Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu akaribisha wawekezaji kutoka India.

$
0
0

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania inahitaji wawekezaji kwenye mashamba makubwa ya kibiashara pamoja na viwanda vya usindikaji mazao ili iweze kuboresha uzalishaji nchini.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Julai 10, 2016) wakati akifungua kongamano la siku moja la wafanyabiashara baina ya Tanzania na India lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua kongamano hilo   lililojumuisha wafanyabiashara 50 kutoka India ambao wameambatana na Waziri Mkuu wa India, Bw. Narendra Modi, Waziri Mkuu Majaliwa alisema Tanzania inayo fursa za uwekezaji kwenye sekta nyingi zikiwemo miundombinu, kilimo, utalii, viwanda na madini.

“Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda lakini pia imelenga kuzalisha malighafi za viwanda ambavyo tunahimiza vijengwe. Lakini pia tumewaita waje kuwekeza kwenye sekta za uvuvi na utalii kwani nazo bado hazijaendelezwa vya kutosha,” alisema.

“Tanzania inazo kilometa 1,424 za fukwe za bahari, pia ina kilometa za mraba 223,000 za eneo la kiuchumi la bahari kuu (EEZ) na kilometa za mraba 54,337 za mito, mabwawa na maziwa ambayo ni sawa na asilimia 6.1 ya eneo la nchi nzima. Kuna fursa nyingi kwenye uvuvi, usindikaji wa samaki na ufugaji wa samaki kwenye mabwawa,” amesema.

Amesema washiriki pia wamepata nafasi ya kusikia fursa za uwekezaji zilizoko upande wa Zanzibar na kwamba kupitia vituo vya uwekezaji TIC na ZIPA wanaweza kupata huduma zote palepale bila kuhangaika kwenye ofisi mbalimbali.

Mapema, akihutubia washiriki wa mkutano huo, Waziri Mkuu amesema kuna fursa nyingine nyingi za kuwekeza kwenye sekta ya mifugo hasa katika uanzishaji wa ranchi za mifugo, usindikaji wa maziwa na nyama, usindikaji wa ngozi na utengenezaji wa bidhaa za ngozi.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema urari wa kibiashara baina ya Tanzania na India umeegemea upande mmoja ambapo India inauza zaidi bidhaa zake hapa nchini Tanzania inavyouza bidhaa zake India. “Ninaamini njia mojawapo ya kurekebisha hali hii ni kwa wafanyabiashara kutoka India kuamua kuwekeza kwa kiwango kikubwa hapa nchini,” aliongeza.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua mkutano huo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Bw. Charles Mwijage alisema Tanzania inahitaji India kama ambavyo India inahitaji Tanzania katika kufanya biashara zake. “India inaongoza kwa kuuza bidhaa zake hapa nchini lakini pia ni miongoni mwa nchi 10 ambazo zinanunua kwa wingi bidhaa zake kutoka Tanzania,” alisema.

Naye, Rais wa Chama cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda wa India (Federation of Indian Chambers of Commerce and Industries - FICCI), Bw. Harshavardhan Neotia alisema biashara kati ya Tanzania na India inaendelea kukua na kwamba fursa zilizopo ni lazima zichangamkiwe mapema. “Fursa za kibiashara ni kama mawio ya jua, ukiendelea kusubiri sana unaweza usiyaone,” alisema.

Mkutano umejadili mada mbalimbali zikiwemo fursa za uwekezaji Tanzania bara na Zanzibar, fursa za uwekezaji kwenye maeneo ya kiuchumi, na uzoefu wa baadhi ya wafanyabiashara kutoka India walioko nchini.
(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMAPILI, JULAI 10, 2016.

VIDEO:Masanja Mkandamizaji amvisha pete mchumba wake.

$
0
0
Miongoni mwa vitu vinavyozungumzwa kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja na picha zinazomuonyesha Masanja Mkandamizaji akimvisha pete msichana anaedaiwa kuwa mchumba wake,kwenye picha hizo Masanja na mchumba wake huyo wanaonekana wakiwa kanisani na baadhi ya waumini akiwemo Mc Pilipili na Emanuel Mbasha.

Hapo chini kuna video ambazo zimewekwa na Mc Pilipili zikionyesha mazingira halisi ya namna shughuli hiyo ilivyokuwa.

CCM Zanzibar Yahofia Kutapeliwa

$
0
0
CHAMA cha Mapinduzi  (CCM)  Zanzibar kimewataka viongozi na watendaji wa chama hicho kuhakikisha mikataba ya kibiashara wanayofunga inapitiwa na kuwashirikisha wanasheria ili kuepuka vitendo vya utapeli.

Kimesema kuwashirikisha wanasheria wakati wa kufunga mikataba ya aina mbali mbali ya kukodisha Mali za Chama hicho kutasaidia kumaliza kero na migogoro ya matumizi mabaya ya Rasilimali za CCM.

Hayo aliyasema  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai katika mwendelezo wa ziara ya  kukagua na kuhakiki mali za Chama hicho huko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Alisema matatizo ya matumizi mabaya ya Mali za chama hicho yanayojitokeza katika maeneo nchini ni kutokana  na baadhi ya viongozi na watendaji kufunga mikataba ama makubaliano na wafanyabiashara bila ya kuwashirikisha wanasheria ama kupata ushauri kutoka kwa viongozi wa ngazi za juu  hali inayopelekea baadhi ya watu kutumia nafasi hiyo kujinufaisha wenyewe badala ya kuangalia maslahi ya CCM.

Vuai alieleza kwamba njia pekee ya kuziweka salama mali mbali mbali za chama hicho ni uwepo wa maridhiano na makubaliano yanayojali na kuzingatia matakwa ya kisheria.

“ Naendelea kusisitiza kwamba mali za CCM hazipo kwa ajili ya kuwanufaisha watu wachache, bali zipo kwa ajili ya kukinufaisha chama ambacho ni taasisi halali ya watu wengi na jambo lolote la umiliki wa Rasilimali zake lazima liendeshwe kwa misingi ya uwazi na usawa kupitia utaratibu halali wa kisheria.

Pia Mali zote kwa sasa ni lazima zitumike ipasavyo kwa mujibu wa matakwa ya sera ya CCM ya siasa kwenda sambamba na ukuaji wa uchumi ndani ya chama chetu.”, alisisitiza Vuai na kuongeza kuwa CCM kwa sasa inaendelea na mipango ya kuhakikisha Rasilimali zake zinatumika vizuri kuimarisha uchumi wa Chama hicho badala ya watu wachache wanaojimilikisha mali hizo kinyume na taratibu.

Alisema lengo la ziara hiyo ni kuhakiki mali za Chama hicho pamoja na kuwakumbusha  Viongozi na Watendaji wa Chama na Jumuiya kwamba chombo pekee kinachomiliki mali zote ni Baraza la Wadhamini la Chama hicho hivyo hakuna chombo kingine  tofauti na baraza hilo kinachoweza kutoa maamuzi ya kuuza mali za Chama.

