Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Wimbo wa Rose Muhando - Wanyamazishe Bwana

$
0
0
Wimbo wa Rose Muhando - Wanyamazishe Bwana

Mikakati Ya Serikali Kufufua Zao La Korosho Kurejesha Furaha Ya Wakulima

$
0
0
Na Ismail Ngayonga-MAELEZO
SEKTA ya Kilimo nchini imeendelea   kuwa   ni   Sekta   muhimu   katika maendeleo ya uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla hususan katika wakati huu tunapojizatiti kufikia uchumi wa viwanda.

Katika mwaka 2017, sekta hiyo ilitoa ajira kwa Watanzania kwa asilimia 65.5, ikichangia asilimia 28.7 ya Pato la Taifa ambapo sekta ndogo ya mazao ilichangia asilimia 16.58.

Takwimu zinaonesha kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2018, ukuaji wa Sekta ya Kilimo ulifikia asilimia 7.1, ukuaji huo ulichangiwa na hali nzuri ya hewa na jitihada za Serikali za kuhakikisha kuwa pembejeo zinawafikia wakulima kwa wakati.

Kutokana na matumizi yasiyoridhisha ya pembejeo muhimu na kutozingatiwa kwa kanuni bora za kilimo, Serikali imeweka mazingira wezeshi kwa kuwezesha pembejeo muhimu zikiwemo mbegu bora, mbolea na viuatilifu kuwafikia wakulima kwa wakati.

Takwimu zinaonesha kwamba matumizi ya zana bora za kilimo yanaongezeka miongoni mwa wakulima ambapo kwa mwaka 2018 wastani wa kitaifa wa matumizi ya zana bora za kilimo umeongezeka hadi kufikia asilimia 20 kwa matrekta na asilimia 27 kwa wanyama kazi ikilinganishwa na asilimia 14 ya matrekta na asilimia 24 ya wanyama kazi mwaka 2013.

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imeendelea kuimarisha mifumo ya masoko na kuratibu mazao makuu ya kimkakati ikiwemo korosho, tumbaku, kahawa, chai na pamba hatua iliyosaidia  kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao hayo kutoka tani 901,641 mwaka 2016/2017 hadi tani 967,184 mwaka 2017/2018.

Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2019/2020, Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga anasema katika msimu wa 2018/2019, Wizara ya Kilimo ililenga kuongeza uzalishaji wa mazao ya biashara hadi kufikia tani 1,356,368 ambapo hadi kufikia mwezi Machi 2019, takribani tani 667,631 ikiwa ni sawa na asilimia 49.2 ya lengo zimezalishwa.

Kuhusu zao la korosho, Waziri Hasunga anasema katika kuendeleza zao hilo Serikali imesambaza miche bora 12,252,197 katika mikoa 17 inayolima zao hilo kati ya miche 13,661,433 iliyozalishwa kupitia mikataba iliyoingiwa msimu wa 2017/2018 baina ya Bodi ya Korosho na wazalishaji 678.

Hasunga anasema katika mwaka 2018/2019, mbegu za korosho kilo 47,484 ambazo zitazalisha miche 6,647,760 ya kutosheleza ekari 391,045 zimezalishwa na Kituo cha Utafiti cha Naliendele na kusambazwa katika mikoa 20 na uzalishaji wa miche unaendelea.

“Mwaka 2018/2019, Wizara imesimamia ununuzi wa pembejeo za zao la korosho kwa utaratibu wa pamoja kupitia zabuni na Vyama vya Ushirika ili kuhakikisha kuwa wakulima wanapata pembejeo kwa wakati na kwa bei nafuu” anasema Waziri Hasunga.

Anaongeza kuwa kupitia utaratibu huo, jumla ya tani 31,500 na lita 520,000 za salfa zimenunuliwa ambapo wakulima wamenunua jumla ya tani 1,994.175 na lita 14,283 na bakaa ya viuatilifu vilivyonunuliwa kwa njia ya zabuni ni tani 29,505.825 na lita 505,717 za salfa ambavyo vinaendelea kuuzwa kwa wakulima kwa ajili ya msimu wa 2019/2020.

Akifafanuza zaidi Waziri Hasunga anasema Wizara kupitia Bodi ya Korosho inaendelea na usajili wa wakulima wa korosho ambapo hadi kufika Machi 2019, wakulima 200,000 wamesajiliwa, ambapo bodi hiyo pia  imeandaa mfumo endelevu ambao utawawezesha maafisa katika kila Halmashauri kukusanya na kuhuisha taarifa kwa kutumia simu za mkononi.

