Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Gari la kwanza kutengenezwa na kampuni ya Kitanzania kuzinduliwa Desemba 30, 2016

$
0
0
KAMPUNI ya Simba Motors imesema ina mpango wa kujenga kiwanda cha kuunganisha magari aina ya pick-up ambacho kitaanza kuzalisha magari kabla ya Desemba 30, mwaka huu.

Ahadi hiyo imetolewa jana mchana (Jumatatu, Oktoba 10, 2016) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Jitesh Ladwa mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam.

“Tumeamua kuunda magari aina ya pick-up kwa sababu ya mahitaji makubwa yaliyopo nchini. Takwimu zinaonyesha kuwa, kwa mwaka Tanzania inanunua magari ya aina hii zaidi ya 4,000. Katika nchi za SADC mahitaji ni pick-up 35,000 kwa mwaka. Tutaanza na mtaji wa dola za Marekani milioni 200 na tumeomba ekari 200 katika eneo la EPZ,” amesema.

“Eneo la kiwanda cha kuunganisha magari peke yake linahitaji ekari 50, kwa hiyo tukiweka na yadi za kupaki magari, eneo la viwanda vingine, eneo la kushusha na kupakia makontena yatakayokuwa yakisafirishwa kwenda nchi jirani, ni lazima tutahitaji eneo kubwa zaidi,” amesisitiza.

Amesema mradi huo wa majaribio, utaanza kwa kutengeneza magari 20 kila mwezi na kwamba kazi ya utengenezaji magari itaongezeka na kufikia 1,000 na baadaye 5,000 kwa mwaka. “Tunataraji gari la kwanza litazinduliwa kabla ya Krismasi, mwaka huu,” amesema.

Bw. Ladwa amesema uundaji wa magari hayo aina ya Foton-Tunland utafanyika kwa ubia baina ya kampuni yao, SUMA-JKT na kampuni Foton International ya China kwa kutumia teknolojia ya Kichina na kwamba magari hayo yanayotumia 4-Wheel Drive, yana uwezo wa kupita kwenye barabara za aina zote.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni hiyo, Bw. Aatish Ladwa, amesema mradi utakapoanza, mbali ya kutoa ajira kwa Watanzania, utawezesha pia kujengwa kwa viwanda vingine vitakavyotengeneza matairi ya magari, vioo, taa, bumpers, viti na filters.

“Tunataraji kujenga uwezo wa wahandisi wazawa, uhamishaji wa ujuzi kwa mafundi wa Kitanzania (technology transfer), kupunguza bei kwa mlaji wa mwisho, kupunguza gharama za uzalishaji, kutekeleza amza ya Serikali ya kuifanya Tanzania kuwa ni nchi ya viwanda, kuongeza ajira kwa wanajeshi, na kuwezesha upatikanaji wa vipuri vya magari kwa urahisi na kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.”

“Kiwanda kitaajiri wafanyakazi 1,500 kwa kuanzia ambao watakuwemo mafundi na watoa huduma mbalimbali, lakini katika kipindi cha miaka mitatu hadi mitano, tunataraji kuongeza wafanyakazi wengine 5,000 wakati uzalishaji ukiwa umepamba moto,” amesema.

Kwa upande wake, akizungumza mara baada ya kulikagua gari la mfano aina ya Foton-Tunland, Waziri Mkuu amesema anawakaribisha kwenye uwekezaji huo hasa ikizingatiwa kuwa magari hayo yana uwezo wa kupita kwenye maeneo ya vijijini ambako barabara zake siyo nzuri.

“Ofisi za Serikali zinayahitaji zaidi haya magari, hospitali zetu za wilayani nazo pia zinayahitaji haya magari ili yaweze kutoa huduma za chanjo kwa watoto, huduma za UKIMWI, kampeni za kupambana na malaria, na huduma kwa mama wajawazito huko vijijini,” amesema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Taarifa Kwa Waombaji Wa Mikopo Ya Elimu ya Juu (HESLB ) Kuhusu Kumalizika Kwa Zoezi La Kurekebisha Taarifa Za Waombaji

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imekamilisha zoezi la kurekebisha fomu za maombi ya mikopo kwa waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017. Zoezi hilo lilianza tarehe 3 na kumalizika tarehe 7 Oktoba 2016.
 
Kwa sasa Bodi inaendelea na hatua za awali za upangaji wa mikopo ambapo taarifa za wanafunzi watakaopangiwa mikopo zitatolewa kwenye tovuti ya Bodi www.heslb.go.tzsiku chache zijazo.
 
NB: Bodi inawakumbusha waombaji mikopo wote kuwa makini na watu wasio waaminifu wanaoweza kutumia fursa hii kujipatia fedha isivyo halali.
 
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

Bakhresa Kujenga Viwanda Zaidi Vya Matunda, Vyakula.

$
0
0

KAMPUNI ya Bakhresa Foods imedhamiria kuongeza viwanda vingine vya usindikaji matunda hapa nchini ili kuongeza thamani kwa mazao ya wakulima.

Ahadi hiyo imetolewa leo (Jumanne, Oktoba 11, 2016) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Said S. Bakhersa wakati alipokutana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kufanya naye mazungumzo ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam.

Bw. Bakhresa amesema wana mpango wa kujenga kiwanda kimoja kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa na kwamba wamefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa watu wanapata usumbufu wa kusafirisha matunda hadi Dar es Salaam ndipo wayauze.

“Kuanzia tarehe 15 Oktoba, tutaanza kupokea matunda kutoka Kahama na maeneo ya jirani, na kwa siku tunapata semi trela zaidi ya 30. Yakimalizika ya kule tunaanza kupokea mengine kutoka mikoa ya Pwani na Kusini.”

“Tukijenga kiwanda Kanda ya Ziwa, tutapunguza adha ya wadau kusafirisha matunda kutoka kule hadi hapa kiwandani na badala yake sisi tutakuwa tunasafirisha concentrated juice na kuileta hapa kwa hatua zaidi za usindikaji,” amesema.

Amesema wana mpango wa kuendeleza usindikaji wa vyakula vya nafaka kwenye mikoa ya Kusini na kwamba hadi sasa wameajiri wafanyakazi zaidi ya 8,000 wakiwemo Watanzania 180 ambao wameajiriwa kwenye matawi yake nje ya nchi. “Hawa tunawalipa kamaexpatriates,” amesisitiza.

