganishwa, pamoja na hazina ndogo zote 24. Hali hii imesaidia kuongeza udhibiti wa malipo ya serikali pamoja na ufanisi katika ulipaji, hali ambayo imesaidia serikili kwa kiwango kikubwa kutekeleza malengo yake.
Katika juhudi za serikali kurahisisha na kuleta ufanisi katika ukusanyaji wa kodi na maduhuli mbali mbali, Benki Kuu imeendelea kufanikisha unganishwaji wa watoa huduma mbali mbali katika mifumo yake ya malipo. Kwenye mfumo wa TACH, Benki kuu imefanikiwa kuongeza Benki nne (4) tangu katika kipindi kifupi ambazo ni TIB Corporate Bank (December 2015), Tanzania Postal Bank (April 2016), Canara Bank Tanzania Ltd (September 2016) na Mwalimu Commercial Bank Plc (October 2016). Aidha, kwenye mfumo wa TISS, Benki Tatu (3) zaidi zimejiunga ambazo ni Canara Bank Tanzania Ltd , Meru Community Bank na  Mwalimu Commercial Bank Plc. Kujiunga kwa Benki hizi kwenye mifumo ya malipo ya Benki kuu, imeongeza wigo wa watoa huduma walio tayari kukusanya mapato ya serikali sehemu mbali mbali.
Ili kuunga mkono juhudi za serikali za kukusanya kodi na mapato mengine, Benki kuu imeongeza muda wa kuendesha mifumo yake ili kuwangezea walipaji muda zaidi wa kufanya malipo kupitia mifumo hii. Muda wa mfumo wa  TISS kufanya kazi umeongezwa kutoka saa 10 jioni hadi saa 2 za usiku. Aidha sasa hivi mfumo huu unafunguliwa pia siku za jumamosi na jumapili kinyume na hapo awali.
Benki kuu imeendelea kushirikiana na nchi nyingine za jumuiya ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla ili kutengeneza na kuendeleza mifumo ya malipo inayovuka mipaka. Mfumo wa malipo wa Afrika Mashariki (East African Cross Border Payment System) umeendelea kuboreshwa ili uweze kutumiwa zaidi na wananchi wanaofanya malipo ndani ya nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki. Katika kipindi hiki, malipo yanayopita kwenye mfumo huu yamezidi kuongezeka, hususa ni yale yanayofanywa kati ya Tanzania na Kenya.
Mifuko ya Udhamini wa Mikopo
Benki Kuu, ambayo ni wakala wa Serikali kupitia Kurugenzi ya Masoko ya Fedha, husimamia Mifuko ya Udhamini wa Mikopo itolewayo na mabenki kwa sekta binafsi pamoja na sekta zinazojihusisha na uzalishaji na uuzaji wa mazao nje ya nchi. Kwa sasa Benki Kuu inasimamia mifuko miwili ambayo ni Mfuko wa Udhamini wa Mauzo Nje ya Nchi (ECGS) na Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo na wa kati (SME-CGS).
Katika kipindi cha Novemba 2015 mpaka Oktoba 2016 dhamana zenye thamani ya:
-          Shilingi 130,867,038,874.85 zilitolewa chini ya Mfuko wa Udhamini wa Mauzo Nje ya Nchi (ECGS). Kupitia mfuko huu, mabenki yameweza kukopesha vyama vikuu vya Ushirika na vya Msingi vinavyojishughulisha na ununuzi wa mazao na pembejeo za kilimo. Hali kadhalika; na
-          Shilingi 918,318,215 zilitolewa chini ya Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo na wa kati (SME-CGS). Mikopo hiyo ilitolewa kwenye sekta za kilimo na ujenzi.
Huduma za Kibenki
Uharaka wa malipo ya mishahara ya wafanyakazi wa serikali: Kwa karibu kipindi cha miezi 11 sasa tangu Novemba 2015, mishahara imekuwa ikilipwa kwa wakati na mara nyingi imekuwa ikilipwa kabla ya tarehe 25 ya mwezi husika ikilinganishwa na siku za nyuma.
Kuchelewa kulipa mishahara kumekuwa kukitokana na uhaba wa fedha hasa baada ya ukomo wa kukopa kufikia mwisho. Hii haikuwa mwenendo mzuri kwani wafanyakazi hawakuwa na uhakika wa siku ya kulipwa mshahara.
Kuongezeka kwa matawi ya Benki Kuu: Moja ya majukumu ya Benki Kuu ya Tanzania ni kusambaza fedha katika matawi yake. Hadi June 2016, Benki Kuu ilikuwa na matawi matano, nayo ni; Mwanza, Arusha, Mbeya, Zanzibar na Dodoma.
Kwa vile Tanzania ina eneo kubwa; shughuli hii imekuwa na changamoto za usambazaji wa noti na sarafu katika maeneo ambayo Benki Kuu haina matawi yake. Ili kukabiliana na changamoto hii Benki Kuu imesaini mikataba na mabenki ya biashara ya usambazaji wa noti na sarafu kama ifuatavyo: -
(i)  Benki ya CRDB katika mikoa ya Mtwara, Kigoma, Sumbawanga, Songea na Tanga
(ii)  NMB katika mkoa wa Tabora
(iii)NBC katika mikoa ya Shinyanga na Bukoba
(iv)  PBZ katika kisiwa cha Pemba
Vituo hivi vyote vimekuwa vikifanya kazi kwa ufanisi; lakini kumekuwa na changamoto mbalimbali; kubwa ikiwa ni udogo wa maghala yake kuhifadhi mahitaji halisi ya noti na sarafu kwa muda muafaka. Hali hii huilazimisha Benki Kuu kupeleka pesa mara kwa mara na hivyo kuongeza gharama za uendeshaji.
Kutokana na changamoto hizi, Benki Kuu imejenga tawi jipya katika mkoa wa Mtwara ambalo limeanza kazi rasmi mefunguliwa tarehe 3 Octoba 2016. Benki Kuu inaamini kuwa tawi hili jipya litakuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi kwenye eneo la kusini mwa Tanzania.
Miradi mikubwa ya viwanda na miundombinu inayoendelea na inayotarijiwa kuanza kazi siku za usoni itachangia katika kuimarisha uchumi.
  1. Ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha  kisasa (Standard gauge)
  2. Ujenzi wa bomba la mafuta la Uganda ambalo litahusu vile vile upanuzi wa bandari  ya Tanga
  3. Ujenzi wa Export Processing Zone ya Kurasini – itakayokuwa mhimili wa biashara kati ya China na Ukanda huu wa Afrika
  4. Mradi wa kuzalisha megawati 240 za umeme wa Kinyerezi II unaoendelea kujengwa.
  5. Miradi ya kupanua viwanja vya ndege nchini kwa mfano- Dodoma, na mingine inayoendelea -katika viwanja vya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya n.k.
  6. Ujenzi wa maghala ya taifa ya kuhifadhi chakula yenye uwezo wa kuhifadhi tani 350 yatakayojengwa kwa msaada wa Serikali ya Hungary katika sehemu mbalimbali nchini hususan katika mikoa inayozalisha mazao ya nafaka kwa wingi.
  7. Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Dangote kilichopo Mtwara ambacho kipo mbioni kuzalisha kulingana na uwezo wake (full capacity);
  8. Kiwanda cha kutengeneza marumaru cha Mkuranga, Pwani ambacho ujenzi wake unaendelea
  9. Kiwanda cha kuzalisha mbolea mkoani Lindi - kinajengwa
  10. Kiwanda cha bidhaa za chuma – mkoani Pwani ambacho kiko mbioni kukamilika.
Hitimisho
Maagizo mbali mbali yaliyotolewa na Serikali ya Awamu ya Tano yamechochea ukuaji wa uchumi katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Mwenendo wa viashiria mbalimbali vya shughuli za uchumi unadhihirisha kwamba hali ya uchumi wa Tanzania ni nzuri na inatoa matumaini makubwa. Matarajio ni kwamba endapo shughuli halali za kiuchumi zitaendelea kutekelezwa, lengo la ukuaji wa pato la Taifa la asilimia 7.2 kwa mwaka 2016 litafanikiwa. Hii inachangiwa pia na ukweli kwamba serikali ya awamu ya tano imejipanga katika kuimarisha uchumi endelevu usiokuwa na mianya ya rushwa; usimamizi thabiti wa rasilimali za umma; na ujenzi wa miundombinu bora kwa lengo la kujenga uchumi wa viwanda chini ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

