Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeto ya Leo Jumapili ya June 19


Lowassa Atoboa Siri Ya Ujio wa TB Joshua Nchini.....Asema Aliitwa na CCM Kumshawishi Akubali Matokeo ya Uchaguzi Mkuu

$
0
0

Aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa amesema hakuridhika na matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25, na kwa kulijua hilo, ‘watawala’ walimleta rafiki yake kutoka Nigeria, TB Joshua ili amshawishi akubali matokeo. 

Lowassa alisema baada ya TB Joshua, muhubiri na kiongozi wa Synagogie Church of All Nations, kukaa naye pamoja na viongozi wengine wa Chadema na kumueleza jinsi ‘walivyoporwa’ ushindi, kiongozi huyo wa kidini alichukia na kusitisha azma yake ya kuhudhuria sherehe za kumuapisha Rais John Magufuli.

TB Joshua aliwasili nchini Novemba 3, siku mbili kabla ya kuapishwa kwa Magufuli kuwa Rais, na alienda Ikulu na baadaye nyumbani kwa Lowassa ambaye alitumia muda mwingi wa ziara yake pamoja naye. 

“Walimuita rafiki yangu TB Joshua, wakaenda wakampokea. Alipokelewa na Rais Magufuli, akapelekwa Ikulu akazungumza na Kikwete,” alisema Lowassa. 

“Baadaye akawaambia wamlete kwangu. Kweli akaja nyumbani kwangu, tukazungumza naye. Sitaki kusema mengi sana niliyomwambia, lakini moja, nilimwambia ukikubali yale matokeo ndugu yangu, heshima yako itashuka hapa nchini na duniani kwa ujumla,” alisema. 

Lowassa alisema hayo jana alipokuwa akizungumza katika mahafali ya Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Wafuasi wa Chadema (Chaso) katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. 

Alisema ni kutokana na msimamo na mazungumzo waliyofanya na TB Joshua ndio yaliyosababisha kiongozi huyo wa kidini maarufu barani Afrika kutohudhuria sherehe hizo za kuapishwa zilizofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Katika hotuba yake, Lowassa alimpongeza Rais Magufuli kwa jitihada anazozichukua za kujaribu kufufua uchumi wa nchi, lakini akasema hakubaliani na mbinu anazotumia. 

Alisema anafurahia kumsikia Rais Magufuli akiihubiri nchi ya viwanda, lakini hana imani na lugha anazotumia.

“Rafiki zangu nawasikia na nafurahi sana wanasema wanataka kujenga nchi ya viwanda. Natamani nchi hiyo, lakini lugha hiyo sina imani nayo sana,” alisema. 

Alisema haziamini lugha hizo kwa kuwa ni vitu visivyowezekana kutokana na ukweli kuwa viwanda vilivyopo haviwezi kufufuka na kuondoa tatizo la ajira lililopo nchini. 

“Wanasema watafufua viwanda, lakini viwanda vilivyopo vili kuwa analojia sasa hivi mambo yote ni ‘digital’. Hicho kiwanda kitafufuliwaje maana hata madukani spea zake hazipo labda zitengenezwe upya,” alisema. 

Alisema tatizo lililopo kwa sasa nchini ni la ajira na kwamba hata kaulimbiu yao kwenye kampeni ilikuwa ajira kwa kutambua kuwa wapo vijana wengi waliomaliza vyuo, hawana ajira na kwamba eneo kubwa litakaloweza kuwaajiri ni sekta ya kilimo. 

Lowassa, ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chadema, alisema anakubaliana na kauli iliyotolewa na Jenerali Ulimwengu aliyoitoa hivi karibuni kuwa Rais Magufuli ameturudisha nyuma miaka 50, akiponda uamuzi wa Serikali kuzuia matangazo ya Bunge kurushwa moja kwa moja. 

“Uamuzi ule si mzuri na una matatizo makubwa kwa kuwa ni kuwanyima wananchi haki yao muhimu ya kuwasikiliza wawakilishi wao,” alisema.

Akizungumzia elimu, Lowassa alisema wakati Chadema na Ukawa waliposema watatoa elimu bure kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu walikuwa wamejipanga, lakini Serikali imebeba sera hiyo bila kujiandaa.

Aliwapongeza vijana kwa kuwa kiini cha mabadiliko na kusema mpaka sasa akikutana na watoto wadogo wanamsalimia kwa kumwambia “Mabadiliko Lowassa”. 

Alisema vijana walifanya kampeni nzuri na kumwezesha kupata kura nyingi zilizowapa ushindi, lakini wakanyimwa ushindi. 

“Tulishinda vizuri sana lakini hata hizo walizotupa, zinatosha kuwaambia kuwa tuliwapa kazi ya kutosha. Nyie mnajua, wao wanajua na mimi najua,” alisema. 

Lubuva aondolewe 
Alisema licha ya kumuheshimu mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva, anapaswa kutimuliwa kwa kushindwa kuisimamia vyema tume hiyo. 

“Tume ya Uchaguzi inapaswa iondoke. It must go na ndio maana nasema iko haja ya kuanza upya kudai Katiba mpya haraka iwezekanavyo,” alisema Lowassa. 

“Kama yupo mtu yeyote anayechukia matokeo ya uchaguzi uliopita, suluhisho lake ni kuwa na tume huru ya Uchaguzi itakayotokana na Katiba mpya. Tusipohangaika na Katiba mpya tutarudi palepale.”

Alirudia kauli yake kuwa baada ya uchaguzi kulikuwa na waliomtaka atangaze “kuingia barabarani”, lakini aliwakatalia. 

“Tutakuwa tunakwenda Ikulu kwa kufagia barabarani kwa damu za watu. No, tutakwenda Ikulu bila damu za watu wakati wowote na Mungu atatusaidia. Nawaambia wale wote ambao hawakuridhika, mnajua nguvu ya umma lakini msiitumie kuwaumiza watu,” alisema. 

Aliwataka viongozi wote wa Chadema kujali maslahi ya wanyonge kwa kuepuka kufanya kazi kwa mazoea. 

Meya wa Jiji la Dar es Salaam ambaye ni diwani wa Chadema, Charles Mwita aliwataka wanafunzi kufanya kazi ya kukijenga chama kwani mabadiliko ya kweli yataletwa na vijana. 

Muasisi wa Chaso, Pamela Maasaio aliwataka vijana wa Chadema kuachana na siasa za kwenye mitandao na badala yake waende mitaani kupiga kelele na kuweka mikakati ya pamoja.

Katibu Mkuu wa Chadema Akwea Pipa Kujinoa Kisiasa Ujerumani

$
0
0

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji anatarajia kuhudhuria kongamano la kujadili sauti za wananchi kupitia Bunge katika maendeleo na Taifa litakalofanyika Ujerumani, Juni 20 hadi 25.

Msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene alisema jana kuwa, kongamano hilo litajadili mikakati ya kampeni na kushinda uchaguzi, hususan kwenye mazingira yenye changamoto mbalimbali za kisiasa huku pia wakijifunza umuhimu na nafasi ya Serikali za mitaa katika maendeleo ya wananchi.

“Katibu Mkuu Dk Mashinji pamoja na washiriki wengine watajadili kwa kina na kubadilishana uzoefu wa ushindani wa siasa kutoka maeneo mbalimbali, huku pia wakijifunza umuhimu wa kutumia teknolojia ya mawasiliano kupambana na changamoto za kisiasa, hasa katika nchi zinazoendelea,” alisema Makene.

Mada nyingine katika kongamano hilo zitahusu mawasiliano kati ya Serikali na wananchi, kuwasaidia vijana kutambua umuhimu wa siasa na kushiriki.

Mbali na Dk Mashinji washiriki wengine watatoka nchi za Ufaransa, India, Ujerumani, Ghana, Ufilipino, Mexico, Mongolia, Argentina, Ukraine, Poland, Bolivia, Cambodia, Syria, Tunisia, Uganda, Kurdistan, Venezuela, Hoduras na Ugiriki.

Makamu Wa Rais Asisitiza Kushirikisha Wanaume Katika Ajenda Ya Mtoto Wa Kike

$
0
0

Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameyataka Mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini (NGOs) yanayoshughulikia masuala ya wanawake na watoto kujenga utamaduni wa kushirikisha wanaume katika kampeni za kumwinua mtoto wa kike kwa lengo la kuleta mabadiliko yanayokusudiwa.

Mheshimiwa Samia ametoa kauli hiyo jana kwenye hafla ya uzinduzi wa Binti club iliyofanyika sambamba na harambee ya fadhili mtoto asome ya kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto 500 wa wilaya ya Kinondoni iliyoandaliwa na Shirika lisislo la Kiserikali la Binti Foundation katika ukumbi wa PSPF jijini Dar es salaam 

Alisema wanaume kama wakala wa mabadiliko wanapaswa kushirikishwa na wajue ajenda ili wawe mabalozi wazuri katika kuzungumzia umuhimu wa kumwinua mtoto wa kike kielimu, kiafya na kwenye masuala ya ujasiriamali.

"Tuwaingize wanaume kama wakala wa mabadiliko, tuwashirikishe, wajue ajenda zetu katika mapambano hayo. wanaume wanashikilia sehemu nyingi, watumie nafasi hizo tulete mabadiliko," alisema Makamu wa Rais na kuongeza "Penye mkusanyiko wa watu 100, ukiingiza wanaume 20, na wakajua madhumuni ya mkusanyiko wetu, wataenda kushawishi wenzao 20,000 huko nje."

Aliipongeza Taasisi hiyo ya Binti Foundation kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika suala la elimu kwani safari ya mtoto wa kike ya kupata elimu inakuwa na ugumu zaidi kuliko wanaume kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za mila potofu, hali ya uchumi katika familia na jinsi jamii inavyomwangalia kutokana na ujanajike wake. 

"Tuna kazi kubwa ya kumtayarisha mtoto wa kike aweze kupambana na changamoto zinazomzunguka," alidokeza.

Mheshimiwa Samia alitumia fursa hiyo kuelezea hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali katika kukabiliana na changamoto za elimu ikiwa ni pamoja na kuondoa ada katika shule za msingi na sekondari, kuboresha ajira za walimu pamoja na maslahi yao, kujenga mabweni kwa wasichana na kuondoa tatizo la madawati ambapo amewashukuru Watanzania kwa kuchangia madawati.

Aliwataka wazazi kuwatunza watoto wao kwani ni zawadi kutoka kwa Mungu na kuhakikisha wanapata elimu zote ya dini na ya dunia ili kuwajenga kimaadili waweze kuwa raia wema. Mtendaji Mkuu wa Binti Foundation Johari Sadik alimweleza Makamu wa Rais kuwa shirika hilo liliamua kuunga mkono jitihada za serikali ili kuwawezesha watoto kumudu masomo yao na hatimaye kufikia malengo yao.

"Kwa hiyo ukiwa na fedha taslimu, ama vifaa kama vile kalamu, madaftari, pedi, vyote tunapokea kwa ajili ya kusaidia watoto ambao malengo yao yanaweza yasitimie kutokana na changamoto hizo," Kampeni hiyo ya fadhili mtoto asome imeanzia kwa watoto 500 wanaoishi kwenye mazingira magumu wa shule za msingi Mwananyamala, Hananasif, Kumbukumbu na Msasani zilizoko katika wilaya ya Kinondoni, mkoa wa Dar es salaam.

Katika hafla hiyo iliyopambwa na onesho la mavazi la watoto Makamu wa Rais ambaye alikubali kuwa mlezi wa Binti Foundation aliahidi kusomesha watoto 100 wakati mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa alitoa ahadi pia ya kusomesha watoto 50.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
19/6/2016

Kubenea Ahojiwa na Kamati ya Bunge, Maadili na Madaraka

$
0
0

Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea ameongozana na mawakili wawili akiwamo Mbunge wa Simanjiro, James Ole Milya (Chadema) kwenda kuhojiwa kwenye Kamati ya Bunge, Maadili na Madaraka inayoongozwa na George Mkuchika. 

Kubenea alihojiwa kwa zaidi ya saa moja kwa tuhuma za kulihusisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Waziri wake, Dk Hussein Mwinyi kwenye ugawaji wa ardhi kwa Kampuni ya Henan Guiji Industry.

Mbunge huyo alifikishwa mbele ya kamati hiyo Alhamis iliyopita ili kujibu mashtaka hayo baada ya Dk Mwinyi kulalamika wakati akihitimisha hoja ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/17.

Dk Mwinyi aliliambia Bunge wakati akihitimisha bajeti ya wizara hiyo kuwa yuko tayari kujiuzulu uwaziri iwapo Kubenea atathibitisha tuhuma hizo mbele ya Bunge.

Kufuatia ombi hilo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alimwagiza Kubenea kupeleka uthibitisho katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili ukachunguzwe.

“Waheshimiwa wabunge pamoja na ombi hilo la mheshimiwa waziri, lakini pia ameleta malalamiko rasmi kwa Spika akiomba tuhuma zilizoelekezwa kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na dhidi yake binafsi zifanyiwe uchunguzi na kumtaka mheshimiwa Kubenea athibitishe na kama atashindwa achukuliwe hatua stahiki,” alisema Dk Tulia.

