Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Maalim Seif Afunguka wakati Wazanzibar wakipiga Kura........"Kilichotokea Zanzibar ni mipango iliyopangwa na CCM"

$
0
0

Aliyekuwa Mgombea Urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Oktoba 25, mwaka jana, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema hatma ya Wazanzibar iko mikononi mwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Maalim Seif alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa ni nini hatma ya Zanzibar baada ya uchaguzi wa marudio uliofanyika jana.

“Mimi sijui, waulizeni CCM wao ndiyo wametengeneza hali hii, wao ndiyo wamekusudia na wanajua wanaipeleka wapi nchi hii, watasema wao,” alisisitiza Maalim Seif.

Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelewa na Vijana wa Baraza la Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema-Bavicha jijini Dar es Salaam jana kumjulia hali.

Baada ya kufutwa kwa uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana, hali ya kisiasa ya Zanzibar imedaiwa kuwa tete haswa kutokana na CUF kudai hawatambui kufutwa kwa uchaguzi huo msimamo wao wakitaka mshindi atangazwe.

Maalim Seif alisema CCM wanafahamu wazi kwamba mshindi aliyeshinda katika uchaguzi wa wa Okotoba 25, ni nani, lakini wameamua kufanya hivyo na kuifikisha Zanzibar hapo ilipo sasa.

Alisema miaka mitano iliyopita kulikuwa kumepatikana maridhiano Zanzibar na walikuwa wameanza kwenda vizuri, lakini kinachoonekana hivi sasa wameanza kuwarudisha nyuma kwa kuvuruga tena maridhiano hayo na kuanza kuleta uhasama.

“Hapo nyuma kulikuwa na uhasama wa kisiasa Zanzibar halafu ukaisha, lakini hivi sasa wanaurudisha, CCM ndiyo wameamua iwe hivyo,” alisema Maalim Seif.

Kadhalika, Maalim Seif alisema anaamini Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec), Jecha Salim Jecha, ametumwa kuitafutia kura CCM.

“Jecha ametumwa kuitafutia kura CCM, lakini ijulikane kwamba hata wafanye vyovyote watakavyofanya, Wanzanzibari ndani ya mioyo yao, wanafahamu Rais wao ni mimi,” alisema Maalim Seif na kuongeza:

“Kinachotokea Zanzibar ni mipango iliyopangwa na CCM ambao pamoja na kwamba wanamfahamu mshindi ni nani katika uchaguzi wa mwaka jana, lakini wameamua kufanya hicho wanachofanya hivi sasa.”

Aidha, alisema kwa sasa hataki kusema chochote, isipokuwa anasubiri Rais atangazwe.

Maalim Seif yuko jijini Dar es Saalam kwa mapumziko mafupi baada ya kuugua na kuruhusiwa kutoka hospitali zaidi ya wiki moja iliyopita.

Matokeo ya awali ya Urais kwa Majimbo ya OLE, Ziwani, Chonga, Wawi na Chake Yanaonyesha Dr. Ali Mohamad Shein Anaongoza

Baadhi Ya Matokeo ya Uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza La Wawakilishi Zanzibar

$
0
0

Matokeo ya uchaguzi wa marudio uliofanyika jana visiwani zanzibar kwa upande wa wajumbe wa baraza la wawakilishi yameanza kutangazwa kisiwani pemba.
 
1.Jimbo la Chakechake aliyeshinda ni Suleiman Said wa CCM

2.Jimbo la Ole mshindi ni Musa Ali Musa wa CCM

3.Jimbo la Wawi mshindi ni Hamad Ali Rashid wa CCM

4.Jimbo la Ziwani mshindi ni Asaa ali Hamad wa UPDP

5.Jimbo la Chonga aliyetangazwa mshindi ni Shaibu Ali wa CCM

Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO Assah Mwambene Ahamishiwa Wizara Ya Mambo Ya Nje

$
0
0
Mkurugenzi wa  Idara  ya  Habari -MAELEZO   Assah  Mwambene   Ahamishiwa Wizara Ya Mambo Ya Nje 
 

TRL Yasitisha Safari Za Kuanzia Dar Es Salaam......Wasafiri Wa Mwanza Na Kigoma Sasa Kuanzia Safari Zao Mkoani Dodoma

$
0
0

Mamlaka ya Reli Nchini (TRL) imesitisha safari zake kutoka Dar es salaam kwenda Mikoani na kuhamishia huduma hiyo mkoani Dodoma kutokana miundombinu ya reli kuharibiwa na mvua za masika zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini.

Mvua hizo zimeharibu miundombinu ya reli ya kati wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam , Kaimu Mkurugenzi TRL, Masanja Kadogosa amesema kuwa kutokana na kusitishwa kwa huduma hiyo ratiba ya huduma mpya inatarajiwa kuanza kesho Machi 22 kwa wasafiri wanaotarajia kusafiri kutoka Dodoma kwenda Mwanza na Kigoma kuanzia majira ya  saa 11 jioni.

Amesema gari moshi jipya ya Delux kwa wasafiri wa Kigoma wanatakiwa kukata stakabadhi ya malipo ya safari siku ya Jumanne saa 2:00.

