Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Maazimio ya Kamati kuu CCM kwenye Kikao Z’bar haya hapa, Escrow, ishu ya Urais 2015 vimejadiliwa

$
0
0
Tarehe 13/01/2015 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake wa Taifa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ilifanya kikao chake cha kawaida cha siku moja Kisiwandui Mjini Zanzibar. Pamoja na mambo mengine baadhi ya mambo yaliyojadiliwa na Kamati Kuu ni pamoja na:-   1. SAKATA  LA  AKAUNTI  YA ESCROW Chama Cha Mapinduzi kimesikitishwa sana na sakata hili.

Wanafunzi 84 UDOM Watiwa Mbaroni

$
0
0
 Wanafunzi 84 wa Chuo Kikuu UDOM wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa amani chuoni hapo. Wanafunzi hao walikamatwa wakifanya maandamano kutoka chuoni hapo kuelekea katika ofisi mbalimbali za viongozi wa Serikali zilizopo Dodoma mjini majira ya saa kumi na moja alfajiri.   Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, David Misime alisema wahusika wa vurugu hizo ni wanafunzi

Sakata la Escrow: Vigogo Wawili Wapandishwa Kizimbani, Tibaijuka, Regemalila nao kupanda kortini.....Wengine 10 waandaliwa mashitaka yao

$
0
0
SAKATA la uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, limeanza kuchukua sura mpya baada ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), kuwafikisha mahakamani vigogo wawili wa Serikali.   Vigogo hao, waliofikishwa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam jana, ni Mhandisi Mkuu wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA), Theophillo Bwakea na Mkurugenzi wa Huduma za

Msafara wa Waziri Muhongo wazomewa Kahama......Wananchi Wapaza Sauti wakidai...."Mwiziiiii....Mwiziiii"

$
0
0
WAZIRI wa nishati na madini Mhe. Sospeter Muhongo amejikuta katika wakati mgumu na msafara wake baada ya kuzomewa na wananchi wa soko la wakulima katikati ya mji wa Kahama wakati akitokea kwenye ziara yake vijijini wilayani Kahama mkoani Shinyanga. Tukio hilo limetokea hivi karibuni wakati waziri huyo na msafara wake wakitokea kata ya Bulungwa kwenye jimbo la Kahama kuelekea kata

Kesi ya Chid Benz Yapigwa Kalenda hadi January 21 Mawaka huu

$
0
0
KESI inayomkabili mwanamuziki wa Hip hop nchini, Rashid Makwiro ’Chid Benz’, imeahirishwa tena leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam mpaka Januari 21, mwaka huu.   Mwanamuziki huyo anakabiliwa na kesi ya kukamatwa na madawa ya kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar wakati akisafiri kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya kutumbuiza

"Kuwazuia Waganga wa JADI sio suluhu ya Mauaji ya Albino" -Kowo

$
0
0
Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi (TAS) mkoani Dodoma, Ludovick Kowo amesema kitendo cha serikali kupiga marufuku waganga wa kienyeji wanaopiga ramli ili kuepusha mauaji ya albino nchini ni fedheha kwa jamii hiyo. Kowo alitoa kauli hiyo leo mjini hapa wakati akizungumza na Mwandishi wetu kuhusiana na kauli ya serikali ya kuwapiga marufuku wapiga ramli nchini ili

Bilion 1.7 zatafunwa Dar es salaam

$
0
0
Kamati ya bunge ya hesabu za serikali za mitaa (LAAC) imebaini ufisadi wa zaidi ya shilingi Bilioni 1.7 katika jiji la Dar es Salaam na kuiagiza TAMISEMI kufuatilia kashfa hiyo. LAAC imebaini ufisadi wa zaidi ya shilingi bilioni moja nukta saba katika jiji la Dar es Salaam na kuiagiza wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) kufuatilia kashfa hiyo na kuwachukulia

Mfanyabiashara auawa kwa risasi Bunda

$
0
0
Mfanyabiashara wa kuuza samaki, Mkome Marwa (39) wa mtaa wa Nyasura wilayani Bunda, ameuawa na watu wasiojulikana baada ya kupigwa risasi njiani akiwa na mke wake, huku mwingine akijeruhiwa katika matukio mawili tofauti wilaya humo. Kamanda wa polisi mkoa wa Mara, Phillipo Kalangi, amesema tukio la kwanza limetokea Januari 12 mwaka huu, saa 3 usiku, eneo la Nyasura wakati Marwa

Rais Kikwete ahudhuria sherehe za kuapishwa Rais wa Msumbiji

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili Maputo, mji mkuu wa Mozambique, usiku wa Jumatano, Januari 14, 2015, kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya wa nchi hiyo, Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi.    Sherehe zinafanyika Independence Square, mjini Maputo leo, Alhamisi, Januari 15, 2015. Mheshimiwa Nyusi anakuwa Rais wa nne wa Mozambique tokea uhuru wa nchi hiyo mwaka 1975.  

