Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Katibu Mkuu CHADEMA, Dr. Vincent Mashinji aripoti rasmi ofisini Kwake

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), DR.Vincent Mashinji jana ameripoti rasmi kwenye ofisi yake mpya jijini Dar es Salaam na kupokelewa na viongozi mbalimbali waandamizi wa chama hicho akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salumu Mwalimu.
Watendaji wa Makao Makuu wakimkaribisha Katibu Mkuu Dr. Vicent Mashinji jana.Hii ni tokea katibu Mkuu huyo kuchaguliwa kwake kwenye mkutano wa Baraza Kuu CHADEMA, uliofanyika jijini Mwanza Machi 12 mwaka huu.
Watendaji wa Makao Makuu wakimkaribisha Katibu Mkuu Dr. Vicent Mashinji. Anayemfuatia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salumu Mwalimu.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya April 13

Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Ukosefu Na Upungufu Wa Nguvu za Kiume

$
0
0

Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  

Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.

Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kufahamu   kuhusu   SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME  tafadhali  tembelea :

Ukisoma  vizuri  kuhusu  mfumo  wa  nguvu  za  kiume, utagundua  kuwa   Suala  la  nguvu  za  kiume  ni  suala  la  kimfumo.  Ili  mwanaume  awe na nguvu  za  kiume, aendelee  kuwa  na  nguvu  za  kiume na  azilinde  nguvu  zake za  kiume, ni  lazima  ogani  zote zinazo  husika  na  mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ziwe  na  afya  njema  na  ziwe  na  ushirikiano   thabiti  na  wenye  afya.

Vile  vile , utagundua  kuwa , mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ni  kama  ifuatavyo:

i.Mishipa  imara  ya  ubongo  na  yenye  afya  njema

ii. Mishipa  imara  ya  uti  wa  mgongo  (  spinal  cords )

iii.Mishipa  imara  itumikayo  kusafirisha  damu  mwilini  (  Blood Vessels )

iv. Mfumo  imara  wa  usafirishaji  damu  mwilini

v. Mishipa  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema

vi. Uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  ubongo, mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume.

Hivyo  basi, ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, na  aendelee  kuwa  na  nguvu  hizo ni  lazima  mambo  yote  muhimu  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume  yawe  imara  pasi na  hitilafu  yoyote.

Hitilafu  yoyote  katika  mambo  hayo, itasababisha  ukosefu na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume  kwa  mwanaume  huyo.  Pale inapotokea    hitilafu  ama  mapungufu  katika  ogani  zaidi  ya  moja  kati  ya  zilizo  tajwa hapo  juu, basi  tatizo  kwa  muhusika  huwa  kubwa  mara  dufu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU &  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Mwanaume   anapopatwa na  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, ubongo  hutoa  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo  husafirisha  taarifa  hadi  kwenye  mishipa &  misuli  ya  uume.

Mishipa  ya  uume inapopokea  taarifa  hiyo, hutanuka. Na  mishipa  ya  uume  inapotanuka, hufanya  mambo  mawili  muhimu  sana :

i.Husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  hivyo  kuruhusu  damu  kuingia kwa  kasi  sana   ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  imara  bara bara.

ii. Huibinya na  kuiziba  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuzuia  kunyonya  ama  kufyonza  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa ya  uume.  (  KAZI  KUBWA  YA  MISHIPA  YA  VENA  ILIYO  KARIBU NA  MISHIPA  YA  UUME  NI KUHAKIKISHA  HAKUNA  DAMU NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME. HIVYO  BASI  DAMU  INAPOINGIA  NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME, MISHIPA  YA  VENA  HU “SENSE” JAMBO  HILO  KWA  HARAKA  NA HIVYO  KUIFYONZA  DAMU  HIYO  KUTOKA KWENYE MISHIPA  YA UUME  YA  KUITOA  NJE YA MISHIPA  YA  UUME.  NA  DAMU INAPOKOSEKANA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME, HUUFANYA  UUME  KUSINYAA  NA  KULEGEA )

Mtu  anayepiga  punyeto  husababisha  mambo  yafuatayo  katika  mwili  wake :

1. Huuwa  nguvu  ya  mishipa  & misuli ya  uume ambayo  ndio  inayo husika  na  kusimama  kwa  uume

2. Mishipa  ya   uume  inapo  sinyaa  na  kukosa  nguvu  yake  ya  asili, husababisha  mambo  yafuatayo :

i.Huondoa  uwezo  wa  mishipa  &  misuli  ya  uume  kutanuka, na  hii  ndio  sababu  inayo  wafanya  waathirika  wa  punyeto  kutumia  nguvu  nyingi  sana  katika  kuufanya  uume  usimame.

ii.Huondoa  uwezo  wa  mishipa &  misuli  ya  uume  kuibana  na  kuiziba  mishipa  ya  vena, na  hii ndio  sababu  inayo  fanya  waathirika  wa  punyeto  kufika  kileleni  haraka  sana, kwani damu  inayo  ingia  kwenye misuli  ya  uume   hufyonzwa  ndani ya  muda  mfupi sana. 
 
 Hii  hutokea  kwa  sababu  mishipa na  misuli  ya  uume inakuwa  imelegea,na  mishipa  ya  vena inakuwa  imepwaya, hivyo  msuguano wowote ule  hufanya  mishipa  ya  vena  kufunguka  na  kufyonza  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  na hivyo  kuufanya  uume  kusinyaa  ndani ya dakika ama sekunde  chache sana.

3. Vile  vile  punyeto  hufanya  uume  kusinyaa na  kurudi ndani  na  kuufanya  uonekane kama  uume  wa  motto mdogo.

Kwa  ufupi  punyeto  husababisha  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuu  zifuatazo :

i.Kwanza   hudhoofisha  na  kuharibu  mishipa  ya  uume,  ambayo  ndio  hufanya  uume kusimama.

ii.Pili  hudhoofisha  utendaji  kazi  wa  mishipa  ya  ateri, ambayo  ndio  hutumika  kama  njia  ya  kusafirisha  damu kupeleka kwenye  misuli  ya  uume  na  ivyo  kuufanya  uume  usimame

iii. Tatu, punyeto  hupelekea  kuvuja  kwa  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kusababisha  damu  kufyonzwa  kwa  haraka  sana  kila  iingiapo ndani  ya  misuli ya  uume  na  matokeo  yake  ni  uume   kusimama  kwa  muda  mfupi  sana  wakati wa  tendo  la  ndoa.

