Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Makamu Wa Rais Kumuwakilisha Magufuli Mkutano Wa 12 Wa Dharura Wakuu Wa Nchi Na Serikali Umoja Wa Afrika


JKT Yakanusha Taarifa Za Vijana Wa JKT Kundi La Kikwete Na Operesheni Magufuli Kukusanyika Kambi Ya JKT Mgulani

$
0
0
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linapenda kukanusha taarifa zinazoendelea kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, zinazoelezea kuhitajika kwa vijana wa JKT kundi la kujitolea Operesheni Kikwete na Operesheni Magufuli kukusanyika katika Kambi ya JKT Mgulani jijini Dar es Salaam tarehe 08 Julai 2019 kwa ajili ya usaili.
 
Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa yanazikanusha taarifa hizo za uzushi zenye lengo la kuwachanganya vijana wetu ambao wamehitimu mafunzo ya JKT na kurejea makwao.
 
Siku zote JKT imekuwa ikisisitiza kuwa vijana wanaojiunga na mafunzo ya JKT ni vyema wakatambua kuwa mafunzo hayo hayana uhusiano wa kupatiwa ajira kwenye vyombo vya ulinzi na usalama mara wamalizapo mkataba, bali mafunzo hayo yanawajengea uwezo wa kujuwa stadi za kazi na stadi za maisha.
 
Jeshi la Kujenga Taifa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wanafatilia kwa karibu kikundi kidogo chenye tabia ya kusambaza taarifa potofu na za uvumi zinazohusu JKT.
 
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 03 Julai 2019.

Tatizo La Ucheleweshwaji Wa Mizigo Bandari Ya Dar Es Salaam Kupatiwa Ufumbuzi

$
0
0
WAZIRI wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwele amesema kuwa Rais John Magufuli ametoa fedha nyingi za matengenezo ya miundombinu ya bandari na reli hali iliyopelekea watumiaji wa reli na bandari ya Dar es Salaam kutoka nje kusifia uimarikaji wa mfumo huo ambao unarahisisha upitishwaji wa mizigo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijiji Dar es Salaam mara baada ya kukutana na wafanyabiashara wa kimataifa wanaotumia bandari ya Dar es Salaam Kamwele amesema kuwa watumiaji wa muindombinu hiyo wamesema kuwa Kuna faida kubwa katika biashara yao licha ya changamoto ya ucheleweshwaji wa mizigo ambayo inapatiwa ufumbuzi kujitokeza mara kwa mara.

Amesema kuwa wafanyabiashara hao wamesema kuwa Sera na sheria ziboreshwe jambo ambalo amewahaidi kukaa na mamlaka husika ili kutatua changamoto zinazoikumba sekta hiyo.

Mhandisi Kamwelwe amesema kuwa baada ya mwezi mmoja watakaa tena na wafanyabiashara hao na kuangalia zaidi namna ya kuitumia vyema bahari ya Hindi na wizara hiyo itakaa na wamiliki wa meli duniani ili kuboresha zaidi uchumi wa nchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya usimamizi wa bandari nchini (TPA) Mhandisi Deusdetit Kakoko amesema kuwa watumiaji wa bandari hiyo wakiwemo wafanyabiashara waliohudhuria mkutano huo wategemee makubwa kupitia bandari hiyo ambapo hadi sasa miundombinu ya tehama na ulinzi vinaimarishwa zaidi.

 Kuhusiana na sera na sheria Kakoko amesema kuwa ushirikiano baina ya wizara hiyo na wizara ya fedha itazaa matunda kwa manufaa ya taifa na watumiaji wa bandari hiyo.

Pia amewataka wadau wateja na mamlaka husika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano pamoja  na kushirikiana ili kuipeleka nchi katika uchumi wa Kati.

Mwisho.

Mtanzania Rashid Mberesero ahukumiwa kifungo cha maisha Kenya Kwa Kuhusukika na Shambulizi la Kigaidi Lililoua Watu 148

$
0
0
Mahakama ya Kenya imemhukumu Mtanzania Rashid Mberesero kifungo cha maisha jela baada ya kumkuta na hatia ya kutekeleza shambulio la kigaidi mwaka 2015 katika Chuo Kikuu cha Garissa, Kenya.

Rashid Mberesero amehukumiwa kutumikia adhabu hiyo, akiungana na watu wengine wawili ambao kwa pamoja wamekutwa na hatia ya kuhusika na shambulio la kigaidi lililosababisha vifo vya wanafunzi 148 katika chuo hicho.

Wakati Rashid Mberesero akihukumiwa adhabu ya kifungo cha maisha jela, washtakiwa wenzake wawili Hassan Edin na Mohammed Abdi jina jingine Mohamned Ali Abikar wamehukumiwa miaka 41 kila mmoja gerezani.

Rashid Mberesero, aligundulika katika eneo la tukio akiwa sio mwanafunzi wala mfanyakazi wa chuo hicho.

