Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Shahidi wa Lembeli atinga kortini na mzigo wa masufuria ......Mawakili wajitoa kesi ya kupinga matokeo ya ubunge Jimbo la Kyerwa

$
0
0

Shahidi wa tatu wa mlalamikaji, James Lembeli katika kesi ya kupinga matokeo ya ubunge yaliyompa ushindi Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini, Jumanne Kishimba (CCM) jana alitinga Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga akiwa na mzigo wa masufuria, akidai alipewa kwa ajili ya kumpigia mgombea ubunge wa CCM. 

Mbele ya Jaji Moses Mzuna anayesikiliza shauri hilo, Cesilia Gregory wa Nyahanga mjini Kahama alikiri kupokea zawadi ya masufuria hayo kutoka kwa Wakala wa Kishimba ili ampigie kura. 

Gregory alidai Oktoba 19, 2015, Kikundi cha Amani waliitwa nyumbani kwa Hamad Hilal na kumkuta Ezra Machogu, ambaye alikuwa ni Wakala wa Kishimba akigawa masufuria yalitolewa kwa ajili ya kumuombea kura mgombea ubunge wa CCM. 

Hata hivyo, kulitokea mvutano baada ya Wakili wa Kishimba, Antony Nansimire kumtaka shahidi kuwataja wanakikundi 20 ambao walipewa masufuria hayo, hivyo kuwataja 22 na kwamba ongezeko hilo lilisababishwa na baadhi ya wanaume waliojiunga kuhamasisha utafutaji wapiga kura wa Kishimba. 

Wakati huohuo, mawakili wa mdai katika shauri la kupinga matokeo ya ubunge Jimbo la Kyerwa mkoani Kagera, Benedicto Mutungirehi wamejitoa.

Hatua hiyo ilifuatia makosa ya kisheria yaliyobainishwa katika hati ya kiapo cha shahidi wa pili, Pastory Bagambila ambaye tayari alikuwa mbele ya Mahakama kutoa ushahidi wake. 

Baada ya kubaini makosa hayo, Wakili Erasto aliiomba Mahakama kumuondoa shahidi huyo kutoka kwenye orodha ya mashahidi kabla ya kutoa ombi la kujadiliana kwa muda na mteja wake. 

Hata shahidi wa tatu, Alistides Boniface alipoitwa naye hati yake ya kiapo ilibainika kuwa na kasoro za kisheria, hali iliyomtia hofu Wakili Erasto kuwa yawezekana viapo vya mashahidi wote 36 vilivyowasilishwa vina kasoro. 

Kabla ya kujitoa, wakili Erasto alimuomba Jaji Maisario Munisi anayesikiliza shauri hilo, kuahirisha kwa muda ili wajadiliane na mteja wao. 

Waliporejea mahakamani baada ya dakika 30, Wakili Erasto alimweleza Jaji Munisi kuwa wanaomba kujitoa kwa maelekezo ya mteja wao. 

Kutokana na hali hiyo, Mutungirehi aliiomba Mahakama kumpa muda kutafuta wakili, ombi lililokubaliwa na Jaji Munisi na kuiahirisha hadi Machi 22.

Mbunge wa sasa wa jimbo hilo kupitia CCM, Innocent Bilakwate anawakilishwa na Wakili Peter Matete.

Baadhi ya maombi yake ya msingi, Mutungurehi anadai kulikuwapo na ukiukwaji sheria, taratibu na kanuni katika kuhesabu kura na kudai kulitawaliwa na usiri bila kumhusisha.

UVCCM Wapinga Balozi Juma Mwapachu Kurejea CCM.....Wataka Waliompokea Watimuliwe

$
0
0

Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi wilayani Hai (UVCCM),Arnold Swai amepinga ya kurejea ndani ya chama hicho kwa mwanadiplomasia na mwanasiasa mkongwe nchini, Balozi Juma Mwapachu.

Balozi Mwapachu, juzi alitangaza kurejea CCM kwa madai ya kuridhishwa na utendaji wa Rais Magufuli.

Akizungumza na wanahabari jana mkoani hapa,Swai alisema kuwa chama hakipaswi kumpokea mwanasiasa huyo kwa madai kuwa ni msaliti huku akienda mbele zaidi na kutaka waliompokea wachukuliwe hatua za kinidhamu kwa mujibu wa kanuni za chama.

"Ni lazima tujiulize, hivi mwanadiplomasia huyo angekuwa tayari kurejea CCM kama mgombea urais wa UKAWA, Edward Lowassa angeshinda urais?" alihoji na kuongeza:

"Hatuwezi kumpokea msaliti  kama  huyu, wakati chama kilipokuwa kwenye mapambano aliondoka tena kwa kejeli, leo chama chetu kimesimama imara chini ya mwenyekiti wetu Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ndio anarudi na wimbo uleule kwamba chama kimemlea, haikubaliki."

Alisema wakati wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,baadhi ya makada maarufu wa CCM walikisaliti chama huku wakitoa kauli za kejeli na kusababisha mpasuko ndani ya chama ambao majeraha yake hayajapona.

Mwenyekiti huyo alieleza kukerwa na kauli  ya Balozi Mwapachu kwamba chama ndo kimemlea na kwamba hayo si maradhi ya kumuua mtu bali yanatibika, lakini dhambi ya usaliti haitibiki

"Nguvu kubwa iliyotumiwa na CCM kuwanadi wagombea wake ilisababishwa na wasaliti kama hawa,nawaomba viongozi wa ngazi za juu kutofumbia macho jambo hili kwani ni hatari kwa ustawi wa chama chetu." Alisema

Balozi Mwapachu alirejea CCM juzi na kupokelwa na mwenyekiti wa CCM kata ya Mikocheni jijini Dar es Salaam, Athuman Mareenda, ambaye alimkabidhi tena kadi ya uanachama wa chama hicho.

Waziri Kitwanga Asema Wabunge Wataendelea Kukamatwa Kama Hawatafuata Sheria za Nchi.

$
0
0

Wakati Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, akidai wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wanakamatwa bila sababu za msingi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, amesema hakuna mtu anayekamatwa bila sababu na kwamba yeyote atakayebainika kufanya kosa, atasweka ndani bila kujali chama chake.

Machi Mosi, mwaka huu, Mbowe aliwaeleza waandishi wa habari kwamba wabunge na madiwani kutoka Ukawa, wanadhalilishwa na kunyanyaswa kila kona nchini na kwamba hizo ni juhudi za kurudisha nyuma maendeleo ya kazi za viongozi hao.

Hivi karibuni, Waziri Kitwanga alisema kuwa wananchi watambue kwamba askari polisi ni rafiki wa raia mwema, hivyo hawawezi kumkamata mtu asiyetenda kosa.

“Nitamshangaa askari polisi, mtu anatenda kosa pale wasimkamate eti kwa sababu tu ni mbunge wa upinzani. Awe wa CCM, awe wa upinzani watakamatwa, mimi nimeshawaeleza.

“Nimeshawaeleza wazi kabisa, mimi nitasimamia haki tu, tofauti na hapo hapana, wewe ungeona yule mama alivyopigwa na wabunge(Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando) inaumiza sana. Nilichukia sana lakini hata sikuwasemesha polisi, nilikaa kimiya tu niwaone watafanyaje.

“Niliamua kuwapima, ‘infact’ (kwa kweli) hawa watu hata dhamana wasingewapa kwa kitendo hicho,” alisema Kitwanga.

