Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya July 29


Agizo la Waziri Mkuu kuhusu wafanyakazi walioajiriwa kwa mkataba

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Halmashauri ya wilaya ya Temeke kuondoa wafanyakazi wa mkataba kwa ili kuwapa ajira ya kudumu kwa wenye sifa na kuwaondoa wasiokuwa na sifa ifikapo Julai 30 mwaka huu.
 
Amesema kitendo cha kutowaajiri na kuwatumikisha kwa mikataba kwa muda mrefu kinasababisha wakose stahiki zao jambo ambalo  halikubaliki.
 
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana(Alhamisi, Julai 28, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo na kusisitiza kwamba ni lazima sula hilo lishughulikiwe haraka kwa sababu hayo ndio matundu watumishi hewa.
 
“Mnawatumikisha watu kama vibarua kwa muda mrefu, hapa kuna wengine wanafanya kazi kwa mikataba kwa miaka mitano hadi sita hii haikubaliki kwani mnawakosesha stahili zao pale mnapowaachisha kazi,” alisema.
 
Awali Kaimu Ofisa Utumishi wa Manispaa hiyo Zaitun Hassan alisema wamekuwa wakitoa ajira za mikataba kwa sababu wamekosa watu wenye sifa za kuweza kuajiriwa hususan madereva.
 
“Kwa mara ya mwisho umetangaza lini nafasi za ajira? Katika mkoa wa Dar es Salaam kweli wanaweza kukosekana madereva wenye sifa za kuajiriwa? Alihoji Waziri Mkuu.
 
Zaitun alisema kuwa madereva wengi wanaojitokeza pindi wanapotangaza ajira wanashindwa kufikia vigezo ikiwemo kuwa na cheti cha VETA na badala yake wanakuwa na cheti cha kidato cha nne tu.
 
Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema kuwa kuna wafanyakazi wengine katika Idara ya Uhasibu na Ujenzi ambao nao wameajiriwa kwa mkataba hivyo amemtaka Ofisa Utumishi kuomba kibali cha kuajiri kwa Katibu Mkuu Utumishi.
 
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kufanya tathmini ya maeneo yote ya shule kwenye mkoa wake na watakaobainika kuingia katika maeneo hayo waondolewe haraka.

Alisema baada ya kukamilisha utengenezaji wa madawati kinachofuatia sasa ni ujenzi wa vyumba vya madarasa, ambapo amezitaka halmashauri kuweka mipango ya kujenga majengo ya madarasa ya ghorofa ili waweze kuwa na madarasa mengi katika eneo dogo.
 
Awali Waziri Mkuu alipokea msaada wa madawati 705 katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Chamazi wilayani Temeke ambapo kati yake Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania umetoa madawati 600 na Jumuia ya Mabohora imetoa madawati 105.
 
Pia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dk. Agustino Mahiga alimkabidhi Waziri Mkuu hundi ya sh. milioni 85 fedha zilizochangwa na watumishi wa wizara hiyo kwa ajili ya kuchangia utengenezaji wa madawati.
 
Dk. Mahija alisema watumishi hao walichanga sh. milioni 100 kwa ajili ya utengenezaji wa madawati ambapo sh. milioni 15 wamekabidhi kwa mkuu wa wilaya ya Manyoni Geofrey Mwambe ambaye alikuwa mtumishi wa wizara hiyo ili naye akatengeneze madawati kwa shule za wilayani kwake.
 
Kwa upande wake Balozi wa Kuwait nchini Jaseem Al Najem amesema Serikali ya Kuwait itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika shughuli zote za maendeleo hususan katika sekta za elimu na afya.
 
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM. ALHAMISI, JULAI 28, 2016

Walimu 4 wamvua nguo na kumchangia viboko binti wa Kidato cha IV Mbeya huku Mwalimu Mwingine Akimtomasa Sehemu za Siri

$
0
0
VITENDO vya ukatili wa kijinsia na dhuluma dhidi ya watoto wa kike vimekuwa vikishamiri kila siku pamoja na kuwepo kwa taasisi za kutetea haki za wanawake  na kuanzishwa kwa madawati ya Kijinsia kwenye vituo vya polisi nchini.
 
Msichana wa kidato cha Nne mwenye umri wa miaka 17,(jina tunalo) anayesoma shule moja ya sekondari ya Kata mkoani Mbeya amekumbwa na kadhia ya kuvuliwa nguo zake za ndani na kucharazwa bakora zisizo na idadi na walimu wanne wa shule hiyo.
 
Tukio hilo ambalo limeripotiwa katika kituo kidogo cha  Polisi Mbalizi wilaya ya Mbeya kwenye jalada la uchunguzi namba MBI/IR/967/2016 na kuwekwa kwenye taarifa yenye namba MBI/RB/2653/2016 linadaiwa kuwahusisha walimu wanne akiwemo Mkuu wa shule hiyo pamoja na walimu watatu.
 
Akizungumza huku akiwa na maumivu makali katika Hospitali Teule ya Ifisi ambako amelazwa akipatiwa matibabu, mwanafunzi huyo alisema kuwa aliitwa na mwalimu wa nidhamu aliyemtaja kwa jina la Neema Mwaikenda aliyekuwa pamoja na Mkuu wa shule hiyo aliyemtaja kwa jina la Mariamu Mwanisenga na mwalimu wa kiume aliyemtaja kwa jina la Adili.
 
Alisema walimu hao walianza kumuadhibu kwa viboko visivyo na idadi huku akiwa amechojolewa nguo zake ambapo mwalimu wa kiume aliyemtaja kwa jina la Adili akaanza kumshikashika sehemu zake za siri.
 
‘’Wakati naadhibiwa na walimu wote, huyu mwalimu wa kiume alianza kunishika  huku chini,na kunitaka niwataje wanaume zangu,nikawa nabana miguu wakazidi kunishambulia kwa vibao na mateke na fimbo,’’alisema mwanafunzi huyo.
 
Alisema sababu zilizosababisha aadhibiwe ilikuwa ni utoro na kuwa siku moja alipokuwa shuleni alioneshwa na walimu fimbo na kuelezwa kuwa fimbo hizo zitamuishia mwilini ndipo akaogopa kufika shuleni kwa siku tatu.
 
Anafafanua kuwa siku aliyofika shuleni ndipo alipokutana na kadhia ya kupigwa na walimu wanne hadi  alipowaponyoka walimu hao na kukimbilia mitaani na kujificha.
 