Kadogosa amesema kuwa jitihada mbalimbali zinaendelea kufuatia mashirikiano kati ya kampuni hodhi ya Rahco pamoja na Shirika la reli nchini ili kuweza kurejesha huduma hiyo kama ilivyokuwa awali.

Amesema kuwa wasafiri wanaotumia usafiri huo waondowe wasiwasi kutokana na jitihada zinazofanywa za urejeshaji wa huduma ya reli.

Breaking News: Dr. Ali Mohammed Shein Atangazwa Rasmi kuwa Mshindi wa Kiti Cha Urais Zanzibar Kwa Asilimia 91.4

$
0
0
Mgombea wa urais kupitia chama cha CCM Visiwani Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ameshinda kiti cha urais kwa jumla ya kura 299,982 awa na asilimia 91.4 ya kura zote halali 328,327 katika uchaguzi wa marudio uliofanyika jana.

Matokeo hayo yametangazwa leo na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha.

Uchaguzi huo wa marudio ulifanywa jana baada ya kufutwa Oktoba 25 kutokana na kile kilichotangazwa na Jecha kuwa ni kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa taratibu za uchaguzi huo.

Uchaguzi huo ulisusiwa na vyama kumi kwa kile walichodai kuwa kufutwa kwa uchaguzi huo mwezi Oktoba ilikuwa ni batili.

Hata hivyo karatasi za kupigia kura zilikuwa na majina yote ya wagombea kama ilivyokuwa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba.

Jecha alifafanua kuwa hakuna hata mgombea mmoja aliyefuata utaratibu wa kujitoa kwa mujibu wa sheria na kanuni.
==> Matokeo yote kama yalivyotangazwa  yako  hapo  chini....

Endelea Kutembelea Mpekuzi kwa habari motomoto..!

Breaking News: Rais Magufuli Atekeleza Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda La Kuhakiki Silaha Upya

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekuwa mtu kwanza kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam la kuhakiki silaha, ambapo bunduki zake mbili aina ya Shortgun na Pistol zimehakikiwa nyumbani kwake Ikulu Jijini Dar es salaam.

Uhakiki huo umefanywa na maafisa wa Jeshi la Polisi wakiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Rais Magufuli amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na Jeshi la Polisi kwa kuendesha zoezi la uhakiki wa Silaha, na ametoa wito kwa watu wote wanaomiliki silaha nchi nzima kuhakikisha zinahakikiwa.

Dkt. Magufuli pia amelitaka Jeshi la Polisi kuongeza juhudi za kukabiliana na watu wanaojihusisha na vitendo vya uharifu ili kutokomeza kabisa vitendo hivyo.

"Ni aibu kumuona askari polisi mwenye silaha ananyang'anywa silaha, ni aibu, na nasema hiyo ni aibu, mpaka jambazi akunyang'anye silaha na wewe una silaha?" Amehoji Rais Magufuli

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna Simon Sirro, amemshukuru Rais Magufuli kwa kuunga mkono zoezi hilo na amesema Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa mafanikio.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ametaka pande zinazogombea kiti cha Umeya katika Jiji la Dar es salaam, kukamilisha mchakato wa kumpata Meya katika uchaguzi uliopangwa kufanyika kesho tarehe 22 Machi, 2016 badala ya kuendelea kurumbana.

Dkt. Magufuli amesema upande wowote uwe tayari kupokea matokeo ya uchaguzi huo, ili Meya apatikane na Jiji liweze kuendelea na mipango yake ya kuwahudumia wananchi bila vikwazo.

"Mahali tunapostahili kushinda kama tumeshinda tushinde kweli, lakini mahali tunaposhindwa napo tukubali kushindwa, na hiyo ndio demokrasia ya kweli"ameongeza Rais Magufuli

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
Kamanda wa Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna CP Simon Sirro kulia akimkabidhi Silaha aina ya Bastola Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna CP Simon Sirro kulia akimkabidhi silaha aina ya shortgun Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiiweka silaha yake vizuri mara baada ya kuhakikiwa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Bad News: Msafara wa Kamati ya Bunge Utawala na TAMISEMI Wapata Ajali Mbaya Bagamoyo ....Watu Watano Wafariki Dunia

$
0
0

WATU watano wamefariki dunia huku nane wamejeruhiwa, katika ajali iliyoyahusisha magari manne, mawili yakiwa katika msafara wa Kamati ya Bunge Utawala na TAMISEMI maeneo ya Kerege, Bagamoyo Pwani.

Waliofariki katika ajali ni Hilda Msele (59), Mkuu wa Idara ya Mipango ya Uchumi, Makame Ally (40), Dereva wa Tasaf, Khalid Hassan (40), Tunsime Duncan, Mwanasheria wa Wilaya  na Ludovick Palangya, Mchumi.

Majeruhi waliolazwa katika hospitali ya Taifa ua Muhimbili ni Ibrahim Matovu, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Bagamoyo, Juliana Msaghaa, Mhandisi wa Maji wilaya, Dorothy Njetile, Mratibu wa Tasaf, George Mashauri, Mweka Hazina wa Wilaya, Amadeus Mbuta, Mshauri wa Tasaf, Julius Mwanganda, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Tauliza Halidi, Mwananchi na Amari Mohamed, Mwananchi.

Aliyepelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo na kuruhusiwa ni Grace Mbilinyi ambaye ni Afisa Utumishi na Utawala wa Wilaya.

