Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Awakomalia Washtakiwa wa Tumbili .....Mawakili wa washtakiwa wapambana ili wateja wao wapatiwe dhamana

$
0
0

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), amewasilisha mahakamani hati ya kupinga dhamana kwa washtakiwa wa kesi ya kusafirisha tumbili 61 kwenda nchini Armenia.

Hata hivyo, jopo la mawakili watano wa utetezi wakiongozwa na wakili maarufu kutoka jijini Dar es Salaam, Majura Magafu, walipinga hati hiyo wakidai haijawasilishwa kihalali mahakamani.

Hati hiyo iliwasilishwa Mahakama Kuu Moshi jana na mawakili wa Serikali, Wancho Simon na Salim Msemo, muda mfupi kabla ya kuanza kusikilizwa kwa maombi ya dhamana ya washtakiwa hao.

Akiwasilisha pingamizi la hati hiyo mbele ya Jaji Mfawidhi, Aishiel Sumari, Wakili Magafu alisema DPP alipaswa kuwasilisha hati tatu tofauti kwa kila maombi badala ya kuwasilisha hati moja.

“Hati hii iliwasilishwa kabla ya amri ya Mahakama yako ya kuyaunganisha maombi ya dhamana ya washtakiwa, kwa hiyo DPP alipaswa kuwasilisha hati kulingana na kila maombi,” alidai Magafu.

Alisema maombi yao ya dhamana yamesajiliwa kwa namba 3/2016, 4/2016 na 5/2016, DPP alitakiwa kuwasilisha hati tatu tofauti kwa maana ya hati moja kwa kila maombi yaliyoko kortini.

“Hoja yetu hapa ni je hati hii ya DPP iko sahihi mbele ya Mahakama yako? Ombi letu ni uitupilie mbali na ombi letu la dhamana lisikilizwe,” aliomba Magafu.

Hata hivyo, wakili huyo alisema kama Mahakama itaona hati hiyo imewasilishwa kihalali, basi iwaruhusu kuzungumzia uhalali wa hati yenyewe kisheria na madhara yake.

Akijibu hoja hiyo, Wakili Simon alisema wakili mwenzake (Magafu) anaipotosha Mahakama na hakunukuu sheria yoyote inayoipa nguvu hoja yake ya kupinga hati hiyo ya DPP.

Wakili huyo alifafanua, hata hati za kuitwa shaurini walizotumiwa hazikuwa tofauti kulingana na namba za maombi, bali walitumiwa hati moja ikitaja maombi yote sehemu moja.

Akitoa uamuzi mdogo kuhusu mabishano hayo, Jaji Sumari alisema amepitia kwa umakini hati ya DPP na kujiridhisha kuwa iko sahihi mbele ya Mahakama.

Hata hivyo, Jaji Sumari alisema hoja ya hati hiyo imewasilishwa kabla ya wakati na kuutaka upande wa mashtaka kuwasilisha kwanza kiapo kinzani leo.

Alisema kama mawakili wa utetezi watakuwa na majibu ya ziada kutokana na kiapo hicho kinzani, wawasilishe majibu kesho na majibizano yasikilizwe Aprili 14, mwaka huu.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya April 12

Kigogo wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) ‘Ajimilikisha’ kiwanja cha shirika.....Naibu Waziri Ampa Siku 7 za Kujieleza

$
0
0
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura, ametoa siku saba kwa Meneja Rasilimali Watu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Neema Mrindoko kujieleza sababu za kuandika jina lake katika kiwanja cha shirika kilichopo Kisarawe mkoani Pwani.

Wambura alitoa agizo hilo juzi alipotembelea kiwanja hicho kilichopo eneo la Kimani ambacho mpaka sasa hakijakamilisha usajili wake na kupewa hati wakati kilinunuliwa na shirika hilo mwaka 2012. 

Kiwanja hicho kimejengwa nyumba za watumishi ambao wangekuwa wakifanya kazi katika kituo cha Kisarawe lakini hazijakamilika.

“Natoa siku saba, mtu huyu awe amenipa maelezo ya kutosha kwa nini hati hiyo imesainiwa na mtu mmoja ambaye ni yeye na ameandika jina lake badala ya jina la Shirika, ina maana alikuwa hajui? Hii ni makusudi,” alisema Wambura.

Wambura alisema mtu huyo amefanya makusudi kwa nafasi yake kushindwa kutambua kukaa miaka yote hiyo bila kupewa hati na kutelekezwa bila kuendelezwa ni ufisadi ambao hauwezi kuvumiliwa.

Awali Wambura alipokuwa akipokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo, Mwanamvua Mrindoko, alisema kiwanja hicho chenye meta za mraba 9,567 kilipimwa na kusajiliwa kwa namba 68,480 mwaka huo huo shirika liliomba kuandaliwa hati.

Mrindoko alisema utaratibu wa ukamilishaji hati ulifanyika na walilipia na kujaza fomu ya maombi ya hati. Ilielezwa kwamba, baada ya TBC kuisaini na kuirudisha Wizara ya Ardhi ilionekana kuwa na upungufu ikarudishwa.

Alitaja upungufu huo kuwa ni hakukuwa na nakala halisi ya kuanzishwa shirika na pia fomu hiyo ilisainiwa na mtu mmoja badala ya wahusika wawili wa TBC na hivyo kukwamisha mchakato wa kupata hati.

Naibu Waziri huyo alipomhoji Ofisa miradi wa wizara hiyo, Macksselin Chota ambaye alikuwepo kwenye ziara, alisema maelezo hayo ni sahihi na kwamba upungufu wanaufanyia kazi. Chota alisema viwanja vingi vya TBC havijapata hati.

