Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Maalim Seif Azungumza na Viongozi wa CUF Kisiwani Pemba.....Asisitiza Kutoshiriki Uchaguzi wa Marudio

$
0
0

Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF) visiwani Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amewataka Wazanzibari na wapenda amani kuondoa shaka na kwamba, atatangazwa kuongoza visiwa hivyo.

Maalim Seif ametoa kauli hiyo kwenye viwanja vya Nngoma Hazingwa, Chake Chake Pemba akiwa na viongozi wa wilaya, majimbo na jumuiya za chama hicho ikiwa ni siku moja baada ya kufanya mkutano wa namna hiyo Unguja.

Kiongozi huyo ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF amesema kuwa, ukweli umedhihiri ndani na nje ya nchi na kwamba hakuna sababu ya kutotangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana.

Amesema,“Jumuiya na waangalizi wote wa uchaguzi wa kitaifa na kimataifa wameshuhudia uchaguzi huo na kujiridhisha kuwa ulikuwa huru, haki na wa uwazi na wanaendelea kushikilia msimamo wao kutaka mshindi wa uchaguzi huo atangazwe.”

Amesisitiza kuwa CUF haitoshiriki uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi mwaka huu kauli ambayo pia imeungwa mkono na wafuasi wa chama hicho Pemba kama ilivyokuwa Unguja.

Mapema Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui amemtaja Maalim Seif kuwa kiongozi aliyebobea kisiasa na anayejali maslahi ya Wazanzibari.

Katika hatua nyingine mawakilishi na madiwani wateule wa CUF  wamepanga kwenda mahakamani kutetea nafasi zao.

Wameeleza kwamba, kwa kuwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imewapa hati za ushindi baada ya kufanya uchaguzi mkuu tarehe 25 Oktoba 2015, mpaka sasa hakuna aliyejitokeza kupinga ushindi wao.

Hata hivyo, Maalim Seif amesema, viongozi hao waliochaguliwa na wananchi katika uchaguzi huo na kisha kupewa shahada zao, watakwenda mahakamani kutetea nafasi zao na kutoruhusu viongozi wengine wa ngazi hizo kuchaguliwa tena kwa vile wao wanavyo vielelezo vyote vya kuchaguliwa kwao.

Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi yaliyobandikwa katika vituo vya kupigia kura na kuthibitishwa na wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo, majimbo yote 18 ya uchaguzi Kisiwani Pemba yalichukuliwa na CUF, sambamba na wadi zote 32 za uchaguzi.

Serikali Yalaani Kitendo Cha Kudhalilishwa Kwa Mtanzania Nchini India

$
0
0

Serikali ya Tanzania imesikitishwa na inalaani vikali kitendo cha udhalilishwaji alichofanyiwa mwanafunzi wa kike wa Kitanzania na Kundi la watu katika jimbo la Bangalore nchini India.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi alipokutana na Wandishi wa Habari kwa ajili ya kuwaeleza hatua zilizochukuliwa na Serikali kufuatia kitendo hicho cha kudhalilishwa kwa mwanafunzi wa Kitanzania nchini India.
 
Balozi Mwinyi alisema kuwa, hatua zilizochukuliwa ni pamoja na Ubalozi wa Tanzania nchini India kuiandikia Serikali ya nchi hiyo kuomba maelezo kamili kuhusu tukio hilo pamoja na kuitaka Serikali ya India kuwachukulia hatua za kisheria watu wote waliohusika pamoja na kuimarisha usalama katika maeneo wanayoishi wanafunzi wa Kitanzania. 
 
Aidha, Balozi Mwinyi alieleza kuwa amemwita Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Sandeep Arya na kumweleza masikitiko ya Serikali ya Tanzania kufuatia kitendo hicho cha kushambuliwa na kudhalilishwa kwa mwanafunzi wa kike kutoka Tanzania.
 
Katika mazungumzo yao, Balozi Arya alieleza bayana kuwa Serikali ya India imesikitishwa na tukio hilo la udhalilishaji na kwamba Serikali imeahidi kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kutekeleza uovu huo.
 
Alisema kuwa Waziri Mkuu wa Jimbo la Bangalore aliongea na umma kuelezea masikitiko yake kuhusu uovu huo na kuahidi kuwa mamlaka za jimbo hilo zitaimarisha usalama katika maeneo yote wanayoishi wanafunzi wa Tanzania na raia wengine kutoka nje.
 
Balozi Arya aliihakikishia Serikali ya Tanzania kuwa India inaheshimu ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na nchi yake, hivyo itashughulikia suala hilo kwa ukamilifu na hadi wakati huu tayari watu watano wanashikiliwa na vyombo vya usalama wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo.

Sanjari na taarifa hiyo, Balozi Mwinyi aliwaomba Watanzania kutohusisha tukio hili la uhalifu na ajali ya Mtanzania, Bw. Christian Benjamin Mlyansi iliyotokea nchini India jana usiku na kusababisha kifo chake.

Alisema kuwa Bw. Mlyansi alipata ajali ya kawaida alipokuwa anaendesha pikipiki ambapo ilipoteza mwelekeo na kugonga ukingo wa kati wa barabara.

Mke wa Kafulila atimuliwa nje ya ukumbi wa bunge

$
0
0

Mbunge wa Viti maalum Chadema Jesca Kishoa ametolewa nje ya ukumbi wa bunge na kutakiwa kutohudhuria vikao viwili vya bunge linaloendelea mjini Dodoma.

Hayo yamejiri katika mkutano wa 7 wa bunge la 11 linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma ambapo Mwenyekiti wa kikao cha leo Andrew Chenge amelikumbusha bunge kuhusiana na kauli aliyoitoa mbunge huyo tarehe 01/02/2016.
  
Mbunge huyo alisema kwamba Waziri Harrison Mwakyembe alihusika kununua mabehewa feki 274 jambo ambalo lilizua mjadala mkali na bunge kumtaka mbunge huyo atoe ushahidi ndani ya siku 3.

Mwenyekiti Andrew chenge amesema kuwa mbunge huyo alitakiwa kwa mujibu wa kanuni za bunge kanuni ya 63(6) atoe ushahidi kwa ofisi ya bunge na ndani ya siku zote ofisi ya bunge haijapata ushahidi huo.

Kutokana na Mbunge huyo ambaye pia ni mke wa aliyekuwa mbunge wa Kigoma kusini David Kafulila NCCR Mageuzi kushindwa kutekeleza maamuzi ya bunge mwenyekiti wa bunge amemtaka kufuta kauli yake na mbunge huyo akakaidi ndipo Mwenyekiti akamuamuru atoke nje mara moja na kutohudhuria vikao vya bunge kwa siku zilizobakia 2.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa Ya Februari 5

Lowassa Aunga Mkono Maamuzi Ya CUF Kutoshiriki Uchaguzi Zanzibar

$
0
0
Ni dhahiri kuwa aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema bado ana ndoto za kuwa rais wa Tanzania baada ya kurudia kauli yake ya kwenda Ikulu, lakini safari hii akisema chama hicho kitaingia Ikulu bila ya kumwaga damu.

