Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali Yakunjua Makucha.....Yakamata mali za kampuni ya Uingereza zenye thamani ya Dola mil 500

0
0
SERIKALI imeiamuru Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuzishikilia akaunti za Kampuni kubwa ya mafuta ya Uingereza (BG Group) hadi pale itakapolipa Kodi ya Ongezeko la Mtaji (capital gain tax) yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 502.

Taarifa zilizoandikwa na gazeti moja la wiki, TRA tayari imetoa maelekezo kwa Benki ya Citi kushikilia akaunti za kampuni hiyo.

TRA inadai kiasi hicho kutokana na faida iliyotokana na BG Group kuziuza hisa zake asilimia 60 kwa kampuni nyingine za nishati za Royal Dutch Shell, Exxon Mobil, Ophir Energy na Statoil.

Biashara hiyo, pia ilihusisha maslahi ya BG, visima vya mafuta namba 1 na 4 vilivyopo kusini mwa Tanzania.

Vyanzo vya habari kutoka Wizara ya Fedha na TRA, vilisema amri hiyo imetolewa kushikilia akaunti za BG Group hadi kodi hiyo itakapolipwa.

Baada ya akaunti kukaguliwa, ilibainika fedha zilizopo katika benki hiyo, ni Dola milioni 5 tu, ikiwa ni sawa na asilimia moja tu ya kiasi inachodai TRA.

Uamuzi huo unazua maswali katika rufaa, ambayo  BG Group imeifungua katika Mahakama ya Kodi Tanzania ikipinga namna tathimini ilivyofanyika kupata kiasi hicho inachodaiwa.

BG Group, inasema haiwezi kulipa kodi kwa sababu iliwekeza Dola milioni 850 ya jumla ya faida iliyopata katika visima Tanzania.

BG Group iliendelea kudai kampuni yake dada, tayari imetumia dola bilioni 1.5 kama uwekezaji, na hivyo kuashiria upotevu wa mtaji.

Kwa mujibu wa Sheria ya Rufaa ya Kodi ya Mapato (2006), mtu yeyote asiyeridhishwa na kiasi cha kodi anachodaiwa anaweza kupinga kwa kumuandikia Kamishina Mkuu.

Ibara ya 12 (3) ya sheria hiyo inasema. “Wakati taarifa ya kupinga kiasi cha kodi kinachodaiwa inapowasilishwa, mtu anayepinga anatakiwa wakati akisubiri uamuzi wa mwisho wa Kamishina Mkuu kwa mujibu wa Ibara ya 13, alipe kiasi cha kodi ambacho hakikupingwa au theluthi moja ya kiasi kilichopingwa, bila kujali ukubwa wa kiwango”.

Lakini wanasheria na wataalamu wa nishati, wameitaka Serikali na BG Group kutatua mkwamo huo, ambao unaweza kuchelewesha uamuzi wa mwisho wa uwekezaji wa dola milioni 30 wa mradi wa usindikaji wa gesi ya asili ya matumizi mbalimbali (LNG), ambao kampuni hiyo ina mipango ya kuijenga kwa ubia na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Ujenzi huo wa mtambo wa LNG, utakaozalisha tani milioni 10 za gesi kwa mwaka, awali ulikuwa ukamilike mwaka 2020.

Lakini chini ya sheria za nchi, ujenzi hauwezi kupitishwa hadi kodi itakapolipwa kwanza.

Serikali imebakia kimya kuhusu suala hilo, lakini Kamishina Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata alisema suala hilo bado halijafika kwake, huku Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akilitaka gazeti hilo kumuuliza Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Dk. James Mataragio, ambaye hakuwa tayari kusema lolote.

Kuna wasiwasi mizozo kuhusu kodi inaweza kuathiri uwekezaji wa kigeni unaotarajiwa kuwekezwa nchini.

Wachambuzi wa mambo wanaamini kampuni ya Shell kupitia hisa BG, imejipanga kimkakati kujipatia vibali vya utafutaji wa mafuta Zanzibar kwa sasa kwa vile inamiliki pamoja na Serikali. Shell imekuwa ikihaha kwa miaka 10 sasa kujipatia vibali vya utafutaji mafuta visiwani humo.

Subiro Mwapinga, mshauri katika kampuni ya ushauri wa masuala ya gesi na mafuta ya Mnazi Bay Consulting Group, alisema mzozo wa sasa wa kodi umeuweka uwekezaji wa LNG katika hatari na unaweza kuathiri miradi mingine, ikiwamo ujenzi wa pipa la mafuta baina ya Uganda hadi Tanga wenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 10.

“Iwapo ukokotoaji wa kodi wa TRA umefanywa kwa kufuata taratibu zote za kimataifa na kuendana na sheria, kuna nafasi ndogo kwa BG Group kuweza kukwepa kulipa kodi, lakini bado hilo lina athari zake linapokuja suala la kubadilisha miundo ya mradi wa LNG, ambayo imepangwa kujengwa kwa ubia na washirika mbalimbali.

Kwa mfano, linaweza kusababisha washirika wengine kujenga miradi yao wenyewe ya LNG,” anasema Mwapinga.

Vyanzo vya habari ndani ya Wizara ya Fedha na TRA vilisema serikali pia imeamua kwa muda kusimamisha maombi ya Shell na BG Group ya kufufua vibali vya kutafiti nishati katika visima viwili hadi mgogoro huo utakapomalizika.

Kibali cha kisima namba 1 kinaishia Desemba mwaka huu, huku cha kisima namba 4 kikiishia Oktoba 2017.

Vibali vya kutafuta mafuta hutolewa kwa kipindi cha miaka minne kisha kufufuliwa kwa miaka minne mingine na kisha kipindi kingine cha miaka mitatu, baada ya hapo kampuni inatarajia kuomba kibali cha uendelezaji.

Kisha kwa mujibu wa kumbukumbu za serikali, kampuni itaongezewa wastani wa chini wa miaka 11 na kuomba vibali vya maendeleo lakini haiko tayari bado kwa hilo.

“Hali hiyo inaonesha Shell inatakiwa kuomba kuongezwa muda kwa kibali cha kutafuta mafuta kwa ajili ya kisima namba 1 na  4, lakini ongezo la muda huwa chini ya mamlaka ya waziri kwa vile liko nje ya kipindi cha miaka 11.  Ni hapo serikali ndiyo iliyoshikilia mpini,” vyanzo vya habari vilisema.

Mbunge wa Karagwe, Innocent Bashungwa (CCM) na mratibu wa zamani wa Taasisi ya Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji Tanzania,alisema usimamizi wa sekta ya mafuta na gesi unahusisha mabilioni ya dola za uwekezaji na miamala mbalimbali katika shughuli za hapa na pale.

“Wakati kunapotokea mabadiliko, migogoro inaweza kuibuka iwapo mfumo wa sheria wa nchi husika hauko wazi kuhusu taratibu za miamala,” alisema Bashungwa.

Mbunge huyo alisema, migogoro ni ishara ya udhaifu wa kisheria na maandalizi ya taratibu. “Naamini Serikali na BG zitapata suluhu kwa amani kwa fedha hizo za ongezeko la mtaji zinazobishaniwa.

“Vinginevyo wanachama wa Chama cha Mafuta na Gesi Tanzania na wawekezaji watarajiwa watalichukulia kama kengele ya hatari ya kitakachowatokea siku za usoni,” alisema mbunge huyo.

Serikali Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Uhaba wa Mafuta ya Petrol na Taa Hapa Nchini

0
0
MAMLAKA ya Udhibiti ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kuna akiba ya kutosha ya mafuta ya aina mbalimbali yanayoweza kutumika kati siku 13 hadi 39 nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi, alisema hayo jijini Dar es Salaam jana katika mkutano na wadau wa sekta ya mafuta nchini wa kupokea maoni juu ya mfumo wa uingizaji wa mafuta nchini.

Tamko la EWURA limekuja kukiwa na tatizo la uhaba wa mafuta ya petrol, dizeli na mafuta ya taa katika baadhi ya mikoa hali iliyosababisha wananchi wa mikoa iliyokumbwa na tatizo hilo kupata adha.

Ngalamgosi alisema akiba ya mafuta ya ndege iliyopo inatosha kutumika kwa siku 30 kwa nchini nzima, petroli ni zaidi ya siku 12, dizeli ni zaidi ya siku 15, mafuta ya taa ni zaidi ya siku 16, mafuta ya viwandani ni zaidi ya siku 39 na mafuta ya migodini zaidi ya siku 13.

Alisema sababu ya kutokea uhaba wa mafuta unaoonekana sasa ni kuwepo kwa sikukuu zilizofululiza na kusababisha magari ya kubeba mafuta kushindwa kusafirisha mafuta, na ama kufika kwa wakati katika mikoa hiyo iliyokubwa na kadhia hiyo.

Jumatano na Alhamisi zilizopita palikuwa na siku kuu za Eid el Fitri.

“Niwaombe Watanzania wawe na subira kwani mafuta yapo yakutosha, hivyo nawaomba wasinunue mafuta kwa kupaniki kwani magari ya kusafirisha mafuta yameanza kusambaza katika mikoa hiyo na hali itatulia kuanzia sasa,” alisema.

Alisema magari ya mafuta yameshapeleka shehena katika mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Songea na Mbinga ambako hali ya upatikanaji wa mafuta imeanza kutulia.

Mafuta ya taa
Ngalamgosi alisema uhaba wa mafuta ya taa ulitokana na meli iliyokuwa ikishusha mafuta ya ndege na petroli kuyachaganya wakati wa kuyasukuma.

Alisema kuwa kutokana na mchanganyiko huo ni wazi kuwa mafuta ya ndege ambayo ndio hutumika kama mafuta ya taa, hayaweza kutumika kwa matumizi ya kawaida.

“Mafuta ya ndege ndio hayo hayo yanatumika kama mafuta ya taa hivyo kutokana na kuchanganyika huko ilipaswa kusafisha matanki yote na mabomba ili kuweka mafuta mapya,” alisema.

Alisema zoezi la kuyasafisha matanki matano lilifanyika kwa wiki tatu mfululizo na kukamilika Julai 2, kabla ya kuanza kupokea mafuta na kuyasambaza Julai 3 mwaka huu katika mikoa ambayo kulitokea uhaba.

Kampuni za ndani
Ngalamgosi alisema EWURA imependekeza kubadilishwa kwa mfumo wa uingizwaji wa mafuta nchini kutoka nchini za nje kwa kuanzishwa mfumo mpya wa kutoa fursa kwa kampuni za ndani kuingiza mafuta nchini.

Ngalamgosi alisema kuwa amekutana na wadau wa sekta ya mafuta ili kupokea maoni ni namna gani wanaweza kuboresha ushindani na wamependekeza kuwa kila meli inayokuja lazima iwe na zabuni yake.

Alisema Tanzania inaingiza meli sita za mafuta kwa mwezi, hivyo EWURA imeona kuwa inapasa kuwa kila meli ya mafuta inayoingia iwe zabuni inayojitegemea.

“Kwa kufanya hivyo kutatoa fursa kwa watanzania kuweza kuingiza mafuta kwa sababu itapunguza gharama na uzuri utakuwa nchi itanufaika kuwa na watanzania wengi kushiriki katika kuingiza mafuta,”alisema.

Aliongeza kuwa kupita utaratibu mpya wanaamini kuwa makampuni ya Tanzania yatapata faida kubwa na TRA kukusanya mapato mengi.

Vijana wa Chadema watii agizo la Mbowe.......Viongozi Wao Kufikishwa Mahakamani Leo

0
0
Jeshi la Polisi limekwama kuwafikisha mahakamani viongozi wanne wa Taifa wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), baada ya kukosea hati ya mashtaka. 

Wanaoshikiliwa ni Mwenyekiti wa Taifa, Patrobas Katambi, Katibu Mkuu, Julius Mwita, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Joseph Kasambala na Mwenyekiti wa Mkoa wa Mbeya, George Tito. 

Akizungumza jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema makosa yametokea wakati wa uandaaji wa hati ya mashtaka.

 “Mahojiano yameisha, charge sheet (hati ya mashtaka) ikaandaliwa, lakini ikarudishwa tuifanyie marekebisho. Muda umepita wa Mahakama watapelekwa kesho (leo),” alisema. 

Hata hivyo, alisema kesi hiyo haina dhamana kwa upande wa kituo cha polisi na hivyo kuwalazimu watuhumiwa hao kuendelea kukaa rumande.

 “Wasubiri kesho (leo) wataka- poenda mahakamani kama wataamua kuwapa dhamana,” alisema Mambosasa. 

Kuhusu baadhi ya watuhumiwa hao kugawanywa katika selo tofauti za Chamwino na wengine kuachwa Kituo Kikuu cha Polisi, Mambosasa alisema huo ni utaratibu wa kawaida ambao unalenga kupata maelezo ya kila mmoja. 

“Hayo ni mahojiano tu ili kila mmoja upate anasema nini ndipo unawaweka sehemu tofauti. Hizo ni taratibu za mahojiano ili wasiendelee na mawasiliano,” alisema. 

Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Patrick Ole Sosopi alisema kisheria watuhumiwa hawatakiwi kukaa rumande kwa zaidi ya saa 24.

“Cha kusikitisha siku ya leo (jana) ambayo walisema wangewaleta mahakamani kwa kile wanachoamini wametenda kosa, lakini hadi sasa muda wa mahakama unaisha viongozi wetu hawajaletwa,”alisema na kuongeza: 

“Na sisi tunataka kuondoka ili tuone taratibu nyingine ambazo zinaweza kutuhakikishia  usalama wa viongozi wetu. Hadi sasa viongozi wetu hawajaletwa mahakamani.” 

Alisema hata kama polisi wanawaona viongozi wao wanamakosa, kisheria hawawezi kukaa na mtu kwa muda wa siku tatu bila kumfikisha mahakamani. 

Alisema utendaji wa polisi nchini ni tofauti na wa nje ya nchi ambapo kwa nchi za wengine, polisi ni sehemu ya huduma na si ya mabavu.

 Alisema hali hiyo inaleta kadhia na masumbuko kwa Watanzania na hivyo kupunguza imani yao kwa jeshi hilo.

 Wakili wa watuhumiwa hao, Fred Kalonga alisema wamekuwa na wateja wao tangu siku walipokamatwa kwa kuhakikisha wanahojiwa kwa mujibu wa sheria.

