Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Nape: CCM Imejaa Majipu

$
0
0

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema ndani ya chama hicho tawala kuna majipu mengi yanayohitaji kutumbuliwa. 

Kwa mujibu wa katibu huyo wa uenezi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, hatua hiyo ndiyo njia pekee ya kuleta mapinduzi na mageuzi ndani ya chama hicho. 

Amesema chama hicho kilishaingiliwa na makolokolo, hivyo yanahitaji kusafishwa yote kwa mustakabali wake. 

Kauli ya Nape ni sawa na ile iliyowahi kutolewa na viongozi wakuu wa nchi. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan mwanzoni mwa mwaka huu akiwa mkoani Tanga alisema ndani ya CCM kuna watu majipu ambao wameficha makucha ili wasijulikane uovu wao. 

Siku ambayo Rais John Magufuli alipewa cheti na Tume ya Uchaguzi (NEC) baada ya kushinda uchaguzi alikwenda kwenye ofisi ndogo za CCM Lumumba na kuhutubia huku akisisitiza kuwa ndani ya chama hicho kuna watu wanafiki. 

Nape anasema pamoja na kutumbua majipu, chama hicho pia kinahitaji kujitathimini muundo wake kwa kuwa uliopo sasa ni mkubwa na hauendani na hali halisi ya kipato cha chama.

“Muundo wetu ni mzigo mzito unaongeza urasimu. Kwa mfano wajumbe wa NEC hivi sasa wapo zaidi ya 400 ni mzigo mkubwa kwa chama matokeo yake walitumia fursa kutafuta ubunge, inahitaji marekebisho makubwa kwa kuwa uchumi wa chama ni mdogo kwa sasa, tunategemea ruzuku tu. "- Nape

Alisema hata katika upande wa watumishi wa chama wapo wengi sana na wote si wanasiasa, robo tu ndiyo wanasiasa.

Kwa mujibu wa Nape, kwa sasa kinachohitajika ni kutengeneza chama kidogo ili gharama ya kuendesha iwe ndogo. 

Alisema sababu nyingine ya kusafisha chama kutokana na urasimu uliopo; “Lazima tupunguze mlolongo wa vikao vya kutoa maamuzi lakini pia tuangalie upya sera na taratibu zetu.” 


 Akizungumzia watu wenye tabia ya kuhama vyama kama ilivyotokea kwa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa na kundi lake, Nape alisema yeye si muumini wa hilo.

“Mimi siamini katika kuhama  vyama ni sawa na kumsilimisha Papa. Kwangu kuchukua watu kutoka upinzani ni sawa na gari zima kuwekewa vifaa chakavu. Watanzania waliopo katika vyama vya siasa hawazidi milioni 10 kwa nini tunyang’anyane wakati kuna zaidi ya watu milioni 45."- Nape


Akizungumzia utendaji wa Rais John Magufuli, Katibu huyo wa uenezi wa chama hicho anayetarajia kustaafu hivi karibuni katika mkutano mkuu alisema ameanza vizuri na kwamba mtindo wake wa kutumbua majipu ndiyo hasa ulikuwa ufanyike baada ya wananchi kukosa imani na Serikali kwa muda mrefu.

 “Yanayotekelezwa hivi sasa na Rais Magufuli ni ripoti yetu. Baada ya kuzunguka nchi nzima tuligundua mambo mengi na ili kukiweka salama chama hatuna budi kuhakikisha tunasafisha uozo wote. 

“Ilifika wakati wawekezaji wamechukua ardhi hawaitumii, wananchi hawana ardhi tena matokeo yake ni migogoro kila kukicha, walimu wanadai haki yao watu wenye mamlaka hawatimizi wajibu wao matokeo yake kukaanza kujengeka hisia kwamba walimu ni wapinzani.

 "Hivi mtu anakuwaje mpinzani kama anadai haki yake? Mlipe kwanza haki yake uone kama ataendelea na malalamiko,” alisisitiza Nape ambaye aliingia rasmi katika siasa akiwa kijana mdogo wa miaka 20 tu. 

Alisema Rais Magufuli amerejesha heshima kwani nchi ilifika mahali ambapo wezi wa mali ya umma walionekana ndiyo wajanja na wale ambao walikuwa wana maadili walionekana legelege. 

Alisema jamii ilipotea na Taifa lilikuwa likijenga jamii ya ajabu ya watu mafisadi, wezi na wasioogopa mali ya umma na hawakuwa na wa kuwazuia kufanya wanavyotaka. 

 Akizungumzia mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya chama chake uliofanyika mkoani Dodoma mwishoni mwa mwaka jana Nape alisema vikao vilikuwa vya moto sana. 

“Wakati mwingine tulikaa katika mkutano mpaka saa tisa usiku na hata mkitoka hamtazamani usoni kila mmoja anaingia katika gari na kuondoka, palichemka sana.” 

Hata hivyo, Nape alisema anashukuru Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Jakaya Kikwete kwa kuwa na kifua na hiyo ndiyo siri ya kufanikisha mchakato huo. 

Alisema Kikwete ni mtoto wa CCM hivyo ilikuwa rahisi kumkata yeyote kwani uzoefu wake ndani ya chama ulisaidia na kwamba itachukua muda mrefu kupata kiongozi kama yeye lakini pia hawawezi kupuuza kazi iliyofanywa na Katibu Mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana. 

“Ukongwe ulituvusha lakini pia wazee wakarekebisha mambo tukavuka salama, hali ilikuwa mbaya lakini ndiyo demokrasia,” alisisitiza Nape ambaye ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe, marehemu Moses Nnauye. CCM itafanya mkutano mkuu Julai 23 mwaka huu.

Wataalamu wa Prescion Air na TCAA Waelekea Zanziba r Kuchunguza Tukio la Ndege Kuwaka Moto

$
0
0

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), wakishirikiana na mafundi wa Kampuni ya Ndege ya Prescion Air wameelekea Zanzibar kuchunguza tukio la ndege ya kampuni hiyo kupata hitilafu na kuwaka moto na kusitisha safari.

Tukio hilo lilitokea Juni 16 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Karume mjini Zanzibar. 

Taarifa iliyotolewa jana na Mkuu wa Mawasiliano wa Prescion Air, Azda Mkullo inasema wamepeleka injini mbadala kwa ajili ya kufungwa.

Inaongeza kuwa baada ya tukio hilo ilimlazimu rubani kuchukua hatua za kuuzima moto na kuirudisha ndege kwenye eneo la maegesho. 

Ndege hiyo wakati ikipata hitilafu ilikuwa imefanya safari zake kati ya Kilimanjaro na Dar es Salaam.Ndege hiyo PW432 ilikuwa na abiria 34 na wahudumu wanne wote walitoka salama.

Maofisa Utumishi 1,500 Hatarini Kutumbuliwa

$
0
0
SERIKALI imeagiza wote waliotengeneza watumishi hewa wafunguliwe mashitaka mahakamani huku ikionya kuwa iko tayari kusimamisha kazi maofisa utumishi wote nchi nzima wanaofikia 1,500 katika sakata hilo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angella Kairuki alisema hayo jana alipokuwa akichangia mjadala wa Hotuba ya Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2016/2017 bungeni mjini Dodoma. 