Taarifa kutoka Ikulu: Rais Magufuli ateua Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC)

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  tarehe 27 Oktoba, 2016 amemteua Bw. Samwel Peter Kamanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC).

Bw. Samwel Peter Kamanga ameteuliwa kushika wadhifa huo kuanzia  tarehe 27 Oktoba, 2016.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Samwel Peter Kamanga alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam


Mfalme wa Morocco aagwa na Rais Magufuli Jijini Dar es Salaam

$
0
0
Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI jana tarehe 27 Oktoba, 2016 ameondoka Jijini Dar es Salaam na kuelekea Zanzibar.

Katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Mtukufu Mohammed VI aliagwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyeambatana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akiwa Jijini Dar es Salaam Mtukufu Mohammed VI aliyewasili nchini tarehe 23, Oktoba 2016 kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli na pia viongozi hao wameshuhudia utiaji saini wa mikataba 21 inayohusu ushirikiano wa Tanzania na Morocco katika masuala mbalimbali ya kiuchumi.

Baada ya kumaliza ziara ya kiserikali ya siku tatu, Mtukufu Mohammed VI anaendelea na ziara binafsi hapa nchini.
 
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Rais Magufuli Akutana Na Kufanya Mazungumzo Na Mkurugenzi Mkuu Wa Mfuko Wa Maendeleo Wa Abu Dhabi Mohamed Al Suwaidi Ikulu Jijini Dar Es Salaam

$
0
0
Mrithi wa Mfalme wa Abu Dhabi na Kaimu Rais, Mtukufu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan amemuahidi Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli kuwa nchi hiyo imedhamiria kuendeleza na kukuza zaidi uhusiano wake na Tanzania hususani katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mtukufu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan ametoa ahadi hiyo kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi Bw. Mohamed Al Suwaidi aliyekutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli jana  tarehe 27 Oktoba 2016.

Mfuko wa maendeleo wa Abu Dhabi unashirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa miradi mbalimbali na katika mazungumzo ya leo Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo ameonesha nia ya kushirikiana zaidi na Tanzania katika maeneo ya ujenzi wa miundombinu ikiwemo reli na barabara, usafiri wa anga na madini.

Pamoja kumshukuru Mrithi wa Mfalme wa Abu Dhabi na Kaimu Rais Mtukufu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan, Rais Magufuli ameialika nchi hiyo kupitia mfuko wake wa Maendeleo na wadau wengine wa maendeleo kuja kuwekeza hapa nchini katika miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa bandari, ujenzi wa viwanda, kilimo, uvuvi, gesi na kushirikiana katika ujenzi wa reli ya kati ambayo itazinufaisha nchi nyingine saba za Afrika Mashariki na kati ambazo hazina bandari.

“Tanzania imeamua kujenga reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) na tayari katika bajeti yetu tumetenga Shilingi Trilioni 1 kwa ajili ya kuanza ujenzi, hivyo tunawakaribisha Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi kushirikiana nasi, wapo wengi ambao wamejitokeza kushirikiana nasi lakini na nyie pia tunawakaribisha, mnaweza kuchukua sehemu ya reli na mkaijenga” alisema Rais Magufuli.