Gazeti la The Citizen Tanzania la Aprili 10 mwaka 2016, lilisema Rashid alikuwa akisoma shule ya upili ya Bihawana mjini Dodoma Tanzania ambaye alidaiwa kutoroka shule baada ya kukatazwa kuvaa kofia kichwani.

Kulingana na mwalimu mkuu wa shule hiyo wakati huo, mwanafunzi huyo alijiunga na shule hiyo mwaka 2015 baada ya kutoka shule ya upili ya Bahi Kagwe.

Licha ya kutoweka katika shule, hakuna aliyefuatilia alikokwenda

Kwa takriban miezi minne wazazi wa kijana huyo walidhani mtoto wao yupo shule lakini haikuwa hivyo.

Haijulikani ni nini haswa kilichomfanya kuingia katika ugaidi.

Wazazi wa Rashid walishangaa kugundua kwamba mtoto wao alikuwa miongoni mwa watu waliopanga na kutekeleza shambulio la Garissa.

Wema Sepetu Aachiwa Huru Na Kisha Kukamatwa Tena

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu, lakini dakika chache baadaye askari magereza walimkamata tena.

Malkia huyo wa filamu anakabiliwa na kesi ya kusambaza picha zinazodaiwa kuwa za ngono mtandaoni.

Taarifa Kwa Umma - Ukaguzi Wa Mikataba Ya Ajira Kwa Madereva

$
0
0
1.Katika kutimiza azma ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, Serikali inaendelea, pamoja na mambo mengine, kuimarisha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara katika sekta mbali mbali hapa nchini, ikiwemo sekta ya usafirishaji. Sekta hii ni miongoni mwa Sekta zenye mchango mkubwa katika kukuza uchumi na kuongeza mapato ya Serikali. Aidha, sekta hii imekuwa ikichangia pia kuzalisha ajira kwa vijana wetu katika nafasi mbali mbali kama vile Madereva, Mafundi na kada nyingine nyingi.

2.Pamoja na mchango mkubwa unaotolewa na sekta hii, zipo changamoto kadhaa ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi na Serikali kwa kushirikiana na wadau.  Kwa upande wa utekelezaji wa Sheria za Kazi, changamoto zimeendelea kujitokeza katika masuala ya Mikataba ya Ajira, Malipo ya Mishahara na Posho mbali mbali, ambapo imebainika yapo Makampuni machache yanayolenga kuchafua kazi nzuri inayofanywa na sekta hii, ambapo makampuni hayo machache yamekuwa yakifanya udanganyifu kwenye Mikataba ya Ajira za Madereva wao pindi yanapofanya maombi ya Leseni za Usafirishaji.

3.Aidha, katika jitihada za kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi; Kitengo cha Usalama Barabarani na LATRA inatarajia kufanya Zoezi Maalum la Ukaguzi kwa lengo la kukagua Mikataba hiyo na kuangalia utekelezaji wa Sheria kwa ujumla.

4.Zoezi hili linatarajiwa kufanyika kwa namna mbili tofauti ambapo; (i) Maafisa Kazi waliopo katika Ofisi za Kazi watapita katika Kampuni zote za Usafirishaji na (ii) Timu maalum ya Maafisa Kazi wa kushirikiana na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Madereva, LATRA na Jeshi la Polisi; Kitengo cha Usalama Barabarani watafanya Ukaguzi wa Mikataba kwenye Vituo Vikuu vya Ukaguzi kama vile Kituo cha Mabasi Ubungo, Kituo cha Kuegesha Malori cha Misugusugu na vituo vingine vinavyofanana na hivyo hapa nchini.

5.Aidha, sambamba na ukaguzi huo, Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Madereva na Vyama vya Waajiri watapatiwa elimu kuhusu haki na wajibu wao katika kutekeleza Sheria za Kazi.

Hivyo, ninapenda kuwaarifu Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji, Wafanyakazi Madereva na Umma kwa ujumla kuwa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu inatarajia kuanza rasmi Zoezi  la Ukaguzi wa Mikataba ya Ajira ya Madereva na Utekelezaji wa Sheria za Kazi kwa ujumla ifikapo tarehe 15 Julai, 2019.

6.Ili kulifanya zoezi hili kuwa lenye ufanisi, ni vema Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji kuhakikisha kuwa Mikataba ya Madereva wenu inakuwepo katika maeneo yenu ya kazi, na kwa upande wa Madereva, kuhakikisha mnakuwa na nakala za Mikataba yenu mnapokuwa katika kazi zenu ili iwe rahisi kwa Wakaguzi kuiona.

7.Aidha, ninapenda kuwaarifu kuwa Zoezi la Ukaguzi wa Mikataba ya ajira na Utekelezaji wa Sheria kwa ujumla litakuwa endelevu na litaendelea pia katika Sekta nyingine hapa nchini.

