Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Sera Ya Viwanda Yasaidia Kupunguza Tatizo La Ajira

$
0
0
MKAZI wa kijiji cha Kabanga wilayani Kasulu mkoani Kigoma, Leonard Nkamba anayejishughulisha na uchongaji wa vyombo mbalimbali vya jikoni ameishukuru Serikali kwa kuanzisha sera ya viwanda kwa kuwa imesaidia kupunguza tatizo la ajira nchini.

Ameyasema hayo leo  (Jumapili, Julai 14, 2019) baada ya kukabidhiwa kiasi cha sh. milioni 2.5 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ili aweze kuongeza mashine itakayomuwezesha kuchonga bidhaa zenye ubora zaidi. Makabidhiano hayo yamefanyika mjini Kigoma.

Bidhaa anazochonga ni vikombe, chupa za chai, hot pot kwa kutumia mti aina ya jakalanda. Mbali na kutengeneza vyombo hivyo, pia mjasiriamali huyo ambaye ameajiri vijana watatu anachonga vibao na kuandika ujumbe mbalimbali kwa kutumia unga wa ngano.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa fedha hizo na Waziri Mkuu, mjasiliamali huyo amesema anaushukuru Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ambao uliona kazi zake na kumuagiza atengeneze seti za vyombo kwa ajili ya zawadi za kumpelekea Rais Dkt. John Magufuli.

“Uongozi wa UWT mkoa wa Kigoma Taifa ulivutiwa na kazi zangu na kuniagiza nitengeneze chupa ya chai, vikombe na hot pot kwa ajili ya kumpa zawadi Mheshimiwa Rais pamoja na Waziri Mkuu ndipo Waziri Mkuu jana aliona kazi zangu na akavutiwa na bidhaa ninazotengeneza ndipo akaniuliza kama kuna changamoto zinazonikabili nikamwabia nahitaji mashine moja yenye thamani ya sh. milioni mbili na nusu akasema umepata na leo sijaamini alivyoniita na kunikabidhi. Namshukuru sana.”

Nkamata ametumia fursa hiyo kuwashauri wananchi wengine hususani vijana waache kulalamikia suala la ukosefu wa ajira na badala yake wajiunge katika vikundi vya ujasiriamali na kuzalisha bidhaa mbalimbali ambazo wataziuza na kujipatia kipato.

Pia amewaomba Watanzania wajenge utamaduni wa kutumia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na viwanda vya ndani kwa kuwa vina ubora wa kutosha na pia watakuwa wanachangia kukuza uchumi wa wajasiriamali na Taifa kwa ujumla. Amesema bidhaa anazotengeneza ni rafiki wa mazingira kutokana na malighafi anazotumia.

Kwa upande wake Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi kujishughulisha na shughuli mbalimbali za ujasiriamali ili waweze kujipatia kipato na kuondokana na umasikini. Pia amesema Serikali ipo tayari wakati wowote watakapohitaji msaada.

Waziri Mkuu amempongeza mjasiriamali huyo  kwa bidhaa mbalimbali anazotengeneza ambazo ni nzuri na za kipekee. Amesemma amefurahi kuona vikombe, chupa za chai pamoja na hot pot zilizotengenezwa na Mtanzania kwa kutumia miti.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Lugola Aagiza Polisi Kuwasaka Wanaotoa Taarifa Za Uongo Kutekwa, Kupotea Kwa Watu Nchini

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Mwibara (MOHA)
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amelitaka Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwafunguliwa mashtaka wanaosambaza taarifa za uongo, ambazo zinatengenezwa kuhusu matukio ya utekaji na kupotea watu wakiwa na lengo la kuichafua taswira ya Serikali.

Lugola amesema baadhi ya watu hao ambao wana nia mbaya ya nchi,  wanakaa mitandaoni kuanzia asubuhi hadi jioni wakizusha matukio hayo machafu wakiwa na lengo la kujipatia umaarufu wa kisiasa kwa kuichonganisha Serikali Rais Dkt. John Magufuli na wananchi wake, ambayo inaendelea kufanya kazi nzuri kwa kuiletea nchi maendeleo kwa kasi zaidi.

Waziri Lugola ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara alipokuwa anajibu maswali mbalimbali ya wananchi wa Mji Mdogo wa Kisorya, Kata ya Kisorya, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo, ambapo mmoja wa wananchi hao alimuuliza Waziri huyo kuhusu Wizara yake imejipangaje kuyasambaratisha matukio ya utekaji, kupotea watu hususani tukio la kupotea kwa mwandishi wa habari.

“Lazima tuwe na uchungu na taifa hili, taarifa hizi zinazoripotiwa na watu kupotea ama kutekwa zipo katika makundi mawili, moja ni taarifa za uongo, za kutengeneza, wakiwa na lengo la kujipatia umaarufu wa kisiasa, wakiropoka hovyo, na miongoni mwa watu hao wanaodaiwa kutekwa ama kupotea, wengine tumewabaini wanajiteka wenyewe, wanajipoteza wenyewe, na kuna wengine wameshafikishwa mahakamani kwa kutoa taarifa za uongo kuwa wametekwa, au kupotea,” alisema Lugola na kuongeza;
“Siku hizi kupitia mitandao ya kijamii, kuna watu wanatunga matukio ya uongo, wanatengeneza matukio ya kutekwa na kupotea, ndugu zangu Watanzania, taarifa hizi zinaweza kuigawa taifa, kusababisha machafuko na kusababisha taharuki katika jamii.”

