Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mfumuko wa Bei Machi 2016 umepungua hadi asilimia 5.4 kutoka asilimia 5.6 ya Februari

$
0
0

Mfumuko wa Bei kwa Machi 2016 umepungua hadi asilimia 5.4 kutoka asilimia 5.6 ya Februari.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo amesema kuwa upandaji wa bei za bidhaa kwa mwaka ulioshia kwa Machi , 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioshia Februari mwaka huu.

Amesema Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 101.93 mwenzi Machi, 2016 kutoka 96.69 mwezi Machi 2015.

Kwesigabo amesema kuwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Machi, 2016 umepungua hadi asilimia 8.5 kutoka 9.5 iliyokuwa kwa Februari, 2016.

Amesema kupungua kwa mfumuko wa bei wa mwezi Machi, 2016 kumechangiwa hasa na kupungua kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Machi 2016 zikilinganishwa na bei za mwezi Machi 2015.

Kwesigabo amesema mwenendo wa bei za bidhaa zisizo za vyakula zinaonyeshwa kupungua kwa mwezi Machi 2016 ikilinganishwa na mwezi Machi 2015 bidhaa hizo ni Gesi asilimia 10, Diseli 5.8, Mafuta 1.0.

Mfumko wa bei unafanana nchi za Afrika Mashariki , kwa mwezi Machi nchi ya Kenya Mfumuko umepungua hadi asilimia 6.45 kutoka asilimia 6.8 kwa Februari, Uganda mfumuko wa bei umepungua hadi asilimia 6.2 kwa Machi 2016 kutoka asilimia 7.0 kwa Februari 2016.

Bosi wa Zamani wa TRA Harry Kitillya, Shose Sinare na Sioi Solomoni Wanyimwa Dhamana

$
0
0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imepuuza ombi la dhamana ya kesi inayowakabili Harry Kitillya, Shose Sinare na Sioi Solomoni ambapo wamerejeshwa rumande.

Kitillya, alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA); Sinare, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwekezaji katika Benki ya Stanbic na Sioi Solomoni, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic.

Dhamana yao imesikilizwa mbele ya Amilis Mchaura, Hakimu Mkazi Kisutu ambapo mawakili wa pande zote mbili waliwasilisha hoja zao.

Dk. Lingo Tenga ndiye aliyeongoza jopo la mawakili upande wa watetezi ambapo upande wa serikali umesimamiwa na Oswadi Tibabyekonya, Wakili Mkuu wa Serikali Mahakama ya Kisutu.

Upande wa utetezi uliomba mahakama kubatilisha mashitaka ya utakatishaji pesa haramu uliosababisha watuhumiwa hao kukosa dhamana. Tibabyekonya ameieleza mahakama kuwa, shitaka la utakatishaji fedha halina dhamana.

Upande wa utetezi ulifanya mapitio ya kesi mbalimbali zinazofanana na kesi hizo ikiwemo kesi namba 314 ya mwaka 2015 kwenye Mahakama ya Rufaa ya Mwanza iliyokuwa ikimkabili Kigunda Francis aliyeshitakiwa kwa kosa kama hilo lakini alipewa dhamana.

Christopher Msigwa, wakili wa serikali amesema kuwa kesi hiyo haina dhamana kwa sababu, kosa hilo linaathiri uchumi wa taifa.

Washitakiwa wamekosa dhamana na wamerudishwa rumande hadi tarehe 22 Aprili mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Jeshi La Polisi Kanda Maalum Ya Dar Es Salaam Limefanikiwa Kuwakamata Watu 63 Wanaodhaniwa Kuwa Majambazi

$
0
0

Jeshi  la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata watu 63 wanaodhaniwa kuwa  majambazi wa kutumia silaha katika operesheni endelevu ya kuwasaka majambazi wanaofanya matukio mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Kamishna wa Polisi kanda maalumu Simon Sirro aamesema, miongoni mwa majambazi waliokamatwa ni Ibrahim Juma(31) mkazi wa Kiwalani Kigilagila, Samweli Mbonea (40) Fundi gereji Mkazi wa Kiwalani pamoja na Anthony Kanywenywe (60) Mwindaji na mkazi wa Kiwalani.

Amesema majambazi hao walikutwa na taa kubwa nne za magari, pawa windo moja na nati za magari na watuhumiwa sita  kati ya waliokamatwa wamekiri kushiriki katika matukio ya unyanganyi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali likiwemo la Riki Hill Hotel katikati ya jiji na Lake oil Buguruni.

Katika tukio jingine  kikosi maalumu cha kupambana na majambazi kimefanikiwa kukamata silaha sita  aina ya SMG  moja ,Short gun pump action tatu na Rifle mbili katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.

Amesema silaha aina ya SMG iliyokatwa kitako ilipatikana baada ya askari kuwafyatulia risasi majambazi hao waliokuwa eneo la vingunguti ndipo walipoitupa silaha hiyo ikiwa kwenye mfuko mweusi wa plastiki na wao kukimbia katika bonde la Mto Msimbazi.

“Tunaendelea kuwatafuta watuhumiwa hao na upelelezi unaendelea ili kubaini mmiliki halali wa silaha hiyo. Hatupotayari kuendelea kuona maovu yakiendelea kufanyika, jeshi lipo imara na tutapambana nao,” alisema Sirro.

Ameongeza kuwa jeshi hilo pia lilifanikiwa kukamata silaha Rifle mbili katika eneo la Masaki ambazo zilikuwa zimefichwa na kufunikwa kwa taulo zikiwa na maandishi ya Collessium Fitness Club  moja ikiwa na namba A 6777013 iliyosajiliwa nchini kwa namba TZCAR 58596, na nyingine ikiwa na namba L 691848176 iliyosajiliwa kwa namba TZCAR 75062.

Wakati huo huo Jeshi la Polisi Kanda maalum Dar es salaam limefanikiwa kukamata jumla ya risasi 15 za silaha ndogo aina ya bastola zikiwa kwenye magazine.

Risasi hizo alikutwa nazo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mamboleo Willium (41) Mfanyabiashara mkazi wa Mikocheni.
 
