Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali Yamwita Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO)..... Yasisitiza Tanzania HATUNA Ugonjwa wa EBOLA

$
0
0
Serikali imemwita Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) hapa nchini kupata kwa kina hoja za Shirika hilo zinazosambaa kupitia vyombo vya habari. 

Mwakilishi huyo amesisitiza kuwa WHO haijasema wala haina ushahidi wowote kuwa Tanzania kuna Ebola na itashirikiana na Serikali.

Aidha, katika mazungumzo hayo WHO imeafiki kuwa kama kuna mahitaji ya kupata taarifa zaidi kutoka Serikali ya Tanzania lazima utaratibu ulioanishwa katika miongozo ya taasisi hiyo na ambayo imeridhiwa na Serikali ifuatwe kikamilifu.

Haya yanajiri wakati shirika la madaktari wasio na mipaka Medicins Sans Frontiers MSF limelituhumu shirika la WHO kwa kutumia mfumo usiofaa wa utoaji chanjo nchini DRC  likisema utaratibu wa mgao unaotumika unaruhusu virusi kujitokeza tena katika jamii ambazo tayari ugonjwa huo ulikuwa umetokomezwa na watu kulindwa kutokana na maambukizi mapya.

Shirika la WHO limekanusha madai kwamba linatoa chanjo kwa mgao na badala yake limesema linafanya kazi kwa bidii kama mashirika mengine kuutokomeza kabisa mlipuko wa ugonjwa wa ebola katika Jmahuri ya Kidemokrasia ya Congo. 


Shirika hilo limesema katika taarifa yake kwamba linashirkikiana na serikali ya Congo kuzifikia jamii nyingi na watu wengi kadri inavyowezekana katika maeneo yaliyoathirika na mlipuko wa ebola na wala halijaweka kiwango wala vikwazo katika utoaji wa chanjo.

Kilichoendelea Leo Mahakamani Katika Kesi ya anaedaiwa kumuua Mkewe kwa kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa

$
0
0
Upande wa Jamhuri leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu umesema upelelezi wa kesi ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara Hamis Said (38), anayetuhumiwa kumuua mkewe, Naomi Marijani, upo katika hatua za mwisho kukamilika.
 

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, amemweleza Hakimu Mkazi, Salum Ally, kuwa upelelezi wa kesi hiyo upo katika hatua nzuri na za mwisho kukamilika..

Wakili Wankyo ameomba shauri hilo liahirishwe hadi tarehe nyingine ambapo kesi imeahirishwa hadi Oktoba 7, 2019 kwa ajili ya kutajwa.

Mshitakiwa anakabiliwa na kosa la mauaji ambapo anadaiwa kumuua Mke wake Naomi kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa ambapo alichukua majivu ya marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake.

Kiboko Ya Maumbile Madogo Na Nguvu Za Kiume

$
0
0
*NGETWA MIX*/
√Hii ndio dawa bora ya mitishamba kiboko ya maumbile Madogo(KIBAMIA) Hurefusha na kunenepesha maumbile  mafupi pia  yaliyoingia ndani kutokana na kitambi ama kuathirika na punyeto

*📌SUPER MORINGA MIX*/
Ni dawabora ya nguvu za kiume yenye mchanganyiko wa miti shamba 10 yenye maajabu yafuatayo:/
🔖(1)Inatibu upungufu wa nguvu za kiume mara dufu na kuimarisha misuri   ilio legea na kusinyaa wakati wa tendo la ndoa/
🔖(2)Kuongeza hamu ya tendo kukufanya uweze kurudia tendo hadi mara tatu bila kuchoka
🔖(3)Itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15-30 kwa tendo la Kwanza na utakuwa na uwezo wa Kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3-4 bila hamu kuisha na inatibu kabisa/
.
*MATATIZO HAYA HUSABABISHWA NA*/
🔖(1)Tumbo kujaa gesi, na kuunguruma chini ya kitovu/
🔖(2) Choo kuwa kama Cha mbuzi/
🔖(3)Ngiri/
🔖(4)Kama umejichua sana punyeto/
🔖(5)Kisukari/
🔖(6)Presha ya kupanda na kushuka/
🔖(7)Vidonda vya tumbo,/
.
Na haya yote husababisha/
📍Kuishiwa kwa nguvu za kiume 📌/
. _______________________
Bado hujachelewa dawa hizi ni mpya kabisa  ni tofaut na ulizo wahi kutumia pia zimeonesha mafanikio kwa watu wengi sana/

