Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Picha 8: Mwigizaji Jackline Wolper atangaza kuhama CHADEMA na kijiunga na CCM

$
0
0
Mwigizaji wa filamu nchini Tanzania Jackline Wolper aliyakuwa akimuunga mkono Edward Lowassa katika uchaguzi Mkuu 2015, ametangaza kujiunga na CCM rasmi jana

Wolper alikaribishwa na mwenyekiti aliyemaliza muda wake Dkt Jakaya Kikwete baada ya kutangaza kujiunga na CCM.

Kitendo hicho kilifanyika katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika jana Julai 23, mkoani Dodoma.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya July 24

Wasanii Wamlilia Kikwete Walipokuwa Wakimuaga Kwa Kustaafu Uwenyekiti Wa Chama Cha Mapinduzi

$
0
0
Wasanii wa Bongo Movie na muziki wa kizazi kimpya wamesema watamkumbuka sana Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Jakaya Kikwete kwa msaada aliyowapatia kipiti cha utawala wake akiwa Rais na Mwenyekiti wa chama hicho.

Wasanii wameyasema hayo usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma walipofanya tamasha la Usiku wa Wasanii kwa ajili ya kumuaga baada ya kustaafu rasmi uwenyekiti wa chama hicho na kumuachia uongozi Rais John Magufuli

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 19

$
0
0

.....DORICE alipozitazama zile nguo zilikuwa ni nguo nzuri sana za kuvutia. Kulikuwa na gauni moja refu linaloacha wazi mikono lenye rangi ya dhahabu inayong'aa sana. Kulikuwa na viatu virefu vinavyoelekeana na rangi ya gauni kidogo, ushungi wenye rangi ya gauni, mkufu wa dhahabu pamoja na hereni.

Dorice alivishangaa vitu vile kwa mshangao wakati huo Mansoor alikuwa akiachia tabasamu mwanana pembeni yake.

"Vaa Dorice!" Ilisikika sauti ya Mansoor ndipo Dorice alipopata nafasi ya kumtazama tena Mansoor. Akapigwa na bumbuwazi baada ya kuona mansoor amevalia nguo tofauti na alizokuwa amevaa mwanzo, alionekana kama mwanaume wa kihindi pale anapofunga ndoa kwa mavazi yake. Dorice alimshangaa sana Mansoor, woga kiasi ukamvaa moyoni mwake kisha akaanza kuzivaa nguo zile alizopewa na Mansoor.

Pindi anapozivaa nguo zile Mansoor alikuwa tayari ameshatoweka eneo lile.Dorice alipovaa nguo zile, alibadilika sana. Alionekana mrembo mno kwa jinsi alivyopendeza. 

Ukimtazama kwa haraka utadhani msichana kutoka India kumbe ni mnyaturu wa Singida. Alijitazama kupitia kioo kilichokuwa mbele yake, akajikiri kwamba kweli Mungu hakumkosea katika uumbaji ila alitumia ufundi wa hali ya juu katika kukamilisha sura na umbile lake.

Bada ya kumaliza kuvaa, Mansoor alitokea tena palepale alipokuwa amesimama mwanzo. Alimshtua sana Dorice lakini tayari alikuwa ameshaanza kumzoea Mansoor hivyo hakuogopa sana.

"Umependeza sana Malkia wangu.. Kwa jinsi ulivyo sitamani hata uende Duniani.. Nahisi wivu sana.." Alisema mansoor huku akimtazama mrembo yule kama waridi likiwa bustanini wakati wa jua la asubuhi.

"Uliniahidi nini?" Aliuliza Dorice kwa hamaki."Usijali... Nitakupeleka duniani kama nilivokuahidi ila nimekuambia tu hisia zangu... Kama unanipenda kweli ni heri ubaki na mimi huku huku kwetu!" Alisema Mansoor kwa sauti ya upole sana. Dorice hakijibu kitu. Wakaondoka pale na kwenda moja kwa moja kwa malkia.

