Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Maelekezo ya Zitto Kabwe Kwa Wanachama wa ACT- Wazalendo Kuhusu Kauli ya Rais Magufuli Jana Singida

$
0
0

Maelekezo ya Kiongozi wa Chama ( KC ) kwa wanachama wote wa ACT Wazalendo ( KC/01/2016 ).

Tangu kukamilika kwa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 Utawala mpya umekuwa ukifanya kila juhudi kuminya uwezo wa Vyama vya Siasa kufanya Kazi zake kwa kisingizio kuwa huu ni wakati wa kufanya Kazi na kwamba Siasa zisubiri mwaka 2020. 

Chama chetu kilipinga kwa nguvu zote uzuiaji huu wa shughuli za kisiasa kwani ni kinyume cha Katiba ya Nchi na Sheria ya Vyama vya Siasa, sheria namba 5 ya mwaka 1992 kama ilivyofanyiwa marekebisho Mara kwa Mara.

Mnamo tarehe 5 Juni 2016 Chama chetu kilifanya Mkutano wa Hadhara Mbagala jijini Dar Es Salaam na kutangaza Operesheni Linda Demokrasia. Lengo la Operesheni hiyo ( Tamko la Mbagala 2016 ) ni kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kuwa Nchi ya kidemokrasia na kuepuka mwelekeo wa Utawala wa Imla ambao ni utawala wa kidikteta. Chama chetu asili ya uundwaji wake ni kupinga tabia za kidikteta tulizokumbana nazo ndani ya Vyama tulivyokuwamo. 

Hivyo ilibidi tuwe mstari wa mbele kupinga dalili zozote za kuielekeza Nchi kwenye Uimla. Vyama unaweza kuunda utakapo, Nchi huwezi kuiunda ndio maana ni LAZIMA Sisi Kama wanachama wa Chama cha Wazalendo kupinga kwa nguvu zote kuminywa kwa Demokrasia na kuilinda kwa nguvu zetu zote.

Kufuatia Tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano kwamba shughuli za kisiasa zimezuiwa kwa niaba yenu nilitaka Vyama vyote vya Siasa nchini na wadau wengine wa demokrasia kuungana kwa pamoja kukataa Tamko hili ambalo linavunja Katiba ya Nchi ambayo Rais ameapa kuilinda na kuitetea. Wito wetu unanukuliwa hapa chini;

"Tunatoa wito kwa Vyama vyote vya siasa nchini kuunganisha nguvu katika kuhakikisha tunapigana vita [ dhidi ya udikteta] pamoja. Huu ni wakati wa vyama vya siasa na wanasiasa kuacha tofauti zao na kupambana kulinda uhuru wa kufanya siasa wakati wowote kwa mujibu wa Sheria."

Hata hivyo, hakuna Kiongozi wa Chama chochote kile ambaye aliona umuhimu wa kuunganisha nguvu na hivyo kujikuta kila Chama kinaendelea na operesheni zake. 

Viongozi wetu akiwemo Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu walifanya juhudi zote kuwasiliana na watendaji wenzao wa Vyama vingine ili kufanya Kazi pamoja japo kwa uratibu lakini hatukupiga hatua yeyote ile.

Hivyo, Sisi sio sehemu ya operesheni yeyote ile iliyotangazwa na Chama kingine chochote kile isipokuwa Operesheni Linda Demokrasia ambayo sasa itaitwa Tamko la Mbagala la Juni 5, 2016.

Akiwa ziarani mkoani Singida, Rais amefafanua agizo lake la kuzuia mikutano ya kisiasa. Rais amesema kwamba hajazuia wabunge na madiwani kufanya mikutano ' KWENYE MAJIMBO YAO'. Kwanza Rais hana mamlaka ya kuruhusu au kuzuia Kazi za Wabunge na madiwani. Haya ni mamlaka ya KATIBA na sheria za Nchi. Hivyo ufafanuzi wake hauna maana yeyote ile.

Jambo la kushtusha ni agizo la Rais kwamba Wabunge hawana mamlaka ya kufanya mikutano nje ya majimbo yao. Hii ina maana hata Viongozi wa kisiasa ambao sio wabunge hawataruhusiwa kufanya mikutano ya kisiasa. Hii HAIKUBALIKI. 

Anna Elisha Mghwira ni Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Taifa, anazuiwaje kufanya mikutano na wanachama wake nchini? Anazuiwaje kuongeza wanachama? Lakini mama Anna Mghwira aligombea Urais, kwanini asifanye mikutano kuwashukuru waliompa Kura japo hazikutosha?

Uchambuzi wa kitaalamu
Ni dhahiri Serikali ya Awamu ya Tano na sasa Chama tawala wameamua kubadili mwelekeo wa Nchi kisiasa ( kwa kubana uhuru wa kidemokrasia ) na kiuchumi ( kwa kuelekeza nguvu kwenye uchumi unaoelekezwa/endeshwa na dola ). Udhibiti wa Vyama vya Siasa ni moja ya hatua ya udhibiti wa jamii kwa ujumla wake. 

Siku za usoni tutaona udhibiti wa waziwazi wa vyombo vya habari na kwa sasa tunaona namna Asasi za Kiraia ( CSOs) zilivyo kimya tofauti na miaka michache ya nyuma. Hizi zimejiweka kimya zenyewe na zitakazoinua sauti zitafuatiliwa na dola. Yote haya yanaturudisha nyuma katika katika kujenga Tanzania ya Kidemokrasia na yenye Maendeleo.

