Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

TCRA Yazifunga Kurasa FEKI za Mke wa Rais Janet Magufuli na Makamu wa Rais Samia Suluhu

$
0
0

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezifungia kurasa za facebook na tovuti ya www.focusvikoba.wapka.mobi baada ya kugundua kuwa zinatumia majina ya viongozi kutapeli watu.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Ally Simba aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, matapeli wanaofanya uhalifu huo wametumia majina ya Janet Magufuli, ambaye ni mke wa Rais na Samia Suluhu ambaye ni Makamu wa Rais kufanikisha utapeli wao.

Dk Simba alisema mamlaka yake imegundua kuwa wahalifu hao wa mtandao huanzisha tovuti, kurasa za facebook na blogu kwa kutumia majina ya viongozi wakuu wa nchi ili kujipatia fedha kutokana na umaarufu wa watu hao.

Alisema matapeli hao hutumia mitandao hiyo kuwadanganya wananchi kuwa kuna fursa za kupata mikopo au misaada kupitia vikundi vya kusaidiana, maarufu kwa jina la vikoba.

“Kwa mfano kuna matapeli walioanzisha ukurasa wa mtandao wa kijamii wa facebook kwa jina la mke wa Rais, Mama Janet Magufuli na kwa jina ma Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan wakilenga kujipatia kujipatia fedha,” alisema Dk Simba.

Aliongeza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 15 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015, mtu yeyote haruhusiwi kujitambulisha kwenye mitandao kwa kutumia utambulisho wa mtu mwingine.

Alisema adhabu ya kosa hilo imeainishwa kwenye kifungu cha 15(2) kinachosema anayepatikana na hatia anaweza kutozwa faini isiyopungua Sh5 milioni au mara tatu ya thamani ya kile atakachokuwa amekipata kupitia utapeli.

Aliwataka wananchi kuwa macho dhidi ya mitandao ya kijamii, tovuti na blogu ambazo zinawataka kutuma fedha au kuchangia kitu chochote ili wapewe mikopo au misaada.

Paul Makonda Atangaza Mikakati Itakayolifanya Jiji La Dar es Salaam Liwe la Kisasa

$
0
0
Siku chache baada ya kuapishwa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekuja na mikakati kadhaa ikilenga kubadilisha mwonekano wa jiji hilo na kulifanya liwe la kisasa.

Miongoni mwa mambo aliyoyagusia ni usafi, ofisi za Serikali kutokuwa za chama, kutenga maeneo ya biashara, sensa ya nyumba kwa nyumba, usalama wa raia na mali zao, watumishi hewa, kurudisha hadhi ya watendaji wa Serikali za Mitaa, elimu na barabara.

Alitoa mikakati hiyo jana alipokuwa akizungumza na wenyeviti na watendaji wa mitaa 559 ya jiji la Dar es Salaam katika mkutano wa kujitambulisha kwao. 

Usafi 
Kuhusu usafi, Makonda alitangaza zawadi ya gari la Sh20 milioni au fedha taslimu kwa mwenyekiti ambaye mtaa wake utaongoza kwa usafi na Sh5 milioni kwa kila mjumbe wa mtaa husika. 

Zawadi hiyo itakayokuwa ikitolewa kila baada ya miezi mitatu, itaanza rasmi Aprili Mosi.

Pia, aliahidi kutoa pikipiki 30 kwa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam ili kuwawezesha askari kuwafuatilia watu watakaotupa taka ovyo barabarani.

“Kampeni ya kushindanisha mitaa bora kwa usafi itaanza kutakuwa na utaratibu wa kukutana na viongozi kwa ajili ya kujadiliana mambo mbalimbali ikiwamo kukabidhi zawadi kwa mwenyekiti atakayeibuka mshindi,” alisema.

Ofisi za Serikali kuwa za chama 
Mkuu huyo wa mkoa ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, alisema ofisi za Serikali ni kwa ajili ya kazi na siyo sehemu ya kufanyia siasa akisema katika uongozi wake haangalii chama, bali kusikiliza matatizo ya kila mtu.

“Ninyi ni kama viongozi wengine, nataka mtimize ahadi zenu mlizowaahidi wananchi kipindi cha kampeni siyo kuleta siasa.Tushirikiane kuleta maendeleo katika jiji hili linalotazamwa na kila mtu,” alisema.

Kutenga maeneo ya biashara
 Makonda alisema matamanio yake ni kuiona Dar es Salaam ya kisasa ambayo itakuwa na maeneo maalumu kwa ajili ya biashara ya vileo, magari, gereji na vifaa vya ujenzi.

“Ninatamani kuona Wilaya ya Kinondoni, Ilala na Temeke zikitenga maeneo maalumu kwa ajili ya maduka ya magari na gereji pia.”

Aliwaagiza wakurugenzi wa manispaa ifikapo Mei Mosi wawe wameainisha maeneo maalumu kwa ajili ya biashara hizo, huku akitoa mwaka mmoja kwa wafanyabiashara husika kuhamia huko.

“Kingine wenyeviti kuanzia sasa ni marufuku maeneo ya pembezoni mwa barabara watu kufanya biashara ikiwamo Ubungo,” alisema Makonda.

Alisema wanaofanya biashara katika maeneo hayo wamekuwa hawalipi kodi hali inayowaumiza wafanyabiashara wa maeneo rasmi na Serikali kukosa mapato.

