Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Lowassa Asaidia Watoto Yatima Dar es Salaam

0
0
Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amewataka Watanzania kujali makundi ya watu wenye mahitaji maalumu hususan katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

 Kauli hiyo aliitoa jana alipotembelea vituo vya watoto yatima jijini Dar es Salaam vinavyoendeshwa na Waislamu kwa lengo la kuwajenga watoto kiimani. Lengo la ziara yake ni kushiriki nao katika utekelezaji wa nguzo ya mfungo wa Ramadhan.

Katika ziara hiyo, Lowassa aliyekuwa ameongozana na waumini mbalimbali wa dini hiyo, alitembelea vituo vitatu vya yatima ambavyo ni Chakuwama kilichopo Sinza, Khairat cha Kigogo na Umra kilichopo Magomeni Mwembechai.

Katika ziara hiyo, Lowassa alitoa msaada wa unga, mchele, mafuta ya kupikia, tende na sukari.

Lowassa alitoa rai kwa watu wenye uwezo kujiweka karibu na jamii inayohitaji msaada, ili kuenzi utamaduni wa Watanzania kusaidiana.“Jamii lazima tuangalie makundi haya kwa kushiriki nao pamoja kwenye mahitaji yao, kula nao pamoja,”alisema.

Mratibu wa misaada hiyo, Sheikh Rajab Katimba ambaye ni Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, alisikitishwa na baadhi ya Waislamu wanaofuturisha makundi ya watu wenye uwezo na kusahau makundi ya wasiojiweza.

“Tusaidiane Waislamu na inashangaza sana kuona jamii inayohitaji msaada inasahaulika na kufuturisha wenye kujiweza kiuchumi, siyo mbaya ila tukumbuke jamii hii yenye uhitaji,” alisema Sheikh Katimba.

Mbali na salamu hizo, dua zilisomwa na watoto wawili, Fadhia Liziki (3) na Nasra Ramadhan (3) wa kituo cha Kigogo kuombea amani.

Asnat Ali (6) wa kituo hicho alitoa shukrani zake, huku akihitaji ukarimu huo uguse kundi la Watanzania wengine walio na nafasi ya kiuchumi. Saida Hassan ambaye ni mmiliki wa kituo cha Sinza chenye watoto 90, alishukuru misaada hiyo huku akiomba ushirikiano zaidi wa kulea watoto hao.

“Kwa upande wetu tunashukuru na tunamwombea aendelee kuwa na moyo huo wa utoaji, msaada huu utatusaidia sana kwenye mwezi huu mtukufu,” alisema Rahima Juma Kishunda ambaye ni mmiliki wa kituo cha yatima Umra.

Ugomvi wa Wabunge wa CCM na UKAWA Wafikia Pabaya........UKAWA Wakataa Kusalimiwa, Wenye Wapenzi CCM watakiwa Kuwaacha

0
0
Sakata la wabunge wa Ukawa kususa vikao vya Bunge vinavyoongozwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson limefika pabaya baada ya baadhi ya wawakilishi hao kuanza kutowasalimia baadhi ya wabunge wa CCM.

Hatua hiyo ilikuwa dhahiri jana baada ya Ukawa kutangaza kuwa hawatashirikiana na wabunge wenzao wa chama tawala katika shughuli za kawaida za kijamii, kama vile michezo na kutumia kantini ya Bunge, wakisema wenzao wameanza kuwabagua.

Mbali na kitendo hicho, wabunge hao pia walitoka kimyakimya bungeni baada ya Dk Tulia kuingia, lakini safari hii hawakufanya mbwembwe za kujiziba midomo kama walivyofanya juzi.

Jana asubuhi, mbunge wa CCM  Kangi  Lugola alisema  kuwa alisikitishwa  baada ya kudai kuwa Mbunge wa Chadema (Viti Maalumu), Lucy Magereli hakumjibu salamu yake wakati akiingia bungeni licha ya kumsalimia mara tatu na kuwa katika umbali mfupi wa kusikika.

“Kusalimia ni jambo la utamaduni wetu. Nilikuwa namsalimia mbunge wa kike wa Ukawa, lakini hakujibu. Lakini, nikajua ni sababu ya wao kufunga mdomo na plasta, nikamtania au kwa sababu ya plasta hujibu ili isije kudondoka hakuitikia,” alisema Lugola.

Alisema ameshtushwa na hali ilipofikia na hajui sababu za msingi za wabunge wa Ukawa kufanya vitendo hivyo, kinyume na udugu na utamaduni wa Watanzania.

Mbunge huyo machachari, alisema Kubenea alimziba mdomo Msigwa kwa mkono ili asizungumze chochote.

Naye mbunge wa  Sumve (CCM ) Richard Ndassa  alisema jambo wanalolifanya wabunge wa Ukawa siyo jema na halina tija kufanywa na wawakilishi hao wa wananchi.

“Sisi ni wabunge, hivi inapofikia kususa kuongea na wabunge wenzako, hatima yake nini?” alisema.

“Mimi nilienda kuwasalimia kama kawaida ambavyo huwa tunafanya kwa wabunge awe CUF, CCM au Chadema, sasa unavyosusa una maanisha nini,” alilalamika Ndassa.

Alisema kitendo cha kutosalimia ni cha juu sana na kwamba iwapo Ukawa wanashauriwa na mtu basi inawapasa kuchuja mambo mengine, likiwamo hilo la kuwasusa wabunge wenzao.

Juzi Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia wakati anawaongoza wabunge wa Ukawa kutoka bungeni aliwatuhumu wabunge wenzao wa CCM kuwa wanawabagua

Naye Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea   alisema;   “Leo  tumekubaliana hatutashiriki katika michezo na wabunge wa CCM, hilo tumeanza leo asubuhi kwenye mazoezi katika viwanja mbalimbali, hivi sasa tunatafakari hata kutafuta uwanja wetu.

“Tukikutana katika uwanja mmoja, sisi tutatumia upande mmoja na wao watatumia upande mwingine, hatuchanganyani, hata salamu leo kuna mmoja kanisalimia nimekwepesha mkono wangu,”
 
Kubenea alisema hata katika mechi zinazoandaliwa kwa ajili ya timu ya wabunge UKAWA hawatashiriki katika kipindi hiki cha wiki mbili zilizobakia za bajeti.
 

“Si katika michezo tu, hata katika mahusiano, tumekubaliana kama kuna wabunge wana mahusiano ya kimapenzi na wabunge wa CCM yasitishwe kwa muda wa wiki mbili mpaka tutakavyoamua vinginevyo,” alisema Kubenea. 


Kitwanga Afunguka Kwa Mara ya Kwanza......Asema Yaliyotokea Anamwachia Mungu, Wiki Ijayo Kutua Bungeni Kwa Kishindo

0
0

ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, amesema yupo imara na amerejea nchini akiwa na matumaini mapya.

Pamoja na hali hiyo, amesema kuwa hivi sasa anajipanga kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha anaisaidia nchi pamoja na wapigakura wake na kuwa na maendeleo ya kweli na Jumatano ya Julai 29, ataripoti bungeni.

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana baada ya kurejea akitokea nchini Israel ambako alikwenda kwa shughuli zake binafsi.

Alisema licha ya mtihani uliomkuta, kwa sasa yupo imara kwa ajili ya kuwatumikia wapigakura wake kwa kuwawakilisha vema ndani ya Bunge.