Awali, wakati akichangia bajeti hiyo, mbunge huyo alisema kampuni hiyo ambayo inataka kuingia mkataba na JWTZ, inajifunga mkataba mwingine na Dk Mwinyi na huenda ukawa umesainiwa na au haujasainiwa.

Hata hivyo, Kubenea na wabunge wengine wa kambi ya upinzani wamesusia vikao vya Bunge vinavyoendeshwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kwa madai kuwa hawatendei haki.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu Ya June 20

Mahafali Mengine ya CHADEMA Yatawanywa na Jeshi la Polisi

$
0
0

Jeshi la Polisi mkoa Kilimanjaro jana liliwatawanya wahitimu wa vyuo vikuu kupitia umoja wa Chadema (Chaso), waliokuwa wamekusanyika mjini Moshi kwa ajili ya mahafali yao.

Dalili za ‘kibano’ hicho zilianza kuonekana asubuhi wakati polisi na askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakiwa wamejihami kwa mabomu ya machozi, walipozingira hoteli ya Keys inayomilikiwa na Philemon Ndesamburo. 

Hoteli hiyo iliyopo maeneo ya Kwa Alfonsi nje kidogo ya mji wa Moshi, ndipo ambako mahafali hayo ambayo yalikuwa yahusishe wahitimu 70 kutoka vyuo vikuu vinne yalikuwa yafanyike.

Wanafunzi hao ni kutoka Chuo Kikuu cha Mwenge (Mwekau), Chuo cha Kikuu cha Ushirika Moshi (Mocu), Chuo Kikuu cha Masoka na Chuo Kikuu cha Tiba KCMC (KCMU Co).

Hata hivyo, polisi wakiwa na magari yaliyokuwa yakipeperusha bendera nyekundu, walivamia hoteli hiyo na kuwataka wahitimu hao kutawanyika kwa amani, kwa vile mikusanyiko ya aina hiyo imezuiwa.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chadema (Bavicha) mkoani Kilimanjaro, Dickson Kibona alilaani tukio hilo akisema hakukuwa na sababu yoyote ya kuzuia mahafali hayo. 

“Wamezuia bila sababu yoyote na hii inakiuka misingi ya kidemokrasia, Katiba ya nchi na sheria ya vyama vya siasa,” adai Kibona.

Kibona alidai kama isingekuwa kuhofia maslahi ya kibiashara ya Hoteli ya Keys ambapo kulikuwapo pia watalii, wangegoma kuondoka kwa kuwa hawakuvunja sheria yoyote ya nchi. 

Mmiliki wa hoteli hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa Kilimanjaro, Philemon Ndesamburo, alisema ndiye aliyewashauri vijana hao kutawanyika kwa amani na kuwataka wasibishane na polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema polisi walipata taarifa kuwa wahitimu hao wangekuwa na mkutano wa kisiasa ambao ulijificha kwa mwavuli wa mahafali.

“Tumewaita viongozi wao na kuwaeleza kuwa mikutano yote ya kisiasa imezuiwa na watawanyike. Walituelewa na wakatawanyika, lakini sisi bado tunaendelea kuimarisha doria mitaani,” alisema.

Hili ni tukio la pili kwa wanachama wa Chaso kutawanywa na Polisi ambapo juzi katika hoteli ya African Dream mjini Dodoma, wahitimu wa vyuo vikuu mjini Dodoma nao walitawanywa na FFU.

Mkuu wa Idara ya Habari wa Chadema, Tumaini Makene alisema Chadema inaendelea kuhifadhi kumbukumbu za matukio yote yanayoendelea nchini, ili kujenga ushahidi utakaojitosheleza pindi itakapoonekana ni mwafaka kuchukua hatua zaidi.

Alifafanua kuwa chama hicho kinatambua hila zinazofanywa na Serikali kwa kulitumia Jeshi la Polisi, na kuwa wanatambua amri zinazotolewa na watendaji wa chama tawala kupitia wakuu wa mikoa na wilaya.

Alisema wanao ushahidi wa matukio yote utakaotumika muda wowote, watakapoamua kuishtaki Serikali ndani au nje ya nchi.

Mabasi ya haraka kuanza kutumia kadi za kulipia Leo.......... Gharama za kuipata zipo hapa

$
0
0

MRADI wa Mabasi Yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam (UDART) imeanzisha huduma kwa wateja wao za kutumia kadi maalumu wakati wa kupanda mabasi hayo itakayoanza rasmi leo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana asubuhi, Mkurugenzi Mtendaji wa UDART,  David Mgwasa alisema wameanza kutoa huduma hiyo ya kadi ili kuwarahisishia wateja wao na kuondoa changamoto ya kusubiri tiketi kwa muda mrefu kabla ya kuondoka.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart  katika matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu alisema kwamba kwa kuanzia wametoa kadi 200,000 ambapo kila kadi itauzwa kwa shilingi 5000 ingawa bei halisi kwa kadi moja ni shilingi 500 na sh.4500 inayobaki itakuwa ni malipo ya mteja wao.

"Shilingi 4500 zitatumika kama malipo ya nauli kwa siku saba hadi nane kwa kwenda eneo lolote na kuwa kadi hizo zitapatikana katika vituo vya Kimara, Mbezi, Morocco, Gerezani, Posta na kuwa zitakuwa ni endelevu" alisema Rajabu.
 
Aliongeza kuwa katika nchi nyingi zimekuwa zikitumia kadi hizo katika kusafirisha abiria na kuwa kwa hapa nchini ni huduma mpya ambayo itakuwa na changamoto zake kabla ya kuzoeleka.
 
Alisema licha ya kuanzisha huduma ya kadi bado ile ya risiti itaendelea kama kawaida ambapo alisema namna ya kujiunga na huduma hiyo unatakiwa kupiga *152*22#.

Kubenea Amshitaki Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson

$
0
0

Wakati Kamati ya Haki, Maadili na Madara ya Bunge imepokea mashtaka dhidi ya Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson, mbunge mwingine wa upinzani ameamua kumshtaki kiongozi huyo kwenye Kamati ya Kanuni ya Bunge.

Mbunge wa kwanza kumshtaki Dk Tulia, alikuwa Mbunge wa Simanjiro (Chadema), James ole Millya aliyewasilisha kusudio lake kwa Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai mashtaka sita na tayari yamewasilishwa kwenye kamati husika.

Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea alitangaza jana uamuzi wake wa kumshtaki Dk Tulia, ambaye ndiye anayeliongoza Bunge kwa sasa.

Dk Tulia atakuwa na kesi mbili, Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka na kwenye Kamati ya Kanuni.

Dk Tulia anakuwa Naibu Spika wa kwanza tangu kuanza Bunge linalojumuisha wabunge wa upinzani, kushtakiwa kwa madai ya kukiuka kanuni na taratibu za Bunge.

