Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa
ILIPOISHIA
“Nafanya hii, kwa ajili yakulipiza kisasi cha mume wangu”
“Ngoja kwanza, nipo tayari kufa, ila ninakuomba usimuue mke wangu”
Nilizungumza kwa ujasiri, nikiwa nipo tayari kwa kufa, Madam Mery akalinyanyua panga lake juu, akalishusha kwa kasi kwenye mkono wangu wa kulia
ENDELEA
Nikatoa ukulele mkali, ulio mfanya madam Mery kusitisha zoezi lake kuukata mkono wangu, panga lake likiwa limesimama sentimita chache kutoka ulipo mkono wangu
“Madam, ninakuomba unisamee”
Nilizungumza huku machozi yakiendelea kunimwagika usoni mwangu, madam Mery akanitazama kwa macho ya hasira yaliyo jaa
ukatili mkubwa, akawatazama Victoria na John ambao macho yao yote yalikuwa kwetu
“Natambua kwamba mimi nimkosaji sana kwako, ninastahili kufa mbele yako, ila si mbele ya macho ya mke wangu.Mtazame jinsi alivyo katika hali yake.Mule ndani amebeba kiumbe kama ulicho kuwa umekibeba wewe, miezi tisa, na Derick akakiangamiza mbele yetu.Yule ni mwanamke mwenzako ambaye anauchungu kama wewe”
Nilizungumza huku machozi yakiendelea kunimwagilka usoni mwangu, madam Mery kwa mbali machozi yakaanza kumlenga lenga, macho yake yamebadilika rangi na kuwa mekundu kiasi huku sura yake ikiwa imejaa mikunjo kwenye paji lake la uso akinitazama kwa uchungu sana
“Mery mimi pia ni binadamu, kumbuka ni mambo mangapi tuliyafanya tukiwa pamoja, vuta kumbukumbu ni vitu vingapi tulishiriki tukiwa pamoja, Eheeee, leo hii unataka kuimwaga damu yangu, leo hii unataka kunisulubu kikatili, le……..”
“Eddy STOP TALKING”(Eddy nyamazakuzungumza)
Madam Merry alizungumza kwa sauti ya juu, yenye uchungu ndani yake.Akalitupa chini panga lake alilokuwa amelishika.Machozi mengi yakaanza kumbubujika usoni mwake, John na Vivtoria wakabaki wakimtazama madam Mery, ambaye taratibu alianza kupiga hatua za kuelekea kwenye gari lake alilo kuja nalo
“Madam Vipi?”
John alizungumza huku akimwafwata madam Mery kwa nyuma
“John ninakuomba uniache”
Madam Mery aluzungumza huku akiunyanyua mkono wake mmoja akimzuia John asimfwae anapo elekea
“Ila madam haya sio makubaliano yetu”
“John sipo sawa nimekuambia usinifwate”
Madam Mery alizungumza kwa sauti ya ukali, huku machozi yakiendelea kumchuruzika usoni mwake.
“Sasa Madam tumfanye nini Eddy?”
Madam Mery akageuka kwa hasira, hadi John akastuka kidogo, akanitazama jinsi machozi yanavyo nimwagika, akayafumba macho yake kwa sekunde kadhaa, akionekana akifikiria kitu cha kufanya juu yangu.
“Kesho nimkute akiwa hai”
Madam Mery alizungumza kwa sauti ya upole, kisha akaelekea lilipo gari lake, akafunguliwa mlango na mlinzi wake, akaingia ndani ya gari na wakaondoka zao.John akalisindikiza magari ya Madam Merry yanayotoka kwenye geti kubwa la Godauni, lilipo fungwa taratibu John akanigeukia, akanitazama kwa macho ya dharau huku Victoria akiwa amejichokea, kwani ninaamini mipango yao waliyo kuwa wameipanga dhidi yangu imeharibika.John akamfwata Victoria sehemu alipo simama, wakanong’onezana kwa muda kasha wakamtama Phidaya ambaye muda wote, amejilaza chini huku machozi yakimwagika kwa uchungu.