8. Mwisho, ninapenda kutoa wito kwa Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji, Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Madereva pamoja na Madereva wote nchini kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Wakaguzi wakati wote wa utekelezaji wa zoezi hili ili kutoathiri utoaji wa huduma kwa wananchi kwa namna yoyote ile.


IMETOLEWA NA
KATIBU MKUU
OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU
3/7/2019

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa 5 July

TTCL Yavuna Wateja Wapya 215,000 Na Kuitikia Wito Wa Rais Magufuli

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, MAELEZO
SHIRIKA la Mawasiliano Nchini (TTCL) katika kipindi cha siku 30 limeweza kusajili wateja wapya 215,000, ikiwa ni Mpango Mkakati wa Shirika hilo katika kujiinua kibiashara na kuongeza wigo huduma ya Mawasiliano kwa Watanzania ikiwa ni utekezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli.

Akizungumza Alhamisi (Julai 4, 2019) katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere, Meneja Mawasiliano wa TTCL Nicodemus Mushi alisema Shirika hilo limetekeleza kwa vitendo agizo la Rais Dkt. John Magufuli alilolitoa kwa Shirika hilo tarehe 21 Mei, mwaka huu.

Mushi alisema hadi sasa huduma za Mawasiliano za Kampuni hiyo katika Mfumo wa 4G zinapatikana katika Mikoa 16 nchini na mpango uliopo ni kuhakikisha kuwa maeneo yaliyobaki yanapata huduma za Shirika kupitia  Mpango Mkakati wa Shirika hilo uliojiwekea na hivyo kuweza kuleta ushindani wa huduma ya mawasiliano na makampuni mengine nchini.

“Mwaka uliopita tulijiwekea Mpango Mkakati wetu ambao utahakikisha kuwa tunaweza kuleta ushindani na makampuni mengine na hivi sasa kama unavyoona tumeweza kupata wateja wapya 215,000 na kupitia maonesho hayo tutaweza kuongeza wateja wengi zaidi ” alisema Mushi.

Aliongeza kuwa kwa sasa Shirika hilo limeweza kupata wateja wengi zaidi wakiwemo watumishi wa serikali, ambapo kwa kutambua umuhimu huo, TTCL imeanzisha kifurushi maalum cha ‘watumishi pack’ ambacho kinaweza kutumiwa na wafanyakazi wote wa serikali kwa kuweza kukamilisha taratibu mbalimbali ikiwemo vitambulisho vya kazi.

Akifafanua zaidi Mushi, alisema kauli zinatolewa na watu mbalimbali kuhusu kauli ya Rais Dkt. John Magufuli kuwataka wafanyakazi wa serikali kutumia huduma za mawasiliano za shirika hilo, ni kuwa zitawahusu watumishi wa umma ambao wanalipiwa huduma za mawasiliano ya simu na serikali na si kinyume na maelekezo hayo.

Aliongeza kuwa malengo ya Taasisi hiyo ni kuweza kujipanga ili kuendelea kutoa huduma bora na zenye viwango ili kuweza kuongoza na kuwa kampuni bora ya mawasiliano inayotoa huduma bora kwa wateja wake nchini.

“Sisi kwa upande wetu tumeendelea kuwalipa vizuri mawakala wetu ikiwemo kutoa kamisheni nzuri kwao ili kuhakikisha kuwa huduma zetu zinazotolewa zinakuwa zinakidhi matakwa ya wateja na soko la mawasiliano kwa ujumla” alisema Mushi.

Profesa Anna Tibaijuka Atangaza Kung'atuka Ubunge

$
0
0
Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka (CCM), amesema hatagombea tena nafasi ya ubunge Uchaguzi Mkuu ujao. Tibaijuka  alitoa kauli hiyo wakati akihojiwa na  Ayo Tv

Pamoja na mambo mengine, alisema anastaafu kwa sababu yeye ni kizazi cha Mwalimu Julius Nyerere ambaye aliwafundisha kung’atuka.

“Mimi 2020 ninastaafu, ninang’atuka kwa sababu sisi ni kizazi cha Mwalimu Nyerere na katika vitu alivyotufundisha ni kung’atuka.

“Katika uchaguzi wa 2015, Muleba Kusini pamoja na kampeni ya Escrow bado nilipita kidedea, kwa kweli nawashukuru wananchi wa Muleba, ni watu wanaotafuta maendeleo, wana kiu ya maendeleo.

“Na ninaposema nastaafu ubunge, haimaanishi kwamba nastaafu Muleba, hivi ni vitu viwili tofauti, mimi ninastaafu uwakilishi, Bunge letu hili lingekuwa Seneti ningesema nitaendelea.

“Lakini sasa ni Bunge la Uwakilishi, hatuna Bunge la Seneti, yaani Bunge ambalo sasa hoja zinalinda masilahi mapana ya umma, hapa tunawakilisha wananchi na mimi naamini tunaweza kupata mwakilishi mzuri wa Muleba,” alisema.

