Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne 16 July


Rais Magufuli Amwagiza Waziri Ummy Kufuatilia Malipo Yote Ya Serikali Kwa Wagonjwa Wa Nje Ya Nchi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli amemwagiza Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kufuatilia malipo yote ya Wagonjwa wanoenda kutibiwa nje ya nchi ili kubaini ubadilifu unaofanywa na baadhi ya watu wasiowaaminifu.
 
Rais Magufuli ameagiza hilo jana wakati akizindua miradi Saba ya huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa Bugando yenye thamani ya shilingi Bilion15, jambo litalosaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma bora kwa ukaribu pamoja na kuokoa kiasi cha fedha miongoni mwa wanaohitaji huduma.
 
“Na kwasababu Waziri wa Afya yupo hapa, akafuatilie malipo yote ambayo tunatakiwa kulipa, kule nje , akikuta kunamalipo yakulipa mtu ambae hakuwa mgonjwa aliyejihifadhi huko, akazilipe mwenyewe ” alisema Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
 
Rais Magufuli amesema kuwa baadhiya Watendaji waliona kupeleka Wagonjwa nje ya nchi kwaajili ya matibabu ni fursa yakujipatia kipato, jambo lililokuwa linapelekea hasara kubwa kwa nchi ya Tanzania kutokana na malipo kwa baadhiya watu wasiostaholi.
 
” Hata kupeleka kwa wagonjwa nje kwa Watanzania ilikuwa ni dili, ilikuwa ni fursa kwa Watendaji, wapo watu waliokuwa wanapewa vibali kwenda kutibiwa India lakini anaumwa mafua, ilikusudi apate safari na msindikizaji, bill zote zinaletwa kwa Serikali ” alisema Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
 
Dkt. Magufuli aliendelea kusema kuwa ni lazima tujenge nidhamu katika nchi, huku akisisitiza kuwa Serikali haijakataza kupeleka wagonjwa nje ya nchi, huku akisisitiza kuwa wagonjwa wanaostahili kupelekwa kwa matibabu nje ya nchi ni wale walioshindikana ndani ya nchi.
 
Aidha, ameagiza kuboresha uzalishaji wa oksijeni ili kuhakikisha zinazalishwa kwa wingi jambo litalosaidia kuokoa kiwango kikubwa cha mapato kinachopotea kwa kuagiza nje ya nchi, pia itasaidia kuongeza ajira kwa wananchi wa Tanzania.
 
“Ninawaomba ndugu zangu, tengenezeni oksijeni nyingi, panueni uzalishaji ili Wizara ya Afya iagize hapa hapa Bugando ili vijana wanaomaliza famasi hapa hapa Bugando wapate ajira hapa yakutengeneza Oksijeni ” alisema Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli

Watalaam wa chuo cha Oxford watoa mafunzo kwa madaktari bingwa

$
0
0
Wataalam kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza wameanza kutoa mafunzo kwa madaktari bingwa wadamu, madaktari wasaratani na wauguzi ambao watatoa Huduma kwa wagonjwa watakaopandikizwa ULOTO mwishoni mwa mwaka huu.

Akizungumza kabla ya kufungua rasmi mafunzo ya wiki mbili, Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo, Ushauri na Utafiti, Dkt. Faraja Chiwanga amesema kwamba mafunzo haya ni mwendelezo wa maandalizi ya kutoa Huduma ya upandikizaji ULOTO (bone marrow transplant) ambayo ilikuwa haipatikani hapa nchini kutokana na kutokuwapo kwa wataalam na ukosefu wa vifaa vya kutoa Huduma husika.

‘’Mafunzo haya yanajumuisha wauguzi zaidi ya 30 pamoja na madaktari bingwa 20 wa magonwa ya damu na saratani wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,’’ amesema Dkt. Chiwanga kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH.

Dkt. Chiwanga amefafanua kwamba mwezi Juni, mwaka huu hospitali ilipeleka wataalam 11 nchini India katika Hospitali ya Apollo iliyopo Chennai kwa kipindi cha mwezi mmoja ili kujifunza kwa vitendo jinsi ya kupandikiza ULOTO (bone marrow transplant).

Takwimuza MNH zinaonyesha kwamba wagonjwa takribani 130 hadi 140 wanahitaji Huduma ya upandikizaji ULOTO kwa mwakana kwamba zaidi ya theluthi mbili ya wagonjwa wenye tatizo la saratani hufariki dunia kwa kukosa Huduma hii. Uwapo wa Huduma hii utasaidia wananchi wengi kutibiwa hapa nchini, kujenga uwezo kwa wataalam wa ndani na kupunguza gharama kwa Serikali kupeleka wagonjwa nje ya nchi.

