Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Wanaofanya Biashara Kienyeji Bila Kujisajili BRELA wapewa miezi miwili Kuzirasimisha

$
0
0
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umetoa muda wa miezi miwili kwa wafanyabiashara wanaotumia majina ya biashara pasipo kusajiliwa wafanye hivyo haraka.

Akizungumza na waandishi wa waandishi wa jijini Dar es salaam  jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Frank Kanyusi alisema katika zoezi la kutoa elimu na kurasimisha majina ya biashara na kampuni linaloendelea katika mikoa mbalimbali imebainika kuwa wafanyabiashara wengi wanatumia majina ya biashara pasipo kuyasajili.

“Sheria ya majina ya biashara inamtaka mfanyabiashara kusajili jina la biashara yake ndani ya siku 28 toka aanze kulitumia,” alisema Bw.Kanyusi na kuongezea kuwa kinyume na hapo atakuwa amevunja sheria ya majina ya biashara.

Alisema baada ya muda huo kupita, patakuwa na msako nchi nzima ili kuwabaini wale wote wanaotumia majina ya biashara pasipo kusajili na kuwafikisha katika vyombo vya sheria au kuwatoza faini.

Alisema kuwa sasa usajili wa majina ya biashara umerahisishwa kwani unafanywa kwa njia ya mtandao kwa kutembelea tovuti ya wakala huo ambayo ni www.brela.go.tzili kupata maelezo yote ya namna ya kusajili jina la biashara.

Aliwataka wafanyabiashara wasiishie kusajili tu jina la biashara bali pia waende katika Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa ajili ya kupata namba ya Mlipa Kodi (TIN) pia waendele katika halmashauri zao kupata leseni ya biashara.

“Kwa kurasimisha biashara serikali itapata mapato kwani wigo wa walipa kodi utaongezeka na pia itakuwa faida kwa wafanyabiashara katika kujengewa mazingira bora ya kufanya biashara,” alisisitiza Bw.Kanyusi.

Alisema BRELA imejipanga kuzunguka mikoa yote nchini ili kutoa elimu juu ya urasimishaji wa majina ya biashara na makampuni kwani imeonekana wananchi hawana uelewa wa kutosha juu ya umuhimu wa urasimishaji.

Hadi sasa BRELA imefanya ziara katika mikoa ya Mwanza, Mara, Geita na Simiyu na wiki hii watakuwa mkoani Shinyanga kwa muda wiki moja katika kuhamasisha wafanyabiashara kurasimisha biashara zao.

Alisisitiza kuwa ni lazima kuhakikisha kuwa biashara zinarasimishwa ili serikali iweze kuwatambua walipa kodi wake ambao watachangia pato la taifa na kuiwezesha Tanzania kuwa ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Mgogoro CUF Kuwaweka Rehani Wabunge wake 9

$
0
0
Licha ya Chama cha Wananchi (CUF) kujivunia uzoefu wa migogoro, huu wa sasa umeweka rehani majimbo yake tisa ya ubunge yaliyopo Bara na hatari ya kupoteza mvuto na wafuasi kama ilivyotokea kwa vyama vingine huko nyuma.

Vyama ambavyo vimewahi kupita kwenye kipindi kigumu kama inavyopita CUF sasa ni NCCR-Mageuzi, UDP na TLP. Lakini zaidi mgogoro wa NCCR-Mageuzi ndiyo unaotaka kufanana na CUF japo kwa mazingira tofauti.

Chama cha UDP kilichopata umaarufu kwa kauli yake ya ‘kuwajaza mapesa watu’ kwenye Uchaguzi Mkuu wa 1995 kilipata wabunge wanne ambao ni wengi kulingana na mvuto wa chama kwa wakati huo.

Lakini, chama hicho kilikumbwa na mgogoro wa uongozi baada ya mwenyekiti wake, John Cheyo kupinduliwa mkutanoni na nafasi yake kuchukuliwa na Nzugule Amani Jidulamabambasi, ambaye hata hivyo hakudumu kwenye nafasi hiyo kutokana na Msajili wa Vyama vya Siasa kutomtambua.

Pamoja na msajili kulipinga kundi lililofanya mapinduzi, chama hicho kilianza kudhoofu na kupoteza mvuto hasa Kanda ya Ziwa ambapo kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2005 kilipata mbunge mmoja- John Cheyo- aliyedumu hadi 2010, kwa sasa chama hicho hakina mbunge na kimepoteza ule mvuto wake wa ‘kuwajaza mapesa watu’.

Augustine Mrema mwanzoni mwa miaka ya tisini alipojiunga na NCCR-Mageuzi baada ya kutoka CCM alikwenda na wafuasi wengi na kukiimarisha chama hicho kilichokuwa hakina nguvu ikilinganishwa na vyama vingine.

Nguvu ya NCCR-Mageuzi ilionekana kwenye Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi  mwaka 1995, ambapo Mrema aliyegombea urais kwa chama hicho alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 1,808,616 na kupata wabunge katika majimbo 19 Tanzania Bara.

Matokeo hayo yalimuonyesha Mrema kuwa tishio kwa chama tawala cha CCM, lakini, baada ya uchaguzi huo mgogoro wa uongozi ndani ya chama hicho ulianza.

Aliyekuwa mwenyekiti wa chama Mrema alianza kupambana na katibu mkuu wake Mabere Marando, hadi chama kuwa na ofisi mbili tofauti, kugawana wajumbe wa baraza la wadhamini, wajumbe wa sekretarieti na kamati kuu.

Mazingira hayo yanataka kufanana na mgogoro wa CUF uliopo sasa kati ya Profesa Ibrahim Lipumba kwa upande mmoja na katibu mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.

Katika mgogoro wa NCCR wakati huo, Msajili wa Vyama vya Siasa wa wakati huo, Jaji George Liundi (sasa marehemu), aliutambua upande wa Marando kiutendaji kwa kuwapa ruzuku bila kutamka hadharani kwamba anaunga mkono kundi lipi.

Nguvu ya msajili ilimdhoofisha Mrema na kundi lake kwa kuwa hawakuwa na fedha za kuendesha shughuli za chama, ndipo akaamua yeye na wafuasi wake kuhamia Tanzania Labour Party (TLP), huku aki tamka ofisi zote mikoani zilizokuwa za NCCR-Mageuzi zibadilike kuwa za TLP.

Licha ya waliobaki NCCR-Mageuzi kuonyesha kufurahishwa na uamuzi wa Mrema wa kuondoka, chama hicho kilichokuwa kikijivunia majimbo 19 ya ubunge, kilianza kudhoofika kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000, kwanza hakikusimamisha mgombea urais, pili kilipoteza majimbo 18 ya ubunge na kubaki na jimbo moja tu la Kifu Gulamhussein Kifu (Kigoma Kusini) ambalo nalo lilipotea kwa njia ya mahakama.

NCCR-Mageuzi, mbali na kupoteza wabunge, pia chama hicho kilipoteza wafuasi na umaarufu iliyokuwa nao, hali ambayo CUF inaonekana kuwa nayo kwa kuwa inapita kwenye njia zile zile.

Hata hivyo, Mrema aliyekuwa akijivunia mtaji wa kura milioni 1.8 alijikuta akipiga mwereka kwenye uchaguzi mkuu wa 2000 alipogombea urais kupitia TLP alikoambulia kura 637,115 na wabunge watano.

Kuonyesha kwamba CUF inapita njia ya NCCR-Mageuzi katika kudhoofika, sasa chama hicho kimegawanyika lakini mbali na hivyo Msajili wa Vyama vya Siasa ameibuka hadharani kuunga mkono kundi moja na sasa ameonyesha dalili za kuwapa nguvu ya fedha.

Hata hivyo, kundi la Profesa Ibrahim Lipumba linaloungwa mkono na msajili likifanikiwa kupata ruzuku litakuwa na nguvu, lakini kwa wananchi chama hicho kitapoteza mvuto na kuweka rehani wabunge wa majimbo tisa wa Bara na madiwani.

Huu ni mgogoro wa tano wa kiuongozi ndani ya CUF baada ya kupitia katika kipindi kigumu wakati wa James Mapalala, aliyekuwa mwenyekiti wake wa kwanza, Naila Jidawi, Michael Nyaluba, aliyeanzisha chama hicho upande wa Bara na Hamad Rashid Mohamed.

Uzoefu wa migogo kwa CUF siyo kigezo kwamba chama hicho hakiwezi kuwa kama vyama vingine vilivyopoteza mvuto na kupoteza wabunge na madiwani waliowapata katika uchaguzi uliopita.

Kesi ya wadhamini 
Katika hatua nyingine, mchakato wa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha Wananchi (CUF), kupata kibali cha kufungua kesi dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na wenzake unaanza rasmi leo wakati maombi yaliyofunguliwa na bodi hiyo yatakapotajwa.

Bodi hiyo ya wadhamini CUF imefungua maombi hayo Mahakama Kuu Masjala Kuu dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili, Profesa Ibrahim Lipumba pamoja na wanachama wengine wa chama hicho waliosimamishwa uanachama wao.