Lowasa alisema hayo jana katika mkutano ulioandaliwa na Baraza la Wazee wa Chadema, tawi la Ubungo kwa ajili ya kumpongeza kwa ushupavu aliounyesha baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana.

“Siku moja tutaingia Ikulu bila kumwaga damu. Msiwe na wasiwasi kwa sababu mimi, dunia na Watanzania wanafahamu kuwa tulishinda katika uchaguzi uliopita,” alisema Lowassa ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Nne kabla ya kujiuzulu.

Lowasa alisema ingawa ana uhakika kuwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita yalichakachuliwa, aliweka mbele amani.

“Nawashukuru Watanzania kwa kunisikiliza, walikuwa wananisikiliza mimi tu baada ya uchaguzi. Ningeweza kuwaambia twende barabarani, sikufanya hivyo kwa sababu najua amani ni muhimu,” alisema.

Uchaguzi wa Zanzibar 
Waziri huyo mkuu wa zamani pia alizungumzia uamuzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutangaza kurudiwa kwa uchaguzi wa rais, wawakilishi na madiwani Machi 20, akitahadharisha kuwa suala hilo linaweza kusababisha mpasuko.

“Hali ya Zanzibar isiposhughulikiwa kwa umakini na umahiri, italeta matatizo makubwa nchini,” alisema.

Alimtaka Rais John Magufuli, akiwa kiongozi wa Tanzania, kuchukua uamuzi na kuhakikisha suala la Zanzibar linatatuliwa.

Alisema UKAWA  inaunga mkono maamuzi ya  CUF kupinga uchaguzi huo kurudiwa kwa kuwa hakuna ushahidi wa kukiukwa kwa taratibu zozote za uchaguzi wa mwaka jana.

“Nashauri wakae chini wazungumze, kwa nini hili la sasa linashindikana wakati CUF walikubali Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwa miaka mitano?” alihoji.

Alisema amani ni jambo la muhimu na linatakiwa lipewe kipaumbele kabla ya uamuzi mwingine kufanyika.

Kuhusu mikakati ya kukiboresha chama, Lowassa, ambaye alipata kura milioni 6.07 na kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais Magufuli aliyepata kura milioni 8.8, alisisitiza uamuzi wake wa kufanya ziara nchi nzima kuwashukuru Watanzania wote ambao walimpigia kura na ambao hawakumpigia.

Lowassa pia alizungumzia uhuru wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), akiituhumu kuwa inaendeshwa na chama tawala.

Alisema katika uchaguzi uliopita, NEC ilipotosha matokeo na kuharibu mchakato wa uchaguzi.

“NEC ilifanya mambo ya hovyo, walipaswa kufukuzwa, ni uongo kusema kuwa ipo huru,” alisema.

Awali, kabla ya Lowassa kusema hayo, mwenyekiti wa wazee hao wa Chadema, Enock Ngombale alisoma risala ambayo ilimpongeza kwa ushupavu aliounyesha kabla na baada ya uchaguzi.

Katika risala hiyo, Ngombale alisema Watanzania wanajua kuwa Lowasa alishinda uchaguzi, lakini walishangazwa na matokeo.

“Wewe ni kiongozi imara, shupavu na mahiri. Watanzania waliamini kuwa ulishinda lakini kilichofanyika ni uchakachuzi,” alidai.

Kadhalika, risala hiyo ilisema Serikali ya Rais Magufuli haifuati sheria na kanuni za utawala bora.

“Tumeona unyanyasaji mkubwa kwa wafanyabiashara, bomobomoa ambayo haifuati misingi ya haki za binadamu,” alisema.

Pia, wazee hao walimshauri Lowassa mambo mbalimbali ya kukiimarisha chama.

Nape Nauye Aanika Siri Ya Mafanikio Ya CCM Kuendelea Kushika Dola

$
0
0

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kushika dola licha ya upinzani mkali kutoka vyama vingine vya siasa hasa vile vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwake, yanaandika historia nyingine ya chama hicho tangu kuanzishwa kwake Februari 5, 1977.

Chini ya Baba wa Taifa Mwalimu, Julius Nyerere chama hicho ambacho ni cha pili kwa ukubwa barani Afrika kikitanguliwa na ANC cha Afrika Kusini, kinajivunia mambo mengi yaliyokifanya kudumu mpaka sasa wakati vyama vikongwe vya nchi nyingine kama Zambia (UNIP), Kenya (Kanu) na Malawi vikiwa vimeshaondolewa madarakani.

Nape ataja siri ya mafanikio 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye anasema mfumo wa chama hicho kujiimarisha kimtandao kuanzia ngazi ya shina kwa maana ya balozi wa nyumba kumi mpaka taifa umekifanya kiendelee kuwa kimbilio la wananchi wengi hadi kufikia kupata wanachama zaidi ya milioni sita, kutoka wanachama wachache waliokuwapo miaka iliyopita.

“Chama chetu kimeendelea kuwa na sura ya kitaifa, kalenda inayojulikana ambayo imekuwa ikiruhusu chaguzi kila baada ya miaka mitano na kuifanya Tanzania kuwa nchi inayofuata misingi ya kidemokrasia,” anasema.

Yapo baadhi ya mambo ambayo chama hicho kinajivunia kwa miaka 39 tangu kizaliwe. 

Kuendelea kushika dola 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Patrick Myovela anasema mafanikio ya chama hicho ni pamoja na ushindi kwenye chaguzi mbalimbali zilizowawezesha kuendelea kushika dola.

“Tumepata ushindi uliotuwezesha kushika dola katika chaguzi kuu zilizofanyika zaidi ya mara sita. Tumeishi kwenye shabaha ya chama chetu ile inayotaka kuendelea kuwa madarakani, tukiunda na kusimamia Serikali,” anasema.

Myovela ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anasema, CCM bado inaaminiwa na Watanzania wengi ndiyo maana wameendelea kukipa kura na kukiwezesha kuunda Serikali. Hiyo imetokana na imani ya wananchi juu ya chama hicho.

Nape anasema mara zote CCM imekuwa ikichagua mgombea urais atakayeweza kushika bendera ya chama hicho kwa umakini zaidi kwa kuzingatia matakwa ya wananchi kwa wakati husika.

Uongozi wa kupokezana 
Kati ya vitu ambavyo vimeiletea sifa kubwa Tanzania ni pamoja na kuwa na uongozi wa kupokezana madaraka. 

Wakati nchi nyingine ikiwamo Uganda, Burundi na Zimbabwe zikivurugana kutokana na vyama vinavyotawala kushindwa kuenzi dhana ya kupokezana, tayari Tanzania imeshapitia awamu tano za uongozi na kila awamu ikiongozwa na rais tofauti.

“Baada ya kuongoza miaka 23, Mwalimu Nyerere aliamua kung’atuka akimuachia Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ambaye aliingia kwa kupigiwa kura licha ya kuwapo kwa mfumo wa chama kimoja,” anasema Nape.

Anasema uongozi huo wa nchi  kupokezana ulimfanya Rais wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa kushikilia usukani akimpokea Mwinyi hadi mwaka 2005 alipomkabidhi Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete na mwaka jana Rais John Magufuli.

