Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Ubalozi wa Marekani nchini Kenya wafungwa baada ya Mtu Mmoja Kuuawa kwa Risasi Nje ya Ubalozi Huo

$
0
0
Jeshi la Polisi jijini Nairobi nchini Kenya linafanya uchunguzi kuweza kubaini kama mtu mmoja aliyeuawa jana karibu na ubalozi wa Marekani alikuwa amekula njama za kushirikiana na watu wengine kufanya shambulio.

Mtu huyo (24) aliuawa jana asubuhi nje ya ubalozi wa Marekani Nairobi baada ya kumshambulia mlinzi kwa kumchoma na kisu tumboni ndipo Afisa mwingine wa Polisi akampiga risasi kichwani. 

Inadaiwa kuwa kijana huyo alikuwa akilazimisha kuingia ndani ya ubalozi huo, na mlinzi alipomzuia ndipo akamchoma kwa kisu.

Maafisa watano wa FBI na maafisa wa Polisi nchini Kenya walikuwa karibu na eneo la tukio ambapo ni nje kidogo ya ubalozi wa Marekani. 

Tukio hilo limepelekea ubalozi wa Marekani kufungwa kwa muda hadi hapo hali ya usalama itakaporejea katika hali yake.


Matokeo darasa la saba: Majina ya watahiniwa 10 waliofanya vizuri na shule 10 bora na Ambazo Hazikufanya Vizuri

$
0
0
Ufaulu kwa watahiniwa wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2016 umepanda kwa asilimia 2.52 kutoka asilimia 67.84 mwaka jana hadi asilimia 70.36, huku wavulana waking’ara katika matokeo hayo ambao wengi wametoka shule za Kanda ya Ziwa.
 
Matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk Charles Msonde ambaye alisema kati ya wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri katika mtihani huo, msichana ni mmoja tu, Justina Gerald wa Shule ya Msingi ya Tusiime ya jijini Dar es Salaam.
 
Kati ya wanafunzi hao 10, watahiniwa saba wanatoka Shule ya Msingi Kwema iliyopo mkoani Shinyanga, wawili Tusiime na mmoja kutoka Kaizirege ya Bukoba mkoani Kagera. 

Dk Msonde alisema jumla ya watahiniwa 555,291 kati ya 789,479 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata jumla ya alama 100 na zaidi kati ya alama 250.
 
“Idadi hii ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 70.36, kati ya hao wasichana ni 283,751 na wavulana 271,540. Mwaka 2015 ufaulu ulikuwa ni asilimia 67.84 kuwapo ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.52,” alisema Dk Msonde.
 
Watahiniwa 16,929 wamepata daraja A, watahiniwa 141,616 wamepata Daraja B, watahiniwa 396,746 wamepata daraja C, watahiniwa 212,072 wakipata daraja D na 21,872 wakipata daraja E . 

Dk Msonde alisema ufaulu katika masomo ya Sayansi na Maarifa ya Jamii umepanda kwa asilimia kati ya 4.06 na 14.76 ikilinganishwa na mwaka 2015 huku masomo ya Kiswahili, Hisabati na Kiingereza ufaulu umeshuka kwa asilimia kati ya 0.39 na 12.51 ukilinganisha na mwaka jana.
 
“Watahiniwa wamefaulu zaidi katika somo la Kiswahili ambalo ufaulu wake ni asilimia 76.81 na somo walilofaulu kwa kiwango cha chini ni Kiingereza lenye ufaulu wa asilimia 36.05,” alifafanua Dk Msonde.
 
Dk Msonde aliwataja watahiniwa waliofanya vizuri na shule zao kwenye mabano kuwa ni:
  • Japhet Stephano, Jamal Athuman na Enock Bundala (Kwema),
  • Justina na Shabani Mavunde (Tusiime),
  • Jacob Wagine, Isaac Isaac, Daniel Kitundu na Benjamin Benevenuto (Kwema)
  •  Azad Ayatullah (Kaizirege).
Wasichana 10 bora:
  1. Justina Gerald (Tusiime)
  2.  Danielle Onditi (Tusiime)
  3. Linda Mtapima (Kaizirege),
  4. Cecilia Kenene (Mugini),
  5. Magdalena Deogratias (Rocken Hill),
  6. Asnath Lemanya (Tusiime),
  7. Fatuma Singili (Rocken Hill),
  8. Ashura Makoba (Kaizirege),
  9. Rachel Ntitu (Fountain of Joy),
  10. Irene Mwijage (Atlas)
Wanafunzi wavulana 10 bora kitaifa,
  1. Japhet Stephano (Kwema),
  2. Jamal Athuman (Kwema),
  3.  Enock Bundala (Kwema),
  4. Shabani Mavunde (Tusiime),
  5. Jacob Wagine (Kwema),
  6. Isaac Isaac (Kwema),
  7. Daniel Kitundu (Kwema),
  8. Benjamin Benevenuto (Kwema),
  9. Azad Ayatullah (Kaizirege)
  10. Benezeth Hango (Kwema).
Shule 10 bora ni:-
  1. Kwema (Shinyanga),
  2. Rocken Hill (Shinyanga),
  3. Mugini (Mwanza),
  4. Fountain of Joy (Dar es Salaam),
  5.  Tusiime (Dar es Salaam),
  6. Mudio Islamic (Kilimanjaro),
  7. Atlas (Dar),
  8. St Achileus (Kagera),
  9. Giftskillfull (Dar),
  10. Carmel (Morogoro).
Shule 10 ambazo hazikufanya vizuri ni:-
  1. Mgata (Morogoro)
  2. Kitengu (Morogoro)
  3. Lumba Chini (Morogoro),
  4. Zege  (Tanga),
  5.  Kikole (Tanga),
  6. Magunga ya Morogoro,
  7. Nchinila (Manyara),
  8. Mwabalebi (Simiyu)
  9. Ilorienito (Arusha)
  10. Chohero (Morogoro)
Mikoa 10 iliyoongoza kitaifa ni Geita, Katavi, Iringa, Dar es Salaam, Kagera, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Njombe na Tabora wakati Halmashauri 10 bora ni Mpanda Manispaa, Geita Mji, Arusha Mji, Mafinga Mji, Chato, Mwanza Jiji, Moshi Mji, Mji Makambako, Ilemela na Hai.

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 31 & 32

$
0
0
Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
“Wewe hulali?”
Rahab aliuliza kwa sauti ya unyonge, huku akimtazama Raisi Praygod kwa macho yaliyo jaa usingizi, hadi akajikuta akirembua.
“Nataka nikaoge”
Rais Praygod akapiga hatua moja, ila Rahab akamshika mkono na kumvuta kwa nguvu na kuangukia kitandani. Rahab kwa haraka akausogeza karibu mdomo wake kwa Raisi Praygod na wakaanza kunyonyana, huku wakionekana kuwa katika hisia kali. Raisi Praygod akalivua gauni lake na kulitupa pembeni. Akalishika la Rahab na akamvua, wote wakabakiwa kama walivyo zaliwa.

ENDELEA
    Hapakuwa na mtu aliye weza kumuonea mwenzake aibu zaidi ya wote kushiriki tendo la ndoa ipasavyo. Rahab akazidi kujituma kitandani kumpa muheshimiwa Raisi mambo matamu ambayo hata Raisi Praygod, hakuwahi kuyapata kutoka kwa mwanamke wa aina yoyote tangu azaliwe. Hata marehemu mke wake, hakuweza kufikia hata aslimia kumi kwa mambo ambayo Rahab anamfanyia juu ya kitanda. Wote wakajikuta wamesahau kwamba wanapita katika kipindi kigumu cha matatizo.
“Rahab”
Raisi Praygod alimuita Rahab, aliye mkalia juu ya kiuno chake akizidi kukatika kadri ya uwezo wake.
“Mmmmmm”

Rahab aliita huku akiwa amebana pumzi zake, huku jasho kwa mbali likimwagika na nywele zake ndefu zikiwa zimekaa shaghala baghala.
“Nataka nikuoe”
“Kweli?”
“Ndio nahitaji uwe mke wangu, wa ndoa”
Rahab kuambia wahivyo hakujibu kwa sauti, ila akajibu kwa vitendo, vilivyo mfanya Raisi kusahau matatizo yote na kuzidi kuchanganyuikiwa kwa penzi hilo la binti mdogo mwenye mwili mwembamba, fulani, ila si shuuhuli ya kupambana pekee yake na maadui, ila hata shughuli ya kitandani anaiweza kwa asilimia mia moja. Hadi wanafikia kileleni wote kwa pamoja wakajikuta wakicheka huku wakiamini kwamba walicho peana kilistahili kwa wao kuweza kukipata kwa wakati huo.