Katika upande wa mafunzo, Hasunga anasema Serikali imeendesha mafunzo ya udhibiti ubora wa korosho ghafi kwa wataalamu 63 katika Halmashauri za Mkuranga, Kibiti, Masasi, Ruangwa, Nachingwea na Tunduru na kuhusisha wataalamu kutoka Bodi ya Usimamizi ya Stakabadhi za Ghala, waendesha ghala na wanunuzi.

Hadi kufikia tarehe 30 Aprili 2019, jumla ya tani 222,825 zimekusanywa kutoka kwa wakulima, kati ya hizo tani 211,184 zimehakikiwa na tani 177,357 zenye thamani ya Tsh Bilioni 578.5 zimelipwa kwa wakulima 379,283, na hizo kuuzwa korosho kwa bei elekezi  ya Tsh 3,300 kwa kilo ya korosho ghafi daraja la kwanza na Tsh. 2,640 kwa kilo ya korosho ghafi daraja la pili bila makato.

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa, Dalili zake Hizi Hapa..Makala
51 minutes ago

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kulundia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.

Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.

Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.

Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Ugojwa huu wa ngiri unaweza kutibika

Mpate mpenzi wako unayempenda na kumfunga mume,mke mpenzi asitoke kwa mwingine .

Kwa Ushauri na Msaada wa Wasaliana na 
0747100745

Rais Magufuli ateua Mwenyekiti mpya Bodi ya Taifa ya Takwimu

Naibu Waziri Kijaji: Serikali imedhamiria kutatua kero za wafanyabiashara nchini

$
0
0
Na Veronica Kazimoto
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amesema Serikali imedhamiria kutatua kero za wafanyabiashara ambapo kwa mwaka huu wa fedha imefanya mabadiliko ya sheria mbalimbali za kodi kwa lengo la kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini.

Akizungumza wakati wa mkutano wa kusikiliza changamoto za wafanyabiashara na wawekezaji uliofanyika Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, Dkt. Kijaji amesema kuwa moja ya sheria ya kodi iliyofanyiwa marekebisho ni Sheria ya Kodi ya Mapato."Miongoni mwa sheria zilizofanyiwa mabadiliko mwaka huu wa fedha wa 2019/20 ni pamoja na sheria ya kodi ya mapato ambapo tumepunguza viwango vya kodi kwa wafanyabiashara wadogo," alisema Dkt. Kijaji.

Naibu Waziri huyo ameeleza kuwa hapo awali wafanyabiashara wenye mauzo ghafi ya kuanzia shilingi 4,000,000 hadi 7,000,000 kwa mwaka walikuwa wanalipa shilingi 150,000 lakini baada ya mabadiliko ya sheria hiyo, kiwango hicho kimepungua hadi kufikia shilingi 100,000 kwa mwaka.

Kwa upande wa wafanyabiashara wenye mauzo ghafi kuanzia shilingi 7,000,000 hadi 11,000,000 walikuwa wanalipa shilingi 318,000 baada ya mabadiliko ya sheria ya kodi ya mapato kiwango hicho kimepunguzwa hadi kufikia 250,000 kwa mwaka

Dkt. Kijaji ameongeza kuwa, kwa wafanyabiashara wenye mauzo ghafi kuanzia shilingi 11,000,000 hadi 14,000,000 walikuwa wanalipa shilingi 546,000 ambapo baada ya mabadiliko ya sheria kiwango hicho kimepungua hadi shilingi 450,000 kwa mwaka.

Vilevile, Naibu Waziri Kijaji amefafanua kuwa, kero nyingine iliyotatuliwa kupitia sheria hiyo ni ile ya wafanyabiashara kuanza kulipa kodi hata kabla ya kuanza kufanya biashara zao ambapo kwa sasa watatakiwa kulipa kodi ndani ya miezi 6 baada ya kuanza biashara.

"Nikisema serikali imedhamiria kutatua kero za wafanyabiashara mjue imedhamiria kweli. Hapo awali, wafanyabiashara wengi walililamikia kitendo cha kuanza kulipa kodi wakiwa ndio wanaanza biashara, lakini mwaka huu wa fedha yamefanyika mabadiliko na sasa wafanyabiashara wapya wataanza kulipa kodi ndani ya miezi 6 wakiwa tayari wamekwishaanza biashara zao," alisisitiza Dkt. Kijaji.

Mkutano huu wa mashauriano kati ya serikali, wawekezaji na wafanyabiashara ni moja ya utekelezaji wa maagizo ya Rais John Pombe Magufuli aliyoyatoa mwezi Juni, 2019 alipokutana na wafanyabiashara Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo aliiagiza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na wizara zote zinazohusika na wafanyabiashara na wawekezaji nchini kwa lengo la kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.