“Niko imara kabisa na nina nguvu na matumaini mapya, nimeingia nchini jana (juzi) nikitokea nchini Israel ambako nilikuwa na shughuli zangu binafsi. Unajua mimi ni mtaalamu (wa mawasiliano) na wewe unajua kabla sijaingia kwenye siasa nilikuwa nafanya nini.

“Kifupi ninasema nilikwenda Israel kwa shughuli zangu binafsi kabisa ambazo kwa kipindi cha wiki tatu nilizokuwa huko nimefanya. Hata wanaosema nilikwenda kulia kwa Bwana nao ni mawazo yao, maana unajua ile ni nchi takatifu kutokana na historia yake,” alisema Kitwanga.

Alipoulizwa amepokeaje hatua ya kufutwa kwake kazi na Rais John Magufuli kwa kile kilichoelezwa ni ulevi, alisema kwa sasa hawezi kusemea jambo hilo kwani aliyemteua ndiye mwenye mamlaka ya kumwajibisha.

“Rais ni mtu mkubwa anaweza kufanya jambo lolote ili mradi havunji sheria, hata kilichotokea kwangu ni mamlaka yake halali, ingawa Mungu ndiye muweza wa kila jambo. Mimi ni Mkristo safi, nasi tumefundishwa kusamehe saba mara sabini na kusahau yaliyopita,” alisema.

Akieleza mikakati yake, Kitwanga alisema kuwa baada ya kuripoti bungeni wiki ijayo, atakuwa na ziara ya wiki tano ndani ya jimbo lake ambako atazungumza na wapigakura wake na kueleza yaliyomsibu hatua kwa hatua.

“Sitaki kuingia ndani sana ila mengine nitayasema nikiwa jimboni, lakini si kwa lengo la kubishana na mtu, na uzuri kila hatua ambayo nimepitia hata wapigakura wangu walikuwepo kwa uwakilishi wa madiwani wa Misungwi ambao walikuwa mjini Dodoma,” alisema.

Mei 21, mwaka huu, Rais Magufuli alimng’oa Kitwanga kuhudumu kama Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kutokana na madai ya ulevi, huku taarifa zaidi za ndani zikieleza kuwa alianza kushughulikiwa bila yeye mwenyewe kujua.

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ) - Sehemu ya Tatu

0
0

Mtunzi: Enea Faidy
Ilipoishia sehemu ya pili ( kama hukuisoma bofya hapa)
...Baada ya kukamilisha yote hayo Madam Mbeshi akasogeza kiti chake karibu na meza kisha akaketi halafu akaanza kusogeza vitu vilivyokuwepo mezani pale lakini ghafla akakutana na karatasi chafuchafu mezani kwake lakini ilikuwa na maandishi.

Akashtuka kidogo halafu akaichukua ili aisome vizuri. Mwalimu Mbeshi hakutaka kuamini kile alichokiona, akataharuki kwa hofu na mshangao....

 Sehemu ya pili
...Mwalimu Mbeshi aliposoma ujumbe ule kutoka kwenye ile karatasi chafuchafu alizidi kuchanganyikiwa sana, mapigo ya moyo yalimwenda kasi kama gari iliyokata breki ikiwa mlimani. akarudia tena na tena ujumbe ule uliosomeka "POLE SANA MWALIMU KWA MASWAHIBU YALIYOKUKUTA SHULENI KWAKO.. MIMI DOREEN MBWANA NIMEFANYA YOTE HAYO! PIA MUDA WA KIFO CHAKO U KARIBU KWANI UMESOMA UJUMBE WA MWANAFUNZI MCHAWI"

Jasho jembamba lilimtiririka mwanamama yule bila kuelewa afanye nini. Akataka kulitupa chini karatasi lile lakini ghafla akaona karatasi lile limebadilika ghafla, sio karatasi tena bali kitu kama ngozi ya binadamu iliyooza sana huku ikitoa harufu mbaya ikiwa imeambatana na funza wengi wakitembea tembea. 

Madam Mbeshi alihisi kinyaa sana huku woga ukiwa umemtawala kupita kiasi kwani katika maisha yake hakuwahi kushuhudia mauzauza ya namna ile hats Mara moja. Alitamani akimbie lakini miguu ilikuwa imeganda kama msumari kwenye sumaku. 

Mbeshi alihangaika sana na wale funza mkononi mwake kwani walizidi kumpanda mwilini kwa kasi na kumtia ghasia. Machozi yalimtoka mwalimu mbeshi lakini kila tone lililodondoka lilikuwa damu. 

Hofu ikamzidia sana, hakuwa na tumaini la kusalimika tena kwani kwa hatua aliyofikia ilitisha sana. Na yote hayo yalisababishwa na binti Doreen Mbwana.

Ghafla mlango wa ofisi ya mwalimu Mbeshi uligongwa lakini Mbeshi hakuwa hata na uwezo wa kuzungumza chochote. Mlango uligongwa sana lakini Mbeshi hakuweza kuufungua ingawa alitamani yule aliyegonga mlango aingie ili iwe ahueni kwake lakini ilishindikana. 

Kila aliponyanyua kinywa ulimi ulikuwa mzito na hakuweza kuzungumza chochote ikambidi atulie kimya akiugulia mateso yake yalimzonga ndani ya muda mfupi tu.

"Masikini Mimi  inamaana ndo nakufa? masikini familia yangu ambayo Mimi ndio tegemezi! ee Mungu nisaidie!" aliwaza Mbeshi huku machozi ya damu yakizidi kutiririka. 

==> Endelea Nayo  << KWA KUBOFYA  HAPA>>

CCM Yawasilisha Gharama Za Uchaguzi Kwa Msajili Wa Vyama Leo

0
0
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) leo kimewasilisha kwa Msajili wa Vyama, hati zake za gharama ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana, na kuwa chama cha pili kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria za uchaguzi nchini.

Ujumbe wa CCM uliongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa CCM, Stanslaus Mamilo na Mwanasheria wa CCM Adamson Sinka na kuwasilisha hati na vielelezo vya matumizi hayo kwa Mwangalizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama, Mkuu wa Masijala Galasia Simbachawene.

Akikabidhi hati na vielelezo hivyo Mamililo alisema, CCM imelichukua swala hilo umuhimu mkubwa ndiyo sababu imefanya hivyo ndani ya wakati kwa kuwa mda wa kuwasilisha matumizi ya gharama za uchaguzi kwa wagombea na vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 2015, ni Juni 25, 2016.

"Sisi hatuwezi kuwa kama vyama vingine kwa kuwa ni Tasisi kubwa ambayo haina budi kufuata kanuni, taratibu na sheria za nchi hasa ikizingatiwa kwamba CCM ndiyo chama tawala hivyo lazima kionyeshe mfanomzuri ili kiendelee kuwa chama cha kuigwa ", alisema Mamilo.Mamililo aliwasilisha hati na vielelezo vya matumizi ya Chama na wagombea wa nafasi mbalimbali kupitia CCM ikiwemo Urais, Wabunge na Madiwani.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa hati na vielelezo hivyo, Galasia alisema, katika vyama vyote vilivyoshiriki katika uchaguzi mkuu uliopita ni CCM na ACT-Wazalendo ndivyo ambavyo tayari vimekamilisha bila shuruti sheria ya kuwasilisha gharama zake za uchaguzi.

