Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali Kusomesha Madaktari Bingwa 365 kwa Ajili ya Kusambazwa Maeneo yenye Uhaba

$
0
0
Na Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.  
Jumla ya madaktari bingwa 365 wanatarajia kuhitimu mafunzo kuanzia mwaka wa wasomo 2019/2020, 2020/2021  na 2021/2022 ambao watasambazwa kwenye hospitali mbalimbali nchini kulingana na uwiano wa wataalamu waliopo pamoja na kuzingatia maeneo yenye uhaba mkubwa.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile amesema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Sonia Jumaa Magogo juu ya mkakati wa Serikali wa kuongeza Madaktari Bingwa nchini.

“Serikali inaendelea kuimarisha huduma za kibingwa katika ngazi mbalimbali za huduma nchini ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,” amesema Dkt. Ndugulile.

Ameendelea kusema kuwa katika mwaka 2017/2018, Wizara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, ilitenga kiasi cha shilingi bilioni 2 zilizotumika kwa ajili ya kusomesha madaktari bingwa 125 wa fani za kipaumbele katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) ambao wanatarajia kumaliza  2020/2021.

Aidha, katika mwaka 2018/2019, Serikali ilitenga kiasi cha Shilingi bilioni 1.8 ili kuendelea kugharamia mafunzo ngazi ya kibingwa katika kada mbalimbali za afya 127 katika Chuo cha MUHAS.

Dkt. Faustine amesema, katika mwaka 2019/2020, Wizara imetenga jumla ya shilingi 1,844,617,090 kwa ajili ya kugharamia mafunzo ya wataalamu bingwa katika fani za vipaumbele.

“Kutokana na uhaba uliopo kwenye hospitali za Rufaa za Mikoa, Wizara itahakikisha fedha hii inatumika vyema katika kusomesha wataalamu wanaotoka kwenye maeneo yenye uhaba mkubwa,” amesema Dkt. Ndugulile.

Aidha, wizara kupitia hospitali za rufaa ngazi ya Taifa na Taasisi za nje zitaendelea kuendesha kambi za udaktari bingwa hapa nchini, kwa lengo la kusogeza huduma za kibingwa na kujenga uwezo wa wataalamu.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi Septemba 5

Waziri Wa Kilimo Japhet Hasunga Afanya Mazungumzo Na Mtendaji Mkuu Wa Kampuni Ya Innovation Africa

$
0
0
Na Mathias Canal, Telaviv-Israel
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb)  tarehe 4 Septemba 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Innovation Africa Bi Sivan Ya’ari.

Katika kikao kazi hicho kilichofanyika katika Ofisi za kampuni hiyo zilizopo Jijini Tel Aviv nchini Israel, Mhe Hasunga amemualika Bi Sivan kutembelea nchini Tanzania ili kuwekeza kadhalika kusaidia katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

Alisema kuwa kampuni hiyo inatakiwa kuongeza mshikamano na serikali ya Tanzania ili kuendelea kutatua sehemu ya matatizo ya wananchi huku kuimarisha mpango wao wa kutoa suluhisho la Israeli na ujuzi kwa wale wanaohitaji kuishi katika vijiji vya Kiafrika.

Waziri Hasunga amemuhakikishia Bi Ya’ari kuwa Tanzania ni nchi nzuri katika uwkeezaji na sehemu salama ya kuishi huku serikali inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli ikiendeleza juhudi za kuboresha maisha ya watanzania na kuimarisha uchumi wa nchi.

Hata hivyo ameipongeza kampuni hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya katika nchi za Afrika katika sekta ya nishati ya jua ikiwa ni pamoja na mchango wao katika kutekeleza miradi ya maji safi, na Kusaidia vituo vya watoto yatima.

Alisema kuwa Tanzania ni sehemu salama na imara katika uwekezaji, kwani serikali imeanzisha kituo cha uwekezaji (TIC) ambacho ni Taasisi ya msingi ya serikali yenye jukumu la kuratibu, kuhimiza, kukuza na kuwezesha uwekezaji.

Tanzania inaongoza kwa uwekezaji katika Afrika Mashariki na imeweza kuvutia uwekezaji wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.18, ikifuatiwa na Uganda dola za Marekani bilioni 0.7 na Kenya dola za Marekani bilioni 0.67. “Kutokana na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali kuvutia uwekezaji nchini, hali ya uwekezaji imeimarika ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Ripoti mbalimbali za uwekezaji duniani zinaonesha kuwa Tanzania imeongoza kwa kuvutia uwekezaji miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki

Taarifa ya Uwekezaji ya Dunia (World Investment Report) ya mwaka 2018 inayotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) imebainisha kiasi hicho kikubwa cha uwekezaji huku Taarifa nyingine ya“The Africa Investment Index (AII) 2018” inaonesha kuwa Tanzania imeshika nafasi ya 13 kati ya nchi 54 za Afrika katika kutoa fursa za masoko na vivutio vya uwekezaji.”

Kwa upande wake Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Innovation Africa Bi Sivan Ya’ari akizungumza katika kikao kazi hicho ameridhia ombi la Waziri Hasunga la kuongeza uwezekano wa kuisaidia Tanzania na kusema kuwa mwanzoni mwa mwezi wa tisa atawasili nchini Tanzania kwa ajili ya kuainisha maeneo ya uwekezaji.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga yupo katika ziara ya kikazi ya siku sita nchini Israel ambapo atakutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Agro Studies ambapo miongoni mwa mazungumzo muhimu itakuwa ni pamoja na kumuomba uwezekano wa kuongezewa nafasi zaidi ili vijana wengi wa kitanzania waende kujifunza mbinu mpya za kilimo nchini Israel.