iv. Punyeto  huathiri  mtiririko  wa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume, kwa  sababu  hudhoofisha  misuli &  mishipa  ya  uume  pamoja  na mishipa ya  ateri  ambayo  ndio  hutumika  katika  kusafirisha  damu kwenda  kwenye  uume

DALILI  ZA  MTU  ALIYE  ATHIRIWA  NA  PUNYETO
Dalili  kuu  za  mtu  aliye athiriwa  na  punyeto  ni  kama  ifuatavyo:

i.           Uume  kusinyaa  na  kuwa  kama  wa  mtoto
ii.         Uume kurudi  ndani
iii.       Uume  kusimama  ukiwa  legelege
iv.       Kufika  kileleni  haraka  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

TIBA   YA   NGUVU  ZA  KIUME  KWA MTU  ALIYE  ATHIRIKA  NA  PUNYETO.
Dawa   asilia  ya  nguvu  za  kiume iitwayo JIKO  ni tiba  bora  na  ya  uhakika  kabisa  kwa  mtu  aliye  athiriwa   na  punyeto.  Dawa  hii, pamoja  na  mambo  mengine  mengi, husaidia  kufanya  mambio  yafuatayo  katika  mwili  wa  mwanaume  aliye  athiriwa  na  punyeto :

i.Kuimarisha  mishipa  & misuli  ya  uume  ulio  legea na  hivyo  kuurejeshea  uwezo wake wa  asili

ii. Hutibu   tatizo  la  uume  kurudi  ndani

iii.Humaliza  tatizo  la  kusimama  kwa  uume  ukiwa  legelege

iv.Hutibu  na  kuponya  kabisa  tatizo  la  kufika  kieleleni  haraka.

BEI  YA  DAWA  :  Dawa  hii  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU (Tsh. 80,000/=)

MAHALI  INAPOPATIKANA :  Dawa  hii  inapatikana  katika  duka  la  dawa  asilia  liitwalo  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  UBUNGO   nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA   karibu  na SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING.

Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu. Watafikishiwa  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  DAR  ES  SALAAM.

Kwa   wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  MABASI

Kwa  wateja  waliopo   Zanzibar  wata fikishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa boti.

Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  ama  DHL.

MAWASILIANO :  WASILIANA  NASI   KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee kila  siku  kwenye  blogu  yetu :

Polisi Wakwama Kuuwasilisha Mkataba wa Lugumi.....Wabunge Watoa Siku 3 Mkataba Huo Upelekwe

$
0
0

BUNGE limetoa siku tatu kwa Jeshi la Polisi kuwasilisha kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) mkataba wa Kampuni Lugumi Enterprises wenye thamani ya Sh bilioni 37.

Hatua hii inakuja siku mbili baada ya jeshi hilo kudaiwa kukaidi agizo la kamati hiyo, iliyotaka likabidhi nyaraka za utekelezaji wa mkataba ufanyiwe tathmini kutokana na malalamiko yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali(CAG) katika hesabu za mwaka 2013/2014.

Akizungumza jana na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Aeshi Hilaly alisema agizo la kamati la kutaka mkataba huo, lilitolewa wiki iliyopita kuwezesha wabunge kuangalia utekelezaji wake.

“Jana (juzi) ilikuwa siku ya mwisho kwa jeshi kuwasilisha mkataba huo ofisi za Bunge, lakini mpaka leo (jana) muda huu ninapozungumza nanyi (saa 7:30 mchana) walikuwa hawajawasilisha. “

"Siku zote tumekuwa tukitoa maagizo kwa mdomo na taasisi nyingi zimekuwa zikitekeleza, lakini hili la mkataba wa Lugumi naona kwa wenzetu limekuwa gumu, hivyo tumeamua kuwakumbusha kwa maandishi,” alisema.

Alisema kamati hiyo imetoa siku tatu tangu barua itakapopelekwa na ofisi za Bunge, kuhakikisha wanatekeleza agizo hilo ili kamati hiyo iweze kupitia utekelezaji wa mkataba huo na baadaye kupeleka mapendekezo kwenye Bunge.

“ Katika suala hili, Kamati haitarudi nyuma, hivyo tunawaomba wenzetu wa Jeshi la Polisi kutupa ushirikiano, si jambo la peke yangu kuamua, ni la Bunge, baada ya kupitia tunapeleka mapendekezo bungeni ambalo ndilo litakaloamua nini kifanyike,” alisisitiza.

Kamati ya PAC ilipokuwa ikipitia hesabu za Jeshi la Polisi, ilibaini kuwapo mkataba tata wa Kampuni ya Lugumi Enterprises .

Kupitia mkataba huo wa mwaka 2011, Kampuni ya Lugumi Enterprises ilipewa zabuni ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi 108 nchini kwa gharama ya Sh bilioni 37.

Inadaiwa kampuni hiyo imekwishalipwa Sh bilioni 34 kati ya Sh bilioni 37 ikiwa ni sawa na asilimia 99 ya fedha zote, huku ikiwa imefunga mashine katika vituo 14 pekee katika jiji la Dar es Salaam, ambavyo pia inadaiwa havijulikani maeneo vilipo.

Wabunge Wadai TANAPA Ni JIPU....Washangaa Shirikia Hilo la Umma Kuwa na Matumzi Makubwa Kuzidi Makusanyo

$
0
0

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limeingia kwenye orodha ya Taasisi za Serikali zenye matumizi makubwa ya fedha ukilinganisha na mapato wanayokusanya, jambo lililoishtua Kamati ya Bunge na kutaka shirika hilo lipunguze matumizi yake.

Hayo yalibainika jana Dar es Salaam wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), ilipokutana na Tanapa kupitia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2013/14.

Katika ripoti hiyo ilibainika kwamba Tanapa kwa mwaka huo wa fedha, ilitumia jumla ya zaidi ya Sh bilioni 151.7 ilhali mapato yao yalikuwa Sh bilioni 149.9 hivyo matumizi ya fedha yaliyozidi ni Sh bilioni 1.8.

Taasisi nyingine ya Serikali ambayo ilikuwa na matumizi makubwa ya fedha za Serikali ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo ripoti ya CAG ya mwaka 2013/14 ilionesha kuwa ilitumia Sh bilioni 18.6 kwa ajili ya matumizi ya watumishi wake.