Amesema hivi sasa Kampuni hiyo imekwishafungua matawi mengine kwenye nchi za Rwanda, Burundi, Msumbiji, Malawi, Zimbabwe na Afrika Kusini.

Kampuni ya Bakhresa Foods inatengeneza vyakula mbalimbali zikiwemo juisi, soda, maji, biskuti, ice-cream, vyakula vya nafaka kama ngano, mahindi, mchele na bidhaa za kuokwa.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu amemhakikishia Bw. Bakhresa nia ya Serikali ya Awamu ya Tano kushirikiana na wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda kwani imedhamiria kukuza uchumi wa Tanzania kupitia uzalishaji wa viwandani.

“Serikali inathamini mchango wa wenye viwanda katika nchi yetu. Tunawashukuru ninyi ambao ni wakongwe kwenye sekta hii, na kwa hiyo tunawaomba msikate tamaa, muendelee kufungua viwanda zaidi ili wananchi wetu wapate mahali pa kuuzia mazao au bidhaa zao,” amesema.

Amemuomba Bw. Bakhresa aangalie maeneo mengine zaidi ya kuwekeza kama vile sekta za hoteli na utalii ili kusaidiana na Serikali kukuza uchumi wa Tanzania.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, OKTOBA 11, 2016.

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 23 & 24

$
0
0

MWANDISHI : EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
“Tutaonana kuzimu”
Kabla hata Rahab ajafyatua risasi ya aina yoyote ndege ikayumba gafla na kuwaangusha raisi na Rahab, kutokana na Samson kuifunga mitambo yote ya ndege, ikiwemo mashine baadhi za uendeshaji wa ndege, zimesababisha marubani kushindwa kuikwepa ndege ya abiria ya shirika la Fly Emirates, ambayo zimekutana kwenye njia moja, marubani wa ndege ya abiria hawakuweza kuiona mapemba ndege ya Raisi wa Tanzania, kutokana na kushindwa kuiona kwenye rada zao, na wakajikuta wakiingonga, ndege ya raisi wa Tanzania kwenye ubavu wa nyuma wa ndege na kuisababisha kugeuka mara mbili na kuanza kwenda chini kwa kasi sana, huku ndege yao ya abiria ikiianza kuwaka moto

ENDELEA
Kelele za abiria zilizo andamwa na  vilio vya uchungu, ziliendelea kusikika kwenye ndege ya raisi wa Tanzania bwana Ptraygod Makuya, kwajinsi ndege inavyozidi kwenda chini ndivyo jinsi ilivyozidi kuwaka mato mwingi na kuendelea kupasuka baadhi ya sehemu na kuzidi kulete maumivu makali kwa kila abiria aliye kubwa na kitu chochote kikali, ambacho kinaugusa mwili wake na kuzidi kumuumiza, huku wengine wakijikuta wakipoteza viungo vyao vya mwili.Hali hii inaendelea sawaswa na hali iliyopo ndani ya ndege ya abiria iliyo gonga sehemu ya nyuma ya ndege ya Raisi.Ndani ya chumba walichopo Samson, Rahab na rais Praygod, hali inazidi kuwa mbaya, kwani computer zote zinaanza kulipuka moja baada ya nyingine, kwa haraka Rahab anajitahidi kushikilia moja ya nguzo ya chuma, huku mkono wake mmoja akimshikilia Raisi ambaya anavutwa na upepo mwingi, unaoingia kwenye chumba chao, ukitokea nje kutokana na ukuta wa chumba chao kutoboka kutokana na motom mkali  unaoendelea kuiteketeza ndege

“Muheshimiwa Raisi endelea kujikaza”

Rahab alizungumza kwa sauti ya juu huku mkono wake wa kulia, akiendelea kumshikilia Raisi, huku mkono wake wa kushoto pamoja na mguu wake wa kulia kwa pamoja vikiwa vimezunguka kwenye nguzo ya chuma inayo endelea kumsaidia asitoke nje ya chumba hicho.Hali kwa upande wa Samson inazidi kuwa ngumu sana kutokana na upepo mwingi kuendelea kuingia ndani ya ndege, kutokana na kipigo kikali alicho kipata kutoka kwa Rahab, ambacho kimempelekea mikono yake kukosa nguvu ya kushikilia kwenye baadhi ya vitu vilivyomo ndani ya ndege.Samson anajikuta akiachia kwenye moja ya sehemu aliyo ishikilia na upepo mkali unamtoa nje, huku akipiga kelele za kuomba msaada, Ndege nayo ikazidi kwenda chini kwa kasi kubwa huku, ikizidi kuchanguka baadhi ya maeneo yake
                                                                                                 ***
Baada ya Fetty kukata simu anawageukia manahodha wawili wanao kiendesha chombo cha kivita kijulikanacho kwa jina la ‘Sabmarine’ au Nyambizi, huku mkononi mwake akiwa ameishika bunduki yake aliyopiga risasi kadhaa pembeni

“Mutafanya kile ambacho mimi nitawaelekeza, Sawa?”

Fetty alizungumza huku bunduki yake akiwa ameielekeza kwa wanahodha hawa, ambao nao ni wanajeshi wa wajeshi la maji nchini Tanzania,

“Sa…wa”
Mmoja alijibu huku mwili wake ukimtetemeka sana, hadi haja ndogo akaanza kuihisi ikimwagika

“Kwanza hapa tulipo ni wapi?”
Anna aliuliza kwa sauti ya ukali
“Hapa tupo bahari ya Pasifiki maharibi kwa bara la Asia, katika nchi ya Australia”

Nahodha mmoja alizungumza huku akitazama kifaa maalumu ambacho kina namba nyingi, ambazo kwa mtu wa kawaida si rahisi kuweza kugundua ni nini kinacho tazwamwa

“Mmmmmmm…..!!”
Halima aliguna huku akiwatazama wezake kwani hakuelewa kitu kinacho zungumzwa hapo ni kitu cha aina gani
“Tutarudi vipi Tanzania?” Agnes aliiuliza
“Tanzania tumeiacha mbali sana?”
“Ndio tutarudi vipi Tanzania” Fetty aliuliza kwa sauti ya ukali, na kuwafanya manahodha kuzidi kutetemeka
“Tutar….”

