Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Sakata la Oparesheni UKUTA Lailazimu Tume ya Haki na Utawala Bora Kuandaa kikao cha pamoja kati ya Chadema, CCM na Jeshi la Polisi

$
0
0

Tume ya Haki na Utawala Bora imeandaa kikao cha pamoja kati ya Chadema, CCM, Jeshi la Polisi na taasisi nyingine tatu, wakati joto la Operesheni Ukuta likizidi kupanda kwa viongozi wa Serikali na vyama vya siasa kutoa kauli zinazotofautiana. 

Chadema imetangaza kufanya mikutano nchi nzima kuanzia Septemba Mosi katika operesheni iliyobatizwa jina la Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), ikidai Serikali ya Awamu ya Tano inakandamiza haki na demokrasia nchini. 

Kabla ya kikao hicho, viongozi wa upinzani wamekuwa wakisisitiza umuhimu wa kuwapo maridhiano katika suala hilo pamoja na Ukawa kususia vikao vya Bunge vinavyoongozwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, lakini kumekuwa hakuna harakati zozote zaidi ya majibizano. 

Hali hiyo ilizidi baada ya Chadema kutangaza operesheni hiyo ambayo imesababisha viongozi wa Serikali, hasa wakuu wa mikoa kuanza kutoa matamko ya kupiga marufuku mikutano yote ya Ukuta kwenye maeneo yao huku chama hicho kikisisitiza kuwa kitaendesha operesheni yake bila ya kujali amri ya kuizuia kwa kuwa kina haki kikatiba. 

Katika kile kinachoonekana ni jitihada za kutuliza hali hiyo,  Tume ya Haki na Utawala Bora imeandaa mkutano utakaohusisha taasisi sita, likiwamo Jeshi la Polisi lililozuia mikutano, CCM inayoendesha Serikali na Chadema inayopinga maamuzi ya Serikali kwa madai kuwa yanakandamiza demokrasia na kukiuka misingi ya utawala bora. 

Habari tulizozipata  zinaeleza kuwa wanaotakiwa kuhudhuria kikao hicho ni makatibu wakuu wa vyama hivyo, Abdulrahman Kinana (CCM), Vincent Mashinji (Chadema) na Ernest Mangu (Mkuu wa Jeshi la Polisi). 

Wengine ni Jaji Francis Mutungi (Msajili wa Vyama vya Siasa), George Masaju (Mwanasheria Mkuu wa Serikali) na katibu mkuu wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD). 

Habari hizo zinasema kuwa mwenyekiti wa Tume, Bahame Nyanduga,  ndiye ambaye amewaita viongozi hao Jumatano ijayo jijini Dar es Salaam. 

Tume ya Haki na Utawala Bora ina jukumu la kuhamasisha hifadhi ya haki za binadamu, kuchunguza jambo lolote, kutoa ushauri kwa Serikali na vyombo vingine vya umma na kuchukua hatua za kukuza, kuendeleza, usuluhishi na suluhu miongoni mwa watu na taasisi. 

Kutokana na hali ya kisiasa ilivyo sasa, mkutano huo hautaweza kumalizika bila ya kuzungumzia majibizano yanayoendelea kuhusu operesheni Ukuta na madai ya ukandamizwaji demokrasia unaodaiwa kufanywa na Serikali. 

Alipoulizwa   kuhusu mkutano huo, Nyanduga alimtaka mwandishi  kuwahoji kwa kina watu waliotoa habari hizo kwa sababu yeye hakutoa taarifa yoyote kwa vyombo vya habari kuhusu ajenda za mkutano huo.

 “Sikutoa mwaliko wala taarifa kwenu (wanahabari),” alisema Nyandyga alipoulizwa  kuhusu ajenda za mkutano huo. 

“Aliyekwambia (suala hilo), akupe taarifa kamili. Nikisema tunajadili nini, haitakuwa na maana ya kuitisha mkutano.” 

Mwezi mmoja uliopita, Rais John Magufuli alitangaza kuzuia mikutano ya kisiasa wakati akipokea ripoti ya Uchaguzi Mkuu uliopita, akisema wanasiasa watafanya siasa mwaka 2020 wakati wa uchaguzi mwingine, akisema wakati huu ni wa kazi na asingependa kuona “mtu yeyote akinizuia kutekeleza ahadi nilizozitoa kwa wananchi wakati wa uchaguzi”. 

Ndani ya kipindi hicho, Chadema imezuiwa kufanya mkutano wa hadhara Kahama mkoani Shinyanga, imezuiwa kufanya hafla ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Dodoma na ACT Wazalendo imezuiwa kufanya mkutano wake wa ndani kujadili bajeti ya 2016/17. 

Hatua hizo zilisababisha Chadema kufungua kesi Mahakama Kuu ikitaka itoe tafsiri baada ya polisi kuzuia mkutano Kahama na baadaye kuzuia viongozi wa chama hicho kuingia ofisi za Chadema za wilaya hiyo. 

Wiki iliyopita akiwa njiani kuelekea Kahama, Rais Magufuli alifafanua kauli yake kupiga marufuku mikutano ya kisiasa, akisema waliozuiwa ni wale walioshindwa kwenye Uchaguzi Mkuu na kwamba wale walioshinda wafanye mikutano kwenye maeneo yao na wasialike mwanasiasa kutoka sehemu nyingine. 

Ufafanuzi huo uliotolewa siku chache baada ya Chadema kutangaza operesheni hiyo ya Ukuta, umeibuka mjadala mpya, huku Jeshi la Polisi na wakuu wa mikoa wakitangaza kupiga marufuku mikutano ya Ukuta, huku wakizuia mwaliko wa wanasiasa kwenye mikutano itakayopata kibali. 

Chadema inasema kuwa ina haki ya kufanya mikutano popote pale kwa kuwa hakuna sehemu ambayo Sheria ya Vyama vya Siasa inakataza kufanya siasa baada ya uchaguzi. 

Takriban wiki mbili zilizopita, Mbowe alitangaza mikakati mitatu iliyoazimiwa na Kamati Kuu ya Chadema, ikilenga kupinga kile ambacho chama hicho inakiita kuwa ni ukandamizaji wa haki na demokrasia unaofanywa na Serikali. 

Mbowe alisema moja ya mikakati hiyo ni kufanya maandamano na mikutano nchi nzima kuanzia Septemba Mosi mwaka huu, kama ishara ya kupinga kauli ya Rais na polisi kuhusu mikutano na maandamano. 

Mbali na mkakati huo, Chadema imeanzisha operesheni Ukuta, ikitaja matukio 11 inayodai kuwa ya ukandamizaji wa demokrasia nchini na mengine 24 kuwa yamesababisha kuanzishwa kwa operesheni hiyo.

 Mikakati hiyo ya Chadema ilipingwa na viongozi wa CCM na Jaji Mutungi kwa madai kuwa imejaa uchochezi. 

Wakati CCM ikiwataka Watanzania kutafakari kabla ya kuamua kuungana na viongozi wa Chadema kudai demokrasia na kugeuka kafara kwa vyombo vya ulinzi na usalama, Jaji Mutungi alisema kauli za chama hicho cha upinzani ni kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa. 

Wiki moja iliyopita, Jeshi la Polisi lilitoa kibali kwa Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa kufanya mkutano wa hadhara jimboni kwake likizuia wanasiasa kutoka maeneo mengine na pia kuzungumzia chama kingine na kuisema Serikali. 

Mkutano mwingine uliofanyika Ikungi na kuhutubiwa na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, uliisha salama lakini muda mfupi baadaye mwanasheria huyo wa Chadema alimakatwa na Polisi na kusafirishwa hadi Dar es Salaam ambako amefunguliwa kesi ya uchochezi.

Serikali Yatangaza Mwongozo Mpya wa Elimu Kuwa Masomo ya Sayansi ni Lazima Yasomwe Na Wanafunzi Wote

$
0
0

SERIKALI imetangaza mwongozo mpya kuwa kuanzia sasa masomo ya sayansi ni lazima kusomwa na wanafunzi wote wanaosoma elimu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. 

Kwa mujibu wa Sera ya Elimu iliyopo, wanafunzi wanaosoma elimu ya sekondari wanaweza kuchagua aina ya masomo watakayo wafikapo kidato cha tatu na kuacha mengine.

Uamuzi huo ulitangazwa jana mjini Tanga  na Waziri wa Elimu, Teknolojia, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako wakati akizungumza na mamia ya walimu wa elimu ya msingi kwenye mafunzo ya muda mfupi kuhusu mtaala mpya wa kufundishia wanafunzi wa darasa la tatu na nne.

Alisema hivi sasa nchi imedhamiria kuingia kwenye uchumi wa kati ambao ni wa viwanda, hivyo suala la sayansi haliwezi kuepukwa kwa sababu ni wakati sasa wa kuwa na wataalamu wengi wa fani za sayansi watakaoweza kutosheleza mahitaji ya sekta ya viwanda nchini.