Amesema tayari serikali imeshatoa agizo hilo la kuwashitaki maofisa wote waliotengeneza watumishi hewa na ikibidi iko tayari kuwasimamisha kazi maofisa utumishi 1,500 waliofundishwa kazi hiyo na serikali.

Kwa mujibu wa Waziri Kairuki, mpaka mwishoni mwa Mei, serikali ilikuwa imebaini uwepo wa watumishi hewa 12, 246 waliokuwa wakitafuna Sh bilioni 25.06 kila mwezi. 

Katika kuelezea athari za ufujaji huo wa fedha za serikali, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji alisema hata katika ulipaji wa madeni ya mifuko ya hifadhi ya jamii, Rais John Magufuli aliagiza uhakiki ufanyike, kabla ya kulipa kwa kuwa penye wafanyakazi hewa, kuna malipo hewa ya wastaafu.

Alitoa mfano wa deni la Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Serikali ilikuwa ikidaiwa Sh trilioni 2.67 lakini uhakiki wa deni hilo ulipofanyika, deni hilo likabainika ni Sh trilioni 2.04, hatua iliyosaidia Serikali kuepusha wizi wa karibu Sh bilioni 600 za wastaafu hewa. 

January na uthubutu 
Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), January Makamba alizungumzia ahadi ya Rais ya kutoa Sh milioni 50 kila kijiji na kufafanua kuwa Sh bilioni 59 zilizotengwa, zitatumika kujifunza namna ya kutekeleza ahadi hiyo.

Aliwataka wabunge wa CCM kukumbuka kuwa chama hicho kilipomtangaza Dk Magufuli kuwa ndiye mgombea urais, kilitoa taarifa duniani ya aina ya Serikali, uongozi na mabadiliko wanayotaka Watanzania. 

Alisema mabadiliko ya kweli hayawezi kutokea bila kuwepo kwa hatua kubwa na uthubutu ndio maana serikali imethubutu kuwa na Bajeti ya Sh trilioni 29.5 na uthubutu wa kutenga asilimia 40 ya bajeti hiyo katika maendeleo.

Kwa mujibu wa January, mahali popote kwenye uthubutu, lazima kutakuwa na watu watakaotia shaka na kuwataka wabunge wa CCM wasitilie shaka uwezo wa serikali katika kukusanya Sh trilioni 29.5 zilizokusudiwa. 

Alisema wabunge wa CCM ndio wengi katika Bunge na Ilani ya Uchaguzi inayotekelezwa ni ya chama hicho, hivyo ni muhimu wamuunge mkono Rais Magufuli kwani akifanikiwa Rais na Tanzania imefanikiwa.

Alikumbusha kuwa maendeleo yanahitaji kujitoa sadaka na viongozi wao wamekubali kujitoa sadaka, hivyo wabunge, wafanyabiashara mpaka wadogo wakiwemo bodaboda, wajitoe sadaka kwa kulipa kodi. 

Alitumia kauli ya Rais John Kennedy wa Marekani aliyoitoa miaka ya mwanzo ya 1960, alipowataka wananchi wa nchi hiyo, kutouliza nchi hiyo itawafanyia nini, bali wajihoji wao wataifanyia nini nchi yao.

Watanzania wanune 
Naye Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alieleza namna Serikali ya China ilivyoridhia kutoa Sh trilioni tano nje ya Bajeti ya Serikali kwa ajili ya ujenzi wa viwanda kwa sekta binafsi, huku ikiahidi kutoa fedha nyingine Dola za Marekani milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo.

Alihitimisha kwa kusema ujenzi wa uchumi wa viwanda ni sawa na vita na wakati wa vita, hakuna anayecheka hivyo Watanzania wote lazima wanune, ili kutimiza malengo ya kuongeza pato la jumla la taifa. 

Aidha, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema pato la jumla la Taifa kwa sasa ni Dola za Marekani bilioni 55 na ili Tanzania ifike katika uchumi wa kati, inatakiwa kuongeza uzalishaji utakaoongeza pato la jumla la Taifa kuwa Dola za Marekani bilioni 200.

Alisema injini za kupeleka uzalishaji na uchumi katika kipato hicho, ziko nyingi na mojawapo ni sekta ya nishati ya umeme ambayo katika bajeti hiyo ya serikali, Wizara ya Nishati na Madini imetengewa Sh trilioni 1.43 ambapo asilimia 94 ya hizo ni za maendeleo na kati ya fedha hizo za maendeleo, asilimia 95 inakwenda kwenye umeme.

Katika kudhihirisha nia ya serikali katika sekta hiyo, Profesa Muhongo alisema katika bajeti inayomaliza muda wake, wizara hiyo imeshapata asilimia 80 ya fedha zilizotengwa katika bajeti ya mwaka huu unaoisha huku Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) ikiwa imeshapata asilimia 80 ya fedha iliyotarajia. 

Aliwaeleza wabunge kuwa katika bajeti waliyopitisha, usambazaji wa umeme vijijini umepangiwa Sh bilioni 534.

Vigogo Kuondolewa kwa Nguvu nyumba za Serikali

$
0
0

VIGOGO wakiwamo wabunge na wananchi wengine, walionunua nyumba za serikali na kutomaliza kulipa madeni yao kwa wakati kama mikataba yao inavyoelekeza, wameanza kuondolewa kwa nguvu kwenye nyumba hizo na nyumba kupigwa mnada ili kupata fedha za kulipa madeni ya Sh bilioni sita.

Madeni hayo serikali inadai kupitia Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). 

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yono Auction Mart ambayo imepewa kazi ya kukusanya madeni hayo ya TBA kutoka kwa wadaiwa sugu hao, Scholastica Kevela alisema kazi ya kuwaondoa vigogo walionunua nyumba hizo au kupangisha bila kulipa, inaanza leo jijini Dar es Salaam.

Kevela alisema katika kazi hiyo, TBA wamewapa orodha ya zaidi ya nyumba 3,000 nchi mzima za walionunua na wengine kupangisha nyumba za TBA ambao wanadaiwa madeni na muda wa kurejesha ulishapita.

“Tuna orodha za nyumba zaidi ya 3,000 nchi nzima, juzi tulianza Mwanza tumeshikilia nyumba zaidi ya 20, kwa kuwatoa watu nje, na juzi Dodoma tumefanya hivyo, tumeshashikilia nyumba 40 zikiwemo za vigogo, kesho (leo), tunaanza zoezi hilo hapa Dar, hatutakuwa na huruma kwa mdaiwa, wote tulishawapa taarifa za kimaandishi, kazi yetu ni utekelezaji tu,” alisema Kevela.

Alisema wanatekeleza kazi waliyopewa kwa sababu hata Rais John Magufuli anasisitiza wananchi kulipa kodi ili nchi iendelee na kuacha utegemezi, hivyo wadaiwa sugu hao muda wa kulipa na hata muda wa ziada waliopewa kuhakikisha wamemaliza madeni yao nao ulipita na wengi hawakulipa, hivyo Yono inaingia kazini kupiga mnada nyumba hizo.

