Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Wabunge Waiponda Bajeti Ya Viwanda

$
0
0

Wajumbe wa Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira wamekerwa na kiwango cha bajeti ya Sh95. 6 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, wakisema haionyeshi malengo ya Tanzania kuelekea kuwa nchi ya viwanda.

Wabunge walisema hayo baada ya Waziri Charles Mwijage kuwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa 2016/17 mbele ya kamati.

 Waziri Mwijage alisema kati ya fedha hizo, Sh 53.5 bilioni (sawa na asilimia 56), zimetengwa kwa matumizi ya kawaida wakati Sh42.1 bilioni (asilimia 44) ni kwa ajili ya maendeleo.

Mbunge wa viti maalumu (Chadema), Hawa Subira alisema wakati wa kujadili taarifa hiyo kuwa kiwango hicho kinaonyesha wazi jinsi Serikali isivyo na nia ya kufufua viwanda kama alivyoahidi Rais John Magufuli.

“Homa ya Magufuli inawaogopesha. Nakuonea huruma waziri (kwa kuwa) unaonyesha kabisa kuwa una nia njema, lakini kwa mtindo huu lazima uumwe,” alisema Subira.

“Tafuteni panadol tuwasaidieni. Tunataka nchi hii kweli iwe ya viwanda. Hatuwezi kufanya kazi namna hii watu mmejaa uoga hata kupanga bajeti ya kueleweka mnashindwa au mkikaa mnaogopa kurekodiwa,” alisema.

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema alisema nchi kuwa ya viwanda na biashara inawezekana, lakini Serikali inapaswa kudhihirisha kwa vitendo badala ya maneno kwa kuwa wizara hiyo ilipaswa kutengewa fedha za kutosha kuonyesha njia ya kuelekea kwenye malengo yaliyokusudiwa, kama kuruhusu safari za nje ya nchi kwa maofisa wa wizara kwa nia njema.

“Lakini kuna mambo yamekuwa yakifanyika ya ajabu. Mimi naweka mambo ya siasa pembeni. Serikali iangalie upya hii bajeti, lakini pia huo mradi wa China Logistics Centre hauna msaada kwa nchi badala yake utaua hata viwanda vidogo vidogo vilivyopaswa kusaidiwa kuinuka. Hatuwezi kuifanya Dar kuwa Dubai wakati viwanda vya ndani havijaimarishwa,” alisema.

Kwa upande wake mbunge wa Nkenge(CCM), Dk Diodorus Kamala alisema wakati mwingine Serikali imekuwa ikiwapa wapinzani kauli kutokana na mambo inayofanya. 

Alisema kiwango hicho cha fedha hakiendani hata na taarifa aliyoiyoa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango hivi karibuni alipowasilisha mapendekezo ya mpango wa bajeti.

“Fedha ni ndogo wakati tunatakiwa tujikomboe kwa kupiga hatua za kimaendeleo kutoka hapo tulipo. Mfano naona wizara imeridhika kuwa pale kwenye jengo la Water Front, badala ya bajeti hii kueleza mpango wake wa kujenga ofisi ya kujitegemea ili kusaidia hata kupunguza matumizi,” alisema.

Akijibu hoja hizo, Mwijage alisema haoni tatizo kwa kiwango cha bajeti alichotengewa kwa kuwa malengo ya wizara yake kwa mwaka huu wa fedha pamoja na mambo mengine ni kuboresha mazingira ya viwanda vilivyopo kisha mwaka ujao ndipo watajikita kujenga vipya.

“Ninachokiona hapa ni kwamba wengi wanataka kuona nchi inakuwa hivyo leo, kumbe tunatakiwa kuanzia kwa kuboresha mazingira ya hivi vilivyopo kwani vingi vinazalisha chini ya asilimia 50 kutokana na vikwazo mbalimbali ikiwamo miundombinu duni,” alisema.

Katika mapendekezo ya mpango wa bajeti ya 2016/17, Serikali imeweka fedha nyingi katika kuboresha miundombinu ya usafiri kama reli, barabara na viwanja vya ndege, uzalishaji wa nishati ya uhakika, hasa umeme unaotokana na gesi na makaa ya mawe na kuboresha rasilimali watu kwa ajili ya kuweka mazingira wezeshi ya kukua kwa viwanda.

ACT-Wazalendo Waishambulia CHADEMA

$
0
0

CHAMA cha ACT-Wazalendo Wilaya ya Shinyanga Mjini kimetamba kuwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, ndicho kitakuwa mpinzani mkubwa wa CCM badala ya Chadema.

Katibu wa ACT-Wazalendo, Wilaya ya Shinyanga, Melkyoli Sebastian alisema hayo baada ya kumuingiza kwenye chama hicho, kada wa Chadema, Ibrahimu Mbogoma. 

Mbogoma alikuwa mwenyekiti wa baraza la wazee kata ya Masekelo manispaa ya Shinyanga.

Sebastian alisema chama chao kimeanza kuaminiwa na wananchi kutokana na sera zake za kiujamaa ambazo zimelenga kumkomboa mwananchi wa hali ya chini bila ya kubagua dini, kabila wala rangi.

Alisema kutokana na sera hizo, ndiyo maana wanachama wa Chadema wameanza kujiunga na chama chao baada ya kusoma alama za nyakati.

“Kujiunga kwa kada huyo aliyekuwa Chadema ni salamu tosha kuwa Chadema inaelekea kufa kiupinzani, nina imani wapo wanachama wengi wa vyama vya upinzani watakuja kujiunga na ACT Wazalendo.

"Sisi tunawakaribisha waje kwa wingi ili tukijenge chama kuelekea Ikulu 2020,” alisema Sebastian. 

Akieleza sababu za kuhama Chadema, Mbogoma, alisema ameamua hivyo kutokana na kuchoshwa na migogoro ndani ya Chadema pamoja na kuongozwa na viongozi wasiojua majukumu yao.

Mbogoma alisema tangu alipojiunga na Chadema mwaka 2010 hajaona mafanikio yoyote licha ya kushika nyadhifa mbalimbali. Alisema amekuwa akikumbana na migogoro ya mara kwa mara. Alisema anaamini ACT-Wazalendo ndicho kitaipindua CCM.

Katibu wa Chadema wilaya ya Shinyanga Mjini, George Kitalama alisema alikuwa hajapata taarifa rasmi za kiofisi za kuhama kwa mwanachama wake huyo. 

Hata hivyo, alisema kila mtu ana haki ya kwenda kujiunga kwenye chama anachokitaka kwa mujibu wa Sheria za nchi.

