Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Lowassa Apata Mapokezi Makabuwa Dakawa Wakati Akiwa Njiani Kuelekea Dodoma

$
0
0
Aliyekuwa mgombea Urais  katika uchaguzi wa Oktoba mwaka jana kwa tiketi  ya  UKAWA, Edward Lowassa jana alipata mapokezi makubwa kwa wakazi wa mnada wa Dakawa baada ya kusimama  na  kuwasalimia.

Lowassa alikuwa safarini  kuelekea Mkoani Dodoma kwa ajili ya mafunzo  ya  wabunge wa UKAWA.
 

VIDEO: JWTZ Yafafanua Kuhusu Rais Magufuli Kuvaa Mavazi ya Kijeshi

$
0
0
January 22, 2016 akiwa njiani Kutoka Arusha Mjini kwenda Monduli kufunga "Zoezi Onesha Uwezo Medani" lililofanywa na Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amir Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli alisimamishwa na wananchi waliojipanga kandokando mwa barabara mara nane.

Rais Magufuli alivaa sare za kijeshi tayari kwa kwenda kufanya kazi za Jeshi la wananchi Tanzania ikiwa ni halali kufanya hivyo kwa mujibu wa Sheria ya Jeshi la wananchi ya mwaka 1966.

Msemaji wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kanali Ngemela Lubinga ametoa ufafanuzi wa Rais Magufuli kuvaa sare hizo


==>Tazama Video Hii Kumsikiliza

Medeye na Guninita Wamvaa Benard Membe Baada ya Kusema Hujisikia Kichefuchefu Akionana na Makada Walioihama CCM

$
0
0

Siku moja baada ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kusema akionana na waliokuwa wanachama wa CCM na kuhamia upinzani anajisikia kichefuchefu, waliokuwa makada wa chama hicho wamemshukia kwa kauli yake hiyo.

Membe alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akitoa maoni yake kuhusu makada waliohama na kusisitiza kuwa wasipokewe endapo watataka kurudi.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye ambaye alitimkia Chadema, alisema kama angesikia maneno hayo kwa mtu mwingine asingeshangaa, lakini siyo kwa Membe.

Mbunge huyo wa zamani wa Arumeru – Magharibi, alisema Membe anapata masilahi yake kwa kutambulika kama waziri mstaafu na wakati anaapa kuwa katika nafasi hiyo alitumia Katiba ambayo hivi sasa kwa kupinga yaliyomo ikiwamo uhuru wa mtu kujiunga na chama chochote cha siasa, anakosea.

Medeye alisema kwa kauli hiyo, Membe hana haki ya kugombea nafasi yoyote ya siasa kwa sababu haamini katika vyama vingi wakati Taifa linaendeshwa kwa Katiba inayokubali suala hilo.

Alisema hata kauli ya Membe ya kutounga mkono uchaguzi kurudiwa Zanzibar akitaka kufanyiwa kazi kasoro chache ni ya kinafiki kwa sababu ameonyesha kutopenda upinzani.

“Hana msimamo hazungumzi vitu kutoka moyoni, kama kweli anakubali vyama vingi na ana uchungu na kinachoendelea Zanzibar, kwa kuwa bado ni mjumbe wa Nec (Halmashauri Kuu ya CCM), angemuomba mwenyekiti wake aitishe mkutano mkuu lijadiliwe hilo na atoe anachokiamini, hakufanya hivyo kwa sababu hakubali vyama vingi, hataki mabadiliko katika siasa anayoitumikia, ” alisema Medeye.

Aliyekuwa kada mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombale Mwiru alisema hawezi kujibizana na watu kwani anajua anachofanya.

Alisema anayo mawazo huru na akitaka kuzungumza jambo lolote atafanya hivyo kwa utashi wake na siyo kujibizana na watu waliozungumza kwa utashi wao.

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita alisema anamheshimu Membe kwa sababu amefanya naye kazi katika chama hicho tawala na kumshauri siku nyingine anapozungumza mambo kama hayo asiegemee upande mmoja.

Alisema licha ya kuwa hayo ni mawazo yake na kila mtu ana uhuru wa kuwaza na kusema anachotaka, alipaswa apime anazungumza nini na kwa manufaa ya nani.

Guninita alisema Katiba ya nchi inamruhusu mtu kuhama chama hata mara 10 alimradi huko anakokwenda atapata vitu muhimu ikiwamo malengo yake binafsi, ya chama husika na mafanikio ya Taifa.

Alisema haikuandikwa ni lazima abaki sehemu anayoamini hana malengo nayo, au asihame kutoka chama kimoja ama kingine

Jokate na Ali Kiba Wamwagana

$
0
0

Mastaa wawili wenye majina makubwa Bongo ambao walikuwa wachumba walioshibana, Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’ na Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ wanadaiwa kumwagana,

Habari ya mjini kwa sasa ni juu ya wawili hao ambao walikuwa gumzo kwa watoto wa mjini, kwa kila mmoja kuchukua hamsini zake na kufanya yake tofauti na walivyokuwa awali huku chanzo cha kutengena kwao kikitajwa kuwa ni wazazi wa sehemu zote mbili kutoridhiana.

Inadaiwa kuwa, mbali na ishu ya wazazi, hivi karibuni Jokate na Kiba waliingia kwenye gogoro kubwa la kimapenzi baada ya kufumaniana kwenye simu, jambo ambalo limeendelea kutokea huku jamaa akiongoza kukutwa na meseji kwenye simu yake za mwanamke mmoja anayedaiwa kuishi nje ya Tanzania.

“Ukisema nikusimulie juu ya kumwagana kwa Jokate na Kiba basi tunaweza kukesha ila mbali na mambo ya wazazi, kwa kifupi tu ni kwamba, hawa watu wameingia kwenye mgogoro na kilichokuwa kikiwagombanisha mara nyingi ni uhusiano wao wa zamani.”

“Mara kadhaa Jojo (Jokate) amekuwa akimlalamikia jamaa (Kiba) kuwa ana demu nje ya nchi ambaye amekuwa akimtundika katika mitandao ya jamii na kujinadi kuwa ndiye mkewe tofauti na wengi wanavyojua kuwa Jokate ndiye mtu wake.

“Mbali na hilo, sasa kuna suala la familia zao kuonesha hali ya kutokubaliana na wao kuoana hasa upande wa Jokate ambao ulionesha msimamo mkubwa kutomtaka hata kidogo Kiba, mambo hayo yamekuwa ni chagizo kubwa katika kuhatarisha mapenzi yao hivyo kufikia hatua hata ya wao kutoendelea kupendana kwa dhati kama ilivyokuwa mwanzo wa penzi lao.”

“Tofauti na watu walivyozoea kuwaona pamoja, kwa sasa wametibuana na hapa tunapozungumza tayari kuna vikao kibao huko nyuma vilishakaa ili kunusuru penzi lao lakini imeshindikana maana kila mmoja sasa hivi anajifanyia mambo yake na hakuna dalili za kurudiana.

“Kiba anaonekana ameshajiingiza kwenye penzi la demu wake wa zamani huku Jokate naye akiwa ‘in love’ na mtu wake mwingine.”

“Kitambo tu nimekuwa nikiwaambia kwa staili waliyokuwa nayo hakika wasingeoana hata kama ukiweka pembeni suala la dini zao kutoendana, maana kuna siku niliwasikia wakiambiana hata kama wazazi wakigoma wao wangefanya kila juhudi hata wazae pamoja tu.

“Lakini ukweli ni kwamba ilishindikana baada ya kuanza kugombana mara kwa mara, pamoja na kwamba Jokate alikuwa akikubalika kwa asilimia zote kwa mama Kiba na hata ndugu wengi wa Kiba walionekana kumpenda waziwazi,” kilisema chanzo .

Alipotafutwa Ali Kiba ili atoe la moyoni juu ya madai hayo ya kumwagana na Jokate alisema kuwa haoni sababu ya kuzungumzia ishu hiyo kwani ni mambo binafsi.


Chanzo: GPL

Mrembo wa UDSM Aliyedaiwa kuwa Msukule Uliokutwa Kwenye Shimo la Mfanyabiashara Dar Anena kwa Uchungu

$
0
0

Picha zinazomuonesha mwanamke aliyekutwa kwenye shimo la mfanyabiashara mmoja jijini Dar es Salaam akiwa katika hali ya kutisha zimetumiwa kufanya upotoshaji kwa kumzushia msichana mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 
Picha iliyounganishwa ikionesha taswira ya msichana huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakidai kuwa hapo ni kabla zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na watu wasio na nia njema na kusababisha usumbufu kwa mrembo huyo.
 
Msichana huyo ambaye anatumia jina la Ms.Adelaide kwenye Instagram amekanusha vikali taarifa hizo huku akieleza kwa uchungu jinsi ambavyo ameathiriwa na uzushi huo.
 
NAJUA WENGI MTAKUA MMEKUTANA NA HIZI HABARI..SIJAJUA NANI ALIEANZISHA HII MADA NA SIJUI IMEANZIA KWA NANI.