Kubenea alisema ameamua kumshtaki Dk Tulia katika kamati hiyo akidai kuwa alivunja kanuni na taratibu wakati akiwasilisha malalamiko ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwa mbunge huyo alisema uongo bungeni.

Akizungumza na wanahabari, mbunge huyo alisema hakuridhishwa na hatua ya Dk Tulia aliyoifanya Mei 13 na kwamba tayari alishawasilisha barua yake yenye hoja tano za mapungufu ya kikanuni kwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah tangu Ijumaa iliyopita.

Kubenea alieleza kuwa Dk Tulia alitumia kanuni ya 71 kupokea malalamiko ya Dk Mwinyi kinyume na utaratibu kwa kuwa kanuni hiyo huruhusu watu wasio wabunge kupeleka malalamiko yao kwa Spika, iwapo masuala yaliyojadiliwa bungeni yamewaathiri.

Alisema wakati akichangia hoja ya wizara hiyo Mei 10, alimtaka Dk Mwinyi aeleze juu ya kuwapo kwa mkataba baina ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Kampuni ya Heinan Guoji Industry & Investment Limited na kama upo haoni kama kuna mgongano wa masilahi kutokana na kushiriki kumjengea nyumba yake.

Hata hivyo, alidai hakuna mbunge aliyesimama kudai hoja hiyo ilikuwa ya uongo kama kanuni ya 63(3) inavyotaka, badala yake siku tatu baadaye alitakiwa kufuta bungeni jambo ambalo anaona Dk Tulia hakumtendea haki.

“Naibu Spika wakati akitoa mwongozo wa Spika alinukuu sehemu tu ya maelezo yangu jambo lilipotosha misingi na mantiki ya mchango wangu bungeni hivyo kuashiria alikuwa na nia mbaya dhidi yangu,” alisema Kubenea na kuongeza: “Hata nilipoomba kufanya hivyo siku aliposoma mwongozo na kunipa nafasi ya kufuta maneno yangu au kuyathibitisha, alikataa na endapo angezingatia mchango wangu wote angetenda haki.”

Katika barua hiyo, Kubenea amelalamika kuwa wakati Dk Tulia anapokea malalamiko kutoka kwa Dk Mwinyi hakumpelekea nakala ili kurahisisha utetezi wake.

Pia, alieleza kuwa Naibu Spika aliamua kimakosa kuwasilisha tuhuma dhidi yake kwenye kamati hiyo bila kuzingatia maelezo aliyowasilisha kwake na vielelezo huku akijua Waziri huyo wa ulinzi alikiuka kanuni ya 63 (3) na 64(2).

Kubenea alisema anaiomba Kamati ya Kanuni yenye nguvu kuliko Spika kusimamisha mchakato unaoendelea kufanywa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge juu ya suala lake hadi pale itakapofanya uamuzi iwapo ilifuata kanuni ama la.

Katika barua hiyo, Kubenea anamuomba Dk Kashililah amjulishe Spika ili aweze kuitisha kikao cha Kamati ya Kanuni kwa mujibu wa kanuni ya 5(5) ili kuona kama kulikuwa na uhalali wa shauri lake na anaamini Katibu huyo wa Bunge atamtendea haki.

Kubenea alishahojiwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Alhamisi iliyopita na kueleza kuwa alikubali kufanya hivyo kwa kuwa kamati hiyo ina nguvu kubwa ya kikanuni ikiwamo kukamatwa.

Kubenea alisema hana wasiwasi na aliyoyasema ila anataka haki itendeke kwa kufuata kanuni na hadi sasa ana vielelezo vya kutosha kuhusu suala lake.

Dk Kashililah alieleza jana kuwa hawezi kuzungumzia kwa kina jambo hilo kwa kuwa taratibu zote za kufuata zinafahamika.

 “Inawezekana ameandika, lakini mpaka ifike tuipokee. Mimi nilikuwepo Ijumaa hadi saa tano usiku sikuiona. Huenda ipo njiani ikifika tutaipokea na tutaifanyia kazi,” alisema Kashililah.

Serikali Yasitisha Ajira Zote Kwa Muda

$
0
0

SERIKALI imesitisha ajira zote, kama njia ya kukabiliana na wimbi la watumishi hewa.

Kutokana na uamuzi huo hivi sasa hakuna nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa Serikali na wakala zake pamoja na utoaji wa vibali wa likizo ya bila malipo.

Katibu Mkuu Utumishi, Dk. Laurean Ndumbaro,  jana alisema kuwa Serikali imesitisha kwa muda utoaji wa ajira, ili kupitia upya muundo wa Serikali na taasisi zake.

Alisema utekelezaji wa mkakati huo utakwenda sambamba na kusitisha kwa muda utoaji wa vibali vya ajira zote mbadala pamoja na uidhinishaji wa ajira hizo zilizopo Sekreterieti ya Ajira katika utumishi wa umma na kwenye mfumo wa taarifa za kiutumishi.

“Ni kweli tumesitisha kwa muda ili kupitia mfumo wa Serikali na hata kuangalia ulipaji wa mishahara kama upo katika malipo stahiki.

“…na hili litakwenda sambamba na hata kusitishwa malipo ya mishahara yanayotokana na upandishwaji wa vyeo kwa watumishi. Tukimaliza zoezi hili ndipo tunaweza kuanza kutoa ajira za Serikali,” alisema Dk. Ndumbaro.

Alisema muundo mpya wa utumishi wa Serikali unakwenda sambamba na uhakiki wa malipo ya mishahara, hivyo ni lazima ujue ni nani unayemlipa kuliko ilivyo sasa.

Kwa mujibu wa maelekezo hayo uhamisho na uidhinishaji katika mfumo wa watumishi ambao wamehamishwa kutoka kwa mwajiri mmoja kwenda kwa mwajiri mwingine ambao atalipwa mshahara mkubwa kuliko ule wa sasa pia utaangaliwa kwa lengo la kupata taarifa sahihi za mtumishi husika.

“Baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki watumishi pamoja na tathmini ya muundo wa Serikali na taasisi zake, wote wataarifiwa ni lini utekelezaji utaendelea,” alisema.

Taarifa kutoka maeneo mbalimbali nchini, zinaarifu kuwa maelekezo hayo yalitolewa Juni 13, mwaka huu na kusambazwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwa makatibu wakuu wote, makatibu tawala wa mikoa, kwa wakuu wa idara za Serikali zinazojitegemea.

Waliotakiwa kutekeleza maelekeo hayo ya Serikali ni wakurugenzi wote wa majiji, manispaa na miji, wakurugenzi watendaji wa halmashauri za wilaya, watendaji wa taasisi za umma na watendaji wa wakala za Serikali kwa upande wa Tanzania Bara.

