Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Breaking News: Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiasha Nchini Aaachiwa Kwa Dhamana

$
0
0
Habari  Zilizotufikia  zinadai kuwa Mwenyekiti wa Jumuia ya wafanyabiasha nchini Tanzania Bwana Jonson Minja ameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa Dodoma baada ya wafanyabiashara kuweka mgomo ambao ulikuwa haujafahamika ukomo wake.   Sakata  hili la wafanyabiashara kufanya mgomo wa kufunga maduka katika mikoa mbalimbali nchini,  jana lilichafua hali ya hewa bungeni

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Tarehe 2 March 2015

$
0
0
Habari  Zilizopo  Katika  Magazeti  ya  Leo  Alhamisi  ya  Tarehe  2  March  2015

Bei Za Vyakula ZAPAA Kuelekea Pasaka

$
0
0
Bei za mazao katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu  za Pasaka katika soko la Kariakoo zimeongezeka kutokana na imani iliyojengeka kwa wafanya biashara kuwa uwezo wa manunuzi unakuwa juu. Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam, Florens Seiya alisema jana katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari.   Seiya alisema kila inapofikia kipindi cha

Waziri Mkuu Asema NEC Ndiyo Itakayoamua Iwapo Kura ya Maoni Ifanyike April 30 au La.......Awataka Wafanyabiashara Wasitshe Mgomo, Atoa Neo kuhusu Mahakama ya Kadhi

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ametoa ufafanuzi kuhusu suala la uandikishaji katika daftari la kudumu la wapigakura na siku maalum ya kupiga kura. Amebainisha kuwa kutokana na hali ilivyo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ndio itakayotoa ratiba kamili kuhusu hatma ya upigaji kura ya maoni.   Aidha, katika mgogoro na mgomo wa wafanyabiashara unaoendelea, amewataka wafungue maduka yao kwa kuwa

Mbasha: "Gwajima Mungu Amenilipa, Njoo Uniombe Msamaha Tumalize Ugomvi"

$
0
0
Licha ya Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kukanusha mara zote kwamba, hahusiki na kusambaratika kwa ndoa ya Mwimba Injili Flora Mbasha na mumewe, Emmanuel Mbasha, lakini mume huyo ambaye amekuwa akimshutumu Gwajima ameibuka na jipya. Jipya aliloibuka nalo Mbasha ni kudai kuwa, msala uliompata Mchungaji Gwajima wa kumtolea maneno yenye kuudhi Askofu wa Kanisa

Mahakama Yaamuru Mtuhumiwa wa Escrow Akamatwe

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetoa hati ya kukamatwa kwa Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma anayekabiliwa na kesi ya kupokea Sh milioni 323.4, kwa kuwa hajafika mahakamani. Aidha imetoa hati kwa wadhamini wa Mujunangoma kufika mahakamani kujieleza kwa nini wasichukuliwe hatua kutokana na kitendo chao na mshitakiwa kutofika

Watoto 147 Wakutwa Misikitini Kilimanjaro Wakifundishwa Mazoezi Makali ya Kareti na Judo

$
0
0
Watoto 140 wenye umri kati ya miaka 10 na 21 wamekamatwa wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wakilelewa katika misikiti mitatu tofauti.   Taarifa zilizopatikana wilayani hapa zinasema watoto hao wamekuwa wakifundishwa mafunzo ya dini ya kiislam kinyume cha sheria.   Kwa mujibu wa taarifa hizo, watoto hao waligundulika baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Hai kupata taarifa na

SUMTRA Yasisitiza Nauli Lazima Zishuke

$
0
0
Siku chache baada ya Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta kutaka uangaliwe uwezekano wa kushusha nauli za vyombo vya usafiri nchini, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imesema inatekeleza agizo hilo na kwamba nauli za daladala na mabasi ya mikoani zitashuka wakati wowote kuanzia sasa. Imeongeza kuwa, licha ya bei ya mafuta kupanda kidogo jana, hakutaathiri kushuka

Gwajima AGOMA Kwenda Kuhojiwa na Mkuu wa Wilaya, Paul Makonda......Asema Tangu lini Mkuu wa Wilaya Akawa Mpelelezi?