Aidha, Dkt. Magufuli aliutaka mfuko huo kufupisha muda unaotumika katika mchakato wa kuanza utekelezaji wa miradi ili kuharakisha matokeo yake na manufaa kwa wananchi.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

RPC Kinondoni Atoa Tahadhari Kwa Wamiliki Wa Magari Jijini Dar Es Salaam

$
0
0


Na Dotto Mwaibale
WAMILIKI wa magari wametakiwa kuchukua tahadhari ya kuzima na kufunga milango magari yao pale wanaposimama kwa dharura kupata mahitaji mbalimbali ili kuyanusuru kuibwa.

Mwito huo umetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Suzan Kaganda wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu tukio la kuibwa kwa gari la Kapteni Innocent Dallu maeneo ya Mbezi Juu huku akiwemo mtoto wake Lightness.

"Napenda kutumia fursa hii kuwaomba wamiliki wa vyombo vya moto kuchukua tahadhari ya kuzima magari yao na kufunga milango wanaposimama maeneo yoyote kupata mahitaji yao kwani si rahisi kumbaini mhalifu kwani wapo kila sehemu" alisema Kaganda.

Alisema katika tukio la kuibwa kwa gari la kampteni Dallu alikuwa amesimama maeneo ya Mbezi Juu bila ya kulizima akinunua mahitaji ambapo walitokea vijana wakaondoka na gari hilo aina ya Toyota Harrier baada ya kumtelemsha mmoja wa watoto aliyekuwemo ndani ya gari hilo aitwaye Philip huku wakiondoka na mdogo wake Lightness.

Alisema watuhumiwa hao walimtelekeza mtoto huyo maeneo ya Golden Bridge katika baa moja na kisha kuondoka na gari hilo ambalo lilipatikana baada kukamatwa na polisi Kiwangwa mkoani Pwani ambapo kijana mmoja Ezekiel Daud anashikiliwa na polisi kwa mahojiano.

Alisema ni vizuri wamiliki wa magari kuzingatia jambo hilo ili kuepusha matukio kama hayo ambayo yanapoteza muda mwingi wa kuyatafuta kwani tukio kama hilo lilitokea hivi karibuni maeneo ya Kinondoni ambapo wahalifu waliweza kuiba gari aina ya Noah lililosimamishwa bila ya kuzimwa na kuondoka nalo na alijapatikana mpaka leo hii.

Ubalozi wa Papa, Makanisa Yaamua Kujenga ofisi Dodoma

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema amefurahishwa na uamuzi wa Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) wa kutafuta viwanja Dodoma ili wajenge ofisi za makao yao makuu pamoja na makazi ya viongozi wao wakuu.

Ametoa kauli hiyo jana  (Alhamisi, Oktoba 27, 2016) wakati akizungumza na Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya wa Jimbo Katoliki la Dodoma pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kikristo ya Huduma za Kijamii (CSSC), Bw. Peter Maduki ofisini kwake mtaa wa Railway, mjini Dodoma.

“Sina shaka juu ya maombi yenu ya kupatiwa viwanja kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu pamoja na makazi ya viongozi wakuu. Sasa hivi Master Plan ya Dodoma kama Makao Makuu ya nchi inapitiwa upya ili izingatie mahitaji ya msingi sababu zamani ilikuwa haijapangwa kwa mazingira ya sasa ya ujio wa Serikali,” alisema Waziri Mkuu.

Alisema wiki tatu zilizopita alimwagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) ili atafute makampuni yenye uwezo wa kupima viwanja kwa haraka. “Hii itatusaidia kutambua tuna eneo kiasi gani na mahitaji halisi ni yapi na nani akija apewe eneo lipi kulingana na mahitaji yake,” aliongeza.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliyashukuru makanisa kwa huduma za kijamii zitolewazo katika sekta za elimu, afya na kilimo kama ambavyo ameshuhudia katika baadhi ya maeneo alikopita hapa nchini.

Pia aliwakubalia ombi lao la kuwa na kikao cha pamoja baina ya watendaji wa Serikali na makanisa ambacho kitajadili namna ya kuimarisha ubia katika utoaji wa huduma za kijamii hususan za afya na elimu.

“Kikao hiki kitalenga kufanya mapitio ya huduma zinazotolewa baina ya Serikali na Makanisa lakini pia kitatusaidia kupata mrejesho wa mambo yanayofanyika kwenye hospitali na shule mnazomiliki katika maeneo mbalimbali hapa nchini,” aliongeza.

Alisema waharakishe kuleta mapendekezo yao ili kikao hicho kifanyike kabla ya Desemba, mwaka huu kwani kitaisaidia Serikali kupata mrejesho wa kuboresha baadhi ya maeneo katika mwaka mpya wa kielimu unaoanza Januari kila mwaka.

Mapema, Baba Askofu Mkuu Kinyaiya alimweleza Waziri Mkuu kwamba wanahitaji eneo la kujenga ofisi za makao makuu na makazi kwa ajili ya kanisa hilo pamoja na makanisa yaliyo chini ya CCT ambayo kwa pamoja yanaunda Tume ya Kikristo ya Huduma za Kijamii (CSSC). Alisema wanahitaji eneo kwa ajili ya ujenzi wa ofisi na makazi ya Balozi wa Baba Mtakatifu.

Alisema walipowasilisha maombi yao CDA, waliahidiwa kupatiwa eneo la makazi tu lakini bado wanahitaji eneo la ofisi. Pia alitumia fursa hiyo kumshukuru Waziri Mkuu kwa jinsi alivyoiwakilisha Serikali kwenye mazishi ya Mhashamu Askofu Mstaafu, Mathias Isuja wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma ambaye alifariki Aprili 13 na kuzikwa Aprili 20, mwaka huu.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa CSSC, Bw. Maduki alisema katika sekta ya afya hadi kufikia Juni 2016, makanisa yalikuwa yanamiliki na kuendesha hospitali 102, vituo vya afya 102 na zahanati 696. “Kati ya hospitali 102, mbili ni za rufaa za kanda na 38 ni za hospitali teule za Halmashauri za Wilaya na hospitali nyingine 62 zinatoa huduma halmashauri mbalimbali,” alisema.