Wakichangia hoja mbalimbali wakati wa kupitia ripoti hiyo hapo jana, Wajumbe wa Kamati hiyo walisema kutokuwepo Bodi ya Shirika hilo, kunachangia watendaji wa shirika hilo kuliendesha ndivyo sivyo.

Mjumbe wa Kamati hiyo, Albert Obama, mbunge wa Muhigwe alisema shirika hilo ni jipu kwa sababu limejilimbikizia ulaji, kana kwamba ni chombo cha watu wachache, ilhali shirika hilo linatakiwa liwe kwa ajili ya ustawi wa uchumi wa nchi.

“Haiwezekani ripoti ya mwaka 2013/14 inaonesha kuwa mapato yenu yalikuwa Sh bilioni 149.9 halafu matumizi yenu ni Sh bilioni 151.8”, yaani mnatumia chote hadi mnadaiwa sasa hii sio sawa, hili ni shirika la umma?” Alihoji Obama.

“Hapa wanakuja na maneno matamu kwamba bajeti ya mwaka huu 2016/17 wamepanga kukusanya mapato ya Sh bilioni 188 lakini matumizi yenu pia mmeainisha yatakuwa Sh bilioni 270, hii ikoje? " Alihoji Obama.

Mjumbe mwingine, Joseph Kakunda mbunge wa Sikonge, alisema Tanapa haina changamoto kubwa, zinazoifanya ishindwe kukusanya mapato makubwa zaidi ya hayo ya sasa na kusema walipaswa kukusanya zaidi ya Sh trilioni moja na sio hizo bilioni 149.

Mrema Ajitokeza Kwa Mara Nyingine Tena Kumkumbusha Rais Magufuli Ampe Kazi Yoyote

$
0
0

Mwenyekiti wa TLP taifa Dkt. Augustino Lyatonga Mrema amesisistiza ombi lake la kazi kwa kumkumbusha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwamba ampe kazi yoyote amsaidie kibarua kigumu alichonacho cha kuwahudumia wananchi

Dkt. Mrema ameyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na EATV kuhusu miaka 32 ya kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Edward Moringe Sokoine ambaye alihudumu kwenye awamu ya kwanza ya Mwl. Julius Nyerere ambapo alifariki akiwa na cheo cha waziri mkuu tarehe 12.04.1984 kwa ajali ya gari.

''Namkumbuka Sokoine kama mtu wa watu aliyehudumia watu, aliyepambana na ufisadi na magendo .Alikuwa anatenda haki kwa wananchi wote .

"Hata mimi nilipokuwa waziri wa mambo ya ndani na naibu waziri mkuu nilijaribu kufanya kama yeye bahati mbaya sikufanikiwa kama yeye kwa sababu sikuwa waziri mkuu au Rais''- Alisisistiza Mrema.

Kuhusu Mrema kuomba kazi kwa Dkt. Magufuli 
Mrema alisema kwa kutambua rekodi yake ya utendaji kazi wa  Rais Dkt. Magufuli, aliwahimiza wananchi wa Vunjo wamchague kipindi cha kampeni na yeye akampigia kampeni na Rais akawaambia wananchi wa Vunjo kwamba Mrema akikosa ubunge atapangiwa kazi nyingine ndiyo hiyo wananchi wanaulizia.

Aidha Mrema alisema kuna maeneo ambayo yeye anafiti siyo lazima apewe madaraka makubwa 

"Mimi sihitaji ukuu wa mkoa au uwaziri, anipe kazi yoyote na nikionana naye nitamkonyeza maeneo ambayo ninafiti ili nimsaidie kutumbua majipu." Alisema Mrema

Hata hivyo Dkt. Mrema alimpongeza Dkt. Magufuli kwamba ni mtendaji ambaye ameamua bila kusukumwa kupambana na mafisadi na kwamba yeye ni alfa na omega na kazi hiyo ameonyesha kwamba atafanya vizuri kuliko Sokoine na Mrema.

Dereva TAXI Atiwa Mbaroni akituhumiwa Kubaka abiria

$
0
0

DEREVA teksi katika Manispaa ya Iringa, Elain Mahenge (27), anashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumbaka mteja wake.

Mahenge, Mkazi wa Semtema, Kihesa katika Manispaa ya Iringa, anadaiwa alikutwa akifanya kitendo hicho dhidi ya mteja wake  saa 3:45 usiku.

Kitendo hicho cha ubakaji kimetokea ikiwa imepita takriban miezi miwili, tangu Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Iringa, kutoa elimu kwa wananchi wa Kihesa juu ya kuwafichua watu wanaodaiwa kufanya vitendo vya ubakaji.

Elimu hiyo ilitolewa kutokana na kuripotiwa kukithiri kwa vitendo hivyo, ikiwamo dhidi ya watoto wa kike na kuwalawiti watoto wa kiume, huku zaidi ya watu 10 wakiwa wameshakamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kujihusisha na unyama huo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Peter Kakamba, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita, katika eneo la Kihesa. Alisema mtuhumiwa alikutwa akimbaka mteja wake huyo, ambaye ni mkazi wa Mgololo, Mufindi mkoani Iringa.

Kakamba alisema mteja huyo alimkodi dereva huyo, baada ya kushuka kwenye gari katika kituo kikuu cha mabasi cha Iringa na kumtaka ampeleke kwenye nyumba ya kulala wageni iliyoko Kihesa.

“Inadaiwa dereva teksi huyo alimchukua stendi hapo na kwenda alikoambiwa ampeleke lakini alipofika njiani kwenye giza alisimama na kisha kumbaka binti huyo,” alisema.

Kamanda Kakamba alisema wakati dereva huyo akiendelea kufanya kitendo hicho, binti huyo alipiga kelele ambazo zilisikika na askari polisi ambao waliokuwa doria usiku huo na wakati polisi wanafika eneo la tukio tayari mtuhumiwa alikuwa ameshamaliza kufanya kitendo hicho na ndipo walipomkamata.

Alisema kuwa mtuhumiwa yuko polisi na ushahidi umeonekana pale pale kwa kuwa mazingira na hali waliyokutwa nayo dereva na binti huyo, yalidhihirisha mtuhumiwa alitenda jambo hilo bila ya huruma tena kwa mteja wake, hivyo mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakani wakati wowote kuanzia sasa.

Aidha kamanda huyo aliwataka wakazi wa mji wa Iringa na viunga vyake kupanda teksi ambazo zimesajiliwa na si kupanda teksi bubu kama aliyokuwa ameipanda msichana aliyefanyikwa unyama huo.