Alisema baadhi ya watu wanaofanya biashara katika maeneo hayo wanashirikiana na wenyeviti wa Serikali za Mitaa husika.

Wakati akiendelea kuzungumzia suala hilo, mmoja wa mwenyekiti alisimama na kutaka kumpa taarifa lakini Makonda alimkatisha akisema: 

“Mkuu wa mkoa akiongea hakuna taarifa, halafu mimi ni mdogo kwenu lakini ndiyo hivyo kiongozi wenu.” Kisha aliendelea bila ya kutoa fursa hiyo.

Alisema atazungumza na wakurugenzi wa manispaa kuangalia namna ya kuandaa utaratibu wa kutenga barabara moja kwa kila kata kwa siku moja ili watu wafanye biashara.

Sensa nyumba kwa nyumba 
Makonda aliwataka wenyeviti hao kupita kila nyumba katika mtaa kuorodhesha idadi ya watu wanaoishi na shughuli zao.

“Kwa kuwapitia nyumba kwa nyumba mtajua watu na shughuli zao hata kuwabaini wahalifu. Hao ndiyo tunaowatafuta, msiwavumilie watoeni msiogope kufa kwa kuhofia kuwataja.”

Alisema hiyo itasaidia pia kujua watu wasiokuwa na ajira hivyo kujipanga namna ya kuwasaidia. 

Usalama wa raia na mali zao 
Makonda alisema kila mwenyekiti wa mtaa anapaswa kuhakikisha wananchi wake wanakuwa salama na hilo litafanikiwa endapo atakuwa na utaratibu wa kujua nani anafanya nini.

Aliahidi kutoa Sh1 milioni kwa polisi atakayepambana na majambazi, huku milioni moja nyingine ikienda kwa mtu atakayesalimisha bunduki au bastola kituo cha polisi.

Watumishi hewa 
Akizungumzia watumishi hewa, alitoa agizo: “Nitakapoagiza orodha ya watumishi hewa ije kamili, kinyume na hapo ofisa utumishi atalazimika kulipa hata madeni yaliyopita maana anaonekana ana nia ya dhati ya kufuga uozo huo.”

Hadhi ya watendaji wa mitaa 
Makonda pia aliwaahidi kuwajengea ofisi wenyeviti wote wa Serikali za Mitaa na kuachana habari za kupanga na kwamba ifikapo Aprili Mosi atawakopesha pikipiki 1,000 ili ziwasaidie katika utendaji wao wa kazi na kuwasaidia kujikimu kimaisha.

“Kuanzia sasa, hakuna mtu kwenda kumuona mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa bila kuanzia kwa mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa husika ili kurejesha heshima ya viongozi hawa.”

Elimu 
Katika elimu aliwataka watendaji na wenyeviti katika mitaa yao kutafuta wadau kusaidia sekta hiyo badala ya kusubiri Serikali.

Barabara 
Kuhusu kero ya barabara, aliahidi kuzishughulikia, huku akiwashangaa wahandisi kwa kukaa ofisini.

Mtazamo wa wenyeviti 
Wakizungumzia maagizo hayo, baadhi ya wenyeviti na watendaji walisema mengi yanaweza kutekelezeka kwa kuwa mkuu wa mkoa ameonyesha nia katika kuhakikisha jiji linabadilika.

“Mengi aliyoyaongea yalikuwa yanafanyika lakini tulikuwa tunakosa msukumo kutoka juu. Kama ameonyesha nia, hatuna budi kumuunga mkono na kuifanya Dar es Salaam kuwa mji wa aina yake,” alisema Mwenyekiti wa Mtaa wa Faru – Buguruni, Simba Said.

Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Ubaya Chuma alisema watendaji wa ngazi za mitaa wamekuwa na mengi ya kufanya lakini hawakuwa na fursa hivyo ujio wa Makonda huenda ukaleta mabadiliko.

Uchaguzi Zanzibar : Mgombea Urais wa CCM Dr. Shein Apiga Kura Asubuhi Hii

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Ali Mohamed Shein akipiga kura katika uchaguzi wa marudio  kituo namba 1 cha kupiga kura namba 1 Skuli ya   msingi Bungi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo,[Picha na Ikulu.]

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika foleni ya wapiga kura ya Uchaguzi wa marudio katika kituo cha kupiga kura Skuli ya msingi Bungi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo,(wa pili kulia) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt.Idriss Muslim Hija, [Picha na Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Ali Mohamed Shein  akipokea karatasi ya kupigia kura kutoka kwa PA (1) Jaffar Suleiman  kituo namba 1cha kupiga kura ya Uchaguzi wa Marudio Skuli ya Bungi wilaya ya Kati Unguja zoezi ambalo limefanyika leo,[Picha na Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Ali Mohamed Shein akifanya mahojiano na waandishi wa habari na kuwaonesha kidole kilichoingizwa wino maalum baada ya kipiga kura ya marudio leo katika kituo namba 1cha Skuli ya Msingi Bungi Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Viongozi mbali mbali waliomsindikiza wakati alipokwenda kupiga katikauchaguzi wa marudio leo katika kituo namba 1cha Skuli ya Msingi Bungi Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja,[Picha na Ikulu.]
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein akiiangalia karatasi ya kupigia kura katika uchaguzi wa Marudio baada ya kukabidhiwa katika chumba namba 3 cha   Skuli ya Msingi  Bungi  Wilaya ya kati  Mkoa wa Kusini Unguja, [Picha na Ikulu.]