‘’Niliwaponyoka walimu nikakimbilia kwenye nyumba ya jirani na shule nikajificha hadi jioni na baadaye kwenda nyumbani, kesho yake mama na dada walinichukua na kunileta hospitali,’’alisema.
 
Mwandishi wa habari hizi alifika shuleni anakosoma mwanafunzi huyo kwa nia ya kukutana na uongozi wa shuleni hiyo ambapo Makamu Mkuu wa shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwansanga alikataa kuelezea chochote.
 
‘’Mie sijui lolote kwanza mie sio msemaji wa shule, kwahiyo sijui lolote juu ya taarifa mnazohitaji,’’alijibu Makamu Mkuu wa shule na kuondoka zake.
 
Kwa upande wake Ofisa Elimu wa Mkoa Charles Mwakalila alisema kuwa adhabu aliyopewa mwanafunzi huyo ni kubwa kupitiliza kwa kuwa zipo taratibu za adhabu kulingana na makosa na kuwa mwanafunzi anapaswa kupigwa viboko vitatu na viboko visivyozidi sita au adhabu mbadala.
 
‘’Adhabu aliyopewa ni kubwa, tutafuatilia na waliokiuka taratibu watachukuliwa hatua za kinidhamu,’’alisema Mwakalila.
 
Naye Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari alipoulizwa juu ya tukio hili alidai kuwa halijafika ofisini kwake na kuwa kwa sasa yeye yupo kikazi wilayani Chunya na mara atakapofika ofisini atafuatilia na kuchukua hatua za kisheria kwa wahusika wa tukio hilo.
 
Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Mariamu Mtunguja ambaye alifika Hospitalini alikolazwa mwanafunzi huyo alisema kuwa amemuangalia mwanafunzi huyo na kuona namna ambavyo damu imevilia kwenye sehemu zake za makalio na kwenye mapaja.
 
Mtunguja alisema kuwa kitendo kilichofanywa na walimu hao ni cha kinyama ambacho hakipaswi kuvumiliwa na kuwa mara itakapobainika atahakikisha walimu hao wanachukuliwa hatua za kinidhamu.
 
Muuguzi Mkuu Msaidizi wa Hospitali Teule ya Ifisi Elimati Sanga alisema kuwa mwanafunzi huyo alifikishwa hospitalini hapo Julai 21 saa 7:00 mchana ambapo alipatiwa matibabu na kulazwa kutokana na majeraha na damu iliyovilia mwilini sehemu za makalio na mapaja.
 
‘’Ameshambuliwa sehemu za mapaja, damu na masikio yake hasikii vyema kutokana na kipigo, anaendelea na matitabu hapa hospitali,’’alisema Sanga.
Muuguzi Mkuu msaidizi wa Hospitali Teule ya Ifisi, Elimati Sanga akielezea madhara aliyopata mwanafunzi anayedaiwa kupigwa na walimu wanne wa shule ya Sekondari Malama
Credit: Mkwinda 

Lowassa Akoleza Moto CCM....Awata Wanaomuunga Mkono Ndani ya CCM Waendelee Kumpa Siri za Serikali

$
0
0
Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na Ukawa, Edward Lowassa ana uhakika kuwa bado kuna wanachama wanaomuunga mkono ndani ya CCM na sasa anawataka waendelee kushikamana naye, kauli ambayo inaweza kuchochea moto ndani ya CCM. 

Katika taarifa yake fupi kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana, Lowassa amewahakikishia wananchi kuwa kwa sasa ana “ari, nguvu na hamasa kuliko wakati mwingine wowote”.

Lowassa, ambaye alikuwa waziri mkuu wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne, alijiondoa kwenye chama tawala Julai 28 mwaka jana baada ya jina lake kuondolewa kwenye orodha ya wagombea urais kwa tiketi ya CCM.

Kuondoka kwake kulisababisha mawaziri wa zamani, wabunge, wenyeviti wa mikoa, madiwani na wanachama wengine wa CCM, wakiongozwa na waziri mwingine mkuu wa zamani, Frederick Sumaye kukihama chama hicho, hali iliyosababisha ushindani kuwa mkubwa kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita, huku CCM ikilalamikia kusalitiwa.

Wakati CCM ikifikiria hatua za kuchukua dhidi ya wasaliti wa chama wanaotuhumiwa kuunga mkono harakati za upinzani wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, Lowassa ameongeza petroli kwenye moto ulioanza kuwaka.

“Kwa wale wenzangu waliobaki CCM na wanaoniunga mkono, tuendelee kushikamana na kunipatia taarifa kwa hatima ya nchi yetu,” amesema Lowassa ambaye kwa sasa ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.

“Nawashukuru Watanzania kwa kuendelea kuniunga mkono mimi na wenzangu ndani Chadema.” 

Kauli hiyo kuwa kuna watu ndani ya CCM ambao wanampatia taarifa mbunge huyo wa zamani wa Monduli na ombi lake la kutaka waendelee kumpa taarifa, inaweza kusababisha hali ngumu zaidi kwa chama hicho, ambacho kinaamini kuwa makada wake walikihujumu wakati wa uchaguzi kwa kumfanyia kampeni kisiri.

Katika uchaguzi huo, Rais John Magufuli alishinda kwa kupata asilimia ndogo ya kura kulinganisha na watangulizi wake. 

Ingawa alipata kura milioni 8.8 na Lowassa kufuatia kwa kupata kura milioni 6.07, ushindi huo ni wa asilimia 58.46 dhidi ya asilimia 39.67 kulinganisha na ushindi wa asilimia 61.17 aliopata Kikwete mwaka 2010 dhidi ya asilimia 26.34 alizopata Dk Willibrod Slaa wa Chadema.

Tangu Januari mwaka huu, CCM imekuwa ikijadili wasaliti hao katika ngazi ya wilaya na taarifa za mapendekezo ya hatua dhidi yao kutumwa Halmashauri Kuu kwa ajili ya uamuzi wa mwisho.

Katika hotuba yake ya kuaga, Jakaya Kikwete alimkabidhi mwenyekiti mpya wa CCM, Rais Magufuli ripoti ya hali ilivyokuwa kwenye uchaguzi, akisema yeye ndiye atakayeamua adhabu dhidi ya wale wote walioonekana kufanya makosa. CCM imeshasema kuwa wasaliti wote ni lazima washughulikiwe.

Katika taarifa yake ya jana, Lowassa ameeleza kuwa uamuzi alioufanya wa kuihama CCM na kujiunga na Chadema “haukuwa rahisi, lakini kwa ushupavu, ujasiri na mwongozo wa Mungu nilifanya hivyo” na kwamba huo ni “uamuzi wa kihistoria katika nchi yetu.