“Nakupenda sana Rahab”
Raisi Praygod alizungumza huku akihema mithili ya mwana riadha wa mwisho kwenye mbio ndefu, aliyekua na kibarua kirefu cha kuwakimbiza wezake wanao kwenda kwa mbio ndefu sana.
“Nakupenda pia Praygod”
Kwa mara ya kwanza Rahab kufungua kinywa chake na kuliita jina la Raisi, kwani siku zote alizoea kumuita muheshimiwa Raisi. Taratibu Rahab akajilaza kifuani mwa Raisi Praygod, huku taratibu akiupa kazi  mkono wake wa kushoto kuchezea nywele nyini lizizopo kifuani mwa raisi Praygod.

“Twende tukaoge”
Raisi Praygod alizungumza, na taratibu wote wakashuka kitandania, wakaingia bafuni na kila mmoja akawa na kazi ya kumuogesha mwenzake kwa kila kona ya mwili. Ukawa ndio mwanzo mpya wa mahusiano kati ya Raisi Praygod na Rahab, kila mmoja aliweza kuufungua moyo kwa mwenzake na kuamini upendo wao umeendana kwa asilimia kubwa sana.
                                                                                                        ***
Kila jinsi  walivyo zidi kuogelea ndivyo jisi walivyo zidi kwenda mbele, huku mara kwa mara wakiwa wanajitokeza kwenye usawa wa bahari kutazama ni wapi wanapo elekea. Ikawachukua muda mrefu sana kuweza kufika pembezoni mwa fukwe za bahari, katika eneo ambalo limetulia sana. Wote wakaivua mitungi ya gesi ambayo walikuwa wameivaa migongoni mwao. Kila mmoja alijihisi njaa kubwa kwenye tumbo lake, kwani waliweza kudumu ndani ya maji takribani masaa nane, wakiwa wanatoroka kutoka sehemu mmoja kwenda nyinine

“Ahaaa kudadadeki, kweli ng’ombe wa masikini hazai”
Halima alizungumza kwa sauti kubwa huku akijilaza kwenye mchanga mweupe ulio kua pembezoni mwa bahari hii kubwa. Hakuna aliye mjibu zaidi ya wezake kuendelea kutazama kila eneo la fukwe hizi zinazo pendeza kuvutia sana.
“Jamani inakuaje?”
Anna aliuliza kwa sauti ya unyonge, dhairi akionekana kuchoka sana.

“Nahisi hapa kwenye fukwe kunaweza kua na nyumba tutembeeni tembeeni, tunaweza kupata msaada”
Samson aliwashauri wezake
“Lakini jamani, hembu kuweni makini. Hapa tulipo fika sote hatupajui. Isije ikawa fukwe ya jeshi ikala kwetu ohooo”
Halima alizungumza huku akijigeuza geuza kwenye mchanga
“Sasa Halima wewe unataka tuendelee kukaa hapa si ndio?”
“Hapana sijasema hivyo Fetty, ila ninacho sema mimi, tuwe makini tusiwe vihere here. Kama pesa tumezikosa, lile lidude nalo limechukuliwa. Yote kwa tamaa zetu”
“Halima huu muda sio wa kulaumiana bwana”
Agnes alizungumza kwa hasira kali.

“Hata kama, jamani lakini hua siku zote nikizungumzaga ukweli, munaniona mimi fala. Sasa huyo Samson tuliye msaidia naye katuileta huku, nilipo kua ninamkatalia tusiwe pamoja naye mimi nilijua tuu haya yatatokea. Haya baba Samson tuambie tunaelekea wapi?”
“Maneno ya Halima, yakamkera kila mtu ambaye, alionekana kuchoka sana kwa shuhuli nzima waliyo ifanya ya kujioko kutoka kwenye jeshi la nchi ya Russia

Wakaanza kutembea kwa umakin, huku wakitazama kila eneoa la fukwe hii. Kigiza kilisha anza kuchukua nafasi yake huku kila mmoja akaizidi kunyong’onyewa kwa kuchoka sana. Hawakukata tamaa zaidi ya kwenda mbele kubahatisha kama wanaweza kupata sehemu ya kujistiri. Hadi inagonga mishale ya saa mbili usiku hapakuwa na mtu aliye baatika kuona nyumba ama uwepo wa watu katika eneo hilo
“Jamani tupumzikeni bwana na kama kuendelea tutaendelea kutembea tukiwa na nguvu”

Halima alizungumza huku akiwa amesimama, wezake wote wakamgeukia na kumkodolea mimacho. Kila mtu akakubaliana na wazo la Halima, wakatafuta moya ya jiwe kubwa lililo toboka na kuweka kijichumba kidogo, wote wakaingia na kukaa humo. Mwanga wa mbalamwezi uliweza kuwaonyesha ndani ya jiwe hilo kubwa, hapakuwa na kitu chochote kinacho weza kuwadhuru.

Baridi kali kwao ndio ikawa ni changamoto kubwa sana iliyo weza kuwatesa miili yao, isitoshe nguo walizo zivaa zilizo tengenezwa kwa material ya mpira hazikuweza kabisa kuizuia baridi hiyo kuendelea kuwapiga kwenye miili yao.

“Mmmm hili puku ni balaaa”
Agnes alizungumza huku akijikunyata, taratibu Samson akatoka ndani ya jiwe na kusimama nje, akatizama kila kona ya fukwe hakuona mtu yoyote, akazunguka nyuma ya jiwe na kujisaidia haja ndogo ambayo ilikuwa imememkamata kwa kipindi kirefu sana. Akiwa katikati ya kujisaidia haja ndogo kwa mbali akaweza kuona mwanga wa taa ukitokea kwenye moja ya nyumba iliyo mbali kidogo toka hapo walipo, kwa haraka akamaliza haja yake na kuzunguka walipo wezake

“Jamani kuna kitu nimekiona tokeni haraka”
Fetty na wezake wakatoka kwa haraka, Samson akawaonyesha mwanga wa taa hiyo . Kwa haraka bila hata ya kujiuliza wakanza kukimbia kuelekea kwenye nyumba hiyo. Kila walivyo zidi kwenda ndivyo walivyo zidi kuiona mandhari ya nyumba hiyo, ambayo ni kubwa kiasi na yagorofa.  Wakafanikiwa kufika kwenye uwanja wa jumba hilo linalo onekana ni jumba la kifahari, ila nje hapakua na taa ya aina yoyote, zaidi ya taa inayo waka kwenye chumba hicho kimoja.

“Jamani, tuweni makini naona tunaenda tu”
Halima alizungumza, kwa kujiamini. Wote wakasimama kutazama mazingira ya jumba hili lililo zungukwa na miti mingi ya minazi. Kwa mbali wakasikia mngurumo wa gari ukiwa unakaribia kufika kwenye jumba hili, kwa haraka wakatafuta sehemu ya kujificha ambayo iliwawezesha kuona mlango mkubwa wa kuingilia ndani ya jumba hilo.

Gari moja ya kifahari aina ya Jaguar, ikasimama nje ya jumba hili. Wakashuka watu wawili walio valia suti huku mikononi mwao wakishika bunduki aina ya Short gun. Mmoja akazunguka upande wa pili wa gari ambapo akaufungua mlango wa gari hiyo. Wote wakamshuhudia bwana Rusev akishuka kwenye gari hilo la kifahari huku akionekana kutazama kila upande wa jumba hilo.


Tamko: CCM yawajibu Lowassa na Zitto Kabwe ..... Pia yakana kushiriki kwenye kuivuruga CUF

$
0
0
Ikiwa imepita siku mbili tangu aliyekuwa mgombea wa kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa kueleza tathimni ya utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano chini Rais John Magufuli, ambapo alidai kuwa, katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi huo, kumekuwepo na ukiukwaji wa misingi ya demokrasia na utumishi wa umma kuwa kaa la moto.

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimevunja ukimya na kumjibu kwa kusema kuwa katika kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita alikuwa wa kwanza kukiuka misingi ya demokrasia. Kuhusu utumishi wa umma kuwa kaa la moto, imemjibu kuwa wanao lalamika hivyo ni wale wanaotumiwa kuficha mafisadi na wakwepa kodi.

Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka amewaambia waandishi wa habari kuwa Lowassa hastahili kuituhumu serikali ya Rais Magufuli kuwa inakiuka misingi ya demokrasia.