Utawala wowote ' regime ' hutaka kupata nguvu ya wananchi katika kujijengea uhalali. Serikali ya Awamu ya Tano imeamua kuichukua vita dhidi ya ufisadi kama njia ya kujijengea uhalali na kwa kweli wananchi wengi waliochukizwa na vitendo vya kifisadi wanaunga mkono juhudi hizo. 

Katika ziara yake ya Singida, Rais amenza kutumia maneno kama ' mabeberu ' na ' Maadili ya Mwalimu Nyerere ' maneno ambayo hayajawahi kutamkwa na kinywa chake. Hii inaonyesha kuwa Rais anaanza kukua/kukuzwa kiitikadi na hii itampa uhalali zaidi mbele ya jamii. 

Hata Uamuzi wake wa kutekeleza maamuzi ya kuhamia Dodoma, na iwapo atatekeleza, itamjengea zaidi uhalali. Rais atautumia uhalali huu kujikita katika utawala na kuminya zaidi Demokrasia.

Maelekezo ya Kiongozi wa Chama ( KC )
1. Chama cha ACT Wazalendo kiliundwa kwa madhumuni ya kurejesha Nchi kwenye misingi. Kupitia Azimio la Tabora linalohuisha Azimio la Arusha tumeeleza misingi hiyo kwa kina. Naelekeza kwamba wanachama wote wa ACT Wazalendo wasome, kuelewa na kujadili Azimio la Tabora na kuchambua muktadha wake katika mazingira ya sasa ya Siasa za Nchi yetu.
 
2. Kila Mwanachama wa ACT Wazalendo asione aibu kuunga mkono maamuzi yeyote ya Serikali au Chama kingine cha Siasa yanayoendana na Azimio la Tabora hususan vita dhidi ya ufisadi na kurejeshwa kwa Miiko ya Uongozi.
 
3. Kila Mwanachama wa ACT Wazalendo akatae kwa namna anayoweza lakini kwa Amani mbinu zozote za kuminya Demokrasia nchini. Tamko la Mbagala la kulinda Demokrasia litumike kuongoza juhudi hizo. Chama chetu hakijatangaza maandamano na hivyo wanachama wetu wasiingie katika mambo hayo. 

Hata hivyo kila mwanachama wa Chama chetu aandike barua kwa Rais Magufuli kwa namna anavyoona yeye kumtaka aache kuingiza Nchi kwenye utawala wa Imla. Chama chetu kina wanachama 431,120 wenye kadi. Ikulu ikipata barua 200,000 kutoka kila kona ya Nchi itafunguka macho.

Mwisho
Nawataka wanachama wa Chama Cha ACT Wazalendo kukumbuka kuwa uasili wa Chama chetu ni kupinga kuburuzwa, ufisadi na Siasa za ujanja ujanja. Tujitahidi kwa nguvu zetu zote kutofanya yale ambayo Sisi tumeyakataa.

Viongozi wa kuchaguliwa kwenye vyombo vya uwakilishi Kama madiwani na wabunge wawe makini sana kutii Chama na misingi ya chama. 

Tuwe mstari wa mbele kupinga ufisadi kwani rushwa ni adui wa Haki. Tuwe mstari wa mbele kutaka kurejeshwa kwa Miiko ya Uongozi. Sisi ndio Chama pekee chenye itikadi iliyo wazi. Tusiammie itikadi yetu popote tulipo na bila woga wala aibu.

Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mb
Kiongozi wa Chama
30/7/2016

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi siku 23 tangu amteue

Taarifa Ya Bunge Kwa Umma Kuhusu Kamati Za Bunge

Taarifa kutoka Ikulu Kuhusu Ziara ya Rais Magufuli mkoani Tabora.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 30 Julai, 2016 ameendelea na ziara yake katika Mkoa wa Tabora akitokea Mkoa wa Singida.

Kabla ya kuingia  Mkoani Tabora, Rais Magufuli amezungumza na wananchi wa Mji wa Misigiri katika Wilaya ya Iramba ambapo amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara katika Mkoa wa Singida kuhakikisha mkandarasi anayejenga daraja la Sibiti anarejea kazini mara moja kukamilisha ujenzi wa daraja hilo.

Rais Magufuli amesema serikali yake imejipanga kumlipa fedha mkandarasi huyo na hivyo hakuna sababu ya kuendelea kusimamisha ujenzi huo.

Mkoani Tabora, Rais Magufuli amezungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake katika vijiji vya Nanga na Ziba na amefanya mikutano ya hadhara katika miji ya Igunga na Nzega ambako amewahakikishia wananchi kuwa serikali yake itahakikisha inatekeleza ahadi zilizopo katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2015.

Katika mkutano wa hadhara uliofanyika Igunga, Rais Magufuli amepokea malalamiko ya wananchi kuhusu kutoanza kutumika kwa kituo cha mabasi na soko na amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Tabora kuhakikisha kituo cha mabasi cha Igunga na soko la Igunga vinaanza kutumika kuanzia Jumatatu ijayo ya tarehe 01 Agosti, 2016.

Kuhusu kero ya maji, Dkt. Magufuli amesema Tanzania imepata mkopo wa dola za kimarekani Milioni 268.35 kutoka nchini India ambazo zitatumika kutekeleza mradi wa kusambaza maji ya ziwa Viktoria katika Miji ya Tabora, Igunga, Nzega, Sikonge  na Uyui pamoja na vijiji vilivyopo kandokando mwa bomba kuu kuanzia mwaka huu ambapo watu milioni moja na laki moja (1,100,000) watanufaika.