“Najivunia kwa uamuzi ule, kwani umewafungua macho Watanzania wengi na kuimarisha demokrasia. Nimeingia Chadema nimewakuta viongozi na wanachama walio na moyo wa dhati wa kuliletea maendeleo Taifa lao kivitendo,” anasema Lowassa katika taarifa yake fupi.

“Watanzania bado wanataka mabadiliko na imezidi kuthibitisha kuwa hawawezi kuyapata ndani ya CCM. Watanzania wanataka sera na mtu mbadala wa kuongoza mabadiliko hayo. Vyote hivyo watavipata ndani ya Chadema na Ukawa kwa jumla.”

Bingwa wa kubikiri Wasichana Nchini Malawi abainika ana UKIMWI........Rais Aamuru Akamatwe Haraka

$
0
0

Rais wa Malawi, Peter Mutharika juzi alitoa amri ya kukamatwa kwa Eric Aniva ambaye hivi karibuni alibainika kufanya kibarua cha kuwabikiri mabinti wa chini ya umri wa miaka 13 zaidi ya 100.

Amri hiyo ya Rais imekuja baada ya kubainika kuwa mwanamume huyo maarufu kwa jina la ‘Fisi’ anaishi na Virusi vya Ukimwi (VVU). 

Mutharika alisema lazima mwanamume huyo akamatwe na hatua kali zichukuliwe dhidi yake kwa kuwa, kwa makusudi alifanya vitendo viovu akijua anaishi na VVU na lengo lake lilikuwa kuwaambukiza mabinti hao.

Aniva aliingia matatani baada ya kukiri katika mahojiano akijinasibu kuwa anaendesha maisha kwa kuwabikiri mabinti na kwamba hulipwa kuanzia dola nne za Marekani mpaka saba ambayo ni wastani wa Sh10,000 kwa kila mtu.

Mwanamume huyo alisema wazazi wa mabinti huwa wanampa kibarua cha kuwavusha kutoka utoto kuingia katika utu uzima na kwamba hatua hiyo ni sawa na tambiko. 

Waombaji wa Mikopo Elimu ya juu Wafikia 69,820 Mpaka Sasa

$
0
0

JUMLA ya wanafunzi 69,820 wameomba mikopo kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) hadi sasa ikiwa zimebaki siku tatu kufikia mwisho wa kupokea maombi hayo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam , Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa bodi hiyo, Cosmas Mwaisoga, alisema mwaka jana walioomba kupewa mikopo walikuwa 65,000, hivyo waombaji wa mwaka huu wameongezeka.

Mwaisoga alisema tofauti na awali, mchakato wa sasa wa kuomba unafanyika kwa njia ya mtandao na baada ya kutumwa kwao, watayapitia na kwa yale yenye kasoro, wahusika wataitwa ili wayarekebishe.

Alisema dirisha la uombaji wa mikopo linatarajia kufungwa Jumapili hii.

Katika hatua nyingine, alisema idadi ya wanaorejesha mikopo imeongezeka maradufu baada ya kutakiwa kufanya hivyo.

“Kwa sasa ni vigumu kutaja idadi yao kwa sababu huwa tunaitoa mwishoni mwa mwezi kwa hiyo kesho tutakuwa na idadi kamili ya waliorejesha, lakini ikilinganishwa na huko nyuma, sasa hivi mwitiko wa wanaorejesha umeongezeka,” alisema.

Mwaisoga alisema sheria inamtaka aliyekopa aanze kurejesha baada ya mwaka mmoja wa kuhitimu masomo yake, lakini anapochelewesha, kila mwaka kunakuwa na penati ya ongezeko la asilimia sita.

Mwanamuziki Koffi Olomide aachiwa huru kutoka jela baada ya kutumikia kifungo kwa siku 2

$
0
0
Koffi Olomide Alikamatwa Jumanne July 26 2016 nyumbani kwake Kinshasa kwa tuhuma za kumshambulia dancer wake wa kike wakati wakiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyata Nairobi na baadaye ikawa imeripotiwa kuwa amehukumiwa kwenda jela miezi 18 na adhabu hiyo kutajwa kuwa haitakuwa na faini.

Taarifa zilizoripotiwa ni kwamba Koffi Olomide kaachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha siku mbili kati ya miezi 18 aliyohukumiwa awali.

 BBC imeripoti kuwa kuachiwa kwa koffi Olomide kumekuja baada ya Mahakama ya Kinshasa kusema kuwa hawakuona sababu za kutosha za kuhukumiwa kwa Koffi Olomide kutokana na tukio alilofanya JKIA.

Pamoja na baadhi ya vyombo vya habari Afrika kuripoti kwamba Koffi alihukumiwa kifungo cha miezi 18 jela , Promoter wake wa nchini  Kenya Jules Nsana amekanusha madai hayo  na kusema  kesi dhidi ya Koffi ilikuwa bado iko kwenye uchunguzi na kwamba baada ya uchunguzi wamebaini hakuna ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani Koffi Olomide.

Promoter Jules amesema Olomide alimpigia simu akamtaka aombe msamaha kwa wakenya wote kwa niaba yake

Vitu alivyoongea bilionea Mohammed Dewji katika mpango wake wa kuinunua Timu Ya Simba

$
0
0

Kuelekea mkutano mkuu wa Simba unaotaraji kufanyika Jumapili ya Julai, 31, shabiki na mkeleketwa wa Simba ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Makampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji amezungumza mipango yake aliyopanga kuifanyia Simba kama akipata nafasi ya kununua hisa asilimia 51 za klabu hiyo.

MO amesema kuwa mipango yake ni kuwekeza Bilioni 20 na amepanga bajeti ya klabu hiyo kwa mwaka iwe Bilioni 5.5, kiasi ambacho anaamini kuwa kitaweza kubadili mwelekeo wa Simba kutoka ilivyo sasa na kurudisha zama zake za kutwaa mataji ya ndani na kufika hatua nzuri kimataifa.

MO alisema amefikia uamuzi wa kutaka kununua hisa katika klabu ya Simba kutokana na mapenzi aliyonayo katika klabu hiyo na hana nia yoyote ya kiabiashara na klabu hiyo kwani tayari ana biashara anazofanya ambazo zinamuingizia pesa nyingi hivyo jambo hilo ni kuona timu aliyo na mapenzi nayo ikifanikiwa.