“Demokrasia ya kweli lazima ianze ndani ya chama, ni demokrasia ipi iliyotoa mamlaka kwa vyama vinavyounda UKAWA kuwanyima wanachama wao haki ya kuomba kupeperusha bendera za vyama walivyoviasisi, kuvitetea kuvigharamia kwa kuamua kumteua mgombea mtunguo ambaye hajapimwa wala hajawahi kuvipigania?,” amehoji.


Ole Sendeka ameongeza kuwa “Kitendo hicho cha kutowashirikisha wanachama na kuwanyima haki yao kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa kulidhihirisha usaliti wa hali ya juu wa misingi ya demokrasia.”


Amesema CCM haigopeshwi na matamko ya Lowassa anayotoa katika vyombo vya habari kwa kuwa havitaiathiri na kwamba imemamua kumjibu kwa madai kuwa anapotosha umma kwa kueleza mambo yasiyo na ukweli.


Ametoa wito kwa vyama vya siasa nchini kutochukulia kwa wepesi masuala ya demokrasia na mabadiliko.


“Wanasayansi wa masuala ya siasa waiangalie demokrasia ya CHADEMA na UKAWA inavyofanya kazi maana ni kihoja, watuambie njia iliyotumika kuwapata wabunge viti maalumu. Kila kiongozi aliteua maswahiba zake na wengine kwa ugeni wao ndani ya CHADEMA,” amesema.


Pia Sendeka amemtaka kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo kutoichukia serikali ya Rais Magufuli kwa kuwa inatekeleza yale aliyokuwa anayapigania.


“Chuki ya Zitto ya kuendelea kunyooshea kidole serikali ya CCM haina tija, sababu inatekeleza yote aliyokuwa akiyapigania,” amesema.


Katika hatua nyingine, Sendeka amedai kuwa CCM haijashiriki kukihujumu chama cha Wananchi (CUF) kama inavyodaiwa na baadhi ya wanasiasa kuwa kinawachonganisha viongozi wa chama hicho ili kigawanyike.


“Hatuna haja ya kuhangaika na CUF na wapanga siasa za uongozi CHADEMA, hatujashiriki kukivuruga na hatuna muda huo,” amesema.


=======
Ndugu wanahabari,

Kwa muda sasa kumekuwepo na usambazaji wa taairifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa wakishirikiana na baadhi ya vyombo vya habari zinazolenga kukejeri, kudhihaki, kukatisha tama, kubeza na kudhoofisha jitihada zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi na Seikali zake katika kuleta maendeleo kwa Watanzania

Kumekuwepo na makala zinazoandikwa na magazeti mawili ya nje ambazo hutolewa kila baada ya miezi miwili na ambazo zinapotosha na kuandika habari zisizo za kweli kuhusu Tanzania

Pia, yapo magazeti mawili ya ndani ambayo yamekuwa yakitoa makala mfululizo kwa kila wiki zinazolenga kumchafua Mheshimiwa Rais na kuichafua taswira ya nchi yetu.

Tumesikitishwa na waandishi wa makala hizo walioamua kujivua uzalendo na kushiriki mpango wa kuiharibu heshima na taswira ya nchi yetu kwa maslahi ya maadui zetu wa nje na baadhi ya wanasiasa. Tunafuatilia kujua nini kinawasukuma kufanya hivyo na kwa maslahi ya nani ilhali sote ni watanzania. Je ni tama ya madaraka tu au mengine?. Hakuna anayepinga ukosoaji bali unapaswa uwe ukosoaji wenye nia njema

Ndugu wanahabari,

Mtakumbuka hivi karibuni aliyewahi kuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa tuhuma za ufisadi ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa, alisambaza taarifa kwa vyombo vya habari aliyoiita tathimini ya mwaka mmoja baada ya uchaguzi mkuu wa octoba 25,2015

Katika taairifa yake, alidai kuwa alileta msisimko mpya katika siasa za Tanzania, kwamba ameshirikiana na wenzake kuionyesha nchi yetu maana ya demokrasia na kukosoa juhudi za serikali na wateule wa Rais.

Demokrasia kimsingi ni dhana inayohusisha ushiriki na kuheshimu mawazo ya wengi katika kufikia uamuzi. Ikiwa maana halisi ni hii, tunajiuliza ni ipi demokrasia aliyoionyesha Lowassa ambayo leo anajisifu kuwa nayo?

- Tulishuhudia akiwa mgombea Urais wa chama ambacho hakijui, hakushiriki kukijenga wala kutoa mchango wowote unaompa hadhi ya kupeperusha bendela huku katiba na kanuni ya chama hicho ikivunjwa. Kidemokrasia anayepewa fursa ya kupeperusha bendela ya chama chochote makini duniani ni kiongozi au mwanachama aliyethibitika kwa imani na matendo, kuzielewa, kuzitekeleza, kuzitetea falsafa, itikadi na malengo ya msingi ya chamahicho. Mgombea ni taswira halisi na alama muhimu inayoakisi dhamira ya chama husika machoni kwa wananchi.

- Demokrasia ya kweli lazima ianzie ndani ya chama, ni demokrasia ipi inayotoa mamlaka kwa vyama vinavyounda UKAWA kuwanyima wanachama wao haki ya kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera za vyama walivyoviasisi, kuvitetea, kuvigharamia na walivyovitumikia kwa kuamua kumteua mgombea “MTUNGUO” (ambaye hajapimwa wala hajawahi kuvipigania). Kitendo hicho cha kutowashirikisha wanachama na kuwanyima haki yao ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa kilidhihirisha usaliti wa hali ya juu wa misingi ya demokrasia

- CHADEMA watuambie njia iliyotumika kuwapata wabunge wa viti maalumu. Ni demokrasia gani inayotoa fursa kwa baadhi tu ya viongozi kuteua wabunge ambao wanakiwakilisha chama chote. Ambapo kila kiongozi aliteua maswahiba zake na wengine kwa ugeni wao ndani ya CHADEMA walikosa watu wanaowafahamu na kuamua kuwateua wanawake maswahiba wao ndani ya CCM. Msingi wa kawaida wa kupata wabunge wa viti maalumu ukiacha kura za maoni, kigezo kingine muhimu ni mchango wa mgombea / mwanachamahuyo katika kukijenga na kukitumikia chama chake. Yaliyotokea kwa CHADEMA kwenye wabunge wake wa viti maalumu ni mapya kwenye ulimwengu wa demokrasia. Inahitaji wataalamu wa sayansi ya siasa kufanya utafiti wa aina hii mpya ya demokrasia

Tulidhani baada ya mwaka mmoja kupita, wenzetu hawa wangelikuwa wamejifanyia tathimini, kujikosoa, kujisahihisha, na hata kufanya uungwana wa kuwaomba radhi wanachama wao kwa uvunjifu mkubwa wa misingi ya demokrasia, katiba na kanuni za vyama vyao

Tunatoa wito kwa vyama vya siasa nchini kutokuchukulia kwa wepesi masuala ya demokrasia na mabadiliko, yasiwe ni nyimbo za kuburudisha au kutoa matumaini hewaq kwa wanachama na wananchi. Kanuni mojawapo ya demokrasia ndani ya vyama ni lazima ionekane katika muundo wake na katika utekelezaji wa muundo huo

Umefika wakati vyama vya siasa vinapaswa kujifunza kuuza sera ili kujenga na sio kusubiri matukio kwa ajili ya kupata huruma ya wananchi. Tunasubiri kushuhudia na kusikia demokrasia demokrasia itakavyoendeshwa katika uchaguzi wa ndani wa vyama hivyo ambapo kuna taarifa mmoja wa vigogo amefanikiwa kupata kiasi cha dola milioni 15 zitakazomsaidia kupanga safu yake ya uongozi

Katika kutimiza mpango huo, tayari yapo mawasiliano ya mara kwa mara ya baadhi ya viongozi wakitoka Zanzibar na sehemu zingine za nchi kuja Dar es Salaaam, na imeonekana dhahiri mazungumzo yao kutowashirikisha viongozi wenzao waandamizi kwani yanalenga kafanikisha mpango huo.

Mheshimiwa Rais Dk John Pombe Magufuli, ameendelea kufanya juhudi kubwa katika kujenga nchi kwa kuimarisha utendaji na nidhamu ya utumishi serikalini, kukusanya mapato na kusimamia matumizi sahihi ya fedha, kupambana na kuzuia mianya ya rushwa pamoja na kusimamia haki, usawa na wajibu kwa raia. Mwenzetu anayaona haya kuwa ni kuufanya utumishi wa umma kaa la moto.