Askari Polisi 54 Watimuliwa Kazini

$
0
0
Rais Magufuli amepongeza utendaji mzuri wa Jeshi la Polisi nchini, huku akieleza kuchukizwa na askari wake wachache wasio waadilifu.

Amebainisha kuwa katika kipindi cha miezi sita iliyopita, askari polisi 157 wamechukuliwa hatua kwa kukiuka taratibu za kiutumishi. Kati yao, 54 wamefukuzwa jeshini.

Rais Magufuli aliyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa nyumba 20 za askari polisi zilizojengwa kwenye Mtaa wa Magogo mjini Geita.

Kutokana na kuwapo kwa changamoto hiyo, Rais Magufuli alimtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchni (IGP), Simon Sirro, kuwa mkali kwa wanaokiuka maadili na kuchafua sifa nzuri za jeshi hilo.

Akifafanua zaidi kuhusu changamoto hiyo, Rais Magufuli alisema baadhi ya askari hao wamewajibishwa kutokana na makosa mbalimbali yakiwamo vitendo vya kushiriki katika kutenda uhalifu ukiwamo ujambazi na rushwa.

Alimtaka IGP Sirro kutokubali wachache walioko katika jeshi hilo, kuchafua heshima na sifa ya jeshi hilo ambalo yeye analiamini na wananchi wanalikubali kwa utendaji wake mzuri.

''Ninapongeza kazi nzuri inayofanywa na Jeshi la Polisi kwani vitendo vya uhalifu ukiwamo ujambazi, hata mkoani Geita, vimepungua sana kama ambavyo pia wananchi wana imani na Jeshi la Polisi kwa uadilifu na utendaji wake," alisema.

"Kuna askari wachache tu ambao wamekuwa wakichafua sifa na heshima ya jeshi, hao wasipewe nafasi. Sirro washughulikiwe hao wachache," Rais Magufuli aliagiza.

Alisema wapo baadhi ya askari polisi wasio waadilifu, wanashirikiana na majambazi kufanya uhalifu, kubambikiza kesi wananchi wasio na makosa.

Alisema askari wa aina hiyo lazima washughulikiwe ili kutochafua taswira ya Jeshi la Polisi na kulishusha hadhi mbele ya umma.

Jacob Zuma: Tuhuma za ufisadi wa fedha ni njama iliiyopangwa dhidi yangu

$
0
0
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema kuwa vikao vya kuchunguza tuhuma za ufisadi dhidi yake, ni njama iliyopangwa dhidi yake.

Zuma aliyasema hayo jana Jumatatu katika kikao cha uchunguzi wa faili la tuhuma za ufisadi wa fedha zinazomkabilia ambapo alikitaja kikao hicho kuwa ni njama dhidi yake.

 Aliongeza kwamba maadui wake hata walipanga njama ya kutaka kumuua, kwa kuwa walikuwa wanataka kutwaa madaraka na kumuweka kando. 

Mwanzoni mwa utetezi wake kwenye kikao hicho alisema kuwa tuhuma hizo zilikuwa na lengo la kumuondoa madarakani. 

Itakumbukuwa kuwa rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini aliondolewa madarakani mwezi Februari mwaka jana. 

Aidha Zuma anatuhumiwa kwamba katika kipindi cha miaka tisa ya uongozi wake, aliwapa fursa watu wake wa karibu kutumia mali ya umma kwa maslahi yao binafsi na pia kuwateua katika nafasi mbalimbali serikalini.
 
Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini ametupilia mbali tuhuma hizo akizitaja kuwa ni za kisiasa tu. 

Katika hatua za kuendelea kumbana Jacob Zuma katikati ya mwezi Agosti mwaka jana Mahakama ya Katiba ya Afrika Kusini ilibatilisha uteuzi wa Mwendesha Mashtaka Mkuu ambaye alipewa kazi na Jacob Zuma baada ya kumpiga kalamu nyekundu afisa aliyekuwepo kabla yake. 

Kadhalika mahakama hiyo ilitoa amri kwamba, mwendesha mashtaka mkuu wa zamani arejeshwe kazini katika muda wa siku 90 kwa lengo la kufuatialia faili la tuhuma za ufisadi dhidi ya rais huyo wa zamani.

VIDEO: Tazama Hapa Kangi Lugola Alivyojitosa Kucheza Mbele ya Rais Magufuli

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola  jana alishindwa kujizuia na kuamua kwenda kuungana na Bendi ya polisi nchini Tanzania  kusakata muziki na kuonyesha naye ni mjuzi wa kucheza hali iliyoibua shangwe kutoka kwa watu waliohudhuria shughuli hiyo.

