Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Hatua iliyochukuliwa na serikali kuhusu madereva 18 waliogoma Bukoba

$
0
0
JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imesitisha leseni za madereva 18 kutokana na mgomo walioufanya kupinga wenzao kupelekwa mahakamani.

Wamiliki wa mabasi 12 ambayo madereva hao walikuwa wanaendesha kwenda sehemu mbalimbali nchini, wamepewa siku saba kujieleza ni kwa nini wasifutiwe leseni za kutolea huduma hizo pamoja na kutakiwa kusitisha ajira kwa madereva hao.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, alisema Julai 23 mwaka huu mkoani Kagera, madereva wa mabasi hayo walifanya mgomo kupinga kitendo cha madereva wenzao kupelekwa mahakamani, kukosa dhamana na kulala rumande kutokana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani ikiwamo kuendesha kwa mwendo kasi.

Kamanda Mpinga alisema dereva yeyote atakayeendesha gari kwa kasi ya zaidi ya kilometa 90 kwa saa atafikishwa mahakamani na sio kutozwa faini kama awali ili kuhakikisha matukio ya ajali yanapungua nchini.

Alisema kutokana na hali hiyo madereva wanaoendesha mabasi yanayoanza safari zake kwenye Manispaa ya Bukoba, walisitisha huduma kwa kushinikiza Mahakama iwaachie wenzao waliokamatwa kwa makosa ya mwendo kasi.

‘’Serikali haitavumilia kuona madereva wasiofuata sheria za usalama barabarani na sheria za kazi na ajira. Jeshi la Polisi ndio tunawapa madereva mafunzo, tunasajili vituo vya mafunzo na kuwapa leseni. Hivyo tunasitisha leseni zao kwa mujibu wa sheria kwa kukiuka kanuni za leseni,’’ alisema Mpinga na kuongeza kuwa askari watakaoachia madereva na kampuni za mabasi kutembea kwa zaidi ya kilometa 90 kwa saa watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Mkurugenzi wa Sumatra, Gilliard Ngewe, aliyataja mabasi pamoja na madereva waliositishiwa leseni kuwa ni Hussein Tegatega na Miraji Kondo wa Kampuni ya RS Express wanaoendesha basi lenye namba za usajili T 425 DDT aina ya Zongtong linalotoka Bukoba kwenda Dar es Salaam.

Said Omary na Amos Danney wa basi la Kimotico lenye namba za usajili T 966 CDY aina ya Nissan linalotoka Bukoba kwenda Arusha na madereva wanne wa mabasi ya Princess Muro yenye namba za usajili T 166 DCA na T 923 DCT yanayosafiri kutoka Bukoba kwenda Dar es Salaam.

Madereva hao ni Ally Mshuza, Twalibu Ondossy, Costa Andrew na Witness Lema.

Madereva wengine ni Musa Tindwa na Gerald Beti wa Kampuni ya Osaka Raha wanaoendesha basi lenye namba za usajili T 968 CPC linalofanya safari zake Bukoba kwenda Dar es Salaam na Paul Ngussa wa basi lenye namba za usajili T 810 BDW aina ya Scania linalotoka Bukoba kwenda Musoma, mali ya Kampuni ya Bunda Express.

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 20

$
0
0
Mtunzi: Enea Faidy

.....EDDY aliumia sana kwa taarifa zile za kifo cha mama yake. Hakutaka kuamini kama kweli mama yake hatakuwa pamoja nao tena. Machozi yalimbubujika kwa kasi huku akimwita mama take kana kwamba alikuwa karibu yake.

Mr.Alloyce alishindwa kuvumilia, alijikuta akiungana na mwanaye kulia. Walilia sana mpaka machozi yaliwakauka, Mr Alloyce alichukua leso yake na kujifuta machozi yake kisha akachukua simu ili awajulishe ndugu na marafiki kuhusu kifo cha mkewe.

Moyo wake ulisita sita sana kwani aliwaza ni jinsi gani ndugu wangeupokea msiba ule wa ghafla bila hata maiti.
"Eddy watanielewaje shemeji zangu? Umesababisha yote haya mwanangu, lakini siwezi kukulaumu!" Alisema Mr Alloyce huku machozi yakimlengalenga.
"Nisamehe dady kwa kuwa chanzo cha matatizo yote!" Alisema Eddy na kuendelea kulia.

Lakini hawakuwa na jinsi ya kufanya kwani tayari maji yalikwisha mwagika na ilikuwa vigumu sana kuzoleka. Ilibidi wakubaliane na kilichotokea ingawa kishingo upande sana.

Mr Alloyce alitafuta namba kwenye simu yake, MTU wa kwanza kumpata alikuwa shemeji yake aishiye jijini Dar ( Dada wa mama Eddy). Simu iliita kisha ikapokelewa, kwa kitete na woga Mr Alloyce akaanzisha mazungumzo.

"Halloo Shem"
"Niambie Shem wake mie.. Kwema huko?" Alisema shemeji yake Alloyce kwa uchangamfu sana kama ilivyokuwa kawaida yake. Hakuijua msiba mzito uliokuwa moyoni mwa Mr.Alloyce.
"Huku sio kwema Shem..!" Aliens Mr Alloyce.
"Sio kwema kuna nini?" Alishtuka.
"Sio kwema naomba kesho mfike nyumbani kwangu tafadhali.."
"Kuna nini shemeji? Naomba niambie tu.. Nini kimetokea?"
"Utajua kila kitu kesho..!"
"Hapana..niambie Leo.. Au MPE mama Eddy simu niongee nae..!" Maneno hayo yalimkata maini Baba Eddy hakuelewa ajibu nini akabaki kimya kwa sekunde chache akitafakari cha kujibu lakini ghafla akasikia sauti Kali ya Eddy ikimwita."Daaaaaaaaady!"

Mr Alloyce alishtuka sana kwani Eddy alikuwa ametoka sebuleni pale dakika chache zilizopita wakati yeye akiongea na simu. Hofu ikamkamata ghafla na kumfanya Mr Alloyce atupe simu sofani na kuelekea sauti ya Eddy inakotokea. Eddy aliita tena "Daaaaaaaady!" Mara hii sauti ile iliambatana na mwangwi mkali uliozidi kumtisha Mr Alloyce.

Alitoka sebuleni na kwenda koridoni lakini hakumuona Eddy. Akasikia sauti ikitokea chooni, alikimbia haraka na kwenda chooni lakini hakumuona, ghafla sauti ya Eddy ikasikika tena ikitokea chumbani kwa Eddy ilibidi amfuate haraka lakini cha kusikitisha Mr Alloyce hakumkuta Eddy ila alikuta damu nyingi zikiwa sakafuni. Alishtuka sana.

Mshtakiwa wa Kuiba Milioni 7 kwa dakika Aongezewa Kesi Nyingine

$
0
0

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) leo inatarajiwa kuwapandisha kizimbani wafanyabiashara wawili akiwemo Mohamed Mustafa Yusufali ‘Choma’ aliyewahi kutajwa kuwa anajipatia Sh milioni saba kwa dakika moja kwa njia za udanganyifu katika mapato ya serikali.

Choma na mfanyabiashara wa Arusha, Samweli Lema, walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana saa 9 mchana kwa ajili ya kusomewa mashitaka yanayowakabili, lakini ilishindikana kwa sababu muda ulikuwa umekwisha.

Washtakiwa hao waliondolewa katika viwanja vya mahakama hiyo jioni na kurudishwa mahabusu kwa kutumia magari ya Takukuru, hivyo leo wanatarajiwa kupandishwa kizimbani kwa ajili ya kusomewa mashitaka yao.

Choma atakuwa anakabiliwa na kesi mbili kwa wakati mmoja, kwa kuwa Julai 12 mwaka huu, alifikishwa mahakamani hapo na wenzake wakikabiliwa na mashitaka 199 likiwemo la kuisababisha serikali hasara ya Sh bilioni 15.6.

Awali kesi ya kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 15.6 inayomkabili Choma na wenzake Alloyscius Gonzaga Mandago, Isaack Kasanga, Taherali Sujjauddin Taherali na Mohamed Kabula ilitajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa. 

