Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Hotuba ya Maalim Seif kwa waandishi wa habari Aliyoitoa Leo Jumapili Tarehe 10/04/2016

$
0
0
HOTUBA YA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD KWENYE MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI – PARK HYATT ZANZIBAR, TAREHE 10 APRILI, 2016
Ndugu zangu Waandishi wa Habari,
Ndugu Waalikwa,

Naanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutujaalia uhai na uzima tukaweza kukutana hapa leo.

Namshukuru Mwenyezi Mungu pia kwa kuijaalia nchi yetu kwa kiasi kikubwa kubaki katika hali ya amani na utulivu licha ya jitihada kubwa zilizofanywa na zinazoendelea kufanywa na baadhi ya watu za kuivuruga amani yetu.

Naendelea kumuomba Mola wetu aendelee kuibariki nchi yetu na watu wake, aijaalie kuwa nchi ya amani na atujaalie hekima na busara katika kuendesha mambo yetu.

Nichukue fursa hii pia kukushukuruni nyinyi waandishi wa habari kwa kuitikia wito wetu na kuja kutusikiliza. Shukrani maalum zije kwenu wale ambao mmesafiri kutoka Dar es Salaam na kuja Zanzibar makhsusi kwa ajili ya mkutano huu.

Tunathamini sana mashirikiano yenu nyote tukitambua nafasi na mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika maendeleo ya nchi yoyote ile.

Mtakumbuka kwamba siku saba zilizopita tulizungumza nanyi ambapo tuliwasilisha kwenu maazimio 13 ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama Cha Wananchi (CUF) kuhusiana na msimamo wa Chama chetu dhidi ya ubakaji wa demokrasia Zanzibar uliofanyika tarehe 20 Machi, 2016 na ambao ulipewa jina la uchaguzi wa marudio.

Leo hii tumekuiteni ili kutimiza agizo nililopewa na Baraza Kuu lililonitaka nizungumze na wananchi wa Zanzibar ili kuwaeleza kwa kina mwelekeo wa hali ya kisiasa ya Zanzibar na hatua zinazochukuliwa na CUF kuhakikisha maamuzi halali ya kidemokrasia ya Wazanzibari waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015 yanaheshimiwa.

UCHAFUZI WA TAREHE 20 MACHI, 2016
Nilieleza kwa urefu katika mkutano wangu na waandishi wa habari wa tarehe 11 Januari, 2016 nilioufanya Dar es Salaam juu ya nini kilitokea baina ya tarehe 25 Oktoba 2015 hadi tarehe 28 Oktoba, 2015, siku ambayo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salim Jecha, alitoa tangazo batili na haramu la kufuta uchaguzi huru na wa haki uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015. Nilieleza pia hoja za kikatiba na kisheria za kwa nini tangazo lile ni haramu na batili na hoja zile hadi leo watawala wameshindwa kuzijibu.

Kwa hoja hizo hizo, nikaeleza kwamba hakuna vifungu vya Katiba wala Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam. 11 ya 1984 vinavyozungumzia kitu kinachoitwa uchaguzi wa marudio ukiondoa pale inapotokea wagombea wanapopata idadi sawa ya kura.

Sikusudii kurudia yale ambayo nilishayaeleza siku ile maana hayo sasa yanaeleweka na kila mtu ndani na nje ya nchi.

Leo hii nataka niwapongeze kwa mara nyengine tena wananchi jasiri na shupavu wa Zanzibar kwa kuitumia tarehe 20 Machi, 2016 kukifedhehesha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa mara ya pili ndani ya miezi sita mbele ya macho ya Watanzania na mbele ya macho ya jumuiya ya kimataifa.

Wananchi wazalendo wa Zanzibar wanaoipenda nchi yao waliwakataa watawala waovu wa CCM na sera zao mbovu zinazoidhalilisha Zanzibar yao kupitia sanduku la kura tarehe 25 Oktoba, 2015.

Watawala waovu wa CCM wakaamua kutumia mabavu na uvunjwaji wa katiba na sheria kuyapindua maamuzi ya Wazanzibari, kwa sababu tu maamuzi hayo yalikuwa ni ya kuwakataa watawala hao.

Kwa miezi mitano kuanzia Oktoba 2015 hadi Machi 2016, watawala waovu wa CCM wakawaingiza wananchi watulivu na wanaopenda amani wa Zanzibar katika idhilali na hilaki kubwa kwa kuwazuilia haki zao za msingi za binadamu ili wasiweze kuonesha hisia zao dhidi ya watawala.

Kwa namna ya pekee na ya ustaraabu wa hali ya juu na wa kupigiwa mfano, wananchi wa Zanzibar wakaisubiri tarehe 20 Machi, 2016 na wakapeleka ujumbe wao kwa watawala hao na kwa dunia nzima kwa njia za amani za kuususia uchafuzi ulioitishwa siku hiyo.

Hali halisi iliyoonekana na kila aliyetaka kuona ni kwamba zaidi ya asilimia 80 ya Wazanzibari hawakwenda kupiga kura siku hiyo ili kuonesha hisia zao na kuthibitisha tena maamuzi yao ya tarehe 25 Oktoba, 2015.

Kituo cha televisheni cha ITV kilichokuwa kikirusha matangazo ya moja kwa moja kutoka katika mikoa mitano ya Unguja na Pemba kilionesha vile vilivyoitwa vituo vya kupigia kura vikiwa havina watu kabisa au vikiwa na watu wachache sana.

Walipowahoji wale walioitwa maofisa uchaguzi na walioitwa mawakala kila mmoja alikuwa akija na majibu yake na takwimu zake zinazopingana na za mwenzake.

Vituo vya televisheni vya kimataifa hasa kile cha Al-Jazeera na CCTV ya China vilionesha na kuripoti vituo vikiwa vitupu. Hata televisheni ya watawala ya ZBC ilikuwa ikipata kigugumizi kuonesha hali ilivyokuwa katika vile vilivyoitwa vituo vya kupigia kura hadi kuamua kukatisha matangazo ya moja kwa moja. Magazeti ya Tanzania na ya nje ya nchi yaliripoti na kuchapisha picha zilizoonesha kususiwa kwa uchafuzi huo ulioitishwa na watawala wakidhani wanajihalalishia haramu yao.

Mitandao ya kijamii nayo ilijaa maelezo na vielelezo kutoka watu na taasisi za kimataifa zinazoheshimika vikionesha hali halisi ilivyokuwa na ujasiri wa Wazanzibari wa kuususia uchafuzi huo.

Na hatimaye nchi 16 zikatoa taarifa yao tarehe 21 Machi, 2016 wakieleza kwamba uchaguzi huo haukuwa wa kuheshimika kwa sababu haukuwa shirikishi na wala haukuwakilisha matakwa ya wapiga kura wa Zanzibar.

Nitumie fursa hii kwa mara nyengine tena kuwapongeza wananchi wote wa Zanzibar kwa ujasiri, uzalendo na ari kubwa walioionesha kwa kuitikia kwa kiasi kikubwa wito wa chama chao cha CUF wa kuwataka wasishiriki katika uhuni na ubakaji wa demokrasia uliopewa jina la uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 Machi, 2016, na hivyo kuudhihirishia ulimwengu kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakina ridhaa ya wananchi wa Zanzibar.

Naungana na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF kuwapongeza waliokuwa wagombea wenzangu wa CUF kwa nafasi za Uwakilishi na Udiwani kwa kusimama na wananchi wa Zanzibar na kutoshiriki katika uchaguzi huo haramu na batili wa marudio, jambo ambalo limethibitisha kwamba hawapo kwa ajili ya kutaka nafasi na vyeo binafsi bali wanachotaka ni kuleta mabadiliko ya kweli kwa maslahi ya watu wote wa Zanzibar.

Pongezi zangu za dhati kabisa zinakwenda kwa wagombea Urais, Uwakilishi na Udiwani wa vyama vyengine vya upinzani ambavyo ni NRA, DEMOKRASIA MAKINI, SAU, UMD, JAHAZI ASILIA, CHAUMMA, UPDP, DP, na ACT-WAZALENDO, na vile vinavyoshirikiana kupitia UKAWA ambavyo ni CHADEMA, NCCR na NLD kwa kuungana pamoja na Wazanzibari kutetea demokrasia yao.

