Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Madereva Bajaji Wafunga Barabara Morogoro....Jeshi la Polisi Lawatuliza

$
0
0
Baadhi ya madereva wa bajaji mjini Morogoro wamelazimika kufunga barabara kufuatia kamatakamata ya polisi iliyofanyika katika mji huo mapema leo.

Madereva hao wamesema wamefikia hatua hiyo baada ya askari polisi na askari wa akiba kuzingira katika maeneo mbalimbali ya katikati ya mji pamoja na kituo cha daladala na kuzikamata bajaji zao.

Hatua hiyo ikakilazimu kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro kikiongozwa na Kamanda Michael Daleli kuingilia kati na kufanikiwa kutuliza ghasia pamoja na kuondoa msongamano uliosababisha shughuli mbalimbali kusimama.

"Barabara iligeuzwa kuwa kituo cha maegesho ya bodaboda na bajaji, sasa tunazifungua na nyinyi ni mashahidi hata misafara iliyokuwa inapita eneo hili ilikuwa inazunguka mbali sana kuelekea pale Ikulu ndogo", amesema Kamanda Daleli.

Naye Mratibu wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini TARURA, Mhandisi Godwin Mpinzile amesema kuwa madereva hao walipewa sehemu za kwenda kuegesha magari yao lakini wamekuwa wakikaidi na ndiyo maana zoezi hilo limefanyika.

Tundu Lissu Abadili Tarehe ya Kurudi Nchini

$
0
0
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema hatarejea Tanzania Septemba 7, 2019 kama ilivyopangwa badala yake atasubiri ruhusa ya madaktari wanaomtibu.

Lissu ametoa kauli hiyo jana Jumanne Septemba 3, 2019 katika mahojiano na Shirika la Utangazaji Uingereza (BBC), alipoulizwa lini atarejea Tanzania.

Amesema  bado madaktari hawajaweka bayana kwamba atarudi lini.

"Nilisema mwanzoni nitarudi tarehe 7 Septemba, 2019 lakini daktari wangu ameniambia ataniona tarehe 1 Oktoba, 2019 na mara ya mwisho ataniona mara ya mwisho tarehe 8 Oktoba, 2019, kwa hiyo ile ratiba ya mwanzo haitawezekana, kwa sababu daktari wangu anataka kuniona." amesema Tundu Lissu

Lissu, amekuwa nje ya nchi tangu Septemba 7, 2017 aliposhambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana akiwa eneo la makazi yake Area D, Dodoma akitoka kuhudhuria vikao vya Bunge.

Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Gazi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume ,Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30 na kukusaidia kurudia   tendo la ndoa .

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara hata kama yupo mbali.

Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Wasiliana na mtaalam kwa; 0747100745

Tupo Mbagala

Wanawake 15 Waingia Ndani Ya 18 Ya Rpc Muroto Kwa Kufanya Ukahaba.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
JESHI la Polisi mkoani Dodoma limewakamata na kuwafikisha mahakamani makahaba 15 ambapo wamehukumiwa kifungo cha miezi sita kila moja huku wanaume wanne waliosadikiwa kuwa ni wateja wao waliachiwa baada ya kukosekana kwa ushahidi.

 Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana, kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto alisema  katika msako wa Septemba 2, mwaka huu saa tatu kamili usiku mtaa wa Uhindini walikamatwa wanawake 15 wakifanya biashara ya ukahaba na kuhatarisha amnai na utulivu katika mtaa huo kinyume na kifungu 176 (a) (f) (g) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kilichofanyiwa marejeo 2002.

 Alisema washtakiwa walifikishwa mahakamani, walisomewa mashtaka na ushahidi dhidi yao ulitolewa na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani kila moja bila kulipa aini.

Alisema msako mwingine umefanyika wamekamatwa makahaba saba na watafikishwa mahakamani 

 AlisemaAlisema makahaba hao waliona fursa ya kuja kufanya matukio ya ngono kitendo ambacho hakikubaliki.

Sasa hivi wako gerezani Isanga wamepokelewa kwa ajili ya nguvu kazi, wataponda kokoto na kufanya kazi nyingine” alisema . Alisema  msako huo utakuwa endelevu. 
 
Makahaba waliohukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani wametakjwa kuwa ni  Suzana Onesmo (27), Mariam Omary (29), Maimuna Issa (38), Bhoke Chacha (30), Swaumu Bakari (26),  Rahma Abdi (28), Magreth Humphrey (27),  Wema Saidi (25),  Jeniffer Wilson (33), Lydia Kilale (30),  Manka Richard (21),  Mwasuma Hassan (26),  Angel Joseph (29), Zaina ramadhani (30) na Tatu Saidi (27). 