Uchaguzi wa Marudio Zanzibar Unaendelea Kwa AMANI na UTULIVU.......Wananchi Wameitikia na Ulinzi Umeimarishwa

$
0
0
Wananchi wa Zanzibar leo wanapiga kura katika uchanguzi wa marudio baada ya kufutwa kwa uchanguzi uliofanyika October 25,2025 kutokana na kasoro zilizojitokeza.

Katika baadhi ya vituo wananchi wamejitokeza na zoezi linaendelea vizuri huku hali ya usalama ikiwa imeimarishwa.

Katika kituo cha shule ya sekondari Muembeladu ambayo ina vituo sita,vituo vitano vinawatu 350 na kituo kimoja kina watu 91. Akizungumza na wanahabari, msimamizi wa kituo hicho amesema zoezi la upigaji kura linaendelea vizuri katika jimbo la Jangombe .

Kwa upande wa kituo cha skuli ya Muembeshauri nako hali ni shwari na zoezi linaendelea vizuri ambapo katika skul hiyo vituo 11 vinatumika watu kupiga kura.
Katika Jimbo la kikwajuni, zoezi  linaendelea vizuri huku mwitikio wa watu ukiwa ni mkubwa.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupiga kura wamesema zoezi hilo limekua rahisi na la  amani tofauti na taarifa zilivyokua zinasambazwa.

Mkazi wa Muembeshauri aliyejitambulisha kwa jina la Hamidu Salum Haji ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwani zoezi la kupiga kura linaendelea kwa amani na utulivu.

Ndugu zangu tusikubali kugombanishwa na watu ambao hawaitakii mema Zanzibar tusimame pamoja katika kutetea nchi yetu” amesema Haji
 
Wakati zoezi hilo linaendelea maduka mengi yamefunguliwa na wafanyabiashara wanaendelea na kazi kama kawaida.

Dr. Shein: Nategemea Ushindi wa Kishindo.

$
0
0

Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar Dkt Ali Mohammed alizungumza na wanahabari baada ya kupiga kura yake katika kituo cha Bungi, Kibera kisiwani Unguja  ambapo alisema anaamini atashinda kwa kishindo na kuhusu kushindwa  alisema tusubiri matokeo ya uchaguzi ndiyo yataamua.

"Nimepata nafasi ya kupiga kura kama haki yangu ya  kimsingi na kumekuwa na utulivu mkubwa kwenye zoezi hili,hali ya ulinzi imeimarishwa. 

"Matumaini yangu ni kushinda kwa kishindo, kuhusu kushindwa ndugu muandishi tusubiri matokeo ndiyo yataamua".Alisema Dkt. Ali Mohammed Shein

==>>Hapo chini kuna video ya Dr Shein akiongea baada ya kupiga kura

Makamu wa Rais Bi Samia Suluhu Apiga Kura Visiwani Zanzibar

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi Samia Hassan  Suluhu amepiga kura viwasini Zanzibar  katika uchaguzi wa marudio unaofanyika leo. 

Bi Samia amrwapongeza wananncji wa Visiwa vya Zanzibar kwa  kukitokeza kwa wingi kupiga kura kuwachagua viongozi  wao. 

Amewataka Wanzanzibar kuwa watulivu mpaka  zoezi hili litakapokamilika na Matokeo  kutangazwa. 

Christopher Ole Sendeka Ateuliwa Kuwa Msemaji Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)

$
0
0
Chama cha Mapinduzi CCM leo kimemtangaza Christopher Ole Sendeka kuwa msemaji mpya wa CCM kuanzia leo.

Sendeka ametangazwa rasmi na Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu Abdulrahman Kinana mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dar.

Picha ya chini Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kushoto ni  Katibu Mwenezi wa chama hicho Ndugu Nape Nnauye ambaye kwa sasa Ole sendeka pichani katikati  amepewa jukumu la kumsaidia kuwa msemaji wa chama

Hamad Rashid: Nina Uhakika wa Kuwa Rais wa Zanzibar au Makamu wa Rais

$
0
0

Mgombea Urais kupitia Chama cha  ADC Mheshimiwa Hamad Rashid ametimiza haki yake ya msingi ya kupiga kura. 

Akizungumza na Waandishi mara baada ya kupiga kura katika kituo cha shule ya sekondari  Wawi Kisiwani  Pemba,  Rashid amesema  anauhakika wa kuibuka mshindi wa kiti cha Urais wa Zanzibar. 

Amesema kama hatashinda Urais,  basi atakuwa Makamu wa Rais

Hotuba Ya Kwanza Ya Ole Sendeka Kama Msemaji Wa CCM

$
0
0

Machi 15, 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akiwaapisha Wakuu wapya wa mikoa, aliagiza pamoja na mambo mengine, viongozi katika ngazi mbalimbali kuhakikisha wanasimamia nguvu kazi ya vijana katika maeneo yao ili waache kukaa kijiweni.