Ombaomba Waanza Kuondolewa Jijini Dar

$
0
0

Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda limeanza kufanyiwa kazi baada ya karandinga kuanza kuwasomba ombaomba waliojaa katika maeneo mengi jijini hapa.

Makonda alitangaza kuanza kuwaondoa ombaomba hao juzi, huku akipiga marufuku wananchi kuwapa pesa kwa kuwa ndicho chanzo cha kuwapo kwao jijini hapa.

Zoezi hilo la kuwaondoa watu hao lilianza juzi usiku katika maeneo ya Mnazi Mmoja, Samora na Kariakoo.

Jana maeneo mbalimbali ambayo aghalabu ombaomba hupenda kukaa  yalikuwa tupu.

Maeneo hayo ikiwamo barabara ya Morocco, Magomeni Usalama, Fire na Baridi hayakuwa na watu wa kundi hilo.

Mmoja wa ombaomba aliyekuwa na watoto wawili alipomuona mwandishi wa habari hizi katika maeneo ya Fire, alitimua mbio na kujificha pembeni mwa barabara, huku akisema: “Tumetoka Dodoma, hatutaki kurudi.”

Kadhalika, operesheni hiyo licha ya timuatimua kuwakumba ombaomba, wapigadebe nao wameunganishwa katika kundi hilo kwa kuanza kuondolewa kwenye vituo vya mabasi.

Baadhi ya wapigadebe hao wamedai ni vigumu kwa Makonda kuwaondoa kwa kuwa wanachofanya ni kwa manufaa ya maisha yao na hawana pa kwenda.

Agizo la kutaka ombaomba wakamatwe na kuondokana na vitendo hivyo liliwahi kutolewa pia na waliowahi kuwa wakuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yusuf Makamba, Abbas Kandoro na Said Mecky Sadiki.

Mkapa, Kardinali Pengo Wammwagia SIFA Rais Magufuli

$
0
0

Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa amesema viongozi wote wanawajibika kuishi kwa mfano wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Hayati Edward Sokoine aliyejitoa kutumikia taifa huku akimtaja Rais John Magufuli ametokana na kuishi namna hiyo.

Alisema hayo juzi baada ya misa takatifu ya kumkumbuka Sokoine iliyofanyika katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa pia na Rais John Magufuli.

Mkapa alisema mfano huo wa Sokoine, ndio ulioiwezesha Tanzania kumpata kiongozi wa sasa, Rais John Pombe Magufuli anayetaka kuonesha misingi ya uongozi bora, uadilifu, kusimamia amani, utulivu na maendeleo.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alimpongeza Rais Magufuli kwa kufuata nyayo za Sokoine katika kuliongoza Taifa.

Akizungumza kwenye misa hiyo, Kardinali Pengo alisema waliwasiliana na Dk Magufuli kwa simu wakati akiwa mapumzikoni Chato mkoani Geita na Rais alimueleza maneno ambayo yanaonyesha kuwa kazi ya urais si rahisi, na jinsi kiongozi huyo wa kiroho alivyompa moyo.

“Sijui ni vizuri nikisema Mheshimiwa Rais, lakini kwa vile uliyataja maneno hayohayo hata kule Chato. Napenda kusema yale uliyosema kwangu binafsi kwa njia ya simu,” alisema Kadinali Pengo.

“Ulisema ‘ningelijua kwamba kuwa Rais ndiyo hivi, wala nisingeligombea urais’ … na mimi nilisema afadhali mtu mmoja afe kuliko Taifa liteketee. Kwa hiyo endelea mbele.”

Kadinali Pengo, aliyeonekana awali kusita kuweka bayana mazungumzo hayo, alisema kwa kuwa Rais Magufuli alishaeleza hayo akiwa Chato, basi angependa aeleze sehemu ya mambo aliyowahi kuzungumza naye kwa simu.

Ingawa Kadinali Pengo hakueleza kile alichozungumza Rais akiwa Geita, Dk Magufuli amekuwa akieleza jinsi kazi ya urais ilivyo ngumu na kila mara kuomba wananchi wamuombee na kumsaidia kutekeleza majukumu yake.

Akiwa kwenye ibada iliyofanyika katika Kanisa la Bikira Maria, Parokia ya Chato, Rais aliwataka Watanzania wote kuendelea kuliombea Taifa ili liendelee kuwa na amani.

Kadinali Pengo alitoa dokezo hilo siku ya kukumbuka kifo cha Sokoine, ambaye amejijengea sifa ya kuwa mpambanaji katika vita dhidi ya uhujumu uchumi, uvivu, wizi wa fedha za umma na matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.

Alieleza katika misa hiyo kuwa watu wanamfananisha Rais Magufuli na waziri mkuu huyo wa tatu tangu nchi ipate uhuru.

Alisema kuna ming’ono kuwa sura ya Rais Magufuli inafanana na ya Sokoine, akisema maneno mengi ya mtaani ni ya ukweli zaidi ya yale yanayoandikwa na vyombo vya habari.
Kwa upande wake, Rais Magufuli aliwasihi Watanzania kuendelea kushikamana, kupendana na kuenzi mazuri yaliyofanywa na viongozi wa taifa waliotangulia mbele ya haki, akiweno aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Sokoine.

Magufuli alihimiza Watanzania kuenzi mazuri yote yaliyofanywa na viongozi wengine waliotangulia mbele ya haki, hususani Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amaan Karume, Magufuli alisema kazi nzuri ya mtu huwa haipotei.

Alisema anamkumbuka Sokoine alivyokuwa kiongozi shupavu, aliyewapenda watanzania, aliyependa kuwatumikia watanzania, mchapakazi, aliyechukia rushwa, aliyechukia ufisadi na aliyechukia uonevu kwa watu wa chini.

“Namuona (Sokoine) ni kielelezo cha pekee katika Taifa letu la Tanzania, miaka 32 iliyopita wakati Mzee wetu Edward Moringe Sokoine alipoitwa na kutangulia mbele ya haki, wakati huo mimi nilikuwa JKT Mpwapwa, ninaikumbuka siku hiyo ilikuwa ya majonzi makubwa,” alisema.

Sokoine alifariki dunia miaka 32 iliyopita, kwa ajali ya gari katika eneo la Dakawa wakati akitokea Bungeni Dodoma.

Risasi Zarindima Mahakamani Wakati Ng'ombe Wakihakikiwa

$
0
0

Milio ya risasi ilirindima juzi na kuzua tafrani wakati Mahakama ya Wilaya ya Bukombe ilipohamia mahabusu ya ngo’mbe kuhakiki idadi ya mfugo iliyokamatwa ndani ya Hifadhi ya Mdendeli Muowisi Kigosi, mkoani Geita.