Katika maombi hayo namba 75 ya mwaka 2016, bodi hiyo inaomba kibali cha kufungua kesi dhidi ya Msajili, Profesa Lipumba na wenzake kadhaa, pamoja na mambo mengine, kupinga uamuzi wa Msajili kumtambua Profesa Lipumba kama mwenyekiti halali wa chama hicho.

Umoja wa Vijana wa CUF (JuviCUF) Watangaza Kususia Ziara ya Profesa Lipumba Mikoa ya Kusini

$
0
0
Umoja wa Vijana wa CUF (JuviCUF) umewataka vijana wa chama hicho kutotoa ushirikiano kwenye ziara ya mwenyekiti aliyevuliwa uongozi na Barza Kuu, Profesa Ibrahim Lipumba na baadhi ya wabunge inayotarajiwa kuanza wiki hii mikoa ya Lindi, Mtwara na Tanga.

Wito huo ulitolewa jana na Mwenyekiti wa Juvi-CUF, Hamidu Bobali alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa ziara hiyo ina lengo la kukipasua chama hiko rasmi.

“Tunajua ziara hiyo inataka kuongeza mpasuko ndani ya chama na mpasuko huo utawapa mwanya maadui zetu ‘kutupiku’ kisiasa,” alisema Bobali.

Bobali, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mchinga kwa tiketi ya chama hicho, alisema pamoja na harakati za Lipumba tayari wabunge wa mikoa hiyo wapo katika kikao kuandaa mikakati ya kuimarisha chama.

Kadhalika Bobali alifafanua kuwa kama Jumuiya wanalaani kitendo kilichofanywa na kikundi cha vijana kilichojiita cha Mkoa wa Dar es Salaam cha kutoa kashfa kwa viongozi wa Ukawa akiwamo Freeman Mbowe na Julius Mtatiro.

Juvi-CUF iliwatoa hofu wananchi wa Zanzibar kuhusu hali ya kisiasa iliyopo visiwani humo, kutokana na hatua mbalimbali za kisheria zinazofuatwa ili kuhakikisha haki inapatikana kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Kuhusu sakata la akaunti ya chama inayoingizwa fedha za ruzuku na za wabunge, alisema hakuna fedha za wabunge zitakazoingia katika akaunti hiyo kutokana na mikataba inayosainiwa inahusu Mbunge na Ofisi ya Bunge na siyo chama.

“Tumechukua hatua kuwaeleza benki kuhusu akaunti kufunguliwa, suala hili linafanywa na bodi ya wadhamini inayoongozwa na Khatau hivyo siyo suala rahisi yeye (Lipumba) akazipata,” alisema Khatau.


Mwalimu Auawa.....Anyofolewa Kiganja cha Mkono wa Kulia

$
0
0

Mwalimu Israel Mlowasa (40) wa Shule ya Sekondari Nkuhungu katika Manispaa ya Dodoma, amekutwa ameuawa nyumbani kwake na kiganja chake cha mkono wa kulia kukatwa na kuondoka na wauaji hao.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi inasema kwamba mauaji hayo yamefanyika juzi maeneo ya Chang’ombe Extension katika Manispaa ya Dodoma.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Nkuhungu, Fidelis Kaishozi alisema mwalimu huyo alipotea tangu Oktoba 2, mwaka huu na taarifa kutolewa Polisi.

Imeelezwa kuwa maiti ya mwalimu huyo ilikutwa katika pagala la nyumba eneo la Nkuhungu.

Hakuna mtu aliyekamatwa kuhusu mauaji hayo, msako mkali unaendelea ili kubaini wahusika na mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Dodoma kwa uchunguzi zaidi wa madaktari.

Mkutano wa ACT- Wazalendo Watoa Maazimio Mazito Dar

$
0
0
Chama cha ACT- Wazalendo kimemuomba Rais John Magufuli kuunda timu ya wataalamu kupitia upya rasimu ya Katiba ya Jaji Joseph Warioba na kuitisha mkutano mkuu wa kikatiba ili kuipitisha. 

Chama hicho kilisema mchakato wa kura za maoni uanze upya ili kupata Katiba Mpya. 

Hayo ni miongoni mwa maazimio matatu yaliyotolewa na chama hicho kwenye mkutano wa siku moja wa kidemokrasia.

Akisoma maazimio hayo, Ofisa Habari wa chama hicho, Abdallah Khamis alisema,“chama kimeazimia mchakato wa kuandika Katiba Mpya uanze kwa kufanya marekebisho ya sheria ya kura ya maoni na Sheria ya mchakato wa Katiba.” 

Alisema, iwapo Serikali itaamua kwenda na Katiba Inayopendekezwa iliyopo sasa chama hicho kitaipinga kwa kufanya kampeni ya hapana kwenye kura ya maoni. 

Alisema wakati mchakato wa Katiba ukiwa umesimama, Baraza la Wawakilishi Zanzibar limepitisha sheria ya kutafuta mafutana gesi kinyume na matakwa ya Katiba ya Muungano ambayo inatambua mafuta na gesi kuwa ni masuala ya muungano. 

“Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia umeshauri kuwa chama kimwelekeze mbunge wake kuwasilisha bungeni hoja binafsi ya kufanya mabadiliko, kwa kuondoa mafuta na gesi kama jambo la muungano ili kuiwezesha Zanzibar kutafuta mafuta na gesi asilia bila vikwazo,” alisema. 

Khamis alisema chama hicho kimeazimia kufanya maadhimisho ya miaka 50 ya Azimio la Arusha Februari, 2017. 

“Katika maadhimisho hayo chama kifanye mkutano mkuu wa Kidemokrasia jijini Arusha na kutanguliwa na Halmashauri Kuu ya chama kwenye ukumbi uleule ambao Tanu ilifanya na kuzaa Azimio la Arusha mwaka 1967,” alisema. 

Ofisa huyo alisema katika maadhimisho hayo chama kimeshauriwa kuwa wataalamu wa ndani na nje waalikwe kujadili mafanikio na changamoto za Azimio la Arusha katika miaka 25 iliyopita. 

Pia, wataalamu watajadili madhara ya kutelekezwa kwa Azimio la Arusha mwaka 1992 huko Zanzibar.

Spika wa Bunge Job Ndugai afumua Kamati ya Bunge na Kuisuka Upya

$
0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amefanya mabadiliko makubwa kwenye Kamati ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, akiwabadilisha wabunge ishirini na wanne waliokuwa wanaunda kamati hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Ofisi ya Bunge, Ndugai ameteua wajumbe wapya kumi na sita wa kamati hiyo ambao pia watakuwa wajumbe wa kamati nyingine.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Spika ametumia Mamlaka aliyonayo kikatiba kuunda Kamati za Bunge kadri anavyoona inafaa, na kwamba mabadiliko haya yamelenga katika kuboresha utekelezaji wa majukumu ya kibunge.

“Kanuni ya 116 (3) –(5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016 inampa Spika mamlaka ya kuteua wajumbe ili wawe wajumbe katika kamati mbalimbali za Bunge ikiwa ni pamoja na mamlaka ya kuongeza, kubadilisha au hata kupunguza idadi ya wabunge katika kamati za kudumu za Bunge,” imeeleza taarifa hiyo.

Mabadiliko hayo yameanza mara moja kuanzia mwezi huu wa Oktoba na kwamba wajumbe wote wameshatumiwa barua tayari kwa maandalizi ya kukutana na kuwachagua viongozi wa kamati hiyo.

Hii ni orodha ya waliokuwa wajumbe wa kamati hiyo na kamati walizohamishiwa kufuatia mabadiliko hayo:

SBL Yazindua Shindano La Wapiga Mziki (DJ) “Mix Master” Itakayoshirikisha Mikoa Mitano

$
0
0
Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) jana imetangaza kuzindua shindano la DJ bora ambalo linalenga  kuibua na kukuza vipaji katika sekta ya muziki na burudani nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa  uzinduzi wa shindano hilo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Serengeti John Wanyancha alisema kuwa  shindano hilo limedhaminiwa na  bia inayozalishwa na kampuni hiyo Smirnof Black Ice, na wakati huo huo  ikimaanisha kuwapatia mashabiki wa muziki  fursa ya kufurahia  vibao vya muziki vya hivi karibuni vitakavyochezeshwa na ma-DJ walio na vipaji vikubwa.

Kwa mujibu wa Wanyancha, Smirnof Black Ice ni chapa inayoongoza  katika vigezo vya bia iliyotayari kunyweka ikiwa ni maarufu mioongoni mwa wanywaji wa tabaka la kati katika maeneo yote ya mjini na vijijini.

“Tunaamini kwamba kupitia shindano hili SBL itawapa wakati mzuri  wapenzi wa muziki watakaokuwa wanatembelea baa  wakati tukitoa fursa maridhawa ya kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji katika ulimwengu wa muziki na ma-DJ."

Mkurugenzi huyo aliyataja majiji ambayo yatakuwa wenyeji wa matukio na idadi ya ma-DJ watakaotoa burudani  katika mabaa kwenye mabano kuwa ni Dar es Salaam (20), Dodoma (4), Arusha (5), Morogoro (4), na Mwanza (5). Shindani hilo linaanza mwezi huu wa Oktoba na  litadumu hadi Desemba.