Lugola pia amesema, kuna baadhi ya taarifa za kweli na Serikali inakubali yapo matukio ya mtu kuweza kupotea au kutekwa, na hata kutoonekana katika familia yake, hiyo haipingwi na Serikali inakubali yapo, lakini pia wapo ambao wanakua kweli wamepotea ama kutekwa, serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama hususani Jeshi la Polisi, limekua likiendelea kuwatafuta watu hao, na wakati linapoendelea kuwatafuta Jeshi linahitaji pia taarifa za wananchi kuwezesha kuwapata watu hao.

“Ndugu wananchi, pia kuna taarifa za upotoshaji kwa watu wanaodaiwa kupotea au kutekwa kweli, lakini wengine wanasambaza taarifa za uongo, tumekuwa tukishuhudia katika baadhi ya migodi ya madini, wakitatafuta utajiri, lakini majumbani kwao walishafanya mpaka matanga wakiamini ndugu yao alishafiriki kwa kutekwa au kupotea, kumbe anatafuta utajiri machimboni,” alisema Lugola.

Alisema Serikali yoyote duniani ambayo imechukua dhamana ya kuwalinda wananchi wake halafu Serikali hiyo hiyo igeuke kuwateka na kuwaua, Serikali ya namna hiyo haipo duniani.

“Naelekeza Jeshi la Polisi, kwa wale ambao wanatunga maneno ya uongo na kuchonganisha Serikali na wananchi, muwasake popote walipo, muwakamate na muwafikishe katika vyombo vya sheria,” alisema Lugola.

Lugola alijibu swali hilo la kuhusu utekaji na upoteaji wa watu baada ya Mkazi wa Kisorya, Mnyaga Semba alipokuwa anataka kujua Serikali imejipangaje kukabiliana na matukio hayo.

“Mbunge wangu, wewe ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, nataka nijue kundi linaloteka watu, kushambulia watu,  na pia jambo hili tena limezuka juzi Waziri wetu wa Mambo ya Nje alipokuwa anahojiwa tukasikia jambo la mwandishi wa habari, Azory mara kazikwa mara hivi, naomba kujua Serikali imejipangaje kukabiliana na jambo hili?,” alisema Semba.

Aidha, Lugola alizungumzia kuhusu uhalifu katika ziwa Victoria, ambapo wananchi wananyang’anywa mashine, nyavu na samaki na wahalifu hao, kuwasababnishia wananchi umaskini, alilitaka Jeshi la Polisi kuwasaka wahalifu hao kwa kufanya operesheni za mara kwa mara katika maeneo hayo ya ziwa kwa lengo la kudhibiti uhalifu huo.

Pia Waziri huyo, alilitaka Jeshi hilo kutowasumbua waendesha bodaboda kwa kuwakamata hovyo barabarani na bodaboda hizo kuzihifadhi vituo vya polisi huku wamiliki wa vyombo hivyo wakiteseka kuzipata.

“Bodaboda akifanya makosa mpigeni faini, na apewe muda wa siku saba kulipa faini hiyo kama inavyokua katika faini za magari. Na nilishasema, bodaboda ambazo zinapaswa kuwepo kituoni ni za aina tatu tuu, ambazo zilizoshiriki uhalifu, zilizookotwa na zilizopata ajali, ndizo nilizoagiza ziwepo kituoni,” alisema Lugola.

Sakata La Kodi Ya Pango La Ardhi Lazidi Kuwa Chungu Kwa Baadhi Ya Kampuni Mwanza

$
0
0
Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amezidi kuzibana Taasisi na Makampuni yenye madeni makubwa ya kodi ya pango la ardhi ambapo ametua mkoani Mwanza na kuyabana makampuni na taasisi nane ambazo kwa ujumla wake zinadaiwa zaidi ya milioni 900.

Kampuni na taasisi alizotembelea Dkt Mabula ni Synergy Tanzania Ltd, Ideal Development Ltd, Birchard Oil Ltd, Shule za Musabe, Taasisi ya Taifa ya Utafiti Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Ndamavyo Auto Spares, Jesse & Company Ltd na Maabara ya Taifa ya Udhibiti Samaki na Mazao ya Uvuvi.

Akizungumza katika ziara yake hiyo ya kufuatilia madeni ya kodi ya pango la ardhi mwishoni mwa wiki, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema ziara hiyo anayoifanya ya kuwafikia wale wenye madeni makubwa inafuatia baadhi ya kampuni na taasisi zinazodaiwa kushindwa kulipa ama kurekebisha madeni yao baada ya kikao cha Juni 11, 2019 kilichowakutanisha wadaiwa zaidi ya 200 jijini Dodoma

katika mwanzo wa ziara yake kwenye shule za Musabe, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  alimueleza mmiliki wa shule hizo Daniel Musabe kulipa deni lake la kodi ya pango la ardhi linalofikia milioni 57.4 katika viwanja vyake vinne anavyomiliki kufikia tarehe 31 Julai 2019 ili kuepuka kufikishwa katika Baraza la Ardhi na Nyumba.