 “Kwa mujibu wa ahadi za polisi kuwa leo (jana) wanaletwa mahakamani. Kuanzia saa 1.30 asubuhi tuko mahakamani na sasa inakwenda saa 9.30 alasiri hakuna mtuhumiwa aliyeletwa. Kimsingi muda wa mahakama umeisha,” alisema. 

Alisema yeye na wakili mwenzake, Azack Mwaipopo walikuwa wanakwenda kufuatilia taratibu nyingine za kisheria za kuwawezesha kupata dhamana. 

“Tunakwenda kufuatilia taratibu nyingine lakini sisi tupo tayari muda wowote wakiletwa tutawadefend (tutawatetea) kwasababu tunaamini kwa mujibu wa maelezo ya wateja wetu wapo sahihi kuliko tuhuma zinazowakabili,” alisema. 

Wanachama wa Chadema walikuwa katika viwanja vya mahakama tangu saa 2.00 asubuhi hadi saa 9.30 alasiri baada ya kuelezwa na wakili wa watuhumiwa kuwa viongozi wa Bavicha hawatapelekwa mahakamani tena. 

Viongozi hao walikamatwa Ijumaa usiku katika baa ya Capetown walipokwenda kunywa na kula chakula. Wanadaiwa kwa tuhuma za kukusudia kuikashfu Serikali. 

Akizungumzia mpango wa vijana wa Chadema kuzuia mkutano wa CCM utakaofanyika Julai 23 mjini hapa, Sosopi alisema wanaiheshimu kauli ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe ya kuwataka kutokwenda kuzuia mkutano huo. 

“Tunaiheshimu kauli ya mwenyekiti na tunatambua kuwa vijana wengi nchi nzima wamejiandaa kwenda kuzuia mkusanyiko huo, lakini sasa tunashughulika na hili la viongozi wetu kukamatwa kwanza,”alisema. 

Alisema baada ya viongozi wao kupata dhamana wataitisha kikao cha Kamati ya Utendaji ya Bavicha haraka ili kujadili suala hilo na watatoa msimamo kama wanakuja na mkakati mwingine ama kuendelea na huohuo.

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi (A Wizard Student) - Sehemu ya 13

0
0
Mtunzi: Enea Faidy


....EDDY hakuwa na jinsi kwani aliona hana sababu yoyote ya kuwaficha wazazi wake juu ya tatizo lake.Aliamua kuwaambia ukweli Ili kama kuna uwezekano wa kumsaidia basi wamsaidie. Kwa kilio cha kwikwi kilichoonesha huzuni kuu iliyotawala moyo wake, Eddy alifungua kinywa na kusema ukweli.

"Sehemu zangu za siri... Zimepotea.. Sielewi zilikoenda!" Maneno ya Eddy yaliibua sura mpya kwa wazazi wake. Walishtuka mshtuko ambao haukuwahi kuwatokea maishani. "Ati nini? Hebu rudia tena..!" Mr.Alloyce hakuamini maneno ya mwanaye. Mama yake Eddy hakueweza hata kufumbua kinywa chake kwani alikuwa amechanganyikiwa kupita maelezo.

"Ndio hivyo baba yangu.. Sina raha ya kuwa hai..!" Eddy alizidi kulia pindi alipozungumza maneno hayo.

Kiukweli kisa kile kiliwakata maini wazazi wa Eddy. Walihisi kuishiwa nguvu kabisa mwilini, walibaki kimya wakiwa wameinamisha vichwa vyao. Huzuni iliyochanganyika na mshangao ndiyo iliyotawala katika jumba lile la kifahari la Mr.Alloyce. Zilipita dakika tano kukiwa na ukimya wa kuogofya. Hatimaye Mr.Alloyce alivunja ukimya ule kwa kumdadisi mwanaye kwa maswali.

"Kuna mtu ulimkosea?"
"Hapana baba!" Alijibu Eddy.
"Sasa ilikuwaje mwanangu?" Mr.Alloyce aliuliza kwa sauti ya upole sana.

"Sijamkosea mtu ila kuna binti anaitwa Doreen..!" Eddy alitaka kusimulia jinsi ilivyokuwa lakini baada tu ya kutaja jina la Doreen hakuweza kuendelea kuzungumza kwani alipigwa Kofi moja zito, likamyumnisha pale kitini, kichwa kikamzunguka akahisi kama radi imempiga. Alipiga ukelele uliowashtua wazazi wake na kufanya wahamaki.

"Eddy nini?"Mr.Alloyce aliuliza kwa mshangao kwani alimuona Mwanaye akidondoka kitini bila kujua kinachoendelea.

Wakazidi kuchanganyikiwa sana, wakamsogelea Eddy na kumwinua lakini Eddy hakuwa na habari, alikuwa kama mzoga ambao unapelekwapelekwa kokote bila kutoa ushirikiano. Hali hiyo ilimtisha sana mama Eddy, akashindwa kuvumilia akaangua kilio kikali.
 

Rais Magufuli aagiza vyombo vya Serikali kuanza kutumia mashine za EFD.

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk John Pombe Magufuli amewaagiza makatibu wakuu kuhakikisha vyombo vyote vinavyokusanya mapato serikalini vinatumia mashine za kielekrtoniki (EFD).
 
Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akizungumza na wakurugenzi wateule wa Halmashauri,Wilaya,Majiji na Manispaa Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi hao wa umma.
 
“Vyombo vya Serikali lazima vianze kutumia mashine za EFD,haiwezekani  wafanyabiashara wawe na mashine za EFD alafu maafisa wa serikali hawana,kama tumeamua kwenda kwa elektroniki lazima twende hivyo”Alisema Rais Magufuli.
 
Aidha amewataka wakurugenzi  wote kuchukua mashine hizi na kwenda nazo katika maeneo yao ya kazi ili ziwasaidie katika ukusanyaji wa mapato ya serikali katika halmshauri zao.
 
Pia amewaagiza wakurugenzi hao kukusanya kodi na kutatua kero za wananchi wa chini zisizokuwa na lazima na kuongezea kuwa kama watakuta watendaji wa chini yao wasioendana  na kasi ya awamu ya tano basi watumie madaraka yao kuwaweka sawa.
 
Rais magufuli pia amewaagiza wakurugenzi hao kusimamia ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi kwakuwa waliahidi kutatua kero za wananchi na wahakikishe wanazitatua ili wananchi waishi vizuri kwa amani ndani ya nchi yao na kuongezea kuwa viongozi wa juu wana imani kubwa sana nao ndio maana hata wakachaguliwa kutoka katika watanzania hawa milioni 50.
 
Aidha Rais magufuli amewataka wakurugenzi hao kusimamia kuanzishwa kwa viwanda vidogo vidogo katika maeneo yao ili kukamilisha azma ya serikali ya awamu ya tano ya kuwa na viwanda.

Mbali na hayo pia amewataka wakurugenzi hao kubadilika kifikra na kuachana na kuongoza kwa historia kwani wananchi wa sasa wamebadilika na hivyo wafanye kazi kwa bidii ili kuwatimizia wananchi yale wanayotaka na hivyo nchi itasonga mbele.

Kituo Cha Dk. Mwaka Chafutiwa Usajili Wake

0
0

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, limekifutia usajili wake wa kutoa huduma za kitabu, Kituo cha Tiba Asilia cha ForePlan Kliniki kilichopo Ilala Bungoni jijini Dar es salaam, kinachomilikiwa na Dkt. Juma Mwaka maarufu kama Dkt. Mwaka, kwa madai kuwa kimekiuka taratibu za kitabu za tiba mbadala.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dkt. Edmund Kayombo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ukumbi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Habari kwa kina baadae.

Maandalizi Mkutano Mkuu Maalum Wa CCM Yaiva

0
0
Maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliopangwa kufanyika Julai 23, 2016 mjini Dodoma yamezidi kuiva.

Taarifa iliyotolewa leo jijini  Dar es Salaam, ikiwa imesainiwa na Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye imesema, mkutano huo utatanguliwa na Kikao cha Kamati Kuu ya Halimashauri Kuu ya Taifa ya CCM (CC) kitakachofanyika Julai 21, 2016, na kufuatiwa na Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) siku ya pili, Julai 22, 2016.

NECTA Imezitaja Shule 10 Bora Kitaifa Pamoja na Shule 10 za Mwisho Kitaifa

0
0
Baraza la mitihani Tanzania(NECTA) imetangaza matokeo ya kidato cha sita 2016, na Kuzitaja shule zilizo fanya vizuri zaidi Kitaifa na zile ambazo hazikufanya vizuri Kitaifa.

Ubora wa shule umepagwa kwa kutumia kigezo cha Wastani wa Pointi (Grade Point Average – GPA) ambapo A=1, B=2, C=3, D=4, E=5 na F=7

Aidha, upangaji wa shule zilizofanya vizuri umezingatia shule zenye idadi ya watahiniwa wasiopungua 30 kama ifuatavyoa:

==>Shule 10 Bora Kitaifa
1. Kisimiri (Government)

2. Feza Boys (Private)

3. Mwanza Alliance Girls (Private)

4. Feza Girls (Private)

5. Tabora Boys (Government)

6. Marian Boys (Private)

7. Kibaha (Government)

8. Mzumbe (Government)

9. Ilboru (Government)

10. Tandahimba (Private)


==>Shule 10  za  Mwisho Kitaifa
1.Mpendae (Unguja)

2.Ben bella ( Unguja)

3.Tumekuja (Unguja) 

4.Green Bird Boys (Kilimanjaro)

5.Jang'ombe (Unguja )

6.Kiembesamaki (Unguja ) 

7.Tanzania Adventist ( Arusha )

8.Al-Ihsan Girls ( Unguja )

9.Azania (Dar es salaam )

10: Lumumba (Unguja)



Makamu wa Rais Samia Suluhu Kumwakilisha Rais Magufuli Rwanda Katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN ataondoka nchini kesho jumamosi kwenda KIGALI nchini Rwanda kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 27 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).

Makamu wa Rais atamwakilisha Rais Dkt JOHN MAGUFULI katika Mkutano huo wa siku MBILI ambao unatarajiwa kufanyika KIGALI – RWANDA kuanzia Julai 17-18 mwaka huu.

Katika Msafara wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN atafuatana na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Balozi AUGUSTINE MAHIGA na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Zanzibar Issa Haji Ussi.

Mkutano huo ambao utahudhuriwa na Makamu wa Rais utaanza kwa vikao vya ndani ambapo viongozi watajikita katika kujadili masuala ya kimkakati ikiwemo umuhimu wa kuliunganisha Bara la Afrika kibiashara kwa kuwa na soko la biashara huria ifikapo mwaka 2017 pamoja na mageuzi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Aidha Wajumbe wa mkutano huo wa 27 wa AU pia watachagua Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika pamoja na Makamu wake, Makamishna WANANE wa sekta mbalimbali na Majaji WANNE wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu pamoja na na kupitisha mapendekezo kuhusu gharama za uendeshaji wa umoja huo na bajeti ya fedha ya mwaka 2017.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN na Ujumbe wake wanatarajia kurejea nchini Julai 19 mwaka huu baada ya kumalizika kwa Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) KIGALI nchini RWANDA.

Dr Mwaka Kama Ameonewa Aende Mahakamani Ili Sheria Ifuate Mkondo Wake- Waziri Ummy Mwalimu

0
0

SEREKALI imemtaka Dk Mwaka kwenda kwenye sheria kama hajaridhika na uamuzi wa serikali  wa kukifungia kituo chake cha tiba za asili.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu wakati akiongea na wadau wa afya katika hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera.

Ummy alisema kuwa uamuzi uliofanywa na serekali wa kukifunga kituo cha afya cha dk Mwaka ni sahihi kwani hajaonewa kwasababu matangazo na huduma alizokuwa akitoa zilikuwa haziendani na maadili na taratibu za udaktari.

"Dk Mwaka asichonganishe wananchi na serekali yao kwamba tumewafungia huduma walizokuwa wakipata kwake wakati huduma alizokuwa akitoa hazikuwa na sifa"alisema Ummy

Alisema kuwa kama anaona ameonewa aende mahakamani ili sheria ifuate mkondo wake."Kama anaona tumemuonea aende mahakamani tutakutana huko"alisema

Waziri ummy Mwalimu yupo Mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo amezindua jengo la wodi ya wazazi iliyojengwa na shirikala jhpiego lenye thamani ya shilingi milioni 150.

Picha: Kwa mara ya kwanza Tanzania imeweza kuweka betri kwenye moyo wa mtoto

0
0
Na John Stephen, MNH
Dar es Salaam, Tanzania.Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)-Muhimbili LEO imefanya upasuaji mkubwa wa moyo kwa mtoto, Happiness John Josephat ambaye amepandikizwa peacemaker (betri ya umeme wa moyo) kwenye mfumo wa moyo wake.

Mmoja wa madaktari wa moyo walioshiriki kwenye upasuaji huo, Dk Godwin Sharau wa taasisi hiyo amesema upasuaji huo umechukua saa moja na kwamba mtoto anaendelea vuzuri.

Dk Sharau amesema mtoto huyo amepandikizwa peacemaker (betri ya umeme wa moyo) ambayo itasaidia kuunganisha mishipa ya fahamu ya umeme wa moyo ambayo inaunganisha vyumba vya moyo vya juu na chini kwenye moyo wa binadamu.

“Upasuaji huu ni wa kwanza kufanyika Tanzania. Upasuaji kama huu unafanyika kwa watu wazima, lakini watu wazima hawahitaji upasuaji wa moyo wa kupandikiza. Watoto wanahitaji upasuaji wa moyo wa kuipandikiza.

“Tatizo la mtoto huyu ni la kuzaliwa. Na ni nadra kutokea. Inaweza kupita miaka mingi bila watoto kutokea tatizo kama hilo. Upasuaji umefanywa kwa ushirikiano wa madaktari wa moyo na madaktari wa matibabu ya moyo nikiwamo mimi (Dk. Godwin Sharau), Dk Michael Valentine kutoka Marekani,  Dk  Kisenge na Dk Sulende Kubhoja, Dk wa usingizi, Dk Anjelan Muhozya na madaktari wengine ambao wamesaidia katika upasuaji huu,” amesema Dk Godwin Sharau.
 
Mama wa mtoto huyo, Elitruda Eligi Malley ambaye ni mkazi wa Sakina-Raskazon mkoani Arusha amewashukuru madaktari wa Taasisi hiyo kwa kufanya upasuaji huo na mtoto wake kutoka salama katika chumba cha upasuaji.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya July 16

Rais Magufuli Atoa Sh bil 12.3 kukarabati Mahakama

0
0

JAJI Mkuu, Mohamed Chande Othman amempongeza Rais John Magufuli kwa kutoa zaidi ya Sh bilioni 12.3 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya mahakama nchini.