Agizo hilo lililenga utekelezaji wa vitendo wa matumizi bora ya rasilimali watu nchini wakiwemo vijana ambao ni nguvu kazi muhimu kwa taifa, kujengewa mazingira mazuri yatakayowawezesha kujiajiri katika shughuli za uzalishaji mali.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinampongeza kwa dhati Rais Magufuli kwa agizo lake hilo lenye lengo muhimu la kuwafanya watanzania kwa pamoja kuwajibika.

CCM inampongeza Rais Magufuli kwani kwa mara nyingine tena amedhihirisha kuwa wapiga kura walio wengi walifanya uamuzi sahihi kwa kumchagua yeye kuwa Rais wa Serikali
ya awamu ya Tano katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.

CCM kama chama anachotoka Rais Magufuli na ambacho ndicho Ilani yake inatekelezwa na serikali kwa kupindi cha 2015/2020, ina kila sababu ya kumpongeza kwa kuanza
vizuri katika uongozi wake wa miaka mitano na tunaamini kuwa katika kipindi hicho, “Tanzania Tunayoitaka” itafika mbali kimaendeleo kwenye kila ngazi.

Historia ipo wazi kuwa wakati Tanzania inapata uhuru wake mwaka 1961, Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliongoza taifa letu na kauli mbiu ya UHURU NA KAZI baadae ikabadilika kuwa Uhuru ni Kazi na sasa awamu ya Tano inaendesha shughuli zake kwa kauli mbiu ya “HapaKaziTu” ambayo kila mmoja ni shahidi kuwa hivi sasa kazi inatekelezwa kwa kasi kubwa.

Utekelezaji wa kauli mbiu ya HapaKaziTu umejidhihirisha katika kipindi kifupi cha uongozi wa Serikali hii yak awamu ya tano katika kudhibiti rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma, matumizi mabaya ya madaraka na na ukwepaji kodi, mambo ambayo matokeo yake yameshaanza kuonekana.

Matokeo hayo ni pamoja na kuongezeka kwa makusanyo ya kodi ya serikali, ambayo yameiongezea serikali uwezo wa kuwahudumia wananchi kujikwamua na umaskini kwa
ustawi wa jamii kwa ujumla.

Aidha CCM kinamuunga mkono Rais Magufuli pia kwa hatua anazozichukua yeye na serikali yake katika kurudisha nidhamu na uwajibikani katika utumishi wa umma.

Kumbukumbu zinaonyesha mpaka sasa watumishi wa umma waliochukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali kwenye utumishi wao, na wengine wakifikishwa kwenye vyombo vya sheria, wamefanyiwa hivyo kwa kufuata sheria na kuzingatia misingi ya utawala bora.

Hata hivyo wapo watu wachache wameamua kupotosha nia njema ya Mheshimiwa Rais na serikali yake kwa kuonesha kuwa haya yanayofanyika ni udikteta na uonevu.

Naomba ifahamike kuwa CCM iliiagiza serikali yake kwenye ilani yake ya uchaguzi ya 2015/2020 kuhakikisha inarudisha nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma kwa hiyo kinachofanywa na Rais Magufuli na serikali yake ni utekelezaji ilani ya CCM na ndiyo mahitaji na matakwa ya watanzania walio wengi.

Watanzania walio wengi wanataka kuuona utumishi wa umma wenye nidhamu na uwajibikaji hivyo tunawaomba watanzania kuwapuuza wale wote wanaotafsiri hatua hizi kuwa ni udikteta na uvunjifu wa sheria, kwani kwa matendo yao na maneno yao wanashabikia uzembe na kutowajibika kazini jambo ambalo CCM haikubaliani nalo.

CCM inawasihi wanachama wake, wapenzi, wakereketwa, mashabiki na watanzania wote kwa ujumla kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono kwa vitendo Rais Magufuli kwa dhamira njema aliyonayo kwa taifa letu, ili hatimaye Tanzania yenye maendeleo ifanikiwe.
………………………………………………………………………

Ndugu Christopher Ole Sendeka
MSEMAJI WA CCM
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,

20/03/2016

CCM kuweka utaratibu mpya wa kuwapokea Wanachama waliokihama Chama hicho na Kukimbilia Vyama vya Upinzani

$
0
0

Siku kadhaa baada ya mwanachama wa siku nyingi wa Chama cha Mapinduzi,balozi Juma Mwapachu, kurejea katika chama hicho baada ya kukihama wakati wa harakati za Uchaguzi mkuu wa mwaka jana, kimekiri kuwa kuna haja ya kusikiliza hisia za wanachama wake na kuangalia upya namna gani wanachama wa Chama hicho walioondoka na kwenda kujiunga na vyama vingine wanapokelewa kufutia mazingira ya siasa yalivyo sasa.

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana , ametoa kauli hiyo jijini Dar Es Salaam,wakati wa mkutano na waandishi wa habari, uliolenga kumtambulisha Mjumbe wa Halmashauri kuu Ya Taifa ya Chama hicho Christopher Ole Sendeka, kuwa msemaji wake, kuchukua nafasi ya Nape Nauye, ambaye sasa ni waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Bwana Kinana, amekiri kuwa ni vyema sasa CCM ikae na kutengeneza namna ya watu fulani kurudi ama kutorudi kabisa katika chama hicho kwa kuwa kwa sasa utaratibu unatambua mchakato kumrejesha mwanachama bila kuangalia alitoka kwa mtindo upi.