Aidha Mkurugenzi huyo alisema kuwa hadhira inayolengwa katika  mashindano hayo ni  vijana walio na umri kati ya miaka 18 hadi 30 na kufafanua kuwa burudani hiyo inawafaa sana  wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vingine vya elimu ya juu pamoja na vijana  walio na weledi.

“Itakuwepo zawadi nono kwa ma-DJ watakaoshinda,” alisema na kubainisha kwamba zawadi hizo zitajumuisha seti ya vifaa vya kuchanganya muziki, kompyuta mpakato na mashine kuchanganya muziki kwa washindi watatu watakaoingia fainali.

“Tunatoa wito kwa ma-DJ wote, wasimamizi wa baa na wapenzi wa muziki katika majiji haya  kushiriki kwa wingi katika shindano hili la kuvutia  ili kufurahia na  burudani inayotolewa na sekta ya muziki nchini Tanzania,” alisema Wanyancha.

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 65 & 66 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

$
0
0
Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa

Ilioishia
“chumbani”
Nilizungumza huku nikizidi kupiga hatua za haraka, nikaingia kwenye lifti pamoja na john, ambaye alikuwa akinifwata kwa nyuma, ikasimama kwenye ghorofa ya tatu, kama jinsi nilivyo minya batani ya ghorofa hii ambayo niyatatu, nikaanza kukimbia kuelekea chumbani kwangu, nilipo muacha mke wangu akiwa amelala, wasiwasi mwingi ukiwa umenitawala, nikafika kwenye mlango wachumba changu, nikaufungua kwa nguvu, kitu cha kwanza kutazama nikitandani, nikastuka kukuta mke wangu hayupo huku shuka jeupe lililo tandikwa juu yakitanda likiwa limejaa damu nyingi, jambo lilizozidi kutustua mimi na john

Endelea
Nikakimbilia kwenye mlango wa kuingilia bafuni, ila sikufanikiwa kumuona phidaya, joto kali la mwili likaanza kuambatana na woga ambao tangu kuzaliwa kwangu sikuwahi kuupata siku hata moja, nikatizama kila shemu ya chumba hadi chini ya uvungu ila sikumuona mke wangu, machozi kwa mbali yakaanza kunilenga lenga, huku nikijaribu kutafakari ni nini nifanye

“kwani alikuwa humu ndani?”
Nilijikuta nikiachia msunyo mkali, baada ya john kuniuliza swali ambalo jibu analo kichwani mwake, kwani muda nilipokuwa ninatoka nilikuwa nipo mwenyewe, na sote tumekuta damu juu yakitanda iweje aniulize kwamba alikuwepo humu ndani, nikatoka kwa hatua za haraka, huku shati nililo livaa likiwa linavuja jasho jingi, sana

“sasa eddy unakwenda wapi?”
John aliniuliza huku akinifwatwa kwanyuma tukielekea zilipo lifti za ghorofa hili, sikumjibu john chochote kwa maana ninahisi, hatambui nini umuhimu wa mke, isitoshe mke mwenye kiumbe change tumboni, kupotea katika mazingira yakutatanisha, tukaingia kwenye lifti ambayo kuta zake nne zina vioo, nikawa na kazi yakujitazama jinsi macho yangu yanavyo tiririsha machozi yanayotoka pasipo kuwa na kilio, huku wekundu ukiwa umetawala kwenye macho yangu, john akanipa kitambaa chake ili nikisaidie kufuta machozi

“nimepata wazo, hembu twende kwenye chumba cha ulinzi kwa maana humu ndani kuna kamera za ulinzi kila kona”

John alizungumza huku akinitazama usoni, wazo lake kidogo likarudisha ufahamu kwani kitu ninacho kifikiria ni phidaya na kiumbe change, kitarajiwa

“samahani dada”
John alizungumza na muhudumu mmoja kwa kingereza, mara baada ya sisi kutoka kwenye lifti iliyo tufikisha chini kabisa katika eneo tulilokuwepo

“bila samahni?”
“ninaomba kuuliza ni wapi kwenye chumba cha cctv camera”
“kwani kuna tatizo?”

“ndio lipo, kuna dada mmoja, ni mjamzito amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha, mume wake alimuacha chumbani akiwa amelala ila tulipo kwenye hatujamkuta”

“mmmm kuseme ukweli, mimi sijaona dada mjamzito akitoka, labda chakuwasaidia nyinyi, nikuwapeleka kwa meneja na yeye ndio atatoa idhini ya nyinyi kupelekwa kwenye hicho chumba”

“asante dada”
Sikuchangia neon lolote zaidi yakuwasikiliza john na muhudumu jinsi wanavyo zungumza, huku macho yangu yakitazama kila upande wa sehemu tulipo simama, nikastukia nikuvutwa mkono na john ambao tayari walishaanza kuondoka na kuniacha mimi nikiwa nimesimama kama sanamu, lakuongozwa na betrii

“kaka, usijali shemeji atapatikana, ninaimani hawezi kuondoka humu ndani ya hoteli kwa hali ile”

John aliendelea kuzungumza huku tukipiga hatua tukimwafwata dada, huyu kwanyuma, tukaingia kwenye moja ya chumba ambapo macho yangu hayakuwa ngeni kwa mtu aliye kaa kwenye kiti hichi huku akionekana kwamba ndio meneja wa hii hoteli

“meneja kuna, hawa wageni wa…..”

Meneja wake akainua mkono, kwa ishara ya kumkatisha mfanyakazi wake, na meneja wake akapiga hatua za haraka hadi sehemu nilipo simama mimi, huku akiwa ametabasamu usoni mwake, akanikumbatia kwa furaha, hapa ndipo nikapata uhakika kwamba ni mlinzi wa baba, ambaye kuna kipindi alinipeleka kwenye benki, nikatoe pesa kwa ajili ya kununulia siku ila ndipo nilipokutana na sheila baada ya jamaa kumkuta akiminyana na sheila aliyekuwa amechanganyikiwa

“eddy umekuwa mkubwa mdogo wangu”
Jamaa alizungumza huku akitabasamu, na mimi nikajikaza niweke tabasamu lakinafki ili mradi tu nisalimieane naye

“eddy mbona kama umepoteza furaha usoni mwako, unatatizo gani?”

Nikamuelezea jamaa jambo linalonisumbua,bila kupoteza muda akaniomba tuelekea chumba maalumu chenye video nyingi zinazoonyesha maeneo mbalimbali ya hotel, tukaanza kuonyeshwa matukio yaliyo pita muda mchache kwenye eneo la chumba chetu kilipo, tukashuhudia kumuaona mwanake aliye valia baibui lililo mficha sura yake akiingia ndani ya chumba change, muda mchache baada ya mimi kutoka, ndani ya dakika kadhaa akatoka akiwa amembeba mke wangu, kwenye mikono yake huku akiwa amemfunika kwa shuka jeupe, kama mtu aliye uwawa.

“peleka mbele kidogo”

Jamaa alizungumza na kumfanya muongozaji wa video hizi kupeleka picha za video mbele kidogo, ambapo tukamshuhudia mwanamke huyo ambaya hadi sasa, hivi sura yake hatukuiona, akimuingiza mke wangu kwenye gari yawagonjwa na kuondoka naye, pasipo watu kumshuhudia

“ujinga huu, ulipo kuwa unafanyika mulikuwa wapi?”

Jamaa alizungumza huku akimfokea mfanyakazi wake anaye ongoza mitambo ya kamera za ulinzia, mwili mzima ukaanza kunitetemeka na kujikuta nikizidi kuchanganyikiwa pasipo kujua ni kitu gani ambacho, nilimemkosea huyu mwanamke aliye mteka mke wangu, kila mmoja akabaki kimya akimtazama mwenzake asijue nini chakufanya


Lipumba Afungua Akaunti Mpya ya Ruzuku CUF.......Benki ya NMB Yalaumiwa kwa Kuvujisha Siri

$
0
0
Siri kwamba Profesa Ibrahim Lipumba amefungua akaunti mpya yenye jina la chama cha Wananchi CUF imefichuka. Wanaolaumiwa kutokana na kufichuka kwa siri hiyo ni watumishi wa benki ya NMB tawi la Ilala.

Prof. Lipumba ni Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa huku chama chake kikiwa tayari kimemfukuza uanachama.

Abdul Kambaya, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma anayetambulika na Msajili wa Vyama Vya Siasa pia huku Baraza Kuu la Uongozi la CUF likiwa limemsimamisha uanachama, amenukuliwa na gazeti la Tanzania Daima, akilaani kitendo cha benki ya NMB kuvujisha taarifa za akaunti mpya ya Prof. Lipumba.

“Aulizwe Meneja wa NMB Ilala, kutoa siri za wateja, hayo ndiyo maadili ya kazi yake? Uko wapi usiri kati ya mteja na benki?” alihoji Kambaya.