Mwanamke Aliyeoa Wanaume wawili Afariki Dunia

$
0
0

MKAZI wa Kijiji cha Ikondamoyo, Wilaya ya Mlele mkoani Katavi, Veronica Salehe (54), aliyeoa wanaume wawili kwa kipindi cha miaka tisa amefariki dunia.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ikondamoyo, John Maganga, alisema Veronica alifariki dunia wiki iliyopita mkoani Tabora alikokuwa amekwenda  kupatiwa matibabu kwa kaka yake.

Maganga alisema kuwa ndoa hiyo iliwezeshwa na mume mkubwa ambaye alikubali kuishi na mume mdogo.

Alisema kuwa Veronica ndiye aliyewaoa wanaume wote wawili na kuishi nao kwa miaka tisa, na kwamba ndiye aliyekuwa na amri kuu katika nyumba yao.

Aliwataja wanaume hao kuwa ni Paulo Sabuni (62) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (47).

Maganga alisema Veronica na mume wake mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita wakitokea Kijiji cha Usumbwa, mpakani mwa Chunya na Tabora.

“Baada ya kufika kijijini hapa, walianza kujishughulisha na shughuli za kilimo na biashara ya kuuza pombe za kienyeji aina ya komoni,” alisema Maganga.

Katika uhai wake, Veronica alibahatika kupata watoto wanne, kati yao wawili wa kike.

Maganga alisema mtoto mdogo wa kiume, ni wa mume mdogo ambaye ana miaka tisa, anayesoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Ikondamoyo, na watoto wengine watatu ni wa mume mkubwa.

Kuhusu maisha ya Veronica ya kuishi na wanaume wawili, Maganga alisema haikuwa siri kijijini hapo kwa sababu walizoeleka kwa wanakijiji.

Alisema mume mdogo alikuwa anaishi kwenye nyumba aliyoachiwa na marehemu baba yake, lakini alikuwa akishinda kwa mume mkubwa ambako kulijulikana zaidi kwa jina la ‘nyumba kubwa’.

“Mambo ya kula, kunywa na mengine, mama   alikuwa akiwapangia zamu kama afanyavyo mume mwenye wake wengi,” alisema Maganga na kuongeza kuwa wanaume hao walikuwa wanaridhika na kufurahia maisha.

Alisema siku mama akichoka kupika, mume mdogo alikuwa akiingia jikoni na kuwaandalia chakula watoto na mume mkubwa maji ya kuoga.

Wakati wa mazishi, wanaume wote walishiriki shughuli zote, jambo ambalo limeacha maswali mengi kwa jamii.

Akizungumzia msiba huo, mume mkubwa alisema kuwa amepata pigo kubwa kwa sababu alikuwa anasaidiwa mno na marehemu Veronica kutokana na biashara zake za pombe za kienyeji ambazo zilisaidia kuendesha maisha ya kila siku.

“Veronica aliugua muda wa miezi miwili, nilikuwa namplekea Kituo cha Afya Urwila kupata matibabu, lakini Mungu kampenda zaidi,” alisema.

Kamati ya Bunge Yaipa Siku 7 Wizara ya Afya Ieleze Kwa nini Watumishi wa Hospitali ya Butimba Walisimamishwa Bila Kufuata Utaratibu

$
0
0
Kamati ya bunge ya huduma za jamii imeitaka Wizara ya Afya ijieleze ndani ya siku saba kwanini aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, aliwasimamisha watumishi wa Afya wa hospitali ya Butimba bila kufuata hatua stahili.

Mapema mwezi huu, Magesa Mulongo aliwasimamisha kazi madaktari 3, manesi 6, na wafanyakazi wengine 2 wa hospitali ya Butimba kwa madai mbalimbali, yakihusisha kifo cha watoto mapacha. Lakini Mulongo alijitetea maamuzi yake kuwasimamisha, akisema ilitokana na tendo walilofanya kutoendana na sheria za kazi.

Mwenyekiti wa kamati Raphael Chegeni, alisema kamati iligundua kwamba kulikuwa na matumizi mabaya ya madaraka katika maamuzi ya mkuu wa mkoa. Na kwamba mkuu wa mkoa hakuomba taarifa ya utenda kazi ili kutambua matatizo ya hospitali.

Mmoja wa wanakamati Mhe. Zitto Kabwe ndiye aliuliza ni kitu gani hasa kilichosababisha mkuu wa mkoa kusimamisha watumishi hao, kwani kuna wagonjwa wengi wanaofariki katika hospitali husika kwa kukosa tiba na wengine wakiwa na shida mbalimbali.

Raphael Chegeni alisema mkuu wa mkoa hakufuata kanuni, zinazohitaji watumishi wa afya kusimamishwa na mabaraza yao.

"Kamati imejiridhisha kwamba mkuu wa mkoa aliwasimamisha wafanyakazi hawa wa afya kwa kutumia nguvu ya kisiasa" alisema Raphael Chegeni. Pia alionya wanasiasa, kuchanganya siasa na utoaji wa huduma za afya, hususani maeneo ya vijijini, kwani mwisho wa siku itawaamiza wakaazi wa vijijini.

Akichangia, mbunge wa viti maalumu, Mhe. Suzan Lyimo alisema viongozi wa serikali wanapaswa kutambua mchango wa watumishi wa afya wanaofanya kazi kubwa kuokoa maisha.

Kamati pia ilishauri wizara kuboresha mazingira ya kazi ya wafanyakazi wa afya, ikiwa ni pamoja na kuboresha mishahara na marupurupu.

Waziri Mkuu kuwa mgeni rasmi harambee ya shule ya Sekondari ya Iyunga

$
0
0
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika harambee itakafanyika kesho katika ukumbi wa Ubungo Plaza kwa ajili ya kuchangia fedha zitakazowezesha kukarabati mabweni manne ya shule ya Sekondari ya Ufundi ya Iyunga yaliyoungua hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Nyerembe Munasa Sabi amesema kuwa wameamua kuomba nguvu kutoka kwa wadau wa elimu na watanzania kwa ujumla kujumuika katika kuchangia shule ya sekondari ya ufundi Iyunga ili waweze kukarabati mabweni yaliyoungua kwa moto.

“ Hadi sasa takribani wanafunzi 421 hawana mahala pa kulala kutokana na kuteketea kwa mabweni na kwa kushirikiana na TAMISEMI tumeamua kusitiza masomo kuanzia tarehe11 March hadi tarehe 01 Aprili ili kupisha ukarabati wa mabweni”

“ Tumeanza ujenzi wa baadhi ya miundombinu iliyoteketea na mabweni ikiwa ni jitihada za wadau mbalimbali waliochangia kutoka Mbeya na nawasihi wanambeya wale waliosoma shule ya Iyunga na shule za Mbeya na watanzania kwa ujumla kujitokeza kesho katika harambee hii” Alisema

Mhe. Nyerembe Munasa Sabi aneongeza kuwa wamepokea michango mbalimbli kutoka kwa wadau wakiwemo Mbeya Cement waliotoa mifuko 1,000 ya saruji kwa ajili ya ujenzi na kwa sasa mahitaji yaliyopo ni takribani Shillingi million 770 ili kukarabati na kujenga majengo mapya kwa ajili ya shule hiyo.

Shule ya Sekondari ya  Ufundi Iyunga yenye wanafunzi takribani 9970 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita imekumbwa na majanga ya moto ambayo yamesababisha athari kwa  watoto kutoendelea na masomo na uharibifu wa miundombinu ila Serikali kupitia TAMISEMI na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya wamejipanga kukusanya  fedha kwa ajili ya ukarabati mkubwa wa shule hiyo.

