Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Asilimia 90 ya Wanafunzi kupata Fedha zao za Mikopo Kesho

$
0
0
Wakati baadhi ya wanafunzi wa elimu ya juu wakiendelea kusubiri kupata mikopo yao, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia kesho, asilimia 90 ya wanufaika watakuwa wameshapata fedha zao. 

Majaliwa alisema hayo jana wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). 

“Taarifa niliyonayo ambayo nimepata asubuhi hii (jana), wachache sana wameanza kulipwa jana (juzi), lakini ulipaji utaendelea mpaka keshokutwa (kesho), tunatarajia kufikia asilimia 90 ya wanaostahili kulipwa watakuwa wameshalipwa,” alisema. 

Majaliwa ambaye ni mhitimu wa UDSM, aliwataka waombaji wa mikopo washirikiane na Wizara ya Elimu kwa kutoa taarifa sahihi ili kurahisisha ulipaji.

“Serikali haitavumilia tena ucheleweshwaji wa makusudi  wa malipo ya fedha za mikopo ya chuo. Kama kuna tatizo, taarifa zitolewe haraka ili kuzuia migogoro kati ya wanafunzi na Serikali yao,” alisema.

Alisema upungufu wa wahadhiri waandamizi umesababishwa na masharti ya ajira za mkataba, unaowataka kuwa miaka 65 na maprofesa kuwa miaka 70.

“Hii inaathiri hali ya utoaji wa taaluma kwa fani za ‘Post-Graduates’. Serikali itaendelea kuweka kipaumbele cha upatikanaji wa fedha za kutosha kwa ajili ya mafunzo,” alisema Majaliwa. 

Alisema licha ya juhudi hizo za Serikali, vyuo pia vinatakiwa kuwa na utaratibu wa kurithishana kazi ili kusiwe na pengo katika utoaji wa taaluma pale baadhi ya wahadhiri wanapostaafu.

Majaliwa ambaye pia alizindua kitabu kilichopewa jina la ‘From Lumumba Street to The Upper Hill and Beyond’, alisema Serikali itatoa ushirikiano katika utekelezaji wa mipango ya chuo hicho. 

Akizungumzia kuhusu masilahi  ya watumishi wa vyuo vikuu, alisema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuondoa malimbikizo ya madai kwa watumishi wote wa umma na sasa inakamilisha uhakiki wa taarifa za kiutumishi ili kubaini watumishi hewa.

 “Serikali inaendelea na maboresho na kuimarisha masilahi kwa watumishi wote wa umma kupitia bodi ya mishahara na mara tutakapokamilisha, tutapanga upya mishahara na motisha kwa watumishi,” alisema.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dk Leonard Akwilapo alisema wizara hiyo imetenga Sh9 bilioni kwa ajili ya kufanya ukarabati wa miundombinu kwenye chuo hicho zikiwamo maabara. 

Awali, katika hotuba yake, Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala aliishukuru Serikali kwa kuanza kufanyia kazi baadhi ya changamoto zanazokikabili chuo hicho ikiwamo upungufu wa hosteli za wanafunzi.

Wazanzibari 40,000 Wafungua kesi Mahakamani Kuupinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

$
0
0
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeingia kwenye jaribio jingine, baada ya Wazanzibari 40,000 kufungua kesi mahakamani kupinga uhalali wake. 

Kesi hiyo ilifunguliwa jana katika Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ) na Rashid Salum Adiy kwa niaba ya wenzake 39,999, katika Masijala ndogo ya mahakama hiyo iliyoko jijini Dar es Salaam. 

Wadaiwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Adiy anasema kuwa msingi wa kesi hiyo ni kwamba Muungano huo haukuanzishwa kisheria. 

“Sisi tunadai Muungano huu hauko kwa misingi ya kisheria na kutokana na ushahidi tulionao, uko kisiasa tu na jambo hili linahitaji mfumo na mwenendo wa kisheria kwa kuwa wenye mamlaka ya nchi ni wananchi,” alisema Adiy. 

Alisema kutokana na nyaraka walizonazo wanapinga hati ya Muungano inayodaiwa ilisainiwa Aprili 22, 1964 na wanapinga uamuzi wa Baraza la Mapinduzi kuridhia Muungano huo. 

Wanapinga barua ya Mei 6, 1964, iliyopelekwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), kuelezea kutambuliwa kwa Muungano huo. 

Pia, wanapinga uhalali wa barua ya Novemba 2, 1964 iliyopelekwa UN ikielezea matumizi ya jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria iliyopitishwa na Bunge Desemba 10, 1964 ikielezea matumizi ya jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Adiy na wenzake wanadai kwa kuwa Muungano ni wa kisiasa, ndiyo maana hauwezi kuleta manufaa kwa pande zote mbili hususani uwiano wa kiuchumi na kielimu. 

Baada ya kuwasilisha nyaraka zao wanasubiri kesi hiyo isajiliwe kwa kupewa namba katika Mahakama hiyo na kupangiwa taratibu za usikilizwaji wake. 

Mbali na Wazanzibari 40,000, pia alisema wanayo majina mengine ambayo watayawasilisha mahakamani baadaye, kesi itakapokuwa imeanza

Waraka wa Lowassa: Uchambuzi wa Serikali ya Magufuli mwaka mmoja baada ya Uchaguzi

$
0
0
Tarehe Kama ya leo mwaka Jana, ilikuwa siku muhimu sana kwa watanzania na Mimi binafsi.Niliwaongoza watanzania kupiga kura nikiwa mgombea wa upinzani.

Naamini nilileta sura na msisimko mpya katika siasa za Tanzania.Nilishirikiana na wenzangu kuionesha nchi yetu Demokrasia maana yake ni nini.

Napogeuka nyuma kuingalia siku ile, nasikia faraja kubwa sana hasa kwa jinsi watanzania walivyotuunga mkono na kuonyesha matumaini makubwa kwetu.Ujasiri na ushapavu wa hali ya juu aliyouonesha Mke wangu Regina wakati wa kampeni,ulinipa nguvu kubwa.

Chini ya Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe,tuliendesha kampeni za kiungwana kama tulivyoahidi.Upepo ule ulivuma kwa kasi mpaka visiwani ambako Maalim Seif aliporwa dhahiri ushindi.

Kwa mujibu wa Tume isiyo huru ya uchaguzi, tulishindwa uchaguzi ule.Hatutaki kuendelea kuyalilia maziwa yaliyokwisha mwagika ambayo hayazoleki, lakini kile ambacho tulikisema wakati ule kwanini tunataka mabadiliko,hivi sasa kila mtu anakiona.

Pamoja na mafanikio machache katika baadhi ya maeneo lakini maisha yamezidi kuwa magumu, ajira imeendelea kuwa bomu linalosubiri kulipuka,Elimu bure iliyoahidiwa siyo inayotekelezwa,utumishi wa umma umekuwa kaa la moto,.Nasononeka sana nikiona viongozi wanavyoshindana kuwasweka ndani madiwani na viongozi wengine wa kuchaguliwa hasa wa UKAWA.

Nawashukuru sana wananchi kwa imani kubwa waliyoionesha kwangu na UKAWA kwa ujumla.Kumalizika kwa uchaguzi ndiyo mwanzo wa uchaguzi mwengine, kwahiyo mapambano ndiyo kwanza yameanza.Kasi,nguvu, ari na hamasa niliyonayo ni kubwa zaidi kuliko wakati mwengine wowote.