Alisema kutokana na uhaba wa wataalamu wa sayansi nchini kwenye maeneo mengi, wizara imeamua kuanzia sasa wanafunzi wote wa elimu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, watalazimika kusoma masomo ya sayansi na kufanya mtihani wa masomo hayo, na kwamba baada ya matokeo kutoka ndipo watafanya uamuzi ama wa kuendelea nayo au la.

Hatua hii kwa mujibu wa Profesa Ndalichako, itamlazimisha mwanafunzi kusoma kwa bidii ili kuhakikisha anafaulu masomo hayo ingawa hivi sasa wanafunzi walio wengi wanadai masomo hayo ni magumu, ndiyo maana wanachagua kusoma masomo ya sanaa.

Alisema ili kuhakikisha azma ya serikali ya wanafunzi wanapata vitendea kazi vya masomo hayo, Sh bilioni 12 zimetengwa kwenye bajeti ya fedha ya mwaka huu kwa ajili ya kununulia vifaa vya maabara kwenye shule zote za sekondari nchini ili kuwepo na zana za kufundishia kwa ajili ya masomo ya sayansi.

"Mafunzo ya vitendo sasa sio mbadala ni lazima, na yatafanywa kama sehemu ya masomo na wanafunzi wote watalazimika kuyafanya kwa vitendo ili wawe na uelewa wa walichosoma kwa manufaa ya taifa,” alisema Profesa Ndalichako.

Alisema Serikali ya Awamu ya tano imedhamiria kuona kiwango cha elimu kinachotolewa nchini kina hadhi sawa na elimu itolewayo na mataifa mengine ili kupata wataalamu wenye sifa zinazokidhi mahitaji ya soko hata kama sio wote wataajiriwa ila hata wale wasiopata ajira wajiajiri kupitia elimu waliyopata.

Aliwataka walimu waliohudhuria mafunzo hayo kuhakikisha wanatumia uwezo wao na elimu waliyopata kufanya kazi kwa mujibu wa maadili ya taaluma ya ualimu ili kuwajengea msingi mzuri wa elimu wanafunzi wa shule za msingi.

Akizungumzia kauli ya Profesa Ndalichako, Mwenyekiti wa Wamiliki wa Shule Binafsi Tanzania (TAMANGOSCO), Mahmoud Mringo alisema ni uamuzi mzuri ila umekuja kwa kuchelewa kwa sababu mahitaji ya wataalamu wa sayansi nchini ni makubwa kuliko idadi ya wanafunzi wanaosoma masomo hayo.

Alisema pamoja na uamuzi huo mzuri uliochukuliwa na serikali, lakini bado kutakuwa na changamoto ya uhaba wa walimu wa masomo hayo, maabara na maktaba na kwamba hali hiyo inaweza kusababisha mahitaji ya walimu hao kutoka nje yakaongezeka.

Katibu wa Tamangosco, Benjamin Mkonya alisema ni hatua nzuri ingawa utekelezaji wake utakuwa na changamoto nyingi kwa sababu hali halisi ya mazingira ilivyo nchini.

Alisema ikiwa serikali inadhamiria kutekeleza azma hiyo ni vyema kipengele cha vigezo vya shule kuwepo ambavyo vimeainishwa ndani ya sheria ya elimu nchini, vikaangaliwa ambavyo ni uwepo wa maabara ya kutosha, maktaba yenye vifaa na walimu wa kutosha.

Alisema iwapo vigezo hivyo vikiangaliwa shule ambazo hazijakidhi vigezo hivyo zikafutwa na vifaa vilivyopo kwenye maabara na maktaba hizo zikaongezwa kwenye shule zenye vifaa hivyo ili kusaidia utekelezaji wa azma hiyo ya kufundisha masomo ya sayansi kwa wanafunzi wote kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Walimu washiriki wameishukuru serikali kwa mafunzo hayo ambayo walisema ni mazuri na yameongeza kiwango chao cha uelewa na kuwaongezea mbinu za ufundishaji sambamba na kukuza morali ya kazi zao.

Pamoja na kushukuru, wameomba wizara hiyo iangalie jinsi ya kuweka posho kwa baadhi ya maeneo ya kazi, hususan kwenye vituo vya kazi vilivyopo pembezoni na kwenye mazingira magumu ili kuwajengea walimu motisha wa kufundisha maeneo hayo.

Walimu waliohudhuria mafunzo hayo ni 480 wanaotoka halmashauri za Bumbuli, Mji wa Handeni na Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.

Waziri Atangaza kiama Kwa Trafiki

$
0
0
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni amesema askari wa usalama barabarani watakaobainika kupokea rushwa watashughulikiwa kwa kuwa wataweka mitego kwa ajili ya kuwakamata.

Alisema wananchi wamekuwa wakilalamikia askari hao kuwa wanapenda rushwa na ndio chanzo cha ajali barabarani na kwamba wanachafua taswira ya jeshi hilo.

Akizungumza na askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam jana jijini humo, Masauni alisema mtego watakaouweka ndilo kaburi lao na kwamba watafungwa kwa sababu ya tamaa ya Sh 10,000, hivyo wajihadhari.

Alisema Taifa linakabiliwa na changamoto ya ajali za barabarani na kwamba wana wajibu wa kuwalinda raia wa nchi hii, badala ya kushiriki kuwaangamiza kwa tamaa ya fedha. Alisisitiza kuwa hawataweza kufikia uchumi wa kati endapo nguvu kazi zitaendelea kupotea kutokana na ajali za barabarani.

“Kuondoa ajali inawezekana na watu watakaoleta sababu za ajabu ajabu hiki sio kipindi chake ni lazima tuzitekeleze kama tulivyopanga kwenye mkakati wetu kwamba ndani ya miezi sita tuwe tumepunguza ajali kwa asilimia 10,” alisema akisisitiza askari kubadilika, kwani ndio wasimamizi wakubwa wa usalama barabarani.

Akizungumzia changamoto zinazowakabili askari hao, alisema kuwa wapo baadhi ya askari ambao wanafanya kazi katika mazingira hatarishi na magumu kama vile kupigwa risasi, kugongwa na magari na kwamba jitihada zao zinatakiwa zitambulike kwa kupandishwa vyeo na mishahara kwa kazi nzuri wanazofanya.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga alisema mkutano huo ni sehemu ya kutoa elimu kwa askari watakaosimamia mkakati huo kuhakikisha ajali zinapungua.

Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Abdulrahman Kaniki alisema ajali za barabarani ni miongoni mwa changamoto zinazolikabili Taifa.

Alisema ni wakati wa askari kuongeza chachu, ari na mbinu katika kutekeleza majukumu yao kwa wananchi na kwamba wapo imara kutekeleza maagizo halali kutoka kwa viongozi wao.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Agosti 7

Rais Magufuli Asali Katika Kanisa La Bikira Maria Parokia Ya Chato, Pia Atembelea Kanisa La Anglikana, AIC Pamoja Na Msikiti Wa Omar Bin-l-khattab Chato Mkoani Geita

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Agosti, 2016 ametembelea Msikiti na Makanisa yaliyopo Chato Mjini Mkoani Geita na kuendelea kuwasihi Watanzania kuombea amani na utulivu katika nchi bila kujali tofauti za dini, makabila na kanda wanazotoka.

Rais Magufuli ametoa ujumbe huo mara baada ya kusali ibada ya Jumapili katika Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato, na baadaye kutembelea Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Stephano Parokia ya Chato, Kanisa la African Inland Church la Chato na kumalizia katika Msikiti wa Omar Bin -L-Khattab wa Chato.

Dkt. Magufuli amesema pamoja na Watanzania wote kuungana kuombea amani na utulivu pia hawana budi kutekeleza kwa vitendo Maandiko Matakatifu ya Biblia yasemayo "Asiyefanya kazi na asile" kwa kuhakikisha kila mmoja anachapakazi kwa juhudi na maarifa ili kuharakisha maendeleo ya Taifa.

"Ndugu zangu nawashukuru sana, muendelee kuliombea taifa hili, taifa letu ni la umoja, sisi wote ni Watanzania, tuendelee kumuomba mola wetu, kudumisha amani yetu, kujenga umoja wetu kwa dini zote, makabila yote na vyama vyote, kwa sababu mola wetu anatupenda sisi sote" Amesema Rais Magufuli.

Aidha, mara baada ya kuwasalimu waumini wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato, Rais Magufuli ameendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo jipya la Kanisa hilo ambapo amefanikiwa kukusanya Shilingi Milioni moja za papo kwa papo.

Tayari Dkt. Magufuli alishachangia ujenzi huo kwa kutoa Shilingi Milioni kumi tarehe 03 Aprili, 2016 na ametoa wito kwa watu mbalimbali kujitokeza kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo.