Myovela anasema ni dhahiri taswira nzuri ya uongozi wa nchi inatokana na uimara wa chama kilichopo madarakani. 

Demokrasia ya vyama vingi
Licha ya kuwapo kwa mabadiliko ya kidemokrasia hususan mfumo wa vyama vingi ulioasisiwa na CCM yenyewe mwaka 1992, chama hicho kimeendelea kushamiri huku kikishinda chaguzi zote kuu na zile za mitaa.

Nape anasema wakati CCM iliamua kuasisi mfumo huo, wananchi wengi walitamani kiendelee kuwa peke yake.

“Kumbuka kwamba wakati wa kura ya maoni ya kuendelea kuwa na mfumo wa chama kimoja au kuwa na vyama vingi vya siasa, Watanzania wengi walipendekeza kuendelea kuwapo kwa chama kimoja, lakini kutokana na demokrasia, CCM iliamua kuruhusu mfumo wa vyama vingi kuanza nchini,” anasema.

Mpaka sasa Tanzania ina vyama vya siasa zaidi ya 20 vilivyosajiliwa, vingi vikiwa vimefanikiwa kushiriki katika chaguzi mbalimbali.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Iringa, Enock Ugulumu ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Iringa anasema kama kingeendelea kuwa na mgombea mmoja kila kinapoingia madarakani, uhakika wa kuwapo mpaka leo usingekuwapo.

“Mfumo wa kubadilishana uongozi ndiyo siri kubwa ya ushindi wa CCM, hatung’ang’anii madaraka kwa sababu Katiba ya CCM imeruhusu demokrasia tangu ndani, mpaka nje kwenye umma.

"Vinginevyo Mwenyekiti wa CCM Taifa asingetaka kutoka kwa miaka yote, angebaki kuwa yuleyule,” anasema.

Vipo vyama ambavyo vimeshindwa kuzingatia mfumo wa kubadilishana madaraka kwa kuwa na viongozi wale wale tangu kuanzishwa kwake.

 Katiba Mpya 
Mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya unaonyesha namna ambavyo CCM ilivyofanikiwa kupokea na kufanyia kazi ushauri na mapendekezo yanayotolewa na wananchi kutoka katika kada zote.

Nape anasema CCM inajivunia kuwa na mchakato huo hata kama haujafikia mwisho. Anasema uwepo wa rasimu iliyopita kwenye Bunge la Katiba kunaifanya CCM ionekane inasikiliza maoni ya Watanzania na kuyatumia inapowezekana.

“Ni chama kilichodumu kwa muda mrefu, kinajivunia kuwa kisikivu na kutimiza mahitaji ya Watanzania.” Anasema bila nia njema ya kukubali mchakato huo uwepo, usingeanzishwa na kufikia hatua ya kura za maoni ilipo sasa.

Kulinda na kudumisha amani nchini
Nape anasema katika tunu za taifa mbazo CCM inajivunia kuziendeleza tangu uhuru kuwa ni kulinda na kudumisha amani.

Katika miaka yote, CCM imekuwa ikiagiza na kusimamia kuhakikisha Serikali inalinda na kudumisha misingi imara ya amani iliyoasisiwa na waanzilishi wa taifa.

Hata hivyo, anasema CCM imeshiriki katika harakati za kutafuta ukombozi wa nchi majirani ili kujihakikishia usalama ndani na  nje ya nchi 

Uhuru, umoja na mshikamano .
Myovela anasema ni ukweli usiopingika kuwa umoja na mshikamano uliopo nchini unatokana na usimamizi mzuri wa Serikali inayoundwa na chama hicho.

Anasema kutokuwa na ubaguzi wa aina yoyote ile ikiwamo udini, ukabila, rangi wala ukanda unatokana na misingi mizuri iliyowekwa na chama hicho tangu kuundwa kwake. 

Nape anasema kitendo cha kuwa na ilani za uchaguzi zinazogusa maisha ya watu wa kila kada, kimeisaidia Serikali kutimiza wajibu wake.

“Kila mwaka wa uchaguzi, CCM imekuwa ikiisimamia Serikali katika kutimiza majukumu yake kupitia ilani ya uchaguzi. Ukisoma ilani zote utagundua CCM haikurupuki, inafanya mambo yake kwa umakini mkubwa. Hili tunajivunia,” anasema Nape.

Anasema msingi wa utawala bora lazima uendane na kile ambacho chama kingependa wananchi wake wafanyiwe kwa kuiagiza Serikali kupitia ilani yake.

Anasema viongozi wa Serikali wamekuwa wakitoa taarifa ya utekelezaji wao wa majukumu kwa chama ili kipate nafasi ya kukosoa na kusonga mbele.

Utawala bora 
Nape anasema Watanzania wameshuhudia uanzishwaji wa mikoa, wilaya, kata na vijiji vipya ili kuwasogezea huduma karibu. 

Maazimio 
Anasema kuna maazimio mbalimbali likiwamo Azimio la Mtowisa lililotaka kila kaya kujitosheleza kwa chakula na Azimio la Zanzibar lililofungua Demokrasia ya ndani ya CCM, haya yote yamechangia katika mafanikio ya CCM.

CT-Scan Iliyopelekwa Muhimbili Ilikuwa Ya UDOM

$
0
0

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto imekiri kwamba mashine ya CT Scan iliyofungwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ilikuwa ni ya kituo cha kisasa cha kutolea huduma za afya cha Benjamin Mkapa kilichopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Akijibu swali la nyongeza bungeni mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Khamis Kigwangalla alisema mashine hiyo iliingia nchini kwa lengo la kupelekwa katika kituo hicho lakini ikapelekwa Muhimbili kutokana na kutokamilika kwa majengo ya kufungwa mashine hiyo katika kituo hicho.

Alisema, uamuzi huo waliuchukua pia kwa sababu hela ya kununua mashine nyingine ambayo itapelekwa kufungwa katika kituo hicho ilikuwepo na kwa sasa mchakato wa ununuzi unaendelea.

Dk Kigwangalla alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM) aliyetaka jibu la Serikali kama ni kweli ilichukua mashine ya kituo hicho na kufunga katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ama ilinunua.

Awali katika swali la msingi msingi, Nkamia alitaka kujua mpango wa Serikali wa kununua mashine mpya ya CT -Scan kwa ajili ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.

 Kuhusu hilo, Dk Kigwangalla alisema, Desemba mwaka jana Serikali ilipeleka mashine ya CT-Scan katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo inatumia teknolojia ya kisasa yenye X-ray tube mbili na uwezo wa kupiga picha ya 128 slice mara mbili.

Mwenyekiti Wa Kijij Chadema Akataliwa

$
0
0

Wakazi wa Kitongoji cha Misungwi D, Kijiji cha Misungwi wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza wamemkataa Mwenyekiti wao, Raphael Kimoka (Chadema) kwa tuhuma za kutowasomea taarifa za mapato na matumizi ya fedha tangu achaguliwe.