Alisema anaamua kung’atuka si kwa sababu ya kuhofia kushindwa, kwani ingekuwa hivyo angeshindwa katika uchaguzi uliopita kutokana na kampeni chafu juu yake.

“Mimi kama kupigwa chini, ningepigwa chini mwaka 2015 au sio. Asiyekubali kushindwa si mshindani, kwa hiyo mimi sistaafu kwa ajili ya hofu, kwanza Muleba anayenishinda ni nani? Ni Mwenyezi Mungu peke yake.

“Kwa kipindi cha miaka 10 nimejifunza, nimeelewa matatizo ya wananchi na wakati ule nilipotoka Umoja wa Mataifa, nilikuja na nia moja ya kujifunza kwamba taifa letu lina tatizo gani.

“Tufanye nini ili tuweze kusogea mbele, kwa hiyo hata bungeni ninaposimama, nikiona kitu hakijakaa sawa huwa sisimami kiitikadi, pia sitaki ushabiki ambao hauna mantiki,” alisema. 

Rais Magufuli kuzindua rasmi hifadhi mpya ya Taifa ya Burigi iliyoko Chato

$
0
0
Rais John  Magufuli anatarajiwa kuzindua rasmi Hifadhi ya Taifa ya Burigi huko Chato siku ya Jumanne Julai 9,  mwaka huu, ambayo imepandishwa hadhi hivi karibuni kutoka lililokuwa pori la akiba la Burigi, ambapo pamoja na mambo mengine, atakabidhi vibali na hati kwa wawekezaji mbalimbali ili kuwekeza katika eneo hilo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangalla amesema hayo jijini Mwanza jana, katika mkutano wa mwaka wa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa).

Alisema ili sekta ya hifadhi iweze kuleta mabadiliko ni lazima jamii wakiwamo wanahabari washiriki katika kutangaza vivutio vya utalii kama njia ya kuongeza idadi ya wageni wa ndani na nje.

“Bila wanahabari sekta ya utalii haiwezi kujulikana hivyo tushirikiane pamoja katika hili.

“Na pia kama mnakumbuka hivi karibuni tumetangaza hifadhi mpya za taifa na Jumanne Rais Magufuli, atazindua hifadhi ya Burigi Chato, lengo ni kuhakikisha wageni waweze kuona maliasili zetu popote pale Tanzania,” alisema Dk. Kigwangalla.

Kijana Atiwa Mbaroni Kwa Kumlawiti Mama Yake Mzazi

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jeshi la polisi Mkoani Dodoma linamshikilia  Kijana mmoja Donald Justine(25] baada ya kumvizia na kumbaka bibi kizee mwenye umri wa miaka 95 huku yakitajwa Matukio ya ukatili kuongezeka kutoka 174 mwaka 2018 hadi matukio 517 mwaka 2019 mkoani humo.

Akizungumza na  waandishi wa Habari Julai 4,2019,Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Kamishna msaidizi wa polisi, Gilles Muroto amesema Katika eneo la Nane nane kata ya Nzuguni, Dodoma Mjini,  kikongwe wa miaka 95, mkazi wa eneo hilo  alibakwa na kijana mmoja Donald Justine(25) aliyemvizia akiwa amelala na kumkaba shingoni kisha kumtendea unyama huo. 

Kamanda Muroto ameyataja matukio mengine ,Katika kijiji cha Mlazo, tarafa ya Mpyayungu, Wilaya ya Chamwino, Makame Wambura, (28) na mtoto wake Fidelika Walioba miezi mitatu(3) baada ya kumwagiwa mafuta ya petrol na mume wake aitwae Elias Warioba (30) na wote wawili kujeruhiwa vibaya na wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma, na hapa kamanda anaelezea tukio lilivyotokea.

Tukio la tatu  katika kijiji cha Manchali, tarafa ya Chilonwa, Wilayani  Chamwino, walimkamata Mazengo Chilatu(28) kwa kosa la kumlawiti mama yake mzazi ambaye  hakujulikana jina wala umri wake kwa kumvizia akiwa amelala.

Lingine katika eneo la Maili mbili jijini humo ,ni tukio la Mwanaume mmoja anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 25- 30 ambaye hakufahamika jina lake alifanya matukio matatu ya ubakaji kabla ya kukamatwa na wananchi na kupigwa na wananchi kabla ya kuokolewa na polisi na baadaye kufariki. 

Ambapo alifanya matukio hayo kwa watu watatu tofauti kabla ya Julai 4  kukamatwa na  wananchi wenye hasira kali na kuupigwa vibaya na kuokolewa na jeshi la polisi hata hivyo alifariki baadaye. 

Hata hivyo, amepongeza kazi nzuri inayofanyawa na wanahabari katika kuripoti habari za ukatili huo, ambapo amesema kwa sasa kumekuwa na mwamko mkubwa wa wananchi kuripoti matukio hayo kwa  jeshi la polisi. 