Malkia alifurahi sana kuona kijana wake ameambatana na mtu ampendae. Radi tatu mfululizo zilipigwa ili kudhihirisha furaha aliyokuwa nayo malkia. Mansoor alitabasam akiwa amemshika mkono mkewe mtarajiwa.

"Harusi ya mwanangu Mansoor... Iwe ya furaha sana kwani amepata kile alichokuwa anahitaji.." Alisena malkia kwa sauti kali. Dorice alimtazama Mansoor kwa woga.

"Usiogope malkia wangu.. Na kuanzia Leo nitakuita Aisha..!"
"Aisha! Kwanini?" Alihamaki Dorice.
"Ukiwa mke wangu huwezi kuitwa Dorice.." Alisema Mansoor.

Wakati Dorice akiendelea kushangaa ghafla upepo mkali ukapigwa, halafu kwa muda huohuo walijikuta wapo eneo lingine lililojaa watu wengi ambao Dorice hakuwaelewa elewa kwa jinsi walivyokuwa.

Msindai : Nimerudi CCM Kwa Kuwa Sasa Hakuna Cha Kupinga

$
0
0

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida na baadaye kuhama chama na kujiunga na CHADEMA, Mgana Msindai ametangaza kurudi CCM.

Msindai alitangaza uamuzi huo jana mjini Dodoma baada ya kupewa nafasi na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete wakati anaendesha mkutano mkuu wa CCM uliomchagua Rais Dk John Magufuli kuongoza chama.

Msindai alisema aliamua kurudi CCM baada ya kuona kuwa sasa hakuna cha kupinga baada ya Rais Magufuli kuchaguliwa kuwa rais wa nchi.

Msindai aliingia CHADEMA baada ya aliyekuwa mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa kujiunga na Chadema mwaka jana wakati wa uchaguzi mkuu.

Kauli ya CHADEMA baada ya wanachama wake kutangaza kujiunga CCM

$
0
0
Wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM jana mjini Dodoma, Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kiliwapoteza wanachama wake watatu baada ya kutangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wanachama hao waliokihama chama hicho ni Fred Mpendazoe ambaye alikuwa mwanachama wa CCM pia aliwahi kuwa Mbunge wa Kishapu mwaka 2005 hadi 2010 kupitia CCM, Mgana Msindai aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida na mbunge wa zamani wa Iramba Mashariki na mwigizaji wa filamu nchini Tanzania Jackline Wolper.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA alipohojiwa jana wakati kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kinaendelea alisema kuwa, hawana muda wa kukaa na kuanza kumjadili mtu mmoja mmoja anayesemekana kuhama chama hicho.

"Kamati Kuu ni kikao kizito sana, hatuwezi kuacha kujadili masuala ya msingi na kuanza kuwajadili hao wanaosemekana kuwa wamehama chama," alisema mjumbe huyo.

Kamati Kuu ya CHADEMA imekutana jana na leo katika vikao vya dharura ikiwa na lengo kubwa la kujadili mwenendo wa hali ya kisiasa nchini.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya July 25

Diwani Akwepa Risasi sita akipambana na majambazi Moshi

$
0
0

Diwani wa Kata ya Kiborlon (Chadema) katika Manispaa ya Moshi, Frank Kagoma ameonyesha ujasiri wa hali ya juu alipopambana na majambazi waliokuwa na silaha za moto.

 Alinusurika kuuawa baada ya majambazi hao waliokuwa na bunduki na bastola kumfyatulia risasi sita alipokuwa akiwafukuza ambazo hata hivyo, hazikumpata. 

Tukio hilo ambalo lilionekana kama sinema, lilitokea mwishoni mwa wiki baada ya majambazi hao kuvamia duka la jumla la kuuza mitumba linalomilikiwa na Menti Mbowe na kupora Sh10 milioni. 

Katika tukio hilo lililotokea saa tano asubuhi eneo la Kiborlon, majambazi hao walimjeruhi kichwani mfanyabiashara huyo anayemiliki pia mabasi ya Machame Safaris. 