Alisema, uwasilishaji wa gharama hizo ni muhimu sana kwa kuwa ni suala la kisheria, kwa kuwa vyama au wagombea wanaoshindwa kutimiza sheria hiyo watachukuliwa hatua ikiwemo kupelekwa makahamani ambako wakipatikana kwa upande wa Chama kitafungiwa kushiriki uchaguzi wowote utakaofuatia na kwa upande wa wagombea mhusika atatozwa faini ya sh. milioni 2, au kifungo cha mwaka mmoja jela au vyote pamoja.

Kulingana na Sheria ya Uchaguzi, chama kinatakiwa kisitumie ghara inayozidi sh. bilioni 17, na kikilazimika kuzidi kiwango hicho kisididi zaidi ya asilimia 15 ya kiwango kinachotakiwa, huku kwa upande wa wagombea kiasi kinachotakiwa ni sh. bilioni saba na kwa wabunge sh. milioni 33 hadi 88 kulingana na mazingira ya jimbo.

Rais Magufuli aeleza sababu za kusitisha ajira serikalini kwa muda

0
0

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali imeamua kusimamisha kwa muda mfupi usiozidi miezi miwili zoezi la utoaji ajira mpya na upandishaji wa vyeo kwa watumishi wa umma kwa lengo la kupisha uhakiki wa watumishi wa umma katika orodha ya malipo ya mshahara na kuondoa watumishi hewa. 
 
Rais Magufuli amesema hayo leo tarehe 22 Juni, 2016 katika Jubilei ya miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) iliyofanyika katika ukumbi wa Benki hiyo, Mtaa wa Mirambo Jijini Dar es salaam.
 
Dkt. Magufuli amesema zoezi hilo halina nia ya kuwakatisha tamaa watumishi wa umma na amewahakikishia watumishi wote wa umma kuwa serikali itaendelea kuajiri watumishi wapya na kuwapandisha vyeo waliopo kama kawaida mara baada ya kukamilika kwa zoezi.
 
"Serikali ninayoiongoza haina nia ya kuwakatisha tamaa wafanyakazi, lengo lake ni kujipanga kwa makosa tuliyoyafanya, na ndio maana nimesema kwa kipindi cha mwezi mmoja hivi au hata mwezi mmoja na nusu, haitazidi miezi miwili, tusiajiri mtumishi yeyote serikalini, lakini pia katika kipindi cha mwezi mmoja hatutawapandisha vyeo wafanyakazi, ninaomba wafanyakazi waelewe hili, kwa sababu tukiendelea tutakuwa tunawapandisha vyeo hata wafanyakazi ambao hawapo, tunafanya ukaguzi wote tukishamaliza wafanyakazi wataendelea kupandishwa vyeo" amesema Rais Magufuli.
 
Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania kwa kazi kubwa iliyoifanya katika kipindi cha miaka 50 katika kusimamia sekta ya fedha na maendeleo, lakini ameitaka benki hiyo kuchukua hatua za haraka dhidi ya baadhi ya changamoto zinazoyahusu majukumu yake.
 
Miongoni mwa changamoto hizo ni idadi ndogo ya watanzania wanaonufaika na huduma za benki hususani waishio vijijini, benki kutoza riba kubwa na hivyo kusababisha wananchi kuogopa kukopa kwa hofu ya kushindwa kulipa, kuilinda thamani ya Shilingi ya Tanzania, na kukusanya kodi ipasavyo kwa miamala inayofanywa kupitia simu za mkononi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA).
 
Changamoto nyingine ni kusimamia ipasavyo maduka ya kubadilishia fedha (Bureau  de change) ili kuthibiti utakatishaji na utoroshaji wa fedha na kuhakikisha ushukaji wa mfumuko wa bei uliotoka asilimia 28 hadi kufikia asilimia 5.1 katika kipindi cha miaka 15 iliyopita unaonesha matokeo katika nafuu ya maisha ya watanzania.
 
Aidha, Rais Magufuli ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania kuchukua hatua mara moja dhidi ya benki ambazo hazizalishi faida zikiwemo benki za serikali, kufuta account mfu (Domant account) na kuanzisha mara moja akaunti moja ya mapato na matumizi ya serikali (Single Treasury Account)
 
Jubilei hiyo imehudhuriwa na Magavana na Manaibu Gavana kutoka nchi 18 za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC), Mabalozi kutoka nchi mbalimbali, Viongozi wa Taasisi za fedha za Afrika na Makatibu wakuu wa Wizara za Fedha na Mipango wa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
22 Juni, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya June 23

Tume Yabaini Ufisadi Mkubwa Bandari....Waziri Aagiza Wahusika Waachishwe Kazi na Wafikishwe TAKUKURU

0
0

SERIKALI imebaini ufisadi mkubwa ndani ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kutokana na kukamilika kwa kazi ya Tume iliyoundwa mahususi ili kuchunguza utendaji wa mamlaka hiyo, na imeagiza kuchukuliwa hatua kwa watu wote wanaotajwa kuhujumu Bandari ya Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa alisema hayo wakati akizindua Bodi mpya ya TPA inayoongozwa na Profesa Ignas Rubaratuka jijini Dar es Salaam jana.

Akiagiza hatua zinazopaswa kuchukuliwa kwa wahusika waliotajwa katika ufisadi na ripoti hiyo, alisema kwanza ni baadhi kufikishwa mbele ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na wengine kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi lakini akionya kuwa ni marufuku kwa wahusika kupewa barua za onyo.

Katika kudhihirisha kukerwa na utendaji wa TPA, Profesa Mbarawa ambaye baadaye alifanya ziara katika maeneo mbalimbali ya Bandari ya Dar es Salaam, aligoma kukabidhi mabegi ya kuwekea nyaraka kwa wajumbe wa Bodi mpya kwa kusema kuwa yalikuwa ni ya gharama sawa na yale yanayotumika kusafiria Ulaya.

Akizungumzia kukamilika kwa kazi ya Tume, Profesa Mbarawa alisema tume hiyo iliyowajumuisha wataalamu mbalimbali imefanya kazi kubwa ya kuchunguza utendaji wa TPA na kubaini ufisadi mkubwa katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya mifumo ya miundombinu kama katika mita za kupima mafuta (flow meters).

Kuhusu mita za kupimia mafuta, aliitaka bodi hiyo kuwa makini katika kusimamia utendaji kazi wa mita hizo alizosema serikali imetumia Sh bilioni 12 kuzinunua ili kuhakikisha kuwa zinafanya kazi vizuri na kwamba zinapoharibika ni lazima uamuzi wa ama kununua mpya au kuzirekebisha ufanywe haraka.

Alisema ufisadi mwingine umebainika katika miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), ambako mingi imewekwa ili kuwanufaisha watu na si serikali, mgongano mkubwa wa maslahi kwa Bodi ya Zabuni uliochangia kukwama kwa shughuli mbalimbali za kimaendeleo, ajira za kindugu, kulindana, mtandao wa wezi, rushwa na uwezo mdogo wa kiutendaji.

Kuhusu mgongano wa maslahi kwa Bodi ya Zabuni ya TPA, ambayo aliagiza ivunjwe mara moja na kuundwa mpya, Waziri Profesa Mbarawa alisema Bodi hiyo imekuwa ikitanguliza mbele kile alichokiita ‘ten percent’ katika kila zabuni na kukiri wazi kuwa bodi hiyo ni chanzo cha matatizo mengi ya Mamlaka ya Bandari.

Alisema kutokana na udhaifu wa Bodi hiyo ya Zabuni, huduma karibu zote zinazotolewa ndani ya TPA zinatolewa na kampuni ambazo ama ni za wafanyakazi wa mamlaka hiyo, au za waume au wake zao, na kama si hivyo basi ni za ndugu, jamaa au marafiki wa wafanyakazi, jambo linalozua mgongano mkubwa wa kimaslahi.