Aliwaagiza Viongozi wa Mkoa huo kupitia upya mikataba yote waliyofunga na wafanyabiashara katika eneo linalomilikiwa na CCM ili kuhakikisha maslahi yanayopatikana yanaendana na mahitaji ya wakati uliopo sasa kibiashara.

Aliwasihi Wana CCM kuendelea na utamaduni wa kuwashirikisha viongozi wa ngazi mbali mbali za chama hicho pindi panapotokea kasoro za kiutendaji ili ziweze kutatuliwa kwa kufuata utaratibu wa kinanuni na kimaadili kwa lengo la kuepuka kauli na malalamiko yasiyofaa ndani ya Chama hicho.

Naibu Katibu Mkuu huyo alisema kazi iliyopo sasa mbele ya CCM ni kuendelea kujiimarisha kisiasa huku ikitekeleza ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2015/2020 kwa kasi na kwa ufanisi zaidi ili wananchi waendelee kuiunga mkono na hatimaye Chama hicho kiweze kuandika historia mpya ya ushindi wa mwaka 2020.

Alisema maeneo ya CCM yaliyopo Nungwi ni Rasilimali kubwa kwani yapo katika ukanda wa Utalii hivyo yanatakiwa kulindwa na kuangaliwa vizuri na wahusika yasije yakaangukiwa mikononi kwa watu ambalo ni matapeli na wapinga maendeleo na  wakatumia fursa hiyo kupandikiza migogoro na mipasuko isiyokuwa ya lazima ndani ya Chama.

Pamoja na hayo alisema endapo uongozi wa Mkoa huo utahitaji msaada wa kisheria Afisi kuu ipo tayari kuwaunga mkono kwa kuwapa mwanasheria wake ili aweze kuwashauri na kuwaelekeza njia bora ya kufunga mikataba rasmi inayotambulikana kisheria.

Nao Viongozi wa Mkoa huo wameahidi kuzifanyia kazi kwa haraka changamoto zilizojitokeza katika maeneo yanayomilikiwa na chama hicho ili kwenda sambamba na matakwa ya sera ya ukuaji wa uchumi ya CCM.

Walisema licha ya CCM ndani ya mkoa huo kuendelea na harakati za kuimarisha shughuli za kisiasa, bado wana fursa ya kuhakikisha rasilimali za chama hicho hasa zilizopo katika maeneo ya uwekezaji katika sekta ya utalii zinakinufaisha chama badala ya watu wachache wanaojali maslahi binafsi.

Mtoto wa miaka minne Auawa, atupwa kisimani

$
0
0
Mtoto wa kike, Rahila Salim Ali (4) amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa umening’inizwa kisimani na vidole vya mikono vikiwa vimekatwa na mashavu kuchubuliwa. 

Tukio hilo limetokea jana asubuhi, katika eneo Njiapanda, Mbagala, Temeke baada ya mtoto huyo kutoweka nyumbani siku nne zilizopita.

Akizungumzia tukio hilo, mama mzazi wa mtoto huyo, Raziah Ramadhani alisema binti yake alitoweka nyumbani saa tano asubuhi, wakati wakiwa pamoja wakitazama televisheni. 

“Alitoka nje kama anaenda kucheza na wote hatukuwa na wasiwasi. Baada ya saa moja tulishtuka baada ya kutomuona, hivyo ikabidi tuanze kumtafuta,” alisema. 

Alisema walitoa taarifa polisi na kwenye baadhi ya vyombo vya habari bila mafanikio hadi jana mwili wake ulipokutwa umening’inizwa kwenye kisima cha nyumba ya jirani yao.

 “Nilipofika nilishangaa kuona nguo zake ni kavu na ana majeraha,” alisema. 

Alisema kisima hicho kina tundu dogo ambalo huenda wauaji walijitahidi kuusukumiza mwili huo ili ionekane kama amefia humo ikashindikana. 

Alisema mpaka juzi mchana, kilikuwa kikitumika na kuwa huenda mwili huo ulining’inizwa usiku wa kuamkia jana. 

Baadhi ya majirani waliliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina na kuwachukulia hatua watu ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.

 Kamanda wa Polisi Temeke, Andrew Satta alisema wanaendelea na uchunguzi:“Taarifa zilizopo ni kwamba amekufa maji lakini kwa hayo mazingira mengine tunaendelea kufanya uchunguzi zaidi.”

Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Ukosefu Na Upungufu Wa Nguvu za Kiume

$
0
0

Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  

Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.

Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kufahamu   kuhusu   SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME  tafadhali  tembelea :

Ukisoma  vizuri  kuhusu  mfumo  wa  nguvu  za  kiume, utagundua  kuwa   Suala  la  nguvu  za  kiume  ni  suala  la  kimfumo.  Ili  mwanaume  awe na nguvu  za  kiume, aendelee  kuwa  na  nguvu  za  kiume na  azilinde  nguvu  zake za  kiume, ni  lazima  ogani  zote zinazo  husika  na  mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ziwe  na  afya  njema  na  ziwe  na  ushirikiano   thabiti  na  wenye  afya.

Vile  vile , utagundua  kuwa , mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ni  kama  ifuatavyo:

i.Mishipa  imara  ya  ubongo  na  yenye  afya  njema

ii. Mishipa  imara  ya  uti  wa  mgongo  (  spinal  cords )

iii.Mishipa  imara  itumikayo  kusafirisha  damu  mwilini  (  Blood Vessels )

iv. Mfumo  imara  wa  usafirishaji  damu  mwilini

v. Mishipa  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema

vi. Uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  ubongo, mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume.

Hivyo  basi, ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, na  aendelee  kuwa  na  nguvu  hizo ni  lazima  mambo  yote  muhimu  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume  yawe  imara  pasi na  hitilafu  yoyote.

Hitilafu  yoyote  katika  mambo  hayo, itasababisha  ukosefu na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume  kwa  mwanaume  huyo.  Pale inapotokea    hitilafu  ama  mapungufu  katika  ogani  zaidi  ya  moja  kati  ya  zilizo  tajwa hapo  juu, basi  tatizo  kwa  muhusika  huwa  kubwa  mara  dufu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU &  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Mwanaume   anapopatwa na  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, ubongo  hutoa  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo  husafirisha  taarifa  hadi  kwenye  mishipa &  misuli  ya  uume.