Ajali hiyo ilihusisha lori la mchanga, gari dogo yaliyokuwa yanatokea Bagamoyo kuja Dar es Salaam, na magari mawili yaliyokuwa kwenye msafara wa Kamati hiyo, yaliyokuwa yanaenda Bagamoyo kwa shughuli zake za kibunge.

Magari yaliyokuwa katika msafara wa kamati hiyo, ni gari la Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) na gari la Mkurugenzi wa Wilaya ya Bagamoyo ambayo yaligongwa na lori hilo la mchanga na kusababisha vifo vya watu hao na kuwajeruhi wengine kadhaa.

Ajali hiyo ilitokea baada ya gari dogo lililokuwa linatokea Bagamoyo kupunguza mwendo ghafla na kusababisha lori lililokuwa nyuma yake kuligonga na kuhama upande wa pili na kuyagonga magari mawili yaliyokuwa katika msafara wa kamati ya Bunge.


Rais Magufuli Ampongeza Dr. Shein kwa Kushinda Urais Zanzibar

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za pongezi Rais Mteule wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, kufuatia ushindi alioupata katika marudio ya Uchaguzi Mkuu wa Rais wa Zanzibar, uliofanyika jana tarehe 20 Machi, 2016.

Katika salamu hizo Rais Magufuli amesema ushindi wa Dkt. Shein umedhihirisha imani na matumaini makubwa waliyonayo wazanzibari kwake na kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Aidha, Rais Magufuli amewapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kushiriki katika uchaguzi huo kwa amani na utulivu, na hatimaye kumpata mshindi wa kiti cha Urais ambaye atawaongoza kwa kipindi cha miaka mitano.

"Naomba nikupongeze kwa dhati Mheshimiwa Rais Mteule Dkt. Ali Mohamed Shein kwa ushindi ulioupata, ushindi ambao umeonesha kuwa wananchi wa Zanzibar bado wanahitaji uwaongoze kwa kipindi kingine cha miaka mitano" Amesema Rais Magufuli.

Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pia ameahidi kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kufanya kazi bega kwa bega na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na amewataka Wazanzibari wote kujielekeza katika maendeleo kwa kuwa uchaguzi umekwisha.

"Ndugu zangu wa Zanzibar uchaguzi umekwisha, kilichobaki sasa ni kushirikiana na serikali yenu kuijenga Zanzibar na ninaamini mnao wakati mzuri wa kuijenga Zanzibar yenye maendeleo chini ya uongozi wa Dkt. Ali Mohamed Shein" amesisitiza Dkt. Magufuli

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

Mabalozi wa nchi za Ulaya na Marekani Waukosoa Uchaguzi wa Marudio uliofanyika Jana Visiwani Zanziba

$
0
0

Mabalozi na wawakilishi wa nchi za Ubelgiji, Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Norway, Hispania, Sweden, Switzerland, Uingereza na Marekani hivi leo wametoa tamko kuhusu uchaguzi wa marudio uliofanyika Zanzibar tarehe 20 Machi 2016:
 
“Tumesikitishwa na uamuzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) wa kuendesha marudio ya uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015, bila kuwepo makubaliano ya pamoja baina ya pande kinzani na ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa visiwani humo uliotokana na majadilino baina ya pande husika. 
 
“Ili uwe wa kuaminika na kukubalika ni lazima mchakato wa uchaguzi uwe jumuishi na unaowakilisha kwa dhati matakwa ya watu.
 
“Tunarejea wito wetu kwa Serikali ya Tanzania kuonyesha na kuchukua uongozi katika suala la Zanzibar na kujielekeza katika kupatikana kwa ufumbuzi wa mgogoro huu kwa kupitia mazungumzo baina ya pande husika kwa lengo la kudumisha amani na umoja katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
“Kwa mara nyingine tunawapongeza wananchi wa Zanzibar kwa utulivu na ustahimilivu waliouonyesha katika kipindi chote cha mchakato huu na kuvitaka vyama vyote na wafuasi wao kuanzisha tena mchakato wa maridhiano ya kitaifa ili kupata ufumbuzi jumuishi, endelevu na wa amani.”

Taarifa ya Habari Ya Channel Ten – Jumatatu Tarehe 21.03.2016

$
0
0

Taarifa ya Habari Ya Channel Ten  – Jumatatu Tarehe   21.03.2016


Waziri Mkuu Amwagiza CAG Kukagua Mapato ya Bandari na Benki ya CRDB......Makampuni 150 ya Uwakala Yafunguliwa

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali aende Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ili akague taarifa za mapato ambazo zilikuwa zikilipwa na mawakala wa forodha na bandari kupitia benki ya CRDB lakini hazionekani kwenye mifumo ya benki.

Ametoa agizo hilo leo jioni (Jumatatu, Machi 17, 2016) wakati akizungumza na mamia ya mawakala wa forodha na bandari waliohudhuria mkutano aliouitisha ili kusikiliza kero zinazowapata katika utendaji kazi wao.

Akizungumza na mawakala hao kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu alisema kuna dalili za kutupiana lawama baina TPA na CRDB kuhusu malipo yaliyikuwa yakifanyika benki halafu fedha hazionekana na wakala anaidaiwa kuwa hajalipia mzigo wakati alishaulipia.