Dkt. Magufuli ameongeza kuwa pamoja na juhudi hizo Serikali imefanya usanifu na upembuzi yakinifu kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kusambaza maji ya kutoka mto Malagarasi kwa ajili ya Miji ya Urambo, Kaliua na Nguruka pamoja na vijiji vilivyopo kandokando mwa bomba kuu ambako watu laki sita (600,000) watanufaika.

Aidha, Rais Magufuli amepiga marufuku wakulima wadogo kutozwa ushuru wa mazao watokapo na mazao mashambani.

“Ninapenda tukusanye kodi, lakini sio kukusanya kodi kutoka kwa watu masikini, mtu ametoka shambani na magunia yake mawili au hata matano halafu nyinyi mnamtoza kodi.

“Mimi sipendi kuwanyanyasa hawa watu wanyonge, mtu akiwa na mazao lori zima hapo sawa lakini sio kwa mtu mnyonge mwenye gunia moja” Amesema Rais Magufuli.

Kuhusu maombi ya Mkoa wa Tabora kutaka kuanzishwa Mkoa mwingine kutokana na ukubwa wa baadhi ya Wilaya Rais Magufuli amesema haoni umuhimu wa kuanzisha Mikoa mipya hapa nchini kwa sasa, na badala yake fedha zitaelekezwa katika huduma kwa wananchi kama vile maji, barabara, miundombinu na huduma za afya.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Nzega

30 Julai, 2016

Mbowe asakwa na polisi, hiki ndicho alichoandika

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya July 31

Picha 9: Rais Magufuli alivyoendelea na ziara yake Igunga na Nzega Tabora

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana July 30 2016 ameendelea na ziara yake katika Mkoa wa Tabora akitokea Mkoa wa Singida.

Mkoani Tabora, Rais Magufuli alizungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake katika vijiji vya Nanga na Ziba na alifanya mikutano ya hadhara Igunga na Nzega ambako amewahakikishia wananchi kuwa serikali yake itahakikisha inatekeleza ahadi zilizopo katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2015.

Katika mkutano wa hadhara uliofanyika Igunga, Rais Magufuli amepokea malalamiko ya wananchi kuhusu kutoanza kutumika kwa kituo cha mabasi na soko na amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Tabora kuhakikisha kituo cha mabasi cha Igunga na soko la Igunga vinaanza kutumika kuanzia Jumatatu ijayo ya tarehe 01 Agosti, 2016.

Kuhusu kero ya maji, Dkt. Magufuli alisema Tanzania imepata mkopo wa dola za kimarekani Milioni 268.35 kutoka nchini India ambazo zitatumika kutekeleza mradi wa kusambaza maji ya ziwa Viktoria katika Miji ya Tabora, Igunga, Nzega, Sikonge
Rais Magufuli  na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nanga Wilaya ya Igunga Masesa Kishiwa Makala kutoka Chadema wakati akiwa safarini kuelekea Nzega Mkoani Tabora.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na wabunge wa Singida
Rais Magufuli katika Kijiji cha Nanga Wilayani Igunga mkoani Tabora.





Mahafali ya KKKT Chuo Kikuu Muhimbili Yapigwa Marufuku Baada ya Wanafunzi Hao Kumwalika Lowassa Kuwa Mgeni Rasmi

$
0
0

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) umezuia mahafali ya wanafunzi  waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT ) yaliyokuwa yamepangwa kufanyika jana mchana chuoni hapo jijini Dar es Salaam, ambapo Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alikuwa amealikwa na wanafunzi kama mgeni rasmi.

Mahafali hayo yalizuiwa jana saa 6 mchana ikiwa ni saa mbili kabla ya muda kuanza

Tangazo lililobandikwa chuoni hapo na kushuhudiwa na wanahabari likiwa linamnukuu Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Apollinary Kamuhabwa liliwataka wanafunzi hao kutoweka mikusanyiko ya aina yoyote chuoni hapo.

Profesa Kamuhabwa kupitia tangazo hilo aliwaonya wanafunzi hao kutojihusisha na masuala ya siasa wawapo chuoni kama ilivyo kwa watumishi wa umma.

Jitihada za waandishi wa habari kuzungumza na uongozi wa chuo hicho ili kupata ufafanuzi ziligonga mwamba baada ya kuelezwa kuwa hawakualika mkutano na waandishi wa habari.

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 22 & 23

$
0
0
MTUNZI: ENEA FAIDY

.....MR ALLOYCE alishtuka sana baada ya kusikia kishindo kalikali nyuma yake. Aliachia chupa ya konyagi kisha akageuka haraka kutazama nini kinaendelea nyuma yake. Hakuamini kumuona mwanaye akiwa amejibwaga chini kama gunia la viazi. Alikuwa anathema kupita maelezo.

"Eddy!" Mr Aloyce aliita kwa mshangao mkubwa. Lakini Eddy hakuitikia zaidi ya kuendelea kuhema kwa nguvu.Mr Alloyce alitupa chini vidonge alivyokuwa amevishika, akamwinamia Mwanaye na kumgusa kifuani ili kusikiliza mapigo ya moyo. Aligundua kuwa mwanaye ni mzima alimsgukuru Mungu. Killed home hang a za Mr Alloyce ni kwamba pindi anarudi sebuleni pale, hakukuta mtu yeyote na wala hakusikia mtu akifungua mlango.