Katika tukio linguine kamanda  Muroto alisema zilikamatwa silaha mbili zikimilikiwa kinyume cha sharia.

 Alisema Agosti 18, mwaka huu katika mtaa wa mazengo kata ya Zuzu, alikamatwa Baraka mgomochi (24), mkazi wa Nkuhungu akiwa na silaha aina ya bastola muundo wa bereta yenye namba AR- 3648-1981 yenye usajili wa TZC 68344 ikiwa na magazine ambayo haina risasi.

 Alisema mtuhumiwa alifukia  silaha hiyo pembeni ya karo la choo na uchunguzi ulifanyika na kubaini silaha hiyo iliibiwa Kurasini Jijini Dar es salaam baada ya watuhumiwa kuvunja nyumba na kuiba.

Katika tukio linguine alisema lilitokea Ilangali, wilaya ya chamwino mkoani hapa, Jeshi la polisikwa kushirikiana na askari wa wanyamapori kutoka mkoa wa Iringa alikamatwa John Gabriel (53) akiwa na silaha aina ya Gobole yenyemba DA 827-08 akiwa anaimiliki kinyume cha sharia na akiitumia kinyume cha sharia kwa uwindaji haramu wa wanyamapori.

Alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.

 Alisema katika msako dhidi ya wavunjaji, wezi, wanaohifadhi mali za wizi, wamekamatwa watuhumiwa wane kwa makosa hayo

 Alisema katika eneo la mailimbili alikamatwa Juma Ally (22),  Joseph Mapunda (28) mkazi wa Sawswa wakiwa na spika tatu kubwa na stendi ya mixer moja mali ambazo ni za wizi.

 Katika eneo la kizota alikamatwa Almando David (19), mkazi wa kizita akiwa na jumla ya televisheni nne aina ya Philips, nchi 30, Tv aina ya Aborder inchi 32, Sony nchi 18 na LG nchi 21 akihifadhi huku akijua ni mali za wizi.

Alisema katika eneo la Ntyuka alikamatwa Allen Jonathan (28) fundi ujenzi akiwa na mabati matano ambayo ni mali ya wizi.

 Pia alisema katika eneo la Changombe na maili mbili walikamatwa watuhumiwa 69 waliokuwa wakitafutwa kwa makosa mbalimbali, pia zimekamatwa bajaji mbili, pikipiki 22, laptop kompyuta mbili na kisu kimoja.

 Alisema watuhumiwa watafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.

Serikali Yasema Itapitia Upya Mfumo Mzima Wa Usambazaji Wa Pembejeo Za Kilimo.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
WIZARA ya Kilimo imesema inapitia mfumo mzima wa usambazaji pembejeo za mazao ili kuondokana na ucheleweshaji na wizi unaoendelea ambao mwisho wa siku unasababisha mkulima kubeba mzigo huo.
 
Naibu Waziri wa wa wizara hiyo HUSSEIN BASHE amesema hayo akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Bunda BONIFAFE GETERE aliyetaka kujua kama wakulima wa pamba katika msimu 2019/2020 watakatwa fedha ya pembejeo. 

Akijibu swali hilo BASHE amesema katika msimu huu wa kilimo mambo mengi yatabadilika katika usambazaji wa pembejeo.
 
Katika swali la msingi  Mbunge wa Ukerewe JOSEPH MKUNDI amehoji mkakati wa serikali wa kufanya utafiti wa kisayansi ili kushauri wananchi wa Ukerewe aina ya mazao yanayopaswa kulimwa na jinsi ya kutumia eneo dogo la ardhi kwa ufanisi.
 
Akijibu swali hilo BASHE amesema Mkakati wa serikali kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania{TARI} ni kufanya utafiti wa tabaka na afya ya udongo katika kanda zote saba za kiikolojia za kilimo nchini ikiwemo kanda ya Mwanza.

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo,Pamoja Na Magonjwa Sugu

$
0
0
SUPER MORISIS; nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-85)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wala kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 18-45

SUNUPER;   Hurefusha na kunenepesha maumbire madogo ya uume uliosinyaa ,  matatizo haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguruma na kujaa gesi hatimae kinyesi kuwa km cha mbuzi, ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia nidawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

ONDOA MATATIZOYAKO YOTE  ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,  kurudisha mali iliyopotea au kuibiwa 

Kwahuduma na msaada wasiliana na DR. GALIMBO  call 0759 208 637

watsap  0620510598

Waitara: Wakuu wa Mikoa na Wilaya Hawana Mamlaka Kusimania Uchaguzi.

$
0
0
 Na  .Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), MWITA WAITARA amesema Kanuni za  uchaguzi wa Serikali za Mitaa za Mwaka 2019 hazijampa mamlaka yeyote Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa wilaya kuwa msimamizi wa uchaguzi.
 