Baba aua mwanawe kisa kufungua redio kwa Sauti Kubwa

$
0
0
BABA mmoja mkazi wa Kijiji cha Maji ya Moto, Wilaya ya Arumeru mkoani hapa, Wilfred Kivuyo amemuua mtoto wake baada ya kumchoma kisu tumboni, kwa kosa la kufungulia redio kwa sauti ya juu.

Kabla ya tukio hilo inadaiwa yalitokea mabishano ya kugombea kupunguza sauti ya redio kati ya baba na mtoto, ambapo baba aliamua kumchoma kisu tumboni mtoto wake na utumbo kutoka nje.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema, tukio hilo lilitokea Oktoba 23, mwaka huu saa tatu usiku katika Kijiji cha Maji Moto na kumtaja marehemu kuwa ni Abraham Wilfred (22), ambaye kabla ya mauti alikuwa nyumbani akiendelea na shughuli zake huku akiwa amefungulia redio.

Alisema siku ya tukio mtuhumiwa huyo alifika nyumbani akiwa amelewa na kumkuta mtoto wake amefungulia redio kwa sauti ya juu, ambapo alimtaka kupunguza sauti hiyo lakini mtoto huyo aligoma.

“Baada ya hapo mabishano na kutoelewana kulijitokeza baina yao wakaanza kupigana, baba alipozidiwa nguvu na mtoto wake alichomoa kisu cha kukunja kwenye mfuko wa suruali kisha akamchoma tumboni na kumsababisha utumbo kutoka nje.

“Mara baada ya tukio hilo mtoto huyo alichukuliwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa ajili ya matibabu, lakini hata hivyo alifariki wakati madaktari wakiendelea kuokoa maisha yake,” alisema Kamanda Mkumbo.

Kamanda Mkumbo alisema Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka mtuhumiwa huyo ambaye baada ya tukio alikimbia ili hatua zaidi za kisheria zisichukuliwe dhidi yake

Mawaziri Uganda Na Tanzania Watembelea Eneo Litakapojengwa Gati Itakayotumika Kupakia Mafuta Kutoka Uganda Kwenye Meli

$
0
0

Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhandisi Irene Muloni wametembelea eneo la Chongoleani mkoani Tanga ambako kutajengwa hifadhi ya mafuta pamoja na gati itakayotumika kupakia mafuta kwenye Meli mbalimbali ili kusafirishwa.

Mafuta hayo yatapakiwa kwenye Meli hizo baada ya kusafirishwa na Bomba kutoka Hoima nchini Uganda kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi.

Akiwa katika eneo hilo Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda aliwaeleza wananchi wa eneo hilo kuwa nchi ya Uganda inaishukuru Tanzania kwa kukubali Bomba hilo lipite katika ardhi ya Tanzania suala ambalo litakuwa na faida mbalimbali kwa Wananchi ikiwemo mabadiliko ya kiuchumi.

Alisema kuwa lengo ni kuona kuwa mradi huwa huo unaanza kazi mwaka 2020 na ndiyo maagizo ambayo Marais wa nchi mbili wameyatoa kwa watendaji wanaosimamia Mradi huo wa Bomba la Mafuta.

Mhandisi Muloni alitumia fursa hiyo kuwaasa wananchi kujiandaa kikamilifu kwa fursa za kiuchumi kwani watekelezaji wa mradi watahitaji huduma mbalimbali kama za chakula, malazi na usafiri hivyo kupitia utoaji wa huduma hizo wananchi nao watapata kipato.

Pia alizishukuru Sekta Binafsi za Uganda na Tanzania kwa kuwa tayari kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha kuwa mradi huo unafanikiwa akitolea mfano kampuni ya GBP ya Tanzania ambayo imeonesha nia ya kununua hisa katika kampuni itakayoanzishwa kwa ajili ya usimamizi wa Bomba hilo la Mafuta.

Pia alizishukuru kampuni za TULLOW ya Uingereza, CNOOC ya China na TOTAL ya Ufaransa kwa kuamua kutekeleza mradi huo ambao utawezesha jumla ya mapipa laki mbili ya mafuta kusafirishwa kwa siku kupitia Bomba hilo la Mafuta lenye urefu wa kilomita 1443.

Kwa upande Profesa Muhongo alisema kuwa Bomba hilo pia litatumika kusafirisha mafuta kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) baada ya nchi hiyo kugundua mafuta.

Alisema kuwa Waziri kutoka DRC anayesimamia Nishati hiyo amefika nchini ili kufanya mazungumzo na Tanzania juu ya kutekeleza suala hilo ambapo inakadiriwa kuwa nchi hiyo itakuwa ikisafirisha mapipa 30,000 hadi 100,000 kwa siku kupitia Bomba hilo la Mafuta.

Alisema kuwa Gati hiyo ya Chongoleani ina uwezo wa kupakua mafuta kwa muda wa mwaka mzima kutokana na kutokumbwa na mawimbi makubwa ya bahari ambayo hupeleka shughuli hiyo kusuasua.

“ Ndugu zangu shughuli ya upakiaji wa mafuta katika Bandari hii itafanyika kwa muda wa mwaka mzima kwani Bandari hii haina mawimbi makubwa yatakayozuia shughuli hii kufanyika, na ndiyo moja ya vigezo vilivyotumika katika kuchagua Bandari hii kupokea mafuta kutoka Uganda,”alisemaProfesa Muhongo.

Kwa upande wa Wananchi, baadhi ya Wananchi hao walisema kuwa wamepokea mradi huo kwa matumaini makubwa ambapo wamesema kuwa wana imani kuwa mara mradi utakapoanza wataweza kupata huduma mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Miundombinu ya barabara n.k.

Naye Profesa Muhongo aliwaasa wananchi hao kuwa na subira wakati Serikali ikiwa inafanya mipango mbalimbali ili kuhakikisha kuwa mradi huo unafanyika kwa ufanisi.

Tigo Digital Change Makers kutoa $20,000 kwa wenye miradi pevu

Kesi ya uchaguzi meya Kinondoni yapata hakimu

$
0
0
Kesi ya  kupinga uchaguzi wa Umeya na Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni iliyofunguliwa na Chadema katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepangwa  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage na imepewa namba 304 ya 2016.

Katika kesi hiyo Chadema kupitia wakili wake, John Malya wanaiomba  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itengue uchaguzi huo.

Pia wanaomba mahakama iamuru uchaguzi huo uitishwe upya na walipe gharama za kesi.

Walalamikaji katika kesi hiyo ni Mustafa Abdul Muro na Jumanne Mbunju dhidi ya Benjamin Sitta, Manyama Mangaru, Mwenyekiti wa Uchaguzi wa Kinondoni, Msimamizi wa mkutano  huo na Meya na Naibu Meya wa Kinondoni.

Mwanasheria wa chama hicho, John Malya alisema wamefika mahakamani hapo ili kueleza walichokifanya si sahihi na kwamba wamekwenda mahakamani hapo kwa ajili ya kutafuta haki.

Wachina wawili mbaroni kwa kosa la utekaji nyara, Polisi latoa tahadhari kwa wananchi

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewakamata raia wawili wa China kwa makosa ya utekaji nyara mfanyakazi wa kasino ya Le Grande iliyopo maeneo ya Upanga, ambaye pia ni mchina aliyefahamika kwa jina la Liu Hong (48).

Kamishna wa Kanda hiyo, Kamanda Simon Sirro leo amewaambia waandishi wa habari kuwa, wachina hao walimteka Hong na kumfanyia vitendo vya ukatili ambapo walitoa masharti ya kupatiwa dola za kimarekani 19,000 ili wamuache huru.