Aidha, aliiomba Mahakama iwaruhusu kumchukua Choma kwa ajili ya kumhoji kutokana na tuhuma mpya zinazomkabili na kuahidi kumrudisha mahakamani kabla saa za kazi hazijaisha.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Shahidi alimuuliza mshtakiwa huyo kama ana lolote la kusema, alikaa kimya lakini baadaye alidai kuwa ameelewa na atakuwa tayari endapo wakili wake atakuwepo kwenye mahojiano hayo.

Hakimu Shahidi aliruhusu upande wa Jamhuri umchukue mshtakiwa huyo na kuahirisha kesi hiyo hadi Agosti 5, mwaka huu. 

Choma ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Superior Financing Solution Limited kwa mara ya kwanza alifikishwa mahakamani hapo Julai 12, mwaka huu akikabiliwa na mashitaka 199 ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo, uhujumu uchumi utakatishaji fedha na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 15.6.

Katika mashitaka ya kughushi inadaiwa alighushi hati za usajili kuendesha kampuni 15 ikiwemo Festive General Business Limited zimesajiliwa kihalali nchini jambo ambalo si kweli. Aidha, anadaiwa kuwasilisha nyaraka hizo za kughushi kwa Kamishna wa Kodi Ofisi za TRA Mkoa wa Kinondoni ili kuonesha kampuni hizo zimesajiliwa na zinastahili kusajiliwa kama mlipa kodi.

Mbali na mashitaka hayo, washtakiwa wote wanadaiwa kutakatisha fedha, kwa kuficha uhalali, chanzo na mzunguko wa Sh 1,895,885,000 kwa kuzikopesha fedha hizo kwa watu mbalimbali na kupokea marejesho ya mikopo huku wakijua fedha hizo zimetokana na njia zisizo halali za kughushi na kukwepa kodi.

Yusufali anadaiwa kati ya Januari 2008 na Januari mwaka huu, kwa vitendo viovu vya kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo kwa Kamishna wa TRA, ameisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 15.6 ambazo zilitakiwa kulipwa kama Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

Mchungaji Anthony Lusekelo Adai Lowassa ni Tishio CCM......Asema Uchaguzi Umekwisha, si Busara Kuendelea Kumpiga V ijembe

$
0
0
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) la Ubungo jijini Dar es Salaam, Anthony Lusekelo maarufu ‘Mzee wa Upako’ amesema kitendo cha viongozi wa CCM kulitaja zaidi jina la Edward Lowassa katika Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho ni ishara kuwa Waziri Mkuu huyo wa zamani ni tishio.

“Nani! Lowassa…. jina lake kutajwa sana katika vikao vya CCM. Hiyo inaashiria kuwa ni mtu tishio. Ndiyo ni tishio,” alisema Lusekelo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam

Lusekelo ambaye hivi karibuni, Rais John Magufuli alishiriki ibada katika kanisa lake, alimzungumzia Lowassa baada ya kuulizwa swali juu ya mtazamo wake kuhusu Mkutano Maalumu wa CCM ambao jina la mgombea huyo wa urais kupitia Chadema na Ukawa lilitajwa na makada wengi wa chama hicho tawala. 

Alisema hilo lilidhihirika hata katika mchakato wa CCM kupata mgombea wake wa urais, kutokana na Lowassa kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa. 

Alisema kitendo cha Waziri Mkuu huyo wa zamani kuzua mjadala katika Mkutano Mkuu wa chama hicho tawala sambamba na wimbi la makada wanaohama vyama vyao, si mambo yanayopaswa kuwa mjadala kwa sababu uchaguzi ulishapita. 

Huku akisema: “Sizungumzi haya kwa ajili ya kujipendekeza, sihitaji ukuu wa wilaya,” Lusekelo aliwataka viongozi kukataa kuendeleza uhasama wa kisiasa na chuki kwa maelezo kuwa mwaka huu uwe maalumu kuzika tofauti hizo, kufanya kazi kulijenga Taifa na kuhubiri amani na umoja. 

Katika mkutano huo, Lusekelo alipongeza kuimarika kwa vyama vya upinzani akaponda mvutano ulioibuka bungeni akisema kukosa uzoefu kwa Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kulichangia huku akiunga mkono kauli ya Rais kuzuia shughuli za siasa na kubainisha jinsi Rasimu ya Katiba ya Tume ya Jaji Joseph Warioba, ilivyopendekeza kupunguzwa kwa madaraka ya Rais. 

Jumamosi iliyopita, katika Mkutano Mkuu wa CCM mjini Dodoma, uliomalizika kwa Rais Magufuli kuchaguliwa kuwa mwenyekiti, mzimu wa Lowassa ulitawala kutokana na kila aliyepewa nafasi ya kuzungumza ama kumtaja kwa jina au kwa mafumbo. 

Mwenyekiti wa CCM aliyemaliza muda wake, Jakaya Kikwete ndiye aliyeanza kuzungumzia hali ya mchakato wa chama hicho kupata mgombea wake wa urais, kuwaulikuwa mgumu na majaribu makubwa na kwamba wazee walifanya kazi kunusuru hali hiyo.

Katika mchakato huo, CCM ilikata jina la Lowassa katika hatua za awali, jambo lililosababisha kiongozi huyo kuhama na kundi la wanaCCM na kujiunga na Chadema ambayo ilimteua kuwa mgombea wake wa urais. 

Hata hivyo, katika mkutano wake wa jana, Lusekelo alisema katika mchakato wa chama hicho tawala kupata mgombea wake wa urais kulikuwa na watu wenye majina makubwa, akiwamo Lowassa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe. 

“Niliwaambia CCM, Membe huwezi kumpuuza, Lowassa naye huwezi kumpuuza maana wanataka madaraka na kwa vyovyote lazima mtapata mtikisiko. Nikawaomba waahirishe suala la kupata Katiba Mpya maana wasingelimaliza na muda ulikuwa mfupi,” alisema na kuongeza: “Kama mwaka huu hautatumika kutibu majeraha yaliyotokea huko nyuma, tutaharibikiwa sana.” 

Alisema mchakato wowote wa uchaguzi na kura ya maoni ndani ya vyama huacha mpasuko na watu hutumia dini na ukabila kubaguana, hivyo lazima baada ya uchaguzi mambo hayo yamalizwe. 

“Tunapaswa kukumbuka kuwa wote ni Watanzania tusahau uchaguzi. Sasa ni wakati wa kuijenga nchi. Amani inatengenezwa, na Mungu huwapa hekima maana kujenga ni kazi na kubomoa ni rahisi, huu ni mwaka wa uponyaji na kurejesha Taifa pamoja,” alisema Lusekelo. 

Alisema kuanza kubagua watu kwa sababu walitoka CCM kwenda Chadema au kutoka Chadema kwenda chama tawala si jambo sahihi huku akitolea mfano mataifa yaliyovurugika kwa kuendekeza siasa za chuki na uhasama. 

Yaliyotokea bungeni 
Akizungumza yaliyotokea bungeni na kusababisha wabunge wa Ukawa kususia vikao vya Bunge vilivyoongozwa na Dk Tulia, Lusekelo alisema Mtanzania anayejua historia ya nchi yake hawezi kufumbia macho suala hilo. 

“Binafsi nawalaumu waliotoka (wabunge wa upinzani) na waliobaki (wabunge wa CCM). Kushindana si kuzuri. Mbatia (James Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi) na wenzake wanapaswa kujua kuwa naibu spika ni mchanga katika siasa waende naye taratibu maana kapewa ubunge tu na kuwa naibu spika,” alisema. 

Huku akiponda uamuzi wa Serikali kufuta urushwaji wa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge alisema: “Nashangaa wazee kama Salim (Ahmed Salim – Waziri Mkuu mstaafu), Pinda (Mizengo – Waziri Mkuu mstaafu) na Warioba. Sijui walishindwa nini kukaa na wabunge hawa ili kumaliza tofauti zao.”

Alisema si jambo jema kuongoza nchi kwa mabavu na kusisitiza kuwa hata uhuru ulipatikana kwa mazungumzo. 

Mchungaji huyo aliusifu utawala wa Rais Magufuli kuwa una kasi kubwa na kwamba licha ya wananchi kulia ukata, watacheka baada ya mwaka mmoja huku akiwananga wanaomponda Kikwete kuwa hawajui mazuri aliyoyafanya. 