Katibu Mkuu huyo wa CCM, ameenda mbali zaidi na kusema kuwa lazima chama hicho kiheshimu hisia za wanachama wake.

Akizungumza baada ya kutambulishwa, Ole Sendeka amesema CCM kinampongeza Rais John Magufuli kwa utendaji wake na kwamba huo ndio msimamo wa Chama na kukanusha maeneo yanayoelezwa kwamba huo ni udikteta na uonevu

Taarifa ya habari ChannelTEN, Machi 20, 2016

$
0
0

Taarifa ya habari ChannelTEN, Machi 20, 2016



Watu Watatu Wanyongwa na Kuchomwa Moto Gesti

$
0
0

Watu watatu wamefariki dunia kwa kunyongwa na miili yao kuchomwa moto ndani ya nyumba ya wageni iliyopo Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.

Mauaji hayo yamegubikwa na utata kutokana na mazingira ya tukio hilo kuwahusisha wapangaji wa nyumba hiyo usiku wa kuamkia jana.

Mmiliki wa nyumba hiyo iliyopo Mtaa wa Kyela Kati, Boniface Mtengela alisema waliouawa ni watatu kati ya watu wanne waliofika kwa pamoja saa nne usiku jana.

Alisema watu hao walikuwa  wanaume watatu na mwanamke mmoja na waliouawa ni mwanamke na wanaume wawili.

Mtengela alisema wanaume wawili walijiandikisha kwa jina la Ali Hassan na mwanamke la Mariam.

“Mwanamume mmoja alipanga chumba namba 14, mwingine 105 na mwenye mke alipanga chumba namba 15. 

"Waliokutwa wamekufa ni wanaume wawili wa vyumba na 14 na 105 pamoja na mwanamke huku mwanamume mwenye mke akitoroka,” alisema.

Mganga Mfawidhi wa Wilaya ya Kyela, Francis Mhagama alisema uchunguzi wa miili ya marehemu hao umebaini kuwa waliuawa kwa kunyongwa kisha kuchomwa moto baada ya kumwagiwa mafuta ya taa.

Uchunguzi katika eneo la tukio ulibaini miili yao iliungua, lakini chumba na magodoro havikuungua. Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Kyela Kati, Timoth Luvanda alisema usiku wa tukio hilo hakusikika kelele zozote.

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi hakupatikana kuzungumzia tukio hilo wala kukamatwa kwa mmiliki wa nyumba hiyo na kuhojiwa katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Kyela.

Mhudumu wa nyumba hiyo, Hagai Yohana alisema mgeni mmojawapo aliondoka kabla ya saa 12 alfajiri akiwa na kidumu na mfuko wa rambo.

Alisema wageni wote waliandikisha kuwa ni wafanyabiashara na hawakuwa na mizigo.

Mwandishi Salma Said Apatikana Baada ya Watekaji Kumuachia Huru

$
0
0

Siku tatu baada ya mwandishi wa Mwananchi na DW, Salma Said kutoweka, jana alipatikana baada ya kukutwa katika Hospitali ya Regency ya jijini Dar es Salaam  na kupelekwa kituo kikuu cha polisi kuhojiwa.

Habari zilizopatikana jana jioni na kuthibitishwa na mumewe, Ali Salim Khamis na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi, Simon Siro zilisema Salma alisajiliwa jana mchana katika hospitali hiyo.

Ali aliyekuwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, alisema kwa ufupi kuwa amepata taarifa hizo na kufika Dar es Salaam kuzifuatilia. 

Kamanda Siro alisema ni kweli Salma amepatikana na ametumwa mkuu wa upelelezi wa kanda hiyo kumfuata hospitali ampeleke kituoni kwa mahojiano. 

“ Tumefungua jalada la uchunguzi wa tukio hili juzi,” alisema Sirro na kuongeza. 

“Wapelelezi walizungumza na mume wa Salma na kuna mambo amewaeleza lakini hatuwezi kuyaweka wazi kwa sasa, hadi uchunguzi utakapokamilika, tumeipata namba ya simu aliyowasiliana nayo na mumewe akiwa huko kunakoaminika amefichwa,” alisema. 
 
Wakati huo huo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika tamko lake ililolitoa jana ilieleza kuwa kutekwa kwa mwanahabari huyo kumezua maswali mengi kwa wananchi, familia yake, wadau na wanahabari wa ndani ya nchi na wale wa jumuia za kimataifa.

“Kutekwa kwa Salma kunatokana na kazi yake ya uanahabari, ndiyo maana ushahidi wa awali uliopatikana kwa njia ya ujumbe wa sauti ukiwa na sauti inayoaminika kuwa ni yake, ulieleza wazi kutekwa kwake kunatokana na yeye kuripoti dosari zinazoendelea katika uchaguzi wa marudio Zanzibar,” alisema Joseph Mbilinyi, Waziri Kivuli wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo wa Kambi ya Upinzani. 
 
Mbilinyi ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema) alidai kuwa matukio mbalimbali yanayoendelea Zanzibar yakiwamo ya matumizi ya nguvu, vitisho na hata vitendo vya kikatili dhidi ya wanaosimamia haki, vinaendelea kuitia Serikali ya CCM doa, Taifa na dunia nzima. 