Kikwete Afunguka Kuhusu Maisha ya uraiani.....Asema anajiandaa kumuachia chama Rais Magufuli ili yeye Abaki mzee mashuhuri

$
0
0

Ikiwa ni takriban miezi mitano tangu kutoka madarakani, Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, amesema kwa sasa anafurahia maisha ya uhuru baada ya kustaafu kwake na kwamba anajiandaa kuwa mzee mashuhuri nchini atakapokabidhi chama.

Kikwete alistaafu rasmi Novemba 5, mwaka jana baada ya kuapishwa kwa Rais wa awamu ya tano, Dk. John Magufuli, ambaye anatarajiwa kukabidhiwa Uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Juni, mwaka huu.

Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Kikwete alisema maisha nje ya Ikulu ya Magogoni, ni mazuri kwa sababu ametua mzigo wa kuhudumia watu milioni 50 na kwamba sasa anaendelea na mambo yake binafsi.

“Maisha baada ya kutoka madarakani, ni mazuri kwa sababu sina presha niliyokuwa nayo, nilikuwa na mzigo mkubwa wa kuangalia taifa hili la watu milioni 50, siyo mzigo mdogo, ni kazi kubwa, una hili, una hili unarudi nyumbani…

“Sasa hivi unarudi nyumbani hauna faili, ninafanya mambo ninayoyapanga mimi, na shughuli ninazofanya ni za kimataifa tu, niko kwenye hili la Libya (mjumbe wa usuluhishi wa mgogoro wa Libya), naondoka karibuni, tuna mkutano Marekani wa mambo ya malaria.

“Nipo kwenye Kamisheni ya Elimu na Waziri mkuu Gordon Brown, (Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza), pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, nafanya shughuli nyingi tu sasa hivi," alisema na kuongeza:

“Kuhusu siasa, bado ni Mwenyekiti wa CCM na baada ya muda, nitakabidhi (chama) baada ya hapo kila kitu nitamuachia mzee Magufuli aendelee nayo, mimi nitabaki ni mzee tu maarufu katika nchi yetu, maisha ni mazuri tu."

Novemba, mwaka jana, baada ya kutoka madarakani, Kikwete kwa mara ya kwanza alionekana eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam alipokwenda kufanya manunuzi na mkewe Salma.

Baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa Kikwete alikuwa amevalia suti maarufu kama ‘kaunda suti’ ya rangi nyeusi, alionekana akiingia katika viunga vya Mlimani City saa 5:00 asubuhi.

Mashuhuda wa tukio hilo, walisema Kikwete aliwasili katika maeneo hayo akiwa katika msafara wa magari manne na pikipiki moja.

Hatua hiyo ilionekana kushangaza baadhi ya watu waliokuwapo katika maeneo hayo, huku wengi wao wakionekana kutaka kumsalimia.

Akiwa kwenye eneo hilo, Kikwete na mkewe, waliingia katika maduka ya Game na kufanya manunuzi kwa dakika zisizopungua 10 hadi 15 na baadaye kutoka nje na walinzi wake wakionekana kubeba mifuko iliyokuwa na bidhaa walizonunua.

Kama ilivyo hulka ya Rais Kikwete, alipotoka nje ya duka hilo, alianza kusalimiana na mtu mmoja ambaye alionekana kufahamiana naye.

Hatua hiyo ilimpa fursa ya kuwasalimia watu wengine waliokuwa karibu na tawi la benki moja.

Baada ya hapo, msafara wake uliondoka na kuelekea barabara ya Sam Nujoma.

Tangu achaguliwe kuwa Rais mwaka 2005, itifaki na majukumu yake ya urais, yalikuwa yakimbana Rais Kikwete na hivyo kushindwa mambo yake binafsi kama walivyo raia wengine.

Aidha, tangu alipoachia kiti cha urais na kumkabidhi Dk. Magufuli baada ya kuapishwa Novemba 5, mwaka jana, Kikwete amekuwa akiishi nyumbani kwake Msoga mkoani Pwani na mara chache amekuwa akienda Ikulu kuteta na Rais Magufuli.

Kikwete aliondoka rasmi Ikulu na familia yake Novemba 6, mwaka jana na kuanza maisha mapya kijijini kwake Msoga.

Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Wamkana Anne Kilango Malecela.....Wadai Hata wao Walishangaa Sana Aliposema Shinyanga Haina Watumishi Hewa

$
0
0

Siku moja baada ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango kuvuliwa uongozi kwa kutosema ukweli, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Hawa Ng’humbi ameiruka taarifa ya kutokuwapo kwa watumishi hewa, ambayo amesema ilimshtua alipoiona kwenye televisheni. 

Mkoa wa Shinyanga unaundwa na wilaya tatu ambazo ni Shinyanga, Kishapu na Kahama zinazoundwa na halmashauri sita ambazo ni Kishapu, Manispaa ya Shinyanga, Mji wa Kahama, Ushetu, Msalala na Shinyanga Vijijini. 

Rais John Magufuli juzi alitengua uteuzi wa Kilango, ikiwa ni siku 30 tangu alipotangaza kumteua kwa maelezo kuwa alitoa taarifa isiyo ya kweli kuwa Shinyanga hakuna watumishi hewa kabla ya kujiridhisha.

 Pamoja na Kilango, Rais Magufuli pia alitengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Shinyanga, Abdul Dachi, kwa sababu hiyo ya kutoa taarifa za uongo.

 Dk Magufuli alichukua uamuzi huo baada ya kutuma timu mkoani Shinyanga kufanya uhakiki na kubaini kuwa kulikuwa na watumishi hewa 45 katika wilaya moja ya Shinyanga kabla ya kwenda wilaya nyingine za Kahama na Kishapu. 

Akizungumzia sakata hilo jana baada ya uamuzi wa Dk Magufuli, Ng’humbi alisema taarifa za kukosekana watumishi hewa kwenye wilaya yake alizisikia kwenye taarifa ya habari ya televisheni Machi 30 na zilimshtua.

 “Binafsi nilishtuka sana nilipoona ikitangazwa kuwa mkoa mzima wa Shinyanga, hakuna mfanyakazi hewa wakati mimi sikuwa hata nimeona taarifa kutoka wilayani kwangu iliyoandaliwa na uongozi wa halmashauri,” alisema Ng’humbi. 

“Nilijiuliza taarifa imefikaje kwa mkuu wa mkoa bila kupitia kwangu? Kusema kweli nilianza kuifanyia kazi taarifa hiyo na ninatarajia ifikapo Ijumaa nitakamilisha kazi hiyo.” 