Katika mahojiano mtuhumiwa huyo alikiri kuwa na risasi hizo kinyume na sheria na kushindwa kueleza mahali alipozipata, mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa  na uchunguzi unaendelea kufanyika

Taarifa Ya CCM Kuhusu Kauli Ya Mhe Lowassa Kubeza Utendaji Wa Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli

$
0
0

Aliyekuwa mgombea Urais wa UKAWA kupitia CHADEMA, Ndugu Edward Lowassa, Aprili 7, 2016 alifanya mazungumzo na Wanazuoni kutoka katika vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi.

Katika mazungumzo hayo, Ndugu Lowasa aligusia masuala mbalimbali ya Kitaifa yakiwemo hali ya siasa nchini, kuachisha kazi watumishi wenye tuhuma mbalimbali, na kile alichokiita tatizo la mfumo nchini.

Alichokifanya Ndugu Lowassa ni kutaka kuwaaminisha Watanzania masuala yasiyo sahihi kwa maslahi ya kisiasa, kwani ukweli ni kwamba; Mosi, Rais John Pombe Magufuli hatafuti umaarufu, badala yake yeye na Serikali yake wanachapa kazi ili kuwaletea maendeleo Watanzania kwa ujumla.

Pili, kuhusu suala la mfumo, Tanzania haina tatizo la kimfumo, kwani iliyopo, iliyowekwa tangu awali na waasisi wa Taifa letu, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume ni imara na imekuwa ikiboreshwa kulingana na mahitaji.

Ifahamike hakuna mahali popote duniani ambako mfumo wa nchi unajiendesha wenyewe, siku zote mfumo huongozwa na kuendeshwa na binadamu ambao kwa udhaifu wa ama kibinadamu au wa kukusudia, hufanya makosa yanayohitaji kusahihishwa kwa taratibu zilizowekwa.
 
Tatu, Hakuna mtumishi aliyeachishwa au kusimamishwa kazi kwa sababu ya hali ngumu ya uendeshaji wa Shirika lolote, isipokuwa hatua hiyo imechukuliwa ili kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali za ukiukaji na matumizi mabaya ya ofisi na madaraka, ubadhirifu, uhujumu uchumi na ufisadi.

Chama Cha Mapinduzi kina ushahidi wa utendaji wa Ndugu Lowasa akiwa Waziri Mkuu namna alivyoendesha zoezi la kusimamisha na kufukuza kazi na kuwadhalilisha watumishi bila kufuata taratibu, hali hiyo ni tafauti sana na hii ya sasa, kwani kila anayesimamishwa kazi, anasimamishwa kwa kufuata taratibu zote, ili kuhakikisha kila mtumishi anatendewa haki ya kusikilizwa.

Na katika hili la kuwasimamisha kazi watumishi wa umma wanaotuhumiwa kwa ufisadi, wizi na matumizi mabaya ya ofisi, Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuunga mkono, kutokana na baadhi yao kuwa kikwazo cha shughuli za maendeleo nchini.

Kiongozi au mwanasiasa anayemkosoa Rais Magufuli katika hatua anazozichukua hivi sasa, ikiwa ni pamoja na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma, ni wa kutiliwa shaka kwani kufanya hivyo ni sawa na kutetea wizi, ufisadi na uporaji wa rasilimali za nchi.

Ndugu Christopher Ole Sendeka
MSEMAJI WA CCM
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
08/04/2016

Majaliwa: Rushwa Inadumaza Maisha Ya Wananchi

$
0
0

WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa amesema vitendo vya dhuluma, ufisadi na jeuri vinavyofanywa na watoaji na wapokeaji rushwa vinasababisha wananchi kukosa haki zao na maisha yao kuwa duni, hivyo amewataka wajumbe na Viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) kupiga vita rushwa katika ngazi zote za utawala kwenye mamlaka zao na kwa nchi.

“Sote tunakumbuka msemo wa rushwa ni adui wa haki na kwamba sitapokea wala kutoa rushwa,” amewasisitiza juu ya umuhimu wa msemo kwa sababu kuna  dalili kwamba rushwa ni kikwazo kikubwa katika utekelezaji wa majukumu ya maendeleo katika ngazi mbalimbali zikiwemo za halmashauri, serikali kuu na taasisi mbalimbali za umma.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo mchana wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa ALAT uliofanyika mjini Dodoma ambapo amesema vitendo vya rushwa vinalalamikiwa sana na wananchi, katika maeneo yote, hususan katika huduma za afya, elimu, ardhi na utoaji leseni mbalimbali katika Serikali za Mitaa.

“Kutokana na ukweli huo, wapo wananchi ambao wameanza kupoteza imani kwa serikali yao kutokana na kuendeleza vitendo vya rushwa miongoni mwa jamii.  Natoa wito kwenu mkiwa wajumbe wa chombo hiki muhimu kupiga vita vitendo vyote vinavyoashiria rushwa katika ngazi zote za utawala kwenye mamlaka zenu na kwa nchi yetu,” amesema.

Amesema hata wakati Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli anazindua Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 20 Novemba, 2015 alibainisha maeneo mbalimbali ambayo ni kero kwa Wananchi mojawapo  ni tatizo la rushwa miongoni mwa jamii.

Waziri Mkuu, Majaliwa amesema kuwa wakati wa kampeni za uchaguzi rais alipata fursa ya kusikiliza malalamiko mengi ya wananchi ikiwa ni pamoja na  kushindwa kwa serikali za mitaa kutekeleza majukumu yake na kuwajibika kwao kama katiba, sheria na sera zinavyoelekeza.

Amesema changamoto nyingine aliyoizungumzia Mheshimiwa Rais ni upotevu wa mapato na kushindwa kukusanya kodi, ubadhirifu, matumizi mabaya ya fedha na  madaraka, ambapo utekelezaji wa baadhi ya miradi upo chini ya viwango huku kukiwepo na wizi, uzembe katika mamlaka za serikali za mitaa. hivyo kusababisha upotevu mkubwa wa fedha.