Hata hivyo, Mmiliki wa Shule hizo ambazo ni za Chekechea, Msingi na Sekondari alimueleza Dkt Mabula kuwa yuko tayari kulipa deni la kodi ya pango la ardhi lakini alishindwa kufanya hivyo kutokana na changamoto za kibiashara ambapo hata hivyo aliahidi kulipa kiasi anachodaiwa kuanzia Agosti 2019 na kumaliza deni lote ifikapo Desemba 2019.

Akiwa katika Kampuni ya Birchard Oil Limited, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Mabula ambaye aliambatana na Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizarani Denis Masami aliitaka kampuni hiyo kulipa kiasi inachodaiwa cha kodi ya pango la ardhi inayofikia milioni 85,235,050 ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya kodi za miaka ya nyuma.

Meneja uhusiano wa Kampuni hiyo inayojishughulisha na uzalishaji Mafuta na Marobota ya Pamba Arshad Jetha alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi kuwa kampuni yake pamoja na kudaiwa kodi ya pango la ardhi kwa baadhi ya viwanja inavyomiliki lakini baadhi yake alishalipia hivyo aliomba kuhakikiwa madeni yake ili kupata deni halisi.

Ideal Development Ltd kupitia Meneja wake Burnanuddin Rajbhai alikiri deni la kodi ya pango la ardhi linalofikia milioni 79 na kuomba kupewa muda wa kulipa katika awamu tatu tofauti. Hata hivyo, Naibu Waziri wa Ardhi alizitaka kampuni na Taasisi zilizokubali kulipa madeni  kuandika barua ya kueleza namna zitakavyolipa na muda wa mwisho wa kulipa madeni yao katika ofisi za ardhi za halmashauri husika na nakala za barua hizo ziende ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi wa Kanda ya Ziwa.

Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo aliionya kampuni ya Ideal Development Ltd kwa kushindwa kutekeleza makubaliano yaliyofikia ya kulipa deni lake na kuieleza kuwa hatua itakayofuata kwa kampuni hiyo ni kufikishwa katika Baraza la Ardhi na suala la kuingia makubaliano ya malipo haliwezi kufanyika kwa mara ya pili.

Kampuni ya Synergy Tanzania Ltd Kupitia kwa Meneja Utawala wake Florence Kivamba iliahidi kuandika barua ya makubaliano ya kulipa deni la milioni 43 inayodaiwa ingawa alioamba kufanya mawasiliano na uongozi wa juu kwa kuwa ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi ilikuwa ya kushtukiza na uongozi haukuwepo.

Akiwa katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Mabula aliueleza uongozi wa Taasisi hiyo kuwa inadaiwa jumla ya shilingi milioni 515,713,900 ya kodi ya pango la ardhi na taasisi hiyo haijawahi kulipa kodi hiyo tangu mwaka 1996.

Mkurugenzi wa NIMR mkoa wa Mwanza Safari Kinuhi alijitetea kwa kueleza kuwa taasisi yake inapaswa kusamehewa kulipa kodi ya pango la ardhi kwa kuwa haiko kibiashara bali inatoa huduma kwa wananchi na kuboresha afya ingawa aliahidi kuwasiliana na uongozi wa juu kuhusiana na suala hilo.

Hata hivyo, Dkt Mabula alimueleza kuwa Taasisi yake inapaswa kufuata sheria wakati wa kuomba kusamehewa kodi ya pango la ardhi huku Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizarani Denis Masami akisisitiza kuwa hata kama Taasisi hiyo itasamehewa kulipa kodi hiyo lakini deni la nyuma lazima lilipwe kwa kuwa sheria ya msamaha itaanza pale tamko la msamaha lilipotoka.

Maabara ya Taifa ya Udhibiti Samaki na Mazao ya Uvuvi iliyopo eneo la Nyegezi ilionekana kutokuwa na hati ya eneo inalomiliki ingawa Afisa Mfawidhi wa Taasisi hiyo Emanuel Mundoko alijitetea kwa kueleza kuwa awali Taasisi hiyo ilikuwa sehemu ya chuo cha Uvuvi na sasa inajitegemea hivyo hawajui madeni halisi wanayodaiwa.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu 15 July

Mzee Makamba, Kinana Watoa Tamko Zito Kupinga Kuchafuliwa Ndani ya CCM

Mapambano Ya Rushwa Yang’arisha Ofisi Ya Rais Na Ofisi Ya Waziri Mkuu

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema juhudi za Serikali za kupambana na rushwa, kudhibiti upotevu wa mapato, matumizi ya fedha za Serikali na kusimamia uwajibikaji kwa watumishi wa umma ni sababu zilizowezesha Ofisi ya Rais pamoja na Ofisi ya Waziri  kuaminika zaidi.

Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na viongozi wa Umoja wa Wanake Tanzania (UWT)  akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma. Amesisitiza kuwa vita dhidi ya rushwa ni endelevu.

Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya rushwa ambapo kwa Afrika Tanzania inaongoza kwa mujibu wa ripoti ya taasisi ya Transparency Internation iliyotolewa hivi karibuni.

Ripoti hiyo mpya iliyotolewa Julai 11, mwaka huu inaonesha kwamba kwa sasa Tanzania inaongoza katika nchi 35 za Afrika  baada ya kupungua kwa vitendo vya rushwa katika sekta nyingi, ambapo Ofisi ya Rais na Ofisi ya Waziri Mkuu zimeonekana kuaminika zaidi.

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwatahadharisha watumishi wa umma kwamba Serikali kamwe haitomvumilia mtumishi atakayebainika  anayejihusisha na vitendo vya rushwa na aliwataka wahakikishe kuwa wanatekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi bila ubaguzi.

Waziri Mkuu amesema Serikali imejipanga vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa, hivyo amewataka wananchi wasisite wakati wote kutoa taarifa kwa vyombo husika pale watakapobaini uwepo wa watumishi wanaojihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa.

“Watumishi wa umma wanatakiwa kutambua kwamba jukumu lao kubwa ni kuwatumikia wananchi kwa kuzingatia maadili na kanuni za utumishi wa umma zilizowekwa kwa mujibu wa sheria na kanuni na si vinginevyo. Serikali hii kamwe haitowaonea haya au kuwafumbia macho watumishi wa hovyo.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kuwa suala la kuwaondoa kazini watumishi wazembe, wasiotimiza wajibu wao ipasavyo pamoja na wale wasiozingatia maadili ya utumishi wa umma ni endelevu kwa sababu Serikali inahitaji watumishi wa umma wenye heshima na nidhamu ya kazi.

Suala la kuwapokea, kuwasikiliza na kuwahudumia wananchi katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma kwa wananchi zikiwemo ofisi za Serikali kuanzia ngazi ya kijiji hadi Taifa ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Tano, hivyo watumishi wa umma wanapaswa kuzingatia jambo hilo.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Kaka Amuua Dada Yake Baada Ya Kumfumania Nyumbani Kwao

$
0
0
NA SALVATORY NTANDU
Mkazi wa  kijiji cha Bugoshi,kata ya Uyogo halmashauri ya  Ushetu Daudi Bundala anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma ya  kumua dada yake Suzana Bundala(21) kwa kumpiga kitu kizito kichwani na kumsababishia kifo,baada ya kumkuta akiwa amelala na mpenzi wake nyumbani kwao.

Kamanda wa  polisi mkoa shinyanga (ACP) Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nakusema tukio hilo lilitokea julai 12 mwaka huu saa tano usiku katika kijiji cha Bugoshi,kata ya Uyogo tarafa ya Mweli wilaya ya kipolisi Ushetu.

Amesema, chanzo cha tukio hilo ni marehemu kukutwa akiwa na mpenzi wake aliyefahamika kwa jina la  Eddy Nkimbila nyumbani kwao kitendo kilichomchukiza Daudi na kumshambulia dada yake na kumsababishia kifo.

Amefafanua kuwa baada ya kumshambulia dada yake na kumsababishia kifo Daudi  alikimbia mara baada ya tukio hilo na juhudi za kumtafuta na kumkamata zinaendelea nakuongeza mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa taratibu za mazishi.

Hata hivyo Kamanda  Abwao ametoa wito kwa wananchi Mkoani Shinyanga kuacha mara moja tabia ya kuendelea kujichukulia sheria mkononi na kufikia maamuzi ya kufanya matukio vya kikatili ambayo yanaweza kusababisha wakachukuliwa hatua za kisheria.

Ufafanuzi Kuhusu Taarifa Zilizoandikwa Kwenye Magazeti Na Mitandao Ya Kijamii Kuhusu Uwepo Wa Dawa Mpya Ya Asili Inayotibu Saratani Ya Tezi Dume

$
0
0
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ilianzishwa kwa sheria ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Namba 23 ya mwaka 1979. NIMR ni taasisi chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Taasisi hii pamoja na kufanya utafiti, inaratibu, inakuza na kusimamia tafiti za afya zinazofanyika nchini na kukuza matumizi ya matokeo ya tafiti hizo.