Kati ya viwanja 55, viwanja 19 pekee ndivyo vyenye hati. Alisema pia viwanja vingi viko katika migogoro mbalimbali kama vile uvamizi na pia uporaji. Naibu Waziri Wambura aliagiza ndani ya siku hizo saba hati ya kiwanja hicho cha Kisarawe iwe imepatikana.

Alitaka shirika pia lieleze ni namna gani watafanya kuendeleza majengo ambayo yameanza kujengwa hapo. 

“Hii inatia mashaka kabisa, mnachelewesha kupata hati na baadaye viwanja vinaingia kwenye migogoro, unafanya hivyo ili baadaye nyie wenyewe mzunguke, tutashindwaje kuamini hivyo?” Alihoji Naibu Waziri.

Wachina Watatu Wahukumiwa kwa Kukwepa Kodi.......Waliuza mali ya Sh550,000 wakaandika risiti ya 200,000

$
0
0

Raia watatu wa China wamehukumiwa kwenda jela kifungo cha miezi sita au kulipa faini ya Sh4 milioni kila mmoja, baada ya kukiri kukwepa kodi ya Sh350,000 kwa kutumia Mashine ya Kielektroniki (EFDs).

Washtakiwa hao ambao walifikishwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala ni Liu Songyue, Liu Pengfey na Jiang Zedong ambao ni wamiliki wa Kampuni ya M/S Sen He Co.Ltd.

Hata hivyo, washtakiwa hao walilipa faini hiyo na kuepa kwenda jela miezi sita.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Juma Hassan alisema washtakiwa hawana kumbukumbu ya makosa ya awali na kwamba, Sheria ya Kodi inaruhusu washtakiwa wenye makosa kama hayo kulipa faini, kifungo au vyote kwa pamoja.

Pia, Hakimu Hassan aliamuru kutolewa kwa hati ya kukamatwa mshtakiwa wa nne ambaye hakufika mahakamani.

Alisema kutokana na washtakiwa kukiri makosa yao, watatakiwa kulipa faini ya Sh4 milioni kila mmoja, au jela miezi sita. 

Kabla ya kutolewa hukumu hiyo, Wakili wa washtakiwa, Nihimia Mkoko alidai washtakiwa wakilipa faini, wataendelea na shughuli zao na kulipa kodi vizuri kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Awali, Wakili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Marcel Busegano alidai washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kutoa taarifa za uongo kwa Kamishna.

Wakili Busegano alidai washtakiwa walitenda kosa hilo Machi 12 maeneo ya Tabata Shule, wilayani Ilala katika Kampuni ya M/S Sen He Co. Ltd.

 Alidai washtakiwa walitoa risiti ya mauzo kwa mteja, Mwise Wambura ya Sh200,000 kutoka kwenye mashine ya EFDs inayomilikiwa na kampuni hiyo.

Aliendelea kuwa siku hiyohiyo, maofisa wa TRA walitembelea eneo hilo kufanya ukaguzi na kugundua kuwa, walikwepa kodi kwa makusudi kwa kujifanya wamepokea kiwango hicho ilhali mteja alilipa Sh550,000.

Mshtakiwa wanne anatakiwa kufikishwa mahakamani hapo Mei 9.

Wafanyakazi 597 wa NIDA Walioachishwa Kazi Kuanza Kulipwa Kesho

$
0
0

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa nchini (Nida) imesema itaanza kufanya malipo ya madai ya wafanyakazi wake 597 waliokatishwa mkataba na mamlaka hiyo hivi karibuni.

Taarifa iliyotolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Modestus Kipilimba, ilisema malipo hayo yataanza kulipwa kesho asubuhi kwenye ofisi za mamlaka hiyo zilizopo katika jengo la BMTL.

Malipo hayo yatafanywa kwa mgawanyo. Mgawanyo wa kwanza utakuwa na kundi la kwanza, pili na tatu, ambao watalipwa kesho na mgawanyo wa pili, utakuwa na kundi la nne na tano ambao watalipwa keshokutwa.

Mgawanyo wa tatu utakuwa na kundi la sita litakalo lipwa Alhamisi, mgawanyo wa nne utahusisha kundi la 7 na 8 litakalolipwa Aprilu 16 na kundi la tano litajumuisha madereva na kada nyingine, litalipwa Aprili 17.

Aidha, taarifa hiyo iliwataka wadai hao kufika kwa wakati sambamba na kuwa na vielelezo na nakala halisi za mikataba yao ya kazi.

Awali, kulikuwa na malalamiko kutoka kwa wafanyakazi hao walioandamana baada ya tangazo la kufutwa kazi kuwa malipo yanayotarajiwa kutolewa na Nida hayasadifu uhalisia wa kile wanachokidai.

Makongoro Nyerere Awataka Watanzania Kuchangamkia Fursa Zilizopo Afrika Mashariki

$
0
0

Wananchi wa Tanzania wametakiwa kuchangamkia nafasi za kufanya baishara zilizopo kwa nchi za Afrika Mashariki kutokana na kuwepo makubaliano ambayo yanawapa wananchi wa nchi za Afrika Mashariki kufanya biashara kwa uhuru.

Hayo yalisemwa jana na Mbuge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere ambaye alidai kuwa nchi za Afrika Mashariki zinashirikiana kwa mambo mbalimbali ikiwepo umoja wa forodha, soko la pamoja, umoja wa fedha na shirikisho wa kisiasa.

Alisema kupitia makubaliano hayo Watanzania wana nafasi ya kwenda kufanya baishara katika nchi zingine bila kuzuiliwa na hivyo kuwa na nafasi ya kusambaza bishaa zao katika nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Huu ni muda wa Watanzania kuchangamkia nafasi zilizopo za kufanya baishara kwa nchi za Afrika Mashariki, vikwazo zilivyopo kwa sasa ni wananchi wengi wa Afrika Mashariki bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu hilo lakini tumejipanga katika hilo,” alisema Nyerere.