Inadaiwa kuwa risasi hizo zilizokuwa zikifyatuliwa na watu wasiojulikana zililenga kuwatisha waliokuwa wakiendelea na kazi ya uhakiki iliyokuwa ikisimamiwa na Hakimu Gabriel Kurwijila na kulindwa na askari 35 mahakamani wa idara ya wanyamapori. 

Katika tuko hilo, askari 10 walilazimika kujibu mapigo na kufanya eneo hilo kugeuzwa uwanja wa vita.

Baada ya askari wanyamapori na polisi kufanikiwa kuwafurusha wavamizi, walitokomea porini kabla ya kutiwa mbaroni.

Kazi hiyo iliendelea na kubaini ng’ombe wote 454 wana afya njema ndipo Hakimu Kurwijila alipoahirisha shauri hilo.

Hata hivyo, uhakiki huo ulibaini uwapo wa ng’ombe wa ziada 139 ambao kwa mujibu wa Wakili wa Serikali Mwasimba Hezron, inawezekana waliwafuata wenzao wanaolindwa na askari wa wanyamapori.

Kutokana na hofu ya kuvamiwa wakiwa njiani kurejea Ushirombo, Hakimu Kurwijila aliamuru askari wanyamapori na polisi kuimarisha ulinzi kuhakikisha wote walioko kwenye msafara wanafika salama.

Kesi hiyo inawakabili washtakiwa watano wanaodaiwa kukutwa wakichunga mifungo ndani ya eneo la hifadhi kinyume cha sheria.

Washtakiwa hao leo wanaanza kujitetea na wanatarajiwa kuitwa mashahidi sita kupinga ushahidi wa upande wa mashtaka.

Washtakiwa hao ni Emanuel Wapi, Musa Manyakenda, John Wapi, Nkwabi Ngeleja na Masan Makura.

Serikali ya Marekani Yaahidi Kuendelea Kuisaidia Tanzania Hasa Katika Sekta za Afya na Elimu

$
0
0

Serikali ya Marekani imeihakikishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kuendeleza uhusiano uliopo baina ya nchi hizo mbili ikiwa ni  pamoja na kutoa ufadhili na misaada mbalimbali ya miradi ya maendeleo hasa katika sekta za afya na Elimu.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari muda mfupi mara baada ya kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani hapa nchini aliyeongozana na Ujumbe wa watu 15 wanaoshughulikia miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Serikali ya Marekani hapa nchini, Waziri wa Mambo ya Nje,Afrika Mashariki,Kikanda na Ushirikiano wa Kimataifa Dr Augustine Mahiga alisema kuwa licha ya kutokea kutoelewana kwa Serikali hiyo na Tanzania hivi karibuni lakini nchi hiyo imesema kuwa haitasitisha kuendeleza miradi muhimu kama vile miradi ya Elimu na Afya  iliyoanzishwa hapa nchini na Seikali ya Marekani sambasamba na kuendeleza Ushirikiano huo katika nyanja zingine za kimaendeleo.

Aidha Waziri Dr Mahiga aliwatoa hofu watanzania na kusema kuwa miradi yote ambayo ilianzishwa hapa nchini kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani itaendelezwa kama ilivyopangwa hapo awali na kuahidi miradi mingine zaidi itakayoleta tija kwa Taifa sambamba na kuleta ajira kwa Watanzania walio wengi.

Kwa Upande wake Balozi wa Tanzania Nchini Mark Childress alisema kuwa upo umuhimu wa kuendeleza mahusiano kati ya Tanzania na Marekani hasa katika utoaji wa misaada mbalimbali ya kimaendeleo hivyo Serikali ya nchi hiyo itaendeleza na kukuza  mahusiano hayo licha ya changamoto mbalimbali za kisiasa zilipo nchini.

Nchi hiyo ya Marekani imeahidi kuongeza miradi mingi zaidi nchini itakayolenga kukuza uchumi wa Tanzania na kuitoa nchi hiyo katika hali ya umasikini iliyopo hivi sasa.

Katika mazungumzo hayo, pia walijadili jinsi ya kuimarisha masuala ya kidiplomasia na namna ya kuzidisa usalama wa kikanda kwa manufaa ya wote.

Lugumi atoroka nchini......Adaiwa kupanda ndege usiku wa manane, haijulinani alikokwenda

$
0
0

Mfanyabiashara  anayemiliki Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd, Said Lugumi, ametoroka nchi.

Lugumi ambaye anatajwa kuwa na ukwasi wa kupindukia katika kipindi kifupi, aliingia mkataba tata na Jeshi la Polisi mwaka 2011, kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi 108 nchi nzima kwa gharama ya Sh bilioni 37.

Taarifa za kutoroka nchi kwa mfanyabiashara huyo, zilielezwa na baadhi ya maofisa wa vyombo vya dola, ambapo inadaiwa kuwa aliondoka nchini Jumatatu wiki hii, siku ambayo Jeshi la Polisi lilitakiwa kuwasilisha mkataba huo Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kwa mujibu wa sheria.

Mfanyabiashara huyo ambaye amekuwa akitembea na msafara mkubwa wa magari ya kifahari, huku akilindwa na walinzi maalumu wa kukodi, ametoroka wakati vyombo vya dola vilikuwa vikimuwinda.

Utata wa Malipo
Pamoja na hali hiyo inaelezwa kuwa licha ya Lugumi kuingia mkataba na Jeshi la Polisi wa Sh bilioni 37, lakini bado alilipwa Sh bilioni 46 nje ya mkataba.

Katika mkataba huo, alilipwa kiasi Sh bilioni 34 ambazo ni sawa na asilimia 99 ya fedha za makubaliano ya mkataba, lakini hadi sasa mashine hizo zimefungwa katika vituo 14 pekee jijini Dar es Salaam ambavyo hata hivyo haijaainishwa maeneo vilipo.

Sakata hili lilibainika wiki iliyopita baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kukutana na maofisa wa jeshi hilo kupitia taarifa ya hesabu zao za mwaka 2013/14 zilizokaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Msafara wake Wapungua
Duru za ndani zinaeleza kuwa tangu Kamati ya Bunge ilipoibua sakata hilo na vyombo vya dola kuanza kuwahoji baadhi ya washirika wake katika biashara, msafara wa mfanyabishara huyo umepungua.

Chanzo kimoja kinasema kwa mara ya mwisho mfanyabiashara huyo alionekana eneo la Oysterbay jirani na Kanisa la St. Peter, huku akiwa na magari mawili badala ya saba hadi 10 kama ilivyokuwa awali.