 "MIMI NI MZIMA NA SIO MSUKULE JAMANI NINA WAZAZI WOTE WAWILI WAPO HAI NA WAMEUMIZWA SANA NA HIKI KITENDO, MY FAMILY MEMBERS WAMEUMIA MNOOO KUPITA KIASI

"LICHA YA HIYO MIMI BADO NI MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU, WANAFUNZI WENZANGU WENYE MAPENZI NA MIMI WANAUMIA SANA PIA WANAPOONA MAMBO KAMA HAYA. 

"PLEASE ACHENI KUENDELEZA HIZI HABARI ZA UONGO, TUSIPELEKANE MPAKA TCRA SASA MAANA TUTAKUA TUNAPOTEZEANA MUDA,” aliandika Instagram.

Benard Membe Azidi Kumkaba Rais Magufuli.....Asema Rais Anawafukuza Watumishi Kiurahisi Kwa Kuwa Hakuwateua Yeye

$
0
0
Wiki hii ilikuwa wiki ambayo waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ameeleza mengi yaliyoteka vichwa vya habari.

Kati ya mambo aliyozungumzia ni pamoja na uamuzi wa Rais John Magufuli  kuwasimamisha na kuwafukuza kazi baadhi ya watumishi wa umma.

Membe ambaye aliwania nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, amekaririwa na gazeti la Mwananchi akieleza kuwa ni rahisi kwa rais Magufuli kufanya hivyo kwa sababu watu anaowasimamisha hakuwateua yeye kwa sababu hawafahamu.

“Ni rahisi kumshughulikia mtu usiyemfahamu, lakini sio rahisi kumshughulikia unayemfahamu. Kwake kufanya hivyo ni rahisi kwa kuwa pia ni rahisi kuwashughulikia watu usiowajua kuliko watu unaowajua, lakini hebu tuone kama atafanya hivyo pia kwa hao aliowateua mwenyewe,” Membe alisema.

UVCCM Mkoa wa Vyuo Wampa Makavu Benard Membe Kwa Kumponda Rais Magufuli

$
0
0
SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ndugu waandishi wa habari, nimewaita hapa kuelezea masikitiko makubwa kutokana na kauli za hivi karibuni za aliyekuwa waziri wa mambo ya nje ndugu Bernard Membe.

 Akifanya mahojiano na kunukuliwa na gazeti la Mwananchi la tarehe 22 na 23 Januari, 2016 , ndugu Membe amekaririwa akitoa kauli zenye maudhui ya kubeza juhudi za mh. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli na kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar. Kauli hizi zilijikita katika maeneo makubwa manne kama ifuatavyo:-

1. Ndugu Membe amebeza juhudi za Rais Dr. John Magufuli za kupunguza ukubwa wa serikali, na kwamba hatua yake ya kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri haijasaidia chochote kwa taifa. Na kwamba ni sawa na kupunguza idadi ya mifuko huku idadi ya mayai ikiwa ni ile ile.

2. Ndugu Membe amekosoa na kubeza hatua ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr. Magufuli ya kupunguza safari za nje zisizo za lazima na tija kwa taifa, na kwamba safari hizo zilikua na neema kubwa kwa watanzania.

3. Ndugu Membe amepinga kufutwa kwa matokeo yote ya uchaguzi visiwani Zanzibar na kudai kwamba dunia nzima inatushangaa kwa uamuzi huo.

4. Ndugu Membe amekosoa mazungumzo ya kutafuta maridhiano baina ya Chama cha CUF na CCM visiwani Zanzibar huku akidai kuwa ni makosa kuwaachia Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein na Maalim Seif Shariff Hamad kufanya mazungumzo peke yao.

Tumesikitishwa sana na kauli hizo na vijana wasomi tumeamua kumjibu kama ifuatavyo:-

KUPUNGUZA UKUBWA WA SERIKALI
Rais Dr. John Magufuli amechukua juhudi za kupunguza ukubwa wa serikali kwa kuanza na baraza la mawaziri.

 Idadi ya mawaziri imepungua kutoka mawaziri 60 wakati wa serikali ya awamu ya nne hadi mawaziri 34 tu katika serikali ya awamu ya tano. Punguzo hili ni idadi ya mawaziri 26.

Gharama za kawaida za kumuhudumia waziri zilizopungua:
a. Kila waziri na naibu wake hupewa gari aina ya GX V8 ambalo thamani yake inakadiriwa milioni 400. Gari hili linahitaji mafuta na gharama ya kulitunza. Hivyo magari 26 yamepungua ambayo gharama yake ya manunuzi na matunzo ni mabilioni ya pesa.

b. Nyumba ya kuishi. Mawaziri wote wanapewa nyumba na serikali. Nyumba hizo zinalipiwa umeme na maji

c. Wasaidizi wa mawaziri. Kila waziri anapewa katibu wake, hivyo serikali imepunguza nafasi 26 za makatibu kwa kupunguza mawaziri 26. Hawa wanalipwa mishahara na posho.

d. Madereva. Kila waziri ana dereva wa serikali anayelipwa mshahara na posho awapo nje ya kituo cha kazi. Hivyo serikali imepunguza mishahara na posho za watu 26.

e. Kila waziri anapewa ulinzi nyumbani kwake wa askari wawili wa jeshi la polisi masaa 24. Hivyo kwa kupunguza mawaziri 26, tumepunguza askari 52 ambao sasa watakwenda kuongeza ulinzi wa raia na mali za wananchi wengine.

f. Kila waziri anatengewa mafungu ya fedha kwa ajili ya mawasiliano, safari zake za kikazi, ziara za mikoani, vikao na majukumu mengine ya kazi ambayo ni mamilioni ya shilingi kila mwezi. Kwa kupunguza mawaziri 26 Rais ameokoa mamilioni ya shilingi kila mwezi.

g. Gharama za kuwahudumia mawaziri 26 wakiwa bungeni Dodoma pia zimepungua.

WIZARA ZILIZOUNGANISHWA
Katika muundo wa baraza la mawaziri la Dr. John Pombe Magufuli alilolitangaza , ziko wizara 5 ambazo zimeunganishwa pamoja. Wizara hizi ni

a. Kilimo, Mifugo na Uvuvi (wizara 3 zimeunganishwa, sasa zina waziri 1)-Mh. Mwigulu Nchemba

b. Wizara ya mambo ya nje, kikanda na kimataifa (wizara mbili zimeunganishwa, sasa zina waziri 1)- Mh. Augustine Mahiga

c. Wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji (wizara 2 zimeunganishwa,sasa zina waziri 1)- Mh. Charles Mwijage

d. Wizara ya elimu, sayansi, teknolojia na ufundi (wizara 2 zimeunganishwa, sasa zina waziri 1)- Mh. Joyce Ndalichako

e. Wizara ya ujenzi, mawasiliano na chukuzi (wizara 3 zimeunganishwa, sasa zina waziri 1) -Mh. Makame Mbarawa

Katika hali hiyo, ni dhahiri idadi ya mawaziri imepungua na hivyo gharama ya kuwahudumia pia imepungua. Kutoka hadharani na kusema hakuna kilichopungua ni upotoshaji mkubwa ambao mtu mwenye uelewa wa kawaida kabisa anaweza kuubaini.

IDADI YA MAKATIBU WAKUU
Makatibu wakuu na manaibu waliohudumu wizara wakati wa serikali ya awamu ya nne walikuwa jumla ni 54. Mh. Rais Dr. Magufuli ameteua makatibu wakuu 29 na manaibu 21. Hivyo hapa pia idadi imepungua na kufanya gharama kupungua pia.

WATANZANIA WANAMSHANGAA MEMBE
Kitendo cha ndugu Bernard Membe kudai kuwa kupungua huku kwa ukubwa wa baraza la mawaziri hakujasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali, ni jambo la ajabu ambalo watanzania wote wanalishangaa na kuliona kuwa ni uongo na upotoshaji mkubwa. Upotoshaji huu unastahili kupuuzwa na kila mpenda mabadiliko ya kweli.

Baada ya Mh. Raisi kuteua baraza lake la mawaziri mwezi desemba, mwanazuoni profesa Samuel Wangwe alikaririwa na gazetila Habari Leo la tarehe 11 Desemba, 2016 akisifu Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli kupunguza idadi ya mawaziri. 

Profesa Wangwe alisema mawaziri ni watu wa kusimamia sera, na watendaji wakubwa ni makatibu wakuu. Aidha, wanaharakati na wadau mbalimbali wote walipongeza kupunguzwa huko kwa baraza la mawaziri wakisema taifa limepunguza mzigo. Lakini ajabu, ndugu Bernard Membe hajaliona hilo. Inasikitisha sana.

Wakati mwingine inatufanya tujiulize, ndugu Membe ambaye alikua miongoni mwa wana CCM waliowania kuteuliwa na Chama kugombea Urais wa Tanzania, na baadae kushindwa kwa kura ndani ya Halmashauri Kuu ya CCM taifa, amesema maneno haya kwa malengo au makusudio yapi?

Waswahili wanasema, aliyepata kapata. Tunamtaka ndugu Membe ajiunge na watanzania kukubali kuwa Dr. Magufuli ndiye Rais wa nchi yetu aliyechaguliwa na wananchi. Hivyo amuache atimize wajibu wake kwa taifa.