"Ba...ba..!" Aliita Eddy kwa shida sana.
"Sema mwanangu...Mimi hapa" aliitikia Mr Aloyce.
"Usife. .!"
"Sifi nani kasema Mimi nakufa? Vipi lakini uko sawa?" Aliuliza mr Alloyce akiwa na hofu sana, alihofia kumpoteza mwanaye kipenzi. Eddy aliitikia kwa kichwa tu akimhakikishia baba yake kuwa yuko sawa.

Mr Alloyce aliendelea kumkagua Mwanaye kila sehemu akidhani labda ana majeraha kwani damu alizozikuta chumbani kwa Eddy zilimtisha Sana. Lakini alipomtazama mwanaye akagundua hana jeraha lolote mwilini mwake, hivyo maswali mengi yalijitokeza akilini mwake. Alijihoji maswali mengi lakini hakuwa na majibu yake.

"Baba... Mama anateseka sana!" Eddy aliongea sauti ndogo ya kujivuta sana akiwa bado amelala pale sakafuni.
"Anateseka wapi?" Mr Alloyce alishtuka sana.
"Alikuja hapa.. Anateseka sana na yote kwa sababu yangu...!" Alisema Eddy kwa huzuni sana huku machozi yakimlengalenga machoni.
"Eddy! Upo sawa kweli?" Mr Alloyce alihisi Eddy hayupo sawa hivyo anaropoka tu anachojisikia.
"Nimefanya makosa sana.. Namtesa mama yangu..."
"Eddy usiseme hivyo.. Unamtesa na nini?"
"Alivyotaka kunipeleka kwa mganga wameamua kumuadhibu...!"
"Kina nani?"
"Wachawi...!"
"Oh My God.."

Maneno Yale yalizidi kumchanganya Mr Alloyce, alishundwa afanyaje kwani ilikuwa ni Mara yake ya kwanza maishani mwake kukumbana na mauzauza ya namna ile. Mara nyingi alizoea kutazama kwenye luninga tu lakini hakujua kama inaweza kumtokea kweli. Maisha yake yalikuwa machungu ndani ya muda mfupi tu kwanu matatizo aliyokuwanayo yalikuwa mazito tena yanaumiza kama gunia la misumari.
"Baba.. Nakupenda..!"
"Nakupenda pia mwanangu!"

Mr Aloyce alijikuta anashusha mchozi tu kila anapomtazama mwanaye kwanu siku zote aliamini mwanaye atakuwa mtu mkubwa sana kutokana na uwezo wake darasani. Alikuwa na akili nyingi lakini Leo amekuwa mtu wa kuteseka tu. Aliwachukia wanadamu wenzake kwa ukatili wanaoufanya juu ya familia yake.

"Baba.."
"Naam mwanangu.."
"Chukua hii." Eddy alimkabidhi baba yake kipande cha karatasi.Mr Aloyce alishtuka kidogo kisha akapokea karatasi like na kulikunjua ili alisome.Ujumbe uliokuwepo pale ulimshtua sana Mr Alloyce. Aliurudia tena"CHAGUA MOJA.
EDDY APONE TATIZO LAKE, MAMA YAKE APOTEE DAIMA. AU MAMA EDDY ARUDI, EDDY ABAKI NA TATIZO LAKE"

Mr Aloyce alibaki mdomo wazi kwa mshangao, kwani ule ulikuwa mtihani mgumu kwake."Karatasi limetoka wapi?" 

Mtuhumiwa wa Mauaji Jijini Mwanza Auawa akijaribu Kutoroka

$
0
0

MTUHUMIWA wa ujambazi Msafiri Suleiman maarufu kama Juma Msukuma ameuawa wakati akijaribu kuwatoroka Polisi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Julai 28 mwaka huu majira ya saa 10.30 jioni katika eneo la Igoma kata ya Igoma jijini Mwanza.

Kamanda Msangi alisema mtuhumiwa siku hiyo alikuwa amekamatwa na Polisi akituhumiwa kufanya matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha akishirikiana na wenzake watatu.

Aliwataja watu hao aliokuwa akishirikiana nao ambao kwa sasa wamekamatwa na polisi kuwa ni Jackson Magesa ( Nyakibimbi), Samwel Mwita na Boniphace Nyamhanga.

Kamanda alisema baada ya mahojiano na polisi mtuhumiwa alikiri kuhusika na uhalifu na akakubali kwenda kuwaonesha askari sehemu aliyoficha silaha maeneo ya Buhongwa mlimani.

Alisema walipofika eneo husika aliwaonesha mkasi mkubwa wa kukatia vyuma na kipande cha nondo, huku akiwathibitishia kuwa silaha alikuwa ameichimbia ardhini katika eneo hilo.

“Wakati askari wakiwa kwenye harakati za kufukua ili waichukue silaha hiyo, mtuhumiwa alitumia mwanya huo kuanza kukimbia huku akiwa na pingu mkononi, askari walifyatua hewani risasi tatu, lakini mtuhumiwa hakutii amri hiyo ndipo alipopigwa risasi mguuni na kufanikiwa kukamatwa”, alifafanua.

Alisema alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa hospitali.

“ Watuhumiwa aliokuwa akishirikiana nao tumewakamata na tumewakuta wakiwa na bunduki aina ya Rifle Mark 4 ikiwa na risasi nne, ikiwa na kitako cha bunduki waliyopora, nyundo moja na vipande vitatu vya nondo”, alisema.