Awapongeza wapinzani 
Akizungumzia nguvu ya vyama vya upinzani, Lusekelo alisema ushindani wa kisiasa umekuwa mkubwa kutokana na kuimarika kwa upinzani:“Chadema ya sasa si ile ya miaka ya 1990. Wanaongoza miji mikubwa na ukiona chama kina wabunge 40 usikipuuze. Hata nguvu ya mfalme ni watu.” 

Mikutano ya siasa
Kuhusu kauli ya Rais kusitisha shughuli za siasa hadi mwaka 2020, alisema jambo hilo linaweza kuonekana baya lakini lina unafuu mkubwa, kwamba Kenya wamelifanya na kufanikiwa kumaliza tofauti za kisiasa. 

“Hivi watu 10,000 wakiandamana na kusema Magufuli aliiba kura itakuwaje? Tuna askari wa kuwazuia! Nadhani wanasiasa wafanye kazi ya utawala katika vyama vyao. Tutulie kwanza tutibu majeraha. Hakuna jambo baya kama kuwaongoza watu wenye njaa maana hawana la kupoteza,” alisema. 

Hata hivyo, Lusekelo alisema Rasimu ya Katiba ilipendekeza Rais kupunguziwa madaraka na huenda madaraka makubwa aliyonayo Rais yakawa sababu ya nchi kuendelea kuwa na amani. 

“Kenya kuzuia maandamano ni ngumu sana lakini hapa kwetu hadi Zitto (Kabwe-Kiongozi wa ACT-Wazalendo) alizuiwa kufanya mkutano wa ndani. Kwetu rais ana madaraka makubwa sana,” alisema huku akiwataka polisi kutekeleza wajibu wao vyema, wakikumbuka kuwa nao ni binadamu.

TCU yakanusha taarifa za kuvifungia udahili wa kozi tofauti vyuo 22 zilizozagaa juzi

$
0
0
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imewatoa hofu wanafunzi waliohitimu katika vyuo vilivyozuiwa hivi karibuni kufanya udahili, huku ikikanusha taarifa za kuzifungia udahili wa kozi tofauti vyuo 22 zilizozagaa juzi.

Hivi karibuni TCU ilitangaza kusimamisha kufanya udahili  vyuo vitano baadhi vikiwamo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Francis cha Ifakara Morogoro, Chuo cha Mtakatifu Joseph cha Dar es Salaam na Chuo cha IMTU cha Dar es Salaam vyote kwa kozi ya udaktari.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa TCU, Eliuther Mwageni alisema kufungiwa kwa vyuo hivyo ni kwa muda mpaka vitakapokabidhi vigezo vinavyotakiwa.

"Kuna vigezo vinavyotakiwa kufikiwa ili chuo kiweze kusajiliwa  na hivi vyuo hatujavifungia ila tumevisimamisha kwa muda mpaka vikidhi vigezo vyetu.

Kuhusu taarifa za vyuo 22 kusimamishwa kudahili wanafunzi katika kozi mbalimbali zilizozagaa kwenye mitandao juzi na jana, Mwageni alisema taarifa hizo ni za uzushi, zina lengo baya hivyo hazina ukweli wowote.


Koffi Olomide akamatwa DR Congo

$
0
0
Mwanamuziki mashuhuri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amekamatwa akiwa nyumbani kwake mjini Kinshasa.

Mwanamuziki huyo amekamatwa kwa agizo la ofisi ya mwendesha mashtaka.

Olomide alitimuliwa kutoka nchini Kenya baada ya video kuonekana akimpiga teke mnenguaji wa kike katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta mapema asubuhi baada yake kuwasili.

Alipangiwa kutumbuiza mashabiki wake Bomas of Kenya siku ya Jumamosi lakini tamasha hiyo ikaahirishwa.

Alikamatwa Ijumaa usiku na maafisa wa polisi wa Kenya na siku iliyofuata asubuhi akaingizwa kwenye ndege na kurejeshwa Kinshasa.

Katika hatua nyingine, waandalizi wa tamasha ambalo Olomide alipangiwa kutumbuiza nchini Zambia pia walitangaza kufuta hafla hiyo kutokana na yaliyotokea Nairobi.

Mwanamuziki huyo, akiandika kwenye ukurasa wake wa Facebook Jumapili, aliomba radhi mashabiki wake na hasa “wanawake na watoto”.

“Najutia sana yaliyotokea… kilikuwa ni kipindi kifupi cha wenda wazimu,” aliambia kituo cha televisheni cha taifa cha RTNC.

Baadaye, aliomba msamaha kutoka kwa raia wote wa DRC ambao huenda alihisi kwamba tabia yake iliwavunjia heshima.

Waziri wa masuala ya vijana na jinsia Kenya, Sicily Kariuki katika taarifa kwa vyombo vya habari baada ya video iliyoonyesha tukio hilo kusambaa, alipendekeza Olomide azuiwe daima kutembelea Kenya.

Kikwete: Nashukuru Mungu Kwa Kuutua Mzigo Salama Huku Nikiiacha Nchi Ikiwa Salama Tulii Kabisa

$
0
0
Na David John Pwani
MWENYEKITI Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Jakaya Kikwete amesema anashukuru Mungu Kwa kuutua mzigo salama huku akiicha nchi ikiwa salama tulii kabisa.

Amesema kuwa safari yake ya urais ilianzia Bagamoyo akitokea wilayani hapo ambapo baada ya hapo alikwenda Kibaha kutangaza nia ya kugombea urasi nakudai kuwa amejisikia furaha kurudi tena Bagamoyo akiwa salama.

Amesema wakati akielekea kutangaza nia ya kugombea urais alikuwa na mtoto wake Ridhiwani Kikwete ambapo yeye alikuwa anaandika na Ridhiwani anachapa kwenye Komputa.

Dkt.Kikwete aliyasema hayo jana wilayani Bagamoyo katika hafla ya kumkaribisha Nyumbani baada ya kuitumikia nchi Kwa miaka mingi, ambapo iliandaliwa na Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani.

Alisema anashukuru Kwa Mara nyingine kurudi mahala alipoanzia na kwamba amemaliza salama na ameacha nchi ikiwa salama na imetulia tulii kama Maji kwenye mtungi.

Akikumbuka mchakato wa mwaka jana wa kumpata Mgombea ulikuwa na mambo mengi lakini mambo yalikwenda salama na hakuna lililokuwa limeharibika .

"Ilikuwa Kazi kubwa si ndogo lakini hatimaye wa kavuka na wakaingia kwenye uchaguzi ambao ulikuwa na vurumai" alisema Dkt.Kikwete .

Aidha alisema kuwa hata hivyo katika uchaguzi huo kulikuwa hakuna mtu ambaye alipatwa na tukio la kumpiga mwezake hali ambayo iliwashangaza hata nchi jirani.

Alisema kuwa katika kipindi chake cha uongozi amefanya kazi kubwa ya kusukuma maendeleo ya wananchi Kwa mikoa yote,wilaya zote bila ubaguzi wowote ule huku akikiri kukabiliana na Changamoto ya kunyoshewa vidole hususani pale alipojaribu kupeleka maendeleo Wilayani Bagamoyo kanakamba wananchi wa Bagamoyo walikuwa hawana haki.

Aidha Dkt.Kikwete alisema kuna wakati alisimamisha fedha za ujenzi wa barabara hiyo na kupeleka fedha hizo kujenga barabara ya Geita, Sengerema,usagala ,na kulizuka na Maneno mengi dhidi yake na hadi kufikia wabunge kulumbana.

Alisema hata hivyo anashukuru kwamba amemaliza salama na Kwa bahati nzuri amepatikana rais ambaye ana ari kubwa ya kuwaletea maendelea watu huku akitaka watanzania kumuunga mkono.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Julyt 27


Picha: Zitto na Maalim Seif walivyokutana kwenye mkutano Marekani

$
0
0

Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wamekutana Katika Mkutano Maalum wa Viongozi wa Kisiasa Ulimwenguni (International Leaders Forum) ambao umefanyika jana  ‘Kwa Saa za Marekani’ Jijini Philadelphia.