Waziri Mkuu, Majaliwa amesema kuna uvujaji mkubwa wa mapato yanayokusanywa na mamlaka za serikali za mitaa kupitia mawakala au hata  baadhi ya watumishi wachache wasio waaminifu, ambapo alitumia fursa hiyo kuwasisitiza usimamizi mzuri wa mapato ya halmashauri na kuhakikisha yanakusanywa kwa njia ya kielektroniki ambapo imebainika kuwa ni salama na itasaidia kupunguza kupovu huo.

“Ninatambua kwamba bado zipo changamoto za utaratibu huu wa kukusanya mapato kwa njia ya elektroniki.  Aidha, zipo taarifa kuwa, baadhi ya watumishi wa halmashauri ndiyo wenye kampuni za uwakala wa kukusanya kodi na tozo mbalimbali za halmashauri, hivyo nawakumbusha watendaji wote kwamba taarifa hizi zikibainika ni za kweli, hatua za kinidhamu zitachukuliwa. Ni vyema wahusika waache tabia hiyo mara moja kwani ni kinyume na maadili ya utumishi wa umma,” amesema.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu, Majaliwa ameyataka mabaraza ya Madiwani yafanye kazi zake kwa mujibu wa sheria, ambapo amekemea tabia ya baadhi ya watendaji wa halmashauri kutokutaka kuulizwa chochote na mabaraza hayo kwa kisingizio kwamba wao ni watalaamu.

Amesema Mabaraza ya Madiwani ndiyo mamlaka ya wananchi katika kusimamia halmashauri hivyo kuwazuia Madiwani kuhoji chochote hata pale ambapo wataalam wamekwenda kinyume na maadili ya taaluma na utumishi wa umma  siyo sahihi kiutendaji, hivyo amewataka watendaji hao kuyaachia Mabaraza hayo  yafanye kazi zake na kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wakea Naibu Waziri wa Nchi, Osisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Suleiman Jafo amesema watahakikisha wanatoa maelekezo wanazisimamia vizuri halmashauri katika ukusanyaji wa kodi kwa mfumo wa kielektroniki.

Pia Jafo amempongeza Waziri Mkuu Majaliwa kwa utendaji wake na kwamba amewathibitishia Watanzania kuwa Rais Dk. John Magufuli hakukosea katika uteuzi huo na kwammba umakini wake katika kuchapakazi umeleta tija nchini.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa ALAT  Taifa, Steven Muhapa akitoa hutuba ya shukurani kwa Waziri Mkuu, amesema maelekezo na maagizo yote yaliyotolewa na Waziri Mkuu wameyapokea na wataenda kuyafanyia kazi.

Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu atishia kufuta halmashauri zitakazoshindwa kukusanya mapato kufikia asilimia 80

$
0
0

Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa ametishia kufuta halmashauri zitakazoshindwa kukusanya mapato kufikia asilimia 80 ya lengo na kuwaonya watumishi wa halmashauri hizo wenye kampuni za uwakala wa kukusanya kodi na tozo mbalimbali, kutozipa kampuni zao kazi hiyo kuepuka mgongano wa kimaslahi.

Majaliwa alisema endapo mtumishi wa halmashauri atabainika kutumia kampuni yake kukusanya kodi atachukuliwa hatua za kinidhamu.

 Alisema hayo jana mjini Dodoma, wakati akifungua mkutano mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT).

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Serikali ya Awamu ya Tano imejikita katika uboreshaji wa huduma za wananchi na ukusanyaji mapato, hivyo halmashauri itakayoshindwa kukusanya mapato kwa asilimia 80 itafutwa.

Alisema kumekuwa na ufujaji mkubwa wa mapato kupitia mawakala na watumishi wachache wasio waaminifu. Alitaka mapato yote ya halmashauri yakusanywe na kusimamiwa vizuri kwa njia za kielektroniki kwa kuwa ndio njia salama. 

“Njia za kielektroniki ni salama na itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza upotevu wa mapato,” alisema.

Alisema, mkakati wa kuwezesha halmashauri kuwa na miradi na uboreshaji wa ukusanyaji wa mapato lazima uheshimiwe hasa wakati huu ambao Serikali inasisitiza umuhimu wa kujitegemea yenyewe.

“Niwakumbushe watendaji wote, tukibaini taarifa za watumishi wa halmashauri kumiliki kampuni za kukusanya ushuru na tozo mbalimbali, hatua za kinidhamu zitachukuliwa. Ni dhahiri kuwa huko ni kuleta mgongano wa kimaslahi,” alisema.

Aliongeza kuwa, rushwa imekuwa ikilalamikiwa na wananchi katika maeneo yote hususan kwenye huduma za afya, elimu, ardhi na utoaji leseni mbalimbali katika Serikali za Mitaa.

“Wananchi wanakosa haki zao na maisha yao yanaendelea kuwa duni kutokana na hali iliyojitokeza ya dhuluma, ufisadi na jeuri wanayofanyiwa na watoaji na wapokeaji wa rushwa. Rushwa ni kikwazo kikubwa katika utekelezaji wa majukumu ya maendeleo ya halmashauri, Serikali Kuu na taasisi mbalimbali za umma,” alisema Majaliwa.

Aliwataka viongozi wa halmashauri kuikomesha kwa kuwa inalalamikiwa kwenye maeneo yao na kuondoa ubadhirifu katika ukusanyaji wa mapato, matumizi mabaya ya madaraka na kukomesha utekelezaji wa miradi chini ya viwango.

Aliwataka viongozi wakuu kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha hakuna huduma inayotolewa kwa kutoa rushwa. Pia, alisema Serikali itaendelea kuimarisha misingi ya kikatiba na namna ya mgawanyo wa madaraka kati ya Serikali Kuu na za mitaa, lengo likiwa kuhakikisha mipango wanayosimamia inaleta manufaa kwenye maeneo yao.

“Wakuu wa mikoa na wilaya wana uwezo wa kuhoji chochote hakuna zuio, lakini hatujaruhusu Mkuu wa Wilaya kuomba fedha, anatakiwa akague miradi na ajiridhishe kuwa inatekelezwa ipasanyo kwa thamani ya fedha inayotengwa,” alisema.