Alisema kwa kutambua changamoto hiyo ya wananchi wengi kutokufahamu nafasi hiyo, wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Tanzania wataendesha programu ya kuwaelimisha Watanzania jinsi wanavyoweza kunufaika na ushirikiano huo.

Alisema programu hiyo ilianza Aprili 4 na itafanyika hadi Aprili, 23 ambapo kwa kuanza wamepanga kukutana na Kamati za Bunge, Taasisi za Elimu ya Juu, vyombo vya habari, kutembelea soko la Kariakoo na soko la Samaki la Feri.

Pia Nyerere aliwataka Watanzania kuwa na mazoea ya kutafuta taarifa mbalimbali kupitia mitandao kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kukutana na fursa nyingi ambazo hawakuwa wakizifahamu awali.

Maneno ya Le Mutuz baada ya Mama yake ‘Anne Kilango Malecela’ kuondolewa kwenye ukuu wa mkoa

$
0
0

Jina lake la kuzaliwa ni William Malecela na jina lake maarufu la mitandaoni ni Le Mutuz ambaye ni mmiliki wa williammalecela.com na jana April 11 2016 aliamua kuwajibu wanaomuandama kutokana na uteuzi wa ukuu wa mkoa wa Shinyanga chini ya Anne Kilango Malecela ambaye ni mama yake  kutenguliwa.

Le Mutuz Aliandika: "Guys naomba kusema hivi nimepigania Rais Magufuli kuwa Rais na ninamuunga mkono kwa juhudi zake za kusafisha uozo hata kama unamuhusu Mama yangu mzazi kwa sababu hata mimi wafanyakazi wa Kampuni yangu wasipofuata masharti yangu kama muajiri ni lazima niwaondoe sasa Nina wafanyakazi 4 ambao ili kuwa nao nilipitia kama watu 100

"Now nimesikia kwamba Mama yangu hakufuata masharti ya muajiri wake so amefukuzwa kazi kwangu sina pingamizi wala ishu na Rais kwa sababu Sheria ni msumeno inatakiwa kukata kote….now naona maneno mengi sana ambayo hayana UKWELI wala Msingi ndani yake

"Nimekaa Majuu Miaka 30 nimerudi Bongo nimesota nimeanzisha Kampuni yangu ya BLOGU YA WANANCHI MEDIA COMPANY LTD na sasa hivi nipo njiani kuhamia kwenye RADIO na TV now katika Maisha yangu sijawahi kuishi kwa kumtegemea mtu ila ninaishi kwa kumtegemea MUNGU‘

"Nilikuwa nafagia Majuu na pia nahangaika Baharini wakati Baba yangu Makamu wa Rais na Waziri Mkuu Leo eti Maisha yangu yataharibika kwa sababu Mama yangu sio RC? hahahaha imenichekesha sana hizi CHUKI guys zitawaua bure mnazitoa wapi? ….I mean Jana nimerudi Nairobi na sasa najitayarisha kwenda South Africa weekend hii na nikirudi ni safari ya Dubai eti Mama yangu kuwa RC wa Wiki Mbili Shinyanga kunahusika na Maisha yangu hapa Mjini Downtown na hizi Safari zangu za kikazi?

"Hahahahahaha imenichekesha sana guys nimeshasema Mara nyingi kwamba ninajua sana kwamba uhusiano wa Public na Watu Maarufu huwa ni feki ila sikutegemea kwamba watu wanaweza kuwa na CHUKI za mpaka kulazimisha kwamba eti u RC wa Mama yangu kwa Wiki Mbili tu unahusika na Maisha yangu hapa Downtown kwamba Nina Ofisi

"Apartment na Kampuni kwa sababu Mama yangu alikuwa RC wa Shinyanga kwa Wiki Mbili tu na sasa Maisha yangu yataisha HAHAHAHAHAH jamani this is the best joke of my life….otherwise guys nimewasikieni ila ninasimama na Rais Magufuli na I feel sorry for my Mum ila ni Kawaida in life na Sheria ni msumeno ….otherwise Lov U guys HAHAHAHAHa and I am Super Humbled U know" – le Mutuz Nation

Baada ya kumtimua Anne Kilango, Rais Magufuli Asema Ametuma Watu Kuwarekodi Mawaziri Wanaolalamika ili nao Awatumbue Majipu

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe  Magufuli amesema amewatuma watu kuwarekodi mawaziri ambao wamesikika wakilalamika 'chinichini' kukatwa kwa fedha za matumizi mengineyo ( OC- Other Charges )  katika bajeti ya serikali ya mwaka ujao wa fedha.

"Mawaziri wengine nasikia wanalalamika kweli,sasa nimetuma watu kuwarekodi kwa sababu mind set (fikra) zao bado hazijabadilika,wanafikiri watu bado tupo kwenye trend  hiyo hiyo,wasomi ni wengi,unaweza ukawateua leo na kesho ukawabadilisha, ili mradi twende kwenye trend ninayoitaka," alisema Magufuli.

Rais Magufuli  aliyasema hayo jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia hatua ya bunge kubana matumizi na kuwezesha kupatikana kwa kiasi cha shilingi bilioni 6 ambazo zitaelekezwa kwenye utengenezaji wa madawati.