Hata hivyo, alipotafutwa Kambaya  ili kufafanua uanzishwaji wa akaunti hiyo, matumizi yake na kama yamezingatia matakwa ya Katiba ya CUF na Sheria ya Vyama Vya Siasa, hakuwa tayari kufafanua akidai kuwa si wakati muafaka.

“Tutaeleza mambo hayo kwa wakati muafaka, kama kuna jambo tunakuwa accused (tunatuhumiwa), iulizeni ofisi ya msajili au benki husika, wao wana taarifa kamili,” alisema.

Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa kupitia Sisty Nyahoza imenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari ikikiri kumtambulisha Prof. Lipumba kwa benki ya NMB ili aweze kufungua akaunti hiyo, hata hivyo amedai kuwa ofisi ya msajili haijui matumizi ya akaunti hiyo.

Taarifa za kufunguliwa kwa akaunti mpya yenye jina la CUF kwa malengo yanayodaiwa ni kuchukua ruzuku za chama hicho zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii Alhamis ya tarehe 06 Septemba mwaka huu.

Uongozi wa CUF taifa kupitia kwa Mbarara Maharagande, Naibu Mkurugezi wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma umesema kuwa, utatoa taarifa rasmi juu ya suala hilo  leo Jumatatu, tarehe 10 Oktoba.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Yatupiwa Lawama Kwa Kuchelewa Kutoa Majina ya Wanufaika wa Mikopo

$
0
0
Wakati vyuo vikuu vikikaribia kufunguliwa, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imelaumiwa kwa kuchelewa kutoa majina ya wanufaika huku yenyewe ikisema itahakikisha majina yanatolewa sanjali na tarehe za vyuo kufunguliwa. 

Pia, HESLB imesema miongoni mwa vipaumbele vitakavyozingatiwa kwenye utoaji wa mikopo katika mwaka wa masomo 2016/2017 ni kwa wanafunzi wenye mahitaji makubwa, waliotoka kwenye kaya masikini, waliosoma shule za kata na waliotoka vijijini. 

Kauli hiyo imekuja baada ya bodi hiyo kutupiwa lawama kwa kuchelewa kutoa majina ya wanufaika wa mikopo kabla hawajaripoti vyuoni, hasa wanafunzi wa mwaka wa kwanza.

Mkurugenzi wa mtandao wa haki za wanafunzi (TSNP), Shitindi Venance alisema hadi sasa wanafunzi wanaojiunga na masomo ya elimu ya juu nchini kwa mwaka wa kwanza wa masomo 2016/2017, ambao wameomba mkopo bado hawajui ni kiasi gani wamepewa. 

Malalamiko ya Shitindi yamerejea kilichotokea mwaka jana baada ya wanafunzi kuripoti vyuoni, lakini majina yalipotolewa na bodi hiyo baadhi yao hawakuwa wanu- faika hali iliyosababisha usumbufu. 

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema miongozo ya utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka huu ni tofauti na mwaka jana. 

“Utaratibu wa mwaka huu ni tofauti kwa kuzingatia wanafunzi wanaoanza masomo na wale wanaoendelea na masomo katika vyuo mbalimbali,” alisema Badru. 

Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa majina ya wanufaika wa mikopo yataanza kutolewa kwa kuzingatia tarehe ambayo chuo husika kinafunguliwa.

 “Kila chuo kinafunguliwa kwa mujibu wa tarehe iliyopangwa kwa hiyo na sisi tunatoa majina kuendana na utaratibu wa chuo husika,” alisema. 

Hata hivyo, Badru alisema uta- ratibu wa kupanga viwango vya mikopo kwa wanafunzi na kisha kutoa orodha ya majina ya wanufaika haihusishi bodi ya mikopo peke yake. 

Alisema kabla ya kuidhinisha majina ya wanufaika na mikopo, lazima Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) iwe imeshatoa orodha ya majina wa wanafunzi ambao imewadahili kwa kuzingatia vigezo vyao, halafu majina hayo yatumwe vyuoni. 

Alisema mzunguko wote huo unahitaji muda na umakini wa hali ya juu ndiyo maana huchukua muda.

Rais Magufuli Apokea Hati Za Utambulisho Kutoka Kwa Mabalozi Wa Nchi Mbalimbali Ikulu Jijini Dar Es Salaam 10th Oktoba 2016

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 10 Oktoba, 2016 amepokea hati za utambulisho za mabalozi wanne wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mabalozi waliowasilisha hati zao za utambulisho Ikulu Jijini Dar es Salaam ni Balozi wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mhe. Mahjoub Ahmed Abd Allah Sharfi, Balozi wa Jamhuri ya Slovakia hapa nchini Mhe. Frantisek Dlhopolcek, Balozi wa Ukraine hapa nchini Mhe. Yevheni Tsymbaliuk na Balozi wa Jamhuri ya Ghana Mhe. Kwame Asamoah Tenkorang.

Rais Magufuli amezungumza na Mabalozi hao kwa nyakati tofauti baada ya kupokea hati zao za utambulisho, ambapo wamesisitiza umuhimu wa kuendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hizo kwa kujikita zaidi katika biashara na uwekezaji.

"Mhe. Balozi najua nchi yenu ya Sudan ina utajiri wa mafuta na imefanikiwa kujenga uchumi wake kupitia mafuta, sisi pia hapa nchini tumebaini uwepo wa mafuta na gesi asilia katika baadhi ya maeneo, ningependa uhusiano na ushirikiano wetu sasa ujielekeza katika kubadilishana uzoefu na ujuzi wa namna tunavyoweza kunufaika na mafuta na gesi"  amesema Rais Magufuli alipokuwa akizungumza na Balozi wa Sudani hapa nchini Mhe. Mahjoub Ahmed Abd Allah Sharfi.

Dkt. Magufuli pia ametoa wito kwa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi za Sudan, Slovakia, Ukraine na Ghana kuja kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali zikiwemo Mafuta na gesi, Kilimo, Uvuvi, Mbuga za wanyama, Madini na ufugaji.

"Hivi sasa Tanzania ipo katika mpango wa ujenzi wa viwanda na pia tunatekeleza mpango wa pili wa maendeleo, hivyo nakuomba Mhe. Balozi uwahamasishe wafanyabiashara na wawekezaji wa Ukraine waje wawekeze katika viwanda kwani soko la uhakika la bidhaa lipo" amesisitiza Dkt. Magufuli alipokuwa akizungumza na Balozi wa Ukraine hapa nchini Mhe. Yevheni Tsymbaliuk.

Aidha, Rais Magufuli amewasihi Mabalozi wa Slovakia, Ukraine na Ghana ambao makazi yao ya Ubalozi yapo Mjini Nairobi nchini Kenya kuanzisha Ubalozi wao hapa nchini ili kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano katika masuala ya biashara na uwekezaji.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Oktoba, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi mteule wa Ghana hapa nchini Kwame Asamoah Tenkorang mara baada ya kupokea Hati yake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Balozi mteule wa Ghana hapa nchini Kwame Asamoah Tenkorang Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan Mahjoub Ahmed Abdallah Sharfi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mahjoub Ahmed Abdallah Sharfi mara baada ya kupokea Hati yake ya utambilisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mahjoub Ahmed Abdallah Sharfi mara baada ya kupokea Hati yake ya utambilisho Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mahjoub Ahmed Abdallah Sharfi mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mahjoub Ahmed Abdallah Sharfi mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Ukraine hapa nchini Yevhemsi Tsymbalik Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi mteule wa Ukraine hapa nchini Yevhemsi Tsymbalik mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi mteule wa Ukraine hapa nchini Yevhemsi Tsymbalik mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa balozi mteule wa Jamhuri ya Slovakia Frantisek Dlhopolcek Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru balozi mteule wa Jamhuri ya Slovakia hapa nchini Frantisek Dlhopolcek mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na balozi mteule wa Jamhuri ya Slovakia hapa nchini Frantisek Dlhopolcek mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.Picha na Ikulu

Mahakama Kuu Yatoa Kibali Kwa CUF Kufungua Kesi Dhidi ya Msajili wa Vyama na Lipumba ....... Bodi Ya Wadhami wa Chama Hicho Yatoa Onyo Kali Kwa Mabenki Hapa Nchini

$
0
0
Wakati taariza zinazomtuhumu Profesa Ibrahim Lipumba kufungua akaunti benki kwa lengo la kuingiziwa fedha za ruzuku ya Chama cha Wananchi (CUF) kinyume cha sheria kwa ajili ya kukivuruga chama hicho zikienea.

Bodi ya Wadhamini ya CUF imetoa onyo pamoja na kuwatahadharisha watu wanaotumika kusaini nyaraka feki kwa lengo la kufungua akaunti hizo, pia imezitahadharisha benki zote nchini kutofungua akaunti yoyote kwa jina la CUF pasipo kupata muhtasari wa bodi halali ya chama hicho.

Katika hatua nyengine, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi CUF, Julias Mtatiro amefafanua kuwa wenye mamkaka halali ya kufungua akaunti ya chama hicho ni Bodi yake ya wadhamini pamoja na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamadi.