Pia tuna tibu  KISUKARI,PRESHA,VIDONDA VYA TUMBO N.K/
._______________________
DR .SELEMANI OMARY ANAPATIKANA  DAR ES SALAAM , PIA UNAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO  NDANI NA NJE YA NCHI .SIMU NO:/
*📞+255788468114*

Ongeza Nguvu Za Kiume, Maumbire Madogo Pamoja Na Tiba Mbalimbali

$
0
0
MASISA 3 POWER nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoazaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wara kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20-40

SUPER MONGERA  Hurefusha na kunenepesha maumbile madogo yaliosinyaa. Matatizi haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguluma na kujaa gesi,ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia ninadawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

Ni DR CHIPUPA  pekee mwenye uwezo wa kumrudisha mume , mke ,mchumb.

Kwa nini uhangaike na matatizo ya uzazi;   ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,

 wasiliana na DR. CHIPUPA 

Call+255 0673878343

watsap +255 0620510598

Huduma hii inakufikia popote ulipo

Download App Yetu Kwenye Simu Yako Ili Uweze Kupata Habari Zetu Kwa Haraka Zaidi

$
0
0
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.

Bashe: Wadau Zalisheni Mbegu Za Mazao Kwa Wingi

$
0
0
Serikali imewataka wazalishaji mbegu za mazao nchini kuongeza uzalishaji na ubora ili nchi iepukane na utegemezi toka nje.

Akizungumza katika kikao cha wadau wa mbegu leo (Jumanne 24.09.2019) jijini Dodoma,Naibu Waziri wa Kilimo Husein Bashe amesema ili Tanzania ifikie malengo ya kukuza  uzalishaji wenye tija katika kilimo lazima ijitegemee kwa mbegu.

Amebainisha kuwa usalama wa chakula unategemea sana uwezo wa nchi kuzalisha mbegu za mazao ndani na si kutegemea wahisani.

 “Kuwa na nchi inayotegemea mbegu za mazao toka  nje kunaondoa dhana ya uhuru na kujitegemea,hivyo kuhatarisha usalama wa chakula na taifa” alisisitiza Naibu Waziri Bashe

Bashe amewaeleza wadau hao  kuwa Wizara ya Kilimo ina lengo la kuhakikisha nchi inajitosheleza kwa mbegu hususan zinazozalishwa nchini.

Ameziagiza Taasisi za Utafiti wa Kilimo(TARI), Kampuni ya Mbegu (ASA) kushirikiana na wadau binafsi kuwekeza mitaji ili kuinua uzalishaji wa mbegu bora ili kukidhi  mahitaji ya wakulima.

“Ni budi sasa taasisi zetu za TARI na ASA zikaanza kuzalisha mbegu mara tatu kwa mwaka kwenye mashamba kwa njia  ya umwagiliaji badala ya kutegemea mvua “ Naibu Waziri alisema

Bashe amebainisha kuwa kwa sasa Tanzania ina utegemezi wa mbegu asilimia 60 kutoka nje ya nchi.

Hali hiyo imesababisha mbegu nyingi kuuzwa kwa bei kubwa na zingine kulalamikiwa na wakulima kuwa na ubora mdogo.

Naibu Waziri Bashe amewataka wadau kutengeneza mpango maalum wa kuongeza uzalishaji kwani serikali pekee haiwezi kutokana na soko la mbegu kuwa kubwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao ,Wizara ya Kilimo  Nyasebwa Chimagu amesema kikao hicho kitajadili kwa mapana changamoto za upatikanaji mbegu bora na mfumo mzuri wa usambazaji mbegu nchini.

Nyasebwa aliongeza kusema kwa sasa wakulima wana malalamiko mengi  kuhusu upungufu wa mbegu ,hivyo wizara na wadau wana jukumu la kutafuta majawabu mapema.