Ametoa pongezi jana wakati akizindua Mahakama ya Wilaya ya Siha na Mahakama ya Mwanzo Bomang’ombe, iliyopo wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa Jaji Chande, ujenzi huo utaanza hivi karibuni kwa wilaya na mikoa ambayo hazina huduma hiyo, ili kusogeza huduma za mahakama karibu na wananchi, hali itakayosaidia kupunguza mrundikano wa kesi katika mahakama nyingine.

Wilaya 26 na mikoa sita hapa nchini, zinakabiliwa na ukosefu wa huduma za mahakama za wilaya pamoja na mahakama kuu, hali inayosababisha wananchi kutumia gharama kubwa kutafuta huduma hiyo katika wilaya na mikoa mingine.

Alieleza kuwa fedha zilizotolewa na Rais Magufuli, zitakwenda kwenye ukarabati na ujenzi wa mahakama za mwanzo, ili watendaji wa mahakama hizo wafanye kazi katika mazingira bora, ikiwa ni pamoja na kuwapo kwa mahakimu na makarani wa kutosha.

Alisema mbali na fedha hizo, pia anaishukuru serikali kwa kuongeza bajeti ya idara ya mahakama kwa mwaka wa fedha 2016/2017, ambapo wanakusudia kujenga mahakama za wilaya 10, Mwanzo 10, ambapo alitaja baadhi ya mikoa ambayo haina Mahakama Kuu kuwa ni mkoa wa Singida, Lindi na Mara.

Alisema asilimia 74 ya kesi za mashauri yapo katika mahakama za mwanzo, ambapo mashauri zaidi ya 1,150 yanayosikilizwa katika mahakama hizo hapa nchini, ambapo aliziagiza mahakama za mwanzo na wilaya kuhakikisha kesi zote za mashauri zinafunguliwa katika mahakama hizo.

Aliagiza ifikapo mwisho wa mwaka huu, hataki kuona wala kusikia kesi iliyomaliza muda wa miezi sita bado inaendelea kupoteza muda na gharama bila ya sababu za msingi, na kutoa wito kwa jeshi la polisi kujitaidi kukamilisha upelelezi wa kesi ili kuwajengea wananchi imani na kutoa fursa kwao kudai na kupata haki zao mahakamani kwa wakati.

Awali Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Moshi, Jaji Aishieli Sumari, alisema changamoto inayoikabili idara ya mahakama ni pamoja na ukosefu wa watumishi na mahakimu katika wilaya ya Siha, ambapo mahakama hiyo tangu kufunguliwa kwake Aprili 4 mwaka huu, tayari imepokea mashauri 87 na yaliyosikilizwa ni 19 kutokana na wilaya kutokuwa na hakimu.

Jaji Sumari alisema Mahakama ya Mwanzo Bomang’ombe imepokea mashauri 285 kuanzia Juni mwaka 2015 ambapo makosa ya jinai yalikuwa 239, talaka sita, mirathi 33, na kesi za madai 15, ambapo hadi sasa mashauri 10 yalikuwa bado hayajamalizika ndani ya miezi sita, tangu kufunguliwa kwa mashauri hayo.

Riwaya:Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 15

0
0
Mtunzi: Enea Faidy

...DORICE alikuwa akiyatafakari maneno ya malkia wa himaya aliyokuwepo kwa wakati ule. Alikuwa haelewi afanye nini na achague lipi kati ya kifo au kuolewa na jini. Alijikuta yupo kwenye wakati mgumu sana mpaka akajuta kutoroka shuleni. Alimlaani sana Doreen kwani ndiye chanzo cha matatizo yote. Alijikuta analia bila kujua msaada wake utatoka wapi.

Akiwa katika wimbi la mawazo alishtushwa na harufu Kali ya marashi iliyomfanya azinduke na kumtazama mgeni wake. Alipoinua kichwa chake alikutana tabasamu mwanana kutoka kwenye sura nzuri ya upole ya kijana Mansoor.

"Nakupenda Dorice.. Olewa na Mimi!" Alisema mansoor kwa sauti tamu iliyojaa huba. Lakini sauti na maneno hayo habvikuwa kitu kwa Dorice, aliachia sonyo Kali iliyodhihirisha chuki kuu dhidi ya Mansoor.

"Kama kuniua niueni! Siwezi kuolewa nawewe!" Dorice alisema maneno hayo kwa ujasiri sana bila kujali jambo hilo lingeonekanaje kwa Mansoor.
Mansoor alihuzunika sana, akatikisa kichwa kama ilivyokuwa kawaida yake . Akashindwa kuyazuia machozi ya damu machoni mwake lakini Dorice hakujali hilo.
"Dorice! Kwanini haunipendi? Au kwa sababu Mimi sio binadamu mwenzio?" Aliongea Mansoor kwa huzuni sana lakini Dorice hakujibu kitu.

"Tafadhali niambie Dorice... Nikufanyie nini ili uamini kuwa nakupenda?" Aliuliza mansoor kwa sauti ya upole.
"Utanifanyia?"
"Ndio Dorice!"
"Naomba unirudishe duniani..."
"Nikikurudisha sasa nitakuoaje? Siwezi ishi mbali nawewe!"
"Umesema utanifanyia nikuombacho.. Umeniahidi!"
"Ndio ila hilo suala gumu... Kwanini hunipendi?"
"Nampenda mtu mwingine.. Na ndie aliyenifanya nipate matatizo haya yote.." Dorice alisema maneno hayo huku machozi yakimlengalenga kwani kila alipomkumbuka Eddy alidondosha chozi na hakutaka kuamini kama Kweli Eddy amemwacha na yupo na Doreen.
"Unampenda nani?"
"Nampenda mtu anaitwa Eddy, siko tayari kimkosa nataka nipiganie penzi langu... Samahani sana Mansoor... Wewe ni mzuri ila sins hisia na wewe kabisa!" Dorice alijikuta akiropoka maneno hayo yote ili kufikisha hisia zake kwa Mansoor. Maneno Yale yaliugusa vyema moyo wa Mansoor, alihuzunika sana ila ilibidi akubaliane na ukweli.
"Nashukuru kwa kuwa mkweli Dorice.. Nakupenda sana ila siwezi kukulazimisha unipende... Hakutakuwa na mapenzi hapo.. . Naumia sana ila inabidi nizielewe hisia zako!" Alisema Mansoor kwa sauti iliyojaa masikitiko makubwa sana ila hakuwa na jinsi. Mansoor alikuwa ni mini mstaarabu kupita kiasi ingawa mama take alikuwa katili tena mwenye roho mbaya sana.

"Umenielewa Mansoor?!"
"Ndio.. Nimekuelewa sana! Ila nisimulie ilikuwaje?"
Dorice alifuta machozi na kutabasamu kidogo ingawa bado alikuwa na maumivu ya mapenzi kwa Eddy. Akajua ule ni msaada wa kwanza kwake kwenye eneo lile, akaamua kumsimulia kila kitu kama ilivyokuwa kati ya yeye na Eddy na kisa cha kutoroka.

Mansoor alihuzunika sana, akamwonea huruma sana Dorice.
"Binadamu wabaya sana..!"alisema Mansoor.
"Inaniuma sana! Nampenda sana Eddy..!"!

Mansoor alichukua kitu kama kioo, akakitazama kwa muda kisha kikamletea picha ya Doreen.
"Mh! Huyu Doreen.. Ni mtu mbaya sana .. In mtu hatari kupita kawaida..!"

Alisema Mansoor kwa mshtuko huku akimtazama Dorice. Dorice alikuwa haelewi chochote akabaki akishangaa tu.
"Doreen ni mchawi sana.. Na kuna kitu anatafuta! Amemharibu sana Eddy... Eddy yupo kwenye wakati mbaya na muda wowote anammaliza..!"

Maneno ya Mansoor yalimshtua Dorice
"Amemfanyaje? Nisaidie kumwokoa Eddy tafadhali..!"
"Mama hatanikubalia ila inabidi nikusaidie Dorice.. Yote ni kwasababu nakupenda.. Nitakusaidia usijali!"
Alisema Mansoor.
"Nitafurahi sana ukinisaidia Mansoor!"
"Usijali.. Ila mama ni kikwazo..!"
"Jitahidi Mansoor!"
Dorice alichanganyikiwa sana baada ya kusikia kuwa Eddy atauliwa muda wowote na Doreen, ilibidi azidi kumsihi Mansoor aweze kumsaidia kwa namna yoyote ile kwani alitambua uwezo mkubwa aliokuwa nao jini yule mstaarabu.

==> Endelea Nayo <<Kwa Kubofya Hapa>>

Ushuhuda: Nilimlisha Mume Wa Mtu Limbwata La Nyama Ya Bundi

0
0
USHUHUDA  WA   THEOFLIDA  WA  YESU : NILIMLISHA  MUME  WA  MTU, LIMBWATA  LA  NYAMA  YA  BUNDI.

Nawasalimu  wa  jina  la  YESU,  jina  kuu  kupita  majina  yote. Jina  langu  ninaitwa  Theoflida , ni mwanamke  mwenye  umri wa  miaka  38  mkaazi  wa    Mbezi  ya  Kimara  jijini  Dar  Es  Salaam, japo kiasili  ni  mwenyeji  wa  wilaya  ya  Ulanga, mkoani  Morogoro..

Nime amua  kuandika  waraka  huu  kwa  madhumuni  makuu  mawili, kwanza  ni  kushuhudia  MATENDO  MAKUU  ambayo  YESU  AMENITENDEA  na  pili, ni  kuwa  hasa  wanawake  wenzangu  kutojihusisha  kabisa  na   masuala  ya  WAGANGA  WA  KIENYEJI  kwa  sababu  waganga  wa  kienyeji ni  MAWAKALA  WA  KAZI  ZA  SHETANI  HAPA  DUNIANI  na   ni  MASHETANI  KABISA!...

Nitaanza  kwa  kuelezea  kisa  kilicho  nipelekea  kuingia  kichwa  kichwa  kwenye  mikono  ya  wakala  wa  shetani..

Nilikuwa  nimepanga  chumba  kimoja  maeneo  ya  Tabata  Mawenzi  huku  nikijihusisha  na  biashara  ya  genge.  Jirani  na  nyumba  niliyokuwa  nimepanga, aliishi   mwanaume  mmoja  na  mke  wake. Mwanaume  huyu  jina  lake  linaanzia  na  herufi  K  hivyo  katika  maelezo  yangu  nitakuwa  nikimtaja  kwa  herufi  K.

K  alikuwa  ni  mwanaume  mwenye  mafanikio  makubwa  katika  maisha  mwenye  kazi  nzuri.   Alikuwa  na  nyumba  zaidi  ya  moja, magari  ya  kifahari. viwanja , mashamba, na miradi mbalimbali  iliyokuwa  ikimlipa  vizuri  sana. Kwa  ufupi    K alikuwa  tajiri  mwenye  maisha  mazuri.

K  na  mke  wake  wote  walikuwa  wenyeji wa  wilaya  ya  Muleba,mkoani  Kagera .  Ndoa  ya  K  na  mkewe  ilikuwa  na  umri  wa  mwaka  mmoja...

 K  na  mke  wake  waliishi  maisha  mazuri  sana....Kwa  sababu  ya  ugumu  wa  maisha  yangu, nikajikuta  naanza  kutamani  maisha  ya  mke  wa  K..  Nikawa  natamani  mimi  ndo  ningekuwa  mke  wa  K  na  kufurahia  maisha  vile  mke  wa  K  alivyo  kuwa  akifurahia. Nilimuona  mke  wa  K kama  mtu  mwenye  bahati  sana  na  kutamani  bahati  hiyo  iwe  yangu.

Baada  ya  wazo  hili  kukomaa  ndani  ya  nafsi  yangu, nikaanza  kutafuta  njia  ya  kumteka  K kimapenzi na  kuchukua  nafasi  ya  mke  wake. Njia  pekee  niliyo  ona  inafaa, ni  kutumia  uchawi.

 Sasa  basi, kuna  rafiki  yangu  mmoja, anaitwa  Pamela. Pamela  alikuwa  anapenda  sana  mambo  ya  waganga  waganga, kwa  hivyo  alikuwa  anawajua  waganga  wengi. Hata  katika  biashara  yangu  ya  genge, alishanipeleka  kwa  waganga  kadhaa  kwa  ajili  ya  kupata  dawa  ya  mvuto  wa  bishara  yangu..

Nilipo  mfuata  Pamela, akaniambia  kuna  mganga  mmoja, ni  mkali  sana  wa  mambo  ya  mapenzi.. Mi mwenyewe  nina  mpango  wa  kumtafuta  lakini najipanga  kwanza  kwa  sababu  bei  zake  ni  kubwa.

Pamela  akasema  alimfahamu  mganga  huyo alipokuwa  katika  kijiji  cha  Mwalusembe, wilayani  Mkuranga..  Siku  hiyo  kuna  fumanizi  lilitokea, mwanaume  alikuwa  anatembea  na  mke  wa  mtu, kumbe  huyo  mwanamke  alikuwa  amewekewa  tego, huyo mwanaume  alipo  muingilia  mwanamke  huyo, wakawa  wamenasana.. Baadae  ikatafutwa  namba  ya  simu  ya mume  wa  mwanamke.  Mume  alipofika  kufumania, akakuta  mke  wake  amenasana na  mgoni  wake.. Akaitwa  huyo  Mganga   kwa  sababu  ndie  aliye  weka  hilo  tego,  alipofika  eneo  la  tukio  alifanya   uganga  wake, wale  wagoni  wakawa  wameachana.. Tukio  hilo  lilivuta  watu  wengi  sana..   Kwa  hiyo  Pamela  anasema, alimjulia  mganga  huyu  kwenye  tukio  hilo... Akafanikiwa  kutafuta  na  kupata  namba  zake.

Pamela   akanipa  namba  za  simu  za  mganga  huyo, nilivyo  mpiugia  akasema  yupo Handeni  kikazi  ila  baada  ya  siku  tatu  atakuwa  Bagamoyo ambapo  atakaa  hapo  kwa  mwezi  mzima  aki  agua  watu wenye  matatizo  mbalimbali.