KUPUNGUZA SAFARI ZA NJE
Katika hatua nyingine ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima serikalini, Raisi ameagiza kufutwa kwa safari zote zisizo za tija kwa nchi, na kwamba safari zote zitatolewa kwa kibali maalum cha Raisi.

Kwa mujibu wa hotuba ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli bungeni mjini Dodoma, safari za nje za miaka miwili pekee (2013-2015) ndugu Membe akiwa waziri wa mambo ya nje, shilingi bilioni 356.324 zilitumika kwa safari za nje huku tiketi za ndege peke yake zikigharimu bilioni 183.160. 

Taasisi zilizoongoza kwa matumizi hayo ni pamoja na wizara ya mambo ya nje aliyokuwa anaihudumia ndugu Membe. 

Tunajiuliza, ni trilioni ngapi zilitumika kwa safari za nje katika kipindi chote cha miaka 8 ambacho ndugu Membe alikuwa waziri? 

Je, huu haukua mzigo kwa taifa? Ndugu Membe anazungumziaje matumizi haya mabovu ambayo yalifanyika yeye akiwa na dhamana ya wizara hiyo?

Watanzania wote tunafahamu na kukubali kuwa safari hizi zilikua mzigo mkubwa kwa taifa, na tunaunga mkono juhudi za kupunguza na kudhibiti safari zisizo za lazima.

BERNARD MEMBE SI MKWELI
Ndugu waandishi, ili kudhihirisha kuwa ndugu Bernard Membe si mkweli kwa anayoyasema kuhusu safari za nje, na kwamba kauli zake kuhusu jambo hili zinakinzana, baada ya hotuba ya Rais Dr. John Magufuli bungeni mjini Dodoma, bwana Membe alinukuliwa akimpongeza mh Rais kwa uamuzi wake wa kupunguza safari za nje kwani kwa maneno yake alisema walikua wanapishana angani kama vile nyumbani kunawaka moto.

Ni Bernard Membe huyuhuyu ambaye leo anatafuna maneno yake bila aibu na kutueleza kuwa safari zile zilikua na neema kwa taifa.

KUHUSU KUTOKUA NA BALOZI KATIKA NCHI ZOTE
Katika kuhalalisha safari za nje zisizo za lazima, ndugu Membe alieleza kuwa Tanzania ina mabalozi 36 tu katika nchi 194 ambazo tunapaswa kuwa na mabalozi.

Tunapenda kumfahamisha ndugu Membe kuwa kutokuwa na balozi katika nchi zote sio kigezo cha kutumia mabilioni ya pesa kwa ajili ya safari zisizo na tija kwa taifa.

Kutokana na kuwa uchumi wetu bado unakua, na haustahamili gharama za kuweka mabalozi katika nchi zote, wako mabalozi wetu nje ya nchi ambao wanawakilisha nchi zaidi ya moja zilizoko katika ukanda mmoja. 

Mfano, balozi Ombeni Sefue aliwahi kuwa balozi wetu Marekani akiwakilisha pia CUBA. Aidha, uamuzi wa nchi kufungua ubalozi katika nchi nyingine hutegemea vigezo mbalimbali kama faida za kiuchumi, kisiasa, kiusalama na kidiplomasia.

RAISI HAJAKATAA KUSAFIRI NJE YA NCHI
Ndugu Membe anapotosha ukweli anaposema Tanzania sio kisiwa na kwamba Raisi na waziri wake wa mambo ya nje lazima wasafiri nje ya nchi watake wasitake.

Tunapenda kumfahamisha ndugu Membe kuwa, mh. Raisi Dr. John Magufuli hajatoa kauli kuwa yeye au wasaidizi wake hawatosafiri nje ya nchi katika safari  muhimu na zenye tija. Isipokuwa, muongozo wa mh. Rais kuhusu safari za nje unalenga kupunguza safari zile ambazo hazina ulazima na tija kwa taifa.

KUHUSU MGOGORO WA UCHAGUZI WA ZANZIBAR
Katika maelezo aliyonukuliwa na gazeti la Mwananchi, ndugu Membe alieleza kupinga kufutwa kwa matokeo yote ya uchaguzi wa Zanzibar yakiwemo ya wawakilishi, na kwamba jambo hili limeihuzunisha dunia.

Kauli hii ya ndugu Membe inatushangaza na kutusikitisha sana. Kwanza tunajiuliza, Je, ikiwa sehemu kubwa ya uchaguzi iligubikwa na udanganyifu na ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi kinyume na sheria za uchaguzi wa Zanzibar, ni kwanini ndugu Membe ashangae uchaguzi wote kufutwa na tume ya uchaguzi ZEC?

Tunamtaka ndugu Membe atueleze, ni dunia ipi hiyo inayotushangaa?

Ni kwanini dunia hiyo anayoitetea ndugu Membe haijashangaa kumuona maalim Seif Shariff Hamad akijitangaza kuwa mshindi kinyume cha sheria za uchaguzi?

Ndugu Membe anapaswa kushangaa, ni kwanini hadi leo hii maalim Seif Shariff Hamad hajakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya kujitangaza kuwa mshindi kinyume cha sheria.

KUHUSU VIKAO VYA MARIDHIANO
Kuhusu vikao vya maridhiano vilivyokua vinaendelea, ndugu Membe amekosoa kitendo cha Raisi wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na maalim Seif Shariff hamad kuachwa wakazungumza wenyewe wawili.

Kwanza tunasikitika kuwa ndugu Membe huenda ama hajui kinachoendelea Zanzibar au ameamua kupotosha umma kwa makusudi.

 Hii ni kwasababu mazungumzo yaliyokua yakiendelea Zanzibar, hayakuwahusisha Dr. Shein na maalim Seif Shariff peke yao. 

Bali yalishirikisha marais wastaafu wa Zanzibar, Raisi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar na makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar.

Pili, katika muafaka wa kisiasa wa Zanzibar wa mwaka 2009/2010 uliopelekea kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, kwa kiasi kikubwa ni maalim Seif Shariff hamad na Rais wa Zanzibar wa wakati huo mh. Amani Abeid Karume pekee walioshiriki mazungumzo.

RAI KWA NDUGU MEMBE
Mosi, tunapenda kumkumbusha ndugu Bernard Membe kuwa yeye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa amewahi kuwa mjumbe wa kamati kuu ya CCM. 

Hivyo anajua utaratibu wa Chama na anayo nafasi ya kuyasema mawazo yake juu ya uendeshaji wa serikali ndani ya vikao halali vya chama. 

Aidha, ndugu Membe kwa nafasi yake kama mjumbe wa NEC na waziri wa zamaniwa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, anayo nafasi ya kutoa ushauri na maoni yake moja kwa moja kwa Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh. Dr. John Magufuli, Mwenyekiti wa CCM taifa Dr. Jakaya Kikwete au kwa Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana.

Kutotumia fursa hizo kutoa maoni yake ni kujishushia heshima mbele ya jamii.

Pili, tunamkumbusha ndugu Membe kuwa yeye sasa ni mstaafu aliyeitumikia nchi yake kwa muda mrefu na nafasi mbalimbali. 

Ni vema sasa akatoa fursa kwa viongozi wengine walioko madarakani kutimiza wajibu wao wa kuwatumikia watanzania. Muda wake umekwisha na sasa ni busara akakaa kimya na kuchunga maneno yake.

Raisi mstaafu wa awamu ya tatu mh. Benjamin William Mkapa aliwahi kusema (nanukuu):-

"Siku moja mtoto mdogo aliwahi kuniuliza. Nani ni bingwa wa kuendesha shughuli za serikali? Nikatafakari sana swali lile, kisha baada ya muda nikamjibu…Ni mwanasiasa aliyestaafu kisha akachunga ulimi wake…"

MWISHO
Tunamshauri ndugu Membe kuuchukua ushauri huu wa Raisi mstaafu Benjamin Mkapa, utamsaidia. Aidha tunamtaka afahamu kwamba watanzania wana imani kubwa na juhudi zinazofanywa na serikali katika kupunguza matumizi, kuziba mianya ya rushwa, ukwepaji kodi na ubadhirifu wa mali za umma. 

Wakati huu si wa kupika majungu, fitina wala ubabaishaji. Ni wakati wa kuungana pamoja kama taifa na kuchapa kazi tu.

Asanteni.

Imetolewa na ndugu

ALLY S. HAPI
KATIBU WA IDARA,
ELIMU, UTAFITI NA UONGOZI,
SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU TANZANIA

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Kuhusu Idadi ya Raia wa Kigeni Waliokamatwa na Nchi Wanakotoka

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga amesema zoezi linaloendelea sasa la kukamata raia wa kigeni wanaoishi na kufanya kazi hapa nchini bila vibali halitawagusa wageni wenye vibali halali.

Mheshimiwa Kitwanga ameyasema haya mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na jumuiya ya raia toka nchini China wakati wa sherehe zilizoandaliwa na raia hao katika Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.

Katika sherehe hizo ambazo ziliandaliwa mahsusi kuukaribisha mwaka Mpya wa Kichina, Mheshimiwa Kitwanga alisema uhusiano wa Tanzania na China ulianzishwa na marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Kiongozi wa China, marehemu Mao Zedong zaidi ya miaka hamsini iliyopita.

