Mwanamke mmoja mwenye umbo la miraba minne ambaye unaweza
kumuita Bonge baada ya jina lake kutopatikana mara moja, wikiendi
iliyopita alifikwa na msala mkubwa alipo bambwa na sungusungu akifanya
mapenzi kwenye kichaka na dereva wa teksi.
Chanzo chetu kilidai kuwa Bonge huyo alikuwa na wenzake wakitoka
kwenye kicheni party, walipofika maeneo ya Sinza-Afrika Sana jijini Dar,
Mwanamke Abambwa na Sungusungu Akifanya Mapenzi Kwenye Kichaka na Dereva teksi.
↧
↧
Treni Mpya Ya Kisasa Yaanza Safari za Mwanza kuelekea Dar
Treni mpya ya kisasa ya Deluxe jana imeanza safari zake kutoka Dar es Salaam kuelekea Mwanza.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Meneja Uhusiano wa Shirika la Reli
Tanzania (TRL), Midladjy Maez, alisema safari hii ni ya pili tangu
treni hiyo izinduliwe Aprili Mosi mwaka huu ambapo ilikwenda Kigoma.
“Safari za Delux zitakuwa kwa wiki mara moja, siku ya Jumapili itaondoka
↧
Serikali Yanawa Mikono Al-Shabab Mtanzania
Wakati mama mzazi wa Mtanzania Rashid Mberesero anayetuhumiwa kuwa kati
ya wafuasi wa Al-Shabaab walioua wanafunzi 148 wa Chuo Kikuu cha Garissa
nchini Kenya akitaka msaada wa Serikali ili akamwone mwanawe huyo,
Jeshi la Polisi limesema halina uwezo wa kumsaidia.
Jeshi hilo limesema halina uwezo wa kumsaidia mama huyo, Fatma Ally
kutokana na sheria mpya za ugaidi zilizopitishwa
↧
Pinda: Watanzania Waishio Ughaibuni Hawatapiga Kura
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema Watanzania waishio ughaibuni
hawataweza kupiga kura wakiwa nje ya nchi wakati wa Uchaguzi Mkuu
unaotarajia kufanyika Oktoba, mwaka huu.
Alisema pamoja na kwamba Watanzania hao wanatakiwa kupiga kura wakati wa
uchaguzi huo, jambo hilo halitawezekana kwa sababu kuna mambo kadhaa
ambayo Serikali inabidi iyatekeleze kabla ya uchaguzi huo.
Waziri
↧
Wanachama wa Chama Kipya Cha ACT- Tanzania Wapigwa Marufuku Kushabikia UKAWA'
Chama cha ACT-Wazalendo kimesema kila mwanachama anapaswa
kuwaunga mkono wagombea watakaopitishwa na chama hicho katika nafasi
mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu ujao, kwani kinyume chake ni kukisaliti
na adhabu yake ni kufukuzwa.
Mwenyekiti wa chama hicho, Anna Mghwira alisema
mwishoni mwa juma kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi
Mkuu, chama hicho kinahitaji
↧
↧
Gwajima Amtaka Rais Kikwete Awakemee Polisi Wanaomuandama......Achangiwa Mamilioni ya Hela na Waumini Wake
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amemwomba
Rais Jakaya Kikwete kuvikemea vyombo vya dola vinavyomfuatafuata
vikihoji mambo binafsi na kwamba akishindwa kufanya hivyo itakuwa wazi
kwamba yeye ndiye anawatuma.
Akihubiri mamia ya waumini wa kanisa hilo jana,
Gwajima alisema amekuwa akifuatwafuatwa na vyombo vya Serikali utadhani
yeye si raia wakati ni Mtanzania
↧
Shule Za Sekondari za Serikali Zafungwa Kwa Kukosa Chakula
Shule mbalimbali za sekondari za bweni zinazomilikiwa na Serikali zimefungwa kutokana na kukosa chakula.
Uchunguzi umebaini takribani kwenye mikoa yote kuna shule zimefungwa na nyingine ziko hatarini kufungwa kwa kukosa chakula.
Mkoani Dodoma Shule ya Sekondari Mpwapwa
iliyopo katika Wilaya ya Mpwapwa ilitakiwa kufunguliwa tangu Aprili 8,
lakini imeshindikana kutokana na ukosefu wa
↧
Zitto Kabwe Afunika Morogoro.....Mamia ya Wananchi Wahudhuria Mkutano wa Chama Chake Cha ACT-Wazalendo
Viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo wakicheza
wimbo wa chama hicho, kwenye eneo la Uwanja wa Ndege mjini Morogoro kabla
kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe hajaanza kuhutubia. (Picha na Said Powa)
Kiongozi wa chama hicho akiwahutubia wananchi.
Wakazi wa Mji wa Morogoro wakigombea kununua kadi za chama cha ACT -Wazalendo kwenye eneo la Uwanja wa ndege mjini Morogoro.
↧
Chama Kipya Cha Siasa Kiitwacho "Chama Cha Kijamaa na Uzalendo" Chasajiliwa Jijini Dar
CHAMA cha siasa ili kiweze kuendeshwa vizuri kwa misingi ya utawala bora
na baadae kifikie malengo yake ya kuchukua dola ni lazima kiwe na
katiba yenye misingi ya kidemokrasia.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam na Msajili Msaidizi wa Vyama
vya siasa, Sisty Nyahoza wakati wa kukabidhi cheti cha muda kwa Chama
cha Kijamaa na Uzalendo Tanzania (C.K.U.T).