Kamatakamata
Wiki iliyopita vyombo vya dola vilianza kuwatia mbaroni watumishi hewa kwa kuwafuata na pingu majumbani.

Hatua hiyo imetajwa kuwa ni mkakati wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli, kuanza kupambana na watendaji ambao wamekuwa wakiisababishia hasara Serikali ya kulipa mamilioni ya shilingi kwa watumishi hewa.

Kutokana na uamuzi huo  ambapo mtumishi mmoja wa moja  za Mkoa wa Kigoma, alifuatwa na askari wa polisi na kutiwa mbaroni nyumbani kwao Ubungo Kibangu jijini Dar e Salaam.

Tukio hilo la aina yake lilitokea mchana wa juzi na kuibua hisia miongoni mwa majirani ambao waalisema kuwa, askari hao walifika nyumbani kwao na mtumishi huyo na kumfunga pingu mikono na miguuni na kuondoka naye.

Kutokana na hekaheka hiyo ya watumishi hewa, taarifa kutoka wilayani Nyasa mkoani Ruvuma, zilidai kuwa walimu watano wastaafu nao walikamatwa na polisi kwa madai ya kupokea mishara hewa.Mbali na walimu hao pia alikuwepo muuguzi mmoja.

Hivi karibuni akizungumza Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki, alisema Serikali imewaondoa jumla ya watumishi 12,246 kwenye mfumo wa malipo ya mishahara kwa sababu mbalimbali, ikiwemo umri wa kustaafu kwa lazima, kufukuzwa kazi, vifo na kumalizika kwa mikataba.

Waziri Kairuki alisema kuondolewa kwa watumishi hao kumeokoa Sh bilioni 25 ambazo zingelipwa kwa watumishi hao.

Alisema kuwa fedha hizo zingepotea endapo watumishi wasingeondolewa kwenye mfumo, ikilinganishwa na watumishi 10, 295 walioondolewa kwenye mfumo kuanzia Machi 15 hadi Aprili 30 mwaka huu.

Alisema pia kuwa watumishi hewa 1,951 wameongezeka ikiwa ni pamoja na Sh bilioni 1.8.

Alifafanua kuwa ofisi hiyo ilitoa maelekezo kwa Makatibu Wakuu, Wakuu wa taasisi za umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa, kuwasilisha taarifa ya watumishi hewa ifikapo Juni 10, mwaka huu. 

Chanzo: Mtanzania

Msaidizi wa Askofu Gwajima atoa Tamko

$
0
0

Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, jana walisali bila kuwapo kwa Askofu wao, Josephat Gwajima ambaye anatafutwa na Jeshi la Polisi. 

Mara nyingi Jumapili, Gwajima ndiye amekuwa akiongoza ibada katika kanisa hilo lililopo Ubungo Kibo, lakini jana iliongozwa na mchungaji Edward Adriano ambaye hata hivyo, hakueleza chochote kuhusu alipo askofu huyo.

Gwajima anatafutwa na polisi baada ya kusambaa kwa sauti inayosikika kama yake akitaka Rais mstaafu, Jakaya Kikwete afikishwe mahakamani kwa yote yaliyofanyika wakati wa utawala wake.

Jana, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema suala la Askofu Gwajima atalizungumza leo.

Alhamisi iliyopita Polisi walizingira nyumbani kwa Gwajima kwa saa saba, wakitaka kumkamata bila mafanikio.

Kamanda Sirro alisema wanamtafuta askofu huyo ili athibitishe kama maneno yenye uchochezi, yanayosambaa kwenye mitandao ni ya kwake.

Ulinzi kanisani 
Ulinzi katika kanisa hilo jana uliimarishwa na vijana waliovaa vizibao vya njano, vilivyoandikwa polisi jamii tii sheria bila shuruti. Idadi ya vijana hao wanaokadiriwa kufika 40, walikuwa wengi kuliko Jumapili nyingine zilizopita.

Licha ya kutokuwapo kwa askofu huyo kanisani hapo, waumini walijaa na wengine kukosa viti huku wengine wakionekana kusimama nje ya kanisa hilo.

Kauli ya  Msaidizi wa Gwajima
Msaidizi wa Askofu Gwajima, Yekonia Bihagaze, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, alisema juzi kuwa taratibu, sheria na kanuni zinapaswa kufuatwa kumkamata kiongozi wao.

"Kanisa la Ufufuo Na Uzima ni makini, tulivu na halikurupuki kwenye maamuzi yake. Na nchi haiongozwi mitandaoni, kama serikali inamtaka mtu ziko taratibu, sheria kanuni za kuzifuata," sehemu ya taarifa ya Mchungaji Bihagaze ilisomeka.

"Kwa sasa kila mmoja anaona nchi inapiga hatua kimaendeleo, ni vema wananchi sasa tukaachana na propaganda kama hizi, ni vema tukaweka shabaha yetu moja kushirikiana na Rais tulijenge taifa Letu. Taifa hili si mali ya mtu mmoja, ni mali yetu sote kwa manufaa yetu na vizazi vingine vitavyokuja.

"Adui wa Rais wetu awe adui yetu sote. Siasa zitakuja tu baadaye ila kwa sasa nchi itulie, watu tuchape kazi, tulipe kodi kwa sababu kuna Rais mwenye nia ya kuipeleka mbele.

"Hakuna duniani Taifa linaloweza kuendelea pasipo wananchi kushirikiana bega kwa bega na kiongozi wao."

Nape Asema Lowassa ni Alama ya Ufisadi, ampa ushauri mgumu

$
0
0

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amenena tena kuhusu uamuzi wa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kupewa nafasi ya kugombea urais.

Nape ameeleza kuwa uamuzi huo uliwasaidia kwa kiasi kikubwa kwani mwanasiasa huyo aliyekuwa na nguvu kubwa ndani ya chama hicho alikuwa alama ya ufisadi kutokana na kukabiliwa na tuhuma nyingi za ufisadi.

“Lowassa alikuwa alama ya ufisadi, alipoondoka aliturahisishia kazi. Watu walikuwa wanahusisha ufisadi na umasikini, walichoka na walikuwa radhi kuchagua hata jiwe lakini sio CCM,” alisema Nape.

Alisema kuwa angepata nafasi ya kumshauri Lowassa katika siasa, angemshauri ajiuzulu siasa kabla hajaondolewa kwa aibu katika medani za siasa.

Kadhalika, Nape alisema kuwa kosa kubwa ambalo lilifanywa na vyama vya upinzani ni kumpokea Lowassa ambaye amedai alikuwa amesababisha CCM kupakwa matope ya uchafu kutokana na kuwa na tuhuma nyingi.