“Nipo tayari kuwekeza Bilioni 20 kama watanipa nafasi lakini tukubaliane kuwa hakuna mtu atagusa pesa hizo pesa, tutauza bondi na kwa kila mwaka tutaingiza Bilioni 3.5 na tutatengeneza mapato ya Bilioni 2 kila mwaka ukijumlisha ni Bilioni 5.5 ambayo itakuwa ni bajeti ya mwaka,

“Inaniuma sana kuona klabu imekuja juzi tu leo inatuzidi mafanikio lakini kama Yanga na Azam bajeti zao kwa mwaka ni Bilioni 2.5 hadi Bilioni 3, sisi tukiwa na bajeti ya Bilioni 5.5 tutakuwa tumewazidi na tutaleta wachezaji wazuri na kocha mzuri,” alisema na kuongeza.

“Dhamira yangu sio kupata Simba kibiashara, mimi Mungu kanijalia nina pesa nina biashara ziadi ya 100, tumeajiri wafanyakazi wanafika 28,000 , jambo ninalolitaka Simba ni kuwekeza, tubadili mfumo, tushinde mataji na sio Tanzania pekee shabaha yangu ni kushinda mataji ya Afrika”

Aidha MO alisema kuwa kama akipata nafasi atazungumza na viongozi wa Simba ili kila mwanachama wa klabu wa muda mrefu apatiwe hisa bure kutokana na kazi kubwa ambayo wameifanya katika klabu hiyo.

“Nitazungumza na viongozi wa klabu tuone jinsi ambavyo tunaweza kuwapa bure wanachama wa klabu ambao wamekuwa na timu kwa muda mrefu, wameshatoka jasho sana na Simba hivyo tutawapa hisa za timu bure,” alisema MO.

Hata hivyo MO aliongeza kuwa yupo tayari kwa lolote kama katika mkutano mkuu wa Jumapili watamnyima nafasi ya kuwekeza katika klabu ya Simba na kueleza kuwa anachoamini kwa sasa Simba haiitaji mdhamini bali Simba inahitaji mwekezaji.

“Mimi wakininyima kwa moyo mweupe kabisa sina tatizo na hili jambo hata likifanikiwa halitakamilika kesho linaweza kuchukua muda sababu kuna mambo ya kufanyiwa marekebisho na kusaini mikataba ila kama nikiona mambo yanakwenda sawa kwa hicho kipindi nitaangalia jinsi gani nitaisaidia Simba sababu nina mapenzi nayo,” aliongeza MO.

Taarifa muhimu kwa wanaodaiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu walioko Dar es Salaam

CHADEMA wamjibu Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya tuhuma za kutumia matusi, uongo, uchochezi

$
0
0

Baada ya kulifanyia uchambuzi na kulitafakari tamko la Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, lililotolewa jana na msajIli mwenyewe, Jaji Francis Mutungi tumeona ni jambo lenye afya kwa ustawi wa demokrasia nchini, kusahihisha upotoshaji uliomo katika taarifa hiyo ili kuendelea kumsaidia msajili na watu wengine, watawala na walio sehemu ya utawala, kuelewa matakwa na maslahi ya wananchi hasa katika wakati huu ambao taifa linapitia.
 
Kwa hakika tumeshangazwa na kauli zilizotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa, ambaye pia ni Jaji wa Mahakama Kuu, kutokana na jinsi ambavyo anaanza kuonesha kuyumba katika kutimiza wajibu wake hasa kwa kutumia weledi na ujuzi wake wa sheria kwa kiwango cha nafasi yake kama jaji.
 
Katika tamko lake alilolitoa jana na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari jana hiyo na leo, ameshindwa kuonesha neno hata moja linaloashiria matusi, kashfa, uongo au hata kuvuruga amani lililotolewa mbele ya waandishi wa habari juzi wakati Chama kikisoma hadharani maamuzi ya kikao cha Kamati Kuu.
 
Ni jambo la kushangaza kuwa Msajili Mutungi, Jaji wa Mahakama Kuu ameweza kuweka vifungu vingi vya kisheria akidai kuwa vimevunjwa lakini hawezi kuonesha ushahidi wa namna vilivyovunjwa au maneno yanayothibitisha kuvunja hizo sheria. 

Hii si sahihi hata kidogo na inakuwa ‘serious’ zaidi inapofanywa na mtu mwenye weledi wa sheria wa kiwango cha Jaji Mutungi.
 
Wakati Jaji Mutungi akinukuu vifungu vya sheria na kanuni akionekana dhahiri kuwa kuegemea na kuwatetea watawala ambao wamedhihirisha kuwa wanatamani nchi irudi enzi za ‘ujima’ wa fikra za chama kimoja, kwa sababu anazozijua mwenyewe amesahau au ameshindwa au amefanya makusudi kwa sababu anazozjijua mwenyewe, kunukuu kifungu cha 4(1) (e) cha maadili ya vyama vya siasa za mwaka 2007, ambacho kinatoa haki kwa vyama vya siasa kuendesha shughuli zao za kisiasa ikiwemo mikutano ya hadhara na maandamano kwa mujibu wa sheria.
 
Tulidhani kuwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye si tu kwamba ni mlezi wa vyama vyote bali pia anasimama kama mwamuzi wa mchezo wa mpira uwanjani, katikati ya timu mbili uwanjani, angelisimamia kifungu hicho muhimu na kukitumia kuwakemea na kuwaonya watawala, akiwemo Rais, Waziri Mkuu na Jeshi la Polisi wasivunje sheria za nchi kuzuia shughuli za siasa nchini kwa sababu yoyote ile kwa sababu hawako juu ya sheria za nchi hii.
 
Aidha, sasa tunaanza kushtuka na kuanza kujiuliza maswali mengi kuhusu kasi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kujijengea utaratibu usiokuwa na kawaida kwa nafasi yake ya kisiasa na kisheria, kuwa na kasi ya ajabu kutoa kauli au matamko yanayoonesha kuwatetea/kuwalinda watawala wanapovunja sheria zinazosimamia vyama vya siasa. 

Jaji Mutungi amekuwa mahiri wa kuvikemea au hata kuvionya vyama vingine tofauti na CCM, kila vinapodai haki za kisiasa ambazo ziko na zinapaswa kutekelezwa kwa mujibu wa sheria, wala si kwa hisani ya mtu yeyote.
 
Waandishi wa habari na umma kwa ujumla watakuwa mashahidi kwa namna ambavyo CCM wamekuwa wakitumia vyombo vya dola, kuvikandamiza, kuvinyanyasa, kuviwekea mazingira magumu na kuvinyima haki za kufanya siasa vyama vingine washindani wake kwa ajili tu ya kulinda maslahi ya chama kilichoko madarakani.
 