Alisema walionunua nyumba za serikali na hawajamaliza kulipa madeni wakiwemo wabunge, vigogo na wananchi wengine wanajitambua, hivyo kuanzia leo wanapaswa kuondoka kwani zitauzwa ili kulipa deni la serikali.

Kadhalika alisema waliopanga kwenye nyumba hizo na bado wanadaiwa kodi msako huo unawahusu na kwamba wataondolewa wote na vitu vyao kupigwa mnada ili kupata fedha za kulipa kodi wanayodaiwa na serikali.

“Sisi tunatekeleza agizo kulingana na mkataba wetu na pia tunamsaidia Rais kukusanya kodi, hivyo wote wanaodaiwa wafahamu tutawafuata walipo na kupiga mnada mali zao ili kulipa kodi ya serikali,” alisema Kevela.

Hata hivyo, alisema mchanganuo wa nyumba hizo na majina ya vigogo na wabunge watatoa baadaye baada ya kufanya upembuzi kwa sababu nyumba za wadaiwa ni nyingi. 

Awali akizungumzia madeni ya wakwepa kodi wa Mamlaka ya Mapato (TRA), waliokwepa kulipia kontena zaidi ya 320 zilizogunduliwa na Rais Magufuli, Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo, Yono Kevela alisema wanaendelea kukusanya madeni ya wadaiwa hao.

Alisema Yono imekamata mali za wadaiwa hao na baadhi zimeshapigwa mnada na nyingine zinaendelea kuuzwa ili kupata fedha za kulipa kodi, na hadi sasa takribani Sh bilioni saba zimeshalipwa kati ya Sh bilioni 18 zilizokuwa zinadaiwa.

CHADEMA Wataka Mkutano Mkuu wa CCM Kumkabidhi Uenyekiti Magufuli Nao Uzuiliwe

$
0
0

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetoa tamko zito kikitaka Polisi kuzuia Mkutano Mkuu wa CCM utakaofanyika mwezi ujao, vinginevyo watatumia nguvu ya umma kuuzuia.

CCM kimeitisha mkutano mkuu maalumu unaotarajiwa kufanyika Julai 23 mjini Dodoma, kwa lengo la Mwenyekiti wa chama hicho, Jakaya Kikwete kumkabidhi uongozi wa chama, Rais John Magufuli.

Kauli ya kutaka Polisi kuzuia mkutano huo kama inavyofanya kwa vyama vingine vya siasa, ilitolewa juzi mjini Moshi na Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Julius Mwita.

Msimamo huo wa Chadema ambao uliungwa mkono na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalim unafuatia Polisi kuzuia mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu ambao ni wanachama wao.

Akizungumza na wanahabari, Mwita alikwenda mbali na kudai kuwa, Chadema watalifungulia Jeshi la Polisi kesi ya madai ya fidia kwa kuvuruga mahafali ya Chaso mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita.

“Ukisoma barua yao wamesema wamezuia mikutano ya hadhara sasa kama wanakuja hadi kwenye vikao vya ndani, hatuwezi kuendelea kukubali jambo hili.Tumetumia busara sana,” alisema Mwita na kuongeza: 

“Msipouzuia Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma Julai 23 tunakuja kuuzuia sisi... yaani muwe tayari kusafiri kwenda Dodoma tukauzuie ule mkutano la sivyo, wauzuie kama walivyouzuia mikutano yetu.” 

Mwita alimgeukia Mwalimu na kumweleza kuwa hiyo ni lugha ya ujana na inatekelezeka, akawahoji vijana wa Chaso waliokuwapo: “Wangapi mko tayari kuja Dodoma?” Wote wakaafiki.

“Intelijensia ya polisi ni ya kiumbea, inayoweza kujua tu Chadema wanakwenda kwenye mkutano, haiwezi kujua watu wamejificha wana bunduki na risasi 300 kwenye mawe kule Mwanza,” alidai.

Mwalimu alisema utaratibu wa Polisi na Serikali lazima ukome na kwamba wao ni viongozi.

Kesi ya Mauaji ya Mwanahabari, Daud Mwangosi Kuendelea Leo

$
0
0

Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, jana iliahirisha kesi ya mauaji ya mwanahabari, Daud Mwangosi inayomkabili askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Iringa (FFU), Pasificus Simon hadi leo. 

Kesi hiyo iliahirishwa baada ya upande wa Serikali kufunga ushahidi wake. Kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa Februari 12, mwaka 2012, leo inaendelea kwa upande wa utetezi kuleta mashahidi wake mbele ya Jaji Paul Kihwelo anayeisikiliza.

Katika kesi hiyo ambayo haikuchukua muda mrefu mahakamani hapo jana, mawakili wa Serikali wakiongozwa na Sandy Hyra na Ladislaus Komanya walisema wamefunga ushahidi kwa mashahidi wanne wa awali.

Baada ya wakili wa utetezi, Rwezaura Kaijage kukubaliana na maombi ya upande wa Serikali kufunga ushahidi wao, Jaji Kihwelo aliiahirisha kesi hiyo hadi leo.

Awali, mtuhumiwa Simon alifikishwa mahakamani hapo akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi ambao hawaruhusi apigwe picha na waandishi wa habari.

Mwangosi aliuawa kwa kupigwa bomu Septemba 2, 2012 katika Kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi alipokuwa akiwajibika kwa kazi za kihabari wakati wa ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Serikali Yaagiza Wakimbizi Wanajeshi, Wenye Silaha Wajisalimishe

$
0
0

Serikali ya Tanzania imewataka wakimbizi wote ambao walikuwa wanajeshi kutoka nchi walizokuwepo, kuripoti kwenye mamlaka husika ili waweze kupewa uangalizi maalum (special protection) kama wanajeshi.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali (Mstaafu) Emmanuel Maganga, wakati wa maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani yaliyofanyika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.

Alisisitiza kuwa wakimbizi ambao wako nchini wakijua ni wanajeshi ni lazima wasajiliwe na mamlaka husika.

Aidha Maganga aliwataka vile vile wakimbizi wote ambao wanamiliki silaha wazisalimishe kwa hiari yao wenyewe.

Alisema kumekuwa na matukio mengi ya ujambazi wa kutumia silaha na hivyo kuhatarisha amani na kuwaamuru wenye silaha kuzisalimisha mara moja ili waende sawa na sheria za nchi walikopata hifadhi.
 
Mkuu huyo wa mkoa pia alitoa wito kwa mashirika ya misaada duniani kutoa misaada inayoowana na misaada inayotolewa kwa nchi zilizoendelea na kuongeza kuwa mahitaji ya binadamu ya msingi hayatofautiani iwe nchi zilizoendelea au zinazoendelea.