Kweli  baada  ya  siku  ya  tatu, nikaenda  hadi  Bagamoyo  kuonana  na    huyo  mganga  ambaye  jina  lake  tu ni  kufuru  kubwa  kwa  Mungu.,. Yeye  anajiita  MUNGU  WA  KABILI  ambayo  tafsiri  yake  ni  MUNGU  WA  PILI.  Lakini  pia  nilishangaa  kumuona  mganga  mwenyewe anaokena  bado  kijana  ambaye sidhani  kama  ana  fikisha  miaka  arobaini.

NAANZA   KWA   KUPIMWA  MWILI  WANGU  KICHAWI
Mungu  wa  Kabili  akasema  kabla, hajaanza  kazi  ya  ‘kumtengeneza’   K , inabidi aanze  kwanza  kuuangalia mwili wangu  ili ajue  kama  ni  msafi  ama  mchafu.

Basi   nikapewa  dawa  nimeze, halafu  nikaambiwa   Yule kuku mweusi ambaye nilienda  nae mwenyewe,  nimshike  kichwani.  Baada  ya  hapo, Dokta  Mungu  wa Kabili  akaanza  kuongea  maneno  yake  ya  kiganga  huku  akiwa  ameshikilia  chungu  chenye  dawa  iliyo  katika  mfumo  wa  maji  maji.. Alifanya  hivyo  kwa  muda  wa  kama  dakika  kumi  na  tano  hivi. Alipomaliza  kufanya  uganga  wake, akaniambia  nimtue  Yule  kuku  mweusi  niliekuwa  nimembeba  kichwani.  Nilipo  mtua  nikashangaa  kumuona  kuku  Yule  amekufa.  Niliogopa  sana .

Basi  Mungu  wa  Kabili, akaniambia  mwili  wangu  ni  mchafu  sana. Roho  ya  mauti  imepandwa  kwenye  mwili  wangu. Hivyo  lazima  anisafishe  kwanza, kutoa  uchafu  ulio pandikizwa  mwilini  wangu  kichawi. Baada  ya  hapo  ndio  tutaendelea  na  zoezi  la  kumfanyia  ulozi  K.

Mungu  wa  Kabili  akaniambia  niende  nyumbani, nirudi siku inayo fuata  jioni  ya  saa  kumi  na  mbili  nikiwa  na  sarafu  350  za  shilingi   mia  mbili  mbili  ambazo  jumla  yake  ni  Shilingi  Elfu  Sabini, mchanga  wa  njia  panda  saba, pamoja  na  wembe  tatu..

NASAFISHWA   MWILI  WANGU  KICHAWI.
Ilipo  fika  saa  sita  kamili  za  usiku, mimi  , Dokta  Mungu  Wa  Kabili  pamoja  na  msaidizi wake, tukaongozona  hadi  njia  panda. Njia  panda  hiyo  ipo   huko  huko  Bagamoyo  porini..

Tulibeba, kigoda, chungu , vifaa  nilivyo kuja  navyo ( mchanga, wa  njia  panda  saba, sarafu 350, pamoja na asali  nusu lita ),  mawe  matatu,  mishumaa ya  rangi  nyekundu, mkaa, pamoja  na  dawa  nyingine  zilizokuwa  kwenye  vibuyu  kama  saba  hivi.

Tulipofika  eneo  la  njia  panda, Mungu  wa  Kabili, alizungushia  dawa  kuzunguka  eneo   tulipoweka  vitu vyetu, akamuagiza  msaidizi  wake, awashe  mishumaa  ambayo  idadi  yake  ilikuwa  kumi  na  nne, mishumaa  hiyo  iliwekwa  kuzunguka  eneo  tulilokuwa  sisi. Baada ya  hapo, ukawasha  moto, kwenye  mafiga  kisha  chungu  kikatengwa  pale, nikaweka  vitu vyangu  vyote  nilivyo  kuja  navyo, na  yeye  Mungu   wa  Kabili, akachanganya dawa  zake  anazo zijua  mwenyewe…

 Baada  ya  kama  dakika  arobaini  hivi, zile  dawa  zikawa  zimecheka, nikapewa  kibuyu  nikaambiwa  nikoge kwa  kuchota  maji  ya  kwenye  chungu  huku  chungu  kikiwa  kinachemka. Nikafanya  kama  nilivyo  elekezwa  huku  mganga  akiwa  anaongea  vitu  vyake  vya  kiganga  ambavyo  sikuweza  kuvielewa..

Nilipomaliza  kuoga, mganga  akanichanja  karibu  mwili  mzima, kisha  nikapakwa  hiyo asali. Baada  ya  hapo, tukarejea  kilingeni .  Mungu  wa   Kabili  akaniambia  nipumzike, ikifika  saa  kumi  na  moja  alfajiri  niamke  kwa  ajili  ya  kupikwa. Akasema  zoezi  la  kwanza  lilikuwa  kunisafisha na  kuniosha  kwanza, ambalo  limeshakamilika,  kinacho  fuatia  ni  kupikwa.

NAPIKWA   KICHAWI…
Ilipofika alfajiri  nilidamka, kama  nilivyo  agizwa  na  mganga  kwa ajili  ya  zoezi  la  kupikwa  kichawi.. Nikaelekezwa  kuingia  katika  chumba  maalumu  ambako  kulikuwa  na  chungu  kikubwa. Ndani  ya  chungu  hicho  yaliwekwa  maji  ya  baharini, majani  ya  mti  unaitwa  muosha  fedha  ama  mfedha  mfedha, majani  ya  mkaratusi  pamoja  na  majani  ya  mti  unaitwa  mkuyu, halafu  ndani  yake  zikawekwa  sarafu  zilizoisha  kutumika  muda  wake, pamoja  na  dawa  nyingine  kama  tano  hivi ambazo sikuambiwa  ni  dawa  gani…

Baada  ya  hapo, nikaambiwa  nikatwe nywele  zangu, pamoja  na  kucha  zangu. Baada  ya  kukatwa  nywele  zangu, vitu  vyote  hivyo  vikachukuliwa vikafungwa  kwenye  kitambaa  chekundu, ndani  ya  kitambaa  hicho  zikaongezwa  dawa  nyingine , halafu vikawekwa kwenye  chungu  kwa  ajili  ya  kupikwa.

Katika  chungu  hicho  pia  vikawekwa  visu  saba, vikiwa  vimesimama.  Baada  ya  kama  dakika  kumi  na  tano  hivi, mganga  akamwambia  msaidizi  wake, ‘ hebu  ongeza  chumvi  humo ‘. Nikatarajia kuona   itakuwa  chumvi  ya  kawaida  ninayo  ijua  mimi, ila  nikashangaa  kuona kinawekwa kipande  cha  mti..

Baadae  nilikuja  kugundua  kuwa,  katika  uganga  na  uchawi  kuna  kitu  kinaitwa  ‘Chumvi ya   Kichawi” kazi  ya  chumvi ya  kichawi  ni  kuukoleza  uchawi  ama  kukoleza  nguvu  ya  dawa.

 Mganga  aliniambia  vitu  vyangu  yaani  nywele  pamoja  na  kucha  vinaniwakilisha  mimi, kwa  hiyo kupikwa  kwa  vitu  vyangu  kunamaanisha  mimi  ndio  nimepikwa. Baada  ya  dawa  kupikwa,   nikapewa  maji  yale  na  kuelekezwa  kwenda  kuoga. Nikaambiwa  nikimaliza  kuoga  niende  nikapumzike  kwenye  chumba  change  hadi  nitakapo  pewa maelekezo  mengine.

NAFANYIWA   TAMBIKO  LA   JUA .
Ilipo  fika  saa  sita  mchana, nikapewa  dawa  Fulani  ya  kujipaka,  halafu  nikapelekwa  kwenye  eneo  la  juani, ambalo  chini  kuna  mchanga.  Hairuhusiwi  kuwa  katika  eneo  hilo  ukiwa na  viatu.   Baada  ya  kukaa  katika  eneo  hilo  kwa  kama  dakika  arobaini  hivi , mganga  alianza  kufanya  uganga  wake  pale  huku  akitamka  maneno  yake  ya  kiganga. Baada  ya  hapo, akanifuata  akanikabidhi  kibuyu  mkononi na  kuniambia nikishike  kwa  mikono  yangu yote  miwili kisha  nizungumz  nizungumze  maneno  yafuatayo :

“  EWE  JUA!   MIMI  NA  WEWE, TU KITU  KIMOJA  SASA!  WEWE  NI  MIMI  NA  MIMI  NI  WEWE. HAKUNA  MTU  YOYOTE  YULE  AWEZAE  KUTUTENGANISHA.

EWE  JUA!TANGU  UANZE   KUWEPO, HAUJAWAHI KUISHIA  NJIANI.

VIVYO  HIVYO, MIMI  PIA, SITO  ISHIA  NJIANI. NITAFANYA  MAMBO  YANGU  YOTE, NITAISHI MIAKA  YANGU  YOTE  KWA KADRI MWENYEZI  MUNGU  ALIVYO  NIKADIRIA , WALA HAKUNA  MTU  YOYOTE  YULE  ATAKAE  WEZA  KUNIZUIA, KWA  CHOCHOTE  KILE  NITAKACHO  TAKA  KUKIFANYA…

KAMA  WEWE  JUA  UMEWAHI  KUISHIA  NJIANI, BASI MIMI  PIA, NITAISHIA  NJIANI. NA  KAMA KUNA  MTU  ANAWEZA  KUKUZUIA  WEWE  JUA, BASI  MIMI  PIA  NAWEZA  KUZUILIKA. LAKINI  KWA  KUWA  WEWE  JUA  HAUJAWAHI  KUISHIA NJIANI, MIMI  PIA, SINTOISHIA  NJIANI. NA  KWA KUWA  HAKUNA  MTU  YOYOTE  ANAYE  WEZA  KUKUZUIA  WEWE  JUA, BASI  MIMI  PIA, HAKUNA  MTU  YOYOTE  ATAKAE  WEZA  KUNIZUA…

Niliagizwa  kutamka  maneno  haya  mara  arobaini.  Kila nilipo maliza  kutamka, nilinyweshwa  dawa  na  mganga, kutoka  kwenye  kibuyu  alicho  kuwa nacho…

Baada  ya  zoezi  hili  kukamilika  tulirejea  kilingeni  ili  lianze  zoezi  la  ‘ kumtengeneza’   K, mume  wa  mtu  mwenye  pesa.

NAPEWA   DAWA  ZA  KUMTEGA  “K”
Tulipo rudi  kilingeni, Mungu  wa  Kabili  akaniambia  nimpe  majina  yangu  kamili  pamoja  na  jina  la  huyo mwanaume  ninae  mtaka. Nikafanya  kama  alivyo  niambia. Akayachukua  yale  majina, akaandika  andika  vitu  vyake  ambavyo  sikuvijua  vizuri, baada  ya  hapo  akachukua  kioo  chake, akawa anatazama  kwenye  hicho kioo, kisha  akachukua  dawa  kutoka  kwenye  kibuyu, akaweka   kwenye  chungu  ambacho  ndani  yake kulikuwa  na  maji…. Baada  ya  kama  dakika  kumi  na  tano  hivi, akaniangalia  halafu akacheka  sana.. Akaniambia  niweke  kiganja  changu   kwenye  kile  chungu  nikafanya  hivyo..

Basi  akachukua  dawa  kutoka  kwenye  vibuyu  vitatu, ambazo  alizifunga  kwenye  vitambaa  vitatu  tofauti  kila  kitambaa  na  dawa  yake, kisha  akanipa  dawa  hizo na  kunipa  maelekezo  yafuatayo : Dawa  ya kwanza, utakunywa  na  maji  ya  kawaida, dawa  ya  pili, utaifunga  kwenye  mto  unao  lalia, halafu  dawa  ya  tatu  utaiweka  chini ya  kitanda  chako.

 Ndani  ya  siku  mbili  hizi, kuna  kitu  utakiona  ukiwa  umelala  usiku. Kitakujia  katika  ndoto. Kitu  hicho  kina  uhusiano  na  mwanaume  unaye  mtaka. Uki kiona  kitu  hicho  tu, basi haraka sana  nipigie  simu  nikuelekeze  kitu  cha  kufanya.. Nikazichukua  hizo  dawa  na  kufanya  kama  nilivyo  elekezwa.

NAMUONA   “ K” KWENYE  NDOTO.
Siku ya  kwanza  sikuona  chochote, ila  usiku  wa siku  ya  pili, nikiwa  nimelala  usiku, niliijiwa na  ndoto ya  ajabu . Katika  ndoto  hiyo, nilimuona   K  akiwa  anatembea  kuja  mahali  kilipo  kibanda  changu  cha  genge.

 Alipofika  kwenye  kibanda changu alisimama  na  kuniulizia  kama  nina  hiriki. Kabla  sijamjibu, ndoto  ikakatika  ghafla… Nilipo stuka  na  kutazama  saa  ilikuwa  majira  ya  saa  sita  na  ushee  usiku.

Hapo  hapo  nikampigia  simu  Mungu  wa  Kabili  na  kumueleza  nilicho  kiona  ndotoni… Akaniambia  vizuri  sana, kisha  akaniuliza, je  hilo  eneo   ambalo  umemuona  huyo  mwanaume  akiwa  anatembea, unalifahamu. Nikamjibu  ndio  nalifahamu.  Akaniambia, kesho  saa  kumi  na  mbili  alfajiri, nenda   kamwagie  ile  dawa  niliyo  kwambia  uitunze  chini ya  kitanda.  Baada  ya  hapo  akaninisisitizia, “ Ukiisha  fanya  nae  mapenzi,  uje  unione haraka  iwezekanavyo,  tufanye  dawa  za  kumfunga..

Nikafanya   kama  alivyo nielekeza, alfajiri  ya  saa kumi  na  mbili, nikadamkia  katika  eneo  hilo, kisha  nikamwaga  ile  dawa  halafu  baada  ya  hapo  nikarudi zangu  nyumbani  kujiandaa  na  kufungua  genge  langu.

NAINGIA   KATIKA   UHUSIANO  WA  KIMAPENZI  NA  “K” MUME  WA  MTU.
Saa  mbili  asubuhi  nilifungua  genge  langu,  nakumbuka  siku  hiyo  ilikuwa  Jumamosi. Mida  ya  kama  saa  nne  hivi,  K  alikuja  hadi  gengeni  kwangu  na  kununua  vitu  mbalimbali  vya  genge, kama  vile  karoti, nazi,pilipili manga  nakadhalika  na  kurudi kwake.

 Baada  ya  kama  masaa  mawili  hivi, K  alirejea  tena  pale  gengeni  kwangu, na  kuchukua  vitu  vingine  zaidi, halafu  akaomba  namba  yangu  ya  simu,  aka save  namba  yangu  na  mimi  nikachukua  yake, kisha  akaondoka zake.