Katika Msikiti wa Omar Bin-L-Khattab na Makanisa ya Anglikana na African Inland Church Rais Magufuli amechangia Shilingi Milioni tano kwa kila moja kwa ajili kuendeleza na kukarabati majengo.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Chato

07 Agosti, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waamini wa kanisa Katoliki wa Parokia ya Chato mara baada ya Ibada katika kanisa hilo Chato Mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihamasisha mchango wa ujenzi wa Kanisa jipya la la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Padre wa Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Henry Mulinganisa mara baada ya kushiriki Ibada katika Kanisa hilo.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na na Padre wa Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Henry Mulinganisa mara baada ya kuwasili kwenye kanisa hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono waamini wa Kanisa Katoliki Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita hawapo pichani mara baada ya kushiriki Ibada katika kanisa hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimsikiliza Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Chato Zacharia Samson mara baada ya kuwasili katika kanisa hilo la Anglikana Chato Mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiimba wimbo wa Amani pamoja na Kwaya ya Kanisa la African Inland Church la Chato Mkoani Geita mara baada ya kuwasili katika kanisa hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia Mwalimu wake wa zamani wa Shule ya Msingi Chato Mkoani GeitaMwalimu Mkuu Mstaafu Jackson Nyamwaga mara baada ya kumuona wakati akitoka katika Kanisa la African Inland Church la Chato Mkoani Geita.

Shekhe wa Bakwata Wilaya ya Chato Hassan Issa Mnubi akiongoza dua ya Kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli nje ya Msikiti wa Omar Bin-L-Khattab Chato Mkoani Geita. PICHA NA IKULU

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 11 & 12

$
0
0


MTUNZI:EDDAZARIA G.MSULWA


.....Maumivu makali yakanitawala katika kifua changu nikajishika kwenye kifua changu na kugungua kuna damu zinanitoka ikanibidi niukaze mkono wangu ili kuzuia damu nyingi kuendelea kuvuja katika sehemu risasi ilipo pita.Manka akaanza kuweseka huku akiwa kama haamini kwa tukio alilo lifanya.Akaitupa bastola chini na kupiga magoti kuangalia eneo aneo alilo nijeruhi kwa risasi

“Eddy nilikuwa ninakutania”
Manka alizungumza huku akilia na kuonekana kuchanganyikiwa kwa kitendo alicho nifanyia.Taratibu nikahisi nguvu zikiniishia huku mwili ukizizima kwa kukosa uwezo wa kufumbua machona taratibu nikajikuta hali nzito ambayo sikuwahi kuipata katika maisha yangu ikiutawala moyo wangu.

                                     
 Macho yangu yakafunguka na kujikuta Mama akiwa amekaa pembeni yangu huku puani kwangu nikiwa na mashine ya kupulia.Mama alipo niona nimefungua macho yangu akaanza kuliita jina langu na nikamuitikia kwa sauti ya chini

“Mwanangu unajisikiaje?’
Nikataka kunyanyuka ila nikashindwa na mama akanirudisha chini na kugundua kuna bandeji kuwa nimefungwa kwenye kifua changu.Kumbukumbu zinanikumbusha dakika za mwisho nilikuwa na Manka ila kuanzia hapo sikuelewa kitu kilicho enedelea hadi mama akawa pembeni yangu.

“Mama nipo wapi?”
“Mwanangu upo hospitalini?”
“Nani kanileta?
“Ni story ndefu kidogo mwanangu ila kwa sasa pumzinka nitakuadisia ukipata nafuu”

   Simu ya mama ikaita akaitazama kwa muda kisha akaipokea na nikamuona sura yake ikiwa imebadilika kidogo na kuwa sura ya hasira

“Ndio ameamka”
“Godwin nakuomba unielewe hapa huna mtoto na huyo mwanao aliye mfanyia mwanangu hivi nilazma nimfunge”
“Ahhhh kwahiyo wewe ndio umemtuma amuue mwanangu si ndio?”

“Sasa lazima nimfunge na kumbuka kuwa tangu mwanangu akiwa utotoni hukuwa na mapenzi naye sasa naomba umuache na wala sihitaji urudi uje umuuone”

 Mama akakata simu huku akiachia msunyo mkali,sasa sikuelewa anazungumza na nani na kumfokea kiasi hicho
“Mama unazungumza na nani?”
“Ahaaa mwanangu nitakuambia”

Mama alanijibu huku akiwa anatabasamu kisha akanibusu katika paji la uso wangu.Simu yake ikaiita tena na ikamlazimu kutoka nje.Sikutaka kujisumbua mama anamfokea nani niahisi watakuwa ni watu wa serikali anao fanya nao kazi.Mama akarudi na kukaa karibu yangu huku machozi yakimlenga lenga akionekana kuwa na hasira kubwa na tangu nizaliwe sikuwahi kumuona mama akiwa katika hali kama hiyo.

“Mama nipo hospitali gani?”
“Ni KCMC”
 Mlango ukafunguliwa akaingia mzee wa makamo akiwa amevalia nguo za polisi huku akiwa na vyeo vingi
“Habari yako mheshimiwa?”
“Salama vipi mumesha mkamata aliye sababisha hili tukio?”

“Ndio muheshimiwa ila ninashindwa kuelewa kwani mzee ananiambia nimuachie huru ili we……”
“Nisikilize wewe mimi si ndio nimetoa  amri yule binti kukamatwa?”
“Ndio”
“Sasa mbona unaniletea Kiswahili.Muwekeni ndani hadi mimi nije sawa”
“Sawa mkuu”

Askari akatoka na kutuacha ndani ya chumba na ukimya ukatawala huku mama akonekana kusongwa na mawazo na mara kwa mara akawa anasunya sikujua kinacho mfanya asunye ni nini.

 Nikakaa hospitali kwa wiki moja nikapewa ruhusa japo sikuwa nimepona vizuri.Safari ya kwenda uwanja wa ndege wa KIA ikaanza huku dereva anayemuendesha mama akiwa makini katika uendeshaji wake kutokana Dokta ameniambia nisifanye kazi ngumu wala kupata mitingishiko ya aina yoyote kwani kidonda changu kinaweza kisipone kwa haraka.Tukakuta ndege ya kukodi ikiwa tayari kwa ajili yetu mimi na mama.Tukapanda na dereva akaondoka na gari ya mama na tukaahidiana naye atatukuta nyumbani.Safari ikaanza taratibu huku ndege aina ya Fast Jet tuliyoipanda ikizidisha kasi kadri muda unavyo kwenda tukiwa angani

  “Pole kaka”,Muhudumu wa kike wa ndege akanipa pole huku akiniwekea juisi kwenye kimeza kidogo kilichopo mbele yangu
“Asante”
“Muheshimiwa huyu ni mwanao”
“Ndio ni mwangu wa kwanza na wamwisho”
“Aisee mtu akikutizama wala hata amini kama unamtoto mkubwa kiasi hichi”

“Unajua kipindi sisi tulipokuwa tunamaliza kidato cha sita mika ya themanini tulipelekwa jeshini sote na ilitusaidia kuweza kuzilinda afya zetu ni tofauti na hao kina Eddy mtu nikimwambia mwanangu ana miaka 20 haamini”
“Mmmm mama umekosea nina miaka 21”

“Sasa sibado haijatimia”
“Sasa muheshimiwa nyinyi si mupo huku ngazi za juu kwanini musirudishe sheria ya wanafunzi wanao maliza kuingia jeshini?”

“Ile imerudishwa sasa sijui huku mwanagu kama ataweza kwa maana mmmm”
“Mama wewe unaniona mimi nimeoza sana”
“Wewe hujioni”

Tukacheka sote na safari ikaendelea,haikuchukua muda sana kutua katika uwanja wa ndege wa mwalimu JK Nyerere.Gari ya serikali ikaja kutuchukua na kutupeleka nyumbani maeneo ya Masaki.Nikakumbuka kuna kitu ninakihitaji kukijua vizuri kutoka kwa mama kwani kila nilipohitaji kumuuliza nilijikuta nikisahau

“Mama hivi pale hospitalini nilifikaje?”
“Eddy mwanagu hata hatujapumzika umeanza kwa maswali?”
“Ndio ama nataka kujua?”
“Kavue nguo zako chumbani kwako upumzike kisha wakati wa jioni tutazungumza ngoja mimi niende ofisini jana kuna kazi niliiacha”

“Kwani mama jana ulikuja ofisini?”
“Ndio kila siku nilipokuwa ninakuja hospitali nilikuwa ninalala Dar asubuhi ninakuja kwa ndege jioni au mchana ninarudi kwa ndege”

“Mmmmm mama mbona nyumba ipo kimya dada wa kazi yupo wapi?”
“Nimemfukuza”
“Kwa nini?”
“Nitakuja kukuambia jioni nikitoka kazini”

Mama akaondoka mimi nikaelekea chumbani kwangu,sikukuta kuna mabadiliko ya aina yoyote tangu nilipo kiacha pindi nanakwenda shule.Nikaingia bafuni nichukua taulo na kulichovya kwenye maji na kuanza kujisujgua sehemu ya mwili kwani ndio oga yangu tangu nikiwa huspitalini hii ilisaidia kidonda kuto kuingia maji.Nikamaliza na kurudi kitandani kutokana nimeshiba nikaamua kulala...