Miili ya waliofukiwa kifusi mgodini yaopolewa

$
0
0
Hatimaye wachimbaji wote watatu waliokufa kwa kufukiwa na kifusi cha jabali katika mgodi wa dhahabu wa Onesmo Goldmine Mawemeru uliopo katika kijiji cha Nyalugusu Wilayani Geita imeopolewa jana usiku baada ya juhudi za siku nne. Hatua hiyo imedaiwa ni matokeo ya ushirikiano na mshikamano mkubwa uliooneshwa katika kutekeleza zoezi hilo kati ya Uongozi wa Mgodi huo, wadau na

"Panya Road" 119 waachiwa kwa kukosekana ushahidi 959 wafikishwa mahakamani

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu  Dar es Salaam limewaachia huru vijana 119 wanaodaiwa  kujihusisha na vitendo vya kihalifu  maarufu kama ‘panya road’  baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.   Kamanda wa kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova amesema vijana hao walianza kukamatwa Januari 3 mwaka huu na hadi sasa wamekamatwa watuhumiwa 1,508.   Kamanda Kova amesema  watuhumiwa 119

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akerwa na tabia ya wananchi wa mkoa huo kujigeuza "Omba Omba"

$
0
0
MKUU wa mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa ametaka wananchi wa mkoa wa Dodoma kuachana na tabia yenye aibu ya kuomba chakula wakati wana fursa za kuzalisha chakula cha kutosha, kujikimu mwaka mzima na ziada kuifanyia biashara.   Alitoa kauli hiyo mwanzoni mwa wiki wilayani Kondoa wakati alipokuwa akizindua msimu wa kilimo mwaka 2015 kwa mkoa wa Dodoma.   Aliwataka wananchi kutambua msimu wa

Walinzi wavunja ofisi waiba fedha, bunduki

$
0
0
POLISI mkoa wa Shinyanga inawasaka walinzi wawili wa Kampuni ya Prosper Security Guard wakituhumiwa kuvunja ofisi ya Jambo Oil Mill and Ginnery Limited kisha kuiba fedha Sh milioni 1.07 na kutoweka na bunduki mbili aina ya Shot gun na risasi saba.   Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha alisema tukio hilo ni la Januari 9, mwaka huu saa 1 asubuhi katika eneo la mtaa wa

Wafanyakazi TAZARA Wasota Mahakamani kusubiri Hukumu

$
0
0
Sakata la mgomo wa wafanyakazi 1,500 wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia  (TAZARA), ulioingia katika siku ya sita, limechukua sura mpya baada ya wafanyakazi hao waliofunguliwa kesi katika Mahakama ya Kazi, kusota kwa siku nzima wakisubiri hukumu yao. Kesi hiyo ilianza kusikilizwa na Jaji Iman Aboud wa mahakama hiyo saa 3:30 asubuhi hadi 6 mchana jana na kisha kuaihirishwa hadi saa 8

Kinana awataka wazanzibari kuikubali Katiba

$
0
0
Watanzania wametakiwa kuisoma na kuielewa vyema Katiba Inayopendekezwa na Bunge Maalumu la Katiba na muda ukifika kuipigia kura ya ndiyo kwani imebeba mambo mengi yenye manufaa kwa wananchi wa pande zote mbili za muungano. Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Abdulrahman Kinana ametoa rai hiyo kwenye wilaya ya mjini, wakati wa siku ya kwanza ya ziara yake ya siku kumi kwenye

Mwanamke auawa kwa kukatwa mapanga

$
0
0
MKAZI wa mtaa wa Kitwana kata ya Busoka wilayani Kahama mkoani Shinyanga Regina  Shija (55) ameuawa kwa kukatwakatwa mapanga kichwani  na watu wasiojulikana kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa Kimapenzi. Afisa mtendaji wa Mtaa huo, Bw. Rafael Jumanne amesema kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 5.00 usiku ambao watu wasiofahamika walivamia nyumbani kwa  Regina akiwa  anajiandaa

"Kuweni makini na wanaotangaza urais mapema"- Askofu

$
0
0
ASKOFU wa Kanisa la Tanzania Field Evangilism (TFE) la Mjini Shinyanga, Edsoni Mombeki amewatahadharisha wananchi kuwa makini na viongozi wanaotangaza nia mapema ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa kuhofia kupata viongozi wasio na sifa ambao baadaye wanaweza kuiyumbisha nchi.   Ametoa tahadhari hiyo kanisani kwake, wakati akifunga maombi ya siku tatu ya kuliombea

Kanisa Lachomwa Moto Mkoani Kigoma.......Mali zote zateketea

$
0
0
Watu wasiojulikana wamelichoma moto na kuliteketeza Kanisa la Evangelical Assemblies of God wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma na kuteketekeza kila kitu kilichokuwemo ndani ya kanisa hilo. Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Venance Mwamoto amesema kuwa tukio hilo la mwanzoni mwa wiki hii, limeacha athari kubwa za mali na kwamba hakuna mtu yeyote ambaye amepata madhara kuhusiana na uharibifu.  

Vinara wa Maandamano UDOM Watimuliwa......Waziri mkuu ( Mwakibinga ) Kafukuzwa Moja kwa moja

$
0
0
Wanafunzi watatu ambao wanatuhumiwa kuwa vinara wa maandamano ya wanafunzi wa programu maalumu ya walimu wa sayansi Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wameachishwa masomo. Wakati mmoja wao akiwa amefukuzwa moja kwa moja, wawili wengine wana nafasi ya kujieleza kuhusika kwao na maandamano hayo, yaliyochafua hali ya hewa na kusababisha wanafunzi 84 kutiwa mbaroni.   Makamu Mkuu wa chuo hicho,

Bei za Petroli na Dizeli Kushuka zaidi March Mwaka huu

$
0
0
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imebainisha kuwa hadi kufikia Machi mwaka huu, bei ya mafuta nchini itaendelea kushuka kulingana na kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia. Hata hivyo, mamlaka hiyo imeonya kuwa bei hiyo ya mafuta nchini haitaweza kupungua kwa kiasi kikubwa, kutokana na kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya dola ya Marekani pamoja na kutokubadilika
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images