Rais Magufuli Akabidhi Gari La Kubebea Wagonjwa Hospitali Ya Wilaya Ya Chalinze

$
0
0
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amekabidhi  gari la kubebea wagonjwa kwa hosipitali ya wilaya ya Chalinze, Ikiwa ni utekelezaji wa ilani na  ahadi ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwa wananchi ikiwa ni pamoja na wa jimbo la Chalinze.

Gari hilo la kubebea wagonjwa limekabidhiwa kwa niaba ya Rais, na Katibu Mkuu Ikulu Peter Ilomo kwa  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi gari hilo, Katibu Mkuu Ikulu Ndugu Peter Ilomo amesema gari hilo limetolewa na Mheshimiwa Rais kwa hosipitali hiyo ikiwa ni kuitikia wito na utekelezaji wa ilani na ahadi ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya kuboresha huduma ya afya kwa wananchi wake kote nchini.

Aidha, Ndugu Ilomo amewaomba viongozi wa jimbo la Chalinze kulitumia gari hilo kwa matumizi yaliyokusudiwa ya kuwahudumia wananchi wa eneo hilo.

Akipokea gari hilo kwa niaba ya wananchi wa jimbo na  Wilaya ya Chalinze, Mbunge wa jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amemshukuru Mheshimiwa Rais    Dkt. John Pombe Magufuli kwa msaada huo na kuahidi kulitumia gari hilo kwa malengo yaliyokusudiwa, na kusema kuwa, utendaji kazi wa Rais Magufuli umekuwa ukiungwa mkono na wananchi wa kada mbalimbali na kuwaomba watanzania kuzidi kumuombea kwa Mungu.

Kwa upande wake Dakta Nasoro Ally Matuzya, amesema gari hilo limekuja kwa wakati muafaka kwa kuwa umezingatia utekelezaji wa malengo ya Milenia hususan lengo namba nne  linalosisitiza kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano

Naye Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Chalinze Ndugu Saidi Omar Zikatimu amesema gari hilo la kubebea wagonjwa litakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa jimbo hilo la Chalinze hususan katika kusaidia kutoa wagonjwa ambao wako katika maeneo ya vijijini wilayani humo na kuwafikisha katika hospitali ya Chalinze na hivyo kunusuru maisha yao kwa kupata huduma za afya kwa haraka.

Mbali na Wilaya ya Chalinze kupata msaada wa gari hilo la kubebea wagonjwa, tayari magari mengine mawili ya kubebea wagonjwa yameshakabidhiwa katika vituo vya afya vya Kiroka na Kisemu mkoani Morogoro.

Hospitali mpya ya Wilaya ya Chalinze imepanda hadhi kutoka kituo cha Msoga ambayo ilikuwa haina gari la kubebea wagonjwa na hivyo kufanya usafirishaji wa wagonjwa kutoka hospitali hiyo hadi hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Pwani ya Tumbi au kutoka maeneo ya vijijini kuwa mgumu.

Imetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu

18 Machi 2016.

Uchaguzi Zanzibar: Chama cha CUF kimewataka wanachama na wananchi wote kukaa ndani siku ya upigaji kura katika Uchaguzi wa Marudio

$
0
0
Siku ya Jumapili, tarehe 20 Machi 2016, Zanzibar itashuhudia, kwa mara nyingine tena, ubakwaji wa demokrasia kwa kufanyika kile kinachoitwa Uchaguzi wa Marudio’ kufuatia tamko binafsi la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, alilolitoa tarehe 28/10/2015 kwamba ameufuta Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25/10/2015 na matokeo yake yote.

Tangazo hilo la Jecha Salim Jecha, lililo kinyume na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam. 11 ya 1984 na linalopingana na Katiba ya Zanzibar, lilikuja baada ya waangalizi wote wa Uchaguzi wa ndani na wa kimataifa ikiwa ni pamoja na Umoja wa Ulaya (EU), Jumuiya ya Madola (The Common Wealth), Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na Waangalizi wa Marekani na Uingereza, kutoa taarifa zao na kueleza kuridhishwa na mwenendo wa Uchaguzi huo na kwamba ulikuwa huru na wa haki kwa sababu ulifuata taratibu za kisheria na ulifanyika kwa amani.
 
Aidha, baada ya kukamilika kwa hatua ya upigaji kura, wadau na washiriki wa ndani wa uchaguzi huo akiwemo, yeye mwenyewe, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Dk. Ali Mohamed Shein, mgombea wa Urais wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na wagombea kutoka vyama vyengine walikiri kwamba uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.
 
Ghafla, kutokana na shindikizo kubwa kutoka kwa viongozi wa Chama chake, ambacho aliwahi kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge kupitia chama hicho na kuanguka katika hatua ya kura za maoni, Mwenyekiti wa Tume alitangaza kuufuta Uchaguzi huo kwa kutumia hoja na maelezo yaliyotolewa na CCM baada ya kubaini imeshindwa kwenye nafasi ya Urais wa Zanzibar.
 
Tokea kutolewa kwa tangazo hilo kumekuwepo na juhudi mbalimbali ndani na nje ya nchi za kutafuta suluhisho kutokana na mgogoro ulioibuliwa kwa makusudi kwa lengo la kukinusuru Chama Cha Mapinduzi CCM kuondokana na aibu ya kushindwa katika Uchaguzi Mkuu wa 25 Oktoba 2015.
 
Miongoni mwa juhudi za ndani ni pamoja na Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kukutana na viongozi mbalimbali akiwemo mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dr. Ali Mohamed Shein, Marais wastaafu wa Zanzibar, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli na Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete ili kufanya mazungumzo na kuiepusha nchi kutokana na migogoro na mifarakano ya baada ya uchaguzi. Viongozi wa dini mbalimbali nao pia walichukua dhamana na dhima ya kuhakikisha kuwa mgogoro wa Zanzibar unapatiwa ufumbuzi kwa lengo la kuibakisha Zanzibar katika hali ya umoja na masikilizano miongoni mwa wananchi wake.
 
Kwa upande wa juhudi za nje, jumuiya ya kimataifa imesikika mara kadhaa ikitoa matamko na kuchukua hatua mbalimbali kuitaka Tume ya Uchaguzi kukamilisha kazi ya uhakiki na majumuisho ya matokeo ya uchaguzi na kumtangaza mshindi. 
 
Jumuiya hiyo pia iliushauri uongozi wa vyama vya CCM na CUF kukaa pamoja kuzungumza jinsi ya uundwaji na uendeshaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar kama yalivyo matakwa ya Katiba ya Zanzibar na kuhakikisha kuwa demokrasia, haki za binadamu na amani vinaenziwa, kulindwa na kutunzwa. 

Kwa makusudi na kwa lengo maalum, hatua zote hizo zimepuuzwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na Serikali zote mbili, na hatimaye Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar alitangaza kufanyika kwa kile kinachoitwa Uchaguzi wa Marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi 2016.
 
Kupuuzwa huko kwa juhudi za ndani na nje, kunakochochewa na baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM na Serikali zote mbili, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi) lililokutana katika kikao cha dharura tarehe 07 Novemba, 2015, mjini Zanzibar kuzungumzia hali ya kisiasa hapa nchini kufuatia Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 lilifikia maamuzi ya kuitaka Tume ya Uchaguzi, pamoja na mambo mengine, irudi kukamilisha hatua zilizobaki za uhakiki na majumuisho ya matokeo ya Uchaguzi. 
 
Kimsingi, Baraza Kuu lilisisitiza halitakubaliana, kwa namna yoyote ile, na hatua ya kufanya Uchaguzi wa marudio kwa kuzingatia kukosekana kwa uhalali wa kisheria katika ufutwaji wa matokeo ya Uchaguzi na kwamba uchaguzi ulishafanyika na kazi ya kuhesabu kura kumalizika.
 