Kamanda Sirro amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Wang Young Jing (37) na Chen Chung Bao (35).Amesema watuhumiwa hao baada ya kufanyiwa upekuzi katika chumba walichomficha Hong walikuta bomba la sindano, kamba za plastiki ambavyo vinasadikika kutumika kumjeruhi raia huyo wa china.

Amesema baada ya askari polisi kufanikiwa kumuokoa Hong walimpeleka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu.

Aidha, Kamanda Sirro ametoa taadhari kwa wakazi wa Dar es Salaam kuwa makini na raia wa kigeni waishio nchini kwa kuwa baadhi yao hushughulika na uhalifu ikiwemo utekaji nyara.

Amewataka wananchi kutoa taarifa pindi watakapobaini kuwa kuna raia wa kigeni wanaonyanyasa wazawa na kufanya vitendo vya kihalifu.

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Bodi Ya Mikopo Ya Wanafunzi Wa Elimu Ya Juu

$
0
0

Baada ya kukamilisha zoezi la Uchambuzi wa maombi ya Mikopo 88,163 yaliyopokelewa hadi kufikia tarehe 11 Agosti, 2016. Jumla ya Wanafunzi wapya 20,183 wamepangiwa Mikopo. Upangaji huu umezingatia vigezo vilivyomo katika mwongozo wa  utoaji wa mikopo uliopitishwa na Bodi ya wakurgezi na kuidhinishwa na wizaya ya elimu sayannsi na teknoloji. Vigezo hivyo ni pamoja na:
 

 I. Vipaumbele vya  kitaifa vinavyoendana na Mpango  wa Maendeleo  wa Taifa wa Miaka mitano, Dira ya Taifa ya  Maendeleo 2025 na Mafunzo ambayo yatazalisha wataalamu wanaokidhi mahitaji  ya kitaifa katika fani za kipaumbele ambazo ni;
• Fani za Sayansi za Tiba na Afya,
• Ualimu wa Sayansi na Hisabati,
• Uhandisi wa  Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia,
• Sayansi Asilia, na
• Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu.
 

i. Uhitaji wa waombaji hususani wenye mahitaji  maalum kama vile ulemavu na uyatima
ii. Uhitaji wa waombaji wanaotoka katika familia zenye hali duni ya kimaisha
o Wadahiliwa yatima waliopata mkopo -873
o Wadahiliwa wenye ulemavu wa  viungo-118
oWadahiliwa  wahitaji wenye  mzazi mmoja-3,448
o Wadahiliwa wahitaji waliofadhiliwa na taasisis mbali mbali- 87
o Wadahiliwa wahitaji wanaosoma  kozi  za kipaumbele-6,159
o Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi zingine-9,867
Jumla-
20,183                                                                                        


Kiasi cha Fedha zinazohitajika
Bajeti iliyoidhinishwa kwa ajili ya ukopeshaji kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 ni shilingi bilioni 483, kwa ajili ya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 25,717, na wanaoendelea na masomo wapatao 93, 295.
 

Hatua zinazofuata
I. Wanufaika wote wanaopungukiwa na sifa watachunguzwa kwa ajili ya kurekebishiwa au kuondolewa katika unufaika wa mkopo
II. Waombaji waliwasilisha taarifa zenye upungufu, taarifa zao zitahakikiwa, na wakibainika kuwasilisha taarifa za uongo watachukuiwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kufutiwa mikopo yao
III. Wanufaika wote watatakiwa kuhuisha taarifa kwa kujaza dodoso. Taarifa za ziada za kiuchumi za wazazi au walezi wao zitatumika kutanua uhalisia. Wale watakaokutwa na hadhi zisizo stahili, watapoteza sifa za kuendelea kupata mikopo na kulazimika kurejesha kiasi watakachokuwa wamepokea tayari.
 

IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

Msimamizi wa Uchaguzi Bunda Akiri Kukosea Kura

$
0
0
Msimamizi mkuu wa uchaguzi katika Jimbo la Bunda Mjini mwaka 2015, Lucy Msoffe amekiri kufanya makosa ya kuandika idadi ya wapigakura wakati wa kutangaza mshindi wa nafasi ya ubunge.

Akizungumza katika mahojiano na wakili wa upande wa mjibu maombi wa pili, Tundu Lissu katika kesi namba moja ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo hilo inayoendelea mjini Musoma jana, msimamizi huyo alisema siku ya kutangaza matokeo alikuwa hajalala tangu tarehe 24 usiku hadi muda ambao alitangaza matokeo saa 11:11 jioni.

Alisema kutokana na uchovu mwingi ndiyo maana akawa anakosea kuandika idadi ya wapigakura mara mbili mfululizo wakati wa kutangaza mshindi. Sehemu ya mahojiano yao ilikuwa:

Lissu: Ieleze Mahakama kuwa wewe ulikuwa msimamizi wa uchaguzi wa majimbo matatu ya Wilaya ya Bunda, jimbo la Mwibara, Bunda na Bunda Mjini kweli si kweli.

Shahidi: Mheshimiwa Jaji ni kweli.

Lissu: Wewe ulikuwa msimamizi wa majimbo matatu ya uchaguzi katika wilaya hiyo kweli si kweli.

Shahidi: Mheshimiwa Jaji ni kweli.

Lissu: Ieleze Mahakama umeshika nafasi ya ukurugenzi kwa muda gani?

Shahidi: Nimekuwa mkurugenzi tangu mwaka 2007 na nimekuwa mkurugenzi katika sehemu mbalimbali hadi 2016.

Lissu: Ulikuwa msimamizi wa Uchaguzi Mkuu 2015 kwa mara ya pili kweli si kweli?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji ni sahihi.

Lissu: Ni kweli kwamba Jimbo la Bunda lilikuwa na vituo vya kupigia kura 467?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji kumbukumbu yangu ninakumbuka kuwa idadi ya vituo ilikuwa 468.

Lissu: Ni kweli kabisa kuwa baadhi ya vituo hivyo viko visiwani?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji ni kweli.

Lissu: Mweleze mheshimiwa Jaji siku ya tarehe 24/10/205 ulilala saa ngapi?

Shahidi :Mheshimiwa Jaji siku ya tarehe 24/10/2015 nililala saa nane au tisa hivi usiku.

Lissu: Tarehe 25/10/2015 uliamka saa ngapi?

Shahidi: Tarehe 25/10/2015 niliamka saa 11:30 alfajiri Lissu: Tarehe hiyo ulianza kupokea masanduku ya kupigia kura kuanzia saa ngapi?

Shahidi: Nilianza kupokea masanduku ya kupigia kura saa 11:30 jioni hadi tarehe 26/10/2015 saa saba mpaka nane usiku.

Lissu: Ni kweli zoezi la kuhesabu kura lilianza tarehe 26/10/2015 asubuhi?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji, ndiyo zoezi lilianza saa 5:11 asubuhi.

Lissu: Ni kweli zoezi hilo lilienda hadi saa 11:11 jioni?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji ndiyo.

Lissu: Kwenye fomu yako namba 24B ya kutangazia matokeo kuna namba 164,794 imefutwa futwa. Kweli si kweli?

Shahidi : Mheshimiwa Jaji ni kweli.

Lissu: Hiyo namba iko kweli idadi ya waliojiandikisha kwenye daftari?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji ni kweli.

Lissu: Pembeni mwa namba hiyo iliyofutwa kuna namba 69,460 kweli si kweli?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji ni kweli.