Waziri Mkuu Majaliwa Uso Kwa Uso Na Askofu Gwajima

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Uzima na Ufufuo katika hafla ya harusi ya Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Amon Mpanju na mkewe Analises iliyofanyiak kwenye ukumbi wa jeshi wa Lugalo jijini Dar es salaam Agosti 6, 2016.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Amon Mpanju akilishwa keki na mkewe , Analises katika tafrija ya harusi yao iliyofanyika kwenye ukumbi wa Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam Agosti 6, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary walihudhuria katika tafrija hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Amon Mpanju akimlisha keki mkewe , Analises katika tafrija ya harusi yao iliyofanyika kwenye ukumbi wa Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam Agosti 6, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary Walihudhuria katika tafrija hiyo.

Waziri Mkuu Majaliwa Awasili Jijini Mbeya Leo

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songwe, Mbeya Agosti 7, 2016 ambako Agosti 8, 2016 atahitimisha maonyesho ya wakulima Nanenane.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakipokea heshima kutoka kwa Skauti wa Mbeya baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Songwe Agosti 7, 2016 ambako Agosti nane atahitimisha maonyesho ya wakulima Nanenane. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakifurahia ngoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songwe, Mbeya Agosti 7, 2016 ambako Agosti 8, 2016 Mheshimiwa Majaliwa atahitimisha maonyesho ya wakulima Nanenane. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makla. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu ya Agosti 8

Polisi wazuia ghafla mkutano wa CHADEMA Chalinze........Mbowe Asema Wapo Tayari Kufa Kwa Kupigania Demokrasia

$
0
0

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limefuta mkutano wa hadhara wa Chadema uliopangwa kufanyika katika Uwanja wa Miembe Saba mjini Chalinze.

Mkutano huo uliokuwa ufanyike jana, ulikuwa uhutubiwe na Waziri Mkuu mstaafu na mjumbe wa kamati ya Chadema, Frederick Sumaye.
 
Mwenyekiti wa Chadema, Mkoa wa Pwani Baraka Mwago alisema jana kuwa alishangazwa na hatua hiyo ya ghafla ya polisi kwa kuwa mkutano huo ulifuata taratibu zote na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chalinze, aliruhusu kufanyika kuanzia saa 6.00 mchana hadi saa 12.00 jioni.
 
Alisema wakati maandalizi yote yakiwa tayari, ilipotimia saa nane mchana waliitwa polisi na kuelezwa kuwa mkutano huo umezuia kwa maelezo kuwa intelijensia ya polisi imeonyesha kuwa ungehudhuriwa na viongozi wengi wa kitaifa, hivyo polisi Chalinze haijajipanga kutoa ulinzi kwa viongozi hao.
 
“Hii sababu imetushangaza kwa sababu kiongozi wa kitaifa ambaye angehudhuria ni Sumaye peke yake."
 
Kwa mujibu wa Katiba ya Chadema kipengele cha 7.5.3 (f) inamtambua mjumbe wa kamati kuu au baraza kuu anayeishi katika mkoa kuwa ni mjumbe wa baraza la mkoa husika.
 
“Kutokana na kipengele hicho, Sumaye ana sifa za kuhudhuria mkutano huu kwa sababu anaishi Kiluvya wilayani Kisarawe,” alisema Mwagu.
 
Alisema lengo la mkutano huo, lilikuwa ni kuutambulisha uongozi mpya wa Chadema kwa wananchi baada ya kufanyika uchaguzi mdogo Juni 4, mwaka huu wilayani Mkuranga.
 
Katibu wa Chadema mkoani humo, Halfani Milambo alisema waliandika barua kuwataarifu polisi na likakubali, lakini walishangazwa kuzuiwa baada ya kufika katika Uwanja wa Miembe Saba walikotakiwa kufanya mkutano.
 
“Tuliwaandikia barua tarehe Agosti 4 na siku iliyofuata Agosti 5 tulikubaliwa na Mkuu wa Polisi Chalinze (OCD), SSP J. Magomi kufanya mkutano kwa masharti,” alisema.
Alitaja masharti ambayo jeshi hilo liliwapa kuwa ni pamoja na kutokuwapo kwa maandamano ya bodaboda, ya miguu au magari, kutokukashifu chama au utawala wa kiongozi yeyote na kuzingatia muda wa kuanza na kumaliza mkutano.
 
Alisema kuwa cha kushangaza jana baada ya kukamilisha maandalizi yote ikiwamo kufanya matangazo na kufunga vyombo vya muziki, baadhi ya viongozi waliitwa kwenye Ofisi ya Polisi Wilaya ya Chalinze na kuambiwa wasifanye mkutano huo.
 
Alisema walielezwa kuwa ujumbe ambao unaenea kwenye mtandao unasema mkutano huo utaleta watu wengi sana, hivyo usalama utakuwa mdogo.
 
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Boniventura Mushongi alisema lengo la Polisi si kuwakataza kufanya mkutano, lakini kilichoonekana ni kuwa walikiuka maelekezo kwani awali walipaswa kufanya mkutano wa ndani na si wa nje.
 
“Sisi hatuwakatazi kufanya mikutano yao, lakini ni vema wafuate makubaliano, maana sisi Jeshi la Polisi tuliwaruhusu wafanye mkutano wa ndani lakini tulishangazwa kuona wanaanza kufanya nje huku wakipiga muziki,” alisema.
 
Mushongi alisema pia polisi inazuia mikutano yote ambayo haina madiwani wala wabunge katika eneo husika, jambo ambalo halikuwa kwenye maelekezo ya OCD.
 
“Chadema katika eneo la Chalinze hawana diwani wala mbunge, hivyo wamekosa sifa za kufanya mkutano huu. Kama ni kikao cha ndani hatuna tatizo wafanye hata wakialika watu 200,” alisema Mushongi.
 
Hata hivyo, Mushongi alisema Chadema Pwani walipopeleka barua ya maombi mkutano huo walipewa masharti hayo.
 
Mbowe: Tuko tayari kwa lolote 
Wakati hayo yakiendelea, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema yeye na makamanda wake wako tayari kwa lolote kwa ajili ya kutetea misingi thabiti ya utawala bora unaoheshimu utawala wa sheria.
 
Akizungumza  jana, Mbowe alisema hakuna mtu wa kuwafundisha makamanda wa Chadema, hivyo mikutano ya Ukuta itafanyika nchi nzima kuanzia Septemba Mosi.
 
“Ambao hawako tayari warudi nyuma, hakuna aliyelazimishwa, watuache sisi tutangulie wa kufa wafe na wa kupona wapone. Haiwezekani mtu apuuze sheria, avunje katiba halafu taifa linyamaze,”alisema.
 
“Sisi tumeamua kuchukua mzigo huo kwa niaba ya wananchi wote. Kama ataua wacha aue tu, kama atatufunga wacha atufunge tu lakini tutakuwa tumeacha legacy (kumbukumbu) duniani,” alisisitiza.
 
Mbowe alisema sifa ya kiongozi bora anayeheshimu misingi ya kidemokrasia ni kuheshimu utawala bora unaoheshimu utawala wa sheria.
 
Kwa mujibu wa Mbowe, Rais anakiuka Katiba na sheria za nchi zinazoruhusu vyama vya siasa kuendesha mikutano ya hadhara na hakuna mtu ndani ya CCM anayezungumzia hilo.
 
Mbowe alisema Rais amejisahau kuwa yeye (Mbowe) ni mwenyekiti wa taifa kama alivyo Rais, hivyo anastahili kuzunguka nchi nzima kujenga uhai wa chama.
 
“Rais anazunguka kwenye mikoa anavisema vyama vya upinzani na kutoa amri mbalimbali lakini sisi (upinzani) hatuna jukwaa la kujibu au kutoa ufafanuzi. Anasema tusubiri hadi 2020,” alilalamika Mbowe.
 
“Rais anatoa amri, wakuu wake wa mikoa wanatoa amri, wakuu wa wilaya wanatoa amri, watu wanafukuzwa kazi ovyo. Nchi haiwezi kwenda kwa staili hii,” alisema.
 
“Wewe unanyanyuka tu na kusema watu wahamie Dodoma kivipi? Issue ya kuhamia Dodoma ni suala la kitaifa siyo mamlaka ya mtu mmoja tu kwa kuwa ni Rais.”

 “Hata Nyerere 1973 alipopitisha hoja ya watu kuhamia Dodoma kilikuwa ni kikao cha NEC ya Tanu. Mpaka leo hakuna sheria ya kuhamia Dodoma na nchi hii inaoongozwa kwa sheria.” 