Juhudi hizi na nyinginezo ikiwemo ununuzi wa ndege mpya, ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, afya na kununua vitanda vya wazazi, kutoa elimu burekuanzia shule ya msingi mpaka sekondari na nyinginezo hazipaswi kukatishwa tama kwa maslahi ya wachache ni vyema kuziunga mkono kwa maslahi ya taifa letu

Katika kipindi hiki cha mwaka mmoja wa Rais Dk. Magufuli madarakani, CCM inawaomba wananchi kuendelea kummunga mkono katika dhamira yake safi yakuwaondolea kero, kuboresha huduma za jamii na kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Imetolewa na;-
CHRISTOPHER OLE SENDEKA
MJUMBE WA NEC NA MSEMAJI WA CCM
28/10/2016

Sumaye: Sirudi CCM hata waninyang’anye Mashamba Yangu Yote

$
0
0

Siku moja baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kutangaza nia ya Serikali kumnyang’anya shamba Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye, mwanasiasa huyo mkongwe amedai hilo halimtikisi.

Sumaye ambaye tayari ameshakabidhiwa notisi ya siku 90 kutokana na kutoliendeleza, amesema kuwa tayari suala hilo ameshaliwasilisha mahakamani na kwamba mwanasheria wake ndiye anayefahamu tarehe iliyopangiwa kesi hiyo.

“Nilienda mahakamani na ikaamuriwa kusiwe na shughuli yoyote, nasubiri tarehe ya kesi ambayo mwanasheria wangu ndiyo anaijua,” Sumaye anakaririwana MwanahalisiOnline.

Mwanasiasa huyo aliyehamia Chadema miezi michache kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka jana, amesema kuwa kama CCM wanataka kumdhoofisha kwa kumnyang’anya mashamba ili arejee haitawezekana.

“Kama walidhani kwa kunifanyia hivi nitarudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wasahau, hata kama nilikuwa na nia hiyo sirudi,” amesema Sumaye.

Serikali imetangaza kuanza mchakato wa kumnyang’anya Sumaye shamba lake lililoko Mwabwepande jijini Dar es Salaam kwa madai kuwa ameshindwa kuliendeleza kwa muda mrefu, kinyume na matakwa ya sheria.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya Octoba 29

Benk ya Twiga Bancorp Yafilisika....BoT Yachukua Usimamizi wake Kunusuru Amana za Wateja wa Benki Hiyo

$
0
0
Benki Kuu ya Tanzania imetangaza rasmi kuchukua usimamizi wa Benki ya Twiga Bancorp kuanzia jana kutokana na upungufu wa mtaji wa benki hiyo kiasi cha kuwa na deni la Shilingi Bilioni 21.

Benki Kuu pia imesimamisha shughuli zote za utoaji huduma za kibenki za benki hiyo kwa kipindi kinachokadiriwa kufikia wiki moja kuanzia jana tarehe 28/10/2016 ili kutoa nafasi kwa ajili ya kupanga taratibu za uendeshaji wa benki hiyo.

Maamuzi hayo yametangazwa jana jijini Dar es Salaam na Gavana wa Benki Kuu, Prof. Benno Ndullu mbele ya waandishi wa habari, na kusema kuwa hatua hiyo ni kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 56 (1)(g)(i) na 56(2) a-d cha taasisi za fedha ya mwaka 2006.

"Uamuzi huu umechukuliwa baada ya kubaini kuwa benki ya Twiga ina upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria ya mabenki na Taasisi za Fedha ya Mwaka 2006 na kanuni zake. Upungufu wa mtaji unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na pia kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa benki ya Twiga kutaharisha usalama wa amana za wateja" Imesema sehemu ya taarifa ya Prof. Benno Ndullu.

Aidha, amewataka watu wote wanaodaiwa na benki hiyo kulipa madeni yao kupitia Benki Kuu ya Tanzania, na kwamba wadaiwa wote watafuatiliwa kokote waliko.

Mbali na maamuzi hayo, benki hiyo pia imeisimamisha Bodi ya Wakurugenzi na uongozi wa benki hiyo, huku ikimteua Meneja Msimamizi ambaye atakuwa na jukumu la kusimamia shughuli za benki hiyo kwa kipindi ambacho itakuwa chini ya usimamizi wa benki hiyo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa usimamizi wa mabenki Bw. Keddedy Nyoni amesema benki hiyo ilianza na mtaji wa bilioni 7.5 lakini sasa ina deni la hadi bilioni 21.

Waziri Mkuu: Tumieni Misikiti Kuhubiri Misingi Ya Uislamu

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Waislamu watumie nyumba za ibada kuhubiri uislamu na misingi yake.

Ametoa wito huo jana mchana (Ijumaa, Oktoba 28, 2016) wakati akishiriki sala ya Ijumaa katika msikiti wa Nunge mjini Dodoma. 

Alisema dini ya Kiislam inafundisha kwamba sala ndiyo msingi mkubwa unaopaswa kufuatwa na kila muumini hivyo ni lazima wafanye ibada kwa wakati.

“Nasisitiza kwamba wote tutumie muda wetu vizuri pamoja na mambo mengine tufanye ibada kwani dini inatuekeza kuwa sala ndiyo msingi mkubwa kwenye Uislamu. Tunayo kazi ya kuimarisha misingi ya dini kwa kutumia nyumba za ibada,” alisema.

Waziri Mkuu alisema Waislamu wana jukumu la kufundisha watoto wao na kuhakikisha wanakua kwenye imani na kujengeka katika maadili mema.

“Dini inajenga maadili mema kwa mtoto na hata mtu mzima. Pia dini inajenga misingi ya uvumilivu na inamuwezesha mtu kumtambua Mwenyezi Mungu. “Tuendelee kuwafundisha vijana wetu umuhimu wa kushiriki kikamilifu kwenye masuala ya kidini ili wakikua waweze kuiendeleza kwa vizazi vijavyo,” alisema.

Waziri Mkuu ambaye alitumia fursa hiyo kujitambulisha kwa waumini wenzake wa mkoa wa Dodoma baada kuhamia rasmi, ameahidi kutoa ushirikiano kwao na pia amewaomba wampe ushirikiano ili aweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

“Nimekuja kujitambulisha. Mimi ni kijana wenu, ndugu yenu. Nimekuja Dodoma rasmi nyumbani na kikazi. Naomba mnipokee na naamini katika kipindi chote nitakachokuwa hapa nitapata ushirikiano nanyi na pia nitawapa ushirikiano,” alisema.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliwaomba waumini hao wawaombee dua wanafunzi wa kidato cha nne ambao wanatarajia kuanza mitihani ya kuhitimu Novemba Mosi, mwaka huu ili waweze kufaulu.

Waziri Mkuu aliwaomba waumini hao waendelea kuwaombea viongozi wa kitaifa wakiongozwa na Rais Dk. John Magufuli ili waweze kutekeleza vizuri majukumu yao na kufikia malengo yanayotarajiwa na wananchi.

Aidha, Waziri Mkuu alichangia sh. milioni moja kwa ajili ya kuendeleza mradi wa ujenzi wa zahanati katika msikiti huo. Miradi inayojengwa na waumini wa msikiti huo kwa sasa ni zahanati, madarasa ya shule ya awali na shule ya ufundi.


Taarifa ya Mamlaka ya Dawa na Chakula TFDA kuhusu Dawa bandia zilizokamatwa

$
0
0

Na Ally Daud-Maelezo
MADAWA bandia na yasiyo sahihi kwa matumizi ya binadamu yamekamatwa maeneo ya Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini baada ya kufanyika ukaguzi maalum wa kutafuta dawa bandia katika maeneo hayo iliyofanyika hivi karibuni.
 
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo wakati wa kutoa Matokeo ya ukaguzi maalum wa dawa uliofanyika katika mikoa ya Kanda za Ziwa na Nyanda za Juu Kusini.
 
“Kutokana na ukaguzi maalum tulioufanya katika Kanda za Ziwa pamoja na Nyanda za Juu Kusini wa kutafuta dawa bandia na zisizo sahihi kwa matumizi ya binadamu tumefanikiwa kukamata dawa bandia za aina tano ambazo zipo kwenye makundi mawili ya Dawa za malaria na Viua vijasumu(Antibiotics)” alisema Bw. Sillo.
 
Aidha Bw. Sillo amesema kuwa ukaguzi huo maalum umeweza kusaidia kukamata dawa ya malaria aina ya vidonge vya Quinine ambayo inadaiwa kutengenezwa katika kiwanda cha Elys Chemical  nchini Kenya na nyingine zinatengenezwa hapa nchini katika kiwanda cha Shelys Phamaceuticals Ltd.
 