Alisema, Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya hahitaji posho kwenye vikao vya halmashauri hivyo wasiogope kuwaalika kwenye vikao vyao. Akizungumzia migogoro ya ardhi, Majaliwa alisema, imekuwa mingi hali inayotoa somo kuwa sasa Watanzania wanajua thamani ya ardhi.

Alisema ili kuondoa migogoro iliyopo, lazima kila halmashauri iwe na mipango ya matumizi bora ya ardhi kuanzia vitongojini mpaka vijijini. Alitaka wananchi waitambue mipaka yao kwa sababu hiyo si kazi ya Waziri bali ni ya halmashauri yenyewe na kila kijiji.

Viongozi wa Amcos Mikononi mwa TAKUKURU

$
0
0

Taasisi  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Kigoma, inawahoji viongozi wa vyama vitatu vya ushirika vya msingi vya mazao na masoko (Amcos) mkoani humu kuhusu tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.

Viongozi hao wanadaiwa kujikopesha Sh mil 500 kinyume na makusudio ya vyama hivyo. Hata hivyo, inaelezwa kuwa, uchunguzi utaendelea kwa vyama vingine 17 vya akiba na mikopo, ambapo viongozi wake tayari wamekwishaanza kufuatiliwa na taasisi hiyo kuhusu tuhuma mbalimbali zinazowakabili.

Mkuu wa Takukuru mkoani hapa, Mussa Misalaba, akizungumza na waandishi wa habari jana alisema, vyama hivyo vinavyotokana na wakulima wa tumbaku katika tarafa ya Nguruka wilayani Uvinza ni miongoni mwa vyama vilivyopata mkopo kutoka Benki ya CRDB, kwa ajili ya wanachama wake.

Mkopo huo kwa mujibu wa Misalaba, ulilenga kusaidia ununuzi wa pembejeo za kilimo, ujenzi wa mabani ya kukaushia tumbaku na gharama za upangaji madaraja na ununuzi wa kuni katika msimu wa kilimo wa 2015/2016.

Vyama ambavyo viongozi wake wanatuhumiwa na kuhojiwa ni pamoja na Matendo AMCOS, Sagara na Nyangabo, vyote kutoka tarafa ya Nguruka wilayani Uvinza.

Hata hivyo, Misalaba alisema baada ya kila mwanachama kuainisha kiasi alichokuwa anataka na kupatiwa mkopo huo na benki, baadhi ya viongozi na wajumbe wa bodi wa vyama hivyo, walikiuka taratibu za uendeshaji na utoaji wa mikopo hiyo, ambapo watu wachache walijikopesha fedha hizo huku idadi kubwa ya wakulima ikikosa .Inaelezwa kuwa, jambo hilo lilizua malalamiko miongo ni mwa wanachama.

Akizungumzia hali hiyo, Ofisa Tarafa ya Nguruka,Thomas Sangai alisema, kitendo cha viongozi hao kujikopesha fedha hizo, kinaathari kwa wakulima kwani wakati wa marejesho fedha hizo zitalazimika kukatwa katika mauzo ya wakulima hao.

Sambamba na hilo, imeelezwa kuwa vitendo vilivyofanywa na viongozi hao kujikopesha fedha hizo na kushindwa kuwafikia wakulima huenda vikasababisha wakulima kutorosha tumbaku na kuuza katika masoko yasiyo rasmi. 

Hatua hiyo inahofiwa kuwa huenda ikachangia kupungua kwa mapato ya halmashauri, yanayotokana na ushuru wa tumbaku.

Singida Washukuru kuwa wa Kwanza Mgawo wa Milioni 50/- za Magufuli

$
0
0

Mbunge  wa Viti Maalumu, Aysharose Matembe (CCM), amesema vijana na wanawake mkoani Singida, wameishukuru Serikali kwa kuchagua mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa 10 ya kwanza itakayonufaika na mgawo wa Sh milioni 50 kila kijiji na kila mtaa.

Matembe amesema wako tayari kuzitumia kwa uangalifu fedha hizo kwa kuhakikisha wanaunda vikundi vyenye malengo madhubuti ya kujenga ili wajikwamue kiuchumi.

Mbunge huyo jana alisema Singida ni miongoni mwa mikoa yenye rasilimali nyingi, ikiwemo ardhi yenye rutuba ambayo kwa kiasi kikubwa wananchi wanaitumia kujishughulisha na kilimo cha mazao mbalimbali yanayochangia kukua kwa pato la Taifa.

Alisema amezungumza na wananchi hao ambapo walikiri fedha hizo kuwa na mchango chanya kwa maendeleo ya mkoa na kaya zao, hivyo kila mtendaji atakayehusika kwa namna moja au nyingine na fedha hizo, anapaswa kuwa mwadilifu ili ziwafikie walengwa kwa wakati.

“Kutolewa kwa hizi fedha ni kama kupatikana kwa maji jangwani kwa vijana na wanawake wa Singida, kwa nyakati tofauti nimezungumza nao na wananipa salamu kuishukuru Serikali kwa kuwatambua na kuieleza kwamba wamejipanga kunufaika nazo.

Wachina kizimbani kwa kukwepa kulipa kodi

$
0
0

Raia wawili wa China, Ma Jun na Huifang Ma leo wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashtaka mawili likiwamo la kushindwa kutumia  Mashine ya Kodi za Kielektroniki (EFDs) katika biashara zao.

Jun na Ma, ambao wote ni  wafanyabiashara na wakazi wa Mtaa wa Narung’ombe eneo la Kariakoo wanakabiliwa na kushindwa kutumia mashine za EFDs pamoja na kushindwa kujisajili katika kodi ya ongezeko la Thamani(Vat) wakati wakijua kufanya hivyo kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Hata hivyo, mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Jun hakuwepo mahakamani hapo kwa madai kuwa yupo nje ya nchi na upande wa mashtaka umeiomba Mahakama kutoa hati kwa ajili ya kumkamata mshtakiwa huyo.