Hata hivyo Kamanda Muroto        amesema matukio  ya ukatili mkoani Dodoma yameongezeka kutoka matukio 174 kwa mwaka 2018 na kufikia matukio 517 huku vyanzo vikitajwa kuwa ni ulevi,mmomonyoko wa maadili,uvivu,imani za kishirikina ,tamaa na ukatili.

Iran yamuita balozi wa Uingereza kuhusiana na kuakamatwa meli yake

$
0
0
Iran imemuita balozi wa Uingereza mjini Tehran kuhusiana na kile ilichosema ni kukamatwa leo kinyume cha sheria meli ya mafuta ya Iran katika kisiwa cha Gibraltar. 

Televisheni ya serikali ya Iran imemnukuu msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Kigeni Abbas Mousavi akithibitisha habari hizo. 

Jeshi la wanamaji wa Uingereza lilikamata meli hiyo ya mafuta ikituhumiwa kwa kupeleka mafuta nchini Syria ikiwa ni hatua ya kukiuka vikwazo vya Umoja wa Ulaya. 

Kitendo hicho kinazusha hofu ya kuongeza mgogoro kati ya nchi za Magharibi na Iran. 

Waziri Kiongozi wa Gibraltar Fabian Picardo alisema katika taarifa kuwa wanaizuilia meli hiyo na shehena yake. 

Meli hiyo inasafiri kwa bendera ya Panama na inaaminika kuwa imebeba mafuta ya Iran.

Kamati Ya Ulinzi Na Usalama Mkoa Simiyu Yaridhishwa Na Kasi Ya Tba Ujenzi Wa Ofisi Ya DC Busega

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Anthony Mtaka imeridhishwa na kasi ya Ujenzi  wa  jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega na majengo ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, chini ya Mkandarasi Wakala wa Majengo nchini  (TBA ).

Hayo yamebainishwa na kamati hiyo ,mara baada ya kukagua ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Busega ambapo ujenzi umeanza mwezi Aprili mwaka huu na  unatarajia kukamilika ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema miradi yote inayotekelezwa na TBA Simiyu imekuwa ikitekelezwa kwa wakati na wakati mwingine imekuwa ikitekelezwa na kukamilika kabla ya muda uliopangwa katika mkataba, huku akiishukuru serikali kwa kutenga fedha za  ujenzi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Busega  ambayo itatua changamoto za  wananchi za upatikanaji wa huduma kwa karibu .

“Tumepata Meneja mzuri wa TBA ambaye anatekeleza miradi yake kwa wakati, miradi yote tuliyompa imetekelezwa mbele ya muda uliowekwa kwenye mkataba; kwa mradi huu umeenda kwa kasi ambayo inaendana na uhitaji wa wananchi wa Busega waliokuwa wanahitaji mahali pa kupata huduma” alisema Mtaka.

Mkuu wa wilaya ya Busega Mhe.Tano Mwera amesema utendaji wa kazi kwa sasa ni mgumu kutokana na ufinyu wa jengo wanalolitumia kama ofisi, hivyo kukamilika kwa jengo hilo kutawasaidia kufanya kazi kwa ufanisi.

“Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kutupa fedha za ujenzi wa jengo hili, litakapo kamilika litatuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi kwa sababu ofisi tunayoitumia sasa hivi ni finyu sana na watendaji wametawanyika sana hivyo inatuwia vigumu kiutendaji”alisema Mwera.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema kazi zote  zinazofanywa na Wakala wa majengo nchini TBA Mkoa wa Simiyu zimekuwa zikifanywa kwa viwango na zinakamilika kwa wakati, huku akiahidi kulipa fedha zilizobakia kwa wakati.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Majengo nchini TBA Mhandisi Likimaitare Naunga amesema mkataba wa ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega ni miezi mitano na wanatarajia kukamilisha ujenzi kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu.

Kukamilika kwa ujenzi awamu ya kwanza ya jengo hilo  utagharimu kiasi cha shilingi milioni mia saba  nukta saba.

Serikali Yasema ni Marufuku mbolea kuchelewa kufika kwa wakulima

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Serikali imetangaza kiama kwa wanaochelewesha mbolea kuwafikia wakulima kwa wakati kwani kuchelewa kwa mbolea ni miongoni mwa sababu zinazopunguza uzalishaji wa mazao mbalimbali ya wakulima nchini.

Mbolea kutofika kwa wakulima kwa wakati ni wazi kuwa Taasisi iliyopewa jukumu la kusimamia na kudhibiti mbolea ya TFRA imeshindwa kufanya kazi yake kwa ufasaha hivyo ikibainika kuchelewa kwa mbolea pasina sababu za msingi watendaji hao watachukuliwa hatua za kisheria.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ametoa kauli hiyo ya onyo leo tarehe 4 Julai 2019 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwenye kikao kazi na wafanyakazi wa Taasisi ya udhibiti wa mbolea Tanzania (TFRA).