Mbali na hayo Bw. Sillo amesema kuwa pamoja na kukamata dawa bandia pia zoezi hilo lilifanikiwa kubaini na kukamata dawa zilizoisha muda wa matumizi , zisizosajiliwa na zenye ubora duni zenye thamani ya Tsh. Milioni 17.463.
 
Bw. Sillo ameongeza kuwa Ukaguzi huo ulitokana na kuwa na taarifa za awali ambazo zilionyesha uwepo wa dawa bandia katika maeneo ya Geita na Mara mwezi Agosti na Septemba mwaka huu  na kusistiza kwamba zoezi hilo la ukaguzi linaendelea nchini kote na watakaokutwa na hatia watachukuliwa hatua stahiki.
 
Kwa upande wa Msajili wa  Baraza la famasi Bi. Elizabeth Shekalaghe amesema kuwa wataalamu wa madawa watakaokutwa na hatia ya kusambaza na kuhudumia dawa bandia watafutiwa usajili na kuacha kutoa huduma  kwa mujibu wa sheria ya dawa , chakula na vipodozi.
 
“Wataalamu wa dawa ambao wanasambaza na kuhudumia dawa bandia watafutiwa usajili na kuacha kutoa huduma  kwa mujibu wa sheria ya dawa , chakula na vipodozi pindi watapogundulika” alisema Bi. Shekalaghe.
 
Zoezi hilo la Ukaguzi maalum wa dawa bandia ulianza Oktoba 4 mwaka huu linafanywa kwa ushirikiano wa TFDA, Jeshi la polisi pamoja na Maafisa kutoka Baraza la Famasi litakuwa endelevu ili kuhakikisha dawa bandia zinatoweka nchini.

Jaji Lubuva Ataka Tume ya Uchaguzi Ifumuliwe.......Apendekeza Wakurugenzi wa Halmashauri Wawekwe Kando Kwenye Usimamizi

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva ameitaka serikali kubadili muundo wa tume hiyo ili iwe na ofisi na watumishi katika kila halmashauri nchini na ofisi ya Zanzibar.

Amesema hatua hiyo itawezesha NEC kufanya kazi zake kwa uhuru zaidi, badala ya kutegemea wakurugenzi wa halmashauri (Ma-DED).

Alisema hayo jana mjini Dodoma wakati akikabidhi taarifa ya tathimini baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.

Tathimini hiyo imetolewa ikiwa ni mwaka mmoja tangu Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi huo. 

Lubuva alisema serikali ifanyie mapitio ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 na Sheria ya Serikali za Mitaa Sura 292 ili kurekebisha vifungu vinavyokinzana.

“Pamoja na hayo, serikali inatakiwa kubadili muundo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kuwa na ofisi na watumishi katika kila halmashauri nchini na ofisi ya Zanzibar, hiyo itafanya tume ifanye kazi zake kwa uhuru zaidi tofauti na sasa kazi hizo zimekuwa zikifanywa na wakurugenzi wa halmashauri,” alisema.

Alisema baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, tume iliamua kufanya tathimini kwa lengo la kupata mrejesho juu ya utekelezaji wa Uchaguzi Mkuu kutoka kwa wadau. Alisema ni mara ya kwanza kwa tume kufanya tathimini tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993.

“Tathimini hii imefanyika ikiwa ni mojawapo ya zoezi linalokamilisha mzunguko wa uchaguzi na kuanza kwa mchakato wa uchaguzi mwingine,” alisema.

Alisema changamoto zilizojitokeza kwa mujibu wa wadau waliohojiwa ni pamoja na mpiga kura kutoruhusiwa kupiga kura katika eneo tofauti na lile alilojiandikisha.

Pia wapiga kura kushindwa kupiga kura siku ya uchaguzi kutokana na kugawa mipaka ya kiutawala na majimbo ya uchaguzi, baada ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura na muda mfupi uliotolewa kujiandikisha na uwekaji wazi wa daftari la awali la wapiga kura.

Alisema tathimini inaonesha katika baadhi ya maeneo, watu waliojitokeza kupiga kura ni wachache, ukilinganisha na idadi ya wapiga kura waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

“Baadhi ya sababu zilizotolewa ni pamoja na uelewa mdogo juu ya umuhimu wa kupiga kura kutokana na elimu ya mpigakura kutowafikia wapigakura wengi, pia wapigakura walijiandikisha katika daftari la kudumu kwa ajili ya matumizi mengine ili kupata kadi kwa ajili ya matumizi mengine na uwepo wa hofu, vitisho na vurugu siku ya kupigakura,” alisema.

Waziri Mhagama, Mkurugenzi wanena
Kwa upande wake, Waziri Mhagama alisema tume inapaswa kupongezwa kwa kukamilisha zoezi zima la Uchaguzi Mkuu, ambalo lilikuwa na changamoto nyingi na ushindani mkubwa wa kisiasa.

Alisema kwa mujibu wa Kifungu cha 15(5) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura 343, tume inapaswa kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura mara mbili kati ya Uchaguzi Mkuu mmoja na mwingine, lakini haikuwezekana kufanyika hivyo baina ya mwaka 2010 na mwaka 2015 kutokana na sababu mbalimbali.

Alisema sababu hizo ni pamoja na ufinyu wa bajeti na kuchelewa kupatikana kwa fedha kwa wakati, lakini serikali itajitahidi kuhakikisha kuwa mapungufu yaliyo ndani ya uwezo wake, yanatatuliwa ili kuiwezesha tume kutekeleza majukumu yake ya kikatiba na kisheria kwa wakati.

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima alisema tathimini ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ilifanyika, ikiwa ni hatua ya kukamilisha mzunguko wa uchaguzi.

Alisema kati ya watendaji 1,029 waliohojiwa, watendaji 929 ambao ni sawa na asilimia 90.3 walisema wana uelewa kuhusu muundo wa tume na watendaji 100 sawa na asilimia 9.7, walikuwa hawana uelewa kuhusu muundo wa tume.

“Kati ya watendaji 929 wa uchaguzi waliohojiwa, 818 sawa na asilimia 88 walisema kuwa muundo wa tume unafaa kuendesha uchaguzi, aidha watendaji 111 sawa na asilimia 12 walieleza kuwa muundo wa tume haufai katika kuendesha uchaguzi,” alisema.

Pia matokeo yanaonesha kuwa, katika watendaji wa uchaguzi 1,014 waliohojiwa, 814 sawa na asilimia 80.3 walisema hakukuwa na changamoto katika njia hizo, watendaji 200 sawa na asilimia 19.7 walieleza njia za mawasiliano zilikuwa na changamoto.

Alisema matokeo ya tathimini yameonesha kati ya watendaji 1,029 waliohojiwa 996 sawa na asilimia 96.8 walikuwa na maoni kuwa utekelezaji wa majukumu ya uchaguzi ulizingatia maelekezo yaliyotolewa na tume, ambapo watendaji 33 sawa na asilimia 3.2 walieleza kuwa utekelezaji haukuzingatia maelekezo hayo.

Aidha alisema wadau wa uchaguzi 1,915 waliohojiwa kuhusu uelewa wao juu ya elimu ya mpiga kura, kati ya wadau 1,463 sawa na asilimia 76.4 walisema walikuwa na uelewa wa elimu ya mpiga kura na 452 sawa na asilimia 23.6 hawakuwa na uelewa.

Kailima alisema wapiga kura 499 walihojiwa, ambapo kati yao wapiga kura 377 sawa na asilimia 75.6 walisema walitumia chini ya dakika 30 kufika kituo cha kupiga kura, wakati wapiga kura 87 sawa na asilimia 17.5 walitumia dakika 30 hadi 60 kufika kituo cha kupiga kura.

CCM Yatekeleza Agizo la Rais Magufuli Kwa Wafanyakazi wa Kampuni ya Uhuru Publications

$
0
0

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetekeleza agizo la Rais John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho la kuwalipa mishahara na haki zao nyingine zinazofikia Sh milioni 609 wafanyakazi wa Kampuni ya Uhuru Publications (UPL) wanaozalisha magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani.

Rais Magufuli alitoa agizo hilo mwezi uliopita alipofanya ziara ya ghafla katika ofisi ya magazeti hayo na kusikiliza malalamiko ya wafanyakazi na baadaye kuagiza ndani ya mwezi huo, wafanyakazi walipwe mishahara na haki zao zote.

Msemaji wa chama hicho, Christopher ole Sendeka akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana alisema pia miongoni mwa maagizo ya Rais Magufuli ni kutaka wafanyakazi hao kutobughudhiwa wala kufukuzwa kazi baada ya kueleza changamoto zinazowakabili na kuhakikisha wanalipwa haki zao.