“Kimsingi bado liko tatizo baina ya Mamlaka ya Bandari pamoja na Benki ya CRDB. Naona kila mmoja hapa anamkana mwenzake. Nitamtuma CAG ili akafanye ukaguzi wa kina ili tujue ni nani kati yao amehusika na upotevu wa fedha,” alisema huku akishangiliwa na mawakala hao.

Alimwagiza pia Kaimu Mkurugenzi wa Bandari, Eng. Aloyce Matei aandae dispatch zote walizotumia kupokelea malipo za kuanzia mwaka 2015 na ikibidi aandae za kuanzia mwaka 2014 ili CAG anapozopitia aweze kupata picha halisi.

Vilevile, Waziri Mkuu alimwagiza Eng. Matei kuhakikisha wananunua mashine ya photocopy ili iwekwe kwenye chumba cha kupokelea stakabadhi za malipo ya benki (bank pay in slip) ili mteja anapoleta nakala ya benki aweze kutolewa photocopy na kubakia na nakala ya malipo aliyofanya,

Waziri Mkuu alisema Serikali inatambua bandari ni eneo nyeti katika kuinua uchumi na mapato ya nchi lakini pia ni eneo muhimu katika kutengeneza ajira. 

“Ninapenda niwahakikishie kuwa bado tutaendelea kukagua bandari hadi pawe safi. Hii bandari ni yenu na mtafanya kazi kama kawaida,” alisema.

Mapema, akizumgumza kwa niaba ya mawakala hao, Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha nchini (TAFFA), Bw. Stephen Ngatunga alieleza matatizo mbalimbali ambayo wao kama mawakala wa forodha wamekuwa wakikumbana nayo kuanzia ulipaji, utoaji wa mizigo na kuitaka Serikali iongeze nguvu katika kuikabilia sekta hiyo.

Alizikosoa baadhi ya sheria ambazo zinaruhusu wamiliki wa bandari kavu kumiliki pia makampuni ya uwakala wa forodha, sheria kadhaa zinazochangia kukwamisha utoaji wa mizigo bandarini, ukaguzi hafifu wa kwenye scanner na uwepo wa vituo vinane vya mizani kuanzia Dar es Salaam hadi Tunduma ambavyo vimegeuka kuwa kero kwa wasafirishaji wa mizigo kwenda nchi jirani.

Wakati huohuo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani amesema Serikali imeamua kuyafungulia makampuni zaidi ya 150 ambayo yalikuwa yamefungiwa kufanya kazi za uwakala wa forodha kutokana na madai ya kuhusishwa na ukwepaji wa kodi.

“Hapa tumegundua kuwa wote siyo wasafi iwe ni mawakala, benki ama bandari. Mkurugenzi wa Bandari, kuanzia leo watu hawa waruhusiwe waanze kufanya biashara lakini nyaraka za nyuma zisiguswe hadi CAG atakapokamilisha uchunguzi wake,” alisema kuibua kelele za shangwe kwenye ukumbi huo.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,11410 DAR ES SALAAM
JUMATATU, MACHI 21, 2016.

Mkuu wa Wilaya ya Njombe Sarah Dumba afariki dunia

$
0
0

Mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba amefariki dunia jana jioni ya  baada ya kuugua ghafla

Mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi amethibitisha kutokea kwa msiba huo, na kueleza kuwa marehemu Sarah alifariki majira ya saa moja jioni katika hospitali ya Kibena mjini Njombe ambapo alipelekwa kwa ajili ya uangalizi wa kiafya.

Dkt Nchimbi amesema kuwa, haijafahamika nini kilichosababisha kifo hicho, lakini huenda ikawa ni "Mshituko" maana jana  asubuhi aliwasili ofisini kama kawaida, na kuendelea na shughuli zake akiwa hana tatizo.

Ameendelea kueleza kuwa, akiwa ofisini kwake, alianza kusema kuwa anajisikia vibaya, na kuamua kugawa majukumu yake kwa watendaji wengine, lakini hali yake ilizidi kutia mashaka na ndipo akapelekwa hospitali.

Dkt Nchimbi amesema, akiwa hospitali hali ilibadilika ndani ya muda mfupi na kuanza kutapika, na ilipofika majira ya saa moja alifariki dunia.

"Nadhani inaweza kuwa ni tension maana tupo kwenye maandalizi ya kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji, na yeye amekuwa akishughulika sana na maandalizi hayo ambayo kilele chake ni kesho, sasa leo amefika ofisini kama kawaida, lakini baadaye akasema hajisikii vizuri, baadhi ya kazi akatuma watu, baadaye alikwenda hospitali, lakini muda mfupi baada ya kufika hali ikabadilika, akatapika sana na hapo ndipo alipopoteza maisha" Amesema Dkt Nchimbi.

Mkuu huyo wa mkoa amesema mipango ya maziko itatangazwa baadaye leo, lakini kwa taarifa za awali alizonazo ni kwamba huenda akapelekwa nyumbani kwao ambapo ni Dar es salaam, ingawa kuna taarifa nyingine zinadai kuwa nyumbank kwao ni Morogoro.

Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu Sarah Dumba. Amin
Sarah Dumba katika picha akipeana mkono na Waziri  Mkuu mstaafu, Mizengo K. P. Pinda

Rais Magufuli Atuma Salamu Za Rambirambi Kufuatia Vifo Vya Wafanyakazi Sita Wa Bagamoyo Waliofariki Ajalini

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, kufuatia vifo vya wafanyakazi sita wa halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, vilivyosababishwa na ajali ya barabarani, iliyotokea leo tarehe 21 Machi, 2016 katika eneo la Kerege Wilayani humo.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa tano za asubuhi, baada ya Lori la kubebea mchanga kuyagonga magari mawili ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ambayo yalikuwa katika Msafara wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na serikali za mitaa, iliyokuwa akitoka kukagua mradi wa Maji wa Mapinga.

Katika salamu hizo Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshituko mkubwa taarifa za vifo vya wafanyakazi hao wa halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, ambao wamepoteza maisha wakiwa wanatekeleza majukumu ya kikazi.

“Kupitia kwako Mkuu wa Mkoa wa Pwani naomba kutoa pole nyingi kwa familia za marehemu wote, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na vifo hivyo, naomba Mwenyezi Mungu awape moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu kutokana na kuondokewa na wapendwa wao” Amesema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi. Amina

Aidha, Rais Magufuli amewapa pole wafanyakazi wengine wanane ambao wameumia katika ajali hiyo, na amewaombea wapone haraka.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
21 Machi, 2016

Watumishi Watatu Manispaa Ya Kinondoni Kusimamishwa Kazi

$
0
0

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeitaka Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuwasimamisha kazi watumishi watatu wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, akiwemo Mwanasheria wa Manispaa hiyo, Barton Mahenge kutokana na matumizi mabaya ya ofisi.

Watumishi wengine waliotakiwa kusimamishwa kazi kutokana na matumizi hayo mabaya ya ofisi na kushindwa kuishauri manispaa hiyo kuhusu mkataba wake na Kampuni ya Oysterbay Villa ni Mchumi Mwandamizi, Ando Mwankuga na Mratibu wa Uwekezaji na Mthamini wa Manispaa hiyo, Einhard Chidaga.

Pamoja na hayo, Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene pamoja na kuahidi kutekeleza maagizo hayo, pia ameapa kuwa atahakikisha watendaji wengine waliohusika katika mkataba huo hata kama wamestaafu au kuacha kazi, wanapatikana na kuwajibishwa.

Akizungumza na uongozi wa manispaa hiyo, Mwenyekiti wa LAAC, Kangi Lugola alisema watumishi hao pamoja na kuwepo kwenye madaraka yao kwa muda mrefu, wameshindwa kushauri namna ya kufikia malengo ya mkataba huo ambayo ni kuongeza mapato na ajira.

Alisema kamati hiyo imebaini kuwa mkataba huo unaohusisha vitalu viwili vilivyopo eneo la Oysterbay namba 277 na 322 vimekuwa vikimnufaisha mwekezaji huyo pekee kwa muda wa miaka sita tangu ujenzi wa majengo ya makazi ukamilike mwaka 2011.

“Kamati hii imetafakari na kuamua kuwa mwanasheria, mchumi na mthamini wa manispaa wasimamishwe kazi ili kupisha uchunguzi dhidi ya mkataba huu. Kamati yangu pia itaunda kamati ndogo itakayoshirikiana na Sekretarieti ya Sheria ya Bunge ili kuupitia kwa kina mkataba huu na kutoa ushauri utakaosaidia manispaa hii,” alisisitiza Lugola.

Alisema baada ya LAAC kupitia mkataba huo imebaini kuwa pamoja na manispaa hiyo kutopata mapato kwa muda wa miaka sita huku majengo yakiwa matupu bila wapangaji kwa kipindi chote, pia uwekezaji wa mradi huo unaojumuisha ardhi, alipatiwa mwekezaji raia wa nje jambo ambalo ni kinyume cha sheria za uwekezaji nchini.

Aidha, alisema mkataba huo umebainisha mgawanyo wa mapato baina ya pande zote mbili zilizoingia ubia ambao hauendani na kiwango cha uwekezaji kwani Manispaa ya Kinondoni iliwekeza kwa kutumia ardhi kupitia vitalu viwili vyenye thamani ya Sh bilioni sita wakati mwekezaji huyo alijenga majengo hayo kwa gharama ya Sh bilioni 11.

“Mkataba unaonesha mgawanyo wa mapato kwa kila upande na upande wa manispaa unapata asilimia 25 kupitia vyumba vyake 17 vya mradi huo, wakati kampuni ya Oysterbay Villa inapata asilimia 75 kupitia vyumba vyake 51,” alisema Lugola katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Naibu Spika Dk Tulia Ackson.

Alisema mkataba huo pia unaonesha kuwa katika kitalu 377 mwekezaji anatakiwa kujenga jengo la ghorofa lenye vyumba 40, lakini katika uhalisia alijenga jengo lenye vyumba 44 huku mgawanyo ukibakia vilevile kama mkataba wa awali ulivyotaka asilimia 25 na 75.