“ Watuhumiwa hao tunawashikilia kwa matukio ya unyang’anyi Nyashishi, Buhongwa, Bulale, Nyambichi na Mwananchi ambapo walipora silaha toka kwa mlinzi wa Kampuni ya Paroma Patrol Security Service”, aliongeza

Chadema Kanda ya Ziwa Watangaza Maandamano hadi Nyumbani kwa Rais Magufuli ( Chato )

$
0
0

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Ziwa kimetangaza kufanya maandamano katika kanda hiyo huku wakidai kuyafungia katika mji wa Chato ambao ni nyumbani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Tamko la Chadema limetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho Kanda ya Ziwa Magharibi, Meshack Micus alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake.

“Sisi kama Chadema kanda ya Ziwa hasa kanda ya Victoria tayari tumeshawaelekeza wanachama wetu wote, viongozi wetu wote na tayari mwitikio ni mzuri. Na hadi leo tayari viongozi wetu wa vitongoji 1973 wameshajiandaa wako tayari kwa ajili ya kufanya maandamano na kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo yao,” alisema.

“Tutaandaa maandamano kutokea Kyelwa, tutaelekea Misenyo, Bukoba vijijini na tutakuja moja kwa moja mpaka Chato. Na wa Mwanza tayari nimeshawaagiza kwamba maandamano yetu tunaenda kuyafungia Chato,” aliongeza.

Tamko hilo limekuja ikiwa ni siku moja baada ya Rais John Magufuli kuwaonya Chadema kutomjaribu kwa kufanya maandamano bila kufuata utaratibu kwani hatawavumilia.

Rais Magufuli aliwataka wananchi kutokubali kudanganyika na kufanya maandamano na badala yake wajikite katika kufanya kazi itakayowaletea maendeleo.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza kile walichokiita ‘Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (UKUTA)’, akiwaalika wafuasi wake kufanya maandamano nchi nzima kuanzia Septemba Mosi mwaka huu.

Live: Mahojiano ya Edward Lowassa na Tido Mhando

Lowassa afunguka mengi Leo....Adai hakuna mwenye hati miliki Ya Nchi

$
0
0

Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowasa amemtaka Rais John Magufuli kuwa na utamaduni wa kufanya mazungumzo na wanasiasa wenzake ili kufikia muafaka wa mambo mbali mbali ya kisiasa nchini.

Lowasa ameyasema hayo leo wakati wa mahojiano na Tido Mhando kupitia kipindi cha Funguka kinachorushwa na Televisheni  ya Azam. Lowasa amesema kuwa siasa ni mazungumzo na siyo kutoa tu amri kama anavyofanya Rais Magufuli.

Kadhalika Lowassa amesema kila mtu ana wajibu wa kuheshimu amani ya nchi na hakuna mtu mwenye hati miliki ya nchi hii.

“Serikali haipaswi kuwa na ghadhabu, inapaswa kuwa na tabia ya kuzungumza. Sisi sote ni Watanzania kwa nini tunaogopa kuzungumza. Mazungumzo ndiyo njia bora ya kufikia maridhiano. Pia Rais Magufuli aitazame Zanzibar, tunasikia watu wanashughulikiwa kwa njia mbalimbali, wanakamatwa, hivyo hawezi kuikwepa Zanzibar kwani hilo ni suala lake.” alisema Lowassa.

Amesema CHADEMA ipo sahihi kutangaza operesheni ‘Ukuta’ hapo Septemba 1, mwaka huu na kwamba bado kuna nafasi ya kufanya mazungumzo kabla ya tarehe hiyo kufika ili kuepusha hali ya migogoro itakayojitokeza siku hiyo itakapofika.

Akizungumzia barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa kukemea operesheni hiyo, amesema barua hiyo imejaa ghadhabu zaidi kuliko kuongelea mambo ya msingi ambayo vyama vya upinzani vimekuwa vikionewa.

Akiongelea suala la wabunge wa upinzani kutoka na kususia bunge, Lowassa amesema hali hiyo ilisababishwa na kutokuwepo kwa Spika Job Ndugai ambaye kwa muda mrefu alikuwa nje ya nchi akiendelea na matibabu.

“Ndugai angekuwepo haya yote yasingetokea kwakuwa ni mtu makini sana na hata kwa Naibu Spika kuna tatizo la Kisaikolojia kwasababu aliingia bungeni kwa njia zisizoeleweka na hivyo kumfanya kushindwa kuhimili kiti vizuri,” amesema.

Hata hivyo amempongeza Rais Magufuli na kudai kuwa amefanya vizuri katika baadhi ya maeneo lakini kuna maeneo mengine ambayo angepaswa kuyapa kipaumbele zaidi akitolea mfano wa elimu na kudai kuwa badala ya kuanza na suala la madawati angeanza na kushughulikia maslahi ya walimu kwanza, na kutoa kipaumbele kwa tatizo la ajira nchini hasa kwa vijana.

Kuhusiana na harakati za Serikali kuhamia Dodoma, Mjumbe huyo wa Kamati Kuu CHADEMA amesema viongozi wote waliotangulia tangu enzi za Mwalimu Nyerere walikuwa na ndoto za kuhamia Dodoma lakini kuna mambo yaliyokuwa yanaingilia mipango hiyo na mwisho kushindikana.

“Napongeza harakati na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhamishia Serikali yote Dodoma lakini napenda kuwaambia wasiende kwa kasi sana wasije wakavunjika miguu,” ameongeza.