Tanzania Kuwa Mwenyeji Wa Mkutano Wa Kimataifa Wa Sheria Kati Ya Afrika Na Asia

$
0
0
Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Mashauriano ya Masuala ya Kisheria ya Nchi za Asia na Afrika (ASIA-AFRICAN LEGAL CONSULTATIVE ORGANISATION (AALCO) utakaofanyika nchini kuanzia tarehe 21 hadi 25, Oktoba jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria PROF. Sifuni Mchome amesema mkutano huo utawakutanisha Mawaziri wa Sheria na Wanasheria Wakuu kutoka nchi za Afrika na Asia ambao kwa pamoja wataangalia maendeleo ya sekta ya sharia na kujadili changamoto mbalimbali zinazozikabili nchi wanachama na jinsi ya kukabiliana nazo.

Prof.Mchome amesema katika mkutano huo Tanzania itakabidhiwa kiti cha Uenyekiti wa Jumuiya hiyo kupitia kwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga ambaye atatumikia kiti hicho kwa mwaka mmoja.

Prof. Mchome alikuwa akizungumza na wadau mbalimbali kutoka Serikalini Ofisini kwake katika Mji wa Serikali Mtumba jijijini Dodoma ambao aliwaomba kuuungana na Wizara ya Katiba na Sheria katika kuhakikisha Mkutano huo utakaoitangaza nchi kimataifa unafanikiwa.

AALCO ilianzishwa mwaka 1956 kwa lengo la kuwa chombo cha ushauri na ushirikiano katika masuala ya sheria za kimataifa kwa nchi za Asia na Afrika.

Toka kuanzishwa kwake AALCO imewezesha nchi wanachama kushirikiana na kubadilishana  uzoefu katika masuala mbalimbali ya sheria za kimataifa na kimechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sheria za kimataifa.

Tanzania ilijiungana umoja huo 1973 na kwa sasa Katibu Mkuu wake ni Mtanzania Prof. Gastorn ambaye alichaguliwa kushika nafasi hiyo mwezi Agosti 2016.

Jinsi Wachawi Wanavyowarubuni Watu

$
0
0
Hakuna  uchawi  wowote  ule  chini  ya  jua  ambao  unaweza kufanya  kazi  kwenye  maisha  ya  mtu  bila  ridhaa  ya  mtu  huyo.


Maneno  mabaya  ambayo  umekuwa  ukitamkiwa  na  watu  wengine  na  kuyasikia  halafu  ukakaa  kimya  bila  kuyakataa  kwa  maneno  au  bila  kuyafuta ndo chanzo cha kujiumiza mwenyewe .   

Mtu  akikutamkia  maneno  mabaya  iwe  kwa  kukusudia  ama  kwa  bahati  mbaya, usiyakubali  hata  kama  anakutolea  mfano  tu.  

Yakatae  na  uyafute  papo  hapo  na  yeye  akiwa  anasikia  au  kama  utashindwa  kufanya  hivyo  basi  hakikisha  baadae  unayakataa  na  kuyafuta  maneno  hayo  kwa  maneno. 

 Ipo mifano  mingi  sana  kuna  watu  walitamkiwa  maneno  mabaya tena  ya  kawaida  kabisa  na  hawakuyafuta  na  miaka  mingi  baadae  maneno  hayo  waliyo  tamkiwa  yamewatokea.

Mifano :  Kuna  jamaa  mmoja  miaka  miwili  baada  ya  kumaliza  chuo na  kupata  kazi, alikutana  na  mtu ambae  walisoma  wote  chuo.  


Huyu  jamaa  alikuwa  amebadilika, amenenepa  na  mwili  umeongezeka. Sasa  katika  maongezi  yao  huyo  mwenzake  akamwambia “ Kaka  kwa  mwili  huu, muda  si  mrefu  madaktari  wataanza  kukukataza  kutumia  baadhi  ya  vyakula “  Yeye  hakujibu  chochote  akawa  anacheka  tu.   Mwisho  wa  siku  miaka  kadhaa  baadae , jamaa akapatwa  na  presha  na  kisukari  na  sasa  hivi  kweli  hatumii  baadhi  ya  vyakula.


Endelea kuisoma hapa << HAPA>>

IGP Sirro Awacharukia Maofisa wa Jeshi la Polisi......"Acheni Ubinafsi, Mimi ndo IGP na Kama Unaona Sitoshi Subiri Zamu Yako Mungu Akipenda"

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro, amewaeleza maofisa wa Jeshi hilo kuwa mara nyingi kinachowasumbua ni ubinafsi na kuwaambia haiwezekani wote wakawa ma-IGP "There is no way" kwani yeye hakujichagua.