Walitoa msimamo huo kwenye mkutano mkuu wa kitongoji uliofanyika juzi.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Misungwi, Amos Seko alisema wakazi hao wamekuwa wakishindwa kufanya shughuli za maendeleo, huku wakiendelea na vikao na kuweka maazimio ya kutokuwa na imani na mwenyekiti wao.

“Leo ni kikao cha mwisho kuhusiana na malalamiko yenu dhidi ya mwenyekiti mliyoyaleta tangu Oktoba 27, mwaka jana. Mtaamua wenyewe hapa ama aendelee au la,” alisema Seko.

Seko alisoma tuhuma nyingine dhidi ya mwenyekiti zilizopelekwa kwake na wakazi hao kuwa ni kutosimamia majukumu yake vizuri, kubagua wananchi wakati wa kutoa huduma, kutohudhuria vikao vya kitongoji vya maafa na kutetea uhalifu.

Mwakilishi wa mkuu wa wilaya ambaye ni Ofisa Tarafa wa Misungwi, Peter Marco alisema tuhuma dhidi ya mwenyekiti huyo ziliwasilishwa kwenye kikao cha halmashauri ya kijiji cha Novemba 11, mwaka jana, Alisema kiongozi huyo alipewa nafasi ya kujitetea, lakini hakufanya hivyo badala yake alitoka nje ya kikao.

Kimoka alipopewa nafasi ya kujitetea, alidai kuwa mkutano huo umeandaliwa kisiasa, hivyo hautambui kwa sababu wengi wao ni wanachama wa CCM.

“Waliohudhuria hawakunitendea haki, sikubaliani nao,” alisema.

Aliongeza kuwa, kwa muda mrefu alijua kulikuwa na mpango wa kutaka kumuondoa madarakani wenye msukumo wa kisiasa.

Serikali Yajieleza Bungeni Kinachosababisha Umeme Ukatike Mara Kwa Mara

$
0
0

Serikali  imesema tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara nchini linatokana na uchakavu na kuzidiwa kwa vituo vya kupoza umeme na miundombinu ya usafirishaji na usambazaji nishati hiyo.

Katika kukabiliana na tatizo hilo Tanesco inachukua hatua za kujenga mifumo ya njia kubwa za umeme wa msongo wa kilovoti 400 (Iringa- Dodoma-Singida-Shinyanga), gridi ya Kaskazini Mashariki (Dar es Salaam, Chalinze,Tanga –Arusha), ya Kaskazini Magharibi (Geita- Kagera –Katavi- Kigoma- Rukwa na Mbeya) na Makambako- Songea wa kilovoti 220.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani wakati akijibu swali la Mbunge wa Magu, Boniventure Kiswaga (CCM). 

Kiswaga alitaka kufahamu serikali imejipangaje kukabiliana na tatizo la kukatika katika kwa umeme.

Pia mbunge huyo alitaka kufahamu, Je serikali itakamilisha lini kupeleka umeme katika vijiji vya jimbo hilo ikizingatiwa mpaka sasa ni asilimia 20 tu ya vijiji ndiyo vina umeme. 

Kalemani akijibu swali hilo, alisema tatizo la kukatika kwa umeme linatokana na uchakavu na kuzidiwa kwa miundombinu ya kupoza umeme pamoja na matukio ya kulipuka kwa transfoma yanayosababishwa na radi hasa kipindi cha mvua pamoja na wizi wa mafuta ya transfoma unaofanywa na wananchi wasio waaminifu.

Alisema Tanesco inakamilisha upanuzi wa usambazaji wa umeme katika majiji makubwa ya Arusha, Dar es Salaam, na Mwanza ambapo kazi hizo zitahusisha ujenzi wa njia mpya za umeme na kupanua vituo vya kupoza umeme.

“Kukamilika kwa kituo cha kupoza umeme cha KIA mkoani Kilimanjaro kumeimarisha upatikanaji wa umeme maeneo ya Mirerani na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA),” alisema Kalemani.

Pia vituo vya kupoza umeme katika jiji la Dar es Salaam vya Gongo la Mboto, Kipawa, Mbagala, na Kurasini vitaunganishwa kwa njia ya sakiti mzunguko kutoka Ubungo na Kinyerezi kuanzia Machi mwaka huu.

Rais Magufuli Asema Yeye si Kichaa wala Dikteta......Aahidi Kuifanyia Mema Nchi hata Akifa awe Rais wa Malaika

$
0
0
RAIS Dk. John Magufuli amesema anapochukua hatua yeye si kichaa, si dikteta, si shetani wala si mnyama, ila ni mpole, lakini amefika mahali lazima afanye hivyo kwani ndani ya Serikali yanafanyika mambo ya ajabu.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam katika kilele cha Siku ya Sheria nchini, alipokuwa mgeni rasmi kwa mara ya kwanza katika uzinduzi wa Mwaka wa Mahakama tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisifu kazi kubwa inayofanywa na Idara ya Mahakama, huku akitangaza uamuzi wa gharama za kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Bunge zaidi ya Sh bilioni nne ni bora zikawasaidia wananchi.

“Ninapochukua hatua mimi si mnyama, si dikteta, si shetani, ni mpole kweli, lakini inafika mahali lazima nifanye, yanayofanyika serikalini ni mambo ya ajabu sana, nataka kutoa sadaka yangu, inawezekana hata nikifa naweza kuwa rais wa malaika,” alisema.

Alipongeza kazi kubwa inayofanywa na mahakama huku akibaki kujiuliza kwanini katika maadhimisho ya siku yao hawarushi matangazo yao moja kwa moja kupitia luninga.

“Mnafanya kazi kubwa, nilipofika niliuliza kwanini hii siku yenu hamrushi ‘live’, nikajibiwa fedha za kurusha ‘live’ zinapelekwa kuwahudumia wananchi.

“Kipindi kimoja kurusha ‘live’ kwa wiki mbili inatumika zaidi ya Sh bilioni nne, ni vizuri kuzikata hizo fedha zinazopelekwa kurusha ‘live’ zikapelekwa katika kesi za ubunge zinazohitaji shilingi bilioni tatu kusikilizwa hadi kumalizika kwake,” alisema.

Alisema mahakama ilikuwa inapewa bajeti ya Sh bilioni 41, lakini mwaka 2015/2016 ilishuka wakatakiwa kupewa Sh bilioni 12 ambazo hadi sasa hawajapewa.

“Kiongozi lazima ufikirie wapi pa kupeleka fedha na wapi pa kunyima, watu wa mahakama mnafanya kazi ya Mungu, nawaahidi ndani ya siku tano nitakuwa nimewapa Sh bilioni 12 zote.

“Sina tatizo la masilahi ya wafanyakazi wa mahakama, katika bajeti ya mwaka huu nitawapa fedha nyingi kuliko bajeti zote zilizopita, fedha zipo,” alisema.

Mahakimu Kutumbuliwa
Rais Magufuli alisema anamwagiza Jaji Mkuu kuwachukulia hatua mahakimu 502 ambao hawakufikia malengo ya kumaliza kesi 250-260 kwa mwaka. Walimaliza kesi chini ya 100.