Mwisho.

Rais Magufuli Ampa Pole Mkuu Wa Majeshi Ya Ulinzi Ya Wananchi Wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo Ambaye Amefiwa Na Mtoto Wake Nelson Mabeyo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Ndugu Nelson Mabeyo mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo nyumbani kwao Msasani jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Mke wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo, Mama Mabeyo ambaye amefiwa na mtoto wake Nelson Mabeyo aliyepata ajali ya ndege Seronera Serengeti mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo msibani Msasani jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo nyumbani kwake Msasani mara baada ya kufiwa na mtoto wake Nelson Mabeyo aliyepata ajali ya ndege Seronera Serengeti mkoani Mara.PICHA NA IKULU

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa, Dalili zake Hizi Hapa..Makala
51 minutes ago

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kulundia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.

Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.

Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.

Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Ugojwa huu wa ngiri unaweza kutibika

Mpate mpenzi wako unayempenda na kumfunga mume,mke mpenzi asitoke kwa mwingine .

Kwa Ushauri na Msaada wa Wasaliana na 
0747100745

Rais Magufuli Ampa Pole Mkuu Wa Majeshi Ya Ulinzi Ya Wananchi Wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo Ambaye Amefiwa Na Mtoto Wake Nelson Mabeyo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Ndugu Nelson Mabeyo mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo nyumbani kwao Msasani jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Mke wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo, Mama Mabeyo ambaye amefiwa na mtoto wake Nelson Mabeyo aliyepata ajali ya ndege Seronera Serengeti mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo msibani Msasani jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo nyumbani kwake Msasani mara baada ya kufiwa na mtoto wake Nelson Mabeyo aliyepata ajali ya ndege Seronera Serengeti mkoani Mara.PICHA NA IKULU

Waziri Mkuu: Tutaendelea Kulinda Viwanda Vya Ndani

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli itaendelea kudhibiti uingizwaji wa bidhaa mbalimbali kutoka nje ili kulinda viwanda vya ndani.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Septemba 25, 2019) alipotembelea kiwanda cha maziwa cha Asas, akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Iringa. Amesema Serikali imedhamiria kukuza uchumi na kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 kupitia sekta ya viwanda.

Waziri Mkuu amesema Serikali inaamini kuwa uchumi wa viwanda ukiimarika uchumi utakuwa kwa kasi kubwa na matokeo yake yataonekana wazi kwa kupanua wigo wa ajira, soko la huduma na shughuli nyingine za kiuchumi.

“Serikali imefanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya mifugo ili kuhakikisha inaleta tija kwa wafugaji na taifa kwa ujumla, hivyo wafugaji endeleeni kuimarisha ushirika wenu. Wizara ya Mifugo iendelee kuwaelimisha wafugaji ili wafuge kitaalamu.”

Waziri Mkuu ameipongeza kampuni ya Asas kwa sababu ni miongoni mwa kampuni chache ambayo imeanza kutoa elimu kwa wafugaji juu ya namna bora ya ufugaji ikiwa ni pamoja na kufuata kanuni bora za ufugaji wa kisasa pamoja na kuwapa uhakika wa soko.

Amesema Serikali inathamini sana uwekezaji uliofanywa na kampuni ya Asas kwa sababu wameitikia wito wa Serikali wa ujenzi wa uchumi kupitia sekta ya viwanda, hivyo itahakikisha wawekezaji wote wananufaika na uwekezaji wao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Maziwa cha Asas, Fuad Abri amesema kiwanda chao kinampango wa kupanua uzalishaji kwa kujenga kiwanda kingine cha kusindika maziwa katika wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya na kipo katika hatua za mwisho kukamilika.

Awali,Waziri Mkuu alizindua kiwanda cha maji cha Mkwawa cha mjini Iringa na kusema kuwa ujenzi huo ni njia ya uhakika ya kupunguza tatizo la ajira na kwamba itaendelea kushawishi wawekezaji wa ndani na nje ili wananchi wengi wapate ajira.

“Serikali imetoa wito kwa wawekezaji wawekeze katika viwanda mbalimbali nchini, hivyo ni muhimu wawekezaji hao wakalindwa na wasibugudhiwe ili waweze kuendelea na uzalishaji wa bidhaa zao. Watumishi mlioajiriwa fanyeni kazi kwa uaminifu.”