WAITARA ameeleza hayo septemba 5 bungeni jijini hapa wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kibamba JOHN MNYIKA aliyehoji sababu ya wakuu wa mikoa na wilaya kupewa mamlaka kwenye usimamizi wa uchaguzi wakati ni makada wa Chama cha Mapinduzi huku akionyesha hofu kuwa uchaguzi huo hautakuwa huru na haki.
 
Akijibu swali hilo WAITARA amesema uchaguzi huo unasimamiwa na waziri mwenye dhamana na utakuwa huru na wa haki hivyo hawana sababu ya kuwa na hofu.
 
Uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 unatarajiwa kufanyika novemba 24 huku msisitizo kwa sasa ikiwa ni elimu ya mpiga kwa wananchi.

Katika hatua nyingine Serikali imesema mpango wa kunusuru kaya maskini umejipanga kuhakikisha malalamiko yaliyokuwepo ya upendeleo,ubaguzi na kuachwa  kwa watu maskini kuandikishwa kwenye mpango huo hayajirudii na mifumo ya kielektroniki itatumika. 

Hayo yameelezwa leo bungeni jijini Dodoma na naibu waziri ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora MERRY MWANJELWA wakati akijibu swali la mbunge wa Tunduru Kaskazini mhandisi RAMO MAKANI. 

MWANJELWA amesema changamoto kubwa ambayo mpango huo umekuwa ukikumbana nao ni kilio kutoka kwa baadhi ya wananchi maskini ambao hawajafikiwa na huduma za mpango huo kwenye vijiji,mitaa na shehia takribani 5,693. 

MWANJELWA amesisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa viongozi na watumishi katika ngazi zote ambao katika maeneo yao watabainika kuwepo watu au kaya zisizo na vigezo kwenye awamu ya pili ya mpango huo.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) Yatangaza bei Mpya za Petrol na Dizeli....Soma Hapa

$
0
0
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) nchini Tanzania imetangaza bei za kikomo kwa bidhaa za mafuta nchini humo zitakazoanza kutumika kuanzia leo Jumatano Septemba 4,2019.

Taarifa iliyotolewa  Jumanne Septemba 3,2019 kwa vyombo vya habari na mkuu wa kitengo wa mawasiliano na uhusiano kwa umma wa Ewura, Wilfred Mwakalosi amesema bei za jumla na rejareja za mafuta za petroli dizeli na mafuta ya taa zimeongezeka.

Mwakalosi amesema mafuta hayo ni yale yaliyoingia kupitia bandari ya Dar es Salaam ambayo yameongezeka ukilinganisha na mwezi uliopita.

“Mwezi huu (Septemba) bei za rejareja za petroli, dizeli na mafuta ya taa zimeongezeka kwa Sh83 kwa lita (sawa na asilimia 3.87), Sh61 kwa lita (sawa na asilimia 2.90), Sh46 kwa lita (sawa na asilimia 2.22),” amesema

Amesema bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli, dizeli na yanayoingizwa kupitia bandari ya Tanga yameongezeka ikilinganishwa na toleo la mwezi uliopita.

“Kwa mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara mwezi huu bei zimeongezeka kwa Sh108 kwa lita sawa na asilimia 4.95 na  Sh72 (sawa na asilimia 3,36),” amesema Mwakalosi.
 
Katika taarifa hiyo, Mwakalosi amesisitiza bei ya mafuta ya taa kwa mikoa ya kaskazini zitaendelea kutumika zile zilizochapishwa mwezi uliopita kwa sababu hakuna shehena ya bidhaa hiyo iliyoingia kupitia bandari ya Tanga.

Kutana na Mohamedi Buruhani Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH .....Anauwezo wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mohamedi Buruhani Mtabibu wa Nyota za Binadamu  Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Mohamed Buruani Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. 

Anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO . Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie ..Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Mohamed Buruhan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN, Anatafsiri Ndoto. ,KUSAFISHA NYOTA, Mvuto wa Mwili na BIASHARA, ...MIGUU Kufa GANZI na mengi zaidi (+255  715971688 au (+255  756914036

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Rais Magufuli Kumpokea Rais Wa Jamhuri Ya Uganda Mhe. Yoel Kaguta Museven

$
0
0
Nchi yetu imepata heshima ya kupokea ugeni wa Mhe. Yoel Kaguta Museven Rais wa Uganda ambaye anatarajiwa kufika hapa nchini siku ya Alhamisi ya tarehe 05/09/2019 kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia tarehe 05/09/2019 hadi 07/09/2019.
 
Mhe. Yoel Kaguta Mseven atapokelewa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport Terminal I na mwenyeji wake hapa nchini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli muda wa saa 12.00 jioni.
 