Amesema uhusiano huo umeendelea kuimarishwa hadi katika nyanja za kiuchumi ambapo hadi sasa kuna zaidi ya Kampuni 500 za Kichina ambazo zinafanya shughuli za kibiashara hapa nchini ambazo zimetoa zaidi ya nafasi 100,000 za kazi kwa Watanzania.

Mheshimiwa Kitwanga alitumia fursa ya sherehe hizo kuwahakikishia wawekezaji wote waliopo hapa nchini kuwa Serikali ya Tanzania italinda biashara zao kufuatana na sheria za nchi.

Kuhusu zoezi linaloendelea hapa nchini la kukamata wageni ambao wanaishi na kufanya kazi bila vibali halali alisema kumekuwa na taarifa za uzushi zinazoenezwa hapa nchini na nje ya nchi kuwa Serikali ya Tanzania inawafukuza wageni kwa vile haihitaji raia wa kigeni hapa nchini.

Amesema taarifa hizo ni za uongo zinazolenga kuichafua Tanzania katika jumuiya ya kimataifa na kusema raia wa kigeni wanaokamatwa ni wale tu wasio na vibali halali vya kuishi na kufanya kazi hapa nchini.

Amesema zoezi hilo ni la kawaida na linafanywa kufuatana na Sheria za Uhamiaji lakini halitawahusu wageni wenye vibali halali vya kufanya kazi na kuishi nchini.

Kati ya mwaka 2014 na Januari 2016 Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imetoa vibali vya ukaazi kwa jumla ya wageni 40,765 toka mataifa mbalimbali na idadi hiyo inaendelea kuongezeka siku hadi siku.

Wageni waliofukuzwa kwa sababu mbalimbali mwaka 2015 ni 1,642.

Aidha, kati ya 08 Desemba, 2015 na 14 Januari, 2016 raia wa kigeni waliokamatwa kwa kuishi na kufanya kazi nchini bila vibali halali ni kama ifuatavyo:
  1. Burundi 284
  2. Kenya 26
  3. Uganda 13
  4. Somalia 7
  5. Ethiopia 157
  6. DRC 34
  7. China 285
  8. India 41
  9. Zambia 40
  10. Nigeria 08
  11. Lebanon 01
  12. Ivory Coast 10
  13. Madagascar 05
  14. Malawi 27
  15. Korea 09
  16. Zimbabwe 01
  17. Ghana 01
  18. Rwanda 03
  19. Afrika Kusini 01
  20. Wenye uraia wa utata 11.
Kati ya hawa, wengine wamemepelekwa katika kambi za wakimbizi, hasa raia waliotokea Burundi, wengine wamepewa amri ya kuondoka nchini na wengine kesi zao ziko katika hatua mbalimbali mahakamani.

MWISHO
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi – 24 Januari, 2016

January Makamba Awasimamisha Kazi Vigogo Watatu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC

$
0
0
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUIMARISHA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA BARAZA LA TAIFA LA HIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA-NEMC

Katika kikao kilichoitishwa na Mhe. January Makamba (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira tarehe 24 January 2016, kuhusu kuimarisha utendaji ndani ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC maamuzi yaliyofikiwa ni kama ifuatavyo:

1. Kuhusu suala la kiwanda cha kusindika minofu ya punda mkoani Dodoma, imegundulika kulikuwa na ukiukwaji mkubwa, wa makusudi na wa wazi wa miiko ya kazi kwa watumishi wa NEMC walioshughulika na kiwanda hicho. Hivyo, Mhe. Makamba ameagiza watumishi wa NEMC wafuatao wasimamishwe kazi mara moja:

a.  Dkt. Eladius Makene -Afisa Mazingira Mwandamizi,
b. Wakili Heche Suguta Manchare - Mwanasheria Daraja la II
c. Mhandisi Boniface Benedict Kyaruzi, Afisa Mazingira.Hatua nyingine za kinidhamu na kisheria zitafuatia

2. Vilevile, imebainika kwamba usimamizi wa watumishi wa NEMC siyo makini na thabiti na kusababisha malalamiko mengi kuhusu utendaji wa Baraza.

Hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Mhandisi Bonaventura Baya apewe barua ya onyo kali  na la mwisho kwa udhaifu katika usimamizi wa watumishi wa Baraza.

3. NEMC kama chombo muhimu nchini kilichopewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira inatarajiwa kazi zake zifanyike kwa ufanisi wa kiwango cha juu kulingana na majukumu yaliyoko kwenye Sheria. 

Hivyo, kwa mapungufu yanayojitokeza Mhe. Makamba, ndani ya wiki moja ataunda jopo la wataalamu wasiozidi watano ili kutathmini utendaji wa NEMC na changamoto mbali mbali katika usimamizi wa hifadhi ya mazingira na kuishauri Serikali ipasavyo.

4. Ili kuimarisha ufanisi na udhibiti wa utendaji wa NEMC, ndani ya wiki moja litatolewa Tangazo litakalokuwa na mambo yafuatayo: 

Anwani ya barua pepe (email), Nukushi (fax), Namba ya simu, Namba ya Whatsapp ili mtu yeyote mwenye malalamiko au aliyewahi kuombwa rushwa chochote na watumishi wa NEMC ambacho ni kinyume na maadili ya kazi yao atoe taarifa mara moja ili uchunguzi ufanyike na hatua zichukuliwe.

5. Kutokana na mapungufu yanayojitokeza katika utekelezaji wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira, ndani ya wiki moja, NEMC ipitie upya orodha ya wataalamu na taasisi elekezi zilizosajiliwa na kufuta wataalamu na taasisi zote ambazo zimekuwa zikikiuka maadili ya kazi zao likiwemo suala la kuwasilisha taarifa zilizo chini ya viwango, kuchelewesha kazi za wateja wao na kutowasiliana na wateja wao kuhusu hatua za utekelezaji wa maombi yao.

6. Ndani ya wiki tatu uitishwe mkutano wa dharura wa Bodi ya NEMC kujadili na kufanya maamuzi juu ya changamoto za utendaji katika Baraza.

IMETOLEWA NA
IDARA YA MAZINGIRA,
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
TAREHE 24.01.2016

Dk. Jakaya Kikwete Aula Kimataifa.......Achaguliwa Kwenye Jopo La Wenyeviti Wa Ushauri Ngazi Ya Juu Ya Afya Ya Mama Na Mtoto Duniani

$
0
0

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea kwa furaha uteuzi uliofanywa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe. Ban Ki-Moon wa kumteua Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais  Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa mmoja wa wenyeviti wa jopo la ushauri la ngazi ya juu kuhusu Afya ya Mama na Mtoto (Every Woman, Every Child) Duniani. 

Kwa niaba ya Serikali, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kwa niaba yangu binafsi napenda kuchukua fursa hii kumpongeza kwa dhati Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa uteuzi huu.

Wakati wa uongozi wa Serikali yake ya awamu ya nne, Mhe. Dkt Jakaya Kikwete amekuwa mstari wa mbele kitaifa na kimataifa katika kusimamia na kutetea huduma bora za afya ya mama na mtoto. 

Mwaka 2005, mara baada ya kuingia madarakani Mhe. Dkt Jakaya Kikwete aliagiza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuandaa Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi (MMAM) akiwa na nia ya kusogeza huduma za afya karibu na wananchi, hususan huduma ya afya ya uzazi na mtoto. Kutokana na jitihada zake hizo, vituo vya kutolea huduma za afya vya umma viliongezeka kutoka 5,172 mwaka 2005 hadi 7,247 mwaka 2015.

Mwaka 2007, Mhe Dkt. Jakaya Kikwete aliungana na Waziri Mkuu wa Norway Mhe. Jens  Stoltenberg na viongozi wengine  wa kimataifa kuanzisha Mtandao wa Viongozi wa Dunia wa kutoa msaada wa kisiasa katika ngazi ya juu kabisa na kufanya uragibishaji  (advocacy) kwa ajili ya malengo ya milenia namba 4 na 5 yanayohusu kupunguza vifo vya watoto na wanawake wajawazito. (Network of Global Leaders Advocating for MDG4 and 5).

Mwaka 2008, Mhe Dkt. Jakaya Kikwete alizindua Mpango Mkakati wa Taifa wa Kuongeza Kasi ya Kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vya watoto wachanga (Road Map to Accelerate Reduction of Maternal Newborn and Child Health 2008-2015). 

Mwaka 2014 alizindua Mpango Mkakati ulioboreshwa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vya watoto (Sharpened One Maternal Newborn and Child Health Plan 2014-2015). 

Sambamba na uzinduzi wa mpango mkakati huo, pia alizindua kadi maalum ya kutathmini utekelezaji katika afua za kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vya watoto.

Kadi hii aliikabidhi kwa Wakuu wa Mikoa wote nchini na kuwaagiza wasimamie kwa karibu na kuwa atafuatilia utekelezaji wake.

Mwaka 2010, Dkt. Jakaya Kikwete aliungana na Mhe. Ban Ki-moon wakati anatangaza nia ya kuwa na mpango mkakati wa kimataifa wa afya ya wanawake na watoto “UN Secretary General’s Strategy for Women’s and Children’s Health 2010-15”. 