Hata hivyo, Nape alimpongeza Lowassa kwa kukubali matokeo ya uchaguzi mkuu kwa kuwa uamuzi huo ulisaidia kuliweka Taifa katika hali ya amani baada ya uchaguzi.

Lowassa amekuwa akikanusha tuhuma zote zilizokuwa zikielekezwa kwake hususan tuhuma za kuhusika na sakata la Richmond lililosababisha ajiuzulu nafasi ya Uwaziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Nne.

Alijiunga na Chadema na kugombea nafasi ya urais akiungwa mkono na vyama vya siasa vinavyounda Ukawa.

Alipata kura takribani milioni 6 na kusaidia kupata wabunge wengi zaidi wa upinzani akiweka historia ya ushindani mkubwa zaidi kuwahi kutokea kwenye uchaguzi mkuu tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini.

Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Ukosefu Na Upungufu Wa Nguvu za Kiume

$
0
0

Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  

Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.

Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kufahamu   kuhusu   SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME  tafadhali  tembelea :

Ukisoma  vizuri  kuhusu  mfumo  wa  nguvu  za  kiume, utagundua  kuwa   Suala  la  nguvu  za  kiume  ni  suala  la  kimfumo.  Ili  mwanaume  awe na nguvu  za  kiume, aendelee  kuwa  na  nguvu  za  kiume na  azilinde  nguvu  zake za  kiume, ni  lazima  ogani  zote zinazo  husika  na  mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ziwe  na  afya  njema  na  ziwe  na  ushirikiano   thabiti  na  wenye  afya.

Vile  vile , utagundua  kuwa , mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ni  kama  ifuatavyo:

i.Mishipa  imara  ya  ubongo  na  yenye  afya  njema

ii. Mishipa  imara  ya  uti  wa  mgongo  (  spinal  cords )

iii.Mishipa  imara  itumikayo  kusafirisha  damu  mwilini  (  Blood Vessels )

iv. Mfumo  imara  wa  usafirishaji  damu  mwilini

v. Mishipa  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema

vi. Uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  ubongo, mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume.

Hivyo  basi, ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, na  aendelee  kuwa  na  nguvu  hizo ni  lazima  mambo  yote  muhimu  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume  yawe  imara  pasi na  hitilafu  yoyote.

Hitilafu  yoyote  katika  mambo  hayo, itasababisha  ukosefu na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume  kwa  mwanaume  huyo.  Pale inapotokea    hitilafu  ama  mapungufu  katika  ogani  zaidi  ya  moja  kati  ya  zilizo  tajwa hapo  juu, basi  tatizo  kwa  muhusika  huwa  kubwa  mara  dufu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU &  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Mwanaume   anapopatwa na  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, ubongo  hutoa  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo  husafirisha  taarifa  hadi  kwenye  mishipa &  misuli  ya  uume.

Mishipa  ya  uume inapopokea  taarifa  hiyo, hutanuka. Na  mishipa  ya  uume  inapotanuka, hufanya  mambo  mawili  muhimu  sana :

i.Husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  hivyo  kuruhusu  damu  kuingia kwa  kasi  sana   ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  imara  bara bara.

ii. Huibinya na  kuiziba  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuzuia  kunyonya  ama  kufyonza  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa ya  uume.  (  KAZI  KUBWA  YA  MISHIPA  YA  VENA  ILIYO  KARIBU NA  MISHIPA  YA  UUME  NI KUHAKIKISHA  HAKUNA  DAMU NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME. HIVYO  BASI  DAMU  INAPOINGIA  NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME, MISHIPA  YA  VENA  HU “SENSE” JAMBO  HILO  KWA  HARAKA  NA HIVYO  KUIFYONZA  DAMU  HIYO  KUTOKA KWENYE MISHIPA  YA UUME  YA  KUITOA  NJE YA MISHIPA  YA  UUME.  NA  DAMU INAPOKOSEKANA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME, HUUFANYA  UUME  KUSINYAA  NA  KULEGEA )

Mtu  anayepiga  punyeto  husababisha  mambo  yafuatayo  katika  mwili  wake :

1. Huuwa  nguvu  ya  mishipa  & misuli ya  uume ambayo  ndio  inayo husika  na  kusimama  kwa  uume

2. Mishipa  ya   uume  inapo  sinyaa  na  kukosa  nguvu  yake  ya  asili, husababisha  mambo  yafuatayo :

i.Huondoa  uwezo  wa  mishipa  &  misuli  ya  uume  kutanuka, na  hii  ndio  sababu  inayo  wafanya  waathirika  wa  punyeto  kutumia  nguvu  nyingi  sana  katika  kuufanya  uume  usimame.

ii.Huondoa  uwezo  wa  mishipa &  misuli  ya  uume  kuibana  na  kuiziba  mishipa  ya  vena, na  hii ndio  sababu  inayo  fanya  waathirika  wa  punyeto  kufika  kileleni  haraka  sana, kwani damu  inayo  ingia  kwenye misuli  ya  uume   hufyonzwa  ndani ya  muda  mfupi sana. 
 
 Hii  hutokea  kwa  sababu  mishipa na  misuli  ya  uume inakuwa  imelegea,na  mishipa  ya  vena inakuwa  imepwaya, hivyo  msuguano wowote ule  hufanya  mishipa  ya  vena  kufunguka  na  kufyonza  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  na hivyo  kuufanya  uume  kusinyaa  ndani ya dakika ama sekunde  chache sana.

3. Vile  vile  punyeto  hufanya  uume  kusinyaa na  kurudi ndani  na  kuufanya  uonekane kama  uume  wa  motto mdogo.

Kwa  ufupi  punyeto  husababisha  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuu  zifuatazo :

i.Kwanza   hudhoofisha  na  kuharibu  mishipa  ya  uume,  ambayo  ndio  hufanya  uume kusimama.

ii.Pili  hudhoofisha  utendaji  kazi  wa  mishipa  ya  ateri, ambayo  ndio  hutumika  kama  njia  ya  kusafirisha  damu kupeleka kwenye  misuli  ya  uume  na  ivyo  kuufanya  uume  usimame

iii. Tatu, punyeto  hupelekea  kuvuja  kwa  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kusababisha  damu  kufyonzwa  kwa  haraka  sana  kila  iingiapo ndani  ya  misuli ya  uume  na  matokeo  yake  ni  uume   kusimama  kwa  muda  mfupi  sana  wakati wa  tendo  la  ndoa.

iv. Punyeto  huathiri  mtiririko  wa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume, kwa  sababu  hudhoofisha  misuli &  mishipa  ya  uume  pamoja  na mishipa ya  ateri  ambayo  ndio  hutumika  katika  kusafirisha  damu kwenda  kwenye  uume