Alisema karibu asilimia 38 ya hospitali hapa nchini zinamilikiwa na makanisa na nyingi ziko maeneo ya vijijini. Pia alisema kuna chuo kikuu kimoja, vyuo vikuu vishiriki vitatu, na vyuo vya mafunzo ya kati 62 ambavyo vinatoa kozi za uuguzi, maabara na ufamasia.

Kuhusu sekta ya elimu, Bw. Maduki alisema makanisa yanatoa elimu kuanzia elimu ya awali hadi chuo kikuu na kwamba hadi kufikia Juni, 2016, makanisa yalikuwa na shuke za msingi 161, za sekondari 369, na vyuo vya ufundi stadi 126. “Pia tuna vyuo vya ualimu 14, vyuo vikuu tisa, vyuo vikuu vishiriki 17 na vituo vya vyuo vikuu saba,” alisema.

Sumaye kunyang’anywa shamba na serikali, apewa notisi ya siku 90

$
0
0
Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema hati ya shamba lililopo maeneo ya Bunju la aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Fredrick Sumaye liko katika hatua ya kufutwa na kwamba Afisa Ardhi Mteule wa Wilaya ya Kinondoni Rehema Mwinuka ameshatoa barua ya notisi ya siku 90.

Lukuvi ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wandishi wa habari.

“Shamba la Sumaye hati yake iko katika hatua za kufutiwa,
Afisa Ardhi Mteule wa Wilaya ambaye anajukumu la kutoa notisi, ameshatoa notisi kwamba hajaendeleza eneo hilo kwa muda mrefu hivyo kwa mujibu wa sheria hati yake inatakiwa kufutwa,” alisema.

Alisema serikali haitofumbia macho wamiliki wa ardhi na mashamba ambao hawajayaendeleza kwa muda mrefu.

Pia, kufuatia ongezeko la matapeli wanaotumia nyaraka za kughushi za barua za toleo (ofa) zinazodaiwa kutolewa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Lukuvi alitoa agizo hususani kwa wakazi wa jiji hilo wanaomiliki ardhi pasipo kuwa na hati miliki, kujisalimisha kwa kupeleka barua zao za ofa kwa Kamishna wa Ardhi ili wapatiwe hati halali.

“Wamiliki wote wanaomiliki ardhi kwa karatasi za ofa halali wazibadilishie ili wapewe hati halali, na atakaegundulika kumiliki ofa feki polisi watawakamata na kupelekwa mahakamani,” alisema.

Alisema asilimia 60 ya watu wanaopeleka kesi za migogoro ya ardhi wizarani, chanzo cha migogoro hiyo ni karatasi za ofa zinazotoka katika halamshauri za jiji na manispaa.

“Natoa miezi mitatu ili karatasi hizi zisitokee tena kila mtu alete barua ya ofa watapewa hati zao ndani ya mwezi mmoja ,wazilete kwa kamishna wa ardhi wa mkoa, baada ya hapo sitasikiliza malalamiko ya watu walioibiwa ardhi wakiwa na ofa ya namna hii.

“Tumieni miezi mitatu vizuri kubadilisha ofa,” amesema.

Hali kadhalika, Lukuvi alipiga marufuku vitendo vya uvamizi wa ardhi na mashamba vinavyofanywa na baadhi ya wananchi, na kuwataka wananchi kutoa taarifa pindi watakapobaini kuwa kuna shamba au ardhi isiyoendelezwa.

“Serikali ina laani uvamizi wa ardhi na mashamba unaofanywa na baadhi ya wananchi sababu baadhi yao yanamilikiwa kihalali na yana hati, serikali ipo na sheria zipo zitafanya kazi yake,” alisema.

Ripoti ya Mkataba wa Lugumi, Polisi Yafika kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Projestus Rwegasira amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Bunge ya kuhakikisha mfumo wa vifaa vya utambuzi wa alama za vidole unafungwa katika wilaya za kipolisi 108 nchi nzima kwa muda wa miezi mitatu.

Zabuni ya kufunga na kusambaza mashine hizo za utambuzi wa vidole katika Jeshi la Polisi ulifanywa na Kampuni ya Lugumi.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati hiyo Naghenjwa Kaboyoka, aliwathibitishia waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuwa ripoti hiyo tayari imekabidhiwa kwa Ofisi ya Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Kaboyoka alisema ripoti hiyo baada ya kukabidhiwa kwa Spika Ndugai ataipitia na baadaye kuiwasilisha kwa kamati hiyo ya PAC.

Juni 30, mwaka huu, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson baada ya kuahirisha Bunge la Bajeti aliiagiza serikali kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi kwa ajili ya kuwadhibiti wahalifu na kuitaka Kamati ya PAC ifuatilie suala hilo.

Dk Tulia alitoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa yenye utata ya kuhusu zabuni yenye thamani ya Sh bilioni 37 ya kufunga mashine hizo katika vituo vyote vya Polisi baina ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi Enterprises Limited iliyotolewa mwaka 2011.

“Ninashauri serikali ihakikishe mradi huu unakamilika ndani ya kipindi cha miezi mitatu kuanzia leo…, mradi huu utasaidia Jeshi la Polisi kuwatambua kwa haraka watu waliohusika katika matukio ya uhalifu mbalimbali,” alisema.

Katika mkataba huo, Lugumi inatakiwa kusambaza na kufunga mashine hizo za utambuzi wa vidole katika wilaya 108 za kipolisi nchi nzima.