Mishipa  ya  uume inapopokea  taarifa  hiyo, hutanuka. Na  mishipa  ya  uume  inapotanuka, hufanya  mambo  mawili  muhimu  sana :

i.Husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  hivyo  kuruhusu  damu  kuingia kwa  kasi  sana   ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  imara  bara bara.

ii. Huibinya na  kuiziba  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuzuia  kunyonya  ama  kufyonza  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa ya  uume.  (  KAZI  KUBWA  YA  MISHIPA  YA  VENA  ILIYO  KARIBU NA  MISHIPA  YA  UUME  NI KUHAKIKISHA  HAKUNA  DAMU NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME. HIVYO  BASI  DAMU  INAPOINGIA  NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME, MISHIPA  YA  VENA  HU “SENSE” JAMBO  HILO  KWA  HARAKA  NA HIVYO  KUIFYONZA  DAMU  HIYO  KUTOKA KWENYE MISHIPA  YA UUME  YA  KUITOA  NJE YA MISHIPA  YA  UUME.  NA  DAMU INAPOKOSEKANA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME, HUUFANYA  UUME  KUSINYAA  NA  KULEGEA )

Mtu  anayepiga  punyeto  husababisha  mambo  yafuatayo  katika  mwili  wake :

1. Huuwa  nguvu  ya  mishipa  & misuli ya  uume ambayo  ndio  inayo husika  na  kusimama  kwa  uume

2. Mishipa  ya   uume  inapo  sinyaa  na  kukosa  nguvu  yake  ya  asili, husababisha  mambo  yafuatayo :

i.Huondoa  uwezo  wa  mishipa  &  misuli  ya  uume  kutanuka, na  hii  ndio  sababu  inayo  wafanya  waathirika  wa  punyeto  kutumia  nguvu  nyingi  sana  katika  kuufanya  uume  usimame.

ii.Huondoa  uwezo  wa  mishipa &  misuli  ya  uume  kuibana  na  kuiziba  mishipa  ya  vena, na  hii ndio  sababu  inayo  fanya  waathirika  wa  punyeto  kufika  kileleni  haraka  sana, kwani damu  inayo  ingia  kwenye misuli  ya  uume   hufyonzwa  ndani ya  muda  mfupi sana. 
 
 Hii  hutokea  kwa  sababu  mishipa na  misuli  ya  uume inakuwa  imelegea,na  mishipa  ya  vena inakuwa  imepwaya, hivyo  msuguano wowote ule  hufanya  mishipa  ya  vena  kufunguka  na  kufyonza  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  na hivyo  kuufanya  uume  kusinyaa  ndani ya dakika ama sekunde  chache sana.

3. Vile  vile  punyeto  hufanya  uume  kusinyaa na  kurudi ndani  na  kuufanya  uonekane kama  uume  wa  motto mdogo.

Kwa  ufupi  punyeto  husababisha  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuu  zifuatazo :

i.Kwanza   hudhoofisha  na  kuharibu  mishipa  ya  uume,  ambayo  ndio  hufanya  uume kusimama.

ii.Pili  hudhoofisha  utendaji  kazi  wa  mishipa  ya  ateri, ambayo  ndio  hutumika  kama  njia  ya  kusafirisha  damu kupeleka kwenye  misuli  ya  uume  na  ivyo  kuufanya  uume  usimame

iii. Tatu, punyeto  hupelekea  kuvuja  kwa  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kusababisha  damu  kufyonzwa  kwa  haraka  sana  kila  iingiapo ndani  ya  misuli ya  uume  na  matokeo  yake  ni  uume   kusimama  kwa  muda  mfupi  sana  wakati wa  tendo  la  ndoa.

iv. Punyeto  huathiri  mtiririko  wa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume, kwa  sababu  hudhoofisha  misuli &  mishipa  ya  uume  pamoja  na mishipa ya  ateri  ambayo  ndio  hutumika  katika  kusafirisha  damu kwenda  kwenye  uume

DALILI  ZA  MTU  ALIYE  ATHIRIWA  NA  PUNYETO
Dalili  kuu  za  mtu  aliye athiriwa  na  punyeto  ni  kama  ifuatavyo:

i.           Uume  kusinyaa  na  kuwa  kama  wa  mtoto
ii.         Uume kurudi  ndani
iii.       Uume  kusimama  ukiwa  legelege
iv.       Kufika  kileleni  haraka  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

TIBA   YA   NGUVU  ZA  KIUME  KWA MTU  ALIYE  ATHIRIKA  NA  PUNYETO.
Dawa   asilia  ya  nguvu  za  kiume iitwayo JIKO  ni tiba  bora  na  ya  uhakika  kabisa  kwa  mtu  aliye  athiriwa   na  punyeto.  Dawa  hii, pamoja  na  mambo  mengine  mengi, husaidia  kufanya  mambio  yafuatayo  katika  mwili  wa  mwanaume  aliye  athiriwa  na  punyeto :

i.Kuimarisha  mishipa  & misuli  ya  uume  ulio  legea na  hivyo  kuurejeshea  uwezo wake wa  asili

ii. Hutibu   tatizo  la  uume  kurudi  ndani

iii.Humaliza  tatizo  la  kusimama  kwa  uume  ukiwa  legelege

iv.Hutibu  na  kuponya  kabisa  tatizo  la  kufika  kieleleni  haraka.

BEI  YA  DAWA  :  Dawa  hii  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU (Tsh. 80,000/=)

MAHALI  INAPOPATIKANA :  Dawa  hii  inapatikana  katika  duka  la  dawa  asilia  liitwalo  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  UBUNGO   nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA   karibu  na SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING.

Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu. Watafikishiwa  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  DAR  ES  SALAAM.

Kwa   wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  MABASI

Kwa  wateja  waliopo   Zanzibar  wata fikishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa boti.

Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  ama  DHL.

MAWASILIANO :  WASILIANA  NASI   KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee kila  siku  kwenye  blogu  yetu :

Wasimamishwa kazi baada ya mama kujifungua kwenye korido

$
0
0

Siku chache baada ya vyombo vya habari  kuripoti mjamzito kujifungulia kwenye korido ya Kituo cha Afya Lyabukande, Shinyanga kwa kukosa huduma, uongozi wa Halmashauri ya Shinyanga umewasimamisha kazi watumishi wawili wa kituo hicho kwa tuhuma za uzembe. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Kiomoni Kibamba ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, jana aliwataja waliosimamishwa kuwa ni pamoja na muuguzi msaidizi wa kituo hicho, Zulfa Mussa na mhudumu katika maabara, Peter Mazengo. 

Kibamba alisema wamewasimamisha kazi na kufunguliwa mashtaka ya kukiuka maadili ya utumishi huku wakipewa siku 14 kujibu kwa utaratibu wa ajira ya utumishi. 

“Baada ya hapo tunasubiri baraza la madiwani ndilo litatoa uamuzi juu yao.” 

Alisema wakati tukio hilo linatokea, watumishi hao walikuwa zamu na kushindwa kumsaidia mjamzito huyo na kitendo hicho kilibainika kuwa cha makusudi na uzembe wa wazi. 

“Awamu hii ya tano ni awamu nyepesi kwa kufanya kazi sababu imenyooka na iko wazi. Mtu anayeona hawezi kwenda na kasi atupishe ili wabaki wanaoweza kutekeleza majukumu yao kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria za nchi na nilishasema mara kwa mara suala hili,” alisema Kibamba. 