Kabla nahodha mmoja ajamalizia sentesi yake, akastushwa na kingora kilichopo pembezoni mwa chumba chao kikianza kulia huku kifaa kingine mbele yao chenye kioo kikukubwa mithili ya simu aina za I pad, kikianza kuonyesha vitu vilili virefu vyenye rangi nyekundu vikija kwa kasi sana

“Mungu wangu, ni mabomu haya”

Nahodha mmoja ambaye umri wake umekwenda kidogo alihamaki huku kajasho kakianza kumwagika usoni mwake akitazama kioo hicho kwa macho yake makubwa kiasi

“Mabonu……!!?”
Anna aliuliza huku naye macho yakiwa yanamemtoka
“Ndio, tumeshakamtwa kwenye rada ya  nchi ya Australia”

Kila mmoja akaanza kuomba sala yake ya mwisho, kutokana na mabomu hayo kuzidi kuja kwa mwendo wa kasi huku yakionekana kukilenga chombo chao ambacho kinapita kwa siri chini ya bahari hii kubwa ya Pasific, katika eneo la jeshi la nchini Australia

==>Endelea  Nayo  <<Kwa  Kubofya  Hapa>>

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Octoba 12

Wafuasi 22 CUF Kortini Kwa Madai ya Kukutwa na silaha za Jeshi la Polisi

$
0
0

Wafuasi  22 wa Kundi la ‘Blue Guard’ la Chama cha Wananchi (CUF) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka manne likiwemo la kukutwa na silaha za Jeshi la Polisi.

Washitakiwa hao ambao ni wakazi wa Zanzibar walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serikali, Patrick Mwita mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa.

Mwita alidai, washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka manne ya kula njama, kuingilia majukumu ya kipolisi kupitia genge la uhalifu pamoja na kukutwa na silaha pamoja na zana za Jeshi la Polisi.

Akisoma mashitaka, Wakili Mwita alidai, kati ya Septemba 20 na 25, mwaka huu kati ya Zanzibar na Dar es Salaam, kupitia kikundi cha Blue Guard, washitakiwa na wenzao ambao hawakufikishwa mahakamani walikula njama za kuajiri watu, wafanye kazi za kipolisi kinyume cha Sheria ya Makosa ya Jinai.

Aliendelea kudai kuwa, washitakiwa wakiwa wanachama wa kundi la Blue Guard waliwaajiri watu kwa ajili ya kufanya kazi za Kipolisi kinyume na sheria.

Wakili Mwita alidai, Septemba 25, mwaka huu katika eneo la Mwananyamala, Dar es Salaam, wakiwa na lengo la kutenda kosa, washitakiwa walikutwa wakiwa na silaha kinyume cha sheria , ikiwemo visu vitano pamoja na mabomu ya machozi 10 kwa ajili ya kuyatumia katika uvamizi.

Aidha, inadaiwa siku hiyo hiyo, Dar es Salaam, washtakiwa walikutwa wakiwa na zana za Jeshi la Polisi ambazo ni mabomu ya machozi yanayotumiwa na jeshi hilo katika majukumu yao.

Baada ya kusomewa mashitaka washitakiwa hao walikana kutenda makosa hayo, hata hivyo Wakili Mwita alidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba wapangiwe tarehe nyingine ya kutajwa.

Upande wa utetezi kupitia Wakili Hekima Mwesigwa uliiomba Mahakama kuliondoa shitaka la tatu katika makosa hayo kwa sababu lina upungufu wa kisheria kwa kutumia baadhi ya maneno kupotosha.

Hata hivyo, Wakili Mwita aliiomba Mahakama kutupilia mbali maombi hayo kwa kuwa shitaka hilo halina upungufu wowote badala yake wametumia lugha ya mkato.

Hakimu Mwambapa alisema baada ya kupitia vifungu vya sheria, amebaini kuwa shitaka halina mapungufu kisheria hivyo ametupilia mbali maombi.

Aidha, alisema washtakiwa hao watapata dhamana endapo watatimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika watakaosaini hati ya Sh milioni mbili kila mmoja, pia wawasilishe vitambulisho vyao mahakamani. Kesi itatajwa tena Oktoba 20 mwaka huu.

Washtakiwa ni Hamis Omary Said (49), Said Mohamed Zaharan (57), Hamid Nassor Hemed (44), Nassor humud Ally (25), Othman Humud Abdlaah (34), Swalehe Ally Swalehe (30), Hamis Hamis Haji (46), Majid Hamis Juma (58), Mohamed Hamis Ally (34), Ramadhan Rashid Juma (30), Juma Hamad Seif (21) na Masoud Iliyasa Fumu (29).

Wengine ni Jecha Faki Juma (40), Mbaruku Hamis Bakari (31, Mohamed Alli Zuberi (43), Muhsin Ally Juma (27), Mohamed Amir Mohamed (30), Ally Juma Salum (35), Juma Hajji Mmanga (26), Ally Nassoro Ally (46), Haji Rashid Juma (32) na Juma Omary Hamis (28).

Kufikishwa mahakamani kwa washtakiwa hao kunatokana na mgogoro unaoendelea ndani ya chama hicho. Septemba 28, mwaka huu, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alitoa taarifa za kukamatwa kwa wafuasi hao kwa tuhuma za kupanga njama za kufanya fujo na kuchoma ofisi za CUF zilizopo Buguruni Ilala jijini Dar es Salaam.

Burundi imeamua kusitisha ushirikiano wake na UN kuhusu Haki za Binadamu

$
0
0
Serikali ya Burundi imechukua uamuzi wa kusitisha ushirikiano wake na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, inayotuhumiwa kula njama katika kuandaa ripoti ya Uchunguzi Huru wa Umoja wa Mataifa (EINUB).

"Kufuatia njama ya Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu nchini Burundi, katika maandalizi ya ripoti ya uongo na yenye utata ya Wataalam wanaodaiwa kufanya Uchunguzi Huru wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi (EINUB), Serikali ya Burundi imeamua kusitisha ushirikiano wowote na kushirikiana katika miundo yake yote, pamoja na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binanadamu hadi itakapotangazwa tena." Maneno haya yameonekana kwenye tangazo lililosainiwa Jumanne hii Oktoba 11, 2016 na Philippe Nzobonariba, katibu Dola na Msemaji wa serikali.

Kwa mujibu wa tangazo hili, uamuzi huo ulifahamishwa maofisa wa Ofisi hii wakati wa kikao cha kazi pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Burundi Alain Aimé Nyamitwe, Jumatatu hii, Oktoba 10, 2016.