Hata hivyo, mashine hizo zilifungwa kwenye vituo 14 pekee wakati tayari kampuni hiyo ilishapokea kiasi cha asilimia 99 za malipo yake.

Katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka wa fedha 2013/14 ilionesha kuwa pamoja na kampuni hiyo ya Lugumi kulipwa asilimia 99 ya malipo sawa na Sh bilioni 34, bado haijakamilisha mradi huo kwa muda wa miaka mitano sasa.

Aprili, mwaka huu, PAC iliunda kamati ndogo kwa ajili ya kuchunguza mkataba huo wa utata baina ya Kampuni ya Lugumi na Jeshi la Polisi.

Mfanyabiashara Arusha kizimbani kwa kunajisi mwanawe

$
0
0
Mfanyabiashara maarufu jijini Arusha na mkazi wa kata ya Sakina, Alistalius Silayo (45) amefikishwa mahakamani akituhumiwa kumnajisi mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 11.

Akisomewa mashitaka na Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Pennina Joackim ilidai kuwa mfanyabiashara huyo alitenda kosa hilo katika vipindi tofauti kati ya Januari na Septemba mwaka huu.

Mwendesha Mashitaka alidai mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha, Patricia Kisinda kuwa mshtakiwa alikuwa akifanya kosa hilo mara kwa mara katika miezi hiyo eneo la Sakina kwa Iddy yaliko makazi yake.

Alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume cha Kifungu cha 158 Kifungu kidogo cha 1(a) cha Sheria na Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 na kufanyiwa marekebisho 2002.

Baada ya kusomewa mashitaka, mshitakiwa alikana shitaka hilo na hakimu alisema dhamana iko wazi ya wadhamini wawili wanaotambulika kisheria. 

Mbali ya hilo, pia wadhamini hao lazima wawe na mali isiyohamishika yenye thamani ya zaidi Sh milioni 10 na wadhamini hawaruhusiwi kutoka nje ya Mkoa wa Arusha bila ya kibali cha Mahakama.

Hata hivyo, wadhamini hao walishindwa kukamilisha taratibu za dhamana mahakamani hapo na hakimu aliwapa muda kukamilisha taratibu katika saa za kazi na kuamuru mshtakiwa kurudishwa rumande hadi taratibu zitakapokamilika. 

Kesi hiyo itatajwa tena Novemba 10, mwaka huu kwani Mwanasheria wa Serikali alidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Maalim Seif afanya ziara Wilaya zote za Unguja na kuzungumza na viongozi wa CUF......Atoa Maneno Mazito Akiikumbuka Octoba 28 Jecha Alipofuta Matokeo Zanzibar

$
0
0
Wakati leo ni mwaka mmoja tangu matokeo ya Uchaguzi Mkuu Zanzibar yafutwe Oktoba 28, 2015, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amemtuhumu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kuwa ndiye aliikwamisha nchi kwa kupindua maamuzi ya wananchi.

Maalim Seif alisema kutokana na uamuzi huo, ndiyo maana mpaka sasa mwenyekiti huyo ameshindwa kuibuka hadharani akielewa alibeba dhima ya Wazanzibari na Watanzania wote wapenda amani. 

Maalim Seif aliyasema hayo jana alipofanya ziara ya siku moja katika wilaya zote saba za Unguja katika kumbukumbu ya mwaka mmoja, tangu Jecha alipofuta uchaguzi huo.

Maalim Seif aliita siku hii ‘black October’ akisema ndiyo siku Jecha alitekeleza kwa makusudi kufuta ndoto ya Wazanzibari ya kupata viongozi wanaowataka.

“Jecha ndiye aliyesitisha ndoto yetu ya kuwa Singapore, alipindua demokrasia na kufuta matokeo bila ya kuwapo kifungu chochote cha Katiba kinachotoa mamlaka hiyo,” alisema Maalim Seif.

Makamu huyo wa kwanza wa Rais mstaafu, alisema kuwa kabla ya Jecha hajatekeleza azma hiyo ovu, waangalizi wote wa uchaguzi kutoka ndani na nje ya nchi na ZEC wenyewe walijiridhisha na kutoa tamko kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.

Waangalizi hao ni pamoja na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Madola, Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Bara la Afrika (SADC), Umoja wa Ulaya (EU) na Umoja wa Afrika (AU). 

“Nasema alichotekeleza Jecha ni dhuluma na mapinduzi ambayo yalilenga kupindua maamuzi halali ya wananchi wa Zanzibar,” alisisitiza Maalim Seif akiwahutubia viongozi na watendaji wa CUF wa wilaya za Unguja.

Alisema yeye na viongozi wenzake wamekuwa wakiwatuliza wananchi na kwenda nao bega kwa bega, wakielewa hakuna popote umma ulipodai haki yao duniani kwa njia za kistaarabu na za kidemokrasia wakashindwa.

“Hivyo tambueni kuwa kimya kingi kina mshindo na haki yetu iliyoporwa haipo mbali kuipata kwani baada ya dhiki ni faraja,” alisema Maalim Seif.

“Jueni kuwa katika kutekeleza hayo zipo njama za waziwazi za kutaka kuipitisha Katiba ambayo haikupendekezwa na Watanzania kupitia maoni yaliwasilishwa kwa Tume ya Jaji Joseph Warioba,” alisema Maalim Seif.

Maalim Seif alisema miongoni mwa njama hizo ni mazungumzo yanayoendelea sasa kujaribu kuibua utaratibu wa kura ya maoni ili kuipitisha Katiba hiyo, chini ya usimamizi wa ZEC na NEC.

Alisema miongoni mwa njama za kuififisha Zanzibar ni mpango wa utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi na kuwakosesha wananchi fursa ya kufaidi raslimali zao.

Jecha hakupatikana jana kuzungunzia madai hayo, lakini Naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alipoulizwa alisema kwa sasa wapo katika mkakati wa kuimarisha chama katika ngazi zote yakiwamo matawi yao.