Mhe. Rais Museveni anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Kongamano baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda. Aidha, Mhe. Rais Museveni anatarajia kuzindua rasmi jengo jipya la Mfuko wa Mwalimu Julius Nyerere lililopo katika Barabara ya Sokoine/Morogoro Dar es Salaam tarehe 6 Septemba, 2019.

Mgeni wetu anatarajiwa kuondoka hapa nchini tarehe 07/09/2019 na atasindikizwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Tunaomba radhi kwamba njia atakazopitia mgeni wetu zitakuwa zinafungwa kwa muda ili kupitisha misafara ya viongozi wetu wakuu watakaoelekea Uwanja wa Ndege wa Mwl. J. K. Nyerere kumpokea Mgeni wetu hususani barabara ya Nyerere mpaka Mgeni wetu atakapokuwa amewasili na siku ya kuondoka.

Kwa kutambua ugeni huu sisi kama wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwa niaba ya wananchi wote wa Tanzania tunamkaribisha mgeni wetu na ajisikie kuwa yuko nyumbani muda wote atakapokuwa hapa jijini.
 
Asanteni sana.
*IMEANDALIWA NA OFISI YA MKUU WA MKOA
DAR ES SALAAM

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa September 6

BREAKING: Rais Mstaafu wa Zimbabwe Robert Mugabe Afariki Dunia

$
0
0
Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe amefariki dunia.

Mugabe alikuwa nchini Singapore akipokea matibabu kwa muda mrefu. Ameiongoza Zimbabwe kutoka 1980 mpaka 2017, alipong'olewa madarakani na  jeshi.

Vijana 60 Kati Ya 100 Wawasili Nchini Israel, Waziri Wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga Awafunda Kuhusu Nidhamu Na Kujituma

$
0
0
Na Mathias Canal, Jerusalem-Israel
Kundi la vijana wa kitanzania 60 limewasili nchini Israel kwa ajili ya kushiriki mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies katika kipindi cha mwaka mmojahuku wengine 40 wakitarajiwa kuwasili tarehe 11 Septemba 2019 kukamilisha idadi ya vijana 100.

Vijana hao wamewasili tarehe 5 Septemba 2019 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ben Gurion Jijini Tel Aviv nchini Israel na kupokelewa na Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb).

Waziri Hasunga amewataka vijana hao kutumia mafunzo hayo kama muarobaini wa kuendeleza sekta ya Kilimo watakaporejea nchini Tanzania hivyo kuwa chachu ya maendeleo yanayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.

“Ninyi mmekuja Israel mkiwa katika mtazamo wa kujifunza hivyo mambo mengine yote wekeni pembeni mzingatie masomo na katika kipindi cha mwaka mmoja mhakikishe mmetumia muda wenu wa masomo vizuri kujifunza, kupata maarifa na ujuzi ili mtakaporejea nyumbani mlete mabadiliko makubwa kwenye kilimo” Alikaririwa Mhe Hasunga

Mhe Hasunga amewataka vijana hao kuwa waaminifu wakati wote wa masomo yao kwani wanaiwakilisha Tanzania hivyo vitendo vyovyote vya utovu wa nidhamu itakuwa ni sehemu ya kulizalilisha Tanzania.

Alisema kuwa vijana hao wanapaswa kuwa na bidii na kuweka pembeni tabia zisizofaa kwani kuwa na maadili mema itawarahisishia vijana hao kupata utaalamu jadidu ambao utakuwa na manufaa makubwa kwao na Taifa kwa ujumla wake.

“Tunataka mabilionea wanaoibuka Tanzania watokane na sekta ya kilimo hususani vijana ambao mmepata fursa ya masomo nchini Israel, Rais Magufuli alishatangaza kuwa wakati wa utawala wake lazima mabilionea wapatikane” Alisema

Aliongeza kuwa ni matarajio ya serikali kuona vijana hao watakaporejea Tanzania wanaanzisha viwanda mbalimbali kwani malighafi nyingi zinatokana na sekta ya kilimo.

Mhe Hasunga amewataka vijana hao kutojihusisha na siasa kwani hivi sasa ni kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Israel. “Acheni kabisa kujiingiza kwenye siasa maana siasa za huku haziwahusu, waacheni waendelee na mambo yao nanyi endeleeni na kilichowaleta” Alisisitiza Mhe Hasunga

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Israel Balozi Job Daud Masima amewataka vijana hao kutekeleza maelekezo waliyopatiwa na Waziri wa Kilimo.