"Kwa maana hii, Burundi inaomba kwa kusubiri, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu kuteua timu itakayoendesha mazungumzo kuhusu makubaliano ya makao makuu, ambayo yataweka wazi majukumu yake, muda na idadi ya wafanyakazi wake nchini Burundi," imeongeza taarifa hiyo.

Uamuzi huu unakuja baada ya maandamano mjini Bujumbura mwishoni mwa wiki iliyopita mbele ya makao makuu ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu ambapo waandamanaji waliomba ofisi hiyo kufungwa haraka iwezekanavyo.

Ripoti ya EINUB ilikuwa chanzo cha azimio HRC33 lililochukuliwa na Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu ambalo linaomba kuundwa kwa Tume ya Kimataifa ya Uchunguzi wa ukiukaji wa haki zabinadammu nchini Burundi.Azimio ambalo lilikataliwa na serikali ya Burundi, ambayo inautuhumu Umoja wa Ulaya kuwa imeandaa na kupanga njama dhidi yake.

UVCCM Wamtembelea Majeruhi Aliyetobolewa Macho na Scormpion.....Wataka Jeshi la Polisi Liyabane Majambazi

$
0
0
UMOJA wa Vjana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umelihimiza Jeshi la polisi nchini kutambua kuwa ujambazi, wizi wa kutumia silaha na uporaji bado ni tatizo linalohitaji kushughulikiwa kwa nguvu zote kama ambavyo nchi ilisimama na kutekeleza operesheni mbalimbali za ukombozi.

Pia, umesisitiza kuwa usalama wa raia na mali zao unahitaji kulindwa ili kuepusha vifo, hasara, unyang’anyi wa mali na vilema vya maisha kutokana na matukio yanayoweza kuwakumba wasio na hatia mijini na vijijini.

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alieleza hayo jana alipomtembelea kumjulia hali majeruhi Said Ally, Mabibo Hostel.

Saidi alijeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwili wake ikiwa ni pamoja na kutobolewa macho katika tukio wizi wa kutumia silaha Buguruni mjini Dar es Salaam, Septemba mwaka huu.

Shaka alisema tatizo la uhalifu, unyang’anyi, uporaji na ukwapuaji mali kwa kutumia nguvu na silaha, linahiaji kutazamwa kwa kina na upana unaostahili na vyombo vyenye dhamana vinavyosimamia usalama wa raia na mali zao.

Alisema kuna haja ya polisi kubuni mbinu mpya za kukabiliana na makundi ya wezi, waporaji na majambazi kabla hawajaleta madhara na hasara kama ilivyomtokea Said ambaye sasa  amesababishiwa ulemavu wa kudumu wa kutoona.

“Kila siku mbinu za uhalifu, ujambazi, wizi wa kutumia nguvu na silaha hubadilika, jukumu la kupambana na matukio hayo hatari ni la polisi kwa kushirikiana na raia wema, janga hili likiachwa wananchi wataishi kwa mashaka na hawatajituma kujiletea maendeleo,”alisema Shaka.

Alisema ikiwa wananchi wanajituma kwa bidii kutafuta fedha na kubuni miradi ya kiuchumi halafu majambazi na wanyang’anyi wanapora na kumfilisi aliyetafuta ndani ya saa chache, hilo linaweza kuwatia hofu mwananchi na wajasiriamali na kuwafanya washindwe kujituma kikamilifu jambo ambalo litakuwa na madhara makubwa katika kuzalisha mali na kukuza uchumi.

Akizungumza kwa masikitiko na huzuni kubwa , Shaka alisema tamaa ya kupata utajiri kwa njia haramu kwa mtu mmoja mmoja au kikundi, kumemsibaishia hasara ya maisha dhidi ya Said ambaye kwa sasa amekoseshwa uwezo wa kuendelea kupiginia maendeleo yake ya kiuchumi na taifa kwa ujumla.

“Ifike mahali tatizo la uhalifu, ujambazi na uporaji lishughulikwe kama harakati za mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi, ukoma na kifua kikuu, tukilipuuza tatizo hili litaigharimu jamii na kuwaletea kadhia ya umasikini wananchi na Tanzania kwa ujumla,”alieleza.

Kwa upande wake majeruhi Said aliishukuru UVCCM kwa kuonyesha kumjali na kufika kumjulia hali kutokana na janga lililomkuta na kumpa msaada huku akiwahimiza waendelee kuikumbusha serikali isimuache kwa sababu amedhulumiwa utu wake na watu aliowatuhumu kuwa ni majambazi bila ya hatia wala kosa lolote.

Said alisifu ujio huo wa ujumbe kutoka Makao Makuu ya UVCCM Taifa ulioongozwa na Shaka, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam Omar Matulanga na makatibu wa umoja huo kutoka wilaya tano za mkoa huo.

Alisema akiwa kijana amefarijika kutembelewa na vijana wenzake huku akiwahimiza wasimchoke kwa sababu sasa amekuwa kipofu na hajimudu tena kimaisha.

“Endeleeni kuikumbusha serikali yetu na wasamaria wema wasinisahau, nina nguvu, akili na maarifa ya kujituma ili nizalishe ila nimedhulumiwa macho yangu na sina hakika kama nitaona kama mwanzoni “alisema

Mashahidi Kesi ya Ester Bulaya wapunguzwa

$
0
0

Mashahidi wa pande zote mbili katika kesi ya kupinga ushindi wa Ester Bulaya katika uchaguzi wa mbunge wa Jimbo la Bunda wamepunguzwa na kuweka mazingira ya shauri hilo kutolewa uamuzi mapema.

Katika kesi hiyo iliyo Mahakama Kuu, Bulaya ataanza kujitetea kwa kuita shahidi mmoja baada ya shahidi wa tatu wa upande wa wawasilisha maombi, Steven Wasira kumaliza kutoa ushahidi juzi.

Upande wa Bulaya, ambaye aligombea kwa tiketi ya Chadema na kumbwaga mwanasiasa mzoefu, Steven Wasira, umedai kuwa umeamua kubakia na shahidi mmoja kutokana na waliowasilisha maombi kuwa na ushahidi dhaifu.

Wakati wajibu maombi wakisema hayo, upande wa wanaopinga ushindi wa Bulaya wametangaza kufunga ushahidi baada ya kuita mahakamani mashahidi watatu pekee tofauti na maelezo ya awali kuwa wangeita watu 15.

Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu anayemwakilisha Bulaya ambaye ni mdaiwa wa kwanza katika shauri hilo namba moja la mwaka 2015, aliieleza mahakama kuwa anakusudia kuita mahakamani shahidi mmoja.

“Ingawa ushahidi uliowasilishwa mahakamani na upande wa waleta maombi ni dhaifu na hauna nguvu kisheria kiasi cha awali tufikiria kutoita shahidi, tumeona ni vyema kuita shahidi mmoja kujenga hoja zetu za kuishawishi mahakama kutupilia mbali shauri hili,” alisema Lissu.

Maelezo hayo ya Lissu ni tofauti na yale aliyoyatoa juzi wakati shauri hilo lilipoahirishwa kwamba asingeita shahidi yeyote kutokana na ushahidi wa wadai kuwa dhaifu na kukosa mashiko mbele ya macho ya sheria.

Waliowasilisha maombi ya kutaka matokeo hayo ya ubunge yatenguliwe ni Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malagila ambao ni wapigakura wa Bunda.

Wakili anayewakilisha waliowasilisha maombi hayo, Constantine Mutalemwa amesema wameamua kufunga ushahidi baada ya kuridhika na ushahidi ambao umeshatolewa na mashahidi watatu. 

Awali, wakili huyo aliieleza mahakama kuwa upande huo ungeita mashahidi 15 kabla ya kurekebisha orodha hiyo na kubakiza 12.

Wakili Angela Kushagala anayemwakilisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali na msimamizi wa uchaguzi ambao ni wajibu maombi namba mbili na tatu, aliieleza mahakama kuwa wanakusudia kuita mashahidi wawili.

Wakati huohuo, Lissu ameiomba mahakama kuondoa ombi lao la awali la kutoendelea na usikilizwaji wa shauri hilo tofauti na awali walipotaka ilitupilie mbali kwa madai kuwa hakuna kesi ya kujibu. 

Lissu alisema upande wa utetezi umepitia upya maombi yao na kugundua kuwa upo uwezekano wa shauri hilo kuchukua muda mrefu iwapo wataendelea kushikilia msimamo wao wa kutaka litupwe.

CUF Tanga Wamgomea Profesa Lipumba

$
0
0

CHAMA cha Wananchi (CUF) wilayani hapa kimetoa tamko la kutomtambua Mwenyekiti wa Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, na kwamba hakitampokea katika ziara yake.

Lipumba anatarajia kuanza ziara mkoani Tanga kesho  huku uongozi wa chama hicho ukisisitiza kutambua uamuzi wa  Mkutano Mkuu uliomwondoa madarakani na wa Baraza Kuu kumvua uanachama.

Mwenyekiti wa CUF wa Wilaya ya Tanga, Rashid Jumbe alitoa tamko hilo jana akieleza kuwa hawatakuwa tayari kukaidi Katiba ya Chama chao na kwamba hawatampokea na hakuna maandalizi yatakayofanyika kumpokea.

"Tumeambiwa Lipumba ana dhamira ya kufanya ziara mkoani hapa. Sisi kwa uamuzi wa Baraza hatumtambui, wala hatujaandaa maandalizi ya kumpokea.

“Wilaya za Korogwe na Muheza ndizo zimesema atazitembelea, lakini sisi hatuko pamoja nao na watakaompokea wataingia kwenye mgogoro mwingine kwa sababu hatambuliki," alisema Jumbe.

Mwenyekiti huyo pia alizungumzia mgogoro baina yao na CCM kutokana na sakata la umeya ambapo alisema  hatima ya mgogoro huo itajulikana baada ya mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29.

Alisema kutokana na sakata hilo walitoa malalamiko kwa viongozi mbalimbali lakini hakuna hatua zozote zinazoendelea, hivyo Kamati ya Utendaji iliwataka madiwani wa chama hicho kutohudhuria kikao chochote cha Halmashauri hadi itakapotoa uamuzi.

"Tumetoa malalamiko yetu kwa viongozi wa CCMna lengo letu ilikuwa tuonane na  Rais lakini tulimpata Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa aliyetwambia kuwa atalifanyia kazi, lakini sasa tumeamua kupeleka malalamiko yetu kwa wenye chama na wao ndio watakaotoa uamuzi juu ya mgogoro huo.

“Hivyo tumeitisha mkutano ambao utakuwa na wajumbe 440 ambapo tuna imani kuwa tatizo letu litakwisha Oktoba 29,” alisema Jumbe.

Africa Yampa Heshima Nyingine Kubwa Mwalimu Nyerere

$
0
0
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amezindua jengo jipya makao makuu ya Umoja wa Afrika ambalo limepewa jina la rais mwanzilishi wa taifa la Tanzania, Julius Nyerere.

Jengo hilo ambalo jina lake kamili ni Jumba la Amani na Usalama la Julius Nyerere limejengwa kwa ufadhili kutoka Ujerumani.

Litakuwa makao ya idara ya Amani na Usalama ya AU na litatumiwa pia na maafisa wa kutoa tahadhari ya mapema kuhusu mizozo barani pamoja na kuratibu juhudi za kulinda amani za AU.

Ujenzi wa jumba hilo, ambalo ukubwa wake wa sakafu ni mita 13,500 mraba na linaweza kutumiwa na wafanyakazi 360, uligharimu euro 27 milioni.

Jengo hilo lina ofisi za kufanyia kazi, vyumba vya mikutano vya kutumiwa na Baraza la Amani na Usalama, chumba cha kuratibia shughuli, maktaba na vyumba vya shughuli za pembeni.

Mwalimu Nyerere, ambaye alikuwa rais wa Tanzania hadi 1985, alikuwa mmoja wa viongozi waanzilishi wa Muungano wa Nchi za Afrika (OAU) ambao sasa ni Umoja wa Afrika (AU).

Bi Merkel amezuru nchi kadha za Afrika zikiwemo Mali na Niger. Hapa anaonekana na Rais Mahamadou Issoufou wa Niger.

Alishiriki sana katika jitihada za kuendeleza bara la Afrika na kusaidia mataifa ambayo hayakuwa yamepata uhuru kujipatia uhuru wake.

Mwalimu Nyerere alipigania sana kumalizwa kwa ubabe wa Wazungu katika nchi za Rhodesia (sasa Zimbabwe), Afrika Kusini, na taifa la Kusini Magharibi mwa Afrika/Namibia (sasa Namibia).