Kuhusu ajira, alisema ripoti imebaini viongozi wa TPA wamekuwa wakiwaingiza kazini ndugu, jamaa na marafiki zao kinyume cha taratibu za utumishi serikalini na alikwenda mbali kwa kusema kuwa TPA ilipohojiwa kuhusu kasoro hizo kupitia kwa mwanasheria wake ilisema; “hakuna tatizo,” jibu alilosema lilimpa mshituko mkubwa.

Kuhusu mazingira ya rushwa, alimuonya Mwenyekiti wa Bodi hiyo mpya kuwa macho na rushwa, akisema watu wanaohujumu utendaji wa Mamlaka ya Bandari ni watu wanaotumia ushawishi wa kiwango cha juu cha rushwa na kutoa siri kwamba wamewahi kufanya jaribio la kumhonga mjini Mwanza na Dodoma bila mafanikio.

“Ripoti imebainisha kuwa wamekuwa wakihonga hata bodi, wanawapa fedha shilingi milioni tano kwa wajumbe wa bodi na hivyo wanapoteza nguvu ya kusimamia mambo. Ikitokea hivyo kwa bodi hii, wewe ni Profesa mwenzangu kwa hiyo ngoma droo lakini nitakuwajibisha. Nitamwomba Rais akuondoe mlango ulioingilia ndio utatokea na hawa wajumbe ambao wapo katika mamlaka yangu nitawafukuza papo hapo,” alionya Mbarawa.

Rais Kagame Kutua Nchini July Mosi Kwa Ziara Rasmi ya Kitaifa

0
0

RAIS Paul Kagame wa Rwanda atafanya ziara rasmi ya kitaifa nchini Julai mosi mwaka huu ambayo pamoja na mambo mengine, atafungua Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF) maarufu Sabasaba siku hiyo kutokana na mwaliko rasmi wa Rais John Magufuli.

Akitoa taarifa rasmi ya serikali jana Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi, Dk Augustine Mahiga alisema ziara hiyo ni mwendelezo wa uhusiano mzuri baina ya nchi hizo mbili.

Alisema Rais Magufuli amemualika Rais Kagame kuja nchini kutokana na ziara yake aliyoifanya nchini Rwanda mapema Aprili mwaka huu ambayo pamoja na mambo mengine, marais hao walikubaliana kushirikiana kwenye nyanja mbalimbali.

“Rais Magufuli amenituma kuwaambia umma kwamba amemwalika Rais Kagame kuja nchini kwa ziara ya kitaifa ambapo atafungua Maonesho ya Sabasaba na pia watasaini mkataba wa makubaliano kwenye mambo waliyoafikiana wakiwa Rwanda,” alisema Balozi Mahiga.

Katika ziara ya Rais Magufuli nchini Rwanda ambako yeye na Rais Kagame walifungua Daraja la Rusumo lililo mpakani mwa nchi hizo, viongozi hao waliafikiana kuendeleza ushirikiano katika sekta tofauti ikiwemo biashara.

Hata hivyo, marais hao waliwataka wataalamu wa nchi hizo mbili kukaa pamoja na kujadiliana kwa kina mambo waliyozungumza ya ushirikiano, na ujio wa Rais Kagame nchini una lengo pia la kuweka saini ya makubaliano baina yake na Rais Magufuli kwenye Mkataba wa Makubaliano wa ushirikiano wa mambo waliyoafikiana.

Aidha, Balozi Mahiga alisema baada ya Rais Kagame kusaini mkataba huo na mwenyeji wake na kufungua maonesho hayo, jioni ataungana na Rais Magufuli kwenye dhifa itakayoandaliwa Ikulu. 

Ziara yake nchini Rwanda ilikuwa ya kwanza nje ya nchi kwa Rais Magufuli tangu achaguliwe kuiongoza Tanzania na kuapishwa Novemba 5, mwaka jana.

Mbunge Ataka UKAWA na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson Wapatanishwe

0
0
Mbunge wa Kasulu Mjini (CCM), Daniel Nsanzugwako amesema bado anaamini katika upatanisho kati ya wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson ili kumaliza tofauti zao.

Mwenyekiti mwenza wa Ukawa James Mbatia amesema wameamua hawatasalimiana na wabunge wa CCM, wala kushirikiana nao kwenye shughuli mbalimbali.

Hata hivyo, Nsanzugwako alisema jana kuwa hawezi kufahamu kama mawazo yake aliyowahi kuyatoa bungeni wakati akichangia hotuba ya bajeti kuu mwaka 2016/17 yamefanyiwa kazi.

“Bado ninaamini katika kukaa pamoja na kujadiliana, miye ni muumini wa reconciliation (upatanishi) na Bunge ni taasisi siyo mtu binafsi hatuwezi kukaa sisi wanaCCM pekee yetu,” alisema Nsanzugwako.

Akichangia katika hotuba ya bajeti wiki iliyopita, Nsanzugwako alimshauri Dk Ackson kuwasamehe wabunge wa kambi ya upinzani na wakae meza moja kujadiliana na kuondoa tofauti zao.

Nsanzugwako alihoji faida wanayoipata wabunge wa CCM kwa wabunge wa Kambi ya Upinzani kususa vikao vinavyoendeshwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.

Kauli hiyo ilionekana kutowafurahisha wabunge wa CCM na Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde alimpatia taarifa Nsanzugwako kuwa hakuna mbunge wa upinzani aliyefukuzwa na Naibu Spika na kwamba kumuomba Dk Tulia awasamehe ni kuondoa ukweli kwamba wabunge wameadhibiwa na Bunge zima na siyo Naibu Spika.

Dk Tulia alisema hakuna mbunge aliyefukuzwa ila wabunge hao wameamua kuondoka kwa utashi wao wenyewe.

Alisema kanuni ya tano ya Bunge imetoa mwongozo wa jinsi ya kuwasilisha malalamiko ya wabunge wanapokuwa na jambo na kiti.

Alisema tayari wabunge wa kambi hiyo wamewasilisha malalamiko yao jambo ambalo ni haki yao kimsingi . Alisema katika Bunge lililopita wapinzani waliwahi kutumia kanuni hiyo kuwasilisha malalamiko yao dhidi ya kiti, lakini hawakususia vikao vya Bunge.

"Napenda kumfahamisha mheshimiwa mbunge kuwa hakuna mtu waliyemuudhi wala wanaohitaji kuomba msamaha. Wao wametoka kwa utashi wao,”alisema.

Katibu wa wabunge wa CCM, Jasson Rweikiza, alisema hizo ni fujo tu za wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani na kwamba hakuna kitu wanachopoteza kwa wao kutoka nje ya Bunge.

Alisema kanuni zinajieleza jinsi ya kufanya iwapo kuna mbunge hakubaliani na kiti cha Spika kwa kupeleka malalamiko yake katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

 “Sisi tutafanyaje sasa kama watu wameamua kufanya fujo, sisi tumeendelea na shughuli za Bunge kwa kujadili kwa kina hotuba zote na kutoa mapendekezo yetu,” alisema.

 Alisema kutoka kwa wapinzani hakuna jambo lilipungua kwani mambo yote yamekwenda sawa na sasa watajadili Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2016 ambayo tayari wabunge wa CCM wamepeleka majedwali ya marekebisho.