Kamati iliyoteuliwa kuchunguza jambo hilo, ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Dk Athuman Pembe ilibaini kuwa baada ya mjamzito huyo kujifungua kwenye korido, watumishi ambao hawakuwapo bali walipata taarifa na kufika kumhudumia mtoto ambaye ana afya nzuri na baada ya muda aliruhusiwa kurudi nyumbani. 

Ilivyotokea 
Tukio la mjamzito huo, Margareth Charles (22), mkazi wa Kijiji cha Kizungungu lilitokea Julai 2 baada ya kuelezwa na mtaalamu wa maabara kuwa hakuna huduma waende sehemu nyingine, lakini mama huyo alishindwa kutokana na uchungu.

Mtendaji wa Kata ya Lyabukande, Julius Lugende alisema wananchi wamekuwa wakikilalamikia kituo hicho kwa muda mrefu na ilifikia wakati waliandamana kuwakataa watumishi waliopo kutokana na wajawazito kunyanyasika na kujifungua bila usaidizi.

Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson Asema Kura za Wabunge wa UKAWA Hazitoshi Kumvua Madaraka ya Unaibu Spika

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson amesema hoja ya wabunge wa Ukawa kutaka aenguliwe kwenye wadhifa huo inafanyiwa kazi na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ambayo iwapo itaridhia, itarejeshwa bungeni kupigiwa kura ambazo hata hivyo, hazitatosha kwa uchache wao. 

Dk Tulia alisema hayo jana wakati akihojiwa na Tido Mhando katika kipindi cha Funguka kinachorushwa na Azam TV.

“Hoja ikishakuja bungeni hapo sasa huwa ni kampeni na baadaye kupigiwa kura. Kwa kuwa waliopeleka hoja ni wabunge wa upinzani, hivyo wanatakiwa kufikisha idadi fulani ambayo kiuhalisia wao kwa sasa hawana,” alisema.

Kwa karibu mwezi mzima kwenye Bunge la Bajeti, wabunge wa Ukawa walimsusia Dk Tulia na walikuwa wakitoka bungeni kila alipoingia, tayari wameanzisha mchakato wa kumuondoa madarakani kwa madai kuwa hawatendei haki na anaminya demokrasia ndani ya Bunge.

Dk Tulia alisema Katiba inatambua kwamba kiongozi aliyechaguliwa anaweza kuondolewa madarakani na wale waliomchagua, hivyo wabunge wa upinzani wametumia haki yao ya msingi na kinachosubiriwa ni hoja yao kufanyiwa kazi.

“Kanuni imeweka wazi na msingi ule umejengwa kwenye Katiba kwa sababu inatambua wale waliomchagua kiongozi wasiporidhika naye wanaweza kumuondoa madarakani. Nafarijika kuona wanachukua hatua, hivyo mimi sina malumbano nao,” alisema.

Hakuna maridhiano 
Dk Tulia alisema hakuna maridhiano yanayotakiwa baina yake na wabunge wa Ukawa kwa kuwa hana malumbano nao, bali kanuni na taratibu zinafuatwa kufanikisha hoja yao ya kumuondoa madarakani.

Naibu Spika huyo alisema maridhiano huwapo baina ya watu wanaolumbana na kwamba, baina yao hakutakuwa na suala hilo.

Lori lakwepa magari manne, lagonga mengine manne na kuua watu wanne

$
0
0
Licha ya lori lililokosa breki katika Mlima Iwambi nje kidogo ya Jiji la Mbeya, kuyakwepa magari manne, limeyagonga mengine manne na kusababisha vifo vya watu wanne na majeruhi 22. 

Ajali hiyo ilitokea juzi usiku katika mji mdogo wa Mbalizi, Barabara Kuu ya Mbeya - Tunduma, ambako lori hilo liligonga basi aina ya Toyota Coaster na magari madogo matatu.

 Katika tukio hilo, watu watatu walifariki muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali Teule ya Ifisi na hadi tunakwenda mitamboni walikuwa hawajatambuliwa, huku mwingine aliyetambuliwa kwa jina Philip Cheyo (39) akifariki jana asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
 
Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Ifisi, Elimate Sanga alisema walipokea miili ya watu watatu na majeruhi 22 wakiwamo sita waliohamishiwa Hospitali ya Rufaa  ya Mbeya kutokana na hali zao kuwa mbaya. Sanga alisema hadi jana asubuhi, ali- kuwa na wagonjwa 12 waliolazwa. 

Ofisa Muuguzi Msaidizi wa Hospitali ya Rufaa, Lucy Elias alisema Cheyo ambaye alikuwa mmoja wa majeruhi sita, alifariki jana asubuhi akiwa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU). 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari alisema wanachunguza chanzo cha ajali hiyo ingawa taarifa za awali zinaonyesha kuwa lori lilifeli breki wakati likiteremka mlima huo. 

Akisimulia tukio hilo, kondakta wa lori hilo, Wilberd Joseph akiwa wodi ya nne ya Ifisi alisema lilianza kuongeza mwendo wakati wakianza kuteremka mlima huo na ndipo dereva akalalamika halina breki. 

“Nilisikia dereva ananiambia, tuombe Mungu, breki zimegoma kabisa, ndipo lori likazidi kuchanganya na dereva alijitahidi kuyakwepa magari zaidi ya manne hivi, lakini tulipoingia mjini kabisa (Mbalizi), kulikuwa na (basi dogo) Hiace ikitokea upande wa kushoto kuingia barabara kuu, alipolikwepa tela likagonga basi jingine aina ya Coaster lililokuwa limesimama upande wa kulia,” alisema kondakta huyo. 

Alisema baada ya kugonga basi hilo lililokuwa likitokea Tunduma kwenda Mbeya, pia liligonga magari mengine yaliyokuwa nyuma ya Coaster hiyo. 

Mmoja wa majeruhi wa basi hilo, Isack Mwaipaja aliyelazwa katika Hospitali ya Ifisi, alisema walipofika Mbalizi dereva wao hakutaka kuingia stendi na aliamua kuteremsha abiria pembeni mwa barabara kuu ndipo ghafla wakasikia kishindo. 

“Bila kujua kinachoendelea nikajiona nimelowa usoni, kupangusa hivi nikaona damu inavunja usoni, kumbe ni lori lilikuwa limetugonga ubavuni na wale waliokuwa nyuma ya basi ndiyo walioumia sana kwani tela lote liliishia huko,” alisema. 

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe Awazuia Vijana wa Chadema ( BAVICHA ) Kwenda Dodoma Kuzuia Mkutano wa CCM

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza kusitisha mpango wa vijana wa chama hicho kwenda Dodoma kuzuia Mkutano Mkuu wa CCM ili kuepusha maafa ambayo yanaweza kutokea. Badala yake, Mbowe amesema wataendelea kusaka haki ya kufanya mikutano ndani na nje ya nchi. 