Hali ya majeruhi huyo inaendelea vizuri. Akisimulia tukio hilo, diwani huyo alisema siku hiyo akiwa maeneo ya Kiborlon, alipigiwa simu kuwa mfanyabiashara huyo amevamiwa na majambazi ndipo alipoendesha gari lake hadi eneo la tukio. 

“Nilipofika pale wale majambazi watatu ndiyo walikuwa wanatoka kwenye duka. Nikampelekea gari yule aliyekuwa ameshika bunduki. Kuona hivyo akafyatua risasi hewani,” alisema Kagoma. 

“Yule mwenye bunduki akaingia uchochoroni kuelekea Barabara ya Stendi ya Kidia. Mwenzake aliyekuwa na bastola naye akawasha risasi nyingine hewani kunitisha,” alisema. 

Baada ya hali hiyo, diwani huyo alilazimika  kujificha kwenye gari na majambazi hao walidandia pikipiki na kuanza kukimbia kuelekea Barabara ya Msaranga, naye akawafuata kuelekea huko. 

“Wakati huo tayari vijana wangu wa bodaboda wakawa nao wamesikia hilo tukio tukaanza kusaidiana kuwafukuza lakini mbele kidogo pale Msaranga wale majambazi wakasimamisha pikipiki yao umbali wa mita 30 kutoka nilipokuwa na mmoja wao mwenye bunduki alifyatua risasi mbili na mwenye bastola risasi mbili kuelekea uelekeo wangu. 

“Nililazimika kujificha kwenye kiti, wale majambazi wakajua wameniua. Wakapanda tena pikipiki ili watoroke. Nikawasha tena gari huku vijana wangu nao wakinisaidia tukaanza kuwafukuza,” alisema. 

Kagoma alisema majambazi hao walipita maeneo ambayo gari haliwezi kupita wakaelekea eneo la Mabogini Moshi Vijijini hadi lango la TPC na baadaye wakaelekea Rundugai wilayani Hai. 

“Kuna eneo vijana wangu wanasema kulikuwa na vumbi sana, ndipo walipowapoteza na majambazi wakatoroka kupitia njia ya reli ili kukwepa polisi waliokuwa wakiwasubiri mbele,” alisema na kuongeza: “Hatukuwa na silaha, lakini tulijitahidi kupambana nao kwa ujasiri. Tatizo nafikiri tulikosea kidogo. Ilitakiwa wakati tukifukuzana nao tuwape polisi uelekeo wa majambazi.” 

Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema jana kuwa Jeshi lake litatoa taarifa rasmi kwa wanahabari leo kuhusiana na msako unaoendeshwa na jeshi hilo. 

“Kuna mambo tumeyafanya tangu tukio hilo litokee lakini kesho (leo) saa sita mchana tutatoa taarifa rasmi pamoja na mafanikio tuliyofikia hadi sasa. Tunaendelea vizuri na upelelezi,” alisema.

Kamanda Mutafungwa, alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ikiwamo kuwafichua wahalifu na mbinu wanazozitua akisema polisi wamejipanga kukabili wimbi jipya la ujambazi.

Mtandao wa haki za binadamu walia na Jeshi la Polisi

$
0
0

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) umelitaka Jeshi la Polisi mkoani Arusha kuwafikisha mahakamani wanachama wake wanne linaowashikilia kwa siku 12 sasa. 

Mtandao huo umedai kuwa watu saba wilayani Longido wanatuhumiwa kutoa taarifa kwa mwanahabari wa Sweden, Susana Nurduland ambaye anafuatilia kwa karibu migogoro ya ardhi wilayani humo. 

Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa alisema uendeshaji wa madai hayo umegubikwa na upendeleo wa wazi jambo lililo kinyume na matakwa ya sheria za nchi kwa watuhumiwa wa makosa ya jinai. 

“Hadi sasa watetezi wanne wamenyimwa dhamana wakati wengine wenye nafasi za kisiasa wamepewa. Hii si sawa,” alisema Olengurumwa. 

Aliwataja walionyimwa dhamana kuwa ni Samwel Nangiria, Supuk Olemaoi, Clinton Kairung na Yohana Mako wakati walioachiwa ni mbunge wa zamani wa Ngorongoro, Mathew ole Timan, Diwani wa Ololosokwani, Yanick Ndina Timan na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mundoros, Joshua Makko. 