“Mahakimu ambao hawajafikia kumaliza kesi 260 hayo ndiyo majipu yako Jaji Mkuu, unatakiwa kuyatumbua, wewe uliniapisha hata mimi, leo unapitisha agizo mwingine anapinga.

“Unatoa siku saba sasa sijui ndiyo watamaliza kutoa hizo hukumu, nakuagiza wachukulie hatua, tusipochukua hatua hakuna kitakachofanyika.

“Walioshindwa kufikia lengo unawabakiza wa nini, wasomi wako wengi, hata ukitangaza leo watajitokeza, niruhusu mimi nitangaze, sitaki kuingilia mahakama,” alisema.

Mabilioni ya NIDA
Akizungumzia hatua yake kwa watendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), alisema ilipewa Sh bilioni 176.6, lakini vitambulisho vilivyotengenezwa havifiki hata milioni mbili na havina sahihi wakati vitambulisho vya kupigia kura fedha iliyotolewa haizidi Sh bilioni 70, lakini vina sahihi za wapigakura wote wa Tanzania ambao ni milioni 23,253,982.

“Utaona ugumu wa kuongoza, nchi inatawaliwa na madudu ya kila aina, wapo watu wanacheza na fedha wanavyotaka wakati wapo watu masikini sana, wengine wanataka bodi zao wakakae Ulaya.

“Hapo ndipo tulipofikia, wengine wanalipwa mshahara kwa mwezi Sh milioni 35, naomba mniombee kabla ya kunihukumu, toeni hukumu kwa haki kwa hawa wanaotaka kuifikisha nchi pabaya, toeni hukumu zao haraka,” alisema.

Kesi za Wakwepa kodi
Rais Magufuli alisema kuna kesi 442 za kukwepa kodi ambazo zingeamuliwa Serikali ingepata Sh trilioni moja, ambayo ingeweza kununua ndege zaidi ya sita.

Alimuomba Jaji Mkuu kuzimaliza kesi 442 na kama zikimalizika fedha hizo Sh trilioni moja ataipa Idara ya Mahakama Sh bilioni 259 na Sh bilioni 750 zilizobakia zitanunuliwa ndege sita na wafanyafakazi 250 ATCL waliopo sasa wataondolewa.

Akizungumzia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alisema kuna kesi 26 za watu waliokutwa na nyara za Serikali, ambazo zipo zaidi ya miaka mitano hazijaamuliwa kwa sababu upelelezi bado.

“Polisi wapo, DPP yupo, upelelezi unaendelea kila siku, hapo unaona tatizo lilipo, DPP upo unapeleleza nini au unatafuta rushwa?” alisema.

Alisema suala la kuanzishwa kwa mahakama ya mafisadi ya wahujumu uchumi halihitaji kwenda bungeni kufanya mabadiliko, lifanywe haraka, mahakama ianze kwani nchi inachezewa.

Pamoja na hali hiyo Rais Magufuli alikubali kupokea maombi yote yaliyotolewa na mahakama na kuyazingatia kwani lazima ayaunge mkono ikiwamo kukubali watumishi wa Idara ya Mahakama wasome na kupatiwa mikopo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

“Nimeamua nchi iende na itaenda, anayefikiria ataikwamisha atakwama yeye, nategemea zaidi mahakama katika kufanikisha hilo,” alisema.

Bilioni 60 Zatengwa Kufufua Kiwanda Cha Matairi cha General Tyres Arusha

$
0
0

Shillingi Billioni 60 zinategemea kutumika kufufua kiwanda ya matairi cha General Tyres kilichopo Jijini Arusha ambacho kimesharudi mikononi mwa Serikali, na fedha hizo zitatumila kurekebisha mitambo ya umeme ya kiwanda hicho na kupata mitambo mipya itakayoendana na teknolojia ya utengenezaji wa matairi duniani.

Akijibu swali la Mhe. Joshua Nassari Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) lililouliza ni lini serikali itafufua kiwanda cha matairi cha General Tyres kilichopo Jijini Arusha kwani ni tegemeo kwa ajira kwa wananchi wa Jijini la Arusha,Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles John Mwijage amesema kiwanda hicho kimesharudi mikononi mwa Serikali na wako mbioni kukifufua ili kianze kufanya kazi ya kuzalisha matairi nchini.

“ Tumeanzisha viwanda nchi ili kuzalisha bidhaa na kutoa ajira kwa watanzania na sio kuwatesa wananchi kwa kukosa ajira au kuagiza bidhaa ambazo tunaweza kuzalisha hapa hapa nchini, hivyo basi Serikali kupitia Wizara yangu tutatenga fedha kwa ajili ya kufufua kiwanda hiki ili kianze kufanya kazi mara moja”

“ Sio tu tutafufua kiwanda cha General Tyres pekee bali tunafatilia viwanda vyote ambavyo vimekiuka sheria na kanuni kwa kutoviendeleza viwanda hivyo ili kuvirudisha mikononi mwa Serikali au kuwatafuta wawekezaji wengine watakaoweza kuviendesha viwanda hivyo” Alisema Mhe. Mwijage.

Aidha Mhe. Charles  John Mwijage amesema ni kweli makampuni mengi yaliyobinafsishwa hayakufanya vizuri katika uendeshaji wake ukiacha mifano ya makampuni machache yanayofanya vizuri yakiwemo Tanzania Breweries Limited (TBL),Morogoro Polyester 21st Century na Tanzania Cigarette Company Limited (TCC), hivyo Wizara yangu ikishirikiana na Msajili wa Hazina juu ya Viwanda ilifanya tathmini iliyoonesha kuwa mashirika mengi yaliyobinafsishwa hawakutekeleza mikataba ya mauziano kikamilifu.

Ameongeza kuwa lengo ni kuhakikisha makampuni yote haya yanazalisha kwa tija ili tupate bidhaa,kodi ya Serikali na ajira kwa wananchi wa Tanzania ili kutimiza adhma ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuli ya kuwa na Tanzania yenye viwanda kwa maendeleo ya taifa.

Serikali kupitia Wizara yetu inaboresha mazingira ya uwekezaji hali itakayowajengea imani kwa wawekezaji na kupelekea kupanua zaidi shughuli zao za kibiashara na pia kuendeleza mpango wa Viwanda vidogo na vya kati unaoshirikisha SIDO na Halmashauri za Wilaya na Mikoa ili kuanzisha Viwanda vya Mkoa vya kuongeza thamani ya bidhaa za Kilimo,Uvuvi na ufugaji kupitia njia hii ajira nyingi zitaongezeka na kupunguza tatizo la ajira nchini.

January Makamba Awapa Makavu Wapinzani

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, amewataka baadhi ya wabunge wa upinzani kuwa na lugha nzuri dhidi ya serikali ili waweze kupata ushirikiano mzuri na viongozi hao pamoja na serikali.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano) Mh. January Makamba amefunguka na kusema kuwa wao kama Chama cha Mapinduzi ndiyo wenye dola na wao ndiyo wanaongoza serikali hivyo amewataka baadhi ya wabunge wa upinzani kuwa na lugha nzuri dhidi ya serikali ili waweze kupata ushirikiano mzuri na viongozi hao pamoja na serikali hiyo pindi watakapo hitaji msaada wowote kutoka serikalini.