Akisoma hati ya mashtaka, mbele ya Hakimu Mkazi Mwanadamizi Mfawidhi wa mahakama hiyo Said Mkasiwa, Wakili kutoka Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Cherubin Chuwa alidai kuwa washtakiwa kwa pamoja walitenda  makossa hayo Machi 23,mwaka huu.

Chuwa alidai siku hiyo ya tukio, washtakiwa hao ambao wanamiliki Kampuni ya HM Textile  Co Ltd  Iliyopo  block 54 katika kiwanja namba 6 kilichopo mtaa wa Agrey  eneo la Kariakoo, walishindwa kutumia  mashine za EFDs kwa ajili ya kutoa risiti kwa wateja wao ambao walikuwa wanafanya manunuzi mbalimbali katika duka hilo ambalo linauza mapazia na nguo mbalimbali, huku wakijua kuwa ni kosa kisheria.

Mwandesha Mashtaka huyo aliendelea kudai kuwa, katika shitaka la pili ambalo pia linawakabili washtakiwa wote, inadaiwa kuwa muda na siku hiyo  hiyo katika duka hilo, washtakiwa walishindwa kujisajili katika kodi ya ongezeko la Thamani(Vat) wakati wakijua kufanya hivyo kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Chuwa alidai washtakiwa hao walishindwa kujisajili katika Kodi ya Ongezeko la Thamani(Vat) ambayo ni kinyume cha sheria , na kwamba mashtaka hayo yamefunguliwa kupitia sheria za TRA.

Hata hivyo mshtakiwa wa  pili, Huifang  alikiri shtaka la kwanza huku shtaka la pili akikana kuhusika.

Kutokana na hatua hiyo wakili Chuwa alisema dhamana ya mshtakiwa huyo iko wazi ambayo ni kuwa na wadhamini wawili kila kutoka taasisi inayotambuliwa kisheria watasaini bondi ya Sh 3milioni na kuwasilisha mahakamani hati yake ya kusafiria.

Mshtakiwa huyo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi April 21, mwaka huu.

Waziri Sospeter Muhongo Asisitiza Mapinduzi ya Kiuchumi katika Sekta ya Nishati na Madini.

$
0
0

Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Sospeter Muhongo amelishauri Baraza la Wafanyakazi wa Nishati na Madini kujikita katika kujadili mwelekeo wa mapinduzi ya kiuchumi kwa kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye viwanda.
 
Mhe. Muhongo aliyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam wakati akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo, ambapo baadhi ya mambo yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni masuala ya usafiri kwa wafanyakazi wa wizara hiyo, upandishwaji vyeo kwa wafanyakazi, mafunzo pamoja na uhaba wa nafasi wa ofisi kwa wafanyakazi.
 
Kuhusu suala la upandishwaji vyeo, Mhe. Muhongo alisema kuwa tayari yeye kama Waziri alishafanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ili kuona namna gani wafanyakazi wanapandishwa vyeo kulingana na elimu pamoja uwezo wao kikazi ambapo alipendekeza kubadili mtindo wa upandishwaji vyeo uliopo sasa kwani ni wa zamani.
 
‘’Sifa za upandishaji vyeo kwa wafanyakzi ni vema ukabadilika pamoja na muda wa utoaji vyeo, hivyo napenda kuwasisitiza kuwaangalia vijana tulio nao kwani pale Wizarani tuna vijana wengi wazuri wenye uwezo mkubwa katika kufanya kazi. Katika kikao hiki ni vema mkajadili namna gani mnawapa kipaumbele vijana katika kuwapandisha vyeo vijana hawa,’’ alisema Muhongo.
 
Kuhusiana na uhaba wa nafasi za ofisi, Mhe. Muhongo alifafanua kuwa, ofisi nyingi za Serikali ziko katika mfumo wa zamani, hivyo amelishauri Baraza hilo kuona namna gani watabadilisha muundo wa ofisi ili watu wakae pamoja katika eneo moja lililo wazi na kufanya kazi kuliko kila mtu kuwa na sehemu yake ya kufanyia kazi hali inayosababisha ufinyu wa eneo na uvivu.
 
Aidha, Amewataka wajumbe wa Baraza hilo kujadili ni namna gani wanaweza kubadilisha hali ya kiuchumi toka asilimia 7% hadi kufikia asilimia 8% mpaka 10% ili kukuza uchumi wa nchi na kutokomeza umasikini.
 
‘’Jukumu kubwa la Wizara ya Nishati na Madini ni kuhakikisha kuwa tunakuza uchumi wa nchi kwa kuhakikisha kuwa kunakuwa na umeme mwingi wa bei nafuu na wa uhakika, na kazi tuliyonayo hapa ni kuongeza uzalishaji wa umeme toka Megawati 1400 hadi kufikia Megawati 5,000 mpaka 10,000 na ikiwezekana hadi 15,000 baada ya miaka 10 ijayo’’, aliongeza Mhe. Mhongo.
 
Kuhusu suala la Mafunzo kwa wafanyakazi hao, Mhe. Muhongo alisisitiza kuwa hakuna mtu anayekatazwa kupatiwa mafunzo kwa maana ya kuongeza elimu juu ya jambo fulani, isipokuwa kuna utaratibu wa kwenda kusoma, ambapo panapotokea umuhimu wa wafanyakazi kwenda kusomea mambo muhimu yenye manufaa kwa umma nafasi hizo ni vema zikatolewa ili nchi iwe na wataalam mbalimbali katika nyanja mbalimbali.
 
‘’Hii Wizara inahitaji watu wasome na waelimike, hivyo tunahitaji watu wasome na wawe wataalam katika maeneo mbalimbali ya kazi lengo likiwa ni kuleta maendeleo ya nchi’’, Alisema Mhe. Muhongo.
 
Aligusia masuala ya Bajeti katika Wizara yake ambapo alifafanua kuwa zaidi ya asilimia 89.5/% ya bajeti itatumika katika kufanya shughuli za maendeleo ya nchi.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Aeleza matumaini yake Kutokomeza malaria Katika Bara la Afrika

$
0
0

RAIS mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amesema, ana imani kwamba kupitia ushirikiano uliopo baina ya serikali mbalimbali barani Afrika, mashirika ya kimataifa, makampuni binafsi na kila mtu katika nafasi yake, ugonjwa wa malaria unaweza kumalizwa kabisa.