Lissu: Shahidi kielelezo P2 kina orodha ya vituo vya kupigia kura uliyowapatia vyama vya siasa kweli au si kweli?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji ni kweli.

Lissu: Kielelezo hicho kilikuwa na idadi ya wapiga kura, kweli si kweli?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji ni kweli.

Lissu: Mwishoni mwa hiyo karatasi uliyoshika kuna idadi ya wapigakura wa jimbo zima la Bunda Mjini wangapi?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji idadi ya wapigakura katika Jimbo la Bunda ni 69,369 .

Lissu: Idadi ya 164,794 ilikuwa ya kimakosa kweli si kweli?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji kweli.

Lissu: Hizo tarakimu zilizokosewa za 164,794 ulizitoa wapi?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji nilizitoa kwenye idadi ya waliojiandikisha kwenye daftari kwenye majimbo matatu.

Lissu: Eleza idadi ya wapigakura kila jimbo.

Shahidi: Idadi ya kila jimbo ilikuwa kama ifuatavyo, Mwibara 59,436, Bunda Mjini 69,369 na Bunda ni 35,898.

Lissu: Jumla yake ni ngapi?

Shahidi: Jumla ni 164,794.

Lissu: Mbona hesabu yako ni tofauti na yangu? Hapa inaonyesha ni 164,703.

Shahidi: Mheshimiwa Jaji labda nilikuwa nimekosea 

Lissu: Ilikuaje ukafuta 164,794 nini kilitokea?

Shahidi: Baada ya kujaza hii fomu na mawakala kusaini hii fomu nilienda kutangaza matokeo na wakati ninatangaza ndiyo wakaniambia kuwa nimekosea na nikafuta.

Lissu: Ulipofuta uliandika namba ngapi?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji niliandika 69,460.

Lissu: Hiyo namba mpya uliyoiandika ya 69,460 vilevile ulivikosea kweli si kweli.

Shahidi: Mheshimiwa Jaji ni kweli nilikosea.

Lissu: Sasa shahidi mueleze mheshimiwa jaji hayo makosa yaliyojitokeza mara mbili katika kujaza fomu yalitokana na nini?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji makosa hayo yaliyotokea mara mbili katika kujaza fomu yalitokana na uchovu niliokuwa nao.

Hadi tunakwenda mitamboni, kesi hiyo ilikuwa inaendelea.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi ya Octoba 27

Aliyejifanya Usalama wa Taifa Ahukumiwa Miaka Miwili Jela

$
0
0
Mahakama  ya Wilaya ya Ilala imemhukumu Seleman Manoti, kifungo cha miaka miwili jela kwa kupatikana na hatia ya kujifanya usalama wa Taifa.

Hata hivyo, mahakama imetoa hukumu hiyo bila mshitakiwa kuwepo mahakamani kutokana na kuruka dhamana kesi hiyo ilipokuwa inasikilizwa.

Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi, Flora Haule alisema kuwa upande wa mashitaka, ulileta mashahidi wanne kwa ajili ya kuthibitisha tuhuma hizo.

Alisema kutokana na ushahidi uliotolewa, mahakama imeridhishwa na ushahidi huo na kwamba mahakama inamtia hatiani mshitakiwa licha ya yeye kutokuwepo.

“Hati ya kumkamata mshitakiwa itolewe na adhabu hii itaanza kutumika pindi mshitakiwa atakapokamatwa kwani alitoroka akiwa na haki ya kusikilizwa,” alisema Hakimu Haule.

Wakili wa Serikali, Ester Kyara aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa iwe fundisho kwa wengine.

Inadaiwa kuwa Novemba 19, 2014 maeneo ya Kariakoo Msimbazi wilayani Ilala, mshitakiwa alijitambulisha kwa Issaya Odelo na Charles Odinga kuwa Ofisa Usalama wa Taifa, kitu ambacho alijua si kweli. 

Katika hatua nyingine, kondakta Ally Salum (23), mkazi wa Mwananyamala, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya kuiba daladala.

Mbali na mshitakiwa huyo, Exavery Kaunga (44) ambaye ni mlinzi na mkazi wa Kiwalani, Minazi Mirefu, aliachiwa baada ya ushahidi dhidi yake kuwa na shaka.

Akitoa hukumu hiyo jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan, alisema kuwa upande wa mashitaka ulileta mashahidi wanne kuthibitisha kosa hilo.

“Nimeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka, nakutia hatiani mshitakiwa kama ulivyoshitakiwa kwa kutumikia kifungo cha miaka mitano jela,” alisema Hakimu Hassan.

Kabla ya kutolewa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali, Grace Mwanga aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa wengine. Hata hivyo, mshitakiwa alipoulizwa ni kwa nini asipewe adhabu kali, hakujibu chochote na mahakama kutoa adhabu hiyo.

Washitakiwa hao walishitakiwa kwa makosa mawili ya kula njama kutenda kosa ambapo inadaiwa kati ya Julai 5, mwaka jana, washitakiwa walikula njama kutenda kosa.

Pia inadaiwa Julai 5,2015 pembezoni mwa barabara ya Nyerere katika Kituo cha Mafuta cha Victoria, washitakiwa waliiba gari lenye namba za usajili T 624 CSH aina ya Eicher mali ya Kampuni ya White Swan.

Kigogo wa Jeshi la Polisi Ashushwa cheo....Mwingine Atimuliwa

$
0
0


Mkuu wa jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu
Jeshi la Polisi limemvua cheo mkuu wake wa kituo cha Himo (OCS), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Zuhura Suleiman kwa tuhuma za kukutwa na gari la wizi aina ya Toyota Rav4. 

Pia, jeshi hilo limemfukuza kazi kwa fedheha (kwa kutolipwa haki zozote) ofisa wake mwingine wa cheo cha koplo, Federika Shirima ambaye naye anatuhumiwa kukutwa na magari mawili yaliyoibwa jijini Dar es Salaam. 

Hatua ya jeshi hilo dhidi ya askari wake imekuja siku chache baada ya kufichuka kwa tuhuma hizo ambazo zilionekana kulipaka matope. 

Alipohojiwa na wanahabari Jumatatu iliyopita kuhusu tuhuma za kukutwa na gari hilo lililoibwa pia Dar es Salaam, ASP Zuhura alikanusha na kusisitiza kuwa hazijui. 

“Hiyo taarifa (ya gari) mbona siijui. Hakuna taarifa kama hizo,” alikanusha taarifa hizo ambazo baadaye zilithibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa ambaye alikiri maofisa wake kukutwa na magari hayo, lakini akasema hawawezi kupewa adhabu kabla ya kuthibitika kuwa amefanya uhalifu.

“Makachero wetu wanashirikiana na kikosi kazi cha Dar es Salaam na watakapobainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,” alisema. 

Taarifa zilizopatikana jana zilisema, ofisa mwenye cheo cha koplo alisomewa barua ya kufukuzwa kazi juzi jioni na muda huohuo na ASP Zuhura naye akasomewa barua ya uhamisho. 

“Kwa cheo cha ASP mamlaka yake ya nidhamu ni katibu mkuu kwa hiyo kilichofanyika ni kumuondoa kwenye wadhifa wa OCS akisubiri uamuzi mwingine kutoka juu,” kilidokeza chanzo chetu. 

ASP Zuhura alipotafutwa kwa simu jana ili kuzungumzia suala hilo hakupokea, lakini Koplo Federika alipopigiwa alipokea na kukana kufukuzwa kazi kisha kukata simu. 