Alieleza kuwa watetezi hao wamenyang’anywa vitendea kazi vyao pamoja na vifaa vya mawasiliano zikiwamo simu za mkononi na kompyuta mpakato. 

Wakili wa Kujitegemea wa kampuni ya Law Guards Advocates, Jebra Kambole alisema hiyo ni kinyume na sheria zinazosimamia haki za binadamu nchini. 

“Kumshikilia mtu muda mrefu bila dhamana pamoja na kunyimwa uwakilishi ni kinyume na Katiba ya nchi. Ni kinyume na Azimio la Umoja wa Mataifa la Watetezi wa Haki za Binadamu la mwaka 1998,” alisema Kambole baada ya kueleza kuwa watuhumiwa hao wamenyimwa haki ya kuwatumia mawakili. 

Licha ya ombi hilo kwa Polisi, mwanachama wa mtandao huo, Rose Sarwatt alimuomba Jaji Mkuu kuingilia kati suala hilo ili kuhakikisha haki inatendekea. 

Aliziomba asasi za kimataifa kukemea na kuishauri Serikali juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea huko Loliondo. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema jeshi lake linasimamia na kutekeleza sheria za nchi na halichagui wa kumkamata kama amefanya kosa la jinai.

 “Lazima ukamatwe labda uwe na kinga. Hata mimi, japo kazi yangu ni kukamata lakini nikifanya jinai nitakamwa tu,” alisema na kubainisha kuwa taratibu zinaendelea kuzingatiwa na zikimalizika, watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani.

Vikongwe wawili wauawa kwa tuhuma za uchawi

$
0
0

Vikongwe wawili mke na mumewe wa Kitongoji cha Nyag’holongo, Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, wameuawa kwa kutumia silaha za jadi na watu wasiojulikana wakituhumiwa kuwa ni wachawi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Isack Msengi alisema tukio hilo lilitokea Julai 22 saa tatu usiku nyumbani kwao.

Aliwataja wanandoa hao kuwa ni Machene Magina (80) na Mkewe Genke Bundara (75) ambao waliuawa na wananchi wakiwatuhumu kwa uchawi.

Msengi alisema watu watano wanashikiliwa na polisi na upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea. Diwani wa Kata ya Nanda, Jumamosi Mathias alisema kundi la watu ambalo halijulikani lilivamia nyumbani kwa familia hiyo wakati wakijiandaa kulala na kufanya ukatili huo.

Mathias alisema akiwa nyumbani kwake, alisikia kelele za watu wakisema; “Tumechoshwa na hawa wachawi. Kwa kuwa hawa wazee ni majirani zangu, nilianza kuhangaika ili kuona jinsi ya kudhibiti maafa hayo,” alisema Mathias.

 Hata hivyo, alisema kabla ya kutoa taarifa polisi, watu hao waliivamia nyumba hiyo na kufanya mauaji hayo ya kinyama kwa vikongwe hao.

Alilaani kitendo kilichofanywa na watu hao kuwa ni cha kikatili dhidi ya wazee kwani tangu aishi nao kijijini hapo hakuwahi kusikia tuhuma za uchawi dhidi yao.

Mathias alitoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kuwahisi wazee kuwa ni wachawi na kujichukulia sheria mkononi, badala yake wawathamini na kuwalinda kwani wazee ni hazina ya Taifa.

Askofu Gwajima amjibu Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba aliyemuita muongo

$
0
0

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amemjibu katibu mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba aliyemtuhumu kuwa ni mwongo akisema leseni yake ni ya kuendesha magari makubwa na siyo vibajaji na maguta. 

Akihubiri katika kanisa lake jana, Gwajima bila kutaja jina la Makamba, alisema: “Siwezi kushughulika na vigari vidogovidogo nyie mnanifahamu, mimi nina leseni ya kuendesha semi trailer …nadhani mmenielewa,” alisema huku waumini wake wakimshangilia. 