Pia, Mhe Hasunga atakutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo nchini Israel kujadiliana nae maeneo mbalimbali na fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya kilimo nchini Tanzania

MWISHO

Serikali Yagiza Kurudiwa Kwa Mchakato Wa Utoaji Vibali Biashara Ya Chuma Chakavu

$
0
0
Serikali imefuta vibali vyote vilivyokuwa vimetolewa kwa wafanyabiashara wa vyuma chakavu na biashara taka hatarishi kwa ujumla bila kufuata sheria na kuagiza mchakato wa utoaji vibali hivyo uanze upya ili kuhakikisha sheria ya mazingira inafuatwa.

Tamko hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene wakati wa Mkutano na wafanyabiashara wa vyuma chakavu uliofanyika jana Septemba 4, 2019 jijini Dar es Salaam.
 
Kutokana na hatua hiyo Mhe. Simbachawene amemugiza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais kuunda haraka timu ya wataalamu kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa vibali vyote pamoja na vyuma chakavu vilivyokusanywa.
 
Alifafanua kuwa vibali vingine vimekuwa changamoto lukuki zikiwemo kutojulikana ukaguzi wake au kutumika kwa zaidi ya biashara moja jambo ambalo limekuwa likiikosesha mapato Serikali.
 
"Serikali hii ya wanyonge haina nia ya kumkomoa mtu katika hili la chuma chakavu tunawajali sana na  ni biashara nzuri lakini ifikie kipindi tufuate utaratibu na kuwa na kibali maana tumebaini kuna dosari nyingi katika vibali vingi vilivyotolewa," alisema.
 
Aidha kwa upande mwingine Mhe. Simbachawene alitangaza kuwa Serikali imerekebisha tozo ya vyuma chakavu ya sh. milioni 10 iliyokuwa inalalamikiwa na wafanyabiashara hao hasa wadogo na kufikia sh. milioni 5 hadi sh. laki 5.
 
Mhe. Simbachawene abainisha kuwa tozo hizo ni takwa la kisheria na haliwezi kujadiliwa au kubadilishwa hadi sheria ipelekwe Bungeni kujadili hivyo haitawezekana kuiondoa na kuwa Ofisi hiyo inaendelea kusimamia.
 
Awali akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Samuel Gwamaka alisema kuwa lengo la hafua hiyo ni kurasimisha baishara ya chuma chakavu na kuwatofautisha wafanyabiashara wadogo na wakubwa ili kuwatengenezea mazingira mazuri.
 
Dkt. Gwamaka alifafanua alibainisha kuwa mfanyabiashara anapowasilisha ombi lake NEMC wanakagua na kuwasilisha Ofisi ya Makamu wa Rais ambayo ikijiridhishe inaliwasilisha kwa Waziri wa Nchi ambaye nae akianatoa kibali ndani ya siku 14.
 
"Hapo nyuma NEMC haikuhusika sana na masuala ya chuma chakavu lakini Waziri alitoa maelekezo na Baraza kuanza kusimamia utekelezaji wake wa kanuni za taka hatarishi na chuma chakavu

Serikali ya Tanzania yalaani Vurugu za Afrika Kusini dhidi ya Wageni

$
0
0
 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Serikali ya Tanzania inaungana na Serikali ya Afrika Kusini kulaani vikali vitendo vya ubaguzi na mashambulizi vinavyofanywa na raia wachache wa nchi hiyo dhidi ya raia wa nchi zingine za Afrika na kuziasa nchi zingine kutolipa kisasi kutokana na vitendo hivyo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wanafunzi 100 kutoka Tanzania wanaokwenda Israel kushiriki mafunzo ya kilimo iliyofanyika  jana tarehe 4 Septemba 2019 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mhe. Prof. Kabudi amesema kuwa, vitendo vinavyofanywa na raia wachache wa Afrika Kusini vya kuwashambulia raia kutoka nchi zingine za Afrika na kuharibu mali zao vinasikitisha na kuivunjia heshima nchi hiyo. Hata hivyo, alisema kuwa Serikali ya Tanzania inaunga mkono kauli ya Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Cyril Ramaphosa aliyoitoa hivi karibuni ya kukemea na kulaani vikali vitendo vinavyofanywa na raia hao wachache.

Aidha, ameongeza kuwa, vitendo hivyo  ambavyo vinatokana na raia hao wengi kukosa ajira, ardhi na pia kutopenda kujishughulisha havihalalishi watu wengine wakiwemo watanzania kulipa kisasi kwa namna yoyote ile.

“Ni jambo la kusikitisha lakini Serikali ya Afrika Kusini inalisimamia kikamilifu na sisi tupo tayari kushirikiana nao ili kulitafutia ufumbuzi wa kudumu.Nawasihi Watanzania wenzangu tusilipize kisasi na tutaendelea kuwalinda raia wa Afrika Kusini waliopo Tanzania kwani tunaamini kuwa Afrika ni moja na waafrika ni ndugu zetu” alisema Prof. Kabudi.