“Chief Secretary(Katibu Mkuu Kiongozi ), huo ndio muelekeo kwa Makatibu Wakuu, waache kudai OC… Nawasikia watu wanadai eti OC ni kidogo. Wakiona hazitoshi basi waache kazi, maana wenzao wabunge wamesema ni nyingi na wamebana matumizi," alisema Rais Magufuli na kuongeza:

"Katibu wa bunge ameonyesha mfano,kwa nini wengine washindwe? Mtaona katika bajeti tumekata hizo OC ambazo zilikuwa ni ulaji mtupu, tumeongeza bajeti ya maendeleo kutoka kati ya bilioni 26 na 27 hivi za mwaka jana hadi asilimia 40, fedha za bajeti ziende kufanya miradi ya maendeleo, zikawasaidie watu masikini."

Hakimu FEKI Atiwa Mbaroni

$
0
0

Mkazi  wa kijiji cha Kanyama Kata ya Bujora Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, Erick Mkundi (23), ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kufanya kazi kama Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kongoro akiwa hana sifa hiyo.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuifanya kazi hiyo kuanzia Januari hadi Aprili 6, mwaka huu alipobainika baada ya kushindwa kujitambulisha kwa Hakimu Mfawidhi wa wilaya hiyo, Edmund Kente, kuwa ni hakimu na bila kuonyesha nyaraka zozote zinazomthibitisha kuwa  na taaluma hiyo.

Aidha, ilidaiwa kuwa Mkundi alijikabidhi katika mahakama hiyo na kuanza kuendesha kesi na hadi anatiwa mbaroni, tayari alishatoa hukumu kwa washtakiwa wanne na wengine kadhaa kuwasotesha mahabusu.

Akizungumza jana, mmoja wa watumishi wa mahakama hiyo aliyeomba jina lake lisitajwe kwa madai kuwa si msemaji, alieleza kuwa walifanya kazi na Mkundi kwa miezi minne wakiamini kwamba ni mtumishi halali wa Idara ya Mahakama.

“Mkundi tuliamini ni hakimu halali, kwani alikuwa akiletwa na gari kama mheshimiwa fulani hivi, lakini baada ya kukamatwa Aprili 7, mwaka huu, ndipo tulipogundua ni mfanyakazi ‘hewa’, alisema mtoa taarifa huyo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Magu, Charles Mkapa, alisema Mkundi alikamatwa baada ya polisi kupewa taarifa zake za kufanya kazi bila kibali.

“Kweli tunamshikilia Mkundi tangu Aprili 7, mwaka huu, kwa tuhuma hizo, lakini taarifa kamili mnaweza kuzipata kwa Hakimu wa Wilaya ya Magu, kazi yetu ilikuwa kumtia mikononi mwa polisi,” alisema Kamanda Mkapa.

Awali, ilisemekana mtuhumiwa huyo aligundulika kuwa ‘feki’ baada ya kushindwa kulipa Sh. 40,000 yakiwa ni malipo ya gari alilokodi kwa ajili ya kutembelea kwenda na kurudi kazini pamoja na maeneo mbalimbali.

Habari zaidi zilidai kuwa mtuhumiwa Mkundi baada ya kushindwa kulipa gharama hizo, mmiliki wa gari alitoa taarifa kwa bosi wake wilayani na ndipo alipoanza kufuatiliwa.

Aidha, Mkundi ilidaiwa alikuwa akipokea rushwa na zawadi mbalimbali kutoka kwa watu aliokuwa akiwahudumia kimahakama, zikiwamo mbuzi pamoja na fedha kwa lengo la kusimamia kwa ukaribu tuhuma zinazowakabili.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Francis Kabwe, alipoulizwa kuhusiana na tukio la ‘hakimu huyo feki’, alisema hajapata taarifa kamili, lakini atalizungumzia suala hilo leo.

Sheikh afungwa jela miaka 30 kwa kubaka

$
0
0

Mahakama  ya Wilaya ya Kigoma imemhukumu Sheikh wa Msikiti wa Goma, Hassan Bamba (48), kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kukutwa na hatia ya kubaka.

Sheikh huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Kitongoni, mwenye umri wa miaka 14 na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu wa Mahakama hiyo, Frola Mtariania, baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo.

Hakimu Frola, akitoa hukumu hiyo, alisema mahakama inatoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa viongozi wengine wenye tabia ya kikatili kama yake.

Alisema upande wa mashtaka ulipeleka mashahidi watano, pamoja na kielelezo cha PF3, ambacho kilithibitisha kwamba Sheikh Bamba mshtakiwa alitenda kosa hilo.

Alipotakiwa kujitetea ili kupunguziwa adhabu, akiongozwa na wakili wa kujitegemea Method Kabuguzi, mshtakiwa aliangua kilio na kuiomba mahakama impunguzie adhabu kwa sababu ana familia inamtegemea.

Pia alidai ni kosa lake la kwanza tena shetani alimwingilia. Hakimu Frola alitupilia mbali utetezi huo na kusema: 

"Mshtakiwa ukiwa kiongozi wa dini, kitendo ulichokifanya si cha kijamii maana wewe ndiwe unayefundisha watu kuachana na maovu cha kushangaza unakuwa ndiye wa kwanza kuyatenda maovu.

"Sasa utakwenda gerezani miaka 30 ili ukajifunze tabia ya kuwa kiongozi bora wa dini, kwa sababu huku uraiani umeshindwa kuishi na jamii."

Awali, akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Anita Julius, alidai kuwa Januari Mosi, mwaka huu, saa 4 asubuhi eneo la Ujiji Kigoma, mshtakiwa huyo alibaka msichana huyo.

Ilidaikwa kuwa siku ya tukio mtoto aliyebakwa akiwa na pacha wake, ambao baba yao ni rafiki wa sheikh huyo, walikwenda kwa sheikh huyo kwa ajili ya kuombewa duwa na kufanyiwa dawa kwa ajili ya kufaulu mtihani wa kuingia darasa la saba.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, baada ya kufika, Bamba alimtuma mwenzake aende shuleni kuchukua mchanga na ndipo alipomfanyika kitendo hicho yule aliyebaki.