Katika hali hiyo ambayo hata imekuwa ikisababisha mauaji na umwagaji damu za watu wasiokuwa na hatia kwa sababu tu ni wafuasi wa vyama vingine, Msajili wa Vyama vya Siasa hajawahi kuthubutu kujitokeza hadharani kuwaonya na kuwakemea CCM na walioko serikalini kuwa kutumia vyombo vya dola kwa manufaa yao ya kisiasa ni kosa kwa mujibu wa sheria za nchi kupitia kifungu cha maadili ya vyama vya siasa cha 5(1)(c), za mwaka 2007.
 
Tulitegemea kwa kutumia umahiri huo huo wa kunukuu vifungu vya sheria na kanuni za maadili ya vyama vya siasa ambao Msajili amekuwa akiuonesha dhidi ya vyama washindani wa CCM kila vinapodai haki za msingi za kisiasa, angekuwa ameutumia pia kuwakemea, kuwaonya au hata basi kuwakumbusha CCM na Rais Magufuli kwa kutumia kifungu cha 5(1) (i) cha kanuni za maadili ya vyama vya siasa za Mwaka 2007, kuwa ni makosa kutumia mamlaka, rasilimali za serikali, vyombo vya dola au wadhifa wa kiserikali, kuvikandamiza vyama vingine kwa manufaa ya kisiasa ya upande mmoja.
 
Si hayo tu, Jaji Mutungi ama aliamua kuwa kimya au alikuwa na kigugumizi aliposikia;
  1. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais John Magufuli na Jeshi la Polisi wakitoa kauli kinyume cha sheria wakitangaza na kuagiza kuzuia shughuli za kisiasa nchini kwa matakwa yao tu.
  2. Mabalozi na wanadiplomasia wakizuiwa kukutana na asasi zisizo za kiserikali au vyama vya siasa.
  3. Kukiukwa kwa misingi ya sheria, kanuni na taratibu za nchi katika uteuzi wa wakurugenzi na makatibu tawala.
  4. Hali tete inayoendelea Zanzibar baada ya watawala kuharibu uchaguzi mkuu mwaka jana kisha wakafanya uchaguzi wa marudio kwa maslahi ya CCM, kinyume kabisa na sheria za nchi.
    Hayo ni baadhi tu ya masuala ya muhimu ambayo ofisi ya msajili ilitarajiwa kuwa ingekuwa mstari wa mbele kukemea na kuonya ili kuweka mizania ya ushindani wa kisiasa katika usahihi wake.
     
    Kwa mwenendo huu ambao usipoangaliwa na kufanyiwa kazi ya kuurekebisha haraka, tunachelea kusema kuwa Ofisi ya Msajili na Jaji Mutungi mwenyewe wataanza kujikosesha uhalali machoni pa Watanzania ambao wasingependa kuona siasa ambayo ni maisha yao, ikifananishwa kama vile ni jambo la kawaida tu lisilokuwa na maana.
     
    Kupitia taarifa hii, tunamtaka Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mutungi kuwa makini na utaratibu huo vinginevyo Watanzania wataanza kuiweka ofisi yake na yeye mwenyewe kwenye kapu moja na aliyekuwa mtangulizi wake, ambaye ilifika mahali wananchi walimuona yeye binafsi, kupitia kauli zake, matendo yake na ofisi yake kwa ujumla, sawa na sehemu ya chama kilichoko madarakani.
     
    CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani nchini hakiwezi kuvumilia wala kukubali hiki kinachoanza kujionesha kuwa ni ‘double standards’ za mtu anayetarajiwa kuwa mlezi na refarii, kujitokeza hadharani pale tu ambapo maslahi ya chama tawala na watawala yanapoguswa lakini anakuwa kimya na hata kuweka masikio nta mara vyama washindani wa CCM vinapokandamizwa, kinyume kabisa cha sheria.
     
    Kama chama chenye wanachama na viongozi wanaojua haki na wajibu wao wa kikatiba na kisheria, tutaendelea kufanya shughuli za kisiasa kwa namna itakayosimamia  haki na matumaini ya wananchi kwa ajili ya amani na utulivu wa kweli, kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi si kwa kufuata matamko, kauli au maelekezo ya mtu yeyote.
     
    Ni kwa kuzingatia dhana hiyo, maana Kamati Kuu katika kikao cha dharura kilichofanyika mwishoni mwa juma lililopita na maazimio yake kutangazwa juzi Jumatano, moja ya maazimio yake ni kuanzisha operesheni ya UKUTA (Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania) ambayo inalenga kuwaunganisha Watanzania wote bila kujali tofauti zao zozote zile, kudai haki na matumaini dhidi ya udkiteta katika nchi yao na kuzuia harakati za watawala kuataka kupora mamlaka ya wananchi na kujiweka juu ya sheria kwa namna ile ile ambayo madikteta hufanya.
     
    Imetolewa leo Ijumaa Julai 29, 2016 na;
    Prof. Mwesiga Baregu
    Mjumbe wa Kamati Kamati Kuu

    Rais Magufuli Atoa ONYO Kali....."Mimi sijaribiwi, wasije kunijaribu. Atakayeleta vurugu atashughulikiwa bila huruma!

    $
    0
    0
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Julai, 2016 ameanza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma, ambapo amezungumza na wananchi kwa lengo la kuwashukuru kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana  na kueleza juhudi zinazofanywa na serikali katika kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo.

    Akiwa Mkoani Singida, Rais Magufuli aliyeongozana na mkewe Mama Janeth Magufuli amewasihi watanzania kufanya kazi kwa juhudi na kujiepusha na vitendo vya vurugu vinavyohamasishwa na baadhi ya wanasiasa huku akionya kuwa serikali yake haitamvumilia mtu yeyote ambaye atathubutu kuchochea vurugu ikiwemo maandamano kinyume cha sheria.

    “Sitaki nchi hii iwe ya vurugu, watakaoleta vurugu mimi nitawashughulikia kikamilifu bila huruma, na wasije wakanijaribu, mimi ni tofauti sana na kama wapo watu wanaowatumia wakawaeleze vizuri, mimi sijaribiwi na wala sitajaribiwa.

    “Wananchi hawa wana shida, na siasa nzuri ni wananchi washibe, siasa nzuri ni wananchi wetu wapate dawa” Amesema Rais Magufuli.