CCM WANAPENDA NAMBA LAKINI HAWAJUI HESABU
Jambo moja ambalo CCM wamejifedhehesha wenyewe ni lile la kutangaza kile walichokiita matokeo ya uchafuzi wao bila ya kuzingatia kwamba takwimu zina sifa moja, huwa hazisemi uongo.

Vijana wana msemo wao siku hizi; wanasema CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu. Matokeo ya tarehe 20 Machi, 2016 waliyoyatangaza ni kwamba eti jumla ya watu waliopiga kura walikuwa 341,865 na kwamba Dk. Ali Mohamed Shein eti alipata kura 299,982 sawa na asilimia 91.4.

Takwimu za uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 zilionesha kwamba jumla ya wananchi waliojitokeza kupiga kura walikuwa ni 402,354 na Dk. Ali Mohamed Shein alipata kura 182,011 sawa na asilimia 46.28.

Wakati huo huo kwa uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia, wapiga kura kwa upande wa Zanzibar walikuwa 417,882 ambapo mgombea wa CCM, Dk. John Pombe Magufuli alipata kura 194,317 sawa na asilimia 46.5.

Kwa hivyo, kwa kutumia takwimu hizi, mtu anapochukua takwimu hizi na kulinganisha wapiga kura 402,354 waliojitokeza tarehe 25 Oktoba, 2015 na wale wanaodai eti walijitokeza tarehe 20 Machi kwamba ni 341,865 watawala wa CCM walichotaka kutuaminisha ni kwamba tofauti ya waliokuwa hawakujitokeza kupiga kura ilikuwa ni 60,489 tu. Suala la kujiuliza ni kwamba iwapo hilo ni kweli kwa nini vituo vionekane vitupu kabisa tarehe 20 Machi, 2016?

Lakini kwa upande mwengine, mtu anapokosa hata tahayuri na kudai Dk. Ali Mohamed Shein amepata kura 299,982 anachotaka kutwambia ni kwamba ndani ya miezi mitano ya idhilali na mateso aliyowapatisha Wazanzibari ameweza kuongeza kura 117,971.

Kufedheheka kwa CCM kunakuja zaidi kwamba walisahau kwamba waliyakubali matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tarehe 25 Oktoba 2015 kwa upande wa Zanzibar ambapo kama tulivyokwisha onesha waliopiga kura walikuwa wengi zaidi wakiwa ni 417,882 (na hilo ungetegemea lingeinufaisha CCM) na bado mgombea wa CCM akapata kura 194,317 sawa na asilimia 46.5. Kwa kutumia idadi waliyotangaza ya kura 299,982 walizompa Dk. Shein wanataka kutwambia kwamba yeye amepata kura 105,665 zaidi kuliko Dr. Magufuli kwa Zanzibar.

Kama takwimu zao zingekuwa sahihi ina maana pia wapiga kura waliomuunga mkono mgombea wa CUF ambao hawakwenda kupiga kura ni 60,489 tu (sawa na asilimia 15 tu). Hivi nani utamdanganya kwamba Maalim Seif Sharif Hamad anaungwa mkono na asilimia 15 tu ya wapiga kura wa Zanzibar? Nani utamdanganya kwamba ndani ya miezi mitano, CCM imeongeza kura 105,665 zaidi ya alizopata mgombea wake Dk. Magufuli kwa upande wa Zanzibar?

Kutokana na ubabe na kiburi cha utawala walicho nacho CCM, wameishia kujifedhehesha kwa takwimu zao za kupika wenyewe. Ndiyo vijana wakasema, CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu.

NINI MWELEKEO WA CUF NA WAZANZIBARI BAADA YA UBAKAJI HUU WA DEMOKRASIA?
Wazanzibari walio wengi wamekuwa wakituuliza nini mwelekeo wa CUF baada ya ubakaji huu wa demokrasia? Wanatuuliza viongozi wao na hasa mimi tunatokaje katika hali hii ambayo imedumu miaka nenda miaka rudi kila pale Zanzibar inapofanya uchaguzi?

Kabla sijalieleza hilo, nataka niweke wazi leo kwamba tulipofanya uamuzi wa kuususia uchaguzi haramu na batili wa tarehe 20 Machi, 2016 tuliamua kusimama juu ya uamuzi unaoheshimu misingi ya kikatiba ambayo watu wa Zanzibar tumeamua ndiyo inapaswa iongoze na iendeshe nchi yetu. Tulijua kwamba uamuzi huo utakuwa na athari kwa CUF na kwa Zanzibar lakini tulijua na tuliamini pia kwamba athari hiyo haiwezi kuwa kubwa zaidi kuliko gharama ya kuikanyaga Katiba na Sheria za nchi yetu na gharama za kupiga teke demokrasia, haki za binadamu na utawala wa sheria.

Tulipima na tukatafakari kwa kina na kuona ni kheri kumeza machungu ya athari binafsi kwetu lakini tusimame kidete na kifua mbele katika kutetea maamuzi ya watu wa Zanzibar waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015, na pia kulinda misingi ya Katiba na Sheria za nchi yetu na misingi ya demokrasia na haki za watu. Tuliona hayo ni kheri kwa huko twendako badala ya kushiriki katika haramu ya ubakaji wa demokrasia na matumizi ya nguvu za kijeshi kulazimisha watawala wasio na ridhaa ya watu.

Tulifanya maamuzi yale pia kwa lengo la kuepusha shari katika nchi yetu. Leo Wazanzibari na dunia nzima ni mashahidi kwamba uamuzi ule ulikuwa sahihi na wa busara. Maana mateso na vitisho walivyokumbana navyo Wazanzibari wakati tumewaachia uchaguzi ule watawala waovu peke yao vilikuwa vya kiasi kile kilichoshuhudiwa.

Je, tungeliamua kushiriki na kusimama kulinda na kutetea ushindi wetu hali ingekuwaje? Bila shaka nchi ingetumbukia katika machafuko ambayo watawala waovu walikuwa tayari yatokee kuliko kuridhia maamuzi halali ya wananchi wa Zanzibar.

Maamuzi yale yamethibitika pia kwamba ni sahihi kwa jinsi watu wa Zanzibar walivyoudharau na kuupuuza uchaguzi haramu na batili wa tarehe 20 Machi, 2016. Watawala waovu wa CCM waliwadharau watu wa Zanzibar na watu wa Zanzibar wakaamua kuwadharau wao tarehe 20 Machi 2016.

Kwa upande mwengine, uamuzi tuliouchukua na kuusimamia pia ni uamuzi uliosimama juu ya misingi ya heshima na misingi ya utu wa watu, ambayo yalikuwa ndiyo malengo sahihi ya Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Hayati Mzee Abeid Amani Karume, malengo sahihi ya Chama cha Afro Shirazi na malengo sahihi ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964.

Kwa hakika, uamuzi wa kuupuuza na kuudharau uchafuzi wa tarehe 20 Machi, 2016 ni ushindi mwengine wa Zanzibar katika historia yake ya kisiasa.

Nimalizie sasa kwa kujibu hoja ya ni upi mwelekeo wa CUF na wa Wazanzibari baada ya ubakaji huu wa wazi wa demokrasia na haki za watu wa Zanzibar?

Kwanza, nirudie na kusisitiza msimamo wetu kwamba hatukubaliani na ubakaji wa demokrasia na haki za watu wa Zanzibar uliofanywa na watawala waovu wakisaidiwa na vyombo vya dola. Kwa msingi huo, Wazanzibari wataendelea kuipinga serikali isiyo na ridhaa ya watu kwa kutumia njia za amani, za kidemokrsia na zinazoendana na misingi ya Katiba na Sheria za nchi yetu.

Jana kumetangazwa kile kilichoitwa ni Baraza la Mawaziri. Msimamo wetu uko pale pale. Kama tusivyomtambua aliyelitangaza Baraza hilo, vivyo hivyo hatulitambui Baraza lake la Mawaziri.

Kwa hakika, kwa sababu msingi wa watawala waliojinyakulia madaraka ni kupitia uvunjwaji wa Katiba, kila kinachofuata kimekuwa kikiendeleza uvunjwaji wa Katiba. Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kupitia Marekebisho ya 10 ya mwaka 2010, Ibara ya 9 (1) inalazimisha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa na muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Ibara za 39, 39A na 42 za Katiba zimeeleza namna Serikali hiyo ya Umoja wa Kitaifa itakavyoundwa. Masharti yote hayo yanaendelea kuvunjwa na mtawala aliyeamua kuyapiga teke maamuzi ya Wazanzibari na kujiweka madarakani kwa nguvu. Kwa hivyo, Serikali yake haiwezi kuwa Serikali inayokwenda na Katiba. Kwa ufupi, si Serikali halali kwa mujibu wa Katiba.

Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF katika kikao chake cha tarehe 2 – 3 Aprili, 2016 lilipitisha maazimio yafuatayo miongoni mwa maazimio yake:

“Azimio Nam. 9:
Haliyatambui matokeo ya uchaguzi huo haramu na batili, na kwa msingi huo halimtambui Dk. Ali Mohamed Shein kuwa Rais wa Zanzibar, haliwatambui waliotangazwa kuwa Wawakilishi na wala haliwatambui waliotangazwa kuwa Madiwani. Baraza Kuu linaungana na wananchi wa Zanzibar waliokataa kuwapa uhalali watu hao na kwa hivyo halitoitambua Serikali, Manispaa na Halmashauri za Wilaya zitakazoundwa na watu hao. CUF haitoshirikiana na Serikali itakayoundwa kwa sababu ni kinyume na Katiba ya Zanzibar, kinyume na Sheria ya Uchaguzi na haikutokana na ridhaa ya watu. Kwa vyovyote vile, Serikali itakayoundwa haitakidhi matakwa ya Katiba ya Zanzibar na hivyo CUF haitoshiriki kwenye uvunjaji wa Katiba ambayo inaeleza kwa uwazi kabisa namna ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

“Azimio Nam. 10:
Linawataka wananchi wote wa Zanzibar kutumia njia za amani, za kikatiba na kisheria ambazo zimewahi kutumika katika nchi nyingine duniani kuwakataa watawala waovu na wasio na ridhaa ya watu waliojiweka madarakani kwa kutumia nguvu na ubakaji wa demokrasia kwa kutoipa ushirikiano Serikali itakayoundwa na watawala hao.”

Baada ya maazimio hayo ya Baraza Kuu, kinachofuata sasa ni utekelezaji wake. Hivi sasa tunapanga mikakati madhubuti ya utekelezaji wa maazimio hayo kwa kutumia njia za amani, za kidemokrasia na za kikatiba ili kutufikisha kwenye malengo yetu ya kuona maamuzi ya watu wa Zanzibar yanaheshimiwa.
Nina hakika kabisa kuwa mikakati tunayoipanga itazaa hatua ambazo zitaibana Serikali haramu na hatimaye itasalimu amri kwa wananchi wa Zanzibar ambayo kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ndiyo wenye mamlaka ya kuiweka madarakani Serikali wanayoitaka. Katika dunia ya leo, hatuwezi kuongozwa na watawala ambao hawakupewa mamlaka na watu wenyewe.

Pili, naipongeza na kuishukuru jumuiya ya kimataifa na washirika wa maendeleo kwa msimamo waliochukua wa kukataa kubariki ubakaji huo wa demokrasia na haki za watu wa Zanzibar na kukataa kushiriki katika uapishwaji wa mtu asiye na ridhaa ya wapiga kura wa Zanzibar. Napongeza hatua ambazo wameanza kuzichukua dhidi ya Serikali za CCM ambazo ndizo zilizosimamia ubakaji huo wa demokrasia na haki za watu. Natoa wito kwao kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya watawala hawa waovu zikiwemo kuwawekea vikwazo vya kusafiri, kufuatilia akaunti zao za fedha nje ya nchi na hatua za kuchunguza matendo yao ya uhalifu dhidi ya binadamu. Wananchi waliodhulumiwa haki zao wanaziunga mkono hatua hizo wakiamini kwamba CCM ni lazima iwajibishwe kwa matendo yake maovu dhidi yao.

Nitumie fursa hii kwa mara nyengine tena kuwataka wananchi wa Zanzibar kudumisha amani ya nchi yetu na umoja wa watu wetu. Nikiwa kiongozi wao ninayewapenda na ambaye nimejitolea kuwatumikia katika umri wangu wote siwezi kuwaongoza kuelekea kwenye fujo na ghasia au vitendo vitakavyopelekea kuiharibu nchi yetu na kuathiri watu wetu. Nina imani kabisa kwamba njia tunayoifuata ni njia ya haki; na haki siku zote itashinda.

Mwaka 2009, mimi na mwenzangu, Dk. Amani Abeid Karume, tuliwaongoza Wazanzibari katika Maridhiano yaliyoashiria mwanzo wa ujenzi wa mahusiano mapya baina ya watu wema wa Zanzibar kwa kuzika siasa za ubaguzi, utengano, chuki, hasama na fujo na badala yake kusimamisha siasa za maelewano, umoja, upendo, mshikamano na udugu katika jamii yetu.

Tulitegemea kuanzia pale tungeendelea mbele kwa kuchukua hatua za kuyaimarisha maridhiano yetu na kuyazamisha zaidi kwenye nyoyo za Wazanzibari. Binafsi nasikitishwa na kuhuzunishwa sana kuona watawala waovu wasiowatakia mema watu wa nchi hii wameturudisha tulikotoka kwa maslahi yao binafsi.

Natoa wito kwa Wazanzibari wenzangu kuwa tukatae kurudishwa kwenye siasa zile za ubaguzi, utengano, chuki, hasama na fujo na kila mmoja afanye lile liliomo katika uwezo wake kuendeleza maelewano, umoja, upendo, mshikamano na udugu katika jamii yetu.

Wazanzibari tumeamua kuisimamisha tena Zanzibar yetu na Zanzibar itasimama tena Inshallah. Hilo sina wasiwasi nalo kama kiongozi wa Wazanzibari waliyenipa ridhaa yao.

HATIMAYE TUTASHINDA.
WANANCHI JASIRI NA SHUPAVU WA ZANZIBAR WATASHINDA.

Ahsanteni sana.

Rais Wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein Awaapisha Mawaziri Leo

$
0
0

RAIS wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha Mawaziri na Manaibu Mawaziri wa Wizara 13 za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Mawaziri wasiokuwa na Wizara Maalum ambao pia ni Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi. 
 
Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa vyama na Serikali pamoja na wananchi kadhaa ambapo miongoni mwa waliohudhuria ni Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid. 
 
Wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Said Hassan Said, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji na Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis. Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib pamoja na viongozi wa vikosi vya Ulinzi.
 
Walioapishwa katika hafla hiyo ni Waziri, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji  Ussi Gavu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora  Mhe. Haroun Ali Suleiman. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ   Mhe. Haji Omar Kheri, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud Mohammed.   
 
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed, Waziri wa Afya Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Riziki Pembe Juma pamoja na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mhe. Moudline Castico. 
 
Wengine ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Balozi Amina Salum Ali, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mhe. Balozi Ali Abeid A. Karume. Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Hamad Rashid Mohammed. Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Mhe. Rashid Ali Juma na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mhe. Salama Aboud Talib. 
 
Kwa upande wa Manaibu Waziri ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Khamis Juma Maalim. Naibu Waziri wa Afya Mhe. Harusi Said Suleiman na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri.

Wengine ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mhe. Mohammed Ahmed Salum. Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo nan Uvuvi Mhe. Lulu Msham Abdulla, Naibu Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Mhe. Bibi Choum Kombo Khamis na Naibu Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mhe. Juma Makungu Juma.
        
Aidha, Dk. Shein amewaapisha Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum akiwemo Mhe. Said Soud Said kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum pamoja na Mhe. Juma Ali Khatib Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum. 
 
Kwa uwezo aliopewa chini ya Vifungu 42, 43,44 na 47 vya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Dk. Shein ameunda Wizara 13 za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuwateua Mawaziri na Manaibu Mawaziri wa Wizara hizo pamoja na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum na Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi.

RC Makonda: Ni marufuku kuwasaidia Ombaomba barabarani jijini Dar

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam  Paul Makonda amepiga marufuku wananchi wanaotoa Pesa kwa Omba omba kando ya barabara kwa kuwa wanachangia uwapo wa watu hao huku baadhi ya watu wakiwatumia watoto hao kujipatia kipato kinyume cha sheria.

Akizungumza jijini dar es salaam Bw.Makonda amesema kumekuwa na Ongezeko kubwa la watoto katika barabara kadhaa za jiji la dar  wakijihusisha na Kuomba pesa huku wanaowatuma wakiwa wamekaa pembeni jambo ambalo ni kinyume na sheria lakini pia linahatarisha Usalama wa watoto hao.