“Tunatoa onyo, kwa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, kwamba tumeshafungua shauri na utaratibu wa kisheria umeshaanza kuchukua mkondo wake, tumesikitika kwamba kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, kinyume cha sheria namba tano 1992 ya vyama vya siasa na kinyume cha katiba, Msajili kwa mara ya kwanza anaziandikia benki zilizosajiliwa na BOT akizitaka kumfungulia akaunti Lipumba za kuwekea fedha,” amesema Mtatiro.

Mtatiro amedai kuwa ”Benki itakayomfungulia akaunti Lipumba ni makosa makubwa. Sababu huwezi fungua akaunti ya taasisi au chama bila ya bodi yake ya wadhamini kukaa kikao na kuandaa muhtasari kwa ajili ya kupeleka benki ili kufungua akaunti.Lipumba na watu wake wameandaa nyaraka feki pamoja na barua ya msajili kutaka kufungua akaunti. Tunajua amepeleka katika benki mbalimbali,

“NMB ilikataa sasa wanapeleka benki ya Exim na ilishapewa taarifa kuwa uhuni huu haukubaliki na masuala ya fedha yako chini ya katibu mkuu kwa mujibu wa katiba ya cuf,” amesema.

Sambamba na onyo lililotolewa na bodi hiyo, Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo imekubali maombi yake ya kufungua shauri la kuitaka mahakama hiyo kutoa amri dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi ya kutoendesha shughuli zake za usimamizi wa vyama vya siasa kinyume cha sheria, pamoja na kutengua barua yake inayomtambua profesa Ibrahim Lipumba kama mwenyekiti halali wa chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasilisha maombi hayo, Wakili Juma Nassoro amesema kuwa Jaji wa mahakama hiyo Munisi, amekubali maombi yao na kwamba jopo la mawakili wa CUF linatarajia kuwasilisha maombi rasmi wiki hii.

“Jaji Munisi baada ya kutusikiliza vifungu vya sheria tulivyotumia, Mahakama imekubali ombi letu ili tuweze kufungua maombi ya kuomba mahakama itamke kufuta barua ya msajili inayomtambua Lipumba kama mwenyekiti halali wa CUF. Pia Itoe zuio rasmi kwa msajili kutofanya shughuli zake nje ya utaratibu ambao amepewa chini ya sheria ya vyama vya siasa,” amesema Nassoro.

Amesema baada ya mahakama kuridhia maombi yao, iliwataka kuwasilisha maombi rasmi ndani ya siku14 kuanzia leo.

“Tumeambiwa tuwasilishe maombi ndani ya siku 14, lakini tutayawasilisha ndani ya siku Saba na tutaiomba mahakakama iyasikilize kwa Hati ya dharula ili shughuli za chama ziendelee,” amesema.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Octobar 11

Tiba Asilia Ya Tatizo La Kukonda Na Kudhoofika Mwili

$
0
0
Utangulizi

Kukonda, kudhoofika  na/ ama  kupungua  uzito  bila  sababu  ni  tatizo  linalo  wakabilia  watu wengi  duniani.
 
Mgonjwa  hupungua    hukonda, kudhoofika  na  kupungua  uzito kwa  kasi  bila   sababu  ya  msingi  kama  vile  kuanya  diet  maalumu  ya  kupunguza  uzito  au  kufanya  mazoezi  maalumu  ya  kupunguza  uzito.
 
Hali  hii  ( kupungua  mwili na  uzito  bila  kufanya diet  au  mazoezi)  inapotokea, ndipo  tunasema, mhusika  amedhoofu  mwili.

Chanzo  Cha  Tatizo  La  Kudhoofu  Mwili
Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitabibu,  tatizo  la  kupungua  uzito na  kudhoofu  mwili, husababishwa  na  mambo  yafuatayo ;

i.Kuugua  magonjwa  na  maradhi  mbalimbali  kama  vile  kisukari  nakadhalika.
ii.Ukosefu  wa  lishe  bora
iii. Msongo  wa  mawazo
iv.Ukosefu  wa  hamu  ya  kula

Dalili   Za  Mtu  Aliye  Dhoofu  Mwili
Dalili  za  mtu  aliye  dhoofu  mwili, hutegemea  na  aina  ya  kirutubisho  ambacho mwili  umekikosa.

Lakini  hata  hivyo, zipo dalili  za  ujumla, ambazo huwatokea  watu wengi wenye  tatizo  la  kudhoofu  mwili.’

Dalili  hizo  ni  pamoja na :
i. Ngozi  kupauka
ii.Kujisikia  uchovu
iii. Mwili  kuwa  mwepesi  na  dhaifu
iv. Kupungua  uzito  kwa   kiwango kikubwa
v. Kupumua  kwa shida
vi. Mhusika kupenda  sana  chakula  cha  aina  moja  tu ilihali  hakiwa  hana appetite kabisa  na vyakula vya  aina nyingine.
vii.Nywele  kunyonyoka
viii. Kukosa  choo  ama  choo  kufunga
ix.  Mapigo  ya  moyo kwenda  kasi
x. Mwili kuishiwa  nguvu
xi. Miguu  kukosa  ganzi
xii.Kwa  wanawake : kupatwa  matatizo mbalimbali  ya  hedhi.

Tiba  Asilia  Ya  Tatizo  La Kudhoofu  Mwili
DAWA-LISHE   ni  tiba asilia inayo tibu  na  kuponyesha kabisa  tatizo la  kudhoofu mwili.

Tiba  hii  husaidia  kuunenepesha na   kuupa  nguvu  mwili  na  kuurejesha  katika  hali  yake  ya  kawaida.

Tiba  hii ni  ya  asili  kabisa ( Pure  HERBAL ), isiyo na  kemikali za  viwandani.

GHARAMA :  Dawa  hii, inapatikana  kwa gharama  ya  SHILINGI  ELFU  HAMSINI (Tshs.50,000/=)

Inauzwa   na  kusambazwa  na  duka  la  dawa  za asili  la  NEEMA  HERBALIST. Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM, nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA, jirani na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING.

Kwa  wateja  waliopo  Dar  Es  Salaam, ambao  hawana  nafasi  ya  kuja  ofisini, watapelekewa  dawa  mahali  walipo  (  Home &  Ofice  Delivery )

Kwa  wateja  waliopo  mikoani, watatumiwa  dawa  kwa  mabasi  mbalimbali.

Kwa  waliopo  Zanzibar, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  boti.

Kwa  wateja  waliopo Mombasa, watatumiwa  dawa  kwa  gari  la  TAHMEED.

Kwa  wateja  waliopo  Nairobi, watatumiwa  dawa  kwa njia  ya  basi  la  DAR  EXPRESS.

Wasiliana  nasi  kwa  simu  namba   0766  53  83  84.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu huduma zetu, endelea  kututembelea  kila  siku, katika  blogu yetu:

Wizara ya Afya yatoa ufafanuzi uwepo wa Dawa nchini

$
0
0
Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa katika baadhi ya vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii vikizungumzia hali ya dawa nchini hasa kufuatia taarifa zilizotolewa na taasisi ya kiraia na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa.

Taarifa hizo zilidai kwamba katika kipindi hiki kuna upungufu mkubwa wa dawa katika bohari kuu ya dawa , Hivyo, kusababisha kukosekana kwa dawa katika vituo vya kutolea huduma za Afya.

Taarifa hizi si sahihi na zinalenga kupotosha umma na kuwatia wananchi wasiwasi. Napenda kuwathibitishia wananchi kuwa Afya ni suala la kipaumbele kwa Serikali ya Awamu ya Tano. Hivyo, ningependa kutoa ufafanuzi kwa wananchi katika masuala yafuatayo; –

Hali ya Upatikanaji wa dawa
Hali ya upatikanaji wa dawa kwa sasa iko vizuri. Dawa muhimu zinazohitajika  sana nchini zinapatikana kwenye maghala ya Bohari ya Dawa (MSD). Mfano kwa upande wa dawa za antibiotics tuna Amoxycillin, Ciprofloxacin, Cotrimoxazole na Doxycycline. Kwa upande wa dawa za maumivu – tunazo za kutosha kama vile paracetamol, asprin na diclofenac.

Pia tuna dawa za kutosha za malaria, Kifua Kikuu, ukoma na dawa za kufubaza makali ya UKIMWI (ARVs). Kwa upande wa chanjo za watoto na wajawazito, ni kweli kulikuwa na uhaba nchini kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita. 

Hata hivyo, wiki iliyopita Serikali imenunua na kupokea dozi milioni 2 za chanjo ya Kifua Kikuu (BCG), dozi milioni 1.2 za Polio na dozi milioni za Polio. Chanjo hizi zinasambazwa katika vituo vya afya nchini.

Dawa nyingine zitaendelea kupatikana katika Bohari kuu ya Dawa kwa kuwa tumeagiza dawa za kutosha kutoka kwa wazalishaji wa ndani na nje ya nchi. 

Aidha, kiasi kikubwa cha dawa zinazowasili Bohari kuu ya Dawa zikifika zinapelekwa kwenye Kanda nane za MSD pamoja na vituo viwili vya Mauzo kwa ajili ya kuwasambazia wateja walioagiza. 