Kikwete alionesha matumaini hayo juzi wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa jitihada za kuutokomeza ugonjwa wa malaria (Malaria no more) zilizoanzishwa na Ray Chambers akishirikiana na Peter Chernin.

Katika hafla hiyo, Kikwete alitunukiwa tuzo ijulikanayo kama White House Summit Awards ikiwa ni kutambua uongozi wake, kujitoa kwake na kubwa zaidi kusimamia uanzishwaji wa muungano wa viongozi wa Afrika dhidi ya malaria (ALMA), muungano ambao hadi sasa una viongozi 49.

Wengine waliotunukiwa tuzo hiyo ni Ray Chambers na Sumitomo Chemical. Akijibu swali la nini anadhani kimechangia katika kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa malaria, Kikwete alisema zipo sababu kadhaa, lakini kubwa ni utashi wa kisiasa wa kusimamia na kuongoza mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Akawaeleza wageni zaidi ya 250 walioalikwa wakiwa ni wawakilishi wa makapuni na mashirika mbalimbali yanayochangia juhudi za kuukabili ugonjwa wa malaria kwamba, upatikanaji na usambazaji wa dawa sahihi za kutibu ugonjwa wa malaria, utengenezaji, usambazaji na matumizi ya vyandarua vyenye viuatilifu na unyunyiziaji wa dawa za kuua mazalia ya mbu ni mambo ya msingi ambayo yamechangia katika kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya April 9

Mrema wa TLP Amuomba Rais Magufuli Atimize Ahadi yake ya Kumpa KAZI Kama Alivyokuwa Amemwahidi Wakati wa Kampeni

$
0
0

Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) taifa, Augustine Mrema amemuunga mkono Rais John Mgufuli kwa kasi yake ya kupambana na ufisadi na kumuomba ampe kazi ili amsaidie kutekeleza jukumu hilo.

Mrema alimuomba Rais Magufuli atambue uzoefu wake kwa kukumbuka jinsi alivyopambana na mafisadi wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu.

Huku akieleza CV yake hiyo, Mrema alimkumbusha Rais kuhusu ahadi aliyompa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana, ya kumpa kazi katika Serikali ya Awamu ya Tano ikiwa atashinda na kuwa Rais.

Akizungumza na waandishi wa habari kijijini kwake Kiraracha mkoani Kilimanjaro, Mrema alisema kuwa anasikitishwa na ukimya wa Rais Magufuli kwa sababu aliamini kuwa angetekeleza ahadi hiyo ya kumpa kazi muda mfupi baada ya kutangaza Baraza la Mawaziri, jambo ambalo hadi sasa hajalifanya.

Alisema, alikutana na Rais Magufuli mwaka jana katika kampeni jimboni Vunjo kwenye eneo la Njia Panda lililopo ndani ya mji mdogo wa Himo na kuambatana naye kwenye mkutano wa hadhara, ambapo alimwombea kura kwa wafuasi wake na kuahidiwa ajira.

“Katika kampeni, Dk Magufuli alifika kwenye mkutano wangu nikamwombea kura kwa kuwaambia watu wangu wamchague kwa kuwa ni mchapakazi na mwadilifu. Aliahidi kunipatia kazi katika Serikali na sasa namkumbusha na kumuuliza mbona yupo kimya?” Mrema alieleza na kuhoji.

Alipoulizwa ni kazi gani inayomfaa katika Serikali ya Magufuli, alisema yeye alishawahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu hivyo yuko tayari kufanya kazi yoyote itakayomfaa ila alitamani zaidi kupangwa sehemu nyeti ili amsaidie kutumbua majipu.

Mrema alimpongeza Rais Magufuli kwa jitihada binafsi za kutumbua majipu anazozifanya na alijigamba kuwa yeye ndio mwenye uzoefu wa kupambana na mafisadi kutokana na rekodi yake nzuri ya kipindi cha Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.

Katika hatua nyingine, Mrema alikanusha taarifa ya kuhongwa fedha ili kufuta kesi ya kupinga matokeo aliyoifungua dhidi ya Mbunge wa jimbo hilo, James Mbatia.

Alisema, taarifa hizo ni za kupuuzwa kwa sababu zinalenga kumpaka matope kwa wananchi wake wa Vunjo.

Mrema alieleza kuwa walifikia maridhiano ya pamoja kuhusu kuondoa kesi hiyo mahakamani na kwamba, hilo lilifanywa kwa kuzingatia maslahi ya wananchi. 

Pamoja na hayo, alikiri kumlipa Mbatia Sh mil 40 ikiwa ni sehemu ya kupunguza gharama alizotumia katika kesi hiyo, ikiwemo malipo ya mawakili wake.

Ridhiwani Kikwete Akana kufanya biashara na Kampuni Ya Lugumi Inayotuhumiwa Kwa Mkataba Tata na Jeshi la Polisi

$
0
0

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, amekanusha taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari kuwa yeye ni mmoja wa wamiliki wa kampuni ya Lugumi, inayodaiwa kupewa zabuni ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole kwenye vituo vya Polisi.

Ridhiwani ametajwa katika habari hizo kuwa ni mmiliki wa kampuni ya Lugumi pamoja na wamiliki wengine ambao ni Said Lugumi na aliyekuwa mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema.

Ridhiwani ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amesema yeye hahusiki na kampuni yoyote ya Lugumi ingawa wana urafiki wa kawaida na mmiliki wa kampuni hiyo.

“Kwanza kabisa mimi si mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo, hilo ni jambo la msingi kabisa watu waelewe na sijawahi kufanya biashara yoyote na Lugumi. Said Lugumi ambaye ni mmiliki wa kampuni hiyo tunafahamiana naye na ni rafiki yangu,” alisema Ridhiwani.