Alisema kuwa wakimbizi waliopo kwenye nchi zilizoendelea hupewa makazi ya kudumu na vyakula tofauti tofauti wakati waliopo kwenye nchi zinazoendelea hupewa mahema na chakula aina moja ambayo ni mahindi.

“Mwaka jana tulishindwa kuadhimisha siku ya wakimbizi duniani kwa kuwa tulikuwa tunawapokea wakimbizi kutoka Burundi,” alisema.

Alisema wakimbizi wameongezeka sana nchini na sasa hivi kuna makambi matatu yanayowahifadhi wakimbizi nchini.
 
Wakati huo huo Tanzania imepongezwa kwa ukarimu wake kwa kuwahifadhi wakimbizi kwa zaidi ya miongo minne sio tu kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na hata duniani.

Mwakilishi mkazi wa shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR , Chansa Kapaya alisema hayo katika sherehe za kuadhimisha siku ya wakimbizi duniani yenye kauli mbiu kuwa “Tupo Pamoja na Wakimbizi, Tafadhali ungana nasi”.

“Tanzania ni mfano wa kuigwa kwa mfano mzuri wa kuwahifadhi wakimbizi wengi duniani na pia kuwatafutia suluhu,” alisema.

Alisema mwaka 2014 Tanzania iliwapa uraia wakimbizi zaidia ya 162,000 baada ya kuishi nchini kwa zaidi ya miaka 40.

Aliongeza kuwa, wakimbizi wanapaswa kuthaminiwa kama binadamu wengine kwa kuwa hakuna mtu anayechagua kuwa mkimbizi.

Kapaya alisema kuwa kwa sasa kambi ya Nyarugusu ina wakimbizi zaidi ya 131,733 ambao ni wengi zaidi na kusababisha msongamano unaohatarisha maisha yao.

Wabunge wa Upinzani Watoka Bungeni Kimyakimya

$
0
0

Wabunge wa Ukawa wameendelea kususia vikao vinavyoongozwa na Dk Tulia Ackson, lakini leo wametoka kimyakimya bila mbwembwe kama za jana.

Kwa sasa kamati ya uongozi ya umoja huo imeingia kufanya kikao kujadili mustakabali wao.

Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amesema watatoa taarifa kamili baada ya kumaliza kikao hicho.


DPP Awaondolea Rufani Mawaziri Waandamizi Basil Mramba Na Daniel Yona

$
0
0
Mkurugenzi wa Mashitaka Tanzania (DPP), ameiondoa mahakamani rufani aliyoikata dhidi ya Mawaziri Waandamizi wa zamani, wa Fedha Basil Mramba na wa Madini Daniel Yona iliyopangwa kusikilizwa jana katika Mahakama ya Rufani Tanzania.

Rufani hiyo iliondolewa jana kabla ya kuanza kusikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Mbarouk Mbarouk, Salum Massati na Profesa Ibrahim Juma.

Mapema Juni 20, mwaka huu, DPP aliwasilisha kusudio la kuondoa rufani hiyo chini ya kanuni ya 77(1) ya Mahakama ya Rufani pamoja na nakala kuwakabidhi mawakili wa utetezi.

Hata hivyo, jopo hilo lilisema kwamba kifungu alichokitumia DPP kuwasilisha kusudio hiyo siyo sahihi kwa kuwa kinatumika kabla ya shauri halijapangwa kusikilizwa.

Jaji Mbarouk alisema DPP alitakiwa kutumia kanuni ya 4(2)(a) ya Mahakama ya Rufani kuomba kuondoa rufani hiyo.Mawakili wa Serikali Waandamizi, Theophil Mutakyawa na Shadrack Kimaro, walieleza nia ya DPP ya kuondoa rufani hiyo, jambo ambalo halikuwa na pingamizi kwa upande mwingine.

Jopo hilo lilikubali maombi ya kuondoa rufani hiyo. Mapema mahakamani hapo DPP alikata rufani kupinga hukumu iliyotolewa Oktoba 2, mwaka 2015 na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam iliyoketi chini ya Jaji Projest Rugazia.

Jaji Rugazia alisema mawaziri hao walitakiwa kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili na siyo miaka mitatu kama Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam ilivyowahukumu,dhidi ya mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka.

Kadhalika, Jaji Rugazia alikubaliana na hukumu ya kumwachia huru Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja.

Hata hivyo, DPP alikata rufani Mahakama Kuu, kupinga adhabu waliyopewa mawaziri hao kwamba ni ndogo kwa sababu jopo la mahakimu watatu waliotoa hukumu hiyo walikosea kumwachia huru Mgonja.

Mbali na kupinga adhabu hiyo, DPP aliomba mahakama kuwaamuru washtakiwa kulipa fidia ya fedha walizosababisha hasara.

Mahakama ya Kisutu, iliwahukumu Mramba na Yona kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya sh. milioni tano, baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya sh. bilioni 11.7 kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni ya kukagua madini ya dhahabu ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.

Kwa sasa mawaziri hao wanatumikia kifungo cha nje baada ya kupendekezwa kuwa miongoni mwa wafugwa wanaohitaji kumalizia sehemu ya kifungo chao wakiwa nje, ikiwamo kufanya usafi katika Hospitali ya Sinza Palestina.

Mahakama yamgomea Mbowe...Yatupilia Mbali Kesi Yao Ya Kupinga Zuio La Polisi

$
0
0
KESI ya madai iliofunguliwa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kuiomba mahakama kupiga marufuku zuio la Polisi, leo limetupiliwa mbali.
 
Mbowe alifungua kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2016, baada ya hivi karibuni Jeshi la Polisi  kupiga marufuku mikutano ya hadhara kwa madai kwamba, hali ya usalama nchini si salama.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai, Kilimanjaro katika shauri hilo, aliwashtaki Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kwa madai wanahusika kuzuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.

Mbowe ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, walitangaza kufanya oparesheni iliyopewa jina ‘Okoa Demokrasia nchini’ iliyokuwa na lengo la kuishtaki serikali kwa wananchi kwa kile alichodai, kuendesha nchi bila kufuata katiba ya nchi.

Hata hivyo, baada ya kupigwa marufuku kwa maandamano, Mbowe alifungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, akiiomba kutengua zuio hilo la polisi.

Mohammed Gwae, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, leo amepitia ombi lililopelekwa mahakamani hapo na upande wa mlalamikaji anayewakilishwa na mawakili John Mallya na Gasper Mwanalelya na kutoa uamzi.

Jaji Gwae akitoa uamuzi wa ombi la walalamikaji amedai kuwa, amefikia hatua hiyo baada ya walalamikaji kukosea kifungu cha kupeleka shauri hilo kortini kitendo kilichosababisha kulitupilia mbali.

Amesema kuwa, walalamikaji baada ya kupeleka ombi hilo kortini, upande wa wajibu maombi unaoongozwa na mawakili, Seth Mkemwa na Robert Kidando waliweka pingamizi wakiomba mahakama kutokusikiliza ombi hilo.

Jaji Gwae amesema kuwa, walalamikaji katika ombi lao walikosea kutumia kanuni ya tano kifungu kidogo cha tatu cha sheria ya mwaka 2014 badala ya kanuni ya tano kifungu kidogo cha pili ambacho kilitakiwa kutumiwa.