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amemwandikia barua Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akimtaka afike mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kwa mahojiano.    Inaelezwa kuwa Makonda alimtumia Askofu Gwajima barua hiyo Machi 30 mwaka huu, akiwa amelazwa katika Hospitali ya TMJ.   Hata hivyo, kiongozi huyo wa kiroho amegoma akisema hawezikwenda

Chama Kipya Cha ACT-Tanzania Chawataka Watanzania Kupiga Kura ya HAPANA Katiba Inayopendekezwa

$
0
0
Chama cha ACT -Wazalendo, kimewataka Watanzania kuipigia kura ya hapana Katiba inayopendekezwa kwa sababu imeleta mgawanyiko katika taifa kutokana na kupatikana kwa njia zisizo za kiuadilifu na mchakato wake kuendeshwa kibabe. Kadhalika, kimesema katiba hiyo haijajibu matakwa na malalamiko ya wananchi kwenye masuala ya mbalimbali, ikiwamo muundo wa serikali, miiko na maadili ya viongozi

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Mstaafu, Jaji Mark Bomani Ataka Kura Ya Maoni ya Katiba Mpya Isogezwe Mbele, Tuendelee na Katiba ya 1977 Kuepusha Machafuko

$
0
0
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) mstaafu, Jaji Mark Bomani, ambaye pia ni mtaalam nguli wa Katiba, ameonya kuwa iwapo upigaji wa kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa utalazimishwa kufanyika Aprili 30, mwaka huu, wakati dalili zote zinaonyesha kuwa haiwezekani, unaweza kuzua mtafaruku mkubwa nchini. Ili kuepusha hali hiyo, ameshauri kura ya maoni iahirishwe hadi baadaye, badala yake

Baada ya Ukuta wa Nyumba Yake Kuanguka, Diamond Akabidhiwa Milioni 14 na Kampuni ya Bima ya UAP Kufidia Hasara Hiyo.

$
0
0
Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’, amekabidhiwa hundi ya zaidi ya milioni 14 kwa ajili ya kufidia ujenzi wa upande wa nyumba yake uliodondoka.   Wakati akikabidhiwa mfano wa hundi hiyo na Kampuni ya Bima ya UAP kwa ushirikiano na Benki ya CRDB, Diamond alisema ukuta wa nyumba yake ulianguka wakati akiwa anamuuguza mama yake aliyekuwa katika hali mbaya.   “Ilikuwa ghafla

Breaking News: Magaidi Wavamia Chuo Kikuu Cha Garrisa Kenya......Waliofariki mpaka sasa ni 15,Magaidi Hayo Bado Yako Ndani

$
0
0
Takriban watu 15 wameuawa baada ya watu watano wanaodaiwa kufinika nyuso zao kushambulia chuo kikuu cha Garrissa Kaskazini mashariki mwa Kenya.   Watu hao wanadaiwa kuingia katika taasisi hiyo mwendo wa saa kumi asubuhi wakati ambapo waislamu walikuwa wakifanya sala yao ya alfajiri.   Hatahivyo maafisa wa polisi wanasema kuwa shambulizi hilo lilifanyika mwendo wa saa kumi na moja

Mwanamke Afanyiwa Ukatili Wa Kutisha Na Mume Wake.....Achomwa Moto Kwa Petrol, Mtoto Wa Mwezi Mmoja Afariki Dunia

$
0
0
Machi 31 mwaka huu, mwanamke mmoja mkazi wa Bwai wilayani Butiama, Kudra Nanja alifanyiwa ukatili na mumewe wa kuchomewa ndani ya nyumba kwa petroli, tukio lililosababisha mtoto wake Tatu Simioni aliyekuwa na umri wa mwezi mmoja u nusu kufariki dunia.