Tokea kutolewa kwa tamko la kufutwa kwa Uchaguzi, kutangazwa kwa Uchaguzi wa marudio, na kutolewa kwa Azimio la Baraza Kuu la Uongozi la CUF, Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejikuta katika taharuki na wasiwasi mkubwa na kupelekea khofu isiyomithilika kuhusiana na hali ya kisiasa na kiusalama ya Zanzibar. 

Kwa mfano, kumeripotiwa matukio mengi ya uvunjwaji wa haki za binadamu ambapo raia wasio na hatia wanapigwa na kujeruhiwa vibaya, nyumba na makaazi ya watu kuvunjwa na kuchomwa moto, maeneo ya vyama vya siasa, kama vile barza za CUF, yamehujumiwa kwa kuchomwa moto na ofisi zake kuvunjwa na kuibiwa mali zote kabla ya kuwashwa moto na kuteketea kabisa. 
 
Kwa mfano, siku ya Jumatatu, tarehe 15, Machi 2016, makundi ya askari wakiwa na silaha za moto walivamia ofisi ya Chama Cha Wananchi CUF iliyopo katika eneo la Mpendae na kuvunja na kuiba vifaa mbalimbali vya ofisi hiyo zikiwemo kompyuta, printers na photocopy machines.
 
Katika tukio hilo, maharamia hao walivunja eneo linalotumika kuhifadhia vifaa vya muziki na kuiba vifaa vyote vya BRASS BAND ya CUF. 
 
Mengi ya matukio haya yamefanywa na kikundi kidogo cha askari wa vikosi vya SMZ, ambacho hutumia magari yenye namba za usajili za SMZ na silaha za moto na kujifunika nyuso zao kwa staili ya ninja kilichoandaliwa maalum kwa ajili ya kuwahujumu raia, wakisaidiwa na vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Sambamba na hujuma hizi kumeibuka mtindo wa kuwatisha raia kwa kuwavamia kuwapiga na kuwabambikizia kesi kwa lengo la kuwashikilia katika vituo vya Polisi, kinyume na utaratibu wa kisheria, na kuwadhalilisha kwa kuwapiga na kuwatolea maneno ya vitisho na matusi.
 
Katika uvamizi uliofanywa katika ofisi ya CUF ya Mpendae, zaidi ya vijana 30 walikamatwa na jeshi la Polisi, lililoshiriki katika uhalifu huo kwa lengo la kuwapatia ulinzi maharamia waliopewa kazi ya kuhujumu ofisi hiyo, na kuwarundika katika vituo vya Polisi na kuwanyima dhamana.
 
Mkakati wa kuwatisha raia ulielekezwa pia kwa viongozi wa CUF. Tarehe 16 Machi 2016, Jeshi la Polisi lilivamia nyumbani kwake na kumkamata Kaimu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma, Mheshimiwa Hamad Masoud na kumuweka ndani na kumnyima dhamana. 
 
Tukio hili la kukamatwa Mheshimiwa Hamad Masoud linafuatia kuwekwa ndani na kunyimwa dhamana kwa aliyekuwa mjumbe wa Timu ya Kampeni inayojulikana kama Timu ya Ushindi ya Chama Cha Wananchi (CUF) ndugu Mohamed Ahmed Sultan Al-Mugheir (Eddy Riyami) tarehe 16, Februari 2016 na kuitwa Polisi Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui tarehe 3 Machi, 2016 kwa kuwataka wanachi wajilinde kutokana na kushamiri kwa vitendo vya hujuma dhidi ya wafuasi wa vyama vya upinzani vinavyofanywa na makundi tuliyoyataja. 
 
Vilevile, jana tarehe 17 Machi, 2016 aliyekuwa Mjumbe katika Timu ya Ushindi ya CUF na Mgombea Uwakilishi wa jimbo la Chukwani, Mheshimiwa Mansour Yussuf Himid, aliitwa na Jeshi la Polisi kwa madhumuni ya kuhojiwa.
 
Sambamba na haya, kumekuwepo na juhudi kubwa zinazoongozwa na Mamlaka mbalimbali ikiwemo Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuvishurutisha vyama vya siasa, hasa vile vilivyotangaza waziwazi kugomea Uchaguzi wa marudio, kushiriki katika uchaguzi huo kwa lengo la kuhalalisha mkakati ulioandaliwa wa kulazimisha ushindi wa CCM ambao waliukosa katika uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba, 2015.
 
Kwa mfano, tarehe 25 Januari, 2016, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar iliwasilisha Makao Makuu ya CUF barua yenye kumbukumbu TUZ/78/16/2015/2016/Vol.I/2 kwa lengo la kutoa taarifa kuhusu uchaguzi wa marudio.
 
Kutokana na barua hii, CUF, kupitia Naibu Katibu Mkuu, Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui, iliiandikia Tume barua yenye kumbukumbu namba CUF/HQ/AKM/ZEC/037/016/055 ya tarehe 05/02/2016 kujibu barua ya Tume ya tarehe 4 August, 2015 yenye kumbukumbu TUZ/78/2015/2016/VOL.VI/68 na barua ya kukumbushia barua yake ya tarehe 17, August, 2015 yenye kumbukumbu CUF/HQ/AKM/ZEC/037/015/032.
 
Kwa barua yake ya tarehe 5 Februari, 2016 CUF iliitaarifu Tume ya Uchaguzi juu ya maazimio ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kutoshiriki katika Uchaguzi ambao umetangazwa kufanyika tarehe 20/03/2016 kwa sababu kufutwa kwa uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba, 2015 ni batili na kwa hivyo marudio ya uchaguzi wa tarehe 20 Machi 2016 ni batili pia, na ni kinyume na Katiba ya Zanzibar na Sheria ya Uchaguzi ya 1984.
 
Aidha, kwa barua hiyo, CUF iliitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar, kutokana na Azimio la Baraza Kuu la Uongozi, kuondoa majina ya wagombea wake wote, akiwemo Maalim Seif Sharif Hamad, katika orodha ya wagombea wa Uchaguzi huo na vile vile yasiingizwe katika karatasi za kura kwa uchaguzi wa marudio.
 
Zaidi, tarehe 8 Februari, 2016 Naibu Katibu Mkuu wa CUF aliwasilisha barua, kwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, iliyokuwa na lengo la kuelezea msimamo wa CUF kuhusiana na kufutwa isivyo halali kwa uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba 2015 na kuitishwa kwa kile kinachoitwa uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 Machi, 2016.
 
Kwa barua hiyo pia, CUF ilibainisha mapungufu ya kisheria na ukiukwaji wa Katiba ya Zanzibar katika tangazo la kufutwa kwa uchaguzi na kwa hivyo kutothibitisha mgombea yoyote katika ngazi zote za uchaguzi wa zanzibar kama ilivyotakiwa kufanya na Tume ya Uchaguzi. 
 
CUF iliikumbusha Tume na kusisitiza juu ya uamuzi wake wa kuitaka tume kuhakikisha haitumii jina, alama, wala picha ya mgombea yoyote kupitia CUF katika karatasi za kura.
 
Hata baada ya rundo la barua hizi za CUF, zenye lugha rahisi na maelezo yanayojitosheleza, kwa Tume ya Uchaguzi kukataa kushiriki katika batili iliyopachikwa jina la uchaguzi wa marudio, tarehe 29 Februari 2016, Tume ya Uchaguzi, kwa mara nyingine tena, iliiandikia CUF barua yenye kumbukumbu namba TUZ/78/16/015/016/VOL. I/200 kuitaka CUF kuwasilisha majina ya mawakala wake katika uchaguzi ambao kimsingi walishautolea msimamo.
 