Kadhalika, Prof. Kabudi alieleza kuwa hadi sasa hakuna taarifa kuhusu Mtanzania kuuawa, kujeruhiwa au kuharibiwa mali kutokana na vurugu hizo. Pia alisema kuwa Wizara itaendelea kutoa taarifa za uhakika kadri zinavyopatikana kutoka kwenye vyanzo vya uhakika ukiwemo Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Wakati huohuo, Mhe. Prof. Kabudi amewaaga wanafunzi 44 kati ya 100 waliochaguliwa kwenda nchini Israel kushiriki mafunzo ya kilimo kwa vitendo kwa kipindi cha miezi tisa kuanzia mwezi Septemba 2019. Wanafunzi hao ambao wengi wamehitimu katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Taasisi ya Kilimo ya Uyole ya Mbeya na Ukiriguru ya Mwanza wanakwenda kushiriki mafunzo hayo ya vitendo kwenye sekta mbalimbali za kilimo ikiwemo uzalishaji na teknolojia. Kati ya Wanafunzi hao, 16 wameondoka nchini tarehe 4 Septemba, 2019, kuelekea Israel, 44 wataondoka nchini tarehe 5 Septemba 2019 na idadi iliyosalia itaondoka tarehe 10 Septemba 2019.

Katika hotuba yake, Mhe. Prof. Kabudi amewataka wanafunzi hao vijana kuzingatia mafunzo hayo ili kuja kutoa mchango wao kwenye mapinduzi ya kilimo ambayo yatachochea mapinduzi ya viwanda nchini. Aidha aliwaasa kuwa waadilifu, kufanyakazi kwa bidii, kushikamana na kujiepusha na vitendo viovu.

“Mnaenda Israel kutafuta ujuzi, uzoefu na ubunifu katika maeneo ya uzalishaji mazao. Hivyo tunaamini kuwa mna nafasi kubwa ya kuja kuibadilisha Tanzania katika eneo la kilimo na mtaleta mapinduzi ya kilimo kwani vijana mpo wengi nchini, mna ari na ni nguvu kazi ya Taifa” alisisitiza Prof. Kabudi.

Akiielezea Israel, Mhe.Prof. Kabudi amesema kuwa nchi hiyo ni nusu jangwa kama ilivyo baadhi ya mikoa hapa nchini. Hata hivyo Israel inaongoza kwa kuuza mazao ya mbogamboga na matunda kwenye nchi za Ulaya kutokana na watu wa nchi hiyo kutumia maarifa katika kugeuza ukame kuwa fursa. Hivyo aliwataka wanafunzi hao kuhakikisha wanapata maarifa na kujifunza mbinu bora na teknolojia za kisasa ili kuja kuendeleza kilimo kikiwemo kile cha umwagiliaji kwenye mikoa kama Singida, Manyara, Shinyanga na Dodoma.

Wanafunzi hao mia moja (100) wamechaguliwa kati ya wanafunzi 1,440 waliotuma maombi ya kwenda kushiriki program ya mafunzo ya kilimo nchini Israel ambayo hufanyika kwa kipindi cha miezi tisa. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliratibu zoezi la upatikanaji wa wanafunzi hao kwa maelekezo ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa mwezi Novemba 2018 alipofanya mazungumzo na Balozi wa Israel nchini, Mhe. Noah Gal Gendler.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam.
4 Septemba 2019

Waziri Jafo Aagiza Halmashauri Kote Nchini Kuwa Na Mpango Mkakati Wa Kufanya Mikutano Na Taasisi Za Dini Angalau Mara Mbili Kwa Mwaka.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Mhe.Seleman Jafo ameziagiza Halmashauri Kote nchini kuwa na Mpango mkakati wa Kukutana na Taasisi za Dini angalau  Mara mbili  kwa Mwaka katika kujadili Mambo  mbalimbali kwani Taasisi hizo zimekuwa  na mchango mkubwa  kwa Taifa .
 
Waziri Jafo ameyasema hayo jijini Dodoma Sept.4,2019 wakati akifunga mkutano  wa  82 wa chama cha Madaktari wa kikristo Tanzania [TCMA] ambapo amesema miongoni mwa watu Muhimu katika Taifa lolote lile ni Madaktari na walimu ,hivyo viongozi wa Dini ni Walimu muhimu wanaosaidia kuelimisha jamii kuwa na maadili mema na Msingi Bora wa kuishi ikiwa ni Pamoja na kuepuka matendo maovu ya dawa za kulevya ,Wizi,Uvivu na Ugaidi.
 
Kutokatana na hilo Waziri Jafo ameagiza Halmashauri kote nchini Kufanya vikao na viongozi wa Dini angalau Mara mbili kwa Mwaka ili kuweza kujadili mambo muhimu ya Kujenga Taifa.
 
”Kati  ya watu muhimu katika Taifa hili na Duniani kote ni Madaktari  na Walimu,Ninyi viongozi wa Dini ni Walimu wazuri mnaobadilisha Tabia mbovu ya watu na kuwa na tabia nzuri .Kuna suala la utoaji wa huduma na Taasisi za kidini zimekuwa zinafanya vizuri,kwa hiyo tu mimi niagize halmashauri kote nchini kuwa na desturi ya kukutana na Taasisi za dini angalau mara mbili kwa mwaka katika kujadili changamoto mbalimbali kwani ninyi mmekuwa msaada kubwa kwa serikali”alisema.
 
Aidha,Waziri Jafo ameipongeza TCMA Kwa kuzindua  kampeni ya “Zijue Namba zako kwa Afya yako “kwani itakuwa chachu kubwa kuelimisha jamii kuhusu masuala ya Afya hususan Elimu ya Magonjwa yasiyoambukiza ambayo yameshamiri kutokana na ulaji usiozingatia Kanuni za bora za Afya hali inayopelekea kuwa na vitambi na Matatizo ya shinikizo la damu[Presha].
 
