Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari zilizopo katika magazeti ya leo Jumatano ya Tarehe 25 March 2015

$
0
0
Habari  zilizopo  katika  magazeti  ya  leo  Jumatano  ya  Tarehe  25  March  2015

NEC: Ni vigumu kura ya maoni kufanyika Aprili

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec),  imeelezea wasiwasi wake kuwa kura ya maoni kwa Katiba inayopendekezwa huenda isifanyike mwezi ujao kutokana na kusuasua kwa uandikishwaji wapiga kura katika daftari la kudumu lawapigakura mkoani Njombe. Akizungumza na waandishi wa habari, jana mjini Njombe, Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva, alisema  kuwa upigaji wa kura hiyo huenda usifanyike

Dawa za kulevya: Wabunge wataka wahusika wanyongwe.

$
0
0
Serikali imewasilisha Bungeni Muswada wa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya ambao unawabana wauza ‘unga’ ukipendekeza kuwa watakaobainika kufanya biashara hiyo haramu watozwe faini ya Sh. bilioni moja au kifungo kisichopungua miaka 30, huku wabunge wakitaka watakaobainika wapigwe risasi hadharani au wanyongwe. Aidha, atakayekutwa analima, kusambaza mbegu, kusafirisha,

Ngonyani: Siombi Radhi,Nipo Tayari Kwa Lolote.....Nilienda Kwa LOWASSA Kwa Ridhaa Yangu na Sitaki Mtu Anichagulie Marafiki

$
0
0
MBUNGE wa Korogwe Vijijini, Bw. Stephen Ngonyani (CCM) ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Umoja wa Wazazi Taifa,   amesema wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu, hapaswi kutafutiwa marafiki wala ndugu walioonesha dhamira ya kuwania uongozi ndani ya chama na kuwaunga mkono. Alisema kitendo chake cha kwenda nyumbani kwa mwanachama wa CCM anayedaiwa kutaka kuwania nafasi ya urais kwenye

Mgogoro Ndani ya Chama Kipya Cha ACT-Tanzania Wanukia Tena.....Mwenyekiti Aliyetimuliwa Amtupia Lawama Zitto Kabwe

$
0
0
SAKATA la uongozi ndani ya Chama cha Mabadiliko na Uwazi (ACT-Tanzania), limeendelea kuchukua sura mpya baada ya uongozi uliodaiwa kuvuliwa madaraka, kudai Bw. Zitto Kabwe ndiye aliyesababisha mgogoro katika chama chao. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Kadawi Limbu alisema chanzo cha mgogoro unaoendelea katika chama hicho ni Bw.

Wezi wa Ng'ombe Wachomwa Moto

$
0
0
Watu watano wamekufa katika matukio matatu tofauti, wakiwemo watatu waliouawa na miili yao kuchomwa moto na wananchi wanaojiita wenye hasira, baada ya kutuhumiwa kuiba ng’ombe 40 katika Wilaya ya Bunda Mkoani Mara.   Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Philipo Kalangi, tukio la kwanza lilitokea Machi 24 mwaka huu, majira ya saa 3:00 asubuhi katika kijiji cha Kunanga wilayani Bunda

Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya Wapitishwa........Ukikutwa na Dawa za kulevya faini bil.1/-, kifungo miaka 30

$
0
0
BUNGE limepitisha rasmi Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya wa mwaka 2014, huku adhabu ya kifo kwa watakaokutwa na dawa hizo, ikishindikana kuingizwa kwenye muswada huo, isipokuwa mapapa na vigogo wa biashara hiyo, wameongezewa adhabu ya faini ya Sh bilioni moja na kifungo cha maisha.   Hata hivyo, baadhi ya wabunge bado wameendelea kung’ang’ania kuwa sheria hiyo ijumuishe

Marufuku kuvuta sigara hadharani

$
0
0
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid amesisitiaza tamko la kupiga marufuku uvutaji wa sigara katika maeneo ya umma ili kuilinda jamii kutokana na madhara yatokanayo na moshi wa sigara.   Tamko la Waziri limekuja ikiwa ni siku mbili tu baada ya maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu Duniani, moja ya magonjwa yanayosababishwa na uvutaji wa tumbaku.   Agizo hilo

Mbunge adai trafiki hupangiwa ‘hesabu’ na wakubwa wao

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Conchesta Rwamlaza, amedai kuna  minong’ono kuwa askari wa usalama barabarani  hupangiwa kiwango cha kukusanya na kuwakilishwa kwa viongozi wao na hivyo kuwafanya kujali zaidi fedha kuliko kusimamia sheria za barabarani.   Akiuliza swali bungeni jana, Rwamlaza alihoji serikali inasemaje kuhusiana madai hayo.   Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo

Mambo matatu yanayoipa CCM nguvu dhidi ya UKAWA

$
0
0
Wakati Taifa likielekea katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu, ushindani wa wazi wa kisiasa kati ya chama tawala (CCM) na vyama vya upinzani kupitia Ukawa unaonekana bayana.   Kambi hizo mbili, zinatunishiana misuli huku kila moja ikijigamba kuibuka na ushindi na hatimaye kushika dola.   Licha ya kauli za majigambo kutoka kambi hizo, bado hakujawa na uhakika

Mbona Makada Wengine Wa CCM Wakifanya Haya Mambo LOWASSA Halalamiki?........Kwa nini Lawama Ziwe Kwa Lowassa Pekee?