 Baada  ya  kama  nusu  saa  hivi, K  akaanza  kunitumia  meseji  za  kunisifu. Alianza  kwa kuniambia  mimi ni  mwanamke  mchapakazi,  najituma  sana , nna  hasira  na  maisha , nnafaa  kuwa  mama kwa  sababu  hata  mume  akifa  anakuwa  na  uhakika  watoto  wake  anawaacha  na  mwanaume  imara.. Mwisho  wa  siku  akanitongoza, na  mimi  sikulazia  damu. Kesho  yake, mimi  na  K tukakutana  kimwili  kwenye  hoteli  moja  iliyopo  maeneo ya  Mbezi Beach.

Siku  hiyo  K  akaniambia  niachane  na  kazi  ninayo  ifanya, atanitafutia  biashara  nzuri  ya  kufanya, pia  nihame  pale  nilipo  kuwa  nakaa, atanipangia  nyumba  inayo  endana  na  hadhi  yake.

NAPEWA   DAWA   ZA   KUMPUMBAZA   MUME  WA  MTU.
Mungu   wa  Kabili  aliniambia, nikisha  fanya  mapenzi  na  huyo  mwanaume, niende  kwake ili  anipe  dawa  za  kumpumbaza. Nilipofika   akaniambia, vitu  vinavyo  hitajika  katika  kutengeneza  hiyo dawa  ya  kumpumbaza  huyo mwanaume, ni  NYWELE  ZA  MWANAUME  MWENDAWAZIMU,  NYWELE  ZA  MWANAUME  ASIYE  SIKIA ( KIZIWI ) , NYWELE  ZA  MWANAUME  KIPOFU  AU  FIMBO  ILIYO TUMIWA  NA  MWANAUME  KIPOFU,  KAMBA  ILIYO  TUMIKA  KUMFUNGA  KONDOO ,  pamoja  na  UCHAFU  WA  JALALANI.

Vitu vyote  hivyo  vilitafutwa  vikapatikana, vikachanganywa  na  dawa  nyingine  za  kichawi,kisha  vikatumika  kutengeneza   uchawi. Nikaambiwa  nitamuwekea  kwenye  maji  ya  kuoga na  nyingine  nitamuwekea  kwenye  chakula .
Halafu  nikapewa  na kibuyu, ndani  ya  kibuyu  kile kulikuwa  na  kipande  cha  nyama. Mganga  akaniambia  hiyo  ni  nyama ya  ndege  wa  usiku  mwana  wa  jinni, ambayo  baadae  nilikuja  kujua  kuwa  ni  Bundi  wa  Kichawi, ambae  ni  tofauti  na  bundi  wa  kawaida.

  Mganga   akaniambia   utapika  nyama, katika  nyama  utakayo  pika ambayo  utamuwekea   ndumba, mwanaume  wako, utachanganya  na  nyama  hiyo, pamoja  na  kucha  zako, na  nywele  zako  za  siri.

Nilipo  rudi  nyumbani, nikafanya  kama  nilivyo elekezwa.

Baada  ya  kufanya  uchawi  huu, K   alikuwa  kama  mwendawazimu  kwangu, hakusikia  wala  kuambiwa  na  mtu  yoyote  Yule. Akawa  anafanya  kila  ninacho  taka  akifanye  mimi.  Akaanza  kuwa  ananipa  mali  zake, magari, viwanja, nyumba, biashara  pamoja  na miradi  yake..

NATEGA  UCHAWI  WA  KUTOA  MIMBA  YA  MKE  MWENZANGU.
Mapenzi  yangu  na  K   yalipamba  moto,  nyumba  aliyo  nipangishia  haikuwa  mbali  sana  na  mahali  alipokuwa  anaishi  yeye  na  mkewe, wao  walikuwa wanaishi  Tabata  Mawenzi, mimi  akanipangia  nyumba  nzima  Tabata  Kimanga.

K alihama   kwa  mke  wake, akawa  anaishi  nyumbani  kwangu.  Taarifa  za  K  kuishi  na  “mchepuko”  zilimfikia   mke wake, lakini  hakuwa  na  kitu  cha  kufanya  kwa  sababu  K  alikuwa  ndio  anamuweka  mjini  yeye  na  familia  yake  na  mwanamke  alikuwa  mama  wa  nyumbani  tu.

Mara  nyingi  K  alikuwa  ananishauri  amfukuze  mke  wake, ili  nikaishi  nae  kwenye  nyumba yake, ili  kuninonyesha  kuwa  ananipenda  sana  na  mimi  ndio  kila  kitu  kwake.

 Ila  kuna  kitu  kimoja, alinifundisha   Mungu  wa  Kabili, kwamba  unapokuwa  mchawi, unatakiwa  uwe  mnafiki. Usiache  kabisa  watu  wajue  kwamba  una jambo  Fulani  kwa  sababu  ya  uchawi .  Hivyo  nikawa  najifanya  kama  namuonea  huruma  mke  wa  K  lakini  moyoni  nilikuwa  nataka  afukuzwe  mimi  nikakae, pale.

Kuna kitu  kimoja  kilikuwa  kinaniumiza  moyo. Mke  wa  K  alikuwa  na  ujauzito  wa  kama  miezi  mitano hivi.  Sikutaka  mwanamke  huyo  azae  na  K   kwa  sababu  nilijua, angezaa  na K  mtoto  angekuwa  kiunganishi  kwao,  Mimi  nilitaka  K  akisha  achana  na  mke  wake, basi iwe  ndio  moja  kwa  moja  na  kusiwe  na  chochote  cha  kuwaunganisha. Hivyo  nikaanza  kupanga  njama  za  kuharibu  ujauzito  wa  mke  wa  K kwa  kutumia  uchawi.

Suala  hili  nikalifikisha  kwa  Mungu  Wa  Kabili. Mungu  wa  Kabili  akaniambia  nitakupa  dawa utaenda  kutega  kwenye  mlango  wake.   Mti huo  ni  wa  ajabu  sana. Jina  lake  linafanana  na  jina  la  moja  kati  ya  wilaya  zilizopo  kusini  mwa  Tanzania  bara.

Baada  ya  kupewa  dawa  hiyo, nikafanya  ujanja  nikaenda  kuitega  kwenye  mlango anaoutumia  kupita. Alipo ruka  mimba  ikatoka. Kutoka  kwa  mimba  ya  mke  wa   K  kulinipa  sababu  ya  kurudi kwa  mganga  kwa  ajili  ya  kuwatenganisha  kabisa  K  na  mke  wake. Nilijua, majirani  wangesema  K  kamuacha  mke  wake  kwa sababu  mke  ana matatizo  ya  uzazi.

NAMTENGANISHA  K  NA  MKE  WAKE.
Nikarudi kwa  mganga  ili  tufanye  uchawi  wa  kumtenganisha  K  na  mke  wake.   Mganga alichukua  nyoya  la  ndege ambaye  simfahamu  jina  lake, pamoja  na  dawa  ambazo  sikuzijua  pia, akachukua  majina  ya  K na  mke  wake, akaenda  kuchoma   jalalani.

Alipomaliza  hapo, tukaenda  kaburini, kwa  ajili  ya  kuuzika  rasmi  uhusiano wa  K  na  mke  wake. Baada  ya  kuzika  uhusiano wa  K  na  mkewe, yalifanyika  matanga  kwa  ajili  ya  kuomboleza  “kifo’ cha  ndoa  ya K. Mganga  alisema, kitu  kilicho  kufa, kinastahili  kupewa  maziko  ya  heshima. Usipofanya  hivyo, roho  ya  kitu  hicho  itakusumbueni.

 Niliporudi  mjini  nikakuta    mke  wa  K  kaondoka  kwake, kahamia  kwa  dada  yake. Mimi  nikahamia  moja  kwa  moja  kwa  K nyumba  niliyokuwa  nimepangiwa  Kimanga  nikamuweka mdogo  wangu  wa  kiume.

NAANZA   KUFUATILIWA   NA  NDUGU  WA  MKE  WA  ‘K’.
Ndugu  wa  mke  wa  K  hawakufurahishwa  na  kuachana  kwa  K na mkewe, hivyo  wakafanya  kila  juhudi  kuwapatanisha, lakini  msimamo  wa  K  ulikuwa  ni  ule  ule, kwamba  hataki  tena kuwa  na  mke  wake  na  ameamua  kuishi  na  mwanamke  mwingine  ambae ni  mimi.   K  alikataa  hata  kushiriki  kwenye  vikao  vya  usuluhishi. Ndugu  wote  wa  upande  wake  na  upande  wa  mke  wake  wakawa  wamemsusia  K.

Watu  wawili    hawakutaka  kukubaliana  na  matokeo. Nao  ni  baba  wa  mke  wa  K, pamoja  na  kaka  mkubwa  wa  mke  wa  K. Watu hawa waligundua  kilichotokea  kati  ya  K  na mke  wake  sio  hali  ya  kawaida bali  ni nguvu  za  ushirikina. Hivyo  wakaamua  kutafuta  suluhisho  kwa  waganga.   Walipo  zunguka    kwa  waganga, hawakufanikiwa, hadi  wakakata  tamaa kunidhuru  kwa njia  ya  uchawi.

Mwisho wa  siku  wakaamua, kunikodia  majambazi, waje  wanipige  risasi. Walijua  mimi  ndio  kikwazo  kwa  mtoto  wao  kurudiana  na  mume wake, hivyo  njia pekee  ikawa  ni  kifo  tu.

Nilisurika  kuuwawa na  majambazi  zaidi  ya  mara  saba. Wakati  huo  Mungu  wa  Kabili  alikuwa Lubumbashi  nchini  Kongo  kwa  shughuli  zake.  Alipo  rejea  nikamfuata  kwa  ajili  ya  kuomba  ulinzi  wake.

Kuna  mnyama  mmoja  wa  mwituni, ana  ndimi  mbili, yani  ulimi  wake  una  ndimi  mbili, Mungu  wa  Kabili  akatafuta  ulimi  wa  mnyama  huyo, mavi  ya  chatu  pamoja  na  dawa  zingine  anazo  zijua, lengo  lake  likiwa  ni  kuwatenganisha  na  kuwafarakanisha  baba  na  kaka  wa  mke  wa  K  ili wasipate  nafasi  ya  kukaa  pamoja  na kunifuatilia.

Halafu  baada  ya  hapo, akaagiza  nipeleke  mchanga  wa  kwenye  kaburi  la  mtu  aliyepita  duniani bila  kuonekana, ili  anitengenezee  dawa  ya  kuwafunga  adui  zangu  wasinione. Pamoja  na  hivyo, akanipa hirizi  iliyo  tengenezwa  kwa   Mti  Mkuu wa  Wachawi.

Katika  ulimwengu  wa  wachawi, mtoto  aliye  kufa  akiwa  tumboni  kwa  mama  ake. Huitwa  mtu  aliyepita  duniani  bila  kuonekana.

Nilivyo  mpelekea  udongo wa  kwenye  kaburi la  mtu  aliye  pita  duniani  bila  kuonekana, mganga  akauchukua  akafanya  ulozi wake, halafu tukaenda  wote  hadi  mtoni, akaenda  akatega  ndumba zake, pale, kesho  yake  tukakuta  chura  amenasa  pale.

Wachawi  wana  amini, roho  za  watoto  wanao  kufa  kabla  hawajazaliwa, huwa  zinaenda  kuishi   mtoni  kama  Chura. Lakini  sio  chura  wote  wapo  hivyo, ni  baadhi. Waganga  wana  utaalamu  wao  wa  kujua  chura yupi  anahusika  hapo.

Basi  kaka  na  baba  wa  mke  wa  K, walikosana  kwa  ugomvi  mkubwa, kiasi  mtoto  akawa anamtukana  baba  ake  mzazi  tusi  la  mama. Na  kuhusu  vitisho  vya  majambazi havikutokea  tena

NATUMIA  UCHAWI  KUOKOA  UHUSIANO  WA  KAKA  ANGU.
Kaka  angu  ambaye  nimempita  miaka  mitano, alikuwa anaishi  kwenye  nyumba  ambayo K  alinipangia. Nyumba  hii  ilikuwa  maeneo  ya  Tabata   Kimanga.  Kaka  angu    alikuwa  katika  uhusiano  wa  kimapenzi  na  mwanamke  ambaye  alikuwa  Baa  Medi  kwenye  bar  inaitwa  Mawenzi  Garden.

Alimuachisha  kazi  ya  ubaa  medi  baada  ya  mimi   kumuwezesha  kiuchumi  kutokana  na  hela  na  mali  nilizo hongwa  na  K  pamoja  na  kumpa  mradi  mmoja  wa  K  ausimamie.  Mdogo  wangu alimpenda  sana  mwanamke  huyo .

Ila  tatizo  moja  la  mwanamke  huyo, alikuwa  na  tabia  ya  umalaya. Umalaya  ulikuwa  kwenye  damu  yake .

Basi  siku  moja  mdogo  wangu  alikuja  kwangu  kunishitakia  kuhusu  tabia  ya  wifi  yangu.  Mdogo  wangu  alikuwa  anampenda  sana  mwanamke  huyo, na  alikuwa  hawezi  kumuacha  kwa  sababu  yoyote  ile,  ila  alikuwa  anamuumiza  sana  kwa  sababu  ya  tabia  yake  ya  umalaya.

“ Ninampa  kila  kitu  huyu mwanamke, ninampa  hela,  nimemfungulia  biashara, nimempa gari, nawasomesha  wazazi  wake  na  kusaidia  familia  yake,. Lakini  haridhiki  tu, mwisho  wa  siku  anatumia  hela  ninazo  mpa  kuhonga  wanaume  wengine.. ( HELA , GARI  NA  VITU  VYOT  AMBAVYO MDOGO  WANGU  ALIKUWA  AKIMPA  WIFI  YANGU,  VILIKUWA   MALI  YA  K  ALIZO CHUMA  KWA  JASHO LAKE  NA  MKE  WAKE)

Nilimuonea  huruma  sana  mdogo  wangu, na  nikaamini  sio  akili  yake  ila  atakuwa  amerogwa  na  mwanamke  Yule. ( UNAJUA  UKIWA  MSHIRIKINA, KILA  KITU  UNAKUWA  UNAAMINI  KIMESABABISHWA  NA  USHIRIKINA  )

Nikamwambia  mdogo  wangu  usijali, kesho  nitakwenda  Bagamoyo  kwa  mtaalamu wangu, nitamuelezea  tatizo  lako, halafu  nitamsikia  atakacho  niambia,  nitakujulisha, ila  usijali  kama  mwanamke  huyo  amekufanyia  mambo  ya  Kiswahili, itajulikana tu  na  utakuwa  huru.