Serikali Yakiri uhaba wa Dawa hospitalini

$
0
0
Makamu  wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amekiri kuwapo  uhaba wa dawa   na vifaa tiba katika hospitali za Serikali nchini.

Amesema uhaba huo wa dawa ni changamoto ya muda mfupi na Serikali inatafuta ufumbuzi wa haraka  kuwahudumia wananchi.

Alikuwa akizungumza  Dar es Salaam jana wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa wodi ya kina mama na watoto katika hospitali zote za rufaa  za Mkoa wa Dar es Salaam.

Samia alisema anatambua changamoto zinazoikabili Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kwamba ni ukosefu wa dawa.

“Natambua katika hospitali zetu za rufaa tuna changamoto ya vifaa tiba na dawa, lakini Serikali tunaifanyia kazi  kila mwananchi aweze kupata huduma hizo kama ilivyopangwa,”alisema.

Alisema   idadi watu wanaoongezeka katika Mkoa wa Dar es Salaam husababisha msongamano wa wajawazito na watoto katika hospitali za Serikali na kuwafanya kina mama walale chini au walale mbali na watoto wao.

“Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni, takriban wanawake 432 kati ya vizazi hai 100,000, hufa kila mwaka kutokana na uzazi na asilimia 80 ya vifo hivyo husababishwa na ukosefu wa vifaa tiba, umbali wa vituo vya afya, upasuaji wa huduma za dharura ya upasuaji kwa wajawazito na kuongezewa damu.

“Kwa Mkoa wa Dar es Salaam peke yake, kuna zaidi ya hospitali 42 zinazotoa huduma za dharura za uzazi kwa kasi ya ukuaji wa jiji na bado Serikali inahitaji zaidi ya hospitali 30 ndani ya miaka 10 ijayo,” alisema.

Kwa mujibu wa Samia, mradi wa ujenzi huo utagharimu Sh bilioni 4.5 kwa hospitali tatu na kila hospitali yenye ghorofa tatu  na uwezo wa kuwekwa vitanda 150, itagharimu Sh bilioni 1.2.

Alisema Serikali imejipanga kuhakikisha hospitali zote za rufaa zinaendelea kuimarishwa ili kutoa huduma bora za afya ikiwamo afya ya mama na mtoto.

Maalim Seif Aziandikia Barua Benki Zote Nchini Kupinga Profesa Lipumba Kuruhusiwa Kufungua Akaunti ya Ruzuku Kwa Jina la CUF

$
0
0
Katibu  Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amemdhibiti mwenyekiti anayetambulika na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba kwa kuandika barua kwa benki zote ili kudhibiti ruzuku ya chama isipite kwenye mikono ya kiongozi huyo.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kumtambulisha Prof. Lipumba Benki ya NMB Tawi la Ilala akitaka apewe ushirikiano wa kufungua akaunti mpya ya chama.

Taarifa kutoka ndani ya CUF zinasema kuwa juzi Maalim Seif, aliandika barua kwa benki zote kuzuia hatua hiyo kwa kuweka zuio la mtu yeyote kufungua akaunti ya chama.

“Unajua hii vita si ya kitoto ni mapambano yaliyopo ndani ya CUF lakini yana nguvu kubwa kutoka katika kila pembe ya watu wanaochukia upinzani. Na pia wapo hata viongozi wakubwa wa dola ambao kila siku wamekuwa wakifanya kazi ya kuivuruga CUF.

“Walitegemea lakini tangu jana (juzi) Katibu Mkuu ameziandikia barua benki zote nchini kuzuia mpango wa Msajili kutaka kuchepusha ruzuku ya chama na kwenda katika mikono ya Lipumba na sasa nakala yake imepelekwa kwa Msajili wa Vyama,” alisema mtoa habari wetu.

Hatua ya Profesa Lipumba kufungua akaunti inatokana na barua aliyopewa na Msajili wa Vyama vya Siasa ya Oktoba 6, mwaka huu iliyosainiwa na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza kwenda kwa Meneja wa Benki NMB Tawi la Ilala.

Katika barua hiyo yenye kumbukumbu namba HA.322/362/14/104  inamtambulisha Profesa Lipumba kutakiwa kufungua akaunti mpya ya The Civic United Front (CUF).

Siri ya Profesa Lipumba kutaka kufungua akaunti mpya yenye jina la Chama cha Wananchi CUF inadaiwa kutolewa na watumishi wa benki wa tawi hilo.

Prof. Lipumba ni Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa, huku chama chake kikiwa tayari kimemfukuza uanachama.

Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa kupitia Sisty Nyahoza ilinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari ikikiri kumtambulisha Profesa Lipumba kwa Benki ya NMB ili aweze kufungua akaunti hiyo, hata hivyo ikikana kujua matumizi ya akaunti hiyo.

Rais Magufuli afuta safari za Viongozi wa Mikoa na Wilaya kwenda Bariadi Kuzima Mwenge wa Uhuru......Awataka warejeshe fedha za Posho walizolipwa

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza viongozi wote wa Serikali walioalikwa kuhudhuria sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa zitakazofanyika tarehe 14 Oktoba, 2016 katika Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu kutohudhuria sherehe hizo na wale ambao walishalipwa fedha ya posho na safari kwa ajili hiyo wazirejeshe.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 12 Oktoba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais Magufuli ametoa maagizo hayo ikiwa ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kubana matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza rasilimali nyingi katika shughuli za maendeleo ya nchi.

Viongozi waliotajwa kutakiwa kufuta safari zao za kwenda Bariadi ni pamoja na Wakuu wote wa Mikoa, Wakuu wote wa Wilaya, Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mameya na Wenyeviti wote wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya pamoja na watumishi ambao huambatana nao wakiwemo madereva na wasaidizi wao ambao kwa idadi hufikia takribani 1,500.

Kwa kuwa sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru huambatana na Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Muasisi wa Taifa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyefariki dunia miaka 17 iliyopita, agizo hilo limewataka Viongozi wote wa Mikoa na Wilaya kubaki katika maeneo yao ya kazi na kujiwekea utaratibu wa jinsi ya kuienzi siku hiyo.