Tukio hilo lilitokea jana  Jumatatu July 15 wakati wa  hafla ya ufunguzi wa nyumba 20 za polisi eneo la magogo mjini Geita.

Uzinduzi huo ulifanywa na Rais wa Tanzania, John Magufuli ambapo bendi hiyo ilionyesha uhodari wake wa upigaji mzuri wa tarumbeta uliombatana na mbwembwe za wapigaji ulikuwa kivutio kilichowafanya viongozi washindwe kuvumilia kukaa kwenye viti na kushuka kutoka jukwaa kuu na kwenda kuwatunza

==>>Tazama Video Hapo Chini

Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) Yavifungulia vyuo ambavyo vilifungiwa Kudahili Wanafunzi

$
0
0
Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imevifungulia vyuo ambavyo vilifungiwa udahili kikiwemo Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji, Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian Bagamoyo, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), na Chuo Kikuu Kishiriki cha Askofu Mkuu Mihayo (AMUKTA).

Akizungumza wakati wa Maonyesho ya TCU yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jana Jumatatu Julai 15, 2019, Mkurugenzi wa Uratibu na Udahili wa tume hiyo, Dk Kokuberwa Katunzi-Mollel alisema vyuo hivyo vimeruhusiwa kufanya udahili baada ya kukidhi vigezo vilivyotakiwa.

Tayari dirisha  la udahili kwa mwaka huu  limefunguliwa kwa awamu ya kwanza kuanzia jana Jumatatu Julai 15 hadi Agosti 10, 2019, hivyo  akawataka wanafunzi wanaotaka kujiunga na elimu ya juu kuanza kutuma maombi.

Msekwa Afunguka Kuhusu Barua ya Makamba na Kinana Kudai Kudhalilishwa na Cyprian Musiba

$
0
0
Katibu wa baraza la ushauri la viongozi wastaafu CCM, Pius Msekwa amesema malalamiko ya makatibu wakuu wawili wa chama hicho atayapeleka ngazi za juu kwa hatua zaidi.

Juzi, makatibu wakuu hao wawili wastaafu wa CCM, Yusuf Makamba na Abdulrahman Kinana, walimwandikia barua Msekwa wakilalamika kudhalilishwa kwa mambo ya uongo na mtu anayejitambulisha kama mwanaharakati na mtetezi wa Serikali.

Msekwa ambaye alisema barua hiyo ambayo ni ya kwanza kuwafikia wao kama Baraza la Wazee Wastaafu, kwa kawaida itapelekwa kwenye chama hicho ambacho ndicho kinachopaswa kuitisha vikao kushughulikia malalamiko yaliyotajwa.


Amesema nakala nyingine za barua hiyo zimepelekwa kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli na Katibu Mkuu, Dk. Bashiru Ally.

“Hii ni mara ya kwanza kupokea malalamiko ya aina hii, kwanza hakuna utaratibu wa kawaida, lakini tutafuata taratibu za chama, tutapeleka kwenye chama chenyewe." Amesema na kuongeza;

“Barua hii nakala yake imeenda pia kwa Mwenyekiti wa chama na Katibu Mkuu"

Deni La Tshs Bil. 7 Lawaweka Pabaya Wadaiwa Sugu Wa NARCO

$
0
0
Na. Edward Kondela
Serikali imesema wadaiwa wote waliowekeza katika ranchi za taifa zinazomilikiwa na Kampuni ya Ranchi ya Taifa (NARCO) walipe madeni yao kabla haijachukua hatua ya kuwanyang’anya maeneo na kuwafikisha mahakamani.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema hayo jijini Dodoma katika ofisi za makao makuu ya NARCO wakati akizungumza na wawekezaji waliopatiwa vitalu 111 katika ranchi za taifa zilizopo maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kulisha mifugo yao ambapo hadi sasa wanadaiwa Tshs Bilioni Saba.

“Lipeni bila shuruti, ahadi yangu kwenu mkifanya majukumu yenu ofisi yangu itawapatia ushirikiano wa kutosha, kwa wale ambao hawalipi watakuwa wamepoteza sifa za kuwa wawekezaji na siyo kwamba itaishia hapo tutachukua hatua za kisheria na watalipa deni ili kusudi watanzania wengine wawekeze ambao wanaweza kulipa hela ya serikali, hulipi nitakuondoa tena nitakufunga.” amesema Prof. Gabriel

Prof. Gabriel ameitaka NARCO kuhakikisha makampuni matano ambayo yanadaiwa fedha nyingi zaidi zinazokaribia tshs Bilioni Moja, yalipe fedha hizo ili kuiwezesha NARCO iweze kufanya shughuli zake na kuboresha ranchi inazozisimamia.