Baada ya mkakati huu kukamilika Desemba  2010, Mhe. Dkt. Kikwete aliteuliwa na Mhe. Ban Ki-Moon kuwa Mwenyekiti Mwenza wa Tume ya Taarifa na Uwajibikaji kwa ajili ya Afya ya Wanawake na Watoto “UN Commission on Information and Accountability for Women’s and Children’s Health”. 

Kazi hii aliifanya kwa umahiri na weledi mkubwa kwa kushirikiana na Mwenyekiti mwenza aliyekuwa Waziri Mkuu wa Canada, Mhe. Stephen Harper. 

Tume hiyo iliwasilisha ripoti yake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwezi Septemba, 2011.  Ripoti hii iliwezesha nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuchukuwa jitihada mbalimbali za haraka na za makusudi za kuboresha afya ya mama na mtoto katika nchi zao. 

Baada ya hapo, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete aliendelea kuwa mtetezi wa afya ya akina mama na watoto, chanjo, kudhibiti malaria na UKIMWI ndani na nje ya Tanzania.

Katika kipindi cha uongozi wake, nchi yetu imepata mafanikio makubwa katika kutimiza malengo ya milenia hususani lengo namba 4 linalolenga kupunguza vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano, ambapo vifo vimepungua kutoka 112 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2005 hadi 81 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2010. 

Aidha, mwaka 2013 ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu vifo vya watoto ilionyesha kuwa Tanzania imefikia vifo 54 kwa kila vizazi hai 1,000 na hivyo kufikia lengo la Milenia namba 4 hata kabla ya mwaka 2015.

Vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi vimepungua kutoka 578 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2005 hadi 454 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka  2010.  Na kutokana na ripoti ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2014 tumefikia vifo 410 kwa kila vizazi hai 100,000.

Afya ya mama na mtoto ni kipaumbele kwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto itaendeleza juhudi hizi na kuhakikisha tunapiga hatua kufikia Malengo Endelevu ya Kimataifa (Sustainable Development Goals 2030).

Tumedhamiria kuwapa uhakika kina mama wa Tanzania wa kutopoteza maisha yao wanapotekeleza haki yao ya msingi ya uzazi. Tutahakikisha tunapunguza au kumaliza kabisa tatizo la vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga. Chini ya Kauli Mbiu ya ‘Hapa Kazi tu” ni dhahiri kuwa hili linawezekana.

Pia, tunaahidi kumpa ushirikiano Mhe. Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete katika jukumu hilo alilopewa ambalo ni heshima kubwa kwa Taifa letu. Tunamtakia kila la kheri katika utekelezaji wa majukumu yake.

Imetolewa na:
Ummy A. Mwalimu (Mb.)
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dodoma
24 Januari  2016.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya Januari 25

Watu Watatu Wafariki Dunia Baada ya Gari aina ya Noah Kugongana Uso kwa Uso na Basi la Adventure Mkoani Dodoma

$
0
0
Watu watatu wamefariki dunia papo hapo baada ya gari aina ya toyota Noah yenye namba za usajili T243 DGB lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Tabora kugongana uso kwa uso na basi la abiria la kampuni ya Adventure lenye namba za usajili T 852 CBF lililokuwa likitoka mkoani Kigoma kuelekea jijini Dar es Salaam katika kijiji cha Buingiri madukani wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
 
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 9 alasiri ambapo kwa mujibu wa mashuhuda na abiria waliokuwa ndani ya basi walisema ajali hiyo imetokana na mwendokasi wa gari aina ya Noah ambalo dereva wake alipoteza mwelekeo na kisha gari hilo kuhama na kulivaa basi na watu watatu kupoteza maisha papo hapo huku mmoja akijeruhiwa vibara.

Muda mfupi baada ya kutokea kwa ajali hiyo jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Dodoma lilifika eneo hilo na kukuta msongamano mkubwa wa magari kutokana na ajali hiyo kuziba eneo la barabara hali iliyowalazimu kuyaondoa magari hayo ili kuruhusu shughuli zingine kuendelea.

kwa upande wake kamanda wa polsi mkoa wa Dodoma David Misime akizungumza katika eneo la tukuio aliwataja miongoni mwa watu waliofariki dunia ni dereva wa Noah aliyetambulika kwa jina la Abdalah Said Hajiru mkazi wa Dar es Salaam huku maiti nyingine mbili zikishindwa kutambulika mara moja ambapo pia jeshi hilo lilifanya jitihada za kuwatafutia basi lingine abiria ili waendelee na safari yao.

Awali kabla ya vikosi vya usalama kufika eneo hilo wananchi wenye hasira walifunga barabara kwa magogo wakidai kuwa wamechoshwa na ajali katika eneo hilo na kuitaka serikali kupitia wakala wa barabara nchini Tanroads kuweka matuta ili kupunguza ajali.

Lowassa na Maalim Seif Wajifungia Dodoma Kujadili Hatma Ya Zanzibar la Sakata la Wabunge wa UKAWA Kugomea Kamati za Bunge

$
0
0

Viongozi wa juu wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), akiwamo aliyekuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema, Edward Lowassa na wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, walijifungia mjini hapa Dodoma kujadili mambo mawili mazito.

Kwa mujibu wa taarifa toka ndani ya kikao hicho, viongozi hao walijadili mustakabali mzima kuhusu kutangazwa kurudiwa kwa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar Machi 20, mwaka huu pamoja na uamuzi wa wabunge wao kugomea Kamati za Bunge.

Aidha, viongozi hao baada ya kufikia uamuzi, jana usiku walikuwa na mkutano na wabunge wa Ukawa kuwaeleza uamuzi waliofikia na nini wanachotakiwa kukifanya wakiwa bungeni.

"Ni kweli viongozi wa juu wamejadili mambo makubwa mawili, hatma ya uchaguzi wa Zanzibar na kuhusu Kamati za Bunge zilivyoundwa, taarifa kamili mtaipata baadae" kilieleza chanzo

Watumishi 6 Watiwa Mbaroni Kwa Ufisadi Wa Milioni 800

$
0
0
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Mika Nyange

WATUMISHI sita wa Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoa wa Shinyanga, wamekamatwa na Polisi.

Wafanyakazi hao ni miongoni mwa waliosimamishwa kazi hivi karibuni na wengine kuwekwa katika uangalizi maalumu kwa tuhuma za kula njama za kujipatia zaidi ya Sh milioni 800, zilitolewa na Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi.

Fedha hizo zilitolewa na mgodi huo kwa lengo la kutekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi wa halmashauri hiyo.

Waliokamatwa ni Katibu wa Bodi ya Zabuni, Joseph Maziku ambaye ni Ofisa Ugavi na Wajumbe, Kulwa Ntaudyimara (Ofisa Utumishi) na Annastazia Manumbu (Ofisa Elimu Sekondari).

Wengine ni Joachim Henjewele ambaye ni Mkuu wa Idara ya Ardhi, Elius Mollel, Ofisa Biashara na Gervas Lugodisha kutoka Ofisi ya Ugavi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Mika Nyange, alikiri kukamatwa kwa watumishi hao.

Alieleza kuwa leo atatoa ufafanuzi juu ya hatua iliyofikiwa kuhusu tuhuma za watumishi hao, baada ya kuwasiliana na Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Kahama.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Anderson Msumba, alisema watumishi hao walikamatwa juzi na Polisi baada ya kampuni moja, kati ya kampuni nyingi zilizohusika katika fedha hizo, kujitokeza katika ofisi za halmashauri kudai malipo, wakati nyaraka zake zinapishana na za kampuni iliyopewa kazi na Bodi ya Zabuni.

Nyaraka za Halmashauri zinaonesha kuwa Bodi ya Zabuni iliipa kazi Kampuni ya Noble Cliff Construction na kuonesha malipo yatafanyika kupitia akaunti ya benki ya NMB, huku madai ya kampuni hiyo yalionesha kulipwa fedha kupitia Benki ya Afrika (BOA).

Baada ya kuwepo mabishano ya kutofautiana kwa mikataba, Msumba alidai alimtuma Mweka Hazina wake kwenda kukagua akaunti hizo na kukuta ile ya BOA, ambayo kampuni hiyo ilidai ilipwe, ilishafungwa siku nyingi na ya NMB ambayo ilipitishwa na Bodi ya Zabuni, ilikuwa ikimilikiwa na mtu binafsi.

Msumba alidai hali hiyo ilionesha kulikuwa na kasoro katika mchakato wa utoaji wa zabuni. Wajumbe wote wa Bodi ya Zabuni ya Halmashauri ya Mji wa Kahama, wamekamatwa kutokana na sakata hilo na hadi jana walikuwa mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi cha wilaya.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Vita Kawawa alitoa tuhuma kuhusu fedha hizo za Buzwagi katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo hivi karibuni.

Baada ya hapo, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Abel Shija, aliwasimamisha kazi watumishi watano kwa tuhuma hizo za kutumia vibaya fedha za Mgodi wa Buzwagi. Aliagiza waliohamishwa na wanatuhumiwa, warejeshwe kujibu tuhuma zao.

Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim Aishangaa ZEC Kufuta Uchaguzi Zanzibar.........Ataka Haki Itendeke ili Kuliepusha Taifa na Machafuko

$
0
0

Waziri  Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, ameshangazwa na uamuzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kufuta uchaguzi visiwani humo.