“Kati ya maeneo yenye  changamoto kubwa ni Magonjwa yasiyo ya kuambukiza watu wanakula Mapochopocho wanafikiri unene ni Fashion ,na gharama ya matibabu kwa magonjwa yasiyoambukiza imekuwa ni kubwa .Kwa hiyo niwapongeze kwa kuzindua kampeni hii ya “zijue namba zako kwa afya yako” lengo ni kutoa elimu juu ya kuzingatia Kanuni bora za afya,na sijaona mtu mwenye kitambi humu”alisema.
 
Rais wa chama cha Madaktari Tanzania Bwire Chilangi amewasilisha mapendekezo kwa serikali ikiwa ni pamoja halmashauri kuelekeza kujaza nafasi za watumishi katika hospitali za  kidini ambazo zina upungufu,kila kituo cha afya kuwa na akaunti ili kuepuka uchelewashaji wa fedha,halmashauri kuzingatia Geografia  na eneo husika katika hospitali za kidini na kupitia huduma zinazotolewa kwendana na uhalisia.
 
Naye  Mkurugenzi  mtendaji wa Taasisi ya kidini ya Christian Social Services Comission[CSSC]inayosimamia  sekta Afya na Elimu kwa Baraza la Maaskofu Makatoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania,Peter Maduki  amesema Makanisa yataendelea kutoa huduma ya Afya na elimu bila ubaguzi milele na milele pamoja na kufuata kanuni na taratibu za serikali na Matumizi mazuri ya Rasilimali Fedha.
 
Chama cha Madaktari wa kikristo Tanzania [TCMA] Kimetimiza takribani Miaka 82 tangu kianzishwe mwaka 1937 ambapo chama hicho kinamiliki hospitali mbalimbali za Rufaa ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Bugando jijini Mwanza.

Wanigeria wenye hasira walipiza kisasi, wapora maduka ya Waafrika Kusini

$
0
0
Maduka ya wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Nigeria yalivamiwa jana ikiwa ni hatua ya kujibu, mashambulizi ya hivi karibuni katika taifa hilo la Kusini mwa Afrika kufuatia wimbi jipya la chuki dhidi ya wageni. 

Mashambulizi ya jana yametokea zaidi katika mji wa kibiashara wa Lagos pamoja na mji mkuu wa Abuja, na miji ya Ibadan na Uyo. 

Vijana walioshikwa na hasira walichoma ofisi za kampuni ya simu ya Afrika Kusini ya MTN, na kuvamia maduka ya Shoprite. 

Maduka mengine yanayomilikiwa na wafanyabiashara wa Afrika Kusini, yalikuwa chini ya ulinzi wa polisi. Maelfu ya vijana pia waliandamana katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka dhidi ya mashambulizi ya chuki dhii ya wageni. 

Umoja wa Afrika, rais wa Nigeria na mwenzake wa Afrika kusini wote wamelaani vurugu hizo.

Taarifa Kwa Umma Toka Bungeni


Walioficha Meno Ya Tembo Wapewa Mwezi Mmoja Wajisalimishe

$
0
0
Na. Aron Msigwa – WMU, Dar es Salaam.
SERIKALI imetoa muda wa mwezi mmoja (kuanzia Septemba 4 hadi Oktoba 4, 2019) kwa wananchi wote wanaomiliki meno ya Tembo kinyume cha sheria, kuhakikisha wanayasalimisha kwenye vyombo vya ulinzi na usalama na kwamba watakaofanya hivyo kabla ya kuisha kwa muda huo hawatashtakiwa.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa muda huo alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam mara baada Kikosi Kazi cha Taifa dhidi ya Ujangili (NTAP) kukamata watuhumiwa 8 wa ujangili, vipande 338 na meno mazima ya Tembo 75 pamoja  na meno mawili ya kiboko.

“Nimewaita hapa ili mshuhudie kazi nzuri iliyofaywa na maafisa wa Serikali na Kikosi Kazi maalum cha kudhibiti ujagili, ninatoa huruma ya mwezi mmoja kwa kila aliye na meno ya Tembo ayasalimishe kwenye chombo chochote cha Serikali na atakayefanya hivyo ndani ya muda huo hatutamshtaki” Amesisitiza Dkt.Kigwangalla.

Dkt. Kigwangalla amesema kukamatwa kwa majangili hao kumetokana na kazi ya muda mrefu ambayo imezaa matunda na matokeo yake kuonekana kwa kukamatwa kwa majangili sugu 8 (nane) akiwemo Bw. Hassan shaban maarufu kwa jina la Nyoni aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu kwa kujihusisha na mtandao wa ukusanyaji wa meno ya Tembo kutoka Tanzania na Msumbiji.

Amesema  mtuhumiwa huyo wa ujangili amekamatwa na jumla ya vipande vya meno ya Tembo 338 na memo mazima 75 pamoja pamoja na meno 2 ya Viboko ambapo kwa mujibu wa Wataalam na Wanasayansi wa Uhifadhi wa Wanyamapori wanaeleza kuwa meno hayo ni sawa na Tembo 117 waliouawa.

Amebainisha kuwa meno hayo yalianza kutafutiwa soko mwaka 2015 wakati Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ilipoingia madarakani, hivyo hatua ya Serikali kuimarisha  Ulinzi wa Rasilimali za Taifa  na kukiongezea uwezo Kikosi cha Kudhibiti Ujangili soko la meno hayo liliharibika.