Sambamba na uamuzi huo, chama hicho kimetaka viongozi sita wa Baraza la Vijana (Bavicha) wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kuachiwa mara moja. 

Mbowe alitoa tamko hilo jana wakati akizungumza na wanahabari jijini Arusha, katika mkutano wa mameya na wenyeviti wa halmashauri 18 zinazoongozwa na Umoja wa Katiba ya wananchi (Ukawa).

 Sababu za kusitisha 
Mbowe alisema wamewataka vijana wa Chadema nchi nzima ambao walianza kujiandaa kwenda Dodoma kuisaidia polisi kuzuia mkutano huo wa Julai 23 kutokwenda kwa sababu polisi wamepewa maagizo ya kuwapiga na kuwajeruhi, hivyo wao hawataki kupambana nao. 

“Nawataka vijana wote wa Chadema waliokuwa wanajiandaa kwenda Dodoma wasitishe na wasubiri maelekezo mapya ya Chadema,” alisema Mbowe. 

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alisema wana taarifa Jeshi la Polisi limejipanga kuwanyima dhamana viongozi wa Bavicha hadi baada ya mkutano wa CCM, ingawa viongozi wote wa chama hicho hawana hofu ya kukaa mahabusu. 

Aliwataka vijana hao kutokwenda Dodoma na wawaache CCM waendelee na mkutano wao kwa kuwa Chadema haina hofu na mkutano wa chama hicho, bali walitaka dunia ione jinsi polisi wanavyofanya kazi kwa maelezo ambayo yanakiuka Sheria ya Vyama vya Siasa na Katiba ya nchi. 

“Wakati sisi tunazuiwa kufanya siasa, Rais anafanya siasa, Waziri Mkuu anafanya siasa, mawaziri wanafanya siasa, wakuu wa mikoa na wilaya wanafanya siasa jambo ambalo si sahihi,” alisema.

 Alisema lengo la Bavicha kwenda Dodoma ni kuchoshwa na uonevu wa kuzuiwa kufanya mikutano ya ndani na hadhara wakati CCM wanaendelea na mikutano yao. 

“Waliona pengine itakuwa busara washinikize polisi kuona maagizo yao ya kuzuiwa mikutano yanatekelezwa kwa wote,” alisema. 

Alilitaka jeshi la polisi kufanya kazi kwa kufuata taratibu kwa kutoa haki sawa kwa wote, kwa kuruhusu vyama vyote kufanya mikutano yao. 

Apinga tamko la Mwigulu
Kuhusu tamko la Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kuhusu mikutano hiyo, Mbowe alisema hawakulielewa tamko hilo la Rais, kuwa mikutano ambayo imezuiwa ni ya hadhara na maandamano na si ya ndani. 

Alisema mikutano ya ndani ya chama hicho imezuiwa kwani Chadema Wilaya ya Kahama walikuwa na mkutano wa ndani wa uchaguzi ambao umezuiwa. 

 Alisema mkutano wa ndani na wabunge wa Chadema mkoani Shinyanga ulizuiwa na pia mahafali za Vijana wa Vyuo Vikuu wa Chadema (Chaso). 

“Lakini wakati haya yanafanyika, CCM waliendelea na mikutano yao na mahafali yao,” alisema. 

Alisema Chadema itaendelea kudai haki ya mikutano na maandamano katika mahakama za ndani na nje ikiwamo ya Afrika ya Mashariki. 

Viongozi wa madiwani 
Katika mkutano wa wenyeviti wa halmashauri 18 zinazoongozwa na Chadema, Mbowe alisema Calist Lazaro, Meya wa jiji la Arusha amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa wenyeviti wa madiwani wa Chadema nchini.

Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob alichaguliwa kuwa katibu wa madiwani wote wa chama hicho na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime, Moses Matiku alichaguliwa kuwa mnadhimu wao. Wote hao watakuwa wajumbe wa Kamati Kuu Chadema. 

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji alisema katika mkutano huo wenyeviti hao wamepatiwa elimu juu kuongoza vyema halmashauri zao ili kuchochea maendeleo. 

“Siku mbili za mkutano huu tumekaa na kuweka mikakati bora ya kuhakikisha halmashauri zinazoongozwa na upinzani zinafanya vizuri,” alisema. 

Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan awataka wanawake kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan amesema ukuosefu wa fedha, taarifa pamoja na ujuzi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ni vikwazo vinavyoendelea kuongeza umaskini nchini ambapo wanawake ndio waathirika wakubwa.

Mama Samia aliyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua mradi wa Green Voices ambao unakusudia kuwasaidia wanawake katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo wamegeuza changamoto kuwa fursa.

“Wote tumeshuhudia jinsi Bara la Afrika linavyopoteza mabilioni ya shilingi kila mwaka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi”. Alisema Mama Samia.
 
Awali Rais wa Mfuko wa Wanawake Afrika Mama Maria Terezo la Vega Fernandes alisema atahakikisha anatimiza dhamira yake ya kuendelea kuwasaidia wanawake wa Tanzania na Afrika katika maeneo ya kilimo, afya, Amani na haki za binadamu.

“ Miradi ya Green Voices imeanzishwa katika nchi mbalimbali duniani kwa lengo la kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo yao”. Alsema Mama Tereza.

Naye mjumbe wa Bodi ya ushauri wa mradi huo Balozi Getrude Mongela alimpongeza mama Tereza kwa juhudi zake za kuwaunganisha wanawake katika kuleta maendeleo na ukombozi wao kwa ujumla.

“Mradi wa Green Voices umenikumbusha maazimio ya mkutano wa Reo De Jenairo uliofanyika mwaka 1992, mkutano wa Cairo na Beijing ambayo ilizingatia ushirikishwaji wa wanawake katika suala zima la mazingira”. Alisema Balozi Mongela.

Naye mratibu wa mradi huo nchini Bi.Sechelela Balisydia amesema wanawake 15 kutoka Tanzania walipata mafunzo ya jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na uongozi nchini Spain.

Aliongeza kuwa baada ya mafunzo hayo wameweza kutoa kutoa mafunzo kwa wenzao 250 kwa kuwashirikisha katika miradi ya ufugaji nyuki, mitambo ya kukaushia mboga inayotumia nishati ya jua na kilimo cha uyoga.

Miradi hiyo ipo katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Kigoma, Mwanza, Morogoro na Kilimanjaro ambapo mradi huo mpaka sasa umetimiza mwaka mmoja

Daraja la Nyerere limezikusanya hizi Bilioni kupitia tozo mpaka sasa hivi

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ‘NSSF’ Prof. Godius Kahyarara ameeleza mapato yaliyopatikana kwenye daraja la Nyerere tangu lilipofunguliwa rasmi May 14 2016.