Naye,Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Bodi ya kiwanda cha Maji cha Mkwawa,Ahmed Huwel alisema kiwanda chao kilianzishwa mwaka 2017 kwa lengo la kuzalisha na kufanya biashara ya maji safi na salama pamoja na kuunga mkono mkakati wa Serikali wa ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Alisema kiwanda chao kimeajiri watumishi158 kati yao wanaotoka nje ya nchi ni watatu tu na kwa upande wa ajira zisizo rasmi ni zaidi ya 3,000 na kwamba wanatarajia kuongeza ajira kwa wananchi wengi zaidi baada ya kukamilisha ujenzi wa kiwanda kingine cha kutengeneza vinywaji baridi.

Akizungumzia kuhusu changamoto zinazokikabili kiwanda hicho alisema ni pamoja na ukatikaji wa umeme wa mara kwa mara hali inayosababisha kuharibika kwa baadhi ya mitambo hivyo ameiomba Serikali iwasaidie.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Wagonjwa Waliopelekwa Na Polisi Muhimbili Watafuta Nduguzao

Zaidiya Wafanyabiashara, Wawekezaji 390 Wasikilizwa Kero Zao Ruvuma

$
0
0
NA.MWANDISHI WETU
Zaidi ya wafanyabiashara na wawekezaji 390 mkoani Ruvuma wamekutana katika mkutano wa mashauriano baina ya Serikali na Sekta binafsi ili kusikilizwa na kupata ufumbuzi wa changamoto wanazokabiliana nazo katika mazingira ya biashara.

Kongamano hilo lililofanyika Septemba 24, 2019 lililoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) kwa kushirikiana na ofisi ya mkoa wa Ruvuma na  kufanyika  katika Ukumbi wa mikutano wa Bomba mbili Mkoani Ruvuma 
 
 Kongamano hilo lilihudhuriwa na Mawaziri kutoka Wizara saba ikiwemo Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano na Mazingira), Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Wizara ya Fedha,  Wizara ya Kilimo, Wizara ya Nishati na Wizara ya Viwanda

Akizungumza wakati wa kufunga kongamano hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masualaya Uwekezaji nchini Mhe.Angellah Kairuki alieleza nia thabiti ya Serikali katika kuwafikia wawekeza wote nchini kwa kuzingatia maelekezo ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli aliyoyatoa tarehe 7Juni, 2019 alipokutana na wafanyabiashara Ikulu Jijini Dar es Salaam.

“mikutano ya Mashauriano kati ya Serikali na sekta Binafsi imejikita kusikiliza na kutatua kero za wawekezaji na wafanyabiashara katika kada mbalimbali ili kutengeneza mazingira ya kuwekeza zaidi ili kukuza uchumi wetu kwa ustawi wa biashara zenu kwa kutambua na kuthamini michango yenu ndani ya jamii na nchi kwa ujumla,”alieleza Waziri Kairuki.

Alieleza kuwa, mikutano hiyo ya mashauriano itaendelea kwa nchi nzima ili kuhakikisha mazingira bora  ya wafanyabiasha na wawekezaji nchini kwa lengo la kufikia adhima ya uchumi wa kati na kuendeea kuwa na nchi yenye maendeleo.

“Mikutano hii inaenda sambamba na utekelezaji wa Kauli Mbiu aliyoitoa Mheshimiwa Rais kuwa Mwaka 2019 ni Mwaka wa Uwekezaji, hivyo nasi Waheshimiwa Mawaziri tumeamua kutekeleza hilo kwa Kauli mbiu ya kwamba “Mwaka 2019 ni Mwaka wa Uwekezaji: Tunasikiliza na Tunatatua”.alisisitiza Waziri Kairuki.

Naye Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji aliwahakikishia wawekezaji kuhusu maboresho yanayoendelea kufanywa na serekali kwa kuwa na punguzo za tozo, ada na kodi mbalimbali walizoainisha kuwa ni kero kubwa kwa wafanyabiashara hao.

“Mhe. Rais alipoingia madarakani alianza kuboresha viwango vya kodi kwa kuhakikisha anaondoa na kufanya marekebisho kwa kodi ikiwemo zile za madini, na hii ni dhamira njema”alieleza Dkt.Kijaji

Aidha alifafanua kuwa, wameendelea kutekeleza kwa vitendo sheria ya fedha  ya mwaka 2019 ambayo imebainisha orodha ya tozo na ada zilizopunguzwa na zilizofutwa na  kuahidi kuendelea kusimamia utekelezaji wa ukusanywaji wa tozo zote nchini na kushughulikia kero za kodi, ada na tozo zinazotozwa bila kufuata sheria na taratibu zilizopo.