Mtoa habari huyo alisema Lugumi aliopoonekana mwishoni mwa juma lililopita, alikuwa na magari mawili likiwamo Toyota GX V8 toleo la mwaka huu, ambalo lilikuwa limebeba walinzi wake, huku mwenyewe akiwa ndani ya gari la kifahari aina ya Escalade.

“Lugumi anaishi Mbweni na awali ilikuwa msafara wake ukipita magari husimamishwa ili kumpisha, na huwa na magari mengi kweli mithili ya kiongozi wa nchi, jamani kuna watu wamejua kuitafuna nchi hii, na sasa huenda unatimia usemi wa Rais Magufuli kuwa ni zamu yao kuishi kama mashetani na si kama malaika,” kilisema chanzo hicho.

Mkataba Wahamishwa
Sakata la mkataba huo wa Polisi na Lugumi limezidi kuchukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kunyang’nywa hoja hiyo na badala yake kuhamishiwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Hatua hiyo inatokana na utata uliogubika mkataba huo ambao unawahusisha vigogo kadhaa wa Jeshi la Polisi pamoja na baadhi ya watendaji wa Serikali ya Rais Dk. John Magufuli, huku ikidaiwa kuwa huenda ikawa njia ya ‘kulindwa’.

Kutokana na hali hiyo, hadi kufikia Jumatatu saa 10 jioni, Makamu Mwenyekiti wa PAC, Aeshi Hilaly, alisema kuwa kamati yao haijapokea taarifa yoyote kuhusu Kampuni ya Lugumi, ambapo kamati hiyo ililitaka Jeshi la Polisi kuwasilisha mkataba huo hadi kufikia leo.

Aeshi alisema wamemuomba Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah, ili aweze kuwaandikia Polisi barua kwa ajili ya kuwasilisha mkataba huo.

“Tumelazimika kumwandikia barua Katibu wa Bunge ili awaandikie barua polisi walete mkabata huo ndani ya siku tatu kutoka leo (juzi) kama walivyotakiwa na kamati yetu,” alisema Hilaly.

Kauli ya Bunge
Alipotafutwa Mkuu wa Idara ya Habari, Elimu na Mawasiliano, Ofisi ya Bunge, Owen Mwandumbya, alisema kama kuna hoja iliyoibuliwa na Kamati ya PAC kisha ikapelekwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, itakuwa ni kwa ajili ya kupata ufafanuzi kuhusu matumizi ya fedha.

“Kama suala hilo lipo Mambo ya Nje, itakuwa si kwa hoja iliyoibuliwa na PAC na hakuna suala linaloshughulikiwa kama limeanzia PAC.

“Na kama litakuwa limekwenda huko ni kwa ajili ya kupata uelewa kuhusu matumizi ya fedha, na unajua hivi sasa hizi  kamati zipo katika maandalizi ya bajeti. Ila hoja kuhamishiwa kamati nyingine hutokana na maelekezo ya Spika wa Bunge. Kwa hoja hii ya PAC bado suala hilo lipo chini yao,” alisema Mwandumbya.

Chanzo: Mtanzania

Ripoti ya NSSF yatua kwa Rais Magufuli

$
0
0

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) inayohusu miradi inayosimamiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), imepelekwa kwa Rais Dk. John Magufuli kwa ajili ya kuipitia.

Awali ripoti hiyo ilitakiwa kuwasilishwa juzi kwenye Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge, baada ya wajumbe wa kamati hiyo kuiomba, lakini ilishindwa kuwasilishwa na viongozi wa NSSF kwa madai kuwa kuna tuhuma za ubadhirifu wa mamilioni ya fedha za miradi mbalimbali inayosimamiwa mfuko huo.

Akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo juzi, Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenister Mhagama, aliwaambia ripoti hiyo imetua mikononi mwa Rais Magufuli, hivyo hawawezi kuipata hadi aisome na kuiwasilisha bungeni.

“Kutokana na hali hii, kamati haiwezi kuipata ripoti hii hadi rais mwenyewe atakapoamua kuiwasilisha,” alisema.

Alisema kuna uwezekano mkubwa mjadala wa ripoti hiyo ukaendelea bungeni, baada ya Rais Magufuli kuipitia na kutoa maelekezo.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya kamati hiyo  jana vilisema  kuwa baada ya Waziri Jenister kutoa taarifa hiyo, wajumbe wa kamati walipinga na kuwataka watendaji wa NSSF waiwasilishe kwenye kamati hiyo kwa sababu wao ndio walioiomba ili waweze kuipitia na kuangalia utekelezaji wa majukumu ya mfuko huo.

Baada ya mvutano huo, Waziri Jenister alisisitiza taarifa alizonazo ripoti ipo kwa Rais, hivyo hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuipata hadi ipelekwe bungeni au atoe maelekezo mengine kwa kuwa yeye ndie mwenye kibali hicho kwa mujibu wa sheria.

Waziri Jenister alipotafutwa kuzungumzia suala hilo jana, alisema wizara yake haiwezi kulizungumzia kwa sababu liko mikononi mwa kamati.

Alisema kisheria ripoti ikifikishwa kwenye mikono ya rais, wizara haina mamlaka ya kujadili tena.

Wiki iliyopita, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mohammed Mchengerwa, wakati akitoa majumuisho ya ziara walizofanya katika taasisi mbalimbali za Serikali na wizara, alisema walibaini kuwapo upungufu katika taarifa ya utekelezaji wa miradi mingi inayosimamiwa na NSSF.

Alisema kutokana na kasoro hizo, kamati iliona ni vema ikapata ripoti ya CAG ili ipitie na kujiridhisha kama miradi imetekelezwa au kuna harufu ya ufisadi.

“Kamati imebaini kuwepo nyumba nyingi zilizojengwa na NSSF ambazo hazikaliwi na watu, hali iliyotutia shaka. Inaonekana baadhi ya watu wamenufaika na miradi hii.

“Tunaamini miradi hii haijawanufaisha wanachama wake bali watu wachache, ndiyo maana tumeagiza ripoti ili tuipitie,” alisema Mchengerwa.

Alisema kutokana na hali hiyo, wameagiza kusimamishwa miradi mipya ya shirika hilo na kuiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Jamii (SSRA), kuhakikisha inasimamia ipasavyo mifuko pamoja na kuangalia miradi inayoanzishwa kama inawanufaisha wananchi na Serikali kwa ujumla.

Utapeli wa Ajira za Polisi Washika Kasi

$
0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mtafungwa

Vijana 11 waliokuwa na shauku ya kujiunga na Chuo cha Polisi Moshi (MPA) wamejikuta wakitapeliwa kati ya Sh. milioni moja hadi milioni 1.5 kila mmoja, baada ya kulaghaiwa na mmoja wa askari mgambo mjini humo kuwa atawapatia nafasi ya kujiunga na chuo hicho.