Prof Kahyarara amesema jumla ya shilingi bilioni 1.3 zimekusanywa kutoka Daraja hilo lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam kupitia tozo mbalimbali zinazolipwa na vyombo vya usafiri vinavyopita darajani hapo.

Prof. Kahyarara ameongeza kuwa fedha hizo zimekusanywa kupitia tozo za magari yakiwemo magari binafsi, magari ya abiria, magari ya mizigo, pikipiki na bajaji zinazopita darajani hapo kila siku.

Kwa upande wake Msimamizi wa Mradi wa Daraja la Nyerere, Bw. Gerald Sondo alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na uongozi wa daraja wana mpango wa kuboresha huduma za malipo ili watumiaji wa daraja hilo waweze kulipa tozo kwa kutumia kadi za kielektroniki………

“Hivi karibuni tunatarajia kuanzisha mfumo wa malipo kwa kutumia kadi za kielektroniki ambapo madereva wa vyombo vya usafiri watakuwa wanatumia kulipa tozo pindi wanapopita darajani”

Aidha alisema kuwa kwa sasa idadi ya magari, pikipiki na bajaji zinazopita darajani hapo ni kati ya elfu 8 hadi elfu 10 kwa siku na wanalipa tozo kulingana na aina ya chombo cha usafiri.

Akieleza kuhusu usalama wa daraja na watumiaji wake, Sondo alisema kuwa ulinzi ni wa uhakika kwa saa 24 kila siku kwani kuna askari wa kutosha pamoja na kamera zinazosaidia zoezi hilo pia kuwa wanaandaa kanuni za matumizi ya daraja ikiwemo faini za uharibifu, uchafuzi wa mazingira, matumizi mabaya ya njia na lugha za matusi.

Daktari feki akamatwa katika chumba cha wagonjwa mahututi hospitali ya Rufaa Morogoro

$
0
0
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Zakaria Benjamini mkazi wa Tungi Manispaa ya Morogoro baada ya kuingia hospitali ya rufaa kwa nia ya kufanya utapeli na kutaka kutoa huduma kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa jeshi hilo Ulrich Matei amesema mtu huyo ameshikiliwa na jeshi hilo kufuatia tuhuma zinazo mkabili na mara baada ya kubaini ukweli wa jambo hilo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.

Jeshi La Polisi Lakamata Vipande Vya Meno Ya Tembo 666 Vyenye Thamani Ya Zaidi Ya Sh.bilioni Nne.

$
0
0
JESHI la Polisi  nchini kwa kishirikiana na Ofisi za Interpol Kanda ya Kusini Mwa Afrika imefanya operesheni  na kukamata vipande vya meno ya Tembo 666 vyenye uzito wa Kilogram 1279.19 vyenye thamani zaidi ya  Sh. Biloni Nne.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna wa  Jeshi  la Polisi (CP), Diwani Athuman wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.Amesema kuwa vipande hivyo vya tembo vimehusisha watu tisa  kati yao mmoja ni Raia wa Guinea na mwingine ni Raia wa Uganda.

Amesema kuwa katika operesheni Usalama  III wameweza kukamata  vitu mbalimbali kutokana na taarifa za kiitelijensia zilizokusanywa wakati wa matayarisho ya operesheni ya Usalama III, ambapo waliweza kukamata mitambo  18 ya kutengenezea gongo pamoja na  lita  za gongo  960  zimekamatwa.

Athuman amesema katika Operesheni  hiyo wameweza kukamata watuhumiwa 265  ambapo baada ya uchunguzi watakaobainika  kuhusika na  vitendo vya kihalifu watafikishwa mahakamani mara moja

Kamishina Othman amesema ametoa rai kwa wanunuzi wa magari nje ya nchi kuwasiliana na ofisi za Interpol za ndani au nje ya nchi magari yanakotoka kwa uchunguzi kabla ya kuyanunua ili kuondoa usumbufu wa kukamatwa mara kwa mara katika operesheni  kama hizi.

Amesema kutokana na operesheni hiyo jeshi la polisi halitakubali kuona kundi la watu wachache linalotishia usalama wa maisha ya raia wema na  mali zao na wataobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria bila kusita.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya July 12

Waziri wa Fedha Dr Philip Mpango Akemea Wanaopotosha Taarifa za Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika huduma za utalii

$
0
0

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, amekemea wanaopotosha taarifa za Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika huduma za utalii.

Amesema kodi hiyo iliwekwa miaka miwili iliyopita; na serikali haina sababu ya kuwaongezea wananchi mzigo huo.

“Hata hao wanaosema utalii umepungua kwa sababu ya kodi hiyo, watoe hizo takwimu tuzione, watalii wanaangalia vitu vingi ikiwemo vivutio, usalama, amani, magonjwa. Wasiotaka kulipa kodi wanawachanganya tu wananchi...tunasisitiza kila mwananchi kulipa kodi. Tunachotaka sisi ni Taifa lifaidike na rasilimali ambazo Mungu ametupatia,” alisema Waziri Mpango.

Dk Mpango alisema hayo jana mjini Morogoro, wakati wa ufunguzi wa kikao cha kazi cha wakaguzi wa ndani wa wizara, idara, wakala, sekretarieti za mikoa na mamlaka za Serikali za Mitaa, iliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA).

Ufunguzi huo ulikwenda sambamba na uzinduzi wa miongozo mitatu ya ukaguzi wa ndani.

Pia, Waziri Mpango aliwataka watumishi wa umma, kufuata na kutekeleza maagizo ya serikali, ikiwa ni pamoja na kufanyia mikutano na semina zote katika kumbi za serikali.

Alisema vinginevyo watachukuliwa hatua kama vile kukatwa mishahara ili kufidia fedha za serikali wanazozitumia kulipia kumbi. Dk Mpango alisema agizo hilo linatakiwa kutekelezwa kuanzia Julai Mosi mwaka huu ili kuokoa fedha za umma.

“Atakayekiuka hili tutamkata mshahara wake maana watoto wanakaa chini, hospitalini hakuna vitanda na magodoro, hakuna maji, hakuna madarasa, hakuna vyoo, hivyo tunatakiwa kupunguza matumizi ambayo si ya lazima ili tuboreshe sekta zingine,” alisema Dk Mpango.

Alisema hata kama semina au mkutano unagharamiwa na wafadhili, ni jukumu la viongozi wa umma kuwaomba kufanyia mikutano hiyo kwenye kumbi za serikali ili fedha zinazobaki zitumike kwa kazi nyingine. 

Aliwaagiza wakaguzi wa ndani kufanya kazi kwa uadilifu na kufuata miongozo ya kitaifa na kimataifa ili kudhibiti mchwa wanaotafuna mali za umma.

Alisema kuna hisia na madai kuhusu uadilifu mdogo wa baadhi ya wakaguzi wa ndani na hivyo kusababisha kushindwa kutoa taarifa za vitendo vya ubadhirifu kwa sababu nao ni sehemu ya washiriki wa vitendo hivyo.