“Sisi hatuwezi kumlazimisha mtu atupende. Kutoshiriki kwao vikao kunaondoa maana nzima ya kuwa wabunge.Safari ijayo wananchi wasiwachague hawa wahuni, wawachague wabunge wanaotokana na CCM,” alisema.

Hata hivyo, katika kikao cha wabunge wa CCM walichofanya katika ukumbi wa Pius Msekwa na kuongozwa na Mwenyekiti wao Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jana wabunge walijadili mambo mawili.

Miongoni mwa mambo hayo ni hofu waliyonao baada ya wabunge wa upinzani kukataa kusalimiana nao na kushirikiana nao kwenye shughuli mbalimbali na kuelezwa kwanini muswaada wa Sheria ya Fedha haujaenda bungeni hadi sasa.

Wabunge hao walielezea hofu waliyonayo juu ya kufanyiwa vitendo vibaya na wabunge wa kambi ya upinzani. Majaliwa aliwaondoa hofu wabunge hao na kwamba hawana haja ya kuwa na hofu kwa sababu nchi iko salama.

Hata hivyo, aliwataka kuwa wavumilivu na kuendelea kushirikiana nao.

Mtoto Anajisiwa na Kisha Kuuawa Kwa Kunyongwa

0
0
 Eneo la Unga Limited, jijini Arusha

Mtoto wa miaka minne amenajisiwa na kuvunjwa shingo na kutupwa kandokando ya njia ya watembea kwa miguu karibu na mfereji wa maji umbali wa mita 50 kutoka nyumbani kwao jijini Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Yusuf Ilembo, tukio la kunajisiwa kwa mtoto huyo wa kike lilitokea Juni 20, mwaka huu saa 3.30 usiku kwenye makaburi ya baniani Kata ya Unga Limited.

Kaimu Kamanda wa Polisi Ilembo alidai mtoto huyo ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa akicheza na wenzake nje kidogo ya nyumbani kwao na ilipofika saa 12 jioni kwa mujibu wa marafiki zake (majina yamehifadhiwa) wanasema alifika mtu mmoja mwanamume mrefu.

Kwa mujibu wa watoto hao, mwanamume huyo alikuwa amevaa suruali na kumwambia mtoto huyo amfuate akamnunulie pipi na hapo ndipo alipomfuata huyo mwanamume huyo na hakurudi tena.

Mshitakiwa Mauaji ya Mwangosi Ana Kesi ya Kujibu

0
0

Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imetupilia mbali ombi la kumuachia huru mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Channel 10 mkoani humo, Daudi mwangosi na badala yake imesema ana kesi ya kujibu.

Akitoa uamuzi wa ombi hilo mahakamani hapo jana, Jaji Paulo Kihwelo, alisema mahakama imeona mtuhumiwa huyo ana kesi ya kujibu na anatakiwa  kupeleka mashahidi makamanani.
 
Akizungumzia uamuzi huo, wakili wa upande wa utetezi, Rwezaura Kaijage, alisema wameridhika na watatoa ushahidi wakiwa na shahidi mmoja ambaye ni mtuhumiwa mwenyewe.
 
“Utetezi tumeridhika na uamuzi wa mahakama, shahidi atakuwa mmoja na ni mtuhumiwa mwenyewe, lakini tunaiombamahakama yako tukufu ushahidi huo utolewe kwa njia ya kiapo,” alisema.
 
Kaijage aliomba utetezi huo utolewe leo kuanzia saa 3: 00 asubuhi. Kwa upande wa wakili wa Jamhuri, Ladislaus Komanya na mwenzake Sunday Hyera, walisema hawana pingamizi lolote la ombi hilo kuwa utetezi utolewe leo.
 
Ulinzi Mkali Mahakamani
Kabla ya Jaji kuingia kwenye chumba cha mahakama, ulinzi mkali wa polisi ulitawala nje na ndani ya mahakama, wakiwamo askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kuzingira eneo hilo.
 
Aidha, waandishi wa habari walipata wakati mgumu kutekeleza kazi yao baada kunyimwa kuingia ndani ya chumba cha mahakama kwa kisingizio kuwa kesi haijaanza, hali iliyolazimu Msajili wa Mahakama hiyo, Ruth Massam, kuingilia kati na kuwataka polisi kuacha lakini hawakumsikiliza.
 
Baada ya mvutano huo, waandishi walikaguliwa na kisha kuruhusiwa kuingia, lakini hali iliendelea kuwa ngumu ndani ya chumba cha mahakama kiasi cha kutishiwa kuvunjiwa vitendea kazi vyao na baadhi ya polisi.
 
Hata hivyo, waaandishi waliendelea kutekeleza majukumu yao hadi kesi ilipoanza.
 
Baada ya Jaji Kihwelo kuahirisha kesi hiyo, mtuhumiwa alishuka kizimbani kimgongo mgongo ili asionekane sura, huku askari wenzake wakimfunika kwa kitambaa na kitenge kichwani, pamoja na bahasha ya kaki. Askari zaidi ya 30 walimzingira ili asipigwe picha.
 
Mwangosi aliuawa Septemba 2, 2012 kwenye ufunguzi wa matawi ya Chadema katika kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi, mkoani Iringa.

Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Ukosefu Na Upungufu Wa Nguvu za Kiume

0
0

Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  

Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.

Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kufahamu   kuhusu   SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME  tafadhali  tembelea :

Ukisoma  vizuri  kuhusu  mfumo  wa  nguvu  za  kiume, utagundua  kuwa   Suala  la  nguvu  za  kiume  ni  suala  la  kimfumo.  Ili  mwanaume  awe na nguvu  za  kiume, aendelee  kuwa  na  nguvu  za  kiume na  azilinde  nguvu  zake za  kiume, ni  lazima  ogani  zote zinazo  husika  na  mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ziwe  na  afya  njema  na  ziwe  na  ushirikiano   thabiti  na  wenye  afya.

Vile  vile , utagundua  kuwa , mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ni  kama  ifuatavyo:

i.Mishipa  imara  ya  ubongo  na  yenye  afya  njema

ii. Mishipa  imara  ya  uti  wa  mgongo  (  spinal  cords )

iii.Mishipa  imara  itumikayo  kusafirisha  damu  mwilini  (  Blood Vessels )

iv. Mfumo  imara  wa  usafirishaji  damu  mwilini

v. Mishipa  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema

vi. Uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  ubongo, mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume.

Hivyo  basi, ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, na  aendelee  kuwa  na  nguvu  hizo ni  lazima  mambo  yote  muhimu  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume  yawe  imara  pasi na  hitilafu  yoyote.

Hitilafu  yoyote  katika  mambo  hayo, itasababisha  ukosefu na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume  kwa  mwanaume  huyo.  Pale inapotokea    hitilafu  ama  mapungufu  katika  ogani  zaidi  ya  moja  kati  ya  zilizo  tajwa hapo  juu, basi  tatizo  kwa  muhusika  huwa  kubwa  mara  dufu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU &  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Mwanaume   anapopatwa na  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, ubongo  hutoa  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo  husafirisha  taarifa  hadi  kwenye  mishipa &  misuli  ya  uume.