    Kuhusu hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali yake ya awamu ya tano tangu aingie madarakani Rais Magufuli ametaja baadhi ya  hatua hizo kuwa ni kufuta ada kwa shule za msingi na sekondari, kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu zaidi ya laki moja na kuongeza fedha za miradi ya maendeleo katika bajeti ya serikali kutoka asilimia 26 ya mwaka 2015/2016 hadi kufikia asilimia 40 katika bajeti ya mwaka huu 2016/2017.

    Hatua nyingine ni kuondoa wafanyakazi hewa 12,500 katika orodha ya waliokuwa wanalipwa mshahara na serikali, kudhibiti upotevu wa mapato serikalini, kutenga shilingi Trilioni moja kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani Standard gauge na pia akazungumzia hatua zilizochukuliwa dhidi ya wala rushwa na wanaojihusisha na ufisadi kwa kuunda mahakama ya mafisadi huku akiapa kuwa katika kipindi chake hakuna fisadi atakayeendelea kutamba.

    Akiwa njiani Rais Magufuli amewasalimu wananchi wa Ikungi na baadaye amefanya mkutano wa hadhara Singida Mjini ambako amesisitiza kuwa serikali yake haiko tayari kumvumilia mtu yeyote atakayekwamisha utekelezaji wa Ahadi na Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.

    Gerson Msigwa
    Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
    Singida

    29 Julai, 2016

    Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya July 30

    Rais Magufuli: Chadema Msiwape Vijana Viroba Ili Watangulie Kwenye Maandamanmo....Tangulieni Ninyi Viongozi Wao Ili Mkione Cha Mtema Kuni

    $
    0
    0

    Juzi Chama cha Demokrasia na maendeleo ‘CHADEMA’ kilitangaza mikakati mitatu ya kupinga ilichokiita ukandamizaji wa haki na demokrasia na kuitangaza siku ya September mosi mwaka kuwa ni siku ya maandamano nchi nzima.

    Jana July 29 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alianza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma, ambapo alizungumza na wananchi  wa Manyoni Singida na kutoa onyo kwa watakaoanzisha maandamano.

    "Wasije wakanijaribu mimi ni tofauti sana, na kama wapo watu wanawatumia wakawaeleze vizuri mimi sijaribiwi na wala sitajaribiwa, siasa nzuri wananchi wetu washibe, wapate madawa, nataka hao wanaotetea maandamano watangulie wao halafu wataona cha mtemakuni"- Alisema Rais Magufuli


    Hapa chini ni sauti ya Rais Magufuli sehemu ya kwanza na ya pili. Msikilize.

    Sehemu ya Kwanza



    Sehemu ya Pili

    Majengo ya Serikali Dar es Salaam kupigwa mnada ili wale wasiotaka kuhamia Dodoma, wahame kwa lazima

    $
    0
    0

    WAKATI suala la serikali kuhamia mkoani Dodoma likiwa dhahiri zaidi kila siku moja inayoongezeka, Rais John Magufuli ametangaza kuuza majengo ya wizara Dar es Salaam, mara atakapohamia yeye katika makao makuu hayo ya nchi.

    Akizungumza jana kwenye mkutano wa hadhara mkoani Singida, katika siku ya kwanza ya ziara yake itakayomfikisha mikoa minne, Rais Magufuli alisema atahakikisha anauza baadhi ya majengo hayo kwa mnada, ili wale wasiotaka kuhama, wahame kwa lazima. 

    Mbali na Singida, mikoa mingine atakayotembelea katika ziara hiyo aliyoanza jana ni Tabora, Shinyanga na Geita, ambako atazungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara.

    Katika mikutano hiyo, Rais Magufuli anatarajiwa kushukuru wananchi kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, na kueleza juhudi zinazofanywa na serikali kutatua kero zao na kuwaletea maendeleo.

    Majengo mazuri 
    Katika tangazo hilo, Rais Magufuli amesema majengo atakayoanza nayo, ni yale yanayotazama bahari; ambayo ndiyo mazuri zaidi, yenye mwonekano mzuri kutoka ofisini.

    “Atakayeng’ang’ania kubaki huko, ajue hana kazi wala mshahara. Hatuwezi kuendelea kukaa miaka hamsini tunaimba tu kuhamia Dodoma, wakati hatutekelezi uamuzi wetu hadi wengine wameshatangulia mbele za haki,” alisema.

    Alisema anajua akiitisha zabuni ya ofisi hizo, wateja watayakimbilia kwa wingi, hivyo wataong’ang’ania kubaki Dar es Salaaam, watakuwa wamejifukuzisha kazi wenyewe.

    Uamuzi huo wa serikali kuhamia Dodoma japo ni wa siku nyingi na utekelezaji wake ulikuwa ukifanyika kidogokidogo kwa baadhi ya wizara na ofisi nyeti kujenga majengo yake katika mji huo, lakini hivi karibuni umepata kasi ambayo haijawahi kupatikana, baada ya Rais Magufuli kutangaza kuhakikisha serikali yote inahamia Dodoma kabla ya 2020.

    Tamko hilo la Rais Magufuli lililotolewa wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM wiki iliyopita na kurejewa katika Sikukuu ya Mashujaa mwanzoni mwa wiki hii, liliungwa mkono mara moja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ambaye alitangaza kuharakisha umaliziaji wa ujenzi wa nyumba yake, ili ahamie katika mji huo Septemba mwaka huu.

    Wizara zenyewe
    Baadhi ya mawaziri waliohojiwa na vyombo mbalimbali vya habari, walikaririwa wiki hii wakisema kuwa suala hilo halina mjadala ni la kutekeleza mara moja. 

    Mbali na waliohojiwa, mawaziri na watendaji wakuu wengine serikalini, walitangaza muda maalumu kwa watendaji wao kuanza kuhamia katika mkoa huo.

    Miongoni mwa mawaziri hao, ni pamoja Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba, ambaye naye wiki hii alikutana na vyombo vya habari na kutangaza kuwa baadhi ya watendaji wa wizara hiyo, wataanza kuhamia Dodoma kuanzia wiki ijayo. 

    Dk Tizeba alikaririwa akisema tayari watendaji wa wizara hiyo wanaotakiwa kuhamia Dodoma wameanza kufanya maandalizi ya safari.

    Wakati Tizeba akitajwa kuwa waziri atakayewahi kuhamia pamoja na wizara yake Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa, naye alitaja utaratibu wa kuhamia Dodoma.

    Profesa Ntalikwa aliwataka wakuu wa idara na vitengo wote wa wizara hiyo, kuanza maandalizi ya kuhamia Dodoma na kuwa wametekeleza agizo hilo ifikapo Septemba, mwaka huu, muda ambao Waziri Mkuu naye anatarajiwa kuwa Dodoma.