CUF kwa upande wake ilimwandikia Mkurugenzi wa uchaguzi barua yenye kumbukumbu CUF/HQ/AKM/ZEC/037/016/056 ya tarehe 03 Machi 2016 kukumbushia msimamo wake wa kutoshiriki Uchaguzi huo na kwamba kutokana na uchaguzi huo kukosa uhalali kisheria na kikatiba, haioni haja ya kuwasilisha majina ya waangalizi kwa uchaguzi huo.
 
Kwa mara nyingine tena, tarehe 8 Machi 2016, Tume iliiandikia CUF barua yenye kumbukumbu TUZ/78/16/2015/2016/VOL.II/6 kutoa taarifa kuhusu kuwasili kwa karatasi za kupigia kura kwa ajili ya Uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 Machi 2016 na kuitaka CUF kutuma majina mawili ya watakaoshiriki katika mapokezi ya karatasi hizo. 

Bila ya shaka, Tume imo katika mpango wa kuilazimisha na kuishurutisha CUF, hata kama haitaki, kushiriki katika uchaguzi huo kama inavyothibika katika hatua mbalimbali za Tume hiyo ikiwa ni pamoja na kuchapicha majina, nembo na picha za wagombea wa CUF katika karatasi za kura kwa ajili ya uchaguzi wa marudio hata baada ya CUF kukataa kushiriki katika uchaguzi huo
 
Tukiwa tunakaribia siku ya Uchaguzi wa marudio, CUF imebaini njama kadhaa mpya zinazoratibiwa na baadhi ya viongozi wa CCM na kutekelezwa na baadhi ya watendaji wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar. 
 
Miongoni mwa mbinu hizo ni pamoja na kutoa vitisho kwa wafanyakazi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na askari wa vikosi vya Idara Maalum ya Zanzibar na askari wa majeshi yaliyo chini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Polisi na Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopo Zanzibar, ya kuhakikisha wanajitokeza kwa lazima katika uchaguzi wa marudio na kuipigia kura CCM.
 
Pia, kumekuwepo na mpango wa kuandaliwa kwa mawakala ‘feki’. Katika hili Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar inashirikiana kwa karibu na kwa kiasi kikubwa na baadhi ya watendaji wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, wakiwemo viongozi wa vikosi vya idara maalum, kuandaa watu, ambao wengi wao ni askari wa vikosi hivyo, watakaopewa vitambulisho vinavyowaonesha kuwa ni mawakala wa CUF, na kutumia majina ya mawakala wa CUF wa 25 Oktoba 2015, na kusambazwa katika maeneo yote ya Uchaguzi nchi nzima.
 
Lengo la mpango huu ni kutaka kuwahadaa wanachi kuwa CUF ilishiriki Uchaguzi kwa kuwa ilitoa mawakala walioshiriki katika Uchaguzi. 
 
Pia, mpango huu unalenga katika kuzusha hali ya kutofautiana miongoni mwa uongozi wa CUF na wanachama wa kawaida ili ionekane uongozi wa juu wa CUF umewasaliti wananchi katika dakika za mwisho kuelekea uchaguzi wa marudio.
 
Kwa upande mwengine, CCM yenyewe imekuwa inaongoza mkakati maalum wa kuwatafuta baadhi ya waliokuwa mawakala wa CUF katika uchaguzi wa terehe 25 Oktoba 2015, na kuwapa fedha nyingi ili wakubali kuwa mawakala wa CUF katika uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 Machi 2016. 
 
Ili kuhakikisha lengo la kuwatumia mawakala hao kufanikisha mchezo wao mchafu waliouanza mara tu baada ya kufutwa kwa uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba, 2015, CCM imekuwa ikiwazaini mawakala hao wa CUF kwa ahadi mbalimbali za fedha na vitu vya thamani.
 
Kutokana na hayo yote tuliyoyaeleza kwa kina, CUF-Chama Cha Wananchi:
 
• Kinatoa wito kwa wananchi wote kufuata kwa umakini na ukamilifu maelekezo na kauli za viongozi wazalendo, wanaoitakia mema nchi hii kwa kuchukua juhudi kubwa kuinusuru na mifarakano ya aina zote, kususia kile kinachoitwa uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili, tarehe 20 Machi, 2016 kwa kukaa majumbani mwao kwa utulivu na kujiepusha na mikusanyiko isiyo ya lazima ili kujikinga na dhamira na matendo maovu ya kiharamia yaliyopangwa na kikundi cha wahuni wachache wa kisiasa dhidi ya raia wasio na hatia.
 
• Kinawafahamisha na kuwatanabahisha wafuasi wake na wananchi wengine wote walioamua kuchagua mabadiliko ya kiuongozi katika nchi yetu katika uchaguzi uliopita kwamba haijawasilisha jina hata moja la mtu yoyote kama mapendekezo yake kwa ajili ya mawakla watakaotumika katika uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 Machi, 2016 kwa hivyo haitokuwa na wakala hata mmoja kwa ngazi yoyote katika uchaguzi wa tarehe 20 Machi, 2016. Ni muhimu kwa wanachi kuachana na propaganda zilizopitwa na wakati zinazoenezwa na CCM kuhusu mikakati ya CUF kuelekea 20 Machi, 2016.
• Mbali na kutoshiriki uchaguzi wa marudio unaosimamiwa na ZEC, pia CUF inawataka wanachama, wafuasi wake na wananchi wote kutoshiriki katika uchaguzi wa marudio katika Jimbo la Kijitoupele unaosimamiwa na Tume ya Tiafa ya Uchaguzi (NEC). CUF inawataka wananchi kususia uchaguzi huo kwa sababu kwa Zanzibar ni ZEC ndio hufanya kazi kama wakala wa NEC, hivyo hakuna haki itakayotendeka katika uchaguzi huo.
 
• Kinawataka wananchi wote kufahamu kuwa suala la kushiriki uchaguzi ni suala la mtu binafsi na hakuna mtu au mamlaka yoyote yenye uwezo wa kulazimisha watu kushiriki katika suala hilo. Chama kinawataka wananchi kuwa watulivu na kuondoa khofu kutokana na idadi kubwa ya askari wa JWTZ na Polisi wanaoranda randa mitaani wakiwa na silaha nzito. CUF inawaomba wananchi kubaki na msimamo wao wa kutoshiriki uchaguzi.
 
• Kinawasihi wale wote waliotishwa kwa kunyang’anywa vitambulisho vyao vya Mzanzibari na vitambulisho vya kupigia kura, kutotishika na hatua zinazochukuliwa sasa na watendaji waandamizi wa SMZ na mawakala wao kwa kukataa dhulma na kutumiliwa nguvu katika mambo yaliyo chini ya khiari zao. Pia, CUF inawasihi wananchi hao kuonesha msimamo wao katika kulinda na kutetea haki zao za kikatiba na kuonesha mapenzi yao kwa nchi yao kwa kukataa ukiukwaji wa Katiba na uvunjwaji wa Sheria za nchi yetu kwa kushiriki katika ukandamizaji na uvizwaji wa demokrasia nchini.
 
• Kinawakumbusha askari wa vikosi vyote, walio na uchungu na mapenzi mema na nchi yetu, kukataa kutumiwa na wanasiasa walioweka mbele maslahi yao binafsi na kuusahau umma wa wananchi wanyonge wa nchi hii.