Mkutano huo ulioandaliwa na asasi ya NDI ‘National Democratic Institute’, ni Sehemu ya matukio maalum kuelekea Mkutano Mkuu wa Chama Cha Democrats (Democratic National Convention), Mkutano ambao utamthibitisha Bibi Hillary Clinton Kuwa Mgombea Urais Kupitia Chama Hicho.

Zitto Kabwe Pamoja Na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim watakuwa Philadelphia mpaka Siku ya alhamis ambapo  mkutano huo unategemewa kumuidhinisha Bi Hillary Clinton Kuwa Mgombea Urais wa Marekani kupitia Chama Hicho.

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) yamkubali Rais Magufuli.....Yamuahidi msaada zaidi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  tarehe 26 Julai, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Frannie Leautier katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma, ambapo ameishukuru benki hiyo kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Tanzania  hususani kutoa mikopo iliyowezesha ujenzi mkubwa wa barabara.

Pamoja na kuishukuru AfDB Rais Magufuli ameiomba benki hiyo kuendelea kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa mipango na miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mpango mkubwa wa uzalishaji wa nishati ya umeme utakaofanikisha ujenzi wa viwanda, ujenzi wa barabara zinazounganisha ndani na nje ya Tanzania na kuunga mkono juhudi za kukabiliana na rushwa.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa AfDB Dkt. Frannie Leautier amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi kubwa alizozianza katika kujenga uchumi wa Tanzania, kukabiliana na rushwa na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya serikali na ameahidi kuwa benki hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi hizo kwa kutoa mikopo ya masharti nafuu itakayofanikisha mipango na miradi mbalimbali ya Tanzania.

"Tanzania ni nchi ambayo inapata fedha kuliko nchi zote za Afrika katika mpango wa AfDB kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Afrika,  hizi ni fedha ambazo zinatolewa kwa mkopo nafuu zaidi kuliko mikopo mingine" Amesema Dkt. Frannie Leautier.

Dkt. Frannier Leautier amebainisha kuwa AfDB inatarajia kuwa Tanzania itanufaika kupitia vipaumbele vitano vya benki hiyo ambavyo ni kusaidia uzalishaji wa nishati, utangamano wa bara la Afrika, maendeleo ya viwanda, usalama wa chakula na kuboresha hali ya maisha.

Aidha, Makamu wa Rais huyo wa AfDB amesema kuanzia mwakani benki hiyo imepitisha miradi mikubwa mitatu kwa ajili ya Tanzania ambayo ujenzi wa nyumba ya makazi, utoaji wa mikopo vijijini kwa ajili ya kuendeleza kilimo na maeneo ya uchumi kupitia benki ya CRDB na kukiendeleza Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Nelson Mandela kilichopo Arusha ambapo benki hiyo itatoa Dola za Marekani Milioni 4.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Mwakilishi Mkazi wa AfDB Dkt. Tonia  Kandiero, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma

26 Julai, 2016

Waziri Mkuu Aongoza kikao cha wadau kujadili utekelezaji wa Serikali kuhamia dodoma ....... Awapa siku 14 wakamilishe na kumkabidhi mpango kazi wao

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Serikali kuhamia siyo siasa kama watu wanavyodhani bali ni utekelezaji wa maamuzi kamili na kwamba Serikali inakamilisha eneo la kisheria juu ya uamuzi huo.

“Hapa tulipofika ni hatua ya utekelezaji wa pamoja na hakuna namna nyingine kwa sababu uamuzi umeshatolewa. Nataka niwahakikishie kwamba hii siyo siasa, tunachokamilisha ni eneo dogo tu la kisheria juu ya uhamishaji wa makao makuu kuja Dodoma na katika Bunge la Septemba sheria hii itapitishwa,” amesema.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumanne, Julai 26, 2016) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa, Serikali za mitaa, viongozi wa dini, wajasiriamali, wazee wa mji huo, wasafirishaji, wafanyabiashara, wakuu wa taasisi za elimu, za kifedha na watoa huduma mbalimbali katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Hazina ndogo mjini Dodoma.

Waziri mkuu ambaye aliitisha kikao cha kazi na wadau hao mjini Dodoma, ameutaka uongozi wa mkoa huo pamoja na wadau wake wakae na kuandaa mpango kazi wa jinsi ya kupokea na kutekeleza uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma.

Pia ametoa siku 14 kwa uongozi wa mkoa wa Dodoma kukamilisha mpango kazi wao na kumkabidhi mapendekezo yao ili yaweze kuingizwa kwenye mpango mkubwa wa Serikali kuu.

“Uongozi wa Mkoa, ukishirikiana na Ofisi yangu kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais TAMISEMI usimamie na kuyaratibu majukumu haya. Ndani ya siku 14 nipate proposal ya kwanza namna mtakavyoyatekeleza. Naagiza kiundwe kikosi kazi chini yenu kitakachowajumuisha makundi yote niliyoyataja,” amesema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu amesema chimbuko la uamuzi wa kuhamia Dodoma kuifanya makao makuu ya Serikali lilikuwa ni ndoto ya Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambayo imeendelea kudumu katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ikiwemo Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2015 chini ya Ibara ya 151.

“Napenda kumshukuru Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, na viongozi wengine wote wa Chama kwa  kusimamia  ndoto ya Baba wa Taifa ya kuhamishia  Makao Makuu hapa Dodoma. Ni imani yangu kuwa wananchi wote mtaunga mkono uamuzi huu muhimu kwa Serikali yetu na wananchi kwa ujumla, amesema.

Akiweka msisitizo juu ya kazi kubwa inayowakabili viongozi hao, Waziri Mkuu amesema masuala yanayotakiwa kufanyika kuanzia sasa ni pamoja na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) kuhakikisha eneo la makazi ya Serikali Kuu litakalotumika kwa ofisi za wizara na taasisi zake, makazi ya watumishi na huduma za biashara elimu na taratibu zote za kisheria za kulitwaa zinakamilika kwa haraka na linakuwa tayari kwa matumizi.

“Natambua kazi iliyopo mbele yetu ni kubwa na inahitaji jitihada za pamoja. Hivyo kila taasisi na mtu mmoja mmoja ana jukumu la kuhakikisha kuwa tunajipanga vizuri na kuweka mazingira ya ujio wa Serikali katika maeneo yote muhimu,” amesema.

Amezitaka Mamlaka za Mipango Miji na hasa CDA wahakikishe wanaweka mfumo mmoja wa upatikanaji wa viwanja ambao utajulikana na kila mmoja, utakuwa wazi usio na urasimu. “Mfumo huu wa viwanja uwekwe kwenye mfumo wa kompyuta na uuzaji wa viwanja hivyo uwe wa kieletroniki kuepusha udanganyifu kutoka kwa madalali,” amesisitiza.

Waziri Mkuu ameonya CDA na Manispaa zisibadili ramani ya mipango miji iliyokwishawekwa awali kama vile maeneo ya wazi kutumika tofauti na makusudio yaliyokusudiwa na akaagiza maeneo hayo yote yarejeshwe na kufufuliwa.

“Natambua katika makazi hapa Dodoma kulitengwa maeneo ya vituo maalum vijulikanavyo kama D Centers kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali. Cha ajabu sasa kuna magenge, groceries na sasa naagiza kwa hadhi ya Makao Makuu haya maeneo sasa yatumike kuwekeza maduka makubwa (shopping malls) ambamo huduma zote mbalimbali hupatikana,” amesema.

Ameitaka Manispaa iboresha usafi wa mazingira na bustani zake kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali kuzitunza. Pia ameitaka manispaa ya mji huo ishirikiane na TANROADS kuboresha barabara zote za mitaa na taa za barabarani mji ukae kisasa, na usalama uwe bora zaidi.

“Eneo jingine muhimu ni Manispaa na CDA kuhamisha makundi mbalimbali ya wafanyabiasahra na huduma za masoko yasiyo rasmi na kuyapa maeneo yaliyo rasmi na bora zaidi.  Hii ni pamoja na maeneo ya maegesho ya bajaji, bodaboda, taxi na daladala. Pia mazingira ya Stendi Kuu yaboreshwe, vyoo vya kulipia pia vijengwe katikati ya mji,” amesisitiza.

Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa Wakala wa majengo (TBA) waorodheshe majengo yote ya Serikali na taasisi zake yanayotumika kwa sasa na yasiyotumika, “Nataka muyawekee utaratibu maalum wa matumizi yake ili tupate kujua yanayoweza kutumika kwa muda kwa baadhi ya wizara na taasisi zake. Hii ni pamoja na jengo jipya la Mkuu wa Mkoa, linaloendelea kujengwa.”

Amewataka wakazi wa Dodoma watumie fursa hiyo kujenga nyumba za kuishi za kutosha, nyumba za kulala wageni na mahoteli ili watu watumishi na wageni wanapokuja wasipate taabu mahali pa kuishi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.

JUMANNE, JULAI 26, 2016.

Ajali: Basi la UDA lagonga Treni Kariakoo....Mmoja Afariki, 45 Wajeruhiwa

$
0
0
Basi la UDA lenye namba za usajili T 696 CVP limegonga treni katika eneo la Kamata Jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo  wakati Basi hilo likotokea stendi ya Gerezani Kariakoo kuelekea Mbagala na kuua mtu mmoja na wengine zaidi ya 45 kujeruhiwa.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Ernest Matiku amesema majeruhi wamepelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu.

Hata hivyo, hakuweza kumtaja jina mtu huyo aliyefariki dunia.

“Ni kweli ajali imetokea kuna kifo cha mtu mmoja na watu wengi wameumia sana ,” amesema Kaimu kamanda huyo.

Majambazi sasa kukamatwa kielektroniki

$
0
0
SERIKALI imeanza mkakati mpya wa kuandikisha wananchi waliopo kwenye vijiji na vitongoji kwa njia ya kielektroniki ili kupata takwimu sahihi zitakazosaidia utoaji wa huduma bora kwa jamii.

Pia mfumo huo utatambua watu wadanganyifu ambao wamekuwa wakidanganya wanakotoka, ikiwemo wezi na majambazi ambao ni lazima waeleze wanakoishi, wanakotokea, jina la mkuu wa kaya wake na namba ya utambulisho wake.

Mfumo huo ambao utasaidia kujua watoto waliozaliwa na watu waliokufa, taarifa zitakazotolewa kwa Mtendaji wa Serikali za Mitaa ambaye atarekodi kwa njia ya simu na taarifa hizo zitafika moja kwa moja kwenye Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ambao wataweka kumbukumbu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mussa Iyombe alisema kuwa ili kufanikisha uhakiki huo, serikali imetenga Sh bilioni 1.6 wakati wahisani wamechangia Sh bilioni 1.4.

Iyombe alisema takwimu hizo pia zitaisaidia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Wakala wa Udhamini na Ufilisi (RITA) katika utoaji wa vitambulisho na hati za kuzaliwa na vifo. Aidha, alisema lengo ni kuhakikisha kila mtu anatumia kitambulisho kimoja pekee kumtambulisha kuliko ilivyo sasa kwamba watu wanakuwa na vitambulisho zaidi ya saba.

"Hii itakuwa dawa ya kuwatambua majambazi, wezi, wahamiaji wa kigeni na hata watoto wanaozaliwa na vifo. Mtendaji wa mtaa atakuwa anarekodi taarifa hizo kutoka kwa mkuu wa kaya ambapo ataeleza watoto waliokuwepo, wapangaji wangapi. Mpangaji pia akitaka kuhama ni lazima aseme anakwenda wapi ili aweze kupokelewa anakokwenda," alisema Iyombe.

Kwa mujibu wa Iyombe, awali walikuwa wanatumia madaftari katika kusajili watu waliopo kwenye vijiji na vitongoji hali ambayo ilikuwa na changamoto kutokana na watendaji wengine kutojaza taarifa za wakazi wao.

Alisema kuwa serikali imekuwa ikikosa taarifa muhimu za awali na kuamua kuanza mfumo huo ambao utafanyika nchi nzima kwa miaka miwili.

Aliongeza kuwa kwa kushirikiana na Chuo cha Takwimu Kusini mwa Afrika waliamua kuanza mfumo huo Kata ya Mapinga wilayani Bagamoyo na kwamba wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Alisisitiza kuwa sensa ya mwaka 2022 itatumia taarifa zitakazokusanywa kwa kipindi cha miaka miwili ijayo ili kuondoa ubabaishaji uliokuwa unafanywa awali.

Pia alisema kwa sasa nchi inapopatwa na janga lolote hutumia taarifa zisizo rasmi kwa ajili ya kutoa msaada, hivyo vijiji vingine kuona kuwa serikali haiwasaidii wanapopatwa na matatizo. 

Kwa upande wake, Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi, Amina Said alisema kuwa kabla ya sensa nyingine Tamisemi wawe wamemaliza uhakiki wa watu kutumia mfumo huo.

Alisema kuwa katika nchi zinazotumia mfumo huo, hakuna sensa kwa kuwa wanazo taarifa sahihi za watu wao.

 "Mfumo huu utaingiza watu wapya na kuwatoa waliokufa ili kufanya makadirio mazuri yatakayosaidia kuwatambua watu wote ikiwemo wavamizi pia itapunguza muda wa kupata idadi ya watu," alisema Said.

Pia alisema kuwa wasimamizi wakubwa wa mfumo huo ni Tamisemi hivyo wananchi washirikiane na viongozi wao kutoa taarifa sahihi ili kuwatambua na si kwa nia mbaya. 

Hata hivyo alisema kuwa kupitia mfumo huo itasaidia wanafunzi kuandikishwa kwenye shule zilizopo maeneo yao kuliko kuandikisha watoto nje ya kata ya mwanafunzi.

Aliwataka wanasiasa na viongozi wote watambue na kushiriki katika kuwaelimisha wananchi na kuwatoa hofu kuhusu mfumo huo ili kutoa huduma bora za jamii. 

Naye, Diwani wa Kata ya Mapinga Bagamoyo ambaye kata yake imefanyiwa majaribio, Ibrahim Mbonde alisema kuwa ameandikisha kaya 341 kwa njia ya kielektroniki na kwamba mfumo umeonesha mafanikio makubwa.

Mbonde alisema serikali imeondoa gharama za kununua madaftari kwa ajili ya uhakiki ambavyo vilikuwa havijazwi. Alisema walikuwa wanashindwa kupata taarifa za watu ikiwemo wajawazito wanaojifungulia nyumbani na wanaokufa na kusababisha kuwepo kwa takwimu za kukisia.

"Kila kaya inakuwa na namba yake hivyo mtu anayeenda kuhakiki na kutaja namba tofauti hutambulika kuwa mdanganyifu. Kwa mfano kwangu watu wapo 23,000 ni lazima tungenunua madaftari mengi, njia hii itasaidia kuleta maendeleo ya Taifa," alisema Mbonde.

Wizara ya Kilimo yatangaza kuhamia Dodoma wiki ijayo

$
0
0

KATIKA kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kutaka serikali kuhamia Dodoma, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba amesema watendaji wa wizara hiyo wataanza kuhamia Dodoma kuanzia wiki ijayo.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa amewataka wakuu wa idara na vitengo wote wa wizara hiyo kuanza maandalizi ya kuhamia Dodoma na kuwa wametekeleza agizo hilo ifikapo mwezi Septemba, mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Dk Tizeba alisema tayari watendaji wa wizara hiyo wanaotakiwa kuhamia Dodoma wameanza kufanya maandalizi ya safari.

Alitoa dokezo hilo mara baada ya kutoa taarifa kuhusu Mkutano wa Ushirikishwaji wa Wadau kwenye Sekta ya Uvuvi, unaoishirikisha pia Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na wadau mbalimbali.

“Ni kweli hata sisi Wizara tuko kwenye maandalizi wiki hii, kwa sababu wiki ijayo tutahamia Dodoma, tunatekeleza agizo la Rais,” alisema Waziri Tizeba.

Kauli ya Waziri Tizeba imekuja siku moja baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutangaza kuhamia Dodoma ifikapo Septemba mwaka huu, huku akiwataka Mawaziri na Naibu Mawaziri kumfuata.

Waziri Mkuu alisema ameshaagiza ukarabati kwenye nyumba yake ukamilishwe ili ifikapo Septemba aweze kuhamia na kuwataka mawaziri kufanya hivyo kwa sababu kila Waziri ana nyumba na ofisi ndogo mjini Dodoma.