Aidha amesema mkakati uliokuwapo kwa kushirikiana na Ustawi wa jamii, Tamisemi pamoja na manispaa kuhakikisha kuwa watoto hao wanakusanywa na kuwekwa katika vituo maalum huku wanaohusika na kuwatumia kufanya kazi hiyo wakichukuliwa hatua.

NEMC Yakipiga Faini ya Milioni 20 Kiwanda cha Karatasi Mufindi (MPM)

$
0
0

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini limekitoza faini ya shilingi milioni 20 Kiwanda cha Karatasi Mufindi (MPM) kilichopo kijiji cha Mgololo kata ya Makungu katika Halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa baada ya kushindwa kufanya maboresho katika mfumo wake wa kuchuja maji taka kabla ya kuingia kwenye mto licha ya kuagizwa kufanya hivyo mara kadhaa.

Bw. Godlove Mwamsojo ambaye ni Mratibu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini amesema adhabu hiyo ambayo ni kwa mujibu wa sheria ya mazingira ya 2014 vifungu vya 186 na 198 inapaswa kutekelezwa katika kipindi cha siku 14.

Amesema kiwanda hicho pekee cha uzalishaji wa karatasi nchini kimeshindwa kudhibiti maji taka yanatoka kiwandani hapo na kutiririshwa katika mto Kigogo hali ambayo amesema inayaweka rehani maisha ya watu na viumbe wengine wanaotumia maji ya mto huo.

Kwa upande wake Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira, Bw. Luhaga Mpina amewataka wenye viwanda nchini kukidhi mahitaji ya sheria mbalimbali ikiwemo ya mazingira sambamba na kuikumbusha NEMC kufanya kazi usiku na mchana bila kuchoka.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya April 11

Ikulu Yafuta Safari ya Wakuu wa Wilaya 10 Kwenda China China

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi John Kijazi

Ikulu imefuta safari ya wakuu wa wilaya 10 na wakurugenzi idadi kama hiyo waliotakiwa kwenda China kwa mafunzo ya uchumi wa kimaeneo kuanzia jana, na kuna uwezekano mkubwa ikatangaza uteuzi mpya leo.

Wakuu hao wa wilaya na wakurugenzi wao  walikuwa waondoke jana kwa ufadhili wa Serikali ya Watu wa China, lakini habari zinaarifu kuwa Ikulu iliamua kutotoa kibali, hali inayozidisha ubashiri kuwa uamuzi huo umetokana na kukamilika kwa uteuzi wa wakuu wapya.

Safari hiyo ilishakamilika kwa kiwango kikubwa baada ya kupata visa na wengi wao kuwasili jijini Dar es Salaam tayari kwa safari hiyo, lakini wakalazimika kurejea kwenye vituo vyao baada ya kukosa kibali cha Ikulu ambacho hutolewa na Katibu Mkuu Kiongozi.

Mara tu baada ya kuapishwa Novemba 5 mwaka jana, Rais John Magufuli alitangaza kudhibiti safari za nje za watumishi na viongozi wa umma kwa kuagiza kuwa Ikulu ndiyo itakayotoa kibali baada ya kujiridhisha na umuhimu wa safari hizo kwa Taifa.

Tangu atoe agizo hilo, ni mawaziri wawili tu ambao wameruhusiwa kwenda Vietnam kwenda kujifunza kilimo na viwanda. Mawaziri hao ni Mwigulu Nchemba (Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi) na Charles Mwijage (Viwanda na Biashara).

Naibu Waziri wa Fedha, Dk Ashatu Kijaji alikwenda nchini Ethiopia kuhudhuria mkutano wa mawaziri wa fedha, wakati kwa nyakati tofauti Makamu wa Rais Samia Suluhu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa walikwenda Afrika Kusini na Botswana.

Mpaka sasa, Rais Magufuli amefanya safari moja tu ya nje alipokwenda Rwanda kwenye maadhimisho ya mauaji ya kimbari.

Lakini safari ya wakuu hao wa wilaya ilikuwa ifadhiliwe na China, kwa mujibu wa habari hizo na hivyo isingeisababishia Serikali kutumia vibaya fedha za walipa kodi.

Uamuzi huo unaonekana kuzingatia zaidi uteuzi wa wakuu wapya ambao taarifa zinasema unaweza kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa, wakati wa wakurugenzi wa wilaya unatazamiwa kutangazwa baadaye wiki hii au wiki ijayo.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene alikiri kuwapo kwa safari hiyo, lakini akasema hajui kama imeidhinishwa na Ikulu kwa kuwa si muhusika.

“Katika hatua za awali nilisaini safari hiyo kuwaruhusu waende China, lakini sijui kama wamenyimwa kibali kwa sababu hilo si suala la ofisi yangu,” alisema Waziri Simbachawene.

Kama ni kweli, alifafanua Simbachawene, inaweza kuwa ni kutokana na umuhimu wao wa kuwatumikia wananchi kwenye maeneo wanayotoka. “Hawawezi kuondoka na kuziacha wilaya zao ilhali wao ndiyo waangalizi,” alisema Simbachawene.

Akiwa Chato mkoani Geita, Rais aliwataka wakuu wa wilaya kuchapa kazi badala ya kuwa na woga wa kutoteuliwa akisema uchapaji kazi ndio utawafanya waendelee kuwapo kwenye nafasi zao.

Rais pia amekuwa akitoa maelezo kadhaa yanayoonyesha atafanya uteuzi kwa kutumia vigezo hivyo, hasa suala la elimu ambayo inakabiwa na tatizo kubwa la uhaba wa madawati na vyumba na majengo, kipindupindu, njaa, migogoro ya ardhi na watumishi hewa.

Halmashauri 26 zinazoongozwa na vyama vya upinzani nchini Zatishia Kujiondoa ALAT

$
0
0

Halmashauri zinazoongozwa na vyama vya upinzani nchini vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) zinakusudia kujiondoa kuwa wanachama wa Jumuiya ya Halmashauri Nchini (ALAT), endapo mapendekezo waliyoyatoa yatapuuzwa.

Akiwasilisha maazimio ya kikao chao jana mbele ya waandishi wa habari mjini Dodoma, Makamu Mwenyekiti wa umoja wa wenyeviti na mameya wa halmashauri zinazoongozwa na (UKAWA) ambaye pia ni Meya wa Jiji la Arusha, Bw. Calist Lazaro, alisema wamependekeza kubalishwa kwa sheria na kanuni za katiba ya (ALAT), ili ziweze kuendana na wakati uliopo na kutoa mazingira rafiki kwa vyama vya upinzani, ili viweze kuwa na uwakilishi katika kamati tendaji ya (ALAT) taifa

Ukawa, ambayo inaundwa na vyama vya Chadema, CUF, NLD na NCCRMageuzi, imeshikilia majiji na halmashauri kubwa nchini baada ya kupata ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015 uliokuwa na ushindani mkubwa. 

Kati ya majiji, miji na halmashauri 26 zilizo chini ya vyama hivyo, kuna majiji matatu ya Mbeya, Arusha na Dar es Salaam, baadhi ya manispaa muhimu za miji kama Iringa, Moshi na Siha mkoani Kilimanjaro, Tunduma (Songwe), Monduli (Arusha), Kinondoni na, Ilala (Dar es Salaam).

Alisema athari itakazopata kama wakijitoa ni kuyumba kifedha kutokana na ukweli kuwa majiji na halmashauri hizo ndizo zinazotoa michango mikubwa kwenye mfuko wa umoja huo.

“Kama mambo tuliyopendekeza hayatafanyiwa kazi, tutajitoa kwenye umoja huu na kuangalia uwezekano wa kuunda umoja mwingine ambao kweli utakuwa ni kwa maslahi ya taasisi hizi za serikali za mitaa,” alisema.

“Halmashauri zetu hazitachangia, Alat wabaki na chombo chao.”

Mbali na michango, Alat pia hutegemea fedha za wafadhili na wadhamini wa shughuli zao.

Kalist, ambaye ni meya wa Jiji la Arusha, aliiutaka uongozi wa Alat kufanya marekebisho ya katiba na kanuni za Alat ziweze kuendana na wakati kwa kutoa mazingira rafiki kwa vyama vya upinzani.