 Ni vyema kwa askari hawa kutambua kuwa wao ni sehemu ya jamii yetu na kwamba shida na maisha magumu tuliyonayo yanawahusu na kuwakumba kama raia wengine wote. Kukataa kwao kuwa ngazi ya viongozi wanaotafuta hadhi na heshima kwa kupitia migongo ya wengine kutawatoa wao katika idhilali ya kutumika kila nyakati za uchaguzi zinapowadia na kutelekezwa hadi kipindi kama hicho baada ya miaka mitano ambapo hutafutwa na kupewa tena ahadi kemkem zisizotekelezwa.
 
• Kinamnasihi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Magufuli kutambua kuwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), lililo chini ya amri yake kama Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, linaendesha vitisho kwa wananchi kutokana na kuonekana kwa wingi wakiwa na silaha nzito katika maeneo ya wananchi. 

CUF inamtaka Mheshimiwa Magufuli kuondosha majeshi yake yanayoshirikiana na Polisi na vikosi vya SMZ kuendesha unyanyasaji na udhalilishaji wa raia wasio na hatia.
 
CUF-Chama cha Wananchi kinawataka wanachama, wafuasi wake na wananchi wote waliochagua mabadiliko ya uongozi wa kisiasa katika nchi yetu na kuonesha msimamo wao wa kuikataa CCM kupitia sanduku la kura tarehe 25 Oktoba, 2015 kutovunjika moyo na siasa uchwara zinazoendeshwa na CCM kwa lengo la kuwatoa katika mstari wa kupigania ushindi wetu mkubwa tulioupata. 

Tunawahakikishia kuwa subra zao na jitihada kubwa inayochukuliwa na Viongozi wa Chama Chetu vitachochea kufikiwa kwa malengo yetu na maamuzi yao ya kuchagua mabadiliko yatazingatiwa na kuheshimiwa.
 
NASSOR AHMED MAZRUI
NAIBU KATIBU MKUU-CUF ZANZIBAR

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda Atangaza Zawadi ya Milioni 1 Kwa Askari Polisi Atakayepambana na Jambazi na Kulishinda

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amekutana na Kamanda wa Polisi kanda maalum Simon Sirro pamoja na Askari Polisi kwa lengo la kujionea mwenendo wa jeshi hilo ambapo wamekubaliana kutoa zawadi ya milioni moja kila baada ya miezi mitatu kwa kila Askari Polisi aliyepambana na majambazi.

"Askari wetu wanafanya kazi katika mzangira magumu na wanachangamoto kubwa. Nmeona nitengeneze mfumo wa kuwapa motisha, kwahiyo nimeongea na Kamanda Sirro nimemuambia kuwa kila askari atakayeonekana amefanya vizuri mimi kama mkuu wa mkoa nitakuwa na zawadi ya milioni moja kwake kama motisha.
 
"Kuna watu wengi wana silaha halali na  wengine wanamiliki isivyo halali, kwahiyo tumekubaliana kuanzia leo hadi tarehe 1 aprili 2016 tunawaomba wana Dar es salaam wote waende kwenye ofisi za polisi kutoa taarifa za uhalali wa silaha zao.

"Tunataka kujihakikishia tunazo silaha ngapi katika mkoa wetu maana kuna wengine wanazitumia kinyume cha taratibu.

"Sasa olewako tukukute unamiliki silaha, tunahitaji kuliona jiji letu la Dar es salaam linaongoza kwa amani, hatutaki kuona majambazi wakipora kwenye mabenki wala kuwapora watu kwa silaha." Amesema RC Paul Makonda

Taarifa ya Habari Ya Channel TEN March 18, 2016

$
0
0

Taarifa  ya  Habari  Ya  Channel TEN  March 18, 2016

Maofisa Uhamiaji wa Mikoa 14 Wahamishwa.....Wengine Zaidi ya 200 Kuhamishwa Pia

$
0
0

Idara ya Uhamiaji nchini imefanya mabadiliko ya maofisa waandamizi kwa kuwahamisha vituo vya kazi kuanzia ofisi ya makao makuu, mikoa, wilaya na mpakani.

Pangapangua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga alilolitoa kwenye kikao chake na viongozi wakuu wa idara hiyo kilichofanyika Februari 23.

Siku hiyo, Waziri Kitwanga aliagiza kufanyika kwa mabadiliko hayo kutokana na kukithiri kwa vitendo vya upitishaji dawa za kulevya na wanyama hai kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na Kilimanjaro (KIA) na kwenye mpaka wa Tunduma, Mtukula, Halolili na Kasumulo.

Pia, aliagiza kuhamishwa kwa wakuu wa upelelezi wote wa wilaya za Dar es Salaam na maofisa wa uhamiaji waliokaa kwenye kituo kimoja kwa zaidi ya miaka mitatu, huku akisema huo ni mwanzo wa mabadiliko makubwa kwenye idara hiyo.

Akitangaza mabadiliko hayo jana, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abbas Irovya (pichani), alisema upanguaji huo unalenga kuimarisha utendaji, ufanisi na dira katika idara hiyo.

“Pamoja na orodha hii ya maofisa waandamizi wanaohama vituo vyao vya sasa kwenda vituo vingine, Idara ya Uhamiaji inaendelea na utaratibu wa kuwabadilisha vituo vya kazi maofisa zaidi ya 200 kutoka sehemu mbalimbali nchini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga,” alisema.

Irovya, ambaye alitangaza mabadiliko hayo kwa niaba ya Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, alisema amewahamisha Ofisa Uhamiaji, Faustine Nyaki, aliyekuwa mkoani Iringa, kwenda Mwanza kuwa ofisa uhamiaji wa mkoa.

Wengine waliohamishwa ni Remigius Pesambili (Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza), anayekwenda kuwa mfawidhi wa ofisi ya Uhamiaji ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Rose Mhagama (Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Geita) anayehamia Njombe.

Assa Mwansansu aliyekuwa Mfawidhi wa Kitengo cha Hati za Ukazi, anahamia Pwani kuwa ofisa uhamiaji wa mkoa, Safina Muhindu (Ofisa Uhamiaji wa Wilaya ya Ilala), anahamia Morogoro kuwa ofisa wa mkoa na Wilfred Marwa (Naibu Ofi sa Uhamiaji wa Tanga), anayehamia Geita kuwa ofisa uhamiaji wa mkoa.

Alisema Evarist Mlay (aliyekuwa Ofisa Uhamiaji wa Wilaya ya Kinondoni) anahamia Wilaya ya Same, wakati Frank Mwakifuna (aliyekuwa Ofisa Uhamiaji Same), anahamia Kinondoni, huku Pilly Mdanku (ofisa wa hati za kusafiria wa Makao Makuu), anakuwa Ofisa Uhamiaji wa Wilaya ya Ilala na George Goda (kitengo cha Hati za Ukazi Makao Makuu) anahamia Temeke kuwa ofisa uhamiaji wa wilaya.

Mwingine aliyehamishwa ni jafari Kisesa, ambaye alikuwa ofisa Uhamiaji wa Wilaya ya Temeke, anahamia Tanga kuwa naibu ofisa wa uhamiaji wa mkoa.

Pia, Julieth Sagamiko (Kitengo cha Hati za Kusafiria cha Makao Makuu) amehamishiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kuwa mfawidhi wa kituo na nafasi yake itashikwa na Fredrick Eustace Kiondo, huku Naibu Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Kagera, Hosea Kagimbo akihamishiwa Holili kuwa mfawidhi wa kituo.

Pia, alisema Kaimu Kamishna, Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli amewabadilisha vituo vya kazi maofisa hao 14, huku baadhi ya maofisa wakistaafu utumishi wa umma akiwamo aliyekuwa mfawidhi wa kituo cha Holili, Kaimu Kamishna, Alphonce Tishe.