“Nataka kuwahakikishia mpaka hapa tunapozungumza sasa hivi hatudaiwi tumeishatekeleza maagizo ya Mwenyekiti, tuko safi labda katika sehemu nyingine,” alisema.

Katika ziara hiyo, Rais Magufuli aliagiza kupatiwa orodha ya taasisi za serikali zinazodaiwa na Magazeti ya Uhuru na Mzalendo, na pia aliagiza kulipwa kwa deni linalodaiwa na Shirika la Hifadhi ya Jamii la NSSF kutokana na kutowasilishwa kwa makato ya wafanyakazi.

Katika mazungumzo yao na Rais, wafanyakazi walilalamikia kutolipwa mishahara yao kwa miezi saba, kutowasilishwa kwa michango ya wafanyakazi kwa NSSF, kuuzwa kwa mtambo wa kuchapisha magazeti katika hali ya kutatanisha, kutotambuliwa katika ajira kwa baadhi ya wafanyakazi, kutolipwa kwa madeni wanayozidai taasisi za serikali na wanaostaafu kutolipwa mafao yao.

Mmiliki wa Shule Iliyofutiwa Matokeo Ya Darasa la 7 Amwaga Machozi Hadharani

$
0
0
Siku moja baada ya matokeo ya darasa la saba kutangazwa, baadhi ya wamiliki wa shule wamelijia juu Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) kwa kufuta matokeo ya wanafunzi wao, huku mmoja wao akibubujikwa na machozi akidai wamehujumiwa.

Ikitangaza matokeo hayo juzi, Necta ilisema imefuta matokeo ya wanafunzi 238 kwa sababu ya udanganyifu, ikiwatuhumu wakuu wa shule sita na walimu kuhusika kuiba mitihani, kuwapa majibu watahiniwa au kuwafanyia mtihani.

Necta ilienda mbali zaidi na kudai kuwa kwenye shule moja, walimu walijificha bwenini, chooni na ofisini ambako wanafunzi waliwafuata na kupewa majibu na baadaye kuyasambaza kwa wenzao.

Lakini, walimu hao  wamepinga vikali tuhuma hizo za kushiriki katika udanganyifu, isipokuwa shule moja tu ambayo ilisema mwalimu aliyehusika ameshachukuliwa hatua.

“Sijafurahishwa na kitendo cha Necta kuifutia matokeo shule yetu. Hiyo ni hujumu,” alisema mmiliki wa shule ya msingi Tumaini iliyopo Sengerema mkoani Mwanza, Kandumula Maunde.

Huku akilia, Maunde alisema wakati tukio hilo lilotokea saa 5:00 asubuhi, hakuwepo na hakushirikishwa.

“Niliitwa kesho yake na kupata maelezo kuwa wanafunzi wa shule yako wamekamatwa kwa sababu wameandikiwa majibu ya mtihani kwenye sketi, sikukubaliana nao,” alisema.

Kwa mujibu wa Necta, mmiliki huyo aliiba na kuandaa majibu ambayo watahiniwa wake waliandika kwenye sare za shule na kuyatumia ndani ya chumba cha mtihani.

Necta imewataja waliohusika kuwa ni mmiliki aliyetajwa kwa jina la Jafari Maunde, msimamizi anayeitwa Alex Kasiano Singoye na wanafunzi wote.

Alisema hakukubaliana na kitendo hicho kwa sababu wanafunzi hao walikuwa wameandaliwa vizuri kujibu mitihani yao.

Maunde aliliomba baraza la mitihani kupitia upya uamuzi wake wa kuifutia shule hiyo matokeo kwa kuwa umeathiri maisha ya wanafunzi waliokuwa na ndoto za kuendelea na masomo.

Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo waliofutiwa matokeo waliiomba Necta kuangalia upya uamuzi huo. Wanafunzi hao walieleza kuwa msimamizi wa mtihani wa siku hiyo alikuwa akiwasumbua na aliwalazimisha waandike maelezo ya kukiri kuwa walikamatwa na majibu.

“Msimamizi alitulazimisha tuandike kwenye ubao baada ya kumaliza mitihani maelezo yakisema tumekamatwa na majibu ya mtihani yakiwa yameandikwa kwenye sketi tulizokuwa tumevaa,” alisema mmoja wa wanafunzi hao, Kefa Matini.

Kwa upande wa shule ya msingi ya Little Flower iliyopo Serengeti mkoani Mara, walimu walisema uamuzi wa kufutiwa matokeo ni adhabu isiyostahili.

Wanafunzi 37 wa shule hiyo  inayomilikiwa na Kanisa Katoliki, Parokia ya Magumu wamefutiwa matokeo. 

Necta imeeleza kuwa mwalimu mkuu wa Little Flowers aliiba mtihani, kuandaa majibu na kumpa msimamizi mkuu pamoja na wasimamizi wengine ili wawape watahiniwa.

Imesema waliohusika ni mwalimu mkuu anayeitwa Cecilia Nyamoronga, msimamizi mkuu (mwalimu), Haruni Mumwi na msimamizi (mwalimu), Genipha Simon na watahiniwa wote.

Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule hiyo, Paskael Chacha alisema uamuzi huo umewaumiza walimu na watoto waliofanya mtihani walioko shuleni na wazazi kwa kuwa hawajapewa sababu za udanganyifu huo na ulimhusisha nani na lini.

“Walimu hawakuwepo shuleni, mkuu wa shule ndiye alikuwa akiruhusiwa kuwepo shuleni kwa muda mfupi. Inanipa shida kujua udanganyifu ulifanyikaje na ulimhusisha nani.

"Hili suala linatupa shida kwa kuwa wasimamizi walioletwa siku ya kwanza si waliofika kusimamia. Sasa taarifa kama hizi zinauma sana,” alisema.

Alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa taarifa zinazodai kuwa siku ya mtihani mtoto mmoja alikamatwa na karatasi ya majibu na kumtaja mkuu wa shule kuwa ndiye aliyempa, mwalimu huyo alikana na kudai kuwa hana taarifa.

Majibu ya Dr. Msonde
Akizungumzia malalamiko hayo, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde alisema wanaosema wameonewa wanatakiwa kuomba radhi na kukubali adhabu kwa sababu waliokamatwa walikutwa na uthibitisho, akitoa mfano wa Shule ya Msingi Tumaini.

Kwa upande wa Shule ya Msingi Little Flower, Dk Msonde alisema ofisa wa baraza la mitihani alishuhudia mwalimu akipitisha karatasi ya majibu kwa wanafunzi .

“Sasa hapo utasema umeonewa? “Tumezoea kuona (matukio ya udanganyifu) yale ya mwanafunzi mmoja, lakini haya yanatisha. Mwalimu au msimamizi anamsaidia mwanafunzi, hii si sawa,” alisema.

Serikali Yarejesha asilimia 52 ya hisa zake UDA

$
0
0

Serikali imefanikiwa kurejesha udhibiti wake kwenye Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) baada ya kurejeshewa asilimia 52 ya hisa zilizonunuliwa kinyume na utaratibu na Kampuni ya Simon Group Limited (SGL). 
 
Kurejeshwa kwa hisa hizo kunatokana na ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwamba mauzo ya hisa hizo yaliyofanywa na Bodi ya Wakurugenzi wa Uda hayakuwa na kibali cha Serikali. 
 
Ripoti ya CAG ya mwaka 2014/15 ilibainisha licha ya utaratibu kukiukwa pia hakuna vilelezo vya fedha za manunuzi zaidi ya kuonyesha Sh320 milioni ziliingizwa kwenye akaunti binafsi ya Mwenyekiti wa Bodi, Idd Simba ambazo hata hivyo alidai ni malipo ya ushauri alioutoa kwa mwekezaji huo. 
 
Kurejeshwa kwa hisa hizo, kutolewa taarifa ndani ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ambayo Jumanne ya wiki hii iliuweka kikaangoni uongozi wa Jiji la Dar es Salaam kuhusiana na sakata la Uda. 
 
Pia, kamati iliwataka Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) George Simbachawene, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju na Msajili wa Hazina Lawrence Mafuru wafike kwenye kamati wakiwa na majibu sahihi kuhusu sakata hilo.
 
 Viongozi hao waliitikia wito huo jana, na baada ya kikao cha faragha Mwenyekiti wa LAAC , Vedasto Mwiru alisema Serikali imeitaarifu kamati yake kuwa imerejesha katika himaya yake fungu kuu la hisa ambazo hazikugawiwa. 
 