Kuhusiana na hali ya kisiasa Zanzibar, Lowassa ametoa rai kwa Rais Magufuli aangalie hali ya Zanzibar kwani yanayoripotiwa kuendelea visiwani humo yanatia kichefuchefu ikiwemo watu kukamatwa na kuteswa.

“Tusiitenge Zanzibar na badala yake juhudi za makusudi zifanyike kuweka mambo sawa kwa kufanya mazungumzo kwani siasa ni mazungumzo,” amesisitiza Lowassa ambaye amedai kuwa ana matumaini makubwa ya kuingia Ikulu mwaka 2020.

Kuhusu kashfa ya Richmond kumfanya aondoke CCM kwa hasira baada ya kukosa ridhaa ya chama hicho katika kugombea Urais, Lowassa amesema hakuondoka CCM kwa hasira isipokuwa alituhumiwa na kuhukumiwa bila kupewa nafasi ya kusikilizwa.

“CHADEMA sikujipeleka mwenyewe bali Kamati Kuu CHADEMA ilinifata na kuniomba nijiunge nao katika kupeperusha bendera yao na mimi niliona ni ‘opportunity’ nzuri hivyo nikakubali nikajiunga nao na tukafanikiwa kupata kura zaidi ya milioni sita, idadi ambayo siyo ndogo hata kidogo,” amejinasibu Lowassa.

Lowassa Uso Kwa Uso na Nape Nnauye Wakati wa Kuaga Mwili wa Mwandishi wa Tanzania Daima

$
0
0
Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema na Ukawa, Edward Lowassa amekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Mnauye leo katika jumuiko la kuuaga mwili wa aliyekuwa Mpigapicha wa Tanzania Daima, Joseph Senga. 

Mwili wa Joseph Senga (58) umesafirishwa leo kwenda nyumbani kwao, Shushi-Nyambichi, Kwimba mkoani Mwanza kwa ajili ya maziko hapo kesho.

Akizungumza wakati wa kuuga mwili wa marehemu Dar es Salaam mapema leo, msemaji wa familia, Charles Kapama amesema maziko yatafanyika kesho saa nane mchana baada ya mwili kuwasili kijijini.

Viongozi mbalimbali walijumuika na ndugu, jamaa na marafiki wa familia hiyo kuuga mwili wa marehemu Senga ambaye alifariki dunia Julai 27 katika hispitali ya BLK, New Dehli India alikokwenda kupatiwa matibabu, katika uwanja wa mpira uliojirani na nyumbani kwake, Sinza jijini hapa.

Viongozi hao ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Mwenyekiti wa Chadema,  Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea.
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga, aliekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, aliefariki Dunia hivi karibuni, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo, iliyofanyika katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri, Jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga, aliekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, aliefariki Dunia hivi karibuni, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo, iliyofanyika katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri, Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga, aliekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, aliefariki Dunia hivi karibuni, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo, iliyofanyika katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri, Jijini Dar es salaam.
 Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Joseph Senga liwa katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri jijini Dar es salaam wakati wakiamuaga kwenda Kwimba, Mwanza kwa Maziko. Mwili wa Marehemu Joseph Senga unatarajiwa kuzikwa mara baada ya kufika.
 Familia ya Marehemu Joseph Senga ikiwa ni yenye huzuni kubwa kuondokewa na Mpendwa wao.
 Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Said Kubenea akizungumza.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akizungumza.

Mbowe Awasili Polisi Kuhojiwa....Lowassa Azuiwa Kuingia

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia  na Maendelea (Chadema), Freeman Mbowe  leo july 31 amewasili makao makuu ya jeshi la polisi kuitikia wito wa kuhojiwa na jeshi hilohuku hali ya  usalama ukiwa imeimarishwa   kabla na baada ya Mbowe kuwasili .
 
Mbowe akiwa na msafara wa magari nane walikutana na ulinzi huo makali ambapo  magari ya Mbowe na Wakili Peter Kibatala ambaye alikuwa na Tundu Lissu ndio yaliruhusiwa kuingia. 

Gari la Edward Lowassa na viongozi wengine wamezuiwa kwenye geti la kuingia kituoni hapo ambapo geti hilo limezibwa na gari la maji ya kuwasha ili kutoruhusu gari yoyote kutoka au kuingia


Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya Agosti 1

Rais Magufuli Asema Hatagawa Chakula cha Bure Kwa Watakaopatwa na Janga la Njaa Bila Sababu za Msingi.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali yake haitagawa chakula cha bure kwa wananchi wanaopatwa na tatizo la njaa pasipo kuwa na sababu za msingi na badala yake amewataka watanzania wajikite kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ikiwa ni pamoja na kuzalisha chakula cha kutosha.

Rais Magufuli amesema hayo jana tarehe 31 Julai, 2016 wakati akihutubia mikutano ya hadhara na kuzungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake akiwa njiani kutoka Mkoani Tabora kuelekea Shinyanga na baadaye Geita anakoendelea na ziara yake.

Pamoja na kuwahimiza wananchi kuzalisha chakula cha kutosha ili kuondokana na njaa Rais Magufuli alisema serikali yake itajikita kuhakikisha inashughulikia tatizo la uhaba wa maji, ujenzi wa miundombinu hususani barabara na reli, kuimarisha huduma za matibabu, elimu na kutengeneza ajira.