Ridhiwani alisisitiza kuwa hana uhusiano wa kibiashara na mtu huyo na kwamba hafahamu ni kwa nini amehusishwa na kampuni ya Lugumi.

“Hapa ni watu tu wanaamua kuingiza tu maneno yao, haya maghorofa ninayotajwa kumiliki Dar es Salaam hata sijawahi kutembelea ujenzi wake, wameamua kuniingiza, Lugumi nafahamiana naye binafsi tu lakini wananiingiza,” alisema Ridhiwani.

Alisema jambo hilo bado liko ndani ya Kamati ya Bunge na baadae ameliona kwenye magazeti ya juzi kuwa Jeshi la Polisi litatoa taarifa yao, hivyo asingependa kulizungumzia kwa undani.

Hivi karibuni Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilitoa siku saba kwa Jeshi la Polisi nchini kupeleka mkataba walioingia baina yao na Kampuni ya Lugumi.

Kamati hiyo ilipokutana na Jeshi hilo kupitia taarifa ya hesabu zao za mwaka 2013/14 zilizokaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Aeshi Hilaly alisema jeshi hilo mwaka 2011 liliingia mkataba na kampuni hiyo kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya Polisi vya wilaya nchi nzima ambavyo viko 108.

Alisema mkataba huo ulikuwa wa Sh bilioni 37 pamoja na kodi na kwamba hadi sasa kampuni hiyo imeshapewa asilimia 99 ya fedha zote ili hali vituo vilivyofungwa mashine hizo ni 14 tu, kati ya vituo vyote 108.

Ridhiwani alisema angependa jamii ifahamu kuwa hana uhusiano na kampuni hiyo kwa kuwa hafahamu kabisa hata malipo yaliyofanywa kati ya Serikali na kampuni ya Lugumi anasikia tu kama ambavyo watu wengine wamesikia.

Maalim Seif Sharrif Hamad Kutoa Mwelekeo Wake Kisiasa Kesho

$
0
0

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad kesho ataelezea mwelekeo wake kisiasa, ikiwamo kufafanua kiundani uamuzi wa chama hicho kususia uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu.

Mgombea huyo wa urais Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana ataeleza mambo hayo ikiwa imepita takribani wiki moja tangu Baraza Kuu la chama hicho kutoa msimamo wake wa kutomtambua Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein pamoja na wawakilishi na madiwani.

CUF kilisusia kushiriki uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu baada ya Oktoba 28 mwaka jana, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya urais, uwakilishi na udiwani, akisema kulikuwapo na ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi.

Habari kutoka ndani ya chama hicho zinaarifu kuwa mkutano wa kiongozi huyo utakuwa wa kwanza kwake, tangu kumalizika kwa uchaguzi wa marudio na ataeleza mambo muhimu yatakayotoa picha halisi ya mwelekeo wake na CUF.

“Katika mkutano uliopita tamko lilikuwa la Baraza Kuu ila keshokutwa (kesho) Maalim Seif atazungumza kama Katibu Mkuu na aliyekuwa mgombea urais. Kuna masuala mengi atayaeleza kwa kina, hasa hili la uamuzi wa CUF kususia uchaguzi,” zilieleza taarifa hizo.

“Atazungumzia kwa kina uchaguzi ulivyokuwa na kujibu maswali ya watu wa kada mbalimbali waliokuwa wakihoji nini hatima ya CUF, baada ya kususia uchaguzi na hivyo kupoteza nafasi za uwakilishi.”

Msanii wa Muziki wa dansi Ndanda Kosovo Afariki Dunia

$
0
0

Msanii wa muziki wa dansi Ndanda Kosovo amefariki dunia asubuhi ya leo katika hosptali ya taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwanamuziki mwenzake Kardinal Gento, Ndanda alikuwa alisumbuliwa na matatizo ya vidonda vya tumbo, maradhi yaliyopelekea kulazwa katika hospitali ya Mwananyamala Dar es salaam.

Kardinali ambaye pia ni mjomba wake, amesema kuwa Ndanda alihamishiwa katika Hosptali ya Taifa Muhimbili siku mbili zilizopita kutoka Mwananyamala baada ya tatizo lake kushindikana kabla ya mauti kumkuta majira ya saa mbili asubuhi ya leo.

"Nilikuwa naye hospitali tangu jana, na nimekesha naye, ilipofika asubuhi hali yake ilikuwa nafuu, nikaondoka kurudi nyumbani kwa ajili ya chakula, nikaacha anafanyiwa mpango wa damu maana alikuwa amepungukiwa damu, lakini muda mfupi baada ya kuondoka hospitali hapo nikapigiwa simu kuwa Ndanda amefariki, ilikuwa mida ya saa 2 asubuhi” Amesema Gento.

Gento amesema taratibu za mazishi zinasubiri mama yake arudi Dar es salaam, ndipo wataamua kama asafirishwe au azikwe huku
 
“Mama yake alikuwa amekwenda Lubumbashi, lakini sasa inabidi ageuze na ndege, akisharudi ndiyo tutajua kama tunazika au tunasafirisha…… mama yake ni dada yangu, kwahiyo Ndanda ananiita mimi mjomba”

Hadi mauti yanamkuta Ndada alikuwa akifanya shughuli za muziki kama msanii wa kujitegemea ‘Solo Artist’ pamoja na shughuli za kibiashara

Rais wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein atangaza Baraza lake la Mawaziri

$
0
0

RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dkt. Ali Mohamed Shein leo Jumamosi, April 9, 2016 ametangaza Baraza la Mawaziri litakalosimamia kazi za serikali kwa kipindi cha uongozi wake wake kwa mujibu wa sheria.

Dkt. Shein amesema amepunguza ukubwa wa baraza hilo kutoka wizara 16 hadi kuwa wizara 13, ambapo wizara tatu amezivunja na kuzigawa ndani ya hizo wizara 13 za sasa. Mawaziri ni 13 na Manaibu waziri 7.

Ameongeza kuwa, mawaziri aliowatangaza leo atawaapisha kesho Jumapili asubuhi katika Viwanja vya Ikulu visiwani Zanzibar.