“Waleta maombi wametumia kanuni ya tano kifungu kidogo cha tatu badala ya kutumia kanuni ya tano kifungu kidogo cha pili kilichotakiwa kuwepo katika kuleta ombi na kama kifungu hiki hakijatumika hapo na ombi halipaswi kupokelewa,” amesema Jaji Gwae.

Hata hivyo Jaji Gwae amesema, licha ya kuwekewa pingamizi na wajibu maombi, walalamikaji wamesema kanuni na kifungu hicho ndivyo vilitakiwa kuwepo na hivyo vinavyopaswa kuwekwa sio sahihi.

Amesema kuwa, katika shauri la namna hiyo, kanuni na vifungu vilivyotakiwa kuwepo ni kanuni ya tano kifungu kidogo cha pili na kanuni ya tano na kifungu kidogo cha sheria ya mwaka 2014 na kwamba wao waliviweka katika maelezo (Statements) badala ya (chember samers).

Mallya, mwanasheria wa mpeleka maombi amesema kuwa, baada ya kukosea kanuni na vifungu hivyo, watapeleka kwa mara nyingine ombi na kulifanyia marekebisho kama Jaji Mohamed Gwae alivyoelekeza.

Rais Magufuli amteua Dkt. Jim Yonazi kuwa Mkurugenzi Mtendaji TSN.

$
0
0
 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Jim James Yonazi kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais Magufuli amefanya uteuzi huo kuanzia tarehe 18 Juni, 2016.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Jim James Yonazi alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa katika Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Dkt. Jim James Yonazi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Gabriel Nderumaki ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
   
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
21 Juni, 2016

Waziri Mwakyembe kulishitaki gazeti la Dira lililosema ametapeli bilioni 2

$
0
0
June 21 2016 Waziri wa katiba na sheria Harrison Mwakyembe amekanusha taarifa za uongo zilizotolewa na gazeti la DIRA ikiwa ni pamoja na kuhusishwa na utapeli. Pia ameahidi kuwapeleka Mahakamani wahusika wote waliosambaza taarifa hiyo bila kuwa na ushahidi.

"Jumatatu ya tarehe 13/6/2016 gazeti la DIRA YA MTANZANIA lilichapisha taarifa iliyosema Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2, kupandishwa mahakamani wakati wowote. Napenda nikiri kuwa sijawahi kushuhudia upotoshaji mkubwa na wa makusudi kama huu " Amesem a waziri Mwakyembe na kuongeza

"Ukiisoma taarifa za gazeti hili utaona waziwazi umakini na weredi wa uandishi wa habari unakosekana, hata jina la wizara yangu limekosewa. Makosa yaliyonukuliwa na gazeti hili ni makosa ya jinai kwahiyo nahakika Dira wanauhakika ni lini Polisi walinihoji 

"Wameona hiyo haitoshi, wiki hii wamekuja na taarifa ya kulizalilisha jeshi letu kwa kusema kifaru chake cha kivita kimeibwa, huku ni kukosa uzalendo na kulitia doa jeshi letu. Tukikaa kimya tutaambiwa tena kuwa hicho kifaru kinatumika kama daladala.

"Tutafungua kesi hii mahakama kuu ya Tanzania na bado mimi na mawakili wangu tunaangalia impact na kuhusika kwa vyombo vikubwa vya  habari  kama ITV na Star Tv  kwa kutangaza taarifa "

Serikali Yafuta Utaratibu Ilioupendekeza Kwa Taasisi Za Dini Kulipa Kodi Kwanza Kwa Bidhaa Watakazonunua

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip mpango amesema amefuta utaratibu alioupendekeza bungeni wa taasisi za dini kulazimika kulipa kodi kwanza kwa bidhaa watakazonunua au kuagiza nje na kodi hiyo kurejeshwa baada ya ukaguzi kufanyika.

Waziri Mpango ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akitoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja za wabunge kuhusu Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Amesema kwa kutambua mchango mkubwa wa taasisi mbalimbali za kidini katika utoaji huduma za elimu na afya anapendekeza kufuta utaratibu huo na badala yake Serikali itaimarisha zaidi hatua mbalimbali za udhibiti wa msamaha ya kodi.

Habari Zilizopo Katika Magazeti yua Leo Jumatano ya June 22

Kodi ya ushuru wa bidhaa katika Ada ya miamala ya benki na simu za mkononi hautamuathiri mtumiaji wa mwisho

$
0
0

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango amewatoa wasiwasi watanzania juu ya kodi ya ushuru wa bidhaa katika miamala ya benki na simu za mkononi kwamba haitawaathiri wao ila makampuni ya simu.

Mhe. Mpango ameyasema hayo Jana mjini Dodoma alipokuwa akitolea ufafanuzi taarifa za upotoshaji zinazoenezwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu namna Serikali itakavyotekeleza Bajeti ya mwaka 2016/2017 iliyopitiswa jana na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Kwa sasa sheria inatamka kwamba ada itatozwa katika kutuma fedha tu, hata hivyo baadhi ya kampuni za simu na benki zimekuwa zikitumia mwanya wa sheria hiyo kupunguza wigo wa kodi kwa kutoza ada wakati wa kupokea,” alisisitiza Mhe. Mpango.

Mhe. Mpango aliendelea kufafanua kuwa, kwa kuwa makampuni ya simu na benki yamekuwa yakitoza ada wakati wa kupokea fedha huku serikali haiwatozi kodi kwa fedha zinazopokewa, hivyo basi Serikali imeamua kutoza ushuru kwenye ada ya kutuma na kupokea fedha au vyote kwa kadri itakavyotozwa.

Aidha Mhe. Mpango alisisitiza kwa kusema kuwa ushuru huo utalipwa na benki na kampuni ya simu na siyo mtumiaji au mpokeaji wa fedha katika miamala itakayofanyika.

Hivyo basi Waziri Mpango ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kuhakikisha kwamba tozo hiyo inaendana na uhalisia wa huduma inayotolewa kwa kufanya ukaguzi wa miamala ya makampuni  ya simu kabla na baada ya tozo ili yasihamishie mzigo kwa mtumiaji wa mwisho.

Kuhusu suala la kulipa kodi Mhe. Mpango amewasisitiza wananchi kulipa kodi kama inavyotakiwa ili Taifa liweze kujenga uwezo wa kujitegemea na kuwaletea wananchi wake maendeleo ya kweli kwa kuwa hiyo ndio dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Muhimbili yaboresha Huduma ya Chakula kwa Wagonjwa........Yawaondolea usumbufu ndugu wa wagonjwa kupeleka chakula mara tatu kwa siku.