Juzi, Makamba aliwaeleza wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM kuwa Askofu Gwajima ni kiongozi wa dini lakini ni muongo na kuwa uongo wake unawaudhi hata waumini wake ambao ni wanachama wa chama hicho. 

Alisema Gwajima amekuwa akisema uongo kuwa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete hataki kuachia madaraka ya uenyekiti wa chama hicho, kitu ambacho Rais huyo mstaafu alikanusha akisema ni yeye alikwenda kumshawishi Dk John Magufuli kuchukua nafasi hiyo kabla ya muda wa uliopangwa kikatiba. 

Katika mahubiri hayo, Gwajima pia alisema mafunzo aliyoyapata tangu akiwa mdogo ni kuogopa kugombana na watu wa aina tatu, walevi, wazee na wagonjwa. 

“Baba yangu alinifundisha nisigombane na walevi, wazee na wagonjwa kwani ukimpiga kidogo mtu wa aina hiyo anaweza kufa,” alisema Gwajima. 

“Hata nyie waumini wangu nawaomba msigombane na watu wa aina hiyo kwani mnaweza kupata matatizo,” alisema. 

Kiongozi huyo aliongoza mamia ya waumini wake kumuombea Rais Magufuli kwa kushinda uenyekiti wa CCM akisema kofia hizo mbili zimempa meno ya kung’ata na zitamwongezea kasi ya kutatua matatizo ya wanyonge nchini.

Rais Magufuli juzi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM baada ya kupata kura zote 2,398 alizopigiwa na wajumbe wa mkutano huo. 

Kutokana na ushindi huo, Gwajima alisema Magufuli amepewa meno ya `kung’ata’ kila upande tofauti na alipokuwa na kofia moja ya urais. 

Alisema kwa muda mfupi aliokaa madarakani, elimu ya msingi na sekondari zimeanza kutolewa bure kitendo ambacho maskini na wanyonge wa nchi hii wameanza kuuona mwanga. 

Alisema ataendelea kumwombea Magufuli kwa sababu kazi anazozifanya zinawanufaisha wanyonge na maskini ambao kwa muda mrefu walipuuzwa katika nchi yao.

“Kuchaguliwa kwake kuwa mwenyekiti ni zawadi kwetu Watanzania, tuendelee kumwombea kila siku ili aendelee kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi,” alisema. 

Alisema nafasi hiyo mpya itamwezesha kupambana na rushwa tatizo ambalo ameonyesha kuwa `atalivalia njuga’ hata ndani ya chama hicho. 

Mbali na Rais Magufuli, Gwajima aliwaombea pia Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, mawaziri na Spika wa Bunge kwamba Mungu awalinde ili wamsaidie Rais kutekeleza majukumu yake. 

Kwa mwezi mzima, Askofu Gwajima amekuwa akitafutwa na Polisi baada ya kusambaa kwa sauti inayosikika kama yake ikitaka Rais mstaafu Kikwete afikishwe mahakamani kwa makosa yote yaliyofanyika katika utawala wake. 

Katika mkanda huo, sauti hiyo inadai baadhi ya viongozi wa CCM wametuma watu mikoani kupiga kampeni ya kutaka Magufuli asipewe uenyekiti ambao umekuwa ukishikiliwa na Kikwete. 

Baada ya sauti hiyo, Gwajima aliondoka nchini kwenda Japan lakini Polisi waliendelea kumsaka hadi Julai 12 walipomkamata katika Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), aliporejea. Alihojiwa na kuachiwa siku hiyohiyo.

Rais Magufuli mgeni rasmi Sherehe za Mashujaa Dodoma

$
0
0

AMIRI Jeshi Mkuu, Rais John Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa Kitaifa, yatakayofanyika mjini Dodoma leo.

Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa maadhimisho hayo kufanyika nje ya Jiji la Dar es Salaam, tangu Tanzania ipate Uhuru wake mwaka 1961. 

Pia, itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kuongoza maadhimisho hayo tangu alipochaguliwa Oktoba mwaka jana.

"Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yatafanyika kitaifa mkoani Dodoma katika Uwanja wa Mashujaa siku ya Jumatatu (leo) Julai 25, 2016 kuanzia saa 1 kamili asubuhi hadi saa 4:30 asubuhi. 

“Mgeni rasmi atakuwa Rais John Magufuli," alisema Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana, kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, jana.

Alisema anaishukuru serikali kwa kuupatia mkoa huo, ambao ni Makao Makuu ya nchi, heshima ya kipekee katika historia ya nchi ya kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo kitaifa.

Rugimbana alitaja shughuli zitakazofanyika siku hiyo kuwa ni gwaride la maombolezo litakaloshirikisha vikosi vya majeshi ya ulinzi na usalama vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Polisi na Magereza.

Kutakuwa pia na upigaji mizinga na uwekaji wa silaha za asili na shada la maua kwenye mnara, kama ishara ya kumbukumbu kwa mashujaa. Shughuli nyingine ni utoaji wa dua na sala, utakaofanywa na viongozi wa madhehebu ya dini.

Rugimbana aliwataka wakazi wa Dodoma kujitokeza kwa wingi siku hiyo kwenye Viwanja vya Mashujaa kushiriki kwenye maadhimisho hayo. Alisema hadi jana, maandalizi yote muhimu kwa ajili ya shughuli hiyo yalikuwa yamekamilika.

Rais Magufuli awasihi watanzania kudumisha amani, umoja na utulivu asisitiza serikali kuhamia Dodoma

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasihi watanzania kuwaenzi Mashujaa kwa kudumisha Amani, Umoja na Utulivu uliojengwa na mashujaa hao.Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo tarehe 25 Julai, 2016 wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa, yaliyofanyika katika uwanja wa Mashujaa Mjini Dodoma.

Pamoja na kutoa rai hiyo Rais Magufuli ameahidi kuwa atahakikisha azma ya Serikali kuhamia Dodoma inatekelezwa kabla ya kuisha kwa kipindi chake cha uongozi wa miaka mitano.

"Tunapoadhimisha siku ya Mashujaa hatuwezi kumsahau Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa alisema makao makuu yawe Dodoma, haiwezekani sisi watoto wake, sisi wajukuu wake tupinge kauli ya Mzee huyu.

"Kwa hiyo nilikwishazungumza na leo narudia hili katika siku ya Mashujaa, mlinichagua ndugu zangu wa Dodoma kwa kipindi cha miaka mitano, hadi sasa miezi minane imepita, nimebakiza miaka minne na miezi minne, nataka kuwathibitishia kuwa katika kipindi cha miaka minne na miezi minne iliyobaki nitahakikisha serikali yangu pamoja na mimi tunahamia Dodoma bila kukosa" Amesema Rais Magufuli.

Kufuatia maelekezo hayo ya Mhe. Rais, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameagiza Mawaziri wote waanze mara moja kuhamia Dodoma na kwamba yeye mwenyewe atakuwa amehamia Dodoma ifikapo mwezi Septemba mwaka huu.

Viongozi wengine waliohudhuria maadhimisho hayo ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid, Mawaziri Wakuu wastaafu Mhe. John Samwel Malecela na Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, Mabalozi na wanadiplomasia kutoka nchi mbalimbali, Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, Viongozi wa vyama vya siasa na dini, maafisa na askari waliopigana vita mbalimbali.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma

25 Julai, 2016

Rais Dkt. Magufuli amemteua Dkt. Samuel M. Nyantahe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Samuel M. Nyantahe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Julai, 2016.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Samuel M. Nyantahe alikuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI).

Dkt. Samuel M. Nyantahe anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Chrisant Majiyatanga Mzindakaya ambaye amejiuzulu wadhifa huo.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
25 Julai, 2016

Waziri Mkuu kuhamia Dodoma Septemba mwaka huu......Asema akishahamia, Mawaziri na Naibu Mawaziri wote wafuatie mara moja

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atahamia Dodoma ifikapo Septemba, mwaka huu kuonyesha kuwa Serikali imedhamiria kutekeleza ahadi ilizotoa kwa wananchi.

Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumatatu, Julai 25, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma na kuwashukuru kwa ushiriki wao kwenye maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa zilizofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma.

“Jana nilimwita Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na kumwambia akamilishe matengenezo kwenye nyumba yangu kwa sababu ninataka kuhamia Dodoma ifikapo Septemba,” amesema na kushangiliwa na mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma waliohudhuria maadhimisho hayo.

Amesema tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, kazi nyingi zimefanyika na wananchi wameziona na kwamba sasa hivi kazi iliyobakia ni utekelezaji wa ahadi alizotoa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.

“Wananchi kazi mmeziona na sasa tunaenda kwenye utekelezaji. Ninatoa agizo kuwa mawaziri na manaibu wote wahame mara moja kutoka Dar es Salaam na kuja Dodoma. Wana ofisi ndogo Dodoma na kwa kuwa wamekuwa wakiishi wakati wote wa Bunge, wahamie mara moja. Mimi nahamia Septemba, na utekelezaji wake nitausimamia kwa juhudi zote,” alisisitiza.

Amewataka wakazi wa Dodoma watumie fursa hiyo kutunza amani ya nchi na kudumisha umoja uliopo na pia akataka watumie fursa hiyo kujenga nyumba za kuishi za kutosha, nyumba za kulala wageni na hoteli za kitalii ili watu watumishi na wageni wanapokuja wasipate taabu mahali pa kuishi.

Wakati huo huo, mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli katika muda wa siku tatu amerudia kusisitiza nia ya Serikali kuhamia  Dodoma katika kipindi chake cha uongozi ili kutekeleza ndoto ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya kutaka makao makuu ya nchi yawe Dodoma.

Akizungumza na mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma kwenye uwanja wa mashujaa huku akishangiliwa, Rais Magufuli amesema atahakikisha Dodoma inakuwa makao makuu ndani ya miaka minne na miezi minne iliyobakia kwenye awamu ya kwnza ya uongozi wake.

“Kama wabunge karibu 300 na mawaziri na manaibu wao ambao hawafiki 30 wanakaa hapa kwa miezi mitatu na maisha yanakwenda, kama makao makuu ya chama kinachotawala nchi yako hapa sioni sababu ni kwa nini Serikali ninayoiongoza iendelee kubakia Dar es Salaam,” amesema.

Mara kwanza kutoa kauli hiyo, ilikuwa ni Jumamosi iliyopita, Julai 23, 2016 wakati akitoa hotuba yake ya kwanza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mkutano Mkuu maalum wa chama hicho.

Rais Magufuli amesisitiza wananchi na wanasiasa kutunza amani na kudumisha amani iliyokuwepo nchini. Pia amewataka Watanzania wote kuendelea kuwaenzi mashujaa walioipigania nchi hii.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,   
DODOMA.

JUMATATU, JULAI 25, 2016.

Picha: Rais Magufuli alivyoisindikiza siku ya mashujaa Dodoma

$
0
0
Rais John Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa, Julai 25, 2016.
 Rais John Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi,Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa, Julai 25, 2016.  Kulia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubei Ali Maulid na wapili kulia ni Spika wa Bunge, Dkt, Tulia Ackson.
 Wananchi wa Dodoma waliojitokeza kushiriki kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma wakimsikilza Rais John Maguguli wakati alipozungumza kwenye maadhimisho hayo mjini julai 25, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Dodoma katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma , Julai 25, 2016. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda  katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma , Julai 25, 2016. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula  na watatu kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Mstaafu ,John Malecela.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Meya wa manispaa ya Dodoma, Jafari Mwanyembwa  katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma , Julai 25, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali , Davis Mwamunyange katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma , Julai 25, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Inspekta Jenerali wa Polisi, Ernest Mangu, Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Davis Mwamunyange na Kamishina Jenerali wa Magereza John Minja(kulia)m katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa  mjini Dodoma , Julai 25, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kamishina Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Minja katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa  mjini Dodoma , Julai 25, 2016. Watatu kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi , Jenerali Davis Mwamunyange na kulia ni Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe, Dkt.John Pombe Magufuli akipokea heshama ya gwaride la Vikosi vya Ulinzi katika maadhimisho ya kilele cha siku ya mashujaa yaliyofanyika katika uwanja wa mashujaa Mjini Dodoma leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipowasili katika Maadhimisho ya siku ya Mashujaa yaliyofanyika katika uwanja wa Mnara wa Mashujaa Mjini Dodoma leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi mara  alipowasili katika Maadhimisho ya siku ya Mashujaa yaliyofanyika katika uwanja wa Mnara wa Mashujaa Mjini Dodoma leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Samia Sulihu Hassan mara alipowasili katika Maadhimisho ya siku ya Mashujaa yaliyofanyika katika uwanja wa Mnara wa Mashujaa Mjini Dodoma leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe, Dkt.John Pombe Magufuli akiweka Mkuki na Ngao katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mashujaa katika uwanja wa mashujaa Mjini Dodoma leo
[Picha na Ikulu.]