Hivyo, kipimo cha upatikanaji wa dawa si kuangalia katika maghala ya Bohari ya Dawa peke yake bali pia katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Ili kuondoa mlolongo wa manunuzi ya dawa, tunapenda kuwataarifu kuwa Bohari kuu ya Dawa imepanua wigo wa upatikanaji wa dawa kwa sasa kwa kutumia mikataba ya muda mrefu (miaka miwili) na washitiri wa ziada wa ndani (Prime Vendors) ili kuhakikisha dawa zinapokosekana MSD zinapatikana kwa haraka kwa Washitiri wa ndani waliothibitishwa katika kila mkoa.

Katika muktadha huo huo, Bohari ya Dawa imefungua maduka ya ziada kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa dawa zaidi ya aina 600 kupitia mfumo wa maduka katika mahospitali kama vile Muhimbili, Mbeya na Arusha.

Bajeti ya dharura kwa ajili ya dawa
Ni muhimu wananchi wakajua kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya manunuzi ya dawa katika mwaka wa fedha 2016/17 zinatosha kuhudumia mahitaji ya dawa kwa mwaka mzima. Hivyo hakuna sababu ya kuwa na bajeti ya dharura.

Niwakumbushe bajeti zilizotengwa kwa ajili ya kununulia dawa na vifaa tiba katika miaka michache iliyopita mpaka hivi sasa, kama ifuatavyo: -.

Mwaka 2011/2012 bajeti iliyotengwa ilikuwa shilingi Bilioni 23.7

Mwaka 2012/2013 bajeti ilikuwa shilingi Bilioni 34

Mwaka 2013/2014 ilikuwa shilingi Bilioni 34

Mwaka 2014/2015 ilikuwa shilingi Bilioni 60

Mwaka 2015/2016 ni shilingi Bilioni 30

Na mwaka huu 2016/17 ni shilingi Bilioni 251.5

Mkakati wa Wizara kwa sasa ni kuhakikisha kuwa fedha hizo zinapatikana kwa wakati kutoka Hazina kulingana na makusanyo ya nchi.

Vilevile ieleweke kwamba tayari serikali imeshatoa kiasi cha shilingi bilioni 20 katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2016/17,  kwenda Bohari kuu ya Dawa kwa ajili ya ununuzi wa dawa na chanjo. Hali hii inathibitisha kuwa suala la upatikanaji wa dawa ni la kipaumbele kwa Serikali ya Awamu ya tano.

Kulipa Deni la Bohari ya Dawa (MSD)
Napenda kuwafahamisha kuwa Serikali imedhamiria kulipa deni lote la Bohari ya Dawa (MSD) ambapo katika mwaka huu wa fedha 2016/17 tayari Bilioni 85 imekwishatenga kwa ajili ya kulipa deni hilo.Jambo ambalo halijawahi kutokea huko nyuma. Kulipwa kwa deni hilo kutasaidia kuhuisha mtaji wa MSD (revolving fund) na hivyo kuiwezesha MSD kuwa na dawa na vifaa tiba kwa kiwango kikubwa.

Aidha serikali imekwisha kuviagiza vituo vyote vinavyotoa huduma za Afya kupitia Halmashauri zao, kuhakikisha zinakuwa na fedha ya mzunguko kwa ajili ya kununulia dawa (revolving fund) na hivyo kupata dawa kwa kulipa fedha taslimu kutoka Bohari ya Dawa badala ya kukopa.

Fedha hizo zitapatika kutoka kwenye vyanzo vyao vingine vya mapato kama vile Bima ya Afya (NHIF, CHF) na gharama wanazochangia wananchi katika kupata huduma. Hii itawezesha kutoendelea kukuza deni kutoka Bohari ya Dawa na kuhakikisha dawa zinapatikana kwa wakati wote.

MSD Kupata Mshindani
Katika mwaka 2015, Serikali ilimpa kazi mshauri mwelekezi wa kampuni ya ushauri iliyobobea kimataifa ya Deloitte ya kulitazama jambo hili kwa ajili ya kuifanyia tathmini MSD pamoja na mambo mengine ikiwemo kuangalia suala ya kutafutiwa mshindani katika manunuzi na usambazaji wa dawa.

Napenda kuwajulisha kuwa tathmini hiyo ilionyesha kuwa MSD kutafutiwa mshindani itakuwa ni kuongeza gharama kubwa kwa serikali kutokana na kurudufisha (duplication) majukumu. 

Pia ilibainika kuwa suala la dawa ni muhimu, hivyo Serikali haiwezi kuliacha kwenye mikono ya watu binafsi.Jambo ambalo lilipendekezwa ni kuifanyia maboresha makubwa MSD ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Utekelezaji wa mapendekezo hayo tayari umeshaanza.

Nchi ambazo zinaiuzia dawa na vifaa tiba MSD
MSD inaagiza dawa na vifaa tiba nje ya nchi zaidi ya asilimia 80 kwa sababu viwanda vilivyoko ndani ya nchi havikidhi mahitaji ya nchi kwa ubora na kiasi. Hivyo, MSD hununua dawa na vifaa tiba kutoka nchi za India, China, Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Ujerumani, Marekani, Ufaransa na sehemu nyingine duniani.

Kwa mfano, tuna dawa zaidi ya aina  nne ambazo zinanunuliwa kutoka Kenya (Dawa ya kutibu malaria kwa akina mama wajawazito ijulikanayo kama Sulfadoxine Pyrimethamine (SP), dawa ya kutibu magonjwa ya maambukizi ya Cotrimoxazole  ya watu wazima na watoto pamoja, Amoxicilline  na Paracetamol ya maji kwa ajili ya watoto.

Ikumbukwe kuwa MSD hununua dawa hizi kupitia mchakato wa zabuni, ikiwa baadhi ya vigezo ni kuangalia usajili wa dawa nchini pamoja na ushindani wa bei. Hata hivyo, ili kukuza viwanda vya ndani, watengenezaji wa dawa wa ndani hupewa hadi 15% ya upendeleo katika mchakato wa tathmini ya zabuni dhidi ya dawa zinazotoka nje ya nchi (Domestic preference).

Kwa upande mwingine mkakati wa serikali sio kuendelea kutegemea dawa kutoka nje ya nchi, kwani kwa kufanya hivi uchumi wa nchi hautakuwa. hivyo basi serikali iko katika hatua za mwisho za utaratibu wa kuwakaribisha wawekezaji wa viwanda vya kuzalisha dawa kuwekeza nchini kwa mpango wa kuwashirikisha wadau wengine katika masuala ya dawa  (PPP).

Hitimisho
Wizara ya afya inapenda kuwahakikishia wananchi kuwa itasimammia ipasavyo utapatinaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba nchini kwa wakati na kwa bei nafuu kwa kuwa Sera ya afya inawataka wananchi kuchangia huduma.

Aidha vituo vya kutolea huduma za Afya vinahimizwa kupeleka mahitaji na maoteo yao ya dawa kwa wakati badala ya kusubiri hadi dawa zote muhimu zimeisha kabisa katika vituo vyao. Pia wanakumbusha kulipa madeni wanayodai na bohari ya dawa sambamba na kuhakikisha fedha inayopatikana katika shughuli za utoaji huduma inatumika kwa ajili ya dawa, vifaa na vifaa tiba.

 Ili kuondoa vikwazo kwa wananchi katika kupata dawa na huduma za afya kwa ujumla wananchi wanahimizwa kujiunga na mifuko ya Bima ya Afya kwani hakuna anayejua leo hama kesho ataugua na Magonjwa hayapigi hodi na wakati mwingine yanakukuta hauna  akiba ya fedha, ila ukiwa na bima wakati wowote unapata matibabu.

Mwisho, Wizara itaendelea kuhakikisha kuwa kuna dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara vya kutosha kwenye vituo vya umma vya kutolea huduma za Afya nchini

CCM Waigomea CUF Zanzibar.....Wasema Hawako Tayari Kujadili Uchaguzi Mkuu 2015

$
0
0
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar  kimesema hakina mpango wa kufanya mazungumzo au makubaliano na Chama Cha Wananchi (CUF) kuhusiana na suala la Uchaguzi uliopita.

Msimamo huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alipokuwa akijibu hoja zilizotolewa na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CUF Ismail Jussa Ladhu katika Mahojiano Maalum na Gazeti moja hapa nchini Juzi.

Alisema  Uchaguzi umekwisha kazi iliyokuwepo mbele ya CCM ni kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho ya mwaka 2015/2020 ili kuhakikisha ahadi zilizotolewa katika kampeni za uchaguzi mkuu na viongozi wa CCM zinatekelezwa kwa vitendo.

Vuai alieleza kwamba kupitia  Mazungumzo na Gazeti la NIPASHE JumaPili Octobar  9, mwaka huu, Jussa alinukuliwa akisema  CUF inaangalia uwezekano wa kufanya mazungumzo na CCM kuhusiana na suala la uchaguzi, jambo ambalo CCM haipo tayari kukaa meza moja na Chama hicho kujadili jambo ambalo lishafanyiwa uamzi halili kwa mujibu wa kanuzi,taratibu na Sheria za nchi.