Katibu mkuu huyo ameitaka pia NARCO kuwekeza katika ranchi zake ili wawekezaji waweze kupata huduma mbalimbali muhimu kwa ajili ya mifugo yao yakiwemo maji na malisho pamoja na kuboreha njia za mawasaliano na wawekezaji, kutengeneza mpango wa uwekezaji na mikakati ya kiusalama.

Aidha Prof. Gabriel ameutaka uongozi wa Umoja wa Wawekezaji wa Ranchi za Taifa (UWARATA) kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kisheria ikiwemo kusajili chama chao ili kiwe na nguvu ya kusimamia wanachama wao katika kuhakikisha wanafanya kazi kwa kufuata taratibu na sheria za nchi na kuwa daraja la mawasiliano kati ya Wizara ya mifugo na Uvuvi na NARCO.

Akizungumza kuhusu deni la tshs Bilioni Saba wanalowadai wawekezaji, kwa niaba ya Kaimu Meneja Mkuu wa Narco Prof. Philemon Wambura, Meneja Masoko wa NARCO Bw. Emmanuel Mzava amesema deni hilo limedumu kwa zaidi ya miaka miwili sasa na wamekuwa wakifanya juhudi mbalimbali za kuwasiliana na wawekezaji ili waweze kulipa na katika kikao hicho kuweka mkakati wa kulipwa deni hilo.

“Baada ya kufanya kikao na katibu mkuu sisi watendaji tuliobaki hapa pamoja na wawekezaji katika vitalu vilivyopo katika ranchi za taifa, miongoni mwa mambo tunayofanya ni kuwekeana sasa kama makubaliano madogo ambayo yameandaliwa kwamba mwekezaji tunamsomea deni lake na tunakubaliana lini analipa deni lake.” Amesema Bw. Mzava.

Nao baadhi ya wawekezaji waliofika katika kikao hicho wamesema kimekuwa na manufaa makubwa kwao ili waweze kutatua changamoto zinazowakabili na kuwa na misingi mizuri ya kuendelea kumiliki vitalu walivyopatiwa na kulisha mifugo yao kwa kufuata sheria za nchi.

Kikao cha katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel, uongozi wa Kampouni ya Ranchi ya Taifa (NARCO) na wanachama wa Umoja wa Wawekezaji wa Ranchi za Taifa (UWARATA), kimefanyika ikiwa ni siku chache baada ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina kuutaka uongozi wa NARCO kubadilika na kutumia maeneo yake kwa ajili ya kuwekeza na kupata faida ili iweze kujiendesha na kutoa gawio serikalini.

Wanachama hao walioshiriki kikao hicho wanatoka katika vitalu 111 vilivyopo katika ranchi za Kagoma, Kikulula, Mabale na Kitengule zilizopo Mkoani Kagera, ranchi zingine ni Uvinza, Usangu na Kalambo zilizopo Nyanda za juu Kusini na ranchi za Mkata, Mzeri, Dakawa zilizopo Mashariki na Pwani.

Mwisho.

Serikali Yawatoa Hofu Wakulima Wa Pamba......Waziri Mkuu Asema Hadi Julai 30 Wakulima Wote Watakuwa Wamelipwa

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
ZAO la pamba ni miongoni mwa mazao makuu ya biashara hapa nchini yakiwemo ya korosho, chai, tumbaku, katani na chikichi ambayo yamekuwa yakitegemewa katika kuinua uchumi wa wakulima na Taifa kwa ujumla.

Hivi karibuni kumetokea hali ya sintofahamu kuhusiana na suala ununuzi wa zao hilo baada ya kutangazwa kwa bei elekezi ambayo ni sh. 1,200 kwa kilo moja katika mikoa yote inayozalisha zao hilo.

Bei elekezi ya pamba kwa msimu huu ilitangazwa Aprili 30, 2019 mkoani Shinyanga na kwamba bei hiyo ilitakiwa ianze kutumika kuanzia Mei 2, 2019. Hata hivyo ununuzi wa zao hilo ulianza kwa suasua jambo ambalo Serikali haikuridhishwa nalo.