DALILI  ZA  MTU  ALIYE  ATHIRIWA  NA  PUNYETO
Dalili  kuu  za  mtu  aliye athiriwa  na  punyeto  ni  kama  ifuatavyo:

i.           Uume  kusinyaa  na  kuwa  kama  wa  mtoto
ii.         Uume kurudi  ndani
iii.       Uume  kusimama  ukiwa  legelege
iv.       Kufika  kileleni  haraka  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

TIBA   YA   NGUVU  ZA  KIUME  KWA MTU  ALIYE  ATHIRIKA  NA  PUNYETO.
Dawa   asilia  ya  nguvu  za  kiume iitwayo JIKO  ni tiba  bora  na  ya  uhakika  kabisa  kwa  mtu  aliye  athiriwa   na  punyeto.  Dawa  hii, pamoja  na  mambo  mengine  mengi, husaidia  kufanya  mambio  yafuatayo  katika  mwili  wa  mwanaume  aliye  athiriwa  na  punyeto :

i.Kuimarisha  mishipa  & misuli  ya  uume  ulio  legea na  hivyo  kuurejeshea  uwezo wake wa  asili

ii. Hutibu   tatizo  la  uume  kurudi  ndani

iii.Humaliza  tatizo  la  kusimama  kwa  uume  ukiwa  legelege

iv.Hutibu  na  kuponya  kabisa  tatizo  la  kufika  kieleleni  haraka.

BEI  YA  DAWA  :  Dawa  hii  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU (Tsh. 80,000/=)

MAHALI  INAPOPATIKANA :  Dawa  hii  inapatikana  katika  duka  la  dawa  asilia  liitwalo  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  UBUNGO   nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA   karibu  na SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING.

Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu. Watafikishiwa  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  DAR  ES  SALAAM.

Kwa   wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  MABASI

Kwa  wateja  waliopo   Zanzibar  wata fikishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa boti.

Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  ama  DHL.

MAWASILIANO :  WASILIANA  NASI   KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee kila  siku  kwenye  blogu  yetu :

Basi la NBS kutoka Dar Kwenda Tabora na Basi la Kisbo, Yamepata ajali Morogoro...Watu Watano Wafariki, 27 Wajeruhiwa

$
0
0

Basi la NBS linalotoka Dar es salaam  kwenda Tabora  limepata ajali mbaya maeneo ya Chakwale wilayani Gairo  mkoani Morogoro. 

Taarifa kutoka eneo la tukio zinaarifu kuwa watu 5 wamefariki na 27  wamejeruhiwa katika ajali hiyo.

Breaking News: Wabunge wa Upinzani Waziba Midomo yao Kwa Karatasi na Plasta na Kisha Kutoka Nje

$
0
0
Wabunge wa Vyama vya Upinzani vinavyounda Ukawa, leo wametoka tena Bungeni kama walivyoazimia kukacha vikao vyote vinavyoongozwa na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, lakini wamekuwa na mtindo wa aina yake.

Tofauti na siku nyingine, leo wabunge hao wa upinzani wamejifunika midomo kwa plasta huku wakiwa wameandika jumbe mbalimbali za kuonesha kuminywa kwa haki ya kujieleza.

Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia aliwaambia waandishi wahabari nje ya ukumbi wa Bunge hilo kuwa wameamua kutoka nje ikiwa leo ni siku ya kuipigia kura bajeti ya Serikali kwani hawakushiriki kuijadili. Pia, alisema kuwa bajeti hiyo ni mbaya inayowaumiza wananchi.

“Ni fedha za watanzania wote walipa kodi tukiwemo sisi. Lakini democratic perspective inasema ‘hakuna kulipa kodi kama hakuna uwakilishi’. Sasa sisi tunawaambia Watanzania, tumejadili na bajeti hii ni mbaya… mbaya sana ya kuwaumiza Watanzania. Ni ya maumivu mabaya sana ya kuwaumiza Watanzania,” alisema Mbatia.

Alisema kwakuwa leo ni siku ya kupiga kura hawatashiriki kwa kuwa hawakushiriki kujadili bajeti hiyo bali wataenda kushtaki kwa wananchi.

Akizungumzia zuio la mikuano ya hadhara, Mbatia amesema kuwa mikutano hiyo itafanyika tu kwani haipangiwi na mtu mmoja bali ni kwa mujibu wa sheria na taratibu za kidemokrasia.
.

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ) - Sehemu ya Pili

$
0
0
Mtunzi: Enea Faidy

Ilipoishia sehemu ya kwanza ( kama hukuisoma bofya hapa)
.....Wakati wanafunzi wengine wakiwalilia wenzao Doreen alikuwa amejitenga peke yake nyuma ya bweni alilokuwa anakaa na kulikuwa na Giza totoro. Alikuwa uchi wa mnyama huku mikono yake ikiwa imeshikilia vitu fulani huku akitamka maneno ambayo aliyaelewa mwenyewe.... 

Sehemu ya pili
...DOREEN aliendelea kuongea maneno aliyoyajua mwenyewe akiwa bado yupo uchi wa mnyama nyuma ya bweni alilokuwa anaishi.

Ghafla kipande kidogo cha karatasi nyeupe kikashuka mikononi mwake bila kuonekana kilikotokea. Doreen alicheka kwa sauti Kali ya kutisha sana kisha akalikazia macho karatasi lile, matone ya damu yaliangukia kwenye karatasi lile kutoka kwenye macho yaliyotisha sana ya Doreen kwani yalikuwa na rangi nyeusi halafu yakawa na umbile kama macho ya paka.

"Nenda mpaka ofisi ya mkuu wa shule ukamalize kazi." alisema Doreen akiwa amelinyanyua karatasi like kwa mkono wake wa kushoto. Karatasi likatoweka mkononi mwake na kupepea kwa nguvu kama vile limerushwa na upepo mkali.

Doreen alipomaliza kazi hiyo akasimama vizuri kama mwanajeshi aliyejipanga kwaajili ya gwaride kisha akainamisha kichwa chake chini akapotea eneo lile.

JWTZ Yakanusha Taarifa za Kuibwa kwa Kifaru.....Lasema Taarifa hizo Hazina Ukweli Wowote

$
0
0

Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)  limekanusha taarifa za kuibiwa kwa kifaru  cha jeshi zilizoripotiwa leo na gazeti la Dira  na kusema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowowte huku  likisisitiza ulinzi katika maeneo ya jeshi uko imara.

Akiongea na  waandishi wa habari leo  kukanusha habari hizo, msemaji wa jeshi hilo, Kanali Ngemela Lubinga amesema jeshi limesikitishwa sana na habari hizo za upotoshaji kwa kuwa zinachafua taswira ya jeshi na taifa kwa ujumla.
 