NIMR ina idara ya tafiti za tiba asili ambayo jukumu lake ni kufanya utafiti juu ya dawa za miti-shamba, ambazo nyingine zimekuwa zinatumika miaka mingi na bibi na babu zetu. Idara ya tafiti ya dawa asilia mwaka huu iliiwakilisha NIMR kwenye maonesho ya Sabasaba katika banda la Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Lengo la kushiriki katika maonesho haya ni kuonesha ubunifu katika tafiti za afya zinazofanyika NIMR. Waandishi wa habari walimhoji mtafiti wa NIMR katika banda la COSTECH na wameripoti kwamba NIMR imegundua dawa ya kutibu saratani ya tezi dume. Kutokana na uzito wa suala hili na kuzingatia mateso ya wagonjwa wenye tezi dume NIMR ingependa kufafanua na kurekebisha taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari na kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Ni kweli kwamba moja ya dawa za miti-shamba ambazo NIMR imetengeneza imeonesha dalili ya kupunguza uvimbe kwa wagonjwa wenye tatizo la kuvimba tezi dume. Dawa hii haijaonesha uwezo wa kutibu saratani ya tezi dume. Dawa hii bado iko katika hatua ya uchunguzi wa kitafiti. Lengo letu la kushiriki katika maonesho ya Sabasaba lilikuwa ni kuonesha ubunifu katika tafiti za afya.

Baadaye kama tafiti hizo zitakuwa na matokeo mazuri zinaweza kutumika baada ya kufuata hatua za kisheria za usajili. Tunaomba radhi kwa wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na ripoti hiyo iliyokuwa inasambaa.

Taarifa imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu
3 Barabara ya Barack Obama
S.L.P. 9653, Dar es Salaam
Simu: +255 22 2121400; Barua pepe: dg_office@nimr.or.tz

NEMC Latoa Ufafanuzi Kuhusu Kelele Chafuzi

Rais Magufuli Azindua Nyumba Za Makazi Ya Askari Wa Jeshi La Polisi Mkoani Geita

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugora watatu kutoka kulia, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, Wabunge pamoja na Viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Nyumba za Makazi ya Askari Polisi katika eneo la Magogo mkoani wa Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wakati akitoka kukagua moja ya nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita.
  Makamishna kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini wakifurahia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa sherehe za uzinduzi wa Nyumba za makazi ya Askari Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita.
 Bendi ya Jeshi la Polisi ikitumbuiza katika sherehe za uzinduzi wa nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita.
 Sehemu ya Mradi wa  nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita ambao umezinduliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo la Magogo mkoani Geita.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Geita mara baada ya  kuhutubia katika uzinduzi wa nyumba hizo za makazi ya Askari Polisi. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Geita wakati akielekea kuzindua nyumba za Askari wa Jeshi la Polisi mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Katoro na Buseresere hawaonekani pichani wakati akielekea Geita mjini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Bwanga wakati akitokea Chato mkoani Geita. PICHA NA IKULU

Gari Yapinduka Na Kusababisha Majeruhi Na Uharibifu Wilaya Ya Rungwe

$
0
0
Mnano tarehe 14/07/2019 majira ya saa 09:00 huko Kanyegele kata ya kiwira tarafa ya Ukukwe wilaya ya Rungwe. Barabara ya kuu ya TUKUYU – MBEYA, Gari na. T. 359 DCA/T. 429 CMH Aina ya Howo mali ya kampuni ya “Overland” iliyopo “Dsm” ikiendeshwa na RAJAB S/O ISSA [40] ikiwa imebeba mafuta aina ya Petrol na Diesel kuelekea Tukuyu iliacha njia na kupindukia kolongoni na kusababisha uharibifu  wa mali na mafuta kumwagika baada ya “Tank” kupasuka. Aidha  msaidizi wa dereva aitwaye SALUMU S/O SAID[40] amepata majeraha. Chanzo cha ajali ni ubovu wa matairi ya gari hiyo.
 
Natoa wito kwa wananchi kutosogea maeneo ya ajali bila kuchukua tahadhari, kwani madhara ya kufanya hivyo ni kupata ulemavu wa viungo, au kupoteza maisha kutokana na hatari mbalimbali kama milipuko ya mafuta.
 
AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO- WILAYA YA MBALIZI.
 
Mnamo tarehe 14.07.2019 majira ya saa 20:30 u0siku, CHRISTINA D/O ANTHONY @ MWALINGO [37] aligongwa na gari huko katika Kata Inyala, Tarafa Tembela, Wilaya Kipolisi Mbalizi, Mkoa Mbeya, barabara ya Mbeya – Njombe na kusababisha kifo chake papohapo.  Gari na dereva hajafahamika. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Igawilo. Ufuatiliaji kumkamata dereva na gari unaendelea.
TUKIO LA MAUAJI -WILAYA YA MBEYA.
 
Mnamo tarehe 14.07.2019 majira ya saa 09:00 asubuhi huko meneo ya mtaa wa Mponja  Kata ya Igawilo, Tarafa Iyunga, Jijini Mbeya, mtu mmoja ambaye amefahamika kwa jina la MARIA D/O FAUSTINE@KISANJI [22] Mkazi wa Mwanyanje alikutwa  amefariki dunia kwenye Pagala linalomilikiwa na mtu aitwaye ESTER D/O JOHN @MWANSHEMELA
 
Inadaiwa kuwa marehemu alikuwa mhudumu wa Bar itwayo SIKALAMANGA inayomilikiwa na DOMINICK S/O ABRAHAM.Ambapo mnamo tarehe 13/07/2019 majira ya saa 23:00 usiku marehemu aliondoka na  mtu asiyefahamika/jinsia ya kiume ambaye alikuwa anakunywa naye pombe. Kiini cha tukio ni ugomvi wa kimapenzi kati ya wawili hao. Msako mkali  unaendelea ili kubaini na kumkamata aliyehusika katika tukio hilo.
 