Mwenzake aliporejea, ilidaiwa kuwa alimkuta pacha wake analia na alipomuuliza alimjibu kuwa amebakwa na Bamba. 

Umati mkubwa wa wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji, wakiwamo waumini wa msikiti aliokuwa akiswalisha, ulikusanyika mahakamani na kushuhudia Sheikh huyo anapelekwa jela.

Moto Wateketeza Soko Karagwe Mkoani Kagera Usiku Wa Kuamkia Leo

$
0
0

Moto mkubwa umezuka na kuteketeza soko la mji wa Kayanga wilaya ya Karagwe mkoani Kagera usiku wa kuamkia leo. 

Moto huo ambao unadaiwa kuwa ulianza majira ya saa 2 ya usiku wa jana umeteketeza vibanda 35  na maduka matano.

Wafanyabiashara wengi katika soko hilo wamesikitishwa na kutokea kwa janga hilo, kwani wengi wao wamesema walikuwa na mikopo na hawakuwa na bima ya mali zao.

Jonasi Nyarugenda ni miongoni mwa wafanyabiashara hao anasema “Moto umeteketeza stoo zangu nne zenye bidhaa mbalimbali kama sukari, mchele, ngano na mafuta, kwakeli ukitathimini kwa haraka siyo chini ya milioni 45 zimepotea.”

Amesema kwamba alikuwa hana bima katika mkopo wake wa milioni 20 kutoka katika benki.

Hasara hiyo kwa kiasi kikubwa imechangiwa na ukosefu wa vifaa vya kuzima moto. Wananchi wa Karagwe imewapasa kusubiri gari la Zimamoto kutoka Bukoba Mjini (magari ya uwanja wa ndege) ambako ni kilomita 120 mpaka kufika karagwe mjini. Hata hivyo magari hayo yalikuta maduka mengi katika soko hilo yamekwishateketea.

Diwani wa kata ya Kanoni wilayani karagwe, Sabi Rwazo amesema tukio hilo limewashtua na ni tukio la kwanza la moto kuunguza soko wilayani humo. 

Anasema tatizo la ukosefu wa gari la zima moto linachangiwa na uhaba wa fedha. 

“Mara nyingi katika bajeti yetu imekuwa ikishindwa kununua gari.” Amesema Rwazo na kusema maombi yao yako serikali kuu.

Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Deodatus Kinawiro amesema kuwa serikali ya wilaya yake  iko katika mchakato wa kupata  gari la zima moto hivi karibuni, 

“Bahati nzuri nilikuwa Dar es Salaam, nimekutana na kamishna mkuu wa zima moto ameniahidi kunipatia gari jipya,” amesema Kinwiro na kuongeza kuwa, “wakati wowote gari hilo litafika wilayani Karagwe.”

Hata hivyo baadhi ya wananchi wanasema hawakubaliani na kauli hiyo ya mkuu wa wilaya kwa sababu wamekuwa wakitozwa kiasi cha TZS 30,000 kwa mwezi ili kuchangia huduma za zimamoto wilayani hapo lakini wanashangaa kwa nini hawapati elimu ya kujikinga na majanga, na hakuna hata gari la dharura.

Mpaka sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana lakini taarifa za awali zimeonesha kuwa kuna Mamalishe mwenye kibanda sokoni hapo aliacha jiko lake bila kuzima hivyo likashika nguo zilizokuwa katika kibanda hicho na kusababisha moto kusambaa ghafla.

Mke wa Waziri Mkuu atoa msaada wa mashuka kwa akinamama waliojifungua katika Hospitali ya wilaya ya Ruangwa

$
0
0

Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa amefanya ziara katika Hospitali ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi na kutoa msaada wa mashuka kwa akinamama waliojifungua.

Pia ametumia fursa hiyo kuwapongeza madaktari na wauguzi wa Hospitali ya wilaya ya Ruangwa kutokana na kuwahudumia vizuri wananchi na kuwaomba  waendelee kufanya kazi hiyo kwa mujibu wa maadili ya kazi yao.

Mke wa Waziri Mkuu ameyasema hayo jana  wakati alipotembelea wodi ya akinamama waliotoka kujifungua na kufurahishwa na hali ya utoaji huduma hospitalini hapo, ambapo  aliwasisitiza kuendelea moyo huo kwa sababu wao ndio wamebeba dhamana ya afya za wananchi.

“Nimefurahi kukuta wazazi wanahudumiwa vizuri na wenyewe wamekiri kwamba huduma zinazotolewa hospitalini hapa ni za kuridhisha, tofauti na tulivyozoea kusikia wagonjwa wakiwalalamikia wauguzi, hivyo ni jambo la kujivunia, hongereni sana” amesema.

Mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika wodi hiyo Hamisa Rashid ambaye amelazwa katika wodi hiyo  amesema alifikishwa hospitalini hapo wiki mbili zilizopita akiwa katika hali mbaya na ameweza kuhudumiwa vizuri na sasa anakaribia kutoka.

“Mimi nilikuwa sijitambui, siwezi kufanya kitu chochote lakini baada ya kuletwa hospitalini hapa madaktari kwa kushirikiana na wauguzi wamenihudumia vizuri na sasa naweza hata kwenda chooni mwenyewe na bila msaada wao mimi ningekuwa nimepoteza maisha kutokana na hali yangu ilivyokuwa,” amesema Hamisa.

Mbali na kutoa msaada huo wa mashuka pia ametoa baiskeli mbili kwa ajili ya wanawake wawili walemavu lengo likiwa ni kuwawezesha kufanya shughuli zao za kijamii kwa urahisi.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Rehema Omary amemshukuru mke wa Waziri Mkuu kwa msaada huo, ambapo alimuomba Waziri Mkuu, Majaliwa awawezeshe kwenda kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazofanywa na walemavu ikiwemo michezo.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amewataka watumishi wa hospitali hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuachana na utendaji kazi wa mazoea kwa sababu umepitwa na wakati.