Uhakiki wa Mishahara Hewa Waanza

$
0
0

Siku chache baada ya wakuu wa mikoa kuapishwa na Rais John Magufuli, imeelezwa kuwa wakuu hao wametoa agizo la kuhakiki taarifa za watumishi wa umma kwenye mikoa yao.

Agizo hilo la Rais linalenga kubaini watumishi hewa katika mikoa na wilaya nchini. Kazi hiyo imeanza kutekelezwa kwenye baadhi ya hospitali za Serikali nchini.

Taarifa zilizoptaikana jana, zimeleza kuwa Hospitali ya Wilaya ya Temeke na nyingine za mikoani, watumishi wote wametakiwa kupeleka viambatanisho kadhaa kwa ajili ya uhakiki wa taarifa zao za ajira.

Chanzo kutoka hospitali ya Temeke kilieleza kuwa viambatanishi hivyo ni pamoja na barua ya ajira, wasifu wa kazi na stakabadhi ya malipo ya mshahara.

Chanzo hicho kilisema kuwa agizo hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na wafanyakazi wanatakiwa kukabidhi viambatanisho hivyo kuanzia wiki hii.

Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Temeke, Joyce Msumba alisema, “Hatuhakiki watumishi wa sekta ya afya tu ni watumishi wote wa umma.”

Alisema watumishi ambao wako nje ya vituo vyao vya kazi, wametakiwa kurejea mara moja kwa ajili ya kazi hiyo.

Mbunge Wa Kigamboni Dkt Ndugulile Achaguliwa Kuwa Mwenyekiti Wa Kamati Ya Ushauri Ya Masuala Ya Ukimwi, Afya Ya Kina Mama Na Watoto Ya Mabunge Duniani

$
0
0

MBUNGE wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya masuala ya Ukimwi, Afya ya Mama na Watoto ya Taasisi ya Mabunge Duniani (IPU). Dk Ndugulile amechaguliwa katika mkutano wa 134 wa Mabunge duniani unaoendelea mjini Lusaka, Zambia.

Mkutano huo ulioanza Machi 17, mwaka huu unatarajia kuisha keshokutwa. Kabla ya kuchaguliwa kwake, Dk Ndugulile alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo. 

Kamati hiyo inajumuisha wabunge wasiozidi 12 ambao huteuliwa na Rais wa IPU kutokana na umahiri na mchango wao katika masuala ya Ukimwi na masuala ya afya ya mama na watoto.

Wajumbe wengine wa kamati hiyo wanatoka nchi za Armenia, India, Bangladesh, Afrika Kusini, Rwanda, Italia, Ubelgiji, Austria, Sweden, Dominica na Marekani. 

Majukumu ya Kamati hiyo ni kushauri, kujengea uwezo na kuhamasisha mabunge duniani kuhusiana na njia bora za kuboresha huduma za Ukimwi pamoja na afya za akinamama na watoto.

Dk Ndugulile ni daktari bingwa katika magonjwa ya maambukizi na pia kwenye afya ya jamii. Pamoja na majukumu hayo mapya, pia mbunge huyo ni Mwakilishi wa bara la Afrika katika Taasisi ya Kimataifa ya Ukimwi, Mjumbe wa Kamati ya Wabunge Duniani kuhusu masuala ya Kifua Kikuu (TB) na Mwakilishi wa Bunge la Tanzania kwenye Bunge la Afrika.

TPDC Yatoa Ufafanuzi Juu Ya Ugunduzi Wa Gesi Asilia Bonde La Ruvu Mkoa Wa Pwani

$
0
0

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linapenda kutoa maelezo kuhusu taarifa iliyotolewa na gazeti la Matanzania, Toleo namba 8129 la Jumapili tarehe 20 Machi 2016 lenye kichwa cha habari “Gesi ya Ruvu shakani”. 
 
Taarifa hiyo ilikuwa na lengo la kupinga kile kilichoelezwa na Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo kuwa ujazo wa gesi iliyogunduliwa na Kampuni ya Dodsal ya Uarabuni wenye kukadiriwa kufikia trilioni 2.17 una mashaka. 
 
TPDC inapenda ieleweke kwamba, Kampuni ya Dodsal iligundua gesi katika kisima cha Mambambakofi-1 kwenye kitalu cha Ruvu mwezi Aprili 2015. Taarifa za ugunduzi ziliwasilishwa baada ya kufanya yafuatayo: 
 
1. Vipimo vya kuangalia uwezekano wa gesi au mafuta kwenye mashapo ambapo kisima kilichorongwa kitaalamu iitwayo “wireline logging”. Vipimo hivyo vilionyesha uwapo wa gesi na kwa kitaalamu inaitwa “cross over”
 
2.   Kuchukuliwa kwa vipimo vya mgandamizo kulingana na urefu wa kisima “pressure vs depth” kwenye eneo lenye mashapo lililoonyesha uwepo wa gesi
 
3.   Aidha zilichukuliwa sampuli za gesi katika mashapo hayo ili kubaini aina ya gesi iliyopo pamoja na tafiti zingine. 
 
Baada ya kupitia vipimo hivyo vitatu, vikaonyesha uwapo wa gesi. Kampuni ya Dodsal ikaiarifu TPDC ambayo nayo ilipitia vipimo vya logging na pressure na kujiridhisha uwepo wa gesi asilia. Sheria inaitaka TPDC kama mwenye leseni kuiarifu Serikali kuhusu kufanyika kwa ugunduzi huo.
 