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu  na wahalifu kwa kuweka mkazo zaidi katika kutoa elimu. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa usalama hali inayopelekea kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu pamoja na ajali za barabarani.
 
WITO:
Natoa wito kwa jamii kuacha, kujihusisha na vitendo vya kihalifu na kujishughulisha na kazi halali kwa ajili ya kujipatia kipato. Ni rai yangu kwa  wananchi/Madereva wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuchukua tahadhari pindi wanapokuwa katika barabara zenye miteremko mikali, na milimani kwani ajali nyingi hutokea maeneo hayo na kusababisha madhara makubwa kwa jamii.

Imesainiwa na:

 [ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Atiwa Mbaroni Kwa Kukutwa na laini za simu 141 zenye usajili wa majina ya watu wengine.

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja MWAKILA S/O ALLY [32], mkazi wa Mwambene, Jijini Mbeya  kwa tuhuma za kupatikana na laini za simu [141] zenye usajili wa majina ya watu wengine.
 
Mnamo tarehe 12/07/2019 majira ya saa 13:00 mchana huko mtaa wa Itongo kata ya Mwambete tarafa ya Iyunga. Mtuhumiwa ambaye pia ni fundi umeme baada ya kukamatwa na kuhojiwa alikiri kumiliki laini hizo za simu 141 za mitandao tofauti zilizosajiliwa kwa majina tofauti ikiwemo “HALOTEL” laini 13, TIGO laini 29, TTCL laini 01, VODACOM laini 78 na AIRTEL laini 20. Pia alikutwa akiwa na vocha zilizotumika  za Vodacom 05, Tigo 04, Airtel 48, Halotel 03 pamoja na simu Itel 03, “Oking” 01 na “Hotwave” 01.
 
Chanzo ni kujipatia kipato. Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
 
       Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Katazo La Magogo Buchani Kuwa Changamoto Dodoma

$
0
0
Na. Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Wafanyabiashara wa Nyama jijini Dodoma wamesema kuwa  katazo la utumiaji magogo katika ukataji wa  nyama  Ifikapo Septemba 30,2019   katika bucha itakuwa ni changamoto kubwa kwao.

Baadhi ya  wafanyabiashara Wanyama katika soko kuu la Majengo  Mkoani  Dodoma wamesema  utumiaji wa  Magogo katika ukataji wa nyama walishaizoea  enzi na enzi  hivyo katazo  la Magogo ya kukatia  nyama buchani itakuwa changamoto kunbwa kwao.

Anna Francis na Juma Abbas ni miongoni mwa wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara ya nyama katika soko kuu la Majengo ambapo wamesema katika utumiaji  wa Mashine za kukatia nyama patakuwepo na changamoto hususan umeme unapokatika huku changamoto zingine ni  chembechembe ya vyuma.

Changamoto nyingine ambazo wamezitaja ni  gharama ya kumudu hizo mashine  kwa urahisi wa kupatikanaji kwani mara nyingi hupatikana  nje ya nchi  hususan nchi jirani ya Kenya.

Ikumbukwe kuwa  hivi karibuni Bodi ya Nyama Tanzania ilisema kuwa ifikapo Septemba 30, 2019 itakuwa mwisho kwa wauza nyama buchani kutumia magogo na endapo mtu atabainika akitumia , hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ambapo Ofisa Usajili kutoka katika bodi hiyo, Geofrey Sosthenes  alibainisha  kuwa magogo  yanasababisha hasara ya upotevu wa nyama, kitaalamu katika kilo 100 inapotea kilo moja, ambapo kwa mwaka muuzaji hupoteza Sh. milioni 3.8 ambayo inatosha kununua machine ya kisasa ya kukatia nyama.

Alichokisema Leo IGP Sirro Kuhusu Watanzania Waliouawa Msumbiji

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema baada ya kufuatilia sakata la mauaji ya Watanzania waliokuwa wakiishi Msumbuji amesema tayari, watu Watano (5) wamekamatwa huku mmoja akiuawa kufuatia msako mkali kati ya Polisi wa Tanzania na Msumbiji.

Ameeleza hayo leo wakati Rais Magufuli anazindua rasmi nyumba 15 za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi  katika eneo la Magogo Mkoani Geita.


“Kumekuwa na upungufu mkubwa sana wa matukio ya uhalifu kwa mwaka jana ikilinganishwa na mwaka huu, ninakushukru Mh.Rais kwa kukubali mualiko wangu wa kuja kutuzindulia hizi nyumba 20 ambazo kwetu ni za muhimu sana na ninaamini zitaongeza morali wa watendaji wetu.
 