Nilipo fika  kwa  Mungu  wa  Kabili, nikamueleza  kila  kitu, akaniomba  majina  ya  mdogo  wangu  pamoja  na  jina  la  huyo  wifi  yangu, akatazama  kwenye  radar  zake, halafu  akacheka  sana.

Mungu  wa  Kabili  akaniambia, hakuna  haja  ya  kumfunga  mwanamke  huyu. Huyu  mwanamke   ana  sumbuliwa  na  damu  ya  umalaya. Umalaya  upo  kwenye  damu  yake.   Hata  tukimfunga  kwa  mdogo  wako, tutakuwa  tunajisumbua  tu, atampenda  sana  mdogo  wako, lakini  atatoka nje  tu  kwa wanaume  wengine. Hapa  cha  msingi,  afanyiwe  dawa  ya  kumfanya  aache  umalaya.

Mungu  wa  Kabili  akachukua  dawa  moja  inaitwa  GEGEZI. Hii  Gegezi  ina  ukubwa  kama  tunda  linaitwa  DADANSI na  ina  mibamiba.

 Halafu  akachukua  dawa  nyingine  ambayo  ni  chakula  cha   ndege  mmoja wa  porini. Ndege  huyo  simkumbuki  jina  lake, ila  ni  mweusi, ana mdomo  mrefu, ndege  huyu  akilia, vinyonga  wote  waliopo  katika  eneo  hilo  wanakimbia, huwa  anakula  vinyonga  pia.,

Sasa  ndege  huyu  huwa  anakula  majani  ya  mti  Fulani  wa  porini  ambao  nimeusahau  jina  lake, hayo  majani  ndio  ambayo  Mungu  wa  Kabili  aliya  chukua.

Kitu  kingine  akachukua   majani  Fulani hivi, hayo  majani  ndio  majani  pekee  yanayo  liwa  na  mnyama  wa  porini  ambae  chakula chake  kikuu  ni  nyama.

 Pamoja  na  dawa  hizo  akachanganya  na  dawa  zake  nyingine  ambazo sikuweza  kujua  ni  dawa gani, halafu  akaagizwa  itafutwe  minyoo ipatayo  saba. Vito  vyote   hivyo  vikaunguzwa  pamoja  kwenye  chungu, hadi  vikawa  unga  unga  halafu  vikachanganywa  na  mafuta   ambayo sikujua  ni  mafuta  ya  kitu  gani.

Mungu  wa  Kabili  akanipa  dawa  hiyo  akaniambia  mpelekee  kaka  ako. Mwambie  akiwa  anafanya  mapenzi  na  huyo mwanamke  wake, afanye  ujanja  wake, achovye  kidole  chake  kwenye  hiyo  dawa  halafu  akichomeke  kwenye  uke  wa  mwanamke   huyo.

Tangu  siku  hiyo, mwanamke  huyo hatokuwa  Malaya  tena .  Nikafanya  kama  alivyo  nielekeza  na  tangu  mdogo  wangu  afanye  hivyo, sikuwahi kumsikia  tena  akinipa  kesi  za wifi  yangu, zaidi  ya  kumsifia   mpenzi wake  ametulia. Mwisho  wa  siku  walifunga  ndoa  na  kuzaa  watoto.

 NAMTEKA   KICHAWI   KIJANA   WA   KIARABU.
Nilimroga  K  kwa  sababu  ya  pesa  zake. Nikiwa  kama  mwanamke  kamili, nilihitaji  kuwa na  mwanaume  ninaye  mpenda  kutoka  moyoni mwangu. Nataka  nitoe  funzo  moja  kwa  wanaume, mnajua   kila  mwanamke  alie  olewa   ambae  hajaokoka  huwa  ana  wanaume  wawili.  Mwanaume  wa  kwanza  ni  mwanaume  ambae  yupo  nae  katika  ndoa, na  mwanaume wa  pili  ni  mwanaume ambae  alitamani  awe  nae  katika  ndoa.  Hivyo  ndivyo  ilivyo  kuwa  kwangu.

Sasa  basi, kuna  kijana  mmoja  wa  kiarabu  ambae  nilikuwa  namzidi  umri  kwa  miaka  minane. Kijana  huyu  aliishi  mtaa  wa  pili  kutoka   nyumba  niliyo kuwa  nikiishi  na  K.

Nilitokea  kumpenda  sana  kijana  huyo   lakini  sikuwa  na  namna  ya  kumuanza, mnajua  mwanamke  kumtongoza  mwanaume  sio  kazi  rahisi.   Nikaona  isiwe  tabu  nikaamua  kwenda  kwa  Mungu  wa  Kabili, ili  anipe  ndumba  za  kumnasa  kijana  huyo  ambae kwa jina  aliitwa  Feisal.

Nilipo fika  kwa  Mungu  wa  Kabili  akaniambia “ Inaonekana  wewe  ni mtundu  mtundu  sana,. Halafu naona   una  mambo  mengi. Sasa  nitakutengenezea  uchawi, ambao  utakuwa  unautumia  mwenyewe  kumnasa  mwanaume  yoyote  unae  mtaka. “. Mungu  wa  Kabili  akaniambia, njia  hiyo  itakuwa  bora  kuliko  mimi  kuwa  naenda  kumuona  kila  mara  kwa  jambo  lile  lile.

Mungu  wa  Kabili  akaniambia, nitafute  kopo  linalo  tumika  chooni, nitafute  nguo  za  marehemu. Hapa  simaanishi  nguo  za  maiti, la  hasha  nina  maanisha  nguo  za  marehemu.

Mfano  wake  ni  kwenu  kuna  mtu  amefariki, nguo  zake  zimegawiwa  kwa  ndugu, jamaa  na  marafiki, sasa  nguo  hizo  ndio  anazo  zitaka.

Mungu  wa  Kabili, akaniambia  niwe  na  uhakika  kwamba  nguo  nilizo pewa  ni  nguo  za  marehemu  kweli, hilo  la  kwanza,  lakini  pili  niwe  na  uhakika   kwamba  marehemu  huyo  alikufa  kifo  cha  Mungu  na  sio  kachukuliwa  msukule.

Nikamuuliza  nitajuaje  kuhusu   mambo  hayo, akaniambia  ni  rahisi  sana. Wewe  ukizipata  nguo  za  marehemu, au  mtu  atakae kuuzia  nguo  za  marehemu, basi  akuonyeshe  mahali  lilipo  kaburi  la  marehemu, halafu  utakuja  kwangu  nikuelekeze  cha  kufanya.

 ( KATIKA  ULIMWENGU  WA  WACHAWI, NGUO  ZA  MAREHEMU  NI  BIASHARA  KUBWA  SANA, KUNA  WATU  WANAISHI  KWA  KUFANYA  BIASHARA  YA  KUUZA  NGUO  ZA  MAREHEMU  MBALIMBALI..MIMI  MWENYEWE  NILIUZIWA  NGUO ZA  MAREHEMU  KWA  BEI  MBAYA ).

Baada  ya  kufanikiwa  kupata  nguo  za  marehemu,  pamoja  na  kuonyeshwa  mahali  lilipo  kaburi  la  huyo  marehemu, nilirejea  kwa  Mungu  wa  Kabili.

Mungu  wa  Kabili  alizichukua  zile  nguo, akakata  kipande  kidogo  kwenye  shati  moja, akapaka  mafuta  ambayo  sikujua  ni  mafuta  ya  nini, akazifunga  kwenye  kitambaa  chekundu, akaweza  kwenye kibuyu, ndani  ya  kibuyu  hicho  akaweka   yai la  kuku mweusi, sindano saba  pamoja  na  mafuta  mengine  ambayo  sikujua  ni  mafuta  ya  nini  ila  wao  wachawi  na  waganga  wanayaita  mafuta  ya  usiku, kisha  akakifunga  kile  kibuyu, halafu  akanikabidhi, akaniambia, ikifika  usiku  wa  saa  moja  , nenda  hadi  kwenye  hilo  kaburi, kisha  ukiweke  kibuyu  hicho  juu  ya  hilo  kaburi  kwa  kukilaza., halafu  asubuhi  pita  katika  kaburi  hilo  uangalie  kwa  makini  kibuyu  hicho, ukikikuta  bado  kimelala  kama  ulivyo  kiacha  basi ujue  huyo  marehemu  kweli  amekufa  kifo  cha  Mungu, lakini  ukikuta  kimesimama, basi  marehemu  huyo  bado  yupo  hapa  hapa duniani, amechukuliwa  msukule.

Nikafanya  kama  alivyo  niagiza, na  kweli  kesho  yake  nikakuta  kibuyu  kimelala  kama  nilivyo  kiweka. Mungu  wa  Kabili  akaniambia  nguo  hizo zinafaa  kwa  ajili  ya  kutengeneza  dawa  hiyo.

Basi  akachukua  hizo  nguo, akaziunguza  kwenye  chungu  cheusi  pamoja  na  dawa  nyingine   kama  aina  kumi  na  mbili, halafu  akazihifadhi  kwenye  kibuyu  na  kunikabidhi,  pamoja  dawa zingine  kwenye  vifuko  vitatu.

Akaniambia, ukimtaka  mwanaume  yoyote  Yule, utamuita  kwa  kutumia  dawa  hii… Mwanaume  utakae  muita  sauti  yako  ataisikia  na  kuitii  mara  moja  kama  ambavyo  marehemu  huyo  alivyoitwa  na  Mungu  na  kuitii  sauti  yake.

Mungu  wa  Kabili  akaniambia  huo  ni  uchawi  mkubwa  sana  katika  mapenzi,  hakuna  mwanaume  nitakae  muita  na  akakataa  kuitika.  Uchawi  huu  hautumiki katika  mapenzi  tu, hata  kama mambo mengine, ilimradi  unacho  taka  wewe  ni  kumuita  mtu.

Kitu  kingine  akaniambia, ukimuita  mwanaume kwa  kutumia  uchawi  huu   zaidi  ya  mara  saba, halafu   akakataa  kuitika, basi  jua  kwamba  mwanaume  huyo kinga  yake  ni  kubwa  sana.

Sasa  basi ukisha  ligundua  hilo, unatakiwa  kutuma  nyoka  wa  kichawi  kuua  kinga  ya  mwanaume huyo. Ukisha ua  hiyo  kinga,  muite  tena  mwanaume  huyo  na  atakuja  haraka  sana.

Nyoka   huyu  sio  nyoka  wa  kawaida  kama  nyoka  wengine. Ni nyoka  wa  kichawi. Ni  jinni. Mungu  wa  Kabili  akanikalisha  kwenye  kigoda na  kuniambia, “ Nitamtengeneza  nyoka  huyu, halafu  nitakukabidhi, umtunze  vizuri  kwa  kufuata  masharti  yake…”

Katika  kumtengeneza  nyoka wa  kichawi, Mungu  wa  Kabili  akachukua  kitovu cha  mtoto. ( KUWENI MAKINI SANA  NA  MAHALI  MNAPOVITUPA   VITOVU  VYA  WATOTO  WENU.. KATIKA ULIMWENGU  WA  WACHAWI  VITUVO  VYA  WATOTO NI  BIASHARA  KUBWA  SANA… KITOVU  CHA  MTOTO  KINAPOENDA KUTUPWA, AMA  KUFUKIWA,  KATIKA  WATU WANAO PEWA  JUKUMU  LA KUVITUPA, HUWA  KUNA MMOJA  WAPO  ANAWEZA  KUWA  SIO MUAMINIFU, HUENDA  KUFUKUA  MAHALI  KILIPOFUKIWA  NA  KWENDA  KUKIUZA  KWA  WACHAWI  NA  WAGANGA )

Alipochukua  hicho  kitovu, akakifunga  kwenye  mti  wa  mnyonyo, halafu  akanyunyizia  dawa    kutoka  kwenye   vichupa  kama  saba. Baada  ya  hapo  akachukua  uzi mwekundu, akafunga  vifundo  saba  kwenye  kamba  hiyo,  halafu  akatupa  kwenda  chini, ilipotua  tu, ikageuka  kuwa  nyoka. Akamshika   huyo  nyoka, akamuhifadhi kwenye  kibuyu  cheusi, chenye  shanga  juu, akafunga  na kitambaa  cheusi  na  kunikabidhi.. Akanielekeza  jinsi  ya  kumtuma  nyoka  huyo  kufanya  kazi  mbalimbali  pamoja  na  masharti  yake.

 Kuhusu  lile  kopo  la  chooni, Mungu  wa  Kabili  akaniambia  amelitumia  kutengeneza  dawa  ya  kujua  siri  za  watu.   Dawa  hiyo  itanisaidia  kujua  kama  mwanaume  niliye  nae ana  hela  au  hana  hela, ana  mke au  hana  mke. Ana  watoto  au  hana  watoto.

Kingine  akanikabidhi  ua  ambalo  natakiwa  kulipanda  nyumbani.  Kupitia  ua  hilo  nitakuwa ninajua  kama  mwanaume  ambae  nipo nae   amepata  hela  au  la.

Kitu cha  mwisho, akaniambia, kwa sababu  nnaonekana  nnapenda sana  wanaume, inabidi  anipe  dawa  ya  kuwatengeneza wanaume  nitakao  kuwa  nao  na  kuwafanya  kutokuwa  na  uwezo  wa  kufanya  mapenzi na  wanawake  wengine  isipokuwa  mimi  tu.   Hii  itasaidia  kuniepusha  na  magonjwa  kama  vile  ukimwi  nakadhalika.

Mungu  wa  Kabili  akanipa  mti mmoja  mrefu, akaniambia  katika  mti  huo, utatumia  zaafarani  nyekundu  au  ya  njano, kuandika  majina  ya  wanaume  wote  ambao  upo  nao kimapenzi  pamoja  na  jina  lako, ukisfanya  hivyo, nenda  kautegeshee  barabarani, ukishagongwa  na  gari  tu, basi  wanaume  hao  watakuwa  wakikutana  na  wanawake  wengine, uume  wao  unakuwa  haufanyi  kazi.