Dkt. Kigwangalla amesema katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya tano Majangili wengi wamekamatwa na mitandao yao kusambaratishwa akisisitiza kuwa yeyote atakayejihusisha na biashara hiyo kwa namna yoyote ile atakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria.

“Mtuhumiwa huyu amehangaika na huu mzigo kwa zaidi ya miaka minne na hili nataka watanzania wajue ya kwamba yeyote atakayejihusisha na biashara hii ya kuuza nyara za Serikali tutamkamata tu maana, sababu ni moja wateja tumebaki ni sisi wenyewe popote utakapojaribu kuuza tutakukamata tu”

Aidha, ametoa onyo kwa wananchi wanaojihusisha au kushiriki kwa namna yoyote ile  na vitendo vya ujangili waache mara moja akibainisha kuwa kazi hiyo kwa sasa haina nafasi nchini Tanzania.

Amesema kuwa kuanzia mwaka huu Wizara yake itaweka Mkakati mpya wa kukomesha vitendo vya ujangili nchini hadi kufikia mwaka 2014 akieleza kwamba mkakati huo utaimarisha kikosi kazi cha kudhibiti ujangili, kuimarisha ushirikiano na wizara nyingine, kuimarisha Jeshi USU na kuweka muundo mzuri utakaozuia mauaji ya wanyama.

Aidha, amefafanua kuwa katika kipindi cha miaka 3 katika Ikolojia ya Selous hakuna Tembo hata mmoja aliyeuawa na majangili akibainisha kuwa meno ya Tembo yaliyokamatwa Agosti 31 mwaka huu ni yale ya ujangili uliofanyika nyuma kabla ya kuingia kwa Serikali ya awamu ya tano.

Amesema Kikosi Kazi hicho cha Serikali kimefanikiwa kuziba mianya yote ya biashara haramu za nyara za Serikali kwa kupambana na uharifu kwa kufuatilia na kusambaratisha mitandao yote ya ujangili ikiwemo mali na silaha za majangili.

Amebainisha kuwa kazi hiyo imefanikiwa kwa kuwa kinajumuisha maafisa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na vyombo vingine vya ulinzi na Usalama  na taasisi za kisheria  na kimekuwa kikifanya kazi nzuri ya kuratibu , kusimamia na kuchukua hatua za kupambana na uhalifu wa rasilimali za Wanyamapori na Mazao ya Misitu kwa kuendesha operesheni zinazoongozwa na taarifa za Kiintelijensia.

Dkt. Kigwangalla ameongeza kuwa Kikosi Kazi hicho kinafanya uchunguzi wa wahalifu na mali zinazotokana na uhalifu, kukamata, kupekua na kushikilia mali za wahalifu wanaojihusisha na ujangili.       

 “Sasa hivi kupitia Kikosi Kazi chetu tumeziba mianya yote, anayefanya biashara tutamkamata, aanayewinda kwenye maeneo ya hifadhi tutamkamata na hata askari wote wanaoshirikiana na majangili tutawakamata kwa kuwa tukimpata jangili mmoja tunahakikisha na mtandao wake wote tumeuvunja” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.

Dkt. Kigwangalla ameeleza kuwa katika kipindi cha mwaka 2016 hadi 2019 Kikosi Kazi hicho kimefanikiwa kukamata watuhumiwa zaidi ya 1072 silaha 539 zikiwemo siala 85 za Kivita na jumla ya risasi 37,921.

Aidha, nyara mbalimbali za Serikali zilikamatwa ikiwa ni pamoja na meno tembo, pembe za faru, ngozi za Simba, Chui na Duma, meno ya Kiboko, Kobe pamoja na mazao ya Misitu.

Pia Dkt. Kigwangalla amebainisha kuwa Kikosi kazi hicho hadi sasa kimefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakubwa wa ujangili wakiwemo Aloyce Francis Ayubu( Kamanda),  Mateso Kassiani Albano (Mateso Chupi)  na Jayzan George Kuchar (China), Haruna Kassa, Frank Silagei na Ojugu (Original).

Wengine ni Haong Nghia Trung, MS. Yang Feng Glan (Queen of Ivory) ambaye amekwishahukumiwa pamoja na Salvius Francis Matembo na Manase Julius Philemon, Boniface Maringo, (shetani), Juma Maringo (Yesu), Godfrey James Nyamicha (Papa), Haidari Omary Sharif, Oliva Lucas Mchua na Mrangilwa Emanueli.

Taarifa Kwa Umma Kutoka Jeshi La Polisi

Serikali Yasema Haishinikizi Udhamini Katika Michezo

$
0
0
Na Shamimu Nyaki –WHUSM
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amesema kuwa Serikali haishikizi ufadhili katika michezo bali wajibu wake ni kuweka mazingira wezeshi kwa mfadhili ambaye anataka kufadhili mchezo wowote kutokana na yeye kuona namna anavyoweza kufaidika katika ufadhili huo.

Mhe.Shonza amesema hayo leo Bungeni Dodoma alipokuwa anajibu swali la Mbunge Mhe.Sophia Mwakagenda (Viti Maalum) aliyeuliza Ni lini Serikali itahakikisha ufadhili unapatikana kwenye michezo inayohusu wanawake hususan michezo ya ngumi.

Akijibu swali hilo Mhe.Shonza ameeleza kuwa ufadhili wa michezo hutokana na mfadhili kuona faida ya kibiashara na kijamii wakati anapofadhili ambapo amesititiza kuwa hivi sasa Tanzania ina ligi kuu ya mpira wa miguu kwa wanawake ambayo inadhaminiwa na Kampuni ya vinywaji ya Serengeti Breweries kupitia bia yake ya Serengeti Lite ambayo imefadhili kutokana na faida walioona itapata.

