Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Meli Yazama na kuua Watu 14.....Basi Lapinduka na kuua watu Wanne

$
0
0
Watu 18 wamepoteza maisha katika ajali mbili tofauti, ambapo katika ajali ya majini meli iliyobeba shehena ya mahindi imezama na kuua watu 14, wakati katika ajali ya barabarani, basi kutoka Handeni mkoani Tanga kwenda Dar es Salaam limeua watu wanne. Katika ajali ya majini, Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda  alisema abiria 14 kutoka nchi jirani ya Burundi wanahofiwa kufa

Bandari kufuru tupu.....Wafanyakazi walipana Posho ya Laki 5 kwa siku tangu 2011

$
0
0
Wakati Msajili wa Hazina amebariki posho mpya za safari za ndani kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) kuwa Sh 500,000 kwa siku kuanzia Januari 2, mwaka huu, imebainika kuwa walishaanza kulipana hivyo tangu mwaka 2011. Hayo yalibainika wakati wa Kamati ya Bunge Hesabu za Serikari (PAC), ilipokutana na Menejimenti ya TPA jijini Dar es Salaam.   Kutokana na kamati hiyo

Hali ni Tete kwa Vigogo Escrow.......Wengine waliopata Mgawo kupelekwa Mahakamani leo, Ngeleja, Lissu watunishiana misuli

$
0
0
HALI inazidi kuwa tete kwa vigogo kadhaa wa Serikali juu ya sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, baada ya kuwapo taarifa kuwa wengi watafikishwa mahakamani.   Iwapo leo vigogo ambao majina yao yamekuwa yakitajwa tangu juzi watafikishwa mahakamani, wataongeza idadi baada ya juzi watumishi wawili wa Serikali kufikishwa katika Mahakama ya Kisutu

Wanafunzi 84 UDOM wafikishwa mahakamani Dodoma

$
0
0
Wanafunzi 84 wa programu maalum ya stashahada ya ualimu katika Chuo Kikuu cha Dodoma(udom) waliofanya mgomo na kuandamana kushinikiza kulipwa madai yao, juzi wamepandishwa kizimbani kwa kosa la kukusanyika bila kibali maalum. Wanafunzi hao ni wa programu maalumu katika masomo ya Sayansi, Hisabati na Teknohama iliyoanza mwaka jana walifanya mgomo huo jana na kuandamana kuelekea

Mwili wa dereva wakutwa umenyongwa ndani ya gari

$
0
0
Mwili wa aliyekuwa dereva wa gari la mizigo Bw Ally Athumani Ally ambaye alikuwa akitafutwa na jeshi la Polisi kufuatia wizi wa milango umekutwa ndani ya gari alilokuwa anaendesha baada ya siku 4 ukiwa umenyongwa na kamba za kubebea mizigo mikubwa huku gari hilo likiwa limeegeshwa kituoni hapo.   Kamanda wa polisi mkoa wa Ilala SACP Mary Nzuki amekili kutokea kwa tukio hilo ambapo

Rais Kikwete akutana na Kamati ya BRN

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Ijumaa, Januari 16, 2015, amekutana na kufanya mazungumzo na wajumbe wa Kamati Maalum Inayojitegemea Iliyofanya Tathmini ya Utekelezaji wa Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).   Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Rais Kikwete amewashukuru wajumbe wa Kamati Maalum Inayojitegemea

Mahakama Yatangaza Mgomo wa TAZARA ni Batili......Wafanyakazi waamuriwa kurudi kazini

$
0
0
MAHAKAMA Kuu, Divisheni ya Kazi imewataka wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kurudi kazini, huku ikiagiza mamlaka hiyo kutowakata fedha wafanyakazi hao katika kipindi chote cha mgomo.   Licha ya Mahakama hiyo kutoa huku ya kuwataka kurudi kazini, wafanyakazi hao wamesema hawatarudi kazini mpaka watakapolipwa mishahara yao yote pamoja na kuonana na Waziri wa

Bomu Lajeruhi watu watano huko Tanga

$
0
0
WAKAZI watano wa kitongoji cha Mafuriko Amboni kilichopo jijini Tanga wamejeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili baada ya kurushiwa bomu la kutupwa kwa mkono na mtu asiyejulikana wakati walipokuwa wakitazama mpira kwenye banda la wazi.   Majeruhi hao ni Hassani Abdallah (72) ambaye amevunjika mguu wa kulia na kupata madhara makubwa kifuani na sasa amelazwa katika hospitali ya mkoa ya

Watuhumiwa 3 wa mauaji wachomwa Moto na wanakijiji

$
0
0
WAKAZI wa kijiji cha Burunde kata ya Karitu wilayani Nzega mkoani Tabora, wamewapiga, kuwaua na kuwachoma moto watu watatu kwa tuhuma za kushiriki kumuua Helena Abel na kumjeruhi mume wake, Said Msoma.   Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Juma Bwile alisema tukio hilo limetokea Januari 15 mwaka huu.   Alisema kuwa Januari 12 mwaka huu Helena Abel

Vijana Watatu wa Ubungo Kibangu wadai kuteswa na wanajeshi wa kambi ya Makoka

$
0
0
WANAJESHI wapatao wanane wanadaiwa kuwatesa na kuwapiga vijana watatu katika eneo la Ubungo Kibangu, Dar es Salaam pasipokuwa na sababu maalumu.   Wakizungumza na mwandishi wetu jana, vijana hao walieleza kuwa walikamatwa na wanajeshi hao na kupelekwa porini kisha wakateswa na kupigwa kwa zaidi ya saa tano bila kufahamu kosa lao na hata walipohoji waliambiwa hawaruhusiwi kuhoji wanajeshi.