Pia amesema amefurahishwa  na kitendo cha wagonjwa kukiri kuwa wanahudumiwa vizuri tofauti na hospitali zingine hivyo kuwataka kuendelea na ari hiyo ya kufanya kazi kwa bidii, maarifa na weledi mkubwa.

Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu

Obama: Tulikosea Sana Kuivamia Libya na Kumuondoa Muammar Gaddafi

$
0
0
Rais wa Marekani Barack Obama amekiri kwa mara ya kwanza kwamba serikali yake ilifeli katika kutatua mzozo wa Libya.

Amesema hilo huenda ndilo “kosa kubwa” zaidi alilolitenda wakati wa utawala wake.

Bw Obama amesema Marekani haikua na mpango mahususi wa jinsi taifa hilo litakavyotawaliwa baada ya kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar Gaddafi.

Alisema haya katika mahojiano na runinga ya Fox News kuangazia mafanikio na mapungufu ya utawala wake.

Hata hivyo ametetea hatua ya kuingilia kijeshi nchini Libya. Marekani na Muungano wa NATO zilitekeleza mashambulio ya anga kuwalinda raia baada ya kuzuka maasi dhidi ya Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Lakini baada ya mauaji ya kiongozi huyo, Libya ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya makundi ya waasi huku makundi mawili yakiunda serikali na mabunge tofauti.
Katika hatua za kurejesha utulivu serikali ya muungano wa kitaifa inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imewasili katika mji mkuu Tripoli ili kuanza mipango ya kuongoza nchi ya kurejesha hali ya kawaida.

Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika Novemba na Rais Obama atakabidhi madaraka kwa mrithi wake Januari mwakani baada ya kuongoza kwa mihula miwili.

Chanzo: BBC

Madudu Kibao Yabainika Katika Uhakiki wa Madeni ya Watumishi Wanayoidai Serikali

$
0
0

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Kassim Majaliwa amesema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) , amefanya uhakiki wa madeni yanayodaiwa serikali na watumishi na kubaini madudu kibao.

Amesema madai mengine yameonyesha mashaka ambapo amewataka wakurugenzi wa Halmashauri na Wakaguzi wakuu wa ndani kujiridhisha ukweli wa madai hayo kabla ya kuyafikisha serikalini kwa ajili ya malipo.

“Madai mengine yanatia mashaka, sisi hatuhitaji kuletewa madeni ya hovyo hovyo ni vema Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakaguzi wa ndani wakajiridhisha kabla kuyapeleka serikalini kwa ajili ya malipo.

"Madeni mengine ya ajabu, mfano unakuta mtumishi mmoja anaidai serikali sh. milioni 30,  jambo ambalo ni gumu hata kama alihamishwa haiwezekani kufikia kiwango hicho, pia kuna baadhi ya majina yamejirudia mara nne,” amesema.

Waziri Mkuu, Majaliwa ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa hospitali ya wilaya ya Ruangwa alipotembelea Hospitali hiyo wakati akiwa katika ziara ya kikazi iliyolenga kukabidhi msaada wa vifaa tiba alivyovitoa kwa ajili ya hospitali hiyo.

Amesema kuwa serikali italipa madeni yote inayodaiwa baada ya kumaliza kuyafanyia uhakiki, hivyo aliwaomba watumishi kuwa na subira wakati serikali ikiendelea zoezi la kuyahakiki ili kuweza kulipa deni sahihi inalodaiwa.

Awali akisoma taarifa ya Idara ya afya kwa Waziri Mkuu, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Dk. Japhet Simeo amesema idara ya afya inakabiliwa na madeni ya watumishi ambayo ni sh. milioni 109,662,483.

Amesema madeni hayo yametokana na likizo, matibabu, uhamisho wa ndani na nje ya wilaya, gharama za mizigo kwa watumishi waliostaafu, ambapo  halmashauri imejipangia utaratibu wa kulipa madeni hayo pindi inapotokea fedha kutoka serikali kuu.

Hata hivyo kasi ya mtiririko wa fedha ni ndogo ukilinganisha na mahitaji halisi ya maslahi ya watumishi ambapo Halmashauri inawapongeza na kuwapongeza watumishi wa Idara ya afya kwa kuendelea kuwa wavumilivu na kuwahudumia wananchi.

Dk. Simeo amesema halmashauri inawapongeza Rais Dk. John Magufuli na Waziri Mkuu, Majaliwa kwa juhudi kubwa wanazozifanya kuongeza mapato nchini, ambapo wana matumaini kuwa watumishi wataboreshewa maslahi na stahiki zao ili kuchochea motisha kiutendaji.

Katika hatua nyingine Dk. Simeo alizungumzia upatikanaji wa dawa, alisema ambao  umeongezeka kutoka asilimia 30 mwaka jana na kufikia asilimia 80 mwaka huu dawa muhimu katika vituo vyote vya kutolea huduma ambavyo viko 32.

Rais Magufuli Aongoza Waombolezaji Kuaga Mwili Wa Mbunge Wa Viti Maaluum Wa Chadema Jijini Dar Leo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Aprili, 2016 ameungana na Ndugu, Jamaa na Marafiki kuuaga mwili wa Mbunge Mstaafu wa Mkoa wa Singida Marehemu Christina  Lissu Mughwai katika ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam.

Christina Lissu Mughwai aliyekuwa Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Singida katika kipindi cha kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, alifariki dunia tarehe 07 Aprili, 2016 katika hospitali ya Agha Khan Jijini Dar es salaam, alikokuwa akipatiwa Matibabu.