Alisema kuwa mbolea inayohitajika kwa wakulima ni Lazima ipatikane kwa wakati katika maeneo ya kilimo. “Kupatikana kwa wakati maana yake ni kwamba kila mtu anapoishi anapaswa kuipata kirahisi kupitia maduka au masoko” Alisema

Aliongeza kuwa kazi ya Taasisi ya udhibiti wa mbolea Tanzania ni kuhakikisha mbolea inawafikia wakulima sio kusalia Jijini Dar es salaam ilihali wakulima wapo mikoa yote Tanzania na endapo mbolea ikikosekana kwa wakulima watendaji wa TFRA watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Kadhalika alisema kuwa kupatikana pekee kwa mbolea kwa wakulima ni jambo moja lakini muhimu ni kuwa na bei nafuu ambazo wakulima wataweza kuzimudu.

“Sasa hivi kuna malalamiko mengi kwa wakulima kuwa mbolea zinauzwa bei ya juu hivyo wameshindwa kuzimudu, haiwezekani mbolea itoke Ulaya ikiwa na bei nafuu lakini kumfikia mkulima inakuwa na bei ghali, hapo ni wazi kuwa TFRA hamjafanya kazi yenu sawasawa” Alikaririwa Mhe Hasunga

Alisema kuwa endapo TFRA itatekeleza majukumu yake ipasavyo mbolea itapungua bei na wakulima watanufaika na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Tanzania.

“Na kama tatizo la gharama linaongezeka kutokana na usafirishaji kuna sababu gani za kutumia magari kusafirisha wakati kuna usafiri muhimu wa reli (TRC) ambapo mawakala wangepakua na kusambaza mizigo hiyo baada ya kufika katika maeneo mbalimbali inapoishia reli” Alisema

Hata hivyo amesisitiza kuwa serikali imeanzisha mchakato wa kupitia mbolea kote nchini ili uagizaji wa mbolea iweze kuagizwa itakayoendana na uwezo wa udongo.

Tume Ya Madini Yatoa Mafunzo Kwa Wachimbaji Wadogo 350

$
0
0
Na Mwandishi Wetu,MAELEZO
SERIKALI kupitia Tume ya Madini imetoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini 350 katika mikoa ya Arusha na Katavi yaliyolenga kuwajengea uwezo wa kutumia njia bora na za kisasa ili kuwawezesha kuachana na matumizi ya matumizi ya Zebaki yanayoathiri mazingira.

Akizungumza  Alhamisi (Julai 4, 2019) katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere , Mkaguzi wa Madini na Mazingira wa Tume hiyo, John  Mataro alisema Tume hiyo imekusudia kuhakikisha kuwa suala la uhifadhi na utunzaji wa mazingira linapewa na kila mchimbaji wa madini nchini.

Mataro alisema Ofisi hiyo imekuwa ikiotoa miongozo mbalimbali kupitia sheria zilizopo kwa ajili ya kuwaelimisha wachimbaji wadogo, na kampeni hiyo itakuwa endelevu ili kuhakikisha kuwa maeneo yote yanayotumiwa na wachimbaji madini hususani wachimbaji wadogo yanazingatia maelezo hayo ili kuweza kuwa na uchimbaji endelevu na salama.

“Malengo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wachimbaji wetu wanaweza kupata kipato cha kutosha ili kuweza kujikwamua kiuchumi, na hili litafanyika kwa kuhakikisha kuwa tunajenga mazingira yenye usalama wa hali ya juu katkika maeneo yote ya uchimbaji yaliyopo nchini” alisema Mataro.

Aidha Mataro aliongeza kuwa Tume hiyo kwa kutambua mchango wa wachimbaji wadogo nchini imekuwa ikiwajengea uwezo wachimbaji hao kwa kujenga mazingira wezeshi ikiwemo kupata mikopo nafuu kupitia taasisi za kifedha ikiwemo Benki, hatua inayolenga kuwapa morali na uwezo wa kumiliki vifaa bora na vya kisasa kwa ajili ya uchimbaji wa madini.

Akifafanua zaidi Mataro alisema mara kwa mara Tume hiyo imekuwa ikifanya ziara katika migodi mbalimbali iliyopo nchini yenye lengo la kuwakumbusha wachimbaji wote hususani wachimbaji wadogo kuzingatia miongozo mbalimbali ikiwemo kuwepo matangazo mbalimbali ya tahadhari katika maeneo ya uchimbaji ili kuweza kutoa taarifa kwa wahusika wanaofika katika maeneo hayo kwa mara ya kwanza.