Jumapili ya Julai 14, mwaka huu ndipo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliamua kuitisha kikao kilichojumuisha wakuu wa mikoa 11 inayolima pamba, wanunuzi wa zao hilo, taasisi mbalimbali za kifedha pamoja na Gavana wa Benki Kuu.

Kikao hicho kilichoitishwa na Waziri Mkuu na kufanyika katika ukumbi wa Mtemi Isike Mwanakiyungi kilikuwa na lengo la kutafakari mwenendo wa zao la pamba ambalo ununuzi wake unaendelea lakini kwa kasi ndogo.

Waziri Mkuu baada ya kusikiliza changamoto za wanunuzi ambao wengi wao waliomba Serikali iwadhamini katika taasisi mbalimbali za fedha walizoomba mikopo kwa ajili ya kununua zao hilo kwa kuwa ilikuwa imekwama. Serikali iliwakubalia.

“Sasa tumefikia muafaka wa jambo hili kibali kitatoka na wote watakaopata dhamana ya mikopo hakikisheni fedha hizo zinaenda kutumia kwa ajili ya ununuzi wa pamba kama ilivyokusudiwa na si vininevyo.”

Hivyo, Waziri Mkuu aliwaagiza wakuu wa mikoa na wilaya katika maeneo yote yanayolima pamba wawasimamie ipasavyo wanunuzi wote ili kuhakikisha fedha zitakazopatikana zinakwenda kutumika kwa ajili ya kununulia pamba.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wanunuzi Binafsi wa Pamba (TCA), Bw. Christopher Gachuma aliishukuru Serikali kwa kukubali kuwadhamini pamoja na Waziri Mkuu kwa maelekezo aliyoyatoa kuhusu suala la ununuzi wa zao hilo.
 
Waziri Mkuu, baada ya kufanya kikao na wadau wa pamba wakiwemo na wanunuzi ambao walikubali kwenda kununua pamba iliyoko kwa wakulima, Julai 15, 2019 alifanya ziara katika wilaya ya Igunga kwa lengo la kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao la pamba.

Akiwa katika ziara hiyo, Waziri Mkuu alianza kwa kukagua ghala la ununuzi wa pamba la AMCOS ya Mbutu na kisha alikwenda katika kijiji cha Mwabakina na kukagua ghala la kununulia pamba la Mwabakima.

Baada ya kukagua maghala hayo Waziri Mkuu alizungumza na wananchi wa maeneo hayo ambao wengi wao ni wakulima wa pamba ambapo aliwahakikishia kwamba hadi kufikia tarehe 30 mwezi Julai mwaka huu pamba yote iliyoko katika mikoa mbalimbali nchini itakuwa imeshanunuliwa na wakulima wote kulipwa fedha zao.

Alisema Serikali imeamua kuingilia kati suala la ununuzi wa zao la pamba kutokana na kusuasua kwa soko lake kwa kutoa dhamana ili kuwawezesha wanunuzi kukopeshwa fedha na benki mbalimbali kwa ajili ya kununulia pamba kutoka kwa wakulima.


“Tunatambua adha mliyoipata tangu kuanza kwa msimu wa mwaka huu na hayo ni mapito tu. Nawasihi muwe na amani kwani Serikali yenu inafuatilia suala hili na Rais Dkt. John Magufuli anataka kuona pamba yote inatoka kwa wakulima ili kuwawezesha kupata tija.”

Kadhalika, Waziri Mkuu aliwasihi wakulima wa zao hilo la pamba na wakulima wa mazao mengine nchini wahakikishe mara baada ya kuuza mazao yao wanatenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kununulia pembejeo watakazozitumia katika msimu ujao.

Wananchi kwa upande wao waliishukuru Serikali kwa hatua yake ya kuingilia kati suala la ununuzi wa zao la pamba pamoja na malipo kwa wakulima ambao tayari pamba yao walishaipeleka katika AMCOS zao.

Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga alisema Serikali itahakikisha inaendelea kutafuta masoko ya mazao hayo ndani na nje ya nchi ili kuwawezesha wakulima kuwa na uhakika wa masoko kwa mazao yao na hivyo kujiongezea tija.

Pia, Waziri huyo alisema mbali na kutafuta masoko, Serikali imedhamiria kufufua viwanda mbalimbali vya nguo hapa nchini ili kuwawezesha wakulima wa zao la pamba kuwa na soko la uhakika. “Kuhusu suala la maghala tunatambua tatizo hilo na tutahakikisha tunayaboresha ili pamba iweze kuhifadhiwa katika mazingira bora”.

Akizungumzia kuhusu changamoto ya viuatilifu, Waziri Hasunga alisema Serikali itahakikisha vinapatikana kwa kuzingatia eneo husika ili kuweza kudhibiti wadudu waharibufu.