January Makamba amesema hayo bungeni na kudai amefadhaishwa na michango ya wabunge wa upinzani ambao walikuwa wakitumia lugha za kuudhi dhidi ya Rais pamoja na viongozi wa serikali.

"Najua kazi ya upinzani ni kulaumu hivi nyinyi wapinzani kwa kazi anayofanya Rais Magufuli leo mngepewa nafasi wapinzani ni kipi ambacho mngefanya zaidi ya hiki? "Alihoji January Makamba

Lakini katika hatua nyingine amesema aina ya uchangiaji nyingine ya wabunge bungeni ni kama walikuwa wakiwatisha watanzania juu ya sakata la Zanzibar na alimaliza kwa kusema kuwa utatuzi wa suala la Zanzibar haupatikani barabarani, haupatikani bungeni bali unapatikana katika Katiba na sheria za Zanzibar pekee na si kitu kingine.

Mbowe Atangaza Baraza lake la Mawaziri Bungeni Leo

$
0
0

Kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani bungeni Freeman Mbowe ametangaza baraza lake la mawaziri kivuli leo bungeni mjini Dodoma.

Mbowe, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chadema ametaja baraza lake ambalo litakuwa na lengo la kuishinikiza serikali ya Rais Magufuli kutimiza kile alichoahidi kwa Watanzania.

Baraza hilo ni kama ifuatavyo;

1.Wizara ya Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.

Mawaziri – Jaffar Michael

Naibu Waziri – Joseph Nkundi na Ruth Mollel

2.Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira

Waziri – Ali Saleh Abdalla

Naibu Waziri – Pauline Gekul

3.Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu

Waziri – Esther Bulaya

Naibu – Yusuph Makame na Maftah Abdalla

4.Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi

Waziri – Magdalena Sakaaya

Naibu Waziri – Emmaculate Swari

5.Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Waziri-Inj. James Mbatia

Naibu Waziri Willy Kombucha

6.Wizara ya Fedha na Mipango

Waziri – Halima Mdee

Naibu Waziri – David Silinde

7.Wizara ya Nishati na Madini

Waziri – John Mnyika

Naibu Waziri – John Heche

8.Wizara ya Katiba na Sheria

Waziri – Tundu Lissu

Naibu Waziri Abdalla Mtolela

9.Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

Waziri – Peter Msigwa

Naibu Waziri – Riziki Shaghal

10.Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Waziri – Juma Omari

Naibu Waziri Mwita Waitara

11.Wizara ya Mambo ya Ndani

Waziri – Godbless Lema

Naibu Waziri Masoud Abdalla

12.Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Waziri – Wilfred Lwakatare

Naibu Waziri – Salum Mgoso

13.Wizara ya Maliasili na Utalii

Waziri Esther Matiko

Naibu Waziri– Cecilia Pareso

14.Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Waziri Anthony Komu

Naibu Waziri Cecil Mwambe

15.Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi

Waziri – Suzan Lyimo

Naibu Waziri Dkt. Ali Suleiman Yusuph

16.Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Waziri – Dkt. Godwin Mollel

Naibu Waziri Zubeda Sakul

17.Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo

Waziri – Joseph Mbilinyi

Naibu Waziri – Devotha Minja

18.Wizara ya Maji na Umwagiliaji

Waziri – Hamidu Hassan

Naibu Waziri– Peter Lijualikali

==> Msikilize Mbowe akitangaza Baraza hilo Leo Bungeni

Rais Dkt. Magufuli Awasalimia Wananchi Wa Msamvu Mkoani Morogoro Leo Wakati Akiwa Njiani Kuelekea Dodoma

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka watu wote waliotelekeza Mashamba na Viwanda walivyouziwa na serikali, kuhakikisha wanafufua mashamba na viwanda hivyo mapema iwezekanavyo, kabla serikali haijavinyang'anya na kuwagawia wanaoweza kuviendesha.

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake njiani, wakati akisafiri kwa gari kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma.

Amesema mkoa wa Morogoro ulikuwa na viwanda vingi na mashamba mengi makubwa ambayo kama waliouziwa wangeyaendeleza, yangezalisha ajira na kuongeza uzalishaji wa bidhaa za viwandani na Mazao ya kilimo, lakini waliouziwa mashamba na viwanda hivyo wameamua kutelekeza ama kubadilisha matumizi, huku wengine wakitumia rasilimali hizo kuombea mikopo katika mabenki jambo ambalo serikali yake haitalikubali.

"Kama nilivyowaahidi wakati wa kampeni na leo narudia, wote walioamua kutumia mashamba na viwanda walivyouziwa na serikali kwa ajili ya kuchukulia mikopo kwenye mabenki badala ya kufanya uzalishaji wavifufue haraka, vinginevyo tutawanyang'anya" amesisitiza Rais Magufuli huku akishangiliwa na wananchi waliomsimamisha katika eneo la Msamvu Mjini Morogoro.

Rais Magufuli pia amesimamishwa na kuwasalimu wananchi wa Wami Dakawa, Magole na Dumila ambako pamoja na kuwahakikishia kuwa atatekeleza ahadi yake ya kuwapa mashamba atakayonyang'anya kutoka kwa walioyatelekeza, amewataka kuachana na migogoro kati ya wakulima na wafugaji na badala yake watatue migogoro hiyo kwa kutumia njia za kisheria.

Aidha, amewataka viongozi wote wa Mkoa hadi vitongoji kushirikiana kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji kabla haijasababisha madhara, na ameonya kuwa migogoro hiyo ikileta madhara itakuwa ni kigezo tosha kuwa viongozi hao wameshindwa kutekeleza wajibu wao na wanapaswa kuachia ngazi.

Pamoja na hayo Rais Magufuli amewahimiza wananchi hao kuchapa kazi kwa juhudi hasa katika kipindi hiki ambacho mvua zinanyesha, na pia wahakikishe kuwa watoto wote wanaopaswa kuandikishwa shule wanapelekwa shule, hasa baada ya serikali kuamua kutoa elimu bure ya kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.

"Tumeamua kutoa elimu bure na tutatoa elimu bure, na jambo hili limeonesha mafanikio makubwa kwa kuwa hata shule zilizotarajia kuandikisha wanafunzi 45 zimejikuta zikiandikisha hadi wanafunzi 600 kwa darasa moja" alibainisha Rais Magufuli.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amekagua kipande cha barabara kuu ya Morogoro - Dodoma kilichoharibiwa na maji ya mvua katika eneo la Kibaigwa Mkoani Dodoma, na kujionea kazi za ukarabati zinazofanywa na wakala wa barabara nchini (TANROADS).

Amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, kuongeza wakandalasi wa kukarabati eneo hilo ili kazi ikamilike haraka badala ya kusubiri mpaka baada ya miezi miwili ilivyopangwa na wizara.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kesho tarehe 06 Januari, 2016 atashiriki maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), zitakazofanyika katika uwanja wa Namfua, Mjini Singida.
Gerson Msigwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
05 Januari, 2016
Rais Magufuli akikagua barabara ya Morogoro-Dodoma eneo la Kibaigwa.