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Alphonce Gagambobyaki alisema hadi sasa ofisi yake haijafahamu nani aliyempa mkuu wa mkoa taarifa ya ukaguzi wa wafanyakazi hewa kwa sababu taarifa aliyonayo mezani haijasainiwa.

 “Kuna tatizo la ofisi hii kukaimiwa na zaidi ya watu wanne tangu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji, Dalikunda Kimulika alipostaafu Februari. Ni vigumu kujua nani alihusika nayo bila kuona saini,” alisema Bagambobyaki. 

Alisema taarifa hiyo inaonekana haikusainiwa kutokana na hofu baada ya watumishi waliobainika kutokuwapo kwenye vituo vyao vya kazi karibu wote kuonekana kuwa na ruhusa maalumu.

“Wakati bado tunajiridhisha kujua ni ruhusa ya aina gani na hawa watumishi wako wapi, ndipo taarifa ilipotangazwa kwamba mkoa hauna watumishi hewa,” alisema.

Hata hivyo, alisema anaamini taarifa sahihi itajulikana baada ya timu maalumu iliyotoka Tamisemi kukamilisha uhakiki wilayani humo jana. 

“Timu ile ya Tamisemi imekwenda mbele zaidi katika uhakiki wake kwa kukagua mtumishi mmoja mmoja hadi vijijini na imekamilisha kazi yake jana,” alisema Bagambobyaki. 

Kuhusu iwapo aliyekuwa mkuu wa mkoa alitumia taarifa zao au la? kaimu mkurugenzi huyo alisema: “Iwapo RC alitumia taarifa zetu au la, hilo siwezi kulisemea kwa sasa.”

Kilango ambaye juzi alisema hakuwa amepata taarifa hivyo asingeweza kuzungumzia kutenguliwa kwake, jana alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kabisa na Dachi akaeleza kuwa ameupokeauamuzi huo kwa kuwa Rais ndiye mteule wake. 

Taarifa ya kutenguliwa kwa watumishi hao wa umma sasa imekuwa kaa la moto kwa wakuu wa wilaya makatibu tawala wao, na wakurugenzi watendaji wa halmashauri za mkoa huo.

Alipoulizwa kuhusu taarifa hizo za watumishi hewa, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro alisema hawezi kuzungumzia lolote.

“Sisemi lolote na wala sizungumziii mkoa,” alisema na kukata simu ambayo haikupokewa tena. 

Kama ilivyokuwa kwa mkuu wake wa wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Shinyanga, Lewis Kalinjuna aligoma kuzungumzia uwezekano wa halmashauri yake kutoa taarifa zilizompotosha Kilango.

“Sitaki kulizungumzia hilo, nawaachia wanaolijua walizungumzie,” alisema Kalinjuna.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Vita Kawawa alikata simu yake mara kadhaa alipopigiwa na baadaye kutuma ujumbe mfupi wa maneno akisema yuko kwenye kikao na kuelekeza atumiwe ujumbe ambao hata alipotumiwa hakujibu.

Watendaji Waongoza Kwa Kuomba Rushwa Pwani

$
0
0

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU)mkoani Pwani imesema serikali ya mitaa katika mamlaka za watendaji wa vijiji ,mitaa na kata inaongoza katika vitendo vya rushwa huku wilaya ya Bagamoyo ikielezwa inaongoza kimkoa .

Aidha idara nyingine zinazoongoza katika vitendo hivyo ni sanjali na idara ya afya,polisi,mahakama,ardhi,sekta binafsi,elimu,tanesco,fedha,vipimo,uhamiaji na maji.

Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa ofisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia january hadi march mwaka huu,kwa waandishi wa habari jana,kamanda wa TAKUKURU mkoani hapo,Suzana Raymond ,alisema walipokea malalamiko 64 kwa kipindi hicho.

Alielezea kuwa kati ya malalamiko hayo malalamiko 49 yanahusiana na vitendo vya rushwa na uchunguzi wake unaendelea ambapo 15 kati ya yake hayahusiani na vitendo vya rushwa.

Kamanda Suzana alisema idara inayoongoza kwa malalamiko ya vitendo hivyo ni serikali ya mitaa ambayo ina malalamiko 18,ikifuatiwa na afya yenye malalamiko 8,polisi matano na Mahakama matatu.

Alitaja upande wa idara ya ardhi imelalamikiwa makosa matatu,sekta binafsi matatu,elimu mawili,tanesco mawili,fedha moja,vipimo moja,uhamiaji moja na maji moja.

“Watuhumiwa hao wengi wao wanalalamikiwa kwa kutumia vibaya mamlaka,kushiriki kuuza ardhi kinyume na taratibu,kutumia fedha za mapato ya kijiji ,mitaa na kata kiholel wakati ni matumizi mabaya ya fedha hizo”alielezea Suzana.

Alisema jumla ya kesi mpya nne zilifunguliwa kwenye mahakama za wilaya na polisi huku kesi 22 zinaenelea kusikilizwa katika mahakama hizo.

Aidha kamanda Suzana alieleza kuwa katika kipindi cha july-september  mwaka 2015 kulikuwa na malalamiko ya vitendo vya rushwa 50 na octoba hadi desemba mwaka huo idadi ya vitendo vya aiina hiyo ilikuwa ni 45.

Hata hivyo taasisi hiyo mkoani Pwani katika kushughulikia kero za wananchi kwenye maeneo yanayoongoza kulalamikiwa ni kuendelea kufanya uchambuzi wa mifumo ili kubaini mianya ya rushwa na kutoa ushauri kwa idara husika na serikali kwa lengo la kuziba mianya iliyopo.

“Tunaendelea pia kutoa elimu kwa umma,kwasasa tumekuwa na utaratibu wa kwenda vijijini kusikiliza kero na malalamiko.

“Kwa malalamiko ambayo hayahusiani na vitendo vya rushwa tunafikisha katika idara yenye dhamana pia idara itaendelea kufanya uchunguzi pale ushahidi utakapopatikana mtuhumiwa ama watuhumiwa watafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake”alisema kamanda Suzana.

Akizungumzia suala la kutoa elimu katika jamii ,Suzana alisema ofisi yao ilielimisha jumla ya wananchi 4,443 kwa njia ya semina 47 na mikutano ya hadhara 11,kuimarisha klabu za wapinga rushwa 30 katika shule za sekondari na msingi mkoani humo.