“Unajua sisi hatuzungumzii tena hayo, uchaguzi ulikwishafanyika na Serikali ikaundwa na sasa inafanya kazi, la msingi tunaimarisha chetu,” alisema Vuai aliyeko katika ziara ya kichama kisiwani Pemba.

Akizungumza katika ofisi za CUF Wilaya ya Kati Unguja, Maalim Seif alisema, “Nataka nikwambieni kilichotendeka kupitia Baraza la Wawakilishi la Zanzibar hivi karibuni wakidai kujadili sheria ya uchimbaji mafuta, ni kiini macho tu, maana hatujaona mabadiliko yoyote katika Katiba ya Jamhuri tukielewa kwamba jambo hilo bado ni suala la Muungano.”

Maalim Seif alihoji pia uhalali wa tamko la SMZ wa kumzuia asiongee na wananchi misikitini, akisema hiyo ni katika njama za kumnyamazisha asiyaeleze hayo.

Hivi karibuni, Waziri wa Nchi, Ofisi za Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed alipiga marufuku hatua ya Maalim Seif kutembelea na kuongea na wananchi misikitini.

Kufuatia hatua hiyo Maalim Seif alihoji akisema,“Je, Mohamed Aboud haelewi wajibu wake, mbona hatujamsikia akikemea uvunjwaji wa Katiba na pia ukiukwaji wa Sheria Na. 5 ya Vyama Vingi vya Siasa ya Mwaka 1992, inayotoa ruhusa kufanya mikutano na maandamano, hayaoni hayo, hajui kuwa yamepigwa marufuku kinyume na Katiba?” 

Jipatie Dawa Asili ya Kuondoa Michirizi, Kuondoa C hunusi, Kuongeza Unene toka Natural Beauty Product

$
0
0

NATURAL BEAUTY PRODUCT Ni kampuni inayosifika kwa kutoa bidhaa original  zenye matokeo mazuri na ya haraka zaidi bila kemiko wala madhara  yoyote.  tunazo za:-👇👇👇👇
1. Kutengeneza shepu hipsi na makalio kwa:- (a) Vidonge maalum @ 150,000/= (b) Dawa ya kunywa au kupaka @  120,000/=
2. Kupunguza au kuongeza maziwa @ 90,000/=
3. Kushepu miguu kuwa (Chupa ya bia)@ 100,000/=
4. Kubana uke na kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke @ 100,000/=
5. Kuondoa mipasuko au (Michirizi) @ 90,000/=
6. Kuwa softi na mweupe mwili mzima kwa:- (a)mafuta @ 90,000/= (b) Vidonge @ 150,000/=
7. Kuongeza unene wa mwili mzima @ 120,000
8. kupunguza tumbo na manyama uzembe kwa:- (a) Mkanda original wa MICRO COMPUTER @ 150,000/= (b) Mkanda wa kawaida au dawa ya kupaka @ 120,000/= (c)  Dawa ya kunywa @ 100,000/=
9. Kuondoa chunusi na madoa sugu @ 90,000/=
10. Kulefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @ 90,000/=
11. Kuondoa mvi milele na zisiludi tena @ 100,000/=
12. Kuongeza uume na nguvu za kiume kwa:- (a) Gel ya kupaka @ 100,000/=  (b)  Vidonge maalum @ 120,000/= (c)  Mashine original ya HANDSOME UP @ 170,000/=
13. Kuondoa vinyweleo @ 80,000/=
14. kuotesha nywele kwenye kipara @ 100,000/=
15. Kuondoa makovu sehemu yoyote @ 90,000/=
N.K Kwa mawasiliano  piga simu namba 065 9618585 au 0759029968. Popote ulipo utapata huduma zetu pia bidhaa  zetu zote zinagarantii na risiti ili kuhakikisha mafanikio yako karibu sana.
   Follow follow follow
      👇👇👇
@Natural2162
@Natural2162
@Natural2162
@Natural2162
        Kwa wateta wa mikoani tunasafilisha kwa njia ya MABASI nchi za nje tunasafilisha kwa njia ya DHL mzigo unaupata bila tatizo lolote.

Bia Ya Kopo Ya Safari Lager 500ml Yaendelea Kubamba Kitaa

$
0
0
Bila shaka umeshaliona tangazo hili matata kabisa la Safari Lager ukipita Barabara ya Kawawa jijini Dar, wajanja wanakwambia utaalamu uliotumia kutengeneza bango hilo la 3D ni wa hali ya juu sana.


Tangazo hili limekuwa likiwavutia wapita njia katika barabarani hiyo na kuwateka hisia zao, “Dah yaani hili tangazo tu lilivyo linakufanya uitafute bia yenyewe uishushe kinywani” alisikika mmoja wa muenda kwa miguu.

Sasa si tu kwamba tangazo linateka hisia na kuwa kivutio, bia yenyewe ina ladha nzuri ya aina yake na inaleta urahisi na unafuu kwa mtumiaji yeyote wa Safari Lager. Kampuni ya Bia ya TBL ilizindua bia hii ya kopo ya kwanza yenye ujazo wa mililita 500 kwa bia ya Kitanzania mwishoni mwa mwezi wa 8 mwaka huu na hadi sasa imeonekana kuwa kipenzi cha watumiaji katika maeneo mbalimbali nchini.