Kamanda Mutafungwa alipopigiwa simu alitaka atumiwe ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) na alipotumiwa na kuulizwa kuhusu suala hilo, hakukanusha wala kuthibitisha zaidi ya kujibu atafutwe leo saa 5:00 asubuhi. 

Kukamatwa kwa maofisa hao kulitokana na kutajwa na mtandao wa wizi wa magari jijini Dar es Salaam uliokuwa mikononi mwa polisi, ambao walisafiri hadi Himo na kuyakamata. 

Akizungumza jana katika mkutano na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema mtandao huo umekuwa ukipeleka magari ya wizi Arusha na Moshi. 

Credit: Mwananchi

Maagizo 10 ya Makamba kwa uongozi wa mkoa wa Katavi baada ya kukamilisha ziara

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba ameendelea na ziara yake katika Mkoa wa Katavi kwa kutembelea kijiji cha Kabege ambapo aliangalia mradi Mkubwa wa Umwagiliaji wa Mwamkulu katika Manispaa ya Mpanda ambao kwasasa umesitisha kutoa huduma zake kwa kukosekana kwa maji ya kutosha katika Mto Katuma.

Katika kikao cha Majumuisho ya Ziara yake ya siku mbili katika Mkoa wa Katavi, Waziri Makamba ameutaka uongozi wa Mkoa huo kudhibiti yafuatayo:

1. Ongezeko la watu na mifugo ambayo kwa kiasi kikubwa inachangia uharibifu wa mazingira.

2. Kusitisha uchepushaji kwa Mto Katuma ambapo taarifa ya Mkoa ilieleza kuna jumla yamabanio 40 ambayo yanatumiwa na watu kuchepusha maji kwa ajili ya manufaa yao binafsi.

3. Uchimbaji hatari wa Madini usiofuata taratibu

4. Kuhuisha sheria ndogo ndogo za mazingira katika ngazi mbalimbali za Serikali za mitaa

5. Kuanisha maeneo maalumu ambayo yatatangazwa katika Gazeti la Serikali kama mazingiranyeti ili kuyapa ulinzi zaidi

6. Kusimamia uondoshwaji wa wavamizi katika Vyanzo vya maji

7. Kufanyika kwa sensa ya mifugo ili kujua Mkoa una mifugo kiasi gani na kubuni namna boraya kuhumudimia mifugo hiyo bila kuathiri mazingira

8. Ameahidi kuaanda andiko maalumu la Mradi wa Ziwa Katuma

9. Mmiliki wa Jema Sitalike Project kutafutwa popote alipo, leseni yake ya madini isitishwe,apigwe faini na kurekebisha eneo alilokuwa akitumia awali kwa shughuli za uchenjuaji wadhahabu.

10. Waziri Makamba meagiza Watendaji kata na Vijiji kutotoa vibali vya uchimbaji wa madini bila kufuata utaratimu wa Wizara ya Nishati na Madini.

Aidha Waziri Makamba amewasili Katika Mkoa wa Kigoma na kutembelea kiwanda cha Nyanza Mines nakuwapongeza kwa kuzalisha chumvi kwa kutumia nishati ya jua ambapo awali kiwanda hicho kilifungiwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutokana na uharibifu wa Mazingira kwa kutumia magogo mengi mwaka 2015. Kiwanda hicho kwa sasa kinazalisha tani 20,000-25,000 ndani ya miezi mitatu.

Mchungaji Rwakatare Kuwatoa Wafungwa Wengiine 43 gerezani kwa Kuwalipia Faini Zao

$
0
0

Mchungaji  Kiongozi wa Kanisa la Assemblies of God (Mlima wa Moto), Getrude Rwakatare amesema ataendelea na mpango wake wa kuwanusuru wafungwa wanaotumikia adhabu magerezani kwa kuwalipia faini ili warejee uraiani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, alisema katika awamu ya pili ameamua kuwalipia wafungwa 43 waliopo katika magereza ya Mkoa wa Dodoma.

“Kampeni hii ya kuwalipia faini kati ya Sh 50,000 hadi 200,000 wafungwa waliopo magerezani imetupa moyo na Watanzania wengi wameguswa na hata kutupongeza. Kutokana na hali hii kanisa letu sasa limefanya hivyo tena na safari hii tunaelekea mkoani Dodoma,” alisema.

Mchungaji Rwakatare alisema kesho watawatoa wafungwa hao mkoani Dodoma ambapo vigezo walivyoangalia ni wanawake wanaonyonyesha, wagonjwa na wazee.

“Nasi tunatimiza maandiko ya Mungu katika kufanya hivi na kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa Parole, Augustino Mrema,” alisema Mchungaji Rwakatare.

Alisema kutokana na makosa mbalimbali ya faini waliohukumiwa nayo wafungwa hayo, kanisa lao limetoa Sh milioni 6.8 kwa ajili ya kulipia faini hizo.

Awali Rwakatare kupitia kanisa lake, aliwalipia wafungwa 78 katika magereza matatu ya Keko, Segerea na Ukonga ya jijini Dar  es Salaam na kuachiwa huru baada ya kulipa faini ya Sh milioni 25 zilizochangwa na waumini wa kanisa hilo.

Madudu Kibao Yaibuliwa Mradi wa NSSF Kigamboni

$
0
0

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limekiri kuwapo ubadhirifu kwenye mkataba wa ubia na Kampuni ya Azimio Housing Estates iliyotakiwa kuendeleza ekari 20,000 za ardhi Kigamboni na kuna hatari ya kupoteza Sh bilioni 270.

NSSF pia imekiri ubadhirifu katika utoaji mikopo kwenye Saccos mbalimbali nchini ikiwamo ya Bumbuli, inayoonekana kukopeshwa zaidi ya Sh bilioni mbili, bila kuwa na sifa huku kukiwa pia hakuna kumbukumbu ya mwaka mzima kama walirudisha mkopo wa awali.

Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF, Profesa Samuel Wangwe alieleza jana mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kwamba Bodi yake ilipoingia madarakani iligundua ubovu wa mkataba huo na kusitisha kutoa fedha na sasa inaangalia namna ya kujitoa bila kupoteza fedha zilizowekezwa.

Alisema uwekezaji huo ambao ardhi ya mwekezaji ilipaswa kuwa ekari 20,000, hatua ya awali ulipaswa kuanza na ekari 300, lakini uchunguzi uliofanyika hivi karibuni ulionesha kuwa kuna ekari 3,500 pekee hali inayoonesha udanganyifu uliofanyika tangu awali.

Pia mwekezaji huyo alidanganya uhalisia wa bei ya ardhi hiyo, kwani alionesha kuwa thamani ya ekari ya moja ni Sh milioni 800 wakati kiuhalisia, ardhi hiyo thamani yake ni Sh milioni 25 peke yake.

Mwenyekiti wa PAC, Naghenjwa Kaboyoka alisema imekuwa vigumu kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)  kuthibitisha uwepo wa viwanja hivyo kwa kukosekana hatimiliki, umiliki wa ekari 19,700 za ardhi ambazo ni sehemu ya mtaji wa Azimio Housing Estates kwa asilimia 20, hivyo fedha za NSSF zinakuwa kwenye hatari ya kupotea.

Alisema NSSF ambayo inamiliki hisa ndogo kuliko Azimio, imewekeza fedha nyingi, zaidi ya dola milioni 129 za Marekani wakati mbia huyo aliwekeza dola milioni 5.5.

Akijibu hoja za Mwenyekiti huyo, Profesa Wangwe alisema mradi huo   ulisimama tangu Februari kutokana na mbia kukosa fedha na kwamba hakopesheki kwani NSSF inamdai.

Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige alisema mradi huo wa Kigamboni ni mchafu na katika mazingira hayo ambayo Bodi pia imeshituka kuwa   mchafu hivyo ni vema NSSF ingejitoa kuliko kuendelea na mkataba mbovu.

“Ni vema ukishagundua kuwa unachezea kitenesi kichafu ambacho kilianza kuchezewa na watu ambao wameshaondolewa, usiendelee kucheza na mtu yule yule ili asije kukuingiza katika matatizo makubwa zaidi,” alisema Maige.

Profesa Wangwe alisema ni vigumu kujitoa haraka kwenye mkataba huo, kutokana na fedha nyingi waliyowekeza ambayo iko hatarini kupotea na kwamba ardhi yote ni ya mwekezaji huyo hivyo wanatafuta namna ya kurudisha fedha waliyowekeza hata kama haitakuwa na faida.

Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aesh Hilaly alihoji kama mkataba unaruhusu mwekezaji huyo kukopa ili kuendeleza mradi huo.

Mkurugenzi wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara alisema mwekezaji huyo alitaka kukopa NSSF ili aendeleze mradi huo ambao umesimama lakini hakopesheki kwa kuwa anadaiwa.

Hata hivyo, baadhi ya wabunge walihoji uhalali wa Saccos kukopeshwa mara mbili kwa mwaka, huku zingine zikikosa mikopo na vigezo vilivyotukia katika kutoa mikopo hiyo.

Kuhusu Saccos ya Bumbuli, Kaboyoka alisema mbunge wake anafahamika, hivyo inashangaza ipewe fedha hizo kwa mwaka mmoja na kuhoji sifa zilizotumika kuzitoa wakati Saccoss zingine hazijapata.

Alisema ni vema ufanyike ukaguzi maalumu kwenye Saccos hiyo kwani fedha hizo ni mafao ya wafanyakazi ingawa pia inatia shaka katika utoaji, kwani awali Saccos hiyo ilipewa zaidi ya Sh bilioni moja na kwamba hesabu hazioneshi, kwamba fedha hizo zilirejeshwa, lakini ndani ya mwaka mmoja ikapewa fedha zingine.

NSSF ilitoa mikopo kwa Saccos tisa kwa kiasi kinachozidi asilimia 50 ya thamani ya mali za Saccos husika, kinyume na sera ya Shirika ya kukopesha na ziliomba kiasi ambacho hazikustahili.

Katika ripoti ya CAG mbali na Bumbuli, Saccos zingine zilizopewa fedha nyingi ni Korongo Amcos, UMMA, SBC, Hekima, Ukombozi, Uzinza, Harbour na Umoja.

Akijibu hoja hizo, Profesa Wangwe alisema Saccos zilizopewa fedha zaidi ya mara mbili kwa mwaka ikiwamo ya Bumbuli iliyopewa Sh bilioni 2.473 kwa mwaka 2014/15, wakati anaingia kwenye nafasi hiyo, aliliona hilo kama tatizo hivyo kuagiza kufanyike ukaguzi maalumu.

Alisema waliokuwa wanasimamia Saccos hizo walisimamiswa kazi tangu Bodi mpya ilipoingia na kwamba walisitisha kutoa mikopo ya aina yoyote katika Saccos zote nchini, hadi uongozi wa Shirika utakapoanzisha utaratibu mpya.

“Watu wote waliohusika na ubadhirifu wameshaondolewa ofisini, tulishituka kuona namna fedha hizo zilivyotolewa, si zote zilizofika kwa wahusika, zingine ziliishia kwenye mikono ya watu, tuliona ni vema ufanyike ukaguzi maalumu,” alisema Profesa Wangwe.

Sakata la posho za madiwani Arusha laibukia bungeni

$
0
0
Sakata la posho za madiwani wa Jiji la Arusha bado halijapoa, baada ya Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini kuliibulia katika Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), akisema linakwamisha ukusanyaji wa mapato. 

Sakata hilo liliibuka jana wakati kamati hiyo ilipokuwa ikipitia na kuhoji hesabu za halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2014/2015. 

Mbunge huyo alisema halmashauri hiyo imekata posho kwa madiwani na watendaji na kuzipeleka fedha hizo kwa walimu, jambo ambalo linawavunja moyo wawakilishi hao wa wananchi kutimiza majukumu yao. 

“Madiwani ndiyo wanawasaidia kuwahamasisha wananchi katika ukusanyaji wa mapato na hao mnawavunja moyo. Mkurugenzi hamuwezi kufikia malengo kama mtakuwa watendaji peke yenu,” alisema Selasini. 

Alisema halmashauri hiyo ikimaliza mvutano huo inaweza kuongeza mapato kutoka Sh12 bilioni hadi Sh18 bilioni na kujiendesha bila kutegemea ruzuku. 

Mbunge huyo alisema katika halmashauri zote nchini hakuna diwani anayelipwa posho ya Sh10,000, kwa nini madiwani wa jiji hilo pekee walipwe kiasi hicho. 

Akijibu hoja hiyo, mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Athuman Kihamia alisema hakuna diwani anayelipwa kiasi hicho cha fedha na kwamba, madiwani wote wanalipwa posho ya Sh40,000 kwa mwezi na nauli Sh10,000 kulingana na kanuni walizokubaliana mwaka 2003. 

Alisema madiwani hao walikuwa na posho zipatazo tano ambazo ni nauli, kujikimu, vikao, madaraka na mawasiliano.

Pia, Kihamia alisema walikuwa wakilipwa Sh150,000 za mafuta kinyume na kanuni walizokubali kuzitumia za mwaka huo. 

“Siwezi kurudia makosa kwa kulipa fedha zisizofuata kanuni na utaratibu, maana mtakuja kunihoji hapa kwa nini nimezilipa,” alisema. 

Mbunge wa Kwela (CCM), Ignas Malocha alimpongeza mkurugenzi huyo kwa kufuata misingi na utaratibu wa kanuni na sheria katika uendeshaji wa jiji hilo.

 Akizungumza nje ya kamati hiyo, Meya wa jiji hilo, Calist Lazaro alitaka liachwe lijiendeshe lenyewe bila kuingiliwa.

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 77 & 78 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

$
0
0
Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa

ILIPOISHIA
Nikiendelea kuitadhimini barabara hii, gafla nikastukia kuliona gari la mbele yetu, nikinyanyuliwa hewani na kitu kama bomu kutegwa, likazunguka hewani mara kadhaa na kutua chini, kitendo kilicho mfanya dereva wetu kufunga breki za gafla, zilizo lifanya gari kuserereka na kuligonga gari lililo anguka na kulisukumia bondeni, kwenye korongo refu, huku matairi ya mbele ya gari letu yakianza kutangulia kwenye korongo, huku ya nyuma yakijitahidi kubaki barabarani.

ENDELEA SASA
Macho yangu yote, yakahamia kwenye gari inayo kuka nyuma yetu kwa kasi kubwa, huku dereva wake akijitahidi kufunga breki zake, akitumia juhudi zake zote

Nikajiluta nikiyafunga macho yangu, kwani kitu kinacho fwata sekunde chache, ni dereva huyo, kutusindikiza kwenye korongo kama alivyo fanya dereva wetu, kwenye gari lilil kua mbele yetu.
Dakika kama mbili, hivi niliendelea kusikilizia ni nini kitatokea, kwetubila haikuwa hivyo. Mwanga mkali wa taa za gari lililo kua nyuma yetu, ukaendelea kunipiga machoni, ni sentimita chache sana, toka lilipo simama gari lililopo nyuma yetu, huku gari letu, likianza kunesa taratibu.