Akiwa Isaka Mkoani Shinyanga Rais Magufuli alisema serikali haitalipa fidia kwa wananchi waliopatwa na maafa ya mafuriko yaliyobomoa nyumba zao mwezi Machi mwaka 2015 na badala yake itajielekeza kutatua tatizo kubwa la uhaba wa maji katika mji huo ambao una makutano ya reli ya kati ya kutoka Dar es Salaam kwenda nchi za Burundi na Rwanda.

Katika Mji wa Kagongwa Rais Magufuli alipokea kilio cha wananchi dhidi ya vitendo vya ujambazi na ametoa siku tano kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha watu wanaojihusisha na ujambazi wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Mjini Kahama, Dkt. Magufuli aliiagiza Wizara ya Nishati na Madini kushirikiana na Mbunge wa Kahama Mhe. Jumanne Kishimba kukokotoa mahesabu vizuri na kubaini kodi ambayo Serikali inastahili kulipwa baada ya Mbunge huyo kudai kuna kiasi kikubwa cha kodi hakijakusanywa kama ambavyo sheria inaelekeza.

Aidha, Rais Magufuli alisema serikali itahakikisha wawekezaji wanaochimba madini wanaacha kusafirisha mchanga wenye madini kwa lengo la kwenda kuchakata nje ya nchi na badala yake ametaka uchakataji huo ufanyike hapa hapa nchini.

Dkt. Magufuli alizungumza na wananchi vijiji vya Segese na Bukoli na kuwahakikishia kuwa Barabara ya Kahama, Segese, Kakola hadi Geita yenye urefu wa kilometa 146 itajengwa kwa kiwango cha lami kama alivyoahidi.

Mjini Geita, Rais Magufuli alipokea kilio cha wananchi wanaodai kuwekewa zuio la kutumia mawe yenye mabaki ya madini ya dhahabu (Magwangala) kwa lengo la kusaga na kuchenjua ili kupata dhahabu, na ametoa wiki tatu kwa Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufanya tathimini na kuwaruhusu wachimbaji wadogo kutumia Magwangala.

Rais Magufuli pia ameiagiza Bodi ya Pamba hapa nchini kuhamisha ofisi zake zilizopo Jijini Dar es salaam na kuzileta katika Mikoa ya kanda ya ziwa ambako uzalishaji wa zao la pamba unafanyika.

Dkt. Magufuli amewaonya viongozi na watendaji wa bodi hiyo dhidi ya vitendo vya usambazaji wa mbegu za pamba zisizoota na amesema ikitokea tena watachukuliwa hatua.

Tarehe 01 Agosti, 2016 Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli anatarajia kukamilisha ziara yake ya siku nne katika Mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Geita

31 Julai, 2016

James Lembeli Aibukia Mkutano wa Rais Magufuli

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia wa wakazi wa Kahama mara baada ya kuwasili akitokea Nzega mkoa Tabora.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akicheza jukwaani wimbo wa kwaya ya Haleluya Kuu kutoka Kanisa la KKKT- Usharika wa Yeru Ndala Shinyanga kabla ya Kuhutubia mamia ya wakazi Kahama mkoani Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mbunge wa zamani wa Kahama James Lembeli mara baada ya kuwasalimia wananchi waliofika kwa ajili ya kumsikiliza Rais katika viwanja hivyo vya Kahama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia wa wakazi wa Isaka mkoani Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameambatana na Mbunge wa zamani wa Kahama James Lembeli ambaye ni mwanachama wa Chadema mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano mjini Kahama mkoani Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akicheza pamoja na Wanakwaya wa Haleluya Kuu kutoka Kanisa la KKKT- Usharika wa Yeru Ndala Shinyanga mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano Kahama mjini mkoani Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia mara baada ya kuoneshwa picha na kijana mmoja aliyeishika picha hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Tinde mkoani Sinyanga. PICHA NA IKULU

Wakili Kibatala: Mkurugenzi wa Bagamoyo Aliyetumbuliwa na Rais Magufuli ameponzwa na Kesi za Uchaguzi zilizoipa ushindi Chadema

$
0
0

Mkurugenzi wa Sheria wa Chadema, Peter Kibatala amempa pole aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Azimina Mbilinyi kwa kuenguliwa kwenye nafasi hiyo, ikiwa ni siku moja baada ya kesi za uchaguzi alizotolea ushahidi wilayani Kilombero kuhukumiwa. 

Akiandika katika ukurasa wake wa Facebook jana, Kibatala alisema: “Tunasikitika nawe, na kukupa pole nyingi sana.” 

Katika ujumbe huo aliothibitisha baadaye kuuandika, Kibatala aliongeza: “Tunakushukuru sana kwa kutoa ushahidi wa ukweli na wa haki katika kesi za uchaguzi majimbo ya Kilombero na Mlimba yaliyotolewa hukumu jana (Julai 29).” 

Wakili hiyo aliongeza:“Wakati wa Uchaguzi Mkuu ulikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilombero na Msimamizi wa Uchaguzi katika Majimbo waliyoshinda Chadema.” 

Juzi, taarifa ya Ofisi ya Rais–Tamisemi iliyotolewa  na Katibu Mkuu, Mussa Iyombe bila kufafanua sababu za kuenguliwa kwake, ilieleza kwamba Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mbilinyi kwa sababu hakuridhishwa na utendaji wake wa kazi. 

Mbilinyi alikuwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilombero kabla ya kuhamishiwa Dodoma na baadaye Bagamoyo. 