“Katika Bunge la Bajeti ya mwaka 2018/2019 zaidi ya kodi, tozo na ada mbalimbali zipatazo 109 zilifutwa na nyingine zipatazo 54 zilifutwa ili kuboresha mazingira ya wafanyabiashara na wawekezaji,”alisisitiza Dkt. Kijaji

Alimalizia kwa kutoa rai kwa wananchi kuendelea kufuatilia kila taarifa muhimu zinazohusu maboresho ya sheria na kanuni mbalimbali zinazohusu ulipaji wa kodi ili kuendana na mabadiliko mbalimbali yanayojitokeza.

=MWISHO=

Kiboko Ya Maumbile Madogo Na Nguvu Za Kiume

$
0
0
*NGETWA MIX*/
√Hii ndio dawa bora ya mitishamba kiboko ya maumbile Madogo(KIBAMIA) Hurefusha na kunenepesha maumbile  mafupi pia  yaliyoingia ndani kutokana na kitambi ama kuathirika na punyeto

*📌SUPER MORINGA MIX*/
Ni dawabora ya nguvu za kiume yenye mchanganyiko wa miti shamba 10 yenye maajabu yafuatayo:/
🔖(1)Inatibu upungufu wa nguvu za kiume mara dufu na kuimarisha misuri   ilio legea na kusinyaa wakati wa tendo la ndoa/
🔖(2)Kuongeza hamu ya tendo kukufanya uweze kurudia tendo hadi mara tatu bila kuchoka
🔖(3)Itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15-30 kwa tendo la Kwanza na utakuwa na uwezo wa Kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3-4 bila hamu kuisha na inatibu kabisa/
.
*MATATIZO HAYA HUSABABISHWA NA*/
🔖(1)Tumbo kujaa gesi, na kuunguruma chini ya kitovu/
🔖(2) Choo kuwa kama Cha mbuzi/
🔖(3)Ngiri/
🔖(4)Kama umejichua sana punyeto/
🔖(5)Kisukari/
🔖(6)Presha ya kupanda na kushuka/
🔖(7)Vidonda vya tumbo,/
.
Na haya yote husababisha/
📍Kuishiwa kwa nguvu za kiume 📌/
. _______________________
Bado hujachelewa dawa hizi ni mpya kabisa  ni tofaut na ulizo wahi kutumia pia zimeonesha mafanikio kwa watu wengi sana/

Pia tuna tibu  KISUKARI,PRESHA,VIDONDA VYA TUMBO N.K/
._______________________
DR .SELEMANI OMARY ANAPATIKANA  DAR ES SALAAM , PIA UNAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO  NDANI NA NJE YA NCHI .SIMU NO:/
*📞+255788468114*

Waziri Mkuu: Kilimo, Mifugo Na Uvuvi Kuchangia Uchumi

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. Magufuli itaendelea kuhakikisha kuwa kilimo, ufugaji na uvuvi unakuwa wa kisasa na wenye tija kwa wananchi sambamba na kutoa mchango unaostahili katika kufikia uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda ifikapo mwaka 2025.

“Katika kuhakikisha azma hiyo ya Serikali inafikiwa, nitoerai kwa wafugaji nchini kuunda ushirika imara utakao wawezesha kupata huduma mbalimbali za mifugo na ushirika huo pia ulenge katika kuboresha uzalishaji na ukusanyaji wa maziwa, upatikanaji wa masoko pamoja na kuongeza kiasi cha usindikaji viwandani.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Septemba 25, 2019)kwenye Maadhimisho ya Siku ya Unywaji Maziwa Shuleni yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwembetogwa mijini Iringa. “Unywaji maziwa shuleni si tu ni muhimu lakini pia inatoa msukumo wa kuboresha afya zetu hususan za watoto shuleni kupitia unywaji wa maziwa.”

Amesema wataalamu wa lishe wanashauri kula chakula bora kinachokuwa na viini lishe vyote muhimu kama wanga, protini, vitamini, madini, mafuta na maji ya kutosha. Hata hivyo, ili kupata chakula bora, wananchi wanapaswa kuchanganya vyakula vya aina nyingi katika mlo mmoja.

Waziri Mkuu amesema kutokana na umuhimu huo, ndiyo maana watalaamu wa lishe wanashauri kuwa mtoto apate glasi moja ya maziwa katikati ya siku itakayompatia lishe ya kutosha hadi atakapomaliza masomo yake kwa siku hiyo. “Kwa bahati mbaya hapa nchini, watoto wengi huondoka asubuhi kwenda shuleni bila kupata chakula chochote. Aidha, shuleni nako mara nyingi hawapati chakula na hivyo hukosa usikivu mzuri katika masomo yao.”