Alisema  Chama hicho kinaweza kukikaribisha Chama chochote cha upinzani kufanya mazungumzo juu ya namna gani ya kuimarisha na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM na siyo suala la Uchaguzi Mkuu kwani umepita kisheria na serikali zinaendelea kuwatumikia wananchi kwa uadilifu.

Alisema kitendo cha kujadili  serikali zote mbili ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa sasa ni kwenda kinyume na Sheria za nchini kwani  serikali hizo zimetokana na maamuzi halali ya wananchi kupitia mfumo wa Uchaguzi wa kidemokrasia.

Aliwataka wafuasi wa Chama hicho na Wananchi kwa ujumla kupuuza  madai yaliyotolewa na Kiongozi huyo hasa mantiki ya kuundwa kwa serikali ya mpito Zanzibar , hatua ambayo haiwezekani na inaashiria kuvunja Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984.

“CCM hatuna mpango wa kukaa meza moja na Chama chochote cha upinzani na sio CUF tu, kujadili Uchaguzi kwani tayari umepita kwa vigezo vyote vya uhalali wa kisheria.

"Pia Hoja na Ajenda  ya kufanyika kwa Uchaguzi wa Mpito Zanzibar  kwa sasa ni ndoto za mchana ama kujifurahisha kwa kutafuta umaarufu wa kisiasa usiokuwa na uzani wala  mafanikio kwa wafuasi wa Chama kinachojenga hoja hizo hapa nchini.”, alisema Vuai na kuongeza kuwa CCM inaamini kwamba Uchaguzi umekwisha na sasa inajipanga na maandalizi ya Uchaguzi ujao wa mwaka 2020.

Naibu Katibu Mkuu huyo, alifafanua kwamba CUF kwa sasa imekosa muelekeo ndiyo maana viongozi wake wanafikia hatua ya kuwadanganya wafuasi wao kwa mambo ambayo kiuhalisia wanajua kuwa hayawezekani kufanyika katika historia ya uwanja wa kisiasa Zanzibar.

Alisema Chama cha kisiasa chochote pamoja na kuwa na jukumu la kushinda na kusimamisha Dola katika uchaguzi mkuu bado kinatakiwa kuwa na miongozo imara ya kusimamia ukweli, haki na uwazi kwa wafuasi na wananchi, vigezo ambavyo vimekosekana ndani ya CUF toka kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Alisisitiza kwamba kazi iliyopo mbele ya Chama hicho ni pamoja na kujiandaa kwa mambo mbali mbali yakiwemo Uchaguzi wa ndani wa CCM wa mwaka 2017, kwa ajili ya kupata viongozi makini na mahodari ambao pia watakuwa na jukumu la kusimamia maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2020.

Alilitaja jukumu la msingi linalotekelezwa na chama hicho ni pamoja na uhakiki wa Mali za CCM ili kujiridhisha zaidi ikiwa ni mkakati wa uimarishaji hali ya siasa na uchumi ndani ya CCM.

Aliwasihi  wafuasi wa Chama hicho na wananchi kwa ujumla kuendelea kuwa watulivu na kushirikiana kikamilifu na serikali zote mbili Serikali ya Awamu ya saba ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya awamu ya Tano ya  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .

Aidha aliwataka wananchi kuwafichua baadhi ya wanasiasa wanaojihusisha na vitendo vya kuharibu amani na utulivu wa nchi.

Adhabu ya Kunyongwa : Wafungwa 472 wasubiri hatma yao kutoka kwa Rais Magufuli

$
0
0
Watu 472 waliohukumiwa adhabu ya kifo kutokana na makosa mbalimbali, wanasubiri saini ya Rais Dk. John Magufuli ili kujua hatima ya utekelezaji wa adhabu zao ama laa.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa kati ya watu hao, wanaume ni 452 na wanawake ni 20.
 
Taarifa hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Hellen Kijo-Bisimba, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu adhabu ya kifo.

Bisimba alisema, watu hao walihukumiwa adhabu ya kifo kutokana na kutiwa hatiani na makakama kwa makosa ya uhaini na mauji.

Licha ya adhabu hiyo alisema hatua ya utekelezaji wake inakwenda kinyume na haki za binadamu kama inavyotafsiriwa katika matamko na mikataba mbalimbali ya kimataifa.

Kutokana na hali hiyo, Dk. Kijo-Bisimba, alisema hadi kufikia Desemba mwaka jana, jumla ya watu 472 walikuwa wamehukumiwa adhabu hiyo.

Alisema wakati watu hao wakisubiri adhabu hiyo, wengine 244 waliopo katika magereza mbalimbali bado wanasubiria maamuzi ya rufaa zao.

“Licha ya adhabu hii kutotekelezwa hapa nchini kwa takriban miaka 22 na miaka 24 ya kwanza ya uhuru, taarifa zinaonesha kuwa hadi sasa ni watu 72 tu ambao wameshanyongwa kutokana na adhabu hiyo,” alisema.

Dk. Kijo-Bisimba alitoa taarifa hiyo katika kipindi cha kuelekea maadhimisho ya siku ya kupinga adhabu ya vifo duniani, ambayo itafanyika katika nchi 70 na kaulimbiu ikiwa ni “Kuua ni Nyenzo ya Kigaidi, Acha Mnyororo wa Kigaidi,”.

“Leo ni miaka 14 tangu wanaharakati walivyoamua kuwepo kwa siku hii tusipokuwa na uhai hatuwezi kufanya kitu chochote hivyo adhabu hii haina maana kwani inaingilia haki ya uhai wa binadamu na kuona si kitu cha thamani,” alisema Bisimba.

Mkurugenzi huyo alisema, hadi sasa nchi 140 duniani zimeshafuta adhabu hiyo, ambapo kwa upande wa Afrika nchi 17 zimeshakubali kufuta adhabu hiyo.

Hata hivyo alisema ni wakati mwafaka kwa Serikali kuondoa adhabu hiyo, ili Tanzania iwe nchi ya 18 katika bara la Afrika kufuta adhabu hiyo, ambayo haina faida yoyote.

Mkurugenzi huyo wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, alisema kuwa adhabu hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa ikiwamo kuwapa marais ugumu kuweka saini kwa mtu kuuawa.

“Ni miaka 22 sasa nchi yetu haijawahi kutekeleza adhabu hiyo kwani Rais ndiye anayeruhusiwa kwa mujibu wa sheria lakini hata wao wanaogopa kufanya hivyo ili mtu mwingine afe badala yake wangetoa adhabu mbadala kwani wengine wanaofanya makosa hayo ni vichaa,” alisema.

Alisema adhabu hiyo ni ya kibaguzi na huwatia hatiani watu maskini wasiokuwa na uwezo wa kujitetea mahakamani au kuweka mawakili.

Dk. Bisimba, ameiomba Serikali isitunge tena sheria ya kifo na ikiwezekana ya sasa ikiwemo iliyoongezwa ya makosa ya ugaidi iondolewe na kutafutwa adhabu mbadala kwa mtu atakayetiwa hatiani.

“Adhabu ya kifo imeainishwa kwenye Sheria ya Kanuni ya Adhabu, sura ya 16 ‘Penal Code’ ambayo ililetwa na utawala wa kikoloni mwaka 1945. Hata baada ya Uhuru 1961 hukumu ya kifo imeendelea kuwa sehemu ya sheria licha ya marekebisho mbalimbali ya sheria hiyo ikiwemo marekebisho ya mwaka 2002.
 
“Adhabu ya kifo hutolewa kwenye makosa ya mauaji chini ya sheria hiyo kifungu 197 na kwenye hati ya kosa la uhaini chini ya kifungu cha 39 (3) (C).

“Pamoja na hayo mwaka huu Serikali imeongeza adhabu ya kifo kama mtu akikutwa na kosa la ugaidi chini ya sheria ya kudhibiti ugaidi ya mwaka 2002 kwenye mabadiliko madogo ya sheria, hii imeengeza makosa ambayo mtu anaweza kuhukumiwa kifo kufikia makosa matatu,” alisema Dk. Bisimba

Alisema kwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu na mikataba mbalimbali ya kikanda na kimataifa ya haki za binadamu, zipo sababu za msingi za kupinga adhabu ya kifo.

“Tunapenda kuweka wazi kuwa hatufurahii watu kuua watu wengine na ndiyo maana hatungependa hata muuaji auawe kwa vile ni sawa na kumkubalia kuua. Adhabu ya kifo ni ya kinyama na isiyo na staha, inayotweza utu wa ubinadamu na hufanya Serikali ionekane pia kama mhalifu kwa kuua.

“Adhabu hii ikitolewa kwa mtu asiye na hatia kimakosa huwezi kuirekebisha kwani mfumo wa utoaji haki huwa pia na mianya ya makosa na hivyo maisha ya mtu yanweza kupotea bure na hakuna ushahidi kama adhabu hii inazuia watu wengine kutotenda makosa kama hayo,” alisema

Mbali na maadhimisho hayo kituo hicho kilizindua kitabu kinachoelezea adhabu ya kifo na ukiukwaji wa Haki za Binadamu cha mwaka 2015.