Nilivyo  rudi  nyumbani  nikafanya  kama  nilivyo  elekezwa  na  kweli   Yule  kijana  alikuja  mara  moja  tangu  nilipo  muita.  Nilifurahi  sana  kumpata  Feisal. Pamoja  na  kwamba  nilikuwa nimemuita  kichawi  ila  nilikuwa  namuheshimu  sana kwa  sababu  nilikuwa  nampenda  toka  moyoni  mwangu.
                                
Baada  ya  kama  wiki  mbili  tangu  nianzee  uhusiano  wangu  na  Feisal, nikagundua  Feisal  ana  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  Uwezo  wake  kitandani  ulikuwa  mdogo  sana.

Kama  kawaida  yangu  nikaenda  kumuona  Mungu  wa  Kabili. Mungu  wa  Kabili  akanipa  dawa   moja  inaitwa  KISHINDO. Akaniambia  utakuwa  unachemsha  unampa  anakunywa  glasi moja asubuhi  na  nyingine  anakunywa jioni, kwa  siku  kumi  mfululizo.  Nikafanya  kama  alivyo  nielekeza. Baada  ya  kumpa  Feisal   dawa  hiyo, nilijilaumu  kwanini  nilifanya  hivyo. Uwezo  wake kitandani  ulikuwa  wa  ajabu, alikuwa anashiriki tendo  kwa  muda  mrefu  sana  na  alikuwa  akirudia  mara  nyingi  bila  kuchoka…

NAMFANYIA   VITUKO    K
Katika  muda  wote  huo, nilikuwa  bado  ninaishi  na  K  kwenye  nyumba  yake  ya  Tabata  Mawenzi. K  alikuwa  kama  Ndondocha  kwangu. Kwanza  nilikuwa  simpi  unyumba  na  nilikuwa nafanya  kila  kitu  ninacho  taka  kukifanya  tena  mbele yake.

Feisal  alikuwa  anakuja  nalala  nae  chumbani, K  analala  pepe  yake  kwenye  chumba  kingine.  Alikuwa  anafanya  kazi  zote  kama  vile  kufua, kufanya  usafi na  kila  aina  ya  kazi  ambayo  houseboy  anatakiwa  kuifanya. 

Na  katika  kipindi hiki  K alikuwa  ameshafukuzwa  kazi  kutokana  na  uzembe  kazini.  Mimi  mwenyewe  nilimpiga  marufuku  kwenda  kazini  kwa  mwezi  mmoja, nilimwambia  achague  kitu  kimoja  kati  ya  kwenda  kazini  au  kufanya  kazi  zangu.

Sasa  basi  nikawa  namfanyia  K vituko, lengo  langu  nikitaka  aondoke  mwenyewe  aniachie  nyumba na  mali zake. Hakuwa  na  faida  yoyote  tena  kwangu. Kazi ameshafukuzwa , mali  zake  zote  pamoja  na  biashara  zake  ninazimiliki  mimi.

Basi  kila  nilipokuwa  nikifanya  mapenzi na   Feisal  nikawa  napiga  kelele ili  kumuudhi  K. Na  hivi  Feisal alikuwa  anatumia  muda  mrefu  basi  na  kelele zangu  zikawa  za  muda  mrefu. Lakini  wapi, K  wala  hata  hakuonyesha  dalili  ya  kwamba  anaweza  kuondoka , undondocha  ulikuwa  umetamalaki kwenye  kichwa chake.

Kwa  kutumia  ndumba  hizo nilizo  pewa  na  Mungu  Wa  Kabili, niliwateka  kichawi  wanaume  wengi  na  kuvunja  ndoa  nyingi  sana.

K  ANAAMUA   KURUDI   KIJIJINI
Nilipoona  K  hana  dalili  ya  kuondoka  pamoja  na kumfanyia  vituko  lukuki, nikaona  niende  kwa  Mungu  wa  Kabili  ili  kama  kuna  uwezekano  wa  kumfukuza  K kichawi.

Nilipofika  kwa  Mungu  wa  Kabili, akafanya  dawa  zake, halafu  ikatengenezwa  ngalawa ndogo, nikaambiwa  nipeleke   nguo  yoyote  ya  K . Nguo ya  K  ikafanyiwa  uchawi halafu  ikafungwa  kwenye  hiyo  ngalawa, tukaenda  baharini  kutegea  wakati  bahari  imesafiri  tukaenda  kuiweka  ngalawa , maji  yalipokuja  yakaondoka  na  hiyo  ngalawa, kesho  yake  tu, K  mwenyewe  akasema  anataka  kwenda  kusalimia  kijijini  kwao  amepakumbuka. Nilifurahi  sana  niliposikia  hivyo, nikamfungia   nguo  zake, nikampa na  nauli pamoja  na  hela ya  kula  njiani..

Kalivyo  rudi  kwao, baadhi  ya  ndugu  zake  hawakuridhishwa  na  hali  ya  K  pamoja  na  maelezo  yake. Mtu  aliyekuwa  tegemeo  la  ukoo  mzima, ghafla  anarudi   kijijini  akiwa  hana  kitu  na  maelezo  yake  yanatatanisha.  Wakaamua  kufunga  safari  hadi  mjini  ili  kufuatilia  mali za  ndugu  yao. Nilipo pata  taarifa  zao, nikaenda  kuwashitaki  kwa Mungu  wa  kabili,  wote  walipeperuka  na sikusikia  chochote  kuhusu  watu  hao.

NAINGILIA   NDOA    YA   WALOKOLE.
Nilitokea kumtamani  mwanaume  mmoja  mlokole  alieishi   mtaa  wa  pili  kutokea  nilipokuwa  naishi. Huyu  nilimpenda  kama  nilivyo  mpenda  Feisal. Alikuwa  mkaka  mzuri  anae jipenda sana.  Kwa  jina  aliitwa   Erasto.   Kikwazo  kikubwa  kwa  Erasto  ilikuwa, kwanza  alikuwa  ameokoka na  pili  alikuwa  na  mke ambaye  alikuwa  ameokoka  pia. Mke  wa  Erasto alikuwa  na  ujauzito mkubwa  tu  wa  kama miezi  mitano  au  sita .

Nasema  kuokoka  ilikuwa  kikwazo  kwa  sababu  Mungu  wa  Kabili  Alisha  nishauri  niwe  makini  sana na   walokole  kwa  sababu  wana  nguvu  za  ajabu. Ila  akaniambia  kuna  walokole  wa  waina  mbili., mlokole  wa  ukweli  na  mlokole  feki. .. 

Hivyo  basi  kama  umemempenda  mwanaume  wa  kilokole,  unatakiwa  kwanza  umpime  kichawi  kujua  kama  ni  mlokole  wa  ukweli  ama  mlokole  feki.

Akaniambia    uchawi  unao  tumika  kupima  nguvu  ya  mlokole, sio  uchawi  wa  kitoto, hauwezi  kufanywa  na  mtu  yoyote, akaniambia   kama  itatokea   nimempenda  mwanaume  wa  kilokole, basi  niende kwake  halafu  yeye  atampima  kama  mlokole  huyo  ni  orijino  au  feki.. Kama  ni  orijino  una  achana  nae  kwanza  unatafuta  njia  nyingine  ya  kumpata,  lakini  kama  ni  feki,unamvuta  kama  watu  wengine.

Akaniambia, ukimpenda  mwanaume  wa  kilokole  orijino  ni  bora  utumie  njia  za  kawaida  kumteka, kuliko  njia  za  kichawi, kwa  sababu  kwa  njia  za  kawaida, ataishia  kukukemea  tu,. Lakini  kwa  njia  ya  uchawi, utapigwa  shot. Hakuniambia   ni  shoti  gani.

TUNATUMIA    UCHAWI   KUPIMA   ULOKOLE   WA   ERASTO.
Ili  kujua  kama  mlokole  ni  orijino  au  feki, wachawi  hutumia  nzi. Hivyo  basi  Mungu  wa  Kabili  alianza  kufanya  uchawi  ili  kupima  kama  Erasto   ana  nguvu  za  Mungu  au  hana  nguvu  za  Mungu.

Siku  hiyo  Mungu  wa  Kabili  akachukua   bakora  ya  kichawi  ambayo  imetengenezwa  kwa  mti  wa Mkomoro,  Mganga  akaniambia  mti  huo   wa mkomoro ni mti wenye  nguvu  nyingi sana  za  kichawi na  wachawi   huutumia  kwa  mambo  mengi  ikiwa  ni pamoja  na  kufufua  wafu.

Mungu  wa  Kabili  akaanza  kwa  kuwaita  inzi na  kisha  kuwatuma   waende kwa  Erasto  ili  kujua  kama ana  nguvu  za  Mungu  au  la.  Lilikuja  kundi  la  nzi  wengi, na  walipo  tua  tu  kwenye  fimbo  yake  wote  wakapasuka  pale  pale.

Mungu  wa  Kabili  akaniambia  kwa  kunisisitiza,   achana  kwanza  na  huyu  Erasto, kesho  ninasafiri  kwenda   Mkuranga , nitakuwa  huko  kwa  siku  saba tunaenda  kupika  uganga . Nitakapo  rudi  tutaangalia  njia  nyingine  ya  kumteka  Erasto.

Waganga   na  wachawi  huwa  wanakuwaga  na    MWAKA WA  UCHAWI  ama  MWAKA  WA  UGANGA, kama  ambavyo  kuna  MWAKA  WA  FEDHA,  MWAKA  WA  MASOMO  nakadhalika.

Unapofika  mwaka  wa   uganga, waganga    hukutana  mzimuni  na  kupika  uchawi, ambao  huuzwa  kwa  waganga  mbalimbali.  Jambo   hilo   hufanyika   kila  mwaka.

Mungu  wa  Kabili  alikuwa  anaelekea  Mkuranga  kwa  ajili ya  kusimamia  zoezi la  upikaji  wa  uchawi  unaoitwa  MANGUBE.   Kwa  hiyo  Mungu  wa  Kabili  akaniambia  nisubiri  kwanza  mpaka  wiki mbili zipite ndio  tuje  tukae  tupange  cha  kufanya  juu  ya  Erasto, kwa  sababu  baada  ya  kutoka  Mkuranga  alikuwa  anaelekea  Liwale  Lindi.

Sikuwa  na  jinsi  zaidi  ya  kukubaliana  na  maagizo  ya  Mungu  wa  Kabili.

NAMTUMIA   ERASTO  NYOKA  WA  KICHAWI.
Baada  ya  siku  tatu  uvumilivu  ukanishinda, nikaamua  liwalo  na  liwe, kama  kuna  baya  litanitokea, Mungu  wa  Kabili  atanisaidia.

Usiku  wa  saa  sita  siku  hiyo, nikamchomea  Erasto, dawa  ya  kumvuta  kwangu  kichawi. Kwa  kawaida   nikishachoma  dawa, usiku  huwa  naota  nafanya  mapenzi  na  mwanaume  nilie  mchomea  dawa  na   kesho  yake, kabla ya  saa  sita  mwanaume  huyo  huwa  ananitafuta, lakini  kwa  Erasto  ikawa  tofauti.  Sikuona   chochote. Nikachoma  kwa siku  saba  mfululizo  hakuna  chochote.

Nikakumbuka  Mungu  wa  Kabili  aliniambiaga  kwamba, kama  nikichoma  dawa  ya  kumuita  mtu  na  mtu  huyo  asije, basi  nijue  kuwa  mtu  huyo  ana  kinga  kubwa, kwa hiyo  natakiwa  nimtumie  nyoka  wa  kichawi, nyoka  huyo  ataenda  kuvunja  kinga  ya  mtu  huyo.

Siku  hiyo  usiku  wa  saa  sita, nikaenda  kuchukua  kile  kibuyu ambacho  kilitumika  kumuhifadhi  Yule  nyoka,  nikamtuma  nyoka  huyo  aende  kuigonga  na  kuivunja kinga  ya  Erasto. Nilipomaliza  kunena maneno  yangu  nikafungua kile  kibuyu  ili  nyoka  atoke, nyoka  alipotoka  akanigonga  kwenye  mguu na  kutokomea.

Nilipiga  kelele  za  ajabu,  house girl wangu  akaenda  kuwaamsha  majirani  na  kupiga  simu  ya  kaka  angu, nikapelekwa  hospitali, hospitali  nikapimwa  lakini  hakikuonekana  kitu, wala haikuonekana  kama  nina  sumu  yoyote  mwilini, lakini  nilikuwa  nasikia  maumivu  makali  sana yaliyokuwa  yanakuja  na  kuondoka, nikapewa dawa   za  kuzuia  maumivu  lakini  wapi. Ilipofika  asubuhi  maumivu  yakawa  yameisha  lakini  nikawa  nimepooza  upande  mmoja.

Nikamwambia  kaka  angu  apige simu  ya  Mungu  wa  Kabili, lakini  Mungu  wa  Kabili  alipopigiwa  na  kuelezewa  kilicho  tokea, akawa  mkali  sana, kwanza  akasema  alinionya  nisifanye chochote halafu  pili  akasema  hawezi  kunisaidia  kwa  namna  yoyote  ile.

Sikuwa  na  jinsi  zaidi  ya  kumueleza  kaka  angu  ukweli. Kilicho  fuatia  tukaanza  kuzunguka  kwa  waganga  wa  kienyeji  kwa  ajili  ya  tiba  yangu  lakini  wapi. Baada  ya  wiki  mbili  nilipelekwa  kwa Mungu  wa  Kabili  Bagamoyo  angalu  aione  hali  yangu  ilivyo  labda  anaweza  kunionea  huruma  lakini, akakataa  kata  kata…. Msimamo wake  ulikuwa  ni  ule  ule, nimefanya  jambo  ambalo  alinikataza  kulifanya  na  pia   hana  uwezo  wa  kunisaidia. Zaidi  aliniambia  hatima  yangu  ni  kifo.

Tulizunguka  kwa  waganga  wa  kila aina  na  kila  sehemu  lakini  wapi  hali  yangu  ikazidi  kuwa  mbaya.

Siku moja  ndugu  yangu  mmoja  wa  upande  wa  mama  angu, alikuja  kuniona  baada  ya  kusikia  nimepooza. Baada  ya  kumsimulia  kuhusu  kisa  changu  alisikitika  sana. Nikapelekwa   kwenye  kanisa  moja  la  kiroho  na  kuombewa. Siku  tatu  tangu  nianze  kuombewa  nilitapika  vitu  vingi  sana  vya  ajabu  ajabu, kama  vile  kucha, nywele,  damu   nakadhalika, na  taratibu  hali  yangu  ikaanza  kutengemaa  na hatimaye   nikapona  kabisa.