Mwiru alisema Serikali imerejesha hisa asilimia 52 ambazo ziliuzwa na Bodi ya Wakurugenzi Wa Uda kinyume cha utaratibu. 
 
“Maelezo yaliyotolewa na Serikali zile share (hisa) zote  ambazo hazikugawiwa ziko salama chini ya mikono  salama ya Serikali hazijauzwa,” alisema. 
 
Mwiru ambaye pia ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CUF), alisema kutokana na maelezo hayo wabunge wametaka mikataba ya kurudisha hisa hizo kwa Serikali ipelekwe kwenye kamati hiyo. 
 
Alisema kamati hiyo inaipa Serikali muda wa wiki mbili kuhakikisha kuwa wanawasilisha nyaraka hizo. 
 
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita alisema wanasubiri majibu ya barua yao ya kuomba ushauri kuhusu uuzwaji wa hisa za jiji za asilimia 51 kutoka kwa mwanasheria Mkuu wa Serikali.
 
Alisema baada ya kupokea ushauri huo watapeleka katika Baraza la Madiwani ili kuona namna ya kwenda mbele pamoja na kuzifanyia kazi fedha walizouza hisa zao ambazo ziko katika Benki Kuu (BoT). 
 
Mwanasheria Mkuu Masaju alisema anakwenda kuandika mambo yote yaliyosemwa ili iwasaidie kamati na Jiji la Dar es Salaam kukamilisha utaratibu huo kisheria.

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 79 & 80 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

$
0
0
Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa

ILIPOISHIA
Gari nne nyeusi, zenye muundo wa gari kama zinazo bebea pesa za mabenki, zikafunga breki katika eneo tulilopo. Wakashuka watu walio valia ñguo nyeusi, makofia meusi yaliyo waficha sura zao, na kubakishs macho yao tu. Kila mmoja mkononi mwake ameshika bundiki, na wote wakanizungu huku wakinitazama kwa umakini.

ENDELEA
   Mmmoja wao akatoa amri ya mimi kuiamsha mikono yangu juu, nikatii pasipo kubishana. Akatoa amri nyingine ya mimi kulala chini, hapo ndipo nilipo anza kuleta ubishi, kwani siwezi kukamatika kirahisi.

Kitendo cha mimi kusogeza mguu nyuma, nikastukia kitu chenye ncha kali kikinichoma mgongoni, kwa haraka nikaupeleka mkono wangu nyuma, kwa ajili ya kukichomoa. Nikakuta ni sindano
yenye dawa, iliyo anza kuvinyong'onyeza viungo vyangu vya mwili. Taratibunikajikuta nikianza kuishiwa na nguvu. Nikaanguka chini, kila nilipo jaribu kunyanyua hata mkono sikuweza, nikajikuta nikiwatazama watu hao walio nikaribia na kuninyanyua. Nikastukia kitu kizito kikinipiga, kichwani, giza kali likanitawala machoni mwangu.

            ********
"Eddy.... Eddy"
Nisauti nyororo, iliyo anza kuisikia taratibu, ikipenya masikioni mwangu. Taratibu nikayafungua macho yangi, nikakutana na sura ya kike, huku kichwa chache kikiwa kimejaa nywele nyingi nyeusi na zilizo ndefu sana.

Macho yake makubwa kiasi, na yadura kiasi, yaliendelea kunitazama huku akiwa ameniimamia, kutoka katika kitanda nilicho kilala.
"Karibu tena duniani" Alizungumza huku akiwa ametabasamu.
"Duniani?"
"Ndio duniani"
"Kwani nilikua, sipo duniani?"
Hakuzungumza chochote zaidi ya kusimama, pembeni ya kitanda nilicho lala.
"Kwa jina ninaitwa dokta, Agines, nimtaalamu katika maswala ya saikolojia"
"Ngoja, hapa ni wapi?"
"Upo Washinton DC, Marekani"
"Ahaaaa?"
"Usishangae, ninaimani kwamna unatambua, nitukio gani ulilo lifanya kwa ajili ya hii nchi, nasi tumeamua kukuweka karibu nasi na kukusaidia kwa kila jambo"

 Akafungua pazia, kubwa lililopo kwenye moja ya ukuta, hapa ndipo nilipo anza kuona majengo makubwa yaliyopo katika mji huu, ambapo ndipo yalipo makao makuu ya serikali ya nchi ya Marekani.
"Tutahakikisha tunakufanyia kila unacho kihitaji"
Akaniandalia chakula, akaniomba nile.
"Ukimaliza kula, kuna watu nitahitaji uonane nao"
"Wakina nani?"
"Utawaona tuu"
Nikamaliza kula, akanionyesha bafuni, nikaoga na kurudi kitandani, huku nikiwa nimejifunga taulo.
"Unaweza kuvaa"
"Mbele yako?"
"Kwani kuna tatizo lolote, tambua kwamba mimi nitakuwa pamoja nawe kwakipindi cha siku tisini"
"Za nini?"

"Eddy vaa bwana, watu hao wanakusubiri."
Nikamtazama kwa muda, nikavua taulo, nikachukua nguo moja baada ya nyingine alizo zipanga kwenye kitanda.
"Umependeza sana"
"Asante"
"Upo tayari"
"Ndio"

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 33 & 34

$
0
0
Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
“Hembu Halima acha roho mbaya, tumekuja pamoja tutaondoka pamoja haiwezekani tumuache mwenzetu hapa”
Fetty alizungumza kwa msisitizo na kuzidi kumchefua Halima. Bwana Rusev akamuamrisha askari kuwasiliana na wezao walio ndani, naye akafanya hivyo kupitia simu ya upepo. Taaa zote nje ya jumba hili zikawashwa, na kuwafanya Fetty na wezake waonekane waliopo, Walinzi wapatao hamsini, wakiwa na bunduki, waliiekekeza mitutu yao katika eneo walilo lala Fetty na wezake na kuwafanya wanyanyuke taratibu huku mikono wakiwa wameinyanyua juu.

ENDELEA
“Hichi ndicho mulichokua mukikihitaji?”
Halima alizungumza kwa sauti ya kunong’oneza akionekana kukasirishwa na kitendo hicho cha wezake kuwa wabisha hadi wametiwa nguviuni na wanajeshi hjao wa bwana Rusev ambaye kwa mara ya kwanza walimuona ni mtu mwema kutokana na ukarimu wake alio waonyesha kipindi akiwapoke na kuzngumza nao hukusiana  na biashara ya kuuza manohari waliyo fanikiwa kuiteka kutoka katika jeshi la wana maji wa Tanzania.

Wakaamrishwa kuelekea sehemu ambapo yupo Samson, akiendelea kulia kwa maumivu makali aliyo yapata kutokana na risasi aliyo pigwa mguuni mwake.

Mr Rusev akaagiza wapelekwe kwenye chumba chenye giza zito na wafungiwe humo hadi kutakapo pambazuka ndipo ajue ni nini awafanye kwani siku zote hua hapendelei mtu kugundua siri zake na isitoshe wao ndio walio sababisha kwa makao makuu ya vikosi vyake kuweza kuvamiwa na jeshi la nchi yake ya Russia na kusababisha vifo vya wanajeshi wake wengi sana.

Fetty na wezake wakingizwa kwenye chumba chenye giza zito, hata kam ni jasiri kiasi gini giza la chumba hicho ni lazima uogope kwani hata mtu wa pembeni yako ha ta hauwezi kumuona zaidi ya kuisikia sauti yake.

                        ***
      Wakafika kwenye jumba la Frednando, ambalo lipo katikakti ya jiji la Mexco, Raisi Praygod na Rahab wakapokelewa kwa heshimwa kubwa na wafanyakazi wa Frednando ambao alisha wapa taarifa juu ya ugeni huo wa rafiki yake kipenzi. Wakakaribishwa kwenye moja ya seble ambayo kuta zake zimepabwa na madini ya dhahabu, huku sofa zake zikiwa zimetengenezwa kwa mtindo ambao Raisi Praygod hakuwahi, kuuona katika maisha yake

“Kaka uajua jumba  lako ni zuri kuliko ikulu yangu?”
“Weee, acha utani kaka”
“Kweli vile Frednando, inanibidi nikirudi hivi Tanzania ikulu yangu niweze kuibadilisha, kidogo mfumo uwe kama huu wako”
“Ila unakumbuka kwamba ikulu si yako, ukimaliza kipindi chako anakuja mwengine?”
“Hata kama ila, kwa kipindi nitakacho kuwepo mimi itanibidi nikae kidogo sehemu ambayo ninaihitaji mimi”

Wakiwa kwenye maongezi ya furaha, wahudumu wakawa na kazi ya kuandaa chakula na vinywaji, kwa ajili ya wageni hawa. Kwa upende wa Rahab, kila kinacho tokea kwake anaona kama ni ndoto, kwani hakutarajia ipo siku atakuja kuishi maisha ya kuheshimiwa kama haya. Moyo wake ukajikuta ukiuchukia ujambazi ambao alikuwa anaufanya na rafiki zake ambao hadi sasa hivi ajui kama wapo hai, kwani kwa fununu alizo kua akizisikia, ni kwamba marafiki zake hao nilazima waweze kunyongwa, hii ni kutokmna na uhalifu mkubwa walio ufanya wa kuwaua askari wengi wa jeshi la polisi.