Baraza la Mawaziri Zanzibar hao ni;

1). Ofisi ya Rais na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi – Issa Haji Ussi Gavu.

2). Katiba na Sheria Utumishi wa Umma – Haroun Ali Sleiman.

3). Tawala za Mikoa na Idara maalum – Haji Omari Kheir.

4). Makamo wa 2 wa Rais – Mohamed Aboud.

5). Waziri wa Fedha na Mipango – Dk. Khalid Salum Mohamed.

6). Afya – Mahmoud Thabit Kombo.

7). Wizara ya Elimu – Riziki Pembe Juma.

8). Viwanda na Masoko – Amina Salum Ali.

9). Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi – Ali Karume.

10). Habari Utalii Utamaduni na Michezo – Rashid Ali Juma.

11). Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi – Hamad Rashid Mohamed.

12). Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto – Mauldine Castiko.

13). Maji Ardhi Nishati na Mazingira – Salama Aboud Talib.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya April 10

Msafara wa Rais Magufuli Kutozidi watu 10.....Balozi Mahega Asema Anategemea Kwenga Ng'ambo hivi Karibuni

$
0
0
Rais John Magufuli anataraji kusafiri tena kwenda nje ya nchi hivi karibuni akiwa na msafara ambao unawezekana usizidi jumla ya watu 10.

Ilimchukua Rais Magufuli siku 153 tangu kuapishwa kwake kufanya ziara ya kwanza ya nje ya nchi baada ya kwenda Rwanda kwa mwaliko wa Rais Paul Kagame Jumanne iliyopita.

Rais alikwenda Rwanda kwa ajili ya kufungua daraja la kimataifa la Rusumo na kituo cha biashara chenye huduma za pamoja, ambacho ni kiunganishi muhimu kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Katika safari hiyo, katika kile kinachoonekana kuwa ni muendelezo wa hatua yake ya kubana matumizi ya serikali kadri iwezekanavyo, Rais Magufuli alikuwa na msafara usiozidi watu 10.

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Mahiga, alisema jana kuwa Rais Magufuli anatarajia kusaifiri tena kwenda nje ya nchi hivi karibuni.

Balozi Mahiga alisema katika safari hiyo, msafara wake utaendelea kuhusisha watu wachache wenye umuhimu katika safari husika ili kuepukana na gharama zisizokuwa za lazima.

Hata hivyo, Balozi hakutaja nchi hiyo itakayofuatia baada ya ziara ya Rwanda wala siku ya kusafiri.

“Rais atasafiri tena hivi karibuni… na utaratibu huu wa kuwa na msafara wa watu wachache hautabadilika,” alisema Balozi Maiga.

Akiwa Rwanda, Rais Magufuli alisema hapendi kusafiri kwenda ughaibuni kwa sababu anapenda kubana matumizi kwa vitendo.

Akizungumzia kauli hiyo, Mahiga alisema ni kweli, mara zote Rais Magufuli amekuwa akisisitiza juu ya umuhimu wa kila mmoja ndani ya serikali yake kubana matumizi yasiyokuwa ya lazima na ndiyo maana amekuwa akilidhihirisha hilo kwa vitendo.

“Rais anachosema kuhusu kubana matumizi ni kweli kabisa… ndiyo maana msafara wake katika ziara hiyo (ya Rwanda) hatukuzidi watu kumi. "Hii inamaanisha hataki kuwapo kwa matumizi makubwa katika safari za nje.”

Aidha, Balozi Mahiga alifafanua kuwa baadhi ya mawaziri na maafisa wengine kadhaa walioshiriki shughuli ya uzinduzi wa daraja la Rusumo waliishia hapo na kurudi wakati yeye na maafisa wachache wa serikali wakiongozana na Rais katika ziara ya Rwanda.

“Nafikiri mliwaona baadhi ya mawaziri pale Rusumo… wale walitokea huku Tanzania na kurudi. Hawakuwamo katika msafara uliokuwa Rwanda,” alisema Balozi Mahiga.

Bulembo: Lowassa ni Fisadi, Namshauri Amwache Rais Magufuli na Badala yake Aende Kijijini Kuchunga Ng'ombe

$
0
0


Mwenyekiti wa  Jumuiya ya wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdalah Bulembo amemtaka waziri mkuu wa zamani Edward  Lowassa  amwache Rais Magufuli aendelee kufanya kazi zake.

Bulembo anakuwa kiongozi wa pili wa CCM kumvaa Lowassa aliyekosoa utendaji wa Rais  Magufuli  wa kutumbua majipu wakati  alipokutana na wanazuoni wa ndani na nje ya nje Alhamisi ya wiki hii, baada ya juzi  msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka  naye kumkosoa kuwa si kweli  kwamba watumishi wa umma wanafukuzwa bila kusikilizwa.

Akizungumza  mjini  hapa jana na wanachama wenzake wakati wa maadhimisho ya miaka 61  ya Jumuiya  hiyo yaliyofanyika kitaifa mkoani Morogoro, Bulembo  alimtaka Lowassa  kutekeleza ahadi yake ya kwenda  Monduli kuchunga  ng'ombe  kama hatochaguliwa kuwa Rais.

"Kama yeye anasema kasi ya Magufuli ni ya muda au anakosea kutumbua majipu, basi tunamkumbusha kauli yake wakati akiongea na vyombo vya habari kuwa  akishindwa urais atarudi kijijini kwake kuchunga ng'ombe, tunaomba aende akafanye kazi aliyoahidi. " Alisema Bulembo.

Alisema anashangazwa na Liwassa aliyekuwa mgombea urais mwaka jana kupitia Chadema  chini ya mwamvuli wa UKAWA  kusema ndani ya CCM kumejaa ufisadi wakati yeye ni fisadi namba moja.

Katika hatua nyingine,  Bulembo  alisema ndani ya CCM kuna majipu yanayohitaji kutumbuliwa wakiwemo  Wasaliti.

Alisema  wanasubiri Rais Magufuli akabidhiwe uenyekiti wa CCM mwezi wa saba mwaka huu ili waanze kuyatumbua majipu hayo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images