Namshukuru  Mungu  sasa  hivi  nimeokoka, nimempokea    Yesu  kama  Bwana  na Mwokozi  wa  maisha  yangu. Mali  za  K  nimezirudisha  na  sasa  ninaishi  maisha  yangu  halali kwenye chumba  cha  kupanga  maeneo  ya  Mbezi  Ya  Kimara.

Ninaumia  sana  moyoni  kuona, nimeseababisha   mateso  kwa wanawake  wenzangu, nimevunja  ndoa  za  watu.   Nimeamua  kumtumikia  Mungu  katika  maisha  yangu  yote. Ninawaomba  msamaha  wale  wote  nilio  waharibia maisha.

CHA  MWISHO  NA  KIKUBWA.. NAWATAHADHARISHA  WANAWAKE  WENZANGU  KUHUSU  WAGANGA  WA  KIENYEJI, HUSUSANI  HUYU  ANAEITWA  MUNGU  WA  KABILI. NI  MTU  HATARI  SANA  NA  MCHAWI  MKUBWA. NAOMBA   MSIENDE  KUFUATA  MSAADA  WAKE  JAMANI  KWA  SABABU  NI MCHAWI.. NAMBA  ZAKE  ZA  SIMU  NI  0744  000  473. MSIPIGE  NAMBA  HIYO  JAMANI, YATAWAKUTA  KAMA  YALIYO  NIKUTA  MIMI. NIMEONA  NIWEKE  NAMBA  ZAKE  HADHARANI   ILI  MZIJUE  NA  KUJIEPUSHA  NAZO, KWA  SABABU  NAONA  ANATANGAZWA NA  VYOMBO  MBALIMBALI  VYA  HABARI. NAOMBA  KILA  ATAKAE PATA  UJUMB  HUU, AMJULISHE  NA  MWENZAKE

YESU  AWAONGOZE  NA  AWALINDE.

Wasomi wamfagilia Sumaye uongozi Pwani Wasema ameonyesha siyo aina ya wastaafu wapenda sifa

0
0
Wasomi nchini wamesema iwapo Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye atakuwa mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, atasaidia kukijenga chama hicho cha upinzani nchini, kuanzia ngazi ya chini. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema jana kuwa Sumaye ambaye juzi alirejesha fomu ya kuwania nafasi hiyo, katika ofisi za kanda hiyo Dar es Salaam, akitumia uzoefu alionao kiuongozi, atakuwa msaada kwa chama hicho. 

Walisema uamuzi huo umeonyesha kuwa hakuhamia Chadema kwa masilahi binafsi. Profesa George Shumbusho wa Chuo Kikuu cha Mzumbe alisema: “Inaonekana (Sumaye) ana lengo la kusaidia upinzani ukue. Kwa mchango na uzoefu wake serikalini ataisaidia sana Chadema maana chama lazima kiwe na nguvu kuanzia ngazi ya chini.”

Sumaye ndiye Waziri Mkuu pekee katika historia ya Tanzania kushika wadhifa huo kwa miaka 10 baada ya kuwa msaidizi wa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa kati ya mwaka 1995 hadi 2005. 

Agosti mwaka jana, Sumaye aliyekuwa kete muhimu katika kampeni za aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa kutokana kuikosoa Serikali na kuwataka Watanzania kutoichagua CCM, alitangaza kuachana na chama hicho tawala na kujiunga na upinzani. 

Shumbusho alisema ameonyesha kuwa yeye siyo aina ya wastaafu wanaopenda sifa na hakwenda kusaka ulaji Chadema huku akibainisha nchi ikiwa na upinzani imara, chama kilichopo madarakani hugangamala. 

Makinda atumbua wakurugenzi 9 NHIF....Wadaiwa Kuhusika na Ufujaji wa Mabilioni ya Pesa

0
0
Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambayo Spika wa Bunge la 10, Anne Makinda ni Mwenyekiti wake, imewatumbua wakurugenzi 9 wa mfuko huo kutokana na ufujaji wa mabilioni ya fedha za umma uliobainika.
 
Uamuzi huo umeripotiwa kuwa umetokana na usimamizi wao mbovu uliopelekea Mfuko kupata hasara ya shilingi bilioni 3.
 
Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na gazeti moja la kila siku, baadhi ya waliosimamishwa kazi na Bodi ya NHIF na idara walizokuwa wanazimamia kwenye mabado ni Grace Lekule (Utawala), Raphael Mwamwoto (Uendeshaji), Frank Lekela (Udhibiti Ubora wa Huduma) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Michael Mhando.
 
Panga hilo pia limewapitia Yujin Mikongoti (Mifuko ya Afya ya Jamii), Ally Othman (Tehama), Rehani Athuman (Tafiti na Masoko), Makala (Sheria) na Jackson Burula (Manunuzi). 

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema kuwa anafahamu kuwepo kwa mtikisiko huo na kwamba majukumu yote alimwachia Mwenyekiti wa Bodi, Anne Makinda.
 
“Nipo Muleba, ila majukumu yote tayari niliyaacha kwa Bodi ya Mama Makinda. Yeye atakuwa anajua kila kitu,” Waziri Mwalimu ananukuliwa.
 
Taarifa hii imekuja ikiwa ni miezi michache imepita tangu Mhasibu wa NHIF mkoa wa Mara, Francis Mchati kusimamishwa kazi akihusishwa na upotevu wa shilingi bilioni 3. 

Mtuhumiwa alikabidhiwa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ambayo inaendelea na uchunguzi kwa hatua nyingine za kisheria.

Aliyeoongoza kidato cha 6 ni tunda la Shule ya Kata, aeleza alivyodharauliwa

0
0

Mwanafunzi aliyeongoza katika matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa jana na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Hassan Gwaay ameonesha moja kati ya tunda bora lililodhihirisha faida ya kuanzishwa kwa shule za kata na Serikali ya awamu ya nne iliyoongozwa na Dk. Jakaya Kikwete.

Gwaay mwenye umri wa miaka 19 ameeleza kuwa alisoma katika shule ya kata ya Mirerani Benjamin W. Mkapa mkoani Manyara alipopata elimu ya kidato cha nne na kupata ufaulu mzuri uliomuwezesha kuchaguliwa kujiunga na shule ya wavulana ya Tabora (Tabora Boys) kuendelea na elimu yake ya kidato cha tano.

Amesema kuwa alipokuwa akisoma katika shule hiyo ya kata, wanafunzi waliokuwa wanasoma katika shule za watu binafsi zenye mazingira bora zaidi ya walikuwa wakimuonesha dharau lakini alitaka kuwadhihirishia kuwa hata katika shule hiyo anaweza kufanya vizuri zaidi yao.

“Sikujali kelele na dharau za watoto waliosoma kwenye shule za kulipia, ambao mara kwa mara walikuwa wakiibeza shule yetu. Nilopomaliza kidato cha nne, nilipata daraja la kwanza alama 10 (Division 1 ya point 10). Ndipo nilipowadhihirishia kuwa hata kwenye shule za kata watu wanafaulu,” Gwaay anakaririwa na gazeti la Jambo Leo.

Mwanafunzi huyo ambaye amelelewa na bibi yake kwa muda mrefu baada ya mama yake kufariki huku akiishi mbali na baba yake (anamsapoti), alisema kuwa baada ya kujiunga na shule ya wavulana ya Tabora kusoma masomo ya Fizikia, Kemia na Hesabu (PCM), aliweka bidii zaidi hasa baada ya  kugundua kuwa wanafunzi aliokutana nao hapo wote walikuwa na akili sana.

Alisema kuwa alipofanya mtihani wa ‘Mock’ alipata Fizikia (A), Kemia (A) na Hesabu (B) na kwaba aliumia sana kuona amepata B. Aliongeza bidi hadi kuibuka na alama A kwenye mitihani yote katika Mtihani wa Taifa na kutangazwa kuwa mwanafunzi aliyeongoza.

Changamoto ya upungufu wa walimu hususan wa Sayansi katika shule nyingi za umma nchini lilimkumba pia Gwaay katika shule ya wavulana ya Tabora, lakini aliipanda ngazi hiyo ndefu kwa nguvu ya ziada bila kukata tamaa.

“Hakuwa na Mwalimu wa Fizikia pale. Tangu najiunga sikuwahi kumwona zaidi ya wakuazimwa ambaye alikuwa akija jioni na mwisho mwa wiki tu na alikuwa akija mara chache. Muda mwingi tulitumia kujisome wenyewe lakini hatukukata tamaa,” alisema.

Shule ya wavulana ya Tabora mwaka huu imerudi kwenye nafasi yake ya ubora ulioaminika miaka mingi iliyopita. Imeshika nafasi ya 5 kati ya shule zote.

Basata Wafungia Wimbo Wa ‘Pale Kati Patamu’ Wa Ney Wa Mitego.

0
0

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo wa ‘pale kati patamu’ ulioimbwa na Msanii Ney wa Mitengo kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili.
 
Msanii huyu amekuwa na tabia na mienendo yenye kuchafua Sekta ya Sanaa yeye binafsi kupitia kutoa kazi chafu na kufanya maonesho yenye kukiuka maadili. Kazi zake zikikiuka maadili na kudhalilisha utu wa mwanamke sambamba na kutoa lugha za matusi na za kudhalilisha watu wa kada mbalimbali.

Ieleweke kwamba kwa mujibu wa kifungu namba 4(L) cha Sheria ya BASATA namba 23 ya mwaka 1984, Baraza limepewa jukumu la kuhakikisha linalinda maadili miongoni mwa wasanii wanapokuwa jukwaani au wanapobuni kazi yoyote ya sanaa.

ikumbukwe kwamba BASATA limeshamuita na kumuonya msanii huyu mara kadhaa kutokana na tabia yake ya kutoa kazi zisizokuwa na maadili na aliahidi kubadilika na kuachana na tabia hiyo.

Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio haya kwa makusudi ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha Sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu kazi ya sanaa kama kazi nyingine. 

Kwa sasa Msanii huyu ametoa wimbo mwingine wa Pale Kati patamu ambao uko mitandaoni ukipambwa na picha chafu zinazoonesha mwanamke akiwa mtupu yaani uchi wa mnyama.

Kwa mantiki hii BASATA halitavumilia wasanii wachache ambao wanataka kuigeuza tasnia ya sanaa na wasanii genge la wahuni wasio na staha na wanaojipanga kuibomoa jamii. BASATA linapenda kueleza ya kufuatayo
 
• BASATA linatamka kuwa limeufungia wimbo huu rasmi kutumika kwa namna yoyote ile.
• Aidha pamoja na adhabu ya kufungia wimbo huu hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
 
Aidha, BASATA linawataka Wasanii wote nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu mara wanapotengeneza kazi zao.
SANAA NI KAZI, TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI

Godfrey Mngereza
KATIBU MTENDAJI.

Taarifa: Rais Magufuli afanya uteuzi wa Viongozi Mbalimbali...... Augustino Lyatonga Mrema ateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka aliyopewa amefanya uteuzi wa viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za Serikali, na pia amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;
  1. Augustino Lyatonga Mrema.
  • Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia leo tarehe 16 Julai, 2016.
  • Augustino Lyatonga Mrema anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mstaafu Mhe. Eusebia Nicholaus Munuo ambaye muda wake umemalizika.
  1. William R. Mahalu
  • Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.
  1. Mohamed Janabi
  • Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
  1. Angelo Mtitu Mapunda
  • Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
  1. Sengiro Mulebya
  • Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
  1. Oliva Joseph Mhaiki
  • Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
  1. Winifrida Gaspar Rutaindurwa
  • Ameteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
  1. Charles Rukiko Majinge
  • Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.
  1. Julius David Mwaiselage
  • Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

Kupandishwa Vyeo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa 25 wa Jeshi la Polisi kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) na kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP).

Waliopandishwa vyeo hivyo ni kama ifuatavyo;

  1. Essaka Ndege Mugasa
  2. Adamson Afwilile Mponi
  3. Charles Ndalahwa Julius Kenyela
  4. Richard Malika Revocatus
  5. Geofrey Yesaya Kamwela
  6. Lucas John Mkondya
  7. John Mondoka Gudaba
  8. Matanga Renatus Mbushi
  9. Frasser Rweyemamu Kashai
  10. Ferdinand Elias Mtui
  11. Germanus Yotham Muhume
  12. Fulgence Clemence Ngonyani
  13. Modestus Gasper Lyimo
  14. Mboje John Shadrack Kanga
  15. Gabriel G.A. Njau
  16. Ahmed Zahor Msangi
  17. Anthony Jonas Rutashubulugukwa
  18. Dhahir Athuman Kidavashari
  19. Ndalo Nicholus Shihango
  20. Shaaban Mrai Hiki
  21. Simon Thomas Chillery
  22. Leonard Lwabuzara Paul
  23. Ahmada Abdalla Khamis
  24. Aziz Juma Mohamed
  25. Juma Yussuf Ally

Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi wengine 34 kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP).

Waliopandishwa vyeo hivyo ni kama ifuatavyo;

  1. Fortunatus Media Musilimu
  2. Goyayi Mabula Goyayi
  3. Gabriel Joseph Mukungu
  4. Ally Omary Ally
  5. Edward Selestine Bukombe
  6. Sifael Anase Mkonyi
  7. Naftari J. Mantamba
  8. Onesmo Manase Lyanga
  9. Paul Tresphory Kasabago
  10. Dadid Mshahara Hiza
  11. Robert Mayala
  12. Lazaro Benedict Mambosasa
  13. Camilius M. Wambura
  14. Mihayo Kagoro Msikhela
  15. Ramadhani Athumani Mungi
  16. Henry Mwaibambe Sikoki
  17. Renata Michael Mzinga
  18. Suzan Salome Kaganda
  19. Neema M. Mwanga
  20. Mponjoli Lotson
  21. Benedict Michael Wakulyamba
  22. Wilbroad William Mtafungwa
  23. Gemini Sebastian Mushi
  24. Peter Charles Kakamba
  25. Ramadhan Ng’anzi Hassan
  26. Christopher Cyprian Fuime
  27. Charles Philip Ulaya
  28. Gilles Bilabaye Muroto
  29. Mwamini Marco Lwantale
  30. Allute Yusufu Makita
  31. Kheriyangu Mgeni Khamis
  32. Nassor Ali Mohammed
  33. Salehe Mohamed Salehe
  34. Mohamed Sheikhan Mohamed
Maafisa hawa wa Jeshi la Polisi Tanzania wamepandishwa vyeo kuanzia tarehe 15 Julai, 2016.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
16 Julai, 2016
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images