Mishipa  ya  uume inapopokea  taarifa  hiyo, hutanuka. Na  mishipa  ya  uume  inapotanuka, hufanya  mambo  mawili  muhimu  sana :

i.Husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  hivyo  kuruhusu  damu  kuingia kwa  kasi  sana   ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  imara  bara bara.

ii. Huibinya na  kuiziba  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuzuia  kunyonya  ama  kufyonza  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa ya  uume.  (  KAZI  KUBWA  YA  MISHIPA  YA  VENA  ILIYO  KARIBU NA  MISHIPA  YA  UUME  NI KUHAKIKISHA  HAKUNA  DAMU NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME. HIVYO  BASI  DAMU  INAPOINGIA  NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME, MISHIPA  YA  VENA  HU “SENSE” JAMBO  HILO  KWA  HARAKA  NA HIVYO  KUIFYONZA  DAMU  HIYO  KUTOKA KWENYE MISHIPA  YA UUME  YA  KUITOA  NJE YA MISHIPA  YA  UUME.  NA  DAMU INAPOKOSEKANA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME, HUUFANYA  UUME  KUSINYAA  NA  KULEGEA )

Mtu  anayepiga  punyeto  husababisha  mambo  yafuatayo  katika  mwili  wake :

1. Huuwa  nguvu  ya  mishipa  & misuli ya  uume ambayo  ndio  inayo husika  na  kusimama  kwa  uume

2. Mishipa  ya   uume  inapo  sinyaa  na  kukosa  nguvu  yake  ya  asili, husababisha  mambo  yafuatayo :

i.Huondoa  uwezo  wa  mishipa  &  misuli  ya  uume  kutanuka, na  hii  ndio  sababu  inayo  wafanya  waathirika  wa  punyeto  kutumia  nguvu  nyingi  sana  katika  kuufanya  uume  usimame.

ii.Huondoa  uwezo  wa  mishipa &  misuli  ya  uume  kuibana  na  kuiziba  mishipa  ya  vena, na  hii ndio  sababu  inayo  fanya  waathirika  wa  punyeto  kufika  kileleni  haraka  sana, kwani damu  inayo  ingia  kwenye misuli  ya  uume   hufyonzwa  ndani ya  muda  mfupi sana. 
 
 Hii  hutokea  kwa  sababu  mishipa na  misuli  ya  uume inakuwa  imelegea,na  mishipa  ya  vena inakuwa  imepwaya, hivyo  msuguano wowote ule  hufanya  mishipa  ya  vena  kufunguka  na  kufyonza  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  na hivyo  kuufanya  uume  kusinyaa  ndani ya dakika ama sekunde  chache sana.

3. Vile  vile  punyeto  hufanya  uume  kusinyaa na  kurudi ndani  na  kuufanya  uonekane kama  uume  wa  motto mdogo.

Kwa  ufupi  punyeto  husababisha  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuu  zifuatazo :

i.Kwanza   hudhoofisha  na  kuharibu  mishipa  ya  uume,  ambayo  ndio  hufanya  uume kusimama.

ii.Pili  hudhoofisha  utendaji  kazi  wa  mishipa  ya  ateri, ambayo  ndio  hutumika  kama  njia  ya  kusafirisha  damu kupeleka kwenye  misuli  ya  uume  na  ivyo  kuufanya  uume  usimame

iii. Tatu, punyeto  hupelekea  kuvuja  kwa  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kusababisha  damu  kufyonzwa  kwa  haraka  sana  kila  iingiapo ndani  ya  misuli ya  uume  na  matokeo  yake  ni  uume   kusimama  kwa  muda  mfupi  sana  wakati wa  tendo  la  ndoa.

iv. Punyeto  huathiri  mtiririko  wa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume, kwa  sababu  hudhoofisha  misuli &  mishipa  ya  uume  pamoja  na mishipa ya  ateri  ambayo  ndio  hutumika  katika  kusafirisha  damu kwenda  kwenye  uume

DALILI  ZA  MTU  ALIYE  ATHIRIWA  NA  PUNYETO
Dalili  kuu  za  mtu  aliye athiriwa  na  punyeto  ni  kama  ifuatavyo:

i.           Uume  kusinyaa  na  kuwa  kama  wa  mtoto
ii.         Uume kurudi  ndani
iii.       Uume  kusimama  ukiwa  legelege
iv.       Kufika  kileleni  haraka  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

TIBA   YA   NGUVU  ZA  KIUME  KWA MTU  ALIYE  ATHIRIKA  NA  PUNYETO.
Dawa   asilia  ya  nguvu  za  kiume iitwayo JIKO  ni tiba  bora  na  ya  uhakika  kabisa  kwa  mtu  aliye  athiriwa   na  punyeto.  Dawa  hii, pamoja  na  mambo  mengine  mengi, husaidia  kufanya  mambio  yafuatayo  katika  mwili  wa  mwanaume  aliye  athiriwa  na  punyeto :

i.Kuimarisha  mishipa  & misuli  ya  uume  ulio  legea na  hivyo  kuurejeshea  uwezo wake wa  asili

ii. Hutibu   tatizo  la  uume  kurudi  ndani

iii.Humaliza  tatizo  la  kusimama  kwa  uume  ukiwa  legelege

iv.Hutibu  na  kuponya  kabisa  tatizo  la  kufika  kieleleni  haraka.

BEI  YA  DAWA  :  Dawa  hii  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU (Tsh. 80,000/=)

MAHALI  INAPOPATIKANA :  Dawa  hii  inapatikana  katika  duka  la  dawa  asilia  liitwalo  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  UBUNGO   nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA   karibu  na SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING.

Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu. Watafikishiwa  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  DAR  ES  SALAAM.

Kwa   wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  MABASI

Kwa  wateja  waliopo   Zanzibar  wata fikishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa boti.

Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  ama  DHL.

MAWASILIANO :  WASILIANA  NASI   KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee kila  siku  kwenye  blogu  yetu :

Magufuli Ashusha Nyundo 7.....Apasua makampuni ya madini, Mafao hewa na miamala ya simu

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli ameendelea na kasi yake ya kutumbua majipu ambapo jana alishusha nyundo kwa majipu mapya 7 yanayotafuna uchumi wa nchi kwa kuiibia Serikali kwa mbinu mbalimbali kupitia miamala ya fedha.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Rais Magufuli alisema kuwa Serikali yake haiwezi kuyavumilia makampuni ya Madini yanayofanya kazi nchini kwa kuendelea kuieleza Serikali kuwa yanapata hasara miaka yote huku yakiendelea na shughuli zake za uchimbaji madini.

Rais Magufuli alisisitiza kuwa kama Makampuni hayo yanasema yanapata hasara kila mwaka ni bora yaondoke nchini.

“Hivyo ni visingizio tu, ni bora tubaki na madini yetu miaka 1,000 watachimba watakaokuja sisi tukiwa tumeoza,” alisema. 

“Wanadai wanapata hasara wakati wana akaunti sehemu nyingine,” aliongeza Rais Magufuli.

Rais Magufuli pia alieleza kuwa tayari amebaini kuwepo kwa malipo ya zaidi ya shilingi bilioni 7 yasiyo ya halali (hewa) kwa wastaafu 2,800 kupitia Benki ya NMB. Katika hilo alieza kuwa tayari ameshatoa maagizo watu hao warejeshe fedha hizo.

Pia, Rais Magufuli amelikamua jipu udanganyifu kwenye miamala ya simu. Alisema amebaini kuwa makampuni ya simu yamefanya miamala yenye thamani ya shilingi trilioni  5.5 ambayo haikukatwa kodi, mwezi Machi mwaka huu.

Aliwataka TCRA kushirikiana na BOT  kuhakikisha wanalishughulikia suala hilo na kurejesha fedha za serikali kupitia kodi.