"Tutulie hivi hivi"
Dereva alizungumza huku akihema sana, askari walio kwenye magari ya nyuma wakashuka kwa haraka, kwenye magari yao, wakaja nyuma ya gari letu na kuanza kujitahidi kulivuta kwa nyuma. Kutokana na uzito wa gari ikawa ni kazi ngumu sana kwao kulivuta. Ikawalazimu kulishikilia na kutuomba tushuke haraka.

Sikutaka nipoteze muda, nikaufungua mlango wa nyuma katika siti niliyo kaa na kutoka nje haraka iwezekanavyo, huku walinzi nilio kua nao ndani ya gari wakitokea kupitia mlango nilio pitia mimi.
Walinzi wakaliachia gari, likaporomoka kwenye korongo. Nikiwa ninatazama huku na kule, nikawaona watu wakiwa juu kidogo ya mlima wakijipanga kwa ajili ya kufanya shambulizi
"Shitiii"
Bila hata ya kuomba, nikachomoa bastola moja ya mlizi aliyo ichomeka kiunoni mwake. Nikafyatua risasi mbili kwa jamaa aliye shika bunduki aina ya 'Snaiper' ambayo ni hatari sana, kutokana na uwezo wake mkubwa.

  Mashambulizi yakaanza rasmi, na watu hawa ambao ndio walio tegesha bomu barabarani. Ikawa ni ambushi moja ambayo hakuna aliye itarajia kama inaweza kutokea kwa wakati huu, askari wawili wakapigwa risasi na kufa hapo hapo.
"Gari la balozi ni lipi?"
Nilimuuliza mlinzi mmoja, niliye simama naye karibu, tukiendelea kujibu mashambulizi ya wavamizi hawa, ambao wanapig a risasi kama wendawazimu

"Lile la mwisho"
"Nilinde"
Jamaa akaendelea kuwafyatulia majambazi risasi, huku mimi nikikimbia pembezoni mwa kuta ya mlima huu, jambo lililo gumu kwa majambazi kuweza kuniona. Nikafika lilipo gari la balozi, nikamkuta akiwa ameinama kwenye siti yeye pamoja na wanae, wakimuomba Mungu wao
"Muheshimiwa unaniamini?"
Nilimuuliza balozi mara baada ya kuingia ndani ya gari na kukaa, katika siti ya dereva.

"Ndio nakuamini."
Kutokana gari halikuzimwa, likanirahisishia wepesi wa kufanya jaribio la kumuokoa balozi pamoja na familia yake. Nikaangalia upenyo ulio achwa na gari, lililo simaba barabarani, nikaamini unanitosha kupita.
Mlinzi akanipa ishara nipite, yeye anaendelea kupambana na wavamizi hawa. Nikafanya kama alivyo agiza, kalilazimisha gari kupita kwenye uwazi wa gari lililopo barabani, chakushukuru Mungu likapita, ikawa kazi ni kwangu kuhakikisha ninasonga mbele.

Japo kuna risasi kadhaa zilipigwa kwenye gari letu, ila hapakuwa na iliyo adhiri matairi zaidi ya kuvunja vioo vya pembeni. Kwa mwendo kasi wa gari hili, ulinifanya niwe makini kwa kila kona ninayo kunja barabarani.
"Ohhh Mungu wangu! tunafwatwa nyuma"
Kaka yake Casey alizumgumza huku, akichungulia kwenye kioo cha nyuma kilicho jaa matundu ya risasi. Sikutaka hata kutazama nyuma kuzihofia kona za papo kwa papo, huku nyengine zikiwa ni kali sana.
"Wapo wangapi?"
”Pikipiki mbili na gari ndogo tatu"
"Muheshimiwa unaweza kutumia, silaha?"
"Eheee?"

Hope Lucy Ruhinda: Napenda Kuwa Na Mwanaume Asie Nipangia Aina Ya Mavazi Ya Kuvaa

$
0
0
Hope  Lucy  Ruhinda  ( 25 ) ni  mwanamitindo  anae  fanya  vizuri sana  katika  tasnia ya  urembo  nchini  Afrika.  

Mwanamitindo  huyu ambaye  ni  mtanzania  kwa  mama, na  mnyarwanda  kwa  baba, kupitia  kazi  zake  za  mitindo , ameonyesha  nia  ya  kufika  mbali  katika  tasnia  ya  mitindo., huku  lengo  lake   likiwa  kufikia  level  za  kimataifa  kama   Naomi  Campbell.

Akielezea  kuhus  safari  yake  katika tasnia  ya  mitindo,  Hope  anasema

“Tangu  nikiwa  shule  ya  msingi, siku   zote  nilikuwa  nikitamani  sana  kuwa muimbaji, dancer  au  mwanamitindo. Lakini  kwa  kuwa  sikuwa  na  kipaji  cha  kuimba  wala  kudance,  nikaamua  kujikita  katika  mitindo “

Akaongeza“ Nilipofika  O-Level  nikaanza  kufanya  modeling  for  fun.  Hapo  nilikuwa  bado  Tanzania. Nilipo maliza  O-Level  huko  Tanzania, nilikuja  kujiunga  na  masomo  ya  A-Level  katika  shule ya  sekondari   ya  FAWE Girls’  Secondary  School  hapa  Kigali.”

Nilipo maliza  A-Level nilienda  kushiriki  Miss  Rwanda, baada  ya  kushauriwa  na  kushawishiwa  na  rafiki  zangu  wa  karibu.  Mwanzoni  nilikuwa  mgumu  kukubali  ushauri wao, lakini  baada  ya  kutafakari  kwa muda, nikaamua  kushiriki.  

Kwenye  mashindano  sikufanikiwa  kuchukua  taji  la  Miss  Rwanda, Nililia  sana  siku  hiyo.  Sababu  kuu  ya  kushindwa  kwangu, walitaka  mtu anaye weza  kuzungumza  Kinyarwanda  fluent, na  mimi  sikuwa  na  uwezo  huo.

Hata  hivyo, shindano  la  Miss  Rwanda  lilinipa  exposure  kubwa  sana. Baada  ya  kuniona,   baadhi  ya  wadau  wa  masuala  ya  mitindo, walinishauri  niingie  kwenye  mitindo.

So  show  ya  Rwanda  Cultural  Fashion  ilipoanza, mwaka  2013  nilijiandikisha na  kushiriki  na kufanya  vizuri  sana.

Niliingia  kwenye  modeling  ili niweze  kublend it na  business. Nina  ndoto za  kuwa  mfanya  biashara  mkubwa, ndio  maana  ninasoma  biashara  pale University  Of  Kigali

Hope  anawashauri  wanamitindo  wafanye  kazi kwa kujituma  na  wawe  wajanja  wa  kutafuta  na  kuzitumia  fursa mbalimbali za  mitindo, kwani  modeling  ni  kazi  kubwa  yenye  fursa  nyingi sana  za  kibiashara.

Ana amini  kuwa  kujulikana  “ exposure’ ni hatua  kubwa  sana  kwa  mwanamitindo  kuweza kupata  nafasi ya  kupata  deals  na  endorsements
Pamoja  na  kwamba, ana  ndoto  za  kuwa  mfanyabishara  mkubwa, lakini  ana amini pesa  si  kila  kitu. Kwake  yeye  kuwa  na  hekima  ni  bora  kuwa  na  pesa  na  mali  nyingi. “ Maarifa  hudumu   daima  milele  lakini, pesa  na  mali  huweza  kuisha  na  kutekeketea  wakati  wowote.