Amesema  jumuiya za kimatifa zilishtushwa na uamuzi huo.Salim amesema kutokana   na hali hiyo, kinachotakiwa hivi sasa ni haki itendeke kwa kila kila upande kukaa na kutafuta suluhisho la kudumu.

“Tanzania haijazoea migogoro ya siasa jambo ambalo si jema katika sura ya kimataifa,” alisema.

Mwanadiplomasia huyo wa kimataifa ametoa kauli hiyo,baada ya Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha, kutangaza kufuta matokeo ya uchaguzi huo Oktoba 28, mwaka jana.

Siku chache zilizopita, Jecha alitangaza kuwa uchaguzi huo   unatarajiwa kurudiwa Machi 20  mwaka huu.

Mwanadiplomasia huyo wa kimataifa aliwahi kushika nafasi mbalimbali ikiwamo ya Katibu Mkuu    wa Umoja wa Nchi za Afrika (OAU) ambayo kwa sasa inatambulika kama Umoja wa Afrika (AU).

Alisema hatua ya kufutwa uchaguzi  wa Zanzibar ni jambo lililowashangaza  wengi kwa kuwa uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu, huku waangalizi wa ndani na nje wakiusifia katika ripoti zao.

“Ni hatua ambayo imewashangaza wengi…imeibua sintofahamu kubwa katika nchi yetu kwa sababu uchaguzi uliopita Tanzania ilipata sifa,baada ya uchaguzi kufanyika kwa amani na utulivu. Lakini kitendo cha kufutwa kumewashangaza wengi na bado suala hili halieleweki.

“Pia hili jambo sidhani kama ni la mtu mmoja…sidhani kama ni la Jecha peke yake. Huu si mustakabali mzuri kabisa, Zanzibar ni nchi ndogo, lakini ina historia kubwa kisiasa hivyo juhudi za pamoja zifanyike kutatua mgogoro huu kwa matakwa ya Watanzania kwa ujumla.

“Viongozi wasisitize amani na utulivu na katika hili la Zanzibar kwa kweli haki itendeke na waache ushabiki wa vyama iwe CCM au Upinzani, wote waweke ushabiki pembeni na watatue mgogoro huu kwa mustakabali wa Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla,” alisema Dk. Salim.

Alisema ingawa viongozi mbalimbali wamekutana na kufanya mazungumzo bila kupata suluhu,pande zote ziendelee kukutana hadi suluhu ya pamoja ipatikane.

Salim, alisema kuendelea kuachia hali hiyo iendelee  kuna hatari ya kujenga uhasama zaidi hivyo ni vema viongozi wafikirie zaidi masilahi ya Zanzibar.

“Nchi ipo katika hali mbaya, migogoro iko kila pahala,Watanzania hatujazoea. Jambo hili la Zanzibar likiendelea litazaa matatizo makubwa katika Taifa letu.

“Waliangalie kwa uzito hata kama tarehe ya uchaguzi imetangazwa waendelee na mazungumzo,” alisema mwadiplomasia huyo  wa kimataifa.

Dk. Salim ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, alipoulizwa   kama Kamati Kuu ya chama tawala katika vikao vyake ilijadili suala la Zanzibar, alisema limegusiwa ingawa haikuzungumzwa na ni nini  kifanyike.

“…japo sikushiriki vikao vyote hivi karibuni kwa sababu nilikuwa katika majukumu mengine, jambo hili limezungumzwa japo halikugusiwa nini kifanyike.

“Jambo hili, linastahili kupewa kipaumbele hata katika vikao vya Kamati ya Kuu ya CUF (Chama cha Wananchi) na vyama vingine kwa sababu madhara yakitokea yataathiri kila upande,” alisema.


Wanasheria Waikosoa ZEC Kufuta Uchaguzi Zanzibar....Wamtaka Rais Magufuli Aingile Kati Kuokoa Jahazi

$
0
0

Wanasheria nchini wamemtaka Rais John Magufuli ingilie kati sakata la Zanzibar kwa sababu sintofahamu inayoendelea kutokea visiwani humo ni aibu ya Tanzania mbele ya Jumuiya ya Kimataifa.

Wakizungumza jana katika mdahalo ulioandaliwa na Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) kujadili changamoto za kisheria zilizojitokeza katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Oktoba 25 mwaka 2015, wanasheria hao walisema Rais Magufuli anaweza kutumia nafasi yake kumaliza sintofahamu hiyo.

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman alisema kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar kumekiuka Katiba na sheria mbalimbali za uchaguzi zinazosimamia uchaguzi.

“Ingawa haya yanatokea Zanzibar, lakini ni suala la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunamtaka Rais Magufuli katika kutumbua majipu alione na hili la Zanzibar tunataka alipasue kabisa.”

Aliongeza kuwa, “kuendelea kutembea nalo linakuwa mzigo mkubwa, kwa hiyo tunamtaka kulipasua ili kutua hilo zigo.”

Othman alisema hakuna sheria yoyote inayompa mamlaka mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kufuta uchaguzi.

Alisema hata vifungu alivyovitumia Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha wakati anatangaza kufuta uchaguzi, vinazungumzia mambo mengine kabisa.

“Ni vema Rais Shein (Ali Mohamed) akajiuzulu kwa sababu yeye ni sehemu ya tatizo la Zanzibar. Hawezi kuendelea kugombea wakati yeye ndiye aliyesababisha mkwamo huo wa kisiasa,” alisema mwanasheria huyo.

Wakili Fatma Karume ambaye pia ni mtoto wa rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume alisema kuna haja ya kubadilisha kifungu cha 119 (10) kinachotaja sifa za mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi kwamba anatakiwa kuwa jaji wa Mahakama Kuu au mtu yoyote mwenye kuheshimika.

“Ni jambo la kushangaza kabisa, yaani Jecha anapewa uenyekiti wa Tume wakati hajui mambo ya kisheria halafu makamu wake ndiyo jaji. Hapa kuna tatizo na amewekwa hapo kwa ajili ya kulinda maslahi ya watu,” alidai wakili huyo.

Fatma alisema hakushangazwa na kitendo cha wanasheria kushindwa kwenda mahakamani kufungua kesi ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi kwa sababu anajua hawana imani na mahakama. Alisema yule aliyemteua Jecha (Rais Shein) ndiye aliyewateua pia majaji.

Mwakilishi wa Chama cha Wananchi (CUF), Ismail Jussa alisema Jecha ni kada wa CCM, hivyo hafai kuongoza Tume hiyo kwa sababu anaonyesha maslahi yake wazi wazi kwa chama hicho.

“Katika uchaguzi wa mwaka 2010, Jecha aligombea katika jimbo la Amani kupitia CCM akashindwa. Shein akaona amteue kuwa mwenyekiti wa ZEC ili kulinda maslahi yake.”

Jecha alitangaza kufuta uchaguzi huo wa rais, wawakilishi na madiwani visiwani humo akisema kanuni na taratibu zilikiukwa.

Uchaguzi huo kwa sasa umepangwa kufanyika Machi 20, mwaka huu.    

Hussein Bashe Amvaa Benard Membe Kwa Kumkosoa Rais Magufuli.......Amtuhumu Kutumia Safari Za Nje Kusafiri Na Hawara Zake!

$
0
0
MBUNGE  wa  Nzega Mjini kwa tiketi ya  Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hussein Mohammed  Bashe amejitokeza hadharani na kumtaka Waziri wa Zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kuacha kulipotosha taifa kutokana kauli zake juu ya utendaji wa Rais John Magufuli.
 
Hivi karibuni, Membe alikosoa hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Rais Magufuli. Pia, alipinga hatua ya kutangaza kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar.
 
==>Kupitia  ukurasa wake wa facebook, Bashe  ameandika;
 
Membe Amuache Ndg Magufuli Afanye kazi.
Membe amekua waziri for ten yrs ametimiza wajibu wake amuache Ndg Magufuli atimize wajibu wake. Aliomba Urais Hajateuliwa asubiri 2020 or 2025 ili akipita aanzishe uvasko dagama tena.

Hoja kuwa serekali haijapungua ama kubwa au ndogo  ama hoja kuwa Safari za nje nimuhimu na Rais amekosea kufuta ama kupunguza ni hoja ya mwanasiasa muflisi .

Membe amekua sehemu ya mfumo dhaifu ulotufikisha hapa kama Taifa,amefaidika na safari za nje yeye binafsi bila manufaa kwa nchi,.

Membe akumbuke kila Rais ana Vission yake .Magufuli anaamini matatizo ya Taifa letu yatamalizwa na sisi wenyewe kwa kudhibiti matumizi ya hovyo na yasiyoyalazima na si kwa safari za Ulaya na kuendeleza Tabia ya Kuwa Omba omba.

Ni muhimu membe afahamu Magufuli ana style yake ,tutampima kwa matokeo as of now hatujaona athari za safari.Membe kama yeye binafsi anatakiwa aseme kufutwa safari kulimuathiri yeye binafsi kwa kukosa nafasi ya Ukatibu mkuu wa Commonwealth thats why leo anakosoa.

