Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Bodaboda Zinazopandisha ‘Mishikaki’ Kupigwa Picha

$
0
0
KATIKA kukabiliana na madereva wa pikipiki wanaopakia abiria zaidi ya mmoja maarufu mshikaki, Jeshi la Polisi mkoani Pwani litatumia mbinu mpya ya kuwapiga picha madereva hao na kuwakamata baadaye wakiwa kwenye vituo vyao. Jeshi hilo litatumia mbinu hiyo ili kuepusha ukamataji kwa kuwakimbiza wale wanaofanya hivyo kwa lengo la kuepuka kusababisha ajali wakati wa kuwakamata madereva hao

Tanesco Yazuia Shughuli za Kilimo Karibu na Nguzo

$
0
0
SHIRIKA la Umeme (Tanesco) limetoa angalizo kwa wanaoendesha shughuli za kilimo, kwa kuwaambia hawatakiwi kulima karibu na nguzo kwani wanapaswa kuacha meta 30 kila upande. Meneja wa Tanesco wa Mkoa wa Shinyanga, Mathias Solongo alitoa angalizo hilo kutokana na kuwapo malalamiko ya wananchi zaidi ya 50 wa kijiji cha Seseko kata ya Mwamalili manispaa ya Shinyanga, dhidi ya Tanesco kuwakatia

Atiwa Mbaroni Akituhumiwa Kumpa Ujauzito Dada Yake wa Miaka 14

$
0
0
POLISI wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa inamshikilia mkazi wa kijiji cha Ulinji, Manispaa ya Sumbawanga mwenye umri wa miaka 28 akituhumiwa kumpatia ujauzito dada yake mwenye umri wa miaka 14 anayesoma darasa la saba. Inadaiwa kuwa mtuhumiwa ambaye amemtaliki mkewe, alirejea kuishi nyumbani kwa wazazi wake kijijini Ulinji miaka miwili iliyopita kabla ya kumpatia ujauzito mtoto huyo wa

Mwanamke Akutwa Kwenye Paa La Jengo La Wizara Ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam

$
0
0
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwanamke mmoja amepanda katika paa la jengo la Wizara ya Fedha na Mipango huku tukio hilo likizua sintofahamu kwa wafanyakazi wa wizara hiyo na wapita njia. Tukio hilo lilitokea jana Dar es Salaam majira ya asubuhi ambapo mwanamke huyo anayedaiwa kuwa raia wa Kenya alipanda juu ya paa hilo na kuanza kupiga kelele. Katika tukio hilo, inadaiwa

Maalim Seif Ajitoa Mazungumzo Zanzibar....Afanya Kikao Kizito Cha Siri Na Lowassa Dar es Salaam

$
0
0
Wakati sintofahamu ya hali ya kisiasa Zanzibar ikiendelea, aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amejitoa kwenye mazungumzo ya maridhiano yaliyokuwa yakiendelea visiwani humo.Mpaka sasa Maalimu Seif, Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein, marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi, Dk. Salmin Amour Juma,  Amani Abeid Karume na  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,

Mahakama Yamwachia Huru David Kafulila

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma imemuachia huru aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kupeleka mashahidi mahakamani hapo kwa zaidi ya siku 60 kwa mujibu wa kifungo cha 25 cha kanuni ya adhabu. Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Slivester Kainda, katika kesi iliyokuwa ikimkabili Kafulila

CCM Kupinga Ushindi wa Meya wa Ilala Mahakamani...... Uchaguzi Meya wa Jiji La Dar ni Jumamosi

$
0
0
Uchaguzi wa kumpata meya wa Jiji la Dar es Salaam unatarajiwa kufanyika Jumamosi katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee, Manispaa ya Ilala. Hatua hiyo inafuatia kukamilika kwa uchaguzi wa Mameya wa Manispaa za Kinondoni, Ilala na Temeke. Kati ya hizo halmashauri mbili zilikwenda kwa Ukawa na moja CCM. Msemaji wa Halmashauri Jiji la Dar es Salaam, Gaston Makwembe alisema jana kuwa

Serikali Yatoa Kauli Kuhusu Dawa Mpya ya UKIMWI

$
0
0
SERIKALI imesema kama Shirika la Afya Duniani (WHO), litapitisha matumizi ya dawa mpya ya ugonjwa Ukimwi wataitumia, lakini kwa sasa haiwezi kuzungumzia tafiti za ugonjwa huo ambazo zipo nyingi. Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Michael John, amesema kwa sasa zipo tafiti nyingi, lakini wao kama wizara wanasubiri mwongozo kutoka WHO ambao ndiyo

Wabunge wa CCM Wapeana Mikakati ya Kuwakabili Wabunge wa UKAWA.......Wamgeuka Rais Magufuli Kuhusu Bomoabomoa

$
0
0
Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamemgeuka Rais Dk. John Magufuli na kutaka kasi yake iangaliwe upya vinginevyo inaweza kukigharimu chama hicho tawala kwa wananchi. Tangu Rais Magufuli aingie madarakani kumekuwa na hatua mbalimbali zilizochukuliwa ikiwamo kuifumua Bandari ya Dar es Salaam na kusimamisha vigogo kadhaa pamoja na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Kampuni