Mbowe alisema kwa kutambua kuwa hakuna sheria ya kuhamia Dodoma, ndiyo maana Ilani ya CCM (2015-2020) imeeleza kutengeneza sheria ya kuhamia makao makuu Dodoma.
 
“Hakuna sheria. Rais hawezi kuamua matakwa yake binafsi yakawa ni sheria ya nchi. Alipaswa apeleke muswada wa sheria bungeni na ipitishwe na Bunge siyo kauli ya mtu mmoja,” alisisitiza Mbowe.
 
Lissu: Tutafuata sheria 
Wakati huohuo, mwanasheria Mkuu wa Chadema na mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesema katika utekelezaji wa Ukuta watafuata sheria kwa kupeleka barua za taarifa ya mikutano kwa wakuu wa polisi nchi nzima saa 48, kabla ya kuanza mikutano hiyo Septemba Mosi mwaka huu.
 
Akizungumza juzi katika mahojiano na Redio ya Sauti ya Ujerumani (DW), Lissu alisema mikutano hiyo itafanywa kwa kufuata sheria na taratibu ikiwamo kutoa taarifa kwa wakuu wa polisi wa wilaya.
 
Lissu ambaye aliachiwa na mahakama juzi kwa dhamana, alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa kwanini chama chake kisitafute njia mbadala ya operesheni Ukuta ambayo Serikali imesema itakabiliana nayo kwa njia yoyote ile.
 
“Tumesema hatutafanya mkutano wowote usiokuwa na taarifa.Tutapeleka taarifa kwa wakuu wa polisi wilaya wote Tanzania nzima kama inavyotakiwa. Sasa hiyo hatuvunji sheria, tunatekeleza sheria,” alisema Lissu.
 
Mbunge huyo, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uchochezi na kuidharau mahakama, alibainisha kuwa mikutano ya hadhara kuanzia Septemba Mosi, itafanyika kwa mujibu wa sheria za nchi kama Katiba ya nchi na sheria ya vyama vya siasa inavyoeleza.
 
Alisema sheria inasema chama cha siasa ambacho kimeandikishwa kikitaka kufanya mkutano wowote wa hadhara wa siasa, kinatakiwa kupeleka barua ya taarifa kwa mkuu wa polisi wa wilaya saa 48 kabla ya mkutano huo.
 
“Sheria inasema huyo ambaye tunampelekea taarifa atupe ulinzi kwenye mikutano yetu. Ndicho tunachotaka,” alisema Lissu.
 
Alipoulizwa kama ni sawa iwapo polisi ikisema haiwezi kuwapa ulinzi na wasifanye mkutano katika eneo husika kwa wakati huo, Lissu alijibu,“(OCD) Ana uwezo wa kutuambia msifanye leo, msifanye kwenye eneo hili au msifanye saa hii, lakini hana uwezo wa kukataa katakata.” 

Mbunge huyo alisema kilichotokea nchini na kinachofanyika sasa si mikutano kudhibitiwa bali inakatazwa.
 
“Hakuna sheria inayokataza au inayowapa mamlaka ya kukataza mikutano moja kwa moja kama hakuna tangazo la hali ya hatari,” alisema Lissu.
 
Alisema kama Magufuli hataki mikutano atangazie dunia kwamba Tanzania ina hali ya hatari.
 
“Akitangaza hali ya hatari tutamwelewa na wengine tutamuuliza kilichotokea ni kitu gani mpaka kuwe na hali ya hatari,” alisema Lissu.

  

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 28

$
0
0
Mtunzi: ENEA FAIDY

.... Leyla alikuwa amechanganyikiwa sana baada ya mumewe kuwa katika Hali ile. Alishindwa kuelewa atafanyaje ili kujimudu katika familia yake kwani Mwalimu John ambaye ni mumewe asingeweza kurudi tena kazini. Kilichomfanya anyong'onyee zaidi ni hali ya Judith kwani hakuweza kuongea wala kusikia. Leyla alikosa raha sana, akakaa kitini akiwa na mawazo mengi sana. Alijiuliza afanye nini ili aweze kuwaokoa wahanga wa tatizo asilojua limetona na nini.

Akiwa katika kutafakari hayo yote ghafla wazo muhimu lilimjia kichwani mwake. Leyla alichukua simu yake na kutafutw namba fulani kisha akapiga. Simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa kisha ikakakata. Leyla hakukata tamaa akapiga tena lakini majibu yakabaki Yale Yale, simu haikupokelewa akajaribu tena na tens simu ikapokelewa.

"Bwana asifiwe mchungaji.." Alizungumza Leyla kwa sauti ya unyenyekevu sana kwani aliyempigia alikuwa ni mchungaji wake.
"Amen.. Unasemaje?" Alijibu mchungaji yule kama vile hataki kuzungumza.
"Samahani mchungaji nina shida... Naomba msaada wako!" Alisema Leyla.
"Shida gani"
"Kuhusu familia yangu!".

"Kama ni mumeo mama... Chukua imani hapo ulipoanza maombi Mimi sina muda... Nina mambo mengi ya kufanya.." Alisema mchungaji yule kwa ukali kiasi jambo lililomtisha sana Leyla kwani hakutegemea kama mchungaji wake angemjibu vile.

"Pastor! Tafadhali nisaidie.." Leyla alimbembeleza mchungaji lakini hakumuelewa. Na mchungaji huyu ndiye aliyefanya mazishi ya mwalimu John.

"Kwasasa sipo nyumbani.. Nipo mbali kikazi..." Alisema Mchungaji yule. Kiukweli ilikuwa vigumu kwa Leyla kuamini maneno ya mchungaji wake kwani Siku zote aliamini mchungaji wake angekuwa ndiye mfariji lakini haikuwa hivyo.
"Cha kukusaidia labda nitawaita wanamaombi waje kukusaidia" alisema mchungaji na kukata simu.

Leyla alishindwa afanye nini kwani hata ndugu zake walimtenga. Ilipita nusu SAA nzima , mlango wake ukagongwa. Alifurahi sana kwani alijua tayari mchungaji amewasiliana na wanamaombi ili waje kuombea familia yake. Alinyanyuka kitini na kwenda moja kwa moja kufungua mlango.

Mkuu wa Wilaya ya Nzega Awapiga Marufuku Madiwani na Wabunge Kufanya Mikutano ya hadhara nje ya maeneo yao waliyochaguliwa

$
0
0

SERIKALI wilaya ya Nzega mkoani Tabora imepiga marufuku wabunge na madiwani wa vyama vyote, kutofanya mikutano ya hadhara nje ya maeneo yao waliyochaguliwa.

Imechukua hatua hiyo ili kuepusha uchochezi wa kisiasa, ambao unaweza kujitokeza na kuhatarisha amani.

Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupulla amesema viongozi hao wanapaswa kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo yao ya uchaguzi.

Amesema mbunge ama diwani, haruhusiwi kufanya mikutano nje ya eneo lake na endapo atabainika, atachukuliwa hatua kali za kinidhamu, ikiwa ni pamoja na kufikishwa katika vyombo vya dola.

Amesema serikali imetoa agizo hilo ili wananchi waweze kupata taarifa za maendeleo na sikuendelea kutoa lugha za kukashifu viongozi wa serikali.

Ngupulla aliongeza kuwa serikali haijakataza mikutano ya siasa, bali viongozi hao wanapaswa kufanya siasa safi katika maeneo yao na si kutoka nje ya maeneo yao, kwani wanaweza kuhatarisha amani ya nchi.

Mama Mwenye VVU Pamoja na mtoto wake wakutwa wamekufa mlimani

$
0
0

MKAZI wa wilayani Chato mkoani Geita, Rose Joseph (32) aliyekuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na mtoto wake mwenye umri wa miaka kati ya minne na mitano, wamekutwa mlimani wakiwa wamekufa katika mazingira ya kutatanisha katika kijiji cha Nafuba kilichoko ndani ya Ziwa Victoria wilayani Bunda mkoani Mara.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Nafuba, Zakaria Kachimu alisema tukio hilo liligundulika juzi saa 9:00 mchana katika eneo la mlima huo, baada ya wananchi waliopita katika eneo hilo kuona kwanza mwili wa mwanamke huyo.

Alisema baadaye wananchi walifanikiwa kumtafuta mtoto wake na kumkuta pia akiwa amekufa katika eneo lingine. 

Kachimu alisema mwanamke huyo alifika kisiwani hapo Julai 25, mwaka huu, akiwa na mtoto mdogo wa kiume aitwaye Kababu, akiwa anatafuta kazi ya kuhudumia kwenye mgahawa.

Alisema kuwa kulingana na afya ya mwanamke huyo kudhoofika, kila sehemu alikokwenda kutafuta ajira hiyo alikataliwa. Baada ya kukosa ajira hiyo mwanamke huyo alikwenda kwa jamaa yake ambaye pia ni mwanamke aliyeko kisiwani hapo na kuishi nyumbani hapo.