Pamoja na Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Viongozi wengine waliohudhuria shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Akson na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bunge Mheshimiwa Freeman Mbowe.

Akitoa salamu kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa George Simbachawene amewapa pole familia ya marehemu na kueleza kuwa katika kipindi chake cha ubunge Mheshimiwa Christina Lissu Mughwai alitoa mkubwa kama mbunge na kama mtaalamu wa Uchumi.

"Mheshimiwa Rais anatoa pole nyingine kwenu familia ya marehemu, ndugu jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, Amina" Amesema Mheshimiwa Simbachawene.

Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai umesafirishwa leo kwenda kijiji cha Mahambe Mkoani Singida kwa Mazishi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
12 April, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji Mwanasheria Tundu Lissu (Mb) kufatia kifo cha mdogo wake Christina Lissu Mughwai aliyefariki Aprili 7 mwaka huu.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimpa pole Mwanasheria Tundu Lissu (Mb) kufatia kifo cha mdogo wake Christina Lissu Mughwai aliyefariki Aprili 7 mwaka huu
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli  akiteta jambo na mwenyekiti wa chama cha CHADEMA Freeman Mboye wakati wa akiaga mwili wa marehemu Christina Lissu Mughwai aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum kutoka Chadema katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli na mke wake mama Janeth Magufuli wakiaga mwili wa marehemu Christina Lissu Mughwai aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum kutoka Chadema katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam atoa siku 6, ombaomba Waondoke Jijini Dar es Salaam

$
0
0

SERIKALI ya Mkoa wa Dar es Salaam imesema kuwa katika kuweka jiji hilo safi imejipanga kuanza na  mambo matatu ambayo ni kuwaondoa ombaomba wa barabarani, kuwabana wamiliki wa majengo makubwa yaliyojengwa kinyume na taratibu pasipokuwa na sehemu za kuegeshea magari na kuwaamuru  wamiliki wa bar kutopiga muziki nje ya utaratibu wa vibali vyao.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa ombaomba walikuja Dar es Salaam kwa nauli zao hivyo lazima warudi walikotoka kwa nauli zao.

Makonda  ametoa siku sita mpaka April 18 ombaomba ndani ya jiji la  Dar es salaam wawe wameondoka

Kuhusu wamiliki wa Bar, Makonda  amesema wamiliki wa bar wanaowapigia watu kelele wafuate sheria walizopewa kama ni mwisho saa sita kupiga muziki iwe hivyo na muziki huo upigwe kwenye maeneo husika.

Amesema mtu ambaye anapiga muziki nje ya utaratibu wa kibali chake maana yake ajiandae kunyang’anywa leseni na kufutiwa kibali chake na faini hiyo atailipa mwenyewe. 

Aidha, Makonda amewataka wamiliki wa majengo makubwa yaliyojengwa kinyume na taratibu pasipokuwa na sehemu za kuegeshea magari walipe faini na kuweka utaratibu  wa kupaki wapi magari yao au kubomoa majengo yao.

Taarifa Ya Habari ya ChannelTEN Jumanne ya Leo Tarehe 12. 04. 2016 “Full video”

$
0
0
Taarifa  Ya  Habari ya ChannelTEN  Jumanne ya Leo  Tarehe  12. 04. 2016  “Full video”

Rais Magufuli Ashiriki Ibada Ya Kumbukumbu Ya Miaka 32 Ya Kifo Cha Sokoine

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na wakristo wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Joseph Jijini Dar es salaam, kusali misa Takatifu ya kumkumbuka na kumuombea aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward  Moringe Sokine aliyefariki dunia miaka 32 iliyopita, kwa ajali ya gari katika eneo la Dakawa wakati akitokea Bungeni Dodoma.

Misa hiyo imehudhuriwa pia na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa na Familia ya Hayati Edward Moringe Sokoine.

Akizungumzia baada ya misa hiyo Rais Magufuli amesema anamkumbuka Hayati Edward Moringe Sokoine, kuwa alikuwa kiongozi shupavu aliyewapenda watanzania, aliyependa kuwatumikia watanzania, aliyekuwa Mchapakazi, aliyechukia rushwa, aliyechukia ufisadi na aliyechukia uonevu kwa watu wa chini.

 "Namuona ni kilelezo cha pekee katika Taifa letu la Tanzania, miaka 32 iliyopita wakati Mzee wetu Hayati Edward Moringe Sokine alipoitwa na kutangulia mbele za haki, wakati huo mimi nilikuwa JKT Mpwapwa, ninaikumbuka siku hiyo ilikuwa ya majonzi makubwa"  Amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo Rais Magufuli amesema kazi nzuri ya mtu huwa haipotei na hivyo amewasihi watanzania kuendelea kushikamana, kupendana na kuyaenzi mazuri yote yaliyofanywa na viongozi wa Taifa waliotangulia mbele za haki, wakiwemo hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Hayati Abeid Amani Karume na Hayati Edward Moringe Sokoine.

Kwa upande wake Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa amemuelezea Hayati Sokoine kuwa ni Kiongozi aliyejitoa kutumikia Taifa, na kubainisha kuwa viongozi wote wanawajibika kuishi kwa mfano wake.

Rais Mstaafu Mkapa amesisitiza kuwa mfano huo wa Hayati Sokoine, ndio ulioiwezesha Tanzania kumpata kiongozi wa Sasa, Rais John Pombe Magufuli anayetaka kuonesha misingi ya uongozi bora, uadilifu, kusimamia amani, utulivu na maendeleo.

Nae Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema Hayati Sokoine hakuwa kiongozi wa kujiangalia yeye, bali Kiongozi kwa ajili ya watu, na amempongeza Rais Magufuli kwa kufuata nyayo za Hayati Sokoine katika kuliongoza Taifa.