Akitoa  maoni  na mtazamo wake  kuhusu  wanaume  anasema “  Wanawake hatuwezi kuishi  bila  wanaume. Vile  vile, wanaume  hawawezi  kuishi bila  wanawake. Hii ndio  sababu  Mungu  aliwaumba  Adam  na  Eva

Kuhusu  aina  ya  mwanaume   anaye mpenda , Hope  anasema :

“ Napenda  niwe  na  mwanaume  ambaye  hanipangii  aina  ya  mavazi  ya  kuvaa.  Pesa  na  muonekano, havina  umuhimu wowote  kwangi,  ili mradi tu ninaishi  maisha  huru  ya bila  kuwa  na  stress. “

Kuhusu  aina  ya  kifo  ambacho  atapenda afe,  Hope  anasema, “ hakuna  mtu  asie  ogopa  kufa, lakini si njambo  baya  kuomba  kifo  chema, na mimi  katika  hilo, ninamuomba  Mungu, siku yangu  ikifika  nife  nikiwa  usingizini.

Kuhusu  asicho kipenda, Hope  anasema  hapendi  uchafu,. Anachukizwa  sana  na  uchafu. Usafi  ndio  kila  kitu  kwangu, hata  nilipo kuwa  Fawe  Girls, nilipewa  cheti cha  kuwa   mwanafunzi msafi.

 Mbali na  mitindo, Hope  anajishughulisha  na  kazi  mbalimbali  za  kijamii, huku  akipenda  zaidi  kuwasaidia  watu w asio  jiweza  na  wanaoishi  katika  mazingira  magumu.

“ Huwa  ninafarijika  sana  moyoni, ninapo  ona  mtu  Fulani amelala  usingizi  mzuri  na  wa  amani, kwa  sababu  ya  msaada  nilio mpa.

MAKALA  HAYA  YAMELETWA  KWETU  NA  NEEMA  HERBALIST  BLOG, KWA  UDHAMINI  MKUBWA  WA   NEEMA  HERBALIST &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC, WAUZAJI  WA  DAWA MBALIMBALI  ZA  ASILI  KAMA  VILE :

1.Dawa  asilia ya  kuunganisha  mifupa, pingili  na kukomaza mifupa.

2.Dawa  asilia ya kuondoa  maumivu ya  misuli, kurekebisha  mishipa  na  misuli

3.Dawa  asilia  kwa  wagonjwa wa  kiharusi (Kupooza)

4.Dawa  asilia ya  kutibu  majeraha

5. Dawa  asilia  ya  kutibu  vidonda ndugu

6.Dawa asilia  ya  kuondoa  uchovu na  kuwashwa

7.Dawa  asilia  ya  kuondoa mafuta  kwenye damu ( kolestrol /lehemu)

8.Dawa  asilia  ya  kutibu tatizo  la  nyongo

9. Dawa  asilia  ya  kutibu  gauti

10. Dawa  asilia  ya  uzazi  wa  mpango

11. Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  Goita

12.Dawa asilia ya  kutibu  tatizo  la  change  la watoto wachanga.

13.Dawa  asilia  ya kutibu  vidonda  vya  tumbo

14.Dawa  asilia  ya  kutibu mzio     ( Allergy)

15.Dawa asilia  ya  kutibu  tatizo  la  degedege  kwa watoto  wenye  umri  wa  kati  ya  miezi  6  hadi  tisa.

16.Dawa asilia  ya  kurutubisha  mayai  ya  uzazi  na  kuzibua  mirija  ya  uzazi  kwa  wanawake.

17.Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  utasa  kwa  wanaume.

18.Dawa  asilia  ya  kusaidia  kugeuza  mtoto  aliye  kaa  vibaya  tumboni ( Mfano: Katanguliza mikono, makalio n.k )

19.Dawa  asilia  ya kupunguza  kitambi, uzito  na  unene  uliozidi.

20.Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  vinyama  vya  puani.

21.Dawa asilia  ya  kutibu  tatizo  la  bawaziri.

22.Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  uchungu  wa  pili  baada  ya  kujifungua.

23.Dawa  asilia  ya  kutibu  majeraha ya moto  pamoja na  makovu yatokanayo  na  moyo.

24.Dawa  asilia  ya  kutiu  tatizo  la  kwikwi

25.Dawa asilia  ya  kutibu  tatizo  la  kutokwa  na  harufu  mbaya  kinywani

26.Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  kutoa harufu  mbaya mwilini

27.Dawa  asilia  ya  kusaidia  kunenepesha  mtu  aliye  dhoofu  mwili

28.Dawa  asilia ya kutibu  tatizo  la  uvimbe  wa  tumboni  ( FIBROID )

29.Dawa  asilia  ya  kisukari

30.Dawa  asilia  kwa  watu  wenye  tatizo  la  moyo, presha  ya  kupanda, presha ya  kushuka, moyo  kupanuka  na  matundu  kwenye moyo.

31.Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  U.T.I, kaswende, kisonono sugu  na  Taifodi.

32.Dawa  asilia  ya  kutibu  magonjwa  mbalimbali ya  ngozi

33.Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo la  kubanwa mkojo na  maumivu  kwenye  njia  ya  mkojo

34.Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  kujikojolea

35.Dawa  asilia  ya  kusafisha  figo  na  kibofu  cha  mkojo

36.Dawa  asilia  ya  kuondoa  sumu  mwilini

37.Dawa asilia  ya  kuondoa  maumivu  ya  hedhi

38.Dawa  asilia  za  kuondoa  sumu  ya  nyoka, na  nge.

39.Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  pumu

40.Dawa  asilia  ya  kuyeyusha uvimbe  kwenye  lango  la  uzazi.

41.Dawa asilia ya kutibu  malaria  sugu

42.Dawa  asilia  ya kutibu  tatizo  la  upara 

43.Dawa  asilia ya  kutibu  tatizo la  kikohozi sugu  na  kimeo.

44.Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  ngiri

45.Mawe  kwenye  figo

46.Kukosa  choo

47.Kukosa  hamu  ya  kula

48. Chango  la  kike

49. Kutanua  nyonga ( Kuzaa  bila  kupasuliwa )

50.Nguvu za  kiume

51. Hamu  ya tendo  la  ndoa  kwa  wanawake.

52.Mtoto kuchelewa  kutembea

DAWA   ZOTE  HIZI  NI  ZA  ASILIA KABISA  NA  HAZINA   KEMIKALI ZA  VIWANDANI.

Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR ES  SALAAM, jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING, nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO PLAZA.

Kwa  wateja  waliopo  Dar  Es  Salaam, ambao  hawana  nafasi  ya  kufika  ofisini  kwetu, watapelekewa  dawa  mahali  popote  walipo.

Kwa  wateja  waliopo  mikoani, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  mabasi.

Kwa wateja  waliopo  Zanzibar, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  boti.

Kwa wateja  waliopo Mombasa, watatumiwa  dawa  kupitia  basi  la  TAHMEED.

Kwa  wateja waliopo  jijini  Nairobi, watatumiwa  dawa  kupitia  basi  la  DAR  EXRESS.

Na kwa  wateja  waliopo  ughaibuni, watatumiwa  dawa  kwa  njia ya  POSTA  au  DHL.

WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA:

0766 – 53 83  84.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu huduma zetu, tutembelee  kila  siku, kupitia :

Serikali Yatangaza Matokeo ya Mtihani Darasa la 7......Bofya hapa Kuyaona

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images