MKAZI wa Dodoma, Ramadhan Zuber ambaye alikuwa abiria kwenye basi la Champion amefariki dunia akiwa safarini.
Akizungumza na Mpekuzi mjini Kibaha, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei alisema kuwa Zuber (29) alikuwa akisafiri toka Dar es Salaam kwenda Dodoma.
Kamanda Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 16, saa 3:30 asubuhi katika kijiji cha chamakweza wilaya ya
Abiria wa Basi la Champion Afariki Dunia Akiwa Safarini
↧
↧
Majambazi Yavamia Duka la M-Pesa na Kupora Milioni 45
MAJAMBAZI watano wakiwa na silaha za moto na mapanga wamevamia duka la fedha la Mji mdogo wa Sirari na kupora Sh milioni 45 za Kitanzania na fedha za Kenya elfu 50.
Katika hekaheka hizo majambazi hao wamejeruhi watu wawili akiwemo mwalimu wa shule ya msingi Sirari anayeitwa Mataigwa Muhono (30) aliyepigwa risasi mguuni na mdogo wa mwenye duka ambaye alikuwa akitoa huduma Mara Masabi (23)
↧
Jokate Amzawadia KANDAMBILI Wema Sepetu
Mbunifu wa mavazi na mtangazaji Bongo, Jokate
Mwegelo amesababisha shosti yake, Wema Sepetu ‘Madam’ afurahi baada ya
kumpelekea zawadi ya kandambili zake za Kidoti pamoja na vipodozi
mbalimbali.
Jokate alisema Wema ni miongoni mwa watu ambao
anawakubali kutokana na mchango mkubwa katika tasnia ya filamu Bongo,
hivyo ameamua kumpelekea zawadi ya bidhaa zake za Kidoti kuonesha
heshima
↧
Ukawa: Muhongo, Werema, Tibaijuka wafikishwe kortini
Wakati maazimio nane yaliyotolewa na Bunge kwenye mkutano wa 16 na 17 mwishoni mwa mwaka jana kuhusiana na kashfa ya uchotwaji fedha zaidi ya Sh. Bilioni 300 za akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yakiwa hayajatekelezwa yote, Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, amesema watu waliofikishwa mahakamani katika sakata hilo ni dagaa tu na kwamba kambare
↧
Wanafunzi 48 wasichana wa shule ya sekondari ya Muungano wanusurika Kufa baada ya bweni lao Kuteketea kwa moto
Wanafunzi 48 wasichana wa kidato cha kwanza wa shule ya sekondari ya
vipaji maalum ya Muungano wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro
wamenusurika kifo baada ya bweni lao kuteketea kwa moto na vifaa vyao
vyote.
Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo ya wananchi Mh Zawadiel Maruchu
amesema, moto huo ulianza kwenye bweni hilo kuanzia saa moja usiku
wakati wanafunzi wakijiandaa kupata chakula
↧
↧
CCM Yakerwa na Viongozi wasiopenda Kujiuzulu
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amewaagiza viongozi wa chama hicho kujenga tabia ya uadilifu katika kutekeleza majukumu yao ya kazi.
Aliyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wa CCM katika ziara yake ya kichama mkoa wa Magharibi.
Alisema sifa kubwa ya kiongozi bora ni yule ambaye anawajibika ipasavyo, ikiwamo unapotokea ubadhilifu wakati wa
↧
Sakata la Escrow: Chenge, Tibaijuka, Ngeleja kikaangoni leo
KAMATI Ndogo ya Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), chini ya
Mwenyekiti wake Philip Mangula, leo inawahoji makada wa chama hicho
waliopokea mgawo wa fedha za Escrow.
Makada ambao watawekwa kikaangoni kutokana na kupokea mgawo huo, ni
aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna
Tibaijuka, Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, Wiliam
↧
Wastara: Bongo Movie Imeingiliwa na Mapepo, wasanii tupige magoti tusali
Msanii anayefanya vizuri kunako kiwanda cha filamu
Bongo, Wastara Juma amefunguka kwamba tasnia ya filamu kwa sasa
inaonekana kama imeingiliwa na pepo mbaya kutokana na mambo kwenda
ndivyo sivyo kila kukicha.