“Bia mpya ya kopo ya Safari ni dhahiri kwamba imetengezwa kumpa umahiri Mtanzania katika safari ya maisha yake. Inapatikana kwa urahisi na kwa wakati muafaka hata wakati mtu anakwenda kwenye mihangaiko yake au kubeba akiwa anakwenda kwenye matembezi au safarini” alisema Meneja Bidhaa wa Safari Lager, Edith Bebwa
Meneja Bidhaa wa Safari Lager, Edith Bebwa alipokuwa akitambulisha bia mpya ya Safari Lager kwenye kopo la mililita 500 ambayo inapatikana Tanzania nzima.
Baadhi ya wateja wakiwa na nyuso za furaha baada ya kujipatia bia mpya ya Safari Lager katika kopo lenye ujazo wa 500ml

Bia ya Serengeti yasherehekea kutimiza miaka 20

$
0
0
  •     SBL yaizindua bia hiyo katika muonekano mpya
  •     Yashinda zaidi ya medali 10 za ubora wa kimataifa
Dar es Salaam  Oktoba 28, 2016- Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo  imetangaza kuanza kwa sherehe maalumu kuadhimisha miaka 20  tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL)  mwaka 1996. Sherehe hizo zinaambatana na uzinduzi upya wa bia hiyo ikiwa katika muonekano mpya.

Akizungumza  jana jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie, alisema mbali na kuonesha mafanikio ya bia ya Serengeti kwa kipindi cha miongo miwilil iliyopita, kampuni ya SBL itatumia kipindi hiki kuwashukuru wateja  wake na umma wa Watanzania  kwa kuikubali bia ya Serengeti kama chaguo lao la hivyo kuifanya kuwa mingoni mwa bia zinazoongoza hapa nchini.

 “Tunawashukuru  wateja wetu, wafanya biashara, wasambazaji, mashirika ya sekta binafsi, serikali na wadau wote  ambao kimsingi wametusaidia  na kuwa nasi  katika safari yetu hii ya mafaniko,” alisema Weesie.

Bia ya Serengeti Premium Lager ni ya kwanza kutengenezwa kwa kimea kwa asilimia 100hapa nchini ikiwa ni ubunifu wa Mpishi Mkuu mtanzania aitwaye Winston Kagusa  ambaye alichanganya mbinu ya utengenezaji wa bia za kijerumani na  vionjo vya hapa nchinikupata kupata kinwaji hiki kinacopendwa na wengi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu, bia ya Serengeti ilizalishwa kwa mara ya kwanza ikilenga kufikia sehemu ndogo maalumu ya soko lakini azma hii ilibadilishwa na kuzalishwa kwa wingi kutokana na ongezeko kubwa la mahitaji ya bidhaa hiyo jambo ambalo lilisababisha kuanzishwa uzalishaji zaidi katika viwanda vya SBL vilivyoko Moshi na Mwanza.

Aidha Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kwamba katika kipindi chote cha miongo miwili bia ya Serengeti imekuwa na vifungashio vya muonekano tofauti tofauti vinavyoakisi mabadiliko ya kinyakati na mahitaji ya wateja wake. “muonekano mpya tunaouzindua leo hii ni muendelezo wa kielelezo hiki kwamba daima SBL tunajali mahitaji ya wateja wetu na tuko karibu nao, amesema Weesie.

“Tunaona fahari kuzalisha Bia ya Serengeti Premium Lager  katika  ubora uleule wa hali ya juu katika viwanda vyote vitatu, na huu ni uthibitisho halisi kutokana na kutambuliwa  na wateja wetu wa ndani  pamoja na medali  zaidi ya 10  za kutambulika kimataifa  ambazo bia hii imeshinda. Tunaahidi wateja wetu kwamba tutaendeleakuzalisha Serengeti Premium Lager  katika ubora wa hali ya juu  kwa kuzingatia vigezo vya ubora vilivyoanishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO),” alisema Weesie.

Uzinduzi wa muonekano mpya wa  bia ya Serengeti pia umekuja na kauli mbiu mpya wa kinywaji hicho cha “Taifa Letu. Fahari Yetu. Bia Yetu.” Aidha kampuni hiyo imewakaribisha wateja wake na wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na binafsi katika hafla ya maadhimisho ya miaka 20 ya bia ya Serengeti yatakayofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Mkurungezi wa Masoko wa SBL , Cesear Mloka akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa kwa maadhimisho ya miaka 20  tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL)  mwaka 1996.Anayefuatia katikati ni Meneja Masoko wa SBL Anitha Msangi na mwishoni kulia ni Mkurungezi mkuu wa SBL  Helene Weesie.Mkutano huu umefanyika mapema jana katika Hyatt Regency Hotel Jijini Dar es salaam.

Mpishi Mkuu mtanzania  Winston Kagusa aliyefanikiwa kuchanganya mbinu ya utengenezaji wa bia za kijerumani na  vionjo vya hapa nchini kupata  kinywaji hiki  cha Serengeti Premium Lager kinachopendwa na wengi.

 Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie akiongoza katika kuzindua chapa mpya ya Serengeti Premium Lager sherehe ambazo zinaambatana na maadhimisho ya miaka 20 ya bia hiyo kulia kwake ni Meneja Masoko wa SBL Anitha na kushoto kwake wa kwanza ni Mpishi Mkuu wa kwanza wa Serengeti Premium Lager Winston kagusa na mwishoni ni Mkurungezi wa Masoko  Cesear Mloka.Hafla hii ilifanyika katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Mawasiliano, SBL John Wanyacha akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika Mkutano wa waandishi wa habari ambapo Bia ya serengeti premium lager inatimiza miaka 20 toka kuanzishwa kwake na pia kuzinduliwa kwa chapa yenye muonekano mpya.Mkutano huu ulifanyika mapema jana katika hotel ya Hyatt Regency

Waandishi wa habari wakichukua matukio katika mkutano huo



Basi la Hood lagongana na lori na kupinduka kwenye mlima Kitonga

$
0
0
Basi la kampuni ya Hood linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Arusha jana  mchana lilipata ajali na kupinduka katika mlima Kitonga mkoani Iringa baada ya kugongana na lori la mafuta.
 
Katika ajali hiyo mtu mmoja amepoteza maisha na wengine 43 wamejeruhiwa. Kati ya majeruhi hao 25 wapo Hospitali ya Itunda Ilula na 18 wapo katika Hospitali ya Mkoa.