“Hili ndio eneo lenye changa la macho, huu mgawanyo haueleweki na kama kweli mnapata asilimia 25, mbona tangu mwaka 2011 manispaa haijapata hata senti tano ya faida ya mradi huu zaidi ya kudai kuwa mnamdai mwekezaji shilingi bilioni 3.5 tena za miaka hiyo…” 

Pamoja na maagizo hayo, pia kamati hiyo, iliitaka Wizara ya Tamisemi ihakikishe inampatia Mwanasheria Mkuu (AG) wa Serikali mkataba huo ili aupitie na kutoa ushauri wake.

Lucy Mayenga Ajisalimisha....Amuomba Rais Magufuli Ampumzishe Ukuu wa Wilaya

$
0
0

Wakati Taifa likisubiri uteuzi wa wakuu wa wilaya huku wanaoshikilia nafasi hizo wakiwa katika chekeche kwa kuzingatia vigezo vitano, Mkuu wa Wilaya Iramba, mkoani Singida, Lucy Mayenga amemuomba Rais John Magufuli asimjumuishe kwenye orodha ya wakuu hao anayotarajia kuitangaza wakati wowote.

Rais Magufuli ameweka bayana vigezo atakavyotumia kufanya uteuzi wa wakuu hao wa wilaya ambavyo ni pamoja na suala la migogoro ya ardhi, tatizo la elimu hasa upungufu wa madawati, njaa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu alivyovitangaza wakati akizungumza na wazee wa Dar es Salaam na katika uteuzi wa wakuu wa mikoa, alizungumzia pia suala la wafanyakazi hewa ambao wamekuwa wakilipwa mishahara bila ya wahusika kuchukua hatua kudhibiti.

Akizungumza kwenye kikao cha UWT, Mkoa wa Shinyanga mwishoni mwa wiki, Mayenga ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalumu alisema aliwasilisha ombi hilo binafsi kwa Rais Magufuli ili apate fursa ya kusimamia biashara zake alizosema zinazodorora kutokana na kubanwa na majukumu ya ukuu wa wilaya.

“Pamoja na ukuu wa wilaya, mimi pia ni mbunge na wakati huohuo ni mfanyabiashara; haya ni majukumu mengi kutekelezwa na mtu mmoja kwa wakati moja,”alisema Mayenga 

Aliwaambia wajumbe waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika Kata ya Nyamilangano, wilayani Ushetu kuwa biashara zake nyingi zilizopo mkoani Shinyanga zimedorora kutokana na kukosa usimamizi wake.

“Ombi hili nililitoa binafsi kwa Waziri Mkuu ambaye alinishauri kusubiri uteuzi; isitafsiriwe kwamba nimeogopa kasi ya utendaji ya Serikali ya Awamu ya Tano.Hapana! Nimeona ni vyema nibaki na ubunge na biashara zangu,” alisema Mayenga ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari.

Baadhi ya wanachama wa UWT waliohudhuria mkutano huo walimpongeza kwa uamuzi huo wakisema unapaswa kuigwa na viongozi wengine wenye majukumu mengi kwa kuachia watu wengine nafasi za kutumikia umma badala ya kung’ang’ania nafasi zote.

“Nampongeza Mheshimiwa Mayenga kwa uamuzi wake wa kuomba asiteuliwe tena kwenye nafasi ya ukuu wa wilaya kwa sababu itatoa fursa kwa watu wengine kutumikia nafasi hiyo,” alisema Selina Mkula.

Katika mkutano huo ambao Mbunge wa Ushetu, Elias Kwandikwa alitoa msaada wa mifuko 60 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule za msingi Nyamilangano na Mitonga pamoja na Shule ya Sekondari Kisuke, wanachama wapya 55 walijiunga na UWT.

Mbunge huyo pia aliahidi kutoa vyerehani 20 kwa makatibu kata wa UWT ili kusaidia harakati za maendeleo ya wananchi kwa kuanzisha vikundi vya kiuchumi katika kata zao.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya March 22

Mwandishi wa Habari Salma Said Asimulia Alivyotekwa

$
0
0
Mwandishi wa habari wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) na DW, Salma Said amedai alitekwa na wanaume wawili baada ya kumkamata na kumuingiza kwenye gari lao kisha kuondoka naye na kumpeleka kusikojulikana.

Salma aliyetekwa Ijumaa iliyopita na watu hao katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akitokea Zanzibar kwa ajili ya kuchunguzwa afya yake kwenye moja ya hospitali za jijini Dar, alisimulia mkasa huo jana mbele ya waandishi wa habari huku akimwaga machozi.

Alisema alipoteremka uwanjani hapo, alimpigia simu dereva wake amfuate na wakati akimsubiri, ndipo wakatokea watu hao.

Salma alisema watu hao walimfunga mtandio wake mweusi usoni ili asibaini mahali walikokuwa wakimpeleka na kumfungia chumbani .Alisema ndani ya chumba hicho kulikuwa na vitambaa.

“Waliponiingiza ndani ya chumba kile siku ya kwanza, wakanifungua tambala usoni kwa hivyo nikawaona nyuso zao, mmoja alikuwa na kovu shavuni, mrefu na mwingine mweupe kidogo, waliniweka kule ndani bila kupata chakula chochote,” alisema.

Salma alisema alitakiwa kurudi Zanzibar kwa ajili ya kuripoti marudio ya Uchaguzi Mkuu wa marudio uliofanyika juzi, lakini alishindwa baada ya watu hao kumteka na kumfungia kwenye chumba hicho.