“Ufadhili haushinikizwi na Serikali bali ni suala la hiari kwa upande wa wafadhili ambao huchukua fursa hiyo pale wamapoona fursa za kibiashara zitakazowanufaisha wao, Hivyo wajibu wa Serikali ni kuimarisha uhusiano na kuweka mazingira wezeshi ili faida ipatikane kwa pande zote mbili”alisisitiza Mhe.Shonza.

Aidha Mhe. Shonza katika kujibu swali la nyongeza la mbunge huyo aliyeuliza ni lini Serikali itatoa vifa vya mazoezi kwa wanamichezo hao, ameeleza kuwa suala la kukuza na kuendeleza michezo nchini linashirikisha pia wadau hivyo ni wajibu wa wanachi wote kuona michezo kuwa ni muhimu katika jamii hivyo kuwekeza katika Nyanja mbalimbali.

Hata hivyo Mhe. Shonza amewaomba wadau wote wa Michezo nchini kusaidia kushawishi makampuni,Taasisi na wadau wote kudhamini na kufadhili maendeleo ya michezo nchini ikwemo wanayoshiriki wanawake.

Kutana na Mohamedi Buruhani Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH .....Anauwezo wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mohamedi Buruhani Mtabibu wa Nyota za Binadamu  Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Mohamed Buruani Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. 

Anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO . Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie ..Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Mohamed Buruhan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN, Anatafsiri Ndoto. ,KUSAFISHA NYOTA, Mvuto wa Mwili na BIASHARA, ...MIGUU Kufa GANZI na mengi zaidi (+255  715971688 au (+255  756914036

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Serikali Yadhamiria Kufuta Kesi Zote Zinazozikabili Kampuni Za Kilimo Ili Kuondoa Changamoto Ya Masoko Kwa Wakulima

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Naibu waziri wa Kilimo Mhe.Husein Bashe amesema moja ya vikwazo vilivyokuwa vinasababisha  Sekta ya Kilimo kuendelea kuwa na Matatizo ni pamoja  na Migogoro na kesi za  muda mrefu dhidi ya Makampuni za Kilimo ambapo serikali imedhamiria   kufuta kesi zote zilizokuwa zinazikabili kampuni hizo ili ziweze kununua Mazao ya wakulima. .
 
Mhe.Bashe amesema ameyasema hayo Sept.3,2019 jijini Dodoma katika mkutano  uliokutanisha wizara ya Kilimo,Wizara ya Viwanda na biashara,Wizara ya Fedha pamoja na wadau wa kilimo hapa nchini.
 
Naibu Waziri Bashe amesema  kampuni za kilimo zilikuwa zikidaiwa zaidi ya Tsh.Trilioni 10  na Serikali hali ambayo ilikuwa inasababisha kushindwa kwenda kutoa huduma kwa wakulima hivyo serikali ina mkakati kabambe wa kufuta kesi na faini zote hizo ili ziweze kutoa huduma kwa wakulima.
 
Aidha,Mhe.Bashe amesema wamekubaliana na Mamlaka ya  Mapato Tanzania[TRA] kuwa ndani ya siku 90 Kuanzia leo Sept.4,2019 suala la madai  kwa kwa Kampuni 4  za kilimo  limekuwa limeisha ili kampuni hizo ziendelee kununua mazao kwa wakulima.
 
Pia Naibu Waziri  Bashe amesema kuna zaidi ya kilo Mil.12  za Tumbaku zipo mikononi mwa Wakulima na Kampuni za kilimo  chini ya Bodi ya Tumbaku Tanzania  zitakutana na wakulima kununua kilo hizo kuanzia Sept.12,2019  .

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku ,Tanzania Tobacco Board[TTB] Hassan Mwakasuvi    amesema ni vyema wakulima  kuheshimu mikataba huku akisema kuwa maazimio ya kikao hicho ni Faraja kwa wakulima katika msimu ujao wa kilimo. 
 
Naye  Mwenyekiti wa vyama vikuu vya wakulima wa Tumbaku Tanzania Emanuel Cherehani ameishukuru serikali kwa maamuzi hayo  huku akiomba kuanza kutekelezwa ndani ya Muda husika uliotajwa ili isiathiri zaidi wakulima huku akiwaomba wakulima kuendelea kutunza mazao yao ya tumbaku.
 
Aidha,Cherehani amesema hapo awali uzalishaji wa zao la tumbaku kwa mwaka 2015 ilikuwa milioni 120 lakini umeshuka mpaka milioni 41 jambo ambalo limeathiri kwa wakulima na Serikali kwa Ujumla.

Huduma Za Benki Ya Wanawake Kutolewa Na Benki Ya TPB Plc

$
0
0
Na. Farida Ramadhan na Peter Haule, WFM, Dodoma
Serikali imesema kuwa kwa sasa hakuna Benki ya Wanawake Tanzania baada ya iliyokuwa Benki ya Wanawake kuunganishwa na Benki ya TPB Plc.

Hayo yameelezwa bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Faida Mohammed Bakar, aliyetaka kujua sababu zilizokwamisha uanzishwaji wa Benki ya Wanawake kwa upande wa Zanzibar.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, huduma za iliyokuwa Benki ya Wanawake Tanzania zinaendelea kutolewa na Benki ya TPB Plc ambapo imeanzisha dirisha maalum la wanawake katika matawi yake yote yakiwemo matawi ya Unguja na Pemba ili kukidhi mahitaji yao kote nchini.