Ofisi ya Kamishna Mkuu TRA Yavunjwa, Kompyuta Mbili Zaibiwa

$
0
0
Watu wasiojulikana  wamevamia  na  kuvunja  ofisi  ya  kamishna Mkuu wa Mamlaka  ya  Mapato  Tanzania (TRA) na kuiba kompyuta  na  vifaa vingine. Habari tulizozipata ambazo zimethibitishwa  na Polisi kanda maalumu  ya  Dar  es  Salaam zinasema miongoni mwa kompyuta zilizoibiwa  ni  ile  iliyokuwa  inatumiwa  na  Dr Philip Mpango  alipokaimu nafasi ya  Kamishna mkuu wa TRA  kabla ya

Serikali yakanusha uzushi unaoenezwa katika mitandao ya kijamii kumhusu Rais Magufuli

$
0
0
Hivi karibuni kumejitokeza uzushi unaosambazwa katika mitandao ya kijamii ya ndani ya nchi na nje ya nchi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amefukuza wageni kutoka nje  waliokuwa wanafanyabiashara zao nchini kwa kuwa serikali yake haitaki wageni kufanya biashara nchini.Serikali haijafukuza wageni kutoka nje ya nchi kufanya biashara nchini

Mkata Vichwa wa Kundi la kigaidi la Dola ya Kiislam (IS) Naye Kauawa

$
0
0
MKATAJI vichwa vya raia kutoka mataifa ya magharibi katika kundi la kigaidi la Dola ya Kiislam (IS), Mohammed Emwazi, ametangazwa kuuawa. Emwazi anatambuliwa zaidi kwa jina la Jihadi John, ndiye aliyekuwa akitumiwa zaidi kwenye video ambazo zilikuwa zikioneshwa na kundi hilo wakati wa kutekeleza mauaji ya raia wa mataifa ya magharibi walilokuwa wakikamatwa na kundi hilo. Raia huyo wa

Ratiba ya Mkutano wa Wabunge Wote Pamoja na Vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge Tarehe 20_25 January

$
0
0
Ofisi ya Bunge inapenda kuwafahamisha Waheshimiwa Wabunge na Wananchi kwa ujumla kuwa, uteuzi wa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge utafanyika kesho Alhamisi tarehe 21 Januari, 2016, na kufuatiwa na Uchaguzi wa Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati husika pamoja na Kamati kupatiwa maelezo juu ya Wajibu, kazi na Mipaka ya kazi ya Kamati na kupokea na kujadili Mpango kazi wa Kamati

Balozi Seif Ali Idd Akutana na Rais Magufuli leo Ikulu.....Amhakikishia Kuna Amani Zanzibar na Wanasubiri Tarehe ya Uchaguzi itangazwe

$
0
0
Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Idd amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa hali ya Zanzibar ni shwari na Wazanzibar wanasubiri kutangaziwa tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi. Balozi Seif Ali Idd ameyasema hayo Ikulu jijini Dar es salaam leo tarehe 20 Januari, 2016 mara baada ya kukutana na kufanya

Daktari feki anaswa hospitali ya Sekou Toure Mwanza

$
0
0
MTU mmoja aliyejulikana kwa jina la David Igwesa, anayedaiwa ni daktari feki amekatamatwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure huku akiwa  amemtapeli mgongwa Sh. 170,000 kwa ajili ya kumfanyia upasuaji. Daktari huyo feki amekamatwa leo saa 4 asubuhi katika hospitali hiyo, baada ya mgonjwa aliyetapeliwa fedha hizo kuanza kudai risiti za fedha alizotoa kwa ajili ya kufanyiwa

Tangaza Biashara Yako Au Bidhaa Yako Kwenye Mtandao huu Kwa BEI NZURI Kabisa

$
0
0
Tunakaribisha  matangazo  ya  aina  zote.Bei  zetu  ni  nzuri  sana  na  kamwe  hutajuta  kutangaza  biashara  yako  kupitia  mtandao  huu.... Mpekuzi  inatembelewa  na  Watu  zaidi  ya  laki 3  kwa  siku.Kati  yao, 46%  ni  wanawake  na  54%  ni  wanaume. Kama  una  tangazo, basi  wasiliana  nasi  kwa  kutuandika  email  ambapo  tutakutumia  bei  ya  matangazo. Email  yetu: 

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli Aongoza Waombolezaji Kuaga Mwili Wa Marehemu Leticia Nyerere

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho  Kikwete nyumbani kwa Baba wa Taifa  Msasani Dar es salaam wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere aliyefariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa  Januari 20, 2016.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

Salam za Rambirambi za Rais Magufuli kwa Msiba wa Asha Bakari Makame , Waziri wa Zamani wa SMZ

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kufuatia kifo cha Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Bi. Asha Bakari Makame kilichotokea jana tarehe 19 Januari, 2016 huko Dubai. Bi. Asha Bakari Makame ambaye kwa nyakati

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Januari 21

TTCL Kurejea Kuwa Mali Ya Umma Kwa Asilimia 100.

$
0
0
SERIKALI ipo katika hatua za mwisho za kuilipa kampuni ya Bharti Airtel ili kurejesha umiliki wa asilimia 100 katika Kampuni ya Simu Tanzania, TTCL. Uamuzi huo unaotarajiwa kutekelezwa kabla ya mwisho wa mwezi huu utaiwezesha TTCL kurejesha hisa zake 35% zilizonunuliwa na Airel mwaka 2001 na kuifanya Bharti Airtel kuwa mbia mwenza katika Kampuni hiyo.  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images