Kauli hiyo ameitoa leo Septemba 24, 2019 wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili cha maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi Makao Mkuu na Makamanda wa mikoa.

Akizungumza na viongozi hao IGP Sirro amesema wakati mwingine wapo wanaona kama yeye hatoshi.

"Wakati nikiwa ninazungumza mwingine anaona hatoshi huyu, ninatosha mimi, kama unajiona kama unatosha na Mungu hakukupa sasa si ukubali sasa mimi nitafanyaje?, hakuna njia ya kunisema nikasema sasa atajuaje kama mimi sitoshi, kamanda wa Kinondoni (Mussa Taibu) unanipata vizuri umenisikia sasa naenda mwaka wa tatu bado unafikiria, kubali yaishe itafika mahali Mungu akiona unatosha atakupa," amesema.

Amesema wakati huu bado Mungu ameona hata kama uwezo wake ni mdogo lakini ndiyo amempa.


"Itafika wakati nami nitaondoka na ninamuomba Mungu nikiondoka niliache Jeshi la Polisi likiwa na heshima yake" Amesema

Katika hatua nyingine IGP Sirro amelipongeza jeshi lake kwa namna ambavyo limeweza kupambana na kukomesha mauaji ya raia yaliyokuwa yakifanyika Wilayani Kibiti mkoani Pwani.

''Habari ya Kibiti ndani ya Jeshi la polisi haitofutika, issue ilikuwa ni kubwa sana na kwa challenge jeshi la polisi,  lakini slogan yetu ya umoja ndiyo nguvu yetu ndio imetufikisha hapa tulipo. 


"Sasa hivi ukizungumzia Kibiti hata viwanja vimepanda bei, wanasiasa wanafanya siasa zao ni heshima ya jeshi lakini pia ni heshima kwa vyombo vingine vya ulinzi na usalama'', amesema

TECNO Kujiweka Karibu Zaidi Na Wateja Wake.

$
0
0
Kampuni ya simu ya TECNO inayotambulika kwa uzalishaji wa simu za viwango vya hali juu imezidi kutanuwa wigo wa soko la simu nchini Tanzania na hii ni mara baada ya uzinduzi wa duka jipya la simu za TECNO maarufu kama ‘TECNO Smart Hub’ Kariakoo kwa lengo ikiwa kufikisha huduma sitahiki kwa wateja wake.
Hii ni Smart Hub ya tatu kufunguliwa nchini Tanzania na kampuni ya TECNO. TECNO smart Hub zimekuwa zikijihusisha na uuzaji wa bidhaa za TECNO tu kama vile simu za mkononi, chaji, battery, powerbank, cover za simu lakini pia zinatoa elimu kuhusiana na utumiaji na utuzaji wa simu.

“TECNO Smart Hub itahudumia wateja wengi zaidi kwa wakati mmoja lakini vile vile kwa bidhaa zetu zina warranty ya mwaka mmoja na mwezi mmoja” alisema afisa wa mahusiano wa kampuni ya simu ya TECNO Bwana Eric Mkomoye.

Uzinduzi huo uliambatana na tafrija fupi kutoka kwa mchekeshaji Mpoki Mujuni almaarufu Mpoki, Jsquare dancers, na michezo mingine ikiwepo luck draw kwa wateja walionunua simu ndani ya siku hiyo na kujishindia fridge, TV na zawadi nyengine kibao.

Kwa maelezo mengi zaidi tembelea @tecnosmarthub.

DPP Atoa Muongozo Kuhusu Wahujumu Uchumi Wanaotaka Kusamehewa

$
0
0
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), Biswalo Mganga amesema ofisi yake ipo tayari kutekeleza ushauri wa Rais  Magufuli aliyetaka kusikilizwa kwa mahabusu wanaokabiliwa na makosa ya uhujumu uchumi iwapo watakuwa tayari kukiri na kurejesha fedha za serikali wasamehewe. .

Mganga amesema jambo hilo linawezekana endapo mshtakiwa mwenyewe ataiandikia ofisi yake barua kupitia kwa Mkuu wa Gereza na kusisitiza kuwa barua hiyo inapaswa kuandikwa na mtuhumiwa mwenyewe aliye gerezani na siyo wakili. .