"Kuna baadhi ya watu wanasema Rais wetu wa sasa ni sura ya Edward Moringe Sokoine" Amesema Kardinali Pengo, na kumtaka Rais Magufuli na serikali yake kusonga mbele na kujenga heshima ya nchi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
12 Aprili, 2016

Tanzania yaongoza Afrika kwa kulima ufuta.....Kidunia Inashika Nafasi ya 3

$
0
0
TANZANIA imetajwa kuwa inaongoza kwa kulima na kuzalisha ufuta Afrika huku ikishika nafasi ya tatu ya duniani.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Maendeleo, Naliendele, Dk Omary Mponda, alisema kuwa Tanzania imefikia hapo baada ya jitihada kubwa zilizofanywa na serikali.

Jitihada hizo zinafanyika kupitia watafiti wake wa masuala ya kilimo kwa kutafiti na kugundua mbegu bora zinazostahimili ukame, magonjwa na wadudu.

Mtaalamu huyo ambaye pia ni mtafiti kiongozi na mratibu wa mbegu za mafuta, alisema kwa sasa Tanzania inazalisha wastani wa tani 460,000 kutoka tani 38,000 zilizokuwa zikizalishwa mwanzoni mwa miaka ya 1980.

Alisema kwa mujibu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO), Tanzania imepanda kutoka nafasi ya saba kidunia mwaka 1998 hadi kufikia nafasi ya tatu ikitanguliwa na India na Mayama.

“Hiki kituo cha utafiti kilianza mwaka 1945 wakati huo kilikuwa kinashughulikia korosho peke yake, lakini kufikia mwaka 1978 tulianza kuingiza utafiti wa mbegu za karanga na ufuta ambapo mpaka sasa tumeshagundua mbegu aina 12 ambazo wakulima wetu wanazitumia”, alisema.

Mtaalamu huyo aliyebobea katika masuala ya utafiti wa mbegu za mafuta, alisema kuwa zao hilo miaka ya nyuma lilikuwa linalimwa katika mikoa ya Kusini ambayo ni Mtwara, Lindi na Ruvuma. Alisema kutokana na hamasa kubwa inayofanywa na wataalamu wa kilimo, tayari mikoa kadhaa inalima zao hilo.

“Huko nyuma hata eneo lililokuwa likilimwa ufuta lilikuwa dogo sana, lakini sasa ni zaidi ya hekta 650,000 zinalimwa ufuta nchi nzima…sasa haya ni mafanikio makubwa na yanayopaswa kujivunia na hiyo inatokana na ugunduzi huu wa mbegu bora”, alisema.

Ufuta ni moja kati ya mazao yanayoongeza kipato kwa makusanyo ya ndani kwa baadhi ya halmashauri za wilaya ikiwemo wilaya ya Liwale, Nachingwea na Ruangwa mkoani Lindi ambapo kwa mujibu wa takwimu zilizopo Ruangwa, msimu uliopita ilipata Sh milioni 400 kutokana na ushuru wa mauzo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aweka jiwe la msingi ujenzi duka la dawa Ruangwa

$
0
0

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa duka la dawa katika Hospitali Wilaya ya Ruangwa, ambalo litatoa fursa kwa wilaya nyingine kama Kilwa, Nachingwea na Liwale kufuata dawa katika duka hilo.

Ujenzi wa duka hilo la dawa ndani ya wilaya ya Ruangwa umefadhiliwa na Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) na unakadiriwa kugharimu Sh milioni 55 mpaka kukamilika kwake.

Litasaidia kuboresha upatikanaji wa dawa hospitalini hapo na katika hospitali zingine zilizoko katika wilaya za jirani.

Majaliwa alisema mbali na ujenzi wa duka la dawa pia hospitali hiyo inatarajiwa kujengewa uzio ili kuepusha vitendo vya uhalifu vinavyoweza kutokea kutokana na kutokuwa nao.

Alisema hayo wakati akizungumza na watumishi wa hospitali ya wilaya ya Ruangwa mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa duka la dawa katika hospitali hiyo.

“Nataka hapa ndio iwe bohari ya dawa, watu kutoka Kilwa, Nachingwea na Liwale wawe wanafuata dawa na vifaa tiba katika duka la dawa lililoko ndani ya Hospitali ya wilaya ya Ruangwa, pia kujengwa kwa duka hili kutasaidia kumaliza tatizo la upungufu wa dawa,” alisema.

Alisema mkakati uliokuwepo ni kuhakikisha vifaa tiba na dawa vinapatikana hospitalini hapo ili kuwawezesha wagonjwa kupata huduma bora.

“Kinachomuuma ni kuona akinamama, akinababa, vijana na wazee wangu wanakwenda hospitali na kuambiwa vipimo hakuna, hivyo nitahakikisha vifaa tiba vyote vinapatikana,” alisema.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Dk Japhet Simeo alimshukuru Waziri Mkuu kwa juhudi mbalimbali anazozifanya ikiwemo kutafuta wafadhili wanaoendelea kusaidia utoaji wa huduma za afya hospitalini hapa.

“Mpaka sasa kuna mradi wa ujenzi wa uzio wa hospitali ya wilaya, ujenzi wa duka la dawa, ukarabati wa majengo na upanuzi wa hospitali na tunamuomba aendelee kuwashirikisha wadau mbalimbali katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika hospitali yetu ya wilaya,” alisema.

Dk Simeo alisema kwa kupitia Waziri Mkuu, wameweza kupata vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 100 kutoka umoja wa kampuni unaotengeneza vinywaji baridi nchini ambavyo jana walikabidhiwa na Meneja wa MSD, Kanda ya Mtwara, Helman Mng’ong’o.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images