Shirika La Posta Kuanza Kupokea Maombi Ya Fomu Za Mikopo Ya Wanafunzi Julai 8 Mwaka Huu

$
0
0
Na Mwandishi Wetu,MAELEZO
SHIRIKA la Posta Nchini (TPC) kupitia Ofisi zake 170 zilizopo nchini kuanzia Julai 8 mwaka huu litaanza kupokea na kusafirisha vifurushi vyenye fomu za maombi ya mikopo ya wanafunzi wa Juu nchini na kuziwasilisha katika Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

Akizungumza  Alhamisi (Julai 4, 2019) katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Meneja wa Usimamizi wa Fedha za Kigeni wa TPC, John Tinga alisema fomu zitasafirishwa zikiwa na bahasha maalum yenye nembo za HESLB na TPC.

Tinga alisema ili kurahisha zoezi hilo, TPC imeweka mawakala wake maalum watakaotumika kwa ajili ya kusaidia huduma za usafirishaji wa maombi hayo ikiwemo kutumia pikipiki katika maeneo yaliyopo sehemu za vijijini ili kuwezesha fomuhizo  kufika kwa urahisi katika ofisi za TPC zilizopo katika Ofisi zake za mikoa na Wilaya zote nchini.

Kwa mujibu wa Tinga alizitaja gharama za usafirishaji wa vifurushi hivyo ni Tsh 16,000 kwa fomu za maombi yatakayotumwa  kutoka mikoani ambayo yatawasilisha katika mfumo wa EMS wakati kwa upande wa DSM gharama za kutuma zitakuwa ni Tsh 8000 na hakutokuwa na gharama nyingine zozote zitakazotozwa kwa wateja hao.

Aliongeza kuwa TPC kwa kushirikiana na HESLB zimejipanga katika kuhakikisha kuwa zoezi hilo linaendeshwa kwa ufanisi mkubwa ili kuwawezesha wanafunzi wote nchini kuwasilisha maombi yao kwa wakati na kuepukana na usumbufu wa kutuma maombi hayo katika tarehe za mwisho.

“TPC imejipanga vizuri kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili na hakuna fomu yoyote ya maombi itakayopotea tunachokihitaji ni kwa waombaji kukamilisha taratibu zote za msingi ikiwemo kuweka jina lake nyuma ya bahasha zetu” alisema Tinga.

Akifafanua zaidi Tinga alisema malengo ya Shirika hilo ni kutoa huduma bora kwa wananchi na wateja wote nchini ili kuhakikisha malengo ya Shirika hilo yanaweza kufikiwa ikiwemo kutoa huduma bora zinazozingatia viwango vya kimataifa.

Katika hatua nyingine, Tinga alisema Shirika hilo pia limeanzisha huduma ya mfumo mpya wa mawasiliano wa ‘Net Smart’ inayowezesha kutuma na kupokea vifurushi vyote kwa njia ya haraka zaidi.

Mali za Freeman Mbowe Kupigwa Mnada Kesho

$
0
0
Mali za Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  zinatarajiwa kupigwa mnada Julai 6, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kampuni ya udalali ya Fosters Auctioneers & General Traders ya jijini Dar es Salaam, mali zitakazopigwa mnada ni kila kitu kilichokuwamo ndani ya Ukumbi wa Bilicanas uliopo Mtaa wa Mkwepu, jijini Dar es Salaam.

“Mnada huo utafanyika kuanzia saa nne asubuhi kwenye ghala la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) karibu na geti namba 3, bandarini,” imesema taarifa hiyo.

Mwalimu ataka kujiua kwa kujikata na chupa kisa ugumu wa maisha

$
0
0
Mwalimu wa Shule ya Msingi Rung’abure iliyopo Serengeti Mkoani Mara, Godfrey Tarimo amejikata na chupa eneo lake la shingo katika jaribio la kutaka kujiua kwa kile alichosema ni kuzidiwa na ugumu wa maisha na mahusiano mabaya na jirani zake.

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Nyerere, Wilaya ya Serengeti, Dkt Tanu Warioba amethibitisha kumpokea mwalimu usiku wa Julai 3, 2019 akiwa ameletwa kwa msaada wa walimu wenzake.

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu amesema hatua kali za kinidhamu na sheria zitachukuliwa kwa mwalimu huyo ikiwezakana hata kufukuzwa kazi.

Isikupite Hii! 👉Naitwa Chief Karim Wa Sultan.....Ni Bingwa Na Mtabiri Wa Nyota

$
0
0
Isikupite hii! 👉Naitwa CHIEF KARIM WA SULTAN Kutoka- TANGA - TANZANIA: Ni Bingwa, Mnajimu na Mtabiri wa Nyota na Matatizo yote ya ndoa/mahusiano.

Natabiri nyota yako, Kung'alisha nyota, Kufungua nyota zako za mafanikio zilizo fungwa  na kusababisha usifanikiwe katika maisha yako, au unajikuta unafanya kazi/biashara unapata hela lakini pesa yako haikai yaani inapita tu katika mikono yako.