Tunafaham maamuzi mengi ya Magufuli kwa sasa hayatafurahisha wengi walofaidika na Miradi kama NIDA  Pesa za Gadafi, walofaidika na Matumizi Mabaya ya Madaraka katika Awamu ya nne, Majipu mengi yanayosubiri Kutumbuliwa ama yaliyotumbuliwa yatafanya jitihada kukosoa muelekeo wa Serekali ya awamu ya Tano.

Hoja ya kutokua na mabalozi magufuli hana siku 100 yeye amekua waziri wa mambo ya nje for 8 yrs hakuona umuhimu wakati huo? Kuwa na balozi kwenye nchi ni jambo Mtambuka na hasa linatazamwa zaidi kiuchumi na kisiasa .

Amekua mmoja wa mawaziri walioua foreign relation yetu wakati wake kumekua na malalamiko mengi juu ya mis use of funds katika wizara yake, kipindi chake Bernad Membe safari za nje walisafirishwa ma girlfirend kwa kutumia Pesa za Umma.

Nimuhimu membe aheshimu Vission ya Magufuli na style yake inafahamika ameathirika directly or Indirect na mchakato wa Majipu na kufunga safari za nje.

Binafsi kama mbunge naunga mkono style ya Magufuli ya uongozi. Aliwahi kusema Sankara " You cannot carry fundamental change without a certain amount of Madness"

Mabadiliko anayofanya sasa Ndg Magufuli yanahitaji Roho Ngumu, wendawazimu kidogo, Kuungwa mkono na wananchi wa kawaida kwani walofaidika na udhaifu wa awali watajitahidi kutaka kuzuia mabadiliko yoyote ambayo yanamfaidisha aliekuwa akinyonywa hapo awali 

Tutasikia watu wa aina ya Membe wengi kwakua style ya Magufuli inaathiri mfumo wao wakuwanyonya wengi na wachache kufaidika.

Wassalaam.

Membe Amuache Ndg Magufuli Afanye kazi.Membe amekua waziri for ten yrs ametimiza wajibu wake amuache Ndg Magufuli...
Posted by Hussein Mohammed Bashe on Sunday, January 24, 2016

Jifunze Kutengeneza Pipi Za Kihindi ,uongeze Kipato Chako.

$
0
0

 ==>Wewe  ni  kijana  wa  kitanzania ?
 ==>Unataka  kuongeza  kipato  chako ?
Kama  jibu  lako  ni NDIO  basi   hii  ni  HABARI NJEMA  SANA  KWAKO. Taasisi  ya  NEEMA  INSTITUTE  OF  N.G.O  MANAGEMENT  kupitia MRADI  WA  UANZISHAJI, UENDESHAJI  NA USIMAMIZI  WA BIASHARA  NDOGONDOGO  inatangaza  nafasi  za  kushiriki  katika  SEMINA  YA  UJASIRIAMALI.   Somo  litakalo fundishwa  ni

 UTENGENEZAJI  WA  PIPI  ZA  KIHINDI.
Pipi  za  Kihindi  ni  bidhaa  inayo  pendwa  sana  na  watoto  wa  shule  ya  msingi  na  hata  sekondari.
 
Washiriki  katika  Semina  hii, watapewa nafasi  za  biashara  katika  shule mbalimbali  za  msingi  zilizopo  jijini  Dar  Es  Salaam.

ADA  YA  KUSHIRIKI  KATIKA  SEMINA  HII    NI  SHILINGI  ELFU   HAMSINI    TU (Tshs.50,000/=)

Fomu  za  kujiunga  katika  semina  hii, zinapatikana  ofisini  kwetu  kwa gharama  ya  Shilingi  ELFU  KUMI  NA  TANO  TU( Tshs.15,000/=).

Tunapatikana  UBUNGO   Dar  Es  Salaam, jirani  na  Shule  Ya  Msingi  Ubungo  National  Housing  nyuma  ya  jengo  la  Ubungo  Plaza.

Mwisho  wa  kuchukua  fomu  ni  tarehe  30  JANUARY 2016  saa  nane  kamili  mchana.

Semina   itafanyika  kwa  siku  tano,  kuanzia  tarehe  01  Februari 2016  hadi  tarehe  05  February 2016.

Kwa  maelezo  zaidi  kuhusu  semina  hii , wasiliana  nasi  kwa  simu  namba  0766  53  83  84    AU   Tembelea  blogu  yetu :www.neemainstitute.blogspot.com

FAIDA   ZA  KUSHIRIKI  KWENYE  SEMINA  KUHUSU  MAFUNZO  YA  UTENGENEZAJI WA  PIPI  ZA  KIHINDI.
Taasisi   ya  Neema  Institute  Of  N.G.O  Management  yenye  ofisi  zake  jijini  Dar  Es  Salaam, katika  eneo  la  Ubungo  imeandaa    SEMINA  KUHUSU   UTENGENEZAJI  WA  PIPI   ZA  KIHINDI  ambayo  itafanyika  kwa  muda  wa  siku  tano, kuanzia  tarehe  01  FEBRUARY  2016  hadi  tarehe  05 FEBRUARI 2016.

Lengo  la  semina  hii  ni  kuwasaidia  wajasiriamali  wadogo  wadogo  na  wale  wa  kati, kupata  ujuzi  utakao  wasaidia  kuongeza  vipato  vyao.

Zifuatazo  ni   faida   za  kushiriki  katika  semina  hii:
1.Mafunzo  yanafundishwa  kwa  njia  ya  nadharia  na  vitendo  ( Theory  and  Practical )kila  siku  kwa  siku  zote  tano  za  mafunzo .  Katika  siku  zote  tano  utakazo  hudhuria  mafunzo  haya, utapata  kujifunza  kwa  vitendo  jinsi  ya  kutengeneza  pipi  za  kihindi. Lengo  letu  ni  kuhakikisha  kila  anaye shiriki  katika  semina  hii, anatoka  akiwa  amewiva  katika  suala  zima  la  utengenezaji  wa  pipi.

2.     NI    BIDHAA  YENYE  SOKO  LA  UHAKIKA :
Pipi   za  kihindi  ni  pipi  zinazo  tengenezwa  kwa  kutumia  malighafi  iitwayo   sukari  guru  pamoja  na   viambatano  (ingredients )  vingine .   Pipi  hizi  ni  bidhaa  inayo pendwa  sana  na  watoto  wanao  soma  katika  shule  za  msingi  na  sekondari .  Kwa  muda  mrefu sasa, wahindi  wanajulikana  dunia  nzima  kwa  kuwa   na  umahiri  mkubwa  wa  kutengeneza   vitu  vitamu  tamu pamoja  na  vyakula  vizuri  kwa  ujumla.  Hivyo  basi  suala  la  pipi  za  kihindi.

Utafiti  wetu  umetuwezesha  kugundua, kwa  biashara  ya  kuuza  pipi  za  kihindi   mashuleni, unaweza  kuingiza  faida  ya  kati  ya  shilingi  Elfu Thelathini  ( Tshs.30,000/=)  hadi   Shilingi  Elfu  Themanini  (Tshs.80,000/=)  kwa siku, kutegemeana  na  kiwango  cha  uzalishaji  wako.
 
 Na  kama  utapata  nafasi  katika  shule  zaidi  ya  moja, kipato  chako  kitakuwa  kikubwa  maradufu.

3.UHAKIKA  WA  KUPATA  NAFASI  YA  BIASHARA  KWENYE  SOKO  LA  UHAKIKA .
Baada  ya  kuhitimu  mafunzo,  kila  mshiriki, atapewa  nafasi  ya  biashara    katika  shule  ya  msingi  yenye  idadi  kubwa  ya  wanafunzi iliyopo  jijini  Dar  Es  Salaam  na  hivyo  kumuwezesha  kutengeneza  kipato  cha  uhakika, kupitia  biashara  ya  pipi za  kihindi. Sisi  kama  Taasisi  tunazo  nafasi  zaidi ya  mia ( 100 ) katika  shule  mbalimbali  za  msingi  zilizopo  jijini  Dar  Es  Salaam zenye  idadi  ya  wanafunzi  kati  ya  mia  nne  (400)  hadi  elfu  moja  (1000).
Nafasi  hizi  za  biashara  tutazitoa  kwa   watakao  hitimu  mafunzo  yetu.
 
Nafasi  hii  utaipata  baada  ya  kumaliza  mafunzo. Mafunzo  yanaanza  Jumatatu na  kuisha  Ijumaa. Siku  hiyo  hiyo  ya  Ijumaa  unapewa  details  za  shule  utakayo  enda  kufanyia  biashara  yako, Jumamosi  na  Jumapili, unazitumia  kufanya  maandalizi  ya  kutengeneza  pipi  zako, na  Jumatatu  unaanza  kuingiza  pesa  kupitia  shughuli  ya  kuuza  pipi  kwenye  shule  ambayo  tutakuwa  tumekupangia.

(  FURSA  YA  KUPATA  NAFASI  YA  BIASHARA  INAWAHUSU  WALIOPO  DAR  ES  SALAAM  TU  )

4.MTAJI  MDOGO  WA  BIASHARA :  Mradi  wa  kutengeneza  na  kuuza  pipi za kihindi  mashuleni, hauhitaji kiasi  kikubwa  cha  fedha  za  mtaji. Hata  kwa  wajasiriamali  ambao  ndio  kwanza  wanaanza  ujasiriamali na  hawana uwezo mkubwa wa  kifedha  wanaweza  kumudu.