Alidai kuwa watu hao walimwambia watamuachia baada ya uchaguzi huo kufanyika na mgombea wa CCM kutangazwa kuwa mshindi.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za Baraza la Habari Tanzania(MCT), Salma aliongozana na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga, Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga na Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Bara (THRDC), Onesmo Ole Ngurumwa, ambao kwa pamoja walieleza kupinga ukatili huo huku wakiliomba Jeshi la Polisi kuwasaka wahalifu waliohusika.

“Walinisababishia maumivu makali, walinipiga mabuti na makofi huku wakiniambia maneno ya vitisho kama ilivyokuwa kwa Dk Ulimboka na Kibanda,” alidai Salma.

Kabla ya watekaji hao kumrudisha katika eneo walilokuwa wamemteka, Salma alidai kuwa watu hao walimpiga kila walipoingia na kutoka nje ya chumba alichowekwa na kumsababishia apumue kwa tabu.

Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kupata ufafanuzi wa taarifa za uvumi wa kujiteka mwenyewe, Salma alijibu swali hilo huku akidondosha machozi: “Hakuna sababu ya kusema uongo, mimi ni Mwislamu na dini yangu inakemea kufanya hivyo.”

Pia, alisema amefanya kazi kwa miaka zaidi ya 20 na matukio ya vitisho yalianza alianza kuyapata muda mrefu kwa kupigiwa simu, kutumiwa meseji na kufuatwa nyumbani kwake.

Salma ambaye alizungumza huku akionyesha ushahidi wa meseji za makundi ya mitandao yanayojadili kufurahishwa na kutekwa kwake, alisema kujiteka ni kauli zisizokuwa na uhusiano wowote na ukweli, kwani alijitambulisha kuwa mwandishi mtetezi wa haki za binadamu na siasa ambazo zinazokinzana na maslahi ya wachache.

Wakati huohuo; Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro alisema ni mapema kuzungumzia tukio la kutekwa kwa Salma kwa madai kuwa bado wanaendelea kufanya uchunguzi.

Mahakama Yatupilia Mbali Maombi ya Kuzuia Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar Es Salaam...

$
0
0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeamuru uchaguzi wa meya na naibu meya wa Jiji la Dar es Salaam, kufanyika leo kama ilivyopangwa.

Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema alitoa uamuzi huo jana akijibu maombi yaliyokuwa yamewasilishwa na walalamikaji, Suzan Massawe na Saad Mohammed Kimji kupitia wakili wao, Elias Nawela dhidi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam.

Wakati Mahakama ikitoa uamuzi huo, Rais John Magufuli amezitaka pande zinazogombea kiti cha umeya Dar es Salaam, kukamilisha mchakato huo katika uchaguzi uliopangwa kufanyika leo, badala ya kuendeleza malumbano.

Rais alitoa kauli hiyo jana Ikulu wakati akihakiki silaha zake. Alisema pande zote ziwe tayari kupokea matokeo ya uchaguzi huo, ili meya apatikane na jiji liweze kuendelea na mipango yake ya kuwahudumia wananchi bila vikwazo.

“Mahali tunapostahili kushinda kama tumeshinda tushinde kweli, lakini mahali tunaposhindwa napo tukubali kushindwa, hiyo ndiyo demokrasia ya kweli,” alisema Rais Magufuli.

Akitoa uamuzi wa Mahakama uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na walalamikaji na walalamikiwa, Hakimu Lema alisema Mahakama haikuona sababu za msingi kati ya zilizowasilishwa na walalamikaji kuishawishi kuzuia kufanyika kwa uchaguzi huo.

“Siyo busara kuendelea na sababu ambazo hazijathibitishwa,” alisema Hakimu Lema alipokuwa akitoa uamuzi huo na kuongeza kwamba kwa kukosekana orodha inayoonyesha majina ya wapigakura, haijulikani kama waleta maombi ni miongoni mwa wapigakura au la.

Hakimu Lema alisema walalamikaji hawakuwa makini tangu awali walipofungua shauri hilo, Februari 5 kwani hawakutokea mahakamani hadi Februari 14, wakili wao Nawela alipojitokeza na kuomba nakala ili awapelekee wajibu maombi jambo linalofanya washindwe kuishawishi Mahakama kuwapa haki yoyote kwa kuwa hawakufuatilia shauri lao tangu awali.

Mapema jana mchana, wakili Nawela aliiomba Mahakama itoe zuio la kufanyika uchaguzi huo na iamuru hali ibaki kama ilivyo hadi pale kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi kwa madai ya kwamba walalamikaji katika shauri hilo, hawajapewa haki yao ya kualikwa kushiriki katika uchaguzi huo.

Alidai kuwa iwapo uchaguzi huo utafanyika, basi maombi yao na kesi ya msingi yatakuwa hayana maana.

Akijibu hoja hizo, wakili Jumanne Mtinange kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, aliiomba Mahakama kuyaondoa maombi hayo kwa madai kuwa hayana msingi wowote.

Mtinange alidai hakuna uthibitisho wowote au orodha ya wapigakura kuonyesha kwamba waleta maombi wamekosekana, hivyo maombi ya kutaka hali ibaki kama ilivyo hayana uzito wowote.