(MWISHO)

MFUNGWA Amshtaki ASKARI Kwa Rais MAGUFULI

$
0
0
Leo July 16, 2019 Rais Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Butimba Mkoani Mwanza kusikiliza kero za Wafungwa.

Mmoja wa wafungwa anayetumikia kifungo cha miaka 30, Kalikenya Nyamboge, amemtuhumu Ofisa Usalama gerezani hapo kuwapa wafungwa simu halafu zikikamatwa wananyan’ganywa vitu vyao walivyo navyo lakini hadi leo hajafanywa kitu chochote.

“Mheshimiwa rais, huyu ofisa akupe mihuri na hizo simu uondoke nazo utajua mwenyewe utaenda kufanyia nini na ikibidi ondoka naye kwani ukifanya hivyo utakiwa umetusaidia sana na ukimuacha atanidhuru.

“Sasa hivi Jenerali Kamishna ametuletea daktari msomi na alivyofika vifo ndiyo vimepungua maana walikua wakikuchoma sindano wanakuua.

“Na si mara ya kwanza wao kuua mimi nilikuwa nimepanga nikitoka nije kukwambia na nikitoka nitakuletea mambo yote yanayotokea huku lakini huyu usimuache maana kwa Mwenyezi Mungu utakua umeandika maelezo ya mauji,” amesema Nyamboge.

Naye mfungwa mwingine Kulwa Alphonce, alikamatwa mwaka 2017 akiwa na mafuta ya dizeli akapelekwa Kituo cha Nyegezi askari wakamuomba Sh milioni moja, akawaambia ana 200,000 tu ambayo walikataa kisha baadaye wakampeleka ‘central’ baada ya hapo akafunguliwa kesi ya mauaji.

Aidha, mfungwa mwingine Shukrani Masegenya, alimuomba Rais Magufuli kuwapunguzia adhabu ya vifungo ili wakatumie ujuzi wao wanaofundishwa nje.


Akizungumza baada ya kuwasikiliza wafungwa na askari magereza , Rais Magufuli amesema kufika kwake gerezani hapo kuna somo kubwa limemuingia na akwenda kulifanyia kazi.

"Niliyoyasikia lazima nifanyie kazi, nimesikia changamoto za wafungwa na nimesikia pia changamoto za askari wangu.Niahidi nitayafanyia kazi yote ambayo nimeyasikia kwenu wote,"amesema Rais Magufuli na kuongeza hayuko tayari kuona askari magereza wanalalamika wakati yeye yupo.

Rais Magufuli amefafanua kwenye gereza hilo la Butimba amegudua mambo mengi , amebaini kuna kuombwa rushwa wafungwa na mahabusu na uamuzi wake wa kufika hapo umetokana na kufahamu mambo mengi ambayo mengine wafungwa wameshindwa kueleza.

Amewahakikishia wafungwa hao kwamba amewaelewa wafungwa na mahabusu hao na kuahidi kuwa amewasikia na yote ambayo ameleezwa yatafanyiwa kazi."Niahidi nimewasikia, nimewasikia na yote nitayafanyia kazi.Naomba muwe wavumilivu na niaminini."

Rais Magufuli amesema hata walioko uraiani ni wafungwa au mahabusu wabadae na kwamba kufungwa au kuwa mahabusu haina maana ya kukosa haki za kibinadamu.

Viwanja Vyenye huduma zote Vinauzwa: Bunju na Mapinga (Baobab sec)

$
0
0
Viwanja Vyenye huduma zote Vinauzwa: Bunju na Mapinga (Baobab sec)

Viwanja vizuri sana, vina umeme na maji, na majirani wa maana. Vipo mtaa wa Kimele B umbali mdogo kutoka Baobab sec...
Viko umbali wa mita 400 tu kutoka barabara kuu ya Mapinga to Kibaha, ambayo imepewa kiwango cha Lami.

Viwanja viko 6 tu, vipo vya 20/25 mita kwa tsh 8m, 25/28 kwa tsh 11m, sqm 2000 kwa tsh 25m na sqm 2400 kwa tsh 30m. Wahi upate kiwanja bora cha makazi au biashara.