Alisema mazingira hayo ni kuwa na uwakilishi katika kamati ya utendaji ya Alat Taifa kama ilivyo bungeni na katika kamati za fedha za halmashauri ambapo suala la uwepo wa uwiano wa kivyama miongoni mwa wajumbe ni la kikanuni.

Pia mameya na wenyeviti hao walitangaza kutoutambua uongozi mpya wa Alat kwa madai ulichaguliwa kinyume cha Katiba ya Alat na kanuni za uchaguzi za mwaka 2009.

“Tunaomba Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua mapato na matumizi ya Alat kwa kuwa fedha hizi ni za wananchi zinazochangwa kupitia halmashauri zao,” alisema.

Miongoni mwa mambo wanayodai kukiukwa katika uchaguzi huo ni pamoja na kumruhusu Meya wa Jiji la Tanga kugombea umakamu mwenyekiti, wakidai kuwa si chaguo la wananchi wa jiji la Tanga kupitia madiwani wao.

Mgombea mwenza wa Lowassa, Juma Duni Haji Arudisha Kadi ya CHADEMA na Kujiunga CUF

$
0
0

Mwanasiasa machachari wa upinzani kutoka Zanzibar, Juma Duni Haji ambaye alikuwa mgombea mwenza wa aliyekuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Lowassa katika uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana kupitia Chadema, amerejea katika chama chake cha CUF.

Duni amerejea CUF ikiwa imepita miezi takribani tisa tangu alipojiunga na Chadema ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad na waandishi wa habari mjini Zanzibar jana, Duni alisema: 

“Nimerudi nyumbani CUF na Chadema nilikwenda ili kutimiza matakwa ya kikatiba kwa kuwa mgombea mwenza wa urais lazima atoke upande wa pili wa Muungano. Hiyo ni kwa mujibu wa matakwa ya Katiba yetu.”

Mara baada ya Lowassa kupitishwa na Chadema na Ukawa kuwa mgombea wa urais, Duni ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa CUF na Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) alionekana kuwa na sifa ya kuwa mgombea mwenza na hivyo kupewa kadi ya Chadema.

Mwanasiasa huyo amekuwa na historia ndefu na mara tatu amewahi kuteuliwa na CUF kuwa mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano, akiwa na aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba.

Jana, Duni alikuwa miongoni mwa viongozi wa CUF waliokaa meza kuu na Maalim Seif wakati Katibu Mkuu huyo akieleza mwelekeo wake na wa chama hicho baada ya kususia uchaguzi wa marudio Zanzibar uliofanyika Machi 20, mwaka huu.

Akieleza uamuzi wake huo Duni alisema: “Sioni ajabu yoyote mimi kurudi CUF. Kwa nini nibaki Chadema? Siwezi kubaki kwa sababu kule nilikwenda kwa ajili ya makubaliano tu.”

Huku akionekana kutotaka kueleza uamuzi wake huo kiundani, Duni alisema pamoja na kuwa amerejea CUF, ushirikiano wa chama hicho pamoja na vingine vinavyounda Ukawa vya Chadema, NCCRMageuzi na NLD, uko palepale.

Akieleza jinsi CUF walivyompokea, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema ni faraja kubwa kwa mwanasiasa huyo kurejea nyumbani.

“Jana (juzi) saa 10.30 jioni katika tawi la CUF la Kibeni lililopo katika Wilaya ya Kaskazini Unguja jimbo la Mkwajuni ndipo Duni alipofanyiwa hafla fupi ya kukaribishwa tena katika chama chetu na kupewa kadi,”alisema Mazrui.

“Alirejesha kadi ya Chadema na kuchukua na CUF. Tunamkaribisha sana na tunampongeza kwa kuiwakilisha vyema Chadema na Ukawa katika Uchaguzi Mkuu.”

Mazrui alisema si jambo la ajabu kwa mwanasiasa huyo kurejea CUF kwa sababu awali alikuwa katika chama hicho ila aliondoka kwa ajili ya kwenda kutimiza matakwa na ushirikiano ndani ya Ukawa.

“Ndani ya Ukawa lengo letu ni moja wala hilo lisikufanye ukafikiri tofauti... usidhani kuwa kuna tofauti yoyote eti kwa sababu ya uamuzi huu wa Duni,” alisema Mazrui.

Waliozalisha Watumishi HEWA Kikaangoni

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka makatibu tawala wa mikoa nchini kuchukua hatua kali dhidi ya wote waliosababisha kuwapo kwa watumishi hewa.

Amesema suala hilo la watumishi hewa limeisababishia Serikali hasara kubwa, hivyo ni lazima watu wote waliohusika katika sakata hilo wabainishwe na wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.

Majaliwa alisema hayo jana alipokuwa akipokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa wa Lindi iliyowasilishwa na mkuu wa mkoa huo, Godfrey Zambi katika siku ya kwanza ya ziara yake ya pili kikazi wilayani Ruangwa. 

Wakati akiwaapisha wakuu wapya wa mikoa Machi 15, Rais John Magufuli aliwapa siku 15 kuhakikisha wanabaini watumishi hewa wote katika mikoa yao na kuwaondoa katika mfumo wa malipo.

Baada ya kufanyika kwa kazi hiyo, jumla ya watumishi hewa 7,795 walibainika ambao wameisababishia Serikali hasara ya Sh7.5 bilioni.

Awali, Zambi alisema Lindi ina jumla ya wafanyakazi watoro 57 na hewa saba ambao walifariki na wengine kustaafu, lakini walikuwa wakilipwa mishahara na kuisababishia Serikali hasara ya Sh36 milioni kwa mwezi.

Wabunge Wahoji Uhalali wa Kisheria wa Rais Magufuli kuhamisha fedha za Muungano na Kuzipeleka Kwenye Ujenzi wa Barabara Mwanza

$
0
0

Baadhi ya Wabunge wamehoji uhalali wa kisheria wa Rais John Magufuli kuhamisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya sherehe ya Muungano na kuzipeleka kwenye ujenzi wa barabara katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Wabunge hao walihoji hilo wakati wa semina iliyofanyika jana katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam , iliyoendeshwa na Dk Haji Semboja kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Harold Sungusia wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali alihoji juu ya mamlaka ya Rais katika kutumia fedha ambazo zilishapangiwa bajeti na Bunge na kuzipeleka kwenye maeneo mengine.

Alihoji pia juu ya nidhamu ya Serikali katika usimamizi wa Bajeti iliyopitishwa na Bunge. Mbunge huyo alisema dhana ya mgawanyo wa madaraka haipo kwa sababu Serikali ina nguvu kuliko Bunge na Mahakama hivi sasa.

Alisisitiza kuwa nguvu hiyo ndiyo inayomfanya Rais afanye kitu chochote anachotaka.

Mbunge wa Viti Maalumu, Lucia Mlowe alisema moja ya majukumu ya Bunge ni kuisimamia Serikali, lakini anashangaa kuona yenyewe ikilisimamia Bunge katika mambo mbalimbali.

Alisema hata suala la Rais kuhamisha fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe ya Muungano, ni kuingilia madaraka ya Bunge, kwa sababu fedha hizo tayari zilikuwa zimeidhinishwa kwa ajili ya matumizi hayo.

“Naomba kupata ufafanuzi kutoka kwa wataalamu hapa, Rais ana mamlaka gani ya kuhamisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya jambo fulani? Pia, ni namna gani wabunge tunaweza kuisimamia Serikali kama hamna uwiano kati ya mihimili hii mitatu,” alihoji mbunge huyo.

Akijibu hoja hizo, Dk Semboja alisema Sheria ya Bajeti ya 2015, inampa mamlaka Rais kupeleka fedha katika eneo analoona inafaa.

Alisema sheria hiyo inatoa sharti moja, kwamba Rais kupitia Waziri wa Fedha, atatoa taarifa bungeni juu ya matumizi ya fedha hizo.

Dk Semboja alisema mamlaka hayo yanatambuliwa pia katika Ibara ya 137 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, hivyo Rais hajakosea kuhamisha fedha hizo kwenda kujenga barabara isipokuwa taarifa ya matumizi itolewe bungeni hata kama matumizi yanaonekana.

“Bunge lazima lifahamishwe kuhusu matumizi ya fedha hizo.Kama ni udhaifu wa kipengele hiki, basi unaanzia kwenye Katiba,” alisema Dk Semboja.

Pia, Sungusia alisema, “Fedha ambazo Rais hawezi kuziingilia ni zile zilizo kwenye consolidated fund (mfuko hodhi), nje ya hapo anaweza kufanya lolote,” alisema mwanasheria huyo.