Alisema maandalizi ya uchaguzi yana gharama na kwamba ni mara ya tatu umeahirishwa, hivyo kuomba uchaguzi wa leo uendelee kama kawaida.

Timu ya mawakili wa Chadema wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala, Omary Msemo na John Mallya walikuwa muda wote wakifuatilia kesi hiyo mahakamani hapo.

Kwa uamuzi huo, kinyang’anyiro cha kugombea umeya sasa kimebaki kwa Isaya Mwita wa Chadema na Omary Yenga wa CCM wanaowania nafasi hiyo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika leo katika Ukumbi wa Karimjee baada ya kuahirishwa mara tatu kwa sababu mbalimbali ikiwamo zuio batili la Mahakama kabla ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene kuiagiza uchaguzi huo ufanyike kabla ya Machi 25.

Baadaye, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Sarah Yohana alitangaza na kutoa barua kwa wajumbe husika juu ya wito wa kikao cha Baraza la Madiwani kitakachokuwa na ajenda ya uchaguzi akisema wajumbe 163 watashiriki kupiga kura, kati yao 87 ni kutoka Ukawa na 76 CCM.

Raia wa Marekani waandamana kumpinga Donald Trump

$
0
0

Kwa mara nyingine tena mgombea wa kiti cha Republican kwenye uchaguzi wa urais nchini Marekani, Donald Trump amekumbana na vikwazo wakati akijiandaa kwenda kwenye mkutano katika jimbo la Phoenix.

Waandamanaji walifunga barabara katika jimbo la Arizona wakati Trump akijiandaa kwenda kufanya mkutano katika eneo la Phoenix na kumzuia asipite.

Mgombea huyo kiti cha Republican kwenye uchaguzi huo alihutubia wafuasi wake katika eneo la Fountain Hills.

Waandamanaji hao walisababisha msongamano wa magari huku wakibeba mabango ya kumpinga Trump.

Mikutano ya mgombea huyo ilikumbwa tena na fujo hivi karibuni akitakiwa aache ubaguzi anaonyesha kwenye kampeni zake.

Mkutano wa Chicago wiki moja iliyopita ulilazimika kuahirishwa baada ya kutokea kwa maandamano makubwa ya kumpinga.

Mamia ya waandamanaji walikuwa wamekusanyika katika jimbo la Illinois na mapigano kuzuka kati ya wafuasi na waandamanaji katika jukwaa ambalo Trump alipanga kutoa hotuba yake.

Wiki iliyopita Shirika la Utafiti la Kimataifa Economist Intelligence Unit ( EIU) lilisema ikiwa Trump atakuwa rais wa Marekani ushindi wake utakuwa ni miongoni mwa hatari 10 kuu zinazokabili dunia.
Shirika hilo lilisema huenda ikawa ni chanzo cha kuvurugika kwa uchumi wa dunia pamoja na kuongeza hatari za kisiasa na ki usalama dhidi ya Marekani.

Shirika hilo lilisema ushindi wa Trump utakuwa hatari zaidi kwa dunia kushinda hata Uingereza kuondoka kutoka Umoja wa Ulaya (EU) au hata makabiliano ya kivita katika Bahari ya South China Sea.

Kuyumba kwa uchumi wa China au Urusi kuingilia kivita Ukraine na Syria na kusababisha vita baridi vipya ni miongoni mwa mambo ambayo yanachukuliwa kuwa hatari zaidi ya ushindi wa Trump.

“Mpaka sasa Trump ametoa maelezo machache kuhusu sera zake na huwa anabadilisha sana msimamo wake,” EIU walisema kwenye ripoti yao ya utathmini wa hatari zinazokabili dunia.

Utathmini huo huangazia pia athari za jambo fulani na uwezekano wa jambo hilo kutokea.

Vigogo 
Miongoni mwa masuala yanayowatia wasiwasi vigogo wa Republican ni msimamo mkali wa Trump dhidi ya wageni nchini Marekan na kuahidi kujenga ukuta katika mpaka wa kati ya Marekani na Mexico.

Pia, aliahidi kuwarejesha makwao wahamiaji milioni 11, ambao hawajapata hifadhi na kuwazuia raia wa kigeni waislamu kuingia Marekani.

Mitt Romney aliyegombea urais mwaka 2012 kwa tiketi ya Republican amemtaja Trump kuwa tapeli na bondia anayecheza na akili za wapigakura huku mgombea urais wa chama hicho mwaka 2008 John McCain ambaye ni seneta wa jimbo la Arizona akisema sera za kigeni ni hatari.

Kundi la vigogo wa Republican linalopinga azma ya Trump lina muda mchache kumzuia mfanyabiashara huyo tajiri kushinda tiketi ya Republican.

Mgombea huyo anapewa nafasi kubwa ya kuchaguliwa kuwania kiti cha urais kupitia chama chake cha Republic.

Awali kwenye uchaguzi uliopita na yeye alijitutumua kuchukua fomu ili achuane na Rais wa sasa Barack Obama lakini aliangushwa vibaya.

Licha ya kushindwa kuteuliwa kwenye chama chake mwaka huu ameamua kujitutumua kwa mara nyingine tena.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images