Habari za uhakika zilizopatikana mjini hapa jana na baadae kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mtafungwa na Mkuu wa chuo hicho, Kamishna Mwandamizi Matanga Mbushi, zinaeleza kwamba, vijana waliotapeliwa wanatokea mkoa wa Mbeya.

Kamanda Mutafungwa alisema jana kwamba, Jeshi la Polisi halijatangaza nafasi za mafunzo hayo na kwamba mtuhumiwa aliyefanya utapeli huo ambaye ni askari mgambo mkazi wa Mbeya, amekamatwa mjini Moshi na anashikiliwa na polisi kwa mahojiano kabla ya kufikishwa mahakamani.

“Tunamshikilia mgambo huyo katika Kituo Kikuu cha Polisi Moshi kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kumuhoji na tutamsafirisha jijini Mbeya kwenda kujibu mahakamani tuhuma zinazomkabili. Hawa vijana walipohojiwa walisema walichukuliwa eneo la Mbalizi, Mbeya,” alisema.

Kufuatia tukio hilo, polisi mkoani Kilimanjaro wamelazimika kutafuta mawasiliano ya wazazi wa vijana hao kwa ajili ya kutuma fedha za nauli za kuwasafirisha kurudi nyumbani hadi hapo kesi ya msingi itakapofunguliwa jijini Mbeya.
 
Wakati vijana hao wanakamatwa katika chuo hicho, walikuwa wamefungashiwa vifaa vyote muhimu kwa ajili ya kujiunga na Jeshi la Polisi.

Alipotafutwa Mkuu wa Chuo cha Polisi Moshi, Mbushi ili kuzungumzia suala hilo, alisema katika uchunguzi wao wa awali wamebaini kwamba kuna askari mmoja mwenye cheo cha koplo kutoka mkoa wa Mbeya alihusika na alichukua fedha hizo lakini hakuja Kilimanjaro.

Alisema mgambo huyo alikamatwa baada ya kufika chuoni hapo akiwa ameambata na vijana hao 11, wavulana wanane na wasichana watatu.

Aliwataka wazazi kuelewa kwamba, nafasi za mafunzo ya polisi hazinunuliwi na wala haziuzwi mitaani, bali muda unapofika huwa zinatangazwa na kuwataka zinapotangazwa nafasi hizo waende wakaulize kwenye ofisi za wakuu wa polisi wa mikoa na wilaya ili waweze kupata uhakika na kujulishwa hatua wanazotakiwa kuzifuata ili kukidhi vigezo vya kujiunga na Jeshi la Polisi.

Hili ni tukio la pili la vijana kutapeliwa fedha wakilaghaiwa kutafutiwa nafasi za kujiunga na mafunzo ya polisi, la kwanza likiwa ni 2015 vijana 90 kutoka jijini Dar es Salaam walipotapeliwa kwa njia hiyo.

Mahakama Yamwachia Huru aliyekuwa Mkurugenzi wa Tanesco William Mhando na mkewe

$
0
0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imewaachia huru aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando na mkewe Eva Mhando .

Mhando na wenzake walikuwa wanashitakiwa kwa makosa sita likiwemo la matumizi mabaya ya ofisi, kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Mhando alikuwa anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka kwa kuipa zabuni Kampuni ya Santa Clara Supplies Ltd huku akijua ana maslahi nayo na kwamba anaimiliki yeye, mke na watoto wake. 

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Hellen Riwa kwa niaba ya Hakimu mwenye kesi hiyo Kwei Lusema amesema  upande wa mashtaka umeshindwa kuthibisha juu ya matumizi mabaya ya ofisi kwani Mhando alikuwa haingii kwenye vikao vya maamuzi ya bodi ya Tanesco kwa hiyo alikuwa hana ushawishi wa moja kwa moja kushawishi kampuni  ya Santa Clara ambayo ni ya mke wake ipatiwe tenda

Muda Wa Uzimaji Simu FEKI Hautaongezwa- Makame Mbarawa

$
0
0

Waziri  wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiiano Profesa Makame  Mbarawa amesema Serikali haitaongeza muda katika zoezi zima la uzimaji wa simu feki ifikapo Juni 16 mwaka huu.

Ameyasema hayo ofisini kwake leo jijini Dar es salaam wakati wa mahojiano na kituo kimoja cha habari hapa nchini.

Amesema Serikali imeamua kuchukua uamuzi huo kutokana na madhara mbalimbali yatokanayo na simu hizo ikiwemo ya kiafya na kusisitiza kuwa serikali inapoteza mapato mengi kutokana na uingizwaji wa simu hizo nchini.

"Tunategemea kuzima simu zote feki kutokana na madhara yake kiafya  hasa kwa watumiaji, kukosekana kwa viwango vya ubora wa simu hizi na hivyo wananchi kupoteza fedha nyingi kwa ajili ya ununuzi wa simu hizi kwani hufa mara kwa mara", amesema Waziri Mbarawa.

Aidha, Profesa Mbarawa ameongeza kuwa kwa sasa Jopo la wataalamu kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) limepelekwa mkoani Singida kwa ajili ya kutoa elimu ya utambuzi wa simu hizo ili kuweza kuwasaidia wananchi kubaini kwa urahisi.

Amesisitiza wananchi kuchukua tahadhari kabla ya kununua simu ikiwemo kumuuliza muuzaji kabla ya kununua, kudai risiti na kuituinza ili kudhibiti uingizwaji na usambazaji wa bidhaa hizo nchini.

Katika hatua nyengine, Waziri Mbarawa amesema kuwa suala la mkongo wa Taifa linaendelea vizuri ambapo Serikali kwa kushirikiana na watoa huduma wa mawasiliano wanaendelea na usimikaji wa minara ya mawasiliano katika sehemu mbalimbali za nchi hususan vijijini ili kuleta huduma bora za mawasiliano nchini.

"Kwa sasa awamu ya nne ya mradi huu wa Mkongo wa Taifa unaendelea, kwani makampuni mbalimbali ya simu yanasimika minara yao katika sehemu mbalimbali za nchi ili kusambaza na kuboresha mawasiliano kwa wananchi", amefafanua Profesa Mbarawa.

Ameongeza kuwa  uwepo wa  mkongo huo nchini kumepelekea mapinduzi katika sekta ya mawasiliano, mabenki na kuiongezea Serikali pato kwani hata nchi za jirani hutumia mkongo huo katika kupata mawasiliano yaliyo bora.

Tathmini imebainisha kuwa kutokana na uwepo wa mkongo huo nchini watumiaji wa simu wamefikia milioni 39.7 na wa intaneti kufukia milioni 17.

Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini, 
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi)

Rais Magufuli Kuweka Jiwe La Msingi La Ujenzi Wa Barabara Ya Juu (Flyover) Ya Tazara Na Kufungua Daraja La Kigamboni Jijini Dara Es Salaam

$
0
0

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya juu (Flyover) katika makutano ya TAZARA na ufunguzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Siku ya Jumamosi tarehe 16 Aprili, 2016 Mheshimiwa Rais ataweka jiwe na msingi la ujenzi wa barabara ya juu katika makutano ya barabara Nyerere na Mandela (Flyover ya TAZARA).

Jumanne tarehe 19 Aprili, 2016 Mheshimiwa Rais atafungua rasmi Daraja la Kigamboni lenye urefu wa mita 680 na barabara unganishi (approach roads) upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa kilometa 2.5.  Ujenzi huu umefanywa na Kampuni ya China Railway 15 Group ilishirikiana na Kampuni ya China Bridge Engineering Group.

Aidha wakati tunasubiri uzinduzi rasmi, Wananchi na magari yenye uzito usiozidi tani 10 yataruhusiwa kutumia Daraja la Kigamboni kuanzia Jumamosi tarehe 16 Aprili, 2016 ili kuwawezesha kuelewa vizuri miundombinu na matumizi ya daraja.

Utekelezaji wa miradi hii ni mojawapo ya jitihada za Serikali za kuboresha miundomninu na kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam.

Imetolewa na;

Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu  (Ujenzi)
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
14 Aprili, 2016

Waziri Mkuu Akutana Na Waziri Wa Biashara Wa Oman

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuendeleza sekta ya viwanda kama mkakati wa kukuza uchumi ili nchi iweze kutoka kwene umaskini na kufikia uchumi wa kati.

Waziri Mkuu amesema hayo leo (Alhamisi, Aprili 14, 2016) alipofanya mazungumzo na Waziri wa Biashara wa Oman, Dk. Ali Masoud Al Sunaidy ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam.

Amesema mbali na kuimarishwa kwa sekta ya viwanda, pia Serikali imelenga kuboresha sekta za nishati, uchukuzi na kilimo ambazo zitawezesha Taifa kufikia malengo yake ya kufikia uchumi wa kati.

“Sekta ya viwanda ni eneo ambalo tunataka kuliimarisha kwa sababu litatuwezesha kuongeza thamani ya mazao na bidhaa zinazozalishwa nchini jambo ambalo pia litakuza  ajira kwa vijana. Hivyo nawakaribisha mje kuwekeza nchini,” amesema.

Pia Waziri Mkuu amemuhakikishia kuwa serikali ipo tayari kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wa kutoka Oman kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali.

Kwa upande wake, Dk. Al Sunaidy amefurahishwa na mazingira mazuri ya uwekezaji nchini na kwamba wapo tayari kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali yakiwemo viwanda vya usindikaji, kilimo kinachotumia teknolojia ya kisasa, na mafuta, gesi, na ujenzi wa bandari.

Akitoa ufafanuzi, Waziri huyo alisema:“Oman ina bandari ya Salala ambayo ni moja kati ya bandari bora duniani yenye uwezo wa kupakua makontena 45 kwa saa. Lakini pia tunayo bandari ya Sohar maarufu kwa bidhaa za viwandani ambayo ina uwezo wa kupakua makontena 32 kwa saa,” amesema.

Dk. Al Sunaidy yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu akiwa ameambatana na wafanyabiashara 80 wa Oman kwa mwaliko wa Kiserikali kwa ajili ya kukuza ushirikiano wa kiuchumi.

Naye Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo amesema anatambua kuwa Oman imepiga hatua katika teknolojia ya gesi asili ya kimiminika (LNG) hivyo ana imani Tanzania itapata ujuzi  kutoka kwao.

Amesema wafanyabiashara hao wana fursa ya kuwekeza kweye ujenzi ujenzi wa viwanda vya mbolea katika mikoa ya Lindi na Mtwara lakini pia wanaweza kuwekeza kwenye bandari za Tanga, Bagamoyo, Kilwa, Lindi na Mtwara ambazo Serikali imepanga kuboresha miundombinu yake.

Taarifa Ya Jeshi La Polisi Kuhusu Utapeli Wa AJIRA Katika Taasisi Mbalimbali

$
0
0

Katika siku za hivi karibuni katika maeneo mbalimbali hapa nchini, kumejitokeza makundi ya watu ama mtu binafsi kutumia mwamvuri wa taasisi fulani kujipatia kipato kwa njia za udanganyifu (utapeli) kwa kuwaahidi vijana kwamba watawapatia ajira katika taasisi hizo.

Makundi haya ya kihalifu imebainika kwamba yapo katika maeneo mbalimbali, hivyo, ni suala ambalo linahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi ili kukomesha vitendo hivyo. 

Juhudi za makusudi zinaendelea kufanyika na jeshi la polisi ili kuwatia mbaroni watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo vya kitapeli.

Aidha, kufuatia kuibuka kwa vitendo hivyo, tayari Jeshi la Polisi limewakamata matapeli wawili wakiwa wamekusanya vijana katika mikoa ya Kilimanjaro na Mbeya, uchunguzi dhidi yao unaendelea na pindi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabiri.

Jeshi la Polisi likishirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama, kimsingi, kazi yetu kubwa ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na Ulinzi na Usalama imara. 

Tutaendelea  kupambana na makundi haya ya kihalifu na utapeli ili nchi yetu iendelee kuwa salama.

Tunawasihi wananchi kufuatilia taarifa kwenye vyanzo sahihi juu ya jambo lolote wanalotaka kulifanya ili kuepuka utapeli unaoweza kufanywa na baadhi ya watu kwa lengo la kujipatia vipato. 

Aidha, wananchi watoe taarifa kwenye vyombo vya usalama kuhusu tabia na mienendo yoyote wanayoitilia mashaka. 

Jeshi la Polisi na vyombo vingine vyote  vya Ulinzi na Usalama viko imara, makundi ya kiuhalifu na wahalifu wote wajue hawana pa kukimbilia, watakamatwa.

Imetolewa na:
Advera John Bulimba – SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi.

Watumishi HEWA Wakopa Mamilioni ya Pesa Benki......TAMISEMI Mwanza Yaongoza kwa Rushwa

$
0
0
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rusha Mkoani Mwanza  Mhandisi Ernest Makale
*******

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mwanza, imebaini kuwepo kwa watumishi hewa zaidi ya watano ambao uongozi wa mkoa huo haukuyawasilisha majina yao kwa Rais Dk. John Magufuli huku yakionekana kukopa fedha benki.