“Chochote mtakachofanya ni Mtanzania amefanya kwahiyo mkifanya mabaya mtasambaza sifa mbaya ya nchi katika Mataifa mengine jambo ambalo halitakiwi”

Balozi Masima hakusita kuwapongeza vijana 45 ambao wamerejea nyumbani Tanzania baada ya kuhitimu masomo yao kwani wameacha alama kubwa na nzuri inayoitangaza Tanzania.

Wakizungumza kwa niaba ya vijana waliowasili nchini Israel kwa ajili ya mafunzo hayo ya Kilimo ya Agrostudie, Janeth Patrick na Simion Jalusi wamemuhakikishia Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga kuwa wataiwakilisha vyema Tanzania ili liweze kufanikiwa kufika kwenye Taifa la Viwanda.

“Tutajifunza kwa bidii kubwa ili elimu tutakayoipata tuweze kuitumia vizuri kwa ajili ya kuboresha sekta ya Kilimo nchini Tanzania” Walikaririwa wakisema

Vilevile, Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Israel Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen na kukubaliana kwa kauli moja serikali za nchi hizo mbili kuingia makubaliano ya kuendeleza kilimo hususani katika utafiti, Tija katika uzalishaji, na Teknolojia.

MWISHO

Rais Magufuli Aomboleza Kifo cha Robert Mugabe

$
0
0
Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. John Pombe Magufuli ameeleza kusikitishwa kwake na kifo cha Rais Mstaafu wa Zimbabwe, Robert Mugabe ambaye ameaga dunia nchini Singapore alikokuwa akipatiwa matibabu.

Magufuli kupitia akaunti yake ya Twitter amemwelezea Mugabe kuwa alikuwa kiongozi shupavu, jasiri ambaye aliupinga na kuukataa ukoloni kwa vitendo.

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais Mstaafu na Baba wa Taifa la Zimbabwe Mzee Robert Mugabe. 

"Afrika imepoteza mmoja wa viongozi Jasiri, Shupavu, Mwanamajumui wa  Afrika na aliyekataa ukoloni kwa vitendo. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina."

Dawa Lishe Ya Asili Ya Kunenepesha Na Kuongeza Mwili.

$
0
0
Je umekonda  na  kudhoofu  mwili  kutokana  na  sababu  mbalimbali  kama  vile msongo  wa  mawazo  na  kuugua  maradhi  mbalimbali kama  vile  kisukari nakadhalika ?

Unahitaji  kurejesha  mwili  wako  katika  hali  yake  ya  kawaida ?  Unahitaji kuongeza mwili na uzito wako ?

Kama  jibu  lako  ni  NDIO  basi  HII  NI  HABARI NJEMA  SANA  KWAKO.

Neema  Herbalist  ni  duka  la  kuuza  dawa  mbalimbali  za  asili.  Tunayo   DAWA  LISHE  YA  ASILI  ambayo inanenepa  mwili  kwa watu  walio  dhoofu  na  kukonda  kwa  sababu  mbalimbali.

Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM  jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

Kwa  wateja  wetu  wa  jijini  DAR  ES  SALAAM  ambao  hawana  nafasi  ya  kufika  ofisini  kwetu  tunayo  huduma  ya  HOME & OFFICE  DELIVERY

Na  kwa  wateja  wetu  waliopo  nje  ya  mkoa  wa  DAR ES  SALAAM  tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  mbalimbali  kama  vile  MABUS  au  BOTI kwa  wateja  wetu wa  ZANZIBAR.

Wasiliana  nasi  kwa  SIMU NAMBA : 0693  005 189



Kambi Ya Kitaaluma Kwa Wanafunzi Wa Kidato Cha Nne Wenye Ufaulu Hafifu Yazinduliwa Simiyu

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amezindua rasmi kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata ufaulu hafifu (daraja sifuri) katika mtihani wa ‘Mock’, lengo likiwa ni kuwasaidia waweze kuongeza ufaulu wao katika mtihani wa Taifa utakaofanyika mwezi Novemba 2019.

Akizindua kambi hiyo Septemba 05, 2019 Mtaka amesema wanafunzi hao watafundishwa masomo manne tu ambayo ni Kiswahili, Kiingereza ,Uraia(Civics) na Historia, hivyo akatoa wito kwa walimu mahiri waliochaguliwa kuwafundisha wanafunzi hao kwa moyo na upendo ili wanafunzi hao waweze kupata alama D na kuendelea katika mtihani wa Taifa.

“Hawa watoto wafundisheni masomo manne, Kiswahili, Kiingereza, Historia na Civics; wafundisheni kwa moyo, wapeni mazoezi ya mara kwa mara katika siku hizi 60 watakazokuwa kambini, muwasaidie watoke kwenye F wapate angalau D nao wapate vyeti, kwa sababu hata ajira siku hizi kigezo ni angalau mtu awe na cheti cha kidato cha nne” alisema Mtaka.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa jamii ya Simiyu kuendelea kuwekeza kwenye elimu ili kuuwezesha mkoa kushindana kiuchumi kwa kuwa maendeleo ya kiuchumi yanategemea maendeleo ya elimu katika eneo husika.