Akizungumza na Gpl, Wastara alisema tasnia ya filamu imekuwa
ni ya migogoro, chuki huku bei ikishuka jambo ambalo siyo sahihi kwani
litawarudisha nyuma wasanii wakati hata
↧
Mvua Kubwa Kulitikisa jiji la Dar es Salaam....Mikoa mingine yatajwa, Tahadhari yatolewa
MAMLAKA ya hali ya hewa nchini (TMA), imewataka wananchi kuchukua tahadhari kutokana na mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha katika maeneo ya Ukanda wa Pwani.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mamlaka hiyo, ilisema mvua hiyo itanyesha kwa zaidi ya milimita 50 ndani ya saa 24 kuanzia Januari 18 hadi 20 mwaka huu.
Maeneo ambayo yataathirika na mvua hizo ni Mikoa ya Ruvuma, Mtwara
↧
↧
Irene Uwoya anataka Watanzania wamwambie ni Kitu Gani Wanakipenda Kwenye MWILI Wake
Mwigizaji Irene Uwoya, hivi juzi aliwauliza swali followers
wake kwenye mtandao wa INSTAGRAM, kuwa kitu gani wanapenda kwenye mwili
wake, mara baada ya kuweka picha yake hiyo hapo juu.
Swali hilo liliibua maoni mengi huku kila mtu akisema lake
na wengine wakisema hili swali ni tata kidogo na wengine wakisema huu ni
uchokozi....
Nimeona sio mbaya nikishare na wewe swali
↧
Tunataka Rais Ajaye Awe na Hofu ya Mungu
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, amewataka Watanzania
kuhakikisha rais watakayemchagua katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu,
lazima awe na hofu ya Mungu.
Dk. Bilal, alitoa kauli hiyo mjini Dodoma jana, wakati akizungumza
katika hafla ya kusimikwa kwa Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la
Dodoma, Beatus Kinyaiya.
Alisema kiongozi huyo, mbali na kuwa na hofu ya Mungu,
↧
Jeshi la polisi ladhibiti wananchi waliotaka kuiba mafuta baada ya lori kuanguka, Morogoro.
Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limefanikiwa kudhibiti wanachi
waliobeba madumu wakitaka kuiba mafuta baada ya lori la mafuta kuanguna
katika eneo la Mikese mkoani Morogoro.
Dereva wa lori Deogras John hilo akizungumzia tukio hilo la ajali
amesema chanzo cha ajali alikua akijaribu kumkwepa mtoto aliyekua akivuka
barabara ndipo gari ikapoteza mweleko na kupinduka mara kadhaa ambapo
↧
Majambazi yateka mabasi 6 jijini Arusha....Abiria Wavuliwa nguo na kuporwa, Wanawake wanyang'anywa hadi shanga na vitu vingine vya ndani
WATU zaidi ya 40 wanaodhaniwa kuwa majambazi, wameteka mabasi sita ya
abiria yanayofanya safari kati ya Jiji la Arusha na Nairobi, Kenya na kupora mali na fedha ambavyo thamani yake haijafahamika.
Tukio hilo ambalo limethibitishwa na Jeshi la polisi, mkoani Arusha llitokea usiku wa kuamkia jana katika eneo la Mbuga Nyeupe, wilayani Longido Mkoa wa Arusha baada ya watu hao kuweka mawe
↧
↧
Rushwa ya Ngono isiwe kigezo cha Uongozi-Bavicha
WANAWAKE wa (CHADEMA), Arusha,wametakiwa kujitokeza kwa wingi, kugombea
nafasi mbalimbali za uongozi bila woga katika uchaguzi mkuu ujao na
kuonywa kujiingiza katika kashfa za kutembea na viongozi wao ili wapate
nafasi hizo.