Suzana alitoa wito kwa jamii kuwa kila mwananchi anapaswa kutambua anao wajibu wa kupambana na rushwa katika eneo lake kwa kukataa kutoa ama kupokea rushwa na kuwaomba watoe taarifa kwa taasisi mara wanapobaini kuna mtu anashiriki vitendo hivyo.

Vijiji 42 Ruangwa Kupatiwa Umeme- Waziri Mkuu Asema

$
0
0

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Kassim Majaliwa amesema vijiji 42 vya wilaya ya Ruangwa vitaunganishiwa umeme katika Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini (REA) awamu ya tatu.

Amesema hadi sasa tayari vijiji 48 vya wilaya hiyo vimeunganishiwa umeme na kwamba lengo lake ni kuhakikisha vijiji vyote 90 vinapata huduma hiyo, hivyo amewaomba wananchi kuendelea kuwa na subira.

Waziri Mkuu, Majaliwa ameyasema hayo jana alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Michenga, Chinongwe, Makanjiro na Chinokole katika mikutano ya hadhara aliyoifanya wilayani Ruangwa.

“Niliwaahidi kuwatumikia, kuwahudumia na kuwasemea ndani na nje ya nchi, nawahakikishia kuwa sitowaangusha hivyo endeleeni kuwa na subira, nitafanya mambo mengi ya maendeleo kama isemavyo kauli mbiu yangu, Ruangwa kwa maendeleo inawezekana.” amesema.

Kwa upande wake Meneja wa TANESCO mkoa wa Lindi, Sotco Nombo amesema tarehe 15 mwezi huu wataanza kusambaza vifaa katika kijiji cha Chinongwe na kwamba hadi kufikia mwezi Mei mwaka huu umeme utakuwa umewaka katika kijiji hicho.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu, Majaliwa amewasisitiza wananchi kuanza kulima kwa wingi zao la muhogo kwa sababu kuna soko la uhahika la zao hilo baada ya kujitokeza kwa wafanyabiashara kutoka China na Marekani wanaotaka kununua zao mihogo nchini.

“Mnataka hela, mnataka hela? ila lazima mfanye kazi…mimi nimewatafutia hela nawaomba mlime mihogo kwa wingi maana kuna wafanyabiashara wanataka kununua mihogo, hela ndiyo hiyo ambayo ni soko la uhakika la mihogo. Nawasihi mchangamkie dili hili,” amesema.

Amesema wafanyabiashara hao wanataka kununua mihogo kutoka wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Liwale kwa ajili ya kusaga unga na kutengeneza vyakula vingine vitokanavyo na zao hilo, hivyo amewaomba wananchi hao kuchangamkia fursa hiyo na kulima mashamba makubwa ya mihogo.

Askofu Josephat Gwajima Apinga kauli ya mkuu wa Mkoa wa Arusha ya Kutaka kuyadhibiti Makanisa ya kilokole katika Makazi ya watu.

$
0
0
April 6 mwaka huu, mkuu wa mkoa wa Arusha mh. Daud Felix Ntibenda alitoa amri ya kuyadhibiti makanisa ya kilokole jijini Arusha kwa madai kuwa yanawasumbua wananchi kwa kupiga vinanda na kuimba usiku kucha.

Ntibenda alitoa  amri  hiyo  ofisini kwake   wakati akizungumza na wenyeviti wa serikali za mitaa na watendaji wa mitaa yote ya jiji la Arusha.

Alisema hataweza kuvumilia makanisa hayo kuzinduliwa kila mahali katika makazi ya watu na kufanya ibada usiku kucha.

"Mimi ni mkristo, sikatazi waumini kusali, lakini nataka kuwe na utaratibu maalumu, sio kila kukicha unakuta kanisa jipya na kibaya zaidi yanasumbua hata wageni wanaoingia jijini hapa." Alisema Ntibenda.

Kutokana na kauli hiyo ya mkuu wa mkoa, Askofu Mkuu wa Kanisa na Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima  amejitokeza hadharani kupinga kauli hiyo huku akihoji kuna baa ngapi mitaani zinazopiga kelele kushinda hata makanisa ya kilokole.

Gwajima amesema Tanzania ni nchi huru, na kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, kila mtu ana haki ya kuabudu muda wowote na wakati wowote atakao bila kuingiliwa na mtu yeyote.

Amesema waumini wa makanisa ya kilokole Tanzania wako zaidi ya milioni 11, hivyo kuwazuia kuabudu ni sawa na kutafuta matatizo mengine.

Gwajima  amesema waumini wa Kiislam huamka saa kumi usiku kuswali kwa sauti kubwa na hakuna mtu huwaingilia kwa  sababu  hiyo ni haki yao kikatiba.

Zaidi, Bonyeza hapo chini kumsikiliza  Gwajima akiongea

Mjambazi watatu wauawa na Jeshi la Polisi Kahama, Shinyanga

$
0
0
Jeshi la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga limefanikiwa kuuwa Majambazi watatu yaliokuwa yamevami duka la mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Emmanuel Mukumbo na kumuua kwa risasi ambapo majambazi hayo yalianza kujibizana risasi na Polisi baada ya raia wema kuijulisha polisi na kufika katika eneo la tukio.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kahama Bw.Vita Kawawa, amesema katika tukio hilo raia mwingine mmoja alipigwa risasi na majambazi hao na kupoteza maisha wakati akipelekwa hospitali huku akilipongeza jeshi la polisi kwa kazi nzuri waliyoifanya.

Akizungumza kwa njia ya simu kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Dismas Kisusi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa jeshi la polisi punde wanapoona dalili zozote za kiuhalifu zinafanyika.

Katika tukio hilo jeshi polisi limefanikiwa kukamata bunduki mbili moja aina ya Short Gun na moja ya kivita aina ya Uzgun, bomu la kutupa kwa mkono, kisu cha kijeshi,risasi sitini,mkandawa kijeshi na magazine mbili za bunduki.