Afisa Elimu mkoa wa Simiyu, Mwl.Ernest Hinju amesema kati ya Wanafunzi 9956 waliofanya mtihani wa  Utimilifu (Mock), 1300 hawakupata alama D hata moja, hivyo waliopata matokeo hafifu (daraja sifuri) wamewekwa pamoja wafundishwe masomo manne ili waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa, huku waliopata daraja la kwanza hadi la nne wakiendelea na kambi kufundishwa masomo yote.

Aidha, Hinju ameongeza kuwa  kambi za kitaaluma zimechangia kuongeza ufaulu kwenye Mtihani ya Taifa wa darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita, ambapo katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ufaulu ulikuwa asilimia 74 mkoa ukiwa nafasi ya 14 kati ya mikoa 26, mwaka  2017 ufaulu asilimia 79.8 nafasi ya 11 na mwaka 2018 ufaulu asilimia 82.5  ukashika nafasi ya 9 kati ya mikoa 26.

Kwa upande wao wanafunzi wa kidato cha nne waliopo kambini  wameshukuru kuwekewa kambi hiyo na wakaeleza imani yao juu ya uwepo wa kambi hiyo ambapo wameomba kambi za kitaaluma Simiyu ziwe endelevu ili ziwasaidie kujifunza na kujiandaa vema na mitihani ya Taifa hatimaye mkoa uweze kufanya vizuri.

“Tunawashukuru viongozi wetu na wazazi wetu kwa kukubali kutuwekea kambi ya kitaaluma, ninashauri kambi hizi zisiishie kwetu ziendelee na kwa wadogo zetu ili mkoa wetu uweze kuongeza ufaulu” alisema Esther Nashoni mwanafunzi shule ya sekondari Bariadi(Bariadi)

Mkuu wa Shule ya Sekondari Simiyu, Mwl.Paul Susu amesema walimu wamejiandaa vema katika kuwafundisha wanafunzi na kuwapa mitihani ya mara kwa mara ili waweze kufanya vizuri, huku akitoa wito kwa wadau mbalimbali wa elimu kujitolea katika ujenzi wa miundombinu ya elimu ili kuwe na miundombinu ya kutosha itakayoongeza nafasi kwa kambi za kitaaluma kufanyika  vizuri.

Kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha nne iliyozinduliwa Septemba 05, 2019 ilianza rasmi Septemba Mosi na inatarajiwa kufanyika ndani ya siku 60 kabla ya kufanya Mtihani wa Taifa mwezi Novemba.

MWISHO

LIVE: Rais Magufuli na Rais Museveni Wakifungua Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda

$
0
0
LIVE: Rais Magufuli na Rais Museveni  Wakifungua Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda

Mabadiliko ya sheria yatoa nguvu zaidi kwa DPP....Wanaokiri makosa kupunguziwa adhabu

$
0
0
Serikali  imewasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2019 kwa lengo la kurekebisha sheria 11.

Sheria zinazopendekezwa kufumuliwa ni pamoja na Sheria ya Mapato Yatokanayo na Uhalifu, Sura ya 256 kwa lengo la kuipa mahakama uwezo wa kutaifisha mali tofauti na iliyopatikana kwa uhalifu endapo itagundulika upatikanaji wake si halali, kufichwa au kutoroshwa nje ya nchi.

Katika marekebisho hayo, pia inapendekezwa uwapo wa kifungu kipya cha 14B kitakachoipa mahakama uwezo wa kuzuia uhamisho wowote wa mali ambao umefanyika kwa lengo la kukwepesha mali kutaifishwa.

Akiwasilisha bungeni jijini Dodoma jana muswada huo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus Kilangi, alisema marekebisho hayo yanalenga wahalifu kutonufaika na mali zozote zitokanazo na makosa ya rushwa, usafirishaji dawa za kulevya, utakatishaji fedha na makosa mengine yanayohusiana.

Alisema kabla ya maombi ya kutaifisha hayajafanywa au ndani ya miaka mitano kuanzia siku ya mwisho ya tukio kutokea, mali hiyo itahesabiwa ni zao la uhalifu.

Prof. Kilangi alisema mapendekezo katika kifungu cha 38 yanalenga kumwezesha Mkurugenzi wa Mashtaka kuwasilisha mahakamani maombi ya upande mmoja ya kuzuia mali pale ambapo mhusika anachunguzwa au hawezi kufika mahakamani au alishahukumiwa kwa kosa linalohusiana na mali iliyotaifishwa.