“Natambua si wakaguzi wa ndani wote ambao uadilifu wao unatiliwa shaka. Nafahamu kwamba wapo waliowajibishwa kwa ajili hiyo. Hivyo naomba muongeze bidii katika mapambano haya na serikali hatutawaonea haya wakaguzi wachache wanaoendelea kuchafua jina la taaluma hii. Tutawachukulia hatua kali za kinidhamu wale wote watakaokwenda kinyume na taaluma hii,” alisema.

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkuu wa JICA Tanzania, Toshio Nagase alisema Serikali ya Japan kupitia JICA imekuwa ikitoa msaada wa kitaalamu kwa Ofisi ya Mkaguzi wa Ndani katika kuwajengea uwezo wakaguzi wa ndani tangu mwaka 2009.

Wauaji 30 wa Albino na Vikongwe Kunyongwa

$
0
0
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema jumla ya watuhumiwa 30 wa mauaji ya vikongwe na wenye ulemavu wa ngozi (albino) nchini, wamehukumiwa kunyongwa, baada ya kupatikana na hatia ya mauaji hayo.

Dk Mwakyembe amesema pia kuwa serikali itaendelea kutoa adhabu kali kwa watu watakaobainika kuendelea kuhusika na mauaji ya watu hao ili kumaliza tatizo hilo, ambalo limeipaka matope Tanzania kwa kuonekana sio kisiwa tena cha amani. Waziri huyo alisema hayo mjini Shinyanga jana, alipofanya ziara yake ya kikazi.

Alisema katika miaka ya hivi karibuni tatizo la mauaji ya wenye ualbino na vikongwe yamepungua nchini na kwamba watahakikisha wanayakomesha kwa kutoa adhabu kali kwa wauaji.

“Tatizo hili la mauaji ya vikongwe na albino linatutia sana doa nchi yetu kimataifa ambayo imekuwa ikisifika kwa amani na utulivu, hivyo natoa mwito kwa wananchi waachane na mauaji ya watu hawa wasio na hatia pamoja na mahakama zifanye kazi kwa kutoa hukumu za haraka kwa watu watakaohusika na mauaji hayo,” alisema Dk Mwakyembe.

Hata hivyo, Dk Mwakyembe alisema serikali itaanza mikakati ya kujenga mahakama za mwanzo kwa kila kata nchi nzima ili kuondoa misongamano za kesi mahakamani na kukarabati majengo ya mahakama ambayo yamechakaa.

Aliwataka wakuu wa wilaya, waunde kamati za maadili ya wilaya.

Akisoma taarifa ya mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Telack, alitaja changamoto ambazo zinawakabili kuwa ni uchakavu wa majengo ya mahakama, uhaba wa mahakimu na magereza ya Shinyanga na Kahama kuwa finyu na hivyo kusababisha mlundikano wa wafungwa.

UKAWA Wakubaliana kuwanyima mafuta wakuu wa wilaya

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameagiza wenyeviti wa halmashauri 18 nchini zinazoongozwa na Ukawa kuacha utaratibu wa kutoa fedha za halmashauri kuwasaidia mafuta ya magari wakuu wa wilaya au kuzitumia kwa ajili ya masuala ya kisiasa ya vyama vyao.

Akizungumza na mameya na wenyeviti wa halmashauri zinazoongozwa na Ukawa katika mkutano uliofanyika juzi mjini Arusha, Mbowe alisema viongozi hao wanapaswa kuhakikisha fedha zote zinazokusanywa na halmashauri hizo zinatumika kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Alisema katika kikao hicho cha mameya na wenyeviti wa halmashauri, wametambua kuwa kuna matumizi mabaya ndani ya Serikali, mbali na wafanyakazi hewa ambao wapinzani wamekuwa wakilalamika tangu mwaka 2005.

Mbowe alisema bado kuna halmashauri ambazo zimekuwa zikitumia fedha kufadhili ofisi za wakuu wa wilaya na chama tawala, jambo ambalo sasa kwa halmashauri za Ukawa halitakuwapo.

“Maeneo ambayo wakuu wa wilaya wamezoea kuomba fedha za mafuta na CCM wamekuwa wakiomba fedha kwa ajili ya kazi zao tunawaambia wasithubutu tena kwenda kwenye halmashauri zinazoongozwa na Ukawa, kwani hatutawapa fedha na tunawaumbua,” alisema.

Mbowe alisema katika halmashauri za Ukawa hawataki kusikia kuna fedha zimetolewa kwa wakuu wa wilaya au chama chochote cha siasa.

Alisema katika kikao hicho wamekubaliana kuanzisha mipango mikakati ambayo itawezesha kubuniwa vyanzo vipya vya mapato ambavyo ni rafiki kwa wananchi, kupatikana kwa ajira na kuboresha huduma muhimu za Watanzania.

Akizungumza baada ya maelekezo hayo, Mwenyekiti wa Madiwani Chadema nchini ambaye pia ni Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro alisema watatekeleza na hawatakubali kuingiliwa na wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na makatibu tawala.

Calist alisema katika halmashauri za Ukawa uamuzi wa mwisho wa uendeshaji wa halmashauri utafanywa na madiwani na siyo mtu kutoka nje ya halmashauri hizo.

“Tutasimama na kutetea mamlaka ya kisheria ya Serikali za mitaa hapa nchini,” alisema.

Katibu wa Madiwani wa Ukawa nchi nzima ambaye ni Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob alisema watahakikisha wanasimamia utendaji mzuri wa halmashauri zote wanazoziongoza ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.

Askofu Gwajima Akamatwa na Jeshi la Polisi Muda Mfupi Baada ya Kutua Uwanja wa Ndege

$
0
0

Hatimaye Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye amekuwa akitafutwa na Jeshi la Polisi kwa siku kadhaa alikamatwa jana katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) alipowasili akitokea Japan.

Baada ya Askofu Gwajima kukamatwa na Kikosi cha Polisi cha Uwanja wa JNIA alipelekwa moja kwa moja Kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya mahojiano akidaiwa alitoa maneno ya uchochezi mwezi uliopita.

Akizungumzia kukamatwa kwake, Kamanda wa Polisi Uwanja wa JNIA, Martin Otieno alisema askofu huyo aliwasili saa 2.45 asubuhi akitokea Japan kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Kenya.

Otieno alisema mara baada ya kukamatwa alipelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya kuhojiwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

“Ni kweli tulimkamata Askofu Gwajima hapa uwanja wa ndege wa JNIA baada ya kuwasili kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya na tulipomuhoji alidai kuwa alikuwa nchini Japan,” alisema Otieno. 

Mwanasheria wake Peter Kibatala alisema Gwajima alifika Kituo Kikuu cha Polisi saa 4.45 asubuhi kwa mahojiano mafupi na aliruhusiwa kuondoka baada ya kujidhamini yeye mwenyewe.