Nayo Wizara ya Nishati na Madini imetoa waraka ikiwataka wakuu wa idara na vitengo wote wa wizara hiyo kuanza maandalizi ya kuhamia Dodoma ifikapo mwezi Septemba mwaka huu.

Agizo hilo lipo katika waraka uliotolewa na Kabibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa jana na nakala yake kutumwa pia kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

Katibu Mkuu huyo alisema agizo hilo linatokana na kauli iliyotolewa na Rais Magufuli katika Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika mjini Dodoma hivi karibuni, ambapo alisisitiza azma ya serikali yake kuhamia Dodoma.

Alisema pamoja na kauli ya Rais, watendaji hao wanatakiwa kuanza maandalizi ya kuhamia Dodoma ifikapo Septemba kutokana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuahidi kuhamia Dodoma mwezi huo na kuwataka Mawaziri na Naibu Mawaziri nao kumfuata.

Makonda aibua ufisadi ujenzi Machinga Complex

$
0
0

TAARIFA YA MRADI WA MACHINGA COMPLEX

1.0 Utangulizi

Mnamo tarehe 19 Aprili, 2016 ofisi yangu ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ilipokea barua ya agizo la waziri wa nchi TAMISEMI juu ya kusimamia uendeshaji wa mradi wa Machinga Complex. Ambapo katika kutekeleza agizo hilo nilichukua hatua ya kwanza na ya muhimu ya kuupitia mkataba wote wa mradi huu ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya haki na wajibu wa pande mbili zilizohusika kwa maana ya Halmashauri ya Jiji na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Kimsingi, tathmini yangu ya mkataba ililenga kubainisha na kujiridhisha juu ya mambo sita yafuatayo; aina ya jengo lililotarajiwa kujengwa, usimamizi wa fedha za mkopo, usimamizi wa ujenzi wa mradi, gharama za mradi, utaratibu wa urejeshaji wa deni na kiwango cha riba kilichoainishwa. Ikukumbukwe tu kwamba, wakati halmashauri ya jiji ikikabidhiwa mradi siku ya kwanza ilikuwa tayari inadaiwa kiasi cha bilioni 19.7 huku mpaka Machi mwaka huu deni lilishafikia kiasi cha bilioni 38 za kitanzania, kutokea kwenye mkopo wa bilioni 12.7

2.0 Uchunguzi

Baada ya kupitia kwa umakini mkataba mzima na kukagua mradi wenyewe, zoezi ambalo lilihusisha kulinganisha kati ya kilichofanyika baada ya mradi kukamilika na taarifa ya upembuzi yakinifu (feasibility study) uliofanyika kabla ya kuanza utekelezaji wa mradi nimebaini yafuatayo;-

2.1 Ukubwa halisi wa jengo

Nimebaini kwamba majengo ya sasa ya machinga complex hayakujengwa kwa ukubwa sawa na ule ambao Halmashauri ya Jiji na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) walikubaliana kwenye mkataba na kupitia kifungu cha 1.1 cha barua ya makabidhiano kinachoeleza kwamba jengo lililokabidhiwa lina sehemu yenye ghorofa 5 na ghorofa 6 ili liweze kumudu idadi ya machinga wasiopungua 10,000 wakati hali halisi baada ya kutembelea jengo hilo ni kwamba jengo lina ghorofa 4 zinazobeba machinga 4,000 tu. Kwahiyo, pamoja na kwamba barua ya makabidhiano ilisainiwa na pande zote mbili licha ya ukweli kuwa maelezo ya jengo yalikuwa tofauti na jengo lenyewe.

2.2 Usimamizi wa fedha za Mkopo

Kwenye usimamizi wa fedha za Mkopo, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambaye ni mkopaji hakuhusika na usimamizi wa fedha za mkopo, hivyo mkopeshaji hakuwa na udhibitisho wa gharama halisi, jambo ambalo si tu limefanya mkopaji kutojua gharama halisi za jengo bali pia kulipokea likiwa limechelewa na likiwa halina ukubwa ulioelezwa kwenye mkataba. Kimsingi, haya yote yanazaliwa na maelekezo ya kifungu namba 4.1 kinachoeleza kwamba, mkopeshaji kusimamia mradi kuanzia hatua ya usanifu hadi kukamilika kwake ikiwa ni pamoja na kufanya malipo moja kwa moja kwa mkandarasi na mshauri wa mradi, kwa maneno mengine pia ni kwamba kifungu hiki kinakinzana na vifungu namba 2.1, 2.2, 10.1 na 11.1 vya mkataba huohuo ambavyo vinaelekeza kwamba mkopeshaji (NSSF) atatakiwa kutoa fedha kwa mkopaji (Halmashauri ya Jiji) kwa ajili ya kugharamia mradi pekee na kuusimamia kama ulivyokubalika kwenye mkataba.

2.3 Kuhusu gharama za mradi

Nimebaini kuwa fedha za mkopo ziliongezeka toka shilingi bilioni 12.14 za kwenye mkataba na kufikia bilioni 12.7 ikiwa ni nyongeza ya shilingi milioni 560, nyongeza ambayo ilifanyika bila makubaliano yoyote kati ya mkopeshaji na mkopaji, hali ambayo haimtendei haki mkopaji. Kwa faida tu ya wanadar es salaam na watanzania wenzangu ni kwamba, halmashauri ya jiji ilitiliana saini ya makubaliano na shirika la hifadhi ya jamii (NSSF) ya mkataba ambao unalenga kuipatia halmashauri ya jiji mkopo wa bilioni 10 kwa ajili ya kutekeleza mradi huu ingawa baada ya muda kidogo mkopeshaji (NSSF) alisema kuwa bilioni 10 na hivyo kufanya marekebisho ya mkataba na kuongeza mkopo wa bilioni 2.14

2.4 Urejeshaji wa deni

Suala la urejeshaji wa mkopo unazua utata pale mkataba unapoainisha kuwa, mkopaji ataanza kulipa marejesho ya deni kuanzia tarehe 31 Desemba, 2008 tarehe ambayo mradi ulikuwa unatarajiwa kuwa tayari umeanza lakini mkopeshaji (NSSF) alikuwa hajamaliza ujenzi, na cha ajabu mkopaji (Halmashauri ya Jiji) alitakiwa kuanza kulipa deni hata kabla ya muda wa grace period kuisha wakati jengo likiwa bado lipo mikononi mwa mkopeshaji ambaye alijitwisha jukumu la ujenzi huku akiwa bado akang’ang’ania kulipwa riba.

mara tu tarehe hiyo ilipofika hata kama mpokeshaji mwenyewe alikuwa bado hajakamilisha ujenzi huku akidai pesa ya riba.

Uwezo wa Mradi

Uwezo wa jengo hilo lililopo hata kama litafanya kazi kwa uwezo wake wote kwa maana ya kujaza nafasi zote zilizopo ni kasi cha sh124,796,666.666 kwa mwezi ambazo ni sawa na kiasi cha sh1,497,560,000 kwa mwaka. Pungufu ya 60% ya lengo la Mradi kama ilivyokuwa kwenye upembuzi yakinifu

3.0 Mapendekezo

3.1 Baada ya uchunguzi huu ulionifanya kuamini mambo makubwa matano niliyoyaainisha hapo chini na ambayo yameniongoza kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua;-
  • Deni halilipiki – ukweli ni kwamba, ukizingatia kiasi cha pesa kinachodaiwa kutoka kwa halmashauri ya Jiji ambacho mpaka sasa ni zaidi ya bilioni 38 utagundua kuwa, halmashauri haiwezi kulipa deni hilo. Ikilinganishwa na uwezo wa jengo hilo deni hili litalipwa baada ya miaka isiyopungua 24 
  • Mkataba wote huu ni wa hovyo na haukupaswa kusainiwa hata kidogo.
  • Kitendo cha kusaini mkataba huu ni hakika na bayana kuwa rushwa ilitumika pande zote mbili, kwa maana haiwezekani ukaacha taaluma yako kwa kiwango hicho cha kutoona udhaifu huu wa wazi wa mkataba huu kama hujapofushwa macho na rushwa.
  • Mkataba huu hauna tija kwa upande wowote ule: sio NSSF kwasababu halmashauri ya Jiji hawana uwezo wa kulipa deni, wala sio kwa Jiji lenyewe kwani halina uwezo wa kutekeleza mkataba kwa kufanya malipo yanayotakiwa na hauna faida vilevile kwa machinga kwa sababu gharama ya kupanga ni kubwa. 
3.2 Mapendekezo
  1. Kuvunjwa kwa mkataba na NSSF kuchukua eneo lao, kwa makubalino ya kwamba, Halmashauri ya Jiji walipwe kodi ya ardhi jambo ambalo linaweza kufanyika kwa urahisi kupitia NSSF na halmashauri ya Jiji kumiliki hisa kwa pamoja. 