    Agizo hilo la Wizara ya Nishati na Madini, liliwekwa katika waraka uliotolewa na watendaji na nakala yake kutumwa pia kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

    Madalali viwanja
    Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana jana alipiga marufuku uuzaji wa viwanja ndani ya mji wa Dodoma, baada ya kubaini kuwepo kwa kundi la madalali kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo kutoka Dar es Salaam kuhamia katika mji huo.

    Katika mkutano wake na waandishi wa habari Rugimbana alisema amepiga marufuku uuzaji huo mpaka baada ya siku 14 baada ya Waziri Mkuu kuhamia Dodoma, wakati Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), ikishirikiana na kikosi kazi kilichoundwa na serikali chini Ofisi ya Waziri Mkuu, watakapotoa utaratibu.

    Alisema kumezuka kundi la madalali kutoka mikoa mingine walioanza biashara ya viwanja na mashamba bila kufuata utaratibu na kanuni, hivyo uongozi wa mkoa wamezuia suala hilo, kwani linaweza kuvuruga na wananchi watakaotoa viwanja kwa madalali hao itakuwa imekula kwao.

    Lengo la serikali kwa mujibu wa Rugimbana, ni kuhakikisha kila Mtanzania mahali alipo anaweza kupata kiwanja huko alipo. Rugimbana alisema mji wa Dodoma ulipangwa siku nyingi; kila eneo na matumizi yake ya ardhi hivyo kuwataka wanaotaka kununua ardhi kuwa makini, ili wasiuziwe maeneo ya makaburi au masoko.

    “CDA watafanya kazi vizuri na Mtanzania yeyote anayeweza kununua eneo huko alipo bila ya kuja Dodoma na atakuja hapa wakati wa kukabidhiwa hati na kiwanja,” alisema.

    “Ndani ya siku 14 tutatoa maelekezo namna ya kupata viwanja Watanzania wawe watulivu utaratibu mzuri unakuja na hakuna Mtanzania ambaye anataka kujenga Dodoma atakosa kiwanja. 

    “Mtu anayetaka, asubiri na mfumo utakuwa wazi kwa kila mmoja na utaratibu wa kisheria utafuatwa,” alisema.

    Miji miwili
    Pamoja na hayo Mkuu huyo wa Mkoa alisema baada ya wizara mbalimbali kuhamia Dodoma, maeneo ya mjini yatakuwa kwa ajili ya biashara na mji wa serikali utakuwa kuanzia Ihumwa hadi Chamwino Ikulu ambapo zitajengwa ofisi za serikali.

    Kuhusu ofisi zitakazotumiwa na wizara mara baada ya kuhamia Dodoma mwaka huu, Rugimbana alisema watatumia ofisi zilizopo mjini kabla ya ujenzi katika eneo la Ihumwa ambako kutakuwa na ofisi hizo za muda.

    ‘’Wizara zikija Dodoma zitaanza kutumia ofisi zilizopo ambazo zilikuwa zikitumika awali kabla ya ujenzi wa ofisi katika eneo la Ihumwa kukamilika,’’ alisema.

    Alisema sababu ya kupeleka mji wa kiserikali Ihumwa, ni kuondoa msongamano wa magari kama ilivyo katika jiji la Dar es Salaam.

    Alifafanua kuwa kutakuwa na miji miwili; mji wa serikali utakaokuwa Ihumwa na mji wa kibiashara utakaokuwa katika Mji wa Dodoma. Aliwatoa hofu watumishi wa wizara mbalimbali watakaohamia Dodoma kuwa kuna nyumba za kutosha za wao kuishi.

    ‘’Dodoma tuna nyumba nyingi sana, watumishi hawawezi kukosa nyumba, tutawakodishia hata nyumba binafsi ili waishi,’’ alisema.

    Audio: Msikilize Rais Magufuli Akizungumzia Jinsi Atakavyoyapiga Mnada Majengo ya Serikali Dar na Atakachofanya Kwa Watumishi Watakaokataa Kuhama

    $
    0
    0

    Rais John Magufuli amesema azma ya Serikali yake kuhamia Dodoma haraka iwezekanavyo ipo pale pale huku akiwaonya wale wataong'ang'ania kubaki Dar es Salaaam kuwa watakuwa wamejifukuzisha kazi wenyewe.

    Alitoa msimamo huo mjini Singida jana kwenye mkutano wake wa kwanza wa hadhara  tangu achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka jana.

    Alisema kuwa licha ya kuhamia Dodoma atahakikisha anauza majengo ya wizara mbalimbali yaliyopo Dar es Salaam kwa mnada ili wale wasiotaka kuhama,wahame kwa lazima.

    Bonyeza Audio ya kwanza  na  ya Pili Kumsikiliza akiongea
     
    Sehemu ya Kwanza


     Sehemu ya Pili

    Bomba la mafuta Kutoka Uganda Hadi Tanga lahujumiwa.....Wananchi Waanza Kuvamia Ili Walipwe Fidia

    $
    0
    0

    WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (pichani), amewaonya wananchi wanaotaka kuvamia njia, litakapopita bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi katika bandari ya Tanga, kwa kujenga nyumba ili kulipwa fidia mradi utakapoanza.

    Aliwaeleza kuwa bomba hilo lililopewa jina la East Africa Crude Oil Pipeline, watakaovamia wanapoteza fedha zao na itakula kwao, kwani watatumia ramani ya satelaiti iliyopigwa Juni mwaka jana, muda ambao mazungumzo ya ujenzi wa bomba hilo yalianza.

    Akizungumza katika mkutano wa makatibu wakuu wa wizara zote pamoja na wakuu wa mikoa ambao bomba hilo linapita, Muhongo alieleza kuwa watu hao hawawezi kudanganya kwa lengo la kupata fedha wakidai kuwa bomba limewakuta.

    Alisema kuna satelaiti 1007 zinazofanya utafiti duniani na mpaka Agosti mwaka jana, zilikuwa zote zikifanya kazi hivyo kuonesha ni majengo gani yalikuwepo katika njia hiyo, hivyo kutaka wananchi wapewe ramani inayoonesha bomba litakapopita ili kuepusha gharama.

    Muhongo alisema leo atakutana na waziri wa Nishati wa Kongo kwa lengo la kujadiliana jinsi nchi hiyo itakavyoshirikishwa kwenye mradi huo mapema, huku akitarajia nchi ya Burundi kuungana katika mradi huo.

    Alisema hatua hiyo itawezesha bomba hilo kutumiwa na nchi hizo kupitisha mafuta.