Pia Takukuru imesema kuwa majina ya watumishi hewa hao baada ya kufanya uchunguzi wamebaini hukopeshwa fedha kwa kisingizio kwamba wao ni watumishi wa Serikali kitendo ambacho ni cha uongo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, Ernest Makale wakati akitoa taarifa ya robo mwaka kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu, ambako alisema  majina yaliowasilishwa kwa Mkuu wa Mkoa huo, John Mongella sio kamilifu.

Amesema watumishi hao hewa wamekuwa wakikopa fedha kutoka benki mbalimbali kwa kutumia nyaraka za kughushi jambo ambalo alidai kwamba kuna baadhi ya watumishi wasio waaminifu wanaohusika kufanya udanganyifu huo.

Amesema pia katika uchunguzi wao unaonesha kuwa majina ya watumishi yaliowasilishwa na baadhi ya halmashauri za mkoa huo sio kamilifu kwani kuna watumishi wengine ambao hawajaorodheshwa.

Makale amesema kuwa kutokana na kuonekana kwa hali hiyo Takukuru inaendelea kufanya uchunguzi wa kina kuwabaini watumishi hewa wengine na watumishi wengine wanaoshirikiana nao.

“Kuna dalili za wazi ambazo zinaonesha kuna watumishi wasiokuwa waaminifu wa halmashauli ambao wanahusika kufanya vitendo hivi vya udanganyifu, atakaebainika atafikishwa mahakamani,” amesema Makale.

Watumishi wadakwa kwa utapeli
Makale pia amesema kuwa Takukuru Mkoa wa Mwanza katika kipindi cha miezi hiyo tayari imewakamata aliyekuwa Meya wa Ilemela, Henry Matata, Justine Lukaza (Mhandisi wa Manispaa ya Ilemela) na Mfanyabiashara, Hemed Hamad kwa kosa la kutoa zabuni feki ya kutoza ushuru kwenye stendi ya mabasi ya Buzuruga jijini hapa.

Watumishi wengine waliokamatwa kwa makosa ya kutumia vibaya madaraka yao ni pamoja na aliyekuwa Mganga wa Wilaya ya Magu, Patrick Mwindunga, Afisa Ugavi wa Wilaya ya Misungwi, Zabron Marwa, anaetuhumiwa kuingia manunuzi feki.

Wengine ni wauguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi, Masalu Kangalukwi na Amon Shija wanaotuhumiwa kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa wagonjwa.

TAMISEMI yaongoza kwa Rushwa
Katika taarifa hiyo, Mhandisi Makale amebainisha kuwa Takukuru imepokea jumla ya malalamiko 45 yanayohusiana na vitendo vya rushwa kutoka kwa wananchi ambapo katika malalamiko hayo, 27 yameelekezwa kwa watumishi wa idara za Serikali za Mitaa (TAMISEMI) hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 60. Kati ya malalamiko hayo 27, malalamiko 13 yameelekezwa katika idara ya ardhi.

Amesema idara zinazofuata kwa kulalamikiwa ni Mahakama yenye malalamiko tisa, polisi malalamiko sita na idara ya afya malalamiko matatu.

Mhandisi Makale amesema kesi 33 zinaendelea Mahakamani kutokana na vitendo vya rushwa Mkoani Mwanza huku kesi sita zikiwa ni mpya katika kipindi cha miezi mitatu na nyingine zikiwa katika upelelezi. 


Mwakyembe: Bora Tufe Masikini Kuliko Kuwapigia Magoti Wazungu

$
0
0

DK. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na Sheria, amesema kuwa Tanzania ni bora iendelee kutaabika na watanzania wafe wakiwa masikini kuliko kuendelea kunyanyaswa na mataifa ya ulaya.

Mwakyembe ambaye hata hivyo hakuyataja mataifa hayo lakini moja kwa moja ilionekana kuyagusa baadhi ya mataifa ya Ulaya pamoja na Serikali ya Marekani iliyovunja uhusiano na Serikali ya Tanzania katika mambo yote yanayohusu miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na mfuko wa changamoto za millenia (MCC).

Mwakyembe ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na watumishi wa wizara ya katiba na sheria jijini hapa, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi kwa mkoa wa Mwanza.

Mwakyembe ambae pia ni mbunge wa Jimbo la Kyela mkoani Mbeya, amesema kuwa anashangazwa na baadhi ya watu wanaotaka kuliingiza taifa katika mambo mabaya yasiofaa na yalioko kinyume na maadili ya watanzania.

Amesema mataifa hayo yamekuwa yakionekana kuilazimisha Tanzania kuingia katika mambo yasiyokubalika na watanzania wenyewe ikiwemo suala la `ushoga` kitendo ambacho alidai ni cha hovyo.

“Ni bora tufe masikini kuliko kuendeshwa kwa hofu, wao wanataka watuendeshe tu, sisi vitu kama vya ushoga vinapaswa kupingwa vibaya na haiwezekani kabisa.

“Vitu kama vya ushoga ni vya hovyo na kama watanzania hatukubaliani navyo, hata maadili yetu yenyewe hayataki mambo kama hayo,” amesema Mwakyembe.

Machi 29 mwaka huu, Serikali ya marekani kupitia kwa bodi ya wakurugenzi wa MCC ilitangaza uamuzi wa kuinyima Serikali Dora za kimarekani Milioni 472.8 ( zaidi ya Sh. Trioni 1 na bilioni 20) kutokana na marudio ya uchaguzi wa serikali ya Zanzibar na sheria ya makosa ya mtandao. 

Hata hivyo, Marekani kupitia kwa balozi wao hapa nchini Mark Childress, jana ilionyesha kulegeza msimamo wao ambapo walisema wataendelea kuisaidia Tanzania hasa katika sekta ya Afya  na  Elimu licha ya changamoto za kisiasa zilizopo

Mahakimu  mizigo  kukiona
Katika hatua nyingine Waziri Mwakyembe, amesema kuwa ofisi yake tayari imekwishaunda kamati za madili za Mahakama, ili kudhibiti baadhi ya mahakimu wanaofanya kazi kwa mazoea na kutokufata maadili.

Amesema kuwa kuundwa kwa kamati hiyo, kutasaidia watu kufanya kazi kwa kuzingatia weledi wa fani hiyo muhimu nchini kwani kuna baadhi ya mahakimu walevi wasiofuata maadili ya kisheria.

“Tuna taarifa wapo baadhi ya mahakimu ambao ni walevi na wengine wanafikia hatua ya kupewa msaada baada ya kuzidiwa na pombe lakini sasa kesho unashangaa huyo hakimu anakuja na yeye kutoa uamzi,” amesema Mwakyembe.