  2. Au NSSF wakabidhi jengo kwa halmashauri ya Jiji, lakini wakae na kukubaliana upya na hivyo kuandika mkataba tofauti na ule wa mwanzo. 

  3. Mwisho, wahusika wote wa pande zote mbili wachukuliwe hatua kwani hatuwezi kutumia fedha za mifuko za hifadhi ya jamii ambazo ni fedha za wanyonge wa taifa hili kwa faida ya wachache waliotanguliza ubinafsi,. 
Imetolewa na:

Paul Makonda
Mkuu wa Mkoa – Dar es Salaam.

Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Dakika Asomewa Mashitaka Mapya 222

$
0
0
WAFANYABIASHARA wawili, akiwemo Mohamed Yusufali “Choma”, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka 222 ya kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 14.

Mbali na Yusufali aliyewahi kutajwa kuwa anajipatia Sh milioni saba kwa dakika moja kwa njia ya udanganyifu katika mapato ya serikali, mshitakiwa mwingine ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Northern Engineering Works Limited, Samwel Lema, ambao wanadaiwa kusababisha hasara kwa kughushi na kukwepa kulipa kodi.

Washitakiwa walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka kwa zaidi ya saa tatu na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi, akisaidiwa na Jackline Nyantori, Diana Lukondo na Wakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai.

Mbele ya Hakimu Mkazi Wilbard Mashauri, ilidaiwa, katika tarehe tofauti kati ya Januari Mosi 2012 na Desemba 31, 2014, washitakiwa hao na wengine ambao hawajafikishwa mahakamani walipanga njama za kuidanganya Mamlaka ya Mapato (TRA) na kujipatia Sh 14,052,011,435.

Wakili Kishenyi akisaidiwa na Nyantori walidai, katika shitaka la tano hadi 103 kuwa, kati ya mwaka 2011 na 2013, jijini Dar es Salaam na Arusha, washitakiwa hao walighushi stakabadhi za malipo kuonesha Kampuni ya Northern Engineering Works Ltd imenunua bidhaa mbalimbali.

Ilidaiwa kuwa stakabadhi hizo zilionesha kuwa kampuni hiyo imenunua bidhaa mbalimbali kutoka kwenye kampuni tofauti tofauti ikiwemo ya Festive General Business Ltd, Ever Global General Trading na Jambo Product Ltd, jambo ambalo si kweli.

Wakili Diana na Swai waliendelea kudai, katika shitaka la 104 hadi 141, kuwa kati ya mwaka 2011 na 2015, Lema alighushi hati ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kuonesha kuwa kampuni yake imenunua bidhaa mbalimbali kutoka kampuni tofauti tofauti ikiwemo ununuzi wa vifaa vya Sh bilioni 1.7.

Wakili Swai alidai katika shitaka la 142 hadi 219 kuwa, kwa lengo la kufanya udanganyifu washitakiwa hao walighushi stakabadhi za malipo kuonesha Kampuni ya Elerai Constructions Ltd, imenunua vifaa mbalimbali kutoka katika kampuni tofauti tofauti ikiwemo Kampuni ya Blue Arrow Tanzania Ltd.

Aliendelea kudai shitaka la 220, linamkabili Lema ambaye anadaiwa kati ya Januari Mosi, 2012 na Desemba 31, 2015, Dar es Salaam, akiwa Mkurugenzi anayehusika kushughulikia Kampuni yake ya Northern Engineering Works Ltd na Elerai Constructions Ltd zilizosajiliwa kama walipa kodi, aliwasilisha nyaraka za uongo.

Inadaiwa aliwasilisha nyaraka ambazo ni marejesho ya uongo ya Kodi ya VAT kwa Kamishna Mkuu wa TRA jambo lililosababisha akwepe kulipa kodi ya Sh bilioni 14,052,011,435. 

Katika mashitaka ya utakatishaji wa fedha, ilidaiwa kati ya Februari Mosi, 2012 na Februari 25, 2013 jijini Dar es Salaam na Arusha, washitakiwa hao walijihusisha na kuhamisha Sh milioni 420 zilizotokana na vitendo vya uhalifu.

Inadaiwa waliziingiza fedha hizo kwenye akaunti namba 1010000541 inayomilikiwa na Iqbal Jaferali Jafferjee iliyopo katika Benki ya I&M tawi la Kariakoo, na kuzitoa huku wakijua zimepatikana kwa njia za uhalifu ambazo ni kughushi na kukwepa kulipa kodi.

Iliendelea kudaiwa katika shitaka la 222 kuwa, kati ya Januari Mosi, 2012 na Desemba 31, 2015, Dar es salaam, kutokana na vitendo vyao vya kuwasilisha marejesho ya VAT ya uongo kwa Kamishna Mkuu wa TRA waliisababishia mamlaka hiyo hasara ya zaidi ya Sh bilioni 14.

Hakimu Mashauri aliwaeleza washitakiwa hao kuwa, hawaruhusiwi kujibu mashitaka yao kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa Mahakama Kuu.

Baada ya kusomewa mashitaka, upande wa Jamhuri ulidai upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa, hata hivyo Wakili Alex Mgongolwa anayeongoza jopo la Mawakili wa Utetezi aliomba kuwasilisha ombi.

Aliiomba Mahakama ifute shitaka la utakatishaji wa fedha kwa kuwa lina mapungufu makubwa ya kisheria ambayo hayawezi kurekebishwa wala kufumbiwa macho isipokuwa kufutwa.

Alidai ili shitaka liwe la utakatishaji wa fedha lazima kuwa na dhamira ya kuficha chanzo cha fedha au lengo la washitakiwa kukwepa adhabu lakini kama hakuna mambo hayo sheria inatoa mamlaka kwa Mahakama kuyafuta mashitaka hayo.

Upande wa Jamhuri uliiomba Mahakama iahirishe kesi hiyo ili wajiandae kujibu hoja za upande wa utetezi. Hakimu Mashauri alikubali ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi kesho kwa ajili ya kusikiliza majibu ya Jamhuri.

Washitakiwa wote walirudishwa rumande kwa kuwa mashitaka yanayowakabili hayana dhamana. Mbali na mashitaka hayo, Choma anakabiliwa na kesi nyingine yenye mashitaka 199 ya kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 15.6 katika mahakama hiyo.

Chadema kutoa tamko zito Leo Ambalo Litarushwa na Vituo Vitatu vya TV

$
0
0

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), leo kinatarajia kulihutubia taifa kupitia vyombo vya habari vya ndani na nje kuhusu maazimio ya Kamati Kuu iliyoketi kwa siku nne mfululizo.

Maazimio hayo ambayo yanaitwa ‘mazito na makubwa’ kuwahi kutolewa na chama hicho katika siku za hivi karibuni, yanatarajiwa kuonyeshwa moja kwa moja na vituo vitatu vya runinga   nchini.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya chama hicho kimeeleza kuwa maazimio hayo ya Kamati Kuu yatatangazwa moja kwa moja kupitia baadhi ya vituo vya runinga  kutoa fursa kwa Watanzania kusikiliza maazimio hayo.

Kamati kuu ya Chadema imefanya kikao chake kwa siku nne mfululizo kikiwa kimeghubikwa na usiri mkubwa.

Taarifa ya chama hicho kwa vyombo vya habari jana, ilisema Kamati Kuu ilimaliza kikao chake cha siku nne jana na leo maazimio yake yatawekwa wazi kwa wananchi kupitia vyombo vya habari.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene, ilisema kupitia mkutano huo yatatangazwa maazimio ya kikao hicho kilichohitimishwa    Dar es Salaam jana.