$
0
0
January Makamba amechapisha vitabu vyake na kugawa kwa wajumbe wote wa mkutano mkuu, mbona Lowassa hakulalamika?   January Makamba alinunua Simu za Gallaxy Sumsang zaidi ya 140 akazigawa kwa wajumbe wa baraza UVCCM ZANZIBAR. January 2013 alipokusanya marais wa vyuo vikuu Tanzania nzima Mt. Uluguru Hotel na kuwalipa laki moja na nusu kila moja ili watoe tamko kuwa anafaa kuwa rais, mbona

Askari Magereza na FFU wakamatwa na noti bandia na sare za JWTZ

$
0
0
Jeshi la polisi mkoani Simiyu linawashikilia askari wawili wa jeshi la magereza na polisi kwa kukutwa na noti bandia ikiwa ni pamoja na sare za jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ). Akitoa taarifa za kukamatwa kwa askari hao, Kamanda wa polisi mkoani hapa Naibu Kamishina, Charles Mkumbo alisema kuwa askari hao walikamatwa juzi majira ya saa 9 mchana katika mtaa wa Old Maswa kata ya

Habari Zlizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Tarehe 26 March 2015

$
0
0
Habari  Zlizopo  Katika  Magazeti  ya  Leo  Alhamisi  ya  Tarehe  26  March  2015

Lowassa Amjibu Nape Nnauye.....Ahoji ni Kikao gani Cha Chama Kilichomtuma Kutoa Tamko??....Apokea Maandamano ya Vijana 60 Toka Mbeya Wakimtaka Agombee Urais

$
0
0
SIKU  moja baada Katibu wa itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye kutoa kauli ya chama hicho kuhusu makundi yanayojitokeza kumshawishi waziri mkuu mstaafu Mhe Edward Lowassa kugombea urais, kuwa yanaweza kumkosesha sifa kiongozi huyo ya kuwania nafasi hiyo, Mh. Lowassa amejibu kauli hiyo na kudai anashangazwa nayo huku akihoji imetokana na maamuzi ya kikao gani ndani

Baba mbaroni kwa kuwabaka watoto wake

$
0
0
Rahma Mashamu ambaye ni mama mzazi wa watoto wawili mmoja wa miaka 11 na mwingine 15 wanaodaiwa kubakwa na baba wa watoto hao akilia kwa uchungu wakati akihojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo, wilayani Kibaha mkoani Pwani. ------- Mkazi mmoja wa Miembe Saba wilayani Kibaha mkoani Pwani amekamatwa na polisi akituhumiwa kuwabaka watoto wake wawili wadogo kwa zaidi ya miaka

Vijana wengi hawana nguvu za kiume

$
0
0
TAASISI ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR),imesema vijana wenye umri wa kuanzia miaka 30 na kuendelea, wanaongoza kwa kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume.   Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,Mkurugenzi wa NIMR,Dk.Mwele Malecela alisema kwa sasa tatizo hilo ni kubwa ambalo linawakumba vijana wengi hususan barani Afrika.   Alisema hali

Bunge mjini Dodoma lapitisha leo muswada ya Sheria ya Takwimu 2014 na muswada wa Usimamizi wa Kodi 2014

$
0
0
Hatimaye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha miswada miwili iliyowekwa kiporo kutoka katika mikutano iliyopita ya Bunge kwa sababu tofauti. Miswada hiyo ni Muswada wa Sheria ya Takwimu na Muswada wa Usamizi wa kodi ya mwaka 2014, ambayo haikuweza kupita kutokana na kukosa akidi na pamoja na kuhitaji kufanyiwa marekebisho. Mswada wa sheria ya Takwimu haukuweza

Rais Kikwete Ateua Wabunge Wawili Wapya

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wabunge wawili (2) wapya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Walioteuliwa ni Dkt. Grace Khwaya Puja na Bwana Innocent Sebba. Rais amefanya uteuzi huu kwa mamlaka aliyopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 66 (I) (e) ambapo amepewa mamlaka ya kuteua wabunge wasiozidi 10.

Mume amuua mkewe kwa Panga Shinyanga

$
0
0
Mwanamke mmoja amefariki dunia mkoani Shinyanga, aitwaye Vumilia Kulwa (21) baada ya kuuawa na mumewe akiwa nyumbani kwa wakwe zake. Kamanda wa polisi wa mkoa wa Shinyanga, Justus Kamungisha, amesema mwanamke huyo mkazi wa kijiji cha Mwongozo kata ya Mwenge tarafa ya Nindo wilayani Shinyanga, ameuawa na mumewe, Singingi Luyengeja (30) baada ya kumkata panga kichwani na kufa papo

Mwalimu Kizimbani kwa kubaka Mwanafunzi Geita

$
0
0
Jeshi la polisi wilayani Chato mkoa wa Geita, limemfikisha kizimbani mwalimu wa shule ya sekondari Makurugusi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha pili. Mwalimu huyo, Iddy Gerald (21), anatuhumiwa kufanya ubakaji huo Machi 23 mwaka huu saa 7:45 usiku ndani ya chumba chake kilichopo katika kijiji cha Makurugusi.   Mbele ya mahakama ya wilaya ya Chato, mwendesha mashitaka
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images