Amesema kuwa lengo jingene la kuunda kamati hiyo ni kutaka kurekebisha baadhi ya tabia za mahakimu wakiwemo wa Mahakama za mwanzo kutenda haki kwa Wananchi wote bila kumpendelea mtu.

Rais Magufuli Atengua Uteuzi Wa Mhariri Mtendaji Wa Magazeti Ya Serikali (TSN) Gabriel Nderumaki.

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Bw. Gabriel Nderumaki.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 14 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia tarehe 18 Machi, 2016.

Kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Bi. Tuma Abdallah kukaimu
nafasi hiyo.

Bi. Tuma Abdallah ni Mhariri Mtendaji Msaidizi wa Magazeti ya Serikali (TSN)

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam-14 Aprili, 2016

Ziara ya Mhe. Salva Kiir, Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Tarehe 15 Aprili 2016

$
0
0

Ziara ya Mhe. Salva Kiir, Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Tarehe 15 Aprili 2016.
 
Mhe. Salva Kiir Mayardit, Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini atafanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini Tanzania tarehe 15 Aprili 2016. 

Rais Kiir anakuja nchini kusaini Mkataba wa kuwezesha Jamhuri ya Sudan Kusini kuwa Mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambapo tangazo la kukubaliwa kuwa Mwanachama wa EAC lilitangazwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC uliofanyika jijini Arusha mwezi Machi 2016.
 
Rais Kiir atawasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 3:00 asubuhi na baadaye ataelekea Ikulu na kupokelewa na Mwenyeji wake, Mhe. Rais John Pombe Joseph Magufuli.

Baada ya hapo, Viongozi hao watashiriki hafla ya uwekaji saini ya Mkataba huo iliyopangwa kuanza saa 5:00 asubuhi na kisha watapata fursa ya kutoa hotuba na kusaini Communique.
 
Rais wa Sudan Kusini atashiriki hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa heshima yake na Mwenyeji wake kabla ya kuondoka nchini baada ya hafla hiyo.
 
Sudan Kusini ni nchi ya sita kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo inaongeza fursa nyingi za kiuchumi ambazo zinaweza kuzifaidisha Nchi Wanachama ikiwemo Tanzania, endapo mipango madhubuti itawekwa kuzichangamkia.

Fursa hizo ni pamoja na za kibiashara kwa kuwa bidhaa nyingi zinazotumika Sudan Kusini zinaagizwa kutoka Nje ya nchi. 

Hivyo, jamii ya wafanyabiashara wa Tanzania wanahimizwa kuchangamkia fursa zinazopatikana nchini humo na ndani ya Jumuiya kwa ujumla.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Dar es Salaam, 14 Aprili, 2016

Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Rais-tamisemi, George Simbachawene Avunja Bodi Ya Machinga Compelex

$
0
0

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amevunja bodi ya Soko la Machinga Complex lililopo Ilala Mchikini Dar es Salaam na kulikabidhi kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

Akizungumza leo katika mkutano wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini (JWT), Simbachawene amesema wazo la kuanzishwa kwa soko hilo lilikuwa zuri lakini Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeshindwa kulitekeleza.

Jengo hilo lilikamilika kujengwa mwaka 2010 likiwa na uwezo wa kuchukua wafanyabiashara 4206, lakini Waziri Simbachawene alisema limeishia kuwa makazi ya popo

Asilimia 71 Ya Watanzania Hawataki Kufanya Kazi.

$
0
0

Na Raymond Mushumbusi – MAELEZO
Utafiti uliofanyika hivi karibuni na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) umebaini kwamba asilimia 71 ya watanzania wanatumia muda mwingi kufanya shughuli zisizokuwa za uzalishaji mali wala tija binafsi kwao na Taifa kwa ujumla.

Akizundua taarifa ya utafiti huo leo jijini Dar es salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Ajira,Vijana na watu wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama  amesema kuwa idadi hiyo hufanya kazi zisizoleta tija kwao na taifa na muda mwingi huutumia kujihudumia binafsi kwa kulala na starehe nyingine.

Ameeleza kuwa takwimu hizo zinaonesha wazi ni kwa namna gani watanzania wanashindwa kujishughulisha katika kufanya kazi zenye kuwaingizia kipato na badala yake wanatumia muda wao mwingi kufanya shughuli zisizo za uzalishaji hasa kufanya starehe mbalimbali.

“Ndugu zangu watanzania unakuta mtu amekaa baa au anacheza “poll table” kuanzia asubuhi mpaka jioni na hujui anafanya kazi gani ya uzalishaji, ndugu zangu tuone aibu basi tujishughulishe tulijenge taifa letu ili kujiletea maendeleo yetu na nchi yetu.”

Aidha, matokeo hayo yamebainisha kuwa asilimia 18.5 ya wananchi wanafanya kazi za uzalishaji na asilimia 10.6 ni wale wanaofanya shughuli za nyumbani zisizo na malipo huku uchambuzi wa kijinsia ukionesha kuwa wanaume asilimia 23.8, wanatumia muda mwingi kwenye shughuli za kiuchumi ikilinganishwa na asilimia 13.5 ya wanawake.

Amefafanua kuwa wanawake ambao ni asilimia 16.5 katika utafiti huo wanatumia muda mwingi kufanya kazi za nyumbani zisizo na malipo ikilinganishwa na asilimia 4.4 ya wanaume.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisa ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa upatikanaji wa Takwimu hizo utaisaidia Serikali kupata mbinu sahihi za kuondokana na tatizo la ajira nchini kwa kuunganisha nguvu kutoka sekta isiyo rasmi ili kuleta changamoto katika soko la ajira nchini.

Amesema kuwa hii ni mara ya tano Tanzania inafanya utafiti huo na kubainisha kuwa ulianza  mwezi Januari hadi Desemba,  2015 ukitumia sampuli ya Sensa  ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyotumika kupata taarifa sahihi ya takwimu hizo.

Aidha, amebainisha kuwa ili kufanikisha utafiti huo NBS imeshirikiana na wadau mbalimbali ikwemo Wizara ya kazi na Ajira,Shirika la Kazi Duniani (ILO),Benki ya Dunia (WB),Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) na Asasi zisizo za Kiseikali.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu),Jenista Mhagama,akizindua ripoti ya matokeo ya utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2014 katika Viwanja vya Karimjee,Dar es Salaam. Wengine wanaoshuhudia ni kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Takwimu nchini,Dk.Albina Chuwa, Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Takwimu za Jamii,Ephraim Kwesigabo na Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani,Marry Kawar.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images