"Kifungu cha 56 kinapendekezwa kufutwa kwa lengo la kuondoa mahitaji yasiyo ya lazima dhidi ya serikali ya kulipa gharama za madhara yanayotokana na amri ya zuio iliyowekwa," Prof. Kilangi alisema.
 
Katika muswada huo, serikali inapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Sura ya 268 ili kuwazuia maofisa sheria au mawakili wa serikali na wanasheria walioko kwenye utumishi wa umma, kufanya kazi za uwakili wa kujitegemea isipokuwa kushuhudia viapo na uhakiki wa nyaraka.

"Mawakili wa serikali wanaweza tu kufanyakazi za uwakili wa kujitegemea kwa kibali maalum cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa sababu maalum.

"Wanasheria wanaokusudiwa ni wanasheria wote katika utumishi wa umma ambao wanaongozwa na Kanuni za Maadili ya Wanasheria katika Utumishi wa Umma," alisema.

Katika muswada huo, serikali inapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Usajili wa Vizazi na Vifo, Sura ya 108, kwa lengo la kupanua wigo wa mfumo wa usajili wa vizazi na vifo vikijumuisha vifo vinavyotokea nje ya nchi.

Prof. Kilangi alisema marekebisho hayo pia yanalenga kuwatambua watendaji wa kata na vijiji kama wasajili wasaidizi baada ya kukasimiwa mamlaka hayo na Msajili Mkuu.

Alisema muswada huo pia unalenga kufanya marekebisho katika Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, Sura ya 20, ili kuwe na makubaliano kati ya Mwendesha Mashtaka na mtuhumiwa au wakili wake, kupunguza uzito wa adhabu pale ambapo mtuhumiwa atakiri kosa analoshitakiwa nalo.

Alisema utaratibu huo utasaidia kupunguza mlundikano wa kesi mahakamani na kupunguza msongomano wa wafungwa magerezani.

Prof. Kilangi pia alisema serikali inapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Urejeshaji Wahalifu, Sura ya 368, kwa lengo la kuboresha utaratibu wa kisheria wa ushirikiano wa kimataifa katika kusaidiana kurejesha watuhumiwa katika kesi za jinai.

Alisema muswada huo pia unalenga kufanya marekebisho katika Sheria ya Mahakama za Mahakimu, Sura ya 11, kwa lengo la kuongeza kiwango cha thamani ya kifedha katika mashauri ya madai yanayosikilizwa katika mahakama hizo kutoka Sh. milioni 50 cha sasa hadi Sh. milioni 100.

Kilangi pia alisema muswada huo unalenga kufanya marekebisho katika Sheria ya Chama cha Msalaba Mwekundu Tanganyika, Sura ya 66, ili itumike pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kupanua wigo wa majukumu ya chama hicho kwa mujibu wa viwango vya kimataifa.

DC Kanali Denice Mwila Aongoza Maelefu Ya Watu Wilayani Misenyi Kuaga Mwili Wa Mmoja Wa Mapacha Aliyefariki Dunia Katika Hospitali Ya Taifa Muhimbili .

$
0
0
Na Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera.
Hatimaye mazishi ya mmoja wa mapacha ANISIA BERNATUS aliyefariki katika hospitali ya taifa muhimbili siku chache baada ya kurejea nchini wakitokea saud Arabia kufanyiwa upasuaji wa kutenganishwa yamefanyika kijijini mabale kata ya mabale wilayani missenyi huku vyombo vya habari vikipongezwa kwa kuibua jambo hilo na kupelekea mapacha hao kupatiwa msaada.

Akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya serikali,mkuu wa wilaya ya missenyi kanali DENICE MWILA amesema kuwa vyombo vya habari hususani redio za kijamii zilizofika omkajunguti na kuripoti tukio la mapacha hao kuzaliwa,vilisaidia kuuhabarisha umma na kupelekea kupatikana misaada mbali mbali kutoka kwa wahisani na wasamaria wema.

Hata hivyo kanali MWILA ametoa pongezi kwa ubalozi wa Tanzania nchini Saud Arabia pamoja na serikali nchini humo kwa kugharamia safari na upasuaji wa mapacha hao pamoja na hospitali zote zilizoshiriki kuwasaidia.
 
Kwa upande wake daktari bingwa wa upasuaji wa watoto kutoka hospitali ya taifa muhimbili dokta ZAITUN BOKHARY amesema kuwa safari pamoja na upasuaji wa mapacha hao umegharimu jumla ya dola za kimarekani elfu 5 za kimarekani zilizotolewa na serikali ya Saud Arabia.
 