Aidha, Rais Magufuli ameagiza Wilaya zote ambazo zimefanya vizuri katika shughuli za maendeleo wakati Mwenge ulipokuwa katika maeneo yao, zitambuliwe kwa kutangazwa rasmi katika siku ya kilele cha Mbio za Mwenge na kwamba zawadi zilizoandaliwa zitapelekwa kwa wahusika kwa utaratibu utakaoelekezwa na Mamlaka inayohusika kutoa zawadi hizo.

Hata hivyo Dkt. Magufuli ameelekeza kuwa kutokana na umuhimu wa Mwenge wa Uhuru kwa Taifa, Viongozi wote wa Serikali ya Mkoa wa Simiyu na Wilaya zake pamoja na wananchi wote wa mkoa huo wajitokeze kwa wingi na kushiriki katika sherehe za kuzima Mwenge wa Uhuru siku hiyo ya tarehe 14 Oktoba, 2016.

Mgeni Rasmi katika sherehe za kuzima Mwenge wa Uhuru atakuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam         
12 Oktoba, 2016

Mwalimu Ashinda Kesi ya Kumtukana Mwanafunzi wa Kidato cha 6 Huko Iringa

$
0
0
Mahakama ya Mwanzo Iringa  Mjini imemuachia huru mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kiwele baada ya kukosa ushahidi wa kumtia hatiani katika kesi ya  kumtukana mwanafunzi.

Mwalimu huyo, Elizabeth Maliga (32) ameshtakiwa kwa madai ya kumtukana mwanafunzi huyo wa kidato cha sita, Rehema Mwakatobe na mama yake.

Amedaiwa kufanya kosa hilo wakati akimsainia Rehema barua ya kumuita mama yake kwenda shuleni hapo kusikiliza kosa la kuchelewa shuleni.

Hukumu hiyo imetolewa wakati Taifa likiwa kwenye mjadala mkubwa baada ya picha za video zilizosambaa mitandaoni kuonyesha kundi la walimu wa Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Mbeya likimshambulia mwanafunzi Sestian Chikungu.

Tayari Serikali imeshatangaza kuwafukuza chuo walimu hao na Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi.

Akisoma hukumu ya kesi hiyo iliyochukua takriban dakika 45, Hakimu wa Mahakama hiyo,  Abdallah Kutvai alisema upande wa mashtaka umeshindwa kuishawishi mahakama kumtia hatiani mshtakiwa huyo.

“Jukumu la kuthibitisha kosa ni la upande wa mashtaka. Hiyo ni kwa mujibu wa kifungu cha tano cha Sheria ya Ushahidi ya Mahakama ya Mwanzo iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

“Mashahidi wa upande wa mashtaka wametofuatiana tarehe za kutendwa kosa hilo. Shahidi namba moja ambaye ni mlalamikaji anasema kosa limetendeka Septemba 13, mwaka huu kwenye kikao cha kujadili mwenendo wa utekelezaji wa adhabu zilizotolewa na walimu kwa wanafunzi shuleni hapo,”alisema Hakimu Kutvai.

Amefafanua kuwa shahidi namba mbili alishindwa kubainisha siku ya tukio na kutaja tarehe tatu tofauti, ambazo ni Septemba 13, 14 na 15, siku ambayo mwanafunzi huyo alipewa barua ya kurudishwa nyumbani kwao Dar es Salaam kumfuata mzazi.

Taarifa mpya ya Mkuu wa Mkoa kuhusu tukio la kupigwa kwa Mwanafunzi Mbeya Day

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala amesema kuwa wanafunzi wa ualimu na walimu waliohusika na tukio la kumpiga mwanafunzi katika Shule ya Sekondari ya Kutwa Mbeya tayari wanaendelea kuhojiwa na Jeshi la Polisi kufuatia tukio hilo.

Licha ya kuwa tukio lile halikuwa adhabu sahihi kwa mwanafunzi, Mkuu wa Mkoa amewataka wazazi kujijengea tabia ya kuwafuatilia watoto wao kwani ameleeza kuwa nidhamu ya wanafunzi wa shule hiyo ni mbovu sana hasa kwa wanafunzi wa kidato cha tatu na cha nne.

Mkuu wa mkoa ameeleza kuwa, kuna wakati darasa lenye wanafunzi 50, mwalimu anafundisha wanafunzi 10 pekee wengine wakiwa hawamo darasani na mara kadhaa wanapishana na mwalimu wakati wanaingia wao wanatoka.

Wanafunzi wengine wamediriki hata kukunjiana ngumi na walimu, hivyo baadhi ya walimu ili kuepusha shari wamewaacha wafanye waoonavyo vyema.

Mkuu wa mkoa amesema kuwa wataendelea kufanya uchunguzi kuwabaini wanafunzi wakarofi zaidi na adhabu stakihi zitachukua hatua mara moja ili kuweza kurejesha nidhamu katika shule mkoani humo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Octoba 13

Nauli za daladala kuanza kulipwa kielektroniki kuanzia mwakani ili kubaini mapato halisi katika sekta hiyo

$
0
0
Mamlaka  ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imetangaza kuanzishwa kwa mfumo mpya wa ukataji wa tiketi za mabasi na daladala kwa njia ya kielektroniki.

Hatua hiyo ina lengo la kurahisisha upatikanaji wa mapato halali ya serikali pamoja na kuwafanya madereva na makondakta, kuajiriwa rasmi na wamiliki wa vyombo hivyo vya usafiri.

Pia mamlaka hiyo imezindua kampeni ya usafi kwa wafanyakazi wa daladala, ambayo inawataka kubadilisha sare za madereva na makondata, ambazo walishonewa na matajiri wao.

Sasa wafanyakazi hao watashona sare zao wao wenyewe ili wawe na uhalali wa kuzimiliki na kuzifanyia usafiri wa mara kwa mara.

Mkurugenzi wa Barabara wa Sumatra, Johansen Kahatano alisema jana kuwa mfumo huo wa tiketi za daladala kwa njia ya elektroniki, utaanza kutumika Januari mwakani.

Lakini, aliongeza kuwa kuanzia Desemba mwaka huu, watafanya mpango huo kwa majaribio kwa mabasi yaendayo mikoani.

“Kwa sasa tumeanza mpango huo kwa majaribio kwa daladala za kampuni ya Christian, Desemba tutaenda kwa mabasi ya mikoani na Januari mwaka kesho, mfumo huo utaanza kwa mabasi na daladala zote,” alisema Kahatano.