Rais Magufuli Apokea Hati Za Utambulisho Wa Mabalozi Kutoka Nchi Mbalimbali Ikulu Jijini Dar Es Salaam.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa nchi ya Jamhuri ya Czech hapa nchini  Pavel Rezac, tukio hilo lilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Ikulu jijini Dar es Salaam Balozi Mteule wa nchi ya  Jamhuri ya Czech hapa nchini  Pavel Rezac.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Mteule wa nchi ya Jamhuri ya Czech hapa nchini  Pavel Rezac mara baada ya kukabidhi hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi mteule kutoka nchi ya  Jamhuri ya Sudani Kusini Mariano Deng Ngor aliyefika Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha hati yake za utambulisho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Mteule wa nchi ya Jamhuri ya Sudani Kusini Mariano Deng Ngor aliyefika Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha hati yake za utambulisho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Brazil hapa nchini Carlos Alfonso Iglesias Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Mteule wa Brazil hapa nchini Carlos Alfonso Iglesias Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Mteule wa Tanzania nchini Kuwait Mahadhi  Juma Maalim Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi Mahadhi alifika Ikulu kwa ajili ya kuagana na Mhe. Rais kwa ajili ya kwenda kuanza kazi yake hiyo rasmi nchini Kuwait.
Kaimu Mnikulu Ngusa Samike kulia akimkaribisha Balozi Mteule wa Brazil Carlos Alfonso Iglesias Ikulu jijini Dar es Salaam katikati ni Kaimu Mkuu wa Itifaki James Mbwana kutoka Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kikanda na Kimataifa.

PICHA NA IKULU

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yapongezwa Kwa Kuendesha Uchaguzi Mkuu wa 2015 Kwa Amani

$
0
0
Kamati ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala imeipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kufanikisha kuendesha Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015 vizuri na kuiacha nchi ikiwa na Amani, utulivu na Usalama.

Hayo yalisemwa jijini Dar ess Salaam jana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh Najma Murtaza Giga walipokutana na Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere convention Center katika kikao mahsusi cha Kupitia Bajeti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya mwaka wa fedha wa 2016/2017.

Aidha, pongezi hizo kwa NEC zilitolewa na wajumbe wa pande zote mbili yaani wa Chama tawala na wale wa upinzani wa kamati hiyo kwa nyakati tofauti. 

Baadhi ya wabunge hao ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mheshimiwa Najma Murtaza Giga(CCM), Twahir Awesu Mohammed (CUF) na Nassor Suleiman Omar (CUF).

Alisema ni jambo la heri sana pale ambapo taasisi ama mtu anafanya kazi ya kutukuka kupewa sifa yake na kupewa moyo ili aendelee  na moyo wa kufanya kazi kwa bidii na hatimaye kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi  si tu kwa manufaa ya taasisi yake bali hata kwa Taifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhan aliiambia kamati hiyo kwamba haikuwa  kazi rahisi kuendesha na kusimamia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na Nchi ikaendelea kuwa na amani na utulivu kwani ushindani wa kisiasa ulikuwa mkubwa kiasi cha kutishia maisha ya watanzania.

“Tulijitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kufuata Sheria Kanuni na taratibu za kusimamia Uchaguzi pamoja na kwamba Bajeti ilikua haitoshi hasa wakati tunaanza zoezi la Uandikishaji wa Wapiga Kura kwa kutumia Teknolojia ya BVR ambapo tulilazimika kuandikisha wapiga Kura kwa kuhamahama” Alisema Kailima.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Uratibu na Bunge Jenista Mhagama aliwashukuru wabunge kwa niaba ya Serikali kwa jinsi walivyothamini na kutambua Kazi kubwa iliyofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kuahidi kufikisha Serikalini mawazo ya kuitafutia Tume fedha kwaajili ya Tume kuzipatia Asasi za Kiraia zinazotoa Elimu ya Mpiga Kura kwani lilijitokeza suala la Ukosefu wa Fedha za Kuendeshea Elimu hiyo.

Bajeti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 ni jumla ya Tsh 4,830,537.167/= ikiwa ni fedha za matumizi ya kawaida OC Miradi ya Maendeleo pamoja na Mishahara ya watumishi.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ulifanyika tarehe 25 Oktoba ambapo aliyekua Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mh.Dkt John Pombe Magufuli aliibuka Mshindi.

Mahakama Yamtia Hatiani Mbunge wa Jimbo la Ubungo Saed Kubenea....Yampa Adhabu ya Kutotoa Lugha ya Matusi Kwa Kipindi cha Miezi Mitatu

$
0
0

Hatimaye  hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Jamhuri dhidi ya Saed Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo  akidaiwa kumtolea lugha ya matusi Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kindononi imefika tamati.

Thomas Simba, Hakimu Mkazi Mkuu katika Mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam amesema, mahakama hiyo imemtia hatiani Kubenea na kumpa adhabu ya kutofanya kosa linalofanana na hilo ndani ya miezi mitatu.

“Mahakama imejiridhisha kuwa, hilo ni kosa lako la kwanza na kwa kuzingatia nia uliyoenda nayo ya kutatua mgogoro wa wafanyakazi, lakini pia imejiridhisha kwa kutumia ushahidi wa upande wa mashtaka, hivyo inakutaka usifanye kosa linalofanana na  hilo na kuletwa tena mahakamani” amesema hakimu.
 
Amesema kuwa, kila upande upo huru kukata rufaa endapo wataona kuwa hukumu iliyotolewa hawaridhiki nayo, ambapo pale pale jopo la mawakili wa Kubenea likiongozwa na Peter Kibatala, waliiambia mahakama kuwa wanaweka nia ya kukata rufaa kwa sababu ushahidi uliotumika kuhukumu umeacha mashaka mengi.
 
Nje ya mahakama Kubenea amewaambia waandishi wa habari kuwa yeye bado ni Mbunge wa Ubungo na wananchi wa Ubungo wasiwe na hofu kwani hizo ni harakati za siasa.
 
John Mallya, mmoja wa mawakili aliyekuwa akimtetea Kubenea amesema kuwa, mahakama  haikupaswa kuegemea kwenye ushahidi wa polisi peke yake kufikia uamuzi huo kwa kuwa polisi wasingeweza kumpinga Makonda.
 
Amehoji ni kwanini upande wa Jamhuri haukuleta mfanyakazi hata mmoja kutoa ushahidi.
 
Kesi hiyo ilifunguliwa tarehe 15 Desemba mwaka jana baada ya viongozi hao wawili kutofautina kwenye Kiwanda cha nguo cha TOOKU kilichopo Ubungo, jijini Dar es Salaam tarehe 14 Desemba mwaka jana ambapo Kubenea alikamatwa na polisi kwenye eneo hilo kwa amri Makonda.
 
Tukio hilo lilitokea kukiwa na mgomo wa wafanyakazi zaidi ya 1800 wa kiwanda hicho ambao walimpigia mbunge huyo aende kutatua mgogoro huo.
 