Taarifa hiyo lazima iambatane na kiasi cha awali kinachobashiri ujazo wa gesi ambao ulikuwa ni futi za ujazo bilioni 160 (0.16TCF). 
 
Sheria hiyo pia inamruhusu mkandarasi kuendelea kufanya uchambuzi zaidi wa kina kutumia taarifa za kisima kilichochimbwa. 

Kwa kufanya hivyo, Dodsal wameleta taarifa ya ongezeko la ujazo wa gesi katika eneo tajwa kiasi cha futi za ujazo trilioni 2.01. Hivyo basi, kwa ujumla wake Dodsal wameleta makadiria ya ujazo wa gesi wenye ukubwa wa trilioni 2.17. 
 
Mkandarasi atahitajika kufanya Drill Stem Test wakati atakapoleta mpango kazi wa kuhakiki ujazo wa gesi na uwezo wa mashapo kuzalisha “appraisal program”.
 
Mnamo Machi 2016, Serikali imetimiza matakwa ya kisheria ya kitalu cha Ruvu kuwa na “Location” na Kampuni ya Dodsal inajiandaa kuleta mpango kazi kama inavyoelekeza sheria mpya Petroleum Act 2015 kifungu namba 64 na 65.

Imetolewa na;
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
Benjamin W. Mkapa Pensions Towers, Tower “A”,
Azikiwe/Jamhuri Street
P.O. Box 2774,
Tel. +255 22 2200103/4
Dar Es Salaam, Tanzania
Website: www.tpdc-tz.com

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya March 21

Kichanga Mwingine Adaiwa Kufariki Dunia Kwa Uzembe Mkoani Mwanza

$
0
0

Matukio ya wajawazito kupoteza watoto kwa madai ya uzembe wa wahudumu wa afya yameendelea kuugubika Mkoa wa Mwanza baada ya mkazi wa Nyarawambo wilayani Sengerema Tatu Muhangwa, kujifungua na mtoto wake kufariki kwa kukosa huduma.

Mama mzazi wa Tatu, Vumilia Nailon alisema mjukuu wake alifariki baada ya wahudumu wa afya katika Zahanati ya Ngoma ‘B’ iliyopo Kata ya Nyamatongo wilayani Sengerema, kuchelewa kumhudumia.

Mhudumu wa afya aliyekuwa zamu, Helena Mulwisha alisema alishindwa kumhudumia mjamzito huyo kutokana na kubaini kuwa mtoto alikuwa kakaa vibaya tumboni na kuwashauri kumpeleka hospitali ya wilaya kwa msaada zaidi.

Nailon alisema:“Nilimfikisha mgonjwa wangu zahanati juzi, saa kumi na moja alfajiri, lakini hadi saa tatu hakuwa amepatiwa huduma yoyote hadi alipojifungua mwenyewe bila msaada na mtoto kufariki.

“Mmoja wa wahudumu wa afya aliyekuwapo alishindwa kumhudumia baada ya kugundua mtoto amekaa vibaya tumboni na yeye hana utaalamu wa kumsaidia.”

Alisema Mulwisha aliwashauri kumpeleka mgonjwa hospitali ya wilaya kwa sababu wauguzi na madaktari walikuwa wakihudhuria semina.

“Baada ya kukosa gari ya kumuwaisha hospitali, tuliamua kutembea kwa miguu umbali wa kilomita mbili, lakini hatukufika baada ya magonjwa wangu kujifungulia njia kwa msaada wa wasamaria wema na mtoto kufariki,” alisema Vumilia.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Dk Henry Nyamete alisema ofisi yake inachunguza tukio hilo na kwamba itachukua hatua za kinidhamu dhidi ya mhudumu wa afya aliyekuwa zamu siku hiyo kwa kushindwa kuwajibika kwa kuita gari la wagonjwa ili kumuwahisha mjamzito huyo hospitali kwa matibabu zaidi.

Waziri Mkuu Atoboa Siri za Mwanajeshi Kuteuliwa Kuongoza Mkoa wa Kagera

$
0
0

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ametoboa siri ya kuteuliwa mwanajeshi kuongoza Mkoa wa Kagera, moja ya mikoa iliyoko pembezoni na yenye tishio kubwa la wahamiaji haramu na matatizo ya ardhi.

Hivi karibuni, Rais John Magufuli alifanya uteuzi wa wakuu wa mikoa 26 ya Tanzania Bara na kumteua Meja Jenerali mstaafu, Salum Mustafa Kijuu kuwa Mkuu mpya wa Mkoa wa Kagera.

Mbali ya Meja Jenerali mstaafu Kijuu, Rais Magufuli pia aliwateua wanajeshi wengine watatu kuongoza mikoa ya Katavi, Geita na Kigoma katika uteuzi huo wa Machi 13. 

Hao ni Meja Jenerali mstaafu, Ezekiel Kyunga (Geita), Meja Jenerali mstaafu, Raphael Muhuga (Katavi) na Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga (Kigoma).

Akifanya majumuisho ya ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera wiki iliyopita, Waziri Mkuu Majaliwa alisema: “Hapa kwenu Kagera kuna tatizo kubwa la waharamiaji haramu na uvamizi wa ardhi.

"Wavamizi wengine wanalima bangi katika maeneo yetu badala ya kufuga na kulima.