“Kuna klitu Frednando nahitaji kukifanya hivi karibuni?”
“Kitu gani?”
“Ninahitaji kumuoa Rahab wangu”
Rahab akastuka kusikia hivyo kwani hakutegemea kwamba inaweza kuwa jambo la haraka kama anavyo hitaji Raisi Praygod
“Waooo, kaka hilo ni jambo jema, tena unaonaje ukalifanya hapa hapa kwangu”
“Ndio maana nikakuamnbia nahitaji kulifanya siku hizi za karibu, kutokana nampenda sana Rahab, bila yeye nahisi kwa sasa ningekua marehemu”
“Kweli kaka, wewe sema ni lini unahitaji kumuoa, niweke mambo sawa si unajua tena”
“Huyu hana siku nyingi hata siku mbili hizi zijazo pia itakua ni sawa”


Ufisadi NSSF: CCM Yataka Akaunti za Zitto Kabwe Zipekuliwe.

$
0
0
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Serikali kuhakiki akaunti na mali za Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT) na wenzake waliokuwa katika kamati za fedha za Bunge, ili kubaini kama zinalingana na kipato walichokuwa wakipata.

Msemaji wa chama hicho, Christopher Ole Sendeka, amesema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari, akimuhusisha Kiongozi huyo Mkuu wa ACT na tuhuma za ufisadi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), alipokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

”Nilikuwa najiuliza hivi chuki ya Zitto kwa Serikali ya Awamu ya Tano, inayopambana na mafisadi imetoka wapi wakati yeye alikuwa anasimamia mashirika hayo.

“Miongoni mwa taasisi hizo alizokuwa akisimamia na baadhi ya marafiki zake ndiyo hao walionunua hekari moja kwa Sh milioni 800, wakati ilikuwa ikiuzwa kwa Sh milioni 25 na walikuwa wamejificha kwa maslahi binafsi,” alisema katika ofisi ndogo za Makao Makuu, Lumumba Dar es Salaam.

NSSF ndiyo iliyonunua hekari 20,000 Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa Sh milioni 800 kwa kila hekari, badala ya Sh milioni 25 na kujikuta katika hatari ya kupoteza Sh bilioni 270, katika mradi wa ujenzi wa mji wa kisasa wa Dege Eco Village.

Kutokana na tuhuma hizo za NSSF zilizoibuka upya katika kamati ya PAC wiki hii, Sendeka alisema ni vema Serikali ikague  kuona kama akaunti za viongozi wa zamani wa kamati hizo, maisha yao na mali walizonazo, zinafanana na mapato halali waliyokuwa wakilipwa.

Alisema alikuwa anaangalia msukumo wa ghafla na mapenzi ya akina Zitto waliyokuwa wanayapata kwa nchi, kumbe ilikuwa ni kichaka cha kuficha baadhi ya maswahiba zao wasichukuliwe hatua.

Aliwahakikishia wananchi kuwa Serikali ya Rais Magufuli haina nia ya kurudi nyuma katika jambo lolote na kuwa itasonga mbele huku akiamini kuwa Serikali iliyochaguliwa na watu haiwezi kufa.

“Tunahakika Serikali ya Magufuli iliyopata ridhaa ya kutumikia watu, haitafutika kwa kelele za mlango wa baadhi ya makuwadi na watu waliolipwa kuchafua taswira ya Tanzania,” alisema.

Aliongeza kuwa Serikali hiyo itaendelea kushughulikia wakwepa   kodi pamoja na kuchunguza mambo aliyoanzisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa bandarini.

Kauli ya Zitto
Akizungumzia tuhuma hizo, Zitto Kabwe alisema hana muda wa kujibu alichoita kuwa ni porojo na vioja vya Sendeka.

Alifafanua kuwa CCM ni chama dola na kuna taasisi nyingi za uchunguzi za Serikali, ikiwemo Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) na Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai (DPP) na kushangaa kwa nini vyombo hivyo havisemi, aseme Sendeka?

Majibu ya ACT Wazalendo kwa Ole Sendeka baada ya kutaka Zitto achunguzwe

$
0
0

Chama cha ACT-Wazalendo kimesema kimeshtushwa na tuhuma dhidi ya kiongozi wake wa chama, Zitto Kabwe kwamba ana miliki mali za kifisadi pamoja na kuhusishwa na ununuzi wa ardhi maeneo ya Kigamboni uliofanywa na NSSF kwa bei ya milioni 800 kwa ekari moja, wakati bei halisi ni milioni 25 na kwamba kitendo hicho kimeitia hasara serikali .

Tuhuma hizo zilitolewa jana na Msemaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Christopher Ole Sendeka, ambapo alivitaka vyombo vya uchunguzi kufanya uchunguzi katika shirika hilo ili kubaini waliohusika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria, huku akimhusisha Zitto katika uchunguzi huo.

Ole Sendeka alitaka akaunti za benki za Zitto pamoja na maisha yake binafsi kuchunguzwa kama yana uhalisia na kipato chake halali.

Tuhuma hizo zimekiibua chama cha ACT, ambapo leo Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa ACT, Habibu Mchange amevitaka vyombo vya uchunguzi haraka iwezekanavyo kuchunguza mali, madeni, akaunti zote za benki pamoja na mfumo wa maisha ya Zitto.

“ACT imeshtushwa na tuhuma, kashfa, porojo na matusi mbalimbali yaliyotolewa jana na Ole sendeka dhidi ya kiongozi wa chama chetu,” amesema.

Amesema kuwa, katiba ya chama hicho huwataka viongozi wote kuweka hadharani matamko ya mali zao na madeni na kwamba Zitto alitekeleza matakwa hayo ya kisheria hivyo mali na madeni yake yako hadharani na mtandaoni.

“Tunaamini kama kuna kiongozi ambaye mali, madeni, maslahi, na akaunti zake viko wazi basi ni ndugu Zitto,” amesema.

Aidha, Mchange amedai kuwa, kilichomsukuma Sendeka kutoa tuhuma hizo kwa Zitto ni harakati zake za kuupinga muswada mpya wa habari.

“Tuhuma za ole sendeka kuna kitu nyuma yake, jitihada za zito za kupambana na mswada wa habari ndizo zilizomuibua, sababu wanataka upitishwe ili kuviua vyombo vya habari,” amesema.

Amesema ACT itaendelea kuisimamia serikali katika mambo ya bungeni kama anavyofanya mbunge na kiongozi wao wa chama.

Ujumbe wa Rais Magufuli kwa Watanzani katika siku yake ya kuzaliwa

$
0
0
Leo Oktoba 29 ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli ambapo alizaliwa Oktoba 29, 1959. 
 
Rais Magufuli alizaliwa mkoani Geita na kitaaluma yeye ni mwalimu aliyebobea katika somo la Chemistry.
 
Katika siku yake hii ya kuzaliwa, Rais Magufuli amewashukuru Watanzania wote kwa kuendelea kumuombea ambapo amesema kuwa ataendelea kufanyakazi kwa bidii na kuwatumikia watanzania wote kwa ajili ya maendelo ya nchi.
 
Kupitia akaunti yake ya Twitter, Rais Magufuli ameandika jumbe hizi;

Rais Magufuli Atengua Uteuzi Wa Mkurugenzi Wa Upelelezi Makosa Ya Jinai (DCI) Diwani Athumani Leo

Rais Magufuli Afanya Ziara Ya Kushtukiza Wizara Ya Maliasili Na Utalii Na Kushuhudia Pembe Za Ndovu 50 Zilizokamatwa

$
0
0
Rais Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza kwa kazi nzuri Katibu Mkuu wa  Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi baada ya kukagua pembe za ndovu 50 zilizokamatwa katika operesheni maalum ya kusaka majangili alipofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii (MPINGO HOUSE) jijini Dar es salaam leo Oktoba 29, 2016.

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images