"Lile tukio lililonipeleka Msumbiji, niliahidi kwa Watanzania kwamba damu ya Mtanzania haipotei, nikuhakikishie Mhe. Rais hadi sasa watano wameshakamatwa na mmoja ameshatangulia mbele za haki, na wanatajana, plan yote ilifanyika hapa kwetu" alisema IGP Sirro.

Waziri Mahiga Ashangaa Watu Wazima Kuchanganywa na Watoto Gerezani

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Augustine Mahiga na Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka, Biswalo Mganga, wameshangazwa wafungwa watu wazima kuchanganywa na watoto chini ya miaka 18 magerezani mikoa ya Simiyu na Mara.

Mbali na hilo, viongozi hao wameshangazwa pia kukuta idadi kubwa ya watu waliopo magereza ya mikoa hiyo, robo tatu wakiwa ni mahabusu huku wengine wakiwa ni wafungwa kamili baada ya kuhukumiwa.

Tukio hilo limetokea jana mara baada ya viongozi hao kuhitimisha ziara ya kikazi ya kuangalia mazingira ya utoaji haki na haki jinai mikoa ya Simiyu na Mara.

Katika ziara hiyo iliyoaanza Julai 9 hadi jana, viongozi hao walitembelea magereza ya Tarime, Mugumu-Serengeti, Bunda na Bariadi na kuongea na wafungwa, watumishi wa mahakama, polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

“Tulikutana na watoto wote tuliowakuta kwenye magereza hayo na kusikiliza kesi zao, ambapo DPP alitoa uamuzi wa kuwafutia kesi baadhi yao,” alisema Balozi Mahiga.

DPP Mganga alisema utaratibu wa kuwachanganya watoto wadogo na watu wazima magereza unakinzana na Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009, ambayo inataka wapelekwe gereza la watoto.

“Kutokana na mazingira ya nchi pamoja na kesi za watoto hao, tumewaelekeza watu wa magereza kuwatengea maeneo yao maalumu, kuwepo kwa gereza lao, pamoja na askari wa kuwahudumia ambao wamepewa mafunzo ya kuwatunza.

“Vile vile tunaomba jamii ibadilike na kuwalea watoto wao katika mienendo mizuri ili wasijiingize katika uhalifu, kwani huko pia tumewakuta watoto wenye kesi za mauaji, huku wengine wakiwa na kesi za kawaida ambazo tumezifuta na wameachiwa huru,” alisema.

DPP Mganga alisema kuna baadhi kulingana na mazingira ya kesi zao hawakuweza kuwafutia ila wameelekeza wawekwe katika mazingira maalumu kama sheria inavyotaka.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao pia walibainisha kuwa baadhi ya wafungwa waliwataja watumishi wa magereza kujihusisha na vitendo vya rushwa, na Dk. Mahiga aliagiza mamlaka za uchunguzi kufanyia kazi tuhuma hizo kisha kuwachukulia hatua kali wahusika.

Rais Magufuli Atoa Neno Kwa Watanzania Kuhusu Uchaguzi Wa Serikali za Mitaa.....IGP Sirro Kasema Jeshi la Polisi Liko Imara Kulinda Uchaguzi Huo

$
0
0
Rais Magufuli amewataka Watanzania kutumia uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Oktoba mwaka 2019 kuwachagua viongozi wazuri na sio watoa rushwa.

Magufuli ametoa wito huo leo Jumatatu Julai 15,2019 wakati akizungumza na wananchi wa Katoro na Buselesele mkoani Geita akiwa njiani kuelekea Magogo Geita ambako atazindua nyumba za askari wa jeshi la polisi.

“Mwaka huu tuna uchaguzi wa serikali za mitaa, chagueni viongozi wazuri, msichague viongozi wanaowapa rushwa, mkikosea kuchagua madhara yake ni makubwa.”

“Mkasimame imara katika kuchagua viongozi ambao mnafikiri wataweza kunisaidia pia na kunishauri vizuri,” amesema

Rais Magufuli pia amesisitiza wakazi wa maeneo hayo kudumisha amani, upendo na umoja na kutokubali kufarakanishwa.

 
Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini  IGP Simon Sirro amemuhakikishia Rais Magufuli kuwa vikosi vyake vimejipanga kuhakikisha amani na utulivu vitatawala katika chaguzi zijazo.

Amesema viongozi wazuri watachaguliwa kukiwa na Amani na utulivu hivyo watahakikisha hali hiyo inatamalaki katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

“Nakuhakikishia amani itatamalaki na uchaguzi utapita salama. Hatutamvumilia mtu au kikundi chochote kitakachojaribu kuvuruga amani. Sisi vyombo vya dola tuko tutahakikisha tunafuata sheria kuhakikisha wananchi wanaishi salama,” amesema

PICHA: Rais Magufuli Alivyotua na Kupokelewa Jijini Mwanza

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mwanza mjini mara baada ya kuwasili akitokea mkoani Geita. PICHA NA IKULU

Watu Watatu Kortini Kwa Kudaiwa Kuiba Madini

$
0
0
Watu watatu wakazi wa Dar es Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi ikiwemo kuiba madini yenye thamani ya Sh. Mil 507,347,000.