5.UTAPATA  FURSA  YA  KUUNGANISHWA  NA  WAJASIRIAMALI  WENZAKO  NA  KUUNDA  TAASISI  ISIYO  KUWA  YA  KISERIKALI.

Washiriki  wa  mafunzo  haya, wataunganishwa  pamoja  na  kuunda  Taasisi  isiyo  kuwa  ya  kiserikali ( N.G.O ), ambapo  wata saidiwa  kuanzisha  VICOBA  pamoja  na  kufundishwa  utengenezaji  wa  bidhaa  nyinginezo  zinazo  pendwa  sana  na  watoto  mashuleni  kama  vile  Ubuyu  wa  Zanzibar  nakadhalika.

6.SEMINA  INATOLEWA  KWA  MUDA  AMBAO  HAUWEZI KUHARIBU  RATIBA  YAKO.
Kutakuwa  na  madarasa  ya  asubuhi  pamoja  na  madarasa  ya  jioni. Madarasa  ya  asubuhi  yanaanza  saa  nne  hadi  saa  sita. Na  madarasa  ya  jioni  yanaanza  saa  kumi  hadi  saa kumi  na  mbili  Hivyo  basi  kama  wewe  ni  muajiriwa  na   hauna  nafasi  muda  wa  asubuhi, unaweza  kupata  fursa  ya  kushiriki  katika  semina hii wakati  wa   jioni  kuanzia  saa  kumi  hadi  saa  kumi  na  mbili.

7.UNAWEZA KUJIFUNZA  KUTENGENEZA  PIPI  ZA  KIHINDI  NA  UKAAJIRI  VIJANA WENGI  WA  KAZI  NA  KUTENGENEZA  FEDHA  MARADUFU.

Unaweza  kujifunza  kutengeneza  pipi  hizi, halafu  ukatafuta  nafasi  ya  biashara  kwenye  shule  mbalimbali  za  msingi   na  kuwaweka  vijana  wa kazi.   Ukipata  nafasi  katika  shule  nyingi, maana  yake  hata  kipato  chako  kitaongezeka  mara  dufu.

Hizo  ni  baadhi  ya  faida  za  kushiriki  katika  mafunzo  haya.

KWA   WALIOPO   NJE   YA  MKOA  WA  DAR  ES  SALAAM.
Kwa  waliopo  nje  ya  mkoa  wa  Dar  Es  Salaam, mafunzo   haya yatatolewa  kwa  njia  ya  Posta. Utapatiwa  DVD  na  VITABU  vinavyo  elezea  STEP  by  STEP  kuhusu namna  ya  KUTENGENEZA  PIPI  ZA KIHINDI.

JINSI   YA  KUJIUNGA  NA  MAFUNZO  HAYA  KWA  WAOMBAJI  KUTOKA  NJE  YA  DAR  ES  SALAAM.
Kama  upo  nje  ya  mkoa  wa  Dar  Es  Salaam, na  unataka  kushiriki  katika  mafunzo  haya, tuandikie  barua  pepe  ya  maombi  ya  kushiriki  katika  mafunzo  haya. Barua  pepe  yetu  ni :  neemainstitute@gmail.com
 
Mwisho  wa  kupokea  maombi  ni  tarehe  30 JANUARY  2016.

EWE  MZAZI !  EWE  MLEZI ! UNA NGOJA  NINI ?
MLETE  KIJANA  WAKO  APATE   MAFUNZO  YATAKAYO  MSAIDIA   KUINGIZA  KIPATO  CHAKE.

EWE  KIJANA!  ZAMA  ZA  KUAJIRIWA  ZIMEPITWA  NA  WAKATI. USISUBIRI  KUAJIRIWA.  NJOO  UPATE  UJUZI  UTAKAO  KUSAIDIA  KUINGIZA  KIPATO KIZURI

Idris Sultan Amtundika Mimba Wema Sepetu

$
0
0

Mshindi wa Big Brother Afrika, Idris Sultan amepasua jipu kuhusu uhusiano wake na Wema Sepetu ambao umekuwa ukizua utata kila siku huku mashabiki wao wakiubatiza majina mbalimbali.

Idris ameweka wazi kuhusu hali ya uhusiano wao na namna anavyomchukulia Wema Sepetu kama mkewe. 

Kwa mujibu wa maelezo yake, yeye na mrembo huyo wanatarajia kupata mtoto ingawa bado hawajafahamu jinsi ya mtoto huyo.

==>Leo, Idris amepost kwenye Instagram ujumbe unaoweka wazi maisha yake na ‘mkewe’ Wema.

“Me and You are not the ordinary. I sleep,eat, talk and wake up to only thinking about you. As much as utadhani kuwa you are blessed to have me no no i am blessed to have you. 

"At 1st it was weird me kuangalia ndani ya kabati langu kuona nguo zako na viatu au ukiwa unaongea na mimi unaniambia vitu kama “Hivi baby unahisi akiwa wa kiume utafanyaje maana naona umekazana na wa kike” au ukiingia jikoni kwangu and take over my house with good food. The way you look at other women wakinisogelea, how you always know when i need a kiss or a tight hug. 

"The way you force me kuangalia Disney channel, how you wake up early these days to make me breakfast. I might bring you the most beautiful rose flower in the world and it will never look even half as beautiful as you are. When you’re jealous unasonya sonya, when am jealous i smile.

" I would move mountains and planets just to make you happy. I will protect you, love you, spoil you, fight with you, cook with you, watch movies together, drive at night for no reason, sit with you and just stare at the stars. You’re more than i ever asked for, you’re my everything “My Wife” heart_eyes,” Idris aliandika.
Me and You are not the ordinary. I sleep,eat, talk and wake up to only thinking about you. As much as utadhani kuwa you are blessed to have me no no i am blessed to have you. At 1st it was weird me kuangalia ndani ya kabati langu kuona nguo zako na viatu au ukiwa unaongea na mimi unaniambia vitu kama "Hivi baby unahisi akiwa wa kiume utafanyaje maana naona umekazana na wa kike" au ukiingia jikoni kwangu and take over my house with good food. The way you look at other women wakinisogelea, how you always know when i need a kiss or a tight hug. The way you force me kuangalia Disney channel, how you wake up early these days to make me breakfast. I might bring you the most beautiful rose flower in the world and it will never look even half as beautiful as you are. When you're jealous unasonya sonya, when am jealous i smile. I would move mountains and planets just to make you happy. I will protect you, love you, spoil you, fight with you, cook with you, watch movies together, drive at night for no reason, sit with you and just stare at the stars. You're more than i ever asked for, you're my everything "My Wife" 😍
A photo posted by Idris Sultan (@idrissultan) on

Waziri wa Ardhi , William Lukuvi Aagiza Kukamatwa kwa Watendaji wote Waliohusika na Kugawa Shamba la Ekari 3,500 Mkoani Morogoro.

$
0
0

Serikali imeliagiza jeshi la polisi na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa kuwakamata, kuwahoji na kuwafikisha mahakamani viongozi na watendaji wote hata kama wamestaafu madaraka yao, walio husika kutoa shamba la hekari 3,500,Morogoro.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, baada ya kutembelea kijiji hicho cha Mlilingwa,Ngerengere  kwa lengo la kujiridhisha juu ya mwenendo mzima wa utoaji wa eneo hilo ambao ulitiliwa mashaka na Rais.

Mhe. Lukuvi amelazimika kukagua sahihi za wana kijiji walio orodheshwa majina yao ambapo wengi wa waliohojiwa wamezikana sahihi hizo na kueleza kushangazwa na hali hiyo na hata baadhi ya majina yaliyotumika  sio ya wanakijiji wenzao na kudai katika kikao hicho hakuna mwenyekiti, mjumbe wala mtendaji aliyekuwa kwenye sakata hilo aliyehudhuria kikao hicho.

Mwakilishi wa kampuni ya Oxfod Trading LTD aliyehudhuria mkutano huo wa kijiji, ameonekana kushindwa kujieleza vyema pale alipokuwa akihojiwa maswali kwa madai bado ni mgeni katika kampuni hiyo na hakuwepo wakati wa mkutano wa kuidhinisha kutolewa kwa eneo hilo.

Baada ya kujiridhisha, waziri Lukuvi ameagiza mtu huyo kukamatwa na ofisa wa polisi ili kusaidia kukamatwa kwa wahusika wote wa sakata hilo na pia kuagiza uchunguzi kufanywa kwenye ofisi zote ili watakaobainika kuhusika na udanganyifu huo wafikishwe mahakamani

Waziri Lukuvi amesema zoezi hilo litakuwa endelevu nchi nzima hivyo kutahadharisha kama kuna mwekezaji yeyote aliyejipatia ardhi kwa njia ya udanganyifu bila kufuata taratibu, ni vyema akaanza upya kufuata maagizo ya serikali,na ikibainika kuna kosa popote shamba lake litafutiwa milki yake na kubadilishwa matumizi kwa mujibu wa sheria.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images