Baadaye mwanamke huyo alikwenda kutibiwa katika zahanati moja iliyoko kisiwani hapo na ikagundulika kuwa ana mambukizi ya virusi vya Ukimwi na kuambiwa aende katika Kituo cha Afya Kisorya kwa ajili ya kujiunga kwa kupewa dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARVs).

Hata hivyo ilielezwa kuwa mwanamke huyo hakwenda kwenye kituo hicho kama alivyoshauriwa na mganga wa zahanati hiyo.

Aidha, Ofisa Mtendaji huyo alisema siku ya tukio wananchi waliopita katika eneo hilo walikuta mwili wa mwanamke huyo katika mlima huo na kuamua kutoa taarifa, ambapo tena walianza kutafuta mtoto wake na kukuta pia akiwa amekufa katika eneo lingine.

Alisema kuwa chanzo cha vifo hivyo ni cha kutatanisha na kwamba huenda mtoto huyo alikufa kwa njaa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’anzi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. Alisema upelelezi unafanyika kujua chanzo cha vifo hivyo.

Brazil yaonesha nia kuwekeza Tanzania kuzalisha umeme wa maji na mabaki ya miwa

$
0
0
Na Veronica Simba

Serikali ya Brazil imeonesha nia kuwekeza katika sekta ya nishati nchini hususan katika kuzalisha umeme kwa kutumia maji na mabaki ya miwa. Hayo yameelezwa jana jijini Dar es Salaam na Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Carlos Alfonso Puente, alipomtembelea Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ofisini kwake na kufanya mazungumzo naye.

Balozi Puente alimweleza Profesa Muhongo kuwa nchi yake inao ujuzi na uzoefu wa kutosha katika uzalishaji wa umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali hususan maji.

Alisema, Brazil ingependa kuchangia kufanikisha azma ya Rais John Magufuli kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.
“Kutekeleza mchakato wa kuifanya nchi kuwa ya Viwanda, unahitaji umeme mwingi unaotokana na vyanzo mbalimbali. Ni bahati nzuri kwamba Tanzania inazo njia za kufanikisha azma hiyo,” alisema.
Alisema kuwa, nchini Brazil, kuna Kampuni kubwa zenye uzoefu wa muda mrefu unaofikia miaka 20 hadi 40 katika kazi hiyo, ambazo huzalisha umeme wa maji nchini mwao na hata nje ya nchi.

Pia, alitaja eneo jingine ambalo nchi yake ina nia ya kuwekeza kuwa ni uzalishaji wa umeme unaotumia mabaki ya miwa ambayo aliielezea kuwa chanzo kizuri cha nishati safi.

Balozi Puente alisisitiza kuwa, Brazil ikiwa ni nchi inayozalisha miwa kwa kiwango kikubwa duniani, itasaidia kuleta mabadiliko katika sekta ya nishati kwa kuzalisha umeme unaotokana na mabaki ya miwa kwa kutumia teknolojia za kisasa.

Kwa upande wake, Waziri Muhongo, akimjibu Balozi Puente, alikiri kuwa kuwa Brazil ina ujuzi, uzoefu na uwezo mkubwa hususan katika maeneo ambayo Balozi aliyataja na hivyo akamwambia nchi hiyo inakaribishwa kuwekeza Tanzania kwa kufuata masharti na utaratibu uliowekwa na Serikali.

Akizungumzia zaidi kuhusu utaratibu wa uwekezaji, Waziri Muhongo alieleza kwamba Serikali ya Tanzania, kupitia Wizara yake, inabadilisha utaratibu wa kupokea wawekezaji katika sekta husika.

Alisema, kunaandaliwa utaratibu maalum utakaokuwa wa wazi na kuruhusu ushindani kwa wenye nia ya kuwekeza kwa malengo ya kupunguza au kuondoa kabisa mazingira ya rushwa na muda mrefu unaotumika katika majadiliano pasipo sababu za msingi.

Profesa Muhongo alifafanua zaidi kwamba, Serikali itaweka mazingira mazuri zaidi ya ushindani kwa kuandaa maelezo ambayo pamoja na mambo mengine yatabainisha aina mbalimbali za vyanzo vya umeme vilivyopo nchini pamoja na maeneo vilipo.

Alisema, Kampuni zenye nia ya kuwekeza zitakaribishwa kupendekeza viwango vya bei vitakavyotumika kuuza umeme utakaozalishwa na zitashindanishwa, ambapo washindi wachache watachaguliwa kwa ajili ya majadiliano kabla ya kuingia mkataba wa uwekezaji husika.
“Kwa hivyo, tunaandaa kabrasha maalum litakalokuwa na maelezo husika na litakuwa tayari mwezi wa Septemba mwaka huu. Kabrasha hilo lenye maelezo litatumika kama mwongozo wa ushindanishaji maombi mbalimbali ya uwekezaji hususan katika kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali kwa uwazi,” alisisitiza.
Alivitaja vyanzo hivyo kuwa ni pamoja na gesi asilia, makaa ya mawe, maji, jua, upepo, jotoardhi, mawimbi ya bahari pamoja na nishati mbadala. Waziri Muhongo alisema kuwa maelezo hayo maalum yatasambazwa kwa wadau mbalimbali wa sekta husika wakiwemo wale wote wenye nia ya kuwekeza ikiwa ni pamoja nan chi ya Brazil kupitia Ubalozi wake hapa nchini.
“Kwa kutumia Kabrasha hilo maalum lenye maelezo husika, wewe Balozi utaweza kuwashawishi wafanyabiashara kutoka nchini kwako kutoa mapendekezo ya uwekezaji ambayo yana vigezo vyote muhimu vinavyoshawishi wapate fursa husika za uwekezaji katika sekta ya nishati,” Profesa Muhongo alimweleza Balozi Puente.
Kuhusu Mradi mkubwa wa ujenzi wa Bomba la kusafirisha mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania, ambao pia Brazil imeonesha nia kuwa ingependa kuwekeza kwa kushirikiana na Tanzania; Profesa Muhongo alisema Serikali itaweza kulisemea hilo baada ya kipindi cha miezi takribani 45 kupita, ambapo mambo yote ya kisheria kuhusu Mradi huo yanatarajiwa kuwa yamekamilika.

Aidha, Profesa Muhongo alitumia fursa hiyo kuomba nafasi za masomo nchini Brazil kwa wanafunzi wa kitanzania katika ngazi za Shahada za Uzamili na Uzamivu katika sekta ya Nishati hususan Mafuta na Gesi, kwa kuzingatia kuwa Brazil imeendelea sana katika sekta hiyo.
“Ninyi mnazo Taasisi bora kabisa za Utafiti duniani. Mnafanya vizuri sana katika maeneo mbalimbali.”
Kwa mujibu wa Profesa Muhongo, Brazil ni miongoni mwa nchi Tano (5) bora duniani zinazozalisha umeme kwa kutumia nishati jadidifu kwa sababu umeme mwingi wanaozalisha unatokana na maji, kutoka katika Mito mikubwa waliyonayo.


Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Carlos Alfonso Puente (Kushoto), akisaini Kitabu cha Wageni ofisini kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kulia), alipomtembelea Waziri na kufanya naye mazungumzo kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili hususan katika uwekezaji kwenye sekta ya nishati.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kushoto), akimsikiliza kwa makini Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Carlos Alfonso Puente (kulia), wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kufanya mazungumzo naye kuhusu masuala ya uwekezaji katika sekta za nishati na madini. Wengine pichani ni Maafisa wa Wizara waliohudhuria mkutano huo.

BAVICHA Waunga Mkono Oparesheni UKUTA........Wasema Maandalizi Yote Yamekamilika, Wasisitiza Kutorudi Nyuma Septemba Mosi

$
0
0

BARAZA la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), limetangaza kuunga mkono operesheni ya Umoja wa Kupambana na Udikteta (Ukuta) iliyotangazwa hivi karibuni na Kamati Kuu ya chama hicho.

Aidha, Bavicha wamemjibu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kwamba hana mamlaka ya kuzuia operesheni hiyo kwa kuwa wanaifanya kisheria na yeye siyo msajili wa vyama vya siasa.

Makonda aliagiza Jeshi la Polisi kuzuia maandamano ya Ukuta, Ijumaa wakati akizungumza na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) katika kambi ya Ukonga.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi, alisema maandalizi ya kuunga mkono operesheni hiyo yamekamilika kwa nchi nzima.

“Kauli ya Mkuu wa Mkoa (wa Dar es Salaam) ya kusema kwamba polisi wahakikishe Ukuta haujengeki, haitekelezeki kwa sababu yeye hana mamlaka ya kufanya hivyo na wala si msajili wa vyama vya siasa hadi atoe kauli hiyo,” alisema Katambi.