Ole Sendeka Aunguruma Babati......Asema Wanaopingana na Sera ya Rais Magufuli Ya "Kupasua Majipu" Wanapoteza Muda wao

$
0
0

Msemaji Mkuu wa CCM ambaye pia ni Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Kata ya Bashneti, wilayani Babati mkoani Manyaraalisema, Chama Cha Mapinduzi kinamuunga mkono na kumtetea kwa nguvu zake zote Rais Dk. John Magufuli katika jitihada zake za kuliinua taifa la Tanzania.

Alisema, CCM itafanya hivyo kwa sababu kazi anayoifanya ya kupambana na wazembe na wezi wa mapato kwenye vyanzo vya uchumi wa taifa inatokana na maelekezo ya ilani ya CCM.
 
Sendeka alisema, CCM inawataka wale wote wanaojaribu kupotosha jitihada zinazofanywa na Rais za ‘kupasua majipu’ wakidai kuwa ni kuwaonea wanaochukuliwa hatia, kuacha mara moja, kwa sababu kinachofanyika ni sahihi na  kipo kwa mujibu wa sheria.
 
Alisema, upasuaji majipu huo unaofanaywa na Rais Magufuli hauchagui chama bali yeyote anayebainika kuwa ni jipu hata akiwa mwana CCM haachwi.
 
Kwa upande wake, Mjumbe wa NEC, Kilumbe Ng’enda, aliwataka Watazania kutambua kuwa Uchaguzi umeshamalizika kwa hivyo asitokee yeyote kuanza kuweweseka, kwa kutoa maneno ya kejeli kuhusu utendaji kazi wa Rais Dk. Magufuli kwa sababu baada ya uchaguzi kumalizika sasa kiichobaki ni kuchapa kazi.
 
Alisema, hakuna sababu za mwanasiasa yeyote kuanza mambo ya fitina za kisiasa wakati huu kwa kuwa kufanya hivyo ni kujisumbua.

Waziri Mkuu Awaweka Kitanzini Wakurugenzi wa Halmashauri Nchini

$
0
0

WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Kassim Majaliwa amesema Mkurugezi yeyote wa Halmashauri nchini atakayeshindwa kutenga asilimia 10 ya mapato kwa ajili ya wanawake na vijana ataondolewa.

Amesema suala la kila Halmashauri kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya kuwawezesha wanawake na vijana kujikwamua kiuchumi na kuondokana na utegemezi ni la lazima na si hiari.

Waziri Mkuu, Majaliwa ameyasema hayo jana (10 Aprili, 2016) alipokuwa anazungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Kitandi, Mtimbo,  Likunja, Nkowe na Namahema ambako alifanya mikutano ya hadhara.

“Halmashauri ambayo itashindwa kutenga asilimia 10  kwa maana asilimia tano kwa ajili ya vijana na tano kwa ajili ya akinamama Mkurugenzi wake atakuwa anatafuta safariiri,” alisema Waziri Mkuu, Majaliwa.

Waziri Mkuu, Majaliwa yupo wilayani Ruangwa, Lindi kwa ajili ya ziara ya kikazi inayolenga kukagua shughuli za maendeleo, ambapo amewasisitiza Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutimiza wajibu wao na serikali haitamvumilia yeyote atakayeshindwa.

Pia Waziri Mkuu, Majaliwa aliwataka wananchi hao kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali ili zitakapofika sh milioni 50 za kila kijiji zilizoahidiwa na Rais, Dk. John Magufuli waweze kunufaika.

Alisema fedha hizo ambazo zitatolewa kuanzia mwezi Julai mwaka huu zitagawiwa katika vikundi mbalimbali vilivyosajiliwa na si kwa mtu mmoja mmoja hivyo amewataka watendaji wa kata na vijiji kuwahamasisha wananchi kujiunga katika vikundi.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu, Majaliwa alisema serikali imefuta tozo tano kati ya tisa za zao la korosho zilizokuwa kero ya muda mrefu na kufanya wakulima wachukie mfumo wa Stakabadhi ghalani.

Acacia kuilipa Serikali Dola mil.20

$
0
0

KAMPUNI ya Acacia Mining PLC imesema itailipa serikali kodi ya dola za Kimarekani milioni 20 mwaka huu baada ya kusainiwa mkataba wa maridhiano kati yake na Mamlaka ya Mapato (TRA) mwezi uliopita jijini Dar es Salaam.

Makubaliano hayo baina ya Acacia na TRA ni kilele cha mchakato uliofanywa kwa lengo la kuendeleza dhamira ya utendaji ya kampuni hiyo nchini Tanzania na kuongeza ushirikiano na wadau mbalimbali wa kampuni hiyo.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Bradley Gordon, alitoa taarifa hiyo kwenye mawasiliano na wafanyakazi wa kampuni hiyo. 

Alisema kutokana na makadirio, kampuni hiyo italipa kodi ya ushirika ya miaka mitatu, endapo kampuni hiyo mwaka huu itaingiza mapato yanayofikia kiasi cha dola za Marekani milioni 80.

Alisema mkataba kati ya Acacia na TRA umetiwa saini na umetambuliwa na pande zote mbili kwamba hakuna kodi yoyote ya mapato yatokanayo na faida ambayo Acacia inastahili kulipa, haitalipwa.

Gordon alisema Acacia Mining ambayo iliingia nchini katika sekta ya madini ikijulikana kama Barrick na baadaye kama African Barrick Gold miaka 15 iliyopita, imekuwa ikitengeneza faida lakini haijarejesha mtaji iliowekeza wa dola za Kimarekani bilioni 3.8.

Hivi karibuni, Baraza la Rufaa za Kodi (TRAT), liliamua katika rufaa iliyokatwa na Acacia kwamba kampuni hiyo ilijenga mazingira ya kukwepa kodi ya dola za Marekani 41,250,426 (Sh bilioni 89) kwa kipindi cha miaka minne mfululizo.

Katika hukumu hiyo iliyotolewa na Mwenyekiti wa TRAT, Jaji Dk Fauz Twaib, ilielezwa kuwa fedha hizo zilizopaswa kulipwa na ABG kwa TRA kama kodi ya zuio katika kipindi hicho, lakini ikakata rufaa kupinga kodi hiyo na baraza hilo kuipa haki TRA.

Hata hivyo, Acacia imepinga uamuzi huo katika Mahakama ya Rufaa. Akizungumzia historia ya mgodi huo, Gordon alisema wakati Barrick ilipoingia Tanzania miaka zaidi ya 15 iliyopita, kulikuwa na shughuli za kiwango kidogo za migodi nchini.

Gordon alisema tangu wakati huo, Barrick, African Barrick Gold na kisha Acacia Mining zimewekeza kiasi cha dola bilioni 3.8 katika ujenzi na uendelezaji wa migodi mitatu iliyopo hadi sasa.

Alisema Tanzania sasa ni mzalishaji mkuu wa nne wa dhahabu duniani, na kwamba kampuni yao ndiyo wazalishaji wakubwa nchini jambo alilosema hawana budi kujivunia. 

Akizungumza madai kwamba wanatoa taarifa za uongo za kupata hasara ili kukwepa kulipa kodi nchini , alisema akaunti zao pamoja na zile za migodi mingine duniani hufanyiwa uhakiki makini.

“Kwa Tanzania peke yake, kuna mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Shirika la Uhakiki wa Migodi, Mahakama ya Udhibiti na Mamlaka ya Mapato Tanzania –taasisi zote hizi zinapembua hesabu zetu.

"Kwa kuwa tuna Soko la Hisa la London lenye umahiri mkubwa nalo pia linafanya kazi makini kuhakiki shughuli zetu,” alisema.

Alisisitiza kuwa hawajakwepa kulipa kodi bali katika biashara, panahitajika kwanza kuondoa gharama zote katika mapato kabla ya kutangaza kwamba wamepata faida.

Alisema katika miaka sita iliyopita pekee, tumelipa zaidi ya dola za Kimarekani milioni 750 kama kodi na mrabaha nchini Tanzania, karibu mara mbili ya kiasi ambacho wanahisa wamepokea kama mgao.

Gordon alisema wamewekeza dola za Kimarekani milioni 65 kwenye miradi ya maendeleo ya jamii . Alisema hivi sasa wanatoa ajira zaidi ya 45,000 nchini.