    Burundi na Tanzania zinaendelea na utafiti katika ziwa Tanganyika na yakipatikana watatumia bomba hilo. Muhongo alisema pia wanatarajia kutumia bomba hilo kusafirisha mafuta kutoka Sudani kusini kutokana na kuwa ni rahisi kuyasafirisha mpaka Uganda na kutumia bomba hilo.

    Bomba hilo la mafuta linatara kutumia Dola za Marekani bilioni 3.5 mpaka litakapokamilika na kutaka katibu mkuu kuunda kamati maalumu ya kudumu ambayo itakuwa na wajumbe wawili au watatu kutoka kila wizara kuhakikisha mradi huo unakamilika.

    Waziri Mkuu Majaliwa Amjulia Hali Spika Wa Bunge, Job Ndugai

    $
    0
    0
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge , Job Ndugai wakati alipokwenda nyumbani kwa Spika jijini Dar es salaam kumsalimia Julai 29, 2016. Mheshimiwa Spika amerejea nchini hivi karibuni akitoka India kwa matibabu. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge , Job Ndugai wakati alipokwenda nyumbani kwa Spika jijini Dar es salaam kumsalimia Julai 29, 2016. Mheshimiwa Spika amerejea nchini hivi karibuni akitoka India kwa matibabu. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Bunge).

    Magufuli: Wapinzani Walisusia Vikao Vya Bunge Kwa Sababu Wanajua na Wao ni Part ya Mafisadi.....Naahidi Ntawanyoosha!!!!

    $
    0
    0
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana  July 29 2016 alianza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma ambapo alizungumza na wananchi kwa lengo la kuwashukuru kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kueleza juhudi zinazofanywa na serikali katika kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo.

    Akizungumza na wananchi wa Manyoni mkoani Singida Rais Magufuli alizungumzia kuhusu wabunge wa upinzani kususia bunge  kwa kujiziba  midomo na makaratasi 

    Alisema wabunge hao wa upinzani waliamua kususia  bunge kwa sababu kilichokuwa kikijadiliwa ndani ya bunge ni mahakama ya mafisadi na wao (wapinzani)  ni sehemu ya mafisadi .

    "Hawakuingia kwenye bunge kwa sababu walijua ni part ya hao mafisadi, nataka nieleze hawatapenya mbele ya serikali yangu, mafisadi lazima wanyooke" Alisema Rais Magufuli

    ==> Bonyeza hapo chini umsikilize akiongea

    Trafik wakusanya milioni 320 kwa siku nne Dar es Salaam

    $
    0
    0

    Jeshi la Polisi Kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Dar es Salaam limekusanya shilingi milioni 320.2 ambapo fedha hizo ni kutokana na tozo za makosa ya usalama barabarani.

    Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam Kamanda wa wa polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema fedha hizo ni kutokana na makosa 10,676 ambayo yamefanywa na watumiaji wa vyombo vya moto.

    ‘’Toka tarehe 25 hadi tarehe 28 tumefanikiwa kukusanya kiasi nilichotaja ambapo makosa mengi ya madereva wa bodaboda tumeanza kuona kwamba tunapowatoza faini ya elfu 30 au 60 haiwapi fundisho lolote ndiyo maana tumekuwa  tukiwapeleka mahakamani ili kupunguza matukio ya uvunjifu wa sheria barabarani’’ Alisema Kamanda Sirro

    Aidha Kamishna Sirro alitumia wasaa huo kuwataka watanzania kutii sheria bila shurti wanapokuwa wanatumia vyombo vya moto barabarani na katika maeneo yao ya kuishi.

    Kiwanda Maarufu Cha Dangote Chatozwa Faini Ya Shilingi Milioni 15 Kwa Uchafuzi Wa Mazingira.

    $
    0
    0

    Serikali kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limekitoza faini ya shilingi milioni 15, Kiwanda maarufu cha kutengeneza simenti cha Dagonte Industry limited  kilichopo  mjini Mtwara kusini mwa Tanzania,  kwa kosa la kukiuka sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.

    Katika siku ya Pili ya Ziara ya ziara ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Mkoani Mtwara Imebainika kuwa kiwanda hicho cha Dangote chenye muda wa miezi mitatu tangu kianze kazi ya kutengenza siment, kimefanya uchafuzi wa mazingira kwa kukosa sehemu maalum ya kuhifadhi taka katika kiwanda hicho, kutokuwa na utaratibu mzuri wa kuhifadhi taka zitokanazo na makaa ya mawe kiwandani hapo, kukosa vyoo kwa ajili ya matumizi ya wateja wao ambao ni madereva na makondakta wanao chukua mzigo wa siment kiwandani hapo, na kusafirisha kwenda sehemu mbali mbali za nchi, pamoja na kutokusakafia sehemu ya nje ya kiwanda hicho ambapo imeelezwa kuwa eneo hilo la nje wakati wa kipindi cha mvua mazingira yake huatarisha afya ya watumiaji wa eneo hilo.

    Kwa Mujibu  wa Naibu waziri Mpina, adhabu hiyo kwa kiwanda cha Dangote inayotakiwa kulipwa ndani ya wiki mbili, inaenda sambamba na urekebishaji wa kasoro hizo kiwandani hapo pamoja na kuhamsha uongozi wa kiwanda hicho kwa kudharau sheria ya mazingira, na kutaka kiwanda hicho kuajiri afisa mazingira ataeshughulia changamoto hizo.

    Kwa upande wake Meneja utumishi na utawala wa kiwanda hicho Bw. James Kajeli aliomba serikali kusamehe adhabu hiyo kwani kiwanda kilikuwa kwenye mpango wa kufanya marekebisho hayo na kuongeza kuwa kutokufanya hivyo kwa wakati ni kujisahau kwa kibinadamu, na kuwa utengenezaji wa baadhi ya miundombimu kiwandani hapo ulicheleweshwa na upatikani wa baadhi ya vibali kutoka katika taasisi za serikali na si kudharau sheria ya mazingira.

    Naibu waziri Mpina Pia alitembelea kiwanda cha kutengeneza gas cha Madiba na kukisifu kwa  utekelezaji wa sheria za mazingira na kuviasa viwanda vya serikali, kuwa mfano katika kutii sheria za mazingira.

    Ziara ya Mhe. Mpina pia ilihusisha ukaguzi wa kiwanda cha kubangua korosho cha micro mix cha mjini Mtwara, kiwanda cha gas cha Solvochemi pamoja na fukwe ya mnazi bay iliyoathiriwa na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
    Viewing all 45270 articles
    Browse latest View live




    Latest Images