$
0
0

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeboresha huduma za chakula kwa wagonjwa wote watakaolazwa kuanzia Julai Mosi, mwaka huu ili kuwaondolea ndugu wa wagonjwa usumbufu na gharama za usafiri wakati wa wanapokwenda kuwaona ndugu zao waliolazwa mara tatu kwa siku katika hospitali hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana Jijini Dar Es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Hospitali ya Taifa Muhimbili Bw. Aminiel Aligaesha alisema hospitali imeingia ubia na mzabuni ili kutoa huduma hiyo kwa wagonjwa wote wanaolazwa.

Kwanini Hospitali imechukua hatua hii
Bw. Aligaesha alisema Hospitali inataka kujikita katika majukumu yake ya msingi ambayo ni kushauri, kuchunguza na kutibu.

“Aidha Hospitali inataka kuwaondelea adha ndugu wa wagonjwa ambao wamekuwa wakiingia gharama kubwa hususani usafiri wa kuja Hospitalini mara tatu kwa siku, ambapo kwa kukadiria gharama ya usafiri wa ndugu mmoja wa mgonjwa ni kati ya shilingi 6,000/= na 10,000/= kwa siku, kulingana na mahali anapotokea bila kujumuisha gharama za kuandaa chakula cha mgonjwa ambacho mara nyingi ni chakula maalumu. 

"Na kama mgonjwa akilazwa zaidi ya siku tano hadi 10 ndugu mmoja wa mgonjwa gharama atalipia fedha nyingi kwenye usafiri” alisema Bw. Aligaesha

Aliongeza kuwa adha ya pili wanayopata ndugu ni usumbufu ambapo inabidi kuacha shughuli nyingine za uzalishaji ili kuja kuleta chakula mara tatu kwa siku, hivyo kuingiliana na shughuli zao za kiuchumi na kimandeleo na kushindwa kuzalisha. Hivyo jukumu hili linachukuliwa na Hospitali kuwaondolea adha hii.
 
“Pia kuna baadhi ya ndugu wamekuwa wakishindwa kuwaletea chakula wagonjwa wao hivyo hospitali ililazimika kuwapatia chakula ambacho kilikuwa kwa ajili ya wagonjwa wanaotoka mikoani wasio na ndugu hapa Dar Es Salaam” alisisitiza Bw. Aligaesha.

Alisema kumekuwepo na ongezeko la msongamano wa watu ndani ya Hospitali toka asubuhi saa 12 mpaka saa 12 jioni, suala linaloingiliana na utoaji huduma hasa saa za mchana kwani muda wa saa 6.00 hadi saa 8.00 mchana ulikuwa unaingiliana na majukumu ya kiutendaji ambapo majopo mbalimbali ya watalaamu yamekuwa yakiendelea na raundi za wagonjwa waliolazwa. Hii wakati mwingine imesababisha mgonjwa kutokupata huduma stahiki kutokana na muingiliano huu.
·                     
“Vile vile msongamano huu ni changamoto kwa ajili ya masuala ya kiusalama ambapo kati ya watu wanaoingia Hospitali kwa kigezo cha kuja kuona wagonjwa kuna wanaoingia kwa lengo la kufanya uhalifu ikiwemo wizi wa mali za Hospitali, magari  pamoja na vifaa vya magari” alisisitiza.
              
Alisema kwa kufanya hivyo, Hospitali itapunguza baadhi ya gharama za uagizaji wa vyakula kwa wazabuni, kulinda upotevu na baadhi ya vyakula kuharibika wakati mwingine kwani utunzaji wa vyakula una mahitaji makubwa.

Bw. Aligaesha alisema Hospitali inakusudia kutoa chakula chenye ubora na viwango vinavyotakiwa kwa wagonjwa ikiwemo kutoa chakula maalumu (special diet) kwa wagonjwa wenye uhitaji huo.

Utaratibu wa chakula cha mzabuni kwa wagonjwa
Kuhusu utaratibu huo Bw. Aligaesha alisema Mzabuni ndiye atakayepika chakula kwa wagonjwa wote waliolazwa na atatayarisha, atakipeleka na kukikabidhi katika wodi husika ambapo jukumu la kumpa mgonjwa kifungua kinywa, chakula cha mchana na jioni linabaki wa Hospitali.
 
Alisema wagonjwa watapatiwa milo mitatu kwa siku yaani asubuhi, mchana na jioni kazi itakayofanywa na muuguzi wa zamu ambaye atahakikisha wagonjwa wote wamepata chakula kufuatana na mahitaji (diet list) iliyowasilishwa jikoni kutokana na mahitaji yao ya kiafya.

Muda wa kuona wagonjwa
Kutokana na uamuzi huu, utaratibu wa ndugu kuleta chakula kwa wagonjwa waliolazwa wakati wa mchana umefutwa na hivyo mchana hatutakuwa na nafasi ya ndugu kuja kutembelea wagonjwa. M

uda wa kutembelea wagonjwa utakuwa asubuhi saa 12 hadi saa moja kamili na saa 10:00 jioni hadi saa 12:00jioni ndipo ndugu wataruhusiwa kuingia ndani kuwaona ndugu zao waliolazwa. Katika muda huo ndugu ataruhusiwa kuja na chakula chochote anachofikiri atamuongezea mgonjwa wake kama matunda n.k

Uchangiaji huduma ya chakula
Bw. Aligaesha alisema mgonjwa aliyelazwa atachangia kiasi cha shilingi 50,000 atakapolazwa ambapo kati ya hizo, shilingi elfu 10,000 itakuwa ni gharama ya kumuona daktari (Consultation), shilingi elfu 10,000 ikiwa ni gharama ya kulazwa na bei ya chakula itakuwa shilingi elfu 30,000 sawa na shilingi elfu 6,000 kwa siku. Wastani wa mgonjwa kukaa wodini ni siku tano. Gharama hizo zinahusika kwa muda wote atakaokuwa amelazwa.

Kwa sasa Hospitali inatoa chakula kwa wagonjwa 650 ambao wamepata rufaa kutoka hospitali za nje ya mkoa wa Dar es Salaam kwa gharama wastani wa shilingi 1.8 bilioni kwa mwaka, sawa na shilingi 150 milioni kwa mwezi kwa vyakula pamoja na  gharama nyingine kama vile za nishati.

Takribani wagonjwa kati ya 600 na 700 ambao rufaa zao ni kutoka Hospitali za Dar es Salaam walikuwa hawapati chakula kutoka Hospitalini, na ilibidi ndugu zao wawaletee chakula. Hata hivyo, Hospitali ilikuwa inawapatia chakula tu kama ndugu zao wakishindwa kufanya hivyo.

Hitimisho.
“Uongozi wa Hospitali unaamini kwamba mabadiliko haya hayatamuongezea mgonjwa gharama, bali yatampunguzia gharama pamoja na ile adha kama ilivyoainishwa hapo juu. Aidha, uongozi unaamini kwamba uamuzi huu unaendana na azma nzima ya kuboresha utoaji huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuboresha mazingira ya Hospitali. Tunaomba ushirikiano wenu katika kutekeleza jukumu hili ili kusudi wagonjwa waweze kuhudumiwa vizuri zaidi” alisisitiza Bw. Aligaesha.