Mkataba tata wa Kampuni ya Lugumi na Jeshi la polisi Kuwekwa hadharani leo

$
0
0

Mkataba tata wa Kampuni ya Lugumi Enterprises uliosababisha kashfa ya ufisadi wa mabilioni ya fedha katika Jeshi la Polisi, leo unatarajiwa kuwasilishwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).
 
Mkataba huo huenda ukawasilishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu, ili kutoa fursa kwa wajumbe wa kamati hiyo kuupitia kipengele kwa kipengele kabla ya viongozi wa jeshi hilo kuanza kuhojiwa juu ya ufisadi huo.
 
Kupitia mkataba huo wa 2011, Kampuni ya Lugumi Enterprises ilipewa tenda ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi 108 nchini kwa gharama ya Sh bilioni 37.
 
Tayari kampuni hiyo imekwishalipwa Sh bilioni 34 sawa na asilimia 99 ya fedha zote, huku ikiwa imefunga mashine katika vituo 14 tu katika jiji la Dar es Salaam ambavyo pia havijulikani vipo maeneo gani.
 
Uwasilishwaji wa mkataba huo ni utekelezaji wa agizo la PAC, ambapo Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Aeshi Hilaly alitoa siku sita kwa Jeshi la Polisi kuwasilisha mkataba huo.
 
Jana Aeshi alisema baada ya kamati yake kupokea mkataba huo wajumbe wataupitia na kuujadili kwa kina ili kuona kama kuna upungufu.
 
“Kesho (leo) ndiyo tarehe 11, tutapokea  mkataba kama tulivyowaomba watuletee, wakituletea tutausoma na kuujadili kwa kina kisha tutawaapa maelekezo,” alisema Aeshi.
 
Alisema iwapo kamati yake haitaridhishwa na maelezo ya viongozi wa Jeshi la Polisi kuhusu mkataba na fedha zilizotumika, upo uwezekano mkubwa wa kuundwa kwa kamati maalumu.
 
“Kama vifaa vimefungwa katika vituo vyote, ni matumaini yetu vitakuwa vinafanya kazi, huwezi kufunga vifaa ambavyo ni vibovu…kama maelezo tutakayoyapokea hayataridhisha kuna uwezekano wa kuundwa kwa kamati ya uchunguzi,” alisema Aeshi.
 
Hivi karibuni Kamati ya PAC ilibaini kuwapo kwa viashiria vya ufisadi katika Jeshi la Polisi kwa kuwaeleza waandishi wa habari kuwa Kampuni ya Lugumi ililipwa Sh bilioni 34 kati ya Sh bilioni 37 za mkataba wote.

Watuhumiwa wa Dawa za kulevya Wazidi Kubanwa

$
0
0

WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Kassim Majaliwa amemtaka Mkuu wa Magereza mkoa wa Lindi, kuhakikisha hakuna mtuhumiwa wa dawa za kulevya atakayetoweka katika gereza la mkoa huo.

Amesema kuna watuhumiwa wa dawa za kulevya ambao wanahifadhiwa katika gereza la mkoa wa Lindi hivyo ni vema akajiridhisha kama ulinzi na usalama wa watuhumiwa hao umeimarishwa.

Hata hivyo, Waziri Mkuu, Majaliwa amemtaka mkuu wa gereza hilo kuwa makini na baadhi ya zabuni wanazozitoa kutoka nje na kuhakikisha ulinzi unaimarisha wakati wote gerezani hapo.

Waziri Mkuu, Majaliwa aliyasema hayo jana (10 Aprili, 2016)  wilayani Ruangwa wakati akipokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Lindi iliyowasilishwa kwake na Mkuu wa mkoa huo, Godfrey Zambi.

“Mkuu wa Magereza wa mkoa atembee gereza ambalo wanashikiliwa watuhumiwa wa dawa za kulevya na aangalie mradi unaolenga kupeleka maji gerezani hapo kama ni kweli au njia…,” alisema Waziri Mkuu, Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu, Majaliwa alimtaka mkuu huyo wa Magereza kujiridhisha kama ulinzi na usalama wao umeimarishwa na kuhakikisha hakuna mtuhumiwa anayetoweka.

Awali akisoma taarifa kwa Waziri Mkuu,  mkuu wa mkoa wa Lindi, Zambi alisema matumizi ya dawa za kulevya hususan kwa vijana ni miongoni mwa changamoto zinazoukabili mkoa huu ambapo wilaya ya Kilwa inaongoza kwa kuwa na waathirika wengi.

Alisema matumizi ya dawa hizo yanasababisha kupunguza kwa nguvu kazi kwani watumiaji wengi ni vijana, hivyo alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na serikali katika kupiga vita matumizi ya dawa hizo kwa kuwafichua wauzaji na watumiaji.

Breaking News:Rais Dkt. Magufuli Amfukuza Kazi Mkuu Wa Mkoa Wa Shinyanga, Mama Anne Kilango Malecela

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga  mama Anna kilango Malecela kuanzia leo.

Utenguzi huo umetokana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Anna kilango Malecela kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hauna watumishi hewa jambo ambalo lilisababisha Ikulu kufanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili ya uchunguzi bado inaendelea.

Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea hundi ya shilingi bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada ya kubana matumizi kwa ajili ya kununulia madawati, Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa  sana na hali hiyo.

Amesema idadi ya wafanyakazi hewa mkoani Shinyanga huenda ikaongezeka zaidi kwani wilaya mbili za mkoa huo bado zinaendelea kuhakikiwa.

Rais pia ametengua uteuzi wa  Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Abdul R. Dachi kwa kumshauri vibaya Mkuu wa Mkoa.
 
Mama Anna Kilango Malecela, ambaye katika awamu ya nne alikuwa Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi na Mbunge wa Same Mashairiki, anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kwanza kuachishwa kazi akiwa amedumu katika nafasi hiyo kwa mwezi mmoja tu..
 

Chama cha Mapinduzi (CCM) kitaendelea kuimarisha miundombinu na mazingira rafiki kwa wafanyakazi wake

$
0
0

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitaendelea kuimarisha miundombinu na mazingira rafiki ya kiutendaji kwa kuwapatia vifaa vya kisasa jumuiya mbali mbali za taasisi hiyo ili zifanye kazi kwa ufanisi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Zanzibar, Najma Murtaza Giga wakati akikabidhi Vifaa mbali mbali kwa Uongozi wa Wazazi Mkoa wa Mjini, huko Afisi ya CCM Amani.

Amesema taasisi hiyo inatakiwa kwenda sambamba na mabadilio ya sayansi na teknolojia kwa kutumia nyenzo za
kisasa zitakazowasaidia watendaji wa taasisi hizo kufanya kazi nzuri na kwa haraka.

Aidha amesema chama hicho kitafanya kila kinachowezekana kuhakikisha kinawapatia Vitendea Kazi Watendaji wa CCM kadri ya uwezo wa kifedha unaporuhusu.

Giga amewasihi viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zingine kuunga mkono juhudi zinazofanywa na jumuiya ya wazazi katika kutoa malezi bora ya kitaaluma na kisaikolojia kwa watoto kwa lengo la kutengeneza viongozi makini na weledi wa baadae.

Nae Katibu wa CCM mkoa wa mjini, Mohamed Omar Nyawenga amewataka watendaji wa chama hicho kuwa wabunifu na kutumia weledi kwa kufanya kazi kwa bidi ili kusaiudia chama kutekeleza ilani ya uchaguzi ya 2015/2020 kwa ufanisi ili wananchi waendelee kuiunga mkono CCM katika chaguzi zote zijazo.

Vifaa vilivyotolewa ni Kompyuta 2, mashine za Printer 2 na mashine za photocopy 4 kwa jumuiya ya wazazi mkoa wa mjini kichama.

Rais Dkt. Magufuli Apokea Taarifa Ya Mwaka Ya Utendaji Wa Taasisi Ya Takukuru Pamoja Na Hundi Kifani Ya Sh. Bilioni 6 Kutoka Bunge Baada Ya Kubana Matumizi.