Hali Bado Ni Tete Kenya....Mapigano Kati Ya Jeshi Na Al Shabaab Bado Yanaendelea Katika Chuo Kikuu Cha Garrissa ambapo Wanafunzi 15 Wameuawa

$
0
0
Takriban watu 15 wanaodaiwa kufunika nyuso zao wameshambulia chuo kikuu cha Garrissa Kaskazini mashariki mwa Kenya.   Watu hao wanadaiwa kuingia katika taasisi hiyo mwendo wa saa kumi asubuhi wakati ambapo waislamu walikuwa wakifanya sala yao ya alfajiri. Kufuatia shambulizi la chuo kikuu cha Garissa ,Shirika la msalaba mwekundu Red Cross limewataka raia wa Garissa kutoa msaada wa

Polisi Wanauawa Na Bunduki Zinaporwa Mara Kwa Mara....Bado Mnataka Tuamini Huu ni Ujambazi?

$
0
0
Wakati Rais Jakaya Kikwete akiingia madarakani mwaka 2005, ujambazi nchini ulikuwa umefikia kiwango cha kutisha, lakini leo hii tunaona umepungua.   Katika siku za karibuni, ambapo utawala wake wa miaka 10, unaelekea ukingoni, kumeibuka aina mpya kabisa ya uhalifu, nayo ni uvamizi wa vituo vya polisi, mauaji ya polisi na uporaji wa silaha, zikiwemo za kivita. Majuzi tu, mesikia polisi

Abiria Wakwama Jijini Mwanza Baada ya Mabasi Kutoka Dar es Salaam Kushindwa Kufika.....SUMATRA Wanataka Mabasi ya Dar-Mwanza Yatumie Spidi 80 tu

$
0
0
Siku moja baada ya Wakala wa Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kutangaza kupungua kwa mwendo kasi wa mabasi yaendayo mikoani hadi kufikia spidi 80, wasafiri jijini Mwanza wamekumbana na adha kubwa ya kukosa usafiri baada ya mabasi kutoka Dar es Salaam kushindwa kufika kwa wakati mjini hapa.    Katika stendi kuu ya mabasi eneo la Nyegezi jijini hapa, wasafiri hao

Breaking News:Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yaahirisha Kura ya Maoni Ya Katiba Mpya.....Zoezi La Uandikishaji Kuendelea Hadi Mwezi Wa 7

$
0
0
Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) imesema kuwa kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa, haitaweza kufanyika tena tarehe 30 April hadi hapo itakapotangazwa tarehe nyingine tena.   Akizungumza na waandishi wa habari  leo  mchana, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi , Jaji Mstaafu Damian Lubavu amesema sababu ya kuhairisha kura hiyo April 30 ni kutokana na kutokamilika kwa zoezi la

Hali ni Mbaya Kenya...Al Shabaab Wanadaiwa Kuanza Kuwachinja Mateka Inayowashikila Katika Jengo La Chuo Kikuu Cha Garissa

$
0
0
Baadhi ya wanafunzi waliouawa au kujeruhiwa darasani **********   Katika style kama ile ya shambulizi la Westgate Mall, wanamgambo wa al-Shabaab wamevamia na kushambulia  chuo  kikuu  cha  Garissa kilichopo katika mji wa Garissa. Zaidi  ya watu 15 wameuawa, na wengine zaidi ya 53 wamejeruhiwa. Mkuu wa jeshi la polisi Kenya, Inspector General Joseph Boinnet amesema kuwa magaidi hao

Waliouawa Na Al Shabab katika Shambulizi Chuo Cha Garissa Wafika 147.......Serikali Ya Kenya Yasema Imewaua Magaidi Wote Waliovamia

$
0
0
Habari  Mpya  toka  kenya  zinaarifu  kuwa,Watu 500 wameokolewa huku 147 wakiuawa wakiwemo wapiganaji  wote  wa kundi la Al shabaab  waliokuwa  wamevamia. Kwa  mujibu  wa  kituo  cha  Televisheni  cha K24  cha  nchini  Kenya, majeshi  ya  KDF  Yakisaidiana  na  Polisi  yamefanikwa  kuwaua  magaidi  wote  na  kuchukua  udhitibi  wa  chuo  hicho. Mapigano  Hayo  Yamechukua  Masaa  14
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images