Nawezesha  NYOTA, ni UTAJIRI usio na kafara yoyote na ni UTAJIRI unaoendana na nyota yako tu.

Hakika watu wengi wanazidi kufanikiwa na kutimiza ndoto zao , Kulipwa haraka haki zako unazodai, Mvuto wa mapenzi, kumrudisha mpenzi, mme au mke aliyekuacha/kukutelekeza.

 Je unapata wapenzi/wachumba lakini wanakuacha bila kujua sababu? Nitakusaidia!

Kufungua kizazi chako kilichofungwa na kusababisha usipate mimba/mtoto au unashika mimba zinatoka/kuharibika na maumivu makali ya tumbo/chango.

 👉KWA TATIZO LOLOTE  LA KINYOTA WASILIANA NAMI 👉WhatsApp : 0763 103 527
au
👉PIGA SIMU  : 0716 681 318
👉 0688 745 790


NB 👉(KWA MWANAUME YOYOTE MWENYE TATIZO LA KUISHIWA AU KUPUNGUKIWA NGUVU ZA KIUME AU KAMA UMEATHIRIKA NA TATIZO LA KUPIGA PUNYETO TUWASILIANE POPOTE ULIPO)*{لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّهُ بِاللَّغْوِ فِي أيْمَانِكُمْ وَلَٰكِنْ يُؤَاخِذُكُمْ بِمَا عَقَّدْتُمُ الْأَيْمَانَ ۖ فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِمَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَنْ لَمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ }* ﴿٨٩﴾ ✨WABILLAHHI TAWFIQ ASALLAM  ALAIKUM✨ 

Jinsi ya kukabiliana na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume

$
0
0
Tunapozungumzia upungufu wa nguvu za kiume tunakuwa katika uwanja mpana zaidi wa tafakari za kibaiolojia na kisaikolojia walizonazo wanaume.

Lakini kwa kufupisha mlolongo wa mambo sehemu kuu tatu zinaweza kabisa kukidhi mchanganuo mzima wa jinsi tatizo hili linavyowasumbua wanaume wengi duniani.

Sehemu kubwa ya malalamiko ya wanaume katika sakata hili yanagusa zaidi maeneo matatu ambayo ni kukosa msisimko, kushindwa kurudia tendo na kukosa kabisa nguvu, huku kufika kileleni mapema kukihusishwa pia kama pacha wa janga hili ambalo linawasumbua zaidi wanaume.
 
Sababu zinazosababisha tatizo la nguvu za kiume zinawekwa katika makundi mawili.
*Matatizo ya kiafya ya mwili (organic causes).
*Matatizo ya kisaikolojia ( Psychological cause).
 
Matatizo ya kiafya:
  1. Magonjwa ya kisukari, (diabetes mellitus).
  2. Ugonjwa wa presha (blood pressure).
  3. Matatizo ya tezi dume (kama mtu amewahifanyiwa operation) (prostatectomy surgery),
  4. Upungufu au mvurugiko wa uzalishaji Homoni za uzazi (hormonal insufficiencies /hypogonadism).
  5. Athari za matumizi ya dawa kwa muda mrefu (drug side effect).
Matatizo haya kwa pamoja hupelekea mishipa ya damu kuziba na mwishowe misuli inakosa nguvu za kuweza kusimama na hatimae uume husinyaa.
 
Tatizo la Kisaikolojia(Psychological reasons)
Ukweli wa mambo ulioibuliwa na wanasaikolojia umebaini wale wote wanaolalamikia/lalamikiwa kuwa hawana nguvu iwe ya kufika kileleni mapema, kutokuwa na msisimko na kushindwa kurudia tendo wamekosa maarifa tu ya kufahamu na hawaijui miili yao na wanaishi kwa kusikia zaidi ya kujitambua.

Watu hao kiuhalisia wanakabiliwa  na matatizo ya kimawazo, kama vile migogoro katika mahusiano, matatizo ya kimaisha na mambo mengine
 
Dalili za tatizo hili
  1. Kushindwa kusimamisha uume mara kwa mara,
  2.  Uume kulala(kusinyaa) katikati ya tendo la ndoa.
  3.  kushindwa kusimamisha ipasavyo.
  4. Kufika  haraka mara baada ya kuanza
  5. kujamiiana.
  6.  Maumivu ya misuli ya uume wakati wa tendo la ndoa.

Magonjwa yanayosababisha tatizo hili:
*kisukari (diabetes)
*presha (blood pressure)
*matatizo yafigo (kidney disorders)
*matatizo ya kisaikologia(psychological cause).
* upungufu wa homoni za uzazi (hormonal insufficiencies).
* Matumizi ya dawa kwa muda mrefu (drug side effect).
* Uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kupita kiasi.
* matatizo ya tezi dume.

Matatizo haya yote Yanatibika kwa dawa. Wasiliana Nami kwa msaada zaidi: 0620510598 au 0759208637

 
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images