Washtakiwa hao ni Donald Njonjo (30) Mkazi wa Kigamboni, Gamba Muyemba (51) Mkazi wa Tandika na Kashif Mohamed (41) Mkazi wa Upanga jijini Dar es Salaam ambao wanadaiwa kuiba madini kwenye Tume ya Madini.

Kwa pamoja wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mwandamizi Mfawidhi, Kelvin Mhina kuwa kati ya Novemba 30, 2017 na Juni 29, mwaka huu katika Ofisi ya Tume ya Madini iliyopo Masaki wilayani Kinondoni, waliiba madini ya dhahabu yenye uzito wa Kilogramu 6.244 yenye thamani ya Sh.Mil 507,347,000 mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika, kesi imeahirishwa hadi Julai 29, 2019 kwa ajili kutajwa na washitakiwa wamerudishwa rumande kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kuwapatia dhamana.

Waziri Jafo Aagiza Hospitali Ya Uhuru Ikamilike Ndani Ya Mezi 6 Iliyopangwa.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Mhe Suleiman Jafo amefanya ziara maalum ya kukagua ujenzi wa Hospital ya Uhuru inayojengwa kwa maelekezo ya Mhe Rais Dk John Magufuli katika Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma ambapo ameagiza ujenzi wa Hospitali hiyo ukamilike ndani ya miezi 6 iliyopangwa..

Waziri Jafo ametoa Maelekezo hayo kwa   Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi(SUMA JKT) linalojenga hospitali ya Uhuru iliyopo wilayani Chamwino mkoani Dodoma kuhakikisha inakamilisha ujenzi huo ndani ya miezi sita kama walivyokubaliana.

Hospitali hiyo inajengwa baada ya Rais Magufuli kuelekeza kufanya hivyo katika sherehe za Uhuru mwaka 2018 ambapo alifuta sherehe hizo na kupeleka Fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hizo kujenga Hospitali mkoani Dodoma.

" Nishukuru leo kwa kufanya ziara hii maalumu ya kukagua ujenzi wa Hospitali hii ambayo ni malekezo kutoka kwa Mhe Rais, lakini pia hata hivyo baada ya gawio la Serikali kutoka Kampuni ya Airtel Mhe Rais alielekeza Fedha hizo kuletwa kwenye mradi wa ujenzi wa Hospitali hii ya Uhuru.

"  Na kama mnavyokumbuka nilikuja siku za nyuma Juni 19 kukagua lakini sikuridhishwa baada ya kukuta ujenzi haujaanza ndio maana nimetoa maelekezo kwamba ujenzi uanze mara moja kwa kutumia vikosi vya Jeshi ili kutimiza azma ya Mhe Rais katika kutoa huduma za Afya kwa wananchi, na tayari wenzetu wa Suma JKT wameshaanza kazi hii," amesema Mhe Jafo.

Amesema tayari eneo lote la Ekari 40 limeshasafishwa ikiwemo kujenga uzio pamoja na ofisi kuleta vifaa vya ujenzi huku pia akieleza kwamba TBA wataendelea kusimamia suala la ramani na kutoa ushauri wa mradi huo na wataendelea kutumia utaratibu wa 'false acount' kutokana na kuwapatia mafanikio katika kufanikisha kazi za Serikali za Mitaa.

" Kwa kweli leo nimeridhishwa na hatua ya awali ambayo tumefikia katika ujenzi wa Hospitali hii, na niwaombe wataalamu wangu kuacha kufanya kazi kwa mazoea na tunapotoa maagizo basi wayatekeleze kwa wakati, lakini ni matarijio yetu hadi kufikia Januari, 2020 tutakua tumeshamaliza ujenzi huu," amesema Mhe Jafo.

Kwa upande wake Mhandisi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania TBA, Daniel Mwakasungura amesema Hospital hiyo ya Uhuru itakuwa ni ya Ngazi ya Wilaya ambapo kwa agizo la Mhe Rais awamu ya kwanza ni kujenga majengo ya wagonjwa wa nje ikiwemo huduma za maabara na Kliniki ya Mama na Mtoto.

" Hela iliyotengwa ambayo Tumeingia mkataba na Suma JKT ni Shilingi Bilioni 3 ambazo zitajenga hivyo nilivyovitaja na tunatarajia kukamilisha mradi huu baada ya miezi sita kama ambavyo tuliekezwa," amesema Mwakasungura.

 Kwa Upande wake,  Mhandisi wa Suma JKT, Luteni Kanali Onesmo Njau amesema walikabidhiwa jukumu la ujenzi huo Juni 19 mwaka huu na tayari washatekeleza maelekezo kutoka kwa Mhe Jafo ikiwemo kuandaa ofisi, sehemu za kuishi kwa watendaji na muda sio mrefu wataanza ujenzi ili kukamilisha mapema kama ilivyoelekezwa.

Waziri Mbarawa Afanya Uteuzi Wa Wakurugenzi Watendaji Wa Mamlaka Za Majisafi Na Usafi Wa Mazingira

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images