Kauli ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kwa wanaotumia picha zake mitandaoni na kupotosha aliyoyasema

$
0
0
Rais mstaafu kutoka kwenye awamu ya nne ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ameamua kujibu kile kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii katika siku za karibuni.
 
Usiku wa kuamkia leo, kupitia akaunti yake ya Twitter, Rais Mstaafu wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete aliandika masikitiko yake juu ya namna watu wanavyotumia picha zake na kupotosha yale aliyoyasema juzi akiwa chuo kikuu cha Dar es Salaam  ili kufanikisha matwaka yao ya kisiasa.
Aidha, Rais Kikwete aliwataka watu hao kumuacha kwani ameshamaliza muda wake wa uongozi hivyo ni wakati wake sasa kupumzika. 

Rais Kikwete pia alikanusha tuhuma za kuwa  anatofauti na Rais wa sasa Dkt John Pombe Magufuli na kusema kuwa anamuunga mkono Rais Magufuli pamoja na serikali yake.
Kauli ya Rais Mstaafu Kikwete ambayo imekuwa ikipotoshwa mtandaoni ni ile aliyoitoa kwenye  maadhimisho ya miaka 55 ya chuo kikuu cha Dar es Salaam ambapo aliwataka  viongozi wapya kuenzi mazuri ya nyuma akimaanisha kwamba hivi sasa yeye ndo Mkuu wa Chuo hicho(Chancellor), hivyo  akaahidi kuyaenzi mazuri aliyoyakuta toka kwa watangulizi wake

“Ukiwa mpya lazima watu waone una mambo mapya, lakini mapya ya maendeleo," alisema Rais Mstaafu Kikwete na kuongeza; “Sio mapya ya kubomoa ya kule tulikotoka,”

Haijalishi Mtandao Wako Uko Vipi…TECNO Phantom 6 Plus Inatereza Tu

$
0
0
Ukiachilia mbali Tecno Phantom 6 Plus kuwa simu iliyotengenezwa na betri inayodumu kwa muda mrefu zaidi, nikufahamishe kwamba simu hiyo pia ina uwezo mkubwa kwa upande wa intaneti.

Tecno Phantom 6 Plus ina kasi ya hatari unapoitumia kupata mambo mbalimbali au kutazama video mtandaoni. 

Sasa ukiunganisha hili la spidi na uwezo wa kukaa na chaji kwa muda mrefu (Ikiwemo kuchaji kwa haraka) inakuwezesha kuitumia kwa muda wote bila mushkeri wala wasiwasi wa aina yoyote wa kuzimikiwa au kutoweza kuangalia video zako kwa wakati. 
Picha hii inaonesha ni kwa jinsi gani Tecno Phantom 6/+ ilivyo na uwezo wa kuchaji betri kwa haraka ndani ya muda mfupi ikitumia USD Type C

Angalia uchambuzi mfupi kuhusu spidi ya Tecno Phantom 6 Plus kwenye upande wa intaneti na tupe maoni yako kwenye kisanduku cha ujumbe.


Unaweza kutembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya Tecno kufahamu zaidi kuhusiana na Tecno Phantom 6 na Phantom 6 Plus.
 

CHADEMA yapinga kununuliwa na Lowassa, yashindwa kuzungumzia tuhuma za ufisadi.

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema ni uongo na ni propaganda za wapinzani wao kwamba Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa alimhonga Mwenyekiti Freeman Mbowe ili kupata nafasi ya kugombea urais mwaka 2015.

Dkt.  Mashinji ameyasema hayo katika kipindi cha Kikaangoni  kinachorushwa na kituo cha EATV kupitia ukurasa wa facebook ambapo wananchi walikuwa wakimuuliza maswali ya papo kwa papo naye anayajibu.

“Si kweli kwamba Mwenyekiti Freeman Mbowe alimhonga Lowassa ili agombee urais kupitia CHADEMA , ni propaganda zinazoenezwa na wapinzani wetu ili kuwadanganya wananchi” Amesema Dkt. Mashinji.

Amesema Lowassa alijiunga na CHADEMA kwa njia halali kwa mujibu wa taratibu za chama, na maamuzi ya kumteua kugombea urais yalifanywa na vikao halali kuanzia ngazi ya Kamati Kuu hadi Mkutano Mkuu.

Kuhusu sababu za CHADEMA kumkaribisha Lowassa licha ya kumtaja miaka mingi kuwa alihusika na ufisadi, Dkt Mashinji, hakutaka kulifafanua kwa undani, lakini aliishia kusema kuwa wao walijiridhisha kuwa hakuwa na hatia yoyote na kwamba kama kweli alikuwa ni fisadi, basi vyombo vya dola vingemchukulia hatua.

"Kama mtu kweli alikuwa ni fisadi, kwanini hakuwahi kuchukuliwa hatua, hata kufikishwa mahakamani?, nadhani hilo tuliache" Alisema kwa ufupi Dkt Mashinji.

Aidha Dkt. Mashinji amewataka watanzania na wapenzi wa CHADEMA kufahamu kwamba chama hicho hakipo kimya bali kinaendelea na mikakati ya kuhakikisha kwamba kinawafikia watanzania kwa kuwatetea kwa kila hali kutokana na mambo yanayoendelea nchini.

Yanga Wamrejesha Kazini Kocha Wao Hans Van Pluijm Leo .......Wakataa Ombi Lake la Kujiuzulu

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwanachama wa Klabu ya Yanga, Mwigulu Nchemba akiwa katika Mazungumzo na Kocha wa Yanga aliyetangaza kujiuzulu kuitumikia klabu hiyo hivi karibuni, Hans Van Pluijm na kumtaka ajeree kwenye kibarua chake cha kuendelea kukinoa kikosi cha Yanga kinachoshikilia Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images