Amelitaka Gazeti la Dira kuomba radhi mara moja na wakishindwa kufanya hivyo hatua Kali na za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao 

==>Zaidi, tazama video hii kumsikiliza

Majibu Ya Hoja Za Wabunge Yaliyotolewa Leo Bungeni Na Waziri Wa Fedha Na Mipango Dkt. Philip I. Mpango (Mb)

$
0
0



JUNI 20, 2016
DODOMA
A.          UTANGULIZI

1.          Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hii kukushukuru  wewe binafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwa kuendesha vizuri majadiliano kuhusu Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa 2015 na Mpango wa Maendeleo wa 2016/17 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2016/17, niliyowasilisha tarehe 8 Juni, 2016.

2.          Mheshimiwa Spika, Kipekee,  ninampongeza sana Mhe. Naibu Spika kwa umahiri na weledi wa hali ya juu alioonesha katika kusimamia Kanuni za Bunge wakati wote wa kikao hiki cha Bunge la bajeti. Hakika viwango vyake ni vya kimataifa. Japokuwa Mhe. Joseph Kakunda, mwanafunzi wangu Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam alichomekea sehemu fulani akidai kwamba mimi ni bahiri, (nadhani alimaanisha bahiri wa kutoa maksi za upendeleo!),  nataka niliambie Bunge lako tukufu kwamba kwa viwango ambavyo Mhe. Naibu Spika alivyoonesha humu ndani, hakika ningempa maksi za haki asilimia 100 kama walivyofanya maprofesa wake wa sheria UD na UCT. Hongera sana.

3.          Mheshimiwa Spika, napenda kutambua michango iliyotolewa na: Kamati ya Bajeti, chini ya M/kiti wake Mheshimiwa Hawa Abdulrahman Ghasia, Mbunge wa Mtwara Vijijini; Mheshimiwa David Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, Naibu Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Wizara ya Fedha na Mipango, na waheshimiwa Wabunge wote waliochangia kwa kuzungumza au kwa maandishi hapa Bungeni. Ninawashukuru wote.
4.          Mheshimiwa Spika, jumla ya Wabunge 158 wamechangia hoja niliyowasilisha. Kati ya hao, 133 wamechangia kwa kuzungumza na 25 kwa maandishi.

B:        HATUA ZILIZOPONGEZWA NA WABUNGE WENGI

5.          Mheshimiwa Spika, Hatua zilizopongezwa na Wabunge wengi wakati wa mjadala juu ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Bajeti ya Serikali 2016/17 ni pamoja na zifuatazo:

·        Kuthubutu kutenga asilimia 40 ya bajeti yote kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo, ikiwa pamoja na kuanza ujenzi wa reli mpya ya kati kwa kiwango cha standard gauge, barabara, umeme, ununuzi wa meli mpya ziwa Victoria na ndege tatu za abiria;
·        Kuongeza ukusanyaji wa kodi na mapato yasiyo ya kodi hadi kufikia wastani wa shilingi 1.2 trilioni kwa mwezi kwa kuziba mianya ya uvujaji wa mapato na kuimarisha matumizi ya vifaa vya kielektroniki (EFDs) katika ukusanyaji wa mapato, na Hazina kutoa fedha hizo kama ilivyopangwa;

·        Kusimamia nidhamu ya matumizi na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ikiwa pamoja na safari za nje, posho, sherehe, kuondoa watumishi hewa katika utumishi wa umma;

·        Kuhimiza azma ya kufanya kazi na kurejesha nidhamu ya watumishi kazini kwa ajili ya maendeleo ya Taifa;
·        Kuwapunguzia wafanyakazi mzigo wa PAYE na SDL kwa waajiri;

·        Kuanzisha mahakama ya kushughulikia mafisadi;

·        Kuweka kipaumbele katika kufufua na kujenga viwanda ili kupanua fursa za ajira na wigo wa kodi; na

·        Kujielekeza kutekeleza Ilani ya CCM 2015, ahadi za viongozi wakuu na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ili kutatua kero za wananchi, hasa masikini.

Bajeti Kuu Ya Serikali 2016/2017 Yapitishwa Bungeni Kwa Asilimia 100.......Serikali Yasema Kodi ya Kiinua Mgongo Itakatwa kwa Watumishi Wote Akiwemo Rais

$
0
0

Serikali ya Tanzania imepitisha bajeti ya shilingi trilion 29.5 kwa kupigiwa kura huku wabunge wa upinzani wakiwa wametoka nje wakiwa wameziba midomo yao kwa karatasi na plasta ikiwa ni ishara ya kuonesha kutoridhika na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson wakigomea vikao vya Bunge vinavyoongozwa na Naibu Spika huyo

Katika vikao vya Bunge la 11, wabunge wa vyama vya upinzani wamekuwa wakisusia vikao hivyo kwa takribani siku 23 sasa kwa madai ya kutokubaliana na ukandamizaji unaofanywa na Naibu Spika wa Bunge Dkt.Ackson Tulia.

Wakichangia bajeti hiyo, Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Mwijarubi Muhongo pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage wamesema bajeti hiyo inalenga kukuza uzalishaji.

Akijibu hoja mbalimbali za wabunge waliochangia katika Bajeti hiyo ikiwa ni pamoja na ya kuongeza fedha katika ofisi ya mkaguzi wa serikali CAG ili kutanua wigo wa ukaguzi pamoja na kuachana na mpango wa kuanza kuwakata kodi wabunge katika mafao ya kiinua mgongo ya Wabunge, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpango amesema msimamo wa serikali upo pale pale.

Kuhusiana na makato ya kodi kwenye mafao ya wabunge, Dkt Mpango amesema kuwa serikali imeamua kuwa itakata kodi hiyo kwa viongozi wote wa kisiasa wakiwemo wakuu wa wilaya, wakuu wa mkoa, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais pia, ili kuweka usawa katika makato ya kodi nchini.

Baadaye jioni wabunge walipiga kura mmoja mmoja kupitisha bajeti hiyo, ambapo wabunge wote 251 waliokuwemo bungeni walipitisha bajeti hiyo kwa kauli moja, ambapo kila mbunge alijibu "Ndiyo" akimaanisha anaipitisha bajeti hiyo.

Mapema Asubuhi mara baada ya dua, wabunge wa upinzani waliziba midomo yao kwa karatasi na Plasta na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge ikiwa ni ishara ya kuonesha kutoridhika na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson.

Mbunge wa Vunjo Kupitia chama cha NCCR Mageuzi, Mhe. James Mbatia kwa niaba ya wabunge hao alisema hawataacha kulalamikia ukiukwaji wa sheria unaofanywa na kiti cha Naibu Spika.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya June 21

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images