 “Waondoeni au punguzeni maeneo yao na lindeni mipaka yetu. Mapori ya Kimisi na Burigi yamegeuzwa maficho ya wahamiaji haramu,” alieleza Waziri Mkuu.

“Ndio maana tumemleta Meja Jenerali Kijuu. Shughuli yake huyu siyo nyepesi. Atatembea mwenyewe huko. Huyu si alikuwa Kamandi ya Infantry (askari wa miguu), kwa hiyo ataimudu shughuli hii vizuri.”

Mkoa huo umewahi pia kuongozwa na wakuu wa mikoa ambao ni wanajeshi katika miaka ya nyuma na baadhi yao ni Abdallah Twalipo, Tumainieli Kiwelu, Ayoub Simba, Fabian Massawe, Silas Mayunga na Enos Mfuru.

Mkoa wa Kagera unakabiliwa na tishio kubwa la wahamiaji haramu wanaingia nchini kutoka nchi jirani na wanamiliki ardhi kinyume cha sheria kutokana na udhaifu wa viongozi waliokabidhiwa dhamana ya kusimamia.

Unapakana na Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Aidha, Waziri Mkuu aliiagiza Idara ya Uhamiaji nchini hasa mkoani Kagera kubadilika ambapo alihoji kwa nini hawavai sare za jeshi lao na kuingia msituni kusaka wahamiaji haramu badala yake wanavaa suti maofisini.

Msanii Chid Benz Anatia HURUMA....Msaada wa Haraka Unahitajika Ili Kumuokoa

$
0
0
Hivi ndivyo Chidi Benz anavyoonekana  kwa sasa.
 
Katika mitandao ya kijamii Jumamosi iliyopita kulisambaa picha za rapa Chidi Benz ambazo zinamuonyesha jinsi alivyokonda na kupoteza ule mwili wake wa kuvutia aliokuwa nao zamani.

Mkali huyo wa wimbo Dar es Salaam Stand Up, anakubalika na vijana wengi kutokana na uwezo wake wa kuandika pamoja na kuchana. Lakini miaka ya hivi karibuni alianza kubadilika baada ya kujiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

Oktoba 24 mwaka 2014, Chidi alikamatwa na madawa ya kulevya katika Uwanja wa Ndege wa JK Nyerere wakati akielekea jijini Mbeya kwa ajili ya show. Lakini kesi hiyo ilimalizika miezi michache baadaye baada ya kuamriwa na mahakama kulipa faini.

Tukio hilo liliwafanya wasanii mbalimbali kuzungumzia hali hiyo huku wakimshauri kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya. Ray C ambaye ni mmoja kati ya waathirika janga hilo ambaye kwa sasa yupo kwenye tiba ya methadone, aliamua kumshauri Chid Benz.

“Pole kaka yangu Chidi Benz. Naumia kuona tatizo uliokuwa nalo bado haujalitafutia jibu la kutatua tatizo lako. Mimi ni dada yako natumeshafanya kazi pamoja, tatizo ulilonalo na mimi nilishakuwa nalo na niliweza kulitatua sababu nilijitambua na kutafuta suluhu, nimejaribu kila njia kukushauri badala yake ukaja na rungu la kimasai na kunitandika nalo nyumbani,” aliandika Ray C kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo Chidi Benz aliendelea na harakati zake huku akijinadi katika vyombo vya bahari kwamba tayari ameshaachana na matumizi ya madawa ya kulevya. Lakini watu wake wa karibu pamoja na marafiki zake walikuwa wanadai kwamba bado hajaacha.

Lakini Jumamosi hii akiwa katika kipindi cha Da Weekend Chart Show cha Clouds TV, Chidi amelionekana amechoka zaidi huku akiowamba wadau mbalimbali kumsaidia.

“Matatizo yangu na stress zangu ambazo niko nazo zinanisababishia mwili wangu unapungua kwasababu siko okay, siko poa, siko sawa yaani,” alisema.

Mmoja kati ya wasanii wakongwe wa muziki wa Hip Hop, Afande Selle, alionyesha kusikitishwa na jinsi madawa ya kulevya yanavyomaliza nguvu kazi ya taifa.

 “Yanapita kwa njia gani madawa ya kulevya hapa nchini? Anayasambaza nani mitaaani kote mitaani? Madawa ya kulevya hayaleti maendeleoooo,madawa ya kulevya yanaua masela leooooo,” alisema Afande Selle.

Pia wadau mbalimbali wamewataka watu pamoja na wasanii wenzake kumsaidia huku Arnold Kayanda, mtangazaji wa BBC Swahili akisema amelipokea kwa masikitiko suala hilo.

“Kama picha hii ni rafiki yangu Chidi Benz kama nilivyotaarifiwa, kwa hisani yenu wote naomba kila mtu kwa nafasi yake amsaidie. Mimi niko mbali lakini nikirudi nitakutana naye,” alisema.

Licha ya wadau mbalimbali kutaka asaidiwe lakini bado tunaona hakuna msaada wa haraka ambao mpaka sasa umechukuliwa ili kumuokoa Chidi Benz. 

Serikali ya Magufuli ni sikivu sana, bila shaka kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inayoongozwa na Waziri kijana mpenda sanaa, Nape Moses Nnauye ataliangalia suala hili.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images