Mtanzania Mwingine Akamatwa kwa Kumtukana Rais Kupitia "WhatsApp"

$
0
0
Mkazi wa Dar es Salaam, Leornad Kyaruzi amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu shtaka la kutoa lugha ya kumdhalilisha Rais John Magufuli.

Kyaruzi alifikishwa katika Mahakama hiyo na kusomewa shtaka linalomkabili mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Magreth Bankika.

Akisoma hati ya mashtaka, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Wankyo Simon alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Juni 2, mwaka huu katika jengo la Tanzania Tower lililopo Barabara ya Sam Nujoma.

Mwendesha mashtaka huyo alidai siku hiyo, mshtakiwa aliandika kupitia simu yake ya mkononi ujumbe wenye lugha ya kumdhalilisha Rais Magufuli na kisha kuusambaza kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp wakati akijua kuwa ni kinyume cha sheria.

Mshtakiwa alikana shtaka hilo na Hakimu Bankika alimtaka kuwa na mdhamimi mmoja kutoka taasisi inayotambuliwa kisheria ambaye atasaini dhamana ya Sh5 milioni na kufanikiwa kutimiza sharti hilo, hivyo kuachiwa kwa dhamana.

Awali, upande wa mashtaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakalika na kuiomba Mahakama kupanga tarehe nyingine. Hakimu Bankika aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 18, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Wakati huohuo, kitendo cha baadhi ya wadau kumchangia Issack Habakuki aliyepatikana na hatia ya kumtukana Rais Magufuli mkoani Arusha, kilitinga bungeni baada ya wabunge kuitaka Serikali kutoa maelezo ya kina iwapo hakimdhalilishi kiongozi huyo wa juu nchini.

Mwongozi huo uliombwa na Mbunge wa Chemba (CCM), Juma Nkamia akimtaka Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe atolee ufafanuzi jambo hilo.

Mahakama mkoani Arusha ilimtia hatiani kijana huyo mapema mwezi huu kwa kumtukana Rais katika ukurasa wake wa Facebook na kumhukumu kulipa faini ya Sh7 milioni au kwenda jela miaka mitatu na wiki iliyopita, wakazi wa Arusha walimchangia Sh4.5 milioni kukamilisha faini hiyo.

Waziri Dk Mwakyembe alisema suala hilo ni zito linalomgusa Rais na kuomba Naibu Spika Dk Tulia Ackson kumruhusu kwenda kufanya mashauriano na kumpa nafasi ya kuja kutoa msimamo wa Serikali katika mkutano huu unaomalizika Julai Mosi. 

Mhariri wa Gazeti la Dira na Mwandishi wake Wapandishwa Kortini

$
0
0
MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewapandisha kizimbani, mhariri na mwandishi wa gazeti la Dira ya Mtanzania, Musa Mkama na Prince Newton kwa kosa moja la kuandika habari za uongo zilizoleta mtafaruku kwa jamii.

Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu Respicius Mwijage, Wakili wa serikali, Timon Vitalis na Hellen Mushi, alidai mahakamani hapo kuwa, mnamo Juni 20 katika eneo la Biafra Kinondoni, Jijini Dar es Salaam washtakiwa hao waliandika na kuchapisha habari za uongo katika gazeti la ‘Dira ya Mtanzania’ toleo la 424 la tarehe 20 hadi 26 ambazo zilisababisha hofu na mshtuko kwa jamii kwa kutoa taarifa za uongo kuwa ’Kifaru cha kivita cha Jeshi la Wananchi(JWTZ), chaibwa.'

Alidai kuwa kitendo hicho ni kosa kisheria na ni kinyume na sheria ya magazeti.

Wakili Vitalis alidai kuwa, upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hata hivyo, washtakiwa hao walikana shtaka hilo na Hakimu Mwijage aliwataka kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja atasaini bondi ya Sh milioni 5.

Washtakiwa hao walikidhi masharti ya dhamana na Hakimu Mwijage aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 5 mwaka huu itakapotajwa tena.

Hata hivyo, chapisho hilo hilo katika ukurasa wa mbele na wa pili lilichapa kwa maandishi makubwa meusi na mekundu taarifa iliyosema: ‘Mwakyembe atuhumiwa kutapeli Bil.2.’ ambayo yalimuudhi Harrison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na Sheria.

Mwakyembe aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wanahabari Mjini Dodoma na kudai kuwa, chombo hicho kimekosa weledi na kimepotosha umma kutokana na chapisho hilo.

“Hii si mara yangu ya kwanza kutuhuma na baadhi  ya habari kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kisiasa, napenda nikiri mbele yenu kuwa sijawahi, kushuhudia upotoshaji mkubwa na wa makusudi na uzushi uliopitiliza na chuki binafsi iliyo bayana kama ambavyo gazeti hili limefanya,” alisema Dk. Mwakyembe na kuongeza;

“Nina taarifa kuwa, wameuza sana magazeti; naambiwa print order (idadi ya nakala) yao imeongezeka na kwamba taarifa yao imesambaa kwenye mitandao ya jamii, hivyo dunia nzima inajua mimi nina tuhuma za wizi, za utapeli.”

Pia alisema, gazeti hilo lililendelea kuandika tena Juni 20 wiki hii kwa kuuthibitishia ulimwengu kuwa, “Dk. Mwakyembe ni tapeli na ushahidi wao mkubwa wametaja barua iliyowahi kuandikwa na Kampuni ya Power Pool mwaka 2010 na mimi kutumiwa nakala kwa mtandao (e-mail) wanayodai ni yangu. Kwa busara za gazeti hili, huo ni ushahidi tosha kuwa mimi ni tapeli.

“Gazeti hilo halina staha na miiko ya uandishi wa habari, kikosi chetu cha jeshi huko Kisarawe kilielezewa kama kikundi cha wahuni hivi kinachopiga wananchi hovyo hovyo, kinapiga risasi za moto hovyo hovyo hadi kumpiga mwananchi moja kiunoni.”

Wakati huo huo alitoa tahadhari kwa televisheni kutosoma magazeti yenye taarifa tata akitoa mfano wa habari zilizoandikwa na gazeti la Dira kwamba, kifari cha jeshi kimeibwa.

“Tutafungua kesi hii Mahakama Kuu ya Tanzania, tutawapa taarifa kila tunavyoendelea. Bado tunaangalia impact (athari) na kuhusika kwa vyombo vikubwa vya habari kama ITV na STAR TV kutangaza taarifa za magazeti tata bila uangalifu ili na wao tuwahusishe katika kesi hii,” alisema na kuongeza;

“Kesi hii, nina uhakika, itajenga msingi imara wa wajibu na uhuru wa vyombo vya habari Tanzania kwa muda mrefu ujao.”

Nape Nnauye Asimulia Alivyotishiwa Maisha Wakati wa Oparesheni ya Kuyavua Magamba Ndani ya Chama

$
0
0
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema wakati wa mchakato wa chama kurejesha imani kwa wananchi hali ilikuwa ngumu kwake hadi kufikia kutishiwa maisha na watu wasiojulikana.