Zaidi ya nchi 70 duniani ikiwemo Tanzania zinaadhimisha siku ya unywaji maziwa na tayari zilishaanzisha mpango wa unywaji maziwa shuleni kwa watoto wao, lengo ni kuhakikisha mtoto anapata lishe kamili na anakuwa na usikivu mzuri katika masomo yake. Mtoto amelengwa kwa sababu ni kundi ambalo ni muhimu katika kujenga Taifa lililo bora na anatarajiwa kurithisha vema vizazi vijavyo.

“Nimearifiwa kuwa hapa nchini programu ya unywaji maziwa shuleni ilianza kutekelezwa katika  mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Iringa, Dar es Salaam na Njombe ambapo shule 40 na wanafunzi 34,561wamenufaika katika kunywa maziwa lita 631,860 ambayo yamekuwa yakitolewa kwa ushirikiano na Serikali, wazazi, wafadhili mbalimbali na wasindikaji wa maziwa. Lengo kuwafikia wanafunzi wote.”

Waziri Mkuu amesema Serikali ina nia ya dhati ya kufanya mpango huu uwe wa kitaifa. Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikishirikiana na wadau wengine itaendelea kuhamasisha unywaji wa maziwa katika shule zetu hapa nchini.  Juhudi hizi zitakwenda sambamba na kuongeza uzalishaji wa maziwa kutoka lita  bilioni 2.7 zinazozalishwa sasa kwa mwaka mpaka lita bilioni saba kwa mwaka ifikapo 2020.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapongeza wafugaji wa Iringa kwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa mafanikio yanayoonekana katika kuendeleza tasnia ya maziwa kupitia ushirika. “Nitoe wito kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha zinawezesha na zinasimamia uundwaji wa vyama vya ushirika imara na pia kuimarisha vyama vya ushirika vilivyopo.”

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Josephat Kandege, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Maafisa wa Serikali, wadau wa mazima pamoja na wananchi.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Tazama Hapa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo Alivyobadilisha Maisha Ya Huyu Mama

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo ametimiza ahadi yake kwa Mama wa Mapacha kwa kumjengea nyumba yakuishi baada ya ile ya awali iliyokuwa haina mazingira mazuri ya kuishi, Jokate amesema watamkabidhi mama huyo nyumba hiyo ambayo inavyumba viwii vyenye tiles, umeme, choo, jiko na mahitaji mengine ya msingi.

Kupitia ukurasa wake wa  facebook DC Jokate ameshare habari hiyo kwa kuambatanisha muonekano wa picha za nyumba ya awali na ya sasa aliyomjengea kwa kushirikiana na baadhi ya makampuni waliojitolea.

”Naomba Mungu aendelee kututumia sisi viongozi na watumishi wake kuweza kugusa na kubadilisha maisha ya watu wengi zaidi. Tujitoe zaidi kuliko kufikiria maslahi yetu binafsi. Hatimaye ahadi tuliyotoa kwa mama wa mapacha waliotenganishwa Muhimbili imetimia. Na leo tunaenda kumkabidhi nyumba mpya ya kisasa ya vyumba viwili yenye tiles, umeme, choo, jiko na mahitaji mengine ya msingi. Ukilinganisha na nyumba ya awali aliyokuwa akiishi ya makuti kule Kimalamisale.

"Kipekee nawashukuru ubatanzania kwa kushirikiana na Ofisi Ya Mkuu Wa Wilaya kusimamia ujenzi kwa kutoa fedha za ujenzi na africanreflectionsfoundation kwa kushirikiana na Ofisi Ya Mkuu Wa Wilaya katika kununua kiwanja. Kwahiyo nyumba na kiwanja ina hati yenye majina ya watoto mapacha. Nimshukuru pia Michael Afisa Tarafa Mzenga kwa kusimamia vizuri ujenzi na mafundi wote walioshiriki. .Tukutane Mzenga leo kwenye makabidhiano.”  Ameandika Jokate

Mahakama yakataa maombi ya Katibu Mkuu CHADEMA Dk Mashinji na Matiko kusafiri nje ya Tanzania

$
0
0
Mahakama ya Hakimu ya Hakimu Mkazi Kisutu imetupilia mbali maombi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Vicnent Mashinji na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko, waliokuwa wanaiomba mahakama hiyo kusafiri kwenda nje ya nchi kwa nyakati tofauti.