"Sina mpango wa kufanya kazi nyingine mbali na Kuigiza"....Lulu Michael

$
0
0
Binti  Mrembo  Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema katika maisha yake ya sanaa hataweza kufanya kazi nyingine mbali na kuigiza kama ambavyo wasanii wengine wanafanya.   Akiongea  na mwandishi wetu, Lulu alisema, amegundua kuwa kila kitu kinatakiwa kifanywe kama kazi na yeye atakuwa akifanya kazi yake ya kuigiza tu na si vinginevyo.   “Napenda kuwa msanii na

Chama cha TLP hatarini kufutwa.....Mrema Apewa Siku 4 za kujieleza

$
0
0
OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, imetoa siku nane kwa Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) Augustino Mrema kutoa maelezo kuhusu tuhuma za kuendesha chama hicho kinyume na katiba.   Hayo yalibainishwa juzi katika taarifa iliyotolewa Dar es Salaam na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza ambayo ilimtaka kuwasilisha maelezo yake kabla ya Januari 23, mwaka huu ili

Mume na mke watiwa mbaroni kwa mauaji ya mganga wa jadi

$
0
0
JESHI la Polisi mkoani Kagera linawashikilia watu tisa kwa tuhuma za mauaji katika matukio mawili tofauti wakiwemo mume na mke waliomuua mganga wa jadi.   Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani hapa Henry Mwaibambe, alisema tukio la kwanza lilitokea saa 3:00 usiku wa Januari 14 mwaka huu katika kata ya Bugarama wilayani Ngara ambapo mganga wa jadi, Alfaxad John (

Wapinzani wasema Watahakikisha wanafunzi waliofukuzwa UDOM wanarejeshwa

$
0
0
KAMBI rasmi ya upinzani bungeni imesema itawasaidia kwenye masuala ya kisheria wanafunzi waliofukuzwa kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kutokana na kuandamana kudai kupewa fedha za kujikimu.   Akizungumza juzi katika ofisi za Bunge, Waziri Kivuli wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Susan Lyimo alisema kuwa tatizo hilo linatokana na serikali kutokuwa na mipango ya kuhakikisha maslahi

Saluni ya Ngono Yafumuliwa jijini Dar......Wahudumu wake ni makahaba, mteja hulipa Elfu 60 kwa tendo moja

$
0
0
Wakati suala la ajira likiwa bado ni kitendawili kikubwa kwa serikali, Jiji la Dar hivi sasa linatisha, baada ya watu kubuni mtindo mpya wa kujipatia fedha kwa kujihusisha na biashara haramu ya ngono katika maeneo yanayotambulika kufanya shughuli nyingine halali. Uchunguzi unaonyesha kuwa zipo saluni nyingi jijini Dar zinazojishughulisha na biashara ya massage (kuchua) lakini ndani

Sakata la Escrow: Vigogo wa BoT, TRA, Tanesco wapandishwa kizimbani

$
0
0
MKURUGENZI wa Fedha wa Benki Kuu, Julius Angello, Meneja wa Misamaha ya Kodi wa TRA, Kyabukoba Mutabingwa na Mwanasheria Mwandamizi wa Tanesco, Steven Urassa wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kupokea rushwa ya zaidi ya Sh bilioni mbili kutoka katika Akaunti ya Tegeta Escrow.   Washtakiwa hao walipandishwa jana kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya mahakimu wawili

Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Pili 2014....Ufaulu waongezeka kwa 3%, BOFYA HAPA KUYAONA

$
0
0
Baraza la Mitihani la Taifa nchini Tanzania NECTA leo limetoa matokeo ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha pili mwaka 2014 kwa wanafunzi waliofanya mtihani huo unaowapa fursa ya kuendelea na kidato cha tatu.   Akisoma taarifa hiyo leo kwa waandishi wa habari katika ofisi za NECTA jijini DSM, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles Msonde amesema kiwango cha ufaulu kwa mwaka 2014

Mapigano ya wakulima na Wafugaji: Mmoja Auawa, 14 Wajeruhiwa Vibaya

$
0
0
Mgogoro kati ya Wakulima na Wafugaji katika bonde la Mgongola , wilayani Mvomero mkoani Morogoro umeibuka tena na kusababisha kifo cha mkulima mmoja na wengine 14 kujeruhiwa.   Waliojeruhiwa wamekatwa sehemu mbalimbli za miili yao na mapanga na sime za wafugaji.   Kati ya wakulima waliojeruhiwa kwenye tukio hilo lilitokea jioni ya Januari 16, mwaka huu ni pamoja na aliyekuwa Kamanda wa

Waislam na Wakristo Wafanya Kongamano la Amani......Wakubaliana Kutokashiana

$
0
0
VIONGOZI wa dini za Kiislamu na Kikristo nchini wamekubaliana kutoandaa mihadhara inayokashifu dini moja na nyingine, miongoni mwa madhehebu ya dini moja au kashfa baina ya waumini na waumini.   Lengo la makubaliano hayo ni kudhibiti madhara ya mihadhara hiyo ambayo imeonekana inachangia uchochezi wa ugaidi na uvunjifu wa amani.   Katibu Mkuu wa Taasisi ya Mashehe na Wanazuoni wa

Makamanda wa mikoa mitatu ya Mwanza, Simiyu na Shinyanga wavunja Ngome hatari ya mtandao wa Ujambazi.

$
0
0
POLISI wa mikoa ya Mwanza, Simiyu na Shinyanga wamefanikiwa kusambatarisha mtandao wa ujambazi kwenye mikoa hiyo baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa wa ujambazi sugu, Njile Samweli (46) mkazi wa kijiji cha Lyoma, Bariadi mkoani Simiyu aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu.   Sambamba na kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo wa ujambazi, pia watuhumiwa watano wanashikiliwa, bunduki moja yenye namba PB
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>