Akizungumza jana na Baraza la Wanawake Chadema Mkoani Arusha
(BAWACHA), Makamu Mwenyekiti Taifa wa Baraza hilo, Hawa Mwaifunga,
amesema kumekuwa na tabia kwa
↧
JWTZ yafanikiwa kupunguza dhoruba Mtwara
Wanajeshi zaidi ya 300 wa Jeshi la wananchi wa Tanzania, wamefanikiwa
kudhibiti sehemu ya ardhi iliyobaki isiendelee kumezwa na maji ya bahari
kwa kutumia mawe na vifusi vya mchanga katika eneo la Msimbati lililopo
Mtwara vijijini.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika eneo la tukio kanali wa jeshi Saidi
Nkambi anayesimamia oparesheni hiyo amesema zoezi hilo linakwenda vizuri
↧
Wapiganaji wa Taifa la Kiislam (ISIS) Wadai Fidia ya Dola Milioni 200 Kuwaachia Mateka wa Japan
Video
ikiwaonyesha mateka wa Kijapan, Kenji Goto Jogo na Haruma Yukawa, walio
katika nguo za rangi ya chungwa, wakiwa na Jihadi John anayedai fidia
ya Dola milioni 200 ili kuwaachia mateka hao.
Waziri Mkuu wa Japana, Shinzo Abe, ambaye anategemewa kuokoa maisha ya mateka wa Kijapan.
Kenji
Goto Jogo (kushoto) mwandishi wa habari wa Japan na Haruna Yukawa
mwanajeshi kutoka kampuni
↧
Aunty Ezekiel Achukizwa na Uamuzi wa Mzee Majuto
Wakati mkongwe wa filamu za kuchekesha, King Majuto
akidai kutoshiriki kazi na msanii yeyote kutokana na kuibiwa, msanii
mwenzake, Aunty Ezekiel amechukizwa na uamuzi huo.
Akizungumza na Uwazi, Aunty alisema kuwa haamini kama wezi wa kazi
zake ndiyo chanzo cha Majuto kuachana na filamu za kushirikishwa bali
inawezekana kuna tatizo lake lingine.
“Suala la wezi lipo miaka mingi na
↧
↧
Waziri Awaomba Radhi Wanafunzi Waliopigwa Mabomu ya Machozi Kenya
Waziri wa Usalama nchini Kenya Joseph Nkaissery amewaomba radhi
wanafunzi wa shule ya msingi waliofyatuliwa gesi ya kutoa machozi wakati
walipokuwa wakiandamana kupinga kunyanga'anywa kipande cha ardhi ambacho
kilikuwa uwanja wao wa kuchezea.
Bwana Nkaissery amempa siku moja mnyakuzi
wa ardhi hiyo kuondoa sehemu ya ukuta iliyobaki baada ya wanafunzi
kuuangusha na kisha kuondoka
↧
Walioteka Mabasi 6 jijini Arusha na Kuwadhalilisha Abiria Wakamatwa na Jeshi la Polisi
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha limewatia mbaroni watu kadhaa kwa
kuhusishwa na tukio la ujambazi wa kuteka mabasi sita ya abiria
yaliyokuwa yanatoka nchini Kenya kuelekea jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa, Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema katika msako huo ulioanza jana
wamefanikiwa kukamata watu hao katika maeneo tofauti
↧
Wanachama, Viongozi wa chama kipya cha ACT Watwangana Ngumi ndani ya Ofisi ya Msajili
Vurugu zimetokea jana kwenye ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
nchini baada ya makundi yanayopingana ndani ya Chama cha ACT-Tanzania
kukutana ana kwa ana katika ofisi hiyo kwa ajili ya kikao cha
usuluhishi.
Baada ya kukutana kwa makundi hayo, ghafla walitokea vijana wanaodaiwa kukodiwa na Mwenyekiti aliyesimamishwa, Kidawi Limbu na kumvamia Katibu Mkuu wa muda wa chama hicho, Samson
↧
More Pages to Explore .....