Wachina Waliokutwa na Vipande 728 Vya Meno ya Tembo Wahukumiwa Kifungo cha Miaka 30 au Faini ya Bilioni 108

$
0
0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewahukumu raia wawili wa China waliokutwa na hatia ya kuua tembo 226 adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela au kulipa faini ya Sh108.7 bilioni.

Pia, imeamuru magari matatu ya washtakiwa hao yenye usajili wa namba T 317 BXG, T 777 BET na T 728 BGP pamoja na vipande 728 vya meno ya tembo walivyokutwa navyo vitaifishwe na Serikali.

Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Cyprian Mkeha alisema katika shtaka la kushawishi askari polisi na maofisa wa wanyamapori wapokee rushwa ya Sh30.2 milioni ili wasiwapekue na kuwafikisha katika mikono ya sheria, kila mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela ama kulipa faini ya Sh1 milioni.

Akiendelea kusoma hukumu hiyo, Hakimu Mkeha aliwaachia huru washtakiwa hao katika shtaka la kukutwa na ganda la risasi.

Raia hao wawili wa China, Xu Fujie na Huang Gin waliokuwa wakitetewa na mawakili, Edward Chuwa na Nehemia Nkoko, waliadhibiwa adhabu hizo baada ya Mahakama kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi tisa wa upande wa mashtaka pamoja na utetezi wao.

Hakimu Mkeha alipokuwa akisoma hukumu hiyo, alisema katika shtaka la kukutwa na vipande 706 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh5.4 bilioni bila ya kuwa na kibali, kila mshtakiwa anatakiwa alipe fidia ya Sh54.35 bilioni na kwamba, iwapo watashindwa watumikie kifungo cha miaka 30 jela. 

Akiendelea kuisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkeha alisema ametoa adhabu hizo kwa kuzingatia uzito wa maombi ya mawakili wa Serikali, Faraja Nchimbi na Paul Kadushi na maombi ya utetezi ya kutaka wapunguziwe adhabu.

“Kwa kuzingatia hali halisi ya kesi, ushahidi, hasara ambayo Taifa imeipata kutokana na Tembo hao 226 waliopoteza maisha kwa kuuawa na washtakiwa ni wazi washtakiwa walitishia maisha ya vizazi vya tembo waliomo ndani ya mipaka ya nchi yetu,” alisema Hakimu Mkeha.

Alisema ameridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka kwa kuwa umethibitishwa pasipo kuacha shaka yoyote.

Kwa upande wa Mawakili wa Serikali, Nchimbi aliiomba Mahakama iwape adhabu kali washtakiwa hao kwa kuwa kati ya kipindi cha 2010 na Desemba 2013, jumla ya tembo 892 waliuawa nchini.

Alisema washtakiwa hao waliingia nchini 2010 hadi Novemba 2013 walipokamatwa kwa makosa hayo na kuwapo kwao rumande, matukio ya mauaji ya tembo yalipungua.

Nchimbi alibainisha kuwa washtakiwa hao waliua robo ya tembo wanaouawa hapa nchini na kwamba, kutokana na wingi wa nyara walizokutwa nazo, inaonekana wazi ni miongoni mwa vinara, wawezeshaji na wahusika wa shughuli za ujangili zinazoendelea nchini.

Alisisitiza kuomba wapewe adhabu kali kwa kuwa tembo ni miongoni mwa wanyama watano wanaoongeza mapato la Taifa kupitia utalii.

Wakili wa utetezi, Nkoko aliiomba Mahakama iwapunguzie adhabu wateja wao kwa kuwa walikwisha kaa rumande miaka mitatu.

Washtakiwa hawa walikamatwa na nyara hizo za Serikali na aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki.

Wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo, upande wa mashtaka ukiendeshwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi, uliwaita mashahidi tisa wakiwamo wapelelezi, majirani wa washtakiwa walioshuhudia upekuzi, maofisa kutoka polisi na Wizara ya Maliasili na Utalii ambao walitoa ushahidi dhidi ya washtakiwa hao.

Miongoni mwa ushahidi wao, walidai kuwa Oktoba 20, 2013, walipokea taarifa kuwa kuna meno ya tembo yanasafirishwa kutoka mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kwenda Dar es Salaam na yangeuzwa eneo la Biafra Kinondoni, Dar es Salaam.

Walidai kuwa Novemba 2,2013, waliona gari likiendeshwa na raia hao wa China walilifuatilia hadi kubaini shehena hizo za meno ya tembo zilipohifadhiwa. 

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya March 19

Zanzibar: Mwandishi wa Habari wa Radio Deutsche Welle(DW-Swahili), Salma Said Akamatwa na Haijulikani Alipo......Hapa Kuna Mahojiano Akiwa Kusikojulikana

$
0
0

Mwandishi wa Habari wa Radio Deutsche Welle(DW-Swahili), Salma Said jana alikamatwa na watu wasiojulikana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Unguja, alipokuwa akisafiri kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia afya yake. 

Akizungumzia tukio hilo jana, mume wa Salma, Ali Salim Khamis ambaye pia ni Mbunge wa Mwanakwerekwe (CUF), alisema alipata ujumbe wa maandishi kutoka kwa mkewe kwamba amekamatwa.

Khamis alisema alipokwenda uwanja wa ndege aliambiwa na mkuu wa polisi wa uwanjani hapo kwamba hana taarifa za tukio hilo jibu ambalo alilipata pia kwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Mjini Magharibi.

Alisema aliamua kwenda kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa ambako pia aliambiwa hawana taarifa za kukamatwa kwa Salma. “Hadi sasa sijui mke wangu yuko wapi bado naendelea kumtafuta.”

Khamis alisema Salma alikuwa tayari amepitia taratibu zote na alikuwa akisubiri kuingia ndani ya ndege ambayo haikutajwa, lakini alisema ndege hiyo iliyokuwa iondoke saa 8.05 mchana ilizuiwa na watu hao wanaodaiwa kuwa ni askari hadi saa tisa kasoro, walipoiruhusu lakini ikidaiwa kuwa waliondoka na Salma kwenda kusikojulikana. 

==> Hapo chini kuna  Mahojiano ya DW na Salma Said akiwa sehemu ambayo haijulikani


Kigogo wa Madawa ya Kulevya Atiwa Mbaroni Dar.......Traffic Dar Wakusanya Milioni 577 za Makosa Barabarani ndani Ya Siku 12 Tu.

$
0
0

Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilo moja, akiwamo anayedaiwa kuwa kigogo wa biashara ya dawa hizo nchini.

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, juzi saa 1.15 usiku katika maeneo ya Mbezi Beach, walimkamata mtuhumiwa wa kwanza akiwa na gari baada ya kumpekua alikutwa na dawa hizo za kulevya. 

Alisema walipomhoji zaidi, alidai kuwa dawa hizo siyo zake, bali za tajiri yake anayeishi Mikocheni jijini hapa ambaye wali panga kukutana naye maeneo ya Mbezi Beach kwa ajili ya kukabidhiana.

Alisema upelelezi unaendelea na utakapokamilika, watuhumiwa watafikishwa mahakamani. 

Kukamatwa kwa kigogo huyo na msaidizi wake ni mafanikio ya jeshi hilo ambalo hivi karibuni lilimkamata kigogo mwingine muuza ‘unga’ jijini hapa hivi karibuni. 