“Mchukueni huyo Malaya mumrudishe mulipo mtoa”
John aliwaamrisha watu wake, wakamnyanyua Phidaya na kumbeba juu juu, japo anajitahidi kujitoa mikononi mwa watu walio mbeba, huku aikiliita jina langu kwa sauyti ya juu, ila hakuifanikiwa kujitoa mikononi mwao John akapiga hatua hadi katika sehemu nilipo fungwa, akanitazama kwa muda, huku macho yake yakiwa yamejaa dharau kubwa, akanitemea mate ya usoni, akiyasindikiza kwa kofi zito lililo tua kwenye shavu langu la kushoto
“Mmmmmm Eddy, unajisikiaje?”
John alizungumza huku akivifikisha viganja vyake, na kuvipuliza taratibu taratibu.Akanishika sikio langu la upande wakulia, akaanza kulivuta kwa nguvu zake zote, nikaendelea kuugulia maumivu ndani kwa ndani, sikutoa sauti yoyote kwenye kinjwa changu
“Waooo, unajifanya komandoo usikii maumivu eheeee?”
John alizungumza, huku akiliachia sikio langu.Akaanza kunitandika vibao mfululizo kwenye mashavu yangu, hasira ikazidi kumiliki nafisi yangu.
“John, tumpeleke kisimani, hapo unajisumbua bure”
Victori alitoa wazo ambalo John alilikubali, wafanyakazi wao wakanishusha kwenye meza, majamaa wawili wakanibeba kwenye mabega yao. kama wawindaji walio beba swala waliye muua kwenye mawindo yao.
Tukaingia kwenye moja ya ukumbi mkubwa wenye mwanga hafifu, unao pita kwa kutumia madirisha machache yaliyopo juu yake.Wakanibwaga chini, na kunifanya nitoe mguno wa maumivu kutokana na kujiumiza sehemu ya paja langu, nililo pigwa risasi Taa kubwa zenye rangi nyeupe zikawaka na kulifanya eneo zima la ikumbu kuponekana vizuri, kuna mashimo makubwa mawili, kwa haraka nikatabua ndio hivyo visima wanavyo vizungumzia, mabaunsa walio kuwa wamenibeba, wakaufunga mwili wangu kwa kamba ngumu aina ya manila.
“Eddy utakufa kifo kibaya sana”
John alizungumza huku akiwa ameniinamia
“Usiombe nikatoka, kwenye mikono yeno, utajuta”
Nilizungumza kwa kujiamini sana, John akaanza kucheka kwa dharau, huku akinipiga piga mashavuni mwangu
“Eddy huwezi kutoka mikononi mwangu, nakujua wewe vizuri sana.Huwezi fanya chochote dhidi yangu.Muda wako umekwisha kaka”
“Angalia wakwako ndio utakuwa umekwisha”
John akaanza kunipiga mateke mfululizo kwenye mbavu zangu, nikaendelea kutoa sauti ya maumivu ila John hakunionea huruma zaidi ya kuendelea kunipiga kwa nguvu zake zote
“Mchukueni na mukamdumbukize kwenye kisima”
John aliwaamrisha watu wake, wakanibeba, kabla hawajaondoka na mimi, Victoria akawazuia.Akapi ga hatua hadi sehemu tulipo simama
“Eddy nakupenda kaka yangu, kwaheri”
Victoria alizungumza huku akinibusu shavuni mwangu, akawarusuhu watu kuonipeleka kwenye kisima kilichopo kwenye huu ukumbi, kwa jinsi walivyo nifunga kamba mwili wangu sikuweza kufanya kitu cha aina yoyote zaidia ya mwili wangu kunyooka moja kwa moja, mithili ya mtu aliye fariki dunia.