Zitto Kabwe na Maalim Seif Kutua Marekani kwa Clinton

$
0
0
ZITTO Kabwe na Maalim Seif Sharif Hamad kwa pamoja wameitwa jijini Philadelphia, Marekani.

Maalim Seif ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) ambapo Zitto ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Wanasiasa hao wameitwa kuhudhuria mkutano mkuu wa Chama cha Demokratiki utakaomthibitisha Hillary Clinton kuwa mgombea urais wa Marekani kupitia chama hicho.

Marekani inatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu tarehe 8 Novemba mwaka huu ambapo Clinton atathibitishwa kwenye mkutano huo kupambana na Donald Trump wa Chama cha Republican.

Maalim Seif na Zitto ndio wanasiasa pekee nchini waliopata mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo.

Abdallah Khamis, Ofisa Habari wa ACT- Wazalendo amesema wakati Zitto akiwa kwenye mkutano huo, atapata fursa ya kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa kisiasa duniani.

Taarifa zinaeleza kuwa, viongozi hao ni wawakilishi wa wanasiasa mahiri kutoka upinzani nchini Tanzania.

Taarifa kuhusu uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa juu ya mauaji ya Daudi Mwangosi.

$
0
0
Mahakama kuu kanda maalumu ya Iringa leo imesendelea na kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha cha Channel Ten mkoani Iringa, Daud Mwangosi, inayomkabili askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Pasificus Cleophace Simon mwenye namba G 2573

Hukumu ya kesi hiyo awali ilipangwa kutolewa July 21 mwaka huu, iliahirishwa hadi leo kutokana na jaji anayesikiliza kesi hiyo kuwa nje ya mkoa kikazi.

Leo July 25 2016 taarifa iliyoripotiwa na kituo cha ITV  ni kwamba mahakama kuu Iringa imemtia hatiani kwa kuua bila kukusudia askari huyo na hivyo hukumu rasmi itatolewa siku ya jumatano.

Wabunge chadema kuhojiwa kwa kukiuka agizo la kutofanya mikutano

$
0
0
Jeshi la polisi mkoani Arusha, limewaita kwa mahojiano, mbunge wa Karatu,Wilbroad Qambalo, mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Arusha, Cecilia Paresso na Mwenyekiti wa halmashauri ya Karatu,Jubilate Mnyenye kutokana na kupuuza agizo la kutofanya mikutano ya hadhara katika jimbo hilo.

Mwingine ambaye ametakiwa kwenda kuripoti polisi ni Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Karatu, Lazaro Bajuta.

Wakizungumza jana baada ya kukabidhiwa barua za wito wa polisi, Qambalo na Paresso walisema wamestuka kutakiwa kuripoti ofisi ofisi ya Mkuu wa upelelezi mkoa wa Arusha jumatano.

Parreso alisema,walipokea barua jana saa sita mchana na kutakiwa kuripoti kwa RCO, saa nane  lakini wakampigia na kumweleza wana ratiba nyingine tayari waende jumatano na akakubali.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkombo alipotakiwa kuelezea agizo hilo alisema yupo likizo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya July 26

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images