“Utaratibu ni kwamba, mtuhumiwa mwenyewe aliyeko mahabusu anatakiwa aniandikie barua kupitia kwa mkuu wa gereza akikiri kosa na kuomba kutubu haraka iwezekanavyo na sisi tutachukua hatua.
 
 “Ni mtuhumiwa mwenyewe ndiye anatakiwa kuandika barua, siyo wakili. Unajua wakili anaweza kubadilika na hata mtuhumiwa kumkana kuwa sijamtuma afanye alichofanya kwa niaba yangu, ndiyo maana mara zote watuhumiwa wanaoomba msamaha na kukiri huandika barua wenyewe kwa mkono wao kupitia kwa mkuu wa gereza” Amesema DPP Mganga.

Akizungumza jana wakati wa kuwaapisha baadhi ya viongozi aliowateua, Rais Magufuli alimuomba DDP ndani ya siku saba kuangalia uwezekano wa kusamehewa baadhi ya watuhumiwa waliokaa muda mrefu mahabusu kwa makosa ya uhujumu uchumi endapo watatubu, akisema anatamani kuona Watanzania wote wanaishi huru ili kushiriki ujenzi wa taifa.

Watu Watatu Wakamatwa Pwani Kwa Kuiba Komyuta Mpakato Za Shule Ya Msingi Msoga

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
JESHI la polisi mkoani Pwani ,linawashilia watu watatu wanaodaiwa kuiba kompyuta mpakato saba zenye thamani ya sh. milioni 4.2 mali ya shule ya msingi Msoga iliyopo Chalinze wilayani Bagamoyo.
 
Aidha Jeshi hilo, limewakamata watu 67 kwa tuhuma za kufanya uhalifu mbalimbali ,katika misako inayoendelea mkoani hapo.
 
Kamanda wa Polisi, mkoani humo Wankyo Nyigesa aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake, kuwa siku ya tukio watu wasiojulikana walivunja kwenye shule hiyo na kuiba vifaa hivyo.
 
Alieleza, tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo baada ya tukio hilo uongozi wa shule ulitoa taarifa polisi ambao walianza msako na walikamata watu hao wakiwa na kompyuta tatu.
 
“Tunaendelea na uchunguzi kwa watu wengine ambao watakuwa na hizo kompyuta nne zilizobakia ili waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,”alisema Wankyo.
 
Katika tukio jingine Said Athuman (32) Mkazi wa mkoa wa Tanga amekamatwa kwa tuhuma za kukutwa na matairi ya pikipiki 100 na 75 ya bajaji ambayo yanadhaniwa kuwa hayakulipiwa ushuru.
 
Alieleza, tukio hilo lilitokea septemba 21 mwaka huu majira ya saa 3:00 usiku eneo la Round About kata ya Dunda tarafa ya Mwambao wilaya ya Bagamoyo.
 
Wankyo alifafanua ,mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia gari aina ya Mazda Pick Up yenye namba T 135 DPU ambapo gari hilo lilikamatwa wakati polisi wakiwa doria na inadhaniwa mali hizo zilipitia kwenye bandari bubu zilizopo Bagamoyo.
 
Pia mkazi wa Lugoba Mtupe Abdala (45) anashikiliwa kwa tuhuma za kusafirishama mbao ngumu 60 kwa kutumia gari lake aina ya Howo lenye namba za usajili T 693 CEH/T 672 DSK bila ya kuwa na kibali.
 
Hata hivyo  ,Wankyo alielezea polisi walimkamata mtuhumiwa septemba 20 eneo la Chalinze Mzee tarafa ya Chalinze wilaya ya Kipolisi Chalinze katika mskao unaoendelea wa usiku na mchana wa kukamata wahalifu.

Kutana na Mohamedi Buruhani Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH .....Anauwezo wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mohamedi Buruhani Mtabibu wa Nyota za Binadamu  Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Mohamed Buruani Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. 

Anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO . Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie ..Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Mohamed Buruhan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN, Anatafsiri Ndoto. ,KUSAFISHA NYOTA, Mvuto wa Mwili na BIASHARA, ...MIGUU Kufa GANZI na mengi zaidi (+255  715971688 au (+255  756914036

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

IGP Sirro Ashangazwa na Makamanda wa Polisi nchini Wanaojihusisha na Siasa

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, amekemea tabia ya baadhi ya Makamanda wa Polisi nchini kujihusisha na shughuli za kisiasa kwa kile alichoeleza kuwa ni kinyume na Katiba ya nchi.

Akizungumza kwenye kikao chake na Wakuu wa Jeshi la Polisi wa Mikoa, IGP Simon Sirro amesema hata jeshi hilo linashangazwa na baadhi ya maafisa wake kujihusisha na siasa.

"Baadhi yetu kujiingiza kwenye harakati za kisiasa si sahihi, kwa mujibu kwa Katiba yetu, lakini kwa 'ushahidi' unashindwa kabisa kujua maadili yako unatakiwa kufanya nini kwenye umma"

“Watu wanataka kusikia unasema nini, wewe sio mwanasiasa unajiaibisha mwenyewe, tujikite kwenye majukumu yetu hayo unayofanya umeyatoa wapi.?

“Halafu unafanya hivyo kwa sababu uko kwenye nafasi hiyo tukikutoa hapo utaweza kufanyia nyumbani kwako? Si Pahala pa kufurahisha watu, wengine wanafanya vitu  kutafuta umaarufu wa kisiasa tu, unamfurahisha nani?” Amesema IGP Sirro

Wafanyabiashara wa Madini Soko Dogo la Madini Katoro waiomba Serikali iwaruhusu kuwa na Wasaidizi wa kununua madini kwenye mialo ya uchenjuaji

$
0
0
Wafanyabiashara wa Madini katika Soko Dogo la Madini Katoro wameiomba Serikali iwaruhusu kuwa na Wasaidizi watakaowasaidia kununua madini maeneo  yenye mialo ya uchenjuaji na kuwauzia kwenye vituo vya ununuzi. 

Wafanyabiashara hao wametoa ombi hilo wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipotembelea  soko hilo  kwa lengo la kujifunza na kuangalia namna masoko ya madini yanavyoendeshwa. 

Akitoa ufafanuzi zaidi kuhusu suala hilo, Naibu Waziri wa Madini  Stanslaus Nyongo amesema kuwa, Sheria na Kanuni za biashara ya madini zinaelekeza kuwa shughuli za uuzaji na ununuzi wa madini zinapaswa kufanyika  kwenye vituo  maalum vya manunuzi hivyo suala la kuwa na wasaidizi kwenye mialo wa kuwauzia wafanyabiashara hao linakinzana na Sheria ya Madini na Kanuni za madini kwenye masoko. 

‘’   Kamati ndiyo inaishauri Serikali, ndiyo Bunge na Wawakilishi wa wananchi. Tutaendelea kutatua changamoto  tunazokutana nazo kwenye masoko. Sote tunajua Masoko ni Mapya, Sheria Mpya, Kanuni Mpya, hivyo tutaendelea  kutatua changamoto hizo yakiwemo masuala  ya vifaa na watumishi,’’ amesema Naibu Waziri  Nyongo. 

Aidha, Naibu Waziri Nyongo amewataka wafanyabiashara wa madini na wachimbaji kuyatumia masoko ya madini  na kueleza kuwa, kufanya biashara ya madini nje ya masoko ni kujiweka kwenye matatizo. Pia, amewasisitiza  kuhusu matumizi sahihi na salama ya zebaki na kueleza kuwa, serikali itaendelea kuangalia njia mbadala za teknolojia ili kuweza kuachana na matumizi ya zebaki. 

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mariam Mzuzuri amewataka wafanyabiashara hao kuendelea kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria na taratibu wakati Serikali na Kamati zikiangalia namna ya kuzifanyia kazi   changamoto zilizowasilishwa kwao. 

‘’ Kwa kuwa masoko haya yanafanya kazi kwa mujibu wa Sheria ni vyema suala hili mtuachie kwanza sisi na serikali ili tuliangalie,’’ amesema Mzuzuri. Kufuatia hali hiyo, Mzuzuri ameitaka wizara kuendelea kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara na wachimbaji wa madini ili wajue namna ya kuyatumia masoko ya madini na kujua mwenendo mzima wa shughuli za madini na biashara ya madini inavyofanyika. 
Katika hatua nyingine, kamati imeitaka Serikali kuhakikisha suala la Ulinzi kwenye masoko ya Madini halisubiri michakato bali linatakiwa kufanyiwa kazi haraka kutokana na rasilimali zilizopo katika masoko hayo. 