Kubenea alifika katika eneo hilo saa 6 mchana na kukutana na wafanyakazi kusikiliza kero zao za muda mrefu.
 
Kisha aliamua kuondoka na viongozi wa wafanyakazi hao na kufanya kikao na menejimenti ya kiwanda hicho kuanzia saa 7 hadi saa 9.
 
Ilipofika saa 10:30, Makonda alifika na kupata taarifa kwa muafaka uliofikiwa kati ya Kubenea, menejimenti na viongozi wa wafanyakazi.
 
Alitoa amri wafanyakazi wakusanyike, akaawaambia kesho atafika huko na Waziri wa Viwanda na Biashara, Waziri wa Kazi na Ajira, na Waziri wa Afya Wanawake, Jinsia na Watoto.
 
Baada ya kutoa maagizo hayo, Makonda alimzuia Kubenea kuhutubia na kuaga wananchi aliokuwa nao tangu mchana, kutokana na hali hiyo (Kubenea) alisema ni vema aseme neno, ndipo mvutano ulipoanza.
 
Makonda alimuru mkutano ufungwe lakini wafanyakazi hawakutawanyika eneo hilo, alipoona hivyo aliamrisha Polisi wamkamate Kubenea ambapo sintofahamu iliongezeka.

Kamanda mpya wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Awataka Polisi Kukabiliana na Majambazi kwa Nguvu zote na Ikibidi Kuwaua Kabla Hawajaua Raia

$
0
0
Kamanda mpya wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amawataka polisi kukabiliana na majambazi kwa nguvu zote na ikibidi kuwaua kabla hawajasababisha madhara makubwa kwa raia.

Msangi ambaye amehamia mkoani Mwanza  akitokea  jijini Mbeya, ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na maofisa usalama na polisi wa vyeo mbalimbali baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi hiyo na SACP, Justus Kamugisha.

Msangi ametoa kauli hio siku chache baada ya John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kusema kwamba, Kamugisha alikuwa mzigo kwenye jiji hilo kutokana na kushindwa kukabiliana na ujambazi.

Katika kipindi cha miezi miwili ya Machi na Aprili mwaka huu, matukio saba ya uhalifu wa kutumia silaha za moto yameripotiwa na katika matukio hayo watu sita walipoteza maisha.

Msangi amesema kuwa, anawashangaa polisi wanaoshindwa kutumia silaha zao kuwakabili watu wanaodaiwa kuwa majambazi na kusababisha vitendo vya uhalifu kuendelea kushamiri jijini humo.

“Tumieni na nyie bunduki zenu kuyaua majambazi. Mbona wao wanaua raia? Haiwezekana uwe na silaha halafu unaacha kuchukua hatua za haraka za watu ambao wanasababisha mauaji na uporaji wa mali za raia,” amesema Msangi.

Msangi amesema, Jiji la Mwanza miezi michache iliyopita limetikiswa na matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha yanayoambatana na mauaji ya raia, kujeruhi na uporaji wa mali zao.

Amesema kuwa, polisi wanapaswa kufanya kazi zao kwa kujiamini na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Kamanda Kamugisha akikabidhi ofisi hiyo aliwahimiza polisi kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia maadili ya jeshi hilo bila kumuonea mtu yeyote yule.

Mke wa Waziri Mkuu Awataka Wananchi Kuwaombea Dua Viongozi Wa Taifa Ili Waweze Kufanya Kazi Zao Kikamilifu

$
0
0

MKE wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa amewaomba wananchi wa wilaya ya Ruangwa kuwaombea dua viongozi wa taifa, Rais Dk. John Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ili waweze kufanya kazi zao kikamilifu.

Amesema kazi nzito inayofanywa na viongozi hao ya kuhakikisha nchi inakuwa salama na inasonga mbele kimaendeleo ni shughuli ngumu na inahitaji nguvu ya Mungu, hivyo ni vema wananchi wakawaombea dua ili kazi hiyo iweze kuwa na tija kwao na taifa kwa ujumla.

Mke wa Waziri Mkuu ameyasema hayo jana alipozungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Chinongwe wilayani Ruangwa, ambapo amewaomba mwananchi hao wajitahidi kuwaombea dua viongozi hao ili malengo yao ya kuwaletea maendeleo yatimie.

Mary ameongozana na Waziri Mkuu Majaliwa ambaye ni mbunge wa Ruangwa, katika ziara yake ya kuwashukuru wananchi waliomchagua kwa nafasi ya ubunge na kisha  Rais Dk Magufuli kumteua kuwa kushika wadhifa huo.

"Nawashukuru sana wananchi kwa kuwa kura zenu ndiyo zilizosababisha Mheshimiwa Majaliwa ambaye ni mbunge wetu kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu, hivyo nawaahidi kuwa tutaendelea kushirikiana,” amesema mke wa Waziri Mkuu.

Amesema licha ya kuongezewa majukumu atahakikisha anaendelea kushirikiana na wanaruangwa ili waweze kuendeleza shughuli za maendeleo katika wilaya hiyo na kwamba wasiwe na wasiwasi kwani hata wasahau kwa kuwa anawapenda na kuwaheshimu.

Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya April 14

Polisi watatu Wafikishwa Mahakamani Wakituhumiwa Kupokea Rushwa

$
0
0

Polisi watatu wa wilayani Urambo, Mkoa wa Tabora wamefikishwa mahakamani kwa mashitaka ya kuomba na kupokea rushwa. 

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Tabora, iliwafikisha askari hao jana katika Mahakama ya Wilaya ya Urambo huku mwingine akidaiwa kukimbia.

Askari hao waliofukuzwa kazi kabla ya kufikishwa mahakamani ni John Okinda, Kabila Pius na Patrick Robart. 

Anayedaiwa kukimbia ni Elisha ambaye polisi inaendelea kumtafuta. 

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Urambo, Hassan Momba, Wakili wa Takukuru, Edsoni Mapalala alidai washitakiwa walitenda makosa hayo Machi 7 mwaka huu.

Mapalala alidai siku hiyo katika kijiji cha Mkirigi, Kata ya Ilege, Wilaya ya Kaliua, washitakiwa hao wakiwa waajiriwa wa jeshi la polisi, waliomba rushwa ya Sh milioni tatu kutoka kwa Dotto Gandulanye ili wasimchukulie hatua za kisheria baada ya kumkuta akiwa na bangi.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images