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Mwaka ya utendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Kamishna Valentino Mlowola Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hundi Kifani yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita kutoka kwa Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson mara baada ya Taasisi ya Bunge kutekeleza kwa vitendo kauli ya kubana matumizi yasio na Tija ili fedha hizo zikanunulie madawati kwa ajili ya wanafunzi.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiitazama Hundi Kifani yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita mara baada ya kukabidhiwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson mara baada ya Bunge kutekeleza kwa vitendo kauli ya kubana matumizi ili fedha hizo zikatumike kwa ajili ya ununuzi wa madawati kwa ajili ya wanafunzi.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson kulia, Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah pamoja na wafanyakazi wengine wa Bunge wakiwa wameishika hundi Kifani hiyo yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita. Rais Dkt. Magufuli ameipongeza Taasisi ya Bunge kutokana na hatua hiyo ya kubana matumizi na kuamua fedha zao zitumike katika kununulia madawati kwa ajili ya wanafunzi.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameishika Taarifa ya Mwaka ya utendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Kamishna Valentino Mlowola Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson kabla ya kukabidhiwa hundi kifani yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika tukio hilo la upokeaji wa Taarifa yaUtendaji wa  TAKUKURU pamoja na upokeaji wa Hundi Kifani kutoka Taasisi ya Bunge Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo katika Hotuba yake ambayo pia alitengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ane Kilango Malecela ambaye alikubali kutoa taarifa ambazo si sahihi kuwa Mkoa wa Shinyanga hauna watumishi hewa, japo katika uhakiki uliofanyika mara baada ya taarifa hiyo kumebainika kuwa kuna zaidi ya watumishi 45 ambao ni hewa.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi  pamoja na Waziri wa Ofisi ya Rais Tamisemi, Utumishi na Utawala bora Angela Kairuki Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na  Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi John Kijazi wapili kulia, Dkt. Tulia Ackson wakwaza kulia, Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah  wakwanza kushoto, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna Valentino Mlowola Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Mhandisi John Kijazi Taarifa ya Mwaka ya utendaji kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Ikulu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Viongozi wa juu wa Jeshi la Magereza pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa JKT wakisikiliza kwa makini maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyokuwa akiyatoa Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Bunge Labana Matumizi na Kuokoa Bilioni 6.....Rais Magufuli Aagiza Fedha Hizo Zikabidhiwe Kwa Magereza Na JKT Ili Kutengeneza Madawati 120.000

$
0
0

Rais Magufuli ameipongeza ofisi ya Bunge kwa kubana matumizi na kufanikiwa kuokoa shilingi Bilioni 6, ambazo zitatumika kutengeneza madawati ya wanafunzi wa shule na amezitaka ofisi na taasisi nyingine za serikali kuiga mfano huo.

Ameagiza fedha hizo zipelekwe Idara ya Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili vyombo hivyo vifanye kazi ya kutengeneza madawati yanayotarajiwa kuwa zaidi ya 120,000 ambayo yatasambazwa katika shule ili kukabiliana na tatizo la wanafunzi wanaokaa chini kwa kukosa madawati.

Hundi Kifani ya fedha hizo imekabidhiwa kwa Mheshimiwa Rais na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Akson, ambaye amesema Ofisi ya Bunge imetekeleza wito wa serikali wa kubana matumizi ambapo kiasi hicho cha shilingi Bilioni 6 kimepatikana kwa kipindi kifupi cha takribani nusu mwaka.

Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilila ametaja maeneo ambayo Bunge limebana matumizi kuwa ni Safari za nje ya nchi, Mafunzo nje ya nchi, Machapisho na ununuzi wa majarida, Shajala, Chakula na Viburudisho, Mtandao, Malazi hotelini, Matibabu ya wabunge na familia zao nje ya nchi, Umeme, Maji, Simu na Uendeshaji wa Mitambo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pia ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga  Bi. Anne Kilango Malecela na Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Abdul Rashid Dachi, kufuatia mkoa huo kutoa taarifa zisizo sahihi kuwa hauna watumishi hewa.

Rais Magufuli ametangaza kutengua uteuzi wa Viongozi hao wa Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 11 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, mara baada ya kupokea Taarifa ya Mwaka 2014/2015 ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), na kupokea hundi kifani ya shilingi Bilioni 6 kutoka Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizotokana na kubana matumizi.

Dkt. Magufuli ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa kuwa Mkoa wa Shinyanga hauna watumishi hewa, aliamua kutuma timu ya ukaguzi iliyokwenda kufanya uchunguzi ambapo hadi kufikia jana tarehe 10 Aprili, 2016 imebaini kuwepo watumishi hewa 45 huku zoezi likiwa linaendelea katika wilaya mbili za Ushetu na Shinyanga Vijijini.

“Na wale wote wa Shinyanga ambao walisemekana ni zero, hakuna mtumishi hewa, walikuwa tayari wameshalipwa shilingi milioni 339.9, nimejiuliza sana, na nikajiuliza sana na kwa kweli nimejiuliza sana na kwa masikitiko makubwa, kwa nini Mkuu wa Mkoa alisema hakuna mtumishi hewa?” Amesisitiza Rais Magufuli

Rais Magufuli amesema baada ya kutengua uteuzi wake, Anne Kilango Malecela atapangiwa kazi nyingine.

Pamoja na hatua hiyo, Dkt. Magufuli ametaka wakuu wa mikoa yote wawafichue watumishi hewa wote ili waondolewe mara moja, na ameagiza timu iliyofanya uchunguzi Mkoani Shinyanga itumike kufanya uchunguzi katika mikoa mingine kwa lengo la kukomesha upotevu mkubwa wa fedha za umma.

Katikati ya Mwezi Machi, 2016 Rais Magufuli aliwaagiza wakuu wa mikoa yote nchini kusimamia zoezi la kuwaondoa watumishi hewa wote katika orodha ya malipo ya mshahara, ambapo mpaka tarehe 31 Machi, 2016 Jumla watumishi hewa 5,507 walibanika.

Kati ya shilingi Bilioni 583 ambazo serikali imekuwa ikitumia kila mwezi kwa ajili kulipa mishahara, kati ya shilingi Bilioni 53 na 54 zimekuwa zikipotea kutokana na kulipa mishahara ya watumishi hewa.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam-11 Aprili, 2016

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza na Vigogo wengine wa Usalama Wapanguliwa

$
0
0
 John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza 

Serikali imepangua uongozi wa vyombo vya dola mkoani Mwanza kwa kuwahamisha vituo vya kazi watendaji wakuu akiwamo Kamanda wa Polisi, Justus Kamugisha aliyehamishiwa mkoani Mbeya.

Mkuu wa Mkoa John Mongella alisema hatua hiyo inalenga kuimarisha utendaji wa taasisi hizo na kukabiliana na matukio ya uhalifu yaliyotikisa mkoa huo tangu kuanza kwa mwaka huu.

“Kwa kipindi kifupi cha wiki mbili tangu nihamie Mwanza, nimeshuhudia matukio kadhaa ya uhalifu, yakiwamo mawili ya ujambazi yaliyoishia kwa raia wema kupoteza maisha na mamilioni ya fedha kuporwa,” alisema Mongella. 

“RPC amehamishiwa Mbeya ambako nadhani labda kuna changamoto kidogo kulinganisha na zile za Mwanza alizoonyesha kushindwa,” alisema Mongella.

Mongella alisema pamoja na RPC, vigogo wengine waliohamishwa kutoka Mwanza ni pamoja na ofisa utumishi wa jeshi la polisi, ofisa Idara ya Usalama wa Taifa na kamanda wa mkoa wa Idara ya Uhamiaji.

Akizungumza na viongozi, watumishi na watendaji wa vyombo vya dola wilayani Magu, Mongella aliwataka kutimiza wajibu kwa kudhibiti na kukabiliana na vitendo vya uhalifu katika maeneo yao, akionya watakaoshindwa watawajibishwa.

“Haiwezekani majambazi yatambe kwa kuvamia, kupora na kuua wananchi watakavyo, na vyombo vya dola na viongozi wenye dhamana ya ulinzi na usalama wapo wanashuhudia. Kila mtu atimize wajibu wake,” alisema Mongella.

Alitumia fursa hiyo kuuagiza uongozi wa polisi wilaya ya Magu kukomesha matukio ya mauaji ya kukata watu kwa mapanga yanayodaiwa kufanywa na watu wanaokodishwa.

Ndani ya kipindi cha miezi miwili ya Februari na Machi, Jiji la Mwanza limekumbwa na matukio sita ya ujambazi ambayo yamechukua maisha ya watu sita waliouawa kwa kupigwa risasi, huku mamilioni ya fedha yakiporwa kutoka maduka ya fedha kwa njia ya mitandao.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images