Update: Polisi Watatu Wasimamishwa Kazi Kupisha Uchunguzi wa Binti wa Kitanzania Kuvuliwa Nguo India

$
0
0
Polisi watatu wamesimamishwa kazi kwa muda mjini Bangalore nchini India kwa tuhuma za kukataa kusikiliza na kupokea malalamiko ya watu walioshambuliwa na kundi la watu ambapo mwanafunzi mmoja wa kike kutoka Tanzania alivuliwa baadhi ya nguo zake. 

Polisi wamesema pia wamekamata watu wanne zaidi kuhusiana na shambulio hilo, na kufikisha idadi ya waliokamatwa kufikia tisa. 

Kundi la watu lilimshambulia na kumvua nguo mwanamke mwenye umri wa miaka 21, baada ya gari la mwanafuzi kutoka Sudan kumgonga na kumuua mwanamke mmoja wa Kihindi. 

Tukio hilo limetokea eneo la Hessarghatta siku ya jumapili. Eneo hilo lina vyuo kadhaa ambapo kuna idadi kubwa ya wanafunzi kutoka Afrika, wakiwemo 150 kutoka Tanzania.

Polisi Dar Yakamata Magari 2 Yaliyotumika Kubeba Kompyuta Zilizoibwa Kwenye ofisi ya Aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Philip Mpango.

$
0
0

Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata magari mawili yakihusishwa na wizi katika ofisi ya kamshina mkuu wa TRA huku yakiwa na vifaa vilivyoibiwa katika ofisi hiyo vikiwa ni pamoja na komputa  na TV.
 
Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema kutokana na oparasheni kali iliyokuwa ikiendeshwa na jeshi ilifanikiwa kuwatia nguvuni watuhumiwa wanne wakiwa na vifaa vilivyoibiwa.

Ameyataja magari hayo  kuwa ni Toyota Noah yenye namba za usajili T 989 CNV  na Mitubish Pajero yenye namba za usajili T 386 CVV .Pia  walinzi wawili waliokuwa zamu kulinda siku hiyo wamekamatwa.

"Katika wizi huo vitu vilivyoibwa ni Compyuta mbili, aina ya Dell pamoja na CPU, Monitor zake na Televisheni moja aina ya Sumsung inchi 40" Alisema Sirro.
Aidha kamanda huyo wa kanda maalum ya Dar es Salaam amesema katika oparesheni hiyo pia jeshi la polisi lilifanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi milioni 150 mali ya Bw Ahmed Huwel mkazi wa Msasani.

Katika hatua nyingine kamanda Sirro ametangaza kusitishwa kwa muda kwa shughuli za ulinzi shirikishi katika vituo vya polisi kutokana na vikundi hivyo kualamikiwa na wananchi kwa kutokuwa na tija katika jamii.

Waziri Mkuu Aahirisha Shughuli za Bunge Hadi Tarehe 19 Mwezi wa Nne.

$
0
0

Serikali katika  kuongeza na kuimarisha uhakika na usalama wa chakula hapa nchini, imepanga kujenga maghala 275 kwa awamu katika sehemu zenye uzalishaji mkubwa wa zao la mahindi ambapo hadi sasa jumla ya maghala 125 yanaendelea kujengwa na kukarabatiwa katika maeneo hayo.
 
Akifafanua hilo wakati akiharisha shughuli za Mkutano wa Pili wa Bunge la 11 lilikuwa na vikao 9, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,Majaliwa amesema Serikali imejipanga katika kuondoa tatizo la upungufu wa chakula nchini kwa kujenga magala mengi zaidi ya kuhifadhi chakula katika maeneo mbalimbali yenye changamoto za upungufu wa chakula.
 
Mhe. Kassim Majaliwa,Majaliwa amesema hali ya chakula kwa mwaka 2015/2016 katika maeneo mengi ya nchi imeendelea kuwa ya kuridhisha kufuatia mavuno mazuri yaliyopatikana msimu wa kilimo wa 2014/2015 na takwimu za Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi zinaonesha kuwa akiba kutoka msimu uliopita nchi ilikuwa na ziada ya chakula licha ya kuwepo kwa maeneo machache ambayo hayakuwa na chakula.
 
“Kutokana na uzalishaji wa mazao ya chakula kwa msimu wa 2014/2015 kuwa Tani milioni 15.5 na mahitaji ya chakula kwa mwaka 2015/2016 kuwa Tani milioni 12.9hivyo  nchi imejitosheleza kwa chakula kwa ziada ya Tani milioni 2.5 sawa na asilimia 120 na napenda kuwahakikishia Watanzania kuwa Serikali itaendelea kuhudumia maeneo yote yenye uhaba wa chakula”
 
“Ili kukabiliana na hali ya uhaba wa chakula katika maeneo hayo, Serikali inaendelea kutoa chakula katika maeneo hayo ambapo jumla ya Tani 23,871.6za chakula zilitengwa kwa ajili hiyo na hadi kufikia tarehe 17 Januari, 2016, jumla ya Tani 11,860.8 zilikuwa zimechukuliwa toka Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwenda kwenye Halmashauri za Wilaya zenye upungufu wa chakula kwa ajili ya usambazaji pia natoa wito kwa Halmashauri ambazo hazijachukua mgao wao kufanya hivyo mara moja ili Wananchi katika maeneo hayo wasizidi kuathirika” Alisema Mhe. Majaliwa.
 
Aidha, Mhe Kassim Majaliwa,Majaliwa  amesema Serikali kwa kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) inaendelea kujenga maghala ya kimkakati kwa ajili ya kuhifadhi akiba ya Taifa na kwa sasa ghala moja lenye uwezo wa kuhifadhi Tani 5,000limeshajengwa Wilayani Mbozi Mkoani Mbeya na Serikali imepata mkopo wenye masharti nafuu kutoka Serikali ya Poland ambao utawezesha kujenga vihenge vya kisasa (silos) vyenye uwezo wa kuhifadhi Tani 160,000 na maghala yenye uwezo wa kuhifadhi Tani 90.
 
Ameongeza kuwa Pamoja na hatua zinazochukuliwa na Serikali, amewataka viongozi wa Mikoa, Wilaya na watendaji katika Halmashauri zote Nchini kuwahamasisha Wananchi kutumia vizuri mvua zinazonyesha nchini kote kwa kulima kwa bidii ili kuweza kuvuna na kujiwekea akiba ya chakula cha kutosha kwa ajili ya kaya zao wakati wote wa mwaka na wawahamasishe wafanyabiashara na wadau wengine kusaidia Serikali kuchukua chakula kutoka maeneo yenye ziada na kupeleka katika maeneo yenye upungufu na kwa kuzingatia maelekezo haya pamoja na juhudi za Serikali zilizooneshwa, tatizo la uhaba wa chakula nchini litapungua, kama siyo kumalizika kabisa.
 