Mahakama hiyo imewataka washitakiwa hao bila kujali nyadhifa zao kuwepo mahakamani kama washitakiwa wengine. Washitakiwa hao sasa watatakiwa kujitetea kwa siku tano mfululizo kuanzia Oktoba 7 hadi 11, mwaka huu na mahakama inategemea hakutakuwepo na sababu nyingine zozote zitakazosababisha kesi hiyo isianze kusikilizwa kwa muda huo.

Akisoma uamuzi huo, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema, safari hizo ni mambo yao wenyewe na hayahusiani na ratiba ya mahakama. Amesema kuwa, iwapo mahakama itaruhusu maombi ya washtakiwa hao kusafiri, itakuwa imefungua mwanya kwa washtakiwa wengine hivyo haitaweza maombi ya wengine.

Hakimu ameongeza kuwa, kesi hiyo ni ya muda mrefu, inalalamikiwa sana, inatakiwa kusikilizwa na kufika mwisho,  na Prof. Safari alisema wana mashahidi wengi hivyo kesi hii inahitaji kupangwa mara kwa mara kwa ajili ya kusikilizwa upande wa utetezi.

Mbali na Mashinji na Matiko, washitakiwa wengine ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe; Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa; Naibu Katibu Mkuu Taifa, Zanzibar, Salum Mwalimu; Mbunge wa Kibamba, John Mnyika; Mbunge wa Kawe Halima Mdee; Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.

Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, Februari Mosi na 16, mwaka jana, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko la kutawanyika.

Ongeza Nguvu Za Kiume, Maumbire Madogo Pamoja Na Tiba Mbalimbali

$
0
0
MASISA 3 POWER nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoazaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wara kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20-40

SUPER MONGERA  Hurefusha na kunenepesha maumbile madogo yaliosinyaa. Matatizi haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguluma na kujaa gesi,ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia ninadawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

Ni DR CHIPUPA  pekee mwenye uwezo wa kumrudisha mume , mke ,mchumb.

Kwa nini uhangaike na matatizo ya uzazi;   ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,

 wasiliana na DR. CHIPUPA 

Call+255 0673878343

watsap +255 0620510598

Huduma hii inakufikia popote ulipo

Askofu Mkuu Yuda Thadeus Ruwa'ichi Aruhusiwa Kutoka Hospitali Moi Leo.....amshukuru Rais Magufuli Na Taasisi Ya Mifupa Ya Muhimbili

$
0
0
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam  Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa'ichi akiongea kwa furaha na wanahabari mara baada ya kuruhusiwa kuondoka Taasisi ya Mifupa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI) alikokuwa akipatiwa matibabu kwa siku kadhaa. 

Wengine ni Askofu Msaidizi Eusebius Nzigilwa  wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface (wa pili kushoto)  na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Profesa Joseph Kahamba (kulia). 

Mhashama Askofu Mkuu Ruwa’ichi, ambaye alifikishwa hapo MOI  akitokea katika Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro (KCMC) Jumatatu Septemba 9 na kufanyiwa upasuaji mkubwa wa ubongo, amemshukuru Mungu kwa yote na pia amemshukuru  Rais John Pombe Magufuli kwa kutoa msaada wa haraka wa ndege ya Rais kumsafirisha hadi Dar es salaam alikopatiwa matibabu 

Pia amewashukuru Madaktari wa KCMC kwa matibabu ya awali na wa MOI kwa kuokoa maisha yake kwa kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu. Vile vile amewashukuru waumini na Watanzania wote kwa ujumla kwa kumuombea.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam  Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa'ichi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili MOI) pamoja na Askofu Msaidizi Eusebius Nzigilwa  wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface (wa pili kushoto)  na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Profesa Joseph Kahamba (kulia) baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali leo Jumatano Septemmba 25, 2019.

Mhashama Askofu Mkuu Ruwa’ichi, ambaye alifikishwa hapo MOI  akitokea katika Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro (KCMC) Jumatatu Septemba 9 na kufanyiwa upasuaji mkubwa wa ubongo, amemshukuru Mungu kwa yote na pia amemshukuru  Rais John Pombe Magufuli kwa kutoa msaada wa haraka wa ndege ya Rais kumsafirisha hadi Dar es salaam alikopatiwa matibabu.

Pia amewashukuru Madaktari wa KCMC kwa matibabu ya awali na wa MOI kwa kuokoa maisha yake kwa kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu. Vile vile amewashukuru waumini na Watanzania wote kwa ujumla kwa kumuombea.