Alitangaza mfumo huo jana wakati wa uzinduzi wa kampeni ya usafi kwa madereva, ambayo inahusisha usafi wa mwili, mavazi na mabasi uliofanyika katika stendi ya Makumbusho, Dar es Salaam. Katika kampeni hiyo, madereva na makondakta watajishonea wenyewe sare zao na sio wamiliki wa magari.

Kahatano alisema chini ya mfumo wa ukataji wa tiketi kwa njia ya kielektroniki, utamfanya mmiliki wa basi kujua mapato yake halisi kwa siku na hivyo atawalipa wafanyakazi wake mshahara na Serikali itapata kiwango sahihi cha kodi. Kwa sasa ukataji wa tiketi za mabasi na ule wa daladala, unafanywa kwa tiketi zilizochapishwa.

Alisema kutokana na mfumo huo mpya, dereva haruhusiwi kumlipa mmiliki hesabu ya kila siku kama wanavyofanya sasa.

Badala yake, mmiliki ndiye atatakiwa kumlipa dereva na kondakta wa gari lake mshahara kila mwisho wa mwezi. Alisema ili malipo hayo yaweze kufanyika ni lazima madereva waajiriwe rasmi na walipwe chini ya mfumo wa ajira.

“Kwa hiyo dereva na mmiliki wataingia mkataba wa ajira tofauti na sasa hivi hakuna mkataba wowote kati ya tajiri na wafanyakazi wake, badala yake wanakubaliana tu kwamba hesabu ya siku ni kiasi fulani cha fedha na dereva anahangaika kukitafuta,” alisema Kahatano.

Kuhusu sare za madereva, alisema kwamba ndani ya wiki mbili madereva wa wilaya ya Kinondoni, wote wanatakiwa wawe wamebadili sare zao na kushona ambazo wamekubaliana na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Awadhi Haji, alisema wao kama wasimamizi wa sheria, watahakikisha ndani ya wiki mbili madereva wote wa daladala wa wilaya ya Kinondoni, wanashona sare hizo mpya ambazo zimepitishwa na Sumatra.

Alisema kutokana na agizo hilo, hategemei kuwaona tena makondakta na madereva wachafu kwa kuwa watakuwa na sare zao binafsi ambazo watazitunza kuliko ilivyokuwa awali.

“Wale ambao watakaidi tutawakamata na kuwafikisha mahakamani.”

Waziri Awapa Ahaueni walimu Waliotoa kipigo kwa mwanafunzi Mbeya.

$
0
0

Baada  ya uamuzi wa kuwafukuza vyuo walimu wanne waliokuwa kwenye mafunzo ya vitendo katika Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Mbeya (Mbeya Day), serikali imesema vyuo husika vinaweza kushauri adhabu mbadala iwapo vitajiridhisha kuwepo kwa mazingira tofauti na yaliyozingatiwa kwenye uamuzi wa kuwafukuza vyuo.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisema hayo juzi alipozungumza na waandishi wa habari mkoani Mbeya alikokuwa katika ziara kwenye shule mbalimbali mkoani humo.

Profesa Ndalichako alisema uamuzi uliochukuliwa na ofisi yake ulizingatia sheria ndogo zilizotungwa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm) zinazoainisha makosa yanayoweza kumfukuzisha chuo mwanafunzi.

Hata hivyo, alisema uamuzi uliochukuliwa unaweza kutazamwa upya na vyuo husika iwapo uzito uliochukuliwa na wizara utaonekana kuwa katika mazingira na uhalisia wa tukio husika.

Walimu wanne waliokuwa kwa vitendo katika shule ya Mbeya Day walifukuzwa vyuo baada ya uamuzi wa serikali kutokana na kuhusika kumpiga mwanafunzi Sebastain Chinguku vibao, mateke na fimbo kwa ukatili Septemba 28 mwaka huu shuleni humo.

Walimu hao walibainika baada ya kipande cha video kusambazwa katika mitandao ya kijamii hivi karibuni. 

Waliohusika na vyuo walivyokuwa wakisoma ni Frank Msigwa (anayedaiwa kumpiga zaidi mwanafunzi makofi kichwani), John Deo na Sante Gwamaka wote wa DUCE-UDSM, na Evans Sanga wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Akijibu swali la idadi ipi ya viboko inastahili kutolewa kama adhabu kwa mwanafunzi anayekwenda kinyume na maelekezo ya shule yake, Profesa Ndalichako alisema binafsi asingependa mwanafunzi achapwe hata kiboko kimoja lakini hilo linawezekana pale wanafunzi watakapozingatia maadili.

“Adhabu yoyote kwa mwanafunzi inatolewa pale anapokuwa amekwenda kinyume na maadili ya shule yake. Kama wanafunzi wote watazingatia maadili sidhani kama kuna mwalimu atakayempiga mwanafunzi hata kiboko kimoja. Haya yote yanatokea kutokana na wanafunzi kukosa nidhamu,” alisisitiza Ndalichako.

Aliwasihi wanafunzi kuzingatia maadili ya shule yao, akisema ndiyo njia pekee ya kuwawezesha kuishi vyema na walimu wao na pia kufanya vyema kitaaluma na kuwasihi wazazi kuwafundisha watoto wao nidhamu ya kuwaheshimu watu wote, akisema malezi hayo yatawapunguzia walimu adha ya kuishi na wanafunzi watukutu ambao kimsingi wanazorotesha utendaji kazi wao.

Tanzia: Aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam Dk. Didas Masaburi afariki Dunia

$
0
0
Meya wa zamani wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi amefikwa na umauti jana majira ya saa tatu na nusu usiku katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na ndugu yake, Dk. Makongoro Mahanga ambaye alieleza kuwa familia ipo katika taratibu za awali za msiba huo na kwamba leo watatoa taarifa rasmi na taratibu nyingine.

“Taarifa za kifo cha Dk. Masaburi ni za kweli ingawa sijaenda hospitali, ninafanya mawasiliano na familia lakini taarifa kamili kuhusu msiba zitakuwa zikitolewa na msemaji wa familia ambaye tutamteua usiku huu, na kesho (leo) tutaeleza kiundani,” Alisema Dk. Mahanga jana usiku.

Marehemu pia aliwahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

Mtandao huu unatoa pole kwa Taifa kwa ujumla kwa msiba huu wa aliyekuwa kiongozi wa ngazi mbalimbali akiutumikia umma. Apumzike kwa Amani. Amina!
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images