Wakati huohuo,Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kupitia kitengo chake cha usalama Barabarani limekamata magari mbalimbali kwa makosa ya usalama barabarani 

Jumla ya Tshs. 577,831,000 zimekusanywa ikiwa ni tozo kwa makosa hayo kwa mida wa siku 12, kuanzia 07/03/2016 hadi tarehe 18/03.2016.

Kamanda Sirro amewataka madereva kuwa makini na waangalifu pindi wawapo barabarani ili kuepuka adhabu zitolewazo ili vipato hivyo viwasaidie katika maisha yao ya kila siku. 

Maandalizi ya Uchaguzi Visiwani Pemba Yakamilika....Wananchi Watakiwa Kujitokeza Kwa Wingi Kesho Kupiga Kura

$
0
0

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imesema maandalizi ya uchaguzi visiwani Pemba yamekamilika na kuwataka wananchi kujitokeza kesho kupiga kura na kuachana na dhana kuwa kutakuwa na vurugu.

Mwandishi wetu alishuhudia malori saba ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) yakipakia vifaa vya uchaguzi katika ofisi ya ZEC Pemba katika tukio lililowafanya baadhi ya wananchi kuacha shughuli zao wakishangaa na wengine wakisema; “sasa shughuli imeanza”.

Ofisa Mdhamini wa ZEC Pemba, Ali Mohammed Dadi alisema wameshapokea karatasi na masanduku ya kupigia kura na fomu mbalimbali. 

Alisema karatasi za uchaguzi wa wawakilishi na madiwani zilianza kusambazwa jana na walitarajia kupokea za urais jana jioni na kuzisambaza leo.

Jana, magari 15 ya polisi aina ya Land Rover yakiwa na askari 10 wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kila moja, zilionekana zikirandaranda katika mitaa ya Pemba.

“Sisi tunachotaka ni amani tu hao askari waje tu watulinde hakuna mfanya vurugu hapa. Hata wakizagaa mtaani kwetu heri tu ili mradi wasituzuie kufanya shughuli zetu, “alisema Ramadhani Hamisi Omar, mkazi wa Chakechake.

Chadema Yawafuata CCM Mahakamani....Yapinga Agizo la Jiji La Dar Kuwazuia Wananchi Kuingia Kwenye Ukumbi wa Uchaguzi wa Meya

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema hakikubaliani na agizo la serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Jiji la kuwataka wanaotakiwa kuhudhuria kwenye kikao cha uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es salaam wawe ni wajumbe pekee watakaopiga kura.

Chama hicho kimekataa agizo hilo na badala yake kinataka wananchi wote wa jiji la Dar es salaam wahudhurie katika kikao hicho.

Msimamo huo wa Chadema unapingana na barua ya wito wa mkutano wa uchaguzi huo iliyoandikwa Machi 15, 2016 na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sarah Yohana, iliyosema kuwa watakaoruhusiwa kuingia katika viwanja hivyo ni wajumbe pekee ambao ni wapigakura. 
Akizungumza na wanahabari jana jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Mwita Waitara alisema sheria na kanuni zinaruhusu wananchi kushiriki kikao hicho cha wazi, hivyo Yohana hana mamlaka ya kuwazuia.

“Sisi tunafuata sheria na kanuni, barua ya mkurugenzi inaeleza kinyume cha utaratibu,” alisema.

Alisema kufuatia hali hiyo, Ukawa umemwandikia barua Mkurugenzi huyo ya kutokubaliana na matakwa yake ya kuzuia wafuasi wa vyama kuingia ukumbini wakati wa uchaguzi kwani ni uvunjifu wa sheria na kwamba hawatakubali, bali watawapigania na kuhakikisha wananchi wanaingia ukumbini.

Katika hatua nyingine, Waitara alisema CCM kwa sasa  inawaandaa wanachama feki wa CCM wakiongozwa na wakili Elias Nawela kufungua kesi ya madai huku wakitaka wajumbe 9 toka Zanzibar na 11 kutoka mikoa mingine kushiriki uchaguzi wa meya.

Alisema, ili kukabiliana nao, wameamua kuwafuata hukuhuko mahakamani  ambapo tayari wameshatuma maombi ya  kujiunga na kesi hiyo  namba 39  ya  mwaka 2016 huku wakiwa na mawakili wao ambapo inatarajiwa kusomwa Machi 21 mwaka huu katika Mahakama ya Kisutu.

NEC yakigomea chama cha CUF ....Yasema Haitumbui Kujitoa Kwa Mgombea Ubunge Wa Chama Hicho

$
0
0

Tume  ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),imesema haitambui  kujitoa kwa Chama cha Wananchi (CUF),katika uchaguzi wa Mbunge  Jimbo la Kijitoupele hapa Zanzibar unaotarajiwa kufanyika kesho Jumapili licha ya kuwa  Tume imepokea barua rasmi toka kwa uongozi wa Chama hicho.

Mkurugenzi wa uchaguzi wa Tume ya Taifa Bw Kailima Ramadhani amesema Tume imefikia maamuzi hayo kutokana na ukweli kuwa barua hiyo ya CUF imechelewa huku maandalizi ya uchaguzi huo yakiwa yamekamilika na ni Wananchi tu kwa sasa Wanasubiriwa kwenda kupiga kura.

Aidha Bw Kailima ameeleza kuwa,kwa kuwa karatasi za kupigia kura zilishachapishwa na kuwasili hapa nchini tayari kwa uchaguzi huo,zitaendelea kuwa na picha za Wagombea wa CUF hata kama wamejitoa katika uchaguzi huo.

Awali,wajumbe wa Tume ya Taifa ya uchaguzi  wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji mstaafu Hamid Mahamood Hamid walitembelea katika vituo mbalimbali  vya kupigia kura katika Jimbo la Kijitoupele ili kujiridhisha na maandalizi ya uchaguzi huo kabla ya uchaguzi kufanyika jumapili.

Tume ilibaini kuwepo kwa baadhi ya kasoro ndogondogo katika baadhi ya vituo vya kupigia kura ikiwa ni pamoja na kubanduliwa kwa karatasi zenye majina ya wapiga kura,mfano katika kituo cha Skuli ya sekondari Kinuni.

Jimbo la Kijitoupele lina jumla ya Wapiga kura wapatao 17,274 na vituo vipatavyo 53 vitatumiwa na wapiga kura ili kumchagua mbunge wa Jimbo la Kijitoupele siku ya Jumapili.

Sambamba na Uchaguzi wa ubunge katika Jimbo la Kijitoupele, marudio ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar Oktoba 25,2015 ambayo matokeo yake yalifutwa uatafanyika Jumapili hiyo pia.

Uchaguzi katika jimbo la Kijitoupele uliahirishwa mwaka jana kutokana na hitilafu ndogondogo zilizojitokeza katika karatasi za kupigia kura,kabla ya kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25,2015.

Rais Magufuli ateua wakurugenzi wakuu wapya NSSF, TBC na RAHCO

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa watendaji wakuu wa Taasisi tatu za serikali kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo.

KWANZA, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Profesa Godius Kahyarara kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Uteuzi huu umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya NSSF namba 28 ya Mwaka 1997, Kifungu cha 42, kinachoeleza kuwa Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuteua Mkurugenzi Mkuu wa NSSF.

Prof. Kahyarara anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ramadhan Dau, ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

PILI, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Ayub Rioba Chacha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Dkt. Rioba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Clement Mshana ambaye amestaafu.

TATU, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Mussa Iddi Mgwatu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO).

Dkt. Mgwatu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Benhadard Tito, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Uteuzi wa watendaji wote watatu umeanza mara moja

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam.
19 Machi, 2016.

Habari Zilizopop Karika Magazeti Ya Leo Jumapili Ya March 20

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>