Na Bunju kipo kiwanja cha 25/25 kwa tsh 20m na sqm 1750 kwa tsh 51m

Kwa taarifa zaidi, call 0758603077 au whatsap 0757489709

Yaliyojiri Leo wakati Rais Magufuli alipokagua maendeleo ya ujenzi wa chelezo na ukarabati wa meli 5 za ziwa Victoria katika Bandari ya Mwanza. https://t.co/5dTsFBOUvz

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 5 kuanzia leo July 16, 2019 kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Wizara ya Fedha na Mipango kuhakikisha vifaa vya ujenzi wa chelezo ya kujengea meli na vifaa vya ukarabati wa meli vilivyokwama katika Bandari ya Dar es Salaam kutokana na mchakato wa kikodi vinafikishwa katika Bandari ya Mwanza.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo alipotembelea Bandari ya Mwanza kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa chelezo, ukarabati wa meli 5 na ujenzi wa meli mpya katika Ziwa Victoria yanayofanywa na kampuni 2 za ukarasi kutoka Jamhuri ya Korea kwa gharama ya shilingi Bilioni 152 kwa ajili hiyo.

Akiwa bandarini hapo, Rais Magufuli ameeleza kutofurahishwa na ucheleweshaji wa takribani mwezi mmoja wa makontena 58 yenye vifaa vya ujenzi vilivyoagizwa na kampuni za ukandarasi za Korea Total Marine Innovation (KTMI) na STX JV SAEKYUNG Construction Ltd za Korea kwa sababu ya kusubiri msamaha wa kodi na amemtaka mkandarasi huyo aache visingizio.

Meneja wa mradi wa ujenzi wa chelezo na ukarabati wa meli Mhandisi Abel Gwanafyo amesema ujenzi wa chelezo pamoja na ukarabati wa meli ya MV Victoria na Mv Butiama umepangwa kukamilika ifikapo Machi 2020.

Kuhusu ujenzi wa meli mpya Meneja Mradi wa ujenzi wa Meli hiyo Mhandisi Vitus Mapunda amesema maandalizi ya vifaa vya meli hiyo itakayokuwa na uwezo wa kubeba tani 400 za mzigo, abiria 1,200 na magari makubwa na madogo 23 yanayohusisha usanifu, ukataji wa vyuma, injini 2 na majenereta 3 yamefikia asilimia 35 na kwamba makontena 300 yenye vifaa hivyo yatawasili nchini Septemba 2019 kutoka nchini Korea.

Baada ya kukagua hali ya meli ya Mv Victoria na Mv Butiama ambazo ukarabati wake umeanza, Rais Magufuli namewasalimu wafanyakazi walioajiriwa katika mradi huo na kuwaagiza wakandarasi kuhakikisha wanalinda maslahi yao na sheria za usalama kazini kuzingatiwa.

Pia Rais Magufuli ameagiza mitambo miwili ya kunyanyulia mizigo (Cranes) iliyokuwa imeuzwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kurejeshwa mara moja.

Ufafanuzi Kuhusu Taarifa Zilizoandikwa Kwenye Magazeti Na Mitandao Ya Kijamii Kuhusu Uwepo Wa Dawa Mpya Ya Asili Inayotibu Saratani Ya Tezi Dume

$
0
0
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ilianzishwa kwa sheria ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Namba 23 ya mwaka 1979. NIMR ni taasisi chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Taasisi hii pamoja na kufanya utafiti, inaratibu, inakuza na kusimamia tafiti za afya zinazofanyika nchini na kukuza matumizi ya matokeo ya tafiti hizo.

NIMR ina idara ya tafiti za tiba asili ambayo jukumu lake ni kufanya utafiti juu ya dawa za miti-shamba, ambazo nyingine zimekuwa zinatumika miaka mingi na bibi na babu zetu. Idara ya tafiti ya dawa asilia mwaka huu iliiwakilisha NIMR kwenye maonesho ya Sabasaba katika banda la Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Lengo la kushiriki katika maonesho haya ni kuonesha ubunifu katika tafiti za afya zinazofanyika NIMR. Waandishi wa habari walimhoji mtafiti wa NIMR katika banda la COSTECH na wameripoti kwamba NIMR imegundua dawa ya kutibu saratani ya tezi dume. Kutokana na uzito wa suala hili na kuzingatia mateso ya wagonjwa wenye tezi dume NIMR ingependa kufafanua na kurekebisha taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari na kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Ni kweli kwamba moja ya dawa za miti-shamba ambazo NIMR imetengeneza imeonesha dalili ya kupunguza uvimbe kwa wagonjwa wenye tatizo la kuvimba tezi dume. Dawa hii haijaonesha uwezo wa kutibu saratani ya tezi dume. Dawa hii bado iko katika hatua ya uchunguzi wa kitafiti. Lengo letu la kushiriki katika maonesho ya Sabasaba lilikuwa ni kuonesha ubunifu katika tafiti za afya.