Alipotafutwa kuthibitisha maneno yaliyoandikwa kwenye ukurasa wake wa facebook, Kibatala alisema:“Ni kweli niliandika kwenye ukurasa wangu wa facebook na ninaomba maneno hayo yabaki kama yalivyo, naona watu wengine wameanza kutafsiri vinginevyo.”

Katika hukumu hizo, Majaji Projest Rugazia na Penterine Kente waliwapa ushindi wabunge wawili wa Chadema, Susan Kiwanga na Peter Liajualikali baada ya kukosekana ushahidi wa kutengua matokeo hayo.

Juhudi za kumtafuta Mbilinyi kuzungumzia hatua iliyochukuliwa dhidi yake hazikuzaa matunda kutokana na simu zake zilizopigwa mara nyingi kutokuwa hewani. 

Mbowe Ahojiwa na Kuachiwa Kwa Dhamana.......Tundu Lissu Asisitiza Oparesheni UKUTA Iko Palepale

$
0
0

MWANASHERIA Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema licha ya viongozi wa chama hicho kutishwa, kukamatwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi, bado msimamo wao kuhusu operesheni Ukuta itakayofanyika Septemba Mosi mwaka huu uko pale pale.

Chama hicho kinatarajiwa kufanya operesheni mpya iliyopewa jina la Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (Ukuta).

Operesheni hiyo inatarajiwa kuwa itakwenda sambamba na uzinduzi wa mikutano ya hadhara nchi nzima, ambayo itafanyika Septemba Mosi, mwaka huu.

Hatua hiyo imefikiwa na kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho iliyoketi kwa siku nne mfululizo wiki iliyopita jijini Dar es Salaam na kutoa maazimio matatu ambayo yatatekelezwa na chama hicho.

Pamoja na mambo mengine, chama hicho kimesema lengo la operesheni hiyo ni kuzuia matukio ya ukandamizaji wa haki na demokrasia nchini, kiliyodai kuwa yanafanywa na Rais Dk. John Magufuli.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam baada ya kuhojiwa na kuachiwa kwa dhamana Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mwanasheria  Lissu alisema msimamo wao uko palepale na hakuna kilichobadilika.

“Wamemuhoji kwa taarifa aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari juu ya msimamo wa chama wa kufanya mkutano nchi nzima. Tatizo jeshi letu wakisikia maandamano, mkutano au mtu anamsema Magufuli basi anatuhumiwa kwa uchochezi, wametumia muda mrefu kumuhoji lakini mwisho wamemwachia kwa dhamana na amewahi ‘Airport’ ili aende kuhudhuria mazishi ya kamanda wetu Senga (Joseph) na watamwita watakapomwihitaji tena,” alisema Lissu.

Alisema pamoja na hayo bado msimamo wa chama hicho kufanya mikutano waliyoiita Operesheni Ukuta ipo pale pale ifikapo Septemba Mosi, mwaka huu.

“Nafikiri ni muhimu sana huko tunapoenda kuzungumza na wenzetu hii kitu inaitwa uchochezi ni nini? Tunashitakiwa kwa sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ambayo waliingiza vifungu vya uchochezi mwaka 1978 lengo lao kuu ni kuwafunga watu midomo na ilitungwa wakati wa mfumo wa chama kimoja.

“Hata hivyo Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ndiye wa kwanza kushtakiwa kwa uchochezi  pamoja na mwandishi Robert Makenge na mwenzao Rashid Bagedae, kwa msingi huo sisi tunafuata nyayo zake,” alisema.

Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), alisema kuitwa mchochezi, ni jambo la ufahari kupinga udikteta kama alivyokuwa Mwalimu Nyerere.

“Nasema hivyo kwa sababu Mwalimu Nyerere ndiye wa kwanza kuitwa mchochezi, ni kitendo cha kufunga watu midomo ili washindwe kuwaita watu wajinga pale wanapofanya ujinga.

“Tume ya Jaji Nyalali mwaka 1992 wakati mfumo wa vyama vingi unatambulishwa na kuanza nchini ilipendekezwa sheria hii ifutwe kwa sababu haiendani na mfumo uliopo lakini hakuna kilichofanyika,” alisema.

Mwanasheria huyo ambaye naye amefunguliwa kesi ya uchochezi katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar, aliwataka wafuasi wa chama hicho kujitokeza kwa wingi Agosti 2, mwaka huu mahakamani hapo.

“Dawa yao si majaji bali umma… umma ufurike, tutawashinda hawa watu makesi yenyewe ni haya ambayo hayana kichwa  wala miguu,” alisema na kushangiliwa na wafuasi wa chama hicho.

Mbowe alifika kituoni hapo akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali wa Chadema akiwamo Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ambaye hata hivyo alizuiwa kuingia katika chumba cha mahojiano.

Askari waliokuwa kwa wingi katika eneo hilo, walisikika wakisema kuwa anayepaswa kuingia ndani ni Mbowe, Mwanasheria Tundu Lissu na Wakili wa Chadema, John Mallya.

Lowassa, wafuasi wa Chadema na waandishi wa habari walilazimika kubaki nje huku askari wakiimarisha ulinzi wakiwa wamebeba bunduki zao huku magari yenye maji ya kuwasha yakiwa yameegeshwa pembeni.

Wakati chama hicho kikijiandaa kutekeleza Operesheni Ukuta Septemba Mosi, tayari Rais Magufuli amezuia operesheni hiyo na kuwaonya wale wote watakaokaidi agizo lake na kuamua kuandamana.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images