Utafiti wadai mtu mmoja kati ya wanne ni kichaa, Wizara yaeleza sababu

$
0
0

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Ummy Mwalimu amesema utafiti unaonesha kuwa kwa kila watu wanne duniani, mmoja ana matatizo ya afya ya akili.

Alisema hayo jana kwenye maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili Duniani yaliyofanyika kitaifa Dar es Salaam chini ya kaulimbiu: “Utu katika Afya ya Akili, Huduma za Kisaikolojia na Afya ya Akili kuwa Huduma ya Kwanza kwa Wote”.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy wananchi wanapaswa kuwa makini kuchunguza afya zao za akili kwa sababu utafiti wa Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaashiria kuwa jamii kwa sasa inakumbwa na maradhi mengi ya namna hiyo.

“Takwimu kwamba kila watu wanne, mmoja wao ana ugonjwa wa akili ni kielelezo tosha kwamba ipo haja ya jamii kujitambua na kuona umuhimu wa kupewa elimu ya afya ya akili na kisaikolojia,” alisema na kufafanua:

“Magonjwa ya akili ni yanayoathiri uwezo wa mtu kufikiri, kuhisi, kutambua na kutenda, hivyo kuwa na tabia au mwenendo ulio tofauti au usioendana na jamii husika kiimani, kimila, desturi na nyanja nyingine za kijamii.”

Aliongeza: “Tunapaswa kukumbuka kuwa hakuna afya njema ya kimwili kama hakuna afya ya akili; na pia nchi yetu ikiwa na wananchi wenye afya bora ya akili ni hazina kubwa kwa Taifa.”

Ummy alibainisha: “Miongoni mwa watu wanaopata matatizo ya kiakili ni wachache tu ambao wanaweza kufikia na kupata huduma ya afya ya akili, hata hao wanaohudhuria vituo vya afya, ni wachache wamekuwa wakipata huduma stahiki.

“Katika nchi yetu tumekuwa tukikabiliwa na matatizo kama hayo kutokana na ufinyu wa bajeti, ukosefu wa wataalamu katika vituo vya kutolea huduma, ukosefu wa vifaatiba na dawa kwa wagonjwa wenye matatizo ya akili, kijamii na kisaikolojia.”

Waziri Ummy alisema hali hiyo inatokana na matatizo yanayoikabili jamii yakiwamo majanga yanayoiandama dunia.

Mwalimu alitoa mfano kwamba, mwaka jana Tanzania ilionesha kuwa na wagonjwa wa afya ya akili 311,789 kulingana na takwimu za waliokwenda hospitali kuchunguzwa.

 Alibainisha kwamba hali hiyo inaashiria kuwa idadi hiyo ni kubwa zaidi, kwa sababu kuna ambao wana matatizo hayo lakini hawaendi hospitali au wamekuwa wakienda kupata huduma tofauti.

Alisisitiza kuwa katika kukabaliana na ukweli huo, jitihada zimefanywa na serikali kutoa huduma za afya ya akili na saikolojia.

Mwalimu alisema Serikali itaendelea kuongeza juhudi katika kutoa huduma na elimu ya afya ya akili kuanzia ngazi ya msingi na kuwa na kitengo maalumu kinachotoa huduma hizo katika hospitali zote nchini.

Hatua nyingine alisema ni kuboresha upatikanaji wa dawa za kutibu magonjwa ya akili katika hospitali zote za Serikali.

Aliongeza kuwa Serikali imeimarisha matibabu ya akili na saikolojia katika hospitali za mikoa na rufaa hii ikiwa ni pamoja na kupeleka wataalamu wa afya ya akili wakiwamo madaktari bingwa na wauguzi ili kuboresha huduma kwa wagonjwa wa nje na waliolazwa.

Alifafanua kuwa sababu za kijamii zinazoweza kusababisha mtu kupata magonjwa ya akili ni umasikini uliokithiri, kutengwa na kubaguliwa na jamii. Sababu zingine alizitaja kuwa ni kunyanyaswa kimwili na kingono, kuwa tegemezi, kupoteza mali, kazi, ulevi, kukosa huduma muhimu na unyanyapaa.

Aliiasa jamii kuachana na Imani potofu kuwa chanzo cha ukichaa ni ushirikina na hivyo kupoteza fedha na mali nyingi kwa waganga wa kienyeji wasio waaminifu.

Samsung wawataka wateja wao kutupa ‘Galaxy Note 7’, zina tatizo la kulipuka kwenye chaji

$
0
0
Kufuatia ripoti za matukio mengi ya watumiaji wa simu za Samsung kulipukiwa na simu hizo wakati wa kuchaji, kampuni hiyo ya Kikorea hatimaye imewataka watumiaje wake kutupa toleo la ‘Galaxy Note 7’ kutokana na tatizo hilo.

Kampuni ya Samsung imetoa tamko rasmi kupitia tovuti yake ikiwataka watumiaji wa simu hizo toleo la ‘Galaxy Note 7’ duniani kote kuchukua tahadhari na kuacha kabisa kuzitumia  wakati ikiendelea na uchunguzi zaidi.

“Tunafanya kazi na Mamlaka husika kufanya uchunguzi kuhusu kuwepo kwa ripoti za matukio yanayohusu Galaxy Note7. Kwa sabababu usalama wa mteja wetu ni kipaumbele, Samsung tunawataka wauzaji wote wa simu zetu duniani kuacha mara moja kuuza Galaxy Note 7,” imeeleza taarifa rasmi ya kampuni hiyo.

Majaribio ya betri ya simu ya Samsung, Galaxy Note 7 yaliyofanywa katika maabara moja nchini Singapore yalipelekea simu hiyo kulipuka moto.

Hivi karibuni, hata hapa Tanzania, kumekuwa na ripoti za matukio ya wananchi wengi kudai kuwa wameripukiwa na simu za Sumsung walipokuwa wanachaji. 

Pia, kulikuwa na taarifa ambazo hazikuthitishwa na Mamlaka kuhusu watu kulipukiwa na simu hizo walipozipokea wakati zikiwa kwenye chaji.

Mfumuko Wa Bei Wa Taifa Kwa Mwezi Septemba 2016 Umepungua Kwa Asilimia 4.5

$
0
0
Na Dotto Mwaibale
MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Septemba, 2016 umepungua hadi asilimia 4.5 kutoka asilimia 4.9 ilivyokuwa mwezi Agosti 2016.

Hayo yabebainishwa na Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraim Kwesigabo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar eas Salaam jana.

” Hii inamanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Septemba, 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi ya upandaji ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti 2016 ” alisema Kwesigabo.

Alisema  Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 103.05 mwezi Septemba 2016 kutoka 98.64 mwezi Septemba 2015.Kwesigabo aliongeza kuwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi mwezi Septemba 2016 umepungua hadi asilimia 6.0 kutoka asilimia 7.0 ilivyokuwa
mwezi Agosti 2016.

Alisema  kupungua kwa mfumuko wa bei wa mwezi Septemba 2016 kumechangiwa na kupungua kwa kasi ya bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Septemba 2016 zikilinganishwa na bei za mwezi Septemba 2015.

Alisema mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoonesha kupungua ni pamoja na bei za dagaa kwa asilimia 11.6 na viazi vitamu kwa asilimia 3.2.

“Kwa upande mwingine mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilionesha kupungua ni pamoja na bei za gesi kwa asilimia 10.4, dizeli kwa asilimia 2.9 na petrol kwa asilimia 2.8."

Akizungumzia mabadiliko ya bei kati ya mwezi Agosti na Septemba 2016 fahirisi za bei zimepungua hadi 103.o5 mwezi Septemba 2016 kutoka 103.28 mwezi Agosti 2016.

Alisema kupungua kwa fahirisi za bei kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula.

Alitaja baadhi ya bidhaa zilizochangia kupungua kwa fahirisi ni pamoja na mchele kwa asilimia 2.6, unga wa mahindi kwa asilimia 1.0, dagaa kwa asilimia 3.0 na mbogamboga kwa asilimia 4.3.

Alisema kwa upande mwingine baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei ni pamoja na dizeli kwa asilimia 2.9, petroli kwa asilimia 2.8 na mafuta ya taa kwa asilimia 2.9

Akizungumzia thamani ya shilingi ya Tanzania kwa mwezi Septemba 2016 kutoka mwezi Desemba 2015 alisema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia sh.97 na senti 04 mwezi Septemba 2016 kutoka mwezi Desemba 2015 ikilinganishwa na shilingi 96 na senti 83 ilivyokuwa mwezi Agosti 2016.

Kwesigabo akizungumzia mfumuko wa bei kwa bidhaa ya nchi za Afrika Mashariki nchini Kenya mfumuko wa bei wa mwezi Septemba 2016 umeongezeka kidogo hadi asilimia 6.34 kutoka asilimia 6.26 mwezi Agosti 2016.

Alisema nchini Uganda mfumuko wa bei wa mwezi Septemba 2016 umepungua hadi asilimia 4.2 kutoka asilimia 4.8 mwezi Agosti 2016.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images