Baadaye kama tafiti hizo zitakuwa na matokeo mazuri zinaweza kutumika baada ya kufuata hatua za kisheria za usajili. Tunaomba radhi kwa wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na ripoti hiyo iliyokuwa inasambaa.

Taarifa imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu
3 Barabara ya Barack Obama
S.L.P. 9653, Dar es Salaam
Simu: +255 22 2121400; Barua pepe: dg_office@nimr.or.tz

Huyu Ndo Mrithi wa Tundu Lissu Aliyepitishwa na Kamati Kuu ya CCM Leo

$
0
0
Chama cha Mapinduzi, CCM kimemteua Miraji Mtaturu kuwa mgombea ubunge wa Singida Mashariki.

Taarifa iliyotolewa na katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole imesema kikao cha Kamati Kuu kimekutana leo Jumanne Julai 16, 2019 chini ya Mwenyekiti wake, Rais John Magufuli jijini Dodoma kikiwa na agenda moja.

Polepole amesema agenda hiyo ilikuwa ni ya maandalizi ya uchaguzi huo kwa kuteua jina la mgombea ambapo Mtaturu ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya (DC) ya Ikungi mkoani Singida ndiye aliyeteuliwa.

Uchaguzi katika jimbo hilo utafanyika Julai 31, 2019 kujaza nafasi iliyoachwa na Tundu Lissu ambapo ilielezwa na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kwamba amepoteza sifa.



Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano 17 July

Raia wa Misri Kortini kwa Tuhuma za Kutorosha Madini yenye Thamani ya Milioni 12

$
0
0
Hany Ahmed (27)  ambaye ni raia wa Misri amefikishwa  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka moja la kutorosha madini aina ya diamond  yenye thamani zaidi ya Sh. Milioni 12.

Akisoma hati ya mashtaka  jana July 16, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba,  Wakili wa Serikali Wankyo Simon alidai,  Julai 10, mwaka huu huko katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wilaya ya Ilala jijini  Dar es Salaam mshtakiwa  alikutwa akisafirisha madini ya diamond yenye uzito wa carats 11:12 ambayo yana thamani ya Dora za Kimarekani 5,238 sawa na Sh. 12,050,131bila ya kuwa na kibali.

Hata hivyo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi. 

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na  kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 30, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa, mshtakiwa amerudishwa rumande.

Prof. Kabudi akutana na Mabalozi wa Nchi za SADC

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) waliopo hapa nchini.

Katika mazungumzo hayo Prof. Kabudi amewafahamisha hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya Mkutanao ya wakuu wa nchi na Serikali wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliyopangwa kufanyika nchini mwezi Agosti 2019

Kwa upande wa waheshimiwa Mabalozi hao walifurahishwa kwa hatua ya maandalizi iliyofikiwa, na kuelezea furaha yao kuhusu uwamuzi wa Serikali kuwashirikisha mapema katika maandalizi hayo.

Tanzania kuwasilisha Umoja wa Mataifa taarifa ya Mapitio ya Hiyari ya Utekelezaji wa Malengo Endelevu.

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akifuatilia ufunguzi wa mikutano ya Jukwaa la Juu la Kisiasa la Ngazi za  Mawaziri  chini ya Umoja wa Mataifa inayofanyika New York nchini Marekani. Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. John Jingu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo.

Waziri Mpango anatarajiwa kuwasilisha kwa mara ya kwanza taarifa ya Tanzania ya  Mapitio ya Hiyari ya Utekelezaji wa Malengo Endelevu.

Viwanja Vyenye huduma zote Vinauzwa: Bunju na Mapinga (Baobab sec)

$
0
0
Viwanja Vyenye huduma zote Vinauzwa: Bunju na Mapinga (Baobab sec)

Viwanja vizuri sana, vina umeme na maji, na majirani wa maana. Vipo mtaa wa Kimele B umbali mdogo kutoka Baobab sec...
Viko umbali wa mita 400 tu kutoka barabara kuu ya Mapinga to Kibaha, ambayo imepewa kiwango cha Lami.

Viwanja viko 6 tu, vipo vya 20/25 mita kwa tsh 8m, 25/28 kwa tsh 11m, sqm 2000 kwa tsh 25m na sqm 2400 kwa tsh 30m. Wahi upate kiwanja bora cha makazi au biashara.

Na Bunju kipo kiwanja cha 25/25 kwa tsh 20m na sqm 1750 kwa tsh 51m

Kwa taarifa zaidi, call 0758603077 au whatsap 0757489709
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images