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa,Majaliwa ameahirisha Mkutano wa Pili wa Bunge mpaka tarehe 19 mwezi April 2016 saa 3 Asubuhi  likaporejea katika Mkutano wa kujadili Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/2017.

Mawaziri wa awamu ya Tatu, Basil Mramba na Daniel Yona sasa kutumikia kifungo cha nje

$
0
0

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeridhia waliokuwa Mawaziri wastaafu Basil Mramba na Daniel Yona kutumikia adhabu ya kifungo cha nje kwa kufanya usafi katika maeneo ya kijamii ikiwemo Hospitali ya Sinza Palestina.

Hatua hiyo inatokana na Mramba ambaye alikuwa Waziri wa Fedha na Yona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, kupitia Mawakili wao kuwasilisha barua mahakamani hapo kutoka Magereza kuhusu kutumikia kifungo cha nje.

Mawaziri hao wa zamani waliwasilisha barua hiyo ya kuitaarifu mahakama yenye kumbukumbu namba 151/DA/3/11/223 ya Desemba 5, mwaka jana, wakiongozwa na jopo la mawakili wao watatu Peter Swai, Cuthbert Nyange na Elisa Msuya.

Katika barua hiyo waliyoiwasilisha kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha ilikuwa na kichwa cha habari kisemacho‘Wafungwa wenye sifa ya kutumikia vifungo vyao chini ya Mpango wa Huduma kwa Jamii”.

Hakimu Mkeha alisema mchakato huo ulianza baada ya Magereza kuwasilisha barua hiyo mahakamani hapo kwa kupeleka majina ya watu wanaotumikia kifungo cha nje ikiwemo mawaziri hao.

Alisema mahakama haihusiani na mchakato huo, kwani ilishamaliza kazi yake ya kuhumu, hivyo jukumu la kutumikia kifungo cha nje ni kazi ya Magereza.

“Baada ya kuleta barua hiyo kisheria mahakama inaishinikiza Ustawi wa Jamii ili ifanye uchunguzi kutokana na majina yaliyowasilishwa mahakamani,”alisema.

Hakimu Mkeha alisema kupitia barua hiyo, Mawaziri hao wa zamani wamepangiwa kutumikia adhabu ya kufanya usafi kwenye Hospitali ya Sinza Palestina kwa saa nne za kila siku.

Alisema awali kabla ya mahakama kuridhia adhabu hiyo, iliwaita Mawaziri hao kwa ajili ya kuwahoji kama wameridhia na adhabu watakayopangiwa sambamba na vipengele vinavyowahusu.

“Kutokana na barua hiyo mahakama ikaona ni vyema kuwaita wahusika wenye ambapo tuliwahoji kama wanaridhia kutumikia adhabu hiyo, ambapo walikubali ndipo tukaridhia,”alisema.

Kuhusu masharti yaliyotumika kuwapatia kifungo hicho, alisema kinatokana na sheria ya Jamii namba 6 ya mwaka 2002, kifungu cha 3(1).

Alisema baadhi ya vigezo vinavyotumika kwa wafungwa kutumikia adhabu ya nje ni muangalio wa ripoti yao ilikuwa inasemaje, umri, washtakiwa kama walishawai kutiwa hatiani, makosa namna yalivyo, kama wanafamilia, pia kama wanakubali kuitumikia jamii, kama wana ajira, tabia za mshtakiwa na umbali wa eneo analokaa na anapofanyia adhabu hiyo.

Inakumbukwa kuwa Oktoba 2, 2015 katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ilitoa hukumu ya rufaa dhidi ya mawaziri wastaafu, Basil Mramba na Daniel Yona ambapo Jaji Projest Rugazia, alikubaliana na hoja kwamba kwa mujibu wa mashtaka yaliyowatia hatiani kwa matumizi mabaya ya Ofisi na kwa mujibu wa kifungo cha 35 cha adhabu PC ambacho Mahakama ilikitumia walipaswa kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka miwili na si miaka mitatu.

Katika rufani hizo, Mramba na Yona, waliwasilisha hoja tano kupinga hukumu iliyotolewa Julai 6, mwaka jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, na jopo la Mahakimu watatu, likiongozwa na John Utamwa.

Aidha DPP alipinga adhabu waliyopewa mawaziri hao kwa madai ni ndogo, pia hakimu alikosea kumuachia huru aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Gray Mgonja na pia iliiomba mahakama iamuru washtakiwa walipe fidia ya fedha walizosababisha hasara.

Katika uamuzi huo Jaji Rugazia alikubali hoja ya kina Mramba kuwa walipewa adhabu mbili kwa kosa moja.
 
“Haikuwa sahihi kuwashitaki kwa kosa la kusababisha hasara wakati kosa hilo lilishakuwa kwenye makosa mengine ambayo ni la tano hadi la 10,” alisema.

Aidha, alisema Yona aliunganishwa kimakosa katika shtaka hilo, hivyo alifuta shitaka hilo pamoja na adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya Sh milioni tano iliyotokana na kosa hilo.
 
“Ninaondoa shitaka la kusababisha hasara, ninafuta adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya Sh milioni tano, hivyo Yona na Mramba watatumikia kifungo cha miaka miwili kwa kila kosa,“ alisema.

Katika uamuzi huo, Jaji Rugazia alisema,“Nakubali Kifungu cha 6 cha Kanuni ya Adhabu kinachotaka mahakama itoe amri washitakiwa walipe fidia, lakini siwezi kutoa amri hiyo.”

Pia alikataa hoja za kina Mramba kuwa hati ya mashtaka ni batili, pia alisema hakukuwa na njama zozote kwa upande wa Jamhuri kutoita mashahidi waliosaini mkataba huo ili kuathiri upatikanaji wa haki, kwa kuwa utetezi walikuwa na haki ya kuomba watu hao wawe mashahidi wao.

Alisema wasitumie maelezo ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, kuficha kosa kwa kuwa alitoa maelekezo kutokana na barua aliyoipata kutoka kwa Mramba na hakujua kama tayari Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ilishatoa angalizo la kutokutoa msamaha huo.

Kwa upande wa Mgonja, Jaji Rugazia alisema anahalalisha kuachiwa kwake huru baada ya kutopatikana na hatia. Alisema, “Siwezi kuilaumu mahakama kwa kumuachia huru”.
 
Katika hukumu hiyo, mawaziri hao walihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya Sh milioni tano, baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 11.7.

Kwa mara ya kwanza washtakiwa hao walifikishwa mahakamani mwaka 2008, wakikabiliwa na mashtaka ya kuisababishia serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya kukagua madini ya dhahabu ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.

Maandammano ya CHADEMA Kesho Kuelekea Ikulu Yapigwa Marufuku

$
0
0

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limepiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika hapo kesho na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuelekea Ikulu jijini Dar es salaam kushinikiza kurejeshwa kwa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Naibu Kamishna wa Polisi Simon Siro amesema Chama hicho kinatakiwa kutumia mbinu nyigine ya kushinikiza kurejeshwa kwa matangazo hayo ya Televisheni ya Taifa na sio kupitia maandano.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya Februari 6

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images