“Nitoe wito kwa wanawake wa Tanzania watumie akaunti ya Tabasamu iliyopo katika Benki ya TPB Plc ili kunufaika na mikopo yenye riba nafuu bila kulazimika kuwa katika vikundi kama Benki zingine zinavyofanya”, alieleza Dkt. Kijaji.

Dkt. Kijaji alisema kuwa Akaunti ya Tabasamu ilifunguliwa na Benki ya Posta kwa ajili ya Wanawake pekee kama Benki ya Wanawake ilivyokuwa ikifanya na pia inatoa mkopo kwa mwanamke mmoja mmoja kwa lengo la kumuwezesha  kufanya shughuli zake za kijasiriamali, kiuchumi na za kijamii kwa maslahi yake na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalum Mhe. Faida Mohammed Bakar, ameipongeza Serikali kwa majibu yake kwa kuunganisha Benki ya Posta na Benki ya Wanawake ili Wanawake waweze kuhudumiwa katika maeneo yote, ambapo awali huduma hizo zilikuwa zinapatikana katika maeneo machache kutokana na ufinyu wa matawi ya Benki ya Wanawake.

Mwisho.


Serikali Yatumia Miradi Kudhibiti Uharibifu Wa Mazingira

$
0
0
Serikali imechukua hatua mbalimbali kupitia miradi inayofadhiliwa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi ili kuweza kudhibiti uharibifu wa mazingira unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi katika Visiwa vya Pemba na Unguja.

Hayo yamesemwa leo Septemba 5,2019 na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akiwa Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Mwantum Dau Haji lililouliza kuwa kasi ya mmomonyoko wa ardhi na uhaba wa udongo katika Visiwa vya Unguja na Pemba vinatishia uhai wa visiwa hivyo. Je, ni hatua zipi za makusudi zimechukuliwa katika kuvinusuru visiwa hivyo?. 

Mhe. Sima alisema kupitia Mradi wa Kujenga Uwezo wa Jamii Kuhimili Athari za Mabadiliko ya tabianchi-LDCF ambao umetekelezwa mwaka 2012 hadi 2018, shughuli mbalimbali zimefanyika zikiwemo ujenzi wa kuta mbili za mita 25 kila moja katika eneo la Kisiwa Panza-Pemba na ujenzi wa makinga bahari (groynes) matano ya wastani wa urefu wa mita 100 kila moja katika eneo la urefu wa mita 538 Kilimani-Unguja. 

Pia Naibu Waziri alitaja upandaji mikoko Pemba maeneo ya Kisiwa Panza hekta 200, Tumbe hekta 10, Ukele hekta 7 na Tovuni hekta 1 na upandaji mikoko Unguja maeneo ya Kisakasaka hekta 8 na Kilimani hekta 1.4. 

Aliongeza kuwa kupitia mradi wa Kupunguza Uharibifu wa Ardhi na Kuongeza Uzalishaji wa Chakula katika maeneo kame nchini (2017-2022), shughuli zinazotegemewa kufanyika katika maeneo ya Micheweni Kata ya Micheweni na Kiuyu Maziwang’ombe ambazo ni kujenga makinga maji katika mashamba (dykes) ili kuzuia maji ya bahari kuingia katika mashamba. 

Nyingine ni kutoa elimu kuhusu kilimo kinachokabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia mashamba darasa, upandaji  wa miti ili kuhifadhi udongo na kutunza mazingira, na uanzishaji wa biashara ndogo ndogo ili kuwezesha jamii kuwa na shughuli mbadala za kujiongezea kipato.  

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi, kudhibiti mmomonyoko wa udongo, na kukabiliana na uhaba wa udongo. Alimalizia Waziri Sima.
 

Safari za ndege za Air Tanzania kwenda Afrika Kusini zasitishwa

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe amesema Serikali imesitisha kwa muda huduma ya usafiri wa ndege zake nchini  Afrika Kusini hadi hali ya usalama nchini humo itakapotengamaa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Septemba 5,  Kamwelwe amesema ndege hiyo imetua nchini jana saa moja usiku lakini itasitisha safari zake za kwenda Afrika Kusini kwa sasa kutokana na  sababu mbalimbali ikiwamo vurugu zinazoendelea nchini humo.

“Sababu hizo ni pamoja na usalama wa chombo chenyewe kutokana na hali ya vurugu iliyopo nchini humo hadi pale tutakapohakikishiwa usalama wetu na abiria.

“Wanasheria wamebaki Afrika Kusini wakiendelea kufuatilia hukumu iliyotolewa na kuhakikisha aliyefungua kesi analipa gharama zote,” amesema.

Vurugu hizo zilianza Jumapili Septemba Mosi, 2019 baada ya raia wa nchi hiyo kuvamia mitaa yenye maduka ya raia wa kigeni na kuanza kupora mali na kuchoma moto.

Pamoja na mambo mengine, amesema leo asubuhi ndege hiyo imefanyiwa ukaguzi iko salama inasubiri kupangiwa safari ya njia nyingine itakayoanza leo

Kutana na Mohamedi Buruhani Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH .....Anauwezo wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mohamedi Buruhani Mtabibu wa Nyota za Binadamu  Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Mohamed Buruani Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. 

Anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO . Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie ..Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Mohamed Buruhan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN, Anatafsiri Ndoto. ,KUSAFISHA NYOTA, Mvuto wa Mwili na BIASHARA, ...MIGUU Kufa GANZI na mengi zaidi (+255  715971688 au (+255  756914036

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Waziri Wa Kilimo Japhet Hasunga Afanya Mazungumzo Na Ujumbe Wa Wakurugenzi 6 Wa Mashav Nchini Israel

$
0
0
Na Mathias Canal, Jerusalem-Israel
Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 5 Septemba 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Wakurugenzi 6 wa Mashav wa Wizara ya Mambo ya nje ya Israel.

Katika mkutano huo wa kazi uliofanyika katika Ofisi za wizara ya Mambo ya nje ya Israel iliyopo mtaa namba 9 Yitzhak Rabin Jijini Jerusalem nchini Israel, Waziri wa Kilimo amewasilisha mambo mbalimbali kuhusu sekta ya kilimo ikiwemo ufuatiliaji wa utekelezaji wake.

Mhe Hasunga ameishukuru serikali ya Israel kwa kukubali ombi la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli la kuongeza idadi ya wanafunzi wanaoshiriki mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies katika kipindi cha mwaka mmoja kutoka 45 ambapo imefikia idadi ya wanafunzi 100.

Katika kikao hicho Waziri Hasunga amewakumbusha Mabalozi hao sita kuhusu ombi la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli la kuongezwa idadi ya wananfunzi kufikia idadi ya wanafunzi 300.

Mhe Hasunga amesema kuwa Balozi huyo amepongeza kwa dhati na kuunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwani ni serikali ya vitendo na uwajibikaji hivyo wapo tayari kuhakikisha kuwa ushirikiano unaboreshwa baina ya nchi hizo mbili.

Kikao hicho pia kimejadili kwa kina namna ya kuboresha zaidi mahusiano baina ya nchi ya Tanzania na Israel hususani katika kuimarisha ushirikiano kwenye nyanja za utafiti, uongezaji thamani wa mazao, na namna ya kuongeza ukubwa wa mashamba na kilimo tija.

Pia, Mhe Hasunga amewasilisha ombi la kupata kampuni mbalimbali za nchini Israel ili kuzuru Tanzania na kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji.

“Tukipata kampuni za kuisaidia Tanzania kwenye maswala ya kilimo cha umwagiliaji tutakuwa na fursa ya kubadili kilimo chetu kutoka kwenye kilimo cha kutegemea mvua na hatimaye kuingia katika kilimo cha umwagiliaji” Alisisitiza Mhe Hasunga na kuongeza kuwa

Serikali ya Israel imekubali kufikiria kuongeza idadi ya vijana kutoka Tanzania wanaozuru Israel kwa ajili ya kujifunza ambapo pia wataongeza uwezekano wa wataalamu mbalimbali wakiwemo maafisa ugani nchini Tanzania kuzuru Israel kwa ajili ya kujengewa uwezo katika utendaji.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Ushirikiano wa mambo ya nje nchini Israel Ndg Yuval Fuchs amesema kuwa serikali ya Israel imeridhia maombi ya Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga na kusema kuwa Israel ipo tayari kushirikiana na Tanzania ili kuboresha sekta ya kilimo kutoka kwenye kilimo cha kujikimu kuwa kilimo cha kibiashara

Vilevile amesema kuwa atazishawishi kampuni mbalimbali kuwekeza nchini Tanzania kwa ushirikiano mzuri na serikali kwani Tanzania kuna ardhi nzuri yenye rutuba kwa ajili ya kilimo.

Kadhalika amempongeza Waziri Hasunga kwa kutembelea nchini Israel kwa ajili ya ziara ya kikazi ambapo amesema kuwa kumekuwa na kikao muhimu kilichojadili namna ya kuboresha kilimo nchini Tanzania.

Kadhalika, Balozi wa Tanzania nchini Israel Balozi Job Daud Masima amesema kuwa kikao cha Waziri wa Kilimo ni muendelezo wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo nchini Israel ambapo ameongeza kuwa kikao hicho kimetoa taswira ya kutafakari kwa pamoja kuona namna mafunzo hayo yanavyowasaidia vijana wa kitanzania.

Amesema Waziri Hasunga amekutana na ujumbe wa mabalozi 6 pamoja na wasaidizi wake wanaohusika na maswala ya Afrika Mashariki, kikao hicho kimetoa heshima kubwa kwa serikali ya Tanzania ambapo vijana 100 watapokelewa nchini Israel na waziri Hasunga leo tarehe 5 Septemba 2019.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya agrostudies Ndg Yaron Tamir amesema kuwa wanafunzi walioshiriki mafunzo hayo kutoka Tanzania wametoa ushirikiano mzuri hivyo mafunzo hayo waliyoyapata wanapaswa kuyaendeleza ili kuboresha kilimo nchini Tanzania.

MWISHO

Rais Magufuli Amjulia Hali Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa Apson Mwang’onda

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa Apson Mwang’onda anayepatiwa matibabu Jijini Dar es Salaam.

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo,Pamoja Na Magonjwa Sugu

$
0
0
SUPER MORISIS; nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-85)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wala kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 18-45

SUNUPER;   Hurefusha na kunenepesha maumbire madogo ya uume uliosinyaa ,  matatizo haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguruma na kujaa gesi hatimae kinyesi kuwa km cha mbuzi, ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia nidawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

ONDOA MATATIZOYAKO YOTE  ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,  kurudisha mali iliyopotea au kuibiwa 

Kwahuduma na msaada wasiliana na DR. GALIMBO  call 0759 208 637

watsap  0620510598
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images