Rais Magufuli pia aliyanyooshea kidole maduka ya kubadilishia fedha za kigeni akiitaka BOT kuyasimamia kwa ukaribu ili yasiwe kichochoro cha kupitishia fedha za dawa za kulevya ama fedha ambazo zinavushwa kinyamela.

Kadhalika, Rais Magufuli aliwataka BOT kuhakikisha kile walichomueleza kuwa wamewezesha kushuka kwa mfumuko wa bei kwa kutoka asilimia hadi asilimia 5.2 kionekane kwa uhalisia ka wananchi na sio kuishia kwenye maandishi.

“Je, [kushuka huko]kumefika kwa wananchi au kumeishia kwenye makaratasi tu? Je, bidhaa za miaka ya 90 na sasa ni sawa?” Rais Magufuli anakaririwa.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemuagiza Gavana wa BOT, Profesa Benno Ndulu kuifuta Benki ya Twiga Bancorp kwakuwa imekuwa ikijiendesha kihasara huku ikivunja sheria. 

Alimtaka Gavana Ndulu kuzichukulia hatua Benki zote zenya muelekeo huo hata kama ni za Serikali.

“Unakwenda Benki unakuta kuna negative (hasi) bilioni 18, mimi nasema katika utawala wangu sitabembeleza Benki isiyofanya vizuri hata kama ni ya Serikali. Kuna Benki moja inapambwa na CCM lakini….” Rais Magufuli alisikika japo hakuitaja Benki hiyo.

Rais Magufuli pia aliitaka BOT kuhakikisha Benki zinaweza kutoa mikopo yenye riba nafuu ili kunusurua taasisi na wananchi wanaokopa katika benki hizo.

Naye Gavana Ndulu alimhakikishia Rais Magufuli kuwa wanaunga mkono juhudi zake na kumkabidhi mfano wa hundi ya shilingi bilioni 4 ambayo watatoa kwa serikali kuchangia madawati katika shule za msingi na sekondari nchini. Gavana ndulu alisema kuwa fedha hizo zimepatikana kutokana na kubana matumizi.

Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova Aagwa...... Aomba kazi Tena Polisi

0
0
Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova, ameliomba jeshi hilo kumpa kitengo cha masoko ili aweze kulitangaza na kuliunganisha na wananchi, ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa maboresho ndani ya jeshi hilo katika kukabiliana na uhalifu.

Kova alitoa ombi hilo jana mjini Moshi katika hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika Shule ya Polisi Moshi (MPA).

Alisema jeshi hilo linaelekea kuzindua mpango wake wa matokeo makubwa sasa (BRN) ,ambao unahitaji msukumo wa jamii katika kusaidia kukabiliana na uhalifu wa aina mbalimbali ukiwamo wa mtandaoni na dawa ya kulevya.

Kova alisema kutokana na utumishi wake wa zaidi ya miaka 40 kwa kushirikiana na wastaafu wengine, wanaweza kusaidia na kuwa kiunganishi baina ya polisi na raia kama njia bora ya kukabiliana na uhalifu kwa kutumia kitengo cha masoko.

“Nimekuwa mtumishi ndani ya polisi kwa miaka 40, ninaweza kutumika hata na Shule ya Polisi Moshi kufundisha na hata kutoa uzoefu wangu ambao utalisaidia jeshi katika kukabili uhalifu, kama mnavyoniona ninazo nguvu za kutosha na ninalipenda Jeshi la Polisi,” alisema.

Katika hatua nyingine, Kamishna Kova aliiomba serikali kuliboresha zaidi jeshi la polisi kwa vifaa, mbinu na teknolojia za hali ya juu ili kukabiliana na matukio ya uhalifu wa aina mbalimbali unaokuwa kulingana na ukuaji wa teknolojia duniani.

Rais Magufuli Awaonya Wanasiasa Wanaomchelewesha Kufanya Kazi

0
0
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli amewaonya wanasiasa wanaomchelewesha kufanya kazi ya kuwatumikia Watanzania.

Rais Magufuli ameyasema hayo muda mfupi uliopita baada ya kupokea ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kutoka kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). 

Amesema haiwezekani uchaguzi umepita na mshindi amepatikana lakini wanasiasa hao wanaendeleza siasa ilhali wananchi wanataka watumikiwe wapate maendeleo.

Rais amesema hatawavumilia viongozi wa siasa wenye lengo baya na nchi na kuwataka waweke maslahi ya Taifa mbele badala ya vyama vyao. 

Amewataka kufanya siasa baada ya miaka mitano ambapo wananchi watawapima kile walichokifanya kwa muda wote huo.

Awali Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema suala la Kura ya Maoni halikusitishwa kama baadhi ya watu wanavyosema bali iliahirishwa kwa kuwa wakati kura hiyo ilipotakiwa kupigwa Aprili Mwaka jana, Tume ilikuwa na jukumu kubwa la kuandaa uchaguzi Mkuu.

Kutokana na hali hiyo, Jaji Lubuva alisema Tume haikuwa na uwezo wa kubeba mambo mawili makubwa kwa wakati mmoja. Jaji Lubuva amesema kutokana na zoezi la Uchaguzi Mkuu kumalizika rasmi, Tume iko tayari kuanza mchakato wa kura ya maoni.

Kuhusu suala hilo la Kura ya Maoni, Rais Dk Magufuli amemhakikishia Jaji Lubuva kuwa serikali italiamualia mara baada ya Tume kulifikisha serikalni. 

Simu Mpya Kutoka Tecno, Camon C9 Yatua Dar Na Camera Ya Hali Ya Juu Na Mfumo Wa Kufungua Simu Kwa Macho

0
0

Teknolojia ya simu inaendelea kukua siku baada ya siku, baada ya simu feki kuzimwa na Mamlaka ya Mawasilinao nchini (TCRA), Tecno Mobile imetangaza kuzindua simu kali ya CAMON C9 yenye uwezo wa hali ya juu katika kupiga picha, uwezo wa 4G LTE na teknolojia mbali mbali za kisasa. Ikiwa simu yako ni miongoni mwa simu zilizofungiwa na TCRA basi ondoa shaka kwani simu hii mpya kutoka Tecno utaipata kwa gharama nafuu kabisa.

Tecno Camon C9 inaanza kuuzwa rasmi tarehe 25 Juni 2016. Unaweza kufanya manunuzi ya awali (pre-order) uwe miongoni wa Watanzania wa awali kujipatia simu hii. Kufanya manunuzi ya awali tembelea exclusive show room za Tecno jijini Dar zilizopo City Mall, Clock tower na Mobile plaza ghorofa ya pili.
Kufanya manunuzi ya awali unahitaji kufanya malipo ya awali ya Tsh. 30,000 ambapo mteja atapata kadi ya “huduma kwa wateja kutoka” Tecno na kifurushi cha zawadi (gift hamper) za bidhaa kutoka Tecno. Kadi ya huduma kwa wateja itatumika katika kutengenezewa simu katika duka zetu za Tecno baada ya kujipatia simu yenyewe.

Mauzo rasmi yanaanza 25 Juni 2016 ambapo watakao kuwa wamefanya pre-order watatakiwa kukamilisha malipo yao dukani hapo na kisha kuingizwa moja kwa moja kwenye droo ya kijishindia zawadi mbali mbali.

Zawadi za Droo
Zawadi ya Kwanza: Samsung LED TV yenye thamani ya Milioni 1.6
Zawadi ya pili: Jiko ya kutumia umeme (washindi wawili)
Zawadi ya tatu: Birika linalotumia umeme (washindi wawili)
Na zawadi zingine nyingi

Kila mteja atakaye nunua Tecno C9 Jumamosi katika First sale itakayofanyka pale City Mall (Showroom inaonekana kwenye picha) atakuwa mshindi.