Mbali ya watu hao kumpigia simu za vitisho nyakati za usiku, pia walikuwa wakimchafua kupitia mitandao ya kijamii lakini anamshukuru Mwenyezi Mungu alivuka salama na chama kimevuka salama.

“Tulipoanza kuzunguka kujenga chama nilitukanwa sana. Watu waliwekeza kunichafua. Watu hao niliokuwa nawanyooshea kidole hawakufurahishwa na hatua ile hivyo wakaweka mkakati wa kutaka kunifukuzisha ndani ya chama na ilifika hatua wakawa wananichafua katika mitandao ya kijamii.

"Nikaamua kujitoa huko mpaka leo hii nimeamua kujitoa katika mitandao na kubaki katika twitter pekee kwa kuwa unaweza kutambua mtumiaji,” alisema Nape.

Akizungumza  nyumbani kwake mkoani Dodoma, Nape ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi na ambaye aliteuliwa kwa mara ya kwanza kushika nafasi hiyo mwaka 2011 Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete alipounda sekretarieti mpya chini ya Katibu Mkuu, William Mukama alisema watu hao walifikia kudai yeye si mtoto wa Mzee Moses Nnauye.

Kamati Kuu chini ya Mukama ilipita mikoani na kaulimbiu ya kuvua gamba iliyoasisiwa na chama kwa lengo la kuwaondoa watuhumiwa ufisadi lakini iliondolewa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2012 ikaundwa mpya chini ya Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana.

Kukata vigogo 
Katibu huyo wa uenezi alisema changamoto kubwa waliyokutana nayo katika mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya CCM ilikuwa kukata majina ya waliokuwa viongozi wa Serikali ambao walijitokeza kugombea nafasi hiyo.

Nape alisema kumpata mgombea wa kupeperusha bendera ya chama hicho kongwe ilikuwa kazi nzito baada ya viongozi mbalimbali wa juu wa Serikali ya Awamu ya Nne kujitokeza wakiwamo, aliyekuwa Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal, Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda na aliyekuwa Jaji Mkuu Augustino Ramadhani.

Vigogo wengine waliowapa wakati mgumu CCM ni aliyekuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Tatu na Nne, Frederick Sumaye na Edward Lowassa, na mawaziri kadhaa lakini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu waliweza kutimiza wajibu wao.

“Kuwaondoa viongozi waliokuwa madarakani ni sawa na kutafuna jongoo kwa meno lakini hatukutetereka na hatimaye tukapata majina matano ambayo nayo yalipigiwa kura na kupatikana jina la mgombea mmoja,” alisema.

“Ingawa vikao vilikuwa vya moto sana na kulazimika kukesha mpaka usiku, kila mmoja alipata nafasi ya kujadiliwa na kutendewa haki siyo kama ilivyovumishwa kuwa wagombea wengine hawakujadiliwa,” alisema.

Nape alisema katika chama chao kila mwanachama ana nafasi sawa hivyo haikuwasumbua kuangalia majina ya watu hao wala nyadhifa zao badala yake waliangalia sifa za mgombea mwenyewe ndani ya chama.

Alisema anashukuru Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Jakaya Kikwete kwa kuwa na kifua cha kuhimili vishindo na hiyo ndiyo siri ya kufanikisha mchakato huo kwa kuwa ni mtoto wa CCM hivyo ilikuwa rahisi kumkata yeyote kwani uzoefu wake ndani ya chama ulisaidia.

Nape alisema itachukua muda mrefu kupata kiongozi kama yeye lakini pia hawawezi kupuuza kazi iliyofanywa na Katibu Mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana na wazee waliorekebisha mambo na kuvuka salama kwa kuwa hali ilikuwa mbaya. 

Bunge laivu 
Nape alisema suala la kuzuia kurushwa moja kwa moja kwa matangazo ya Bunge si lake na kwamba lilipitishwa na wabunge wenyewe. 

“Mimi ni msimamizi wa Serikali. Watu wanapotosha, nilichofanya ni kulinusuru Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), kwa miaka 10 mfululizo Bunge lilishindwa kuwalipa fedha zao ambazo ni Sh4.5 bilioni kila mwaka.

“Hili liwe fundisho kwa wabunge, kuna vitu wabunge wanapitisha hawavijui baada ya muda wanaona madhara yake wanaanza kulalamika kumbe walivipitisha wenyewe...Suala la Bunge kuanzisha kituo cha televisheni pia walilipitisha wenyewe, leo hii Katibu wa Bunge anavyotumia fedha kama ingekuwa haipo katika bajeti wasingemwacha,” alisema.

Askofu Gwajima Kusakwa na Interpol Popote Alipo

$
0
0

Siku moja baada ya wakili wa Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, Peter Kibatala kuwaandikia barua Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Simon Sirro amesema hawafanyi kazi kwa kufuata barua ya askofu huyo. 

Sirro alithibitisha kupata barua hiyo, lakini akasema kuwa wanaendelea kumtafuta popote pale alipo na wakifahamu watamtia nguvuni.

Sakata la kutafutwa kwa kiongozi huyo linazidi kushika kasi kutokana na sintofahamu ya kubaini alipo, ikiwamo kambi ya muda wa saa saba iliyowekwa na polisi nyumbani kwa Gwajima, ambayo haikuwa na mafanikio wiki iliyopita.

Baada ya sintofahamu ya wiki nzima huku kukiwa na uvumi kuwa yupo nje ya nchi na wengine wakidai yupo nchini, juzi wakili Kibatala aliwasilisha barua Polisi akidai mteja wake yupo nje ya nchi na aliposafiri hakuwa anajua kama anatafutwa na polisi.

Katika barua hiyo Kibatala alisema ameelekezwa na mteja wake kufikisha ujumbe huo na akirejea atajisalimisha polisi kuitikia wito huo.

Jana Kibatala alisisitiza kuwa:“Kwa sasa yupo nje ya nchi akihubiri injili, alisafiri kabla ya kupata taarifa kuwa anatafutwa na polisi ana mashauri katika Mahakama ya Kisutu Julai Mosi, hivyo kabla ya hapo atakuwa amesharejea.”

Lakini Sirro alisema barua hiyo ni kujitetea ambako hakuna maana na wanachofanya wao ni kuendelea kumtafuta badala ya kusubiri ajisalimishe kama ulivyoandikwa waraka huo.

“Suala la kutupa taarifa za kujifanya alikuwa hafahamu kama anatafutwa si kweli, tukifahamu mahali alipo hata sasa hivi tunakwenda kumkamata, hatufanyi kazi kwa kufuata maelekezo yake,” alisema Kamanda Sirro.

Sirro alifafanua kuwa bado wanafuatilia kubaini kama yupo nchini au nje ya nchi, wakitambua ni nje nchi atakamatwa huko huko kwa msaada wa Interpol.

“Hatujafahamu alipo hata huko nje Interpol wapo kuwashughulikia watu kama hawa wanaofanya ukorofi nchini na kukimbilia nje ya nchi wakidhani wanatatua tatizo, kumbe wanaliahirisha,” alisema Sirro.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images