Alisema demokrasia ya
↧
↧
Lipumba na Wafuasi Wake Wapata Dhamana Upya
Mwenyekiti wa chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, na wanachama
wenzake ambao mwanzo walifunguliwa kesi ya kushiriki maandamano haramu,
wamepewa dhamana upya katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Dhamana hiyo imetokana na kesi yao ya awali ambayo ilifutwa na kuanza kupitiwa upya.
Katika kupewa dhamana upya, watuhumiwa hao japokuwa walikuwa nje kwa
dhamana,
↧
Polisi Yawaonya Wamiliki wa Mabasi
Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani limewaonya wamiliki wa
mabasi ya abiria kuacha tabia ya kuwaamuru madereva wao kwenda mwendo wa
kasi na kwamba halitasita kuchukua hatua dhidi ya wamiliki hao.
Aidha,
jeshi hilo pia limesisitiza umuhimu wa madereva wote wa vyombo vya moto
nchini kwenda kusoma kwani hatua hiyo itawapa umahiri wa kazi yao na
hivyo kupunguza kiwango cha
↧
Mama Ajifungua Mtoto na Kisha Kumtupa Katika Shimo la Takataka ( Jalala) jijini Mwanza
Mama mmoja mkazi wa kata ya Mkuyuni-Sokoni wilayani Nyamagana jijini
Mwanza (jina lake halikufahamika mara moja) amejifungua mtoto wa kiume
na kisha kumtupa kwenye shimo la kutupa taka (jalala) eneo a Mkuyuni
jijini hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari, mmoja wa watoa taarifa kwa
viongozi wa serikali aliyetoa sharti la kutotajwa jina lake amesema:
“Mimi ni mfanya usafi
↧
Rais Kikwete: Sijapokea Majina ya Waliohukumiwa Kunyongwa
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amesema kuwa hajaletewa majina ya watu 16 waliohukumiwa kifo kutokana na
mauaji ya maalbino nchini kwa sababu safari ya kisheria ya majina hayo
kufikishwa kwake ni ndefu.
Rais Kikwete aliyasema hayo Jumapili, Aprili 12, 2015 wakati
alipozungumza katika ibada maalum ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa
Askofu
↧
↧
Miili 15 ya Waliokufa Katika Ajali ya Basi Morogoro Yazikwa Pamoja
Mamia
ya wakazi wa wilaya za Kilosa na Kilombero wamejitokeza katika
mazishi ya pamoja ya watu 15 kati ya 19 waliofariki katika ajali ya
basi ya Nganga ambalo liligongana na fuso kisha kuwaka moto katika eneo
la Iyovi na kuzikwa katika kaburi la pamoja kwenye makaburi ya Msamvu
Ruaha wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Akizungumza kwa niaba ya serikali,mkuu wa wilaya ya Kilosa
↧
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Tarehe 14 April 2015
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Tarehe 14 April 2015
↧
Lowassa atajwa tena.....Kada mkongwe atoa ya moyoni juu ya kifungo chake.
Wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikiendelea kutafakari jinsi kitakavyompata mgombea wake atakayepeperusha bendera ya urais katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu, Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho mkoa wa Arusha, Yona Merisho Nnko (74), ametoa ya moyoni akisema adhabu iliyotolewa na chama chao kwa makada sita kwa madai ya kuanza mapema kampeni za urais, inamlenga
↧
Serikali Yapata Kigugumizi Shule za Sekondari Kufungwa Kutokana na Kukosa Chakula
Kizungumkuti kimezidi kujitokeza katika suala la kufungwa kwa shule za sekondari za bweni za serikali kwa kile kinachoelezwa ni ukosefu wa chakula kutokana na wazabuni kugoma, baada ya serikali kutoa tamko ikieleza kuwa kuwa imelipa fedha za wazabuni hadi Machi, mwaka huu.
Katika tamko hilo, serikali inazikana taarifa zinazotolewa na baadhi ya wakuu wa shule hizo kuwa zinakabiliwa na
↧
↧
Madereva Wa Mabasi Kugoma Tena April 18 Iwapo Sharti la Mikataba Halitatimizwa......Msimamo huo Walimweleza Zitto Kabwe
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Bw. Zitto Kabwe, ameitaka Serikali kuhakikisha madereva wote wa magari ya mizigo na mabasi ya abiria, wanapewa mikataba ya ajira kabla ya Aprili 17, mwaka huu.
Bw. Kabwe aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Uwanja wa Ndege, mkoani Morogoro baada ya kushiriki mazishi ya watu zaidi ya 17 walioteketea kwa
↧
Nape awajibu wanaoishinikiza CCM itoe ratiba ya uchaguzi
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape
Nnauye, amesema chama hicho hakitaendeshwa kwa mashinikizo ya watu
wanaotaka kitangaze haraka ratiba ya uteuzi wa wagombea wake kwa ajili
ya uchaguzi mkuu ujao.
Kauli ya Nape imekuja baada ya baadhi ya makada wa
chama hicho kuhoji inakuwaje CCM kinachelewa kutoa ratiba ya mchakato
wa uchaguzi, wakati muda unasonga.
↧
JWTZ iliandaa mabasi 300 kuukabili mgomo wa madereva
Kutokana na mgomo wa madereva wa mabasi ya abiria nchi nzima uliofanyika Ijumaa iliyopita, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilikuwa limeshaandaa mabasi 300 ambayo yangetumika kusafirisha abiria, imebainika.
Chanzo cha habari kutoka serikalini kimebainisha kuwa JWTZ ilikuwa imeweka tayari mabasi hayo na kuwa walikuwa wakisubiri taratibu za kufanya kazi hiyo, ikiwa ni
↧