Baadhi ya sifa za Camon C9 itauzwa katika maduka ya Tecno ikiwa katika rangi 3 tofauti na hizi ni baadhi ya sifa zake.

Camera ya hali ya juu
Kama mpenzi wa picha Camon C9 imekupa Camera unaihitaji kwani inaweza kutambua sura na kupiga selfie kali hata ukiwa gizani.

Pia Camera yake ina urembo wa kweli (make-up) ambayo itafanya picha zako kuwa na mvuto wa asili kitaalamu imeitwa

(Insert video)

Watu 50 ndani ya selfie moja

Inasemekana Tecno Camon C9 ina uwezo wa kujaza watu wengi kwenye selfie moja zaidi ya simu yoyote duniani. Camera ya C9 inachukua angle kubwa zaidi hivyo kukuwezesha kupata selfie nzuri hivyo kuchukua watu wengi zaidi.
Jinsi mpya ya kupiga selfie ukitumia Camera ya kati
Tecno Camon C9 itaondoa issue za selfie kutokuwa kati kwa kutumiacamera iliyo katikati ya simu ambayo wameita “The Perfect Selfie camera”

Umeshawahi kufikiria macho yanaweza kufungua simu?  Camon C9 ina Iris recognition

Sasa hutokuwa sababu ya kuweka password zinazofanana na lugha ya kirumi kwasababu Tecno imebadilisha mfumo wa namna unaweka neno la siri kwenye simu kwa kuleta teknolojia mpya ya IRIS recognition ambayo inatumia macho kufungua simu. Tecno Camon C9 inatumia teknolojia hii kumuwezesha mmliki wa simu ku-unlock simu kwa kuitizama tu.
Unaweza kutembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya Tecno kujua zaidi









Serikali yapokea msaada wa Shilingi Bil. 440 toka Benki ya Dunia.

0
0

Na Eliphace Marwa-Maelezo
Benki ya Dunia imeahidi kuendelea kuisaidia Serikali ya Tanzania kifedha ili iweze kutekeleza majukumu yake ya utoaji wa huduma za msingi za kijamii nchini kupitia miradi mbalimbali iliyo chini ya Benki hiyo.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia hapa nchini Ms. Bella Bird wakati wa kusaini hati ya makubaliano kuwa kutokana na umuhimu wa kusaidia kaya maskini kupitia mradi wa TASAF, Benki ya Dunia imetoa kiasi cha Dola za Kimarekani 200 sawa na shilingi za Kitanzania Bilioni 440.

“Ili Tanzania iweze kupambana na umaskini inahitaji kuhakikisha kaya maskini zinapata huduma bora za afya na elimu ili kuweza kutimiza malengo yake, Benki ya Dunia itaendelea kutoa msaada wa kifedha ili kufikia malengo yaliyoainishwa na serikali,” amesema Ms. Bella Bird.

Aidha Mkurugenzi huyo Mkazi amefafanua kuwa Benki ya Dunia inatambua umuhimu wa kupambana na umaskini katika maendeleo ya nchi zote duniani ikiwemo Tanzania katika kuleta maendeleo endelevu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile amesema kuwa katika kipindi cha miaka hamsini ya ushirikiano na benki ya Dunia katika mwaka wa fedha 2015/16 Serikali imeshuhudia mchango mkubwa wa kifedha na kitaalam toka Benki ya Dunia.

“Napenda kuchukua fursa hii kuishukuru Benki ya Dunia kwa msaada wake mkubwa wa kitaalam na kifedha kwani mpaka sasa Serikali iko katika majadiliano na Benki ya Dunia ili kuboresha bandari yetu ya Dar es Salaam,” amesema Dkt. Dkt. Likwelile.

Aidha Dkt. Likwelile amezitaka Taasisi zote zinazopata fedha kutoka Benki ya Dunia zitumie fedha hizo vizuri ili ziweze kuwanufaisha walengwa na kuleta tija kwa Taifa.

Benki ya Dunia inaisaidia Serikali ya Tanzania kwa kutoa ushauri wa kitalaam pamoja na fedha kupitia miradi yake mbalimbali ili iweze kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kupambana na umaskini hapa nchini.

Watanzania Kumiliki Hisa Katika Kampuni za Mawasiliano Hapa Nchini.

0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma.
Serikali kufanya marekebisho ya Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kieletroniki ili kuwezesha watanzania kumiliki hisa zitakazouzwa na Kampuni za Mawasiliano kupitia soko la hisa.

Hayo yamesemwa leo Bungeni  Mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Pichani)alipokuwa akiwasilisha Bungeni  muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2016.

“Mhe. Naibu Spika, sehemu ya nne inapendekeza marekebisho katika sheria ya Posta na   Mawasiliano ya Kielektroniki, sura 306 kama ifuatavyo, kufuta kifungu cha 6(2d) na kukiandika upya ili kuweka sharti kwa kampuni za mawasiliano kuwasilisha Katiba ya Kampuni itakayothibitisha muundo wa umiliki wa hisa kama mojawapo ya taarifa zinazopaswa kuwasilishwa wakati wakuomba leseni,” alifafanua Mhe. Mpango.

Aidha Mhe. Mpango aliendelea kwa kusema kwamba, watoa huduma za Mawasiliano ya Kielektroniki watawekewa sharti la kuuza hisa zao kwa Umma na kusajili hisa zao katika soko la hisa Nchini Tanzania ili kutoa fursa kwa watanzaniai kununua hisa na kumiliki asilimia 25 ya Kampuni hizo.

Kutokana na marekebisho ya sheria hiyo, kampuni za huduma za Mawasiliano ya kielektroniki ambazo tayari zimesajiliwa hapa Nchini zitawajibika kujioredhesha katika soko la hisa na kuuza hisa zao ndani ya kipindi cha miezi sita kuanzia Julai 01, 2016.
 
Vile vile kampuni ambazo zitasajiliwa baada ya Julai 01, 2016 zitawajibika kuuza hisa zao na kujioredheshsha katika soko la hisa ndani ya kipindi cha Miaka miwili kuanzia Julai 01, 2016.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti  Mhe. Hawa Ghasia amesema kwamba kamati imekubaliana na marekebisho hayo aidha kamati inaishauri Serikali  kuweka tafsiri ya watanzania ili kuwezesha hisa hizo kuuzwa kwa watanzania  pekee na pia kuangalia suala la miezi sita kwa makampuni yaliyosajiliwa lisilete utata kwenye utekelezaji wake.

Rais Mgufuli Afanya Uteuzi Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Na Mamlaka ya Uvuvi

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 23 Juni, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi inasema uteuzi huu umeanza tarehe 21 Juni, 2016.

Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Cuthbert Mhilu ambaye amemaliza muda wake. Prof. Maboko ni Mhadhiri wa Jiolojia katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Omari Ali Amir kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Omari Ali Amir alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
 
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi inasema uteuzi wa Dkt. Omari Ali Amir umeanza tarehe 21 Juni, 2016.

Utaratibu wa kujaza nafasi ya Mkurugenzi Mkuu na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa bahari kuu ni wa kubadilishana kila baada ya miaka mitatu kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, ambapo Mkurugenzi Mkuu akitoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi Naibu Mkurugenzi Mkuu hutoka upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kinyume chake.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images