Makamu Mwenyekiti amesema hayo kufuatia ombi la kuimarishwa kwa Ulinzi katika Soko la Katoro lililotolewa na Wafanyabiashara wa Madini sokoni hapo wakati  wa ziara yake mkoani Geita.   

Naye, Mjumbe wa Kamati hiyo Fred Mwakajoka ametaka taasisi zote za serikali zinazoshirikiana na Tume ya Madini kuendesha masoko hayo ziwepo katika masoko hayo ili kurahisisha utendaji wa majukumu ya masoko . 

Baada ya kutembelea soko la Katoro, Kamati hiyo pia imetembelea Soko la Madini Kahama na baadaye  itatembelea  Nzega. Ziara ya kamati kutembelea masoko imefanywa na kamati hiyo baada ya kutembelea Soko Kuu la Madini Geita na Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.

Jeshi La Polisi Mkoani Dodoma Lamnasa Mtu Mmoja Akijaribu Kutorosha Madini

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni.Dodoma.
MTU mmoja Khalifa Mohamed Kinyaka (51) anashikiliwa na jeshi la Polisi Mkoani Dodoma, kwa tuhuma za kutorosha na kusafirisha viroba sita vya madini vyenye uzito wa kilogramu 410.75.

Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma Gilles Muroto, amesema mtu huyo alikamtwa katika basi la abiria la Jambo Express, lenye namba za usajili T 704 DLF, linalofanya safari zake kati ya Katesh na Dar es salaam.
 
Amesema mbinu iliyotumiwa na mtuhumiwa ni kupanda basi tofauti na lile alilopakia viroba vingine vitano, katika basi la Emigrace lenye namba za usajili T 730 DGL lililokuwa likiendeshwa na Adrian John Temba (32), likitokea Babati Manyara kuelekea jijini Dar es salaam.
 
Hata hivyo uchunguzi wa Jeshi la Polisi unaonesha kuwa madini hayo yametoka katika machimbo ya Kijiji cha Yobo Kwahemu Wilayani Chamwino, na juhudi za kuwapata washiriki na wanunuzi zinaendelea ili kuweza kuwafikisha Mahakamani.
 
Akifafanua juu ya taratibu husika za usafirishaji madini, Mhandisi Migodi wa Ofisi ya Madini Dodoma Sasi Marwa, amesema muhusika alipaswa kuwa na vibali toka eneo husika na kwamba tathmini itafanywa ili kujua thamani halisi ya madini hayo.
 
Tukio hili linakuja ikiwa ni muda mfupi baada ya Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma, kuwakamata watu zaidi ya 70 kwa  makosa mbalimbali   Septemba 21 mwa ka huu , ikiwemo usafirishaji wa mafuta ya vyombo vya moto kwa njia hatarishi.


Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano September 25

Walimu Mkoani Kagera Watakiwa Kuwa Mabalozi Wazuri Wa a Kulipa Kodi Ili Kukuza Uchumi Wa Nchi.

$
0
0
Na Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti  amewataka walimu mkoani humo kuwa mabalozi wazuri kwa kulipa kodi ili kuweza kuchangia ukuaji wa pato la nchi.
 
Mkuu wa Mkoa Gaguti amesema hayo Septemba 23, 2019 wakati akifungua kongamano la Walimu na Benki ya NMB Bukoba katika siku ya walimu kwenye ukumbi wa Hoteli ya ELCT Bukoba .
 
Ameongeza kwamba walimu  ni  jeshi kubwa kila watakapo kuwa wenasimama waendelee kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ulipaji kodi na kuwahamasisha wananchi kudai risiti kila wakinunua bidhaa na kuwahamasisha wanaouza kutoa risiti.
 
Mkuu wa Mkoa Gaguti ametoa rai kwa benki ya NMB kuona namna ya kuwapunguzia riba walimu sababu ni wadau wakubwa wa benki hiyo tangu mwanzo.
 