Taarifa hiyo ilisema Chadema kitatoa tamko zito la ukubwa wa aina yake.

“Licha ya mambo hayo chama kitatoa matamko mazito na makubwa ya aina yake ambayo hayajawahi kutolewa na chama chetu katika siku za karibuni."

Taarifa hiyo ilisema Kamati Kuu ilipokea taarifa ya kina juu ya masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na hali ya siasa nchini kwa sasa ambayo inatishia hali ya uchumi na ustawi wa jamii nzima kwa ujumla, hivyo taifa zima kuwa katika majaribu makubwa ya kukosa mwelekeo wa  uongozi.

“Kupitia mkutano huo, Chadema kitatoa mwelekeo wa hali ya nchi hasa wakati huu ambao taifa linaonekana kukosa dira ya uongozi kwa ajili ya ustawi wa Watanzania wote kwa ujumla” kilisema chanzo hicho ambacho hakikutaka kuwekwa wazi jina lake.

“Kupitia mkutano huo, chama kitazungumzia mipango ya kujiimarisha kuendelea kuwatumikia wananchi na kusimamia dira ya mabadiliko na uhuru wa kweli nchini,”alisema Makene.

Alipoulizwa kuhusu taarifa hizo, Makene alisema suala hilo halijathibitishwa rasmi kama mkutano huo   utaonyeshwa moja kwa moja katika runinga.

“Hata mahali utakapofanyika mkutano huo bado hapajajulikana, nitakupigia simu kesho asubuhi (leo) kukujulisha wapi tamko hilo litatolewa."  Alisema

Mawakili zaidi ya 100 Waandamana kudai haki

$
0
0
MAWAKILI wa kujitegema zaidi ya 100 mkoani Arusha, jana waliandamana kwenda kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, kulaani kile walichokiita ukandamizwaji wa sheria za nchi na kazi ya uwakili unaofanywa na polisi.

Wanasheria hao wanalaani kitendo cha wakili mwenzao, Shilinde Ngalula, kukamatwa, kufungwa pingu na kufunguliwa mashtaka akiwa kazini Loliondo wilayani Ngorogoro.

Mawakili hao walitembea zaidi ya hatua 400 kabla ya kuzingirwa na polisi ambao waliwataka kuunda kamati ya watu wachache kwenda kuzungumza na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo.

Uamuzi wa kufanya maandamano hayo, ulipitishwa jana mjini hapa baada ya mawakili hao kufanya kikao cha pamoja viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Awali, mawakili hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Wakili Modest Akida, pia walikubaliana kutoendelea na kesi za wateja wao waliokuwa mahakamani.

Akizungumzia maandamano hayo, Akida alisema yalilenga kupinga kitendo cha Jeshi la Polisi wilayani Ngorongoro, kumkamata na kumfungulia mashitaka Wakili Ngalula.

Wakiwa tayari wameandamana umbali wa takribani hatua 400 kutoka mahakamani hapo, vikosi vya askari polisi waliovalia kiraia na wale wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa ndani ya magari mawili, waliwazunguka na kuwaamuru kusimama.

Mkuu wa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha, Thomas Mareko, aliwataka wanasheria hao kufuata sheria katika kudai na kuwasilisha malalamiko yao.

“Nyinyi ni wanasheria, mpaka hapa tayari mmeshaandamana kinyume cha sheria za nchi, nawaomba chagueni wawakilishi nitawasindikiza mnakokwenda na wengine rudini mkaendelee na majukumu yenu,” alisema Mareko.

Baada ya maandamano hayo kuzuiwa, mawakili hao waliwachagua wawakilishi waliokwenda kuwasilisha malalamiko yao kwa Kamanda Mkumbo na wengine walirudi katika viwanja vya mahakama kusubiri taarifa.

Awali, akizungumza katika viwanja hivyo, Wakili George Njooka alisema mawakili nchini wameanza kudharauliwa na vyombo vya dola.

“Hawa watu walianza na vyombo vya habari, wakaenda kwa wanasiasa na sasa wamekuja kwa mawakili, nawaomba tuanzie hapa twende kwa RPC atuambie haya maelekezo tunayoambiwa yanatoka juu, yanatoka kwa nani,” alisema Wakili Njooka.

Wakili Qamara Peter aliwakumbusha mawakili wenzake kuwa haki siku zote haiombwi bali inadaiwa.

Askari aliyepatikana na hatia ya kumuua mwandishi Daudi Mwangosi bila kukusudia, amehukumiwa miaka 15 jela

$
0
0
Leo July 27 2016 Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Iringa imetoa hukumu ya kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwanahabari wa kituo cha Television cha chanel Ten, Daud Mwangosi.

Mahakama hiyo imemuhukumu kwenda jela miaka 15 mshtakiwa wa mauaji hayo, askari wa polisi kikosi cha kutuliza ghasia ‘FFU’ Pacificius Simon.

Hukumu hiyo imekuja baada ya juzi mahakama hiyo kumkuta na hatia askari huyo ya mauaji ya bila kukusudia ya Mwangosi yaliyofanyika September 2 2012 kwenye kijiji cha Nyololo, Mufindi  wakatia CHADEMA ikifanya uzinduzi  wa matawi, huku kukiwa na katazo la mikutano au makusanyiko ya kisiasa kutokana na seriakali kuongeza muda wa sensa ya watu na makazi

Nay Wa Mitego Afungiwa na BASATA....... Atozwa Faini Ya Tsh. Milioni 1

$
0
0

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungia kwa kipindi kisichojulikana Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kwa jina la Nay wa Mitego hadi hapo litakapojiridhisha kwamba ametekeleza maagizo yote aliyopewa na Baraza sambamba na yeye kubadilika katika kubuni kazi zenye maadili na zisizo dhalilisha watu wa kada mbalimbali.

Maagizo aliyopewa Msanii Nay ni pamoja na kulipa faini (adhabu) ya kiasi cha Shilingi milioni 1, kufanya marekebisho ya mashairi ya wimbo wake wa ‘Pale Kati’, kufuata sheria, kanuni na taratibu za urasmishaji sekta ya Sanaa kwa maana ya kusajiliwa na BASATA na kuhakikisha wimbo wake umefuata taratibu zote.

Aidha, Msanii Nay ameagizwa kuwaomba radhi watanzania kwa kutoa kazi ya muziki yenye kuvunja maadili na kudhalilisha watu wa kada mbalimbali hususan wanawake.

Maamuzi haya yamefanyika kwa mujibu wa kifungu cha 4(2) cha sheria nambari 23 ya mwaka 1984, ikisomwa pamoja na kifungu cha 30(1)(2) na waraka wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo wa tarehe 16/7/2009 ambayo kwa sasa inafahamika kama Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Adhabu hizi zimetolewa kufuatia BASATA kufanya kikao cha pamoja na Msanii huyu jana siku ya Jumanne tarehe 26/07/2016 kwenye Ukumbi wa Baraza na yeye kukiri makosa na kuahidi kubadilika.

Makosa aliyosomewa na yeye kuyakiri kwa maandishi ni pamoja na;
1. Kujihusisha na shughuli za Sanaa pasipo kusajiliwa na BASATA.
2. Kutoa wimbo wa “Pale Kati” na kuupakia katika mitandao ya kijamii bila kuuleta kufanyiwa uhakiki wa maudhui yake.

3. Maudhui ya wimbo wa ‘Pale Kati’ kwa sehemu kubwa hayafai kwa matumizi ya wazi na ni kinyume cha sheria za nchi na maadili ya mtanzania.
 
Ikumbukwe kwamba mnamo tarehe 16/07/2016 BASATA lilitoa taarifa kwa umma ya kuufungia wimbo wa Pale Kati kufuatia kubeba maudhui yenye uvunjifu mkubwa wa maadili na kupambwa na picha dhalilishi kwa wanawake.

Aidha, tarehe 12/02/2016 BASATA liliufungia wimbo wa Shika Adabu Yako wa Msanii huyuhuyu kwa makosa yanayofanana na haya. Hivyo adhabu hii imetolewa ili kumpa muda wa kujifunza, kujitathimi na kujirekebisha kama kweli ana nia ya kuendelea kufanya kazi ya muziki 
 
SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI
Godfrey L. Mngereza
KATIBU MTENDAJI, BASATA.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images