“Zipo kesi nyingi zinazoonyesha wakuu wa mikoa kufanya kazi ambazo haziwahusu, hivyo kauli yake tutaipima kisheria,” alisema na kuongeza:

“Yeye akitaka aendelee kusema chochote akijisikia, lakini sisi tunamwambia kwamba mikutano yetu iko pale pale na tutaifanya nchi nzima.”

Katika mazungumzo yake na FFU, Makonda alisema askari wanafahamu sheria, hivyo wasisubiri mtu yeyote kuja kuwakumbusha juu ya jambo hilo.

Aidha, aliwataka polisi hao kutosubiri maelekezo mengine kwa kuwa Amiri Jeshi Mkuu ambaye ni Rais John Magufuli ameshaagiza kutofanyika kwa maandamano ya Ukuta yaliyopangwa kuwa Septemba mosi.

Makonda aliliagiza jeshi hilo kuhakikisha kwamba sheria zinafuatwa na kusiwapo kitu kinaitwa Ukuta ili wananchi waendelee na kazi zao kama kawaida.

Lakini Mwenyekiti wa Bavicha jana alisema: “Tunamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu, ajiandae kutuma jeshi lake kulinda mikutano yetu.”

Kuhusu onyo la Rais Magufuli aliloitoa akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Singida kwamba Chadema isimjaribu kwa Ukuta, Katambi alisema chama hicho hakimjaribu.

Alisema Chadema itafanya maandamano nchi nzima kwa sababu kwa njia hiyo wanamsaidia kutoa mawazo yao kama vyama vya siasa kwa ajili ya kumsaidia kuendesha shughuli zake vizuri zaidi.

“Hatuna shida ya kumjaribu Rais, na wala si kwamba tunamchukia, na wala hatuna sababu ya kupinga uwapo wake, na hata ukiulizwa sasa kwamba Rais wako ni nani, lazima useme ni John Magufuli,” alisema Katambi.

“Tunapotoa dosari na kasoro tunamsaidia kuendesha nchi yake na watu walio chini yake.”

“Sisi kama vyama vya siasa tuna haki, tunajua yeye ndiye Rais, kama sisi hatukuweza kupata nafasi ya hiyo, haimaanishi kwamba ni vita, isipokuwa kupitia vyama vyetu, tuna sehemu ya kutoa mawazo yetu katika kuifanikishia serikali yake kuongoza vema pamoja na watu wake wa chini tena kwa mujibu wa sheria na inamsaidia yeye kuwa bora zaidi.
“Kwa hiyo kauli ya Rais sisi hatuna tatizo nayo.”

Katambi alisema taratibu zote za kisheria katika kutekeleza mikutano hiyo zitafuatwa.

Kamati Kuu ya chama hicho ilisema lengo la operesheni hiyo ni kuzuia matukio ya ukandamizaji wa haki na demokrasia nchini.


Mwigulu Nchemba 'Atangaza Vita' Kwa Wauza Madawa ya Kulevya Nchini

$
0
0
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametoa siku 14 kwa maofisa wanaohusika na udhibiti wa dawa za kulevya kwenye mpaka wa Tunduma mkoa wa Songwe, kuwakamata watu wanaohusika na uvushaji wa dawa hizo kutoka nchini kwenda nchi jirani ya Zambia na nyingine zilizopo ukanda huo.

Nchemba alitoa agizo hilo jana, alipofanya ziara ya kukagua mpaka huo, ambapo alisema ni jambo lisilofichika kuwa kwa sasa Tanzania imechafuka kutokana na dawa za kulevya.

Alisema kutokana na Watanzania wengi kukamatwa katika nchi mbalimbali duniani, wakijihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya, imefikia hatua kwa baadhi ya nchi kufikiria kuongeza masharti zaidi kwa kila atakayejitambulisha kuwa Mtanzania.

“Hatuwezi kuacha nchi ikachafuka kwa sababu tu ya watu wachache.Ukienda China Watanzania zaidi ya 200 wanashikiliwa kwa dawa za kulevya, Pakistan wapo, India, Afrika Kusini ni Watanzania. Hili linatuchafua sana,” alisema Nchemba.

Aliutaja mpaka wa Tunduma kuwa miongoni mwa maeneo yanayoongoza kwa kupitisha dawa hizo na kutaka nguvu kuongezwa zaidi ili kuwezesha misako.

Alisema wapo watu ambao si makondakta wa mabasi wala abiria, lakini wamekuwa wakisafiri kila siku kwenye mabasi, hatua inayodhihirisha kuwa ndiyo wanaojihusisha na usafirishaji wa bidhaa hizo haramu.

Alisema watu hao wamekuwa na ushirikiano na watu wengine katika miji ya jirani, kabla ya kufika mpakani ikiwemo kijiji cha Mpemba wilayani Momba mkoani Songwe, ambapo wakifika hapo basi husimamishwa na mzigo kushushwa, kisha kusafirishwa kwa njia za panya hadi ng’ambo ya nchi.

“Wakati ninyi mnafanya utaratibu wa kawaida wa kupitisha gari husika hapa mpakani, wao wanavusha kupitia njia za panya. Basi likishavuka na mzigo unakuwa umefika Zambia wanakutana na kuupakia tena kisha wanaendelea na safari. 

“Na katika hili ni lazima mzungumze pia na wenzenu wa upande wa pili, wadhibiti pia mji unaofuata baada ya huo wa mpakani maana huko ndiko wanakopakia tena. Kama mtashindwa katika wiki mbili, nitakuja mimi mwenyewe na nitawakamata tu,” alisisitiza.

Kiwanja Cha Ndege Dodoma Kukamilika Mwishoni Mwa Agosti

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa vitendo wakati alipokagua maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma.

Imeelezwa kuwa upanuzi na ukarabati wa kiwanja cha ndege  cha Dodoma utakamilika mwishoni mwa mwezi Agosti ili kuruhusu ndege za abiria sabini mpaka tisini kuweza kutua na kuruka na hivyo kurahisisha usafiri wa anga kwa ukanda wa kati.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa baada ya  kutembelea  kiwanjani hapo kukagua hatua ya mwisho ya ujenzi iliyofikiwa ambapo amesema kasi ya Mkandarasi Chicco anayetekeleza kazi hiyo inaridhisha katika kuhakikisha kiwanja hicho kinakamilika kwa muda na kwa viwango vilivyokubalika.

Amesema mpaka sasa ni asilimia themanini ya kazi iliyotekelezwa kwa siku arobaini na tano tangia kuanza ukarabati hivyo kasi iliyotumika kwenye kiwanja hiki itatumika kwenye ujenzi wa viwanja vingine nchini.

"Tunaamini kabisa kwa kasi ya mkandarasi na msimamizi mtakamilisha ujenzi huu haraka na viwango tulivyokubaliana katika mkataba ili ndege kubwa zianze kutua na kuruka" amesema Prof. Mbarawa.

Naye Msimamizi wa ujenzi wa kiwanja hicho kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Eng. Mhandisi Mbila Mdemu amesema kazi ya ukarabati na upanuzi inaendelea kufanywa usiku na mchana kwa kuzingatia ubora na viwango na kukamilika kwa wakati

"Tulipewa kazi hii na tunaahidi kuwa  itakamilika kama tulivyoelekezwa ili kuwapa wananchi wanaozunguka mikoa ya Dodoma na jirani fursa ya kutumia usafiri wa Anga", amesema Eng. Mdemu.

Ameongeza kuwa kazi zinazokamilishwa sasa ni kumalizia sehemu ya maegesho ya ndege na tabaka la mwisho kwenye barabara  ya kuruka na kutua ndege.

Mradi wa upanuzi na ukarabati wa kiwanja cha  ndege cha Dodoma umegharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa zaidi ya shilingi bilioni 11.8 na kukamilika kwake kutaongeza idadi ya safari za ndege zitakazosafirisha abiria wa mikoa ya kanda ya kati.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipokea taarifa ya maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma kutoka kwa Eng. Guo Zhingjian wa kampuni ya Chicco inayojenga kiwanja hicho, Mkoani Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa kutoka Eng. Guo Zhingjian wa kampuni ya Chicco inayojenga kiwanja hicho Mkoani Dodoma.

Waziri Mkuu Aitaka Tra Kuacha Tabia Ya Kuwapandishia Wafanyabiashara Kodi Kiholela

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania kuimarisha kitengo cha tathmini ili kuweka viwango halali ambavyo havitawagandamiza wafanyabiashara na uwepo uwazi kuhusu viwango stahili vya kodi wanavyotakiwa kulipa.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana jioni (Jumapili, Agosti 07, 2016) wakati alipozungumza na viongozi wa mikoa ya Mbeya, Katavi, Songwe, Rukwa, Ruvuma, Iringa na Njombe mara baada ya kuwasili mkoani Mbeya kwa ajili ya kufunga maadhimisho ya maonyesho ya nane nane kwa mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yanayofanyika mkoani Mbeya.