 Pia amewataka walimu kutanua wigo wa kuunda vikundi vya pamoja mfano kwenye Kata na kuomba mikopo ya miradi mikubwa na ya pamoja ili kuinua vipato vyao hasa pale wanapostaafu. 
 
 Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Sekondari Gabulanga iliyopo wilayani Missenyi bwana Mutalemwa Makwabe kwa niaba ya Walimu wenzake amesema kuwa wanaishukuru benki hiyo kwa namna inavyoendelea kuwajali walimu pamoja na kutoa misaada mbalimbali katika shule uku akitaja kuwa shule yake iliwahi kupatiwa misaada mbali mbali na benki hiyo ikiweno madawati pamoja na mbao za kuezekea.

Kwa upande wake Meneja wa NMB kanda ya ziwa bwana Ibrahimu Agustino amesema kuwa benki hiyo inatenga 1% kila mwaka katika kuhudumia jamii  na kuongeza kuwa kwa mwaka huu wametenga shilingi bilioni moja na mpaka sasa wametoa zaidi ya milioni mia sita katika  kusaidia jamii.




Waziri Mkuu: Imarisheni Mahusiano Na Wadau

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mahusiano kati ya Serikali na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa kidini, kimila ni muhimu yakaimarishwa.

Ameyasema hayo jana (Jumanne, Septemba 24, 2019) wakati akipokea taarifa ya mkoa wa Iringa alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Iringa kwa ajili ya ziara ya kikazi.

Waziri Mkuu alisema ni lazima mahusiano hayo yakadumishwa katika ngazi zote kwa sababu Serikali ipo kwa ajili ya wananchi wote na inawahudumia bila ya ubaguzi.

Aliwataka viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia maeneo mbalimbali nchini wahakikishe wanatekeleza majukumu yao ipasavyo na uwajibikaji wao uwe na tija.

 Waziri Mkuu amesisitiza kuwa watendaji wahakikishe suala la ukusanyaji wa mapato linapewa kipaumbele katika maeneo yao.

“Ukusanyaji wa mapato ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa kwa sababu miradi ya maendeleo kama ujenzi wa shule haiwezi kutekelezeka bila ya kukusanya mapato.”

Awali, Akisoma taarifa ya mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi alisema mkoa huo umepewa zaidi ya sh. bilioni saba kwa ajili ya ujenzi wa hospitali za wilaya.

Alisema fedha hizo zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa hospitali kwenye Manispaa ya Iringa (98%), Halmashauri ya wilaya ya Iringa (90%), Kilolo(99%), Mufindi (89%).

Mkuu huyo wa mkoa alisema mbali na fedha hizo za ujenzi wa hospitali pia Serikali imetoa zaidi ya sh. bilioni tatu kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya.

Akizungumzia kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa, kiongozi huyo alisema wanaendelea na maandalizi.Mkoa una vijiji 360, mitaa 222 na vitongoji 2,216

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

Iran Yaiachia Huru Meli Ya Mafuta ya Uingereza

$
0
0
Meli ya mafuta iliyokuwa na bendera ya Uingereza na ambayo ilikuwa ikishikiliwa katika bandari ya Abbas nchini Iran kwa zaidi ya miezi miwili, imeanza safari kuelekea Uingereza. Tovuti maalum inayofuatilia safari za baharini imeripoti hayo.

Hapo jana, msemaji wa serikali Ali Rabiei alitangaza kuwa mchakato wa kisheria umekamilika na meli hiyo inayomilikiwa na Sweden iko huru kuondoka. 

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, tovuti ya Tanker Trackers imeandika kuwa picha za satelaiti zinaonyesha kuwa meli hiyo imeondoka. 

Mnamo Julai 19, kikosi maalum cha askari wa mapinduzi nchini Iran kiliizingira meli hiyo kwa jina Stena Impero katika mlango bahari wa Hormuz. 

Meli hiyo ilikamatwa kufuatia tuhuma  za kushindwa kuitikia wito wa dharura uliotolewa baharini. 

Hata hivyo kukamatwa kwa meli hiyo kulitizamwa kama ni kulipiza kisasi baada ya maafisa wa Uingereza kuikamata meli ya Iran mapema mwezi Julai kwa tuhuma za kusafirisha mafuta kupeleka Syria.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images