“Askofu Gwajima amehojiwa leo (jana) na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu na amejidhamini yeye mwenyewe, ameruhusiwa kuondoka hivyo tunasubiri chochote kitakachoendelea,” alisema Kibatala bila kueleza mahojiano yalivyokuwa.

Askofu Gwajima alikuwa anatafutwa na polisi tangu mwezi uliopita baada ya kusambazwa mkanda kwenye mitandao ya kijamii unaodhaniwa una sauti yake akipendekeza Rais mstaafu Jakaya Kikwete kufikishwa mahakamani kwa yote yaliyofanyika wakati wa utawala wake ambayo sasa Rais John Magufuli anayashughulikia kwa mtindo wa kutumbua majipu.

Katika mkanda huo, sauti hiyo inadai kuwa baadhi ya viongozi wa CCM wametuma watu mikoani kupiga kampeni ya kutaka Rais Magufuli asipewe uongozi wa chama hicho kwa sasa kama ilivyo utaratibu wa chama hicho na kwamba hilo likifanyika basi Rais abadili katiba ili mstaafu huyo aweze kufikishwa kortini.

Tangu ulipotolewa mkanda huo, makachero wa polisi wamekuwa wakipiga kambi nyumbani kwa Askofu Gwajima kwa lengo la kumkamata lakini hawakumpata.

Baadaye ilikuja kufahamika kwamba askofu huyo alikuwa amekwenda nje ya nchi lakini haikujulikana ni nchi gani.

Hata hivyo, baada ya kutafutwa na polisi, Gwajima kupitia wakili wake Kibatala alisema atakaporejea nchini atakwenda moja kwa moja polisi kwa ajili ya mahojiano.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amekuwa akisisitiza kwamba jeshi litaendelea kumtafuta askofu huyo kwa kushirikiana na polisi wa kimataifa, Interpol.

Wanafunzi Chuo Kikuu Kizimbani Kwa Mauaji

$
0
0
WATU watatu wakiwemo wanafunzi wawili wa vyuo vikuu vilivyoko jijini Dar es Salaam wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka ya mauaji.

Wanafunzi hao ni wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Hussein Mustafa (26) na wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Haruna Nkuye (24) ambao wanashitakiwa pamoja na fundi makenika Rajabu Ally (41) wote wakazi wa Dar es Salaam.

Washitakiwa hao wanaodaiwa kuhusika na mauaji hayo kwenye tukio la ujambazi katika Benki ya CRDB eneo la Chanika Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, walisomewa mashitaka na Wakili wa Serikali Jackson Chidunda mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi.

Akisoma hati ya mashitaka, Chidunda alidai Desemba 8, mwaka jana katika eneo la Chanika, Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, washitakiwa walimuua Ramadhani Halili, Shan Rajabu na Thomas Otemu.

Hakimu Shahidi alisema washitakiwa hawatakiwi kujibu mashitaka kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo isipokuwa Mahakama Kuu.

Upande wa jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa ili wamuunganishe mshtakiwa Mohamed Ungando ambaye jana hakuwepo mahakamani.

Awali, mshitakiwa Mustafa aliiomba mahakama imsaidie apate matibabu kwa kuwa viungo vinamuuma kutokana na adhabu alizopewa akiwa mahabusu.

Hakimu Shahidi alisema gerezani kuna utaratibu wa matibabu, kama hatatibiwa kesi itakapotajwa tena aijulishe mahakama. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 14, mwaka huu.

Jeshi la Polisi Laanza Uchunguzi Dhidi Ya Vijana Wanaojiunga na Vikundi Vya Kikaidi Vya Al- Shabaab na IS

$
0
0
JESHI la Polisi nchini, limesema linafanya uchunguzi kubaini baadhi ya vijana wanaojiunga na vikundi vya kigaidi, vikiwamo IS na Al-Shabaab ili wawachukulie hatua za kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa  Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athuman, alisema wimbi la vijana hao kujiunga na makundi hayo yanayopigwa vita duniani kote, linatokana na ushawishi wa baadhi ya watu.

“Tuna taarifa za kuwapo baadhi ya vijana wa Kitanzania wanaojiunga na vikundi vya ugaidi… suala hili ni la kiintelijensia zaidi, hatuwezi kulizungumzia kiundani, tunaendelea kulifanyia kazi, tutakapofikia sehemu nzuri tutawaambia,” alisema Athuman.

Alisema wakati suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi, jeshi hilo liliendesha operesheni maalumu ya siku mbili, ambayo ilishirikisha nchi 26 za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Alizitaja nchi hizo kuwa ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Angola, Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Lesotho, Malawi, Madagascar, Mauritius, Msumbuji, Namibia, Afrika Kusini, Swaziland, Zambia, Zimbabwe, Comoro, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Shelisheli, Sudan Kusini na Somalia.

Alisema operesheni hiyo iliyojulikana kama ‘Operesheni Usalama III’ ilishirikisha nchi zaidi ya 26 na ilisaidia kukaguliwa kwa magari 1,632 ambayo kati ya hayo, 10 yalikuwa ya wizi huku matano yalibainika yameingiliwa ‘chases’.

Alisema operesheni hiyo pia ilisaidia kukamatwa  pikipiki 12 za wizi, huku 18 zikiendelea kufanyiwa uchunguzi zaidi kutokana na kutokuwa na vibali halali.

Athuman alisema operesheni hiyo ilisaidia pia kukamatwa aina mbalimbali ya dawa za kulevya, zikiwamo heroine gramu 83, bangi kilogramu 398.6, mirungi kilogramu 30, bunduki aina ya shotgun moja, gobole 11, risasi 104, mkuki mmoja na vipande 15 aina ya exprojel v6, cotex na detonator.

Alisema walikamata wahamiaji haramu 43  maeneo mbalimbali nchini, kati yao 18 ni raia wa DRC, ambao walikamatwa mikoa ya Rukwa na Kagera, wakati 22 wanatoka Burundi waliokamatwa mikoa ya Shinyanga, Tabora na Kagera na raia wawili wa Rwanda walikamatwa Kagera na mmoja wa Kenya alikamatwa Tabora.

“Katika operesheni hii tulifanya ukaguzi katika kampuni mbalimbali zinazofanya biashara ya madini ambapo tatu zilionekana kukosa uhalali wa kupewa leseni ya kuendelea kufanya biashara ya madini,

“Kampuni hizi ni Delicore Metal Company Ltd, Madandwa Gold Mining Export Import (T) Ltd na Alex Mining Co. Ltd, na tatizo lao linaendelea kushughulikiwa na Wizara ya Nishati na Madini. Pia yalikamatwa madini aina ya Acquqmiline Smoky Quartz kilogramu 20.

Alisema pia walikamata gamba moja la kasa mkoani Ruvuma, mbao 410 zilizokuwa zikisafirishwa bila kibali mikoa ya Pwani, Iringa na Morogoro, nyama ya pundamilia kilo 45 na bidhaa bandia.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images