‘‘TRA waendelee kukusanya mapato vizuri ila kuna wakusanya kodi wanaotaka kuharibu mkakati wa Serikali kwa kufanya mambo ya hovyo kwa kuwaongezea viwango vikubwa vya kodi kuliko kodi stahili wanavyotakiwa kulipa na kufanya suala hili liwe kama tatizo au adhabu kwao jambo ambalo si sahihi. Naagiza watendaji wa TRA wanaofanya hivyo wasakwe na wachukuliwe hatua“, alisema.
 
‘‘Wafanyabiashara mnaoonewa kwa chuki binafsi na watendaji wa TRA toeni taarifa ili muweze kufanya biashara zenu kwa uhakika bila ya wasiwasi lengo ni kuwafanya muweze kulipa kodi sahihi kwa mujibu wa sheria“, alisema.

Ili kufanikisha mpango huo Waziri Mkuu amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kuwasikiliza wafanyabiashara ambao wana malalamiko ya kweli ya kutotendewa haki katika kutozwa kodi kwa sababu mchango kupitia kodi ni kwa ajili ya kuendeleza uchumi wa Taifa.

Katika hatua nyingine ameitaka idara ya Uhamiaji ijikite katika kudhibiti watumishi wasiokuwa waaminifu ambao wamekuwa  wakichukua rushwa kutoka kwa wageni wanaotoka nje ya nchi na kuwaingiza nchini bila ya kuwa na vibali maalumu.

‘‘Ni lazima tuhakikishe hakuna uingiaji holela ndani ya nchi na hasa kwa  wanaoingia bila vibali maalumu kwani bila ya kudhibiti suala hilo tunaacha mianya ya kuingia watu wasiokuwa na nia njema na Taifa letu. Watu watakaobainika wameingia nchini bila ya vibali wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria,“ alisema.

Alisema kitendo cha mipaka kushindwa kudhibitiwa na kuruhusu uingiaji holela wa watu wasiokuwa na vibali chini kunasababisha Serikali kushindwa kuteleza ipasavyo mipango yake ya kuwahudumia wananchi kulingana na idadi halisi.

Mbali na kuiagiza Idara ya Uhamiaji pia Waziri Mkuu alisema wakuu wa mikoa ya mipakani wana jukumu la ziada la kuhakikisha wanadhibiti mipaka yote na kuhakikisha hakuna watu wanaoingia nchini bila ya kuwa na vibali.

Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka wakuu wa mikoa kote nchini kuendelea kuimarisha hali ya ulinzi na usalama katika maeneo yao na kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani na utulivu ili Watanzania waweze kutekeleza shughuli zao za maendeleo kama walivyojipangia.

“Natambua kuwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ndio wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama katika maeneo yenu, endeleeni kuimarisha hali ya ulinzi na usalama. Nchi hii tunahitaji  iwe tulivu na salama na ni wajibu wenu kuhakikisha kwamba lolote linalotokea mnalikabili vilivyo“, alisema.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Makalla alipokuwa akisoma taarifa ya mkoa huo kwa Waziri Mkuu alisema mkoa huo una jumla ya viwanda 1,653 kati yake vikubwa ni tisa, vya kati 19 na vidogo 1,625  na bado wanaendelea kuzisimamia halmashauri kutenga maeneo zaidi kwa ajili ya kuongeza na kupanua viwanda.

Mhe. Makalla alisema katika eneo hilo la viwanda mkoa una kiwanda kimoja cha kusindika nyama cha Tanganyika Pachers kilichopo wilayani Mbeya ambacho hakijawahi kufanya kazi tangu kilipojengwa na kufungwa mitambo mwaka 1975.

Mkuu huyo wa mkoa alisema usimamizi wa kiwanda hicho uko chini ya Masajili wa Hazina na kwamba tayari kuna muwekezaji amepatikana kwa ajili ya kukiendesha hivyo ameiomba Serikali kuharakisha taratibu za mikataba ili kiweze kuanza kufanya kazi.

Mwenge Wazua Balaa Jijini Mwanza.......Mkurugenzi Atishia Kuitisha Daftari la Mahudhurio saa tisa Usiku, Walimu Watakiwa Kukesha Wakiushangilia

$
0
0

Mbio za Mwenge wa Uhuru zimetua Kanda ya ziwa huku zikizua sintofahamu kwa watumishi wa umma waliotakiwa kutokukosa mkesha wake ili kukwepa rungu la Mamlaka za kinidhamu dhidi yao.

Taarifa kutoka wilayani Sengerema zilieleza kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ameagiza watumishi wote wa wilaya hiyo kuhakikisha wanahudhuria mkesha huo na kwamba daftari la mahudhurio litaitishwa majira ya saa 6 usiku, saa 9 usiku na saaa 12 usiku.

Hayo yamebainishwa katika Tangazo rasmi lililosainiwa na Msangi M.A kwa niaba ya Mkurugenzi, Magessa Boniface.

Aidha, katika Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, imeelezwa kuwa walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari waliitwa katika kikao na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mary Tesha ambaye aliwaeleza kuwa ambaye hatahudhuria mkesha huo atakumbwa na adhabu ikiwa ni pamoja na kushushwa vyeo.

Hata hivyo, Mkuu huyo wa Wilaya alipotafutwa, alikana kuwaeleza walimu hao kuwa wangeshushwa vyeo kama wasingehudhuria ingawa alikiri kuwa alikutana nao.

“Sijasema hayo, nilichosema ni kuwa Mwenge ni jukumu letu watumishi tunapaswa kushiriki. Hao walimu ni wajumbe wa Kamati za Mbio za Mwenge hivyo wanapaswa kushiriki. Hilo la kufukuza, kuwawajibisha hapana,” alisema Tesha.

Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Nyamagana, Asha Juma alisema kuwa ingawa amesikia kuwepo kwa maagizo hayo, hajapata malalamiko kutoka kwa walimu.

“Najuwa wanahamasisha watumishi waende, lakini nadhani wangetafuta njia nyingine ya kuwahamasisha sio vitisho,” alisema Katibu huyo wa CWT.

Serikali Awamu Ya Tano Imedhamiria Kupambana Na Vitendo Vya Rushwa Na Ufisadi-makamu Wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN amewahakikishia watanzania kuwa serikali ya awamu ya TANO inadhamira ya dhati ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii kwa kuendelea kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi,kudhibiti matumizi yasiyolazima, kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa kodi ili fedha zinazokusanywa zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi.

Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN amesema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya NANE NANE kitaifa katika uwanja wa NGONGO Manispaa ya LINDI mkoani LINDI kwa naiba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JOHN POMBE MAGUFULI.

Katika hutoba yake kwa mamia ya wananchi waliofurika katika viwanja vya NGONGO, Makamu wa Rais amesema azma ya serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo itatimia iwapo tu wananchi wataunga mkono jitihada za serikali katika kulipa kodi kwa wakati,kudai risiti,kufanya kazi kwa bidii, kukemea vitendo vya rushwa kama hatua ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020.

“Napenda kuwahakikishia kuwa tuna dhamira ya dhati ya kuendelea kuwatumikia na kuwaboreshea huduma zote za kijamii pamoja na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla bila kujali mikoa mnayotoka,jinsia,dini au itikadi za vyama vyenu.”

Kuhusu uimarishaji wa shughuli za kilimo nchini, Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN amesema maadhimisho ya sikukuu ya NANE NANE ni moja katika ya juhudi za serikali za kuboresha shughuli za kiuchumi katika taifa ambapo asilimia 75 ya wananchi wanajihusisha na shughuli za kilimo,mifugo na uvuvi kote nchini.

Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuzipa kipaumbele sekta za kilimo,mifugo na uvuvi na kuongeza bajeti katika sekta hizo ili ziweze kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza pato la taifa na uchumi wa nchi kwa ujumla.

Makamu wa Rais ameeleza wananchi kuwa serikali imeweka mikakati na mipango inayolenga kusaidia uimarishaji wa shughuli za kilimo kote nchini kwa kuongeza matrekta makubwa na madogo kutoka 7,491 mwaka 2005/2006 hadi 16,478 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 hivyo kupunguza matumizi ya jembe la mkono kutoka asilimia 70 hadi asilimia 12.

Aidha amefafanua kuwa serikali imeongeza idadi ya maafisa ugani katika kilimo kutoka 3,379 mwaka 2005 hadi 2006 hadi 8,756 mwaka 2015/2016 na serikali pia imefufua mashamba ya mbegu kwa kuhusisha sekta binafsi, Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa katika kuzalisha mbegu bora za mazao ya chakula nchini.

Kwa Upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dakta PHILIP MPANGO amehimiza wananchi kote nchini kulipa kodi ipasavyo ili fedha zitakazopatikana zipelekwe kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami huku Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiwataka wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara waongeze uzalishaji wa mazao ya biashara ambayo watauza ndani na nje ya nchi katika hatua ya kukuza pato la familia na taifa kwa ujumla.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
8-Aug-16
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images