Hata hivyo ameeleza kuwa tatizo lililopelekea pacha ANISIA kupoteza maisha ni kuwa alianza kutapika wakiwa kwenye ndege kutoka Saud Arabia kuja nchini na walipofika nchini walimpeleka moja kwa moja katika hospitali ya taifa muhimbili ambapo alipoteza maisha akiwa katika chumba cha uangalizi maalum.

Mgogoro Kati Ya Wafugaji Na Wakaulima Kijiji Kashanda Wilayani Karagwe Sasa Kupatiwa Mwarobaini Wake

$
0
0
Na Avitus  Benedicto Kyaruzi, Kagera;
Mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu zaidi ya miaka kumi na kusababisha uvunjifu wa amani kati ya pande mbili za wananchi ambao ni  wakulima na wafugaji katika Kijiji cha Kashanda Kata Bugene Wilayani Karagwe sasa utapatiwa ufumbuzi wa kudumu mara baada ya Mkuu wa Mkoa kuingilia kati ili kurejesha amani ya kudumu katika eneo hilo.
 
Baada ya kuwa anapokea malalamiko mengi kwa muda mrefu kuhusu Kijiji Kashanda Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti aliamua kufika eneo la kijiji hicho cha Kashanda Septemba 4, 2019 pamoja na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama ili kujionea mwenyewe jinsi mgogoro ulivyo  ili uweze kuutolewa maamuzi sahihi.
 
Mhe. Gaguti alipofika katika eneo hilo la Kashanda alikuta ni eneo ambalo halina wananchi ambao wanaishi kama kijiji bali aliwakuta baadhi ya vijana kutoka Wilayani Ngara wakiwa wanafyeka miti na vichaka wakiendelea kulima katika maeneo mbalimbali wakidai kuwa nao wameajiriwa kulima na wamiliki wa maeneo hayo.
 
Aidha, Mkuu wa Mkoa Gaguti hakukuta mifugo ya aina yoyote ile katika eneo hilo bali baadhi ya wakulima ambao walikuwa wamefyeka miti na vichaka ndani ya eneo hilo wakiendelea kulima kwa ajili ya msimu wa kupanda maharage na mahindi na mazao mengiyo.
 
Kwa maelezo kutoka katika uongozi wa Wilaya ya Karagwe wakiuelezea mgogoro huo walimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa baada ya kutokea uvunjifu  wa amani mara kwa mara wakulima wakijihami na siraha za jadi kama mapanga, mikuki na upinde na wakiwashambulia wafugaji, wafugaji waliamua kuondoa mifugo yao katika eneo hilo ambalo walitengewa kwa kwaajili ya kulishia mifugo yao hasa ng’ombe.
 
Mkuu wa Mkoa Gaguti baada ya kutembelea eneo la kijiji hicho cha Kashanda na kuona hali halisi alisema kuwa amelielewa eneo lenyewe la mgogoro, pili ndani ya muda mfupi sana ataitisha kikao cha pamoja uongozi wa kijiji hicho cha Kashanda, uongozi wa Wilaya ya Karagwe pamoja na wataalam wote wa ardhi wanaohusika na atatoa maamuzi yenye maslahi mapana ya wananchi, Wilaya na Taifa kwa ujumla.
 
Kijiji cha Kashanda kipo Kata Nyakahanga Tarafa Bugene Wilayani Karagwe na kina hekta za mraba 3,370.319 na kiliandikishwa kwa hati namba KAG/KIJ 507 chini ya kifungu namba 22 cha sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) ya mwaka 1982 na hati hiyo ilitolewa tarehe 23 Mei, 1989.
 
Pamoja na kijiji cha Kashanda kuandiskishwa na kusajiliwa na Serikali hakikutajwa kama kijiji cha wafugaji bali kinatajwa kama vijiji vinginevyo vilivyosajiliwa na Serikali. Aidha, kwa maelezo ya wananchi wa eneo hilo pamoja na Wilaya ni kwamba kijiji Kashanda kilianzishwa kwa kumega maeneo ya vijiji vya Bishehe, Omulusimbi, Chonyonyo na Chabalisa ili wafugaji wapate sehemu ya kulishia mifugo yao lakini baadae eneo hilo lilianza kuvamiwa na wakulima.
 
Kutokana na mgogogo huo kusababisa uvunjifu wa amani wa mara kwa mara kati ya wafugaji na wakulima wanaolivamia eneo hilo Mkuu wa Mkoa Gaguti amesema kuwa sasa basi lazima mgogoro huo ufike mwisho na ijulikane wazi ni shughuli zipi zinatakiwa kuendelea kufanyika katika eneo hilo ufugaji au kilimo. 

“Nataka Mkoa wa Kagera migogoro ya ardhi ikomeshwe kabisha na uwe mkoa wa mfano.” Alimaliza kwa kusisitiza Mhe. Gaguti
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images