PICHA NA ISSA MICHUZI

Waziri Kairuki Aipa Siku Saba TIC Kuwafikia Wawekezaji Wazawa

$
0
0

NA MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji nchini Mhe.Angellah Kairuki ameutaka uongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kutembelea na kugakua mazingira ya wafanyabiashara na wawekezaji wazawa waliopo mkoa wa Ruvuma ndani ya siku saba.

Ametoa kauli hiyo alipotembelea na kukagua kiwanda cha kutengeneza kahawa cha Wilaya ya Mbinga cha MCCCO pamoja na kiwanda cha DAE kwa lengo la kukagua mazingira na utendaji wa viwanda hivyo Mkoani Ruvuma.

Ziara hiyo iliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe.Christina Mdeme pamoja na watendaji kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Viwanda, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Nishati, Wizara ya Madini, Wizara ya Ardhi, pamoja na baadhi ya taasisi za serikali ikiwemo na Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC).

Waziri Kairuki alitoa maelekezo hayo baada ya kubaini kuwa kituo hicho  hakijawafikia wawekezaji wazawa kikamilifu hususani waliopo mikoani ili kuwatambua na kuwaelimisha kuhusu fursa zinazotolewa na taasisi hiyo.

 “Ninawaagiza TIC mfike katika viwanda hivi ndani ya siku saba kuanzia sasa ili kuwatembelea na kuwaeeleza huduma zinazotolewa na taasisi yenu ikiwemo fursa zilizopo na endapo wataona inafaa wajisajiri kwa kuwa ni suala la  hiari,”alisisitiza Waziri Kairuki

Aidha alieleza kuwa ipo tija ya kuwatambua wawekezaji wazawa waliopo nchini ka kuzingatia mchango wao katika uchumi wa viwanda kwa kuzingatia mwaka 2019 ni mwaka wa uwekezaji.

“Naelewa kuwa ipo miradi mingi iliyofikiwa na TIC zaidi ya asilimia 72 hivyo niwatake mfike haraka mkoani Ruvuma hususan katika viwanda hivi vya kahawa, ili kuvitambua na kueleza fursa na umuhimu wa kujisajili na Taasisi hii ili kuendelea kuchangia na kuwa na tija zaidi katika uchumi wa nchi,”alisisitiza

Mkurugenzi wa Sera Mipango na Utafiti wa TIC Mafutah Bunini amesema katika kuboresha utendaji wao wamefungua ofisi za kanda saba ili kuwafikia kwa urahisi wawekezaji wa ndani na kwamba wanaotoa uzito sawa kwa wawekezaji wa ndani na nje.

“Na katika hili ndiyo maana viwango vya mitaji ya uwekezaji vinatofautiana kwa wawekezaji wa nje na ndani ambapo mwekezaji wa ndani anatakiwa awe na mtaji wa dola laki moja lakini mwekezaji wa nje ni dola laki tano.

Naye Meneja wa Kiwanda cha kutengeneza kahawa cha Wilaya ya Mbinga (MCCCO) amemuahakikishia Waziri kuwa wataendelea kuboresha mazingira mazuri ya wafanyakazi na kuongeza thamani ya bidhaa zao za kahawa na kuhakikisha jamii iliyowazunguka inanufaika na kiwanda hicho.

“tunaishukuru Wizara ya Uwekezaji kwa jitihada inazofanya za kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kuondoa vikwazo mbalimbali vilivyokuwepo awali hali inayosababisha uwekezaji kukua kwa kasi”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha kutengeneza kahawa cha DAE Bw. Danistan Komba ambaye pia ni mkulima wa kahawa alimpongeza waziri kwa kutembelea kiwandani hapo na kueleza changamoto za masoko ya kahawa na kuiomba Serikali kuendelea kuwaangalia wawekezaji hao wazawa.

“Kipekee napongeza ujio wako, japo tunachangamoto ya masoko kwa kuzingatia kiwanda kina uwezo wa kuzalisha tani 36,000 kwa mwaka na kuuza katika baadhi ya nchi,”alieleza Komba

Alifafanua kuwa, pamoja na changamoto za uhaba wa masoko, kiwanda kimekuwa kikishiriki katika maonesho ya nchi zinazolima kahawa ikiwemo Kenya, Uganda,Rwanda,Burundi na Ethiopia.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Cosmas Nshenye alieleza kuwa, ziara hiyo imeleta chachu kwa wafanyabiashara na wawekezaji wazawa kwa kuzingatia kuwa, Serikali imeahidi kutoa ushirikiano wa kina katika kutatua changamoto zao ikiwemo kuwataka TIC kufika na kuwatembela katika muda alioagiza.

=MWISHO

Latest Images